Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

Mdau Maggid Mjengwa azindua kitabu cha Simulizi za Mzee Mandela leo

$
0
0
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Ikolo Investment,Maggid Mjengwa akizungumza na wadau mbalimbali waliohudhulia kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa Kitabu cha "Simulizi za Mzee Mandela" kilichoandikwa na Maggid Mjengwa mwenyewe.hafla hiyo imefanyika jioni ya leo kwenye Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa,jijini Dar es Salaam.
Mgeni Rasmi Kwenye Uzinduzi huo,Ndugu Mobhare Matinyi akisisitiza jambo mbele ya wadau mbali mbali waliohudhulia kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa Kitabu cha "Simulizi za Mzee Mandela" kilichoandikwa na Maggid Mjengwa,hafla hiyo imefanyika jioni ya leo kwenye Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa,jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa wadau waliokuwepo kwenye uzinduzi huo akiuza swali.
Wadau wakinunua vitabu hivyo vya  "Simulizi za Mzee Mandela" mara baada ya uzinduzi wake.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Ikolo Investment,Maggid Mjengwa akisaini kwenye vitabu hivyo vilivyonunuliwa na wadau hao.

ROSE MUHANDO AWAKUNA WAKAZI WA TANGA UWANJA WA MKWAKWANI LEO.

$
0
0


Mwimbaji mahiri wa nyimbo za kiroho a.k.a Injili,na anaetamba na wimbo mpya wa Facebook,Rose Muhando akiwa sambamba na skwadi lake zima wakilishambulia jukwaa vilivyo jioni ya leo ndani ya uwanja wa Mkwakwani wakati wa muendelezo wa tamasha la Krisimasi lililofanyika leo Mkoani Tanga.Tamasha hilo ndio kwa mara ya kwanza linafanyika mkoani humo,limezindundiliwa jijini Dar siku ya Krisimasi ndani ya uwanja wa Taifa na kuhudhuriwa na watazamaji lukuki.Tamasha hilo baada ya kufanyika mkoani Tanga,kesho litafanyika jijini Arusha na baadae mkoani Dodoma likiwajumuisha waimbaji mbalimbali wa nyimbo za Injili.

 Pichani kulia ni Mwimbaji wa kimataifa wa nyimbo za kusifu na kuabudu kutoka nchini Zambia,Epfrahim Sekeleti akiimba pamoja na mwimbaji mwingine mahiri wa nyimbo injili hapa nchini,Bon Mwaitege pichani shoto.

Rais Shein wa Zanzibar katika Mahafali ya 9 ya Chuo Kikuu cha Taifa SUZA

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti waa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa SUZA,akisalimiana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Ali Juma Shamuhuna,wakati alipowasili Chuo Kikuu cha Taifa,kampasi ya Tunguu,katika sherehe za mahfali ya 9 ya chuo hicho,ambayo wahitimu wa fani mbali mbali wamepatiwa Shahada,Stashahada na Vyeti.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti waa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa SUZA,akisalimiana na walimu wa Chuo Kikuu cha SUZA,alipowasili katika mahfali ya 9 yaliyofanyika kampasi ya Chuo Tunguu,Wilaya ya Kati Unguja, leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti waa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa SUZA,(wa pili kulia) akiongoza maandamano wakati wa sherehe za mahfali ya 9 chuo hicho,yaliyofanyika kampasi ya Chuo Tunguu,Wilaya ya Kati Unguja leo,yaliyowashirikisha baadhi ya wahitimu na walimu.

