Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110175 articles
Browse latest View live

WAZIRI LUGOLA AWAKATALIA WALIOPEWA URAIA MAKAZI YA WAKIMBIZI KUSHIRIKI UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA NCHINI

$
0
0
Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi makazi ya Katumba, Mkoani Katavi, leo, ambao amewakatalia raia wa makazi ya Katumba, Ulyankulu na Mishamo kushiriiki uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni, kwa kuwa maombi yao bado yanafanyiwa kazi. 
Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akimsikiliza Mkazi wa Kijiji cha Ndui Station, Kata ya Katumba, Mkoani Katavi, Zephania Mshinga (84) wakati alipokuwa anatoa historia yake alivyokimbia vita Burundi mwaka 1972, na kuingia nchini kwa ajili ya kuokoa maisha yake. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

…………………………………………………

Na Mwandishi Wetu, Katavi

WAZIRI wa Mambo ya ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amesema wananchi waliopewa uraia katika Makazi ya Wakimbizi ya Katumba, Ulyankulu na Mishamo nchini hawatashiriki kugombea na kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni, kwa kuwa maombi yao bado yanafanyiwa kazi.

Akijibu maombi ya raia hao waliopo Kata ya Katumba, Mkoani Katavi, Waziri Lugola alisema maombi yao wanayo na Serikali inayafanyia kazi kwa ukaribu zaidi, hivyo wanapaswa kuwa wavumilivu kusubiri majibu yao.

“Serikali inawajali, inawathamini, na pia maombi yenu tunayo, na tunayafanyia kazi kwa ukaribu zaidi kwa kuwa Serikali ya Rais Dkt. Magufuli ni sikivu, naomba muendelee kusubiri bila kuwa na uharaka wowote,” alisema Lugola.

Akisoma hotuba ya wananchi hao katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Ndui Station, Diwani wa Kata hiyo, Seneta Baraka alisema wananchi hao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo kutopata haki ya kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu 2019.

“Ombi letu kwako mheshimiwa Waziri ni kuturuhusu kufanya uchaguzi katika mazingira haya sawa na ilivyofanyika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, ikiwa haiwezekani basi ombi letu na changamoto zitatuliwe na tupewe fursa ya kufanya uchaguzi mara baada ya changamoto hizo kutatuliwa,” alisema Baraka.

Baraka alisema raia hao walimuomba Waziri huyo, kubalidilisha hadhi ya eneo la Katumba, Mishamo Mkoani Katavi, na Ulyankulu Mkoani Tabora, kuwa na hadhi ya Serikali ya Mitaa kwa kuwa hadhi ya makazi ya wakimbizi inawanyima fursa nyingi za kimaendeleo.

Maombi mengine waliyoyatoa kwa Waziri huyo ni kukamilisha mchakato wa uraia kwa vijana wao uliofanyika mwaka 2017, wakidai kuwa Serikali ilikamilisha mchakato wa uraia wa awamu ya kwanza uliofanyika mwaka 2007, wapo ambao maombi yao hayajakamilika hadi sasa.

Pia waliomba usajili wa laini za simu kwa wenzao ambao hawajakamilisha mchakato wa uraia ili waweze kupata vitambulisho vya taifa.

Akijibu changamoto hizo, Waziri Lugola aliwaambia raia hao maombi hayo yapo mezani kwake na Serikali inayafanyia kazi kwa ukaribu na watapewa majibu mara watakapomaliza kuyafanyia kazi.

Kwa ombi la usajili wa laini za simu, Lugola alisema hiyo ni haki yao kupata vitambulisho, nakuwaahidi kuwa suala hilo litashughuliwa kwa kuwa zoezi hilo ni endelevu.

Kwa upande wake, Mkazi wa Kata hiyo ambaye alikimbia vita mwaka 1972 akitokea nchini Burundi, Zephania Mshinga ambaye ana umri wa miaka 84, alisema Tanzania ni nchi salama, na pia hayupo tayari kuiacha nchi hiyo ambayo ina amani, utulivu, na watu wakarimu.

“Msiombee vita jamani, nilifika hapa Tanzania mwaka 1972 wakati Burundi kulipokuwa na vita, nashukuru nimepewa uraia na kama nikinyang’anywa uraia huu sina mahali pa kwenda, siwezi kurudi nilipotoka maana miaka mingi imepita, sasa ni mkazi wa hapa, naishukuru Serikali ya Tanzania,” alisema Mshinga.

Waziri Lugola yupo Mkoani Katavi kwa ziara ya siku tano ya kikazi, akikagua miradi ya maendeleo, kuzungumza na askari na watumishi wa Wizara yake, pamoja na kusikiliza kero za wananchi katika mikutano ya hadhara mkoani humo.

Waziri Mwakyembe ahudhuria maonesho ya mavazi Tamasha la JAMAFEST

$
0
0

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akifuatilia kwa makini maonesho ya mavazi wakati wa Tamasha la Utamaduni wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) hapo jana katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza akionesha vazi alilobuniwa na mbunifu wa mavazi wakati wa Tamasha la Utamaduni wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) hapo jana katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria maonesho ya mavazi wakati wa Tamasha la Utamaduni wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) hapo jana katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mbunifu mkongwe wa mavazi hapa nchini Tanzania, Mustapha Hassanali akizungumza wakati wa maonesho ya mavazi katika Tamasha la Utamaduni wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) hapo jana katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la JAMAFEST nchini Tanzania, Joyce Fissoo akizungumza wakati wa maonesho ya mavazi katika Tamasha la Utamaduni wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) hapo jana katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa maonesho ya mavazi wakipita jukwaani wakati wa Tamasha la Utamaduni wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) hapo jana katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akifuatilia ratiba kwa makini ya maonesho ya mavazi wakati wa Tamasha la Utamaduni wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) hapo jana katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Mshindi wa taji la Dunia kwa warembo wasiosikia, Winfrida Brayson aki

DANGOTE APEWA WIKI MOJA KUWASILISHA RIPOTI YA UTENDAJI TIC

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika masuala ya Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki akioneshwa namna mfumo wa TEHEMA unavyorahisisha utendaji kiwandani hapo na Mhandisi Brezil Omary wakati wa ziara yake kiwandani hapo.
Sehemu ya wajumbe waliposhiriki katika kikao cha majumuisho ya ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki wakati wa ziara yake katika kiwanda cha Dangote Mkoani Mtwara.
Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Sekta ya Uzalishaji Balozi Celestine Mushi akizungumza jambo wakati wa kikao hicho.
Viwango wa Kiwanda cha kutengeneza saruji cha Dangote Bw. Issawema akiwaonesha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika masuala ya Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki pamoja na Naibu Waziri ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula matumizi ya mifumo ya TEHAMA katika kuendesha kiwanda hicho.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika masuala ya Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki akisisistiza jambo kwa uongozi wa kiwanda cha kutengeneza Saruji cha Dangote kilichopo Mkoa Mtwara alipotembela kukagua na kusikiliza changamoto za wawekezaji mkoani humo.Katikati ni Mtendaji Mkuu wa kiwanda hicho Bw.Jagat Rathee.
…………………………………………………….



Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji Mhe. Angellah Kairuki ametoa muda wa wiki moja kwa Kiwanda cha kutengeneza saruji cha Dangote kuwasilisha taarifa ya utendaji ambazo kwa zaidi ya miaka miaka mitatu hawajaziwasilisha Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kama sheria na taratibu za nchi zinavyoelekeza.

