Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

NDEREMO MAHAKAMANI WAKATI MICHAEL WAMBURA AKIACHIWA HURU

$
0
0

Na Karama Kenyunko, Michuzi TV

FAMILIA ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Wambura imeshindwa kuzuia furaha yao na kujikuta ikipiga makofi mahakamani baada ya Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu kumuachia huru kiongozi huyo wa zamani wa TFF.

Pamoja na kuachiwa huru mahakama imemtaka Wambura kulipa fidia ya Sh 100,998,121 kwa awamu tano.

Hatua hiyo, imekuja baada ya upande wa mashitaka kumfutia Wambura mashitaka ya uhujumu uchumi na kumsomea mashitaka ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu ambapo alikiri kutenda kosa hilo.

Akisoma adhabu hiyo, hakimu mkazi Mwandamizi Mfawidhi, Kelvin Mhina amesema mshitakiwa atatakiwa kulipa fedha hizo kwa awamu tano kuanzia leo, Sh. Miliini 20, Desemba 31, mwaka huu ( Sh 20,249,531), Machi 31,2020, Juni 30 na Septemba 30, 2020 ambapo fedha atakazotakiwa kulipa ni Sh 20,249,531 kama ilivyopangwa kwa miezi.

Aidha mahakama imemtaka mshitakiwa kutokufanya kosa lolote la jinai kwa miezi 12 na kwamba rufaa ipo wazi kwa asiyeridhika.

Kabla ya kutolewa adhabu, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alidai hawana rekodi ya makosa ya nyuma ya mshitakiwa hivyo, aliomba mahakama itoe adhabu kulingana na makubaliano ili iwe fundisho kwake na wengine.

Kwa upande wake , Wambura amedai hilo ni kosa lake la kwanza hivyo, ameiomba mahakama impe adhabu itakayomsaidia kushiriki kufanya shughuli nyingine za kijamii.

Mapema, akisoma makubaliano hayo, Wankyo amedai kuwa wameingia makubaliano na mshitakiwa huyo baada ya kukiri kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu hivyo wameamua kuondoa mashitaka ya kughushi, kutoa nyaraka za uongo na utakatishaji fedha ambayo ni mashitaka ya uhujumu uchumi na kwamba Wambura na upande wa serikali wamekubaliana kulipa fedha yote kwa awamu tano.

Baada ya kusoma makubaliano hayo, Hakimu Mhina alimuapisha mshitakiwa na kumuuliza kama alisaini kwa hiari yake na kudai alifanya hivyo kwa hiari yake.

Akisoma mashitaka mapya, Wakili Simon alidai Julai 6,2004 na Oktoba 30,2015 maeneo ya Ilala kwa udanganyifu Wambura alijipatia Sh 100,998,121 kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa lengo la kuonesha malipo ya mkopo wa Dola za Marekani 30,000 kutoka Kampuni ya Jekc System Limited.

Katika maelezo ya awali, Simon alidai Wambura kipindi hicho akiwa katibu Mtendaji wa TFF, Novemba 28,2002 waliingia makubaliano ya mkopo wa Dola za Marekani 30,000 lengo kufadhili michuano ya Chalenji kipindi hicho mwenyeji alikuwa Tanzania.Alidai Wambura alisaini makubaliano hayo kwa niaba ya TFF na kwamba walitakiwa kurudisha fedha zote pamoja na riba ya asilimia tano mara baada ya mashindano kukamilika.

Alidai Januari 13,2014 Kampuni ya Jekc System Limited iliandika barua kwa mshitakiwa na kwa njia ya udanganyifu Wambura aliilaghai TFF kwa kujaribu kuonesha alichaguliwa na kupewa mamlaka ya kisheria kukusanya fedha hizo kwa niaba ya TFF.

Wambura alifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo akiwa na mashitaka 17 ikiwemo ya kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, kutoka nyaraka za uongo na utakatishaji fedha.


TANTRADE YAJIPANGA KUPATA OFISI YA KUDUMU YA KUTOA HUDUMA YA KLINIKI YA BIASHARA

$
0
0

Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa Majaliwa akipata maelezo toka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE Bw Edwin Rutageruka alipotembelea Kliniki ya Biashara inayoratibiwa na TanTrade wakati wa Ufunguzi wa Maonesho ya Pili ya SIDO kitaifa yaliyofanyika katika Uwanja wa Bombadia Mjini Singida. Kliniki hii inashirikisha Taasisi za Serikali ikiwemo TRA, BRELA, TBS, FCC, MKEMIA MKUU, TFS, WMA, SIDO na 
imedhaminiwa na NBC.Mkurugenzi Mkuu amemweleza Mhe.Waziri Mkuu kuwa TanTrade kwa kushirikiana na Taasisi nyingine wanajipanga kupata ofisi ya kudumu kwa ajili ya kutoa huduma ya Kliniki ya Biashara

AFISA MANUNUZI, MZABUNI, KINAMPANDA WAKAMATWA KWA KUGHUSHI NYARAKA

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikagua mlango, kwenye ukarabati wa Chuo cha Ualimu Kinampanda, mkoani Singida, na kutoridhishwa na vitasa hafifu vilivyotumika katika milango hiyo, Oktoba 6.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimhoji Afisa Manunuzi wa Chuo cha Ualimu Kinampanda, Bw. Francis Muyombo (kushoto), kwa kukiuka taratibu za manunuzi ya Serikali na kughushi nyaraka, Oktoba 6.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikagua maktaba ya Chuo cha Ualimu Kinampanda, mkoani Singida, wakati akikagua ukarabati wa Chuo hicho Oktoba 6.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikagua ukarabati wa Chuo cha Ualimu Kinampanda, mkoani Singida, Oktoba 6.2019.
………………………

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwagiza Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Singida, Bw. Adili Elinipenda amkamate Afisa Manunuzi wa Chuo cha Ualimu Kinampanda, Bw. Francis Muyombo kwa kukiuka taratibu za manunuzi ya Serikali na kughushi nyaraka.

Pia alimwagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, ACP Sweetbert Njewike amkamate na kumhoji Bw. Joseph Kisaka ambaye alikuwa mzabuni wa chuo hicho kwa kuwapatia (kusupply) vifaa ambavyo ni chini ya kiwango.

Alitoa agizo hilo jana jioni (Jumapili, Oktoba 6, 2019), wakati akikagua ukarabati wa majengo ya chuo hicho kilichopo wilayani Iramba, mkoani Singida ambako alibaini delivery note ikionesha kitasa kimoja kimenunuliwa kwa sh. 70,000 badala ya sh. 25,000.

Waziri Mkuu alisema quotation ya manunuzi inaonesha kwamba walipaswa kununua vitasa ambavyo vinafunga mara tatu (vya 3-level) lakini alipokwenda kukagua milango kwenye mabweni, ukumbi, na bwalo alikuta ni vitasa vya kufunga mara moja (vya 1-leavel).

“Serikali imetoa sh. bilioni 1.4 kwa kila chuo ili kufanya ukarabati wa vyuo vya elimu kikiwemo hiki cha kwenu. Ninyi mnanunua vifaa kinyume na utaratibu wa Serikali, hamvikagui, mnaweka tu vitu hafifu ambavyo havidumu. Haiwezekani!”

“Quotation yenu hapa inanionesha mlinunua vitasa 368 vya 3-level kwa gharama ya shilingi 70,000 kila kimoja. Lakini vitasa vilivyoko mlangoni ni vya 1-level ambavyo vinauzwa shilingi 25,000. Haya ni mabweni ya wanafunzi, wanaingi na kutoka kila wakati, ni kwa nini mnaweka vitu cheap wakati mnajua vitaharibika mapema? Maelekezo ya ununuzi wa Serikali yakoje?”

