Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110088 articles
Browse latest View live

MKUTANO MKUU SEKTA YA MAENDELEO YA JAMII SASA OKTOBA 21

$
0
0
Mkutano wa 14 wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii kwa mwaka huu uliopangwa kufanyika  Oktoba 8 hadi 11 umesogezwa mbele na utafanyika tena  Oktoba 21 hadi 24 mwezi huu kwa sababu ambazo hazikuweza kuzuilika.

Akizungumza na vyombo vya habari kuhusiana na mabadiliko hayo Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike amesema kufuatia mabadiliko hayo Wizara yake inaomba radhi kwa washirikli na waajiri kuhusu usumbufu uliojitokeza kwani sababu za kusogeza mkutano huo ziko nje ya uwezo wa Taasisi.

Bw. Golwike ameutaja Mkutano wa mwaka wa Sekta hiyo wa mwaka 2018 kuwa wenye mafanikio makubwa kwa kuwa uliongeza wigo wa ushiriki  kwa kuhudhuriwa na wataalam wa maendeleo ya Jamii kutoka Serikali za Mitaa na hata Sekta binafsi, NGOs na Taasisi za Elimu ya Juu na mategemeo yake kwa mwaka huu matarajio ni zaidi ya hapo.

Bw. Golwike amekitaja Chama cha Kitaaluma cha Sekta ya Maendeleo ya Jamii maarufu CODEPETA kuwa kimekuwa msaada mkubwa katika kufanikisha maandalizi ya Kongamano la Wanataaluma hao maarufu Nchini kwa kushirikisha Wizara pamoja na  wadau wengine hapa Nchini.

Bw. Golwike pia ameviambia vyombo vya  habari kuwa Wizara tangu mwaka 2001 imekuwa ikifanya Mkutano Mkuu wa Wataalam wa Maendeleo ya Jamii Nchini  kwa lengo la kubadlishana uzoefu  na utendaji kazi katika kutekeleza majukumu ya Sekta ya Maendelepo ya Jamii.

Jumla ya Mkutano 13 imekwishafanyika na kuhudhuriwa na wataalam wa Kada ya Maendeleo ya Jamii kutoka Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Taasisi za Wizara na Wizara za Kisekta zikiwemo Taasisi za Kiraia hapa nchini.
Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike akizungumza na waandishi wa habari leo jijini  Dodoma kuhusu kusogezwa mbele kwa Mkutano Mkuu wa Maendeleo ya Jamii kutoka tarehe 08-10/2019 mpaka tarehe 21-24/10/2019. 

Vodacom Yawapongeza Wateja wake kote nchini

$
0
0
Mkurugenzi wa Huduma Kwa Wateja Vodacom Tanzania, Harriet Lwakatare (kulia) akimuhudumia Mteja, Peter Mbuya Mkazi wa Tabata Kimanga kwenye duka la Voda lililopo makao makuu ya kampuni hiyo leo, Katikati ni Mtaalam wa Mtandao kutoka Vodacom, Hendrick Rupia. Hii ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.
Meneja wa Vodacom Kanda ya Kati, Andrew Temu (kushoto) akimkabidhi zawadi Emmanuel Machela (34) Mkazi wa Nzuguni Dodoma leo,Kampuni hiyo imekabidhi zawadi hizo katika wiki ya huduma kwa wateja inayoendelea. Anayeshuhudia katikati ni msimamizi wa maduka ya Vodacom Kanda ya Kati,Suzana Mwaipopo.
Meneja wa Vodacom Kanda ya Kati, Andrew Temu (kushoto) akimkabidhi zawadi Omari Lubasi mkazi wa Kikuyu Mjini Dodoma leo akiwa ni miongoni mwa wateja waliopata zawadi hiyo katika wiki ya huduma kwa wateja wa Kampuni ya simu ya Vodacom. Anayeshuhudia katikati ni msimamizi wa maduka ya Vodacom Kanda ya Kati, Suzana Mwaipopo na makabidhiano hayo yalifanyika Ofisi za Vodacom Kanda ya Kati Mjini Dodoma.
Mkurugenzi wa Biashara Vodacom Tanzania, Linda Riwa (kulia) akinyanyua juu Champagne kuzinduzi rasmi wiki ya huduma kwa wateja iliyofanyika kwenye duka la Voda makao makuu jijini Dar Es Salaam leo. Pembeni yake ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja Vodacom, Harriet Lwakatare.
Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja Vodacom Tanzania, Harriet Lwakatare akimlisha keki mmoja kati ya wateja waliokuwepo dukani siku ya leo.

Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja Vodacom Tanzania, Harriet Lwakatare akizungumza na waandishi na wateja waliohudhuria siku ya huduma kwa wateja wa Vodacom Tanzania, Pia alitoa shukurani kwa wateja na wafanyakazi wa Vodacom kwenye wiki hii na alitoa wito kwa wateja wasajili laini zao kwa alama ya vidole kote nchini.. Kulia ni George Lugata, Mkuu wa Idara ya Mauzo na Usambazaji wa kampuni hiyo.

DC KOROGWE AWAONYA WAANDIKISHAJI NA WAANDAAJI WA ORODHA YA WAPIGA KURA NI WALE WATAKAOBAINIKA KUWAANDIKISHA RAIA WA KIGENI

$
0
0
 MKUU wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa waandikishaji na waandaaji wa orodha ya wapiga kuwa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2019 ambapo aliwataka wawe makini ili wasijikute wameingia matatani kulia ni Afisa Tarafa ya Korogwe Michael John kushoto ni Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Korogwe mji Kassim Kaoneka
 Afisa Tarafa ya Korogwe Michael John akizungumza kwenye mafunzo hayo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa 
 Mwanasheria wa Halamshauri ya Korogwe mji Mwanasheria wa Halmashauri ya Korogwe mji Madgalena John akizungumza wakati wa mafunzo hayo 
 Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Korogwe mji Kassim Kaoneka akizungumza kulia ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa
 Sehemu ya waandikishaji na waandaaji wa orodha ya wapiga kura Korogwe wilayani Korogwe wakiwa kwenye mafunzo hayo
 Sehemu ya waandikishaji na waandaaji wa orodha ya wapiga kura Korogwe wilayani Korogwe wakiwa kwenye mafunzo hayo



 MKUU wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa kushoto akiagana na Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Korogwe mji Kassim Kaoneka mara baada ya kufungua mafunzo hayo katikati ni 
MKUU wa wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga Kissa Gwakisa amewaonya waandikishaji na waandaaji wa orodha ya wapiga kura wilayani humo watakaobainika kuwaingiza raia wa kigeni kwamba hawatasalimika badala yake watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.


DC Kissa aliyasema hayo leo wakati akifungua mafunzo kwa waandikishaji na waandaaji wa orodha ya wapiga kuwa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2019 ambapo aliwataka wawe makini ili wasijikute wameingia matatani.


Alisema kwamba pamoja na kuwepo kwa mafunzo hayo lakini wapo baadhi ya waandikishaji na waandaaji wa orodha ya wapiga kura kwenye uchaguzi huo wanaweza kufanya tofauti na maelekezo hivyo watahakikisha wanashughulikiwa kwa mujibu wa sheria zilizopo.


“Ndugu zangu wasimamizi uchaguzi wilayani, wanasimamia uchaguzi wasaidizi ngazi ya wilaya, Kata, Vijini na Mitaa kuhakikisha wanakuwa waaminifu na nidhamu wakati wa kutekeleza majukumu yenu na hii itasaidia kuepusha malalamiko huku akiwaonya watakaokwenda kunyume watachukuliwa hatua kali dhidi yao “Alisema DC Korogwe.


Aidha Mkuu huyo wa wilaya aliwataka wasimamizi hao kuwa mfano mzuri katika utekelezaji wa majukumu yao kwa kuhakikisha wanatenda haki ili uchaguzi uweze kwenda kwa haki na usalama bila kuwepo na malalamiko ya aina yoyote ile.


“Lakini pia niwaambie kwamba elimu hii muende kuitoa na ngazi za chini..kupiga kura ni haki ya kila mtanzania hivyo tunawategemea kama Taifa kundi hili lipo kila kila wilaya kwa nyie wa hapa nataka kuona mfano mzuri Korogwe Uchaguzi uende vizuri kusiwe na malalamiko”Alisema DC Kissa.


