Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live

MAGAZETI YA LEO JUMANNE SEPTEMBA 24, 2019


165 Villages in Tanzania to Benefit from More Efficient and Reliable Solar Powered Pumps

$
0
0
Dar es Salaam, September 24, 2019.  About 165 rural Tanzanian villages in nine regions will have access to sustainable water supply through improved solar pumping systems through a new grant agreement signed between the Government and the World Bank amounting to US$4.5 million from the Global Partnership for Results-Based Approaches (GPRBA).

The World Bank’s long-term engagement in the water sector will now include a large pilot on “Solar Water Pumping via Innovative Financing” which will support the Government of Tanzania in moving from dated and inefficient diesel-powered pumps with clean and climate-friendly solar pumping systems. These new systems will help decarbonize off-grid water pumping in rural Tanzania and significantly reduce the cost of water extraction for at least 500,000 beneficiaries.

“The project opens up new resources of available funding to help close the vast investment gap for rural water supply in Tanzania and shift the focus to mobilizing private sector financing consistent with the World Bank's Maximizing Finance for Development (MFD) approach,” said Ms. Zaruhi Tokhmakhian, Acting Head, GPRBA.

This is the first attempt to leverage private sector financing in Tanzania’s rural water supply sector. To supplement GPRBA’s grant and to diversify sources of funding, the project uses a blended finance approach, combining debt finance and output-based subsidies. GPRBA funds will facilitate a 60 percent subsidy against loans for the Community-Based Water Supply Organizations (CBWSOs) to replace their diesel generators with solar-powered pumping systems. The debt finance will account for 40 percent of the investment and the CBWSOs will be able to repay the loan over a four-year period with additional money made available by eliminating the use of diesel fuel.

In addition, an innovative mobile-banking payment platform will be piloted to manage revenue collection from water sales and loan payments from participating CBWSOs directly to the participating local bank. The funding also includes a technical assistance component for training the CBWSOs to perform at a greater capacity for improved impact, and to encourage their practice of loan repayment to increase their creditworthiness and ability to borrow for future activities.

“The introduction of solar water pumping systems is expected to significantly reduce operation and maintenance costs for the CBWSOs, providing them with financial resources to lower the price of water to users and expand service to presently unserved communities,” said Prof. Kitila Mkumbo, Permanent Secretary, Ministry of Water.

To address the growing concern of the delivery of safer water for consumption, this project will also install simple chlorinators to improve the water quality delivered to communities. When fully achieved, a range of benefits will emerge from expanded access through the rehabilitation of water schemes including: increased reliability and sustainability of service, reduction of operating and maintenance costs, private sector involvement through a five-year service agreement, as well as other operational efficiencies and service improvements.

“With this project, we are seeking to introduce new technologies at scale to better facilitate private sector financing and sustainable rural water supply. It is our hope that the combination of solar water pumps, pre-paid meters, chlorination, remote sensors and 5-year service agreements will form the synergies which will shape a new era for the sector,” said Bella Bird, World Bank Country Director.

WAZIRI MKUU MAJALIWA ATOA POLE KWA MKUU WA MAJESHI NA FAMILIA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole Mkuu wa Majeshi nchini, Jenerali Venance Mabeyo wakati alipokwenda kuhani msiba wa mototo wa Mkuu wa Majeshi , Nelson Mabeyo, Msasani jijini Der es salaam, Septemba 24, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitia saini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Nelson Mabeyo, mtoto wa Mkuu wa Majeshi nchini, Generali Venance Mabeyo, nyumbani kwa Mkuu wa Majeshi, Msasani jijini Dar es salaam, Septemba 24, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole, Tina Mabeyo, Mke wa Mkuu wa Majeshi nchini, Jenerali Venance Mabeyo wakati alipokwenda nyumbani kwa Mkuu wa Majeshi, Msasani jijini Dar es salaam kuhani msiba wa mtoto wa Mkuu wa Majeshi, Nelson Mabeyo, Septemba 24, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkuu wa Majeshi nchini, Jenerali, Venance Mabeyo wakati alipokwenda nyumbani kwa Mkuu wa Majeshi, Msasani jijini Dar es salaam kuhani msiba wa mtoto wa Mkuu wa Majeshi, Nelson Mabeyo, Septemba 24, 2019. Kulia ni Jaji Mkuu waTanzania, Profesa Ibrahim Hamis Juma na kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Balozi Ombeni Sefue.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Biashara ya kakakuona yashika kasi nchi za Asia

$
0
0

Na Bakari Kimwanga -Aliyekuwa Thailand

TAASISI mbalimbali za kimataifa zimekuwa na mkakati madhubuti wa kulinda rasilimali hasa wanyama akiwamo kakakuona ambaye kwa sasa yupo hatarini kutoweka.

Hali hiyo inachangiwa kwa kiasi kikubwa na usafirishaji haramu wa wanyamapori kutokana nchi za Afrika hasa zile za Afrika Magharibi zikiwamo Ghana na Nigeria, na kwa upande wa Afrika Mashariki Kenya ikitajwa kama sehemu ya uchochoro wa ukusanyaji wa wanyama hao na kuwasafirisha kwenda nchi za Asia.

Timu ya wanahabari watano kutoka nchini ilitembela nchini Thailand na kuzunguka kwenye maeneo mbalimbali ikiwamo sehemu maalumu za wanyama waliokamatwa kutoka nchi za Afrika, Idara ya Forodha Uwanja wa Ndege wa Suvarnabhumi na soko la bidhaa ya wanyamapori.

Wanahabri hao waliungana na wenzao wa nchini Thailand, ambapo kila upande uliweza kutembelea kwenye nchi za wenzake kwa lengo la kubadilishana uzoefu na taarifa kuhusu usafirishaji haramu wa wanyamapori, chini ya ufadhili wa USAID Protect Tanzania na USAID Wildlife Asia, kwa kushirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET).

Kutokana na hali hiyo, nchi ya Ghana imelazimika kuingia katika mkakati wa kuangalia upya sheria zake za wanyamapori kutokana na biashara ya kakakuona ambayo imekithiri kwa kasi kubwa.

Hali hii imesababishwa na hofu ya kwamba nchi hiyo inatumiwa kuendesha biashara haramu.Zaidi ya kilo 31,000 ya magamba ya kakakuona ilikamatwa duniani kote mwaka huu, hali hiyo inabainishwa na ripoti ya Shirika la Kimataifa la Ustawi wa Wanyama (IFAW).

Katika kipindi cha Mei na Juni mwaka huu, shehena mbili kubwa zilinaswa nchini Malaysia, ambapo pia kilo 700 zilipatikana zikiwa zimesafirishwa kupitia Ghana. Huku shehena nyingine kubwa zikikamatwa pia nchini Uganda, Cameron na Ivory Coast.

Mmoja wa maofisa wa juu wa IFAW, Mark Hofberg, anasema magamba mengi kutoka kwa mnyama huyo Afrika yameuzwa ili kufikia mahitaji yake katika Bara la Asia, ambako hutumiwa katika dawa za jadi.

Kakakuona anapatikana zaidi katika nchi za Afrika na Kusini Mashariki mwa Asia.Aina mbili kati ya nane ya mnyama huyo wameorodheshwa kuwa hatarini, wakiwekwa katika orodha nyekundu ya aina ya wanyama walio hatarini.

“Kuongezeka kwa kamatakamata ya mizigo hiyo kunaweza kuwa ishara kwamba mamlaka husika zinalichukulia suala hili kwa uzito, lakini nchi nyingi hazina sheria kali za kuadhibu wafanyabiashara haramu.

“Kwa biashara hii kupungua kwa kiasi kikubwa, kunahitajika adhabu na hukumu kali,” anasema Hofberg.Kakakuona ni mnyama aliyehifadhiwa nchini Ghana, ambapo Mwenyekiti wa Tume ya Wanyamapori wa Ghana, Nana Kofi Adu-Nsiah, anasema sheria kali inahitajika.

Sheria zilizopo za ulinzi wa wanyamapori zilipitishwa katika miaka ya 1960 na tume hiyo inataka ziangaliwe upya ili kufikia viwango vya kimataifa.Kutokana na ujangili huo mpya ambao sasa unashika kasi, watu watatu walikamatwa nchini Ghana kuhusiana na mizigo iliyonaswa Juni, mwaka huu, nchini Malaysia.