MKUU WA MKOA WA RUKWA INJINIA STELLA MANYANYA AKABIDHI MSAADA WA BOTI KUSAIDIA MAMA WAJAWAZITO NA WAGONJWA MWAMBAO WA ZIWA RUKWA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiwakabidhi funguo ya boti na "Life Jacket 8" kwa Uongozi wa kijiji cha Ilanga/Muze ikiwa ni sehemu ya msaada wa boti na Injini moja kusaidia huduma za afya ya mama wajawazito na wagonjwa mwambao wa Ziwa Rukwa.Msaada huo wenye thamani ya Shilingi Milioni 20 umetolewa na Mfadhili Bi. Adrianne Strong kwa kushirikiana na waumini wenzake wa Kanisa la University United Methodist Church la Washington DC Marekani, Mfadhili huyo alishawishika kutafuta msaada huo baada ya kufika Mkoani Rukwa katika kufanya utafiti na kubaini mambo mengi ikiwemo umbali kati ya wananchi na vituo vya kutolea huduma za afya.
Hapo awali yalifanyikamajaribio ya Boti kabla ya makabidhiano rasmi.
Kabla ya makabidhiano ya Boti hiyo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa aliamuru Boti hiyo kupelekwa ziwani kwa ajili ya majaribio.
Haikuwa kazi rahisi kwani Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya aliwaongoza viongozi wengine wa Chama na Serikali ya Mkoa na Halmashauri kuvua viatu na kukanyaga maji ili kuweza kufikia Boti hiyo iliyobebwa na wananchi wa kijiji cha Ilanga hadi ziwani.
Wananchi wa kijiji cha Ilanga wakishirikiana kubeba Boti hiyo hadi ziwani.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiongea na wananchi wa Kijiji cha Ilanga muda mfupi kabla ya kukabidhi msaada huo kwa uongozi wa kijiji. Katika hotuba yake hiyo aliwashukuru wote waliosaidia upatikanaji wa msaada huo ambao ni Bi. Adrianne Strong na waumini wenzake wa Kanisa la University United Methodist Church la Washington DC Marekani, Dkt. Francis Mashigala wa Hospitali  Kuu ya Mkoa wa Rukwa aliyekuwa anaratibu msaada huo na Bwana Hussein Kandoro (Mwanasheria Ofisi ya Waziri Mkuu) aliyesaidia kusafirisha Boti hiyo kufika Mkoani Rukwa. Kwa upande mwingine aliuita mwaka huu mpya 2014 kuwa ni mwaka wa afya ambapo alihamasisha juu ya upimaji wa virusi ya Ukimwi, kupiga vita unyanyapaa na Ukimwi, mama wajawazito kujifungulia kwenye vituo vya afya na kupeleka shule watoto wenye umri wa kwenda shule.  
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halamashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Ndugu Adam Misana akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ilanga na kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kuzungumza na wananchi wake. Katika kauli yake alisistizia agizo la Mkuu wa Mkoa wa Rukwa la kuhakikisha kuwa shughuli za uvuvi katika ziwa Rukwa zinafungwa kwa muda wa miezi mitatu kuanzia Januari hadi Machi kupisha mazalio mapya ya Samaki. Alisema kuwa doria zitaendeshwa katika Ziwa hilo na yeyote atakaekamatwa akivua katika kipindi hicho hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake. 
Dkt. Francis Mashigala wa Hospitali Kuu ya Mkoa wa Rukwa aliyekuwa mratibu wa msaada huo wa Boti akitoa maelezo mafupi juu ya msaada huo  kwa wananchi wa kijiji cha Ilanga.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa na Msafara wake walipata fursa ya kutembelea Shamba darasa la moja ya shule zilizopo katika kata ya Mtowisa kwenye kijiji cha Ilanga ambalo limepandiwa kwa mbolea aina ya Minjingu Mazao. Serikali ya Mkoa ikiongozwa na Injinia Manyanya ilitoa agizo kwa kila shule kuwa na shamba angalao ekari tano zitakazotumika kama shamba darasa na kusimamiwa na Afsa Ugani wa eneo husika na kupatiwa ruzuku ya pembejeo inayotolewa Serikali. 

Mpango huo una faida mbili ambapo licha kuwa shamba darasa pia utatibu tatizo la ukosefu wa chakula mashuleni na hivyo kuongeza mahudhurio na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi.  (Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)

Article 23

BURIANI NDUGU YANGU TONY BARETTO

$
0
0
Tony Baretto
Na Muhidin Issa Michuzi
Nilikuwa nje ya Dar es salaam kikazi siku ya Jumanne wakati Catherine-Rose, binti yake, aliponipigia simu na kunifahamisha habari hii ya kustua na kusikitisha. 
Lakini simu yake ilikuwa ni moja ya nyingi  nilizopokea siku hii zikiwa na habari hizi za kustusha.

Ya kwanza ilitoka kwa rafiki yetu Mukesh Josh, aliyeanza kwa kunipa pole, mapema asubuhi. Nilipomuuliza ya nini, akashangaa kwa kusema huna habari kuwa rafiki yako Anthony  Baretto amefariki dunia?

Kabla ya mwangwi wa habari hiyo iliyoufanya moyo wangu unyong’onyee kutwa nzima kwa huzuni haujatuama, simu ya pili ikaita. 
Hii ilikuwa inatoka Arusha kwa rafiki yetu mwingine Sukhdev Chattbar . Alinipigia kutaka kuthibitisha habari hiyo. Tulilia kwa pamoja nilipomthibitishia kwamba ni kweli Braza Tony is no more…

Kwa hali ya kawaida, na kama Mola asingemchukua miaka mine iliyopita kwa ajali ya gari, ni wazi simu ingine  ingetoka kwa kaka Hamidu Bisanga (aliyekuwa mmoja wa Brotherhood yetu mie, Tony, Suk Chat, Mkumbwa Ally, Jajis Merali na Danfold Mpumilwa a.k.a Dan Lutte). Lakini simu ya nne, ya tano na nyingine nyingi  ziliendelea kunimiminikia kutoka kila kona, kwani wengi walijua urafiki wangu na Tony na familia yake.

