Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110017 articles
Browse latest View live

NAIBU WAZIRI WA MADINI AKABIDHIWA KITUO CHA UMAHIRI MKOANI MUSOMA

$
0
0
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo kushoto, anaefata ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Madini Issa Nchasi wakikabidhiwa funguo ya jengo la Umahiri na Meneja wa SUMA JKT Kanda ya Ziwa Kapteni Fabian Buberwa




Jengo la kituo cha umahiri lililopo Musoma
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo mbele katikati akifanya ukaguzi wa jengo la umahiri kabla ya makabidhiano, mbele kulia ni Meneja wa SUMA JKT Kanda ya ziwa Kapteni Fabian Buberwa, kushoto ni kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mara Samwel Mayuki, nyuma kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Musoma Dkt. Vicent Naano, nyuma kushoto ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Madini Issa Nchasi
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Caroline Mthapula akitoa maelezo juu ya sekta ya madini Mara, kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Madini. Issa Nchasi, anaefata ni Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, na kushoto ni Meneja wa SUMA JKT Kanda ya ziwa Kapteni Fabian Buberwa 

Kaimu Meneja wa Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) Veronica Francis akiwakirisha taarifa za Kituo cha umahiri cha Musoma 
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Wizara ya Madini Issa Nchasi akitoa taarifa za kukamilika kwa jengo la kituo cha umahiri Mara 
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo mbele katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na Viomgozi wa Serikali, Wizara ya Madini pamoja na Wachimbaji wadogo wa Mkoa wa Mara
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Mara




Na Tito Mselem, Musoma

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo Oktaba 07, 2019 amekabidhiwa jengo lenye thamani ya shilingi bilioni 1.2 ambalo litatumika kama kituo cha umahiri kwa wachimbaji wadogo wa Madini Mkoani Mara.

Jengo hilo lililojengwa na Mkandalasi SUMA JKT na kukabidhiwa kwa Wizara ya Madini kupitia Naibu Waziri Nyongo,nae pia kalikabidhi jengo hilo kwa Tume ya Madini ambapo limekamilika na liko tayari kwa ajili ya matumizi.

Aidha Jengo hilo la umahiri ni kati ya majengo saba ya umahiri na jengo moja la taaluma lililopo Chuo cha Madini Dodoma (MRI) yaliyojengwa kwa jumla ya thamani ya Bilioni 11.9 na SUMA JKT kupitia mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) ambayo yamejengwa katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Kagera, Musoma, Bariadi, Chunya, Mpanda, Handeni Tanga na Songea.

Akizungumza kwenye makabidhiano hayo Naibu Waziri Nyongo ameipongeza SUMA JKT kwa kazi nzuri waliyoifanya ya ujenzi wa jengo hilo ambalo limekamika kwa wakati.Naibu Waziri Nyongo amesema lengo kuu la kuanzisha vituo hivyo ni kuwasadia wachimbaji wadogo kufanya shughuli za madini kwa tija kwa kuwapatia elimu ya uchimbaji katika vituo hivyo.

“faida ya ujenzi huu ni kutoa mafunzo ya kitaalamu yahusuyo Madini, tutatoa mafunzo ya Utafiti wa Madini, ikiwa ni pamoja na kuonesha mikanda ya Madini ilipo na muelekeo wake, uchimbaji wa madini wenye tija na salama, Uchenjuaji wenye kuleta uvunaji mkubwa wa madini na hivyo kuwapatia faida kubwa wachimbaji”, alisema Nyongo.

Inakadiliwa kuwa baada ya mafunzo kupatiwa kwenye vituo hivi, wachimbaji watavuna madini kwa zaidi ya asilimia 80 ukilinganisha na hapo awali ambapo wachimbaji wengi walivuna dhahabu kwa asilimia 30 tu,

Imeelezwa kuwa katika vituo hivi vya umahiri kutakuwa na mafunzo ya kuomba leseni kwa njia ya mtandao na kutakuwa na usagaji wa mawe na kupima sampuli mbalimbali za madini.Aidha Nyongo ametoa rai kwa wachimbaji wadogo wa Mkoa wa Mara wakitumie kituo hicho cha umahiri ili viwaletee tija na faidsa katika shughuri za uzalishaji madini.

Kwa upande wake kaimu meneja wa mradi wa usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) Veronica Francis alisema kuwa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini (GST) ulifanya utafiti wa kijiolojia na kubaini maeneo saba nchini kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya umahiri.

“Utafiti umebaini kuwepo kwa kiwango kikubwa cha dhahabu katika eneo la Buhemba yenye takribani wakia 10,737 zenye viwango vya 0.7g/t ndiyo maana kituo hiki kikaja kujengwa hapa Musoma ili kiwasaidie wachimbaji wadogo kupata mafunzo ya namna bora ya uchimbaji madini,” alisema Veronika.

Pia Mkuu wa Wilaya ya Musoma Dkt. Vicent Naano ameipongeza Wizara ya Madini kwa Kujenga kituo cha umahiri katika Mkoa wa Mara maana kitawasaidia sana wachimbaji kufanya kazi kwa uhakika na sio kubahatisha.

MILIONI 921,000,000 KUTATUA TATIZO LA BARABARA YA MKUTA HADI MPANGATAZARA

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akimuonyesha kaimu meneja wa wilaya ya Mufindi Mhandisi Selemani Mjohi kwa namna gani daraja hilo lipo hatarini kubomoka
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akikagua moja ya madaraja ambavyo yamelalamikiwa kwa ubovu .
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akipata maelezo kutoka kwa kaimu meneja wa wilaya ya Mufindi Mhandisi Selemani Mjohi kwa namna gani watatengeneza barabara hiyo ili ichochee maendeleo kwa wananchi


NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

JUMLA ya milioni mia tisa ishirini na moja zinatumika katika kutatua Tatizo la barabara kuanzia Mkuta hadi Mpangatazara kwa kiwango cha changalawe katika jimbo la Mufindi Kaskazini kwa lengo la kurahisisha shughuli za kimaendeleo ambazo zimekuwa zikihusisha barabara hiyo.

Akizungumza kwenye mikutano ya hadhara ya mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa,kaimu meneja wa wilaya ya Mufindi Mhandisi Selemani Mjohi alisema kuwa pesa tayari imepatika na tayari wameshawapata wakandarasi ambao watatengeneza barabara hizo.

“Mheshimiwa mbunge na wananchi wako mwezi huu wa kumi tunaanza kutengeneza barabara hii ambayo imekuwa kimbilio la maendeleo kwa wananchi wa jimbo hili hasa katika biashara ya usafirishaji wa zao la mbao ambalo ni chanzo kikubwa cha mapato kwa wananchi wa jimbo la Mufindi Kaskazini” alisema Mjohi

Mhandisi Mjohi alisema kuwa barabara hiyo inayotengenezwa itapita katika vijiji vya Ifwaji,Ifupira,Kidete,Ikanga,Ihanu,Ibwanzi,Lulanda,Isipii na Mpanga Tazara kwasababu vijiji hivi vipo barabarani kabisa lakini vijiji zaidi ya arobain vitanufaika na barabara hiyo kimaendeleo.

“Barabara hii ikikamilika itahudumia zaidi ya vijiji arobaini ambavyo vipo pembezoni au vinazungukwa kwa namna moja au nyingine na barabara hii ambayo imegharimu mamilioni ya pesa ambazo zimetafutwa na mbunge wa jimbo hili” alisema Mjohi

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa aliwahakikishia wananchi kuwa barabara hiyo itatengenezwa kwa kuwa fedha ametafuta na amewakabidhi kwa TARURA wilaya ya Mufindi na tayari wameshapata wakandarasi wawili ambao watatengeneza barabara hiyo kwa kiwango cha changalawe.

“Mimi mbunge wanu nimeshafanya kazi yangu ya kutafuta fedha nimepata na nimekabidhi kwa wataalam hivyo kazi iliyobakia ni kuhakikisha wataalum wanasimamia vilivyo barabara hii ili ijengwe kulinga na gharama ambazo zimetolewa” alisema Mgimwa

Mgimwa mgimwa alisema kuwa barabara hiyo inaumhimu mkubwa kwenye biashara ya zao la mbao kwa kuwa ndio baishara kuu inayofanyika katika barabara hiyo na kuwakumbusha wananchi kuwa barabara hiyo ni yao na wanapaswa kuisimamia.

Nao wananchi waliendelea kumkubusha mbunge umuhimu wa barabara hiyo kimaendeleo kwa kuwa wananchi wamekuwa wakiitumia katika shughuli za kimaendeleo za kila siku.