Waziri Kairuki ambaye aliongozana na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula Katika ziara yake ya kutembelea, kukagua maeneo mbalimbali ya uwekezaji na kuongea na wawekezaji na wafanyabiashara wa Mkoa wa Lindi septemba 27,2019 ameuelekeza uongozi wa kiwanda hicho kuhakikisha kila baada ya miezi sita wanawasilisha taarifa za kiutendaji TIC.

Waziri Kairuki aliwaeleza masikitiko yake viongozi wa kiwanda hicho kwa kutowasilisha taarifa za utekelezaji wao ikiwemo zinazohusu historia ya mradi, mipango ya upanuzi, kodi wanazolipa, faida pamoja na changamoto wanazokabiliana nazo na ushauri wao.

“Nimesikitishwa sana na suala hili la kutopeleka taarifa zenu TIC ambapo inafahamika suala hilo ni la kisheria na lazima litekelezwe kwa wakati,hivyo kuanzia sasa nimewapa wiki moja mhakikishe taarifa hizo zinawasilishwa haraka,”alisisitiza Waziri Kairuki.

Aidha amewapongeza Dangote kwa uwekezaji huo mkubwa pamoja na kuanza ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme wao wenyewe megawati 25 ambao megawati 5 zitaingia kwenye gridi ya taifa.

Amewataka wawekeze na maeneo mengine siyo kwenye saruji tu na kuagiza TIC kupitia mikataba ya utendaji ya wawekezaji wote mahiri kuona ni wapi wanaweza kuwekeza zaidi.

Wakiwa Mkoani Lindi Waziri Kairuki na Mhe. Mabula walitembelea mgodi wa madini ya uno (graphite) uliopo katika Kijiji cha Matambalale Kusini Wilaya ya Ruangwamkoani Lindi na kuona shughuli za awali za mradi huo ambapo Meneja wa kampuni ya Lindi Jumbo inayochimba madini hayo Bw Paul Shauri amesema mgodi utajengwa kwa muda wa miezi tisa na wanatarajia kuwekeza zaidi ya dola za kimarekani milioni 30.

Akiongea mgodini hapo Dkt.Mabula ameziagiza Halmashairi zote vijiji vyenye maeneo ya uwekezaji kufanya zoezi la kuandaa mpango wa matumizi ya ardhi watenge maeneo ya uwekezaji wayahaulishe yawe mali ya kijiji ili mwekezaji akipatikana watimize masharti mengine tu.

“Hakuna sababu ya mwekezaji kuanza kuhangaika na mambo madogo kama hayo ambayo yanampotezea wakati ni lazima halmashauri zijipange ili kumwekea mwekezaji mazingira mazuri avutiwe kuwekeza”alisema Dkt.Mabula

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Hashim Mgandilwa akiwakaribisha Mawaziri hao amesema Serikali ione kuna sababu ya kuharakisha ujenzi wa miundombinu ikiwemo barabara za wilaya hiyo kwani kuna makampuni mengi makubwa yameonesha nia ya kuwekeza.

Amesema wilaya hiyo pia inakabiliwa na changamoto ya mipaka ya asili na kwamba suala hilo tayari linaendelea kutatuliwa kwa viongozi na watendaji kutoa elimu kwa wananchi.

ZIARA YA WAZIRI KAIRUKI MGODI WA MADINI YA GRAPHITE RUANGWA -LINDI

$
0
0
Meneja wa Kampuni ya Uchimbaji madini ya Lindi Jumbo Paul Shauri akionesha michoro ya muonekano wa eneo la mgodi wa madini aina ya uno (Graphite) wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika masuala ya Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki pamoja na Naibu Waziri ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula.
Naibu Waziri ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula akizungumza jambo wakati wa kikao cha majumuisho cha ziara ya kutembelea miradi ya uwekezaji katika Wilaya ya Ruangwa mkoni Lindi pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika masuala ya Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki (aliyekaa kulia) kilichofanyika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Bw. Hashim Mgandilwa akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa kikao hicho cha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika masuala ya Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki pamoja na Naibu Waziri ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula katika ofisi zake Mkoani Lindi.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Ruangwa Bw. Barnabans Essau akisalimia wakati wa kikao hicho.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika masuala ya Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki pamoja na Naibu Waziri ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angelline Mabula wakiwa katika ziara ya kukagua eneo lililotengwa kwa ajili ya uchimbaji wa madini aina ya uno (Graphite) lililopo Wilayani Ruangwa Lindi Septemba 27, 2019.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

NDITIYE: HUTAWEZA KUPIGA WALA KUPIGIWA MPAKA USAJILI LAINI YAKO

$
0
0
Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanzakushoto)akikabidhi kitabu chenye orodha ya minara iliyojengwa na Mfuko waMawasiliano kwa Wote kwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Kibondo, Ayubu Sebabili, akiwa ziarani Kigoma. Anayeshuhudia wa kwanza kulia ni Justina Mashiba, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mfuko huo.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) akimsikiliza kwa makini Justina Mashiba (wa kwanza kushoto), Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, akitoa maelezo kuhusu mnara wa Itaba wakati wa ziara yake ya kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano, Kigoma.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) akitoa maelekezo kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Justina Mashiba ((wa kwanza kushoto) ya kuhakikisha kuwa mnara wa Itaba, unawaka muda wote ili wananchi wapate mawasiliano, akiwa ziarani Kigoma.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye
(aliyesimama)akihamasisha wananchi wa Kijiji cha Kigina kusajili laini za simu zao za mkononi wakati wa ziara yake mkoani Kigoma ya kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (anayetembea mbele) akitoka kukagua mnara wa Itaba akiwa katika ziara yake ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano mkoani Kigoma.

****************************

Na Prisca Ulomi, Kigoma.

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amesema kuwa mwananchi hataweza kupiga wala kupigiwa simu kama hajasajili laini ya simu yake ya mkononi kwa alama za vidole ifikapo tarehe 31 Desemba, 2019.

Nditiye ameyasema hayo akiwa kwenye ziara yake ya kikazi Mkoani Kigoma kwenye wakati akihamasisha na kuelimisha wananchi wa Kata ya Ruhita, Kibuye, Mrufiti, Itaba, Murungu, Rugongwe, Kasulu na Kibondo mjini umuhimu wa kusajili laini zao za simu za mkononi.

“Serikali imeamua watanzania wote wasajili laini zao za simu za mkononi kwa kutumia alama za vidole ili kila anayepiga simu au kupigiwa atambulike ili kupunguza changamoto zinazojitokeza ili mawasiliano yaweze kuchangia kikamilifu uchumi wa chi yetu,” amesema Nditiye.

Amefafanua kuwa Sekta ya Mawasiliano imeshika nafasi ya tatu kwa mwaka 2016/2017 na ya nne kwa mwaka 2017/18 kwa kuchangia pato la taifa kwa kiwango cha asilimia 13.1 na kuwa kati ya Sekta tano bora zinazochangia pato la taifa. Serikali ieamua kusimamia kikamiifu Sekta hii ili kuhakikisha kuwa inadhibiti wizi wa mtandaoni kupitia simu za mkononi, ulaghai, uchochezi, utapeli a matumizi mengine ya simu za mkononi kwa kuwa kila mwanachi atakuwa amesajili laini yake ya simu ya mkononi kwa alama ya kidole.