Si urafiki tu, bali pia undugu wa karibu, tangia najiunga na Tanzania Standard Newspaper (TSN) wachapaji wa magazeti ya serikali ya  Daily News na Sunday News January 1, 1990.

Yeye Tony, Mzee Wenceslaus Mushi, Isaac Mruma, Charles Kizigha, Vicent Urio (RiP) Ernest Millinga (RiP), Jonas Marios, Jonas Mwasumbi, Chattbar,  Bisanga (RiP), Reggie Mhango (RiP), Charles Rajabu, Mkumbwa Ali,  Attilio Tagalile, Willie Chiwango, Adam Lusekelo (RiP)  Khadija Riyami, Emmanuel Bulugu (RiP), Mzee Mdimi, Bob Karashani, Stephen Rweikiza, Rose Kalemera, Ichikaeli Maro, Pudenciana Temba, Joyce Mhaville, Halima Shariff, Chemi Che-Mponda, Mzee Boniface Byarugaba  ndio walionipokea Daily News kwa mikono miwili na kuwa mwanga wangu mkuu wa kunionesha njia sahihi lakini iliyojaa kona na mabonde na gharika ya tasnia hii adhimu ya habari.

Nadiriki kusema Tony na   wote hao niliowataja kuwa ndio walionitaga, walionilea na kunifikisha hapa padogo nilipo kitaaluma. Sijui nifanye nini ama niseme kitu gani kuwalipa fadhira hiyo.

Ni vigumu kuamini kwamba Tony, aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Matangazo cha Tanzania Standard Newspapers (TSN) wachapaji wa magazeti ya serikali ya Daily News na Sunday News, hatunaye tena.  Utendaji kazi wake uliojaa utani na ucheshi  wakati wowote, uwe wa matatizo ama fanaka, ulikuwa hauna mfanowe.

Nakumbuka siku moja wafanyakazi wa Daily News tulipofika kazini pale mtaa wa Maktaba jijini Dar es salaam asubuhi moja na kukuta milango imetiwa kufuli na mwenye nyumba wetu (Printpak) kutokana na kutolipa pango. Hakuna aliyeamini kuwa pamoja na kufungiwa nje, gazeti la siku ya pili yake lingetoka kama kawaida, kwani kila kitu kilikuwa kimefungiwa ndani.


 Lakini siyo Tony. Hata kabla ya saa tatu haijatimia tayari yeye na Reggie  Mhango  walishafungua ofisi chini ya mti pembezoni mwa jengo la ofisi yetu, baada ya kumuomba muuza kahawa na kashata nafasi katika meza yake pale. Wakaongoza mapambano ya kutengeneza gazeti kwa ushujaa ambao sintousahau.
 Na kweli, kesho yake Daily News lilikuwa mitaani kama kawaida. Vinginevyo  kwa mara ya kwanza katika historia yake ya  miaka 75 wakati huo, gazeti hilo lisingeona mwaka wa jua!  
Huyo ndiyo alikuwa Tony Baretto.

Ni kweli kwamba mtu anapoaga dunia ndiyo watu humtaja kwa maneno ya sifa na uzuri wake wakati alipokuwa hai, lakini si uwongo kwamba Tony alikuwa si mtu wa kawaida, na aliyestahili sifa zote hizo na za ziada.  Nembo zake kuu tatu – Upara, macho makubwa nyuma ya miwani na madevu (kama ya gaidi, tulimtania, naye alicheka tu) hazitosahaulika kwa sie tuliofanya naye kazi na pia kuwa karibu kifamilia.

Buriani kaka yangu,  ndugu yangu, mshauri wangu na mwanafamilia wangu Anthony Baretto.  Eelewa kuwa huko ulikotangulia, ambako sote tutafuata kwa muda tofauti, hatutakusahau milele. Mke wako Pearl, na watoto wako Catherine-Rose na John-Paul tutalia nao na kusherehekea pamoja maisha yako yaliyojaa bashasha na mapenzi kwa binadamu wenzio.

SISI TULIKUPENDA, ILA MOLA  KAKUPENDA ZAIDI

NA AIWEKE ROHO YAKO MAHALI PEMA PEPONI



SHEREHE YA KUUKARIBISHA MWAKA DMV

$
0
0
Rais wa Jumuiya Bwn. Iddi Sandaly akitoa salamu za mwaka mpya kwa Watanzania waliofika Capitol Heights, Maryland kushuhudia mkwsha wa mwaka mpya.
Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Bwn. Abbas Missana akitoa salamu za mwaka mpya kwa Watanzania DMV na marafiki zao kwa niaba ya Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula.

Juu na chini wanajumuiya wanaojitoa mhanga kwenye majukumu mbalimbali ya Jumuiya.
Juu na chini walimu wa darasa la kiswahili wakitunukiwa vyeti kwa juhudi zao za dhati za kufundisha darasa hilo DMV.
Juu na chini wadau wakichukua zawadi zao baada ya kushinda bahati nasibu ya papo kwa hapo.

