Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 311 | 312 | (Page 313) | 314 | 315 | .... | 3285 | newer

  0 0

  Baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya awali ya ukocha waliokabidhiwa vyeti vya kozi hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na vyeti vyao. (picha zote na Denis Mlowe).
   Baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya awali ya ukocha waliokabidhiwa vyeti vya kozi hiyo kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa shule ya kimataifa ya Southern Highland Kitova Mungai.

   Mwenyekiti wa Chama cha Soka Wilaya ya Mufindi Gervas Choga akimkabidhi cheti ya kozi ya awali ya ukocha Lupyana Massawe, kulia ni mkurugenzi wa Hazina Foundation William Mungai makabidhiano yaliyofanyika katika ukumbi wa John's Corner mjini Mafinga. 

  ==========  =========  ===========

  WAKABIDHIWA VYETI VYA UKOCHA WA AWALI


  Na Denis Mlowe, Mufindi


  ASASI isiyo ya Kiserikali ya Hazina Foundation iliyoko Mafinga imekabidhi vyeti 26 kwa wahitimu wa kozi ya awali ya ukocha kwa walimu wa Shule za Msingi na Sekondari wa Wilaya ya Mufindi.


  Akikabidhi vyeti hivyo Mwenyekiti wa Chama cha Soka Wilaya ya Mufindi Gervas Choga aliwataka wahitimu hao kwenda kuvumbua vipaji vilivyojificha mashuleni na kuwaendeleza soka katika wilaya ya Mufindi.


  Alisema mafunzo waliyopata ni muhimu sana kwa maendeleo ya soka la wilaya ya hiyo na taifa kwa ujumla na serikali inatakiwa kuwekeza  katika michezo na kuondokana na siasa iliyotawala sasa kwa watu wengi kujiingiza katika mpira kwa lengo la kupata umaarufu na mwisho kujiunga katika siasa.


  Choga alisema vipaji vya soka vinaanzia shule za msingi hivyo ni jukumu la kila mmoja wenu kuweza kuandaa michezo ya kila mara katika shule mnazofundisha na maeneo yanayowazunguka.


  “Nitahakikisha kila mmoja wenu anayafanyia kazi mafunzo haya na hakuna hata mmoja nisiyemjua hivyi katibu nakuagiza wafatilie wahitimu hawa na kuona wanafanya jambi kuhusu soka la wilaya yetu linakuwa, naomba vijana mtusaidie katika kuendeleza soka kwa kupitia mafunzo mliyopata” alisema Choga


  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Hazina Foundation,William Mungai aliwataka wahitimu kuyatendea haki mafunzo hayo kwa kuwafundisha watoto mpira wa kisasa kuweza kufikia malengo ya kukuza soka la Mufindi na Taifa kwa ujumla.


  Wiliam Mungai alisema mafunzo ya ukocha yatakuwa endelevu kwa walimu na wadau mbalimbali watakohitaji kujifunza ukocha ngazi ya awali na asasi ya Hazina itagharamia mafunzo hayo kwa vijana wa wilaya hiyo.


  Alisema mafunzo hayo yanatakiwa kuanzia ngazi ya chini na bila kubagua jinsia kwa  kufundisha vijana wenye uwezo n kuthamini mpira wa miguu kunakuwa na faida kubwa na manufaa kwa vizazi vijavyo


  Wiliam Mungai iliitaka serikali kuwekeza katika vyuo vyingi vya ufundishaji michezo kwa faida ya miaka ijayo katika kukuza michezo na kuongeza pato  la Taifa.


  “Naomba sana  vijana wangu mwende mkafundishe soka la kisasa kwa vijana wetu nategemea sana kila mwaka kuongezeka kwa vipaji katika wilaya yetu na msiishie hapa na kozi hii ya awali mjiendeleze katika fani  yenu na kama mnavyojua soka la Tanzania kwa sasa lipo nyuma sana so tuanzie huku chini kwa kuibua vipaji vya kutosha” alisema Willam Mungai.


  Mafunzo hayo yalioendeshwa na Kocha Bonifas Mkwasa mwezi Juni 25 hadi Julai 6  mwaka huu kwa udhamini mkubwa wa asasi ya hazina Foundation inayomilikiwa na Wiliam Mungai na makao makuu yako mjini Mafinga.


