Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

TANZANIA YAITAKA JUMUIYA YA KIMATAIFA KUWEKA MAZINGIRA SAWA YA BIASAHARA

$
0
0


Tanzania imeitaka Jumuiya ya Kimataifa kuhakikisha uwepo wa uwanda na vigezo sawa vya kibiashara ili kuliwezesha bara la Afrika kushiriki kikamilifu katika uchumi jumuishi sambamba na kuwa na mpango kabambe wa kumaliza migogoro katika Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) baada ya njia ya kijeshi inayotumiwa na Jumuiya ya Kimataifa kutozaa matunda.

Akihutubia kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika Mkutano wa 74 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unaofanyika New York,Marekani,Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi ameiambia Jumuiya ya Kimataifa kuwa baada ya mbinu za kijeshi kutumika kutafuta suluhu katika Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kushindikana wakati umefika wa kutafuta majawabu mapana zaidi kuhusu hali ya usalama nchini humo.

Mbali na kutaka Jumuiya ya Kimataifa kuwa na mpango kabambe juu ya utatuzi wa migogoro katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,pia Tanzania imeitaka Jumuiya hiyo kuondoa vikwazo dhidi ya Zimbambwe huku ikisisitizwa kuwa wanaoteseka katika suala hilo ni wanawake,watoto na wazee wakati ambapo jambo lililosababisha Zimbabwe kuwekewa vikwazo halipo tena.

Pia Tanzania imetoa msimamo wake wa kuendelea kuiunga mkono Umoja wa Mataifa kwa madai ya uwepo wa vitendo vya baadhi ya Mataifa Makubwa dunani kuupuuza Umoja wa Mataifa na kwamba inabariki mageuzi ya kimfumo na utendaji yanayofanyika katika umoja huo na kutoa wito kwa Mataifa ulimwenguni kuheshimiana.

Pro. Kabudi ametoa shime kwa Nchi za Bara la Afrika kuanza kutumia rasilimali na malighafi zake ili kujiletea maendeleo kwa kuwa Bara hilo ni tajiri licha ya kulazimishwa kuwa masikini na kwamba wakati sasa umefika kwa Afrika kujitegemea kwa kutengeneza bidhaa zake na kuondoa tatizo la ajira kwa vijana bara hilo badala ya kugeuzwa soko la Mataifa yaliyoendelea na sehemu ya kuchukulia malighafi ya kuendleza viwanda katika mabara mengine.

Pia ameitaka Jumuiya ya Kimataifa kuhakikisha uwepo wa uwanda na vigezo sawa vya kibiashara jambo litakaloliwezesha bara la Afrika kushiriki kikamilifu katika uchumi jumuishi na kuongeza uwezo wa kibiashara.

Mara baada ya kumaliza kuhutubia katika Mkutano mkuu wa 74 wa Baraza la Umoja wa Mataifa mabalozi na viongozi mbalimbali kutoka bara la Afrika,Marekani,Ulaya na Asia walijipanga mstari na kumpongeza Prof. Palamagamba John Kabudi kwa hotuba yake thabiti na ya kusisimua ambayo imeweka misimamo mbalimbali kwa manufaa ya mataifa yote. 

Jumla ya ndugu wa wagonjwa 95 wanaotibiwa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wafanyiwa uchunguzi wa viashiria vya magonjwa ya moyo bila malipo

$
0
0
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Agness Lugendo akimpima msukumo wa damu mwilini (BP) bila wa malipo ndugu wa mgonjwa anayetibiwa katika Taasisi hiyo aliyejitokeza kufanyiwa vipimo vya awali vya viashiria vya magonjwa ya moyo kwa ndugu wa wagonjwa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Moyo Duniani iliyofanyika katika taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Faustina Mwapinga
akimpima bila malipo kiwango cha sukari kwenye damu ndugu wa mgonjwa anayetibiwa katika Taasisi hiyo aliyejitokeza kufanyiwa vipimo vya awali vya viashiria vya magonjwa ya moyo kwa ndugu wa wagonjwa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Moyo Duniani iliyofanyika katika taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Afisa Lishe wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Husna Faraji akitoa elimu ya jinsi ya kuepuka magonjwa ya moyo kwa ndugu wa wagonjwa wanaotibiwa katika taasisi hiyo waliojitokeza kufanyiwa vipimo vya awali vya viashiria vya magonjwa ya moyo kwa ndugu wa wagonjwa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Moyo Duniani iliyofanyika katika taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Benson Bisane akimpima uzito, urefu pamoja na uwiano wa urefu na uzito bila malipo ndugu wa mgonjwa anayetibiwa katika taasisi hiyo aliyejitokeza kufanyiwa vipimo vya awali vya viashiria vya magonjwa ya moyo kwa ndugu wa wagonjwa wakati wa maadhimisho ya siku ya Moyo Duniani iliyofanyika katika taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.

*****************************

Na Alice Mbilinyi -JKCI

28/09/2019 Jumla ya ndugu wa wagonjwa 95 wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wamefanyiwa uchunguzi wa viashiria vya magonjwa ya moyo bila malipo pamoja na kupewa elimu ya jinsi ya kuyaepuka magonjwa hayo wakati wa maadhimisho ya siku ya moyo Duniani.

Kati ya ndugu hao wa wagonjwa waliofanyiwa vipimo asilimia 50 walikutwa na uzito mkubwa, asilimia 20 walikutwa na shinikizo la juu la damu ambapo asilimia tano walianzishiwa dawa za kutumia.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam Dkt. Alexander Morosso alisema wagonjwa wengine sita wamekutwa na matatizo yanayohitaji uchunguzi zaidi na hivyo wameanzishiwa kliniki.

“Asilimia kubwa ya watu tuliowapima walikutwa na tatizo la uzito mkubwa hii inaonesha kuwa watu hawafanyi mazoezi na kutozingatia lishe bore hivyo basi tumewashauri wapunguze kula vyakula vyenye mafuta, kuthibiti uzito wa mwili na kufanya mazoezi angalau dakika 30 kila siku”,

“Wote tuliowapima siku ya leo tumewashauri wawe na tabia ya kupima afya zako mara kwa mara ili kujua hali zao za afya na kugundua mapema kama kuna tatizo kwani wengi tuliowapima na kuwakuta na matatizo hawakuwa wanajuwa kuwa wanamatatizo ya shinikizo la juu la damu”, alisema Dkt. Mrosso.

Kwa upande wake Afisa Lishe wa Taasisi hiyo Husna Faraji alisema katika upimaji huo wametoa elimu ya jinsi ya kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo kwa kufuata mtindo bora wa maisha ikiwa ni pamoja na kutmia maziwa yaliyopunguzwa au kuondolewa mafuta, kupunguza ulaji wa nyama nyekundu, hususan zenye mafuta, kula zaidi nyama ya kuku au samaki na kuepuka kula vyakula vilivyokaangwa au vyenye mafuta kama soseji, nyama ya kusaga, keki, maandazi, vitumbua na viazi vya kukaanga.

“Nimewashauri kina mama wabadilishe njia ya kupika vyakula badala ya kukaanga wachemshe, wapike kwa mvuke, kuoka au kuchoma na watumie mafuta kidogo wakati wa kupika pia waongeze ulaji wa vyakula vya jamii ya kunde, mbogamboga na matunda. Pia waongeze matumizi ya nafaka hasa zile zisizokobolewa kama unga wa dona, unga wa atta, ulezi na mtama”,alisema Husna.

Aidha Husna aliwashauri kupanga shughuli ambazo watazifanya kila siku kwa kutembea kwa miguu, kutumia njia ndefu ya kutembea badala ya ile ya mkato, kupunguza muda wa kutazama televisheni na kufanya shughuli zinazotumia viungo vya mwili kama kufua, kuosha vyombo, kuosha gari, kusafisha nyumba, kazi za bustani, kufyeka majani, kutumia redio, kwani mara nyingi unaweza kufanya shughuli mbalimbali huku ukisikiliza redio, kuepuka msongo wa mawazo, kuepuka uvutaji wa sigara au utumiaji wa tumbaku na kuepuka au kupunguza matumizi ya pombe.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Taasisi hiyo Anna Nkinda alisema kila mwaka maadhimisho ya siku ya moyo hufanyika tarehe 29 mwezi wa tisa ambayo kwa mwaka huu ni siku ya jumapili. Lakini kwa kuwa Taasisi hiyo kwa mwaka huu ilipanga kufanya upimaji kwa ndugu wa wagonjwa wanaowatibu na siku ya jumapili hakuna kliniki ya wagonjwa wa nje ikaona ifanye upimaji huo siku ya jumamosi tarehe 28/09/2019.

“Katika kuadhimisha siku ya moyo Duniani tumefanya upimaji wa urefu na uzito, tumeangalia uwiano baina ya urefu na uzito, tumepima kiwango cha sukari kwenye damu msukumo wa damu mwilini (BP) na kutoa dawa kwa watu waliokutwa na matatizo. Tumetoa elimu ya jinsi ya kuepuka magonjwa ya moyo na lishe bora kwa wagonjwa kwa kuwa ndugu wa wagonjwa ndiyo wauguzaji tukaona nao tuwafanyie upimaji na kutoa elimu kwao ambayo itawasaidia kufahamu magonjwa wa moyo”, alisema Anna.

Nao ndugu wa wagonjwa ambao wamefanyiwa upimaji pamoja na kupewa elimu waliishukuru Taasisi ya Moyo kwa huduma hiyo kwani wao kama wauguzaji wa wagonjwa ni muhimu wakafahamu ugonjwa ya moyo pamoja na lishe bora kwa wagonjwa.