Viongozi wa Serikali wanaamini sheria mpya zitazuia nchi za Afrika Magharibi kutumiwa kuwa hatua ya usafiri kwa wanyama hao wanaosafirishwa lakini pia kuna wasiwasi pia juu ya uwindaji wa ndani wa kakakuona.

Wanyama hao ambao wana ukubwa wa sentimita 30 hadi 100 wanaweza kuuzwa kwa karibu dola za Marekani 45 au Euro 38. Na wale wanaowauza kwa kawaida huwa ni watu masikini.



UTAFITI

Watafiti wamegundua kuwa kakakuona anatumika kwa ajili ya chakula na magamba yake yanatumiwa kama viungo.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na USAID Wildlife Asia, uliainisha sababu za kuwapo kwa biashara haramu ya bidhaa za wanyamapori kama tembo, faru, kakakuona na tiger kunatokana na imani na tamaduni zao hasa kwa raia wa nchi za Thailand, China na Vietnam, ambapo pia inaelezwa kuwa asilimia 20 ya tembo wa Afrika wanadaiwa kuuawa na sehemu ya viungo vyao (pembe) husafirishwa kwa njia ya zisizo halali na kuingia kwenye nchi hizo.

“Mtu anatoa zawadi iliyotengenezwa kwa mazao ya wanyamapori kwa familia, marafiki, masuala ya kijamii na mitandao ya kibiashara kwa mazao ya wanyama wote wanne,” anaeleza mtaalamu wa mawasiliano na kubadilisha tabia wa USAID Wildlife Asia, Wenweena Tangsathianraphap.

Naye mfuatiliaji na mtaalamu wa uthamini na ufuatiliaji USAID Wildlife Asia, Pakprim Oranop, anaweka wazi suala hili na kusema kwamba bara hilo mtu kuvaa kidani au kitu chochote kilichotengenezwa kwa kiungo chochote cha mnyama ni ishara kwamba naye atakuwa jasiri kama mnyama aliyetokana na bidhaa hiyo au anajihakikishia ulinzi.

Hata hivyo, pia wapo wenye imani kwamba inaongeza nguvu za kiume au uwezo wa mwanamume kutambulika kuwa rijali, na wengine wakitumia kama dawa ya kuwafanya kuwa imara kama mnyama husika.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na USAID Wildlife Asia, ya kwanini watu wanatumia bidhaa za wanyamapori, walibaini kuwa kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya imani na utamaduni kwa wanaotumia bidhaa za wanyamapori.

“Wengi waliamini kuwa anapotumia kitu chochote kilichotengenezwa kwa jino la tembo, pembe ya faru au tiger (chui) basi naye atakuwa na matendo ya kishujaa kama huyo mnyama, ndiyo maana wengi wameendelea kutumia,” anaeleza.

Katika utafiti wa walaji wa mwaka 2018, kati ya watu 10 waliohojiwa ambao ni wanunuaji na watumiaji kwa miezi 12 iliyopita, ulibainisha kuwa nchini China watumiaji wa bidhaa za tembo asilimia 4.01 ni vya tofauti, asilimia 3.86 waliamini katika imani za kiroho na asilimia 3.79 waliamini katika urembo.

Kwa upande wa kakakuona, asilimia 4.14 waliamini inaponya maradhi mbalimbali, 3.72 inaleta afya njema na maisha mazuri na asilimia 2.74 inaongeza nguvu za kiume.



HALI ILIVYO THAILAND

Asilimia 94 ya waliohojiwa nchin Thailand, wanasema wanatumia bidhaa za meno ya tembo kwa kuwa ni kitu cha tofauti na thamani kubwa, asilimia 88 wanasema inaleta matumaini na bahati, wakati asilimia 79 wanasema inawalinda dhidi ya adui na majanga.

Kutokana na hali hiyo, Mwakilishi wa Shirika la Kudhibiti Usafirishaji wa Wanyamapori Asia (Traffic), Monica Zavagli, anasema biashara ya mazao ya wanyamapori inahusisha watu wenye mtandao mkubwa na wenye fedha nyingi ambazo huzitumia kununua nyara hizo.

“Hii biashara ni kubwa ambayo inatumia zaidi ya Dola za Marekani bilioni tisa hadi 30 kwa mwaka, mtandao huu unatumia taasisi za kifedha kuhamisha fedha na benki zina uwezo wa kuchunguza kwamba fedha hizo zinatokana na nini kama zinahusisha ujangili,” anasema.

“Hata hivyo, nchi kama Tanzania imefanya vizuri kuwa na sheria kali, lakini jitihada zaidi zinahitajika katika kushirikisha taasisi za fedha, kwa kufuatilia mali na mienendo yao kama fedha hizo zinahusisha biashara hiyo itasaidia kumaliza mtandao huo,” anasema Monica.

Mkuu wa USAID Asia, Craig Karkpatrick, anasema ripoti ya polisi wa kimataifa imeonyesha kuwa biashara haramu ya mazao ya wanyamapori ipo na inafanyika kwa kiasi kikubwa.


HALI ILIVYO TANZANIA

Kwa mujibu wa ripoti ya hali ya uchumi kwa Taifa ya mwaka 2017, inaonesha kwamba sekta ndogo ya wanyamapori ilikusanya zaidi ya Sh milioni 29 ikilinganishwa na zaidi ya Sh milioni 38 mwaka 2016, sawa na upungufu wa asilimia 22.7.

Kati ya mapato hayo, mapato kwa sarafu ya ndani yalikuwa Sh 2,904,631,101.82 na sarafu ya nje yalikuwa ni Dola za Marekani 11,940,029.80 ikilinganishwa na Sh 242,843,673,275 na Dola za Marekani 17,473,260 mwaka 2016.

Kwa mujibu wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamis Kingwangalla, Serikali inaendelea na jitihada za kulinda rasilimali za wanyamapori dhidi ya ujangili na uvunaji usio endelevu.

Katika kipindi hicho, anasema kulikuwa na siku za doria 262,770 zilizofanyika katika maeneo ya wazi na yaliyohifadhiwa ikilinganishwa na siku za doria 518,809 zilizofanyika mwaka 2016.



NYARA ZILIZOKAMATWA

Kutokana na doria hizo, nyara za Serikali za aina mbalimbali zilikamatwa ambazo ni pamoja na meno ya tembo 296 yenye jumla ya uzito wa kilo 929.8; nyamapori kilo 12,776; meno mawili ya simba, kakakuona 644; ngozi 10 za chui na ngozi moja ya simba.

Anasema pia jumla ya silaha 5,309 zilizohusika katika ujangili zilikamatwa zikiwamo SMG tisa, hunting rifles 14, shotgun 56, gobore 212, bastola mbili na nyaya za kutegea wanyama 5,016.

Huku watuhumiwa 3,889 wa makosa mbalimbali yakiwamo ujangili nao walikamatwa na kesi zao kuamuliwa na waliopatikana na hatia walilipa faini jumla ya Sh milioni 1.108 na wengine kufungwa jela miezi 12. Kesi 3,011 zilizobaki zilikuwa zinaendelea katika mahakama mbalimbali nchini.


MSIMAMO WA CITES

Katika mkutano wa wawakilishi wa nchi 183 wanachama wa mkataba wa kimataifa wa viumbe vilivyo hatarini kutoweka (CITES), uliofanyika hivi karibuni Geneva, Uswisi kwa lengo la kuimarisha mikakati ya kulinda viumbe hao, wanatoka na mapendekezo 56 yenye lengo la kuimarisha na kulinda viumbe vya porini.

Katibu Mkuu wa CITES, Ivonne Higuero, anasema tayari nchi hizo wanachama zimewasilisha mapendekezo 56 yenye lengo la kubadili na hatimaye kuimarisha kanuni za kulinda viumbe vya porini wakiwamo wanyama pamoja na maua, ambavyo vinauzwa kwenye soko la kimataifa.

