Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110144 articles
Browse latest View live

BODI YA UTALII YAWATAKA WANANCHI KUJITOKEZA KWA WINGI KUPIGIA KURA VIVUTIO VYA UTALII IKIWEMO MLIMA KILIMANJARO

$
0
0
Na Karama Kenyunko-Michuzi TV

BODI ya Utalii Tanzania (TTB) imewataka wananchi kujitokeza kwa wingi na kupigia kura vivutio vya utalii ikiwemo kuuchagua mlima Kilimanjaro na Tanzania ili kuweza kuingia katika kinyang'anyiro cha kuwania tuzo za taasisi ya kimataifa ya world Travels Awards ya nchini Uingereza na hatimae kushinda.

Mkurugenzi Mtendaji wa TTB, Devota Mdachi ametoa rai hiyo leo Septemba 23,2019 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya tuzo hizo ambazo sherehe zake kwa washindi zitafanyika Novemba 28, mwaka huu Muscat Oman.

Amesema, katika kinyang'anyiro hicho Tanzania kama kituo cha utalii kinachoongoza kwa safari za kitalii duniani, 2019 inashindanishwa na nchi nyingine 17 za bara la Afrika ambazo in Kenya, Botswana, Namibia, Afrika Kusini,Uganga ambia na Zimbabwe.

"Lakini kuingia tu kwenye kinyang'anyiro hicho haitoshi, jambo la maana zaidi ni kupiga kura, jambo linalotakiwa ni kushinda ili mlima wetu wa Kilimanjaro na Tanzania kama kituo cha Utalii viweze kushinda. Amesema Mdachi.

Amesema Mlima Kilimanjaro uko katika kundi la kivutio cha Utalii kinachoongoza 2019 ukiwa unashindanishwa na vituo vingine 13. 

" Mbali na mlima Kilimanjaro, Kisiwa cha Zanzibar kinashindanishwa na visiwa 18 katika kundi la Kisiwa ambacho ni Kituo cha Utalii kinachoongoza duniani pamoja na Hoteli ya Diamonds la Gemma dell'Est ya Zanzibar ambayo imeingia kugombea tuzo ya duniani katika kundi la Hotel za ufukweni zinazoongoza duniani kwa mwaka huu ikishindanishwa na hotel zingine 17," amesema.

Vituo vingine ni Thanda Island, Essaque Zalu ya Zanzibar, Beyond Mnemba Island Lodge, Chumbe Island Coral Park, Greystoke Mahale na Singita Sasakwa Lodge.

Aidha ameeleza jinsi ya kupiga kura tembelea tovuti ya taaaisi ya World Travel Awards ambayo ni www.world travelawards.com kisha unaingia katika eneo la kupiga kura kisha unajisajili, baada ya hapo utafuata maelekezo mpaka kufikia kupiga kura ambapo amewataka wananchi kuhakikisha wanaupigia kura Mlima Kilimanjaro katika kundi la vivutio vya utalii vinavyoongoza duniani. 
Mkurugenzi Mtendaji wa bodi ya Utalii (TTB),  Devota Mdachi akizungumza na waaandishi wa habari juu ya kuwepo Kinyang'anyiro cha 
 Kuwania tuzo za World Travel Awards zinazotarajiwa kutolewa Novemba 28, mwaka huu huko Muscat Oman. 
 Mwandishi wa Habari, Kibwana Datchi akielekezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TTB, Devota Mdachi namna ya kipiga kura katika kinyang'anyiro hicho.
Mkurugenzi Mtendaji wa bodi ya Utalii (TTB),  Devota Mdachi akiwaonyesha  waaandishi wa Habari namna ya kupigia kura vivutio vya Utalii vya Tanzania ukiwemo Mlima Kilimanjaro ili uweze kupenya katika Kinyang'anyiro cha Kiwania tuzo za World Travel Awards zinazotarajiwa kutolewa Novemba 28, mwaka huu huko Muscat Oman.

Mahakama Kisutu yawaachia huru washitakiwa watano waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi TV,

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewaachia huru washitakiwa watano waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka ya  kujiunganishia isivyo halali bomba la mafuta mali ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).

Hatua hiyo imekuja baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kuwasilisha hati mahakamani hapo kuonesha kuwa hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya washtakiwa na anaondoa kesi hiyo chini ya kifungu namba 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai  ( CPA), sura ya 20 , iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002

Wakili wa Serikali Mwandamizi,  Wankyo Simon amedai kuwa kesi hiyo leo ilikuja kwa ajili ya kutajwa, lakini DPP hana nia ya kuendelea na kesi hiyo dhidi ya washitakiwa hao.Baada ya kueleza hayo,  Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba alisema kupitia kifungu hicho, mahakama imewafutia mashitaka washitakiwa wote  na inawaachia huru.

 Washitakiwa walioachiwa katika kesi hiyo ni Audai Ismail (43) ambaye ni mkazi wa Kibaha, Chibony Emmanuel, Roman Abdon, Amina Shaban na Zubery Ally.

Washitakiwa wote kwa pamoja walikuwa wanakabiliwa na mashitaka matatu likiwemo la kujiunganishia isivyo halali bomba la mafuta, mali ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kinyume cha sheria.

Katika mashitaka ya kwanza, inadaiwa  kati ya mwaka 2015 hadi Januari 8, mwaka huu katika eneo la Tungi Muungano wilaya ya Kigamboni, washitakiwa kwa pamoja wanadaiwa kujiunganishia bomba la mafuta ya dizeli lenye upana wa inchi moja kutoa katika bomba lenye upana wa inchi 24, bila kuwa na kibali kutoka TPA.

Pia wanadaiwa kuharibu miundo mbinu ambapo wanadaiwa kutoboa  bomba la hilo, ambalo  lilikuwa likitumika kusafirisha mafuta,  mali TPA.


Inadaiwa washitakiwa waliharibu  bomba la mafuta mazito lenye upana wa inchi 28, ambalo lilikuwa likitumika kusafirisha mafuta ghafi, mali TPA.

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA BALOZI WA ZIMBABWE NCHINI MJINI DODOMA

$
0
0
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akiteta jambo na Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania, Lt. Jenerali Mstaafu, Anselem Nhamo Sanyatwe baada ya mazungumzo yaliyofanyika leo katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Mjini Dodoma.
Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania, Lt. Jenerali Mstaafu, Anselem Nhamo Sanyatwe akizungumza na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya kongwa wakati alipowatembelea leo Mjini Dodoma. Kushoto kwake ni Spika wa Bunge na Mbunge wa kongwa, Mhe. Job Ndugai na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe. Deogratius Ndejembi.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa pili kushoto) akiongozana na Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania, Lt. Jenerali Mstaafu, Anselem Nhamo Sanyatwe (wa pili kulia) wakati alipotembelea Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa leo Mjini Dodoma. Wa tatu kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe. Deogratius Ndejembi na Wa tatu kushoto ni Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Kongwa, Ndg. White Zuberi.

WATU WATATU WAKAMATWA PWANI KWA KUIBA KOMYUTA MPAKATO ZA SHULE YA MSINGI MSOGA-WANKYO

$
0
0

***********************************
NA MWAMVUA MWINYI,PWANI

JESHI la polisi mkoani Pwani ,linawashilia watu watatu wanaodaiwa kuiba kompyuta mpakato saba zenye thamani ya sh. milioni 4.2 mali ya shule ya msingi Msoga iliyopo Chalinze wilayani Bagamoyo.

Aidha Jeshi hilo, limewakamata watu 67 kwa tuhuma za kufanya uhalifu mbalimbali ,katika misako inayoendelea mkoani hapo.

Kamanda wa Polisi, mkoani humo Wankyo Nyigesa aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake, kuwa siku ya tukio watu wasiojulikana walivunja kwenye shule hiyo na kuiba vifaa hivyo.

Alieleza, tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo baada ya tukio hilo uongozi wa shule ulitoa taarifa polisi ambao walianza msako na walikamata watu hao wakiwa na kompyuta tatu.

“Tunaendelea na uchunguzi kwa watu wengine ambao watakuwa na hizo kompyuta nne zilizobakia ili waweze kufikishwa kwenye vyombo vya sheria,”alisema Wankyo.

Katika tukio jingine Said Athuman (32) Mkazi wa mkoa wa Tanga amekamatwa kwa tuhuma za kukutwa na matairi ya pikipiki 100 na 75 ya bajaji ambayo yanadhaniwa kuwa hayakulipiwa ushuru.


Alieleza, tukio hilo lilitokea septemba 21 mwaka huu majira ya saa 3:00 usiku eneo la Round About kata ya Dunda tarafa ya Mwambao wilaya ya Bagamoyo.

Wankyo alifafanua ,mtuhumiwa huyo alikuwa akitumia gari aina ya Mazda Pick Up yenye namba T 135 DPU ambapo gari hilo lilikamatwa wakati polisi wakiwa doria na inadhaniwa mali hizo zilipitia kwenye bandari bubu zilizopo Bagamoyo.

Pia mkazi wa Lugoba Mtupe Abdala (45) anashikiliwa kwa tuhuma za kusafirishama mbao ngumu 60 kwa kutumia gari lake aina ya Howo lenye namba za usajili T 693 CEH/T 672 DSK bila ya kuwa na kibali.