Alishukuru Zuhura Issa, “Mama yangu anatibiwa katika Taasisi hii, baada ya kusikia leo tunafanyiwa upimaji nimefurahi kwani nami nimepata faida ya upimaji pamoja na elimu. Ninaomba upimaji kama huu uwe unafanyika mara kwa mara”,.

Kila mwaka tarehe 29 mwezi wa tisa huwa ni maadhimisho ya siku ya moyo Duniani ambapo wadau mbalimbali wanafanya upimaji kwa wananchi pamoja na kutoa elimu kuhusu magonjwa hayo. Kauli mbiu ya mwaka huu ni : “Kwa moyo wangu, kwa moyo wako, sote pamoja kwa mioyo yetu , tunatimiza ahadi”.

TGNP MTANDAO YATAMBULISHA MRADI WA SAUTI YA MWANAMKE NA UONGOZI TANZANIA

$
0
0
Mratibu wa Mradi wa Sauti ya Mwanamke na Uongozi Tanzania,Shakila Mayumana akizungumza wakati wa kutambulisha mradi huo leo Septemba 28,2019


TGNP Mtandao imetambulisha rasmi mradi wa Sauti ya Wanamke na Uongozi Tanzania 'Women's Voice and Leadership - Tanzania' utakaotelezwa kwenye mikoa 9 kwa lengo la kujenga uwezo kwa wanawake wa Tanzania, vikundi na Taasisi za kutetea haki za wanawake ili kuwezesha wanawake na wasichana na kuongeza ulinzi wa haki za wanawake na wasichana kufikia usawa wa kijinsia.

Mradi huo utakaodumu kwa kipindi cha miaka mitano 'Aprili 2019 hadi Machi 2023' kwa ufadhili wa Global Affairs Canada (GAC) umetambulishwa rasmi leo Jumamosi Septemba 28, 2019 kwa washiriki wa mradi waliohudhuria Tamasha la 14 la Jinsia 2019 katika kikao cha kutathmini Tamasha la Jinsia la 14 kilichofanyika kwenye ukumbi wa TGNP Mtandao Mabibo Jijini Dar es salaam. 

Mratibu wa Mradi wa Sauti ya Wanawake na Uongozi Tanzania, Shakila Mayumana amesema mradi huo utatekelezwa katika mikoa tisa ambayo ni Dar es salaam, Morogoro, Shinyanga, Mbeya, Dodoma, Kilimanjaro, Mtwara, Mara na Kigoma. "Tulichagua mikoa ambako TGNP inafanya kazi zake, lakini pia kwenye maeneo yenye vuguvugu na yale yaliyosahaulika.Na hii inatokana na masuala tunayofanyia kazi ikiwemo sekta ya maji, afya, elimu, kilimo na uziduaji 'mafuta, gesi na madini' na Ukatili wa Kijinsia", alisema Mayumana. 

Aliwataja walengwa wakuu katika mradi huo kuwa ni watu binafsi, jamii, taasisi na vikundi vya wanawake na kubainisha kuwa pia makundi ya jamii ya wafugaji, wawindaji na wanaoishi kwa kula matunda, mizizi na asali pia yameongezwa kwenye mradi huo. Mayumana alitumia fursa hiyo kuitaka jamii kuachana na mila na desturi potofu zinazokandamiza haki za wanawake na kuwahamasisha wanawake kudai haki zao ikiwemo kujitokeza kugombea katika nafasi mbalimbali za uongozi. Kwa upande wake, Mwanachama wa TGNP Mtandao, Rehema Mwateba alisema mbegu ya mabadiliko inaanzia kwa mtu mmoja mmoja huku akiwasisitiza wanawake kusimamia ukweli katika kudai haki kwani ukweli siku zote unashinda.
Mratibu wa Mradi wa Sauti ya Mwanamke na Uongozi Tanzania,Shakila Mayumana akizungumza wakati wa kutambulisha mradi huo leo Septemba 28,2019 katika ukumbi wa TGNP Mtandao Mabibo Jijini Dar es salaam. Mradi huo utatekelezwa katika mikoa tisa nchini Tanzania. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mratibu wa Mradi wa Sauti ya Mwanamke na Uongozi Tanzania,Shakila Mayumana akitambulisha mradi huo kwa washiriki wa mradi waliohudhuria Tamasha la 14 la Jinsia 2019. Wanaharakati hao wa haki za wanawake wanatoka mikoa ya Dar es salaam,Morogoro,Shinyanga,Dodoma,Kilimanjaro,Mtwara,Mara na Kigoma.
Mratibu wa Mradi wa Sauti ya Mwanamke na Uongozi Tanzania,Shakila Mayumana akielezea malengo ya mradi huo.Alisema lengo la mradi ni kujenga uwezo kwa wanawake wa Tanzania,vikundi na Taasisi za kutetea haki za wanawake ili kuwezesha wanawake na wasichana na kuongeza ulinzi wa haki za wanawake na wasichana kufikia usawa wa kijisia. 
Mratibu wa Mradi wa Sauti ya Mwanamke na Uongozi Tanzania,Shakila Mayumana akizungumza wakati wa kutambulisha mradi huo.
Wanaharakati wa haki za wanawake wakiandika dondoo muhimu wakati wa kutambulisha mradi wa Mradi wa Sauti ya Mwanamke na Uongozi Tanzania.
Kulia ni Mwanaharakati wa haki za wanawake na watoto mkoani Mbeya Flora Mlowezi akichangia hoja wakati wa kutambulisha mradi wa wa Sauti ya Mwanamke na Uongozi Tanzania. 
Mwanachama wa TGNP Mtandao,Rehema Mwateba akichangia hoja wakati wa kutambulisha mradi wa Sauti ya Mwanamke na Uongozi Tanzania. 
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Same mkoani Kilimanjaro,Abdulrahman Mfuru akiwasisitiza wanawake kuomba mikopo inayotolewa kwenye halmashauri ili wainuke kiuchumi.
Wanaharakati wa haki za wanawake wakiwa ukumbini wakati wa kutambulisha mradi wa Sauti ya Mwanamke na Uongozi Tanzania. 
Wanaharakati wa haki za wanawake wakiwa ukumbini wakati wa kutambulisha mradi wa Sauti ya Mwanamke na Uongozi Tanzania. 
Wanaharakati wa haki za wanawake wakiandika dondoo muhimu wakati wa kutambulisha mradi wa Sauti ya Mwanamke na Uongozi Tanzania.
Wanaharakati wa haki za wanawake wakiwa ukumbini. 
Wanaharakati wa haki za wanawake wakiwa ukumbini. 
Wanaharakati wa haki za wanawake wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mradi wa wa Sauti ya Mwanamke na Uongozi Tanzania kutambulishwa leo Septemba 28,2019 katika ukumbi wa TGNP Mtandao Mabibo jijini Dar es salaam.
Wanaharakati wa haki za wanawake wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mradi wa wa Sauti ya Mwanamke na Uongozi Tanzania kutambulishwa leo Septemba 28,2019 katika ukumbi wa TGNP Mtandao Mabibo jijini Dar es salaam.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

DANGOTE APEWA WIKI MOJA KUWASILISHA RIPOTI YA UTENDAJI TIC

KITUO CHA UCHENJUAJI DHAHABU JEMA AFRIKA CHAPEWA ONYO LA MWISHO

$
0
0
Waziri wa Madini Doto Biteko (wa pili kulia), Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainabu Taleck ( katikati), Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (wa kwanza kulia) na Afisa Madini Mkoa wa Kimadini Kahama, Mhandisi Joseph Kumburu wakiangalia baadhi ya Kaboni inayochenjuliwa katika Kituo cha Kuchenjua Dhahabu cha Jema Afrika.
Afisa Madini Mkoa wa Kimadini Kahama, Mhandisi Joseph Kumburu akizungumza jambo wakati wa ziara ya Waziri wa Madini Doto Biteko katika kituo cha Kuchenjua Dhahabu cha Jema Afrika. Wengine wanaosikiliza ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainabu Tacleck na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo .
Waziri wa Madini Doto Biteko, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainabu Taleck, Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko wakiteta jambo na Kamati ya Ulinzi na Usalama mara baada ya kukitembelea Kituo Kidogo cha Ununuzi wa Dhahabu Mwime.
Kamishna wa Madini Mhandisi David Mulabwa ( kushoto) na Watalaam kutoka Tume ya Madini wakifuatilia jambo wakati wa kikao cha ndani baina ya ujumbe wa Wizara na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Shinyanga.
Waziri wa Madini Doto Biteko akizungumza jambo wakati wa kikao cha ndani kabla ya kuanza ziara. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainabu Taleck.

……………………………..

Na Asteria Muhozya, Kahama

Waziri wa Madini Doto Biteko ametoa Onyo la Mwisho la Kukifungia Kituo cha Uchenjuaji Dhahabu cha Jema Afrika kilichopo Wilayani Kahama.

Hatua hiyo inafuatia kubainika kwa jaribio la wizi wa dhahabu uliofanywa na baadhi ya wafanyakazi wa kituo hicho kutaka kuiba dhahabu ya mteja.

Akizungumzia tukio hilo, Waziri Biteko amewataka wamiliki wa kituo hicho kuandika barua ya kuweka makubaliano na Serikali ya kutojirudia tena kwa vitendo vya wizi kituoni hapo.

‘’Ni jicho la huruma tu tukiwapeleka mahakamani mali zenu zitataifishwa. Tunajua mmewekeza mitaji yenu na mna mikopo. Nilishamwambia mmiliki kuwa kituo chako kina rekodi ya wizi. Rais anawapenda, anawapigania ili watanzania wamiliki uchumi wa madini lakini mnamuangusha kwa kutofuata taratibu,’’ amesisitiza Waziri Biteko.