NAIBU WAZIRI WA AFYA ATOA TAARIFA YA UZINDUZI MKAKATI KUPUNGUZA VIFO VYA MAMA NA MTOTO ZANZIBAR

$
0
0
Naibu Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman akitoa Taarifa kwa Waandishi wa Habari kuhusiana na uzinduzi wa mkakati wa Kupunguza Vifo vya mama na mtoto pamoja na Uzinduzi wa Boti ya kuwasaidia Wazazi watakaopata matatiza katika Visiwa vya Pemba Uzinduzi utakao fanyika 9/10/2019 Zanzibar ,hafla iliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja mjini Unguja.
Mratibu wa Huduma za Mama na Mtoto Wanu Bakari akitoa maelezo kuhusiana na Uzazi salama katika mafunzo ya Waandishi wa Habari yanayohusu huduma na kupunguza vifo vya mama na Mtoto katika ukumbi wa Hospitali ya wagonjwa wa Akili Kidonge Chekundu Zanzibar.
Mkuu wa kitengo cha Uhamasishaji na Mafunzo ya Uzazi salama Kassim Issa Kirobo akitoa mafunzo kwa Waandishi wa Habari kuhusiana na Uzazi katika ukumbi wa Hospitali ya wagonjwa wa Akili Kidonge Chekundu Zanzibar.
Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Dk,Fadhil Mohamed Abdalla akitoa hotuba ya makaribisho kwa Mgeni Rasmi katika mkutano wa Waandishi wa Habari kuhusu otoaji wa Taarifa ya uzinduzi wa mkakati wa Kupunguza Vifo vya mama na mtoto pamoja na uzinduzi wa Boti ya kuwasaidia Wazazi watakaopata matatiza katika Visiwa vya Pemba uzinduzi utakaofanyika 9/10/2019 Zanzibar ,hafla iliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja mjini Unguja.

Petroli, Mafuta ya Taa yachangia mfumuko wa bei wa Taifa kupungua

$
0
0
Charles James, Michuzi TV

MFUMUKO wa bei wa Taifa kwa mwaka ulioisha wa Septemba 2019 umepungua kwa asilimia 3.4 kutoka asilimia 3.6 kwa mwaka ulioisha Agosti huku mfumuko wa bei za vyakula na vinywaji ukiongezeka 

Akizungumza jijini Dodoma, Kaimu Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Bi Ruth Dawson amesema kupungua huko kwa mfumuko wa bei kunamaanisha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioisha Septemba mwaka huu imepungua.

Bi Ruth amesema mfumuko wa bei za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi ulioishia Septemba 2019 umeongezeka hadi asilimia 4.0 kutoka asilimia 3.7 kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti.

Amesema kupungua kwa mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia Septemba kumechangiwa hasa na kupungua kwa bei za bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi Septemba 2019 ukilinganisha na Septemba 2018.

" Baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zimepungua bei kwa mwezi Septemba 2019 zikilinganishwa na bei za mwaka 2018 ni pamoja na mafuta ya taa kwa asilimia 1.0, Petroli kwa asilimia 3.3, Majiko ya Gesi kwa asilimia 1.5, Dawa za kuulia wadudu nyumbani kwa asilimia 2.2 na mafuta ya nywele kwa asilimia 1.3," Amesema Bi Ruth.

Amesema mfumuko wa bei za Taifa unapima kiwango na kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi nchini.

Akizungumzia mfumuko wa bei kwa Nchi nyingine za Afrika Mashariki kwa mwaka ulioishia Septemba, 2019, Kenya mfumuko umepungua hadi asilimia 3.83 kutoka asilimia 5.00 huku Uganda ukipungua kutoka asilimia 2.1 hadi asilimia 1.9.
 Kaimu Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Bi Ruth Dawson akitoa taarifa ya mfumuko wa bei ya Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba mwaka huu

30TH MEETING OF THE SECTORAL COUNCIL OF MINISTERS RESPONSIBLE FOR EAC AFFAIRS AND PLANNING UNDERWAY IN ARUSHA

$
0
0
The 30th Meeting of the Sectoral Council of Ministers responsible for EAC Affairs and Planning(SCMEACP) is currently underway at the EAC Headquarters in Arusha, Tanzania.

The six –day meeting kicked off with the Session of Senior Officials, which will run up to 8th October, 2019.This will be followed by the Coordination Committee, which consists of the Permanent/Principal Secretaries on 9th October, 2019, dedicated session of the Ministers to receive the report of the EAC Audit Commission for the FY 2017/18 and the annual report of the EAC Audit and Risk Committee for the FY 2017/18 on 10th October, 2019; Ministerial session of Ministers of the 29th and 30th meetings of the SCMEACP on 11th October, 2019; and the dedicated session of Ministers to consider the report of the EAC AD HOC Service Commission on Workload analysis and job evaluation on 12th October, 2019.    

The SCMEACP will, among others, consider the report on implementation of previous decisions of the SCMEACP; a progress on the status of implementation of the EAC Common Market;  status of EAC integration (2000 – 2017); consideration of the global and sector-specific priorities for the FY 2020/21;  terms of reference for the formulation of the 6th EAC development strategy (2021/22 – 2025/26); the report of the meeting of Chiefs of Immigration and Directors of Labor; and  the status of Partner States’ contributions to the EAC budget.

In addition, the Sectoral Council will consider ;report on political affairs, progress  on COMESA-EAC-SADC tripartite free trade area negotiations; proposal for the establishment of a regional procurement web portal; and the revised concept note on the EAC 20th anniversary observance.    
  A section of participants during the session of Senior Official.
EAC Director General Customs and Trade, Mr Kenneth Bagamuhunda on the extreme right making his remarks during the Senior Official session. Sitting beside him, from (L-R) Mr Raphael Kanothi, the Rapporteur from Kenya, Chairperson of the senior officials session, Mr Emmanuel Kamugisha from Rwanda and EAC Deputy Secretary General in charge of Productive and Social Sector, Hon Christophe Bazivamo.

Airtel Africa Announces Partnership with Mastercard to Transform Digital Payments Landscape and Connect 100 Million Consumers in Africa

$
0
0
 ·         Partnership will connect millions of  Airtel Money customers to a global online market place, across multiple digital payment use cases and provide access to Mastercard’s global network of merchants
·         Airtel Money customers, even those without a bank account, can now make online payments globally with their Airtel Money Mastercard virtual card
·         Mastercard’s’ enabling infrastructure and proposition(s) will enable a superior digital experience which Africa consumers are aspiring to and by so doing ultimately drive greater adoption and usage for the Airtel Money customers

NAIROBI (8/10/2019): Airtel Africa today announced a partnership with Mastercard, giving over 100 million Airtel Africa mobile phone users across 14 African countries access to Mastercard’s global network.

The Mastercard virtual (non-plastic) card allows Airtel Money customers, even those without a bank account, to make payments to local and global online merchants that accept Mastercard cards, while ensuring that the customer’s financial data is always secure and private. In addition, Airtel Money customers will also be able to make in-person payments at outlets via Quick Response (QR) codes (whereby payments are made from an Airtel mobile phone by scanning the QR code displayed at checkout or by entering a merchant identifier, at any location worldwide that Mastercard QR is accepted). To date, there are over 1 million merchant locations across Africa that accept Mastercard QR payments.

Airtel Money customers will also benefit from competitive pricing and preferential exchange rates for international payments, and gain access to other  domestically relevant use cases including bill payments , merchants payments and value added services such as cash management solutions.

Raghunath Mandava, the CEO of Airtel Africa said, “Airtel and Mastercard have a shared passion for digital transformation and making mobile financial services accessible to everyone across the continent. Through our partnership we will enable over 100 million Airtel Africa customers make safe mobile money purchases online and in person. The partnership will also significantly bolster Airtel’s position as one of the the largest offline-to-online digital payment network in Africa. We are really excited to embark on this partnership with a globally trusted brand like Mastercard. This partnership is truly revolutionary in our market, giving millions of people better access to the digital and online world.”

Amnah Ajmal, Executive Vice President for Market Development, Mastercard Middle East and Africa, said, “Across the MEA region our digital partnerships strategy remains focused on enabling digital transformation for our partners so that their consumers can enjoy seamless access to payments and a superior experience. We are very excited to partner with Airtel to lead the transition to digital by enabling access to their millions of consumers for online and in-person payments across the globe. Mastercard is uniquely positioned as a single technology provider to enable our digital partners like Airtel to transition seamlessly into digital”.


Mobile internet connections are expected to grow rapidly in Africa due to low cost smartphones and high-speed GSM networks being rolled out by Mobile Network Operators like Airtel.  This growth in internet connections is creating increased demand for digital content, social media, m-commerce even online education and a need to make online payments easily and securely by both banked and unbanked consumers.

Historia Fupi ya Marehemu William Nicholaus Lobulu

$
0
0
Mzee William Lobulu alizaliwa 20 Desemba 1951 Sanawari, Arusha.