“Mapendekezo mengi yanalenga kuhakikisha kuwa viumbe hivyo vilivyoko hatarini na ambavyo vinaendelea kuuzwa, vinasalia endelevu na hivyo mapendekezo yanataka vibali kutoka CITES ili kuruhusu biashara yao,” anasema Higuero.

Anasema mapendekezo mengine yanataka kupigwa marufuku kwa biashara za viumbe vilivyoko kwenye orodha I ilihali mengine yanataka kuwa viumbe ambavyo tayari idadi yao imekaa sawa vihamishwe kutoka orodha ya I kwenda orodha ya II ya mkataba wa CITES.

Anakumbusha kuwa kanuni zilizo wazi na zinazotekelezeka kwa kuzingatia sera thabiti ni muhimu katika kulinda utajiri wa asili na kufanikisha malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs), ambayo yalipitishwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa mwaka 2015.



Mwakilishi wa Shirika la Kudhibiti Usafirishaji wa Wanyamapori Asia (Traffic), Monica Zavagli
Mwandishi wa makala haya Bakari Kimwanga, akiuliza swali katika mafunzo nchini Thailand.
 

WAZIRI JAFO ATEMBELEA TAMASHA LA JAMAFEST JIJINI DAR

$
0
0
WWAZIRI wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo amesema kuwa Tamasha la utamaduni na sanaa la nchini za Afrika mashariki litumike kukiuza kiswahili ili na nchini mwanachama wa Afrika mashariki waweze waongee lugha hii adhimu ambayo sasa ni lugha rasmi katika jumuiya za Afrika.

Amesema hayo alipotembelea maonesho ya Tamasha la Uatamaduni na Sanaa la nchi za Afrika amashariki al-maalufu kama JAMAFEST linaloendelea kufanyika katika uwa nja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


"Nimetembelea mabanda mbalimbali na kujionea bidhaa mbalimbali za asili na utamaduni wa maeneo mbalimbali katika nchi za Afrika Mashariki za wajasiriamali wa nchi zote".

Amesema kuwa wizara ya Tamisemi ni chumvi, Afya, elimu vipo chini ya wizara yake, lakini wizara ya habari utamaduni, Sanaa na Michezo hususani Maafisa Utamaduni wa Mikoa,Wilaya na Halmashauri wako TAMISEMI,hivyo unaweza kuona kwanini yupo hapa.

Hata amewapongeza wizara ya habari na utamaduni kwa kufanya kazi nzuri pamoja na kuhakikisha tamasha hili linafanyika kama lilivyopangwa na kwa mafanikio makubwa hasa kukidhi kiu ya wananchi wanaohudhuria tamasha hili adhimu.

Pia amesema kuwa amefurahishwa na maandalizi ya Tamasha la JAMAFEST na amewasihi wananchi kuja kwenda Uwanja wa Taifa kujifunza tamaduni mbalimbali kutoka nchi za Afrika Mashariki.


Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo akimsikiliza mkuu wa kikundi cha kukuna nazi ikiwa washiriki ni washindi katika makundi mbalimbali walioshindanishwa kukuna nazi. Mashindano hayo yanafanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika maonesho ya Tamasha la JAMAFEST.Ikiwa wamepata washindi wa tatu kutoka makundi tiofauti wakiwa wananwake wawili pamoja na mwananume mmoja.

 Washiriki wa kukuna nazi wakisubiri filimbi ipigwe katika mashindano ya kukuna nazi wakiwa na kipimo cha ulaini wa nanzi pamoja na atakayewahi kumaliza na ikiwa safi. Washiriki ni washindi katika makundi mbalimbali walioshindanishwa kukuna nazi. Mashindano hayo yanafanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika maonesho ya Tamasha la JAMAFEST.
Washiriki wa mchezo wa kusuka ukiri wakicheza mchezo wao wa asili kusuka ukili. Hii ni katika Tamasha la JAMAFEST linaloendelea kufanyika jijini Dar es Salaam. 
 Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo  akiangalia jinsi wasuka ukili walivyofanikiwa kutengeneza bidhaa mbalimbali kwa kutumia ukili. Hii ni katikaTamasha la JAMAFEST linalofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika maonesho ya Tamasha la JAMAFEST.
 Mambo ya Utamaduni yakioneshwa. Hapa ni Mishale na Mikuki.
 Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo akiangalia meza na viti vilivyotengenezwa na Mianzi. Yote hayo ni katika tamasha la JAMAFEST linaloendelea kufanyika katika uwanja wa Taiafa jijini Dar es Salaam.
 Utamaduni na sanaa ya Matanzania.
Mambo ya utamaduni kutoka Burundi.

JUMUIYA YA MARIDHIANO BAGAMOYO YAPIGWA PINI, KUACHA KUINGILIA MAMLAKA NYINGINE

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI, BAGAMOYO

BARAZA la Madiwani Halmashauri ya Bagamoyo Mkoani Pwani, limeiasa Jumuiya  ya Maridhiano wilayani humo kuacha kuingilia mamlaka nyingine ambazo zipo kisheria na badala yake zitekeleze majukumu yao ya kikazi  .

Baadhi ya madiwani akiwemo, diwani wa kata ya Fukayose ambae pia ni mwenyekiti wa halmashauri ya Bagamoyo Ally Issa, waliyasema hao wakati wa baraza lililowakaribisha viongozi wa Jumuia hiyo, kwa lengo la kuwatambua na kufahamu mipaka ya kazi zao.

Aidha inadawa waliwahi kufika ndani ya kata ya Fukayose kuhoji taarifa ya mapato na matumizi, jambo ambalo ni kinyume na malengo ya Jumuiya inayolenga usuluhishi na kuweka sawa mambo pale penye migongano.

Nae diwani wa kata ya Yombo Mohammed Usinga, alisema baadhi ya viongozi hao wanatekeleza mambo nje ya taratibu kwani wamekuwa wakifika katika ofisi ya kata na kumtaka mtendaji kutoka nje ya ofisi ili wafanye mkutano.

Awali Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Dauson Shigea alisema Jumuiya hiyo imesajiliwa kisheria na inafanya kazi ya maridhiano na wanaikana kamati ya amani kutokana na kwamba haipo.

Akitoa ufafanuzi huo, juu ya mkanganyiko wa kushahabiana majukumu ya kazi baina ya jumuiya ya maridhiano na kamati ya amani, mkuu wa wilaya ya Bagamoyo ,Zainab Kawawa alisema ,kamati hiyo ipo na inafanya kazi kwa mujibu wa taratibu kitaifa,kimkoa na kiwilaya.

Zainab alikemea asitokee mtu ,kundi la watu ,Jumuiya ama taasisi yeyote kupotosha na kuvumisha kuwa kamati ya amani imekufa kwa maslahi binafsi.

"Nilishapokea taarifa pia zisizo rasmi kuwa wilayani humo kuna Jumuiya ya maridhiano na yeye bado sijaifahamu na kimsingi inafanyaje kazi zak".

Nae Katibu wa BAKWATA wilaya ya Bagamoyo ,ambae pia ni mratibu wa kamati ya amani wilayani humo, Hashim Juma alipoulizwa kuhusu kufutwa kwa kamati hiyo alisema hana taarifa hizo kwani endapo hatua hizo zingechukuliwa wangepewa taarifa za kimaandishi kutoka ngazi ya kitaifa na kimkoa.
  Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo ,Zainab Kawawa 