Kocha Mkuu wa Italy Cesare Prandelli aishauri Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

$
0
0
Na Othman Khamis Ame, 
Ofisi ya Kamau wa Pili wa Rais wa Zanzibar 
Kocha Mkuu wa Italy Cesare Prandelli ameishauri Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo kuandaa mpango maalum utakaomuewezesha kusaidia kuinua kiwango cha mchezo wa Soka hapa Nchini. 
Kocha Cesare ameamua kusaidia kukuza kiwango cha soka cha Zanzibar kufuatia ukarimu wa watu wake pamoja na mazingira mazuri yaliyopo ndani ya Visiwa vya Zanzibar unaoleta ushawishi wa watalii na wageni wengi kupendelea kutembelea Visiwa hivi. 
Gwigi huyo wa Taaluma ya kufundisha Soka Nchini Italy alieleza hayo wakati akibadilishana mawazo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo Ofisini kwake Mtaa wa Vuga Mjini Zanzibar.
 Kocha Cesare alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba angependelea kuona Zanzibar inamjengea mazingira ya chuo maalum cha soka atakachoweza kufundisha wakati anapokuja mapumziko ya kila mwaka hapa Zanzibar. “ Nimeamua kuisaidia Zanzibar kisoka kwa vile muda wangu wa mapumziko ya mwaka karibu mwaka wa tatu sasa nautumia hapa Zanzibar. Sasa ingekuwa ni jambo la msingi na busara muda huo nikatumia taaluma yangu kwa vijana wangu wa hapa Zanzibar. Najihesabu kwamba Zanzibar ni makazi yangu ya pili katika maisha yangu ukiachilia Italy “. Alifafanua Kocha Mkuu huyo wa Soka Nchini Italy.
Alieleza kwamba wakati umefika kwa chama cha soka cha Zanzibar { ZFA } kikaanza kufanya mawasiliano ya ushirikiano na shirikisho la soka Nchini Italy ili kutoa fursa itakayomjengea njia muwafaka ya kuanza kusaidia kufundisha soka hapa Zanzibar. 
Kocha Cesare alifamisha kwamba mawasiliano hayo kwa njia moja ni mwanzo wa kuongeza uhusiano wa karibu zaidi kati ya wananchi na jamii za Zanzibar na wenzao wa Italy. Alieleza kwamba Zanzibar kwa kiasi kikubwa imekua kiuwezeshaji ikilinganishwa na mataifa mbali mbali ulimwenguni jambo ambalo limesaidia wawekezaji wengi nje ya nchi kushawishika kutaka kuwekeza vitega uchumi vyao ndani ya Visiwa vya Zanzibar. 
Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iko tayari kushirikiana na Kocha Mkuu huyo wa Italty katika azma yake ya kutaka kusaidia kunyanyua kiwango cha mchezo wa Soka hapa Zanzibar. 
Balozi Seif alisema Kocha Cesare Pzandell yuko huru wakati wowote ule kusaidia, kushauri au kuelekeza masuala yoyote yanayohusu fani yake ya mchezo wa soka ili utaalamu wake uweze kusaidia wanamichezo hapa Nchini. 
“ Kwa kuwa uwepo wako nchini utasaidia kunyanyua kiwango cha soka Zanzibar uko huru kutusaidia katika kutushauri na kutuelekeza katika muelekeo wa kunyanyua kiwango chetu cha soka hapa Nchini “. 
Balozi Seif alimfungulia milango wazi kocha huyo wa Italy Cesare. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliiagiza Wizara ya Habari, Utamduni, Utalii na Michezo kujipanga vyema katika utaratibu wa kumuandalia mpango maalum utakaomuwezesha kocha huyo kuanza kutoa taaluma ya soka hapa nchini. 
Mapema Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamduni, Utalii na Michezo Dr. Ali Saleh Mwinyikai alisema Kocha Mkuu wa Soka wa Italy Cesare Pzandell tayari ameshaonyesha nia ya kujenga uhusiano mzuri na wakaribu na Zanzibar katika masuala ya soka na kusema kwamba atafarajika zaidi atakapoona Zanzibar katika siku chache zijazo inapanda chati katika medani ya Soka Duniani Huu sasa ni mwaka wa tano kwa Kocha huyo wa Soka Nchini Italy Cesare Pzandell kutumia mapumziko yake ya mwaka hapa Zanzibar. 
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Kocha Mkuu wa Soka wa Italy Cesare Prandelli ambae  yuko nchini kwa mapumziko ya mwaka mpya.
 Mke wa Kocha Mkuu wa Soka wa Italy Mama Novella Benini wa pili kutoka kulia pamoja na wenzake akiokaa nao wakimsikiliza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif hayupo pichani akitoa baraka zake kwa Kocha wa Nchi hiyo  Cesare Prandelli kufundisha soka hapa Nchini.
  Kocha Mkuu wa Soka wa Italy Cesare Prandelli  akitia saini mpira wa Soka kabla ya kumkabidhi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  Ali Iddi kama ni zawadi maalum. 
 Kocha Mkuu wa Soka wa Italy Cesare Prandelli akimkabidhi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif zawadi ya mpira maalum wa soka hpo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi zawadi maalum za kanga za kusherehekea miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar Mke wa Kocha Mkuu wa Soka wa Nchini Italy Mama Novella Benini hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. 
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

UJENZI WA BARABARA YA MKATO YA JANGWANI-KIGOGO NIAJE?

