Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 313 | 314 | (Page 315) | 316 | 317 | .... | 3286 | newer

  0 0

  Mmoja wa wafanyakazi katika ofisi ya Mhandisi wa manispaa ya Dodoma akitoa amri ya kuondoa kimoja ya vibanda vilivyojengwa kiholela katika stendi ya daladala Jamatini wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa vibanda vya wafanyabishara.
   Mhandisi masaidizi manisaa ya Dodoma Luanda akitoa maelekezo kwa mama lishe waliopo katika stendi ya Daladala ya Jamatini kujenga vibanda sawa na vipimo vilivyowekwa sawasawa na utaratibu na sheria ndogo ndogo za manispaa hiyo.
   Mwajuma Salum maarufu Bibi Ndonga (64) akimlalamikia kwa kumuonyesha Mhandisi msaidizi wa manispaa ya Dodoma Luanda stakbadhi ambazo amekuwa akilipia katika kipindi cha miezi miwili bila kukabidhiwa eneo la kuweka kibanda chake cha biashara na viongozi wa eneo hilo mhandisi
  huyo alifika kuona utaratibu uliotumika kujenga vibanda vya biashara.
   Asikari wa kutuliza Ghasia wakiwa na mtutu wa Bunduki kusimamia uhakiki wa vibanda vya wafanyabiashara katika stendi ya Daladala Jamatini Dodoma kama utaratibu uliyowekwa ulifuatwa wakati wa ugawaji na ujenzi.

  PICHA NA JOHN BANDA

  0 0

  Join Us Tomorrow at Hill Park Parking Lot, from 12.00 Noon for a Rotaract Kwanza Car Wash Fundraiser!All at the University of Dar es Salaam. Not to miss! Music, Volunteering and much more. Bring a friend and the car! Each car wash is 5,000 and we are trying to raise 250,000/= to support an orphanage center here in Dar es Salaam.


  0 0

  DC KANGOYE KAZINI
  MKUU wa Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Christopher Kangoye, amesema vijana wakiwezeshwa kikalimifu kushiriki shughuli za uzalishaji, umasikini Tanzania utakuwa historia.


  Pia, amewaasa vijana kutumia elimu walizonazo katika kujiajiri ili kuharakisha maendeleo badala ya kukaa vijiweni na kubaki kuwa walalamishi na wakati mwingine kutumiwa na wanasiasa kama ngazi ya kutimiza malengo yao.
  Kangoye, ambaye amekuwa mhamasisha mkubwa wa vijana nchini, amesema Tanzania inaweza kuwa taifa linalotoa misaada kwa nchi zingine na kuachana na utegemezi iwapo vijana wataitambua na kutumika kikamilifu kwa shughuli za maendeleo.
  Aliyasema hayo juzi wakati alipokuwa akizungumza na vijana katika sherehe za kusimikwa Kamanda wa UVCCM wilaya na makamanda wa Kata wilayani Kongwa, ambapo Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai, alisimikwa kuwa Kamanda wa Vijana wilaya.
  Kangoye, ambaye alikuwa mgeni rasmi, aliema Hayati Baba wa Taifa, Julius Nyerere na Nelson Mandela ni alama ya harakati za vijana katika maendeleo na ukombozi wa Bara la Afrika na kwamba, walianzisha mageuzi hayo wakiwa vijana.
  ‘Vijana wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kukataa umasikini kuanzia ngazi ya familia hadi taifa kwwa kufanya kazi kwa bidii ili kuleta mageuzi ya kiuchumi katikka taifa letu. Tanzania inaweza kuwa taifa linalotoa misaada badala ya kuwa tegemezi iwapo vijana watajitambua na kuitoa kuleta maendeleo.
  ‘Muda wa kukaa vijiweni na kuilalamikia serikali haupo, tuna fursa na rasilimali nyingi zinazoweza kuleta mageuzi ya kiuchumi na kutufanya kuwa taifa tajiri,’ alisema Kangoye.
  Alisema harakati zozote ziwe na kisiasa, kiuchumi na kijamii huanzia kwwa vijana na kwamba, ni wakati sasa wa kuamka na kuleta mageuzi kwa maslahi na ustawi wa Tanzania ya sasa na inayokuja.
  Naye Ndugai akizungumza baada ya kusimikwwa kuwa Kamanda wa Vijana wilayani humo, aliungana na Kangoye kwa kuwataka vijana kujituma katika shughuli za uzalishaji ili kuacha kuwa tegemezi.
  Alisema kuna vijana wengi wenye elimu na ujuzi wa kutosha, lakini hawataki kufanya kazi na badala yake wanasubiri serikali iwafanyie kila kitu, jambo ambalo amesema haliwezekani.

  ‘Tufanye kazi ndugu zangu ili tuachane na umasikini na kuwa tegemezi, fursa zipo za kutosha kinachotakiwa ni kuamua kama alivyosema DC Kangoye ili tulete mageuzi kwenye taifa letu’ alisema.