  0 0
 • 12/27/13--07:31: Rais Kikwete arejea nchini
 •  Makamu wa Rais Dk.Mohamed Gharib Bilal akimlaki Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya Kuwasili nchini akitokea jijini New York Marekani ambapo alikwenda kwa ukaguzi wa kawaida wa afya yake.Akiwa nachini Marekani Rais Kikwete alialikwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban ki Moon nakufanya naye mazungumzo kuhusu ushiriki wa majeshi ya Tanzania katika ulinzi wa Amani katika nchi mbalimbali.(picha na Freddy Maro).
  Makamu wa Rais Dk.Mohamed Gharib Bilal akizungumza na Rais Dkt.Jakaya Kikwete Mrisho mara baada ya kumlaki muda mfupi baada ya Kuwasili nchini akitokea jijini New York Marekani ambapo alikwenda kwa ukaguzi wa kawaida wa afya yake nchini Marekani. Rais Kikwete alialikwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban ki Moon na kufanya naye mazungumzo kuhusu ushiriki wa majeshi ya Tanzania katika ulinzi wa Amani katika nchi mbalimbali

  0 0

  Naibu Waziri wa wizara ya Sayansi na Teknolojia Januari Makamba akizungumza na baadhi ya Maaskofu na Wachungaji wa mkoa wa Mwanza katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Kampuni ya The Great Zone Entertainment, inayojishughulisha na matamasha ya muziki wa Injili na sanaa.
  Bishop Alex Lwakisumbwa ambaye ni mwenyekiti wa P.C.T mkoa wa Mwanza akizungumza  katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Kampuni ya The Great Zone Entertainment, inayojishughulisha na matamasha ya muziki wa Injili na sanaa, ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa wizara ya Sayansi na Teknolojia Januari Makamba.  
  Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa jiji la Mwanza Bishop Charles Sekelwa akizungumza  katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Kampuni ya The Great Zone Entertainment, inayojishughulisha na matamasha ya muziki wa Injili na sanaa, ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa wizara ya Sayansi na Teknolojia Januari Makamba. 
  Sehemu ya baadhi ya baadhi ya watumishi wa Mungu waliohudhuria hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na Kampuni ya The Great Zone Entertainment, inayojishughulisha na matamasha ya muziki wa Injili na sanaa, ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa wizara ya Sayansi na Teknolojia Januari Makamba. 
  Hafla ikiendelea katika ukumbi wa Victoria Palace Hotel jijini Mwanza.

  0 0

   Baadhi ya shehena za vipodozi  zilizokamatwa na jeshi la polisi mkoa wa Iringa baada ya kushushwa katika roli katika makao makuu makuu ya jeshi mkoa wa Iringa.
  Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhani Mungi akionyesha shehena ya vipodozi vilivyokamatwa na jeshi hilo mkoani  Iringa katika makao makuu ya jeshi hilo jana.(picha na Denis Mlowe)
  =========   ========   =========
  SHEHENA ZA VIPODOZI FEKI ZAKAMATWA MKOANI IRINGA

  Na Denis Mlowe,Iringa

  JESHI la polisi mkoa wa Iringa limefanikiwa kukamata shehena ya vipodozi vyenye thamani ya mamilioni ya shilingi iliyokuwa inasafirishwa kutoka nchini Zambia kwenda jijini Dar es Salaam vilivyopigwa marufuku kwa matumizi ya binadamu.

  Shehena hizo zilikuwa zimebebwa na gari aina ya lori la mafuta lenye namba za usajili T 247 BHP na tela lenye namba usajili T 598 BMK mali ya World Oil Ltd ya jijini Dar es Salaam.

  Waliokamatwa na shehena hiyo ya vipodozi ni  Dereva wa lori Mohamed Sadru(23) na Kassimu Kaifa anayesadikika ndio mwenye mali.

  Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhani Mungi  amethibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao na kusema kuwa walipata taarifa za kiitelejensia kutoka Tunduma kuwa kuna lori linasafirisha shehena hiyo kutoka nchini Zambia.

  Mungi alisema walijiweka tayari kulikamata gari hilo kwa kukaa barabara kuu kuanzia saa moja jioni hadi ilipofika saa kumi alfajiri ndipo gari lilipofika na kukamatwa.

  Anaongeza kuwa maafisa wa polisi mkoa wa Iringa walijipanga vizuri kuweza kulikagua gari hilo na waligundua kuna shehena kubwa ya vipodozi vilivyopigwa marufuku na TFDA na kuwaweka chini ya ulinzi dereva na roli hilo.