Hata hivyo alisema kwamba wataendelea kupewa semina ili kuweza kuwasaidia kuondokana na kufanya makosa kwenye uchaguzi huo ikiwemo kuzingatia nidhamu ya hali ya juu wakati mkitekeleza majukumu yenu mapya.


“Mpo kwenye nafasi nyeti Taifa linawategemea yale mambo siri mfanye siri lazima mtambua kwamba mnajukumu kubwa na zito kwa watanzania lakini mkizingatia maelekezio mnayopewa itakuwa chachu kubwa ya kusimamia vema uchaguzi bila kuwepo wa manunguniko”Alisema Mkuu huyo wa wilaya.


Awali akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo Mwanasheria wa Halmashauri ya Korogwe mji Madgalena John alimuhaidi Mkuu huyo wa wilaya kwamba hawatamuangusha wala kuiangusha serikali na watakwenda kuitendea haki serikali yao na wananchi wa wilaya hiyo.


Alisema kwamba wanakwenda kufanya jukumu hilo nzito ambalo wamekabidhiwa na serikali  na wanaimani baada ya neno kutoka kwake limewapa mwanga mpya ambao utakuwa chachu katika kutekeleza majukumu yao .


“Nikuhaidi Mh DC hatutakuangusha wewe wale serikali tutakwenda kuitendea haki serikali na wananchi wa korogwe jukumu hilo zito lakini tutalifanya kwa ufanisi mkubwa “Alisema .


Mwisho.

KESI YA UCHOCHEZI INAYOWAKABILI VIONGOZI TISA WA CHADEMA YAKWAMA KUSIKILIZWA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeshindwa kuanza kusikiliza utetezi wa kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi tisa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akiwemo Mwenyekiti wake,  Freeman Mbowe , kwa sababu ya Mbunge wa Bunda Mjini Ester Bulaya, anaumwa.

Mapema, wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa kesi hiyo leo Oktoba 7,2019 imekuja kwa ajili ya kuanza kusikilizwa kwa ushahidi wa upande wa utetezi lakini mshtakiwa Bulaya hayupo.

Mdhamini wa Bulaya, Shukurwa Tungaraza  ambaye alikuwepo mahakamani hapo alidai mshitakiwa Bulaya ni mgonjwa na amelezwa hivyo anahitaji mapumziko kwa siku tatu mfululizo.

Baada ya kueleza hayo, Nchimbi alidai mshitakiwa atakuwa na mapumziko hadi Oktoba 10 na ukizingatia mahakama ilikuwa imepanga kusikiliza kesi hiyo mfululizo kwa wiki hii hivyo, wanaomba isikilizwe Oktoba 11, mwaka huu.

Mapema kabla ya taarufa hiyo ya kuugua Bulaya, wakili wa Utetezi, Profesa Abdallah Safari alidai wanashahidi mmoja ambaye ni Benson Kigaila na kwamba baada ya kujadiliana na upande wa mashitaka wanaomba kesi hiyo ianze kusikilizwa Oktoba 15,17, na 18.

Hakimu Simba alikubaliana na hoja hiyo na kuahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 15,16 na 18 mwaka huu kwa ajili ya kusikilizwa

Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine ni, Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Taifa Zanzibar, Salum Mwalimu,  Mbunge wa Kibamba, John Mnyika,  Mbunge wa Kawe  Halima Mdee, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, katibu mkuu, Vicent Mashinji, mbinhe wa Tarime Mjini Esther Matiko na Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya.

Wote wanakabiliwa na mashitaka 13 likiwemo la kula njama, ambapo wote wanadaiwa kuwa, Februari Mosi na 16, mwaka jana, Dar es Salaam walikuĺa njama ya kutenda kosa la kufanya mkusanyiko usio halali na kukiuka tamko kutawanyika.

RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA MSIKITI WA ISTIQAAMA BOMANI MJINI SUMBAWANGA, AHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA UWANJA WA NELSON MANDELA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dit. John Pombe Magufuli akivua viatu kabla ya kuingia na hatimaye kuufungua msikiti wa Istiqaama Bomani wa Mjini Sumbawanga leo Jumatatu Oktoba 7, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dit. John Pombe Magufuli akipata maelezo toka kwa Shehe wa Mkoa wa Rukwa Shehe Rashidi Akilimali kabla ya kuufungua msikiti wa Istiqaama Bomani wa Mjini Sumbawanga leo Jumatatu Oktoba 7, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Shehe wa Mkoa wa Rukwa Shehe Rashidi Akilimali na viongozi wengine akikata utepe kuufungua rasmi msikiti wa Istiqaama Bomani wa Mjini Sumbawanga leo Jumatatu Oktoba 7, 2019

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Shehe wa Mkoa wa Rukwa Shehe Rashidi Akilimali na viongozi wengine wakiitikia dua inayoongozwa na msaidizi wa Rais Alhaj Ali Masella baada ya kuufungua rasmi msikiti wa Istiqaama Bomani wa Mjini Sumbawanga leo Jumatatu Oktoba 7, 2019
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi mchango wa shillingi milioni tano kwa asili ya kukamilishia vifaa vya kuswalia kama vile mazulia Shehe wa Mkoa wa Rukwa Shehe Rashidi Akilimali akishuhuduiwa na viongozi wengine baada ya kuufungua rasmi msikiti wa Istiqaama Bomani wa Mjini Sumbawanga leo Jumatatu Oktoba 7, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi katika Uwanja wa Nelson Mandela Mjini Sumbawanga mkoani Rukwa leo Jumatatu Oktoba 7, 2019
Umati wa wananchi ukimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipowatuhutubia katika Uwanja wa Nelson Mandela Mjini Sumbawanga mkoani Rukwa leo Jumatatu Oktoba 7, 2019 PICHA NA IKULU

KOROGWE MINI MARATHON KUTUMIKA KUMUENZI BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE, KUTIMUA VUMBI OCTOBA 13 MWAKA HUU MJINI KOROGWE

$
0
0
MKUU wa wilaya Korogwe Kisa Gwakisa akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusiana Mashindano ya Riadhaa ya Korogwe Mini Marathon yanayotarajiwa kuanza kutumia vumbi Octoba 13 mwaka huu mjini humo ambayo yatatumika kumuenzi Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ikiwemo pia kuchangia maendeleo ya wilaya hiyo kulia ni Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano hayo Juma Mwajasho kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini Mary Chatanda na Afisa Tarafa ya Korogwe Michael John
Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano hayo Juma Mwajasho akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kisa Gwakisa,Mbunge wa Jimbo la Korogwe mjini Mary Chatanda na Afisa Tarafa ya Korogwe Michael John
MBUNGE wa Jimbo la Korogwe Mjini Mary Chatanda akizungumza kwenye mkutano huo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa kushoto ni Afisa Tarafa ya Korogwe Michael John
MKUU wa wilaya ya Korogwe Kisa Gwakisa katikati akimkabidhi medali za mashindano hayo Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano hayo Juma Mwajasho kulia kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Korogwe mjini (CCM) Mary Chatanda
MASHINDANO ya Riadhaa ya Korogwe Mini Marathon yanatarajiwa kuanza kutumia vumbi Octoba 13 mwaka huu mjini humo ambayo yatatumika kumuenzi Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ikiwemo pia kuchangia maendeleo ya wilaya hiyo.


MASHINDANO ya Riadhaa ya Korogwe Mini Marathon yanatarajiwa kuanza kutumia vumbi Octoba 13 mwaka huu mjini humo ambayo yatatumika kumuenzi Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ikiwemo pia kuchangia maendeleo ya wilaya hiyo.

Mashindano hayo yameandaliwa na Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa yakiwa na lengo la kuibua na kuendelea vipaji vya vijana wilayani humo ikiwemo kumuenzi Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa alisema kipindi hiki ni muhimu sana kutokana na kwamba watanzania wamempata Rais Dkt John Magufuli ambaye anafafana na Baba wa Taifa ambaye amekuwa akifanya kazi kubwa ya kuwapa watanzania maendeleo. 