Alipoulizwa wametumia utaratibu gani kununua vifaa hivyo, Mkuu wa Chuo hicho, Bw. Hamisi Njau alisema walikuwa wakitumia kamati ya manunuzi ambayo mwenyekiti wake alikuwa ni Makamu Mkuu wa Chuo na Katibu wake ni Afisa Manunuzi, Bw. Muyombo.

Bw. Muyombo alipoulizwa kama walikuwa wanayo BOQ ambayo ilikua ikiwaongozwa kufanya manunuzi, alijibu kwamba hawakuwa nayo bali alikuwa wakiorodhesha mahitaji yao na kuyapeleka kwa mhandisi.

Alipoambiwa aeleze tofauti ya vitasa vya 3-level na vya 1-level, Bw. Muyombo alijibu kwamba waliambiwa na mhandisi kwamba ndani ya kitasa kuna kibati ambacho kinatofautisha vitasa hivyo.

Waziri Mkuu alisema alisema Serikali inakataa udanganyifu kwenye manunuzi na haitavumilia watumishi wasiokuwa waaminifu. “Tena hili duka la huyo Kisaka ni la nguo wala siyo la hardware (vifaa vya ujenzi).”
Alimwambia Mkuu wa Chuo hicho alipaswa kusimamia ikiwa ni pamoja na ujenzi na ukarabati unaofanyika chuoni hapo.

Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ilitoa sh. 1,439.235,746 ili kukarabati chuo hicho kwenye maeneo ya utawala, maeneo ya kujifunzia, kumbi na mabweni ya wanachuo. Awamu ya kwanza ya fedha hizo iliingia Novemba, 2017 na awamu ya pili ikaingia Juni 2018.

Akizungumza na wanafunzi wa chuo hicho baada ya kufanya ukaguzi huo, Waziri Mkuu alisema Serikali inafanya kazi kubwa ya kuboresha miundombinu ya elimu nchini. “Mheshimiwa Rais alitoa sh. bilioni 1.4 kwa vyuo vyote ili kukarabati na kuboresha hadhi ya vyuo hivyo vikiwemo vya Monduli, Patandi, Kinampanda, Mtwara, Songea, Nachingwea, Korogwe, Kasulu na Butimba.”

“Nimeingia kwenye maktaba yenu nimeona bado vitabu vilivyopo ni vya muda mrefu, lakini kwa upande wa ajira bado tunaendelea kuajiri kwa awamu. Julai mwaka huu tuliajiri walimu 4670 na sasa hivi tumepata kibali cha kuajiri walimu 16,000,” alisema.

BENKI YA DUNIA YAIPATIA TANZANIA MKOPO NAFUU WA DOLA MILIONI 450 KUSAIDIA KAYA MASIKINI

$
0
0
Na Eva Valerian, WFM, Dar es Salaam

Benki ya Dunia imeipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa dola za Marekani milioni 450 sawa na shilingi za Tanzania trilioni 1.035, kwa ajili ya utekelezaji wa Awamu ya Pili ya mpango wa kunusuru kaya masikini unaotekelezwa na Mfumo wa Maendeleo ya Jamii- TASAF, awamu ya tatu.

Tukio hilo limefanyika Jijini Dar es Salaam kati ya Katibu Mkuu-Hazina Bw. Doto James na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird.

Bw. James amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya kupatikana kwa mafanikio makubwa ya awamu mbili zilizopita kwa kusaidia kaya masikini kwa kuongeza kipato na huduma za kijamii, kiuchumi ikiwemo kuwaendeleza watoto wao.

“Mpango huu katika kipindi cha pili ni kuwezesha kaya masikini kutumia fursa ya kuongeza kipato na huduma za kijamii na kiuchumi na kuwekeza katika maendeleo ya watoto wao” alisema Bw. James

Alisema malengo mengine yatakuwa ni kutekeleza miradi inayotoa ajira za muda ikihusisha ujenzi wa miundombinu hususan kwenye sekta mahususi kamavile afya, elimu, maji, kuimarisha taasisi na mifumo.

“Awamu hii ya pili inakwenda sambamba na Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano, Mkakati wa Kukuza Uchumi na na Kupunguza Umasikini Zanzibar (MKUZA) utakao iwezesha Tanzania kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025” aliongeza Bw. James

Katika hafla hiyo Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Ikulu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF Dkt. Moses Kusiluka, alisema kuwa kaya masikini watumie fursa hii kwa kuongeza kipato na huduma za jamii kwa lengo la kupunguza umasikini uliokithiri.

Alisema nia njema ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kuwajali wanyonge na kwa kupitia fedha hizo anaamini jamii itanufaika na ameahidi kuzisimamia fedha hizo kikamilifu ili zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa.

Alisema TASAF itahakikisha kuwa kaya zinazoishi katika umasikini uliokithiri zinapata stadi na elimu ya utunzaji wa fedha na hatimaye kupata fursa ya kukopa katika taasisi mbalimbali za fedha na hivyo kukuza uchumi wa kaya zao na kujenga rasilimali watu hasa watoto wanaohudhuria kliniki na wale walioko shuleni ambao wanaishi katika mazingira magumu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird amesema Benki yake imefurahishwa na namna Serikali ya Tanzania kwa usimamizi mzuri wa fedha na ilivyotekeleza kwa ufanisi mpango huo wa kunusuru kaya masikini katika awamu zote za uwepo wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF

Alisema kuwa kupitia fedha hizo, jamii itaimarisha lishe, maisha ya watu na kuongeza mahudhurio ya wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari darasani pamoja na huduma za afya.

Kwa upande wake Katibu Mkuu kutoka Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bw. Shaaban Mohamed, ameishukuru Benki ya Dunia kwa kutoa mkopo huo wenye masharti nafuu na kueleza kuwa Zanzinbar imekuwa mnufaikaji mkubwa wa mpango huo wa kunusuru Kaya Masikini.

Mwaka 2000, Serikali ilianzisha Mfumo wa Maendeleo ya jamii –TASAF kwa madhumuni ya kusaidiana na vyombo vingine vya Serikali kupunguza umasikini. Awamu ya kwanza (TASAF I) ilitekelezwa mwaka 2000 – 2005 ambapo jumla ya miradi ya kijamii 1,704 yenye thamani ya shilingi bilioni 72 ilitekelezwa ikiwemo ujenzi wa madarasa, miundombinu ya umwagiliaji pamoja na mabwawa ya kuhifadhi maji wakati wa mvua, ujenzi wa barabara vijijini, vituo vya afya, nyumba za walimu kwenye Halmashauri 40 za Tanzania Bara na Zanzibar.

Mwaka 2005 – 2013 awamu ya pili (TASAF II) ilitekeleza miradi ya kijamii 12,347 yenye thamani ya shilingi bilioni 430 katika Halmashauri 126 za Tanzania Bara, Unguja na Pemba, na kuwanufaisha watu 18,682,208.