  Katibu wa UVCCM Wilaya ya Kongwa, Asia Alamga, alisema kabla ya kuwasimika makamanda hao walifanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwa ni pamoja na kutembelea wafungwa, wagonjwa kwenye hospitali za wilaya na kata na kutoa misaada ya kijamii.

  0 0

  Makamu mwenyekiti taifa wa chama cha mapinduzi (CCM) Phillip Mangula amewataka viongozi wa matawi kusimamia ipasavyo kanuni za uchaguzi na uongozi na maadili wa chama hicho kwa kupiga vita rushwa hasa kuelekea katika chaguzi za serikali za mitaa zinatarajiwa kufanyika mwaka huu.

  Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dar es salaam katika salama za mwaka wakati akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu ya tawi la ofisi ndogo za chama hicho lilipo Mtaa wa Lumumba.

  Amewataka viongozi hao kuweka misingi mizuri ambayo itawezesha kupatikana viongozi wazuri ambao hawatokani na mianya ya rushwa ili kuwa na dira nzuri kuelekea katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika 2015.

  “Nataka kanuni za uchaguzi na uongozi na maadili ziheshimiwe ili kupata viongozi ambao hawatatokana na rushwa, na hakikisheni katika vikao vyenu vya chama mnasimamia agenda mbili ambayo ni uchaguzi na kujadili mwenendo wa katiba mpya”.

  “Mkifuatilia hatua moja hadi nyingine katika mchakato wa kuipata katiba kuanzia ushiriki wa wajumbe wa bunge maalum hadi katika mjadala wa wajumbe wakipitia kifungu kimoja hadi kingine mtakuwa na nafasi kubwa ya kutoa maoni yenu pale itakaporudi kwa wananchi,”alisema Mangulla.

  Akizungumzia uwepo wa serikali tatu katika rasimu ya katiba mpya, Mangula amesema bado ni mapema mno kuzungumzia hatia ya suala hilo kwani mchakato wa kuipata katiba bado mrefu ambao mbali na wawakilishi wa bunge maalumu la katiba utashirikisha tena wananchi ambao watapiga kura yao ya mwisho.

  Mbali na kuwapongeza tume ya katiba mpya kwa kufanya kazi kwa uwazi, amewapongeza wanachama wa ccm kwa jinsi walivyoshirikia ama mmoja mmoja au katika kundi katika kuhakikisha wanatoa maoni yao katika rasimu ya katiba ambayo imewasilishwa kwa Rais Jakaya Kikwete mwishoni mwa mwaka jana.

  0 0

  Kwako michuzi na wato wote wanaoitakia mema nchi yetu, 
  Naandika hii nikiwa na hasira iliyochanganyika na majonzi. Yaani hata sijui nianzie wapi. Awali ya yote naomba urudishe ukurasa wa kwanza zile picha za uharibifu wa barabara ulizoposti majuzi. 
  Mimi niko hapa Sao Paulo huku Brazil. Nilistushwa sana sana na picha hizo pamoja na maelezo yake, kadhalika na maoni ya wadau wako. Ni dhahiri wengi ya wadau wako aidha ni kuendeleza tu tabia ya kubeza na kuponda kila kilicho mbele yao ama ni kwa sababu hawana habari ya kinachoendelea. 
  Katika research niliyofanya katika mitandao ya kijamii na ya magazeti juu ya swala hilo, nimejikuta nafikia mahali kuamini kuwa swala hili halina tofauti na lile la Operesheni Tokomeza, ambapo mawaziri wane wamemwaga unga hivi hivi kiutani utani, japo hawahusiki moja kwa moja. Hii inaitwa uwajibikaji. 
  Siku chache baadaye nimesoma Wizara ya Maliasili na utalii ikitamka kuwa baada ya kusitishwa kwa Operesheni Tokomeza, Tembo wawili huuwawa na majandili kila siku. Hii haiukubaliki, kilichokosewa na kirekebishwe haraka na ianze tena kama alivyoahidi JK. 
  Kwa upande wa barabara sioni kama kuna sababu ya Waziri Magufuli awajibike, kwa maana yeye amekuwa mstari wa mbele kusimamia sheria kibao kamataarifa hii niliyosoma mahali kuwa Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli, amesema ataendelea kusimamia sheria ya barabara namba 30 ya mwaka 1973 hadi anaingia kaburini kwa kuhakikisha hakuna magari ambayo yanazidisha uzito na kuharibu barabara.
   “Nchini Ujerumani, uzito wa magari yote ni tani 40, Uingereza tani 40, Ufaransa 40, Urusi 38 lakini Tanzania tani 56, wakati mwingine tunakamata hadi tani 96,” aliongezea kwa kuwaga data kama kawaida yake katika taarifa hiyo. 
  Hata hivyo nimesoma mahali pengine tena kuwa miezi miwili iliyopita Waziri Mkuu alisema sheria hiyo ilegezwe ili tume iundwe. Yaani magari yenye uzito yaendelee kutanua tukisubiri tume! 
  JAMANI! HIVI KWELI TUSUBIRI TUME IUNDWE WAKATI BARABARA ZINAKUFA HIVI HIVI TUNAANGALIA KWA MANUFAA YA WACHACHE??? LET’S BE SERIOUS FOR ONCE! 
  Hilo kaka halikubaliki. Nashauri wakati tume hiyo ikisubiriwa kuundwa (hata sijui ya kazi gani katika kuzuia uharibifu wa barabara, maana data hapo juu zinatusha) Dokta Magufuli aruhusiwe aendeleze juhudi zake za kukomboa barabara zetu. 
   Nasema hivi kwa sababu kama ilivyo katika kusitishwa Operesheni Tokomeza, barabara zetu zinaangamia kwa kilomita kibao kila dakika. Nimesoma mahali pengine kuwa gharama za kukarabati hizo barabara zilizoathirika kwa uzito wa magari ni takriban dola bilioni 350 ambazo ni hela za walipa kodi. Hili halikubaliki asilani!!! 
  Namalizia kwa kumuomba Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Peter Kayanza Pinda afikirie upya swala la kulegeza sheria. Hapana. Asifikirie bali achukue hatua za haraka sana chini ya kauli mbiu ya BIG RESULTS NOW! 
  Mdau Nehemia
  Sao Paulo, Brazil
   Taswira hizi ni za barabara ya Morogoro road ambako sehemu kibao zimeharibika bila shaka kutokana na  uzito wa magari. Mwenye data atusaidie....