Hata hivyo ,Wankyo alielezea polisi walimkamata mtuhumiwa septemba 20 eneo la Chalinze Mzee tarafa ya Chalinze wilaya ya Kipolisi Chalinze katika mskao unaoendelea wa usiku na mchana wa kukamata wahalifu.

FORUMCC YAWAKUTANISHA WADAU ZAIDI YA 30 KUCHAMBUA NA KUPITIA TAFITI ZINAZOCHANGANUA CHANGAMOTO ZINAZOIKUMBUKA SEKTA YA NISHATI JADIDIFU

$
0
0
 Mmoja ya wadau wa sekta ya  nishati jadidifu akichangia jambo wakati wa kikao cha wadau wa nishati jadidifu waliokutana leo jijini Dar es Salaam
 Baadhi ya wadau wa sekta ya nishati jadidifu wakijadiliana wakati wa kikao cha wadau hao kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam ambacho limeandaliwa na FORUMCC kwa ufadhili wa HIVOS katika kufanikisha matumizi ya nishati jadidifu ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi
 Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la FORUMCC Euster Kibona (katikati)akiwa katika majadiliano kuhusu nishati jadidifu wakati wa kikao cha wadau wa nishati hiyo waliokutana leo jijini Dar es Salaam
 Mkurugenzi wa FORUMCC Rebeca Munna akizungumza jambo wakati wa kikao cha wadau wa sekta ya nishati jadidifu waliokutana leo jijini Dar es Salaam
 Meneja Programu kutoka Shirika la FORUMCC Angella Damas (katikati) akichangia jambo wakati wa kikao cha wadau waliokutana kujadiliana kuhusu nishati jadidifu
 Mkurugenzi wa FORUMCC Rebecca Munna (wa kwanza kushoto)akishiriki kwenye kikao cha wadau mbalimbali kujadili nishati jadidifu
Jophilline Bejumula kutoka asasi ya Climate Action Network Tanzania ( wa pili kushoto) akichangia mada wakati wa kikao cha majadiliano kilichowakutanisha wadau waliokutana kuweka mikakati kuendeleza nishati jadidifu nchini Tanzania kama sehemu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.



 Na Said Mwisehe,Michuzi TV

WADAU zaidi ya 30 kutoka katika asasi za kiraia na taasisi za Serikali ambazo zinafanya kazi moja kwa moja katika nishati jadidifu nchini Tanzania wamekutana kwa ajili ya kuchambua upitiaji wa tafiti mbalimbali ambazo zimechanganua changamoto zinayoikumbuka sekta ya nishati jadidifu.

Pamoja  na mambo mengine  wadau hao wametumia nafasi hiyo kujadiliana mambo mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha nishati jadidifu inapewa kipaumbele ikiwa ni mkakati wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Akizungumza kuhusu kukutana kwa wadau hao Meneja Programu kutoka Shirika la FORUMCC ambao ndio waaandaji wa mkutano wa wadau hao leo jijini Dar es Salaam Angella Damas amesema kuwa wamekutana ili kuchambua na kupitia tafiti ambazo zimechanganua changamoto zinazozikumba sekta ya nishati jadidifu Tanzania.

Alipoulizwa kwanini nishati jadidifu, Angella amesema kuwa mbali na uwezekano wa kuisha kwa nishati kama mafuta, mabadiliko ya tabia nchi yanapelekea dunia kulazimika kutafuta nishati kupitia njia ambazo ni endelevu (sustainable). 

"Nishati jadidifu inatoa fursa ya kupunguza kuchafua dunia, na pia inazi-address changamoto zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi- kwa mfano, umeme wa grid kama ule unaotumia maji unaweza kukabiliwa na mapungufu kukitokea ukame, ila nishati jadidifu zina njia nyingi za kupatikana kama umeme wa jua, upepo na geothermal hivyo zinatoa fursa mbadala.

Ameongeza kwa kutambua umuhimu huo wa nishati jadidifu, ndio maana FORUMCC imeamua kuwakutanisha wadau hao na kisha kubadilishana uzoefu, kupeana mawazo na kubwa zaidi kujadiliana kwa pamoja na hatimaye kutoka na sauti ya pamoja ambayo italeta mabadiliko chanya katika nchi yetu hasa kwa kuzingatia nishati jadidifu ina faida kubwa sana na umefika wakati wa kupewa kipaumbele.

Pamoja na mambo mengine wadau hao wamejadili namna ambavyo masuala ya jinsi wanavyoweza kuingizwa katika eneo hilo la  nishati jadidifu huku wengine wakitoa rai kuwa ni vema kuaangaliwa upya kwa sera ya nishati na hasa ambayo itajikita katika nishati jadidifu ambayo itawasaida watoa maamuzi na viongozi wa kisiasa kushiriki kikamilifu kuendeleza nishati hiyo nchini ikiwa ni sehemu ya chachu ya maendeleo.

Hata hivyo kwa mujibu wa FORUMCC ni kwamba moja  wa mradi ambao wanausimamia unahusu nishati jadidifu ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ambapo katika hilo ni kuhakikisha nishati safi iwe inamhusu kila mtu na kwamba nishati ndio kichocheo kikubwa cha maendeleo katika nchi na mkutano huo umewakutanisha wadau hao kupitia Shirika la HIVOS ambao ndio wafadhili wa nishati jadidifu.

Awali wakati akifungua kikao hicho Mwenyekiti wa   Bodi ya FORUMCC Euster Kibona amesema maoni na mawazo ya  wadau ni muhimu katika kuhakikisha nishati jadidifu inapewa nafasi na hiyo ni pamoja na kuibua  mijadala itakayokuwa na tija kwa jamii kuhusu matumizi ya nishati jadidifu.

"Suala la nishati ni muhimu katika maendeleo na hivyo bila majadiliano hatutafika katika mahali.ambapo tunatamani, tumeamua majadiliano kuhusu nishati jadidifu yawe huru na tuna kila sababu ya kushirikiana kwa pamoja na lengo ni kuwa na mpango wa pamoja kuhusu nishati jadidifu."amesema Kibona.

Wakati huo huo wadau mbalimbali wametumia nafasi hiyo kuzungumzia umuhimu wa kuhakikisha changamoto zilizopo katika eneo la sekta ya nishati jadidifu zisiwe sababu ya kukwamisha mipango na mikakati yao katika kuendeleza matumizi ya nishati hiyo.


Pia wamesema wakati wanatamani  kuhusu nishati jadidifu wameshauri kuwepo kwa haja ya kuweka mikakati ya kuhakikisha elimu kuhusu matumizi ya nishati jadidifu inapaswa kipaumbele

Wananchi Waendelea Kujitokeza Tamasha la Nne la JAMAFEST

$
0
0
Kikundi cha ngoma toka Tanzania kikitoa burudani ya ngoma ya kabila la wagogo wakati wa Tamasha la Utamaduni wa nchi za Afrika Mashariki (JAMAFEST)mapema hii leo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kikundi cha ngoma toka Tanzania kikitoa burudani ya ngoma ya kabila la wanyihaS wakati wa Tamasha la Utamaduni wa nchi za Afrika Mashariki (JAMAFEST)mapema hii leo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wa shuule msingi Umoja toka Tanzania wakitoa burudani ya ngoma ya kabila la wanyasa wakati wa Tamasha la Utamaduni wa nchi za Afrika Mashariki (JAMAFEST)mapema hii leo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wa shuule msingi Fontain Gate toka Dodoma nchini Tanzania wakitoa burudani ya ngoma wakati wa Tamasha la Utamaduni wa nchi za Afrika Mashariki (JAMAFEST)mapema hii leo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Wananchi wakipata burudani ya ngoma wakati wa Tamasha la Utamaduni wa nchi za Afrika Mashariki (JAMAFEST)mapema hii leo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Wasanii wa maigizo toka nchini Kenya wakitoa burudani wakati wa Tamasha la Utamaduni wa nchi za Afrika Mashariki (JAMAFEST)mapema hii leo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Wasanii toka kituo cha Jeshi la Uokovu wakitoa burudani wakati wa Constantine Kanyasu
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu akiangalia bidhaa mbalimbali za kitamaduni wakati alpotembelea Tamasha la Utamaduni wa nchi za Afrika Mashariki (JAMAFEST) mapema hii leo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

KAMATI YA BUNGE YAPONGEZA UANZISHWAJI MASOKO YA MADINI

$
0
0
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Msukuma akiwa ameshika dhahabu zenye uzito wa kilo moja kila moja katika soko la Madini Geita baada ya Wajumbe wa Kamati hiyo kutembelea soko hilo. Wanaoshuhudia kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Nishati na Madini Dustan Kitandula, kulia nyuma ni Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo pamoja wajumbe wengine na wadau waliokuwa sokoni hapo.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel (wa pili kulia) akiwaongoza Wajumbe wa Kamati kutembelea Soko la Madini Geita. Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Dustan Kitadula na wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo pamoja na wajumbe wa kamati hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel akiwaeleza jambo Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini walipotembelea soko la Madini Geita.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel akimkabidhi Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Dustan Kitandula Mwongozo wa Uwekezaji katika Mkoa wa Geita. Mwongozo huo ulizinduliwa Septemba 22 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa wakati wa uzinduzi wa Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini.
Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Geita Mhandisi Gabriel Mapunda (kushoto) akiwaeleza jambo Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Nishati na Madini wakati walipotembelea soko la Madini Geita.