Amewahamasisha wananchi waishio maeneo mbali mbali mkoani humo wakatialipofanya nao mkutano wa hadhara kuwa kuanzia mwezi Oktoba mwaka huu,wataalamu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania wakiambatana na kampuni za simu za mkononi, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Jeshi la Polisi na Uhamiaji watafika maeneo mbali mbali mkoani humo ili kuendesha zoezi la kusajili laini za simu kwa wananchi wote wanaotumia na kumiliki simu za mkononi.

Amesema kuwa zoezi hili litafanyika kwa umakini mkubwa ili kuhakikisha kuwawatanzania halali wanaotambulika na wenye kadi ya NIDA au namba ya utambulisho kutoka NIDA wanasajili laii zao ili kuepusha kufanya usajili kwa watu wasiohusika kwa kuwa mkoa wa Kigoma uko mpakani ambapo kuna mwingiliano wa watu kutoka nchi za jirani.

Naye Japhet Amos, mkazi wa kijiji cha Kigina kilichopo kata ya Rugongwe, Kigoma akizungumza kwa niaba ya wananchi wenzake alimuomba Nditiye kuhakikisha kuwa wananchi wanapata kitambulisho cha NIDA au namba ya utambulisho kwa wakati ili wasizimiwe simu zao mara baada ya tarehe ya wisho iliyowekwa na Serikali kufika a kuomba huduma hiyo ya usajili itolewe bure.

Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Kanda ya Kati, Antonio Manyandaaliwafahamisha na kuwatoa hofu wananchi wote nchi nzima kuwa huduma ya kusajili laini ya simu ya mkononi kwa alama ya kidole ni bure na hakuna mwananchi yeyote atakayelazimika kulipia gharama hiyo na ametoa wito kwa wananchi kuiarifu TCRA yenye ofisi zake sehemu mbali mbali nchini kuhusu jambo hilo endapo mwananchi yeyote atatozwa gharama za kusajili laini yake na wakala wa kampui yeyote ya simu.

“Usajili wa laini ya simu kwa alama ya vidole ni bure nchi nzima, mwananchi haruhusiwikulipa gharama yeyote kwa ajili ya kusajili laini ya simu,” amesisitiza Manyanda.

Katika hatua nyingine, akiwa ziarani mkoani humo, Nditiye amekagua upatikanaji wamawasiliano kwenye kata ya Kibuye, Murungu, Rugongwe na Itaba na kutembeleaminara inayotoa mawasiliano kwa wananchi waishio maeneo hayo na kubaini uwepowa mawasiliano wakati wa asubuhi na jioni na kufifia au kukosekana kabisa wakati wausiku ambapo ameiagiza UCSAF kwa kushirikiaa na TCRA na kampuni za simu zenyeminara yake maeneo hayo kuongeza betri za kutosha ili kuapata umeme wa jua wakuendesha minara hiyo kwa lengo la kuwawezesha wananchi kupata huduma za
mawasiliano hata nyakati za usiku.

“Mawasiliano yako chini sana, mtu anapatikana kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumina moja jioni, matukio yanatokea usiku hatuna msaada na tuna mtandao mmoja tu waVodacom,” amesema Emil Mfanye, Diwani wa Kata ya Murungu akizungumza kwaniaba ya wananchi kwenye mkutano wa hadhara wa Nditiye na wakazi wa kijiji chaKumhasha alipokuwa kwenye ziara yake mkoani humo ya kukagua upatikanaji wahuduma za mawasiliano, kuhamasisha wananchi kusajili laini za simu kwa alama ya
vidole na kutoa elimu ya manufaa ya anwani za makazi na postikodi

KISA CHA NYOKA ALIYEVAMIA MKUTANO WA WAZIRI MKUU

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemzawadia Askari Polisi PC Alphonce Daniel Mwambenga sh. 200,000 kutokana na ujasiri wake wa kumdhibiti kwa kumkanyaga nyoka mkubwa aliyekuwa akieleakea jukwaa kuu wakati Waziri Mkuu akihutubia katika Kilele cha Wiki ya Viziwi Duniani kwenye Uwanja wa Kichangani, Kihesa mjini Iringa, Sepotemba 28, 2019. Kitendo hicho kilifanyika kimyakimya hivyo hapakuwa na taharuki yoyote . Pichani, Mheshimiwa Majaliwa akimkabidhi Mwambenga fedha hizo. Wapili kulia ni Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa, kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Stella Ikupa na kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara y a Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Dkt.Avemaria Semakafu. Wa tatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happy na wa nne kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Dkt. Abel Nyamkahanga. 
Askari Mwambenga akiwa amemkanyaga nyoka huyo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Nyoka akiuawa na baada ya kuuawa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Mfumo wa LIPA wa Vodacom M-Pesa unaleta mapinduzi katika mifumo ya malipo Tanzania

$
0
0

· Maelfu wahudhuria gulio la Vodacom M-pesa jijini Dar es salaam. 

· Wateja na Umma kwa ujumla kunufaika na huduma za M-pesa zinazoruhusu malipo kwenda mitandao na mabenki yote. 

Kampuni ya mawasiliano ya simu inayoongoza Tanzania, Vodacom Tanzania PLC leo imezindua huduma yake ya LIPA KWA SIMU katika gulio la M-pesa lililofanyika Mlimani City Mall jijini Dar es salaam. Gulio hilo lina lengo la kuongeza ufahamu wa upana wa huduma za kifedha zinazotolewa na mfumo wake mpya wa malipo. 

Akiongea wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa M-Pesa Epimack Mbeteni alisema kwamba Vodacom Tanzania iliona hitaji la kupanua mfumo wa LIPA kwa M-Pesa kutoka katika mfumo wa M-Pesa, na kuanza kupokea malipo kutoka mitandao na benki zote na kufikia katika kuwezesha malipo ya kidijitali katika mifumo ya rejareja na manunuzi mitandaoni. 

Amesema kwamba Vodacom imezindua huduma ya "Lipa Kwa Simu" kuhamasisha matumizi ya mifumo ya malipo ya kidijitali kama njia kuu ya malipo nchini, na kuhama kutoka katika utegemezi mkubwa wa fedha taslimu uliopo sasa. 

"Lipa kwa Simu ni hatua ya kimapinduzi iliyochukuliwa na kampuni ya Vodacom kuelekea katika kujenga jamii isiyotumia fedha taslimu kwa kusaidia ushirikiano wa malipo katika mitandao na benki zote. Kwa kutumia huduma ya Lipa kwa Simu, wafanyabiashara na wamiliki wa biashara wanaweza kupokea malipo kutoka katika mitandao na benki zote na kuongeza ufanisi na usalama katika biashara zao. Na kwa upande wa wateja, bila kujali unatumia mtandao gani, sasa unaweza kufanya malipo kupitia mfumo wa LIPA kwa kutumia gharama za kawaida za kuhamisha fedha. Jambo ambalo linaondoa mahitaji ya kutembea na kiasi kikubwa cha fedha taslimu," alisema Mbeteni. 

Vodacom imewezesha LIPA kwa Simu kwa makundi mbalimbali ya wafanyabiashara wa sekta zote kama Baa, Hoteli, migahawa, Supamaketi, Vituo vya mafuta, kumbi za sinema, maduka ya dawa, Maduka ya vifaa vya ujenzi na kadhalika kwahivyo inapatikana kote. 