“Mafanikio yaliyopatikana katika awamu zote mbili imepelekea Serikali kutekeleza awamu ya tatu (TASAF III) mwaka 2012, ambayo itatekelezwa kwa miaka 10 mpaka 2023 katika vipindi viwili ambapo kipindi cha kwanza kitafikia ukomo mwaka huu 2019, na Awamu ya Pili ambayo mkatabata wa mkopo umesainiwa, utakamilika mwaka mwaka 2023.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango (katikati) na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird, wakitia saini mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa dola milioni 450 uliotolewa na Benki hiyo kwa Tanzania kwa ajili ya kutekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaosimamiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF, Jijini Dare Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya TASAF Dkt. Moses Kusiluka akishuhudia tukio hilo pamoja na Afisa Mkuu na Afisa wa Dawati la Benki ya Dunia kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Patrick Pima.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird, wakibadilishana hati za Mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa dola milioni 450 uliotolewa na Benki hiyo kwa Tanzania kwa ajili ya kutekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaosimamiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF, Jijini Dare Salaam. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango akimueleza jambo Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird,mara baada ya kusaini mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa dola milioni 450 uliotolewa na Benki hiyo kwa Tanzania kwa ajili ya kutekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaosimamiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF, Jijini Dare Salaam.
 Wadau mbalimbali wakiwa katika tukio la kutiwa saini kwa Mkataba wa Mkopo wenye Masharti Nafuu wa dola milioni 450 uliotolewa na Benki ya Dunia kwa Tanzania kwa ajili ya kunusuru kaya masikini kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF, Jijini Dar es Salaam, tare 7 Oktoba 2019

USAID YAWEZESHA UPATIKANAJI WA UDHAMINI WA MIKOPO KUPITIA AMANA BANK

BENKI YA DUNIA YAIKOPESHA SERIKALI MKOPO WENYE MASHARTI NAFUU KUKABILIANA NA UMASKINI NCHINI.

$
0
0
Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia zimetiliana saini mkopo wenye masharti nafuu wa dola za Kimarekani milioni 450 kugharamia sehemu ya pili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii -TASAF.Mkataba huo umetiwa saini na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Dotto James kwa niaba ya serikali na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird.

Akizungumza baada ya kutia saini mkataba huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango amesema kupatikana kwa fedha hizo ni kiashirio kingine cha Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dr. John Magufuli ilivyokusudia kuweka mazingira wezeshi ya kuondoa kero ya umaskini kwa wananchi wake.

Amesema Mkopo huo wenye masharti nafuu utaelekezwa zaidi katika kusaidia jitihada za Serikali za kutatua kero ya umaskini nchini kote kwa kuwashirikisha wananchi ambao ni walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wenye uwezo wa kufanyakazi kushiriki kwenye miradi ya maendeleo kwenye maeneo yao na kisha kulipwa ujira kama njia mojawapo ya kuwaongezea kipato.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird amesema Tanzania imekuwa mfano bora katika kuhudumia wananchi wanaokabiliwa na umaskini mkubwa kupitia mfuko wa hifadhi ya jamii jambo ambalo limeifanya Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo ya Dunia kuridhia kiasi hicho kikubwa cha fedha kutolewa kwa utaratibu wa Mkopo wenye masharti nafuu .

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Taifa ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF- Dr. Moses Kusiluka ameishukuru Serikali kwa kutambua mchango mkubwa unaotolewa na TASAF katika kusaidia jitihada za kupunguza umaskini nchini.

Amesema kupatikana kwa fedha hizo kutasaidia kuwafikia wananchi wenye uhitaji mkubwa nchini kote na kuwa kichocheo cha kuharakisha maendeleo na hatimaye kuliwezesha taifa kupunguza umaskini kwa kiwango kikubwa na kuboresha miundombinu katika sekta za elimu, afya maji huku mkazo mkubwa ukiwekwa katika kukuza uchumi wa kaya za walengwa.

Katika hatua nyingine Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bw. Ladislaus Mwamanga ameishukuru serikali kwa uamuzi wa kuendelea kutekeleza Mpango wa kunusuru Kaya Maskini na kuahidi kusimamia kwa uaminifu raslimali fedha ili ziweze kunufaisha taifa kupitia Walengwa.

Amesema uzoefu uliopatikana katika sehemu ya kwanza ya Mpango umeonyesha kuwa Walengwa wengi wamebadili maisha yao kwa kutumia fursa zinazotolewa na Mpango huku akitaja sekta za elimu, afya na uzalishaji mali kuwa zimechangia kwa kiwango kikubwa kuboresha maisha ya Walengwa.

Hafla hiyo imehudhuriwa pia na wawakilishi wa mashirika yanayochangia fedha kwa ajili ya kutekeleza shughuli za serikli kupita Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF. Utekelezaji wa sehemu ya pili ya Mpango wa Kunusuru Kaya maskini unatarajiwa kuanza wakati wowote baada ya kuzinduliwa rasmi na utahudumia takribani Kaya milioni 1.3.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dotto James (kushoto) na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird (kulia) wakitia saini mkataba wa kuipatia Tanzania Mkopo wenye masharti nafuu kutoka Benki ya Dunia kutekeleza sehemu ya Pili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kupitiaTASAF. 



Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Ikulu Dr. Moses Kusiluka (katikati) akizungumza mara baada ya kutiwa saini ya mkopo wenye masharti nafuu kati ya serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia ,fedha zitakazotumika kutekeleza sehemu ya pili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unatekelezwa na serikali kupitian TASAF.Kulia kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bw. Dotto James na kushoto kwake ni Mkurugenzi Makazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird.
Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bi. Bella Bird (katikati) akizungumza baada ya kutia saini mkopo wenye masharti nafuu kwa ajili ya kutekeleza miradi ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa kamati ya taifa ya Uongozi ya TASAF ,Dr. Moses Kusiluka na kulia kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Bw. Dotto James.
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Bw. Ladislaus Mwamanga (aliyevaa miwani) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) baada ya serikali kutia saini mkataba wa mkopo wenye masharti nafukutoka Benki ya Dunia, fedha zitakazotumika kutekeleza mradi wa kupunguza umaskini nchini .  

Dkt. Makakala amewataka Maafisa Uhamiaji Mikoa yote nchini kuimarisha Mapambano dhidi ya Wahamiaji haramu

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Peter Makakala Jumatatu Oktoba 7, 2019 amewataka Maafisa Uhamiaji Mikoa yote nchini kuimarisha Mapambano dhidi ya Wahamiaji haramu.

Akizungumza na Watumishi wa Uhamiaji Mkoa wa Rukwa (mjini Sumbawanga), Dkt. Makakala amesema kuwa nchi yetu inaelekea kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na baadae Uchaguzi Mkuu. Hivyo Maafisa Uhamiaji Mikoa yote nchini wametakiwa kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo kwa kutoa Elimu kwa umma pamoja na kuhakikisha kuwa Wahamiaji haramu hawashiriki zoezi hilo.

Kwa ushirikiano na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Idara ya Uhamiaji inatarajia kutoa Elimu ya Uraia kwa kuanzia na Mikoa ya Kagera, Kigoma, Rukwa, Katavi na Geita. Maafisa Uhamiaji wote nchini wametakiwa kuandaa vipindi maalum vyenye lengo la kuwajengea uwezo na uzalendo wananchi hususan katika masuala ya Uraia.
“Kila Mwananchi anao wajibu wa kulinda usalama wa nchi yetu kwa kutoa taarifa za Wahamiaji haramu. Kumhifadhi au kumsaidia Mhamiaji haramu kupata kitambulisho cha mpiga kura na kushiriki zoezi la kupiga kura kwa ama kuchagua au kuchaguliwa ni kukosa uzalendo kwa nchi yetu” amesisitiza Dkt. Makakala.

“Taifa lolote Duniani liwe kubwa au dogo haliwezi kukamilika bila ya raia wake kwani raia hao ndio wenye nchi na wanaotakiwa kunufaika na haki zitolewazo na serikali kwa raia wake kwa mujibu wa katiba ya nchi ikiwa ni pamoja na haki ya kuchagua au kuchaguliwa katika nafasi za uongozi Kwa upande mwingine ni raia hao ndio wenye wajibu wa kulinda nchi yao” aliongeza Dkt. Makakala.