MAKAMU WA RAIS SAMIA AMUWAKILISHA RAIS MAGUFULI KWENYE MIAKA 25 YA CHUO KIKUU HURIA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hasssan, akiangalia Vitabu vya kumbukumbu ya Utafiti wa aina mbalimbali kwenye maonesho ya kilele cha Maadhimisho ya kutimia Miaka 25 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyofanyika leo Sept 24,2019 Kinondoni Jijini Dar es salaam, Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli kwenye maadhimisho hayo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hasssan, akihutubia kwenye kilele cha Maadhimisho ya kutimia Miaka 25 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyofanyika leo Sept 24,2019 Kinondoni Jijini Dar es salaam, Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli kwenye maadhimisho hayo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hasssan, akizungumza na Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Mhe. Mizengo Kayanda Peter Pinda Wakati wa kilele cha Maadhimisho ya kutimia Miaka 25 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyofanyika leo Sept 24,2019 Kinondoni Jijini Dar es salaam, Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli kwenye maadhimisho hayo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hasssan, akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Kinondoni baada ya kuhutubia kilele cha Maadhimisho ya kutimia Miaka 25 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyofanyika leo Sept 24,2019 Kinondoni Jijini Dar es salaam, Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli kwenye maadhimisho hayo.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hasssan, akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mafunzo katika Chuo Kikuu Huria Prof. Emmanuel Kigabe, kuhusu Vitabu vya kumbukumbu ya Utafiti wa aina mbalimbali kwenye maonesho ya kilele cha Maadhimisho ya kutimia Miaka 25 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyofanyika leo Sept 24,2019 Kinondoni Jijini Dar es salaam, Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli kwenye maadhimisho hayo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hasssan, akipata maelezo kutoka kwa Sebastian Sambuo Mushi, kuhusu Utaalamu na Biashara ya Mchele kwenye maonesho ya kilele cha Maadhimisho ya kutimia Miaka 25 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyofanyika leo Sept 24,2019 Kinondoni Jijini Dar es salaam, Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli kwenye maadhimisho hayo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

WAZIRI KIGWANGALLA ATOA SOMO KUHUSU UHIFADHI KWA WANANCHI WANAOISHI HIFADHI YA NGORONGORO

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na viongozi na Wazee wa Kimila wa Kabila la Masai wanaoishi katika eneo la hifadhi ya Ngorongoro , viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro alipokutaa nao kujadili changamoto za hifadhi ya Ngorongoro na hatua shirikishi za uhifadhi zilizopangwa kuchukuliwa na Serikali kwa wananchi wanaoishi katika eneo hilo.
Baadhi ya viongozi na Wazee wa Kimila wa kabila la masai wanaoishi katika eneo la hifadhi ya Ngorongoro wakifuatilia kwa makini mkutano kati yao na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla wilayani Ngorongoro.

PICHA – Aron Msigwa – WMU.

MATUKIO KATIKA PICHA ZIARA YA WAZIRI KAIRUKI KIWANDA CHA KUCHAKATA MAHINDI CHA JKT MLALE

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki akioneshwa mitambo ya kuchakata mahindi na kusaga unga wa sembe na Mkuu wa Kikosi cha JKT Mlale Kanali Absolomon Shausi alipotembelea kukagua namna Kikosi hicho kilivyowekeza katika shughuli za uzalishaji.Kiwanda hicho kipo Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.
Baadhi ya mifuko ya unga wa sembe inayotengenezwa na kiwanda cha JKT Mlale iliyohifadhiwa tayari kwa ajili ya kupelekwa sokoni
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kikosi cha JKT Mlale Kanali Absolomon Shausi kuhusu magunia ya pumba za mahindi yaliyohifadhiwa baada ya kuchakata na kutoa unga wa sembe katika kiwanda hicho.
Baadhi ya vijana wa JKT wakiimba wimbo wa kumkaribisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki (hayupo pichani) alipotembelea kiwanda cha kuchakata mahindi cha JKT Mlale mkoni Ruvuma.Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki akiteta jambo na Mkuu wa Kikosi cha JKT Mlale Kanali Absolomon Shausi alipotembelea kiwanda cha kuchakata mahindi cha JKT Mlale mkoni Ruvuma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki akipokea zawadi ya unga wa sembe unaotengenezwa katika kiwanda cha kuchakata mahindi kinachomilikiwa na Kikosi cha JKT Mlale alipotembelea kiwandani hapo Septemba 23, 2019.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki akizungumza na vijana wa JKT waliopo katika kikosi cha JKT 842 Mlale wakati wa ziara yake.
Sehemu ya Watumishi wa Serikali waliohudhuria wakati wa ziara hiyo katika kiwanda cha kuchakata mahindi cha JKT Mlale wakifuatilia maelezo ya Waziri Kairuki (hayupo pichani).(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki akisalimiana na baadhi ya watumishi wa Kikosi cha JKT 842 Mlale wanaosimamia kiwanda cha kuchakata Mahindi kinachohudumiwa na kikosi hicho wakati wa ziara yake ya kukagua mazingira ya uwekezaji katika mkoa wa kiwanda hicho kilichopo Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma tarehe 23 Septemba,2019.

Kamanda wa Kikosi cha JKT Mlale Kanali Absolomon Shausi akiwasilisha hotuba yake kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki (hayupo pichani) wakati wa ziara yake katika kiwanda hicho.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki wa kwanza kushoto akifuatilia uwasilishwaji wa hotuba ya Mkuu wa Kikosi cha JKT Mlale Kanali Absolomon Shausi wakati wa ziara yake katika kiwanda cha kuchakata Mahindi kinachosimamiwa na kikosi hicho Septemba 23, 2019

Mkuu wa Kikosi cha JKT Mlale Kanali Absolomon Shausi akiwasilisha hotuba yake kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki (hayupo pichani) wakati wa ziara yake katika kiwanda hicho.

WAZIRI KAIRUKI ATEMBELEA KIWANDA CHA KUCHAKATA MAHINDI CHA JKT MLALE

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki akisalimiana na baadhi ya watumishi wa Kikosi cha JKT 842 Mlale wanaosimamia kiwanda cha kuchakata Mahindi kinachohudumiwa na kikosi hicho wakati wa ziara yake ya kukagua mazingira ya uwekezaji katika mkoa wa kiwanda hicho kilichopo Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma tarehe 23 Septemba,2019.
Kamanda wa Kikosi cha JKT Mlale Kanali Absolomon Shausi akiwasilisha hotuba yake kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki (hayupo pichani) wakati wa ziara yake katika kiwanda hicho.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki wa kwanza kushoto akifuatilia uwasilishwaji wa hotuba ya Mkuu wa Kikosi cha JKT Mlale Kanali Absolomon Shausi wakati wa ziara yake katika kiwanda cha kuchakata Mahindi kinachosimamiwa na kikosi hicho Septemba 23, 2019.
Mkuu wa Kikosi cha JKT Mlale Kanali Absolomon Shausi akiwasilisha hotuba yake kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki (hayupo pichani) wakati wa ziara yake katika kiwanda hicho.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki akioneshwa mitambo ya kuchakata mahindi na kusaga unga wa sembe na Mkuu wa Kikosi cha JKT Mlale Kanali Absolomon Shausi alipotembelea kukagua namna Kikosi hicho kilivyowekeza katika shughuli za uzalishaji.Kiwanda hicho kipo Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.
Baadhi ya mifuko ya unga wa sembe inayotengenezwa na kiwanda cha JKT Mlale iliyohifadhiwa tayari kwa ajili ya kupelekwa sokoni.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kikosi cha JKT Mlale Kanali Absolomon Shausi kuhusu magunia ya pumba za mahindi yaliyohifadhiwa baada ya kuchakata na kutoa unga wa sembe katika kiwanda hicho.
Baadhi ya vijana wa JKT wakiimba wimbo wa kumkaribisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki (hayupo pichani) alipotembelea kiwanda cha kuchakata mahindi cha JKT Mlale mkoni Ruvuma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki akiteta jambo na Mkuu wa Kikosi cha JKT Mlale Kanali Absolomon Shausi alipotembelea kiwanda cha kuchakata mahindi cha JKT Mlale mkoni Ruvuma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki akipokea zawadi ya unga wa sembe unaotengenezwa katika kiwanda cha kuchakata mahindi kinachomilikiwa na Kikosi cha JKT Mlale alipotembelea kiwandani hapo Septemba 23, 2019.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki akizungumza na vijana wa JKT waliopo katika kikosi cha JKT 842 Mlale wakati wa ziara yake.
Sehemu ya Watumishi wa Serikali waliohudhuria wakati wa ziara hiyo katika kiwanda cha kuchakata mahindi cha JKT Mlale wakifuatilia maelezo ya Waziri Kairuki (hayupo pichani).

MAWAKALA PEMBEJEO ZA KILIMO NA MIFUMO ARUSHA WATOA USHAURI KWA SERIKALI

$
0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Blog,Arusha

CHAMA cha Mawakala wa pembejeo za kilimo na mifugo mkoani Arusha kimeishauri Serikali kuwashirikisha katika mchakato wa upangaji wa bei elekezi za mbolea kwani ukubwa wa bei hizo unawapa changamoto kubwa wakati wa uuzaji.

