Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110151 articles
Browse latest View live

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA MHANDISI MANYANYA AFURAHISHWA TAMASHA LA JAMAFEST KUKUZA MILA NA DESTURI

$
0
0
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya akicheza ngoma katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu. Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara amefurahishwa jinsi Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam lilivyoweza kukuza mila na desturi za Mwafrika. Akizungumza mara baada ya kutembelea katika uwanja wa Taifa leo Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya amesema kuwa amefurahishwa jinsi walivyoweza kusogeza ajenda ya Biashara nchini. "Nafurahi kwamba maonesho haya yameshirikisha watu wote, nimefurahi kuone watu wenye ulemavu wanatengeneza bidhaa nzuri ambazo zinawapatia kipato," amesema. Amesema kuwa amefurahiswa kuona Mila na desturi zinafanana, ukiachana masuala madogomadogo tunaweza kushirikiana kwa karibu ili kujenga uchumi mkubwa kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. "Nimetembelea banda la Jumuiya ya Afrika Mashariki na nimeangalia takwimu za nyuma kidogo za biashara za nchi wanachama zinaonesha biashara inaongezeka, kwa kiasi kikubwa Sana, kwa hiyo jukumu kubwa ni kujenga amani ili kujenga uchumi wa nchi zetu," amesema. Ameongeza kuwa Tamasha la JAMAFEST ni fursa kubwa kwa wa EAC, kwa hiyo tunaweza kuangalia utaratibu wa kupunguza muda wa miaka miwili ili kuwawezesha watu wetu kufanya biashara na kupanua soko baina ya nchi Wanachama wa EAC. Mhandisi Stella Manyanya bidhaa zinazopatikana hapa JAMAFEST zinatufundisha kuwa Nchi za Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla tuna vipaji vikubwa sana kutoka kwenye Sanaa na Utamaduni wetu.
Ngoma kutoka nchini Tanzania ikiburudisha katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya akingalia burudani ya ngoma katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam.
Watoto wa kitanzania akionyesha umahili wa kupiga ngoma katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam.
Burudani ikiendelea katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya (kulia) akingalia bidhaa wa wajasiliamali wa jumuiya ya Afrika Mashariki katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya (katika) akingalia burudani ya mchezo wa bao katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam.
Burudani ya sarakasi ikipamba.
Mchezo wa manyoka nyoka ukiendelea.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa pili toka kulia) akifuatilia burudani ya ngoma katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam.

Kampuni binafsi ya ulinzi SGA yatoa mafunzo ya usalama bure

$
0
0





Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya SGA Security, Eric Sambu (kushoto) akizungumza jijini Dar Es Salaam leo wakati wa kuadhimisha miaka 35 ya kutoa huduma za ulinzi nchini. Kulia ni Meneja wa Wateja na Mawasiliano wa kampuni hiyo, Aikande Makere.



Kampuni ya ulinzi, SGA Security, imetoa mafunzo ya bure ya usalama kama sehemu ya utoaji wa huduma kwa jamii na kuwazawadia watumishi wake wa muda mrefu ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 35 ya kuwepo nchini Tanzania.

Wiki iliyopita kampuni hiyo ilitoa mafunzo kwa wateja wake wakubwa juu ya mbinu mbalimbali za kisasa za kupambana na changamoto za kiusalama.

Semina hiyo kwa wateja wake ilifanyika Ijumaa Septemba 27 jijini Dar es Salaam na mafunzo yaliongozwa na wataalam waliobobea kwenye masuala ya usalama ambapo zaidi ya mameneja 80 wa usalama wa makampuni makubwa na mabenki nchini walihudhuria.

Akizungumza wakati wa tukio hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa SGA, Eric Sambu, alisema kwamba kampuni hiyo ya ulinzi imeamua kutoa huduma kwa jamii kama sehemu ya kusheherekea mafanikio yake nchini.

SGA pia imetoa mafunzo ya usalama kwenye shule 12 za msingi mkoani Dar es Salaam ambapo wanafunzi zaidi ya 2,000 walinufaika. Mafunzo hayo yalikua juu ya majanga ya moto, huduma ya kwanza, mazingira, afya na usalama kwa ujumla.


Ikiwa ina watamushi zaidi ya 5,800, nchini Tanzania, SGA kwa sasa ndio kampuni kubwa ya ulinzi nchini.Katika shughuli za kuadhimisha miaka 35 nchini, kampuni pia imeanzisha ‘Club 20’ ambao wanachama wake ni watumishi walioitumikia kampuni kwa zaidi ya miaka 20.

SGA aliwatuza watumishi 16 waliotumikia kampuni kwa muda mrefu ambao pia wamefikia muda wa kustaafu.Wakati huo huo, mwakilishi kutoka jeshi la polisi nchini ameipongeza SGA kwa kujali maslahi ya watumishi wake na kuongoza kwa mfano, akisema kwamba kampuni nyingi binafsi za ulinzi hazifuati miongozo iliyotolewa kuhusiana na mafunzo, usimamizi, ukaguzi na mishahara.


Amezitaka kampuni nyingine za ulinzi kuiga mfoano wa SGA.

Ikiwa ina waajiriwa zaidi ya 80 waliotumikia kampuni kwa zaidi ya miaka 20 kwenya biashara ya faida kubwa, SGA ina kila sababu ya kusherehekea, amesema Sambu. SGA pia ina watumishi takribani 2,200 walioajiriwa kwa zaidi ya miaka 10.

“SGA ni kampuni ya kwanza binafsi ya ulinzi kuingia Tanzania na imedhihirisha kwamba kuwajali watumishi wake ni muhimu kwa mafanikio ya kampuni,” Sambu amesema.
Watumishi wa SGA wakishiriki kwenye Siku ya Usafi Duniani kama sehemu ya kuadhimisha miaka 35 ya kuwepo nchini Tanzania



“Kampuni mama ina watumishi za ya 18,000 na suala la muhimu kwetu ni watu. Tumewekeza sana katika utoaji wa mafunzo na tunahakikisha kwamba mishahara yetu inaongoza kwenye soko kama sehemu ya kuwapa motisha watumishi wetu,” aliongeza.

Amesema kwamba kampuni anaadhimisha miaka 35 ya utoaji huduma nchini Tanzania huku ikiwa inakua siku hadi siku, hususan katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Ameeleza zaidi kwamba mafanikio ya kampuni yameletwa na watumishi wake ambapo amesema ni waaminifu, waadilifuna wachapa kazi kwa bidii.Matukio ya hivi karibuni kwenye mazingira ya kibiashara nchini yamekuwa kama fursa ya kujifunza na kuwawezesha wafanyakazi wetu kwenda sambamba na matakwa ya wateja,” ameongeza.

“Kila mara tunajipanga upya katika utendaji wetu, huku tukiwekeza kwenye teknolojia na watumishi wetu kuhakikisha kwamba hakuna jambo linaloharibika,” amesema Sambu.SGA ni kampuni kongwe binafsi ya ulinzi Tanzania, ikiwa imeanza kazi mwaka 1984 kama Group Four Security. Inatoa huduma mbalimbali zikiwemo za walinzi, usalama wa kielektroniki, huduma za dharura na usafirishaji wa fedha.

“Tuna magari 224 na vituo 12 mikoani na watumishi wanaojituma, tuna miundombinu ya kutosha kuwahudumia wateja popote pale nchini,” Sambu amesema.enaja Rasilimali Watu wa SGA, Ebenezer Kaale, alisema kwenye tukio hilo kwamba watumishi wengi walioajiriwa kwa miaka mingi wanafanyakazi kwenye idara ya kusafirisha fedha, idara nyeti inayohitaji uadilifu na nidhamu ya hali ya juu.

Ikiwa ina mafanikio makubwa kwenye huduma za fedha, ambapo kampuni imehodhi asilimia 90 ya soko, watumishi kwenye idara wanastahili pongezi kwa mafanikio hayo.

Meneja wa Mahusiano ya Wateja, Aikande Makere, amesema kwamba kazi za SGA zitarahisishwa ikiwa wateja wanaenda na wakati kwa kufahamu mbinu za kisasa za kupambana na changamoto za kiusalama.

TAEC YATOA MAFUNZO YA UCHUNGUZI WA MIONZI KWA WAFANYAKAZI WA TPA

$
0
0
Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) imetoa mafunzo ya ukaguzi wa mizigo kwa kutumia teknolojia ya Nyuklia kwa wafanyakazi 22 wa Kitengo cha Midaki (scanner) katika Bandari ya Dar es Salaam. 

Mafunzo hayo ya wiki mbili yamelenga kuwapa uwezo wafanyakazi wanaoshugulikia ukaguzi wa mizigo katika midaki (Scanner) katika eneo la Bandari kwa lengo kuongeza kasi na weledi katika ufanyaji kazi kwa lengo la kuharakisha ukaguzi wa mizigo Bandarini. 

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania, Prof Lazaro Busagala amewataka wafanyakazi hao kuhakikisha kuwa wanafanyia kazi mafunzo waliyoyapata kwa lengo la kuongeza ufanisi wa ukaguzi wa mizigo kwa njia ya teknolojia ya Nyuklia. 

“Hakikisheni mnatumia mafunzo haya katika kufanya kazi kwa weledi na kuongeza tija ili kusiwe na ucheleweshwaji wa mizigo hapa bandarini” alisema Prof Busagala. 