  0 0

  Familia ya Hayati Jenkins Kafumba wa Kanisa Road, Chang’ombe, Dar es Salaam, inasikitika kutangaza kifo cha mama yao mzazi, Mama Grace Kafumba kilichotokea asubuhi ya leo, Ijumaa, Januari 3, 2014, katika Hospitali ya Tumaini mjini Dar es salaam.

  Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Kanisa Road, Dar es Salaam.

  Habari ziwafikie ndugu, jamaa na marafiki wote walioko Bagamoyo, Malawi, Canada, Uingereza, Afrika Kusini na popote pale walipo.  Bwana alitoa na Bwana ametwaa. 
  Jina lake na lihimidiwe.
  AMINA

  0 0

  Mbunge Amina Mwidau, akimkabidhi kikombe cha ushindi Nahodha wa timu ya APL Mwera Shabani Athuman, baada ya timu hiyo kutawazwa kuwa mabingwa wa ligi ya Mwidau CUP, mjini Pangani leo.
   Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga, Amina Mwidau (CUF), akihutubia kabla ya kuchezwa kwa fainali kati ya timu ya APL Mwera na Torino (kulia) ni Katibu wa Chama cha Soka Wilaya ya Pangani, Salehe Swazi.
   Mgeni rasmi katika Mashindano ya Mwidau CUP, Amina Mwidau akijadiliana na viongozi wenzake wakati wa mchezo wa fainali ya Mwidau CUP kati ya APL Mwera dhidi ya Torino leo mjini hapa.
  =========     ========  =========
  APL Mwera yaibuka kidedea Mwidau CUP

  Na Mwandishi Wetu, Pangani.

  TIMU ya Soka la APL kutoka Kata ya Mwera, imetoka kifua mbele huku wakitangazwa mabingwa wapya wa kombe la Mwidau CUP. Timu hiyo iliibuka na ushindi dhidi ya timu ya Torino ya mjini Pangani, ambayo ilishindwa kufua dafu kwa kufungwa kupitia penati.

  Hadi dakika tisini za mchezo huo wa fainali hiyo ya Mwidau CUP zinamalizika timu zote zilishindwa kutambiana na kulazimika kutoka suluhu ya bao 1-1.

  Kutokana na hali hiyo timu hizo ilizilazimu kuingia katika hatua ya matuta ambap kati ya penati nne zilipingwa kwa kila timu, Torino ilipoteza penati mbili huku APL Mwera ilipoteza moja hali hiyowafanya kuibuka na ushindi na kutawazwa mabigwa wa ligi hiyo.

  Timu hizo hadi zinakwenda mapumziko katika kipindi cha kwanza kila timu ilitoka huku ikishindwa kuona nyau ya mwenzake lakini ilipofika dakika ya 57, mchezaji Christopher Gunda wa APL alifanikiwa kuziona nyavu za Torino. Hata hivyo katika dakika ya 62 Torini ilijibu mapigo na kusawazina bao hilo ambapo hadi dakika 90 timu zote zilishindwa kutambiana na kuamua kupigwa matuta.

  Awali akihutubia kabla ya kuanza kwa mchezo huo mgeni rasmi katika mashinda hayo ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga, Amina Mwidau (CUF), aliwataka vijana kuthamini michezo kwani ajira ambayo imekuwa na manufaa kwa Taifa.