Pia wameiomba Serikali kuangali namna ya kuwapunguzia bei za leseni na kodi ya mapato kwa kuwa biashara wanayoifanya ina sura ya kutoa huduma zaidi kuliko biashara.

Wakizungumza leo wanachama wa chama hicho wakati wa mkutano huo uliofanyika mkoani hapa wamesema lengo la kukutana kwao pamoa na mambo mengine watajadili rasimu ya Katiba ya chama hicho na kupatiwa vyeti vya mafunzo waliohitimu ya namna ya kutambua viatilifu feki na vizuri.

Kuhusu bei ya mbolea, Mwenyekiti wa Chama cha Mawakala wa Pembejeo za Kilimo Mifugo wa Mkoa wa Arusha (ARAAFARMA) Titus Rweyumamu amesema bei kubwa za mbolea ambazo zinapangwa zinawaumiza wao kwani wateja wengi wao wengi ambao ni wakulima wanashindwa kuzimudu.

"Ingekuwa vizuri iwapo Serikali ingekuwa inatushirikisha katika mchakato wa upangaji wa be.Sisi ndio tunajua wateja wetu wapo maeneo gani na uwezo wao kiuchumi ili kumudu bei za pembejeo hizo za kilimo na mbolea.

"Ni imani yetu kuwa tutashirikiana vizuri na Serikali kufanikisha lengo la kuwa hudumia wakulima ili kufikia malengo yao ya uzalishaji wa mazao ya kilimo kwa kiwanago cha juu na hii inawezekana kabisa,"amesema .

Kwa upande wake Katibu wa Chama hicho Humphrey Mswia amesema wataendelea kushirikiana na Serikali nao ili waendelee kutoa huduma bora kwa wakulima wote.

Pia amesema lengo kubwa la kukutana ili kupita rasimu ya Katiba ya chama hicho ambacho kinafanya kazi ya kuwaleta pamoja mawakala wote wa pembejeo mkoani Arusha kwa lengo la kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria za nchi.

"Mkakati wetu ni kutoa huduma bora kwa wakulima ili kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao ya kilimo na mifugo pamoja na kufanikisha kauli mbiu ya Serikali ya viwanda. Tunafahamu kilimo ndicho kitakachotoa malighafi kwa ajili ya viwanda vyetu,"amesema.

Ameongeza kuwa wataendelea kufanya utafiti wa matumizi bora ya pembejeo, dawa na Masoko.Pia kufanya utetezi na ushawishi kwa wakulima mawakala wa pembejeo za kilimo na mifugo kutoa elimu ya kuhifadhi na kuendeleza mazingira kwa wanachama najamii nzima kwa ujumla. 

Wakati huo huo mgeni rasmi wa mkutano huo ambaye ni Ofisa Mipango Mkoa wa Arusha Moses Mabula amesema Serikali itashirikiana nao bega kwa bega kuhakikisha wanawapa huduma bora wakulima na wafugaji.

Amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha wananchi wake wanapata elimu ya matumizi sahihi ya pembejeo za kilimo.Aidha amewaahidi wanachama hao kuwatafutia wataalamu ambao watawapa elimu na mafunzo ili nao wawaelimishe wakulima.

Pia amesema itaendelea kutafuta ufumbuzi wa changamoto ambazo zimeanishwa na chama hicho.
 Afisa mipango ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha Moses Mabula akitoa nasaaha zake mara baada ya kuwafungulia mkutano wao 

TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA KIMATAIFA WA SHERIA KATI YA AFRIKA NA ASIA

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria PROF. Sifuni Mchome katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali kutoka Serikalini baada ya kumalizika kwa kikao cha kufahamishana kuhusu Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa AALCO utakaofanyika mwezi Oktoba jijini Dar es Salaam.
Wadau kutoka taasisi mbalimbali serikalini wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome alipokuwa akizungumza nao kuhusiana na Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano wa AALCO utakaofanyika mwezi ujao jijini Dar es Salaam.
Wadau kutoka taasisi mbalimbali serikalini wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao kuhusiana na Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano wa AALCO utakaofanyika mwezi ujao jijini Dar es Salaam.







Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria PROF. Sifuni Mchome akizungumza katika kikao na wadau mbalimbali kutoka Serikalini (hawako pichani) kuhusiana na Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Mashauriano ya Masuala ya Kisheria ya Nchi za Asia na Afrika (ASIA-AFRICAN LEGAL CONSULTATIVE ORGANISATION (AALCO) utakaofanyika nchini kuanzia tarehe 21 hadi 25, Oktoba jijini Dar es Salaam.
…………………

Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Mashauriano ya Masuala ya Kisheria ya Nchi za Asia na Afrika (ASIA-AFRICAN LEGAL CONSULTATIVE ORGANISATION (AALCO) utakaofanyika nchini kuanzia tarehe 21 hadi 25, Oktoba jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria PROF. Sifuni Mchome amesema mkutano huo utawakutanisha Mawaziri wa Sheria na Wanasheria Wakuu kutoka nchi za Afrika na Asia ambao kwa pamoja wataangalia maendeleo ya sekta ya sharia na kujadili changamoto mbalimbali zinazozikabili nchi wanachama na jinsi ya kukabiliana nazo.

Prof.Mchome amesema katika mkutano huo Tanzania itakabidhiwa kiti cha Uenyekiti wa Jumuiya hiyo kupitia kwa Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga ambaye atatumikia kiti hicho kwa mwaka mmoja.

Prof. Mchome alikuwa akizungumza na wadau mbalimbali kutoka Serikalini Ofisini kwake katika Mji wa Serikali Mtumba jijijini Dodoma ambao aliwaomba kuuungana na Wizara ya Katiba na Sheria katika kuhakikisha Mkutano huo utakaoitangaza nchi kimataifa unafanikiwa.

AALCO ilianzishwa mwaka 1956 kwa lengo la kuwa chombo cha ushauri na ushirikiano katika masuala ya sheria za kimataifa kwa nchi za Asia na Afrika. 

Toka kuanzishwa kwake AALCO imewezesha nchi wanachama kushirikiana na kubadilishana uzoefu katika masuala mbalimbali ya sheria za kimataifa na kimechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya sheria za kimataifa.

Tanzania ilijiungana umoja huo 1973 na kwa sasa Katibu Mkuu wake ni Mtanzania Prof. Gastorn ambaye alichaguliwa kushika nafasi hiyo mwezi Agosti 2016.

WANAOJIHUSISHA KUFANYA NGONO NA WANAFUNZI WAONYWA MKOANI ARUSHA

$
0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

SERIKALI ya Mkoa wa Arusha imekemea tabia ya baadhi ya watu wanaofanya vitendo vya ngono na wanafunzi kwani tabia hiyo imekuwa ikisababisha mimba za utotoni na hatimaye kukwamisha ndoto za wanafunzi hao katika maisha.

Akizumgumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, Mkuu wa Wilaya ya Longido Frank Mwaisumbe amesema wenye tabia hiyo ya kujihusisha na vitendo vya ngono na wanafunzi waache tabia hiyo mara moja.

Mwaisumbe aliyekuwa katika mahafali ya 10 katika Shule ya Msingi Arusha Alliance iliyopo jijini hapa amesisitiza Serikali haitavumilia kuona vitendo hivyo vinaendelea na itawachukulia hatua kaliza kisheria wote watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo viovu dhidi ya wanafunzi.

"Waacheni wanafunzi wasome kwa manufaa yao ya baadaye.Kwanini wawafuate watoto wadogowakati wako watu wazima ambao wako na
uhitaji wa kuolewa na mnaishi nao huko mitaani,"amesema Mwaisumbe.

Pia amewasihi wanafunzi kuzingatia maadili mema waliyofundishwa shuleni hapo na kuacha kujihusisha na makundi maovu mitaani ikiwemo vitendo vya ngono na utumiaji wa madawa ya kulevya.