Amewatahadharisha wamiliki wa vituo vya uchenjuaji nchini kuhusu wizi wote wa dhahabu unaofanyika na kuwasisitiza kwamba, unafahamika na kuwataka wote wanaojihusisha na vitendo hivyo kujiepusha na kwa wale wasiotaka kufanya kazi zao kwa uaminifu watafute biashara nyingine.

Mbali na kutembelea kituo hicho, pia, Waziri Biteko na ujumbe wake wametembelea Kituo Kidogo cha Ununuzi wa dhahabu kilichopo katika eneo la Wachimbaji wadogo wa Mwime ambapo amewapongeza kwa kufuata taratibu na Sheria na kuwataka kufanya kazi zao kwa amani.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Taleck amesema Mkoa huo unahitaji wawekezaji lakini walio waaminifu.Ameongeza kuwa, wizi na udanganyifu katika kiwand cha uchenjuaji Jema Afrika ulibainiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama na kutumia fursa hiyo kuwatahadharisha wote wasiofuata taratibu kuwa serikali inawaona na itawafikia.

Katika ziara hiyo, Waziri Biteko pia ameongozana na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Shinyanga, Kamishna wa Madini Mhandisi David Mulabwa na Watalaam kutoka Tume ya Madini.

Aidha, ziara hiyo imefanywa wakati ambapo wizara na wadau wengine wa madini wanashiriki Maonesho ya Pili ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini Mkoani Geita yanayotarajiwa kuhitimishwa Septemba 29, 2019.Ziara hiyo imefanyika Septemba 28, 2019

Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Afunga Tamasha la JAMAFEST

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akisisitiza jambo kwa washiriki wa Tamasha la Utamaduni wa nchi za Afrika Mashariki kabla ya kulifunga tamasha hilo hii leo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Picha na WHUSM –Dar es Salaam
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd (katikati) akiwasili katika Tamasha la maonesho ya utamaduni wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ajili ya kufunga tamasha hilo lilofanyika kwa siku nane katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe.
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akifurahia jambo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (katikati) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Aloyce Nzuki wakati Makamu wa Rais alipotembelea banda lawizara hiyo kwa ajili ya kufunga Tamasha la maonesho ya utamaduni wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki lilofanyika kwa siku nane katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akiangalia picha mbalimbali za kumbukumbu katika banda la Maliasili na Utalii kabla ya kufunga Tamasha la maonesho ya utamaduni wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki lilofanyika kwa siku nane katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akimkabidhi cheti Mwenyekiti wa Kitaifa wa Kamati ya Tamasha la Utamaduni wa nchi za Afrika Mashariki wakati wa kufunga tamasha hilo lilofanyika kwa siku nane katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akimkabidhi cheti Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Kiagho Kilonzo wakati wa kufunga Tamasha la Utamaduni wa nchi za Afrika Mashariki lilofanyika kwa siku nane katika uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam.
Msanii Mrisho Mpoto (mwenye nguo nyeusi) akitoa burudani na kikundi chake wakati wa kufunga Tamasha la maonesho ya utamaduni wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki lilofanyika kwa siku nane katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Dkt.Kalemani atoa Mwezi mmoja nguzo za umeme zilizohifadhiwa zisambazwe

$
0
0
Na Zuena Msuya , Singida
Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani amewagiza mameneja wa Shirika la Umeme Nchini(TANESCO)wote nchini kuwa katika kipindi cha mwezi mmoja wanasambaza kwa wateja  nguzo zote za akiba zilizohifadhiwa katika vituo na maeneo mbalimbali nchini.
Kalemani alisema hayo, Septemba 28,2019, baada ya kuona nguzo zaidi ya Elfu mbili zikiwa zimehifadhiwa katika kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Singida, wakati wa ziara yake ya  kukagua ujenzi upanuzi wa kituo hicho kinachojengewa uwezo wa kupoza na kusambaza umeme wa Kilovolti(kV) 400.
Dkt.Kalemani, alisema kuwa hapendezwi kuona wateja wanalalamikia suala la ukosefu wa nguzo na kushidwa kuunganishiwa umeme katika maeneo mbalimbali wakati kuna nguzo zimerundwika mahali kwa ajili ya matumizi ya akiba.
"Wananchi wanahitaji nguzo kila siku,mnawaambia hakuna nguzo, ajabu nguzo kama hizi zimehifadhiwa sehemu mbalimbali mnadai ni za matumizi ya akiba,sasa akiba ya nini wakati wananchi bado wanauhitaji , pia maeneo  mengi nguzo zimeharibika zinataka kubasilishwa, nawapa Mwezi mmoja zisionekane hapa na maeneo mengine yote!", Alisema Dkt.Kalemani. 
Katika hatua nyingine, alimtaka mkandarasi wa Kampuni ya KC International LTD inayotekeleza ujenzi wa upanuzi wa Kituo cha Kupoza na kusambaza umeme cha Singida kuongeza nguvu kazi ili kuharakisha ujenzi wa kituo hicho ambao unatarajiwa kukamilika mwezi Januari 2020.
Kazi ya ujenzi katika hatua ya awali katika kituo hicho imekamilika na kufikia 95% ambapo pia  tayari wamekamilisha baadhi ya maeneo zitakaposimikwa transofoma kubwa nne ambapo mbili kati ya hizo zitakuwa na uwezo wa 125 MVA kwa kila moja na mbili nyingine zitakuwa na uwezi wa 250 MVA kila moja, pia kazi ya kukamilisha ujenzi wa jengo la kuendeshea mitambo inaendelea .
Mradi huo ukikamilika utakuwa na uwezo wa kuzalisha umeme wa Megawat(MW) 432 ambapo kwa sasa mahitaji ya umeme kwa Mkoa wa Singida ni MW 15 tu, hivyo kituo hicho kitaimarisha upatikanaji wa Umeme wakutosha na wauhakika katika Mkoa huo na mikoa iliyo karibu.
Kituo cha Kupoza na kusambaza umeme cha Singida ndiyo kitakuwa kituo kikubwa na pia  njia panda kubwa ya kusambaza umeme kwenda katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa kupitia Mkoa wa Shinyanga, Kanda ya Kaskazini kupitia Babati Mkoani Manyara, hadi Namanga Mkoani Arusha na baadaye Nchini Kenya.
Gharama za upanuzi wa kituo hicho ni Dola za Kimarekani milioni 60 sawa na Bilioni 130 za Kitanzania, fedha hizo ni mkopo kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika(AfDB), Shirika la Maendeleo la Japan(JICA) pamoja na Fedha za ndani.
 Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani(kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt.Rehema Nchimbi (kushoto) wakibadilishana mawazo baada ya Waziri wa Nishati, kuwasili mkoani humo kwa ziara ya kikazi ya siku moj
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani(kushoto) akipata maelezo ya namna kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Singida, kinavyofanya kazi, kutoka kwa  Meneja wa kituo hicho, Mha. Malili Mipawa(kulia).
 Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani, akikagua eneo itakaposimikwa moja ya transifoma katika kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Singida.
 Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani, akitoa maelezo kwa Mkandarasi na wasimamizi  katika Ujenzi wa upanuzi wa Kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Singida, baada ya kukagua shughuli za ujenzi zinazoendelea katika kituo hicho.
 Mafundi wakiendelea na kazi ya ujenzi wa upanuzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Singida, wakati  Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani, alipofanya ziara ya kukagua shughuli za ujenzi katika kituo hicho.
Moja ya Transifoma kubwa ikiwa imesimikwa katika kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Singida kwa lengo kukiongezea uwezo kituo hicho hadi kufikia kV 400.

Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani( katikati) akikagua nguzo zilizo hifadhiwa katika kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Singida

TAMASHA LA JAMAFEST LAMALIZIKA KWA MAFANIKIO

$
0
0

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Balozi Seif Ali Iddi akitoa hotuba ya kufunga rasmi Tamasha la Nne la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST ) lililofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 21 hadi 28 Septemba 2019. Tamasha hilo la aina yake lilizishirikisha nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwemo Burundi, Rwanda, Kenya, Uganda na Tanzania. Wakati wa Tamasha hilo vikundi mbalimbali vya sanaa na utamaduni kutoka nchi hizo vilishiriki. Katika hotuba yake Mhe. Balozi Iddi alitoa rai wadau wa sanaa na utamaduni kujikita kwenye ubunifu kwa ajili ya kukuza uchumi kupitia sanaa. Tamasha la JAMAFEST ambalo hufanyika kila baada ya miaka miwili limepangwa kufanyika mwaka 2021 nchini Burundi
Mhe. Balozi Iddi akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Bw. Christopher Bazivamo alipowasili kwenye Tamasha la JAMAFEST
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Eliabi Chodota akifuatilia hotuba ya Mhe. Balozi Iddi (hayupo pichani)

Sehemu ya wageni waalikwa wakiwemo viongozi wa dini wakiwa kwenye sherehe za ufungaji wa Tamasha la JAMAFEST
Sehemu nyingine ya wageni waalikwa

Mhe. Balozi Seif Ali Iddi akipata maelezo kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki kuhusu Banda la Maonesho la Wizara hiyo  alipotembelea mabanda mbalimbali ya maonesho yaliyofanyika wakati wa Tamasha la JAMAFEST
Mhe. Balozi Iddi akipata maelezo kwenye Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii
Mhe. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akimsikiliza mmoja wa washiriki wa maonesho alipotembelea Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii
Mhe. Balozi Iddi akiwa kwenye banda la Zanzibar
Mhe. Balozi Iddi akiwa kwenye Banda la Rwanda