Awali akitoa taarifa ya Utendaji kazi katika Mkoa wa Rukwa, Afisa Uhamiaji Mkoa wa Rukwa, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Elizeus Mshongi ameeleza kuwa mkoa wa Rukwa unapokea idadi kubwa ya wahamiaji haramu, wengi wao wanatoka katika Mataifa ya Zambia, D.R Congo na Burundi.
Kwa kipindi cha cha kuanzia Januari hadi Agosti, 2019; jumla ya wahamiaji haramu 128 wamekamatwa na kuchukuliwa hatua mbalimbali ikiwamo kushitakiwa na kuondoshwa nchini.

Naibu Kamishna Mshongi ameongeza kuwa Mkoa unaendesha zoezi la kuwatambua na kuwaorodhesha Wahamiaji walowezi. Kupitia Zoezi hilo jumla ya Walowezi 5,743 wametambuliwa na kuorodheshwa.

Aidha, Idara ya Uhamiaji inatoa wito kwa Wahamiaji walowezi wote wanaoishi nchini kujitokeza na kujiorodhesha, watakaoshindwa kufanya hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani na kuondoshwa nchini.

MNYETI AWASHUKIA WANASIASA UCHWARA SIMANJIRO

$
0
0
MKUU wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti amewashukia vikali baadhi ya wanasiasa Wilayani Simanjiro wanaowagawa wananchi katika makundi ya uchaguzi wa serikali za mitaa kwa tiketi ya CCM ili wapate nafasi ya kuchaguliwa katika uchaguzi mkuu wa ubunge 2020. 

Mkuu huyo wa Mkoa wa Manyara Mnyeti aliyasema hayo jana katika kijiji cha Narakauo Kata ya Loiborsiret kwenye siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tano wilayani Simanjiro. 

"Mwisho wa wanasiasa uchwara wa wilaya ya Simanjiro wanaotumia nafasi ya makundi na kugawa wananchi ili wapite katikati yao na kupata ubunge imefika mwishoni," alisema Mnyeti. 

Alisema anataka kuona Simanjiro mpya moja yenye wananchi wenye kutaka maendeleo na siyo kugawanywa na baadhi ya wanasiasa uchwara wanaogawa wananchi kwa maslahi yao ya kutaka kugombea ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Alisema yeye ni mjumbe wa kamati ya siasa ya mkoa ndiyo sababu wakafuta mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa ndani ya CCM wilayani Simanjiro na kuagiza uanze upya kwa lengo la kuondokana na ubabaishaji. 

"Wananchi wa wilaya ya Simanjiro hivi sasa wanataka maendeleo hawahitaji tena siasa uchwara zisizo na muelekeo wenye manufaa kwao kwa kutumia nafasi ya uchaguzi wa serikali za mitaa," alisema Mnyeti. 

Mkuu wa wilaya ya Simanjiro, mhandisi Zephania Chaula aliwataka wananchi wa eneo hilo kutowachagua viongozi wanaojihusisha na uuzaji wa ardhi ili kuepusha migogoro ya ardhi. 

Mhandisi Chaula aliwataka wakazi wa wilaya hiyo kutumia nafasi hiyo vizuri ya uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kuwaondoa madalali wa kuuza ardhi na kuondokana na migogoro ya ardhi. 

"Mkitumia makosa kwa kuchagua madalali wa ardhi baadaye msije ofisini kwangu kunisumbua kwani mtakuwa mmewachagua wenyewe na vijana wa sasa wanasema itakula kwenu," alisema mhandisi Chaula.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti akizindua madarasa matatu ya shule ya msingi Loong'swani kata ya Terrat Wilayani Simanjiro.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti akizungumza na wananchi wa Kata ya Terrat kwenye ziara yake ya siku tano wilayani Simanjiro jana.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti (wapili kushoto) Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro mhandisi Zephania Chaula (kushoto) wakipiga makofi baada ya kukagua nyumba ya kisasa ya mfugaji wa kijiji cha Narakauo Isaya Mongele, kulia ni Diwani wa Kata ya Loiborsiret Ezekiel Lesenga Mardadi.

Rais Magufuli afungua mradi wa uboreshaji huduma ya Maji safi na usafi wa Mazingira Rukwa

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli wanne kutoka kulia walioshika utepe, Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa, Waakilishi wa Umoj wa Ulaya nchini (EU) Waakilishi wa Serikali ya Ujerumani kupitia Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KFW) akifungua mradi wa uboreshaji wa huduma ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Sumbawanga mkoani Rukwa.
 Sehemu ya Miundombinu ya uboreshaji wa huduma ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Sumbawanga mkoani Rukwa ambayo imezinduliwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli leo mjini Sumbawanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia picha ya kuchorwa yenye taaswira yake wakati akiondoka katika uwanja
wa Nelson Mandela mara baada ya kuwahutubia wananchi.
PICHA NA IKULU

WAJUMBE WA MABARAZA YA KISWAHILI BAKIZA NA BAKITA WAKUTANA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Viongozi wa BAKITA na BAKIZA wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kikao cha mashauriano.Kutoka kulia waliosimama mbele ni Bi Mwanahija(Katibu Mtendaji - BAKIZA), Dkt.Muhammed Seif Khatib( Mwenyekiti - BAKIZA),Dkt.Sewangi( Katibu Mtendaji- BAKITA) na Dkt.Samwel( Mwenyekiti - BAKITA) na wajumbe wengine.

..............................................

Viongozi wa Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) na Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA) wamekutana jijini Dar es salaam ili kujadiliana mambo mbalimbali kuhusu maendeleo ya Lugha ya Kiswahili katika mkutano uliofanyika kwenye ofisi za Baraza la Kiswahili la Taifa, jijini Dar es Salaam huku mambo kadhaa ya mashirikiano yalijadiliwa.

Katika majadiliano hayo Ilisisitizwa mabaraza mawili yafanye kazi kwa karibu ili kusadia watanzania kutumia kiswahili kwa ufasaha na usahihi.

Kikao hicho pia kilikubaliana wajumbe kutoka pande zote za Muungano wawe wajumbe wa Mabaraza yote mawili pi kuwepo na kiungo thabiti ili kurahisisha shughuli za uendelezaji wa lugha ya kiswahili kwa pande zote mbili.

Jambo lingine lilijadiliwa ni pamoja na Maneno mapya ya fani na kitaaluma( Istilahi) zinapoandaliwa kwa ajili ya matumizi ni vyema Mabaraza yote yashirikishwe kwa karibu na kukubaliwa kwa maelewano kutimiza malengo ya kukuza kiswahili kwa mafanikio makubwa.

Wajumbe hao pia walikubaliana kuwa uandaliwe mkutano wa vyama vya Kiswahili vya Tanzania kwa ajili ya kukimarisha Kiswahili na kuleta utangamano wa wadau wa lugha hii adhimu ya Kiswahili

SERIKALI IPO TAYARI KULIPA DENI LA SHILINGI BILIONI 13 KWA WAKULIMA WA KOROSHO

$
0
0
Serikali imesema ipo tayari kulipa Deni la shilingi Bilioni 13 kwa wakulima wa korosho  Wilayani Tandahimba.

Hayo ameyasema Naibu Waziri wa Kilimo Omari Mgumbo wakati akijibu maswali na kusikiliza kero mbalimbali za  wananchi wa Kijiji Cha Nachunyu 

"Msema kweli mpenzi wa Mungu,tulishindwa kuendelea kuwalipa kwakuwa fedha ilituishia,lakini Sasa tumeshapata fedha baada ya kuuza korosho zetu zote tan220,000  kwaiyo fedha tunayo tunauhakika wa kuwalipa wakulima,"alisema Mgumbo

Alisema  serikali inatarajia kulipa madeni kwa wakulima na vibarua Tanzania nzima shilingi Bilioni 89  ambazo zipo.