Alifanya kazi Shirika la Habari Tanzania (SHIHATA) baada ya kuhitimu Shahada ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na baadaye alipata Shahada ya Uzamivu Chuo Kikuu cha Meriland, Marekani alipokuwa  Mkufunzi katika Chuo cha Uandishi wa Habari Tanzania, (TSJ).

Alifanya kazi za uandishi wa habari, uhariri pamoja na kuchapisha gazeti la "Arusha Times".

Pia alifanya kazi ya ushauri yaani "consultancy" inayohusiana na masuala ya machapisho katika mashirika ya mbalimbali ya kitaifa na kimataifa.

Marehemu alibatizwa kanisa la KKKT Ilboru. Alifunga ndoa ambayo ilibarikiwa Kanisa la KKKT Mjini Kati mwaka 1986. Mzee William ameacha mke na watoto watatu na mjukuu mmoja. 

Alikuwa akisumbuliwa na asthma ambayo ilimshika ghafla na taa yake ikazima alipoitwa mbinguni saa 12 asubuhi Jumapili tarehe 6 Oktoba 2019.

Familia inatoa shukrani kwa wote waliohusika kumhudumia marehemu kwa hali na mali kuhusiana na afya yake.

Tunashukuru Wachungaji, Wainjilisti na Wazee wa Kanisa na watumishi wote waliokuwa wakimpa huduma mbalimbali za kiroho.

Marehemu atakumbukwa kwa ushirikiano, upole, ucheshi na moyo wa huruma kwa watoto na watu wote kwa ujumla. 

BWANA ametoa, BWANA ametwa jina la BWANA lihimidiwe.

DC KINONDONI AFANYA ZIARA MBEZI JUU KUKAGUA UTEKELEZAJI WA UTATUZI WA CHANGAMOTO YA UPATIKANAJI MAJI

$
0
0
Na Ripota Wetu,Michuzi TV

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam Daniel Chongolo amefanya ziara katika Kata ya  Mbezi Juu kwa lengo la kujionea utekelezaji wa utatuzi wa changamoto ya upatikanaji wa maji kwa wananchi wa eneo hilo.

Akizungumza akiwa katika Kata hiyo leo Oktoba 8 ,2019  Chongolo amesema amefanikiwa kuona kinachoendelea kwa sasa katika kutatua changamoto ya maji kwa wananchi wa Mbezi Mtoni na maeneo yanayozunguka eneo hilo.

" Tumekubaliana na DAWASA Kawe kushughulikia changamoto hizo kwa haraka, nami baada ya wiki mbili nitarudi tena kuangalia maendeleo ya kazi ya kuwafikishia maji wananchi. Lengo la Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Jemedari wetu Rais John Magufuli ni kuhakikisha kuwa wanaKinondoni wote wanapata maji safi na salama ifikapo 2020,"amesema

Ameongeza kuwa mpaka sasa tupo zaidi ya asilimia 80 na kuongeza matanki matano yamekamilika na kila moja lina uwezo wa kihifadhi lita milioni sita." Mungu ni mwema, kwani ni hakika mama wa Kinondoni ikifika 2020 atasahau kubeba ndoo ya maji kichwani,".
 MKUU wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam Daniel Chongolo akielezwa jambo kutoka kwa mmofa wa Wafanyakazi wa DAWASA Kawe,akiwa kwenye ziara yake katika Kata ya  Mbezi Juu kwa lengo la kujionea utekelezaji wa utatuzi wa changamoto ya upatikanaji wa maji kwa wananchi wa eneo hilo.
 MKUU wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam Daniel Chongolo akimsikiliza mmoja wa Wananchi wanaoishi katika eneo hilo la Mbezi Juu kuhusu changamoto ya upatikanaji wa maji kwa Wananchi.


RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA BARABARA YA SUMBAWANGA –KANAZI KM 75 PIA AFUNGUA MIRADI YA MAENDELEO NKASI MKOANI RUKWA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaack Kamwelwe kuashiria ufunguzi wa barabara ya Sumbawanga-Kanazi km 75 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami katika sherehe zilizofanyika Kanazi mkoani Rukwa.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Kanazi mara baada ya kufungua barabara ya Sumbawanga-Kanazi km 75 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami katika sherehe zilizofanyika Kanazi mkoani Rukwa. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli watano kutoka kulia walioshika utepe, Wabunge wa mkoa wa Rukwa, Kamati ya Miundombinu, Mawaziri, akakata utepe kufungua barabara ya Sumbawanga-Kanazi km 75 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami katika sherehe zilizofanyika Kanazi mkoani Rukwa. 
Sehemu ya Barabara ya Sumbawanga-Kanazi km 75 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami kama inavyoonekana.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua moja ya chumba cha hospitali ya Wilaya ya Nkasi mara baada ya kuweka jiwe la msingi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gril la dirisha la moja ya chumba  cha hospitali ya Wilaya ya Nkasi mara baada ya kuweka jiwe la msingi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifungua kituo cha Afya cha Nkomolo Nkasi mkoani Rukwa.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, Waziri wa Tamisemi Selemani Jafo, Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugora, Mbunge wa Nkasi Ally Keissy, akikata utepe kuashiria ufunguzi kituo cha Afya cha Nkomolo Nkasi mkoani Rukwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mbunge wa Nkasi Ally Keissy mara baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli, wakiangalia zoezi la uandikishaji la wapiga kura wa Viongozi wa Serikali za mitaa Nkasi mkoani Rukwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na mwanachi wa Nkasi Albina Kasanya (74) ambaye alikuwa amemaliza kujiandikisha katika kituo cha Hospitali ya Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari wa Nkasi waliokuwa pembezoni mwa majengo ya hospitali ya Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa. 
Sehemu ya Majengo ya Hospitali ya Wilaya ya Nkasi ambayo ipo katika hatua za mwisho kukamilika Nkasi mkoani Rukwa.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Bi Paskalia Mikael mara baada ya kusimama katika kijiji cha Chala mkoani Rukwa wakati akielekea Nkasi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanachi wa Chala mara baada ya kuwasili kijijini hapo.
Wanafunzi wa Kasu Sekondary Wakishangilia mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwasili katika kijiji hicho.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanachi wa Kasu mkoani Rukwa. PICHA NA IKULU

RAIS DKT. MAGUFULI AENDELEA NA ZIARA YAKE WILAYANI NKASI MKOANI RUKWA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi kijiji cha Chala wilayani Nkasi Mkoa wa Rukwa akiwa njiani akitokea Sumbawanga leo Oktoba 8, 2019.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisoma mango kabla ya kuikata utepe kuzindua barabara ya Sumbawanga-Kanazi mkoani Rukwa leo Oktoba 8, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia wananchi wakijiandikisha katika daftari la mpinga kura eneo la Nkomolo Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa leo Oktoba 8, 2019. Akitoa maelezo kushoto ni Katibu Tawala Msaidizi wilaya ya Nkasi Bw. Albinus Mugonya.
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akituza viaja wa kwaya ya JKT walipotumbuiza wakati wa mkutano wa hadhara Mjini Nyamanyere wilaya ya Nkasi Mkoa wa Rukwa leo Oktoba 8, 2019
 Sehemu ya barabara ya Sumbawanga-Kanazi yenye urefu wa kilometa 75 iliyozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Oktoba 8, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Mama Felista Mkombo baada ya kuamuru ofisi za Mkjuu wa Wilaya na Mkuu wa Polisi Wilayani Nkasi kumpa shillingi milioni 15 kama fidia ya kuibiwa ng'ombe zake 25 Mjini Namanyere wilayani Nkasi PICHA NA IKULU

JUMLA YA WAGONJWA 28,876 WENYE MATATIZO YA MOYO WATIBIWA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI)

$
0
0
Jumla ya wagonjwa 28,876 wenye matatizo ya moyo wametibiwa kwa kipindi cha miezi mitatu ya Julai hadi Septemba mwaka huu katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).

Hayo yamesemwa jana na Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Magonjwa ya Moyo Dkt. Peter Kisenge wakati akieleza taarifa ya kazi zilizofanywa na Kurugenzi yake katika kikao cha menejimenti kilichofanyika jana katika Taasisi hiyo.

Dkt. Kisenge ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo alisema wagonjwa waliotibiwa katika Taasisi hiyo wanaume walikuwa 12,566 na wanawake 16,310 ambapo 6,590 sawa na asilimia 22.8 walikuwa wagonjwa wapya.

“Tumeona wagonjwa kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani pamoja na nchi za Ethiopia, Malawi, Zimbabwe, Visiwa vya Comoro na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Wagonjwa waliotibiwa na kurudi nyumbani walikuwa 27,882 na wagonjwa 994 walilazwa kati ya hao 500 ni wanawake na 494 ni wanaume idadi ya vifo vikiwa ni asilimia 6”, alisema Dkt. Kisenge.