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Midaki (Sscanner) Bandarini, Bw. Mtani Rugina amesema kuwa wataendelea kuhakikisha wafanyakazi wote waliopo kwenye maeneo ya ukaguzi wa mizigo bandarini hapo wanapata mafunzo ili kuboresha ufanisi katika ufanyaji kazi wao. 

TAEC itaendelea na jukumu lake la kutoa mafunzo ili kuhakikisha usalama katika maeneo yote yenye vyanzo vya mionzi unakuwa wa kiwango cha juu.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), Prof. Lazaro Busagala (wa pili kushoto), akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya uchunguzi wa mionzi, Frank Mwamakula, ambaye ni mmoja wa wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA). Mafunzo hayo yametolewa leo na Tume hiyo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), Prof. Lazaro Busagala, akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya uchunguzi wa mionzi kwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari Tanza(Na Mpiga Picha Wetu).

Washiriki wa mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo.



Kwanza TV Yafungiwa , Ayo TV na Watetezi wapigwa faini

$
0
0


Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeifungia Kwanza TV kwa kipindi cha miezi sita ili waweze kujirekebisha katika uendeshaji luninga katika mitandao.

Kwanza TV walikutwa na kosa la kuchapisha habari iliyokuwa inamuhusu Dkt.Gwajima kupata ajali ya gari ambapo katika utetezi wao walidai kuwa taratibu za kihabari zilifuatwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui Joseph Mapunda amesema kuwa Kwanza Tv walikutwa na makosa ya habari ya ajali ya Dkt.Gwajima ambayo haikufafanunua ni Gwajima yupi ambapo ni kosa katika uandishi.

Amesema Kamati hiyo ilisema kuwa ajali hiyo ilikuwa inamhusu Katibu Mkuu wa Tamisemi Afya Dkt.Doroth Gwajima hivyo kulifanya watu wengine kushindwa kujua ni Dkt.Gwajima gani kutokana na kutokwepo kwa majina yote.

Aidha Kamati hiyo imetoa faini ya sh.milioni tano kwa Ayo na Watetezi TV kwa kila mmoja kulipa fedha hiyo kwenye mamlaka hiyo kutokana na kushindwa kuchapicha Sera ya maudhui na miongozo katika luninga zao na kuweza kuona watazamaji. Mapunda amesema vyombo vya habari vifuate taratibu , kanuni na sheria katika kutangaza au kuhabarisha umma kwa kuzingatia misingi ya uandishi.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA Joseph Mapunda akitoa hukumu kwa vyombo vya habari viliyokiuka maudhui ya utangazaji leo jijini Dar es Salaam.



DAWASA YAENDELEA KUWANASA WANAOHUJUMU MIUNDO MBINU YA MAJI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii


MAMLAKA ya Majisafi na Majitaka Dar es salaam imewataka wananchu kujisalimisha kwenye ofisi za mamlaka hiyo ili waweze kuunganishiwa maji kiuhalali na kuacha kuchepusha maji kwani ni kosa kisheria.

DAWASA wameendelea na ukaguzi wa miundo mbinu ya maji inayohujumiwa na wananchi wasio waaminifu na kusababisha mamlaka kupata hasara.

Zoezi hilo limekuwa endelevu kwa Mkoa wa kihuduma DAWASA Kawe na kufanikiwa kugundua maeneo ya watu mbalimbali wakiwa wanaunganisha maji kwa njia wa wizi.

Matukio ya wizi wa maji yameendelea kuvumbuliwa kwa kasi kubwa ambapo jitihada za Mamlaka zimefanikiwa kuwakata watu mbalimbali wanaohujumu miundo mbinu na kulipa hasara Mamlaka.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufanikiwa kugundua wizi wa maji katika eneo la Maringo Kawe, Fundi Mita Idara ya Biashara DAWASA Martin Kilembe amesema wameweza kupata taarifa ya wizi wa maji katika maeneo haya na wamechunguza na kugundua wizi mkubwa unaofanywa kwa kujiunganishia maji nyuma ya mita ya maji.

“kujiunganishia maji nyuma ya mikta ni kosa kisheria unakuwa unahujumu shirika na utakapobainika sheria itachukua mkondo wake, eneo hili lote lilikuwa ni la mtu mmoja na lina mita nne za maji ambapo mita mbili tulishawakatia maji na mita mbili zingine zinaendelea kufanya kazi,”amesema Kilembe.

“Katika mita zilizobaki kuna moja inahudumia sehemu ya kuoshea magari (Car wash), nyingine inahudumia nyumba hii na zingine zilishakatiwa maji ila tumeona wanaendelea kupata maji”

Kilembe amesema, wamegundua sehemu walikofanya maunganisho ya maji na wamekuwa wanafanyia ujenzi wa ukumbi wa starehe lakini mita yao ikiwa imekatwa na inaonesha maunganisho ya maji wanayotumia kutoka katika bomba kuu lililopo nyuma ya jengo hilo.

"Ni kosa kisheria, na mteja anaunganisha maji nyuma ya mita anakuwa amefanya hujuma na hasara kwa serikali na makosa haya yanapelekea kulipa faini au kufunguliwa kesi na kupelekwa mahakamani na atalipa gharama zote za uharibifu uliofanywa," 

Kilembe amesema, miundo mbinu hii ni ya muda mrefu na kipindi cha nyuma mita za maji zilikuwa zinafungwa kwa ndani, sasa kuna haja ya kuanza kupitia maeneo yote na mita hizo zitolewe nje.

DAWASA imeendelea kuwataka wananchi kuacha kuhujumu miundo mbinu ya maji kwani utakapokamatwa sheria itachukua mkondo wake na hakutakuwa na huruma kwa mtu yoyote na faini ni kuanzia miaka 5,000,000 hadi milioni 50 au kifungo kisichopungua miaka saba au vyote viwili.

Wateja wa DAWASA wameombwa kuacha kuchepusha maji na zaidi wajisalimishe kwenye mamlaka ili kuweza kupata huduma ya maji kwa uhalali na kuacha kuhujumu miundi mbinu ya Mamlaka.
Mita ya maji jnayohudumie eneo la Car Wash ikiwa ndani ya uzio wa nyumba iliyokutwa imechepusha maji.
Fundi Mita Idara ya Biashara ya Mamlaka ya majisafi na majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Martin Kilembe akisoma mita ya maji iloyopo ndani ya uzio mmoja ambapo kwa mujibu wa wasoma mita haina tatizo lolote na imekuwa inalioiwa kila mwezi, zoezi hilo limefanyika Mkoa wa Kihuduma DAWASA Kawe.
Fundi Mita kutoka Idara ya Biashara ya Mamlaka ya majisafi na majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Martin Kilembe akionesha mita ya maji iliyokatwa ila ujenzi wa maji ukiwa unaendelea kwa kutumia maji ya DAWASA.
Jengo linalojengwa kwa kutumia maji ya wizi kitoka DAWASA.
Fundi Mita kutoka Idara ya kutoka Idara ya Biashara ya Mamlaka ya majisafi na majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Martin Kilembe akitoa maelekezo kwa mafundj wa DAWASA wakati wa zoezi la kutafuta maunganisho ya maji yanayopeleka maji kwa mmiliki wa jengo la burudani anayotumia kwa ajili ya ujenzi, zoezi hilo limefanyika Mkoa wa Kihuduma DAWASA Kawe.
Fundi wa DAWASA akionesha maunganisho ya maji nyuma ya mita yanayopeleka maji kwenye jengo linalojengwa la ukumbi wa burudani wakitumia kwa ujenzi.
Fundi Mita kutoka Idara ya Biashara ya Mamlaka ya majisafi na majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Martin Kilembe akizungumza na waandishi wa habari wakati wa zoezi la kuendelea kuwatafuta wanaohujumu miundo mbinu ya maji kwa kuchepusha maji na kulipa hasara mamlaka na serikali kwa ujumla zoezi hilo limefanyika Mkoa wa Kihuduma DAWASA Kawe.
Picha Zote na Zainab Nyamka


NMB yaahidi makubwa Kikao Kazi cha Maofisa wa Polisi

$
0
0

BENKI ya NMB, imewahakikishia askari wa Jeshi la Polisi na wafanyakazi wa Serikali nchini, huduma bora, rafiki na sahihi za kibenki, zitakazokuza pato la mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla, ili kuendana na kasi ya maendeleo kuelekea Uchumi wa Kati.

Ahadi hiyo imetolewa na Meneja Mwandamizi wa Wateja Binafsi na Kati wa NMB, Ally Ngingite, katika siku ya pili ya Kikao Kazi cha Maofisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Makao Makuu, Makamanda wa Mikoa na Vikosi, kinachofanyika katika Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam.

Kikao Kazi hicho kiliozinduliwa Septemba 24 na Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro, kimefika ukomo jana Ijumaa Septemba 27, 2019 ambapo kwa siku nne maofisa hao wamejadili juu ya mafanikio, changamoto na
mikakati ya Kamisheni katika Kuzuia, Kupambana na Kutanzua Uhalifu.

Kupitia Kikao Kazi hicho kinachofanyika chini ya Kaulimbiu: Umoja Wetu Ndiyo Nguvu Yetu, Tudumishe Usalama Katika Uchumi wa Viwanda, wadau wa Jeshi la Polisi wamealikwa kushiriki, ikiwemo NMB iliyotoa ahadi ya
ushirikiano wa kudumu, sambamba na huduma bora kwa askari polisi nchini.