$
0
0
 Barabara mpya ya mkato inayokatiza Jangwani na kutokea Kigogo jijini Dar es salaam ambayo ina miaka kadhaa haijaisha na kuzua maswali yasiyo jibu hadi leo. Barabara hii inayojengwa kupunguza msongamano katika barabara za Morogoro road na Uhuru road hadi sasa imekamilika nusu tu, sehemu za Jangwani. 
Baada ya kufuatilia swala hili Globu ya Jamii imepata taarifa za uhakika kwamba kuna baadhi ya wamilliki wa majengo yanayotakiwa kupisha ujenzi huo wamegoma kuomndoka na wamefungua kesi mahakamani na hivyo kusababisha ujenzi huo kutoweza kuendelea katika maeneo husika. 
Hii ndiyo shida ya hapo ambayo hatma yake inasubiri  maamuzi ya mahakama kufuatia kesi hiyo iliyofunguliwa na watu 7 miaka mitatu iliyopita. Na hakuna kitachoendelea hadi hapo...

Fare Thee Well Ton Bar

$
0
0
 By Danford Mpumilwa
The year was 1986. It was June to be more precise.  I was in Dar es Salaam working with the then Tanzania Tourist Corporation. I had just been offered a job with Arusha International Conference Centre. But perhaps due to the normal fear of change and of the unknown I was not keen on taking up the job. After all I still loved what I am doing in Dar es Salaam.
Then one morning I woke up in my humble abode in Mwenge and realized that apart from me and my bed and blankets everything else has been stolen by thieves who must have broken into my house while I was deep asleep. This was deeply upsetting, but what was more troubling to me was the simple fact that the thugs had stolen all mu suits, shirts and ties. Yes suits.
For those who know me I do indeed love my suits. To make matters worse during those years one could not buy any suits in Dar es Salaam. They were simply not there. Not there at all. The suits I had were on account my being able to travel on official business around the world promoting Tanzania’s abundant tourist attractions.
As I headed to the office in the morning in the single pair of clothing they had left me – some worn out jeans and T-shirt, I decided there and then that this was the last nail on the coffin, and I had to immediately proceed to Arusha and take up my new job. But I had to communicate this major decision to my close buddies – and who were those? Those were none other than Ton Bar and Ham Bis otherwise known as Tonny Barreto and Hamidu Bisanga my buddies from the days I was at the Daily News.  Those were the nom de guerre we had at the Daily. For example I was called Dan Pum; we had Ul Mwambu for Uli Mwambulukutu;  Abdango for Abdallah Ngororo; MwamHa for Mwamoyo Hamza; Adluse for Adam Lusekelo and many others.
Well my buddies, Tan Bar and Ham Bis organized a hasty meeting to plan for my departure. And we met in Tonny Barreto’s apartment in the city centre one evening. The main issue was how was I going to begin a new job without any proper clothing?
That is when Tonny asked his wife, the lovely and beautiful  Pearl, to bring out all of Barreto’s clothes which were now too tight for him on account of the now generous  body so we could choose what suits me. To cut the whole story short we ended up selecting a few pairs of suits and jackets. To my surprise Barreto insisted that I also take his wedding suit. I was confounded. How about the fond memories that went with the suit? He insisted that notwithstanding the memories he would be more delighted that I took the suit. That is how I ended up in Arusha with a black wedding suit courtesy of the big hearted Barreto. Those were his blessings to me.
Our friendship had begun many years before when I was still at the Daily News. The charming and amiable Barreto was the darling of everyone at the Daily whether young or old, senior or junior. He would enliven any moment when everyone was feeling low. He would go all out of his way to assist anyone facing any problems whether official or domestic. He was indeed very generous and big hearted.
No wonder when I decided to establish the Tantravel Magazine at the Tanzania Tourist Corporation, it was to Barreto and the late Bisanga to whom I turned to. The trio of us became the founding Editors of that magazine which is still published to-date.
And he was a great family man, and encouraged everybody to be so. Notwithstanding the challenges faced he managed with the close cooperation of his wife Pearl, to bring up two brilliant and inspirational children Catherine-Rose and John-Paul.
So when SukChat a.k.a. Sukdev Chatbar  called me the other day announcing his passing on.  I felt numb. It was only the other day when we were toying with the idea of establishing a serious magazine in Dar es Salaam. Now what will I do as all my fellow soldiers have gone. 
May God Bless His Soul! 
Amen! 