  “Cha kushangaza gari la mafuta kuweza kubeba  vipodozi hivi vilivyopigwa marufuku hivyo tukaamua kuwashirikisha wadau wengine ambao ni TRA, TFDA na Tanroad kuweza kubaini makosa ambayo watuhumiwa hao wamefanya katika usafirishaji wa shehena hiyo.” Alisema Mungi

  Mungi alisema uchunguzi wa awali unaonyesha shehena hiyo ina thamani kubwa na ndio maana watuhumiwa walikuwa wanasafirisha kwa njia ya magendo na wanaendelea kuchunguza kubaini thamani halisi ya mzigo huo.

  Kwa upande wake Mratibu wa Mamlaka wa Chakula na Dawa (TFDA) mkoa wa Iringa, Deodata Rukupwa alisema shehena iliyokamatwa asilimia 100 ina kemikali iliyopigwa marufuku ya Hydroqunone na mamlaka hiyo.

  Alisema vipodozi hivyo vitateketezwa kwa pamoja na jeshi la polisi na gari hilo kutaifishwa na serikali kutokana na kubeba mzigo wa magendo.

  Rukupwa aliwataka wananchi kuwa makini katika kutumia vipodozi vilivyopigwa marufuku na serikali na kutoa taarifa wanapobaini kuna vipodozi vilivyopigwa marufuku vinauzwa.

  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali mtoto Andrew Simba(15) aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wakati Rais alipowatembelea na kuwafariji baadhi ya wagonjwa katika wodi ya Mwaisela leo.(picha na Freddy Maro).


  0 0

  Na Ali Issa MAELEZO – ZANZINBR

  Rais mstaafu  wa awamu ya sita wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume amesema majumba ya Mpapa yaliyokabidhiwa kwa wananchi 24 kutoka shehia 6 ya jimbo la bambi  yanahitaji kulindwa na kutuzwa ili yaweze kudumu zaidi uhai wake.

  Hayo ameyasema huko bambi wakati alipokua akiyakabidhi nyumba hizo kwa familia kadhaa katika sherehe za kuzifungua nyumba hizo kwa wakazi waliopewa,ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanbar.

  Amesma azma ya awali ya mapinduzi ya Zanzibar ni kumpatia makazi bora mwananchi wa Zanzibarna hiyo ndio iliokuwa azma ya Rais wa awamu ya kwaza,Hayati Abeid  Aman Karume ya kuwajengea wananchi wake makazi hayo,hivyo azma hiyo ipo palepale na serikali haitorudi nyuma.

  Amesema ujenzi wa nyumba hizo,umemalizika na kuazia leo ni huru kwa wananchi kuzitumia kwa kuweka familia zao. Sambamba na kuyatunza kwa ubora.

  Nae Waziri wa Ardhi,Maji,Ujenzi na Nishati wa Zanzibar,Mh. Ramadhani Abdalla Shaban amesema wameshapitisha maamuzi ya kuazisha Shirika la Nyumba ambalo litasimamia ujenzi na ukarabati wa nyumba zote na maendeleo yake kwa kushirikiana na wakazi wanao ishi kwenye nyumba hizo.

  Aidha akijibu maombi ya wana kijiji wa Mpapa kuhusiana na tatizo la maji katika nyumba hizo,amesema zitapatiwa maji si muda mrefu,tatizo la maji Mpapa litakuwa historia kwa kushirikiana na Mbunge na mwakilishi wa jimbo hilo.

  0 0

  Jumla ya watahiniwa 411,127 kati ya 427,609 waliofaulu mtihani wa kumaliza darasa la saba mwaka 2013 wamechaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari katika shule mbali mbali za Serikali hapa nchini

  Hata hivyo, kwa mujibu wa ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI, wanafunzi 16,484 watashindwa kujiunga na elimu ya sekondari kwa wakati muafaka kutokana na uchache wa madarasa.

  Akitangaza idadi ya wanafunzi walichoguliwa kujiunga na elimu ya sekondari katibu Mkuu Ofisi ya waziri mkuu TAMISEMI Jumanne Sagini amesema kutokana na tatizo la upungufu wa madarasa ameziagiza halmashauri zote nchini kuhakikisha zinakamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa hadi ifikapo machi mwaka mwakani.

  Aidha, Sagini anaeleza takwimu za wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari.