  “Kwa imani yangu ninaamini hata hapa Pangani tunao wachezaji wazuri kupitia timu zetu hizi zilizoshiriki ligi hii ya Mwidau CUP ambao wana uwezo wa kufanya vizuri katika timu kubwa za ndani na nje ya nchi yetu,” alisema Mwidau


  0 0  Aida Nakawala 25 mkazi wa kijiji cha Chiwanda Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya, hivi karibuni alijifungua watoto wanne  mapacha kwa mkupuo(Quadliplets) katika usiku wa kuamkia Mwaka mpya anaendelea vizuri.  Mwanamke huyo ambaye kwa hivi sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wazazi ya Meta akiwa na watoto wake wote wanne alijifungua majira ya saa 10 alfajiri usiku wa kuamkia Januari Mosi Mwaka huu katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi na watoto wakiwa na uzito wa kawaida tofauti na matarajio ya Wengi.

  Muuguzi na msimamizi wa Watoto katika chumba cha Joto Sista Frolence Maisa amesema hali za watoto ni nzuri ambapo mama mzazi anahitaji kupatiwa vyakula vinavyoweza kumuongezea maziwa mengi kutokana na idadi ya watoto aliyonayo.


  kikosi cha blog ya Mbeya yetu  Kikiongozwa na Joseph Mwaisango ambacho kilifika kumjulia hali kiliguswa na hali hiyo na kujitolea kamsaada kidogo wa nguo za watoto sabuni  chupa na dishi  hivyo kuwaomba wadau wengine kumsaidia mama huyo ili aweze kuwalea vizuri watoto wake.

  Katibu msaidizi wa hospitali ya  Rufaa Mbeya Mwansasu akipokea msaada huo kwa niaba ya mzazi
  KATIKA hali isiyokuwa ya Kawaida Mwanamke mmoja, Aida Nakawala 25 mkazi wa kijiji cha Chiwanda Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya, hivi karibuni alijifungua watoto wanne  mapacha kwa mkupuo(Quadliplets) katika usiku wa kuamkia Mwaka mpya anaendelea vizuri.'

  Mwanamke huyo ambaye kwa hivi sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wazazi ya Meta akiwa na watoto wake wote wanne alijifungua majira ya saa 10 alfajiri usiku wa kuamkia Januari Mosi Mwaka huu katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi na watoto wakiwa na uzito wa kawaida tofauti na matarajio ya Wengi. 

  Kwa mujibu wa Muguuzi wa Hospitali ya Wilaya ya Mbozi aliyemfanyia huduma mwanamke huyo, Grace Konga alisema mzazi huyo ni miongoni mwa wazazi 9 waliojifungua katika Mkesha wa Mwaka mpya huku yeye akivunja rekodi kwa kujifungua watoto wanne kwa njia ya kawaida. 

  Muuguzi huyo alisema watoto hao walizaliwa wakiwa na uzito uliotofautiana kwa mtoto  wa kwanza hadi wa mwisho kuanzia kilogramu 1.6,1.5,1.5  na  2.0 ambapo baada ya kuona hali hiyo ilibidi kumpa rufaa kwa ajili ya msaada zaidi katika Hospitali ya wazazi ya Meta ambapo wapo katika Chumba cha Joto hadi sasa. 

  Aidha kwa mujibu wa Muuguzi na msimamizi wa Watoto katika chumba cha Joto Sista Frolence Maisa amesema hali za watoto ni nzuri ambapo mama mzazi anahitaji kupatiwa vyakula vinavyoweza kumuongezea maziwa mengi kutokana na idadi ya watoto aliyonayo. 
  Alisema kwa hivi sasa watoto wananyonya vizuri amb  po maziwa yakipungua kwa mama itahitajika msaada wa maziwa ya Kopo aina ya Laktojeni ili watoto waendelee kupatiwa maziwa kama kawaida na afya zao kuimarika.

  Kwa upande wake Mzazi wa watoto hao Aida Nakawala alisema hali yake kiuchumi siyo nzuri kuweza kumudu kuwalea watoto hao na kuongeza kuwa mume wake ni mkulima aliyemtaja kwa jina la Web Simkanda hivyo anaomba msaada wa hali na mali kutoka kwa wasamaria wema.

  Alisema huo ni uzao wake wanne ambapo mtoto wake wa kwanza anaumri wa miaka saba, anayefuata ana miaka miwili na miezi tisa huku mwingine akiwa amefariki dunia mara baada ya kujifungua kabla ya uzao huu unaofanya kuwa na watoto Sita.

  Alipoulizwa kuhusu kuwepo kwa hali kama hiyo ya kujifungua watoto zaidi ya mmoja katika familia yao alisema Mama yake mzazi amewahi kujifungua mapacha wawili tu na hakuna mtu mwingine aliyewahi kuzidisha idadi hiyo ya watoto kama yeye .

  Hata hivyo kutokana na kuguswa kwa  mahitaji ya binti huyo na wanawe kikosi cha blog ya Mbeya yetu ambacho kilifika kumju ulia hali kiliguswa na hali hiyo na kujitolea kamsaada kadogo hivyo kuwaomba wadau wengine kumsaidia mama huyo ili aweze kuwalea vizuri watoto wake.