Go and rest in Eternal Peace Anthony Baretto

$
0
0

By Franklin Mziray

Really. Tony is of the ages. What a loss. He was a great friend when I worked with him. Banyan I used to call him, much as he was not one. 

Tony worked in advertising and many a times he would come over to Editorial to ask me look at some copies and do a re-write. He was quite hard self motivated chap whose bald was iconic to the display of the advertising pages.

Even when I left the Daily News, I still worked with him because my new employer was ad erasing quite a lot and sometimes we would need to put a notice for something after the pages are closed.

And even when again he too left he Daily News we continued th e association and did a few ads with his own company, by then in partnership with my friend Mikidad Mahamoud, the legendary radio broadcaster turned politician.

And socially, Tony was everywhere charming people and if you never met him at a party, you should know how good he was with charanga.

It is so sad I am not around there to celebrate his promotion to glory, but let all the family know that our sympathies are with them and as a catholic, the Prayers too.

Go and rest in Eternal Peace 
ANTHONY BARRETO 

Amen

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TOKA TFF Januari 3, 2013

MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI WATAKIWA KUTIMIZA WAJIBU WAO KWA WATOTO YATIMA

$
0
0
 Mbunge wa Mufindi Kusini Menrad Kigola akizungumza  na mmoja wa watoto waishio katika mazingira hatarishi katika kituo cha itulituli.(picha zote na Denis Mlowe)
Mbunge wa Mufindi Kusini Menrad Kigola akiwa katika sherehe za mwaka mpya 2014 na watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi jijini 
=========  ========  =========
NG’O WATAKIWA KUTIMIZA WAJIBU WAO KWA WATOTO YATIMA

Na Denis Mlowe,Mufindi.

WAKURUGENZI wa mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) yanayoanzishwa kwa lengo la kuhudumia jamii na hasa watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu nchini wametakiwa kutimiza malengo ya uanzishwaji wa mashirika hayo kwa kuwanufaisha walengwa badala ya kuangalia maslahi yao binafsi.

Hayo yamesemwa na Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini (CCM) Menrad Kigola wakati wa hafla fupi ya kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi laki 7 kwa kituo cha watoto yatima na wale wanaoishi ktk mazingira magumu wa kituo cha Ifulifuli kilichopo wilaya Mufindi mkoani Iringa na kuongeza kuwa kumekuwa na utitiri wa NGOs ambazo zimekuwa zikipata mamilioni ya pesa kutoka kwa wahisani lakini badala ya kuwasaidia walengwa waliokusudia pesa hizo huishia kuwanufaisha watu wachache kwa manufaa yao binafsi.

Kigola ambaye pia alipata wasaa wa kula chakula cha mchana na watoto hao kwa lengo la kuukalibisha mwaka mpya amewataka watoto yatima kote nchini kutojiona wa thamani ya chini kufutia maswaibu wanayoyapitia na badala yake kuwekeza muda wao mwingi kusoma hali itakayosaidia Taifa  kuwa na hazina kubwa ya wasomi ktk siku za usoni.

Alisema imekuwa ni kawaida ya baadhi ya asasi zinazolea watoto yatima kutumia misaada wanayopatiwa kwa manufaa ya waanzilishi kuliko malengo halisi ya asasi hizo.

“Kuna baadhi yenu mmekuwa mnaanzisha asasi kwa lengo la kuwanyonya watoto yatima hakika haimpendezi mwenyezi MUNGU kuwatumia watoto yatima kwa manufaa yenu” alisema Kigola

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kituo hicho kinachomilikiwa na kikundi cha MPENDE JIRANI,Wilson Ngogi ameitaka serikali kupitia vyombo vyake kuweka mikakati madhubuti itakayosaidia kubaini mashirika yanayokwenda kinyume na sheria na taratibu za uanzishwaji wake.

DK.SHEIN AFUNGUA MAONESHO YA MIAKA 50 YA MAPINDUZI

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiwapungia Mkono Maafisa katika banda la Tume ya Uchaguzi Zanzibar,alipotembelea  Maonesho ya Miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar,yaliyofanyika jana viwanja vya Beit el Ras,ikiwa ni katika
shamra shamra za sherehe za Mapinduz
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed akisalimiana na Maafsa katika banda la Ofisi ya Mufti wa Zanzibar,alipotembelea  Maonesho ya Miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar,yaliyofanyika jana viwanja vya Beit el Ras,ikiwa ni katika shamra shamra za sherehe za Mapinduzi,(katikati) ni Katibu wa Mufti Fadhil Suleiman Soraga
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipotembelea banda la Ofisi ya
Vitambulisho vya Taifa,wakati alipofungua  Maonesho ya Miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar,yaliyofanyika jana viwanja vya Beit el Ras,katika shamra shamra za sherehe za Mapinduzi

 Watoto hawakua nyuma kufika katika banda la Sober House,wenye Makamo yao Kwamchin Mwanzo,katika kujionea  maonesho ya Miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar,yaliyoanza jana katika viwanja vya Beit el Ras, ikiwa ni katika shamra shamra za sherehe za Mapinduzi.