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi wa TRA, Richard Kayombo ameipongeza huduma hii inayotolewa na M-Pesa na kusema kwamba imerahisisha na kuleta ufanisi katika mifumo ya malipo ya Umma kwa sababu sasa wateja wanaweza kulipia bili, tozo na huduma nyingi za kijamii kupitia mfumo huu wakiwa sehemu yeyote ile, iwe nyumbani au maeneo yao ya kazi. 

"Serikali inajivunia kuwa mshirika katika huduma ya fedha kupitia simu za mkononi, kwa sababu watu wanaweza kufanya malipo kwetu. Iwe katika mifumo ya mahakama za manispaa, polisi au huduma za afya na nyinginezo. Jambo hili limeongeza uwazi na hali ya kukidhi taratibu za malipo kwa jamii," aliongeza Kayombo. 

Gulio la M-Pesa lililofanywa na kampuni ya Vodacom lilivutia maelfu ya wateja, wafanyabishara na jamii kwa ujumla ambao walikuja kujifunza na kuona jinsi ambavyo mfumo mpya wa Lipa kwa Simu umerahisisha huduma ya malipo nchini. 

Kwa upande wake, Bi Mwajuma Hamisi amesherehekea mfumo wa Lipa kwa Simu akisema kwamba ni mfumo ambao utaleta mabadiliko kwa kuwa hakutakuwa na haja tena ya kutembea na kiasi kikubwa cha fedha au kulipia gharama za miamala za kuhamisha fedha kutoka benki kwenda katika simu za mkononi. 

"Nimenunua vipodozi na vitu vingine kutoka kwa wafanyabiashara mbalimbali hapa katika gulio na nilichofanya ni kuscan msimbo wa majibu ya haraka (QR Code) katika tili ya Lipa kwa Simu na niliweza kulipa moja kwa moja kutoka katika benki yangu. Hii ina maanisha kwamba ninaweza sasa kufuatilia malipo yangu yote kadri yatakavyokuwa yanafanyika kutoka benki," aliongeza bi Mwajuma.

Msemaji Mkuu wa Jeshi la Uhamiaji, Mrakibu Mwandamizi Al-Hajj Ally Mtanda akitoa maelezo kuhusiana na huduma za idara ya Uhamiaji kwa Mkurugenzi wa M-pesa Vodacom Tanzania PLC, Epimack Mbeteni leo jijini Dar Es Salaam, kwenye gulio la M-Pesa (M-Pesa Expo).

Wasanii watakaokiwasha Tigo Fiesta 2019 _Saizi yako jijini Mwanza watembelea Duka la Tigo leo.

$
0
0


Msanii bongofleva Billnass akisajili laini yake kwa mfumo wa alama za vidole alipotembelea duka la Tigo eneo la Samaki barabara ya Stesheni jijini Mwanza.Mapema leo kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Tigo Fiesta 2019_Saizi yako Jijini Mwanza.
Msanii wa Nyimbo za Injili Goodluck Gozbert akiwa Pamoja na msanii chipukizi wa Bongofleva Badest walipofika kusajili laini zao kwa alama za vidole na kuona huduma mali mbali duka la Tigo eneo la Samaki barabara ya Stesheni jijini Mwanza.Mapema leo kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Tigo Fiesta 2019_Saizi Yako Jijini Mwanza.

Msanii bongofleva kutoka kundi la Weusi Gnako akisajili laini yeke kwa mfumo wa alama za vidole katika duka la Tigo eneo la Samaki barabara ya Stesheni jijini Mwanza Anayeshuhudia pembeni yake ni Meneja Huduma kwa wateja kanda ya ziwa Beatrice Kinabo.Mapema leo kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Tigo Fiesta 2019 Jijini Mwanza.
Msanii bongofleva Billnass akiangalia simu zinazouzwa katika duka la Tigo eneo la Samaki barabara ya Stesheni jijini Mwanza pembeni yake ni Meneja Huduma kwa wateja kanda ya ziwa Beatrice Kinabo.Mapema leo kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Tigo Fiesta 2019 Jijini Mwanza.
Wasanii watakaotumbuiza katika tamasha la Tigo Fiesta 2019 _Saizi yako Jijini Mwanza wakifurahi jambo mara baada ya kutembelea na kusajili laini kwa alama za vidole na kuona huduma mbalmbali zinazotolewa na duka la Tigo eneo la Samaki barabara ya Stesheni jijini Mwanza.Mapema leo kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Tigo Fiesta 2019 Jijini Mwanza.
Wasanii watakaotumbuiza katika tamaha la Tigo Fiesta 2019 _Saizi yako Jijini Mwanza wakiwa katika picha ya Pamoja mara baada ya kutembelea na kusajili laini kwa alama za vidole na kuona huduma mali mbali duka la Tigo eneo la Samaki barabara ya Stesheni jijini Mwanza.Mapema leo kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Tigo Fiesta 2019 Jijini Mwanza.

Ali Kiba apagawisha sherehe za miaka sita ya ‘Six Degrees South’

$
0
0
MSANII wa Bongo Flava Ali Kiba (King Kiba) akitowa burudani wakati wa hafla ya kusherehekea miaka 6 ya Mgahawa wa Six Degrees South, mitaa ya Mji Mkongwe wa Zanzibar.(Picha na Othman Maulid).
MSANII wa Kizazi Kipya Bongo Flava King Kiba Ali Kiba akilishambulia jukwaa la mgahawa wa Six Degrees South Shangani Jijini Zanzibar, wakati wa hafla hiyoiliofanyika jana usiku.(Picha na Othman Maulid)

SMZ YATILIANA SAINI NA MFUKO WA KHALIFA FUND LEO UAE.

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein na Mrithi wa Utawala wa Abu Dhabi na Naibu Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi wa Nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan, wakishuhudia utiaji wa saini, kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar umewakilishwa na Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe. Balozi.Mohamed Ramia Abdiwawa na kwa upande wa Mfuko wa “Khalifa Fund” umewakilisha na Mwenyekiti wa Mfuko wa “Khalifa Fund” Sheikh. Hussain Ali Nowais alisaini kwa niaba ya Serikali ya (UAE). (Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Mrithi wa Utawala wa Abu Dhabi na Naibu Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi wa Nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan,baada ya kumalizika kwa hafla ya utiaji wa saini na Mfuko wa Khalifa Fund, uliofanyika katika makaazi ya Mtawala huo Mjini Abu Dhabi leo.(Picha na Ikulu).
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akiwa katika picha ya pamoja (kushoto) Mrithi wa Utawala wa Abu Dhabi na Naibu Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi wa Nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan,na Mwenyekiti wa Mfuko wa “Khalifa Fund” Sheikh. Hussain Ali Nowais, na kulia Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe.Balozi Mohammed Ramia Abdiwawa.(Picha na Ikulu)

WACHEZAJI LUGALO UGANDA WACHUANA VIKALI TANZANIA LADIES OPEN MOSH

$
0
0

Wachezaji Kutoka kulia Merci Nyanchama wa Kenya Peace Kabasweka wa pili kulia wakibadilishana matokeo na Angel Eaton wakwanza Kushoto na Hawa Wanyenche wa Pili Kushoto wote wa Lugalo mara baada ya kumaliza mchezo kwa Siku ya pili ya mashindano ya wazi ya Wanawake Tanzania katika Uwanja wa TPC Moshi (Picha na Luteni Selemani Semunyu).