 
Mhe. Balozi Iddi akiwa kwenye banda la Burundi

Mhe. Balozi Iddi akiwa kwenye banda la Uganda

Msanii Mrisho Mpoto akitumbuiza wakati wa sherehe za kuhitimisha Tamasha la JAMAFEST
Wasanii kwenye JAMAFEST

Watoto kutoka Dodoma wakitumbuiza

DKT. MWANJELWA ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA UJENZI WA JENGO LA KITUO CHA KUMBUKUMBU NA NYARAKA ZA TAIFA JIJINI MWANZA

$
0
0
 Meneja wa Wakala wa Majengo Tanzania, Mkoa wa Mwanza, Bw. Victor Baltazar akitoa ufafanuzi wa michoro ya ramani ya Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Kanda ya Ziwa jijini Mwanza kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua ujenzi wa kituo hicho.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (katikati) akielekeza jambo kwa Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Firimin Msiangi (kushoto) wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Kanda ya Ziwa jijini Mwanza leo. Kulia ni Meneja wa Wakala wa Majengo Tanzania, Mkoa wa Mwanza, Bw. Victor Baltazar.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Firmin Msiangi wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Kanda ya Ziwa jijini Mwanza leo.
  Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Firimin Msiangi akiwasilisha taarifa ya utekelezaji ya ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Kanda ya Ziwa, wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) ya kukagua ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Kanda ya Ziwa jijini Mwanza leo.
Meneja wa Wakala wa Majengo Tanzania, Mkoa wa Mwanza, Bw. Victor Baltazar akisoma taarifa ya utekelezaji ya ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Kanda ya Ziwa jijini Mwanza wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) ya kukagua ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Kanda ya Ziwa jijini Mwanza leo. Wengine ni watumishi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa (hawapo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Kanda ya Ziwa jijini Mwanza leo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Firimin Msiangi.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua ujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Kanda ya Ziwa jijini Mwanza leo.

Wenye viwanda nchini waagizwa kulipa tozo na ada katika mabonde-Profesa Mkumbo

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Serikali imesema kuwa vyazo vya maji vinatakiwa kulindwa kwa wenye viwanda wanatakiwa kulipa tozo zilizoaininishwa kisheria kutokana na wenye viwanda kutumia kiasi kikubwa cha maji.

Hayo ameyasema Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo wakati alipokutana na wenye viwanda katika Ofisi ya Bonde la Wami/Ruvu  jijini Dar es Salaam, amesema kuwa watamshauri Waziri Mwenye dhamana kuwa kuwepo kwa tozo moja kwa wenye viwanda nchini kulipa katika mabonde.

Amesema kuwa mabonde Tisa nchini ndio wana mamlaka ya kuchukua tozo wa ajili ya kuhifadhi maji kwani kuwepo kwa hayo maji inatokana na mabonde hayo kulinda vyanzo vya maji.

“Mabonde haya yanahitaji kugharamia vyazo kwa maji hivyo wenye viwanda wasipolipa shughuli za mabonde hazitafanywa katika ufanisi wa kulinda maji hayo wanayoyatumia katika uendeshaji wa viwanda vyao”amesema Profesa Kitila Mkumbo.

Amesema kuwa mahitaji ya maji ni ya kila siku na kuna watu wanafanya kazi ya kuangalia katika vyazo vyake na kisha watu kuyatumia kutokana na kusimamiwa na hayo mabonde.

Nae Mwakilishi wa Wamiliki wa Wenye Viwanda nchini (CTI) Hussein Sufiani amesema kama wenye viwanda wamekubali kulipa tozo na ada.
 Katibu wa Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanya mazungumzo na wamiliki wa Wenye Viwanda (CTI) kuhusiana na ulipaji wa tozo za maji katika mabonde katika mkutano ulifanyika katika ofisi za Bonde la Wami/Ruvu jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi  wamiliki wa Wenye Viwanda (CTI) Hussein Sufiani akizungumza kuhusiana na majadiliano kwa wenye viwanda katika ulipaji wa tozo na ada katika mkutano ulifanyika katika ofisi za Bonde la Wami/Ruvu jijini Dar es Salaam. 

Serikali yavunja Mkataba na Mkandarasi Ujenzi wa Jengo la Polisi Manyara

$
0
0
Serikali imewahakikishia wananchi wa Mkoa wa Manyara kuanza na kumalizika kwa Mradi  Ujenzi wa Ofisi ya Makao Makuu ya Jeshi la Polisi  ambao ulisimama tangu mwaka 2012 kutokana na gharama kubwa ya ukandarasi na sasa utajengwa kwa kutumia utaratibu mpya wa serikali wa nguvu mali ambao utapunguza gharama za ujenzi kulinganisha na kutumia mkandarasi

 Hayo yamesemwa leo  na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni alipotembelea mradi huo uliopo katika eneo la Komoto Kata ya Bagara Wilayani Babati Mkoani Manyara ambao gharama za awali za mradi huo ni  Milioni Mia Tano Themanini na Moja,Laki tatu na Thelathini.

“Serikali tunawahakikishia wananchi wa Mkoa wa Manyara kujengwa kwa jingo la polisi ili masuala ya ulinzi na usalama yaweze kuwa imara katika mkoa huu,tayari timu maalumu kutoka makao makuu ya polisi ilishafika hapa na kuona jinsi mradi huu utakavyoweza kuendelea baada ya kusimama kwa takribani miaka saba sasa,” alisema Naibu Waziri Masauni

“.... juhudi mbalimbali zishaanza na hivi navyozungumza tayari Jeshi la polisi mkoani hapa likishirikiana na wadau wameshafanya harambee na kufanikiwa  kukusanya  takribani  kiasi cha Shilingi Milioni Arobaini na Tano na sisi kama Wizara tutachangia ujenzi huo” aliongeza Masauni

Akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea eneo la mradi Mbunge wa Babati Mjini Pauline Gekul alisema Jeshi la Polisi linafanya kazi katika mazingira madogo,ofisi ni ndogo hali inayopelekea huduma kutolewa kwa uchache tofauti na mahitaji

“Nashukuru kuona serikali leo imefika kuona maendeleo ya huu mradi kwa kweli polisi wanahitaji jingo jipya ili kazi ya kulinda amani na utulivu iwe rahisi kwao,tunashukuru pia wadau mbalimbali wameanza kutuunga mkono ikiwa pia na ujenzi wa nyumba kwa ajili ya makazi ya askari wetu” alisema Mbunge  Gekul

Awali akitoa taarifa ya Uhalifu Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara,Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Cyprian Mushi alikiri kupungua  kwa uhalifu huku akikiri kuwepo changamoto katika kutatua baadhi ya kesi za ubakaji baada ya familia za mtuhumiwa na familia ya mtuhumu kutotokea mahakamani baada ya kuzimaliza kesi hizo kifamilia.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (meza kuu) akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Manyara baada ya kuwasili leo kwa ziara ya kikazi huku akitoa taarifa ya Serikali kuvunja Mkataba na Mkandarasi wa Ujenzi wa Jengo la Ofisi la  Polisi mkoani hapo lengo ni kuepuka gharama za ujenzi huo.Wa kwanza kulia ni Mbunge wa Babati Mjini,Pauline Gekul.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara,Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Cyprian Mushi akizungumza mbele ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (meza kuu),wakati wa ziara ya Ukaguzi wa Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Ofis za Polisi mkoani hapo. .Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (meza kuu) akisalimiana na Maafisa wa Jeshi la Polisi  baada ya kuwasili leo kwa ziara ya kikazi huku akitoa taarifa ya Serikali kuvunja Mkataba na Mkandarasi wa Ujenzi wa Jengo la Ofisi la  Polisi mkoani Manyara  lengo ni kuepuka gharama za ujenzi huo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul akiongozana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kushoto),baada ya kumaliza Kikao na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Manyara juu ya Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Jeshi la Polisi mkoani hapo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

WAZIRI KAIRUKI AFANYA ZIARA KATIKA KIWANDA CHA KUTENGENEZA UNGA WA MHOGO-CSTC LINDI

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula wakisalimiana na uongozi wa kiwanda cha kutengeneza unga wa muhogo cha (CSTC) walipotembelea kiwandani hapo kwa lengo la kukagua mazingira ya kiwanda hicho, ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake mkoani Lindi ili kusikiliza na kutatucha changamoto za wawekezaji.
 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula akijibu hoja za masuala ya ardhi kwa watendaji wa kiwanda cha kutengeneza unga wa muhogo cha (CSTC) kilichopo Wilaya ya Lindi Vijijini alipotembea mwishoni mwa wiki.
 Kaimu Meneja uzalishaji wa kiwanda cha kutengeneza unga wa muhogo cha CSTC Bw. Jean Smile akitoa maelezo kuhusu mitambo ya kuchakata mihogo katika kiwanda hicho kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki (kushoto kake) pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula (kulia kwake) kilichopo Lindi alipotembelea kiwandani hapo
 Kaimu Meneja uzalishaji wa kiwanda cha kutengeneza unga wa muhogo cha CSTC Bw. Jean Smile  akitoa maelezo kuhusu mitambo ya kuchakata mihogo inayotumika katika kiwanda cha CSTC kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula kilichopo Lindi Vijijini alipotembelea kiwandani hapo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula (mwenye kofia) wakiangalia moja ya mfuko wa unga wa muhogo uliotengenezwa na kiwanda hicho.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki akiuliza swali kwa Kaimu Meneja uzalishaji wa kiwanda cha kutengeneza unga wa muhogo cha CSTC Bw. Jean Smile (wa kwanza kushoto mwenye kofia) wakati wa ziara yake kiwandani hapo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula (mwenye kofia) na Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe Shaibu Ndemanga (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na uongozi na watumishi wa kiuwanda cha kutengeneza unga wa muhogo kilichopo Lindi.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

DKT. SALIM ATUNUKIWA NISHANI YA JUU YA URAFIKI YA JAMHURI YA WATU WA CHINA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mheshimiwa Xi Jinping, leo asubuhi tarehe 29 Septemba 2019 amemtunukia Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa. Dk. Salim Ahmed Salim, Nishani ya Juu ya Urafiki ya Jamhuri ya Watu wa China ikiwa ni sehemu ya matukio ya maadhimisho ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China iliyofanyika jijini Beijing.  Mheshimiwa Dkt. Salim anakuwa mwafrika wa kwanza kupewa heshima na tuzo hiyo ya juu katika historia ya China.