Dkt. Kisenge aliendelea kusema kuwa watoto waliotibiwa katika Taasisi hiyo walikuwa 1,516 ambapo wa kike walikuwa 800 na wavulana 716 kati ya hao wagonjwa 374 walikuwa wapya.

Dkt. Kisenge alisema, “Wagonjwa wengi tuliowaona walikuwa na matatizo ya shinikizo la juu la damu, kutanuka kwa moyo,valvu, matundu, mishipa ya damu ya moyo na magonjwa ya moyo ya kuambukizwa yanayosababisha makovu katika valvu za moyo kutokana na kupata mafindofindo kwenye tezi za koo (Rheumatic Heart disease) ”,.

Wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua na kuzibuliwa mishipa ya damu ya moyo pamoja na kuwekewa vifaa vinavyousaidia moyo kufanya kazi vizuri walikuwa 352 kati ya hao watoto 87 sawa na asilimia 24.7 na hakukuwa na mgonjwa aliyepoteza maisha.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Upasuaji Dkt. Anjela Muhozya alisema wamefanya upasuaji kwa wagonjwa 153 kati ya hawa wagonjwa 122 walifanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua, wagonjwa 23 walifanyiwa upasuaji wa mishipa ya damu na nane walifanyiwa upasuaji wa mapafu.

“Tumefanya upasuaji wa kubadilisha valvu kwa wagonjwa ambao valvu zao zilikuwa na shida, kurekebisha mishipa ya damu ya moyo na kupandikiza mishipa ya damu ya moyo (Coronary Artery Bypass Graft – CABG). Wagonjwa waliopoteza maisha ni watatu sawa na asilimia 2.5”, alisema Dkt. Anjela.

Dkt. Anjela alisema changamoto kubwa wanayokutana nayo katika matibabu ya wagonjwa wa moyo ni wagonjwa wengi kufika katika Taasisi hiyo huku mioyo yao ikiwa imechoka. Na kuwaomba wagonjwa kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara ili kujuwa kama wanamatatizo ya moyo au la na kama watakuwa nayo waweze kupata matibabu kwa wakati.

Naye Cecilia Nthala kutoka nchini Malawi ambaye mtoto wake anatibiwa katika Taasisi hiyo alishukuru kwa huduma ya matibabu ya moyo aliyoipata .

“Nilipata taarifa ya Taasisi hii kupitia tovuti na mitandao ya kijamii, kwa kuwa mtoto wangu ana matatizo ya moyo nikawa nafuatilia kwa ukaribu huduma mbalimbali wanazozitoa baada ya kuridhika nazo nikaamua kumleta mwanangu ili naye apate huduma ya matibabu”, alisema Cecilia.

“Kwa kipekee ninawashukuru wauguzi na madaktari kwani muda wote wako karibu na mimi najiona kama vile niko nchini kwetu Malawi. Ninawaomba muendelee kutoa huduma kama hii mliyoitoa kwangu kwa wagonjwa wengine mnaowatibu”, alishukuru Cecilia.

Simamieni Wafungwa Kutatua Uhaba wa Makazi ya Askari – CGP Kasike

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akikagua moja ya tanulu la matofali ya kuchoma katika mradi wa ufyatuaji tofali za kuchoma katika Kambi ya Mkwajuni , Wilayani Songwe, leo Oktoba 8, 2019 alipotembelea katika ziara yake ya kikazi Mkoani Songwe.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(kulia) akikagua matofali ya kuchoma katika mradi wa ufyatuaji tofali za kuchoma katika gereza la wilaya ya Mbozi alipotembelea hivi karibuni katika ziara yake ya kikazi Mkoani Songwe.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike akiwasili jana Oktoba 7, 2019 katika ziara yake ya kikazi Gereza Ngwala.
Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Mhe. Samwel Opulukwa(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(wa pili toka kulia) alipotembelea Ofisi za Mkuu wa Wilaya hiyo leo Oktoba 8, 2019. Kulia ni Mkuu wa Magereza Mkoani Songwe, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Lyazeck Mwaseba(Picha na Jeshi la Magereza.

……………………..

Na Mwandishi wetu, Songwe; 

KAMISHNA Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike amewataka Wakuu wa magereza Tanzania Bara kuhakikisha kuwa wanatekeleza ipasavyo agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu ujenzi wa nyumba za makazi ya askari wa jeshi hilo kote nchini kwa kutumia nguvu kazi ya wafungwa waliopo magerezani. 

Akizungumza Mkoani Songwe mara baada ya kukagua miradi ya ufyatuaji wa matofali ya kuchoma na ujenzi wa nyumba za maafisa na askari katika magereza ya Ileje, Mbozi, Ngwala na Kambi ya Mkwajuni iliyopo Mkoani Songwe, Kamishna Jenerali Kasike amesema ujenzi wa makazi za askari unaoendelea katika vituo mbalimbali nchini ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli katika kutatua changamoto ya makazi kwa watumishi wa Jeshi hilo.

“Mkakati wa utatuaji wa changamoto ya uhaba wa nyumba za Maafisa na askari lazima utiliwe mkazo na kupewa kipaumbele katika kuwatumia wafungwa waliopo magerezani katika suala la ujenzi sambambamba na uzalishaji wa chakula chakutosha ili kuipunguzia Serikali gharama za kuwahudumia wahalifu wote walipo magerezani, ” alisema Kamishna Jenerali Kasike.

Katika hatua nyingine, Kamishna Jenerali Kasike ameupongeza Uongozi wa Wilaya ya Songwe kwa kuanzisha ujenzi wa Gereza jipya katika mji wa Mkwajuni ambao ni Makao Makuu ya Wilaya ya Songwe.

Kamishna Jenerali Kasike amesema uwepo wa gereza hilo katika wilaya ya Songwe utasaidia katika kumaliza tatizo la msongamano wa wafungwa na mahabusu kwenye gereza la wilaya ya Mbozi.

“Kutokuwepo kwa magereza ya wilaya kunasababisha msongamano wa wafungwa na mahabusu katika magereza ya jirani, pamoja na kuchelewesha upatikanaji wa haki hivyo nimpongeze sana Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Mhe. Samwel Opulukwa pamoja na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama kwa kuwezesha kuanza kwa ujenzi wa Gereza hili kimsingi utatatua tatizo la msongamano wa wafungwa na mahabusu katika Gereza Mbozi,” amesema Jenerali Kasike.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Songwe. Mhe. Samwel Opulukwa ameshukru ujio wa Kamishna Jenerali katika ziara yake ya kikazi katika Gereza la Ngwala pamoja na Kambi ya Mkwajuni ili kujionea hali halisi ya Uendeshaji wa Jeshi hilo, Wilayani Songwe.

“Kamishna Jenerali nikuhakikishie tu kuwa Uongozi wa wilaya utashirikiana na Jeshi la Magereza katika kuhakikisha kuwa tunakamilisha ujenzi wa gereza hili jipya la Mkwajuni ili kusaidia kuondoa usumbufu wa wahalifu kwenda gereza la wilaya ya mbozi,” Alisistiza Mhe. Opulukwa.

Kwa sasa, wakazi wa wilaya hiyo ya Songwe ambao wanakabiliwa na tuhuma mbalimbali au waliohukumiwa vifungo hupelekwa katika Gereza la wilaya ya Mbozi kitendo ambacho kinawanyima wafungwa na mahabusu fursa ya kuonana na ndugu au mawakili wao kutokana na umbali uliopo ambapo kutokana na juhudi za Mkuu wa Wilaya hiyo tayari Bweni moja la Wafungwa lenye uwezo wa kuhifadhi waha;lifu 150 limekamilika pamoja na Ofisi ya Utawala na ujenzi wa Ukuta wa gereza unaendelea katika Kambi hiyo ya Mkwajuni.

Mkurugenzi Mkuu bank M akiri tuhuma za uhujumu uchumi, alipa fidia zaidi ya bilioni 6 na faini ya milioni 2

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv

MKURUGENZI Mkuu wa bank M nchini Tanzania, Sanjeev Kumar (64) amehukumiwa kulipa faini ya sh.milioni mbili baada ya mahakama kumtia hatiani katika mashtaka mawili yaliyokuwa yakimkabili likiwemo la kuisababishia serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania hasara ya zaidi ya sh. Bilioni sita.

Pia mahakama imemuamuru mshtakiwa huyo kulipa fidia ya sh. 6,039,103,579 ambazo anatakiwa kumaliza kuzilipa ndani ya miezi ishirini na nne.  ambapo leo Oktoba 8/2019 amemriwa kulipa USD,300,000 ambazo ni sawa na zaidi ya sh. Milioni 690  na amezilipa.