Wachezaji Merci Nyanchama wa Kenya na Peace Kabasweka kulia na Angel Eaton na Hawa Wanyenche kushoto wa Lugalo wakipongezana mara baada ya kumaliza mchezo kwa Siku ya pili ya mashindano ya wazi ya Wanawake Tanzania katika Uwanja wa TPC Moshi (Picha na Luteni Selemani Semunyu).

********************************

Na Luteni Selemani Semunyu

Mashindano ya golf ya wanawake Tanzania yamefikia siku ya pili huku wachezaji kutoka klabu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo wakichuana vikali na mchezaji kutoka Uganda Peace Kabasweka.

Mchezaji huyo wa Uganda aliongoza tangu siku ya kwanza kwa fimbo mbili dhidi ya Angel Eaton wa Lugalo akifuatiwa na Hawa Wanchenche wa Lugalo pia.

Licha ya kuongoza kwa fimbo mbioli siku ya kwanza mchezaji huyo kutoka uganda alisema bado mchezo ni mgumu na matumaini ya kuibuka na ushindi bado ni magumu na mwamuzi ni siku ya mwisho ya mchezo

“ Wachezaji kutoka Lugalo ni Wakali na Wanajituma na Idadi ya Fimbo ninazoongoza ni chache hivyo ukifanya mzaha kidogo basi ni rahisi kufungwa hivyo bado naweza kusema Mchezo ni Mgumu” Alisema Kabasweka

Naye Mchezaji kutoka Lugalo Angel Eaton aliyekuwa akimfuatia alisema peace ni Mchezaji mzuri na mchezo bado uko upande wake lakini hakuna kukata tamaa mpaka dakika ya mwisho.

“ Nimetumwa na klabu yangu ushindi hivyo nitapambana kuhakikisha ubingwa unakwenda lugalo mengine tumwachie mungu kwani kuna wachezaji wazuri tu na wanacheza vizuri mpaka sasa “ Alisema Angel.

Kwa Upande wake mchezaji Hawa Wanchenche naye kutoka kutoka klabu ya Lugalo alisema wamepangwa kundi moja leo kutokana na mchezao mzuri na hapa tunawania ubingwa lakini pia nafasi kushiriki mashindano nchini Uganda.

Kutoka Kenya ambao nao wameshiriki katika mashindano haya mchezaji Merci Nyanchama kutoka kwa upande wake alisema amecheza vibaya hivyo hana matumaini ya ushindi lakini kiujumla mashindano ni mazuri na yamevutia.

WAZIRI MKUU MGENI RASMI SIKU YA WAZEE DUNIANI

$
0
0
Kamishna wa Ustawi wa Jamii Dkt. Naftali Ng’ondi akizungumza na waandishi wa habari leo mkoani Mtwara kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani Oktoba Mosi yatakayofanyika Kitaifa Mkoani Mtwara kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Mkoa wa Mtwara Meja Mstaafu Mohamed Mbwana, kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa Jamii Bi. Mwanaisha Moyo na wa pili kushoto ni Katibu wa Baraza la Wazee Mkoa wa Mtwara Mzee Seif Namtapika.
Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa Jamii Bi. Mwanaisha Moyo akielezea jinsi Serikali ilivyojipanga kuwahudumia Wazee nchini katika kikao na waandishi wa habari leo mkoani Mtwara kuhusu Maadhiishoya Siku ya Wazee Duniani Oktba Mosi yatakayofanyika Kitaifa Mkoani Mtwara.
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Mkoa wa Mtwara Meja Mstaafu Mohamed Mbwana akielezea ushiriki wa Wazee katika Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yatakayofanyika kitaifa Oktoba Mosi Mkoani Mtwara wa pili kulia ni Kamishna Wa Ustawi wa Jamii Dkt. Naftali Ng’ondi.Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW.

*****************************************

Na Mwandishi Wetu Mtwara

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (MB), anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yatakayofanyika katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Manispaa ya Mtwara, Mkoani Mtwara.

Hayo yamesemwa leo mkoani humu na Kamishna wa Ustawi wa Jamii Dkt. Naftali Ng’ondi alipokuwa akitoa taarifa kuhusu Siku ya Wazee Duniani kwa niaba ya Wazriri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinisia, Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu.

Kamishna Ng’ondi amesema kuwa Chimbuko la Siku ya Kimataifa ya Wazee ni tamko la Baraza la Umoja wa Mataifa kupitia azimio Na. 45/106 la Mwaka 1990 ambalo linazitaka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuadhimisho siku ya Kimataifa Wazee kila ifikapo tarehe 01 Oktoba ya kila Mwaka.

“Lengo ni kuongeza uelewa wa jamii kuhusu haki na mahijaji ya wazee. Kwa msingi huu, kupitia siku hii jamii hupata fursa ya kutafakari mafanikio, fursa na changamoto ili kuendelea kuboresha hali ya maisha ya Wazee” alisema Kamishna Ng’ondi.

Ameongeza kuwa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wazee Duniani hutoa fursa kwa wazee wenyewe, Serikali, Jamii, Vyama vya Siasa, Madhehebu ya dini na Mashirika yasiyo ya Kiserikali kuungana, kushiriki, kutafakari, kubainisha na kutatua changamoto zinazowakabili wazee katika utekelezaji wa maazimio, mikataba na matamko mbalimbali ya Kikanda na Kimataifa yanayowawezesha wazee kuleta maendeleo yao na jamii nzima.

Ameitaja Kauli Mbiu kwa mwaka huu kuwa ni “Tuimarishe Usawa Kuelekea Maisha ya Uzeeni” ikiwa na lengo la kuhimiza nchi wanachama kuweka Mipango na mikakati ya kupunguza tofauti za watu katika jamii na kutoa fursa kwa makundi maalum kufaidika na fursa zilizopo na maendeleo yaliyofikiwa katika nchi husika.

Amesisitiza kuwa Serikali imejidhatiti katika kutoa huduma kww wazee ukizingatia ongezeko la idadai ya wazee duniani huku taarifa zinaonesha kuwa idadi ya Wazee duniani inaendelea kuongezeka. Kwa sasa wazee wanakadiriwa kufikia milioni 700 duniani. Idadi hii inatarajia kufikia bilioni 2 ifikapo kwama 2050 na kufanya asilimia 20 ya idadi ya watu wote duniani kuwa ni wazee. Aidha, nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania zitakuwa na ongezeko kubwa la wazee. Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, Tanzania inakadiriwa kuwa na Wazee 2,507,568 (Wanawake 1,307,358, Wanaume 1,200,210) sawa na asilimia 5.6 ya wananchi wote.

“Ongezeko hili la idadi ya wazee ni kiashiria cha kuendelea kuimarika kwa hali ya upatikanaji wa huduma za msingi kwa jamii ikiwemo huduma ya afya ,upatikanaji wa chakula na huduma bora za matibabu; hivyo kuchangia kuongezeka kwa umri wa kuishi. Sote hatuna budi kujivunia na kuenzi mafanikio haya” alisisitiza Kamishna Ng’ondi.