  Amesema idadi ya ufaulu kwa mwaka huu imeongezeka ikilinganishwa na mwaka jana na hivyo kusababisha kuwepo cha changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa 412.

  Jumla ya wanafunzi 867,983 wa shule za msingi walisajiliwa kufanya mtihani huo wakiwemo wasichana 455,896 sawa na asilimia 52.52 na wavulana 412,087 sawa na asilimia 47.48.

  0 0
 • 12/27/13--19:00: ngoma azipendazo ankal
 • Cyndi Lauper  anakupa 'Time After Time'

  0 0
 • 12/27/13--22:59: IN EVERLASTING MEMORY
 • Mom, it has been nine years now since 
  God and His angels called you away from us.

  We still feel the sorrow and sadness due to your absence. But we believe you are in Heaven, praying for us and guiding us in our daily lives.

  You are sadly missed by your beloved husband- Joshua Daniel Minja, your children- Andrew, David, Alfred and Peter, your daughters-in-law- Dr. Irene and Ngianasia and your lovely grandchildren Danielle, Esther, Gabrielle, Joshua and Robert without forgetting all other members of the family, relatives and friends who loved you whole heartedly.

  You will forever live in our hearts and ask God to give you a peaceful rest. 
  In time we shall join you in heaven.


  Amen.


  0 0


  0 0

  NAIBU wa Waziri wa Wizara ya Sayansi na Teknolojia January Makamba ametaka ujio wake Jiji la Mwanza usihusishwe na Kampeni za chini kwa chini za Urais bali ni kutekeleza ombi la Umoja wa waendesha pikipiki Mkoa wa Mwanza kuwasaidia kupata Bima ya Afya baada ya kuwawezesha kupata pikipiki 1745 za FEKON na si vinginevyo.

  Kauli hiyo ya Makamba ameitoa leo wakati wa kufungua kongamano kubwa la siku moja la Umoja wa Madereva wa pikipiki Mwanza lililofanyika katika uwanja wa michezo wa Nyamagana Jijini hapa, alisema kwamba kuna baadhi ya watu wameanza kuhoji ujio wangu Mwanza “Niko hapa kwa ajili ya shughuli hii mliyonialika bali kuja kushiriki Kampeni muhimu ya Bima ya Afya kwa ajili ya Usalama wa badae” na si vinginevyo.

  Makamba amesema kwamba upatikanaji wa Leseni kwa urahisi na uharaka usiwe tiketi ya Kifo  kwa wananchi (ZAIDI MSIKILIZE KWA KUBOFYA PLAY)

  Awali kabla ya kongamano hilo madereva hao wa bodaboda walifanya maandamano toka makao makuu ya ofisi zao yaliyopo mtaa wa malango mmoja wilayani Nyamagana jijini Mwanza hadi katika uwanja wa historia wa Nyamagana.
  Wadau wa Bodaboda wakiingia uwanja wa Nyamagana.
  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA .

  0 0

  Mwanamke wa Kitanzania mwenye umri wa miaka 28 amekutwa na kilo 1.1 za madawa ya kulevya aina ya heroin alizokuwa amezihifadhi tumboni mwake,baada ya kukamatwa huko Macao, nchini China. Dawa hizo zenye jumla ya vidonge 66 vinakadiriwa kuwa na thamani ya dola za Kimarekani 137,720.