Nishani hiyo ilipokelewa na Bi. Maryam Salim, Binti ya Dk. Salim Ahmed Salim ambaye pia ni Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Albania kwa niaba ya Baba yake kutokana na kushindwa kuhudhuria kwa sababu za kiafya. Katika tukio hilo, Serikali ya Tanzania iliwakilisha na Balozi wa Tanzania nchini China Mheshimiwa Mbelwa Kairuki.


Hafla hiyo kubwa ya kitaifa ya kukabidhi nishani ilihudhuriwa na viongozi waandamizi wa Chama na Serikali ya China akiwemo Makamu wa Rais Mheshimiwa Wang Qishan, Waziri Mkuu Mheshimiwa Li Keqiang, Spika wa Bunge Mheshimiwa Li Zhanshu na Wajumbe wote wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Baraza la Taifa.


Mbali na Dk.Salim,  wengine waliotunukiwa Nishani ya Urafiki ni pamoja na Kiongozi wa Chama cha Kikoministi cha Cuba Jenerali Raul Castro, Dada wa Mfalme wa Thailand Maha Chakri Sirindhorn, Kiongozi wa Jumuiya ya Urafiki ya China na Urusi Ndugu Galina Kulikova, Waziri Mkuu Mstaafu wa Ufaransa Jean-Pierre Raffarin na Bi  Isabel Crook  kutoka Canada.


Vilevile  Rais Xi alitoa Nishani  ya Jamhuri na Nishani ya Heshima ya Taifa kwa raia 36 wa China kwa kutambua mchango wao mkubwa katika maendeleo ya Taifa la China kupitia kazi zao katika fani mbalimbali.


Nishani ya Juu ya Urafiki ya Taifa la China imetolewa kwa Dkt. Salim  kutokana na mchango wake wa kuiwezesha Jamhuri ya Watu wa China kuwa Mwanachama wa Umoja wa Mataifa mwaka 1971 alipokuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.  Aidha, mchango wa Dk. Salim katika kuimarisha mahusiano kati ya China na Tanzania wakati aliposhikilia nyadhifa mbalimbali umetajwa kama sababu ya kutunukiwa Nishani hiyo. Vilevile, mchango wa Dk.Salim katika kujenga mahusiano kati ya China na Afrika akiwa na nafasi ya Katibu Mkuu wa OAU umetajwa kuwa sababu nyingine ya kutunukiwa Nishani.


Tukio la Kutoa Nishani limetangazwa moja kwa moja na Televisheni zote za Jamhuri ya Watu wa China na kushuhudiwa na watu zaidi ya Milioni 500.


Kwa mujibu wa maelezo ya Balozi wa Tanzania nchini China Ndugu Mbelwa Kairuki Kupitia tukio la leo, mamilioni ya Wachina hususan vijana wamepata fursa ya kufahamu nafasi na mchango wa Tanzania na Bara la Afrika katika historia ya taifa lao. Aidha, tukio la leo limeifanya Tanzania kufahamika kwa watu wengi zaidi nchini China kupitia tukio mara moja. Hatua hiyo itaamsha udadisi na hamasa miongoni mwa Wachina wengi wa kizazi kipya kutaka kuifahamu zaidi Tanzania. Hali hii yaweza kujitafsiri katika fursa kubwa ya kukua kwa utalii, biashara na wawekezaji ikizingatiwa kuwa  wananchi wa China hutoa mwitikio mkubwa kwa nchi ambazo husemwa vizuri na kuthaminiwa na Serikali yao.


Aidha Balozi Kairuki ameeleza kwamba maadhimisho ya miaka 70 ya Jamhuri ya Watu wa China mwaka huu yanaambatana na maadhimisho ya miaka 55 ya urafiki na udugu kati ya China na Tanzania kufuatia kuanzishwa kwa mahusiano rasmi ya kidiplomasia mwaka 1964. Uhusiano wa China na Tanzania uliotokana na uhusiano mzuri wa waasisi wa mataifa haya mawili, Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Mao Tsetung. Uhusiano huo umeendelezwa na viongozi wa pande zote mbili ambao umekuwa ukiimarika siku hadi siku. Uhusiano huu umekwenda mbali zaidi ya uhusiano kati ya Serikali na Serikali na kushamiri kwa uhusiano wa watu kwa watu.


Ni kwasababu hiyo, katika maadhimisho ya miaka 70 ya Taifa la China, Jumuiya ya Urafiki wa watu wa China na Tanzania ni miongoni mwa Jumuiya za mataifa 17 yenye urafiki wa majira yote na China walioalikwa  kushiriki kwenye maadhimisho hayo na tarehe 1 Oktoba 2019 watakuwa na gwaride lao maalum. Katika jumuiya hizo 17, Kutoka Barani Afrika ni Tanzania na Zambia ndio watahudhuria.


Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,


Bi. Maryam Salim akiwa katika picha na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Xi Jinping na picha ya chini akiwa na Balozi wa Tanzania nchini China, Mhe. Mbelwa Kairuki mara baada ya kupokea nishani.

TIMU YA MAOFISA WAKUU WAANDAMIZI WA JESHI LA POLISI NA MAKAMANDA WA MIKOA NA VIKOSI KUTEMBELEA MRADI MKUBWA WA KUZALISHA UMEME KATIKA MTO RUFIJI

$
0
0
 Mhandisi Steven Manda akiwatembeza sehemu mbalimbali  Maofisa wakuu waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Mikoa na Vikosi walipotembelea mradi mkubwa wa kuzalisha umeme katika Mto Rufiji mkoani Pwani baada ya kufanya ziara ya siku moja katika mradi huo.(PICHA NA JESHI LA POLISI)
 Kamishna wa Polisi Zanzibar Cp Mohamed H. Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa Wakuu waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Mikoa na Vikosi baada ya kutembelea mradi mkubwa wa kuzalisha umeme katika mto Rufiji mkoani Pwani.
Wa kwanza kulia ni Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Mohamed H. Hassan, akiongoza Maofisa Wakuu waandamizi wa Jeshi la Polisi na Makamanda wa Mikoa na Vikosi kutembelea mradi mkubwa wa kuzalisha umeme katika mto rufiji.(PICHA NA JESHI LA POLISI)

TUSIKWEPE JUKUMU LA KUWATUNZA WAZEE-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka vijana na jamii kwa ujumla wasikwepe jukumu la kuwatunza wazee kwa sababu nguvu zao za uzalishaji mali zimepungua kutokana na kazi waliyoifanya wakiwa vijana kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa familia zao na Taifa kwa ujumla.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema Serikali inaendelea kutekeleza Mkakati wa Kitaifa wa Kutokomeza Mauaji ya Wazee uliozinduliwa Januari, 2019 ili kwa kutokomeza ukatili kwa wazee ifikapo 2023 na kuhakikisha wazee na watu wenye ulemavu wanatambuliwa na kulindwa dhidi ya ubaguzi, uonevu, ukatili na mila potofu.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumapili, Septemba 29, 2019) wakati akizindua kambi ya utoaji wa huduma za afya kwa wazee na watu wenye ulemavu katika viwanja vya Kichanganimjini Iringa. Kambi hiyo imeandaliwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Dkt. Ritta Kabati katika kuadhimisha siku ya Wazee Duniani.

Amesema wajibu wa kuwahudumia au kuwasaidia wazee na watu wenye ulemavu ni wa kila mmoja na wanapaswa watambue kwamba wazee hao wamelitumikia Taifa kwa muda mrefu tena kwa namna mbalimbali ikiwemo kuwaletea na kuhakikisha wanapata mafanikio hayo ambayo wanajivunia sasa.

“Kwa msingi huo, tunao wajibu wa kuwajali wazee wetu kwa hali na mali ikiwa ni sehemu ya matunda ya uwajibikaji wao kwetu na kwa Taifa kwa ujumla. Hivyo basi, tutumie vema Kambi hii kuwasaidia wazee wetu na watu wenye ulemavu kwa kutambua afya zao na kuwapatia matibabu ya kiafaya ili waendelee kuwa salama na wenye furaha nasi tuvune busara zao.”

Kutokana na umuhimu wa kuwatunza wazee na kuwasaidia watu wenye ulemavu, Waziri Mkuu ametoa rai kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa, wananchi na wadau mbalimbali kuendelea kuimarisha upatikanaji wa fursa, haki na ustawi wa wazee ikiwemo kuondokana kabisa na vitendo vya ukatili dhidi yao.