Kwa upande wake Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa Jamii Bi. Mwanaisha Moyo amesema kuwa Wizara kwa kushirikiana na uongozi wa mkoa wa Mtwara watatoa huduma za afya na Ustawi wa Jamii kwa wazee na wananchi wote wakakojitokeza katika madhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yakayoanza terehe 29 mwezi wa Tisa mpaka kilele Oktoba Mosi.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Mkoa wa Mtwara Meja Mstaafu Mohamed Mbwana ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muu gano wa Tanznaia Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwjali wazee katika huduma za Afya na msamaha wa kodi za majengo ya makzi ila wameiombaSerikali kupeleke mswaada wa Sheria ya Wazee Bungeni ili kundi hilo litambulike kikamlifu

NAIBU WAZIRI JULIANA SHONZA NA SUBIRA MGALU WANOGESHA MAONYESHO YA MAVAZI YA JAMAFEST 2019

$
0
0
 Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Juliana Shonza akipita kuonyesha mavazi wakati maonyesho ya Mavazi ya Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST 2019) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Wanamitindo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (kulia) akipita mwanamitindo kuonyesha mavazi. 
Naibu Waziri wa Nishati Mhe Subira Mgalu akipita kuonyesha mavazi wakati maonyesho ya Mavazi ya Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST 2019) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST 2019), Bi. Joyce Fisoo akipita kuonyesha mavazi.
Mbunge wa Viti maalumu (CCM), Halima Bulembo akipita kuonyesha mavazi wakati maonyesho ya Mavazi ya Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST 2019) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Mwanamitindo akipita kuonyesha vazi la ubunifu wakati maonyesho ya Mavazi ya Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST 2019) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe afuatilia maonyesho ya mavazi ya Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST 2019) yaliyofanyika Dar es Salaam, Tanzania.
 Mbunifu wa mavazi Mustafa Hassanali akizungumza wakati maonyesho ya Mavazi ya Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST 2019) yaliyofanyika usiku wa leo jijini Dar es Salaam, Tanzania.
 Mshereheshaji Taji Liundi akiunguruma katika maonyesho ya Mavazi ya Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST 2019) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Wanamitindo wenye mahitaji maalum wakionyesha mavazi katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST 2019) yaliyofanyika usiku wa leo jijini Dar es Salaam, Tanzania.
 Mbunifu wa mavazi Khadija Mwanamboka akipita katika wakati maonyesho ya Mavazi ya Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST 2019) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Wanamitindo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakipita kuonyesha mavazi wakati maonyesho ya Mavazi ya Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST 2019) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe akizungumza wakati wa maonyesho ya mavazi ya Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST 2019) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe akimvalisha tuzo maalum ya mavazi ya Vazi la JAMAFEST 2019 kwa Mwanamitindo Whitney yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe akipewa zawadi ya kofia na Mbunifu wa Mavazi kutoka nchini Burundi.
Burudani ya ngoma ikiendelea.
Wanamitindo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakipita kuonyesha mavazi wakati maonyesho ya Mavazi ya Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST 2019) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.

SERIKALI INATAMBUA UMUHIMU WA LUGHA ZA ALAMA-MAJALIWA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha nakala za andiko la Urasimishaji wa Lugha za Alama Tanzania aliouzindua katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Viziwi Duniani kwenye uwanja wa Kichangani, Kihesa mjini Iringa, Septemba 28, 2018. Kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Stella Ikupa na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happy. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu






Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Urasimishaji wa Lugha za Alama Tanzania katika Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Viziwi Duniani kwenye uwanja wa Kichangani, Kihesa mjini Iringa, Septemba 28, 2018. Kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Stella Ikupa na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happy. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Baadhi ya washiriki wa Maadhimisho ya Kilele cha Wiki ya Viziwi Duniani wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia kwenye uwanja wa Kichangani, Kihesa mjini Iringa, Septemba 28, 2019. (Picha na OIfisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia washiriki wa Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Viziwi Duniani kabla ya kuhutubia kwenye uwanja wa Kichangani, Kihesa mjini Iringa Septemba 28, 2019. Kulia ni Mkalimani wa Lugha ya Alama, Jonathan Livingstone. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).





WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali inatambua umuhimu wa kuwa na lugha moja ya alama ili kuwezesha mawasiliano ya watumiaji wa lugha hiyo, hivyo itaendelea kusimamia uendelezaji, usanifu na urasimishaji wa Lugha ya Alama ya Tanzania, ambao ameuzindua leo(Jumamosi, Septemba 28, 2019). 

Amesema hatua hiyo itawezesha utoaji wa elimu katika ngazi mbalimbali pamoja na kuboresha mawasiliano katika jamii na tayari imetoa mafunzo ya lugha hiyo awamu ya kwanza kwa walimu 82 wa shule za Sekondari nchini na kwamba zoezi hilo ni endelevu.

Ameyasema hayo leo (Jumamosi, Septemba 28, 2019) wakati akihutubia wananchi kwenye kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Viziwi Duniani katika Uwanja wa Kichangani – Kihesa, wilayani Iringaakiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Iringa. 

Kaulimbiu ya siku ya Viziwi Duniani kwa mwaka huu inasema “Haki ya Matumizi ya Lugha ya Alama kwa wote”. Kaulimbiu hiyo inalenga kuondoa vikwazo vya mawasiliano miongoni mwa Watanzania ambao ni Viziwi.

“Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo imeanza kurasimisha Lugha ya Tanzania, kutayarisha vifaa vya kufundishia Lugha ya Alama ya Tanzania na kufundisha walimu katika shule za Msingi na Sekondari nchini. Mchakato huo utachukua muda wa takribani miaka miwili kukamilika.”

Amesema Serikali itahakikisha kuwa lugha ya alama ya Tanzania inatambulika na kutumika kikamilifu kama chombo cha mawasiliano miongoni mwa Viziwi nchini ili kuwawezesha kushiriki katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa Taifa lao. 

Waziri Mkuu ameongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imedhamiria na inatekeleza kwa dhati jitihada za kutoa kipaumbele kwa Watanzania wanyonge ambao hawakuwa wakinufaika ipasavyo na rasilimali za nchi. 

“Serikali yenu sikivu inatambua vikwazo vya aina hiyo na inatekeleza maelekezo ya Ilani ya CCM ya 2015/2020, ambayo inaielekeza Serikali ihakikishe watu wenye ulemavu wanapata elimu kwa kupata vifaa maalumu na kushiriki katika shughuli za kijamii.”

Hivyo, Waziri Mkuu amesema Serikali ya Awamu ya Tano itaendelea kuwekeza kwenye miundombinu na mazingira rafiki yatakayowawezesha watu wenye ulemavu kwenda wanapotaka, kutumia vyombo vya usafiri na kupata habari kama walivyo wengine. Amesema katika ofisi yake ataajiri mkalimani wa lugha za alama.

Amesema Serikali itaendelea kuboresha mahitaji maalumu ya watu wenye ulemavu kwa kuwawezesha kupata taarifa mbalimbali kwa urahisi kwa kutumia lugha ya alama, alama mguso, maandishi ya nukta nundu, maandishi yaliyokuzwa au njia nyingine zinazofaa.

Waziri Mkuu amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo imeanza kurasimisha Lugha ya Tanzania, kutayarisha vifaa vya kufundishia Lugha ya Alama ya Tanzania na kufundisha walimu katika shule za Msingi na Sekondari nchini. Mchakato huo utachukua takribani miaka miwili kukamilika.

“Serikali kwa kutambua umuhimu wa kuwa na shule maalumu ya Serikali ambayo inahudumia watoto wenye mahitaji maalumu imeanza ujenzi wa Shule Maalumu Patandi katika Mkoa wa Arusha. Shule hiyo inatarajiwa kuchukua wanafunzi 600 wa Msingi na Sekondari na itagharimu sh. bilioni 2.8.”