  Mwanamke huyo alikuwa akisafiri kutoka Thailand akielekea Macao Jumanne iliyopita. Aliwaambia polisi kuwa alikuwa anaelekea Guangzhou ambao ni mji wa jimbo la Guangdong huko Chima.
  Pichani ni mwanamke huyo wa Kitanzania (akiwa amefunikwa uso) aliyekamatwa na kilo 1.1 za heroin huko Macau. Hapo amepigwa picha na vidonge vyake wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari mjini Macau, Disemba 19, 2013.  0 0
 • 12/28/13--00:24: Article 11
 • Ndugu zangu, 
  Nami nitapata fursa ya kutoa hotuba. Nitazungumzia umuhimu wa kuhifadhi historia kwenye maandishi ili iwe ni kumbukumbu ya miaka mingi kwa wengine kujifunza. Maana, historia haibadiliki, lakini inapotea.
  Na taifa linalodai kuwa watu wake wameelimika tunalipimaje?
  Jibu; Ni kwa kuangalia idadi ya machapisho yanayozalishwa kila mwaka. Kuangalia pia ubora wa machapisho hayo.
  Na machapisho ni jambo moja, na kuyasoma machapisho hayo ni jambo jingine kabisa.
  Tuna lazima ya kuwajengea watu wetu kiu ya kupenda kusoma. Ni moja ya malengo yangu ya kuandika kitabu cha ' Simulizi Za Mzee Madiba'. Kwamba watu watafute vitabu zaidi vya kusoma. 
  Leo Jumamosi pale Makumbusho ya Taifa nitasimulia utoto wangu na jinsi nilivyoanza kuelewa maana ya vita vya ukombozi kutoka Ubaguzi wa rangi Afrika Kusini kutokana na kucheza mpira na watoto wa wakimbizi wanachama wa ANC waliokuwa wakikaa jirani na sisi pale Biafra Kinondoni. 
  Leo Jumamosi kutakuwa na nafasi pia ya kuulizana maswali, kujadiliana na kupeana ufafanuzi, kama Watanzania.
   Mgeni Rasmi Kwenye Uzinduzi Ni Ndugu Mobhare Matinyi.
  Siku Njema.
  Maggid Mjengwa 

  0 0

  DSCF1967Vicky Mwakoyo ambaye ni Creative Meneja wa kampuni ya  Tan Communication Media inayomiliki kituo cha Radio 5 Arusha akimkabidhi Mlezi mkuu wa kituo cha Moshono Fundation msaada katika kampeni ya Ushindi  kwa ajili ya kuwafariji watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi katika vituo jijini Arusha juzi tarehe 26/1213 katika viwanja vya Matongee  Carnivo.
  DSCF1941
  KAMPUNI ya Tan Communication media imetoa misaada ya chakula yenye thamani ya shilingi milioni moja na laki mbili kupitia kampeni ya Ushindi  kwa ajili ya kuwafariji watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi katika vituo kumi jijini Arusha.
  Akizungumza wakati wa chakula cha pamoja  cha mchana jana Meneja mbunifu wa kampuni hiyo Vicky Mwakoyo alisema kuwa lengo ni kuwafariji watoto hao ambao jamii ya watanzania imewasahau.
  Mwakoyo alisema kuwa  watanzania wanatakiwa kubadilika na kuwajali watoto yatima ikiwa ni pamoja na kutenga muda wao kukaa  na kucheza nao ikiwa ni pamoja na kuwapatia zawadi mbalimbali ili wasijione kama ni wapweke na wameachwa peke yao.
  “Watoto wote ni sawa na watoto hawa hawajapenda ni mapenzi ya Mungu hivyo tunawajibu wa kutenga muda wetu na kukaa na watoto hawa kama hivi leo unaona wamefurahi kama watoto wengine wenye wazazi”alisema Mwakoyo
  Aidha aliongeza kuwa ni vyema jamii ikajenga utamaduni wa kuwasaidia watoto hawa na isiishie misimu ya kipindi cha sikukuu tu kwa kuwa wanamahitaji ya chakula kila siku.
  “Naomba niiombe serikali kupitia Wizara ya maendeleo ya jamii jinsia na watoto kuangalia namna ambavyo inaweza kushirikiana na vituo vya kulelea watoto yatima kwa kuwapatia fungu ili kupunguza ukali wa maisha katika vituo hivyo kwa kuwa vina mchango mkubwa kwa taifa”alisema meneja huyo
  Tukio hilo liliofanyika katika viwanja  vya  Matongee  Carnivo  limewakutanisha watoto Yatima zaidi ya Mia moja na hamsini ambapo walipata nafasi ya kushiriki michezo mbalimbali kama kuvuta kamba,kukimbia kwenye magunia,mashindano ya kula na kuimba muziki.
  Vituo hivyo vilivyopatiwa misaada ni pamoja na Bethlehemu,Moshono Foundation,Tumain,Mama na Watoto,St.Joseph,Camp Mosses,Kambarage Lemara na Karama.

  0 0

  Wadau,

  Nipenda kuwataarifu kwamba maandalizi ya  ule mpambano wa kumaliza mwaka 2013 kati ya Wahenga Veterans na Golden Bush Veterans  yamekamilika na game itachezwa uwanja wa TP al-maarufu Nangwanda Sijaona. Mechi itaanza saa kumi na nusu, yaani masaa matatu yajayo.