“Vituo vyote vya kutoa huduma za afya vya umma kutoa huduma bora na za haraka kwa wazee wetu wenye vitambulisho. Tengeni dirisha maalumu kwa ajili ya kuwahudumia ili wasikae kwenye foleni muda mrefu. Serikali itaendelea kuweka miundombinu na mazingira rafiki ili kuwawezesha kupata mahitaji yao.”

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kusimamia maelekezo yake kwa Halmashauri zote nchini kuwatambua wazee wasiojiweza na kuwapatia vitambulisho vya matibabu bila malipo. “Namshukuru Mbunge wa Viti Maalum Ritha Kabati amebainisha mafanikio yanayoendelea kupatikana kutokana na utekelezaji wa agizo hilo.

“Haidhuru nasi tukiiga mfano wa Mheshimiwa Ritta Kabati, Mbunge wa Viti Maalumu na kaka yangu Mheshimiwa Pinda, Waziri Mkuu Mstaafu kwa moyo wao wa kizalendo kabisa kuona kuna haja ya kusaidia na kuunga mkono juhudi za Rais wetu mpendwa Dkt. John Magufuli za kuwahudumia wanyonge.”

Hata hivyo, Waziri Mkuu ameendelea kuziagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha zoezi hilo linakuwa endelevu kwa kuwatambua na kuwapatia vitambulisho wazee wote nchini wasio na uwezo ili waweze kunufaika na huduma ya matibabu bila malipo pamoja na huduma zingine za kijamii.

Vilevile, Waziri Mkuu amesema kwa kuwa Novemba 2019 nchi inatarajia kufanya uchaguzi wa Serikali za Mitaa, wazee kama sehemu ya jamii wana haki ya kushiriki katika uchaguzi huo kwa kuchagua viongozi wanaoona watafaa kuwaongoza na wao kuchaguliwa kuongoza katika nafasi mbalimbali. Hivyo wasaidiwe kushiriki zoezi hilo.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu Mstaafu na Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa, Peter Pinda alimpongeza Dkt. Ritta kwa uamuzi wake wa kuandaa kambi hiyo ambayo itatoa fursa kwa wazee kupima afya zao na kupatiwa huduma pamoja na kutoa viungo bandia kwa baadhi ya walemavu.

“Uzee ni hali siyokwepeka upende usipende ila unaweza kucheleweshwa kutegemea na aina ya matunzo wanayopatiwa. Nashauri wazee wapate vyakula bora tena kwa uwiano sahihi, vyakula hivyo ni pamoja na vya jamii ya mizizi, mikunde, nafaka, mbogamboga na nyama ili waweze kuimarisha afya zao.”

Awali, Waziri Mkuu alipokea taariza za ujenzi wa jengo la Ustawi wa Jamii Manispaa ya Iringa lilojengwa kwa ufadhili wa Mkurugenzi wa Kundi la Makampuni ya Asas, Salim Abri kwa gharama ya sh. milioni 60.

Kwa upande wake,Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Iringa Tiniel Mmbaga alisema kukamilika kwa jengo hilo kutawawezesha kutoa huduma bora kwa jamii na kwa wakati kwani awali maafisa watano walikuwa wakilundikana katika chumba kimoja hali iliyosababisha wateja kushindwa kueleza matatizo yao baada ya kukosekana kwa usiri.

Alisema kwa siku wanashughulikia malalamiko yahusuyo masuala ya migogoro ya familia ikiwemo matunzo ya watoto kuanzia 15 hadi 30 pamoja na wanawake zaidi ya 50 ambao kila mwezi wanakwenda kuchukua fedha kwa ajili ya matunzo ya watoto zinazotolewa na wenza wao kufuatia kuwepo kwa migogoro baina yao.

Shughuli hiyo, imehudhuriwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dkt. Augustine Mahiga, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- TAMISEMI Josephat Kandege, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na wenye UlemavuStela Ikupa pamoja na Maafisa wengine wa Serikali. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda wakati alipowasili kwenye uwanja wa Kichangni Kihesa mjini Iringa kuzindua Kambi ya Kutoa Huduma za Afya kwa Wazee na Walemavu, Septemba 29, 2019.  Wa pili kushoto ni Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa na wa pili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wazee wakati alipozindua  Kambi ya Kutoa Huduma za Afya kwa Wazee na Wenye Ulemavu kwenye Uwanja wa Kichangani Kihesa mjini Iringa, Septemba 29, 2019.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akislimiana na Bibi Costancia Alfred Mapunda   wakati alipozindua  Kambi ya Kutoa Huduma za Afya kwa Wazee na Wenye Ulemavu kwenye Uwanja wa Kichangani Kihesa mjini Iringa, Septemba 29, 2019.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakizungumza na wazee waliojitokeza kupata huduma za tiba na vipimo wakati Waziri Mkuu alipozindua  Kambi ya Kutoa Huduma za Afya kwa Wazee na Wenye Ulemavu kwenye Uwanja wa Kichangani Kihesa mjini Iringa, Septemba 29, 2019.
  Baadhi ya wazee wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati  alipozindua  Kambi ya Kutoa Huduma za Afya kwa Wazee na Wenye Ulemavu kwenye Uwanja wa Kichangani Kihesa mjini Iringa, Septemba 29, 2019.
 Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum, Ritta Kabati na baadhi ya viongozi wa CCM walioshiriki katika uzinduzi wa   Kambi ya Kutoa Huduma za Afya kwa Wazee na Wenye Ulemavu kwenye Uwanja wa Kichangani Kihesa mjini Iringa, Septemba 29, 2019
 Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Happi akizungumza wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipozindua  Kambi ya Kutoa Huduma za Afya kwa Wazee na Wenye Ulemavu kwenye Uwanja wa Kichangani Kihesa mjini Iringa, Septemba 29, 2019.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akimkabidhi Tuzo ya Shukurani, Mkurugenzi Mkuu wa Makmpuni ya ASAS, Salim Abri kutokana na mchango wake mkubwa katika huduma mbalimbali za jamii mkoani Iringa. Tuzo hiyo imetolewa na Halmashauri ya Mji wa Iringa.  Wa pili kushoto ni Waziri Mkuu Mstaafu na Mlezi wa CCM Mkoa wa Iringa, Mizengo Pinda, wa pili kulia ni Naibu Waziri Ofis ya Waziri Mkuu, Stella Ikupa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wazee wakati alipozindua  Kambi ya Kutoa Huduma za Afya kwa Wazee na Wenye Ulemavu kwenye Uwanja wa Kichangani Kihesa mjini Iringa, Septemba 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Wakazi wa Bukoba waipokea Elimu ya Mpiga Kura kuelekea Uboreshaji wa Daftari

$
0
0
 Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura ya Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) upande wa Habari  Daniel Kasokola (katikati ya wanafunzi) akieleza jambo kuhusu watu wenye ulemavu wakati Gari la Matangazo la NEC lilipotembelea Shule ya Sekondari ya Rugambwa iliyopo Manispaa ya Bukoba kutoa Elimu ya Mpiga Kura kuelekea Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa mkoa wa Kagera, Kigoma na Wilaya ya Chato unaoanza Oktoba 2 hadi Oktoba 8, 2019. 
 Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura ya Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) upande wa Habari  Daniel Kasokola (katikati) akifafanua nafasi ya watu wenye ulemavu katika Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura akiwa na baadhi ya wanafunzi wenye ulemavu wanaosoma Shule ya Sekondari ya Rugambwa ya Manispaa ya Bukoba.
 Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura ya Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) upande wa Habari  Daniel Kasokola (kulia mwenye fulana nyeusi) akifafanua jambo mbele ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Rugambwa ya Manispaa ya Bukoba.
 Afisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Yasinta Mlula akiwaeleza jambo wakazi wa Manispaa ya Bukoba wakati Gari la Matangazo la Tume lilipokuwa likitoa Elimu ya Mpiga Kura kwenye Stendi ya Mabasi ya Mjini Bukoba kuhusu Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
  Mkazi wa Manispaa ya Bukoba mwenye ulemavu akiwa na Afisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Ibrahim Dedu wakati Gari la Matangazo la Tume (halipo pichani) lilipokuwa likitoa Elimu ya Mpiga Kura kwenye Stendi ya Mabasi ya Mjini Bukoba kuhusu Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
 Afisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Christina Njovu akimweleza jambo mkazi wa Manispaa ya Bukoba mwenye ulemavu wakati Gari la Matangazo la Tume lilipokuwa likitoa Elimu ya Mpiga Kura kwenye Stendi ya Mabasi ya Mjini Bukoba kuhusu Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
 Gari la Matangazo la Tume ya Taifa ya Uchaguzi likipita karibu na Stendi ya Mabasi ya Mjini Bukoba kutoa Elimu ya Mpiga Kura ikiwa ni maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa mkoa wa Kagera, Kigoma na Wilaya ya Chato unaoanza Oktoba 2 hadi Oktoba 8, 2019.
 Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura ya Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) upande wa Habari  Daniel Kasokola akizungumza na wakazi wa Manispaa ya Bukoba wakati Gari la Matangazo la Tume lilipoweka kambi kwenye eneo la wazi katika Manispaa ya Bukoba kutoa Elimu ya Mpiga Kura.
 Afisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Monica Wabukundi, akiwasiliza vijana kwenye Stendi ya mabasi ya Mjini Bukoba wakati Gari la Matangazo la Tume lilipokuwa likitoa Elimu ya Mpiga Kura kwenye stendi hiyo kuhusu Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Afisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Moshi Makuka (mwenye fulana nyeupe karibu na Gari la Matangazo) akitoa Elimu ya Mpiga Kura kwenye moja ya mitaa ya Mjini Bukoba akiwa na Gari la Matangazo la Tume kuhamasisha wananchi kujitokeza kwenye kuhusu Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa mkoa wa Kagera, Kigoma na Wilaya ya Chato unaoanza Oktoba 2 hadi Oktoba 8, 2019. 