Ngingite aliwataka maofisa na makamanda hao kuwa mabalozi wema wa benki hiyo kwa askari walio chini yao kote nchini na kwamba wanapaswa kuifanya NMB kama mshirika wa kweli katika kujikweza kiuchumi kupitia mikopo na aina nyingine za uwezeshaji kutoka katika benki hiyo.

“Makamanda na maofisa wote mlioshiriki Kikao Kazi hiki, mkitoka hapa huku mnafikiria namna sahihi ya kuboresha maisha yenu ya sasa na baadaye, kukuza pato lenu kuelekea Uchumi wa Kati, maana yake ni kuwa askari wote nchini walioko chini yenu watafikia kufanya hivyo pia.

“Unafuu wa huduma zetu kwa Askari wa Jeshi la Polisi, majeshi mengine na Wafanyakazi wa Serikali, unatokana na ukweli kwamba tunatambua, kuthamini na kujali mchango wenu kwetu kama taasisi ya kifedha,” alisema Ngingite,
ambaye alipokea maoni mbalimbali kutoka kwa makamanda hao.

Aliwaomba askari hao wanapoamua kukopa, kuhakikisha wanaitumia mikopo hiyo kwa usahihi, na kwamba siri ya mafanikio iko katika kufikiria kabla ya kukopa, kufanya uwekezaji mdogo baada ya kukopa ili kutanua pato lao na hatimaye kupunguza makali ya marejesho.

Akizindua Kikao Kazi hicho juzi, IGP Sirro aliwataka askari hao kuhakikisha wanajitoa kadri wawezavyo katika kulitumikia taifa na kwamba yeye anatamani kumaliza nafasi yake Jeshi likiwa na heshima, ambayo itapatikana kwa kila mmoja kuacha unafiki, kwani likichafuka, watachafuka wote.

DKT.MASSANGWA AONGOZA IBADA YA MAZISHI YA NELSONI ALIYEFARIKI KWA AJALI YA NDEGE

$
0
0





Jeneza lililobeba Mwili wa Marehemu Nelson Olotu likiwa kanisani tayari kwa Ibada ya Maziko.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika ibada ya mazishi katika kanisa la KKKT Usharika wa Sasi mtaa wa Ilmeshorori,Dayosisi ya Kaskazini Kati

Umati wawatu waliojitokeza wakiwa nje ya kanisa baada kumalizika kwa Ibada
Gari lioilobeba mwili wa Nelson likiondoka eneo la kanisa kuelekea makaburini kwaajili ya maziko.


Na.Vero Ignatus,Arusha

ASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati Dk.Solomon Masangwa jana ameongoza ibada ya mazishi ya aliyekuwa mwanafunzi wa Urubani Nelson Olotu (25) aliyefariki kwa ajali ya ndege Septemba 23 mwaka huu, huko Seronera Serengeti Mkoani Mara.

Aidha katika ajali hiyo pia mtoto wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF) Jenerali Venance Mabeyo, Nelson Mabeyo ambaye alikuwa rubani wa ndege namba 5H-AAM ya kampuni ya Auric air alipoteza maisha.

Akizungumza katika ibada hiyo jana iliyofanyika katika Usharika wa Sasi mtaa wa Ilmeshorori, Dayosisi ya Kaskazini Kati,Dk.Masangwa aliwapa pole wazazi na ndugu wote walioguswa na msiba huo na kuwataka kuwa na utulivu katika kipindi hicho cha majonzi.

"Binadamu siku zetu za kuishi hapa duniani fupi na zimejaa dhiki,hivyo hakuna ambaye ajuaye siku wala saa ya kifo kitakapompata, kutokana na fumbo hili inatupasa kila mmoja kukesha tukiomba,"alisema

Alisema ajali za ndege zinasababishwa na mambo mbalimbali kuanzia inaporuka,ikiwa angani na inapotua hivyo ni suala la kumwachia mungu.

"Baadhi ya sababu hizo ni makosa ya rubani,matatizo ya kiufundi,hali ya hewa,vyuma,wakati wa ndege kupaa na wakati wa kutua,huweza kusababisha ajali katika hili hakuna wa kulaumiwa,"alisema

Aidha alisema katika mazingira hayo huwezi kumlaumu mtu yoyote sababu hata rubani akijitahidi kukwepa ajali lakini bado mazingira ya ajali yanaweza kuwepo.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro alitoa salamu za pole kwa niaba ya serikali na kusema kazi ya mungu haina makosa.

"Huyu Nelson angemaliza safari ya masomo yake angetusaidia sana Serikali na taifa,lakini makusudi ya mungu lazima yatumike na tumwachie yeye,"alisema

Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya,ametoa pole na kusema hakuna mwenye jibu kwanini mtu mwenye umri mdogo kama walivyo vijana hao waliofariki katika ajali hiyo na katika kipindi hiki ambacho wazazi wao walikuwa wakiwahitaji kuliko kipindi chochote.

"Mahali salama na pekee ni kujikabidhi mikononi mwa mungu,"alisemaKatibu wa Chama cha Marubani nchini,Khalid Lqbal amesema marehemu alikuwa mpole,mnyenyekevu, msikivu ba mwenye kupanga kujifunza zaidi.

"Hivyo tumepoteza kijana mdogo ambaye angekuja kuwa msaada hapo baadaye,"alisemaPia amesema vifo vya vijana hao Nelson Olotu na Nelson Mabeyo ni pigo kubwa kwa taifa na sekta ya masuala ya anga.


Kwa upande wa kaka wa marehemu aliyesoma histori fupi ya marehemu,Calvin Olotu alisema marehemu alisoma shule ya Msingi Trust St.Patrick mwaka 1998 na kumaliza 2009 na Sekondari ya Duluti ambayo alimaliza mwaka 2013.

Baada ya hapo alijiunga shule ya Urubani mwaka 2014 katika Chuo cha Aviation College Dar esalaam na kuhitimu mwaka 2015 kisha alikwenda kujiunga na Chuo cha urubani Nairobi nchini Kenya cha PRO-ACTIVE AVIATION COLLEGE na kuendelea na ground School na Flight mpaka mwaka 2019.

Calvin alisema marehemu alikuwa mtoto wa tatu katika familiya ya mzee Wilberd Phillemon Olotu na mauti yalipomkuta akiwa safarini katika Hifadhi ya Serengeti na amezikwa nyumbani kwa wazazi wake Kambi ya Chupa Wilaya ya Arusha.

BASATA:MSANII ASIPOJISAJILI SHERIA ITACHUKUA MKONDO WAKE

$
0
0
Florah Mgonja Mratibu wa kazi za sanaa Kanda ya Kaskazini ,akiwa katika ofisi za Utamaduni Jijini Arusha

Na.Vero Ignatus,Arusha.


Baraza la sanaa nchini lipo mkoani Arusha kwaajili ya kuratibu shughuli zote za sanaa ,kwa maana ya usajili na uratibu wa wadau kwa ujumla wakiwemo wamiliki wa kumbi,bendi ,studio ,washehereshaji,DJ,waandaaji wa matamasha pamoja na matukio mbalimbali ya sanaa kanda ya kaskazini.



Florah Mgonja ni Mratibu wa kazi za sanaa Kanda ya Kaskazini amesema   baraza hilo limeanzishwa kwa mujibu wa sheria no 23 ya mwaka 1984 ,na kanuni zake za mwezi February 2018, zinawatambua wasanii pamoja na kazi zao ,pia zinamtambua Afisa utamaduni kanuni ya mwaka 2018 kipengele cha 22,kinamtanbua Afisa huyo kuanzia ngazi ya wilaya hadi Taifa.



Amewataka wasanii kwenda kujisajili ili waweze kuhudumiwa sambamba na kauli mbiu ya Basata inavyosema kuwa sanaa ni kazi na  kama zilivyo kazi nyingine hivyo ni vyema wakajisajili ili watambulike .



Mgonja amesema wasanii wengi wamekuwa wakilalamika kuwa wanasajiliwa na hawaoni faida,watambue kuwa faida zipo nyingi kwani Basata lipo dawati ambalo msanii hupewa fursa mbalimbali, na kazi zao namna zinaweza kulindwa kisheria.



“Vipo vinandaumiza vingi ambavyo vinachukua kazi nyingi za wasanii,kama umesajiliwa serikali ipo kwaajili ya kuangalia haki ya msingi ya msanii na tunaishughulikia kwa namna gani ili msanii aweze kusonga mbele”alisema Flora.



Mratibu huyo wa kazi za sanaa kanda ya kaskazini, amesema kuwa kwa sasa wapo wanatoa elimu kwa wasanii na vikundi mbalimbali,ila wakati unakuja kwa wasanii ambao hawatajisajili sheria itachukua mkondo wake .



Aidha amesema Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania linatarajia  kupitisha Sheria amabayo itawabana wasanii ili kuwasaidia kiuchumi badala ile ya Mwanzo ya mwaka 1984 sheria No 23 kuwa na mapungufu.



Florah Mgonja ni Mratibu wa kazi za sanaa Kanda ya Kaskazini ,akisisitiza jambo kwa waandishi wanhabari (hawapo pichani)katika ofisi Utamaduni Jijini Arusha.
Aidha amesema kulikuwa na malalamiko juu ya COSOTA,BODI YA FILAMU,BASATA kutokana na utendaji kazi wake kwani msanii alikuwa kote anatozwa kwa sasa serikali imaangalia namna gani hizi Taasisi tatu zinakuwa mamlaka ya usimamizi wa kazi za sanaa ambapo michakato tayari imeshaanza na inaratibiwa na TCRA.