Akisoma adhabu hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi amesema, mshtakiwa atatakiwa kulipa faini ya sh. Milioni moja kwenye kila kosa na kulipa fidia ya sh. 6,039,103,579.Akifafanua adhabu hizo, Hakimu Shaidi amesema, mshtakiwa anapaswa kulipa USD 300,000 leo leo na pia fedha itakayobaki inapaswa kulipwa katika kipindi cha miezi 24 kuanzia tarehe ya leo (8/10/2019) na fedha zinazobaki kiasi cha sh. 5,349,103,579 anapaswa kila mwezi kulipa sh. 222 ,879,315 ambazo anatakiwa kulipa kabla aka tarehe 8 ya Kalenda ya kila mwezi mpaka atakapomaliza..

Pia mahakama imeamurui hati ya kusafiria ya mshtakiwa huyo ibaki katika Ofisi za DPP  na safari zake zote zitafatiliwa na ofisi hiyo. 

Kabla ya kusomwa kwa adhabu hiyo, Wakili wa serikali Jackiline Nyantori  alidai, hawana kumbukumbu za nyuma za mshtakiwa hivyo, ameiomba mahakama itoe adhabu kulingana na makubaliano ili iwe  fundisho kwake na  wengine.

Akisoma makubaliano hayo, Wakili Nyantori amedai, DPP na mshtakiwa  wameingia makubaliano baada ya kukiri makosa yake hivyo wameamua kuondoa mashtaka ya  kughushi,  ya kutakatisha fedha, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kuwasilisha nyaraka za uongo.

Baada ya kusoma makubaliano hayo, Hakimu Shaidi  alimuapisha mshtakiwa na kumuuliza  kama alisaini kwa hiari yake na kudai alifanya hivyo kwa hiari yake.

Akisoma mashitaka mapya, Wakili Nyantoru alidai katika shtaka la kwanza, Januari 20,2016 mshtakiwa hiyo akiwa Mkurugenzi Mkuu wa Benki M Tanzania alishindwa kusimamia majukumu yake vizuri na kuisababishia Serikali kupata hasara ya Sh. 6, 039, 103,579.

Katika shtaka la pili,  imedaiwa, siku na mahali hapo mshtakiwa Kumar, akiwa kwa njia ya ulaghai ndani ya Benki M Tanzania na huku akijia akijua kuwa ni udanganyifu alijipatia USD  287,000.
 MKURUGENZI Mkuu wa bank M nchini Tanzania, Sanjeev Kumar (64) amehukumiwa kulipa faini ya sh.milioni mbili baada ya mahakama kumtia hatiani 

KIKWETE AFUNGUA RASMI KONGAMANO LA KUMBUKIZI YA MIAKA 20 YA KIFO CHA BABA WA TAIFA

$
0
0

*Asema dhamana ya uongozi haimpi kiongozi kuwa na haki kuliko raia, ahimiza amani na kudumisha uhuru na umoja.

Na Leandra Gabriel, Michuzi Tv

LEO Oktoba 8, Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amefungua kongamano la kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha baba wa taifa lililobeba mada kuu ya "Urithi wa Mwalimu Nyerere katika Uongozi, Maadili, Umoja na Amani katika Ujenzi wa Taifa" kongamano lililofanyika katika chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na kuhudhuriwa na viongozi wa Serikali na vyama mbalimbali vya Siasa.

Akizungumza wakati wa ufunguzi huo Dkt. Kikwete amesema kuwa kumkumbuka Mwalimu Nyerere ni jambo analostahili na hiyo ni kutokana na mambo mengi aliyoyafanyakwa nchi, barani Afrika na ulimwenguni kwa ujumla.

" Mwalimu ni mkombozi wetu kwa kuwa alitukomboa kutoka kwa ukoloni, ni ngumu kuacha kazi yenye mshahara lakini mwalimu aliacha kazi yake na kuwa Rais wa TANU kazi ambayo haikuwa na mshahara na kujitoa kwa ajili ya kudai uhuru ambao hujui utapata au la na hujui utaupata lini, na alitumia maneno yenye umaarifa na uhodari ambao umetufikisha hapa" Ameleeza Dkt. Kikwete.

Amesema kuwa siku zote Mwalimu alisisitiza kutokubaguana kwa makabila na dini pamoja na kusisitiza utu miongoni mwetu.

"Dhamana ya uongozi haikufanyi uwe na haki kuliko raia wengine, kujishusha hakukufanyi usiwe kiongozi bali kutekeleza majukumu yako kwa weledi kutakufanya uwe bora zaidi" Ameeleza.

Aidha amesema kuwa Mwalimu aliwapenda sana vijana na kutambua umuhimu wa vijana na aliwapa fursa ya kujifunza uongozi wa juu na hiyo ni kutokana na nafasi ya vijana katika taifa;

" Lazima tuwape vijana nafasi katika ujenzi wa taifa tuwape nafasi, mawazo hayapigwi rungu bali mawazo yanashindwa na mawazo yaliyo na nguvu zaidi" ameeleza.

Vilevile amesema kuwa urithi tulioachiwa na Mwalimu ambao sasa ni tunu zinazotutambulisha  tuzitunze ili nchi yetu iendelee kuwa na amani.

Awali akieleza historia ya Chuo hicho Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Shadrack Mwakalila amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa chuo hicho wamekuwa wakipambana na ujinga kwa kutoa mafunzo ya uongozi, maadili, uzalendo na utawala bora hali iliyopelekea Chuo hicho kuwa kitovu cha uongozi, maadili na uzalendo.

Amesema kuwa Chuo hicho kimejipanga kutoa mafunzo ya muda mfupi ya uongozi kwa taasisi mbalimbali pamoja na kutoa mafunzo ya muda mrefu ya uongozi katika ngazi za shahada mbalimbali.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya chuo hicho Stephen Wasira amesema kuwa licha ya makongamano hayo lazima pia mitaala ya elimu iangalie zaidi suala la kujua historia ya nchi ili kuweza kujenga uzalendo.

" Huwezi kuwa mzalendo kwa kuifia nchi usiyoijua hivyo lazima elimu iwaandae vijana kupitia mitaala ya elimu na hiyo ni pamoja na wataalamu wa historia kuandika vitabu vya ukombozi vitakavyotoa maarifa kwa kizazi cha sasa na baadaye" ameeleza Wasira.

Amesema kuwa kama Mwalimu alivyotumia lugha ya Kiswahili bila mkalimani na sisi hatuna budi kukitunza na pamoja na kuimarisha uhuru na umoja ambavyo ni misingi ya kujivunia.

Kongamano hilo limehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Rais wa kwanza, Waziri Mkuu na Spika mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba, Makamu wa Rais wa awamu wa nne Dkt. Gharib Bilal, Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi Dkt. Bashiru Ally,  Mama Fatma Karume, Chifu Wanzaki Nyerere pamoja na viongozi mbalimbali vya vyama na Serikali.

RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE ATUMIA KONGAMANO LA KUMBUKA MWALIMU NYERERE KUZUNGUMZIA UHURU WA MAWAZO,VIONGOZI KUJISHUSHA

$
0
0
Na Said Mwishehe, Michuzi TV

RAIS Mstaafu Jakaya Kikwete amesema kuna kila sababu ya Watanzania kuendeleza misingi imara iliyoasisiwa na Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere huku akisisitiza umuhimu wa watu kuwa huru kutoa mawazo yao badala ya kuyazuia.

Pia ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa Mwalimu Nyerere enzi za uhai wake licha ya kuwa Rais wa nchini bado hakujali nafasi yake kwani aliamini katika utu na hivyo alikuwa anafikika kwa urahisi na akipenda kujikweza kwa cheo chake kwa kujiona yeye ni Bora au yuko juu zaidi ya Watanzania, siku zote alijishusha na kujiweka kundi la watu wa kawaida sana.

Kikwete ameyasema hayo leo Oktoba 8,mwaka 2019 wakati anafungua Kongamano lililoandaliwa na Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ambapo katika kongamano hilo viongozi mbalimbali wastaafu na waliopo katika utumishi wamehudhuria .

Wakati Kukwete anazungumza katika kongamano hilo ametumia nafasi hiyo kuzungumza masuala mbalimbali yanayohusisha mchango wa Mwalimu Nyerere katika kujenga misingi imara ya Taifa letu ambapo amewataka Waatanzania kuendelea kuienzi na kusimamia kwa maslahi mapana ya nchi yetu.

"Mwalimu Nyerere aliamini kwenye utu,hivyo cheo chake cha Rais hakikusababisha ajione yeye ni Bora zaidi ha wengine,alijishusha na kila mtu alimfikia.Unapokaa na Mwalimu Mwalimu Nyerere unakuwa huna hofu .Ukiwa na cheo bado hakukuondolei ubinadamu wako, "amesema Rais mstaafu Kikwete.