Alisema lengo kubwa ni kumuenzi baba wa Taifa Nyerere ikiwa ni kutimiza miaka 20 ya kumuenzi lakini pia kuchangia maendeleo wilaya ya Korogwe huku akitoa wito kwa wananchi wajitokeza waungane pamoja kushiriki kwenye mashindano hayo.

“Wakati tunaadhimisha kumbukumbu ya Baba wa Taifa letu sisi Korogwe kupitia Mashindano ya Korogwe Mini Marathon sisi kama Korogwe tutakuwa tumetimiza jukumu letu la kumuenzi baba wa Taifa kwa vitendo”Alisema DC Kissa.

Aidha alisema kwamba watatumia mashindano hayo kuchangisha fedha kwa ajili ya kujenga madarasa 70 ya magufuli ambayo wanahitaji wadau wajitokeza kuwasaidia kwenye harakati hizo za kuhakikisha wanainua sekta ya elimu kwa kuondosha changamoto zilizopo

“Tunawashukuru sana Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) ambaye ni mdau namba moja wamechangia kwenye mashindano haya lakini pia wamewachangia milioni 30 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa nimeona kuna mwamko mkubwa kutokana na mashindano hayo sana lakini pia niwashukuru wadau wengine akiwemo Mwekezaji wa Mkonge Gomba, Klabu ya Sas Cyclne tunaamini kwa mchango wao tutafika mbalimbali sana “Alisema DC huyo 

Pia alisema kwamba wamejipanga kuhakikisha kunakuwa na mambo mazuri ambapo kutakuwa na kikimbia kilomita 5 ambapo Mkuu huyo wa wilaya atakimbia ,Kilomita 5 watakimbia pia walemavu kwa kutumia baiskeli na magongo huku akiwaomba wananchi wa Korogwe ambao ni wenyeji lakini nje kuna mwamko mkubwa sana.

Mkuu huyo wa wilaya aliwataka wanakorogwe kujitokeza kwa wingi huku akieleza kwamba wameongea na hifadhi ya Mkomazi ili waweze kupeleka wanyama kwenye mashindano hayo mahali yanapoanzia na yatakapokuwa yakiishia huku akiitaja Hotel ya Rocky Excutive Lodge wamekuwa wadau wakubwa kwenye mashindano hayo.

Awali akizungumza katika mkutano huo Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini (CCM) Mary Chatanda alisema kwamba wao wameunga mkono jambo hilo kwa ni jema wanawatangazia wananchi wajitokeza kwa wingi kwa kufanya hivyo watakuwa wamejitendea haki wenyewe .

Mbunge huyo alisema kwamba jambo hilo ni jema sana kwani kama alivyosema DC ni kupata fedha kwa ajili ya kuchangia maendeeo huku akiwataka vijana wajitokeze kwa ajili ya afya zao.“Niwahamasishe wananchi wa Korogwe mjini wajitokeze kwa wingi lakini pia wajasiriamali wajitokeze kwa wingi waweze kuweka mali zao kwenye mashindano hayo ili waweze kupata kipato kutokana na wanunuzi”Alisema.

Kwa upande wake Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano hayo Juma Mwajasho alisema kwamba mashindano hayo yatanzia kwenye viwanja vya Chuo cha Ualimu Korogwe na yatapita njia ya Dar- Arusha hadi kwenye mzunguko njia ya kuelekea Handeni na Kurejea yalipoanzia.

Alisema kwamba pia kutakuwa na mashindano ya baiskeli kilomita 60,Kilomita 10 ya kujifurahisha ikiwemo ya riadha ya Kilomita 10 na kiimota 5 ya kukimbia kujifurahisha huku akiweka bayana zawadi zenye thamani ya milioni 2 kwa ujumla zitatolewa na washiriki wote watakaomaliza kilomita 60 na 10 watapata medali.

Hata hivyo alisema kwamba wanategemea kupata washiriki wengi kwenye mashindano hayo ambapo zaidi ya washiriki 500 watashiriki kwenye mashindano hayo huku wengine wakitokea nchi jirani ya Kenya ambao wameunganishwa kupitia Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi.

SHIRIKA LA TTCL LAZINDUWA WIKI YA HUDUMA KWA MTEJA

$
0
0



Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Mh. Balozi Mteule Mohamed Mtonga (kushoto) akikata keki kuashiria uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja wa TTCL leo jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Corporation, Waziri Kindamba akishuhudia.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Mh. Balozi Mteule Mohamed Mtonga (kushoto) akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa TTCL Corporation, Waziri Kindamba (kulia) kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja wa TTCL leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Waziri Kindamba (wa pili kushoto) akimlisha keki Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Mh. Balozi Mteule Mohamed Mtonga mara baada ya kuzinduwa Wiki ya Huduma kwa Mteja wa TTCL iliyofanyika katika duka la huduma kwa wateja wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Mh. Balozi Mteule Mohamed Mtonga (kulia) akimlisha keki mmoja wa wateja wa TTCL kwenye hafla ya uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja wa TTCL leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Mh. Balozi Mteule Mohamed Mtonga (kushoto) akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja wa TTCL leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Waziri Kindamba.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Waziri Kindamba (kulia) akizungumza na wateja wa TTCL (hawapo pichani) kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja wa TTCL leo jijini Dar es Salaam.
Kulia ni mmoja wa wafanyakazi wa TTCL akimuhudumia mmoja wa wateja kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja wa TTCL leo jijini Dar es Salaam.
Kulia ni mmoja wa wafanyakazi wa TTCL akimuhudumia mmoja wa wateja kwenye uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja wa TTCL leo jijini Dar es Salaam.


SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation) leo limezinduwa rasmi maadhimisho ya wiki ya huduma kwa mteja huku likisisitiza kuwa shirika hilo litaendelea kuleta mapinduzi makubwa katika eneo la utoaji huduma pamoja na ubunifu kwenye bidhaa zake.

Akizinduwa maadhimisho hayo, Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Mh. Balozi Mteule Mohamed Mtonga amesema shirika litaendelea kufanya mapinduzi makubwa eneo la utoaji huduma pamoja na ubunifu katika bidhaa zake ili kuhimili ushindani uliopo sokoni.

Alisema ripoti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa mwaka unaoishia Desemba 2018, ilibaini kuwa TTCL ni Shirika la huduma za Mawasiliano linalokua kwa kasi, huku likiongoza kwa idadi ya ongezeko la wateja na hata huduma ya T PESA nayo ikitajwa miongoni mwa huduma zinazostawi kwa kasi kubwa.

"Hadi sasa, tumeweza kuwafikia asilimia 2 ya Wateja wa huduma za simu Nchini , yaani Wateja zaidi ya milioni mbili huku huduma ya T PESA ikifikisha Wateja zaidi ya laki nne, Mawakala elfu kumi na nne na miamala ya takribani Tsh bilioni tano za Kitanzania."

Aidha alisema katika kuwajali zaidi wateja wake kihuduma TTCL imezinduwa rasmi huduma ya TTCL App na namba maalum ya WhatApp ya Huduma kwa wateja kuboresha zaidi huduma zake.

Akifafanua zaidi juu ya huduma hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Waziri Kindamba aliongeza kuwa kila mwaka, wamekuwa wakiwapatia wateja wao huduma mpya na huduma ya mwaka huu itaenda sambamba na utoaji wa zawadi kemkem za kuonesha shukrani kwa wajeja wao.

"Mwaka huu 2019, tunawaletea huduma ya TTCL App ambayo ni Application itakayowawezesha Wateja wa TTCL Corporation kujiunga na vifurushi, kuongeza salio na kupata salio la akaunti yake kupitia simu za mkononi (i.e simu janja) na tablets."

Akifafanua zaida huduma hizo, alisema ndani ya TTCL App mteja ataweza kuongeza na kuangalia salio kupitia App hiyo itakayopatikana bure kwa wateja wa TTCL bila kujali kama ana kifurushi cha intaneti muda huo.Wateja watakaotumia TTCL App wataweza kupata huduma za ziada kama dondoo za afya, soko la hisa na kubadilisha fedha, kuona matangazo mbalimbali ya TTCL, kuunga kifurushi kwa namba nyingine, kumnunulia rafiki muda wa maongezi nk.