"Utaratibu utafanyika katika malipo hayo lakini fedha kwa Sasa ipo,sababu tulikuwa tunalipwa kwa malipwani yaani mzigo upakiwe kwenye meli ndipo malipo  yafuaate kwaiyo tumemaliza zoezi hilo ," alisema Mgumbo

Aidha alisema maghala yapo wazi tayari kwa kupokea mzigo mpya hivyo muda wowote  wataanza kupokea korosho kutoka kwa wakulima
 Naibu Waziri wa Kilimo Omari Mgumbo na Mkuu wa Wilaya Sebastian Waryuba akipata maelezo kutoka kwa mkulima Ahmad Ulenje
Naibu Waziri wa Kilimo Omari Mgumbo  akifafanua jambo wakati akijibu maswali na kusikiliza kero mbalimbali za  wananchi wa Kijiji Cha Nachunyu 
,kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya Sebastian Waryuba .

BENKI YA EXIM YAZINDUA MAADHIMISHO YA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

$
0
0


Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Tanzania, Bw Jaffari Matundu (katikati) akiongea na mmoja wa wateja wa benki hiyo kupitia simu alipotembelea chumba cha mawasiliano kwa wateja (Call centre) cha benki hiyo wakati wa hafla ya Maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja iliyofanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wengine ni pamoja na Mkuu wa Idara ya Amana wa Benki hiyo, Bi Agnes Kaganda (Kushoto)
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Tanzania, Bw Jaffari Matundu (katikati) akiongea na mmoja wa wateja wa benki hiyo kupitia simu alipotembelea chumba cha mawasiliano kwa wateja (Call centre) cha benki hiyo wakati wa hafla ya Maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja iliyofanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Tanzania, Bw Jaffari Matundu (katikati) akiongea na mmoja wa wateja wa benki hiyo (wa pili kushoto) alipotembelea tawi la Benki hiyo Makao Makuu wakati wa hafla fupi ya Uzinduzi wa Maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja iliyofanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam leo. Pamoja nae ni maofisa waandamizi wa benki hiyo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Tanzania, Bw Jaffari Matundu (katikati) akiongea na mmoja wa wateja wa benki hiyo (kulia) alipotembelea tawi la benki hiyo la Makao Makuu jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja. Pamoja nae ni maofisa waandamizi wa benki hiyo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Tanzania, Bw Jaffari Matundu (alie keti) akipokea zawadi za aina mbalimbali ikiwemo vinywaji baridi kutoka kwa baadhi ya wafanyakazi wa Idara ya huduma kwa wateja wa benki hiyo wakiongozwa na Mkuu wa Idara ya Huduma kwa wateja ya benki hiyo Bw Frank Matoro (Kushoto) wakati wa hafla fupi ya Uzinduzi wa Maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja iliyofanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Idara ya Huduma kwa wateja wa benki ya Exim Tanzania wakiwahudumia vinywaji na zawadi nyingine wafanyakazi wa wenzao kutoka benki hiyo wakati wa hafla fupi ya Uzinduzi wa Maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja iliyofanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Tanzania, Bw Jaffari Matundu (alievaa koti) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo Tawi la Makao Makuu ya benki hiyo alipotembelea tawi hilo wakati wa hafla fupi ya Uzinduzi wa Maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.

KUMBILAMOTO AFANYA UKAGUZI MACHINJIO YA VINGUNGUTI,ARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI

$
0
0
Na Humphrey Shao,Jamhuri Digital.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto leo amefanya ziara katika Machinjio ya Vingunguti kukagua namna jinsi ujenzi unavyondelea na kuzungumza na wamachinga na Mama lishe namna Manispaa ilivyojipanga kuboresha  eneo la kufanyia biashra ndani ya siku saba.

akizungumza na wafanyabiashara hao Mstahiki Meya, Omary Kumbilamoto amesema kuwa manispaa imeamua kuboresha eneo la nje ya machinjio ambapo vijana na mamalishe wanafanya biashara zao ambalo kwa sasa lipo katika mazingira mabovu.

"Nimekaa na Mkurugenzi wangu tukaona si vyema hapa panajengwa machinjio ya kisasa  halafu hatua chache tu wenye nchi yao mnafanya biashara katika mazingira magumu, hivyo tunawaomba mtupishe kwa muda wa siku saba ili turekebisha eneo hili kwa kujenga vizimba vya mama lishe na vya kuchomea nyama pamoja na kuweka paa la juu ili tuweze kuwawekea mazingira bora ya kufanya kazi" amesema Kumbilamoto.

Pia kumbilamoto alipata fursa ya kutembelea eneo ambalo machinjio mapya yanajengwa na kuridhishwa na kasi ya utendaji kazi na kusema kwa uharaka huo anaamini mafundi hao wa shirika la nyumba la Taifa watamaliza ujenzi huo ndani ya muda uliopangwa kama Mh Rais Dk. John Pombe Magufuli alivyoagiza.

Aidha kumbilamoto alipata fursa ya kutembelea eneo ambalo wanataraji kuwahamishia wauza nyama inayochinjwa katika machinio hayo ya kisasa hili wasiwe mbali na eneo lao .

Amesema machinjio mapya yamekuja na changamoto nyingi hivyo nasi tunakabiliana nazo kama viongozi hivyo tupo katika mazungumzo na watu wa Wizara ya Kilimo hili waweze kutupatia eneo lao lililopo jirani na machinjio hili tuweze kujenga soko la kuuzia nyama kwa muda wakati marekebishi ya soko lao yakiwa yanaendelea.
 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akivuka vidimwi vya maji kukagua eneo la wafanyabiashra ndogondogo nje ya machinjio ya Vingunguti

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akizungumza na wafanyabishara waliopo nje ya machinjio ya Vingunguti ambao wanataraji kuboreshewa eneo lao la lufanyia kazi.
 Mmoja ya Mama Lishe wanaofanya biashara katika eneo hilo akimshukuru Mstahiki meya kwa hatua ya waliyofikia kuwaboreshea eneo lao la Biashara.
 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akikagua eneo la Wizara ya Kilimo ambalo wauza nayama wanatakiwa kuhamishiwa kwa muda

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akizungumza jambo na mkandarasi anayejenga Machinjio ya Vingunguti kutoka shirika la nyumba la Taifa 
 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto akipasua mawe katika site ya ujenzi wa Machinjio ya Kisasa Vingunguti

CEED TANZANIA YATOA MAFUNZO YA KUKUZA NA KUSIMAMIA BIASHARA KWA WAJASIRIAMALI NCHINI

$
0
0
Bwana Archad Kato kutoka kampuni ya uzalishaji mvinyo ya Alko Vitanges wamezungumzia fursa,uzoefu pamoja na changamoto mbalimbali katika ukuzaji wa biashara zao.

Bi Elizabeth Swai akizungumza uzoefu wake wakatiwa semina ya CEED Tanzania Dodoma

Dodoma, Kituo cha Ujasiriamali na Maendeleo ya Utendaji (CEED), yawakutanisha wajasiriamali mbalimbali jijini Dodoma katika semina iliyolenga kutoa elimu ya usimamizi na ukuzaji biashara zao ndani ya jiji la Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari, mwakilishi kutoka CEED Tanzania Fred Laiser amesema semina hii ni kwa ajili ya kuwapa ujuzi wa namna ya kuboresha biashara zao, ushindani wa kusaka fursa mbalimbali kutoka na kuongeza kwa idadi kubwa ya watu baada ya serikali kuhamishia shughuli zake hapa Dodoma.