  0 0

   
   Mmoja wa wanachama watatu wa CHADEMA waliovuliwa nafasi zao za uongozi ndani ya chama, Zitto Kabwe kupitia kwa Wakili wake, Alberto Msando,jana ameanza kufanya ‘FORUM SHOPPING’ kwa kupeleka maombi Mahakama Kuu ya Tanzania, akiomba Kamati Kuu isijadili na kuamua jambo lolote kuhusu uanachama wake, kwenye kikao maalum kinachofanyika leo.

  Awali muombaji kwa namna ambayo inaweza kuitwa kuwa ni kuvizia, alitaka Mahakama Kuu hiyo itoe amri kutokana na ombi lake hilo, bila upande wa chama kuwepo mahakamani, lakini kwa bahati nzuri mawakili wa chama, Mwanasheria Mkuu wa chama, Tundu Lissu na Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu, Peter Kibatala; wakafanikiwa kuwepo kortini, hivyo wakawa-served maombi hayo kisha mahakama ikalazimika kusikiliza Preliminary Objections (PO) kutoka kwa mawakili wa CHADEMA dhidi ya waleta maombi.

  Maombi hayo ya wakili Msando kwa niaba ya Zitto yamefunguliwa mahakamani dhidi ya Baraza la Wadhamini CHADEMA na Katibu Mkuu wa Chama.

  Hoja za mawakili wa CHADEMA katika PO zilikuwa ni katika maeneo matatu ambayo ni vifungu vya kisheria ambavyo waombaji walikosea;

  1. Vifungu vya sheria walivyotumia waombaji kuomba court injunction, haviipatii Mahakama Kuu mamlaka ya kufanya maamuzi hayo wanayoomba ifanye. Kwa sababu kwa ujumla ukikosea vifungu hasa vinavyohusu msingi wa kesi, ni sawa na kwamba hakuna kesi.

  2. Hati ya kiapo ya waleta maombi haikuwa na facts kama inavyotakiwa badala yake ilikuwa imejaa maneno ya ubishi ubishi.

  3. Mahakama haiwezi ku-entertain kusikiliza migogoro ya ndani katika vyama vya hiari mf; vyama vya siasa, dini na michezo (ambavyo uanachama wake ni wa hiari), kwa sababu mojawapo ya principle ni kwamba ili mtu awe mwanachama anakuwa amekubaliana na katiba, kanuni, taratibu na makatazo ya chama husika.

  Aidha katika maombi yake kuna vitu vingine ‘muhimu’ ambavyo mleta maombi amejikuta akivionesha kuwa anakubaliana na taratibu za chama lakini wakati huo huo tena anataka mahakama imsikilize;

  · Amekiri kuwa amevuliwa nafasi za uongozi na amekata rufaa

  · Amekiri kuwa ameandikiwa mashtaka kwa maandishi na yeye amejibu

  · Amekiri kuwa ameandikiwa kuitwa mbele ya kikao cha Kamati Kuu ili asikilizwe utetezi wake kwa mdomo.

  Kwa maneno yake hayo ni kwamba anakubaliana na na process ya chama na kwamba anajua atasikilizwa lakini tena wakati huo huo anataka mahakama imsikilize. Huo ndiyo msingi wa Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA kusema kuwa kuhangaika huko ni sawa na kufanya ‘FORUM SHOPPING’.

  Mleta maombi angeweza kuwa na hoja katika maombi yake iwapo angeona kuna breach of natural justice kwenye suala lake. Kitu ambacho hakijatokea na hata yeye kwenye maelezo yake anakiri hivyo.

  Uamuzi wa Mahakama Kuu

  Katika uamuzi wake, Jaji Utamwa amesema chama kitaendelea na shughuli zake kama kawaida.

  Hivyo kikao maalum cha Kamati Kuu kilichopangwa kufanyika kesho Januari 3, 2014, kitafanyika na kitajadili agenda zote (kama zilivyotolewa awali) na masuala yote yanayohusu uendeshaji wa chama, isipokuwa hakitajadili na kuamua kuhusu uanachama wa Zitto pekee, hadi Mahakama Kuu itakaposikiliza ombi lake kesho saa 3 asubuhi.