Amesema kwa wale wote a,mbao wanafanya kazi bila kusajiliwa sheria itafuata mkondo wake kwasababu kwa sasa Basata ipo katika kuelimisha ,itafika mahali tukishaeka mambo sawa ikiwemo sheria na hizi mamlaka kuwa pamoja ,tutahakikisha kuwa kila anayejihusisha na shughuli za sanaa anasajiliwa.



Amesema zipo faida nyingi za msanii kujisajili ikiwemo sheria,kazi zao kutunzwa kupata fursa mbalimbali huku akiwataka wale ambao wameshajisajili kuhuhisha vibali vyao ,kwa msanii binafsi ni shilingi 45,000 kwa vikundi 85,000 ikiwa imejumlishiwa na fomu.



Amebainisha kuwa kwa sasa msanii hawezi kwenda nje ya kwa kupitia viwanja vya ndege  nchi kama hajasajiliwa Basata,hivyo umuhimu wa kujisajili ni mkubwa, kwani hata msanii akipata shida akiwa nje ya nchi ni rahisi kusaidika kama amesajiliwa.



Amesema Basata ipo kwaajili ya kushughulikia usajili kwa wasanii sambamba na ushauri wa namna ambavyo wanavyoweza kuendesha shughuli zao za sanaa kwani fursa zipo nyingi sana.



Aidha Basata ilianza usajili kwa mwaka wa fedha 2018-2019 na usajili ulikuwa mzuri na wasanii waliitikia kwa wingi,hivyo kwa mwaka huu wengi wanahuisha vibalivyao kwa wale waliokwisha sajiliwa tayari ambapo wamekuwa mabalozi kwa wengine .



Ameeleza kuwa kwasasa Basata imewarahisishia kazi wasanii,badala ya kwenda Jijini Dar es salaam imewafuata hadi mkoa husika kwaajili ya kuwafanyia kushughulikia usajili wao .



Hata hivyo ameeleza kuwa msanii anapojisajili 25% ya makusanyo katika usajili huu unarudi halmashauri kama sehemu ya uendelezaji wa shughuli za sanaa. 

RC BYAKANWA AZITAKA TAASISI ZA KIBENKI KUWAFIKIAWAKULIMA - MTWARA

$
0
0
Katika kuelekea Msimu wa Ununuzi wa Zao la Korosho 2019/2020 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa amezitaka taasisi za kibenki kuhakikisha zinawafiki na kuwafungulia akaunti wakulima wa zao la korosho kutokana na kuondokana na utaratibu wa kuwalipa wakulima mkononi.

Byakanwa ameyasema hayo mara baada ya kufungua Tawi la benki ya TPB lililopo Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara ambalo limeweza kutoa mikopo zaidi ya shilingi Bilion Nne mpaka sasa na kuwafikia wakulima wa korosho zaidi ya 2500 kwa mwaka huu pekee

Akiongea mbele ya wateja pamoja na wananchii waliohudhulia hafla hiyo Byakanwa ametumia nafasi hiyo kuzitaka taasisi za kibenki zilizopo katika mkoa wa Mtwara kuhakikisha zinawafikia wakulima wa korosho hasa  katika maeneo ya vijijini.

 “Ninazitaka benki zote kuhakikisha zinawafikia wakulima wote wa korosho kwa sababu hatutakuwa na utamaduni wa kumlipa mkulima mkononi lakini pia tumeondokana na utaratibu wa mkulima mmoja kupokea malipo ya wakulima zaidi ya watano wale ambao hawajafungua akaunti kwa hiyo niiombe TPB kuiona hiyo kama fursa”amesema Byakanwa

Aidha Byakanwa ameongeza kuwa anafarijika kuona huduma nzuri za benki hiyo kutokana na kutopata malalamiko yoyote kutoka kwa  wakulima hasa wa zao la Korosho.

“Ninafarijika na ubora mnazozitoa huduma mnazozitoa kwa wakulima wetu kwa mwaka wa pili huu sijapata malalamiko yoyote ya mkulima yoyote kuhusina na benki ya TPB sio masasi sio Mtwara”

Sabasaba Moshingi ni Mtendaji Mkuu wa benki hiyo anasema kuwa TPB tayari imeongeza idadi ya matawi hapa Nchini kutoka 32 na kufikisha 77 ambayo yameweza kuongeza idadai ajira pamoja na kutoa huduma za kifedha kwa Jamii husika.

“Benki imeendelea kutoa gawiwo kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo na mwaka huu kutokana na faida ya mwaka jana tumeweza kutoa gawiwo la shilingi Bilioni moja na million mia mbili kwa wanahisa wake ambao mwanahisa mkubwa ni serikali lakini tumeweza kuongeza idadi ya matawi na hili la masaSI ni miongoni ya matawi mapya ambayo tunafungua”Amesema Moshingi.

5733.Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa akifungua Tawi jipya la benki ya TPB lililopo wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara ambalo tayari limeweza kuwafiki wakulima wa zao la korosho zaidi ya 2500,kusoto kwake ni mtendaji mkuu wa benki hiyo Sabasaba Moshingi.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa akikata utepe kuashiria ufunguzi wa tawi la Benki ya TPB Wilaya ya Masasi Mkoa wa Mtwara ambalo Tayari limetoa mikopo ya zaidi ya shilingi billion Nne kwa wakulima wa zao la Korosho Wilayani hapo.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa akiongozana na Mtendaji mkuu wa benki ya TPB Sabasaba Moshingi mara baada ya kutembelea na kukagua huduma mbalimbali zinazopatikana katika  tawi jipya la benki hiyo iliyopo Wilaya ya Masasi,Mtwara.
Kikundi cha Ngoma Mchema Group kutoka wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara kikitumbuiza ngoma za kitamaduni za kabila la Wamakua katika uzinduzi wa Tawi la Benki ya TPB Masasi Mkoani Mtwara.
Mkuu wa Mkoa wa mtwara Gelasius Byakanwa akiwa katika Picha ya Pamoja na Wafanyakazi wa benki ya TPB mara baada ya kufanya ufunguzi wa tawi la benki hilo wilya ya Masasi Mkoani Mtwara.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa akiwa amebeba mtoto wa mmoja wa wananchi walioshiriki katika uzinduzi wa tawi la Benki ya TPB lililopo Masasi Mkoa wa Mtwara,kushoto ni Mtendaji Mkuu wa TPB Sabasaba Moshingi.
Saidi Mbito kulia akiwa na Sulpis Likanda wakiwa na zawadi ya Ngao waliopewa na Benki ya TPB kama moja ya shukurani kwa kufanya kazi muda mrefu na benki hiyo.

MKURUGENZI APEWA SAA NNE KUSITISHA MKATABA WA UJENZI

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Iringa Mjini na Iringa Vijijini pamoja na vionzi wa Vyama vya siasa na Viongozi wa Dini kwenye ukumbi wa Kichangani mjini Iringa, Septemba 28, 2019.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happy na kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Abel Nyamahnga.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Iringa Mini na Iringa Vijijini pamoja na vionzi wa Vyama vya siasa na Viongozi wa Dini wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Kichangani mjini Iringa, Septemba 28, 2019. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happy na kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Abel Nyamahnga.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa muda wa saa nne kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Himid Njovu awe ameandika barua ya kusitisha ujenzi wa ukumbi wa mikutano na sherehe katika eneo la shule ya msingi Gangilonga.

Amesema maeneo yote ya taasisi za elimu nchini hayaruhusiwi kujengwa miradi ambayo haihusiani na masuala ya elimu, hivyo amtaka mkurugenzi huyo kusitisha mkataba na mtu aliyemkodisha eneo hilo na kisha alizungushie uzio kwa matumizi ya shule.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Septemba 28, 2019) wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa, Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na Madiwani wa Halmashauri hizo akiwa katika siku ya tano ya ziara yake ya kikazi mkoani Iringa.

“Mkurugenzi kafute mikata yote ya ujenzi wa miradi katika eneo la shule ya Gangilonga pamoja na shule ya Wilolesi kwa sababu maeneo hayo hayaruhusiwi kujengwa miradi isiyohusiana na elimu. Eneo hilo lisafishwe na ujengwe uzio.”

Kwa upande wake, Mwanasheria wa Manispaa ya Iringa Nocholous Mwasungura amesema aliandaa mkataba wa kupangisha eneo kwa maelekezo ya Kamati ya Fedha, ambapo Waziri Mkuu alimuuliza kwa nini hakuwashauri kuhusu suala hilo kwa sababu tayari Serikali ilishatoa waraka wa kuzuia jambo hilo.

Pia, Waziri Mkuu amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Happi ofisi ya ardhi ya Manispaa ya Iringa kutokana na kuwepo kwa malalamiko mengi kutoka wananchi juu ya Afisa Ardhi ambaye anadaiwa kujigawia viwanja vingi pamoja na kugawa kiwanja kimoja kwa mtu zaidi ya mmoja.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Happi aliwaonya watumishi hao kutojihusisha na vitendo vya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka pamoja na kuacha chuki, ubinafsi na roho mbaya na badala yake washikamane na wafanye kazi wa bidii.