‘’Sisi CEED Tanzania lengo letu kuu ni kuwasaidia wajasiriamali hapa nchini kukuza biashara zao. Leo tupo hapa Dodoma kwa lengo kuwapa elimu na kutoa fursa mbalimbali za kibiashara ambazo wajariamali wanaweza kuzichangamkia. Pia kuwakutanisha na wenzao wajifunze namna ya kukuza biashara zao, kutatua changamoto zao.’’ Alisema Bwana Laiser.

Mbali na hilo, Bwana Fred Laiser ametumia nafasi hii kuwataka wajasirimali mbalimbali nchini kujitokeza kwa wingi katika semina mbalimbali za ujasiriamali hasa zinazoendeshwa na CEED Tanzania kwaji ajili ya kupata ujuzi wa biashara zao na pia kufahamiana na wajasiriamali kutoka kila kona ya Tanzania.

Kwa upande wa wanufaikaji wa mafunzo haya Bi.Elizabeth Swai mwanzilishi wa kampuni ya ufugaji kuku ya AKM Glitters Limited na Bwana Archad Kato kutoka kampuni ya uzalishaji mvinyo ya Alko Vitanges wamezungumzia fursa,uzoefu pamoja na changamoto mbalimbali katika ukuzaji wa biashara zao.

‘’Nawapongeza sana CEED Tanzania kwa kutupa nafasi hii ya kujifunza na kukutana na wajasiriamali wenzetu ili kujifunza mambo mbalimbali kutoka kwao.Moja ya changamoto inayotukabili sisi wajasiriamali hapa nchini ni kushindwa kuendeleza biashara zetu mara baada ya kuanzisha. Wengi tunapenda kujiajiri lakini wachache ndio wanaofikia malengo yao.Ili kutatua changamoto hizi inatupasa kujifunza vitu vipya kila siku na kujaribu mara kwa mara mpaka pale biashara itakapoweza kujiendesha yenyewe ‘’. Alisema Bwana Archad Kato.

Kwa upande wake Elizabeth Swai ametumia nafasi hii kuwataka wajasiriamali kutumia vizuri teknolojia katika kujifunza masuala mbalimbali kwasababu teknolojia imerahisisha kila kitu kwasasa. Rahisi kupata taarifa mbalimbali zitakazowasaidia kujielimisha ba kukuza biashara zao.

Semina hii imeudhuliwa na wajasiriamali takribani 52 kutoka kona mbalimbali za Dodoma na nje ya Dodoma ambapo Kwa pamoja wamewesha kujadili masuala mbalimbali katika kukuza biashara zao, namna ya kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili katika shughuli zao za kila siku za ujasiriamali.

UPU WAKUBALIANA MALIPO YA GHARAMA MPYA ZA KUSAFIRISHA VIFURUSHI NA MIZIGO

$
0
0
Kiongozi wa Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa 3 wa Dharura wa UPU Dk. Jim Yonazi akisainiMakubalioano ya Malipo mapya ya kusafirisha Vifurushi huko Geneva, Switzerland.Wakishuhudia kutoka kushoto; Ms Neema Manongi (Afisa Itifaki wa UN Ofisi ya Geneva), Bw.. Elia Madulesi, Mkuu wa Uhusiano Kimataifa wa Shirika la Posta Tanzania Bwana Haruni H. B. Lemanya, kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)

Na Innocent Mungy – WUUM-M

Mkutano wa 3 wa Dharura wa Baraza Kuu la Umoja wa Posta Duniani (UNIVERSAL POSTAL UNION) umefanyika jijini Geneva, Switzerland, kuanzia tarehe 24 hadi 26 mwezi Septemba, 2019, umekubaliana gharama mpya za malipo za usafirishaji wa barua, vifurushi, vipeto na mizigo kjwa nchi wananchama wa umoja huo.

Tanzania ilihudhuria mkutano huo, ikiwa na ujumbe uliongozwa na Naibu Katibu Mkuu-Mawasiliano, Wizara ya ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt. Jimmy Yonazi pamoja na wajumbe wengine kutoka Shirika la Posta nchini (TPC) pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA.

Nchi wananchama wa Umoja UPU waliohudhuria Mkutano huo walifikia makubaliano kuhusu malipo ya gharama mpya za kusafirisha vifurushi za kimataifa, zikiwa zimezingatia gharama za uendeshaji wa kupokea, kuhifadhi na kusafirisha hadi kufikisha vifurushi hivyo bila kuleta hasara kwa Posta itakayofanya kazi hiyo. Gharama hizo ni zilipendekezwa na nchi wanachama wa UPU wakati wa Mkutano Mkuu wa wa UPU wa mwaka 2016 (Universal Postal Congress) uliofanyika Instanbul Uturuki.

Mnamo tarehe 17 Oktoba, 2018, Marekani ilipeleka barua UPU kujitoa kwenye umoja wa Posta Duniani (UPU) ikilalamikia viwango vya malipo ya kupokea, kuhifadhi na kusafirisha vifurushi hadi kwa wenyewe kutokana na gharama kubwa ya uendeshaji, na kukataa kupokea vifurushi hivyo kama bei hazitaongezeka kufidia gharama za uendeshaji. Umoja wa Posta Duniani ulishughulikia suala hilo kwa haraka ili kuhakikisha kuwa umuhimu wa kutatua suala hilo unaenda sambamba na umuhimu wa kuwepo ushirikiano mzuri ndani ya Umoja huo.

Maamuzi hayo ya makubaliano wa viwango vipya vya malipo ya kusafirisha vifurishi ndani ya nchi wanachama 130, yalifikiwa siku ya pili ya Mkutano huo ambao ulikubaliana kukubali mapendekezo kutoka fungu V kati ya mapendekezo mengine yaliyofahamika kama A, B, C ambayo hayakukidhi maoni ya nchi nyingi wananchama wa UPU.

Kabla ya kufikia makubaliano ya viwango vipya vya malipo, Tanzania ilikuwa imependekeza viwango vilivyoko kwenye fungu V. Katika Taarifa yake kwa Baraza Kuu la UPU, Mkuu wa Ujumbe wa Tanzania Dk. Jim Yonazi, aliupongeza Uongozi wa UPU kwa kuhakikisha kuwa makubaliano yanafikiwa na kupendekeza kwa wajumbe wa Mkutano huo kukubali viwango vipya vya malipo vilivyoko kwenye fungu V.

“Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaungana na wajumbe wa Mkutano huu kumshukuru Mwenyekiti wa Mkutano huu na Mkurugenzi Mkuu wa UPU kwa namna mnavyoendesha Mkutano huu muhimu. Napenda pia niwashukuru wajumbe wote wa nchi wanachama wa UPU ambao wanakubaliana na mapendekezo yaliyoko katika kifungu cha V. Huu ni ushindi wetu sote kwani tumejadiliana kwa umakini mkubwa na kufikia uamuzi ambao ni bora kwetu sote. Sisi Tanzania tunapendekeza na kuwaomba wote tukubaliane na mapendekezo haya.” Aliwasema Dkt. Jim Yonazi wakati akiwakilisha msimamo na mapendekezo ya Tanzania.

Akifunga mkutano huo, Katibu Mkuu wa UPU Balozi Bishar A. Hussein aliwapongeza wajumbe Zaidi ya 800 kutoka nchi wanachama 130 kwa kufikia makubaliano ya pamoja kuhusu gharama mpya za kusafirisha vifurushi kwa nchin wananchama wa UPU.

Balozi Hussein aliuleza Mkutano huo kuwa ‘hakuna changamoto yeyote inaweza kutushinda kama tukiamua kufikia maelewano kwa faida ya nchi zetu’. Aliwashukuru wanachama wan chi wanachama wa UPU kwa kwa kutatua changamoto kubwa ambayo miezi kadhaa nyuma ilionekana kubwa na isiyo na ufumbuzi.