"TTCL App haitaji usajili maalumu ili kutumia. Sisi tumetimiza wajibu wetu, kazi kwenu Wateja wetu, kufurahia huduma hii nzuri na rahisi sana kuitumia. Pamoja na TTCL App, tumewaongezea Wateja wetu njia nyingine rahisi ya kuwasiliana nasi kupitia Huduma ya WhatsApp ambapo kwa namba 0738 151511, alisema.
Huduma zikiendelea kwenye duka la TTCL Samora jijini Dar es Salaam sambamba na maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Mteja.
Tupo tayari kuwahudumia wateja wetu kwa bashasha...! Ndivyo wanavyoonekana watoa huduma wa TTCL kwenye maadhimisho hayo.

MTENDAJI MKUU AMUELEKEZA MKANDARASI KUKAMILISHA HARAKA JENGO LA MAHAKAMA -MANYARA

$
0
0
Na Christopher Msagati, Mahakama ya Hakimu Mkazi-Manyara 
Mtendaji Mkuu- Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga amefanya ukaguzi katika jengo jipya la Mahakama ya Hakimu Mkazi Manyara na kuridhishwa na  hatua ya jengo hilo lilipofikia. 

Akikagua jengo hilo mapema Oktoba 06, 2019, Bw. Kattanga alisema, “hatua ya jengo lilipofikia ni nzuri, hata hivyo natoa rai kwa Mkandarasi kukamilisha marekebisho madogo yaliyotolewa ili kazi za Mahakama ziendelee.”

Pamoja na Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Wajumbe wengine walioambatana nae katika ukaguzi huo ni pamoja na Mhandisi Mkadiriaji Majengo kutoka Mahakama ya Tanzania, Bw. Raphael Bandiho, Wakandarasi wa jengo hilo kutoka Kampuni ya Vumwe General Services and Supplies Limited (VGSS),  Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)- Mkoa wa Manyara.

Wengine ni Wasimamizi na washauri katika mradi huu, Tanzania Electrical, Mechanical and Electronics Services Agency (TEMESA-Mkoa wa Manyara) pamoja na wenyeji ambao ni Mtendaji wa Mahakama Mkoa wa Manyara, Bw. Jacob Swalle, Hakimu Mkazi Mfawidhi Mkoa wa Manyara, Mhe. Simon Kobero na Afisa Tawala wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Manyara Bwana Christopher Msagati.

Kwa kipindi kirefu, Mahakama ya Hakimu Mkazi Manyara ilikuwa ikitumia jengo la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM- Manyara) wakati wakisubiri jengo hilo la Mahakama likamilike. 

Aidha; ilipofika mwezi Agosti mwaka huu shughuli za kuhamia katika jengo hilo jipya zilianza rasmi na walihamia katika upande mmoja wa Jengo ambao tayari ulikuwa umekamilika wakati Mkandarasi akiendelea kukamilisha upande mwingine wa jengo.

Inatarajiwa kuwa mradi wa jengo hili utakamilika hivi karibuni ndipo likabidhiwe rasmi kwa Mahakama kuendelea na shughuli zake kikamilifu.
 Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Bw. Hussein Kattanga  (wa tatu kulia) akionyeshwa kitu na Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Manyara pindi alipokuwa akikagua jengo la jipya la Mahakama ya Hakimu Mkazi Manyara, Bw. Jacob Swalle pindi alipokuwa akikagua jengo jipya la Mahakama hiyo lililopo katika hatua za mwisho za ukamilishwaji wake.
 Muonekano wa jengo jipya la Mahakama ya Hakimu Mkazi-Manyara lililopo katika hatua za mwisho za ukamilishwaji wa marekebisho madogo madogo.
 Mtendaji Mkuu-Mahakama Hussein Kattanga   akizungumza jambo wakati wa ukaguzi wa jengo hilo

Mtendaji Mkuu-Mahakama ya Tanzania, Bw. Kattanga akiendelea na ukaguzi.

MKURUGENZI MANISPAA YA SINGIDA AAGIZWA AWAONDOE WAKUSANYA MAPATO WATATU

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwagiza Mkurugenzi Manispaa ya Singida, Bw. Bravo Lyapembile awaondoe kazini watumishi watatu wanaokusanya mapato kwenye stendi ya mabasi ambao wameajiriwa kindugu na wanatumiwa kuiba mapato.

Ametoa agizo hilo leo (Jumatatu, Oktoba 7, 2019), akizungumza na madiwani na watumishi wa Manispaa ya Singida pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Singida kwenye mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Roman Catholic, mjini Singida.

“Kuna vijana watatu pale stendi ambao mmewaweka kindugu. Yupo Kennedy Francis (mtoto wa Mkurugenzi); Selemani Msuwa (ndugu yake diwani) na Salehe Rajab Kundya (shemeji yake diwani mwingine). Andika barua leo hii, hawa vijana waondoke kwenye hiyo kazi, na upeleke timu nyingine ya watu waaminifu,” amesema.

Waziri Mkuu amesema kuna mchezo unachezwa wa kukusanya mapato lakini hayapelekwi benki na wahusika wakuu ni ni mweka hazina wa Manispaa, Bw. Aminieli Kamunde na Mkaguzi wa Ndani, Bw. Ibrahim Makana.

Amewaonya watendaji wa kata wanaohusika kukusanya mapato wahakikishe kuwa kila wanapokamilisha makusanyo, wanazipeleka fedha hizo benki na kupatiwa risiti. “Kuna wakusanyaji wanaoshirikiana na baadhi ya Wakurugenzi na Waweka Hazina. Waheshimiwa Madiwani hakikisheni mnasimamia hizo mashine zinazokusanya mapato na mjue ni nani amepatiwa. Ombeni taarifa mjue nani anayo na yuko wapi.”

“Ninawasihi Mstahiki Meya na Mwenyekiti wa Halmashauri msiingie kwenye huu mkumbo kwa sababu tunataka fedha zilizokusanywa kutoka kwa wananchi zirudi kuwahudumia wananchi.”

Waziri Mkuu amekemea tabia ambayo ameikuta kwenye Halmashauri nyingine ya kubadilisha matumizi ya fedha ambako Mkurugenzi au Mweka Hazina wanawadai watendaji wa kata wawapatie shilingi milioni mbili. “Kwenye eneo hilo, msikubali kupeleka fedha mkononi kwa afisa yoyote. Ninyi pelekeni benki na mpatiwe risiti,” amesisitiza.

Amesema tabia nyingine ambayo ameikuta katika ziara hii, ni kubadilishwa kwa matumizi ya fedha na kuacha malengo kusudiwa ya fedha zilizotumwa. “Fedha inayotoka Serikali kuu ikiletwa inakuja na maelekezo mahsusi. Unakuta fedha inakuja kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya, wao wanahmisha na kujilipa posho au inahamishiwa kwenye mradi mwingine.”

“Au unakuta fedha la kulipa likizo za walimu inatumika kwenye miradi ya afya, na Afisa Elimu upo. Na unajua kwamba walimu wanadai likizo zao, unaona sawa tu. Ni lazima tuchukue hatua kwa sababu huu ni mwaka wa nne wa Serikali ya awamu ya tano, na wanajua nini Serikali hii inataka. Tukiwaachia, wataendelea kufanya ubadhirifu tena na tena.”

“Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi, simamieni mapato ya ndani na siyo muwe sehemu ya ulaji wa fedha za umma. Waheshimiwa Madiwani simamieni sheria inayosimamia utoaji iwa asilimia 10 ya mapato kwa wanawake, vijana na wenye ulemavu ili kila mmoja apate haki yake,” alisisitiza.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Singida, Bw. Rashid Mandoa akamilishe malipo ya madiwani ambayo ni malimbikizo. “Nenda kalipe malimbikizo ya wadiwani ambayo yanafikia shilingi milioni 104,” alisema.

Pia amemtaka awasilishe kwenye mfuko wa Hifadhi ya jamii, michango ya madereva ya sh. 15,000 ambayo wamekuwa wakikatwa tangu mwaka 2015/2016 lakini haijawasilishwa. “Hawa walikuwa LAPF, wamekatwa hela zao lakini bado hazijapelekwa.”