……………….
Naibu Waziri Nyongo asema Geita inaibeba Sekta

Asteria Muhozya, Boaz Mazigo na Greyson Mwase Geita

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Dustan Kitandula amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli kutokana na kuwepo mfumo rasmi wa mapato ya madini yanayotokana na uanzishwaji wa masoko ya madini na Vituo Vidogo vya Ununuzi katika mikoa mbalimbali nchini.

Ameyasema hayo wakati kamati hiyo ilipokutana na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel wakati wa ziara yao mkoani humo inayolenga kuangalia namna masoko ya madini yanavyoendeshwa pamoja na kuangalia Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanayoendelea mkoani humo katika Viwanja vya CCM Kalangalala.

Aidha, ameupongeza mkoa wa Geita kutokana na kuweka mazingira mazuri ya uendeshaji wa soko la madini ikiwemo mwamko mkubwa wa wadau wa madini wanaotumia soko hilo na kueleza kuwa, soko hilo ni la mfano mzuri wa masoko huku biashara kubwa ya madini ya dhahabu inaendelea kufanyika vizuri sokoni hapo.

Ameongeza kuwa, masoko hayo yamewezesha kupatikana kwa mapato ambayo kabla ya kuanzishwa kwa masoko fedha nyingi zilikuwa zikipotea kutokana na tabia za utoroshaji madini hali ambayo hivi sasa inadhibitiwa na uwepo wa masoko hayo.

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti ameutaka mkoa huo kuangalia namna masuala ya Ulinzi na Usalama yanavyosimamiwa katika uendeshaji wa masoko hayo na kueleza kuwa, yapo malalamiko ambayo yametolewa ikiwemo ucheleweshaji wa muda wa kufungua masoko hayo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel amesema kuwa yapo mapinduzi makubwa yaliyofanywa mkoani humo ambayo yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na Sekta ya madini yakiwemo masuala yanayohusu huduma za Afya na Elimu.

Pia, ameieleza kamati hiyo kuwa, wachimbaji mkoani humo wanapata hamasa ya kuyatumia masoko hayo hali ambayo inapelekea kupata bei halisi ya dhahabu ikiwemo hamasa ya kuanzishwa kwa biashara mbalimbali ambazo zimechangiwa na uwepo wa masoko.

Pia, Mkuu huyo wa Mkoa ameeleza kuhusu mpango wa mkoa huo wa kuwa na eneo rasmi la shughuli za maonesho ambayo lengo ni kufanywa Kimataifa. Mkuu wa Mkoa alisema hayo wakati akijibu hoja ya Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ambaye ameshauri kuhusu maonesho hayo kimataifa zaidi.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Nyongo ameupongeza mkoa huo kwa kuwa na soko linalongooza nchini kwa kuzalisha na kuuza madini likifuatiwa na soko la Madini Chunya.

Naibu Waziri ameongeza kuwa, ni soko linaloongoza kwa kukusanya mrabaha wa serikali ambapo hivi sasa zaidi ya Shilingi Bilioni 2 zinakusanywa kwa mwezi sokoni hapo.

Akizungumzia mauzo ya Soko la Madini Chunya amesema hivi sasa soko hilo linauza hadi kilo 150 kutoka kilo 20 na hivyo kutumia fursa hiyo kuwataka wachimbaji wote na wadau wa madini nchini kuyatumia masoko hayo na kutoyaogopa.

Pia, Naibu Waziri amezuia kukamatwa kwa wadau wote wa madini wanaofuata Sheria na taratibu katika kuyatumia masoko hayo na kuwataka waachwe wafanye shughuli zao.

Akijibu hoja iliyotolewa na wadau wa madini sokoni hapo kuhusu soko hilo kufanya kazi hadi siku ya Jumapili, Naibu Waziri amesema Wizara kupitia Tume ya Madini na Mkoa wa Geita utaangalia namna ya kulifanyia kazi suala hilo na kuongeza kwamba, tayari Wizara imepata kibali cha kuajiri watumishi wapya hivyo upungufu wa rasilimali watu utafanyiwa kazi

Pia, Naibu Waziri ameupongeza Mkoa huo kuwa na ubunifu wa hali ya juu na kuulezea kuwa, unaibeba Sekta ya Madini. Pia, ameipongeza Kamati hiyo kutokana na namna inavyoishauri Wizara jambo ambalo linaiwezesha sekta kusonga mbele.

Naye, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Geita, Daniel Mapunda akizungumza wakati wa ziara hiyo amesema kwamba wadau wote wanapokelewa sokoni hapo ikiwemo wachimbaji wasiokuwa kwenye mfumo rasmi. Aidha, ameongeza kuwa, kwa wateja wasiojua kusoma na kuandika wanaofika katika soko la madini kwa ajili ya kupata huduma, wanasaidiwa na maafisa wa Tume ya Madini waliopo kwenye soko hilo namna zuri ya kuweka taarifa zao kwenye nyaraka mbalimbali zinazotumika kwenye ofisi hiyo.

Mbali na Kamati hiyo kutembelea soko la Madini Geita, pia imetembelea maonesho ya madini. Aidha, katika ziara hiyo, Wajumbe hao wa Kamati wamekabidhiwa Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa huo uliozinduliwa wakati wa ufunguzi wa Maonesho hayo Septemba 22, 2019, na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa.

SERIKALI YAFUTA MAPORI TENGEFU 12 NA HIFADHI SABA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa taarifa kuhusu uamuzi wa Serikali wa kuridhia misitu ya hifadhi iliyopoteza sifa itolewe kwa mwananchi kwa ajili ya shughuli za Kilimo na Mifugo ili kuwandolea kero za uhaba wa ardhi. Kauli hiyo aliitoa kwenye ukumbi wa Waziri Mkuu, jijini Dar es salaam, Septemba 23, 2019.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



……………..

*Ni utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli la Januari 2019

*Maeneo yote kutolewa kwa wananchi, vijiji 920 kubaki ndani ya hifadhi

Serikali imeridhia kufuta mapori tengefu 12 yenye ukubwa wa ekari 707,659.94 ambayo yamepoteza sifa na imeamua yagawiwe kwa wananchi kwa ajili ya shughuli za makazi, kilimo na mifugo.

Uamuzi huo umefikiwa leo (Jumatatu, Septemba 23, 2019) kweye kikao cha Baraza la Mawaziri kilichoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Dkt. John Joseph Pombe Magufuli, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Akitoa taarifa mara baada ya kikao hicho, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Mawaziri wa kisekta wakiongozwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. William Lukuvi walichambua na kuandaa taarifa ya mapendekezo ya utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi nchini iliyowasilishwa katika kikao cha Baraza la Mawaziri cha leo.

“Mawaziri walichambua na kubaini kuwa vijiji vyenye migogoro ni 975 na siyo 366 kama ilivyotangazwa awali, Baraza limeamua kwamba vijiji 920 vitabaki ndani ya hifadhi, mipaka irejewe upya, vipatiwe vyeti vya ardhi vya kijiji pamoja na kupangiwa mipango ya matumizi bora ya ardhi,” amesema na kuongeza kuwa orodha ya vijiji hivyo itatangazwa baadaye.

Waziri Mkuu amesema Serikali imeridhia Misitu ya Hifadhi saba yenye ukubwa wa ekari 46,715 iliyopoteza sifa itolewe kwa wananchi kwa ajili ya shughuli za makazi, kilimo na mifugo ili kuwaondolea kero za uhaba wa ardhi.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amesema Serikali imeridhia kumega hifadhi za misitu 14 kwa ajili ya kilimo na mifugo na kufuta mashamba 16 yasiyoendelezwa ili yapangiwe matumizi ya kilimo na mifugo.

“Vijiji 55 vilivyobaki vinaendelea kufanyiwa tathmini ya kina maeneo yaliyobaki ndani ya hifadhi na kuwasilisha mapendekezo yake kwa ajili ya uamuzi. Uchambuzi na taarifa itatolewa,” amesema na kuongeza kuwa orodha ya maeneo ya vijiji, mapori ya wanyama, misitu na mashamba yaliyofutwa itatangwa baadaye.

Pia amesema Baraza limeamua ardhi ya mita 500 zilizotengwa kama buffer zone (eneo kinga) kwenye maeneo ya vijiji vinavyopakana na hifadhi za wanyama ziachiwe vijiji husika na wananchi wasiondolewe kwenye maeneo hayo.

Ameyataja maamuzi mengine yaliyofikiwa kwenye kikao hicho kuwa ni Ofisi ya Makamu wa Rais imetakiwa ikamilishe mwongozo utakaobainisha matumizi ya ardhi ndani ya hifadhi ya mita 60 za mito, vyanzo vya maji, maziwa na bahari.

Maamuzi mengine ni kuzitaka Wizara na taasisi zote za Serikali zilinde maeneo yao kwa kuweka alama za kudumu zinazoonekana; na kwamba wananchi hawaruhusiwi kuvamia maeneo mapya na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya uvamizi wowote kuanzia leo.