"Jitahidi sana kwenye masomo na kujiendeleza kielimu kwani elimu mliyoipata hapa ni mwanzo tu wa safari ya kimasomo ambayo iko mbele
yenu kwani mtatakiwa msome hadi vyuo vya elimu ya juu na kutimiza ndoto mlizojiwekea katika maisha,"amesema.

Awali Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ArushaAlliance Silas Msuya amesema shule hiyo ilianzishwa mwaka 2007 ikiwa na wanafunzi 18 na sasa imefikisha wanafunzi 800.

Amesema katika mahafali hayo jumla ya wanafunzi 133 wamehitimu na kutumia nafasi hiyo kuwaomba wakawe mabalozi pindi watakapokuwa majumbani kwao wakisubiri matokeo ya mtihani.
Mkuu wa Wilaya yaLongido,Frank Mwaisumbe alipokuwa akizungumza  kwa niaba ya mkuu wa mkoa katika mahafali ya kumi ya shule ya msingi ya Arusha Alliance iliyopo jijini humo.

DKT. KIJAJI AAGIZA MILANGO YA KITUO CHA AFYA BUSI ING’OLEWE BAADA KUTOKIDHI VIWANGO

$
0
0
Dkt. Alpha Kwilasa wa Kituo cha Afya Busi, wilayani Kondoa mkoani Dodoma, akimueleza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambae pia ni Mbunge wa Kondoa Vijijini Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji jinsi walivyojipanga kuanza huduma ya upasuaji ali[potembelea chumba cha kuhifadhia damu salama katika Kituo cha Afya Busi.
Milango iliyowekwa katika Kituo cha Afya Busi, ambayo Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambae pia ni Mbunge wa Kondoa Vijijini Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji ameagiza kung’olewa baada ya kuwa chini ya kiwango alipotembelea Kituo hicho.
Jengo la Maabara katika Kituo cha Afya Busi linalotumika kutoa huduma kwa wanakijiji wa kijiji hicho wilayani Kondoa.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango ambae pia ni Mbunge wa Kondoa Vijijini Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akionesha ufa kwenye fremu ya mlango aliyoagiza ing’olewe kwa kuwa chini ya kiwango kabla ya kuleta madhara kwa wagonjwa na watumishi wa Kituo hicho alipotembelea Kituo cha Afya Busi, wilayani Kondoa.
……………………

Na Josephine Majura, Kondoa

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amemuagiza Kaimu Mhandisi wa Wilaya ya Kondoa, Felcitism Tesha kung’oa milango yote katika Kituo cha Afya Busi kutokana kutokuwa na viwango vya kuridhisha.

Ametoa agizo hilo alipofanya ziara ya kikazi katika Kijiji cha Busi wilayani Kondoa kukagua utekelezaji wa miradi ya Ujenzi wa Vituo vya Afya vinavyojengwa kwa fedha za Serikali.

Dkt. Kijaji ambae pia ni Mbunge wa Kondoa Vijijini alisema kuwa hajaridhishwa na milango iliyowekwa katika kituo hicho kwa kuwa ubora wake hauendani na thamani ya fedha iliyotolewa kwa ajili ya utengenezaji wa milango hiyo.

Alisema fedha iliyotengwa kwa ajili ya milango hiyo ni kubwa zaidi ya milango inavyoonekana, hali inasababisha kuhatarisha usalama wa wagonjwa na watumishi wa kituo hicho.

“Nina agiza milango yote iliyowekwa ikiwa chini ya kiwango ibadilishwe kwa gharama za fundi aliyepewa tenda hiyo bila kutumia hata shilingi moja ya Serikali, milango haina hata mwaka imeanza kupasuka.”,alisisitiza Dkt. Kijaji.

Aidha, alitoa wito kwa Uongozi wa Wilaya kwa kushirikiana na Kamati ya Ujenzi ya Kijiji hicho kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kikamilifu katika kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo inayofadhiliwa na Serikali ili kubaini mapungufu na kuyafanyia kazi mapema.

Aliongeza kuwa fedha zilizotolewa na Serikali ni nyingi hivyo lazima vifaa vinavyotumika katika ujenzi wa vituo hivyo viendane na thamani ya fedha hizo na Wananchi waone kazi nzuri na kubwa inayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano katika Sekta ya Afya.

Naye Kaimu Mhandisi wa Wilaya ya Kondoa, Bw. Felcitism Tesha alimuahidi Dkt. Kijaji kwamba atatekeleza agizo hilo na kuhakikisha milango hiyo inabadilishwa kwa haraka kabla ya kuleta madhara kwa wagonjwa na watu wengine katika kituo hicho.

Kwa upande wake Mwanakijiji wa Busi, Bw. Hussein Ally, ameishukuru Serikali kwa juhudi mbalimbali inayofanya katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo hasa huduma za jamii na kusifia huduma inayotolewa na watumishi wa Kituo cha Afya Busi.

WAZIRI LUGOLA ASHANGAZWA NA KAZI ZA MIKONO ZA WALEMAVU KATIKA TAMASHA LA JAMAFEST

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania Kangi Lugola akiangalia kitenge aina ya Batiki mara baada ya kutembelea banda la watu wenye ulemavu katika Tamasha la JAMAFEST linaloonesha utamaduni na sanaa wa nchi za Afrika mashariki linaloendelea kufanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania Kangi Lugola akizungumza na Fundi Selimala ambaye ni mremavu wa macho mara baada ya kutembelea banda la watu wenmye ulemavu waliohudhuria katika maonesho ya tamasha la JAMAFEST linaloonesha utamaduni na sanaa wa nchi za Afrika mashariki linaloendelea kufanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kazi za mikono zikiendelea katika banda la watu wenye ulemavu katika tamasha la JAMAFEST.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania Kangi Lugola akizungumza na fundi cherehani mara baada ya kutembelea banda la watu wenye ulemavu katika maonesho ya tamasha la JAMAFEST linaloonesha utamaduni na sanaa wa nchi za Afrika mashariki linaloendelea kufanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania Kangi Lugola akiangalia nguo za wajasiliamali zilizoshonwa kwa mkono hii ni katika Tamasha la Maonesho ya JAMAFEST linaloendelea kufanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania Kangi Lugola akiangalia maua ya asilia katika banda la mimea asilia lililopo katika Tamasha la JAMAFEST linalohusisha nchi sita za afrika mashariki linalofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania Kangi Lugola akiangalia kwa mshangao Mkoba uliotengenezwa kwa vifuu vya nazi na shanga kwaajili ya kupendezesha. Hii ni katika Tamasha la JAMAFEST linaloonesha utamaduni na sanaa wa nchi za Afrika mashariki linaloendelea kufanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania Kangi Lugola akizungumza na afisa wa wizara ya maliasili na utalii katika maonesho ya tamasha la JAMAFEST linaloonesha utamaduni na sanaa wa nchi za Afrika mashariki linaloendelea kufanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

SHULE YA PRECIOUS TALENT YAFUNGWA HADI WIKI IJAYO

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Globu ya Jamii.

SHULE binafsi ya Precious Talent iliyopo Ngando, Nairobi nchini Kenya imefungwa hadi wiki ijayo ili kupisha uchunguzi wa vifo vya wanafunzi nane waliofariki baada ya kuangukiwa na ukuta wa darasa hapo jana.

Kupitia televisheni ya Citizen nchini humo imeripotiwa kuwa mmiliki wa shule hiyo bado anahojiwa na jeshi la Polisi katika kituo cha  cha kabete ambako baadhi ya wazazi pia wamefika kituoni hapo kwa ajili ya kuandikisha maelezo yao.

Mkuu wa polisi wa kituo cha polisi cha Kabete amesema kuwa uchunguzi umeanza kwa kuuliza maswali kwa mmiliki na kwa baadhi ya wazazi na baadaye kwa mamlaka zinazotoa vibali ya ujenzi, leseni na jengo na hatua zote za kusimamisha shule.

Vilevile amesema kuwa wanahitaji muda zaidi ili kuweza kufahamu chanzo hasa cha kuanguka kwa ukuta huo uliosababisha wanafunzi wanane kufariki dunia.