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema katika mapitio ya Kanuni za Maudhui ya Vyombo vya Habari, Kanuni za mwaka 2011, Serikali imeingiza kipengele kipya kinachovitaka vyombo vyote vya habari kuwa na wakalimani wa lugha ya alama kwa vipindi muhimu. Baadhi ya vyombo vya habari ikiwemo Shirika la Habari Tanzania (TBC) vimekuwa vikitekeleza agizo hilo. 

“Napenda kutumia maadhimisho haya kuagiza vyombo vyote vya habari kuhakikisha kwamba agizo hili linatekelezwa ipasavyo. Serikali kwa upande wake itaendelea kuhakikisha kuwa haki na mahitaji ya Watu wenye Ulemavu vinapatiwa ufumbuzi kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Watu wenye Ulemavu Na. 9 ya Mwaka 2010.”

Amesema anajua ajua changamoto wanazokumbana nazo viziwi wanapotaka kupata huduma mbali mbali katika vituo vya kutolea huduma za afya, mahakama, vituo vya polisi, nyumba za ibada na maeneo mengine muhimu kwa kuwa hayana wakalimani wa lugha ya alama.

Waziri Mkuu ametoa wito kwa taasisi zote za Serikali na binafsi zihakikishe zinakuwa na wakalimani wa lugha ya alama. “Pia naagiza kwamba mitaala ya vyuo vya Afya, Polisi, Mahakama na vinginevyo ihakikishe inazingatia kuongeza kozi ya Lugha ya Alama kama somo la lazima. Hii itasaidia kuzalisha watalaamu wa lugha ya alama ambao wataweza kuwahudumia wenzetu viziwi ipasavyo.”

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) Nidrosy Mlawa ameishukuru Serikali kwa kuwaamini watu wenye ulemavu na kuwateuwa kushika nafasi mbalimbali za uongozi, lakini waomba iongeze nafasi za ajira kwa watu wenye ulemavu ili nao waweze kujikwamua kiuchumi na kusaidia Taifa.

Pia, ameiomba Serikali iwe na wakalimani wa lugha za alama kwa ajili ya kuwawezesha watu wenye ulemavu waweze kupata taarifa zinazolewa na viongozi wao. Wameomba Serikali ikamilishe mchakato wa urasimishaji wa Lugha ya Alama ya Tanzania. WaziriMkuu amesemamaombi na mapendekezo yao ni ya msingi na muhimu kwa maisha ya Viziwi. Lengo la Serikali ni kuboresha huduma zetu kwa Viziwi hapa nchini. 

Maadhimisho hayo yamehudhuliwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- TAMISEMI Josephat Kandege, Naibu Waziri - Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na wenye UlemavuStela Ikupa, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Ave Maria Semakafu pamoja na viongozi wa CHAVITA.

CGP - PHAUSTINE KASIKE AONGOZA KIKAO KAZI CHA MAAFISA WAANDAMIZI WA JESHI LA MAGEREZA, LEO MKOANI MOROGORO

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Phaustine Kasike, akisalimiana na Naibu Kamishna wa Magereza, Afwilile Mwakijungu mara baada ya kuwasili kwenye Viwanja vya Nanenane, Mkoani Mororogoro tayari kwa Kikao Maalum cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo. Kikao hicho kimefanyika kwa siku moja leo 28 Septemba, 2019 Mkoani Morogoro.
Kamishna wa Huduma za Urekebishaji na Urekebu, Tusekile Mwaisabila akitoa utambulisho mfupi wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza kabla ya kumkaribisha Kamishna Jenerali wa Magereza kufungua rasmi kikao kazi hicho.
Wajumbe wa Kikao hicho ambao ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa makini maelekezo kutoka kwa Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike (hayupo pichani).
Mkuu wa Magereza Mkoani Lindi, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Josephine Mbogo(kushoto), Mkuu wa Magereza Mkoani Geita, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Edith Mbogo(katikati) na Mkuu wa Magereza Mkoani Pwani, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Rehema Ezekiel kwa pamoja wakiteta jambo mara baada ya ufunguzi wa Kikao kazi cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza ambacho kimefanyika kwa siku moja leo 28 Septemba, 2019 Mkoani Morogoro.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Phaustine Kasike akitoa hotuba ya ufunguzi wa Kikao Maalum cha Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza leo 28 Septemba, 2019 Mkoani Morogoro.
Meneja wa SACCOS ya Magereza(TPS SACCOS), Kamishna Msaidizi wa Magereza, Abdallah Missanga akitoa ufafanuzi wa huduma mbalimbali zinazotolewa na Chama hicho cha Ushirika cha Jeshi la Magereza mbele ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza.

FFU ALIYEUWA NYOKA KWENYE MKUTANO WA WAZIRI MKUU APONGEZWA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemzawadia  Askari Polisi PC Alphonce Daniel Mwambenga sh. 200,000 kutokana na ujasiri wake wa kumdhibiti kwa kumkanyaga nyoka mkubwa aliyekuwa akieleakea jukwaa kuu wakati Waziri Mkuu akihutubia katika Kilele cha Wiki  ya Viziwi Duniani kwenye Uwanja wa Kichangani, Kihesa mjini Iringa, Sepotemba 28, 2019.  Kitendo hicho kilifanyika kimyakimya hivyo hapakuwa na taharuki yoyote .  Pichani, Mheshimiwa  Majaliwa akimkabidhi Mwambenga fedha hizo. Wapili kulia ni Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa, kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Stella Ikupa na kulia  ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara y a Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Dkt.Avemaria Semakafu.  Wa tatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happy na wa nne kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Dkt. Abel  Nyamkahanga.  

 Askari Mwambenga  akiwa amemkanyaga nyoka huyo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



Nyoka  akiuawa na baada ya kuuawa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

RAIS MSTAAFU ALHAJ ALI HASSAN MWINYI ATEMBELEA TAMASHA LA UTALII VIWANJA VYA VERDE ZANZIBAR

$
0
0
Rais  Mstaaf wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi akitembelea mabanda ya maonesho ya Tamasha la Pili la Utalii Zanzibar, linalofanyika katika viwanja vya Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar, akimsikiliza mwakilishi wa Kampuni ya MCL
 RAIS Mstaaf wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Wafanyakazi wa Kampuni ya Ulinzi ya GS,wakati akitembelea mabanda ya maonesho ya Tamasha la Pili la Utalii Zanzibar katika viwanja vya Hoteli ya Verde Mtoni Jijini Zanzibar leo
 RAIS Mstaaf wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Vijana wa Kampuni ya Ulinzi ya Masai wakati alipotembelea maonesho ya Tamasha la Pili la Kimataifa la Utalii Zanzibar, lililofanyika katika viwanja vya Hoteli ya Verde Mtoni Jijini Zanzibar
RAIS Mstaaf wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi akimsikiliza Mkurugenzi wa Masoko wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Dkt. Miraji, akitowa maelezo ya sekta ya utalii wakati alipotembelea banda la maonesho la Kamisheni ya Utalii Zanzibar viwanja vya hoteli ya Verde Mtoni Jijini Zanzibar leo.28-9-2019.(Picha na Othman Maulid)