Januari, mwaka huu, Rais Magufuli alitoa maagizo kwa Mawaziri nane wa sekta zinazohusika na matumizi ya ardhi wachambue na kuandaa taarifa ya mapendekezo ya kutatua migogoro ya matumizi ya ardhi nchini.

Maagizo hayo yalikuwa ni pamoja na: Kutoviondoa vijiji na vitongoji 366 vilivyomo ndani ya hifadhi; Kubainisha maeneo ya hifadhi ambayo yamepoteza sifa ili yaweze kugawiwa kwa wananchi kwa shughuli za ufugaji na kilimo na kuhakiki na kurekebisha mipaka baina ya hifadhi za misitu, wanyama na makazi.

Mengine ni kumega baadhi ya hifadhi za Taifa, mapori tengefu na misitu, kuwagawia wafugaji na wakulima; Kufanya mapitio ya sheria mbalimbali zinazohusiana na matumizi ya ardhi; Kupitia upya Sheria ya Vyanzo vya Maji inayozungumzia uhifadhi ndani ya mita 60; Kuwasilisha mapendekezo ya kufutwa mashamba yasiyoendelezwa na kugawa kwa wananchi kwa ajili ya uzalishaji wa mazao ya kilimo na mifugo na kuendelea kulinda na kuhifadhi maeneo ya hifadhi za misitu, wanyamapori na vyanzo vya maji.


WAZIRI MKUU MAJALIWA AFAFANUA UTEKELEZAJI WA MAAGIZO YA RAIS DKT. MAGUFULI KUHUSU MAPENDEKEZO YA KUPATA UFUMBUZI WA MIGOGORO YA MATUMIZI YA ARDHI NCHINI

$
0
0
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa akizungumza na Wanahabari juu ya utekelezaji wa Maagizo ya Mhe. Rais Dkt.John Pombe Magufuli kuhusu Mapendekezo ya kupata ufumbuzi wa Migogoro ya Matumizi ya Ardhi Nchini,Mkutano uliofanyika Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dar es salaam leo Septemba 23, 2019.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa akiwa na Mawaziri nane wa Sekta zinazohusika na Matumizi ya Ardhi alipokuwa akizungumza na Wanahabari (hawapo pichani) juu ya utekelezaji wa Maagizo ya Mhe. Rais Dkt.John Pombe Magufuli kuhusu Mapendekezo ya kupata ufumbuzi wa Migogoro ya Matumizi ya Ardhi Nchini, Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dar es salaam leo Septemba 23, 2019.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri nane wa Sekta zinazohusika na Matumizi ya Ardhi mara baada ya kuzungumza na Wanahabari juu ya utekelezaji wa Maagizo ya Mhe. Rais Dkt.John Pombe Magufuli kuhusu Mapendekezo ya kupata ufumbuzi wa Migogoro ya Matumizi ya Ardhi Nchini. Mkutano uliofanyika katika Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dar es salaam leo Septemba 23, 2019.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa akizungmza na Waziri wa Ardhi Mhe. William Lukuvi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya pamoja ya Mawaziri nane wa Sekta zinazohusika na Matumizi ya Ardhi iliyoundwa na Mhe. Rais Dkt.John Pombe Magufuli kuhusu Mapendekezo ya kupata ufumbuzi wa Migogoro ya Matumizi ya Ardhi Nchini. Mkutano uliofanika katika Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dar es salaam leo Septemba 23, 2019. Picha na Ikulu

Rais Dkt. Magufuli Aongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri Ikulu leo.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam leo Septemba 23, 2019. Picha na Ikulu

RAIS MAGUFULI AMJULIA HALI ASKOFU MKUU WA JIMBO KUU KATOLIKI LA DAR ES SALAAM ANAYEPATIWA MATIBABU TAASISI YA MIFUPA MUHIMBILI (MOI)

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana kwa furaha na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mhashamu Yuda Thadeus Ruwa’ichi ambaye anapatiwa matibabu katika Taasisi hiyo ya Mifupa Muhimbili (MOI) mara baada ya kufanyiwa upasuaji wa Kichwa 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza sala ya kumuombea Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mhashamu Yuda Thadeus Ruwa’ichi ambaye anapatiwa matibabu katika Taasisi hiyo ya Mifupa Muhimbili (MOI)

Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Dar es Salaam Mhashamu Yuda Thadeus Ruwa’ichi akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli ambaye alienda kumjulia hali katika Taasisi hiyo ya Mifupa Muhimbili (MOI). Wakwanza kulia ni Askofu Msaidizi Eusebius Nzigilwa wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, kushoto ni Padre Dkt. Alister Makubi Paroko wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es salaam 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Askofu Msaidizi Eusebius Nzigilwa wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam kulia, Padre Dkt. Alister Makubi kushoto, Paroko wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es salaam wakifurahia jambo pamoja na Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Dar es Salaam Mhashamu Yuda Thadeus Ruwa’ichi ambaye hali yake imezidi kuimarika mara baada ya kufanyiwa upasuaji katika taasisi hiyo ya MOI. PICHA NA IKULU.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 23 Septemba, 2019 amemjulia hali Askofu Mkuu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mhashamu Yuda Thaddaeus Ruwa’ichi anayepatiwa matibabu katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) Jijini Dar es Salaam. 

Mhe. Rais Magufuli amemkuta Baba Askofu Mkuu Ruwa’ichi akiwa anaendelea vizuri tofauti na hali ilivyokuwa alipomtembelea tarehe 10 Septemba, 2019 siku aliyoletwa MOI akitokea Hospitali ya KCMC Mkoani Kilimanjaro alikougua ghafla baada ya kupatwa na ugonjwa wa kiharusi. 

Akiwa MOI, Baba Askofu Mkuu Ruwa’ichi amefanyiwa upasuaji na timu ya Madaktari Bingwa wa ubongo na mishipa ya fahamu kwa mafanikio na sasa anaendelea vizuri. 

Mhe. Rais Magufuli ameeleza kufurahishwa kwake na kuimarika kwa hali ya Baba Askofu Mkuu Ruwa’ichi na amewapongeza Madaktari Bingwa wa MOI kwa kumtibu kwa mafanikio makubwa. 

Aidha, Mhe. Rais Magufuli, Baba Askofu Mkuu Ruwa’ichi, Baba Askofu Mkuu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Mhashamu Eusebius Nzigilwa na Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro Padre Dkt. Alister Makubi wamesali sala ya pamoja ya kumshukuru Mungu kwa uponyaji na kuwaombea wagonjwa wote wapone haraka. 

Baada ya kutoka MOI, Mhe. Rais Magufuli amewajulia hali wagonjwa waliolazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) akiwemo Baba Mzazi wa Daktari wa Rais, Mzee Wilson Ngwale aliyelazwa hospitalini hapo. 

Kabla ya kutembelea wagonjwa, Mhe. Rais Magufuli amekwenda Msasani Jijini Dar es Salaam kumpa pole Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (JWTZ) Jen. Venance Salvatory Mabeyo ambaye amefiwa na mwanae Nelson Venance Mabeyo (aliyekuwa Rubani) ambaye amefariki dunia leo asubuhi baada ya ndege aliyokuwa akiiendesha kupata ajali muda mfupi baada ya kuruka kutoka uwanja mdogo wa ndege wa Seronera Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara. 

Mapema leo asubuhi, Mhe. Rais Magufuli ameongoza kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam. 


Gerson Msigwa 
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU 
Dar es Salaam 
23 Septemba, 2019

AWESO AWATUMBUA MENEJA WAKALA WA MAJI VIJIJINI PANGANI,MENEJA WA MAMLAKA YA MAJI SAFI PANGANI

$
0
0
 NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso akikagua mradi wa Maji Kijiji cha Msaraza Kata ya Bushiri wilayani Pangani wakati wa ziara yake
Sehemu ya watumishi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) wakiwa kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya ya Pangani wakifuatilia kwa umakini taarifa ya wilaya ya Pangani kuhusu maji aliyokuwa akisomewa Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso
 NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM)  akizungumza na watumishi wa wilaya ya Pangani wakati wa ziara yake wilayani humo
 NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) kushoto akimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah wakati wa ziara yake wilayani humo
 KATIBU Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange akizungumza wakati wa ziara hiyo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Pamngani Zainabu Abdallah kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Pangani Rajabu Abdallah
 Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Pangani Rajabu Abdallah  akizungumza wakati wa ziara hiyo kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange
 MWENYEKITI wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani Seif Saidi akizungumza wakati wa ziara hiyo kushoto ni Afisa Tawala wa wilaya ya Pangani Gibson George
 AFISA Tawala wa wilaya ya Pangani Gibson George akizungumza wakati wa ziara hiyo
 NAIBU Waziri wa Maji Jumaa Aweso kushoto akilakiwa na Katibu Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange wakati alipowasili


Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso amemsimamizi kazi Meneja wa Wakala wa Maji Vijiji Pangani ( DM) RUWASA PANGANI Ladislaus Modestus huku akiagiza Mkurugenzi wa Usambazaji wa Maji na Usafi wa Mazingira (Ruwasa) Makao Makuu Mkama Bwire kuondoka naye kutokana na kushindwa kusimamia miradi ya maji huku mingine akiwa haitambui.

Pia ameagiza Meneja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira wilaya ya Pangani Adam Sadick kusimamishwa kazi kutokana na kushindwa kusimamia miradi na bili za maji na kupelekea mamlaka kupata hasara. 