Akizungumzia zaidi Mwalimu Nyerere, Rais huyo mstaafu amesema kuwa Mwalimu hakuwa na kinyongo na mtu eti kwasababu ametoa mawazo tofauti ya na kwake kwani eliminj katika Uhuru wa mawazo na mawazo hayapigwi rungu bali yanajibiwa kwa mawazo bora zaidi na hatimaye mambo yanakwenda vizuri.

"Hata CCM ni Chama nyenye maarifa mengi sana na kinachotumia akili lakini msingi wake mkubwa Mwalimu aliruhusu Uhuru wa mawazo.Niwakumbushe mwaka 1992 uamuzi wa busara kafanyika kwa kuingia katika mfumo wa vyama vingi,iliundwa tume wakati huo kukufanya maoni ambayo Mwenyekiti wake alikuwa Jaji Fancis Nyarari.

"Wakati ule upepo wa vyama vingi ulikuwa unakuja.Ukafanyika utafiti kupitia tume hiyo ambapo asilimia 80 walitaka mfumo wa Chama kimoja na asilimia 20 Chama kimoja. Mimi nilikuwa wa Kamati Kuu,si haba nimekaa ...mjadala ulikuwa mkubwa na mkali, hata hivyo ikaamriwa asilimia 20 wameshinda na ilikuwa uamuzi wa kimkakati.

"Chama hiki kina maarifa mengi, na msingi mkubwa CCM wana uhuru wa mawazo.Kupoteza uhuru wa mawazo ndani ya Chama ni kwenda kukiharibu.Mwalimu alikuwa na akili sana ,yeye peke yake ni sawa na wajumbe 500.Alikuwa na uwezo wa kuchambua na anawasikiliza na kisha anakuja na samari yake ambayo inamaliza hoja zote ambazo hazikuwa na maana"amesema Kikwete.

Amesisitiza Mwalimu hakuna na kinyongo na mtu mwenye mawazo tofauti na yeye,alikuwa na moyo mzuri sana."Niwakumbushe wakati wa uhujumu uchumi tulikutana Karimjee na ajenda ikawa ajenda ya uhujumu uchumi.Kuna mjumbe mmoja alimwambia Mwalimu hawezi kuchukua zilizo ili akamwachia Sokoine kupambana na wahujumu uchumi , lakini Mwalimu alicheka tu.

'Wazee walitaka kumjua aliyeshauri vibaya...lakini aliwajibu washauri wake wa nini,kwani ni washauri wake,hivyo washughulike na yeye."Mwalimu anatufundisha kama ulishauriwa ukakubali lawama zibaki za kwako na sio kumlaumu aliyekushauri.

Kikwete amesema kongamano ambalo limeandaliwa na Chuo hiko ni muhimu na la kupongeza kwani kinatoa fursa ya kukumbuka yale yaliyofanywa na Mwalimu na kuongeza Mwalimu kukumbukwa ni jambo ambalo anastahili, wala sio hisani na kwanini amefanya mambo mengi kwa Tanzania na Afrika na hata kwa duniani na utaamua kuyaorodhesha utakesha.

Ametaja baadhi ya mambo ambayo Mwalimu ameyafanya kwa ajili ya nchi ni kwamba Mwalimu ndio mkombozi wetu kwani ametukomboa kwa kututoa katika ukoloni.Mwalimu aliamua kuanzisha safari ya kuondoa ukoloni na ndipo Tanu ikaanza na Mwalimu akawa Rais, na baada ya uamuzi huo Serikali ya Mkoloni ikamtaka kuchagua abaki Tanu awe au Mwalim lakini yeye akaamua kubaki kuwa Mwalim.

"Ni uamuzi mgumu lakini kwa moyo wake wa upendo aliamua kujitoa yeye kwa ajili ya wengine. Hilo ni jambo kubwa sana kwa kuonesha moyo wa kujitolea, wangapi leo wanaweza kujitolea maana hata mshahara ukiwa mdogo watu wanaandamana.

"Mwalim Nyerere alikuwa na karama ya maneno na tumepata Uhuru kwa maneno, usione vyaelea ujue vimeundwa, umahiri wake ndio umetufikisha hapo. Kwa wenzetu imeshindikana hadi wanatumia nguvu. Tatu Mwalimu aliamini kwenye umoja na ndio maana kwa kushirikiana na swahiba wake mzee Karume walianzisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

"Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haikuweo kwenye ramani ya dunia lakini hao wazee wameweza kuanzisha nchi yetu na mafanikio yake sote tunayaona.

Jambo la nne Mwalimu amesaidia kujenga taifa lenye umoja , amani na mshikamano, nchi yetu hii ina kabila zaidi ya 120 lakini wote tumebaki kuwa wamoja.Kulikuwa wamoja.Kulikuwa watu wenye dini na wasio na dini lakini tukabaki na umoja wetu,"amesema Kikwete na kuongeza tukianza kubaguana kwa dini au kabila hatutabaki salama.

Wakati jambo la tano la kukumbuka,Kikwete amesema Mwalimu alikuwa mtu wa kawaida mbele ya watu wengine.Ukikaa na Mwalimu hupati hofu ya kuwa naye kwani alikuwa ni Rais aliyejishusha na alikuwa wa kawaida.Alifanya hivyo kwa kuamini kuwa Rais haina maana wewe ni zaidi ya watu wengine.

"Ni jambo nzuri kutambua kujishusha na unapojishusha hakuondoi nafasi yako, ukiwa binadamu hakuondoi nafasi yako.Jambo la sita aliamini Uhuru wa Tanganyika hauna maana kama nchi nyingine za Afrika hazitakuwa zimejikomboa kutoka mikono ya wakoloni Mwalimu alifanya kila linalowezekana kukomboa nchi nyingine za Afrika,"amesema Kikwete kwenye kongamano hilo.

Alizungumzia pia Mwalimu Nyerere alivyokuwa anawapenda vijana na akakumbusha hata yeye(Kikwete) mwaka 1968 akiwa kidato cha tatu alikuwa kiongozi wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Kibaha na kwamba mwaka1982 akapata nafasi ya kuingia Halmashauri Kuu ya CCM.UVCCM ndio sehemu ya kujifunza fursa ya uongozi.Nimeingia Halmashauri Kuu ya Chama mwaka huo na hapo ukawa mwanzo na mwisho wa siku nikawa Rais.

'Kuna mambo mengi ya kujifunza kutoka kwa Mwalimu, niwapongeze Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kwa kuandaa kongamano hili.Baadhi ya mambo wamekuwa tunu ya taifa na lazima. hizo tunu tuzilinde.Kwa Tanzania hii sote ni wamoja pamoja na kuwa na makundi mbalimbali ya watu.

"Watanzania wenzangu, wanachama wenzangu tushikamane katika kusimamia tunu ya amani.Amani haina Chama ,dhehebu wala kabila.Umoja hauna chama,kabila wala dini.
Makongamano hayo ni muhimu kwani kukumbusha mambo ya msingi ya taifa letu,"amesema Kikwete.
 RAIS Mstaafu Jakaya Kikwete mbaye alikuwa mgeni rasmi kwenye Kongamano  hilo lililoandaliwa na Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere,akizungumza jambo mbele wageni waalikwa mbalimbali waliohudhuria.
 Viongozi mbalimbali wastaafu na waliopo katika utumishi wamehudhuria Kongamano  hilo lililoandaliwa na Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere . 


 Wadau mbalimbali wakiwa ukumbini wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye Kongamano  hilo lililoandaliwa na Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ambapo Viongozi mbalimbali wastaafu na waliopo katika utumishi wamehudhuria .  
RAIS Mstaafu Jakaya Kikwete mbaye alikuwa mgeni rasmi kwenye Kongamano  hilo lililoandaliwa na Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere,akisalimiana na Wageni waalikwa mbalimbali waliohudhuria

UTAFITI WA MAFUTA NCHINI WASHIKA KASI

$
0
0
Mtambo/Rigi inayotumika katika Ucchorongaji wa Visima vifupi vya utafiti wa Mafuta katika Bonde la Eyasi wembere.
Wachimbaji (drillers) kutoka Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) ambao ndio wamepewa kandarasi ya kuchimba visima vya utafiti katika Bonde la Wembere wakiendelea na kazi.
Wataalamu wa masuala ya miamba kutoka TPDC wakiangalia baadhi ya Sampuli za Utafiti wa Mafuta katika Bonde la Eyasi Wembere. Sampuli hizi zinazopatikana katika kila hatua ya uchimbaji unavyoendelea

…………………..