  Hivi sasa Golden Bush Veterans tunapanda chakula cha mchana kwa pamoja hapa Star Light Hotel, na tunategemea kuanza msafara mrefu kuelekea uwanjani kuanzia saa tisa na nusu. Msafara utanzia start light Hotel  hadi uwanja wa St James Park “Kinesi” ambapo tutasimama kwa muda ili kupata maelekezo kutoka kwa kamati yetu ya Ufundi na Mambo ya Kale jinsi ya kuingia uwanjani. Kazi hiyo itafanywa na mwenyekiti wa kamati bwana Jeremiah Mulungu ambaye ndiye atakuwa mkuu wa msafara kuanzia St James Park hadi Nangwanda Sijaona.

  Huwezi amini mpaka hivi sasa uwanja wa TP umefulika watazamaji wa kila aina, watoto, vijana, wazee kila mmoja akiwa na hamu kabisa ya kuona mtanange huu wa kukata na shoka. Ikumbukwe kwamba Wahenga walishinda mechi kama mwaka jana, hivyo Golden bush wanaingia kwa ajili ya kulipa kisasi.

  Baada ya game timu zote mbili pamoja na jamaa na marafiki zetu waalikwa, tutajumuika pamoja ili kufanya tafakari ya jinsi tulivyomaliza mwaka 2013.

  Nichukue nafasi hii kuwakaribisha wapenzi na wakereketwa wa soka, waje waone football ya hali ya juu sana ambayo itachezeshwa na Mwamuzi anaetambuliwa na FIFA.

  Karibuni sana.

  Ticotico

  0 0

  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu David Pelo Kivuyo aliekuwa Diwani wa zamani wa Makuyuni. Marehemu Pelo, ambaye pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli, alifariki tarehe 22 Desemba na kuzikwa nyumbani kwake Makuyuni leo Desemba 28. Alifariki kutokana na maradhi ya shinikizo  la damu.

  0 0
 • 12/28/13--03:33: yale yaleeee......
 • Salamaleko Ankal na timu yako nzima ya Globu ya Jamii,

  Naomba unisaidie kushea na Wadau Dukuduku langu hili,nililokumbana nalo leo baada ya kutoka duka la dawa Maeneo ya msikiti wa Wangazija na hospitali ya Hindu Mandal baada ya kukuta kukuta gari langu limetiwa pingu kama. 

  Tukio hilo limetokea mapeka leo pale nilipoegesha gari nje ya duka hilo na kuingia ndani kwa ajili ya kununua dawa baada ya Krismas nzima kuwa mahututi kwa mguu kuvimba,niliegesha gari katika eneo wazi ambapo hakuna kibao chochote kinachoonyesha ishara ya HAKUNA KUPAKI GARI HAPA na mbele niliona kuna gari la serikali limepaki hapo nami nikapaki nyuma yake.

   Lakini cha kushangaza kama si kustaajabisha,ni pale nilipotoka dukani na kukuta gari langu limefungwa na na kukutana na Vijana wa Tambaza Auction Mart wakinitaka nilipe faini ya laki moja. 

  Nilipowauliza kuwa mbona hakuna kibao cha No Parking na hajanizuia wakati naegesha gari na huku mkiniona wakati naingia pharmacy tena kwa kuchechemea, vijana hao hakutaka kuelewa somo lolote zaidi ya kuniambia niende Anatoglo nikalipe faini halafu nije kuchukua gari langu. 

  Kiukweli haki haitendeki juu ya swala hili linaloendelea hapa mjini,maana imekuwa kama ni mradi wa mtu wa kutafuta hela kwa nguvu,maana haiwezekani sehemu haina alama yeyote na watu wanakuona hawaji kukutaarfu kuwa sehemu hii haipaswi kuegeshwa gari na labda kaegeshe eneo lile,lakini hawa jamaa wanakutegea umeegesha halafu na wao wanakuja na machuma yao na kufunga gari.

  Kitu cha pili kwa akili ya kawaida tu mtu anaonekana ni mgonjwa na hawezi kutembea na hajazuia mtu hamwezi mkatoa ushauri? 

  Halmashauri ya Ilala mnapaswa kufanya utaratibu mzuri wa kuwafanya hao Tambaza Auction wakusanye hela na watoe uthibitisho kama wafanyavyo polisi . Hii kwenda hadi Anatoglo kulipa faini kisha ndio urudi kuchukua gari lao ni sawa na ucheleweshwaji unaofanywa na STRABAG Ubungo. 