Agizo la Naibu Waziri Aweso linatokana na mhandisi huyo kushindwa kusimamia miradi ya maji wilayani humo na hivyo kupelekea wananchi kukosa maji hali ambayo ilimchukiza Naibu Waziri huyo ambaye alikuwa kwenye ziara wilayani humo.

Alisema kwamba mkurugenzi huyo anapoondoka aondoke na mhandisi huyo ambayo ameshindwa kuendana na kasi ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji ambayo ni muhimu kwa ustawi wa maisha yao .

Aidha alisema kwamba hatua hiyo inatokana na kwamba mhandisi huyo kupewa fedha za kusimamia mradi milioni 26 lakini bado hafiki kwenye maeneo yanayotekelezwa miradi

“Ndugu yangu wewe ni mhandisi wa maji upo hivi kama ungekwa daktari si ungekuta umekwisha kuua watu hatuwezi kukubali kuona hali kama hii na hatupo tayari kuona watu wa namna hii”Alisema

“Kutokana na kwamba Mhandisi huyo anapata fedha za kusimamia miradi ya maji kwenye wilaya hii na anashindwa kufanya hivyo hata ukiangalia msafara wangu ameupoteza wewe hautufai ni bora ukaondoka naye “Alisema Naibu Waziri Aweso. 

Hata hivyo Naibu Waziri huyo aliagiza kuundwe tume itakayobaini nini changamoto iliyopo kwenye usimamizi wa miradi ya maji Pangani jambo ambalo limepeleka kushindwa kufanyika kwa ufanisi mkubwa kama ilivyo maeneo mengine.

“Pia eneo la kibinda linachangamoto kubwa ya maji mimi kama mbunge wakati sijawa Naibu Waziri nilimfuata Waziri Kamwele nikamuambia suala hilo…niambieni kwamba mradi wa kibinda mabomba yanafika lini? Alihoji Naibu Waziri huyo.

Awali akizungumza wakati akitoa taarifa ya wilaya ya Pangani Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu Abdallah alimueleza Naibu Waziri Aweso kwamba wananchi mji wa Pangani wana changamoto ya maji zaidi ya wiki tatu na hivyo kupelekea wananchi kukosa maji.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kutokana na kwamba alikuwa likizo aliporudi alikwenda kwenye eneo la mradi kwa ajili kukagua maji na juzi ameenda kwenye mradi huo na amegundua changamoto tatu awali ni mfumo wa umeme kwa maelekezo wa meneja wa Pasawa.

Alisema tatizo hilo la mfumo wa umeme limesababishwa na tatizo kubwa la umeme kuingia na mfumo kuharibika huku akieleza kwamva changamoto nyengine ni pampuni kuwa na uwezo mdogo kuliko inavyopaswa kutumika kwenye maji.

“Wataalamu wanasema pampu ina uwezo mdogo mimi nashangaa wakati ikinunuliwa …mashine ya kuvuta umeme na kuzima mashine zipo mbili na moja ni mbovu na pampu zaidi ya milioni 22 ni mbovu anasema maelezo ya mkandarasi mfumo wa umeme mbovu”Alisema Mkuu huyo wa wilaya ya Pangani.

Mwisho

Serikali yavitaka Vyuo Vikuu kufanya tafiti za Afya nchini

$
0
0
Charles James, Michuzi TV

SERIKAL imesema kuna haja ya kuwa na tafiti nyingi za afya ambazo zitasaidia kujua sekta hiyo inakabiliwa na changamoto zip ili ziweze kutatuliwa kwa haraka na ufanisii.

Akizungumza leo jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Huduma za Afya na Ustawi wa Jamii TAMISEMI, Dk Ntuli Kapologwe amesema ni vema kama Serikali wafanye tafiti ili kurahisisha utendaji kazi katika mfumo wa Afya nchini.

Dk Kapologwe ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa tathimini ya miradi ya afya ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Mzumbe.

“Wakati tukielekea katika uchumi wa kati ifikapo 2025 ni lazima tuhakikishe sekta ya afya inakuwa vizuri,na tunajua mfumo wa afya umekaa kama ‘Pyramid’ tunataka huduma bora zianzie kuanzia anapoingia katika hospital apate huduma nzuri,”amesema.

Kapologwe amesema kuna umuhimu wa kupata tafiti nyingi ambazo zitaisaidia sekta ya afya kujua kuna tatizo gani na kuweza kuyatatua kwa wakati hivyo kumsaidia mwananchi wa chini ambaye siku zote ndio kimbilio.

Aidha,amesema kuna haja ya tafiti hizo ziunganishe sera na utekelezaji huku akitaka zishiishie tu kwenye machapisho bali zifike kwa wahusika na kutekelezwa.

“Tafiti zisiishie tu kwenye machapisho,sisi kama wizara tunataka tafiti nyingi ambazo zitatusaidia katika utendaji kazi wetu,. Mfano sasa hivi tumejenga majengo mengi tunataka tafiti Je,huduma kwa sasa zipoje,? Je huduma ni bora? Amesema Dk Kapologwe.

Dk Kapologwe amesema kuwa kipimo cha utendaji kazi kwa sasa kipo kwa mwananchi kwa kuhakikisha anapata mahitaji yake yote ambayo ni muhimu.Aidha amevitaka vyuo vikuu nchini kushirikiana na Ofisi za Mkuu wa Mkoa na Wilaya ili kuweza kushughulikia changamoto na kuzitambua ndani ya kipindi cha muda mfupi.

Nae Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Prof Ganka Nyamsongoro amesema kuwa watanzania wanapaswa kujijengea utamaduni wa kutumia takwimu ili kupata tija katika kazi zao.
Mkurugenzi wa Afya na Ustawi wa Jamii TAMISEMI, DK Ntuli Kapologwe akizungumza katika uzinduzi wa mkutano wa tathimini ya miradi uliondaliwa na Chuo Kikuu cha Mzumbe Jijini Dodoma leo.

DAWASA YAWAVALIA NJUGA WAHUJUMU MIUNDOMBINU YA MAJI KAWE

$
0
0

MAMLAKA ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) leo Septemba 23 imekagua miundombinu ya maji katika Mikoa ya kihuduma ya mtaa wa Muzimuni kata ya Kawe  na katika ukaguzi wao wameshuhudia wananchi wakitumia maji kwa njia udanganyifu na kusababisha hasara kwa wateja halali waliounganishwa na wanaolipa bili.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua miundombinu ya maji katika mtaa wa Muzimuni kata ya Kawe Meneja Mapato wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Edger Zawayo amesema kuwa zoezi hilo ni endelevu hivyo ni vyema wanaohujumu miundombinu hiyo wakaacha mara moja kabla ya sheria kali za kisheria dhidi yao hazijachukuliwa.

Zawayo amesema kuwa mmoja wa watuhumiwa wa kuhujumu miundombinu ya maji amekamatwa na atafikishwa mahakani na sheria itafuatwa ili liwe fundisho kwa wengine.

Amesema kuwa wananchi wazitumie ofisi za mamlaka hiyo kwa kupata huduma ya maji na sio kuhujumu huduma hiyo kwa wateja ambao wameshalipia huduma zao.

"Tutaendelea kuwashughurikia wale wote ambao wanahujumu miundo mbinu ya maji na hatutawafumbia macho maana wanasababisha hasara kubwa kwenye mamlaka hiyo" Alisema Zawayo

Amesema kuwa kila mwananchi awe mlinzi wa mwenzake kwa kutoa taarifa kwenye ofisi za Serikali za mitaa na ofisi za DAWASA zilizokaribu ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Amesema kuwa adhabu kwa wahujumu wa miundombinu hiyo ya maji ipo palepale, yaani faini  kuanzia shilingi milioni tano hadi hamsini, na amewashauri wananchi kuwa waaminifu ili kutokutwa na kadhia hiyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa wa Muzimuni Hassan Ngonyani  amewaasa wananchi wa mtaa huo juu wa wizi wa maji wanaoufanya  badala yake wafuate taratibu maalumu na kupata huduma hiyo ya maji kwa uhalali.