Imeelezwa kuwa mmoja ya wazazi waliofika kituoni hapo ameieleza Citizen Televisheni kwamba amempoteza mtoto wake wa miaka (13)aliyekuwa anasoma darasa la nane ambaye angefanya mtihani wa taifa mwaka huu.

Mzazi huyo ameeleza kuwa alitembelea shule hiyo siku ya ijumaa na aliona sehemu ya darasa imedidimia na alipomuuliza mwalimu aliambiwa mahali hapo waliweka kuni na alihakikishiwa hakuna tatizo lolote.

Kufuatia janga hilo Serikali nchini humo itagharamia matibabu kwa majeruhi pamoja na mazishi kwa watoto waliopoteza maisha.

Bodi ya Filamu yawaasa kutembelea bodi hyo katika tamasha la Jamafest

$
0
0
Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Dkt. Kiagho Kilonzo akizungumza na waandishi habari katika maonesho ya Tamasha la Utamduni wa Juimuiya ya Afrika Mashariki (Jamafest)linalofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 

Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Nchini  Dkt.Kiagho Kilonzo ameutaka umma wa watanzania kutembelea bodi ya Filamu katika tamasha la Utamaduni wa Jumuiya ya Afrika Mashariki  (Jamafest) katika kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na bodi hiyo.

Kaimu Katibu Mtendaji Dkt.Kilonzo ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi habari katika maonesho hayo na kuwaasa watanzania kutumia chombo hicho katika kukuza sanaa ya filamu nchini kwa kuleta maendeleo.

Amesema kuwa katika maonesho hayo wataona vitu mbalimbali ambavyo vimefanywa na watanzania  kwa kutengeneza filamu ambazo zina maadili na pale ambapo wanaona filamu zilizozalishwa hazina maadili wanachukua hatua kuhakikisha hazionyeshwi.

Dkt. Kilonzo amesema kuwa maonesho hayo ni fursa kwa Tanzania na kuona namna ya nchi wanachama wengine  wanavyofanya utamduni wao  huku  wakijifunza utamduni wetu.

"Natarajia wataopita katika banda la bodi ya filamu watajifunza vitu vingi ambavyo vitawasaidia kuingia katika sekta ya filamu na kuweza kuzalisha ajira zao pamoja na taifa kupata maendeleo katika sekta hiyo"amesema Dkt. Kilonzo.

MAAGIZO YA IGP SIMON SIRRO KWA MAKAMANDA JESHI LA POLISI NCHINI

$
0
0
Na Said Mwishehe, Globu ya Jamii.

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro ametoa maagizo kwa makamanda wa Polisi wa Mikoa na vikosi vya Polisi kujiepusha na vitendo vya rushwa na kufanya kazi kwa weledi wa hali ya juu pamoja na kushiriki kikamilifu kuunga mkono jitihada za Serikali kufanisha Tanzania ya viwanda.

Akizungumza leo Septemba 24,mwaka 2019 jijini Dar es Salaam wakati  wa kufungua mkutano wa siku tatu wa  kutathimini utendaji kazi wa Jeshi hilo IGP Sirro  ametumia nafasi hiyo kueleza mambo kadhaa ili kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria huku pia akikemea tabia ya vitendo vinavyofanywa na baadhi yao kiasi cha kuchafua sifa ya jeshi hilo.

IGP Sirro amesema jeshi la Polisi lazima liendelee kulinda usalama wa raia na mali zao na hatarajii kuona jeshi hilo linakuwa chanzo cha migogoro kati yake na wananchi.

Katika mkutano huo IGP Sirro amesema kuwa amezungumzia umuhimu wa Jeshi la Polisi kuhakikisha katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajia kufanyika Novemba mwaka huu linafanya kazi zake kwa umakini zaidi ikiwa pamoja na kuhakikisha nchi yetu inaendelea kuwa salama na amani iliyopo inaendelea kudumu.

"Haturajii jeshi letu la polisi kuwa chanzo cha kuvuruga amani, tunakwenda kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa na mwakani uchaguzi mkuu, ni lazima tuwe makini kwa kuhakikisha tunafanya kazi kwa weledi,"amesema.

Kuhusu rushwa, IGP Sirro amesema bado kuna baadhi ya askari polisi wamekuwa wakitengeneza mazigira ya kupata rushwa ambapo ametumia nafasi hiyo kutoa onyo kwa wenye kujihusisha na rushwa ndani ya jeshi hilo.

"Kuna baadhi ya askari polisi bado wanaendeleza vitendo vinavyoashiria kuomba rushwa kwa wenye kutenda makosa na hasa barabarani.Jeshi la Polisi halitaki kuona rushwa kwa watumishi wake na hivyo wenye tabia ya kujihusisha na rushwa kuacha mara moja,"amesema IGP Sirro.

Amewataka makamanda na makamishina wote nchini kuhakikisha wanasimama kidete kukomesha rushwa na kuwataka kila mmoja kwa nafasi yake kukemea vitendo vya rushwa."Bado kuna askari polisi wanachukua rushwa hadharani wanaposimamisha mabasi."

Pamoja na mambo mengine IGP Sirro ametumia nafasi hiyo kuonesha kusikitishwa na baadhi ya makamanda wa mikoa kutokamilisha kwa wakati ujenzi wa nyumba za watumishi katika mikoa yao ambapo amewaagiza kuharakisha ujenzi wa nyumba hizo.

Kuhusu jeshi la polisi kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk.John Magufuli amesema ili maendeleo ya nchi hii yaweze kupatikana yanahitaji nchi kuendelea kuwa salama na hivyo jeshi hilo litaendelea kutimiza majukumu yake kikamilifu. "Jeshi la Polisi tutaendelea kusimama imara kulinda usalama wa nchi yetu."

Wakati huo huo IGP Sirro amewataka makamishna wa mikoa kuwaanda askari vijana ambao watashika nafasi zao ili wao kurejea makao makuu kwa ajili ya utungaji wa sheria na ushauri  kwani ni vyema kuwa na damu changa itakayoweza kufanya kazi kwa nguvu zaidi kuliko kung'ang'ania nafasi hizo za ukamishna.

KAIRUKI AIPA SIKU SABA TIC

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu katika Masuala ya Uwekezaji nchini Mhe.Angellah Kairuki ameutaka uongozi wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) kutembelea na kukagua  mazingira ya wafanyabiashara na wawekezaji wazawa waliopo mkoa wa Ruvuma ndani ya siku saba.

Ametoa kauli hiyo alipotembelea na kukagua kiwanda cha kutengeneza kahawa cha Wilaya ya Mbinga cha MCCCO pamoja na kiwanda cha DAE kwa lengo la kukagua mazingira na utendaji wa viwanda hivyo Mkoani Ruvuma.

Ziara hiyo iliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe.Christina Mdeme pamoja na watendaji kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Wizara ya Viwanda, Wizara ya Kilimo, Wizara ya Nishati, Wizara ya Madini, Wizara ya Ardhi, pamoja na baadhi ya taasisi za serikali ikiwemo na Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC)

Waziri Kairuki alitoa maelekezo hayo baada ya kubaini kuwa taasisi hiyo haijawafikia wawekezaji wazawa kikamilifu hususani waliopo mikoani ili kuwatambua na kuwaeleimisha kuhusu fursa zinazotolewa na taasisi hiyo.

“Ninawaagiza TIC mfike katika viwanda hivi ndani ya siku saba kuanzia sasa ili kuwatembelea na kuwaeeleza huduma zinazotolewa na taasisi yenu ikiwemo fursa zilizopo na endapo wataona inafaa wajisajiri kwa kuwa ni suala la hiari,”alisisitiza Waziri Kairuki

Aidha alieleza kuwa ipo tija ya kuwatambua wawekezaji wazawa waliopo nchini ka kuzingatia mchango wao katika uchumi wa viwanda kwa kuzingatia mwaka huu 2019 ni mwaka wa uwekezaji.