Fundi viyoyozi wa mbezi beach atimka na Milioni 20 za Vodacom leo

$
0
0
 Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu akisisitiza jambo wakati wa Droo kubwa ya Mwezi ambapo Bwana. Willison Urio (33) Mkazi wa Mbezi Beach Jijini Dar aliibuka Mshindi wa Shilingi Milioni 20. Pamoja nae katika Picha ni Ofisa huduma za ziada wa kampuni hiyo Mathew Kampambe na Ofisa Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Chiku Saleh. Ili kushiriki katika Promosheni hiyo Mteja anatakiwa kutuma neno PROMO kwenda namba 15544.

Ofisa Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Chiku Saleh akihakiki namba ya Mshindi wa Milioni 20 wakati wakuchezesha  Droo kubwa ya  Mwezi,kabla ya Meneja  Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu (katikati) kumpigia mshindi huyo ambapo Bw. Willison Urio (33) Mkazi wa Mbezi Beach Jijini Dar aliibuka Mshindi. Anaeshuhudia ni Ofisa wa huduma za ziada wa Vodacom Tanzania Mathew Kampambe. Ili kushiriki katika Promosheni hiyo Mteja anatakiwa kutuma neno PROMO kwenda namba 15544.


        *Shilingi Milioni 119 bado kushindaniwa na Bodaboda 115
              *Jumla ya bodaboda 315 na Tsh. Milioni 211 tayari zimetolewa

Huku siku zikiwa zinahesabika kwa Promosheni ya Timka na Bodaboda inayoendeshwa na Vodacom Tanzania kufikia ukingoni, Neema imeendelea kuwashukia maelfu ya Watanzania na safari hii ni kwa Bwana.  Willison Urio Mkazi wa Mbezi Beach jijini Dar es Salaam ameibuka Mshindi wa Shilingi Milioni 20.

Promosheni hiyo ambayo imeboresha maisha ya mamia ya Watanzania Tangu kuanza kwake imemuibua mshindi huyo ambae akizungumza kwa njia ya simu wakati alipopigiwa simu akiwa mapumzikoni Mkoani Kilimanjaro alisema kupitia mchezo huo ameona mwanga katika maisha yake kwani alikuwa akijipa matumaini kuwa ipo siku ndoto yake itatimia.

“Maisha ya sasa  ni magumu sana na nivigumu kwa mtu wa kawaida kupata kiasi kikubwa cha fedha kwa mkupuo, yaani ni vigumu kuamini kwamba mtu unaweza kupata Milioni 20 kiurahisi tu, lakini leo nimeamini kupitia Vodacom haya yote yanawezekana.

“Sasa nimeona mwanga katika maisha yangu, nitajiendeleza kibiashara na kuhakikisha ninakuwa na mafanikio na kuendelea kuwaunga mkono Vodacom kwa kuyabadilisha maisha yangu” alisema Urio  na Kuongeza.

Imekuwa vigumu kwangu kuamini kama nimeshinda kiasi hiki cha fedha ninamshukuru sana Mungu, Kuna siku nilisikia mama mmoja kutoka Arusha ameshinda milioni 10, nilikaa siku zote na kujipa matumaini kuwa ipo siku nami nitashinda na sikukata tamaa niliendelea kushiriki katika mchezo huu na leo nimejibiwa maombi yangu na nimeona matunda ya kutokukata tamaa, alisema Urio.

Akizungumzia juu ya promosheni hiyo Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu amesema “mwitikio umekuwa mkubwa sana tangu tunaanza mpaka hapa tulipofikia kwani watu wamekuwa wakijishindia bodaboda kwa ajili ya usafiri ama kuanzisha biashara na pia fedha taslimu ambazo zimekuwa zikitumika kufanyia biashara na matumizi mengine ya kimaisha.”

“Nia ya Vodacom ni kuhakikisha inaboresha maisha ya wateja wake ambao wamekuwa wakituunga mkono siku zote na kutufanya kuendelea kuwa namba moja, Tunawaahidi tutaendelea kushirikiana nao na kuhakikisha tunaboresha maisha ya wateja wetu kwa kuwaletea promosheni zaidi na zaidi.”

Nkurlu aliongezea kwa kusema “mitaji ni kilio kikubwa cha wajasiriamali wengi nchini. Kuunga mkono jitihada za wajasiriamali nchini kote ni lengo mojawapo la kampuni yetu, hivyo tunaamini kwa bodaboda pamoja na fedha hizi tunazozitoa kwa washindi zitasaidia kupiga hatua kibiashara na kuboresha maisha yao”.