Naye,Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesera aliiomba Serikali izisaidie halmashauri za wilaya hiyo vyombo vya usafiri kwa sababu magari mengi ni chakavu hali inayosababisha Mkurugenzi wa Manispaa awe anaomba lifti kwake. Waziri Mkuu amewataka waombe kibali cha ununuzi wa magari na watumie fedha zao za ndani.

DAWASA YASHIRIKI MAONESHO YA BIASHARA JIJINI DAR

$
0
0
Mamlaka ya maji safi na maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) wameshiriki maonesho ya kufanya malipo ya Serikali kwa kutumia mtandao wa Vodacom Tanzania yaliyoandaliwa na mtandao huo.

Maonesho hayo yameanza tarehe 26 hadi 30 Septemba  yakifanyika katika viwanja vya Mlimani City leo jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii  kutoka Mamlaka ya maji safi na maji Taka Dar es Salaam (DAWASA), Neli Msuya amesema maonesho hayo yamekuja kuwawezesha watanzania kulipa malipo mbalimba kwa kutumia mtandao wa Vodacom.

DAWASA ni moja ya wateja wakubwa wa mtandao huo ambapo bili za maji utaweza kulipa kupitia mtandao wa Vodacom kwa njia rahisi na bila malipo yoyote.

Huduma zingine zinazotolewa na Mamlaka hiyo ni maunganisho mapya na kulipa bili za wateja. Mamlaka hiyo imehaidi kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja wao pamoja na kuweka mifumo rahisi na rafiki ambayo itawasaidia wateja kuifikia huduma kwa urahisi.
 Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii  kutoka Mamlaka ya maji safi na maji Taka Dar es Salaam (DAWASA), Neli Msuya akitoa maelezo kuhusu kazi zinazofanywa na Mamlaka hiyo kwa wananchi waliotembelea banda hilo wakati wa maonesho ya wafanyabiashara yaliyofanyika katika viwanja vya Mlimani City jijini Dar es Salaam
 Maofisa wa Mamlaka ya maji safi na maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) wakiendelea kutoa huduma kwenye banda la mamlaka hiyo wakati wa maonesho ya wafanyabiashara yaliyofanyika katika viwanja vya Mlimani City jijini Dar es Salaam.
 Ofisa wa Mamlaka ya maji safi na maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) Carolyn Njuju akitoa maelezo kwa baadhi ya kazi zinazotolewa kwa mshereheshaji Taji Liundi(wa pili kushoto) wakati wa maonesho ya wafanyabiashara yaliyofanyika katika viwanja vya Mlimani City jijini Dar es Salaam
   Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii  kutoka Mamlaka ya maji safi na maji Taka Dar es Salaam (DAWASA), Neli Msuy(kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na maofisa wa DAWASA wakati wa maonesho ya wafanyabiashara yaliyofanyika katika viwanja vya Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Huduma zikiendelea kutolewa kwenye banda la DAWASA

IFM ANDAENI RASILIMALI WATU WA DIGITALI AMBAKO MAFISADI NA WEZI WAMEHAMIA HUKO-DKT. MPANGO

$
0
0

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Philip Mpango amesema kuwa Chuo cha Usimamizi wa Fedha kwnda kwa kasi katika teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwani mafisadi na Wezi wanakwenda kidigitali kujipatia fedha hivyo lazima rasilimali watu wa kutosha katika teknolojia.

Waziri Mpango aliyasema hayo wakati akizundua Baraza la Uongozi wa Chuo hicho lilofanyika jijini Dar es Salaam, amesema  kuwa masoko ya mitaji, dhamana na bidhaa nayo lazima yaanze kuangaliwa kwa mtazamo mpya kwa kuwa aina za huduma za kifedha kunyumbulika kwani  wahalifu, wakiwemo mafisadi, wezi wa fedha za umma na matapeli, wameanza kwenda kidigitali.

Dkt.Mpango amesema IFM ni muhimu ianze kujielekeza kuchangamkia fursa na pia kujibu changamoto zinazoambatana na uchumi wa kidigitali ambako ndiko dunia inakoelekea kwa kasi licha ya kukua kwa miamala kupitia simu za kiganjani na kompyuta tayari pia zipo sarafu za kidigitali na miamala mikubwa inafanyika kwa njia hizi hivyo hakuna chaguo bali ni lazima kuanzia sasa mafunzo na utafiti unaofanyika hapa IFM ujielekeze kufungulia ubunifu na uvumbuzi wa vijana wa kitanzania utakaowawezesha kuelewa mabadiliko hayo.

Amesema kuongoza vema sekta ya fedha katika mazingira ya muunganiko wa kidigitali katika sekta ya fedha kitaifa na kimataifa na pia ushindani mkali  kwani hakuna budi kuangalia upya uhasibu na namna ya kuandaa vitabu vya mahesabu na ukaguzi wa miamala ya fedha katika mazingira haya mapya. Kadhalika, masomo ya tasnia ya kibenki na bima.

Dkt.Mpango amesema kila mmoja aliyeuliwa katika baraza hilo ni kwa sababu Serikali imejiridhisha kwamba mnao ujuzi, weledi, uzalendo na uzoefu mkubwa katika uongozi.

 Aidha amesema  kuwa wajube wa baraza wanajua na kuthamini mchango mkubwa wa taasisi za elimu ya juu katika nchi kupitia kazi zake za msingi za kufundisha, kufanya utafiti na kutoa ushauri hivyo, Serikali ina matarajio makubwa kwamba Baraza kweza kukisimamia chuo vizuri.

“Baraza lipeleke cha IFM na mbele zaidi ili kiweze kutoa mchango mkubwa kuliko ilivyo sasa katika maendeleo ya Taifa letu. Tutashangaa sana kama atatokea mmoja wenu akaja kubainika baadaye kwamba anatumia uwepo wake kwenye Baraza kusimamia maslahi binafsi au ya kundi fulani badala ya maslahi mapana ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha na Taifa kwa ujumla”amesema Dkt. Mpango.

“Katika kutekeleza yote panahitajika ushirikiano mzuri na wa karibu sana kati ya Baraza la Uongozi na Menejimenti ya Chuo  hivyo, napenda nisisitize kuwa mivutano isiyo na tija kati ya Baraza na Menejimenti ya Chuo ama ndani ya timu ya menejimenti ya Chuo chetu adhimu isipatiwe nafasi kabisa”amesema Dkt Mpango.

Amesema Baraza lione umuhimu wa kukiongoza Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kwa kuweka jicho la pekee katika maeneo mawili. Kwanza, ni kujitathmini kama kweli elimu inayotolewa katika Chuo hiki na wahitimu wa Chuo hiki vinakidhi mahitaji ya kujenga uchumi wa viwanda na kuibadilisha Tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati itakapofika mwaka 2025 na kuendelea kujenga nchi ya kipato cha juu.

Dkt. Mpango amesema Serikali ya awamu ya tano ni kwamba Chuo hiki kitaendelea kusimamia vizuri maandalizi ya rasilimali hii adhimu ya Usimamizi wa Fedha, itakayokidhi mahitaji ya uchumi wa kati unaongozwa na Sekta ya viwanda ifikapo mwaka 2025.

Nae Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha Profesa Tadeo Satta amesema Chuo kinafanya tafiti na huduma za ushauri services) kwa jamii katika fani za usimamizi wa fedha, uhasibu, benki, bima, kodi, hifadhi za jamii, teknolojia ya mawasiliano ya habari (ICT), sayansi ya komputa na nyinginezo.

Amesema chuo cha Usimamizi wa Fedha kimedhamiria kuwa Kituo Bora cha Mafunzo kwa Taaluma na Utaalamu na vile vile kuleta chachu ya mabadiliko katika fani za fedha na zinazoshabihiana

Katika Mpango Mkakati wa Chuo kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 – 2020/2021 Chuo kimeainisha malengo yafuatayo ambayo yanaendelea kutekelezwa kuboresha mafunzo ya kitaaluma na kitaalamu, utafiti na ushauri elekezi, Kuimarisha Uwezo wa Utendaji wa Rasilimali Watu na zana za kufanyia kazi, Kuboresha mifumo ya utawala bora na uongozi,Kuimarisha Uwezo endelevu wa Fedha,Kuboresha Huduma za Afya na kupunguza maambukizi ya VVU na UKIMWI pamoja ,Kuzingatia na kuendeleza Mkakati wa Taifa wa kupambana na rushwa na mpango wa utekelezaji wa Mkakati huo.