  Imetolewa na-

  Kurugenzi ya Habari-Chadema

  0 0
  0 0

  Sarafu ya thamani ya sh 50,000 iliyotengenezwa kwa madini ya fedha kwa asilimia 92.50
  Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Benno Ndulu
  ---
   BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa sarafu maalumu ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye thamani ya sh 50,000. Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu, amesema kuwa sarafu hiyo iliyotengenezwa kwa madini ya fedha kwa asilimia 92.50, imetolewa kwa ajili ya kumbukumbu tu na haitaingizwa katika mzunguko wala kutumika kwa kulipia malipo ya aina yoyote.
   Sarafu hii imetolewa maalumu kama maadhimisho ya miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar, haitatumika kwa manunuzi. Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki ya BoT ilimnukuu Profesa Ndulu akisema sarafu hiyo imetolewa kwa idadi ya vipande 3,000 kwa ajili ya tukio hilo na kuwahimiza wananchi kuinunua kwa ajili ya kumbukumbu hiyo.
  Kwa mujibu wa Gavana Ndulu, kutolewa kwa sarafu hiyo kunakwenda sambamba na utaratibu wa Benki Kuu kutoa sarafu maalumu za aina hiyo kama sehemu ya maadhimisho ya kumbukumbu ya matukio mbalimbali muhimu ya kitaifa na kimataifa.
  “Kwa kawaida, baada ya muda, thamani ya sarafu kama hizi huongezeka na kuwa na faida zaidi kwa wanaozimiliki,” alisema Profesa Ndulu.
  Gavana Ndulu alieleza sarafu hizo zitapatikana Januari 5 kwa bei ya sh 50,000 katika matawi ya benki za biashara zitakazokuwa zimepata sarafu hizo kutoka Makao Makuu ya Benki Kuu, Dar es Salaam na matawi ya Benki Kuu yaliyoko Zanzibar, Arusha, Mbeya na Mwanza.
  “Benki za biashara zinaweza pia zikasambaza sarafu hizi kupitia matawi yake,” alisema gavana na kuongeza taarifa za usambazaji zitatolewa na benki hizo.
  Katika sarafu hiyo, upande wa mbele unaonyesha sura ya hayati Sheikh Abeid Aman Karume na maandishi yanayosomeka: ‘Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi’.
  Upande mwingine wa sarafu unaonyesha nembo ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, maandishi yanayosomeka: “Miaka Hamsini ya Mapinduzi”, thamani ya sarafu na miaka 1964-2014.  0 0

   Makamanda na Wapiganaji wa Jeshi la Magereza wakiwa katika sherehe ya kuukaribisha Mwaka mpya wa 2014 usiku wa kuamkia leo  katika Viwanja vya Bustani ya Bwalo Kuu la Maafisa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam
   Maofisa na Askari wa Jeshi la Magereza wakipita mbele ya Mgeni rasmi kwa ajili ya kutosti glasi za vinywaji katika Sherehe ya kuukaribisha Mwaka mpya wa 2014.
    Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akimpongeza mmoja wa Maofisa wa Jeshi la Magereza, Stafu Sajin Luckson Mtenga ambaye amezawadiwa zawadi ya Kipoza joto kutokana na kutenda kazi zake kwa kujituma na kuonesha nidhamu kiutendaji kwa Mwaka uliopita  wa 2013.
  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akitoa hotuba fupi kwa Maofisa wa Jeshi la Magereza (hawapo pichani) katika sherehe za kuaga Mwaka 2013 na kuukaribisha Mwaka mpya wa 2014. Sherehe hizo zimefanyika usiku wa kuamkia leo  katika Viwanja vya Bustani ya Bwalo Kuu la Maafisa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam. Picha na Inspekta Lucas Mboje

  0 0

  DAR ES SALAAM, Tanzania.

  MAKAMU Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula amecharuka na kusema kwamba Wana-CCM ambao wameanza sasa kutangaza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwakani, ni wasaliti wakubwa ndani ya Chama.

  Mangula, ametoa karipio hilo, leo (jana) wakati akitoa Salamu za Mwaka Mpya wa 2014 katika mkutano wa dharura wa Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi Tawi la Ofisi Ndogo ya Makao Makuu jijini Dar es salaam.

  Huku akinukuu kanuni zinalzolinda Maadili ya Uchaguzi na uteuzi wa wagombea ndani ya Chama, Mangula, alisema hadi sasa hakuna kikao chochote cha ngazi ya juu cha Chama, kilichoruhusu wanachama kuanza kutangaza nia za kugombea uchaguzi hadi pale itakapofika mwaka 2015.

  Makamu huyo wa CCM (Bara), alisema, wanachama wanaojipitisha sasa kwa wananchi kwa namna moja au nyingine kwa lengo la kutangaza nia ya kuwania nafasi katika uchaguzi mkuu ujao, ilihali muda wa kufanya hivyo haujafika ni wasaliti au waasi ndani ya Chama.

  Mangula alisema, wanaofanya hivyo ni waansi na wasaliti wakubwa kwa sababu wanaibua na kuendeleza makundi mapemba huku wakijua kwamba hali hiyo hukifanya chama kuwa na wakati mgumu wakati wa uchaguzi.

  Kutokana na hali hiyo, amesisitiza kuwa Chama, hakipo tayari kuona au kuwavumilia watu wachache ndani ya Chama wanaoendelea kuvuruga umoja, mshikamano na misingi ya Chama kwa sababu tu ya umangimeza na uroho wa madaraka uliokiuka kiwango.

  Mangula aliwataka wana-CCM na kwa jumla wakiwemo hao wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, kuzingatia wakati wote misingi mizuri ambayo itawezesha kupatikana viongozi wazuri ambao hawatokani na mianya ya rushwa ili kuwa na dira nzuri kuelekea katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika 2015.HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

   TAARIFA YA  KUAHIRISHA SAFARI YA TRENI YA
  ABIRIA KWENDA BARA HADI JUMAPILI JANUARI 05, 2014

   
  Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL unawatangazia abiria wote na wananchi kwa jumla  kuwa kutokana na sababu za kiufundi unasikitika kuwa treni ya abiria iliyopangwa kuondoka jana  Ijumaa Januari 03, 2014 saa 3 usiku  imeahirishwa  hadi  kesho Jumapili Januari 05  Machi 16, 2013, saa 3 usiku.