WAZIRI MKUU MSTAAFU DK. SALIM AHMED SALIM ATUNUKIWA NISHANI YA JUU YA URAFIKI YA JAMHURI YA WATU WA CHINA

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mheshimiwa Xi Jinping,  leo asubuhi tarehe 29 Septemba 2019 amemtunukia Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa. Dk. Salim Ahmed Salim, Nishani ya Juu ya Urafiki ya Jamhuri ya Watu wa China ikiwa ni sehemu ya matukio ya maadhimisho ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China iliyofanyika jijini Beijing.  Mheshimiwa Dkt. Salim anakuwa mwafrika wa kwanza kupewa heshima na tuzo hiyo ya juu katika historia ya China.

Nishani hiyo ilipokelewa na Bi. Maryam Salim, Binti ya Dk. Salim Ahmed Salim ambaye pia ni Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Albania kwa niaba ya Baba yake kutokana na kushindwa kuhudhuria kwa sababu za kiafya. Katika tukio hilo, Serikali ya Tanzania iliwakilisha na Balozi wa Tanzania nchini China Mheshimiwa Mbelwa Kairuki.

Hafla hiyo kubwa ya kitaifa ya kukabidhi nishani ilihudhuriwa na viongozi waandamizi wa Chama na Serikali ya China akiwemo Makamu wa Rais Mheshimiwa Wang Qishan, Waziri Mkuu Mheshimiwa Li Keqiang, Spika wa Bunge Mheshimiwa Li Zhanshu na Wajumbe wote wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Baraza la Taifa.

Mbali na Dk.Salim,  wengine waliotunukiwa Nishani ya Urafiki ni pamoja na Kiongozi wa Chama cha Kikoministi cha Cuba Jenerali Raul Castro, Dada wa Mfalme wa Thailand Maha Chakri Sirindhorn, Kiongozi wa Jumuiya ya Urafiki ya China na Urusi Ndugu Galina Kulikova, Waziri Mkuu Mstaafu wa Ufaransa Jean-Pierre Raffarin na Bi  Isabel Crook  kutoka Canada.

Vilevile  Rais Xi alitoa Nishani  ya Jamhuri na Nishani ya Heshima ya Taifa kwa raia 36 wa China kwa kutambua mchango wao mkubwa katika maendeleo ya Taifa la China kupitia kazi zao katika fani mbalimbali.

Nishani ya Juu ya Urafiki ya Taifa la China imetolewa kwa Dkt. Salim  kutokana na mchango wake wa kuiwezesha Jamhuri ya Watu wa China kuwa Mwanachama wa Umoja wa Mataifa mwaka 1971 alipokuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.  Aidha, mchango wa Dk. Salim katika kuimarisha mahusiano kati ya China na Tanzania wakati aliposhikilia nyadhifa mbalimbali umetajwa kama sababu ya kutunukiwa Nishani hiyo. Vilevile, mchango wa Dk.Salim katika kujenga mahusiano kati ya China na Afrika akiwa na nafasi ya Katibu Mkuu wa OAU umetajwa kuwa sababu nyingine ya kutunukiwa Nishani.

Tukio la Kutoa Nishani limetangazwa moja kwa moja na Televisheni zote za Jamhuri ya Watu wa China na kushuhudiwa na watu zaidi ya Milioni 500.

Kwa mujibu wa maelezo ya Balozi wa Tanzania nchini China Ndugu Mbelwa Kairuki Kupitia tukio la leo, mamilioni ya Wachina hususan vijana wamepata fursa ya kufahamu nafasi na mchango wa Tanzania na Bara la Afrika katika historia ya taifa lao. Aidha, tukio la leo limeifanya Tanzania kufahamika kwa watu wengi zaidi nchini China kupitia tukio mara moja. Hatua hiyo itaamsha udadisi na hamasa miongoni mwa Wachina wengi wa kizazi kipya kutaka kuifahamu zaidi Tanzania. Hali hii yaweza kujitafsiri katika fursa kubwa ya kukua kwa utalii, biashara na wawekezaji ikizingatiwa kuwa  wananchi wa China hutoa mwitikio mkubwa kwa nchi ambazo husemwa vizuri na kuthaminiwa na Serikali yao.

Aidha Balozi Kairuki ameeleza kwamba maadhimisho ya miaka 70 ya Jamhuri ya Watu wa China mwaka huu yanaambatana na maadhimisho ya miaka 55 ya urafiki na udugu kati ya China na Tanzania kufuatia kuanzishwa kwa mahusiano rasmi ya kidiplomasia mwaka 1964. Uhusiano wa China na Tanzania uliotokana na uhusiano mzuri wa waasisi wa mataifa haya mawili, Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Mao Tsetung. Uhusiano huo umeendelezwa na viongozi wa pande zote mbili ambao umekuwa ukiimarika siku hadi siku. Uhusiano huu umekwenda mbali zaidi ya uhusiano kati ya Serikali na Serikali na kushamiri kwa uhusiano wa watu kwa watu.

Ni kwasababu hiyo, katika maadhimisho ya miaka 70 ya Taifa la China, Jumuiya ya Urafiki wa watu wa China na Tanzania ni miongoni mwa Jumuiya za mataifa 17 yenye urafiki wa majira yote na China walioalikwa  kushiriki kwenye maadhimisho hayo na tarehe 1 Oktoba 2019 watakuwa na gwaride lao maalum. Katika jumuiya hizo 17,  Kutoka Barani Afrika ni Tanzania na Zambia ndio watahudhuria.

WANAWAKE WATAKIWA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA ILI KUTOA MCHANGO KATIKA MAENDELEO YA TAIFA

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akimkabidhi
kadi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mmoja wa wananchi aliyejiunga na
CCM akitokea chama cha upinzani.



Mkuu wa Wilaya ya Newala, Mhe. Aziza A. Mwangosongo akizungumza na
Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wilayani Newala wakati wa
Maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)
yaliyofanyika wilayani humo jana na kuwahimiza wananchi kufanya
maandalizi mapema ya kuwanunulia vifaa vya shule watoto waliohitimu
darasa la saba.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akizungumza
na wanachama wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) (hawapo
pichani) wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Wanawake
Tanzania (UWT) yaliyofanyika jana wilayani Newala.

Baadhi ya wanachama wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wilayani
Newala wakimsiliza Mgeni Rasmi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe.
George H. Mkuchika (Mb) wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Umoja wa
Wanawake Tanzania (UWT) yaliyofanyika wilayani humo jana.
*********************************

Na James K. Mwanamyoto, Newala

Wanawake nchini wametakiwa kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali katikauchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 24 Novemba,2019 kwani wana nafasi kubwa katika mchango wa maendeleo ya Taifa.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishiwa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) ambayealikuwa mgeni rasmi wa Maadhimisho ya Siku ya Umoja wa WanawakeTanzania (UWT) wilayani Newala.

Mhe. Mkuchika amewaasa wanawake nchini, kutotegemea nafasi za upendeleowalizotengewa na Serikali na badala yake wachukue fomu na kuingia katikakinyang’anyiro na wanaume kugombea nafasi zilizotangazwa kwa mujibu wakanuni zinazosimamia uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

“Serikali ya kijiji ndio inayozungumzia suala la maendeleo ya kijiji, hivyo kijijiambacho hakina zahanati, mjumbe mwanamke ni hodari wa kukumbusha ujenziwa zahanati kwani anatambua umuhimu wa zahanati”, amefafanua Mhe.Mkuchika.

Mhe. Mkuchika amesema Serikali inataka wanawake washiriki katika vikao vyaSerikali ya kijiji na mtaa ili wawe chachu ya mafanikio katika vijiji na mitaa, kwaniwananchi katika maeneo hayo wanahitaji kupata huduma bora toka Serikalini.

Mhe. Mkuchika ametoa hamasa kwa kina mama kuwa mstari wa mbele
kuwahimiza akina baba kutekeleza ahadi waliyoitoa ya kuchangia chakula chawatoto wa shule ili kuwawezesha watoto hao kusoma vizuri pasipo kukabiliwa nachangamoto ya njaa.

Aidha, Mhe. Mkuchika ametumia fursa hiyo kuwaeleza wananchi mafanikio yayaliyoletwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika sekta ya afya kwa kujengahospitali za wilaya nchini.

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufulitangu aingie madarakani amejenga hospitali nyingi za wilaya kuliko alizozikuta,kwani amedhamiria ndani ya utawala wake kila wilaya nchini iwe na hospitaliyake na ushahidi wa wazi uko katika Wilaya ya Newala ambayo imenufaika naujenzi wa kituo cha afya cha Mpunye na Kitangali”, amesema Mhe. Mkuchika.

Mhe. Mkuchika ameongeza kuwa, kwa upande wa ujenzi wa barabara, mara
baada ya Serikali kuweka lami, wananchi wameweza kusafiri kwa muda mfupikutoka mkoa mmoja kwenda mwingine akitolea mfano wa abiria wanaosafiri kwamabasi kutoka Mbinga na Newala kwenda Dar es Salaam wamekuwa wakitumiasiku moja badala ya siku mbili kama ilivyokuwa huko nyuma, halikadhalika naKutoka Lindi kwenda Dar es Salaam mabasi yamekuwa yakiondoka asubuhi nakurudi siku hiyo hiyo.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Newala Mhe. Aziza A. Mwangosongo amempongezaMhe. Rais, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa elimu bure kwa watoto ambaondio taifa la kesho na amewataka wazazi wa wanafuzi waliohitimu darasa lasaba wilayani humo kuunga mkono azma ya Mheshimiwa Rais kwa kufanyamaandalizi mapema ya kuwanunulia vifaa vya shule ikiwepo sare za shulewatoto wao ili waweze kunufaika na elimu ya sekondari inayotolewa bure naSerikali.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania(UWT) ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Bi. Zainabu Msuweta amemshukuruMhe. Mkuchika kwa nasaha zake na kuahidi kuwa UWT itazifanyia kazi ili ziwezekuwa na manufaa kwa wanawake wilayani Newala.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na UtawalaBora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) amepata mwaliko wa kuwaMgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Wanawake Tanzania(UWT) wilayani Newala, wakati akiwa mkoani Mtwara kwenye ziara yake yakikazi ya kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma mkoani humo.