Amesema kuwa wananchi wote wanaohitaji huduma ya maji watumie ofisi zilizopo kila mahali na ni vyema wakafuata taratibu na kulipa bili na sio kuhujumu maji kwa wateja halali na kuwasababishia hasara.
  Mtaalamu wa Mambo ya Mita kutoka Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Da es Salaam (DAWASA) Mohammed Mwakimila(kushoto) akionesha bomba la maji lililokuwa limeunganishwa kwenye bomba la mteja kinyemela na kuelekezwa kwenye Duka la Dawa lililopo katika mtaa wa Muzimuni kata ya Kawe leo wakati ukaguzi wa miundombinu ya maji ya Mamlaka hiyo. Katikati ni Mwenyekiti wa mtaa wa Muzimuni kata ya Kawe, Hassan Ngonyani na  Mtaalamu wa Mambo ya Mita kutoka Idara ya Biashara ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Da es Salaam DAWASA Martin Kulembe(kulia) wakishuhudia tukio hilo.
 Mtaalamu wa Mambo ya Mita kutoka Idara ya Biashara ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Da es Salaam DAWASA Martin Kulembe(katikati) akionesha wizi uliokuwa unafanywa kwa mteja anayetuhumiwa kujiunganishia maji pamoja na Mwenyekiti wa mtaa wa Muzimuni kata ya Kawe, Hassan Ngonyani(kulia) wakati wa ukaguzi wa miundombinu ya maji katika mtaa huo.
 Mwenyekiti wa mtaa wa Muzimuni kata ya Kawe, Hassan Ngonyani akizungumza na wafanyakazi wa DAWASA pamoja na baadhi ya wateja wa Mamlaka hiyo mara baada ya kujionea wizi uliokuwa unafanyika kwa kuhujumu miundombinu ya Mamlaka hiyo wakati wa ukaguzi wa miundombinu ya maji katika mtaa wa Muzimuni kata ya Kaweleo jijini Dar es Salaam.
 Sehemu ya maungio ya maji ya wizi yalipokuwa yakichukuliwa kutoka kwenye bomba la mmoja wa wateja wa DAWASA likitoka maji mara baada ya kulikata bomba hilo wakati wa ukaguzi wa miundombinu ya maji katika mtaa wa Muzimuni kata ya Kaweleo jijini Dar es Salaam.
 Moja ya mita ya maji ikiwa ndani ya nyumba kinyume na utaratibu wa mita kukaa nje ya nyumba ili kuondoa udanganyifu na wizi wa maji.
Mita ya maji ya DAWASA ikiwa imeunganishwa mambomba mengi na bila kutumia utaratibu uliowekwa na mamlaka hiyo haya yote yalibainika mara baada ya maofisa wa DAWASA kufanya ukaguzi katika mtaa wa Muzimuni kata ya Kawe.

RAIS DKT. MAGUFULI AMPA POLE MKUU WA MAJESHI YA ULINZI YA WANANCHI WA TANZANIA JENERALI VENANCE MABEYO AMBAYE AMEFIWA NA MTOTO WAKE NELSON MABEYO

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha Ndugu Nelson Mabeyo mtoto wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo nyumbani kwao Msasani jijini Dar es Salaam. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole Mke wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo, Mama Mabeyo ambaye amefiwa na mtoto wake Nelson Mabeyo aliyepata ajali ya ndege Seronera Serengeti mkoani Mara.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole Mke wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo, Mama Mabeyo ambaye amefiwa na mtoto wake Nelson Mabeyo aliyepata ajali ya ndege Seronera Serengeti mkoani Mara. 
 . Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo msibani Msasani jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza sala pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo na familia yake wakimuombea marehemu   Nelson Mabeyo ambaye alifariki kwa ajali ya ndege Seronera Serengeti mkoani Mara.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Jenerali Venance Mabeyo msibani Msasani jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU





Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Geita wazinduliwa

$
0
0
Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Geita umezinduliwa jana tarehe 22 Septemba 2019 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa wakati wa Maonyesho ya Teknolojia ya Dhahabu kwenye Uwanja wa Kalangalala Mjini Geita. Zaidi ya watu 1000 walishiriki uzinduzi huo, ikijumuisha viongozi mbalimbali wakiwamo Mawaziri, Wabunge, Wakuu wa Mikoa na Madau wa Madini.

Katika uzinduzi huo Waziri Mkuu alibainisha jitihada mbalimbali ambazo Serikali imefanya kuhakikisha Madini yananufaisha Nchi na Watu wake.

Waziri Mkuu Majaliwa amewaonya watoroshaji Madini na kusema Serikali ipo makini na imejidhatiti vya kutosha na kwamba haitokuwa na huruma nao. Aidha alisema kwa wale wasiotaka kuelewa na kuacha kutorosha madini Serikali itashughulika nao.

Kwa upande wake, Waziri wa Madini Doto Biteko amesema kwa sasa Serikali na Makampuni yanayomiliki migodi wanaheshimiana kwani Makampuni hayo yanatii magizo na kufuata sheria za nchi.

Waziri Doto amesema kabla ya kufunguliwa kwa masoko ya madini nchini makusanyo ya dhahabu yalikuwa kilo 101 kwa mwezi lakini baada ya masoko kufunguliwa makusanyo yameongezeka na kufikia kilo 1,974 hivi sasa.

Akizungumza mbele ya Waziri Mkuu, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Mbaga Kida, alisema ESRF chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na kwa kushirikiana na Serikali imekuwa ikiandaa Miongozo ya Uwekezaji katika Mikoa kwa lengo la kuchambua na kuainisha fursa za uwekezaji zilizopo katika mikoa husika ili kuwavutia wawekezaji.

Dkt. Kida alisema mpaka sasa ESRF imesaidia Mikoa 17 kuandaa Miongozo ya Uwekezaji ambapo mikoa 11 imekamilisha na Mikoa 6 iko katika hatua mbalimbali na kuongeza kuwa ESRF itaendelea kuandaa Miongozo ya Uwekezaji katika mikoa iliyobaki kuanzia mwezi wa kumi mwaka.

Alisema kazi hii ya Uandaaji wa Miongozo ya Uwekezaji imeweza kuibua fursa nyingi kwenye Mikoa husika zikiwa katika sekta na ngazi zote.

"Kwa mfano mheshimiwa Waziri hapa Geita kuna fursa kubwa katika sekta ya madini hasa uchimbaji na uongezaji thamani wa madini ya dhahabu kwa wawekezaji wadogo, wa kati na wakubwa. Fursa nyingine zipo katika sekta ya viwanda, kilimo, ufugaji, uvuvi, ujenzi, utalii, na huduma. Maelezo ya kina juu ya fursa hizo yapo kwenye Mwongozo wa Uwekezaji ambao utauzindua leo hii”alisema Dkt. Kida.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa ESRF Miongozo hii ya Uwekezaji ngazi ya Mikoa itachangia katika Mwongozo wa Uwekezaji wa Taifa na kwamba ESRF itaendelea kushirikiana na mikoa katika utekelezaji wa miongozo hii kwa kusaidia kufanya upembuzi yakinifu (feasibilty studies), kuandaa Miongozo ya Biashara (Business Plans) kwa baadhi ya fursa ambazo mikoa itapenda kuwekeza, na kunadi fursa zilizopo kwenye Miongozo.

Aidha Kida alishukuru wataalamu wa ESRF walioshiriki kuandaa mwongozo huo na kuufanikisha. Aliwataja kwa majina waliofanikisha kuwa ni pamoja na Margareth Nzuki, Dk Oswald Mashindano, Prof. Godwin Mjema; Doris Lyimo na Mussa Mayala Martine.

Mkurugenzi wa ESRF aliwapongeza pia viongozi wa Mkoa wa Geita kwa jitihada zao za kuuweka wazi mkoa huo na kuwataka wadau wote kuhakikisha Mwongozo huo unatumika ipasavyo ili kuleta matokeo yaliyo kusudiwa katika mkoa wa Geita na Taifa kwa ujumla.
 Mkurugenzi wa Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk.Tausi Kida akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri mara baada ya kuwasili kwenye uwanja Kahangalala mjini Geita kwa ajili ya kushiriki kwenye ufunguzi wa Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu yaliofanyika sambamba na uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji wa mkoa wa Geita ulioandaliwa na ESRF kwa ufadhili wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Geita Mjini, Joseph Kasheku (kulia) maarufu kama Musukuma mara baada ya kuwasili kwenye uwanja Kahangalala mjini Geita kwa ajili ya kushiriki kwenye ufunguzi wa Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu yaliofanyika sambamba na uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji wa mkoa wa Geita ulioandaliwa na ESRF kwa ufadhili wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP). Katikati ni Mkurugenzi wa Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk.Tausi Kida
 Mkurugenzi wa Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk.Tausi Kida na Prof. Godwin Mjema ambaye ni mmoja wa watu waliofanikisha kuandaa mwongozo wa uwekezaji wa mkoa wa Geita wakielekea kwenye eneo maalum lililotengwa mara baada ya kuwasili kwenye uwanja Kahangalala mjini Geita kwa ajili ya kushiriki kwenye ufunguzi wa Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu yaliofanyika sambamba na uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji wa mkoa wa Geita ulioandaliwa na ESRF kwa ufadhili wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
 Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi, Robert Gabriel akitoa salamu na kuwakaribisha wageni wakati sherehe za ufunguzi wa Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu yaliyofanyika katika uwanja wa Kahangalala mjini Geita.
  