  Taarifa imefafanua kuwa kutokana na mvua kunyesha mkoani Dodoma na mikoa jirani eneo  kati ya stesheni za reli ya kati za Gulwe na Godegode zimejaa maji na kufunika njia ya reli mkesha wa mwaka mpya wa 2014!.
  Tokea juzi Januari  02, 2014 Wahandisi na mafundi wa kampuni za TRL na Rahco kwenye sehemu husika wakifanya tathmini  na kusimamia ukarabati wa maeneo mawili  reli  yaliyoharibika.

  Kwa mujibu Mkururgenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Kipallo Amani Kisamfu anayeongozwa kikosi kazi cha kukarabati amesema kazi ya ukarabati inafanywa usiku na mchana kuona huduma zinaanza mapema iwezekanavyo ikiwemo huduma ya  usafiri  wa treni za abiria uliopangwa kuanza tena hapo kesho Jumapili Januari 05, 2014.

  Kutokana na dharura hii treni za kutoka Mpanda, Kigoma na Mwanza kuja Dar zimebadilishiwa muda na siku ya kuondoka hivyo basi,  badala ya kuondoka jana Ijumaa Januari 03, 2014 sasa zitaondoka kesho Jumapili Januari 05, 2014 saa 2 asubuhi.

  Aidha taarifa  hii iwafikie wadau wote wa usafiri na huduma ya reli ya kati na kwamba uongozi wa TRL unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza..

  Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mhandisi Paschal Mafikiri.
  TRL Makao Makuu,
  Dar es Salaam.
  Januari 04, 2014

  0 0


  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na uongozi wa Wilaya ya Nkasi alipotembelea shamba la shule ya Msingi Matala ambalo pia linatumika kama shamba darasa ukiwa ni mpango ulioanzishwa na uongozi wa Mkoa wa Rukwa kusaidia elimu ya kilimo mashuleni na kusaidia upatikani wa chakula kwa wanafunzi. Katika mpango huo kila shule Mkoani Rukwa imetakiwa kuwa shamba ekari zisizopungua tano ambazo zitapatiwa ruzuku ya pembejeo inayotolewa na Serikali na kusimamiwa na afisa ugani wa eneo husika na kuwa shamba la mfano kwa wananchi katika Kilimo bora.
  Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta akimuongoza Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi unaondelea wa mradi wa maji katika kijiji cha Matala Wilayani humo jana.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Matala Wilayani Nkasi jana. Mradi huo unaofadhiliwa na Serikali, mpaka kukamilika kwake utatumia zaidi ya Tshilingi milioni 300. Jumla ya vijiji kumi (10) katika wilaya ya Nkasi vinategemewa kupata maji ya uhakika kutokana na miradi inayoendelea ambapo zaidi ya Tsh. Bilioni tisa zimeshatengwa kukamilisha ujenzi wake. Changamoto zinazoikabili miradi hii ni kuchelewa kwa fedha kutoka Wizara ya maji pamoja na uhaba wa mabomba na viungio vyake kutoka viwandani.
  Picha ya pamoja.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akimkabidhi jezi Kapteni wa Timu ya Matala FC Filbert Ndiela kama moja ya kampeni zake Mkoani Rukwa kuhamasisha michezo kwa vijana, ujasiriamali na kujituma katika shughuli za maendeleo. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta. Katika hotuba yake Injinia Manyanya alitoa onyo kali kwa wananchi wenye tabia ya kulima kwenye vyanzo vya maji na kuwaomba wananchi kujali afya zao kwa kujitolea kupima VVU na kinamama wajawazito kujifungulia kwenye vituo vya afya au zahanati.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya baada ya hotuba yake na kabla ya kuondoka kwenye mkutano wa hadhara wananchi walimuomba awachezee ngoma yao ya kabila la kifipa ambayo aliitendea haki vilivyo kama anavyoonekana pichani kulia. (Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akikata utepe kufungua Kituo cha Afya Bumbwini Kiongwe,Jimbo la Bumbwini Wilaya ya Kaskazini B,Mkoa wa Kaskazini Unguja jana,katika shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akifungua pazia  kukifungua Kituo cha Afya Bumbwini Kiongwe,Jimbo la Bumbwini Wilaya ya Kaskazini B,Mkoa wa Kaskazini Unguja jana,katika shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar,(kulia) Waziri wa Afya Juma Duni Haji.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Daktari dhamana Abdulwahab  Mohamed,baada ya kukifungua Kituo cha Afya  Bumbwini Kiongwe,Jimbo la Bumbwini Wilaya ya Kaskazini B,Mkoa wa Kaskazini Unguja jana,katika shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar,
    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimuuliza suala Daktari wa huduma za Mama na  Mtoto,Halima Abdalla Saidi,wakati alipotembelea sehemu mbali mbali zinazotoa huduma katika kituo cha Afya Bumbwini Kiongwe,Jimbo la  Bumbwini Wilaya ya Kaskazini B,Mkoa wa Kaskazini Unguja,baada ya  kukifungua jana,katika shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.