Serikali yavunja Mkataba na Mkandarasi Ujenzi wa Jengo la Polisi Manyara

$
0
0
Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul akiongozana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kushoto),baada ya kumaliza Kikao na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Manyara juu ya Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Jeshi la Polisi mkoani hapo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (meza kuu) akisalimiana na Maafisa wa Jeshi la Polisi baada ya kuwasili leo kwa ziara ya kikazi huku akitoa taarifa ya Serikali kuvunja Mkataba na Mkandarasi wa Ujenzi wa Jengo la Ofisi la Polisi mkoani Manyara lengo ni kuepuka gharama za ujenzi huo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (meza kuu) akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Manyara baada ya kuwasili leo kwa ziara ya kikazi huku akitoa taarifa ya Serikali kuvunja Mkataba na Mkandarasi wa Ujenzi wa Jengo la Ofisi la Polisi mkoani hapo lengo ni kuepuka gharama za ujenzi huo.Wa kwanza kulia ni Mbunge wa Babati Mjini,Pauline Gekul.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

**********************************

Na Mwandishi Wetu

Serikali imewahakikishia wananchi wa Mkoa wa Manyara kuanza na kumalizika kwa Mradi Ujenzi wa Ofisi ya Makao Makuu ya Jeshi la Polisi ambao ulisimama tangu mwaka 2012 kutokana na gharama kubwa ya ukandarasi na sasa utajengwa kwa kutumia utaratibu mpya wa serikali wa nguvu mali ambao utapunguza gharama za ujenzi kulinganisha na kutumia mkandarasi

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni alipotembelea mradi huo uliopo katika eneo la Komoto Kata ya Bagara Wilayani Babati Mkoani Manyara ambao gharama za awali za mradi huo ni Milioni Mia Tano Themanini na Moja,Laki tatu na Thelathini.

“Serikali tunawahakikishia wananchi wa Mkoa wa Manyara kujengwa kwa jingo la polisi ili masuala ya ulinzi na usalama yaweze kuwa imara katika mkoa huu,tayari timu maalumu kutoka makao makuu ya polisi ilishafika hapa na kuona jinsi mradi huu utakavyoweza kuendelea baada ya kusimama kwa takribani miaka saba sasa,” alisema Naibu Waziri Masauni

“Juhudi mbalimbali zishaanza na hivi navyozungumza tayari Jeshi la polisi mkoani hapa likishirikiana na wadau wameshafanya harambee na kufanikiwa kukusanya takribani kiasi cha Shilingi Milioni Arobaini na Tano na sisi kama Wizara tutachangia ujenzi huo” aliongeza Masauni

Akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea eneo la mradi Mbunge wa Babati Mjini Pauline Gekul alisema Jeshi la Polisi linafanya kazi katika mazingira madogo,ofisi ni ndogo hali inayopelekea huduma kutolewa kwa uchache tofauti na mahitaji

“Nashukuru kuona serikali leo imefika kuona maendeleo ya huu mradi kwa kweli polisi wanahitaji jingo jipya ili kazi ya kulinda amani na utulivu iwe rahisi kwao,tunashukuru pia wadau mbalimbali wameanza kutuunga mkono ikiwa pia na ujenzi wa nyumba kwa ajili ya makazi ya askari wetu” alisema Mbunge Gekul

Awali akitoa taarifa ya Uhalifu Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara,Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Cyprian Mushi alikiri kupungua kwa uhalifu huku akikiri kuwepo changamoto katika kutatua baadhi ya kesi za ubakaji baada ya familia za mtuhumiwa na familia ya mtuhumu kutotokea mahakamani baada ya kuzimaliza kesi hizo kifamilia.

WAZIRI LUGOLA AWATAKA WANANCHI KUTOA TAARIFA ZA WAHAMIAJI HARAMU KUONDOA UJAMBAZI, UTEKAJI MIKOA YA MIPAKANI NCHINI

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akimsikiliza mkazi wa Kijiji cha Ikola, Wilayani Tanganyika, Mkoa wa Katavi, Ramadhani Juma, alitoa kero yake katika mkutano wa hadhara kijijini hapo, leo.Lugola amewataka wananchi wa mikoa ya mipakani nchini kutoa taarifa za wahamiaji haramu ili kudhibiti matukio ya ujambazi, utekaji katika maeneo hayo.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ikola, Wilayani Tanganyiko, Mkoa wa Katavi, leo. Lugola amewataka wananchi wa mikoa ya mipakani nchini kutoa taarifa za
wahamiaji haramu ili kudhibiti matukio ya ujambazi, utekaji katika maeneo hayo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Kijiji cha Ikola, Wilayani Tanganyika, Mkoa wa Katavi, leo. Lugola amewataka wananchi wa mikoa ya mipakani nchini kutoa taarifa za wahamiaji haramu ili kudhibiti matukio ya
ujambazi, utekaji katika maeneo hayo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola
(kushoto), akimsikiliza Kaimu Mkuu wa Wilaya ya
Tanganyika, Liliani Matinga akizungumza katika mkutano
wa hadhara na wananchi wa Kijiji cha Ikola, Wilayani
Tanganyika, Mkoa wa Katavi, leo. Lugola amewataka
wananchi wa mikoa ya mipakani nchini kutoa taarifa za
wahamiaji haramu ili kudhibiti matukio ya ujambazi,
utekaji katika maeneo hayo. Picha na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.

****************************************

Na Felix Mwagara, MOHA-Katavi

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewataka wananchi wa mikoa ya mipakani nchini kutoa taarifa za wahamiaji haramu ili kudhibiti matukio ya ujambazi, utekaji katika maeneo hayo.

Lugola alisema uhalifu katika mikoa hiyo licha ya kuwa imethibitiwa kwa kiasi kikubwa lakini bado baadhi ya mikoa ukiwemo Mkoa wa Katavi, wahalifu utumia njia zisizo rasmi kuingia nchini na kufanya matukio ya uhalifu.

Akizungumza na mamia ya wananchi wa Kijiji cha Ikola, Wilayani Tanganyika, Mkoa wa Katavi, leo, Lugola aliwataka wananchi hao kutoa taarifa kwa vyombo vya dola, kwa mtu au watu ambao wanawatilia mashaka ili kudhibiti matukio mbalimbali ya uhalifu.

“Mnapaswa kuwa wazalendo kwa kutoa taarifa za wahamiaji haramu katika maeneo yenu ili kuisaidia serikali yenu kuwasambaratisha wahamiaji haramu ambao wanafanya uhalifu wakishirikiana na Watanzania wasiowaaminifu waishio mipakani, hii haiwezekani, na kamwe Serikali haiwezi kuchezewa,” alisema Lugola.

Lugola aliongeza kuwa, Tanzania ina Serikali ambayo ipo makini katika kuwalinda watu wake, hivyo kwa majambazi ambao wanafanya matukio mbalimbali ya utekaji lazima washughulikiwe ipasavyo bila kuonewa huruma.

“Wahamiaji haramu wapo mitaani kwetu, na mnawajua, hivyo mnapaswa kutoa taarifa kwa maafisa uhamiaji, Jeshi la Polisi au vyombo vingine vya dola nchini, ili Serikali ya Dkt. Magufuli iweze kuwatia mbaroni haraka iwezekanavyo,” alisema Lugola.

Kwa upande wake, Afisa Uhamiaji Mkoa wa Katavi, Kamishna Msaidizi, Vicent Haule alikiri kuwepo na changamoto hiyo, na kuahidi kuwasaka wahamiaji haramu kupitia vyanzo vyote vya uchunguzi.

Haule alisema maeneo ya mipakani yana changamoto licha ya kuwa ofisi yake inafanya kazi usiku na mchana kupambana na wahamiaji haramu, na wapo tayari kupokea taarifa za wahamiaji hao watakapopewa na wananchi.

“Tunamshukuru sana mheshimiwa Waziri kwa kutupa maelekezo mbalimbali, hasa ya kuhusu masuala ya wahamiaji haramu, na uraia hasa pale makazi ya Katumba na Mishamo, kwasababu amewataka wakazi waliopewa uraia wasivunje sheria za nchi kwa kwenda Burundi na kurudi nchini bila kufuata sheria,” alisema Haule.

Aidha, Lugola aliwataka Polisi kuwasaka na kuwakamata majambazi na kuwasambaratisha bila woga wowote maana mhalifu hawezi kuchekewa.

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Lilian Matinga, alimshukuru Waziri Lugola kwa kufika katika wilaya hiyo na kuahidi maagizo yote aliyoyatoa kwa Wilaya hiyo watayafanyia kazi kupitia vikao vyao vya kamati ya ulinzi na usalama.

Waziri Lugola amemaliza ziara yake Mkoani Katavi kwa ksuikiliza kero mbalimbali za wananchi kupitia mikutano ya hadhara na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani humo.
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live


Latest Images