Mwenyekiti wa Baraza hilo Balozi Dkt.Benson Bana amesema changamoto katika chuo hicho watazifanya kuwa fursa katika kufanikisha matarajio ya serikali katika ujenzi wa uchumi wa viwanda.
 Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Philip Mpango katikati akizungumza wakati akizundua Baraza la Uongozi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) uliofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha Profesa Tadeo Satta akitoa maelezo kuhusiana na mikakati ya chuo hicho katika uzinduzi wa baraza la uongozi wa chuo uliofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa baraza la Uongozi wa Chuo hicho Balozi Dkt.Benson Bana akitoa maelezo kuhusiana na baraza lilivyojipanga katika kutekeleza majukumu ya kusukuma chuo katika uzinduzi wa baraza hilo jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Uongozi na Menejimenti ya IFM wakiwa kwenye mkutano huo
 Picha ya Pamoja na Baraza la uongozi na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango
Picha ya Pamoja Menenejimenti ya IFM na Waziri wa Fedha na Mipango 

SBL yazindua kampeni ya ‘Usitumie Kilevi na Kuendesha Chombo cha Moto’ mkoani Tanga

$
0
0
Tanga, Septemba 27, 2019-Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imezindua kampeni inayolenga kutoa elimu kwa umma juu ya unywaji wa kistaarabu, ikiwa ni moja ya hatua muhimu inayochukuliwa na kampuni hiyo kuzuia ajali nyingi zinazosababishwa na madereva wanaoendesha wakiwa wametumia vilevi 

Kampeni hiyo inayobeba ujumbe wa, “Usitumie Kilevi na Kuendesha Chombo cha Moto’ imezinduliwa jijini Tanga leo katika Stendi ya mabasi na kuwakutanisha pamoja wadau mbalimbali ikiwamo Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani, madereva, abiria, na wadau wengine katika sekta ya usafirishaji 

Akiongea wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani (RTO) Tanga, Solomon Mwangamilo, amesema kwa kulishirikisha jeshi la Polisi kampuni ya SBL imeiunga mkono serikali katika kuelimisha umma juu ya unywaji wa kistaarabu na kusisitiza umuhimu wa kutatua tatizo hilo. 

RTO amesema baadhi ya watu na haswa madereva hunywa kiasi kikubwa cha pombe pasipo kujali madhara yanayoweza kusababishwa na kitendo hicho na kuonya kuwa vitendo vya aina hiyo vinaweza kusababisha ajali mbaya barabarani. 

“Sote tunafahamu kuwa matumizi ya vileo yana uhusiano mkubwa na uendeshaji mmbovu ambao unaweza husababisha ajali mbaya za barabarani zenye athari kubwa kwa jamii zetu. Athari zake siyo tu zinawagusa watumiaji wa vilevi bali hata maisha ya wengine na kusababisha upotevu wa maisha na ulemavu kwa watu ambao wangeweza kuchangia uchumi wa nchi,” amesema. 

RTO ameongeza kusema kuwa pamoja na kusababisha vifo visivyotarajiwa na majeraha, unywaji usiokuwa wa kistaarabu una maadhara makubwa kwenye sekta ya afya kwa kuwa kiasi kikubwa cha fedha kinatumika kwa ajili ya huduma, madawa na vifaa tiba kwa waathirika wa ajali za barabarani na hivyo kuwa ni mzigo kwa Serikali. 

Akizungumzia namna kampeni hiyo itakavyoisadia jamii, mkuu huyo wa usalama barabarani amesema, “sote kwa pamoja ikiwamo askari, madereva, jamii na wadau wengine tuna jumuku la kutafuta suluhisho la kumaliza tatizo la kutumia vilevi na kuendesha vyombo vya moto. Ninayo furaha kuona SBL pamoja na kwamba biashara yao ni kuuza vilevi, wameona wanawajibu wa kuhimiza unywaji wa kistarabu”. 

Akiongea wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL John Wanyancha amesema kampeni ya unywaji wea kistaarabu inalenga kuielimisha jamii kuwa wanywaji wanapaswa kunywa kwa kiasi na kuhakikisha unywaji wao hauna madhara kwao na kwa watu wanaowazunguka. 

“SBL imedhamiria kuungana na serikali na wadau wengine kuhakikisha kuwa jamii na haswa madereva ambao wanakunywa na kuendesha vyombo vya moto wanaelimishwa juu ya madhara ya vitendo hivyo na kutakiwa kubadilisha tabia,” amesema Wanyancha. 

Kampeni hii ambayo imekuwa ikifanyika katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania, inalenga kuwafikia vijana na watu wengine kwa kuwaeliisha juu ya madhara ya unywaji usiokuwa wa kistaarabu huku ikiwataka kubadili tabia kwa manufaa yao na jamii kwa ujumla
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoani Tanga, Solomon Mwangamilo, akimvalisha reflector mmoja wa madereva wa pikipiki (bodaboda) katika tukio la uzinduzi wa kampeni ya ‘Don’t Drink and Drive’ inayoendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti ikiwa na lengo la kutokomeza ajali za barabarani zinazosababishwa na madereva walevi. 




SERIKALI KUTUMIA CHANZO CHA MTO PANGANI KUTATUA TATIZO LA MAJI MIJI YA HANDENI,MUHEZA,PANGANI NA KOROGWE

$
0
0
 NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) akizungumza wakati wa ziara yake kushoto ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly kulia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo
WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) kushoto akimsikiliza kwa umakini  Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo wakati wa ziara yake wilayani humo katika aliyevaa kofia ya kijani ni Mbunge wa Jimbo la Muheza Balozi Adadi Rajabu
 NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) kushoto akimsikiliza kwa umakini Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini wakati wa ziara yake leo
 NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM)  kushoto akiangalia chanzo cha maji cha Mto Pangani kilichopo eneo la Mandera wilayani Korogwe wakati wa ziara yake ya kukagua chanzo hicho leo
NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) kulia akitembelea kwenye maeneo mbalimbali kwenye chanzo hicho akiwa na Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini (CCM) Mary Chatanda wakati wa ziara yake.
 NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) kulia akikagua kwenye maeneo mbalimbali kwenye chanzo hicho akiwa na Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini (CCM) Mary Chatanda kushoto wakati wa ziara yake.
 NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) katikati aliyevaa koti akiwa na Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Thimotheo Mzava na Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini (CCM) Mary Chatanda wakati wa ziara yake wakiangalia chanzo cha maji

Chanzo cha Maji cha Mto Pangani ambaho kitatumika kwenye miradi hiyo ya maji

SERIKALI imesema kwamba itatumia chanzo cha Mto Pangani kutatua tatizo la maji kwenye miji ya Handeni, Pangani, Muheza na Korogwe ili kuondosha kero hiyo ambayo imedumu kwa muda mrefu kwenye maeneo hayo

Hatua hiyo imekuja baada ya serikali kupata fedha dola milioni 500 kutoka Serikali ya India kuweza kutekeleza miradi wa maji kwenye miji 28 hapa nchini ambapo zaidi ya wananchi 600,000 watanufaika

Hayo yalisemwa leo na Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso wakati alipofanya ziara yake kwenye wilaya za Muheza na Korogwe kukagua chanzo maji cha Mandera ambacho kitatumika kuchukua maji katika mradi mkubwa wa ukarabati wa mradi wa HTM kwa ufadhili wa fedha za india kwa miji minne.

Alisema kwamba kutokana na hilo changamoto ya aji kwenye miji hiyo itakuwa imepata ufumbuzi kutokana na juhudi kubwa ambazo zimefanywa na serikali kuweza kupatikana fedha hizo kwa ajili ya utekelezaji wa miradi.

“Labda niwaambie kwamba Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt Magufuli imedhamiria kumaliza changamoto ya maji kwenye mji wa Muheza na maeneo mengine kwa lengo la kumtua mama ndoo kichwani “Alisema Naibu Waziri Aweso.

Alisema kwamba wakati wa utekelezaji wa mradi wa kutoka Maji Mto Pangani kwenye miji hiyo matenki makubwa na eneo la kutibu maji yatajengewa eneo la Segera na baadae kupelekea maeneo husika kwa ajili ya wananchi kupata huduma hiyo muhimu.

“Lakini chanzo hicho kitakuwa ni cha mserereko kuhakikisha wanapunguza gharama za uendeshaji wa mradi huo hivyo ni imani yangu kwamba mradi huo utakapokamilika wananchi wataondokana na adha ya maji kwa dhani ya Rais kumtua mama ndoo kichwani “Alisema

Hata hivyo alisema kwamba wahandisi wa Halmashauri wamekwisha kupita maeneo yote na hivyo hivi sasa wanasubiri kibali kitakapotoka mradi huo utaanza mara moja ikiwemo kutangaza tenda kuwapata wakandarasi ili mradi huo uanze kwa wakati.

“Labda niwaambieni kwamba sisi kama viongozi wa wizara hatutakuwa kikwazo kuhakikisha mradi huo unaanza kutekelezwa kwa wakati kuwawezesha ananchi waweze kupata maji”Alisema

Naibu Waziri huyo alisema kwamba wanatambua uwepo wa changamoto kubwa ya maji wilaya ya Muheza lakini mradi wa maji utakaotokaa Pongwe utasaidia kupunguza adha hiyo lakini mradi huo mkubwa utapunguza tatizo la maji.

Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu alisema ujio wa ziara ya Naibu Waziri huyo ni ishara kwamba wilaya ya Muheza inakaribia kufurika maji kutokana na uwepo wa chanzo hicho kikubwa cha Mto Pangani.

“Naamini Kata nyingi zitanufaika hivyo niombe wakandarasi waje mapema kazi hiyo ianze haraka kwa sababu wananchi muheza wamevumilia muda mrefu na kuna kilio cha tatizo hilo hivyo kupitia mradi huo wanaweza kuondokana na adha hiyo “Alisema Mbunge Balozi Adadi.

Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo Mkurugenzi Mtendaji Mtendaji wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira (HTM) Mhandisi Yohana Mgaza alisema kwamba chanzo cha Mandera hicho kitatumika kuchukua maji kwenye mradi mkubwa wa ukarabati wa mradi huo wa HTM kwa ufadhili wa fedha za India kwa miji hiyo.

Alitaja miji hiyo kuwa ni Korogwe, Handeni,Pangani na Muheza na vijiji vitakavyokuwa pembeni ya bomba ambapo mradi huo ni mkubwa na utanufaisha watu zaidia ya laki sita.