“Watu hao pia wamekuwa wakikatwa sh. 5,500 za Bima ya Afya tangu wakati huo lakini hadi sasa michango yao haijawasilishwa na matokeo yake wakienda hospitali hawatibiwi. Hakikisha malipo yao yanaenda,” alisema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB agawa chai kwa wateja

$
0
0
MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, amewaongoza baadhi ya watendaji wa benki hiyo kugawa chai kwa wateja wao.

Akizungumza akiwa kwenye tawi la Kariakoo Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja, Nsekela alisema ni wiki muhimu kwa wateja wa CRDB.

Alisema ni wiki ya viongozi wa benki hiyo kutoka matawi yote kuwafuata na kuwahudumia wateja kwa upendo chini ya kaulimbiu ya 'Ulipo tupo kukupa Magic'.

"Hii ni wiki ya huduma kwa wateja duniani kaulimbiu ya dunia ni 'The magic of service' na sisi benki yetu tunashiriki kwa kuwahudumia wateja wetu.

"Tunawaambia ulipo tupo kukupa Magic. Tumeandaa vitu vingi vizuri naamini wateja wetu watafurahia," alisema Nsekela.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akifungua Shampeni kuashiria kuanza kwa wiki ya huduma kwa wateja inayoadhimishwa sehemu mbalimbali duniani, katika hafla iliyofanyika kwenye tawi ya Benki ya CRDB, Karikoo jijini Dar es salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akimiminia Shampeni  mmoja wa wateja wa Benki hiyo, waliofika kupata huduma kwenye tawi ya Benki ya CRDB, Karikoo jijini Dar es salaam.











TAZARA YATEKELEZA AGIZO LA RAIS DKT MAGUFULI LA KUSAFIRISHA SHEHENA YA MAHINDI KWENDA ZIMBABWE

$
0
0
TAZARA imetekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli ,la kusafirisha shehena ya Mahindi tani Elfu 17,ambazo imeelezwa kuwa zitasafirishwa kwa awamu mbili kutoka Tanzania kwenda nchini Zimbawe,ambapo awamu ya kwanza imekwishaanza.

KIGWANGALA ATOA SIKU 14 KWA MANAIBU KATIBU WAKUU NA KATIBU MKUU KUWASILISHA MCHAKATO WA MSWAADA WA SHERIA UUNDWAJI JESHI USSU

$
0
0
Baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya jeshi ussu wakionyesha uwezo wao wa kupanga risasi ndani ya dakika mbili kwenye maonesho yaliyofanyika mbele ya Mhe.Waziri wa utalii na maliasili.
Gwaride la wahitimu wa mafunzo ya jeshi ussu wakipita mbele ya Waziri wa utalii na maliasili katika sherehe hizo.
Mmoja wa wahitimu wa mafunzo ya awali ya jeshi ussu akipita juu ya kamba katika moja ya maonesho yaliyofanyika mbele ya waziri wa utalii na maliasili Mhe.Khamis Kigwangaka katika sherehe ya kuhitimisha mafunzo hayo

Na Jusline Marco-Arusha

Waziri wa maliasili na utalii Dkt.Khamis Kigwangala ametoa siku 14 kwa manaibu katibu wakuu na katibu mkuu wa wizara hiyo kuwasilisha mchakato wa mswada wa sheria ya uundwaji Jeshi Ussu ofisini kwake ili iweze kuwasilisha bungeni.

Ametoa agizo hilo katika sherehe za kuhitimisha mafunzo ya Awali ya Jeshi Ussu katika kituo cha mafunzo cha Mbulu-mbulu kilichopo katika kata ya Kambi ya simba,Wilayani Karatu Mkoani Arusha.

Dkt.Kigwangala amesema kuwa kutokukamilika kwa mswada huo ni mapungufu ya wizara kwani amekuwa akielekeza mara kadhaa mswada huo ukamilike na umekuwa haukamilishwi.

"Katika maagizo niliyopewa na Mhe.Rais sikusudii kujiona nikitumbuliwa kwasababu ya kuchelewa kutimiza wajibu wangu,"Alisema Dkt.Kigwangala huku akiongeza kuwa kama ni madokezo ameandika mara kadhaa lakini wamekuwa wakijivuta.

Ameongeza kuwa kwa  zaidi ya miaka kumi tangu ilipoelekezwa na sheria ya uhifadhi ya wanyamapori haijawahi kuanza ila kwasasa taasisi mbalimbali za uhifadhi wa wanyamapori zimeanza kuonyesha bidii katika kuwapatia mafunzo wafanyakazi wao kwenye eneo la Jeshi Ussu.

Vilevile ametoa jukumu kwa bodi ya mamlaka ya uhifadhi wa wanyamapori Ngorongoro kupeleka ushauri wa mapendekezo yaliyotolewa ya kufanya kiwtuo hicho kuwa kamili kwa kuangalia vigezo vyote vitakavyowezesha kufanya kituo hicho kuwa kituo cha kudumu.

Awali akitoa risala yake kwa mgeni rasmi  mkuu wa kutuo hicho Kanali Martin kilugha  amesema kuwa jumla ya wahitimu wa mafunzo hayo ni 112 ambapo katika mafunzo hayo wakufunzi wa ndani wametumika,wakufunzi wa hifadhi pamoja na wakufunzi wa muda kutoka katika jeshi la JWTZ kwa ajili ya kuimarisha Jeshi Ussu.

Amesema kuwa wahitimu hao wamefundishwa mafunzo mbalimbali ya uhifadhi ikiwemo utimamu wa mwili,na ulinzi wa nadharia na vitendo na kufaulu kwa madaraja mbalimbali.

Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Mrisho Gambo amesema kuwa kumekuwa na matukio mengi ya ujangili ya kuuawa kwa wanyama hivyo wahitimu wa mafunzo hayo wanapaswa kufahamu kuwa wanajukumu kubwa la kuhakikisha wanalinda rasilimali za nchi.

"Niwaomba wahitimu walio chini ya uongozi wako Mhe.Waziri wakapambane na ujangili ili kukomesha mchezo huo na rasilimali za nchi ziweze kuwa salama kwa faida ya wananchi kwani huo ndio msimamo wa Rais wetu ndiyo maana ameridhia tuende kwenye mfumo wa kijeshi kama sehemu yake ya kuonyesha dhamira ya kupambana na ujangili na kulinda rasilimali zetu".Amesema  Mkuu huyo.

WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI YAJIPANGA KUCHANGIA PATO LA TAIFA KWA ASILIMIA 10-PROFESA OLE GABRIEL

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

KATIBU Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel, amesema sekta ya mifugo na uvuvi inachangia takribani asilimia 7.9 ya pato la Taifa.

Wazara hiyo imejipanga huku kuboresha sekta hiyo na kutarajia kufikia asilimia 10 hadi 25 ifikapo 2025 pamoja na uzalishaji wa malighafi katika sekta ya viwanda .

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa wadau wa Sekta ya Mifugo wakiwemo wastaafu, Ole Gabriel amesema uboreshwaj kwa sekta hiyo kutafanya Tanzania kuwa ya viwanda na kuwafanya wafugaji kuwa na uchumi wa kati ikiwa ni kuchana na ufugaji wa mazoea.

Amesema ili kufikia lengo la kuongeza pato la taifa watanzania wanapaswa kupenda vitu vya ndani na kuhakikisha wananunua bidhaa za ngozi zinazotokana na mifugo hali ambayo italeta tija kwa nchi.

“Tatizo kubwa la Watanzania bado wanaumwa ugonjwa wa kununua vitu vya nje na sio ndani ya nchi wakiamini ndio bora wakati bidhaa zilizopo ni bora sana kwani uzalishaji madawa ya mifugo na vyakula vyake vinazalishwa hapa hapa nchini ”alisema Prof. Ole Gabriel

Aidha alisema Wastaafu waliofanya kazi katika sekta hiyo wanawajibu wa kuendelea kuisaidia serikali ya awamu ya tano katika kutoa mafunzo mbalimbali katika vyuo vya mifugo ili mchango wao uendelee kuonekana katika jamii.