Igunga,Tabora

Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) imeanza kufanya utafiti wa mafuta ya petroli katika bonde la Eyasi Wembere, Utafiti huu unahusisha uchorongaji wa visima vitatu vya utafiti vyenye urefu wa mita 300 kila kimoja na hivyo kufanya jumla ya mita 900 zitakazochorongwa katika Bonde la Eyasi Wembere ambapo Kisima namba moja kinachorongwa katika Kijiji cha Kining’nila Wilaya ya Igunga,kisima namba 2 na 3 vitachoroongwa katika wilaya za Meatu Mkoani Simiyu na Iramba Mkoani Singida.

Akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi rasmi wa uchorongaji wa kisima namba 1, Meneja utafutaji wa Mafuta na Gesi kutoka TPDC, Bi Venosa Ngowi alisema kuwa utafiti huu unakuja kufuatia ukusanyaji taarifa za bonde hilo uliofanyika mwaka 2015 kwa kutumia ndege maalumu. Bi Ngowi alisema baada ya utafiti huo wa kutumia ndege, ulionesha eneo la Bonde la Eyasi Wembere kuwa na miamba tabaka mizuri ambayo inaweza kutumika kwaajili ya utafiti wa Mafuta na gesi hivyo uchorogaji huu wa visima vifupi vya utafiti ni awamu ya pili kufuatia utafiti wa 2015/16.

Bi Ngowi aliendelea kwa kusema kwamba eneo lote la Bonde la Eyasi Wembere ni muhimu kwaajili ya utafiti huo kutokana na aina ya miamba inayopatikana. Akizunguzmia mita zilizochorongwa Katika kisima namba 1 kilichoanza kuchorongwa katika Wilaya ya Igunga amesema tayari zimechoronga mita 116 kati ya 300 zinazopaswa kuchorongwa.

Nae Meneja Mradi wa Utafutaji Mafuta katika bonde la Eyasi Wembere, ndugu Sindi Mduhu alisema eneo la Bonde la Eyasi Wembere ni kubwa na linaanzia katika Mikoa ya Manyara, Singida,Simiyu, Tabora pamoja na Arusha. Baada ya ukusanyaji takwimu za eneoo hilo, kilichofanyika ilikuwa ni kuzichakata na kuzitafsiri ili kuweza kuona ni wapi palio na miamba tabaka yenye kina kirefu ambacho kianweza kutunza mafuta. “Kijiji cha Kining’inila ni mojawapo ya eneo ambalo lilanishwa kama moja ya eneo ambalo uchoroongaji wa visima unaweza kufanyika”.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt James Mataragio aliyefika ene la utafiti kwaajili ya kujionea kinachoendelea katika utafiti huo alisema utafiti huo unafanyika kwa matumaini kuwa Tanzania inaweza kugundua mafuta. “Tunafanya Utafiti kwa kutegemea kwamba kwa kipindi kisichozidi miaka mitano (5) huenda tukagundua mafuta na hivo leo nawadhibitishia watanzania kwamba kazi hiyo inaendelea”. Dkt. Mataragio aliendelea kwa kusema “ kama kule Uganda huenda tukawa na mafuta”.

Uchorongaji huo utafuatiwa na ukusanyaji wa taarifa za mitetemo ili kuonesha maeneo ambayo yanaweza kuwa na mafuta.

Dkt.mataragio aliongeza kwa kusema kuwa ni nia ya dhati ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuhakikisha kwamba TPDC si kwamba tu inachimba gesi yake yenyewe bila pia kuhakikisha inagundua mafuta. “ Mhe. Rais angependa kwamba katika kipindi ambacho atakuwa madarakani tuwe tumekwishagundua mafuta kwani tayari tunayo gesi asilia ambayo kwa mwaka 2020 tutaongeza visima vingine ambavyo tutavifanya wenyewe TPDC na sio kwa kutumia wawekezaji kutoka nje ya nchi”. 

Kwa upande wa ushirikishaji makampuni ya ndani katika utafiti huo, Dkt Mataragio alisema kazi yote inafanywa na TPDC kwa kushhirikiana na STAMICO ambalo ni shirika la Serikali na ndiye Mkandarasi Mkuu katika mradi huo.

Akitaja sifa za maeneo ambayo mafuta yanaweza kugundulika, Dkt.Mataragio alisema ni maeneo ya Bonde la Ufa ambapo kama ilivyo kule nchini Kenya katika eneo la Lokcha au Turkana lipo katika Bonde la Ufa na kule wamegundua mafuta. Vile vile ukienda Uganda Ziwa Albert ambalo lipo katika Bonde la Ufa nao vile vile wamegundua mafuta. Kwa upande wa Tanzania, katika eneo la Ziwa Tanganyika ambalo lipo katika Bonde la ufa kuna matonetone ya mafuta hivyo ni dalili nzuri ya uwezekano wa upatikanaji wa mafuta na tayari ukusanyaji wa taarifa za eneo hilo ulikwishafanyika hivyo kitakachofuatia ni ufuatiliaji.

Dkt. Mataragio aliongeza kwa kutaja gharama za mradi wa uchoorgaji visima hivyo mbapo kwa visima vyote vitatu hadi vikamilike vitagharimu fedha za Kitanzania shilingi milioni mia tatu ambapo katika utafiti wa ndege jumla ya shlingi za Kitanzania shilingi bilioni mbili nukta nne (2.4) zote zikiwa ni fedha za ndani na Serikali. 

Mwenyekiti wa Kijiji cha Kining’inila Christopher Njilezengo ambapo ndipo utafiti huo unafanyika, aliipongeza Serikali kwa kukubali kuwekeza katika mradi huo kwani utakuwa na tija kwa taifa endapo utafanikisha upatikanaji wa mafuta. “Tunaishukuru sana Serikali kupitia TPDC kwani tunaamini ya kwamba wanatekeela sera ya chama cha mapinduzi chini ya uongozi shupavu wa Mhe. Rais Magufuli ambapo asingekuwa yeye basi mambo hayo wasingeyaona”.

Bi. Neema Masanja mkazi wa Kijiji cha Kining’inila ambapo ndipo utaifit uanfanyika aliiipongeza Serikali kwa utafiti huo na kunonesha matumaini makubwa katika utafiti unaofanyika na endapo mafuta yatapatikna. “ Mafuta yakipatikana itawezesha upatikanaji wa fursa mbalimbali kwa wanachi ili kuleta maendeleo katika Kijiji chetu na taifa”.

Tayri baadhi ya wanachi wa Kijiji hicho wameanza kuonja neema ya utafiti huo ambao kuna baadhi yao wamepatiwa kazi mbali mbali zisizohitaji elimu kubwa kama vile upishi, ulinzi pamoja na vibarua.

UFUNGAJI WA MAFUNZO YA UPISHI NA UKARIMU UKUMBI WA SHEIKH IFRISA ABDULWAKIL KIKWAJUNI ZANZIBAR LEO

$
0
0
KATIBU Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ndg. Salum Maulid Salum (kulia) akimkabidhi Cheti Mshiriki wa Mafunzo ya Upishi na Ukarimu Ndg. Rajab Abass Rajab, wakati wa ufungaji wa Mafunzo hayo yaliotolewa na Taasisi ya China National Research Institute of Food&Fermentation Industrieskulia kwa Katibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Mr. Dong Jianhui, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakili Kikwajuni Jijini Zanzibar. Leo
MSHIRIKI wa Mafunzo ya Upishi na Ukarimu yaliotolewa na Taasisi ya China National Research Institute of Food &Fermentation Industries, akitowa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki wa mafunzo hayo yaliowashirikisha Wanafunzi kutoka katika Taasisi za Serikali na Binafsi yaliochukuwa wiki nne.wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.
WASHIRIKI wa Mafunzo ya Upishi na Ukarimu yaliotolewa na Taasisi ya China National Institute of Food & Fermentation Industries, wakiwa katika picha ya pamoja na Vyeti vyao baada ya kukabidhiwa na kufunga mazunzo hayo katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.
KATIBU Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ndg. Salum Maulid Salum akihutubia wakati wa ufungaji wa Mafunzo ya Upishi na Ukaramu yaliotolewa na Taasisi kutoka China National Research Institute of Food &Fermentation Industries, hafla hiyo ya ufungaji wa mafunzo hayo imefanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar
WASHIRIKI wa Mafunzo ya Ukarimu na Mapishi wakionesha kwa vitendo jinsi mafunzo hayo waliyoyapata kupitia Taasisi ya China National Research Institute of Food &Fermentation Industries, wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.
MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya China National Research Institute of Food &Fermantation Industries Mr. Dong Jianhui, akizungumza wakati wa hafla ya ufungaji wa mafunzo hayo ya Upishi na Ukarimu, yaliotolewa na Taasisi yake, hafla hiyo ya ufungaji wa mafunzo hayo imefanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar
WANAFUNZI wa Mafunzo ya Upishi na Ukarimu wakifuatilia hafla hiyo ya ufungaji wa mafunzo yao katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abdulwakil Kikwajuni Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)

Mfumuko wa Bei wa Taifa Washuka hadi Asilimia 3.4

$
0
0
Kaimu mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bi. Ruth Minja akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari leo Oktoba 8, 2019 wakati akitangaza Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Septemba 2019 ambao umeshuka hadi asilimia 3.4 kutoka asilimia 3.6 kwa mwaka unaoishia mwezi Agosti, 2019.
Sehemu ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano na Kaimu mkurugenzi waTakwimu za Jamii na Sensa ya Watu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bi. Ruth Minja leo Oktoba 8, 2019 wakati akitangaza Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Septemba, 2019 ambao umeshuka hadi asilimia 3.4 kutoka asilimia 3.6 kwa mwaka unaoishia mwezi Agosti, 2019.
(Picha zote na MAELEZO)


Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi septemba, 2019 umepungua hadi asilimia 3.4 kutoka asilimia 3.6 kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2019.