Nae Mwenyekiti wa Mkutano huo ambaye pia ndio Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Posta la Uturuki, Kenan Bozgeyikaliushukuru uongozi wa UPU kwa kazi kubwa ya kuhakikisha Mkutano huo wa Dharura unafanyika na kufikia maamuzi kwa niaba ya nchi zote wanachama.


MKUTANO WA MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA USHIRIKA WA AKIBA NA MIKOPO KITAIFA, WAANZA LEO JIJINI ARUSHA

$
0
0
Naibu Mrajis wa vyama vya Ushirika Tanzania Bw. Charles Malunde amewataka viongozi na watendaji wa Vyama vya Akiba na Mikopo kuendelea kuimarisha utendaji wa vyama hivyo vya Ushirika wa kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu za Vyama vya Ushirika hususani katika uendeshaji wa vyama    vya Akiba na Mikopo. 

Bw.Malunde ameyasema hayo katika Mkutano wa kumi wamaadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Ushirika wa Akiba na Mikopo Kitaifa katika siku ya kwanza ya mkutano huo ulioanza Jijini Arusha leo. Mkutano ulioandaliwa na Chama Kikuu cha Ushirika wa Akiba na Mikopo Tanzania SCCULT (1992) Ltd.

Mwenyekiti wa SCCULT Dkt.Gervas Machimu akiwakaribisha wajumbe wa mkutano huo amewaomba wajumbe hao kutumia mkutano huo kujadili masuala ya vyama vya Akiba na Mikopo, kubadilishana uzoefu, mawazo na kujifunza mambo ya msingi ya uendeshaji wa vyama hivi ili kuongeza tija na ufanisi katika vyama vyao.

Dkt.Machimu ameeleza mkutano huo umelenga kuwakutanisha Viongozi, wajumbe wa Bodi, Wanachama na wadau wa Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo ili kujadili kwa pamoja fursa, changamoto na kuchangia mawazo katika kuendeleza vyama hivi vyenye mchango na kuleta suluhisho la Mtaji miongoni mwa wananchi. 

Mwenyekiti alifafanua kuwa Kauli Mbiu ya Mkutano kwa mwaka huu isemayo “Huduma kwa Jamii kufikia ulimwengu” imelenga kuelekeza vyama hivi kuendeleza na kuongeza juhudi za kuwafikia wananchi wengi zaidi kwa lengo la kuboresha uchumi na kuleta maendeleo. Mkutano huo unaoendelea kuanzia leo tarehe 08/10/2019 hadi 10/08/2019.
Wajumbe wa mkutano wa kumi wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Ushirika wa Akiba na Mikopo wakijisajili kwaajili ya kuanza mkutano, Leo jijini Arusha.
Wajumbe wakiendelea kujisajili tayari kuanza mkutano, Jijini Arusha

MKUU WA MKOA WA KUSINI AHIDI KUSHIRIKIANA NA WANANCHI NA KUTATUWA CHANGAMOTO

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud akitoa hotuba na kuomba Ushirikiano na Viongozi wenzake pamoja na Wananchi wa Mkoa huo katika Mkutano wa kukaribishwa huko Ofisi za Wilaya ya Kusini Unguja, wa kwanza (kushoto) Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Idrissa Kitwana, na wa kwanza (kulia) Mwenyekiti wa Halmashauri Wilaya ya Kusini Juma Mussa. 
Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Idrissa Kitwana akisoma muhtasar wa Taarifa ya Wilaya ya Kusini katika Mkutano wa kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud huko Ofisi za Wilaya ya Kusini Unguja. 
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kusini Unguja Abdul-azizi Hamadi Ibrahim akitoa maelezo kuhusu Chama Cha Mapinduzi katika Mkutano wa kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud huko Ofisi za Wilaya ya Kusini Unguja. 
Baadhi ya Vijana wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) na Watendaji wa Mkoa wa Kusini Unguja wakifatilia Mkutano wa kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud huko Ofisi za Wilaya ya Kusini Unguja. Picha na Maryam Kidiko – Maelezo Zanzibar.

Na Mwashungi Tahir ,Maelezo 

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud amewahakikishia wananchi wa Mkoa huo kuwa atashirikiana na viongozi wenziwe wa Mkoa huo kutatua changamoto zilizopo. 

Amezungumza hayo na watendaji pamoja na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) huko Makunduchi katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja wakati wa kukaribishwa na kupewa taarifa za utekelezaji wa kazi katika Wilaya huo.

Amesema atakuwa na utaratibu wa kukaa pamoja na wananchi ili kusikiliza changamoto zilizopo na kuzitafutia ufumbuzi kwa kuhakikisha maendeleo yanapatikana.“Nitaweka siku maalum ya kukaa na wananchi wazielezee changamoto zilizopo ndani ya Mkoa huu ili kuzitatua na kuhakikisha tunazifanyia ufumbuzi”, alisema Mkuu wa Mkoa huyo.

Miongoni mwa changamoto zilizokuweko katika Mkoa huo ni sekta ya Afya, udhalilishaji, mmong’onyoko wa maadili, uingiaji wa wageni kiholela bila ya kufuata sheria za nchi.Aidha alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iko kwa ajili ya kuhudumia Wananchi na kufahamu kero zao kwa kila sekta na kuzifanyia kazi kwa lengo la kuona wanaishi kwa amani na utulivu.

Pia amewaomba vijana wawe watulivu kwani wanaandaliwa mazingira mazuri ya kujipatia maisha kwa kuzitumia fursa zilizopo.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Idrissa Kitwana Mustafa akisoma Muhtasari wa Taarifa ya Wilaya hiyo amesema hali ya usalama katika Wilaya hiyo iko vizuri na wananchi wanaendelea kufanya kazi zao kwa amani.Sambamba na hayo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kusini Kassim Mtoro Abuu akiwasilisha Muhtasari amesema wamepata mafanikio ya kinga ya chanjo kwa watoto ikiwemo pepo punda na kifaduro.

Aidha wameahidi watakuwa nae karibu Mkuu wa Mkoa kwa kumpa mashirikiano ili aweze kufikisha huduma kwa jamii na kuleta maendeleo katika mkoa huo.

DKT. MWANJELWA AWATAKA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA ITILIMA KUTOOMBA UHAMISHO BILA KUWA NA SABABU ZA MSINGI

$
0
0

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Mkuu wa Wilaya hiyo. Kulia ni Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma, Mhe. Balozi Mstaafu John Haule.
Baadhi ya Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza wakati wa kikao kazi kilichofanyika katikaukumbi wa Ofisi za Mkuu wa Wilaya hiyo.
Muuguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, Bi. Dalahile Malele akiwasilisha malalamiko yake kuhusu kutojibiwa kwa maombi yake ya uhamisho wakati wa kikao kazi kati ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na watumishi wa Halmashauri hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi za Mkuu wa Wilaya.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akitia saini kitabu cha wageni kabla ya kikao chake na watumishi wa Halmashari ya Wilaya ya Itilima kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo.

……………………………….

Na Happiness Shayo, Itilima

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) amewataka watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, kuacha mara moja tabia ya kuomba uhamisho pasipokuwa na sababu za msingi na badala yake watumie ujuzi walionao ili kuleta maendeleo katika eneo hilo.

Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) ametoa wito huo wakati wa kikao kazi chake na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, mkoani Simiyu kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya hiyo.