MAJALIWA AKAGUA UKARABATI WA CHUO CHA MAENDELEO YA WANANCHI,AWEKA JIWE LA MSINGI LA MRADI WA MAJI ILULA

$
0
0


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ukarabati wa majengo ya Chuo cha Maendeleo ya Wananchi cha Ilula akiwa katika ziara ya wilaya ya Kilolo, Septemba 27, 2019. Kushoto kwa Waziri Mkuu ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Tekinoloji, Dkt. Avemaria Semakafu na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happy. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa Ilula wilayani Kilolo, Septemba 27, 2019. Kushoto ni mkewe Mary, kulia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Jasephat Kandege, wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happy na wa pili kushoto ni Mbunge w Kilolo, Venance Mwamoto.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa Ilula wilayani Kilolo, Septemba 27, 2019. Kushoto ni mkewe Mary, kulia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Jasephat Kandege, wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happy na wa nne kushoto ni Mbunge wa Kilolo, Venance Mwamoto.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa Ilula wilayani Kilolo Septemba 27, 2019. Wa pili kulia ni mkewe Mary, wa pili kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Iringa, Ally Happy na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kilolo, Asia Abdallah. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

SERIKALI YATOA ONYO KALI KWA WATENDAJI KATA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaonya baadhi ya Watendaji Kata na askari nchini ambao wamekuwa wakishindwa kuzifikisha sehemu husika kesi za watu waliowapa ujauzito wanafunzi na amesema watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Ameyasema hayo jana jioni (Ijumaa, Septemba 27, 2019) wakati akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Ilula Sokoni, kata ya Nyalumbu wilayani Kilolo akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Iringa.

“Wanafunzi bado wanaendelea kupewa ujauzito na kukatishwa masomo yao huku watu waliohusika na vitendo hivyo wakishindwa kuchukuliwa hatua stahiki kwa sababu baadhi ya watendaji na askari wamezikalia kesi zao na kushindwa kuwafikisha polisi.”

“Watoto wa kike lazima walindwe ili wamalize masomo yao waje kulitumikia Taifa lao. Serikaliimeweka sheria kali ya kumlinda mtoto wa kike lengo ni kumuwezesha amalize masomo yake ili aweze kujikwamua kiuchumi na aondokane na utegemezi.”

Waziri Mkuu alisema watoto wa kike wanatakiwa kuheshimiwa katika jamii na adhabu iliyowekwa na Serikali ni kifungo cha miaka 30 jela kwa mtu atakayemuoa, kumpa ujauzo na hata ukikutwa naye nyumbani kwako, katika nyumba ya wageni.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka wananchi hususan waishio vijijini wasikubali kurubuniwa na kugawa ardhi yao kwa watu mbalimbali wanaofika kwenye maeneo yao na kutaka wauziwe ardhi bila ya kuzihusisha mamlaka husika.

“Eneo lenu hili la Ilula ni zuri hivyo msikubali kurubuniwa kuuza ardhi yenu kwa sababau inathamani kubwa. Viongozi wa Kata na Vijiji hakikisheni mnaratibu vizuri na muandae mpango wa matumizi bora ya ardhi ili kuepuka migogoro.”

Waziri Mkuu alisema wananchi hao wanatakiwa wawe makini na ardhi na mamlaka zinazohusika na ardhi lazima zihusishwe katika ugawaji wa ardhi kwa sababu wakigawa hovyo watasababisha vijana wao hapo baadaye wakose maeneo ya kilimo.

Akizungumzia kuhusu uboreshwaji wa huduma za afya, Waziri Mkuu ameahidi ujenzi wa kituo cha afya katika kata ya Ilula ili kuwapunguzia wananchi kutembea umbali mrefu hadi Iringa mjini kwa ajili ya kufuata huduma hizo.

Alisema kituo kitakachojengwa kitakuwa na chumba cha kujifungulia, chumba cha maabara kwa ajili ya vipimo mbalimbali, huduma za mama na mtoto, mapasuaji, wodi ya wanaume na wanawake, aliwataka wananchi waendelee kuwa na imani na Serikali yao.

Waziri Mkuu alisema suala la kuboresha na kusogeza huduma mbalimbali za kijamii kwa wananchi zikiwemo za afya limepewa kipaumbele na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli ambaye anataka kuona wananchi wakiwa na afya nzuri ili waweze kushiriki ipasavyo katika shughuli zao za kimaendeleo.

Kabla ya kuhutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara, Waziri Mkuu alikagua ujenzi wa mradi wa maji Ilula na kuweka jiwe la msingi. Pia, Waziri Mkuu alikagua shughuli za ukarabati wa chuo cha Maendeleo ya Wananchi Ilula.

Awali, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Josephat Kandege aliwahimiza wananchi hao wajiunge katika Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ili wawe na uhakika wa kupata huduma za matibabu ya bure wao na familia zao.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Happi alisema kuwa awali eneo la Ilula lilikuwa linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo yam ogogoro ya ardhi ambayo kwa kushirikiana na watendaji wenzake walifanikiwa kuitatua.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia Mkutano wa Hadhara kwenye uwanja wa Ilula Sokoni wilayani Kilolo, Septemba 27, 2019.
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akiwasalimia wananchi katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye Uwanja wa Ilula Sokoni wilayani Kilolo, Septemba 27, 2019. Kulia ni Mbunge wa Kilolo, Venance Mwamoto na wa pili kushoto ni Mwenyekititi wa CCM wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Abel Nyamahanga.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Serikali Kutumia Bilioni 100 Kumaliza Tatizo la Maji Kilwa

$
0
0

Waziri wa Maji, Prof. Makame Mbarawa akipokea taarifa ya ujenzi wa tenki la maji la Mradi wa Maji wa Mpigamiti uliopo katika Wilaya ya Liwale, mkoani Lindi. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Liwale, Sarah Chiwamba.
Waziri wa Maji, Prof. Makame Mbarawa akikagua ujenzi wa tenki la maji la Mradi wa Maji wa Mpigamiti uliopo katika Wilaya ya Liwale, mkoani Lindi.
Tenki la maji la Mradi wa Maji wa Mpigamiti katika Wilaya ya Liwale, mkoani Lindi.
Waziri wa Maji, Prof. Makame Mbarawa akisalimiana na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa mara baada ya kuwasili wilayani hapo, kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai.
Waziri wa Maji, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Mb) akiwa na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Kilwa, wa pili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai.
Waziri wa Maji, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Mb) akihutubia wakazi wa Kilwa Kivinje katika Wilaya ya KIlwa, mkoani Lindi.

………………….

Serikali imepanga kutumia Shilingi bilioni 100 katika kufanikisha utekelezaji wa mkakati wa kumaliza tatizo la maji la muda mrefu katika mji mkongwe wa Kilwa, mkoani Lindi. 

Mpango huo ni wa muda mrefu wa kufikisha huduma ya majisafi na salama kwa wananchi wa Kilwa, ni sehemu ya utekelezaji wa ujenzi wa miradi ya maji katika miji 29 nchini Kilwa ikiwa ni mji mmojawapo, utakaogharimu jumla ya Shilingi trilioni 1.2 zinazotokana na mkopo wa bei nafuu kutoka Benki ya Exim ya India.

Akitoa ufafanuzi wa utekelezaji wa mradi huo mbele ya wakazi wa Kilwa Kivinje, Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa amesema kazi ya upembuzi yakinifu imeshakamalika na taarifa zake zipo nchini India kwa ajili ya kupata kibali, akisema baada ya kupata kibali Serikali itatangaza zabuni na ifikapo Januari, 2020 inatarajia kumpata mkandarasi na kuanza kazi.

Profesa Mbarawa amesema jumla ya gharama za ujenzi wa mradi huo ni Shilingi bilioni 100 na utamaliza kabisa tatizo la maji Kilwa. Lakini akisema kuwa kabla ya mradi huo kuanza, utekelezaji wa mradi wa maji wa Shilingi bilioni 1.3 utakaohudumia maeneo ya Kilwa Kivinje, Kipatimu, Somanga na Pande utaanza hivi karibuni kama mpango wa muda mfupi wakati wakisubiri mradi huo mkubwa.

‘‘Niwatoe hofu wananchi wa Kilwa kuwa tutaanza kutekeleza mradi wa maji kama suluhisho la muda mfupi, wakati utaratibu wa ujenzi wa mradi mkubwa ukiendelea. Tutatoa kipaumbele kwa maeneo yenye changamoto kubwa ya maji ikiwemo kwa kuwa ndio lengo la Serikali’’, Profesa Mbarawa amesema.

Akitoa shukrani zake kwa Serikali kwa niaba ya wakazi wa Kilwa, Mbunge wa Jimbo la Kilwa, Salum Bungala amesema hakika wamefarijika sana na jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano za kumaliza tatizo la maji mjini Kilwa na inathibitisha kwa vitendo kuwa maendeleo hayabagui itikadi za kisiasa kwa kupeleka maendeleo kwa wananchi wote.

Awali, Waziri wa Maji, Profesa Mbarawa alikagua Mradi wa Maji wa Mpigamiti uliopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Liwale na kubaini mapungufu katika ujenzi wa tenki la maji la huo yanayosababisha usalama wa tenki hilo kuwa mdogo.