Prof. Ole Gabriel alisema katika mkutano huo watapata fursa ya kujadili mambo saba ikiwemo namna ya kuondoa vikwazo vya biashara ya mifugo ndani na nje ya nchi,kushauriana namna ya uboreshaji wa viwanda vya Mifugo,Namna ya kupata pembejeo za Mifugo kwa bei nafuu,Kudhibiti uingizaji wa mazao ya mifugo na mifugo ambayo zipo chini ya viwango na kujadili Mkakati wa uboreshaji wa Sekta ya mifugo.

Nae Mdau wa Uzalishaji wa Dawa za Mifugo wa Kampuni ya Farm Base Salim Mselemu amesema kuwa wanashirikiana na serikali vizuri kwa kuwaamini katika dawa.

Amesema kuwa Farm Base ni kampuni ya wazawa hivyo nia yao ni kuona wafugaji wanapata bidhaa bora katika kuendeleza sekta ya mifugo nchin.

“Wafugaji wengi wanafuga kwa mazoea wanaangalia bei ya kuuza na sio kuangalia bei ya gharama alizotumia katika utunzaji wa mifugo yake nah ii inawaangusha wafugaji wengi,”alisema Prof. Ole Gabriel

Kwa Upande wake Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Dkt Mary Mashingo alisema wanaishukuru wizara hiyo kwa kuwakutanisha pamoja katika mkutano huo na kujadili masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya mifugo.

“Mataifa mengi wazee waliostaafu katika sekta mbalimbali wamekuwa wanafanya kazi na kujitoa katika kutoa utaalamu wao huku wakijipangia muda wa kufanya kazi hizo,”alisema.
Bidhaa za Dawa zinazozalishwa na Farm Base wakionesha katika Mkutano Wastaafu wa Wizara hiyo pamoja na wadau sekta  Uvuvi uliofanyika jijini Dar es Salaam
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza na Wastaafu wa Wizara hiyo pamoja na wadau sekta  Uvuvi katika Mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu Mstaafu  wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi  Dkt Mary Mashingo akitoa namna sekta ya mifugo inavyoweza kuwa na mchango kwa wafugaji kupata mikopo Benki ya TIB Wastaafu wa Wizara hiyo pamoja na wadau sekta  Uvuvi katika Mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wastaafu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na wadau wa Mifugo wa Uvuvi katika Mkutano wa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel.
 Mdau wa Uzalishaji wa Dawa za Mifugo wa Kampuni ya Farm Base Salim Mselemu akizungumza namna wanavyoshirikiana serikali katika uzalishaji wa dawa za mifugo katika Mkutano wa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Elisante Ole Gabriel akiwa katika picha  ya pamoja Wastaafu wa Wizara hiyo pamoja na wadau sekta  Uvuvi uliofanyika jijini Dar es Salaam..

Kampuni ya Tigo yazindua maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja kwa kuhimiza ubora wa huduma.

$
0
0
Meneja wa Huduma kwa wateja wa Tigo , Mwangaza Matotola akizungumza na waandishi wa habari Mapema leo katika uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja .Mkutano ulifanyika Kituo cha huduma kwa wateja cha Tigo,Jijini Dar Es Salaam. 
Wafanyakazi wa kiting cha huduma kwa wateja wakipozi kwa picha mara baada ya uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja .Mkutano ulifanyika Kituo cha huduma kwa wateja cha Tigo,Jijini Dar Es Salaam. 
Meneja wa Huduma kwa wateja wa Tigo , Mwangaza Matotola akiwa katika picha ya Pamoja na wafanyakazi wa kitenge cha huduma kwa wateja mara baada ya uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja .Mkutano ulifanyika Kituo cha huduma kwa wateja cha Tigo,Jijini Dar Es Salaam.


 Kampuni inayolenga kuleta mageuzi ya kidijitali katika maisha ya watanzania, Tigo, leo imezindua maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja kwa kutambua mchango wa watoa huduma wake katika kuhakikisha wateja wanapata huduma zenye ubora.

Wiki hiyo inayoadhimishwa ulimwenguni kote imebeba kauli mbiu isemayo “Magic of Service” yaani huduma ya maajabu na imezinduliwa rasmi leo na itamalizika Oktoba 11.

Akizungumza wakati wa hafla iliyofanyika katika Kituo cha huduma kwa wateja cha Tigo, Meneja wa Huduma kwa wateja, Mwangaza Matotola amesema wiki hii itaadhimishwa kwa aina yake kwa kuhimiza ubora wa huduma ili kuendana na mahitaji ya wateja.

“Huduma kwa wateja ni kitovu cha biashara yetu na ndiyo maana tunaweka kipaumbele katika kuhakikisha wateja wanapata huduma zenye ubora na weledi siku zote hivyo katika wiki hii tumejizatiti kuhimiza dhamira yetu ya kutoa huduma zenye kukidhi mahitaji ya wateja,” alisema Matotola.

Wiki hiyo itaambatana na matukio mbalimbali ikiwamo kutembelea kituo cha huduma kwa wateja, kujumuika na wateja pamoja na wadau ili kujadili namna bora zaidi ya kuendeleza huduma za kampuni hiyo.Meneja huyo aliwahimiza wateja kutumia huduma mbalimbali za kimtandao kama WhatsApp, Twitter, Facebook na Instagram pale wanapohitaji huduma au msaada kutoka kwa wataalamu wenye weledi.

“Tigo imeendelea kuwekeza katika kuboresha huduma kwa kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wetu na zaidi tumewekeza zaidi katika kujenga miundombinu ya kituo chetu cha mawasiliano ili kuhakiisha wateja wanapata huduma za uhakika,” alisema

Aidha, wiki hiyo itahitimishwa kwa kutoa tuzo kwa mfanyakazi bora wa mwaka ambaye ameonesha weledi mkubwa katika utoaji wa huduma ikiwa ni njia ya kutoa hamasa kwa wafanyakazi wengine.

Serikali yaahidi kuwawekea mazingira mazuri wawekezaji

$
0
0
Na woinde shizza, Arusha .

SERIKALI  imesema kuwa itahakikisha inaendelea kushirikiana na
wawekezaji hapa nchini ikiwa ni pamoja na kuwawekea  mazingira mazuri
ili waweze kufanya shughuli zao pasipo kuwa na bughudha  zozote,kwani
wamekuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa pato la Taifa.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Mifugo,Elisante Ole Gabriel
aliyasema hayo mwishoni mwa wiki alipokuwa katika ziara yake ya
kutembelea kiwanda cha kusindika nyama cha Happy Sausage kilichopo
Sakina jijini hapa.

“Wawekezaji wamekuwa na mchango mkubwa sana katika kuinua pato la
taifa pamoja na uchumi wa n chi kwa ujumla ikiwa ni pamoja na
kuchangia kupatikana kwa ajira nyingi kwa wananchi hivyo hawana budi
kuthaminiwa kwa mchango wao huo’’alisema Katibu Mkuu huyo.

Ole Gabriel alisema kuwa anatambua changamoto mbalimbali
zinazokikabili kiwanda hicho cha Happy Sausage ikiwemo mgogoro wa muda mrefu kati yake na halimashauri ya jiji la Arusha hali ambyo imekuwa
ikichangia kusuasua kwa uzalishaji na kuhahidi kulipatia ufumbuzi
ndani ya muda mchache.

Awali akimkaribisha Katibu Mkuu huyo,Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa kiwanda hicho,Andrew Mollel alimweleza katibu mkuu huyo kuwa kiwanda hicho kilianzishwa mwaka 1990 na kwamba kimekuwa kikizalisha bidhaa zenye ubora ambapo kwa sasa kimejipanga kutanua soko lao kufikia nchi zote za Afrika Mashariki.