Mkurugenzi wa Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk.Tausi Kida akitoa taarifa kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ya mwongozo wa uwekezaji wa mkoa wa Geita iliyoandaliwa na taasisi yake kwa ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa na Maendeleo (UNDP) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu uliofanyika sambamba na uzinduzi wa mwongozo huo kwenye uwanja wa Kahangalala mjini Geita.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua Mwongozo unaoonyesha fursa za uwekezaji katika mkoa wa Geita wakati alipofungua Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu kwenye uwanja wa Kahangalala mjini Geita. Wengine pichani kutoka kushoto ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, Waziri wa Madini, Doto Biteko, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi, Robert Gabriel na kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Geita, Alhaj Said Kalidushi.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha Mwongozo unaoonyesha fursa za uwekezaji katika mkoa wa Geita mara baada ya kuuzindua wakati alipofungua Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu kwenye uwanja wa Kahangalala mjini Geita. Wengine pichani kutoka kushoto ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, Waziri wa Madini, Doto Biteko, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi, Robert Gabriel na kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Geita, Alhaj Said Kalidushi.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Waziri wa Madini, Mh. Doto Biteko (wa pili kushoto) Mwongozo unaoonyesha fursa za uwekezaji katika mkoa wa Geita mara baada ya kuuzindua wakati alipofungua Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu kwenye uwanja wa Kahangalala mjini Geita.Wanaoshuhudia tukio hilo ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi, Robert Gabriel (wa pili kulia) na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Geita, Alhaj Said Kalidushi (kulia).
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi, Robert Gabriel (wa pili kulia) Mwongozo unaoonyesha fursa za uwekezaji katika mkoa wa Geita mara baada ya kuuzindua wakati alipofungua Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu kwenye uwanja wa Kahangalala mjini Geita.
 Msanii wa muziki wa Injili nchini Emmanuel Mbasha akitoa burudani wakati wa hafla ya uzinduzi wa Maonyesho ya Pili ya Tekinolojia ya Dhahabu na Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa wa Geita uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kahangalala mjini Geita.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na meza kuu katika picha ya pamoja na wadau wa ESRF na UNDP mara baada ya kuzindua Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu yaliyoenda sambamba na uzinduzi wa Mwongozo unaoonyesha fursa za uwekezaji katika mkoa wa Geita katika hafla iliyofanyika kwenye uwanja wa Kahangalala mjini Geita.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na meza kuu katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa GGM mara baada ya kuzindua Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu yaliyoenda sambamba na uzinduzi wa Mwongozo unaoonyesha fursa za uwekezaji mkoa wa Geita katika hafla iliyofanyika kwenye uwanja wa Kahangalala mjini Geita.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na meza kuu katika picha ya pamoja na kamati ya maandalizi mara baada ya kuzindua Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu yaliyoenda sambamba na uzinduzi wa Mwongozo unaoonyesha fursa za uwekezaji katika mkoa wa Geita hafla iliyofanyika kwenye uwanja wa Kahangalala mjini Geita.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na meza kuu katika picha ya pamoja na viongozi wa CCM wa mkoa wa Geita mara baada ya kuzindua Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu yaliyoenda sambamba na uzinduzi wa Mwongozo unaoonyesha fursa za uwekezaji katika mkoa huo hafla iliyofanyika kwenye uwanja wa Kahangalala mjini Geita.
 Mkurugenzi wa Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk.Tausi Kida na Mkuu wa Idara ya maarifa na Ubunifu wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Margareth Nzuki (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na mdau wa Geita wakati sherehe za ufunguzi wa Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu yaliyofanyika katika uwanja wa Kahangalala mjini Geita.
 Mkurugenzi wa Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk.Tausi Kida katika picha ya kumbukumbu na Mkuu wa mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri wakati sherehe za ufunguzi wa Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu yaliyofanyika katika uwanja wa Kahangalala mjini Geita.
 Kutoka kushoto ni Meneja wa Data wa ESRF, John Kajiba, Mkurugenzi wa Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk.Tausi Kida, Mkuu wa mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri pamoja na wabunge wa viti maalum wa mkoa wa Geita wakiwa kwenye picha ya pamoja.

WAFANYAKAZI BENKI YA NMB WAFANYA USAFI HOSPITALINI AMANA

$
0
0
WAFANYAKAZI wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam jana walijitolea kufanya usafi katika Hospitali ya Amana ya jijini Dar es Salaam pamoja na kukabidhi vifaa mbalimbali vya kufanyia usafi, ikiwa ni kuadhimisha siku ya usafi duniani zilizofanyika Septemba 21, 2019.

Akizungumza na wanahabari mara baada ya zoezi hilo katika Hospitali ya Amana, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Bw. Badru Idd alisema zoezi hilo ni utaratibu wa kawaida ambao NMB imejiwekea kuona ni jinsi gani inarudisha sehemu kidogo ya mapato yake katika jamii.

Alisema mbali na zoezi la kufanya usafi hospitalini hapo, wafanyakazi hao walikabidhi vifaa tofauti vya kufanyia usafi vikiwemo vifaa vya kuzolea na kuhifadhia taka, mifagio, vifaa vya kudekia, seti za vifaa vya kujikinga wakati wa kufanya usafi, buti za kufanyia usafi, makoleo maalum ya taka na dawa za usafi.

"...Leo tumekuja Hospitali ya Amana kwa ajili ya kujitolea kufanya usafi kuitikia maadhimisho ya usafi duniani, tumejipanga kufanya usafi maeneo mbalimbali ya nchi kwa kuwa tuna mtandao mpana vivyo hivyo wenzetu maeneo mbalimbali wanafanya usafi kama sisi. Na sisi kama kanda ya Dar es Salaam tumeamua kuja kufanya usafi Hospitali ya Amana."

Akifafanua zaidi alisema NMB pia imekuwa ikitumia fungu hilo katika kusaidia jamii kwenye elimu, afya pamoja na majanga pale yanapojitokeza kwa jamii yetu. "Hii yote ni kuleta ukaribu wa Benki yetu na jamii...hatuji tu kuomba biashara kwa jamii bali tunajitokeza kushiriki, na kusaidiana na jamii katika kufanya shughuli zao. Vifaa vyote tulivyokabidhi leo ni fedha zilizochangwa na wafanyakazi wetu kwa hiyari kujitolea kusaidia jamii," alisema Bw. Idd.

Aidha aliongeza kuwa NMB wakati wote imekuwa ikishirikiana na jamii katika shughuli mbalimbali, ikiwemo kutenga asilimia moja ya pato lake baada ya kuondoa gharama zote, na kwa mwaka huu imetenga zaidi ya bilioni moja kwa aajili ya shughuli za kijamii, huku hadi kufikia mwezi Julai, 2019 NMB imekwishatumia zaidi ya milioni 450 kwa shughuli kama hizo.

Ofisa Muuguzi Kiongozi wa Hospitali ya Amana, Vicent Semkamba (kulia) akipokea sehemu ya vifaa vya kufanyia usafi kutoka kwa mmoja wa maofisa wa Benki ya NMB jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni msaada uliotolewa na wafanyakazi wa benki hiyo walipojitolea kufanya usafi katika hospitali hiyo.
Mmoja wa maofisa wa Benki ya NMB jijini Dar es Salaam akifyeka majani kwa kutumia mashine maalum Hospitali ya Amana walipojitolea kufanya usafi katika hospitali hiyo.
Sehemu ya wafanyakazi wa Benki ya NMB jijini Dar es Salaam wakifanya usafi maeneo mbalimbali ya Hospitali ya Amana leo ikiwa ni kujitoa kushiriki matendo ya kusaidia jamii.
Sehemu ya wafanyakazi wa Benki ya NMB jijini Dar es Salaam wakifanya usafi maeneo mbalimbali ya Hospitali ya Amana leo ikiwa ni kujitoa kushiriki matendo ya kusaidia jamii.
Ofisa Afya Hospitali ya Amana, Avit Maro (kulia) akiwashukuru wafanyakazi wa Benki ya NMB mara baada ya zoezi la kufanya usafi katika hospitali hiyo. Katikati ni Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Bw. Badru Idd.

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Bw. Badru Idd (kushoto) akitoa maelekezo kwa wafanyakazi wa benki hiyo kabla ya kuanza kufanya usafi katika Hospitali ya Amana walipojitolea. Mbali na kujitolea kufanya usafi wafanyakazi hao pia walikabidhi vifaa mbalimbali vya kufanyia usafi hospitalini hapo.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Bw. Badru Idd (kulia) akimkabidhi sehemu ya vifaa vya kufanyia usafi Ofisa Muuguzi Kiongozi wa Hospitali ya Amana, Vicent Semkamba (kushoto) ikiwa ni msaada uliotolewa na wafanyakazi wa benki hiyo walipojitolea kufanya usafi katika hospitali hiyo. Mbali na kujitolea kufanya usafi wafanyakazi hao pia walikabidhi vifaa mbalimbali vya kufanyia usafi hospitalini hapo.

VIONGOZI WA SIMBA 'NGOMA' BADO NGUMU

$
0
0
DHAMANA ya aliyekuwa rais wa klabu ya Simba Evans Aveva na makamu wake, Godfrey Nyange maarufu kama Kaburu, imebakia kwenye sintofahamu kufuatia mabishano makali ya kisheria baina ya upande wa serikali na ule wa utetezi, na kusababisha washitakiwa hao kurudi rumande hadi Septemba 27, mwaka huu.

Hatua hiyo imekuja baada ya upande wa mashtaka kudai kuwa kusudio la kukata rufaa walilopeleka Mahakama Kuu linaifanya mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kutoendelea na hatua yoyote ikiwemo washtakiwa hao kupatiwa dhamana hadi itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.

Akiwasilisha hoja za upande wa mashtaka, wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa wamepeleka kusudio la kukata rufaa dhidi ya uamuzi uliowaona washitakiwa hao hawana kesi ya kujibu katika mashitaka ya utakatishaji fedha, chini ya kifungu 379 (1) (a) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.

Amedai kutokana na kusudio hilo, wanaomba mahakama kusimama kufanya yale yote yaliyotakiwa kufanyika ikiwemo ,washitakiwa kupewa dhamana hadi rufaa hiyo itakaposikilizwa na kutolewa maamuzi katika mahakama Kuu.