Akitoa maelekezo baada ya kukuta mapungufu hayo, Profesa Mbarawa amesema ataunda timu ya wataalam kwa ajili ya kuchunguza, kubaini tatizo na hatua zinazotakiwa kuchukuliwa. Akisisitiza kuwa endapo uwezekano wa kukarabati tenki hilo utashindikana, itabidi lijengwe tenki jipya.
Hata hivyo, ametoa onyo kwa Kampuni ya Don Consult ambayo ilifanya kazi ya usanifu wa mradi huo akisema kuwa endapo itabainika mapungufu hayo yametokana na uzembe wao ni lazima achukue hatua stahiki kwa kampuni hiyo.

Akisisitiza Serikali haitarudia tena makosa ya kuwekeza fedha nyingi bila kupata matokeo chanya kwenye miradi ya maji na kila mradi utakaokamilika ni lazima uwe na thamani halisi ya fedha zilizotumika.

Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa amemaliza ziara yake mkoani Lindi kwa kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya maji katika wilaya zake zote za Lindi, Ruangwa Nachingwea, Liwale na Kilwa.

WAZIRI BITEKO ATAKA WANAOTOROSHA MADINI KWENDA NJE YA NCHI KUACHA MARA MOJA

$
0
0
WAZIRI wa Madini Doto Biteko akizungumza na wananchi wa wilaya ya Tunduuru wakati wa ziara yake mkoani Ruvuma
 MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme akizungumza wakati wa ziara hiyo kulia ni Waziri wa Madini Doto Biteko
MKUU wa wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma Julius Mtatiro akizungumza katikati ni Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme kulia ni Waziri wa Madini Doto Biteko 


WAZIRI wa Madini Doto Biteko amewataka watu wanaotorosha madini hapa nchini kwenda nchi za nje waache mara moja biashara hiyo kwani ni zilipendwa badala yake wayapeleke kwenye masoko mbalimbali ili kuweza kuyauza.

Biteko aliyasema hayo akiwa kwenye ziara yake mkoani Ruvuma ambapo alisema kwamba badala yake wafanyabiashara hao kupeleka madini yao na wayauze huku akieleza iwapo wanataka kibali cha kusafirisha madini watapata ndani ya masoko hayo.

Alisema kwamba unaweza kununua madini ukafungiwa na unaweza kusafirisha huku akiwaomba viongozi wa serikali watu wa wizara ya madini, mamlaka nyengine wawasaidie watanzania kunufaika na madini yao.

 “Ndugu zangu tusiwafanye watanzania wawe watoshaji wa madini tukiwa tunawafuata kila wakati utawafanya watu wasifike kwenye soko na wafurahie kufanya vitendo ambavyo sio vizuri “Alisema.

Waziri Biteko pia aliwataka watanzania wajanja wajanja wanaotaka kuuza madini feki teknolojia imekuwa hivi sasa hivyo wasijiingize kwenye matatizo kwa maana hawatasalimika.

“Katika mkoa wa Ruvuma na nchi ya Tanzania kuna maeneo yanayozalisha madini ya vito kwa wingi ni Tunduru ipo na ni wilaya zinazozalisha vito kwa wingi.. Tulikuwa tunafanya baishara kubwa lakini maisha ya watu wa tunduru yalikuwa hayaonyeshi kama kulikuwa na maisha ya namna hiyo”Alisema

“Madini yalikuwa yanatoroshwa kupelekwa nje ya nchi lakini Rais wetu Dkt John Magufuli akasema tufunge breki tuanzisha masoko ya madini hatua ambayo imeweza kuwasaidia sana sekta ya madini hapa nchini “Alisema

Alisema kwamba katika kumbukumbu zake mwezi February  mwaka jana alikutana na wageni wengi ambao wananunua madini kupitia leseni za wenyeji huku wakiwapa kupewa fedha kiduchu jambo ambalo lilikuwa likiwaumiza watanzania wengi.

Waziri huyo alisema kwamba lakini Rais Dkt Magufuli akawataka watengeneze utaratibu wa kusimamia madini hayo ili yaweze kuwa na manufaa kwa watu wa tunduru na mkoa kwa ujumla.

“Watu wa Tunduru wanahitaji fedha wajenge nyumba nzuri,fedha wasomeshe watoto,wale vizuri wakae kwenye mazingra mazuri hata mtu akiihtaji kuoa aweze kuona bila mkopo”Alisema

Kongamano la kuombea uchaguzi Serikali za Mitaa kufanyika Singida

$
0
0
Mratibu wa Kongamano la kuombea nchi amani kutoka Taasisi ya Mudir Markaz Safina, Sheikh Said Kinyogoli(katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Kongamano hilo mjini hapa jana.Kulia ni Sheikh Najim Humoud na kushoto ni Imamu Sheikh Abubakar Masuala. (Picha Boniphace Jilili).



Na Boniphace Jilili, Singida 


Kongamano kubwa la kuiombea nchi amani kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa kufanyika mkoani Singida.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, Mratibu wa Kongamano hilo Sheikh Said Kinyogoli alisema limeandaliwa na TaasAsi ya Mudir Markaz Safina chini ya baraza kuu la waislam Tanzania (Bakwata),lengo likiwa ni kuiombea nchi amani katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.

"Panapo kusekana amani hauwezi kufanya jambo lolote liwe la kijamii na la kimaendeleo kwani ukijaribu mara unasikia bomu linalipuka kwasababu hakuna amani." alisema Sheikh Kinyogoli.

Sheikh Kinyogoli alisema kongamano hilo litafanyika kwa siku saba katika viwanja vya Shule ya Msingi Ukombozi mjini hapa, kuanzia siku ya jumatano wiki hii na litashirikisha watu wote bila kujali itikadi za kidini, ambapo watakuwepo masheikh, Hilary Kipozeo, Hashim Mbonde na Mzee Yusuph wote kutoka Dar es salaam. 

Wengine ni Sheikh Jafari Abdulahaman kutoka Morogoro, Sheikh Mohamed Makarani-Mwanza pamoja na Sheikh Ibrahim Mlumbango kutoka Kigoma. 
Alisema sanjari na kuiombea nchi amani pia watakuwa wanaadhimisha mwaka mpya wa kiislam ambapo watatoa nasaha za kidini ili watu wawe na hofu ya Mungu.

Sheikh Juma aliongeza kuwa katika kongamano hilo yatatolewa mafunzo ya ujasiriamali kwa ajili ya watu kujifunza mbinu za kujitegemea kwa kufanya shughuli mbalimbali za uzalishaji ili kujiinua kiuchumi.

TUTAHAKIKISHA MALIGHAFI ZINAZOHITAJIKA VIWANDANI ZINAPATIKANA - MHE HASUNGA

$
0
0
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Vwawa Mkoani Songwe tarehe 27 Septemba 2019. (Picha Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo) Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songwe Serikali imesema kuwa inaimarisha mikakati yake ili kuwa na uwezekano wa kuwa na malighafi toshelevu katika viwanda vyote nchini. 

Ifahamike kuwa malighafi nyingi zinazotumika viwandani asilimia kubwa zinatokana na sekta ya kilimo hivyo moja ya mkakati madhubuti ni kusimamia kwa weledi sekta hiyo ili kuwa na malighafi nyingi na za kutosha. Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 27 Septemba 2019 wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Vwawa Mkoani Songwe. 

Alisema kuwa miongoni mwa majukumu muhimu ya Wizara ya kilimo ni kuimarisha Mchango wa sekta ya kilimo ili wakulima waweze kuongeza uzalishaji na tija. "Ni lazima tuhakikishe kuwa watu wanazalisha kwa ajili ya biashara sio chakula pekee na gharama wanazotumia ni lazima wahakikishe zinarudi ili waone faida ya kilimo" Alikaririwa Mhe Hasunga Waziri Hasunga ameeleza kuwa serikali kupitia wizara ya kilimo ina jukumu la kuhakikisha umasikini unapungua kwa kuongeza uzalishaji kwa wakulima ili kilimo kiendelee kuingiza fedha nyingi za kigeni na kuchangia kwa wingi pato la Taifa. 

Kadhalika ametaja Mikakati mingine ya wizara ya kilimo kuwa ni pamoja na Pembejeo (Mbegu bora, Mbolea, na Viuatilifu) kufika kwa wakati kwa wakulima ambapo amesisitiza kuwa wananchi wanapaswa kununua mbegu Bora kwani zinaweza kukinzana na magonjwa na nyingi zinastahimili ukame. Kuhusu masoko ya mazao ya wakulima waziri Hasunga amesema kuwa wizara yake imekuja na mkakati maalumu wa kuanzisha kitengo cha masoko kitakachokuwa na majukumu ya kubainisha masoko ya mazao mbalimbali ya wakulima. 

"Ni lazima kufanya biashara kisasa kwa kujua mahitaji ya soko kabla ya kuzalisha mazao ya kilimo ili wakulima wanapozalisha tayari wawe wanajua watauza wapi mazao yao" Alisisitiza Mhe Hasunga Katika mkutano huo uliohudhuriwa na mamia ya wananchi ambao ni wakazi wa mamlaka ya mji mdogo wa Vwawa na ameneo ya jirani, Waziri Hasunga amewataka wananchi kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli katika kuimarisha ufanisi wa shughuli za maendeleo katika Jimbo la Vwawa na Taifa kwa ujumla.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Vwawa Mkoani Songwe tarehe 27 Septemba 2019. (Picha Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)

Viewing all 110151 articles
Browse latest View live




Latest Images