“Kiwanda kimeshindwa kufikia malengo ya kuongeza uzalishaji kutokana
na kujikuta ikikwamishwa kufanya ukarabati wa kiwanda hicho ilihali
serikali kupitia vizara ya mifugo na uvuvi kwa nyakati tofauti imekuwa
ikikitaka kiwanda hicho kufanya ukarabati imekuwa ndio changamoto yetu
kufikia malengo ya uzalishaji”.alisema Mollel

Mwenyekiti huyo wa bodi aliongeza kuwa pia halimashauri ya jiji la
Arusha imekuwa ikikwamisha ukuaji wa kiwanda hicho kwani imekataa
kutoa kibali cha ukarabati na upanuzi wa majengo ya kiwanda
hicho(building permit) jambo linalokwamisha uongezaji wa thamani na
uzalishaji hali ambayo imekuwa  ni changamoto kubwa sana kwao na
kuiomba serikali kuu kuu kuingilia kati.

Mollel aliiomba Serikali kumpatia eneo lenye ukubwa wa ekari 300
katika eneo la Muriet jijini hapa ili aweze kuanzisha shamba kubwa la
mifugo litakalokiwezesha kiwanda hicho kufuga mifugo mingi ikiwemo
nguruwe kwani tayari  wamekwishafanya mazungumzo na serikali ya
Ujerumani ambapo imewaahidi kuwapatia mbegu za nguruwe wanaokua kwa muda mfupi ukilinganisha na  wa hapa Tanzania ambao huchukua muda mrefu kukua.
 Picha ikionyesha  Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Mifugo,Elisante ole Gabriel akikagua ngozi wakati alipofanya ziara juzi ya kutembelea kiwanda cha ngozi cha Salex kilichopo jijini  Arusha ambapo alisifia Kiwanda hicho kwajinsi kinavyofanya kazi nakubainisha kuwa serikali ipo nao bega kwa bega kulia kwakwe ni Meneja wa kiwanda hicho Paulo Dismas (Picha na Woinde shizza, Arusha 
Mwenyekiti Wa bodi ya kiwanda cha Happy sausage Andrew Mollel watatu Julia akimueleza katibu mkuu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Mifugo,Elisante ole Gabrieli alieshika nyama jinsi wanavyochambua Nyama kwaajili ya kutengeneza sausage ambapo alisema mifupa inayobaki wanaiweka kwa ajili Ya kuwauzia watu wanaotengenezea chakula cha kuku


RAIS DKT. MAGUFULI AHUTUBIA WANANCHI WA SUMBAWANGA MKOANI RUKWA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mamia wa wananchi wa Sumbawanga katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa mpira wa Nelson Mandela mkoani Rukwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mamia wa wananchi wa Sumbawanga katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa mpira wa Nelson Mandela mkoani Rukwa
Sehemu ya Wananchi wa Sumbawanga waliohudhuria mkutano wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli uliofanyika katika uwanja wa mpira wa Nelson Mandela mkoani Rukwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi wa Sumbawanga mara baada ya kuwahutubia katika uwanja wa mpira wa Nelson Mandela mkoani Rukwa. PICHA NA IKULU


KUFUATA MIONGOZO HUPUNGUZA USUGU WA WADUDU DHIDI YA DAWA

$
0
0
Mwakilishi kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) Bi. Comfort King-Giboie akisisitiza jambo mbele ya timu ya Afya ngazi ya Mkoa (RHMTs) juu ya namna ya kujikinga dhidi ya maambukizi kwa kufuata miongozo (IPC guideline) katika Mkoa wa Kigoma.
Wataalamu wa Afya ngazi ya Mkoa wakifuatilia kwa makini mafunzo ya namna ya kujikinga dhidi ya maambukizi kwa kufuata miongozo ya IPC, yaliyoandaliwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Shirika lisilo Lakiserikali la MSH kupitia mradi wa MTaPS.
Afisa kutoka Kitengo cha Uhakika Ubora, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Erick Kinyenje akitoa mafunzo ya namna yakuchanganya dawa za kuua vijidudu mbalimbali katika maeneo yakutolea huduma za Afya.Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dkt. Paul Chaote aakieleza jambo mbele ya Watoa huduma za Afya ngazi ya Mkoa, wakati wa mafunzo ya namna bora yakujikinga dhidi ya maambukizi mkoani Kigoma.


Na WAMJW – KIGOMA

Watumishi wa Sekta ya Afya nchini, wameaswa kufuata miongozo na taratibu za utoaji huduma za Afya wakati wa kutoa huduma kwa mgonjwa (IPC Standards) ili kupunguza tatizo la usugu wa wadudu dhidi ya dawa.

Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dkt. Paul Chaote, wakati akifungua mafunzo ya namna ya kujikinga dhidi ya maambukizi kwa kufuata miongozo (IPC Guidline) wakati wa kumuudumia mgonjwa Mkoani Kigoma.

Dkt. Paul Chaote amesema kuwa usugu wa dawa ni moja kati ya tishio kubwa kwa Afya ya binadamu nchini, huku akidai kuwa Shirika la Afya Duniani (WHO) limeshauri nchi wanachama kuanzisha mikakati ya kukabili dhidi ya tatizo hili.

“Usugu wa dawa umekuwa moja ya tishio kubwa kwa Afya ya Wananchi katika jamii, hivyo Shirika la Afya Duniani (WHO) linashauri kuanzishwa kwa afua/mikakati mbali mbali ili kuweza kupambana na tatizo hili la usugu” Alisema Dkt. Paul Chaote.

Dkt. Paul Chaote aliendelea kusema, matumizi ya dawa yasiyo na ulazima yanaweza kupelekea tatizo la usugu wa wadudu dhidi ya dawa, huku akisisitiza kufuata miongozo ya njia za kukinga (IPC Standards) wakati wa kumuhudumia mgonjwa, kama njia kuu ya kupambana dhidi ya usugu wa wadudu dhidi ya dawa.

“Kufuata miongozo ya IPC (Infection, Prevention, Control) ni njia yenye gharama nafuu ambayo tunaweza kuifanya, ambayo itakuwa msaada mkubwa katika lengo letu la kupambana dhidi ya usugu wa wadudu dhidi ya dawa” Alisema Dkt. Chaote.

Naye, Afisa kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Boniface Marwa amesema kuwa takwimu zinaonesha kuwa watu 700,00/ hufariki Dunia kutokana na tatizo linalosababishwa na usugu wa wadudu dhidi ya dawa, huku akidai kuwa asilimia 89% ya vifo hivyo hutokea Barani Afrika na Asia.

Aliendelea kwa kusisitiza kuwa jitihada za makusudi ni lazima zichukuliwe na kila mtaalamu katika Sekta ya Afya ili kupambana na tatizo hili linalozidi kuwa tishio Duniani, huku akisisitiza juu ya kufanya tafiti mbali mbali ili kupata dawa mpya zitazoweza kupambana na wadudu sugu.

“Takribani watu 700,000 hufariki Duniani, kutokana na tatizo la usugu wa wadudu dhidi ya dawa, na asilimia 89% ya vifo hivyo hutokea Barani Afrika na Asia” Alisema Dkt. Boniface Marwa.

Kwa upande wake Afisa kutoka Kitengo cha Uhakiki Ubora, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Erick Kinyenje amewataka Wataalamu kutoka Sekta ya Afya mkoa wa Kigoma kuhakikisha wanapeleka Elimu juu ya muongozo wa kudhibiti na kukinga magonjwa (IPC Guidline) walioipata kwa watumishi wenzao katika maeneo yao ya kutolea huduma za Afya ili kukinga maambukizi katika maeneo hayo.

“Niwaombe mtusaidie kuifikisha Elimu hii mlioipata hapa kwa wWataalamu katika maeneo yenu yakutolea huduma za Afya, na kuisambaza miongozo hii ya njia bora za kukinga na kudhibiti maambukizi ya magonjwa katika maeneo hayo, hii itasaidia kupunguza maambukizi na jambo litalosaidia kupunguza usugu wa wadudu dhidi ya dawa”, alisema Bw. Erick Kinyenje.

Mafunzo hayo yaliyofadhiliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Management Science for Health (MSH) kupitia mradi wa Medicines, Technology and Pharmaceutical Services (MTaPS), yanatarajia kuendelea katika mikoa yote iliyo katika hatari ya kupata ugonjwa wa Ebola ili kuhakikisha ugonjwa huo hauingii nchini.