“Naelewa kuwa ipo miradi mingi iliyofikiwa na TIC zaidi ya asilimia 72 hivyo niwatake mfike haraka mkoani Ruvuma hususan katika viwanda hivi vya kahawa, ili kuvitambua na kueleza fursa na umuhimu wa kujisajili na Taasisi hii ili kuendelea kuchangia na kuwa na tija zaidi katika uchumi wa nchi,”alisisitiza

Mkurugenzi wa sera mipango na utafiti wa TIC Mafutah Bunini amesema katika kuboresha utendaji wao wamefungua ofisi za kanda saba ili kuwafikia kwa urahisi wawekezaji wa ndani na kwamba wanaotoa uzioto sawa kwa wawekezaji wa ndani na nje.

“Na katika hili ndio maana viwango vya mitaji ya uwekezaji vinatofautiana kwa wawekezaji wa nje na ndani ambapo mwekezaji wa ndani anatakiwa awe na mtaji wa dola laki moja lakini mwekezaji wa nje ni dola laki tano
Naye meneja wa kiwanda cha kutengeneza kahawa cha wilaya ya Mbinga (MCCCO) amemuahakikishia Waziri kuwa wataendelea kuboresha mazingira mazuri ya wafanyakazi na kuongeza thamani ya bidha zao za kahawa na kuhakikisha jamii iliyowazunguka inanufaika na kiwanda hicho.

“tunaishukuru Wizara ya Uwekezaji kwa jitihada inazofanya za kuboresha mazingira ya uwekezaji kwa kuondoa vikwazo mbalimbali vilivyokuwepo awali hali inayosababisha uwekezaji kukua kwa kasi”

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha kutengeneza kahawa cha DAE Bw. Danistan Komba ambaye pia ni mkulima wa kahawa alimpongeza waziri kwa kutembelea kiwandani hapo na kueleza changamoto za masoko ya kahawa na kuiomba Serikali kuendelea kuwaangalia wawekezaji hao wazawa.

“Kipekee napongeza ujio wako, japo tunachangamoto ya masoko kwa kuzingatia kiwanda kina uwezo wa kuzalisha tani 36,000 kwa mwaka na kuuza katika baadhi ya nchi ikiwemo.Alifafanua kuwa, pamoja na changamoto za uhaba wa masoko, kiwanda kimekuwa kikishiriki katika maonesho ya nchi zinazolima kahawa ikiwemo Kenya, Uganda,Rwanda,Burundi na Ethiopia.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Cosmas Nshenye alieleza kuwa, ziara hiyo imeleta chachu kwa wafanyabiashara na wawekezaji wazawa kwa kuzingatia kuwa, Serikali imeahidi kutoa ushirikiano wa kina katika kutatua changamoto zao ikiwemo kuwataka TIC kufika na kuwatembela katika muda alioagiza.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu katika Masuala ya Uwekezaji nchini Mhe.Angellah Kairuki akiweleza jambo wawekezaji waMgodi wa Makaa ya Mawe ya kutoka kampuni ya Mil Coal,Mbinga mkoani Ruvuma. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu katika Masuala ya Uwekezaji nchini Mhe.Angellah Kairuki amkimsikiliza mmoja wa Wakulima wa zao la Kahawa,wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu katika Masuala ya Uwekezaji nchini Mhe.Angellah Kairuki akipewa maelezo kwenye moja ya kiwanda  kinachotengeneza tengeneza kahawa wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma 

MAFUNZO YA MASHEHA WA KUSINI KUHUSU KUTATHMINI HALI YA KUKABILIANA NA MAAFA

$
0
0
Mkuu wa Kitengo cha Mipango Utawala na Rasilimali Watu kutoka Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Haji Faki Hamdani akitoa mafunzo kwa mwenyeviti wa kamati za kukabiliana na maafa cha kutathmini hali ya majanga katika shehia za wilaya ya kusini unguja huko katika Ukumbi wa Afisi za Mkuu wa Wilaya Makunduchi kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Elimu Ushauri Nasaha na Tafiti Haji Ame Haji na Mwenyekiti wa Masheha Ali Haji Mkadam wa Bwejuu Dongwe.

Wenyeviti wa kamati za kukabiliana na maafa kutoka katika shehia mbali mbali za Wilaya ya Kusini Unguja wakisikiliza mafunzo kwa Mkuu wa Kitengo cha Mipango, na Rasilimali Watu kutoka Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Haji Faki Hamdani ambae hayupo pichani kuhusu jinsi ya kukabiliana na maafa katika shehia zao huko katika ukumbi wa Mkuu wa Wilaya ya Kusini Makunduchi.


Wenyeviti wa kamati za kukabiliana na maafa kutoka katika sheha mbali mbali za Wilaya ya Kusini Unguja wakisikiliza mafunzo kwa Mkuu wa Kitengo cha Elimu Ushauri Nasaha na Tafiti Haji Ame Haji ambae hayupo pichani kuhusu jinsi ya kushirikiana na vyombo vya uokozi wakati wa zoezi la uwokozi pindi maafa yakitokea huko katika ukumbi wa Afisi ya Mkuu wa Wilaya Makunduchi.

*************************************

Na Khadija Khamis- Maelezo Zanzibar 24/09/2019.

Masheha wa Wilaya Kusini Unguja wametakiwa kujua majukumu ambayo yanayowapasa kukabiliana nayo pindipo yakitokea maafa katika shehia zao ili kupunguza adhari zinazoweza kujitokeza .

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Kitengo cha Mipango, na Rasilimali Watu kutoka Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Haji Faki Hamdani wakati wa kikao cha kutathmini hali ya majanga katika shehia za Wilaya ya Kusini Unguja na Wenyeviti wa kamati ya kukabiliana na maafa

Alieleza kuwa Masheha wa shehia mbao ndio wenyeviti wa kamati ya kukabiliana na maafa iko haja ya kuongoza zoezi la kuondoa au kupunguza viashiria vya majanga katika shehia husika pamoja na kutoa elimu ya kukabiliana na maafa katika shehia zao.

Alifahamisha kuwa masheha waweze kuielimisha jamii njia sahihi za mawasiliano wakati wa dharura inapotokea pia kutenga eneo la makazi wakati wa dharura ndani ya Shehia zao .

Aidha alisema janga ni tukio ambalo linaweza kupelekea maafa na kusababisha adhari kubwa kwa jamii na vilevile maafa ni tukio kubwa ambalo linapelekea adhari ikiwemo vifo na upotevu wa mali .

Mkuu huyo aliwataka masheha kuwa pamoja na jamii hasa kwa wale ambao wamepatwa na majanga ili kuweza kuwafariji pamoja na kushajihisha wengine kwa kuweze kuwasaidia .

“Rasilimali watu ni hazina kubwa kwa maendeleo ya shehia na nchi kiujumla hivyo jamii iweze kuweka tahadhari katika majanga ambayo yanasababishwa na binaadamu “.alisema Mkuu huyo .

Hata hivyo alisema kuna majanga ambayo huwezi kuyaepuka ambayo yanasababishwa na majanga ya kimaumbile ikiwemo kimbunga ,mvua kubwa za mafuriko mtetemeko wa ardhi na mengineyo hayo husababisha vifo na upotevu wa mali kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi .

Nae Mkuu wa Kitengo cha Elimu Ushauri Nasaha na Tafiti Haji Ame Haji amewataka wenyeviti hao kuratibu ufanyaji wa tathmini ya awali juu ya athari iliyojitokeza baada ya maafa na ripoti iwasilishwe kwa wahusika pamoja na kufahamisha aina ya mahitaji wanayohitajia wahanga .

Vilevile mkuu wa kitengo cha elimu huyo aliwataka wenyeviti hao kutunza kumbukumbu za matukio ya majanga yanayotokea katika shehia zao ili kusaidia kurejesha hali kulingana na uwezo wao.

Kwa upande wa wenyeviti hao wamesema kuwa wanakazi kubwa kuielewesha jamii kwani wananchi hawajui majanga wala ajali wanachotaka wao wafanye wapendalo .

Wenyeviti hao waliiyomba Serikali za Halmashauri kufika katika maeneo ya shehia zao ili kuona hali halisi ya mpango miji inayojengwa na kuweza kutoa ushauri kwa wananchi .

Wenyeviti hao walisema kuwa Sheha ni jina kubwa lakini halina kitu hivyo wakati mwengine hupata wakati mgumu kwa jamii ambapo huwa ni tegemeo lao kubwa la kupata kupewa mkono wa pole .
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live




Latest Images