Amedai, walikuwa na ushahidi wa kutosha katika mashitaka ya utakatishaji fedha na kwamba suala la kuweka masharti ya dhamana limetokana na kuwaondolea mashtaka ya utakatishaji fedha ya kwamba washitakiwa hawana kesi ya kujibu kwenye mashtaka hayo.

"Pale ambapo kuna kusudio kinachofanyika ni kuacha kuendelea kusikiliza kesi hii hadi maamuzi yatakapotolewa," amedai Wankyo na kuongeza kuwa wana haki ya kukatia rufaa maamuzi yaliyotolewa kwa sababu hayo ni maamuzi ya mwisho na hivyo, suala la dhamana libaki kama lilivyo.

Akijibu hoja hizo, Wakili wa Utetezi, Nehemiah Nkoko ameiomba mahakama itupilie mbali maombi ya upande wa mashitaka kwa sababu lengo lao ni kuona washitakiwa hawapati dhamana katika kesi hiyo.

Amedai, mahakama imesikiliza mashtaka yote katika kesi hiyo na kufikia uamuzi wa kuwa washitakiwa wana kesi ya kujibu katika mashitaka mengine isipokuwa ya utakatishaji fedha.

"Mahakama hii inamamlaka ya kutoa dhamana kwa sababu tayari ilishataja masharti na kilichobaki ni kuangalia kama wadhamini wametimiza masharti hayo au la," amedai Nkoko.

Ameendelea kudai kuwa, wakati mahakama hiyo ilipowaona hawana kesi ya kujibu katika mashitaka hayo mawili, upande wa mashitaka waliulizwa kama walikuwa na pingamizi wakajibu kuwa hawana pingamizi la washitakiwa kupata dhamana.

Alidai mahakama haiwezi kusimamisha utoaji wa dhamana kwa sababu tayari ilishatoa masharti.Baada ya mabishano makali ya kisheria, Hakimu Simba amesema atatoa uamuzi Septemba 27,2029 washtakiwa yao wamerudishwa rumande

Septemba 19, mwaka huu baada ya mahakama kuwakuta washtakiwa hawana kesi ya kujibu katika mashtaka ya utakatishaji, Wakili wa Takukuru Leornad Swai aliulizwa kama anapingamizi lolote juu ya dhamana alidai hawana pingamizi na Hakimu Simba aliwapatia masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya Sh milioni 30 kwa kila mmoja pamoja na kuwa na vitambulisho.

Mbali na Aveva na Kaburu, mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa klabu hiyo, Zacharia Hanspope ambaye yeye yuko nje kwa dhamana.

Katika keai hiyo, shtaka la kwanza, Aveva na Kaburu wanadaiwa kula njama ya kutenda kosa la matumizi mabaya ya madaraka ambapo wanadaiwa kutumia vibaya madaraka yao kwa kuandaa fomu ya kuhamisha fedha Dola za Marekani 300,000 kutoka kwenye akaunti ya Simba iliyoko benki ya CRDB Azikiwe kwenda kwenye akaunti binafsi ya Aveva iliyoko benki ya Barclays.

Pia wanadaiwa kwa pamoja walighushi nyaraka iliyokuwa ikionesha Simba inalipa mkopo wa USD 300,000 kwa Aveva kitu ambacho sio kweli.Aveva anadaiwa katika benki ya CRDB alitoa nyaraka ya uongo ikionesha Simba wanalipa mkopo wa USD 300,000

Aveva anadaiwa kuwa katika Benki ya Baclays Mikocheni alijipatia USD 187,817 wakati akijua zimetokana na kughushi.Kaburu anadaiwa kumsaidia Aveva kujipatia fedha hizo kutoka kwenye akaunti ya Simba wakiwa wanajua fedha hizo zimetokana na zao la kughushi. 

Aveva, Kaburu na Hans Poppe wanadaiwa kughushi hati ya malipo ya kibiashara wakionesha kwamba nyasi bandia zilizonunuliwa na Simba zina thamani ya USD 40,577 huku wakijua kwamba siyo kweli

Katika mashitaka ya nane, Aveva anadaiwa kuwasilisha hati ya malipo ya kibiashara ya uongo kwa Levison Kasulwa kwa madhumuni ya kuonesha kwamba Simba wamenunua nyasi bandia zenye thamani ya USD 40,577

Aveva, Kaburu na Hanspope wanadaiwa kuwasilisha nyaraka za uongo kuonesha kuwa Simba imenunua nyasi hizo za bandia.

Taasisi inayofadhili uwezeshaji kwa wanawake yapongezwa

$
0
0
TAASISI ya kitazania ya Foundation for Civil Society imepongezwa kwa kuwa mstari wa mbelea katika kusaidia kutatua changamoto zinazoikabili jamii ya Kitanzania.

Pongezi hizo zilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Afisa Mtendaji wa Kata ya Kigamboni, Nobert Kamugisha baada ya Taasisi hiyo kufadhili mafunzo ya kuwajengea uwezo wanawake wilayani humo yanayoratibiwa na Taasisi isiyokuwa ya Kiserikali ya Tanzania Association of Women Certified Accountant(TAWCA).

Kamugisha alisema kuwa ni jambo la kujivunia kuona kuwa kumeanza kuwa na mwamko kwa watanzania kujisimamia wenyewe katika kuendesha mambo yetu badala ya kusubili kila kitu kutoka kwa wahisani.

“Hili ni jambo la kuungwa mkono kuoana kwamba kuna Taasisi ya kizalendo ambayo imeweza kuchukua hatua ya kufadhili ukabilianaji wa changamoto za watanzania baladala ya kungoja kila wakati watu kutoka nje.

“Kwani hatujui kuwa watu hao wanapokuwa wanawahoji wanajamii wetu wanakuwa na lengo gani jingine mbali na hilo, hivyo ni sisi kama serikali ya kigamboni tushirikiana na taasisi hii yenye lengo ya kuwakomboa wanawakem kifikra kupitia kampeni yake ya bado naweza,” alisema Kamugisha.

Katika hatua nyingine Kamugisha alizitaja changamoto zinazoikabili kata ya kigamboni na wilaya kwa ujumla kuwa ni uongezeko la vitendio vya ukatili, mimba za utotoni na ukosefu wa elimu ya kujisimamia kwa kina mama.

“Kupitia kampeni hii ya bado naweza inayolenga kuwainua wanawake wakiwamo wale waliopoteza matumaini tunaimani kuwa tunaweza kurejesha mwanga mwingine kwa jamii yetu,” alisema.

Upande wake, Tumaini Lawrence ambaye ni Mkurungezi Mtendaji wa TAWCA alisema wameamua kupelekea mradi huo wenye kauli mbiu ya bado naweza Wilayani humo kutokana na kuwa na uhitaji mkubwa wa elimu kwa wanawake ambao wamekuwa wakikata tamaa ya kutimiza malengo yao kutokana na sababu mbalimbali.

“Tumeamua kuleta mradi huu Kigamboni kutokana na kubaini kuwa kuna uhitaji mkubwa wa elimu, kwani wasichana wengi wameshindwa kutimiza ndoto zao baada tu ya kupata ujauzito, lakini pia akina mama wamekata tamaa baada ya kufanyiwa unyanyasaji kwani wengi wao wanesema kuwa waume zao wamekuwa wakiwageuza kuwa vitega uchumi.

“Pia tunahitaji kutoa elimu kwa wazazi ili kuwalinda watoto na ndoa za utotoni ambazo pia zimekuwa zikiongezeka wilayani humu, kwani tunaamini kuwa wazazi wakiwezeshwa kupata elimu basi itakuwa rahisi hata kwa familia kujikwamua na changamoto zinazoweza kuepukika,” alisema Tumaini.

Mradi huo unafadhiliwa na shirika la Kitanzania la Foundaton for Civil Society.
 Mkurugenzi mtendaji wa TAWCA,Tumaini Lawrence akitoa neno kwenye hafla hiyo iliyofanyika katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere jana.

  Baadhi ya maafisa maendeleo wa Manispaa ya Kigamboni walioshiriki kwenye hafla hiyo wakifuatilia mjadala.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Kigamboni, Nobert Kamugisha akifuatilia majadiliano hayo. 

BALOZI WA BURUNDI NCHINI TANZANIA AHUDHURIA TAMASHA LA JAMAFEST JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Balozi wa Burundi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Gervais Abayeho (kulia) akisalimiana na wacheza ngoma kutoka nchini Burundi waliokuja kushiriki katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Balozi wa Burundi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Gervais Abayeho (kulia) akisalimiana na wacheza ngoma kutoka nchini Burundi waliokuja kushiriki katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.

 Balozi wa Burundi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Gervais Abayeho na viongozi alioambatana nao akisalimia wananchi waliofika katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Wacheza ngoma kutoka nchini Burundi wakitoa burudani katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Wacheza ngoma kutoka nchini Burundi wakitoa burudani katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Wacheza ngoma kutoka nchini Burundi wakitoa burudani katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Balozi wa Burundi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Gervais Abayeho (kulia) akiwa pamoja na wacheza ngoma kutoka nchini Burundi waliokuja kushiriki katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Viewing all 110144 articles
Browse latest View live




Latest Images