“Ninyi ni wataalamu na mna ujuzi mbalimbali, hivyo wananchi wa Itilima wanahitaji huduma yenu na kuongeza kuwa, kama mnaona Itilima hakuna maslahi kwenu, inawapasa kutumia ujuzi wenu kuhakikisha mnaongeza mapato ili muweze kunufaika na ongezeko hilo” Dkt. Mwanjelwa amesisitiza.

Dkt. Mwanjelwa amewatahadharisha Maafisa Utumishi kuhakikisha wanajiridhisha na sababu za watumishi kuomba uhamisho na kuhakikisha kuna mbadala wa mtumishi atakayepewa uhamisho, lengo likiwa ni kutoathiri utoaji huduma kwa wananchi.

“Maafisa Utumishi mnatakiwa mjiridhishe na sababu zinazotolewa na watumishi wanaoomba uhamisho kama ni za msingi na iwapo wametengewa bajeti katika mwaka husika”, Dkt. Mwanjelwa amesema.

Dkt. Mwanjelwa amewataka watumishi hao kutulia katika vituo vyao vya kazi ili waweze kuwahudumia wananchi kwani Serikali iliwaajiri kwa sababu hiyo. Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, Bi. Elizabeth Gumbo amekiri kuwa, wilaya hiyo ina changamoto kubwa ya watumishi kuomba uhamisho hivyo amewataka kutafakari upya ili waendelee kuwatumikia wananchi wa Itilima.

Aidha, Bi. Gumbo ameahidi kuhakikisha watumishi wa wilaya yake wanafanya kazi kwa bidii ili kuendana na kasi ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Dkt. Mwanjelwa yuko mkoani Simiyu kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watendaji na watumishi wa umma ikiwa ni pamoja na kusikiliza kero za watumishi hao na kutatua changamoto zinazowakabili.

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA KALI ZA KINIDHAMU WATUMISHI WATAKAOBAINIKA KUJIHUSISHA NA RUSHWA YA NGONO

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akizungumza na watumishi wa umma wilayani Tunduru wakati wa kikao kazi chake na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kilichofanyika wilayani humo jana.
Baadhi ya watumishi wa umma wilayani Tunduru wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi cha waziri huyo na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kilichofanyika wilayani humo jana.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akifafanua hoja za watumishi wa umma wilayani Tunduru (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi chake na watumishi hao kilichofanyika wilayani humo jana kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Mhe. Julius Mtatiro akimshukuru Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) kwa kuitembelea wilaya yake na kufanya kikao kazi na watumishi wa wilaya hiyo jana kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Watumishi wa umma wilayani Tunduru wakiwa katika kikao kazi na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi hao kilichofanyika wilayani humo jana.

………………………….

Na James K. Mwanamyoto, Tunduru

Serikali haitosita kuwachukulia hatua kali za kinidhamu watumishi wa umma watakaobainika kujihusisha na rushwa ya ngono katika maeneo yao ya kazi, kwani kitendo hicho kinadhalilisha na kushusha hadhi ya utumishi wa umma nchini.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) wakati wa kikao kazi chake na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru kilichofanyika wilayani humo jana kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji. 

Mhe. Mkuchika ametoa kauli hiyo kufuatia baadhi ya Walimu wa shule za msingi wilayani Tunduru kushikiliwa na vyombo vya dola kwa kujihusisha na vitendo vya rushwa ya ngono jambo ambalo halileti taswira nzuri kwa umma, ikizingatiwa kuwa Walimu wana jukumu la kuwalea wanafunzi katika maadili mema.

“Inakuwaje Mwalimu unaepaswa kuwa mfano bora wa kuigwa kimaadili unataka rushwa ya ngono kwa mwanafunzi, kitendo hicho kinamuathiri mwanafunzi husika kitaaluma na kisaikolojia”, Mhe. Mkuchika amefafanua.

Mhe. Mkuchika ameongeza kuwa, hivi karibuni ofisi yake imesitisha ajira ya Mhadhiri mmoja wa chuo kikuu nchini, ambaye alituhumiwa na kubainika kuwaomba rushwa ya ngono wanafunzi wa kike ili waweze kufaulu mitihani yao kwa upendeleo.

“Wanafunzi wa kike wa chuo hicho waliandika barua ya malalamiko kwenye ofisi yangu na baada ya kuwahoji na kufanya uchunguzi wa kina kwa kushirikiana na vyombo vya dola ikabainika kuwa ni kweli hivyo akafukuzwa kazi,” Mhe. Mkuchika ameeleza.

Mhe. Mkuchika amewatahadharisha watumishi wa umma nchini kuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) iko kazini na ina utayari wa kumshughulikia mtumishi yeyote atakayetumia cheo chake vibaya ili kujinufaisha na rushwa ya ngono.

Aidha, Mhe. Mkuchika amesema nchi yetu imebahatika kuwa na viongozi wenye utashi wa kupambana na rushwa kuanzia Awamu ya Kwanza ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius K. Nyerere hadi Awamu hii ya Tano, inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ambaye amejipambanua kwa vitendo kwa kuanzisha Mahakama ya Mafisadi na Wahujumu Uchumi.

TUME YA USHINDANI YATOA ELIMU MAONESHO YA SIDO KITAIFA 2019 SINGIDA

$
0
0
Mwanasheria na Afisa Mlinda Mlaji wa Tume ya Ushindani (FCC) Exavery Ngelezya (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu elimu ya utambuzi wa bidhaa bora na bandia iliyotolewa kwa wananchi katika maonesho ya pili ya viwanda vidogo (SIDO) Kitaifa 2019 yanayoendelea Uwanja wa Bombadia Mkoani Singida. Kulia ni Afisa Uhusiano na Mawasiliano ya Umma, Adefrida Ilomo.
Afisa Uhusiano na Mawasiliano ya Umma wa FCC, Adefrida Ilomo akizungumza na waandishi wa habari.


Na Dotto Mwaibale, Singida

TUME ya Ushindani (FCC) imetoa elimu kwa wananchi na wadau mbalimbali katika maonesho ya pili ya viwanda vidogo (SIDO) Kitaifa 2019 mkoani Singida kuhusu bidhaa bandia.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika maonesho hayo Afisa Mawasiliano na Mahusiano ya Umma wa tume hiyo Adefrida Ilomo alisema tume hiyo imetoa elimu kwa wananchi kuhusiana na utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa sheria.

"Tumekusudia kutoa elimu kwa wananchi wanaotembelea banda letu inayohusu masuala ya ushindani, utetezi wa mlaji na udhibiti wa bidhaa bandia" alisema Ilomo.

Ilomo alisema tume hiyo imeanza kutoa elimu ya wajibu wa wazalishaji na wajasiriamali katika kusajili nembo zao ili waweze kulindwa na sheria ya alama za bidhaa dhidi ya wazalishaji wanaoiga bidhaa zao kwa nia ya kudanganya au kutapeli.

Alitaja wajibu mwingine wa wazalishaji au wajasiriamali ni kuhakikisha wanaonesha taarifa zote muhimu katika vifungashio kwa mujibu wa sheria au alama za bidhaa ya 1963 na sheria ya ushindani ya mwaka 2003 na kuwa wajibu wa wafanyabiashara na watoa huduma ni kuwasilisha taarifa zao kwa ajili ya mapitio ya mikataba yote ya mlaji.

Mwanasheria na Afisa Mlinda Mlaji wa FCC Exavery Ngelezya alitoa wito kwa wananchi kutambua bidhaa bora na kuzibaini zile za bandia ili kuepuka madhara yatokanayo na bidhaa hizo bandia.

Kwa upande wa wajasiriamali wametakiwa kuhakikisha kutomlisha mlaji bidhaa zisizo na ubora hivyo ni vyema kupitia taratibu zote kabla ya kupeleka bidhaa zao sokoni 
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images