MKANDARASI WA BARABARA YA NYAKANAZI-KIBONDO MKOANI KIGONA KUKAMILISHA KAZI IFIKAPO JANUARI 2020

$
0
0
SERIKALI imemtaka mkandarasi Nyanza Road Works anayejenga barabara ya Nyakanazi-Kibondo ya km 50 mkoani Kigona, kukamilisha barabara hiyo ifikapo Januari mwakani.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), Mhe. Elius John Kwandikwa amesema hayo mara baada ya kukagua ujenzi wa barabara hiyo ambapo amesisitiza hakuna muda utakaoongezwa kwa mkandarasi huyo kwa sehemu hiyo ya barabara.
“Fedha unazodai tumekulipa hivyo hakikisha unatukabidhi barabara hii mapema januari 2020 kama mkataba unavyoonesha”, amesema Naibu Waziri Kwandikwa.
Aidha amewataka mameneja wa Wakala wa Barabara TANROADS wa mikoa ya Kagera na Kigoma kumpa ushirikiano wakutosha ili kukamilika kwa barabara hiyo kuwe sambamba na kukamilika kwa  daraja la Muyovosi ambalo ni sehemu ya ujenzi wa barabara kabla ya msimu wa mvua nyingi.
Barabara ya Nyakanazi-Kibondo Km 50, ni sehemu ya barabara kuu ya Kidahwe-Kasulu-Kibondo-Nyakanazi yenye urefu wa KM 296 ambayo ni barabara ya kimkakati na kiuchumi kwa mikoa ya Kigoma, Kagera, Geita na Shinyanga.
Naye Meneja wa TANROADS mkoa wa Kigoma Eng. Narcis Choma amemhakikishia Naibu Waziri Kwandikwa kuwa mkoa wake umejipanga kikamilifu kusimamia miradi yote ya barabara ili kuufungua kiuchumi kwa kuhuisha huduma za kilimo, uvuvi, utalii, biashara na uchukuzi. 
Naibu Waziri Kwandikwa yuko katika ziara ya siku tatu mkoani Kigoma katika kukagua na kutoa maelekezo kwenye miradi ya miundombinu mkoani humo.
 Kazi ya ukarabati mkubwa wa sehemu zilizoathirika zaidi katika barabara ya Lusahunga –Rusumo Km 95.4 ikiendelea mkoani Kagera.
 Muonekano wa sehemu ya barabara ya Nyakanazi-Ushirombo Km 110 ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami unaendelea.
 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), Mhe. Elius John Kwandikwa akiteta jambo na mkandarasi wa Nyanza Roads Works anayejenga kwa kiwango cha lami barabara ya Nyakanazi-Kibondo Km 50 ambayo ni sehemu ya barabara kuu ya Kidahwe-Kasulu-Kibondo-Nyakanazi yenye urefu wa KM 296.
 Muonekano wa nguzo za msingi wa daraja la Muyovosi linalounganisha mikoa ya Kagera na Kigoma kupitia wilaya za Biharamulo na Kakonko ambalo ujenzi wake unaendelea katika barabara ya Nyakanazi-Kibondo Km 50.

 Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Kigoma Eng. Narcis Choma (wapili kushoto) akisisitiza jambo kwa mkandarasi Nyanza Roads Works anayejenga daraja la Muyovosi katika barabara ya Nyakanazi-Kibondo Km 50 (wapili kulia), ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), Mhe. Elius John Kwandikwa akifuatilia.


Government hails profit making Arusha International Conference Centre (AICC) Posted: 28 Sep 2019 12:58 PM PDT

$
0
0

From Assah Mwambene, Arusha

The Arusha International Conference Centre (AICC) was yesterday credited as one of the government institutions that were being run on profit margins and contributing immensely to the economy of the country.

Speaking to the AICC staff and management here yesterday, Deputy Minister for Foreign Affairs and East Africa Cooperation, Dr. Damas Ndumbaro said the government, especially the Ministry of Foreign Affairs was proud to have such a profit-making institution.

“AICC is one of the leading institutions in the ministry of Foreign Affairs and the government is proud for operating on profit margins,” he said.

The Deputy Ministry who also toured various conference facilities including hospital and estates at Kaloleni and Kijenge, praised the institution for what he called a successful SADC summit last month.

He cited the successful hosting of the SADC summit has made the Tanzania proud, adding that everyone who attended the summit hailed the government.

The Deputy Minister also called on the AICC workers to sustain the pace and device more innovative ideas that would make AICC an economical formidable institution in the future.

“The future of AICC depends on the innovative idea yoFrom Assah Mwambene, Arusha

The Arusha International Conference Centre (AICC) was yesterday credited as one of the government institutions that were being run on profit margins and contributing immensely to the economy of the country.

Speaking to the AICC staff and management here yesterday, Deputy Minister for Foreign Affairs and East Africa Cooperation, Dr. Damas Ndumbaro said the government, especially the Ministry of Foreign Affairs was proud to have such a profit making institution.

“AICC is one of the leading institutions in the ministry of Foreign Affairs and the government that we are proud off for operating on profit margins” he said.

The Deputy Ministry who also toured various conference facilities including hospital and estates at Kaloleni and Kijenge, praised the institution for what he called a successful SADC summit last month.

He said successive hosting of the SADC summit has made the government proud, adding that everyone who attended the summit hailed the government.

The Deputy Minister also called on the AICC workers to sustain the pace and device more innovative ideas that would make AICC an economical formidable institution in the future.

“The future of AICC depends on the innovative idea your device today, please be first patriotic to your country and your line of duty. There is a big difference to be patriotic to your country and being patriotic to a person” he said.

In his response, the AICC Managing Director, Mr. Elishilia Kaaya thanked the Deputy Minister for the credit to AICC, saying however that the government especially the president Dr John Pombe Magufuli and the Ministry deserves to shoulder the praise since they worked round the clock to ensure that everything went well.

“Honestly speaking the government is the one that needs to be credited for the job well done in hosting the summit since you were in the driving seat. We were just supplementing government efforts.” Mr. Kaaya told the Deputy Minister.

On the Deputy Minister’s call to make more efforts in scouting for more International association meetings, especially by the Department of Conference and Marketing, the DG said AICC will work on the challenge and ensure that all the instruction given by the Deputy Minister are fulfilled. 

The Deputy Minister was on a two-day working tour of AICC and other Multilateral institutions, including UN Residual mechanism, African People’s and Human Rights Court, which were operating in Arusha.

u devise today, please be first patriotic to your country and your line of duty. There is a big difference to be patriotic to your country and being patriotic to a person” he said.

In his response, the AICC Managing Director, Mr. Elishilia Kaaya thanked the Deputy Minister for the credit to AICC, saying however that the government especially the president Dr. John Pombe Magufuli and the Ministry deserves to shoulder the praise since they worked round the clock to ensure that everything went well.

“Honestly speaking the government is the one that needs to be credited for the job well done in hosting the summit since you were in the driving seat. We were just supplementing government efforts.” Mr. Kaaya told the Deputy Minister.

On the Deputy Minister’s call to make more efforts in scouting for more International association meetings, especially by the Department of Conference and Marketing, the DG said AICC will work on the challenge and ensure that all the instruction given by the Deputy Minister are fulfilled. 

The Deputy Minister was on a two-day working tour of AICC and other Multilateral institutions, including UN Residual mechanism, African People’s and Human Rights Court, which were operating in Arusha.

UJENZI WA STESHENI MPYA YA SGR DAR WAFIKIA HATUA HII,MUONEKANO WA DARAJA WAZIDI KUBADILIKA

Viewing all 110175 articles
Browse latest View live




Latest Images