  0 0

  Waziri Mkuu, MIzengo Pinda  akizungumza na wazee wa Mpanda, kijijini kwake, Kibaoni wilayani Mlele leo Januari  4, 2014.

  0 0

   Mgeni rasmi ambaye ni Kamishna wa Fedha na Utawala, Gaston Sanga akiwasalimu Wanabonanza wa Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Dar es Saalam(hawapo pichani) kwa Kauli mbiu ya "Familia Kwanza" kabla ya kuzindua rasmi "Family Bonanza" lililoandaliwa na Maofisa, Askari wa Jeshi la Magereza wa Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Dar es Salaam pamoja na familia zao. Bonanza hilo limejumuisha Michezo mbalimbali ikiwemo Mpira wa Wavu, Mpira wa Pete, Mpira wa Miguu, Kukimbia na Gunia na Kuvuta Kamba.
   Bendi ya Jeshi la Magereza ikiongoza Maandamano Maalum yaliyoandaliwa na Wanabonanza wa Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Dar es Salaam wakiingia rasmi katika Viwanja vya Michezo vya Chuo Ukonga kabla ya uzinduzi rasmi wa Bonanza hilo ambalo limezinduliwa leo Januari 04, 2014 na Kamishna wa Fedha na Utawala, Gaston Sanga
   Kamishna wa Fedha na Utawala, Gaston Sanga akikagua Kikosi cha Timu cha Maafisa na Askari wa Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Dar es Salaam kabla ya kuchuana vikali na Timu ya Wanafunzi wa Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga wanaosomea Stashahada ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo Januari 04, 2014 katika Viwanja vya Michezo vya Chuo hicho.
   WakinaMama wa Kambi ya Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga wakichuana vikali katika Mchezo wa kuvuta kamba iliyowahusisha na Maafisa Wanawake wa Jeshi la Magereza wanaofanya kazi Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Dar es Salaam leo katika Bonanza hilo.
  WakinaMama wa Kambi ya Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga wakichuana vikali katika Mchezo wa kukimbia na Gunia wakati wa "Family Day Bonanza" lililohusisha Maofisa, Askari pamoja na familia zao. Bonanza hilo limefanyika leo Januari 04, 2014 katika Viwanja vya Michezo vya Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Dar es Salaam(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

  0 0

  Haya sasa… Mchakato wa Kupata Washiriki 30 wa Maisha Plus
  Na washiriki 10 wa Mama Shujaa wa Chakula , 2014 Umeanza!

  Fomu zinapatikana: 

  IRINGA - EBONY FM 87.8
  SONGEA- JOGOO FM 93.0
  SHINYANGA- FARAJA FM 21.3
  ZANZIBAR - ZENJI FM 96.8
  MOROGORO- ABOOD RADIO 89.7
  MWANZA- PASSION FM 99.9
  MTWARA- PRIDE FM 87.8
  BUKOBA- RADIO VISION 98.0FM
  MBEYA- BOMBA FM 104.0
  TABORA- CG FM 89.5
  DODOMA – IMPACT FM 94.4
  ARUSHA- RADIO 5 104.5

  Pamoja na ofisi  za zifuatazo: ..... ACTIONAID,ADGL KIVULINI, CONCERN, COWEA, CVM/APA, KICKSTAR-Money Maker, LBTIC, INADES FORMATION, NORWEGIAN CHURCH AID, OXFAM, SHDEPHA+, RISE TANZANIA,TREE OF HOPE, SASA Foundation, PWC, UZIKWASA, ADP Mbozi, VSO Tanzania, WOPATA, WOWAP, WOMEN PARALEGALS, KAWOCONET, MZALENDO PUB kwa Dar es Salaam.

  Nani Anapaswa kuchukuwa Fomu:
  Mama Shujaa:  Wakina Mama na wasichana Wakulima na Wafugaji, kuanzia miaka 18 na kuendelea

  Maisha Plus:  Vijana, wasichana na wavulana kuanzia umri wa miaka 21 mpaka 26

  fomu hizi zinaweza kujazwa moja kwa moja kupitia tovuti yetu ya www.maishaplus.tv na kupitia Facebook.com/MaishaPlus

  Mwisho wa kurudisha Fomu ni: Tarehe 24 Mwezi wa Kwanza 2014

  Mwaka huu kutakuwa na washiriki Maisha Plus kutoka Burundi, Rwanda, Uganda, Kenya pamoja na Tanzania.


  Wahi kuchukua fomu yako sasa ujishindie Mamilioni ya Pesa.   
  MAISHA PLUS/MAMA SHUJAA WA CHAKULA 2014


older | 1 | .... | 313 | 314 | (Page 315) | 316 | 317 | .... | 3286 | newer