  Meya wa Ilala Jerry Silaa angalia usumbufu huu unapoteza masaa mengi ya uzalishaji.

  Mdau aliekumbwa na Mkasa.

  0 0

  Redds Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa ( kushoto) akipinga hodi ikiwa ni ishara ya kukaribishwa katika Kituo cha kuleta watoto yatima Mgolole cha Masista wa Moyo Safi wa Maria wa Morogoro , ambapo alifuatana na warembo wengine wawili, Miss Tanzania mshindi wa tano, Elizabeth Perrty, na Sabra Islam Miss Morogoro 2013, wazazi wake na Viongozi wa juu wa Kamati ya Miss Tanzania na kupokelewa na Mama Mkuu wa Kituo hicho, Sista Flora Maria Chuma ( mwenye kutabasabu ) Desemba 25, mwaka huu walipotembelea kwa ajili ya kutoa zawadi ya vyakula vya aina mbalimbali ikiwa ni mpango wake wa kusaidia makundi ya aina hiyo.
  Redds Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa akigawa zawadi za vyakula vya aina mbalimbali kwa baadhi ya watoto yatima wanaolelewa na Kituo cha Mgolole cha Masista wa Moyo Safi wa Maria wa Morogoro , Desemba 25, mwaka huu ikiwa ni sehemu ya kusaidia watoto wa aina hiyo , akiwa ameambatana na warembo wengine wawili, Miss Tanzania mshindi wa tano, Elizabeth Perty, na Sabra Islam Miss Morogoro 2013, wazazi wake pamoja na Kamati ya Miss Tanzania.


  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Mhe. Mohammed Aboud akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Stemp Mpya ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar,uliofanyika leo kwenye viwanja vya Posta Kijangwani Zanzibar ikiwa ni sehemu ya shamrashamra ya sherehe za Mapinduzi kutimia miaka 50.
  Posta Master Mkuu Deos Hamis Mndeme, akitowa maelezoya Stemp Mpya baada ya kuzinduliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais waZanzibar Mohammed Aboud, katika viwanja vya Posta Kijangwani Zanzibar ikiwa ni shamrashamra ya sherehe za Mapinduzi kutimia miaka 50.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Mhe. Mohammed Aboud  akizungumza na wafanyakazi wa Shirika la Posta katika viwanja vya Ofisi ya Posta Kijangwani wakati wa Uzinduzi wa Stemp Mpya ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
  Posta Master Mkuu Tanzania Bwa, Deos Hamis Mndeme, akitowa maelezo baada ya kufungulia Kituo cha Mawasiliano kwa Jamii, kilichoko katika jengo la Posta Kijangwani.
  Burudani ikitolewa kwenye sherehe hiyo.
  Maofisa wa Posta na wageni waalikwa wakifuatilia uzinduzi huo wa stempmpya na kituo cha Mawsiliani kwa Jamii.

  0 0

  Na Andrew Chale

  MBUNIFU mkongwe wa mitindo na mavazi nchini, Asia Idarous Khamsin, usiku wa leo Desemba 28 anatarajiwa kupamba shoo kali kwa kuonesha mavazi kwenye Usiku wa Real Unique Tanzania’ utakaofanyika ndani ya Regency Hotel, jijini Dar es Salaam huku ukisindikizwa na Skylight Bend.

  Akielezea juu ya onesho hilo la ‘Usiku wa Real Unique Tanzania’ , Asia ‘Mama wa Mitindo’ alisema kuwa itakuwa ni ya kipekee katika kufunga mwaka wa 2013 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2014.

  “Ni hatua ya kipekee kwa mimi kuweza kuonesha shoo yangu hii leo katika “Usiku wa Real Unique Tanzania” kwani ndio shoo ya funga mwaka, hivyo wadau wa mitiondo na mavazi watapata kufurahia onesho hilo sambamba na burudani kali kutoka kwa bendi maalufu ya Skylight.” Alisema Asia Idarous.

  Mbali na kupamba shoo hiyo kwa kuonesha mavazi yake, Asia Idarous pia ndiye mgeni rasmi kwenye usiku huo wa funga mwaka wa Real Unique Tanzania.

  Aidha, katika shoo hiyo, kiingilio ni shilingi 25,000. Huku kwa viti maalum, VIP kikiwa sh 50,000.

older | 1 | .... | 311 | 312 | (Page 313) | 314 | 315 | .... | 3285 | newer