VIGOGO SITA WA KAMPUNI YA SIX TELECOM AKIWEMO WAKILI DK.TENGA WAHUKUMIWA KULIPA FAINI YA MILIONI 155/- AU KIFUNGO CHA KWENDA JELA MWAKA MMOJA

$
0
0
Na Karama Kenyunko,  Michuzi TV

VIGOGO sita wa Kampuni ya Six Telecom akiwemo Wakili  maarufu Dk. Ringo Tenga wamehukumiwa kulipa faini ya Sh.milioni 155 au kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela. 

Pia wamehukumiwa kulipa fidia ya dola za Marekani 3,748,751.19 ambayo ni sawa na takribani Sh.milioni nane za Tanzania

Aidha washitakiwa hao kila mmoja ametakiwa leo leo kulipa dola 150,000 kila mmoja mbayo tayari  wameishalipa. Pia Mahakama imeamuru kutaifishwa kwa nyumba ya washitakiwa iliyopo Mikocheni kiwanja Namba 33 yenye  thamani ya zaidi ya Sh.bilioni moja.

Mbali na Tenga, washitakiwa wengine waliohukumiwa ni Hafidhi Shamte au Rashidi Shamte ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni wa hiyo, mfanyabiashara na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Peter Noni, Mkuu wa fedha wa kampuni hiyo Noel Chacha, Kampuni ya Six Telecoms na Frank Mwalongo.

Akisoma adhabu hiyo leo Oktoba 7,mwaka 2019 Hakimu Simba amesema katika kosa la kwanza, mshitakiwa wa kwanza hadi watano, atatakiwa kulipa faini ya Sh.milioni 10 kila mmoja au kifungo cha miezi 10, katika shtaka la pili washtakiwa hao watatakiwa kulipa faini ya Sh milioni 10 au kifungo miezi 12.

Katika shtaka la tatu, washitakiwa wametakiwa kulipa faini ya Sh.milioni tano au kifungo cha miezi 12 huku katika shtaka la nne watatakiwa kulipa faini ya Sh.milioni tano.

Aidha, Hakimu Simba ametoa amri sita ikiwemo washitakiwa kulipa fidia ya dola 3,748,751.19, washitakiwa kulipa dola 150,0000 na kiasi kilichosalia ambazo ni dola  3,581,115 ilipwe ndani ya miezi sita kuanzia leo.

Pia amesema, mshitakiwa wa sita ambaye ameunganishwa katika kesi hiyo atatakiwa kulipa faini ya Sh.milioni 30.Hakimu Simba amesema, endapo washitakiwa watashindwa kufanya hivyo DPP anamlaka ya kuchukua hatua za kisheria .

Mapema kabla ya kusomwa kwa adhabu hiyo, Wakili wa Serikali Mkuu Faraja Nchimbi alidai washtakiwa hao ni wakosaji wa kwanza kwani hawana kumbukumbu ya makosa ya nyuma ya washitakiwa,.pia ameiomba Mahakama katika kutoa adhabu, ifikirie kutoa adhabu chini ya kifungu cha 194 cha Sheria namba 4 ya 2019 ikizingatia makubaliano waliyoingia kati ya upande wa mashitaka na washitakiwa na kusajiliwa katika mahakama hiyo.

Alidai Mahakama itoe amri kwa washitakiwa kulipa fidia ya Dola za Marekani 3,748,751.19 na mshitakiwa wa kwanza hadi wa tano, walipe leo fidia ya Dola za Marekani 150,000 na wakubali kukabidhi nyumba iliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam

Pia alidai mshitakiwa wa kwanza hadi wa tano atatakiwa kulipa fedha zilizobaki kwa miezi sita kuanzia tarehe ya leo huku pia wakiiomba mahakama kuamuru mshitakiwa wa sita kulipa Sh.milioni 30 kama hasara aliyosababisha kwa Serikali.

Wakili wa utetezi Alex Mgongolwa amedai washitakiwa hao ni wakosaji wa kwanza na kwamba kumbukumbu zinaonesha kuwa hatima ya shauri hilo imetokana na sheria hiyo.Hivyo aliiomba Mahakama ijikite kwenye makubaliano katika kutoa adhabu kama yalivyosajiliwa mahakamani hapo.

"Mashitaka yote yanatoa uchaguzi wa adhabu ya faini hivyo, tunaomba mahakama iwape adhabu nyepesi," alidai Mgongolwa.Kwa mara ya kwanza washitakiwa hao walifikishwa mahakamani Novemba 20,2017.

Washitakiwa hao wanadaiwa kuwa  kati ya Januari 1, mwaka 2014 na Januari 14,mwaka 2016 maeneo ya Dar es Salaam, walitoza malipo ya mawasiliano ya simu za kimataifa chini ya kiwango cha Dola za Marekani 0.25 kwa dakika kwa lengo la kujipatia faida.

Pia katika kipindi hicho, wanadaiwa kuhujumu miundombinu ya Mamlaka ya Mawasiliano nchini(TCRA) kwa kutoza gharama chini ya kiwango na kushindwa kulipa kiasi cha Dola za Marekani 3,282,741.12 kwa TCRA, kama malipo ya mapato na kushindwa kulipa ada za udhibiti za dola  466,010.07 kwa TCRA.

Pia washitakiwa hao wanadaiwa kuwa waliisababishia TCRA hasara ya dola  3,748,751.22 ambazo ni sawa na Sh. bilioni nane.


 VIGOGO sita wa Kampuni ya Six Telecom akiwemo Wakili  maarufu Dk. Ringo Tenga wamehukumiwa kulipa faini ya Sh.milioni 155 au kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela. Pia wamehukumiwa kulipa fidia ya dola za Marekani 3,748,751.19 ambayo ni sawa na takribani Sh.milioni nane za Tanzania

Mkutano wa 30 wa Baraza la Mawaziri la kisekta linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango.

$
0
0
Mkutano wa 30 wa Baraza la Mawaziri la kisekta linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango umefunguliwa leo kwenye Ukumbi wa Mikutano uliopo katika Jengo la Jumuiya ya Afrika Mashariki, jijini Arusha na utafanyika kuanzia tarehe 7 hadi 12 Oktoba 2019.
Mkutano huo unaanza na vikao vya awali ambavyo ni kikao cha Maafisa Waandamizi kinachofanyika tarehe 7 na 8 Oktoba 2019 na utafuatiwa na kikao ngazi ya Makatibu Wakuu kitakachofanyika tarehe 9 na 10, na kumalizia na ngazi ya Mawaziri tarehe 11 na 12 Oktoba 2019.
Pichani; Wapili kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa kikao cha ngazi ya Wataalamu na Afisa Mwandamizi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kutoka Jamhuri ya Rwanda, Bw. Emmanuel Kamugisha akiongoza kikao hicho. Pembeni ya Mwenyekiti wa pili kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Christophe Bazivamo, kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Forodha na Biashara, Bw. Keneth Bagamuhunda, na kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Bw. Raphael Kanoth. 
Wakurugenzi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia majadiliano katika kikao cha ngazi ya wataalamu. Wapili kushoto ni Kiongozi wa Ujumbe wa Tanzania katika kikao hicho ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama, Balozi Stephen Mbundi, kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji, Bw. Benard Haule, wa pili kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Bi. Caroline Chipeta na kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, Bw. Gerald Mweli. 
Ujumbe wa Tanzania ukifatilia majadiliano katika kikao cha ngazi ya wataalamu. 
Mkutano ukiendelea. 

Viongozi wa BAKITA na BAKIZA baada ya kikao cha mashauriano jijini Dar es salaam

$
0
0
Picha ya pamoja ya viongozi wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA)  na wa Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA)  baada ya kikao chao cha mashauriano kilichofanyika makao makuu ya BAKITA Kijitonyama, jijini Dar es salaam. Kutoka kulia waliosimama mbele ni Bi Mwanahija  Ali Juma (Katibu Mtendaji - BAKIZA), Dkt.Muhammed Seif Khatib( Mwenyekiti - BAKIZA), Dkt. Selemani Sewangi (Katibu Mtendaji- BAKITA) na Dkt. Method Samwel (Mwenyekiti - BAKITA) na wajumbe wengine.
Viewing all 110088 articles
Browse latest View live




Latest Images