“Ninawasihi wateja wengine wa Vodacom waendelee kushiriki katika Promosheni hii ili nao wapate mafanikio ambayo wengine wameyapata na wanayoendelea kuyapata kwani mwishoni mwa mwezi huu watachezesha droo kubwa ya kupata mshindi wa Milioni 30”. Alimalizia Meneja Uhusiano huyo.

Hadi kufikia sasa zaidi ya watu 315 wamejishindia pikipiki”bodaboda”huku jumla ya fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni 211 zikiwa tayari zimekwisha tolewa kati ya Milioni 330. Huku Milioni 119 zikisubiria washindi.

Ili kujiunga na promosheni hii wateja wote wa Vodacom wanatakiwa kutuma neno PROMO  kwenda namba 15544.



Tanzania Freight Forwarders Association visit the Ministry of Foreign Affairs

$
0
0
Hon. Dr. Mahadhi Juma Maalim (MP) (left-seated), Deputy Minister for Foreign Affairs and International Co-operation today met with the members of the Tanzania Freight Forwarders Association and the Zanzibar Freight Forwarders Bureau, who had just paid a courtesy visit at his office in Dar es Salaam. The team discussed with the Deputy Minister about challenges and business opportunities that exist in their agencies, including membership opportunities in different international organizations that deal with matters related to freight forwarders. 
A group photo of Deputy Minister Mahadhi Juma Maalim that include Mr. Ahmed S. Nassoro (left-seated), Secretary General of the Zanzibar Freight Forwarders Bureau, Mr. Stephen J. Ngatunga (2nd right-seated), President of the TAFFA, Mr. Shaban Geva (left-standing), National Treasurer, Ms. Naomi Zegezege (2nd left-standing), Foreign Service Officer (Legal Department) in the Ministry of Foreign Affairs and Mr. Solomon A. Kasa (center-standing), Secretary General of the TAFFA.  
All photos by Tagie Daisy Mwakawago 

Article 11

Funeral Announcement Tony Barretto (Anthony Edgar)

$
0
0
The family of the Late Tony Barretto, his wife Pearl and children Catherinerose (CR) and Johnpaul (JP), regret to announce his untimely demise on 31st December, 2013, in Dar es Salaam.

We gather to celebrate his life on Saturday 4th January, 2014, at the Diamond Jubilee Hall, Upanga (Malik Road) as follows:
9:00am -10:30am Spiritual Service 10:30 am-12:30pm Last respects 2:00 pm Crematorium (Makumbusho Bagamoyo Road) Tony's request was that there be no mourning colours or floral tributes.

Friends wishing to send condolence messages or donate to the charities that Tony supported please contact Johnpaul Barretto, by email: madevu.tb@gmail.com or send to Bank M Limited, Kisutu Branch, Tshs A/C: 0210025551 or US$ A/C: 0210025552 May his soul rest in eternal peace

Huduma za NHIF zapongezwa Zanzibar

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Hamis Mdee akipima afya yake kwenye banda ya NHIF katika maonesho ya maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
Mwakilisho wa NHIF Zanzibar Ismail Kangeta (Katikati) akitoa elimu ya umuhimu na namna ya kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya katika maonesho hayo.
Ofisa Elimu kwa Umma wa NHIF, Grace Michael akifafanua jambo kwa wananchi waliofika katika banda la Mfuko huo. 

WAAMUZI 11 WAPATA BEJI ZA FIFA

$
0
0
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limewapatia beji waamuzi kumi wa Tanzania kwa mwaka 2014.

Waamuzi wa kati waliopata beji hiyo ni Ramadhan Ibada, Oden Mbaga, Israel Mujuni na Waziri Sheha.

Waamuzi wasaidizi ni Josephat Bulali, Ferdinand Chacha, Hamis Changwalu, John Kanyenye, Ali Kinduli, Erasmo Jesse na Samuel Mpenzu.

WATATU WAOMBEWA ITC SHELISHELI
Shirikisho la Mpira wa Miguu la Shelisheli (SFF) limetuma Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) maombi ya Hati ya Uhamisho ya Kimataifa (ITC) kwa wachezaji watatu wa Tanzania.

Wachezaji walioombewa hati hiyo ili wakajiunge na timu ya La Passe FC inayocheza Ligi Kuu nchini humo ni Salum Kinje aliyekuwa akiichezea timu ya Simba, Semmy Kessy aliyekuwa Lipuli ya Iringa na Rashid Gumbo aliyekuwa timu ya Mtibwa Sugar.

TFF inafanyia kazi maombi hayo na mara taratibu zitakapokamilika hati hizo zitatolewa.

Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari na Mawasiliano
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images