Hayo yamesemwa na Kaimu mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watukutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bi. Ruth Minja wakati akitangaza mfumuko wa bei leo Jijini Dodoma.

“Kushuka kwa mfumuko wa bei kunatokana na kupungua kwa bei za bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi cha mwezi Septemba 2019 ikilinganishwa na bei za kipindi cha Septemba,2018”. Alisisitiza Bi. Minja.

Akifafanua amesema kuwa baadhi ya bidhaa zilizopungua bei kwa mwezi Septemba ni mafuta ya taa asilimia 1.0, Petroli asilimia 3.3 ,majiko ya gesi asilimia 1.5, dawa za kuulia wadudu nyumbani asilimia 2.2 na mafuta ya nywele asilimia 1.3.

Aliongeza kuwa mfumuko wa Bei wa bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba, 2019 umeongezeka hadi asilimia 4.0 kutoka asilimia 3.7 kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2019.

Akizungumzia nchi za Afrika Mashariki Bi. Minja amesema kuwa mfumuko wa Bei nchini Kenya kwa mwezi Septemba umepungua hadi asilimia 3.83 kutoka 5.00 kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2019.

Kwa upande wa nchi ya Uganda, mfumuko wa Bei kwa mwaka unaoishia mweziSeptemba 2019 umepungua hadi asilimia 1.9 kutoka asilimia 2.1 kwa mwaka unaoishia mwezi Agosti, 2019.

WAZIRI MKUU AWASILI RUANGWA KUSHIRIKI MBIO ZA MWENGE

$
0
0


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Lindi, Oktoba 8, 2019. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewasili wilayani Ruangwa, mkoani Lindi ili kushiriki mbio za mwenge kitaifa hapo kesho. Mwenge huo umewasili mkoani humo leo.

Akizungumza na viongozi wa kitaifa na kimkoa mara baada ya kuwasili mkoani humo, Waziri Mkuu amesema kesho ataungana na wakazi wa Ruangwa kuupokea mwenge huo. "Kesho nitaungana na wana Ruangwa ili kesho kutwa uendelee wilaya ya Nachingwea," amesema.

Waziri Mkuu ambaye ni mbunge wa jimbo la Ruangwa, amesema: "Nimeiona hamasa kubwa waliyonayo wanaLindi huu ya mapokezi ya mwenge wa uhuru lakini kikubwa zaidi ni ugeni mkubwa wa wageni akiwemo Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli."

Amesema mbali ya maadhimisho ya kumaliza mbio za mwenge nchi nzima, mwaka huu Tanzania inaadhimisha kumbukumbu ya miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa. 

"Tuendelee kuwahamasisha wanaLindi na Watanzania wote washiriki kwenye makongamano yanayofanyika nchini kote. Kumbukumbu ya Baba wa Taifa isaidie kuelimisha vijana wetu ambao hawajui historia ya kazi za waasisi wa Taifa letu."

"Pia walioko madarakani, watumie fursa hii. Waige na kuenzi kazi za viongozi kama Mwalimu Nyerere na pia wajenge tabia ya kujua tabia ya ulipotoka, na mahali ulipo."

Mapema, akitoa taarifa ya maandalizi ya kilele cha mbio za mwenge kwa Waziri Mkuu, Waziri wa Nchi OWM - Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama alisema mbio hizo zilianza Aprili 2, mwaka huu na leo zimeingia Lindi ambao ni mkoa wa 31.

Alisema hadi kufikia tarehe 14, ambayo ni siku ya kilele utakuwa umepita katika Halmashauri 195 za nchi mzima. "Katika kipindi hicho chote, vijana wetu sita ambao ni wakimbiza mwenge, walizindua miradi ambayo wameridhika nayo na ile yenye dosari, hawakusita kuikemea," alisema. 

Alisema makongamano mbalimbali yameandaliwa ili kuenzi kifo cha Baba wa Taifa ambaye Oktoba 14, atatimiza miaka 20. Pia vijana 88 ambao walipanda mlima Kilimanjaro ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu hizo watashiriki sherehe hizo mjini Lndi.

MMOJA WA WATUHUMIWA UHUJUMU UCHUMI VITAMBULISHO VYA TAIFA AKIRI KOSA,AHUKUMIWA KULIPA FIDIA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv.

MMOJA wa watuhumiwa wa uhujumu uchumi wa vitambulisho vya Taifa (NIDA) Astery Ndege, amehukumiwa kulipa fidia ya Sh 293,446,400.23 kama hasara aliyosababisha kwa Mamlaka hiyo kufuatia kukiri kosa lake hilo

Ndege ambaye ni mkurugenzi wa Kampuni ya Aste Insurance Brokers, ameachiwa huru peke yake huku washitakiwa wengine katika kesi hiyo ambao ni aliyekuwa mkurugenzi wa NIDA, Dickson Maimu, Meneja Biashara wa NIDA, Avelin Momburi,  Ofisa Usafirishaji, George Ntalima, Mkurugenzi wa Sheria, Sabina Raymond na Xavery Kayombo wakiendelea kubaki rumande.

Hatua hiyo imekuja baada ya Ndege kuandika barua ya kuomba msamaha kwa DPP, kukiri makosa ya kuisababisha NIDA hasara ya zaidi ya Sh bilioni 1.1 yalipopelekea kuingia kwa makubaliano.

Akisoma hukumu hiyo, hakimu Mkazi Mwandamizi, Salum Ally amesema mshitakiwa atatakiwa kulipa faini ya Sh milioni nne kwa mashitaka mawili aliyokiri ya kuongoza genge la uhalifu na kusababisha hasara hiyo na kuongeza kuwa amezingatia kitendo cha mshitakiwa kukiri kosa lake na sheria inayoelekeza mshitakiwa kulipa faini. 

Mapema kabla ya kusomwa kwa hukumu hiyo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Ladislaus Komanya aliwasomea washitakiwa wote mashitaka 50 badala ya mashtaka 100 yaliyokuwa yakiwakabili awali ambapo amedai washitakiwa wanakabiliwa na mashitaka 50, yakiwemo ya kutumia nyaraka kumdanganya mwajiri, kughushi, kutoa nyaraka za uongo, kutakatisha fedha na kusababisha hasara ya Sh 1,175,785,600.93 kwa NiDA.

Hata hivyo, ni mshtakiwa ndege pekee ndiye amekiri kutenda makosa ya kujihusisha na genge la uhalifu na kusababisha hasara ya zaidi ya Sh bilioni moja, huku wenzake wakikana mashtaka hayo.

Kufuatia kukiri mwenyewe, mahakama ilimtia hatiani.

Wakili Komanya aliiomba mahakama kutoa adhabu kwa mshitakiwa kulingana na makubaliano waliyoingia. Pia amedai mshitakiwa ni mkosaji wa mara ya kwanza na kwamba kitendo cha kaomba msamaha kitasaidia kupunguza msongamano wa watu gerezani. 

Kwa upande wake wakili wa utetezi, Godwin Nyaisa amedai mshitakiwa hajaisumbua mahakama kwa kuwa amekiri na anajutia kosa lake na tayari amekubali kurejesha sehemu ya hasara kama ilivyoainishwa kwenye makubaliano yao.

Amedai mpaka sasa mshitakiwa amekaa gerezani miezi 10 hivyo, anaomba apatiwe adhabu ya faini.
Katika mashitaka  kusababisha hasara inadaiwa Maimu,Ndege na Ntalima wanadaiwa kati ya Julai 19, 2011 na Agosti 31 mwaka 2015 katika maeneo tofauti ya Dar es Salaam kwa udanganyifu walisababisha hasara jumla ya Sh 1,175,785,600.93 kwa NIDA.
Viewing all 110017 articles
Browse latest View live


Latest Images