Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110129 articles
Browse latest View live

DC Ndejembi aagiza TAKUKURU kuchunguza miradi miwili ya maendeleo

$
0
0
Charles James, Michuzi TV

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe Deo Ndejembi amemuagiza Kamanda wa TAKUKURU wilayani humo kufanya uchunguzi kwenye miradi miwili ya Soko la Mazao lililopo Kata ya Mkoka na Mnada wa Mifugo uliopo Kijiji cha Mbande.

DC Ndejembi ametoa maagizo hayo wakati alipofanya ziara ya kutembelea miradi hiyo akiambatana na Wawakilishi kutoka Ubalozi wa Denmark ambao wanashirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kupitia mradi wa 'Local Investment Climate' kujenga miradi hiyo.

Amesema muonekano wa miradi hiyo haiendani na kiasi kilichotumika kuijenga hivyo ni vema TAKUKURU wafanye uchunguzi ili kuweza kujiridhisha.

" Tumefanya ziara kwenye hii miradi ambayo tunaijenga kwa kushirikiana na LIC ambayo iko chini ya Ubalozi wa Denmark lakini sijaridhishwa hata kidogo na thamani ya fedha kwenye haya majengo, ukiangalia muonekano wa hii miradi na kiasi kilichotumika unaona kabisa kuna walakini hapa.

" Huu mnada tumeambiwa thamani yake ni Shilingi Milioni 56, Hapa Soko hili mpaka sasa wameshatumia zaidi ya Milioni 200 lakini kinachoonekana hakiendani na thamani ya fedha hata kidogo. Hivyo niwatake TAKUKURU kuchunguza mara moja miradi hii na waniletee ripoti ili tuweze kuchukua hatua.

DC Ndejembi amesema Serikali ya awamu ya tano haiwezi kukubali kufumbia macho kasoro zozote ambazo wataziona kwenye miradi ambayo inatekelezwa na wao kama wasaidizi wa Rais Magufuli watahakikisha wanasimamia kwa nguvu uadilifu katika kazi bila kumuonea mtu.

Aidha katika ziara hiyo DC Ndejembi pia ameiomba Taasisi ya LIC kutoa sapoti yao kwenye mradi wa Kiwanda cha Maziwa ambacho kinajengwa wilayani hapo ili kiweze kukamilika ambapo anaamini kitatoa ajira nyingi kwa vijana pamoja na kuongeza mapato lakini pia kitaitangaza Wilaya hiyo.

" Niwashukuru ndugu zetu wa LIC mmekua mkishirikiana sisi kwenye miradi ya maendeleo, niwaombe pia muweze kutusaidia kukamilisha kiwanda hiki ambacho naamini kitaongeza mapato kwenye Wilaya yetu, kitapunguza changamoto ya ajira lakini tutakua tumemuunga mkono Rais Dk John Magufuli katika kuifanya Tanzania kufikia uchumi wa kati kupitia Sera yake ya viwanda," Amesema DC Ndejembi.

Kwa upande wake Mkuu wa Maendeleo ya Biashara kutoka Ubalozi wa Denmark, Jema Ngwale amempongeza DC Ndejembi kwa hatua aliyoichukua ya kuagiza TAKUKURU kuchunguza miradi hiyo ili kuweza kujiridhisha na kiasi kilichotumika.

" Sisi tutaendelea kushirikiana na Wilaya ya Kongwa katika kuwaletea miradi wananchi, Kuhusu sapoti yetu kwenye kiwanda cha maziwa jambo hilo tumelichukua na tukuahidi Mhe DC tutalifanyia kazi," Amesema Jema.
 Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe Deo Ndejembi akizungumza na Wawakilishi wa Balozi wa Denmark waliofika ofisini kwake ambapo walifanya mazungumzo na kukagua miradi inayojengwa kwa ushirikiano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa na Ubalozi huo.
 Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe Deo Ndejembi akizungumza na watumishi kutoka Halmashauri ya Wilaya hiyo pamoja na Wawakilishi kutoka Ubalozi wa Denmark wakati wa ziara ya kukagua miradi inayojengwa kwa ushirikiano wa Halmashauri ya Kongwa na Ubalozi huo.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe Deo Ndejembi akikagua ujenzi wa Mradi wa Soko la Mazao lililopo katika Kata ya Mkoka wilayani humo


WAZIRI JAFO AOMBA TAMASHA LA JAMAFEST KUKUZA KISWAHILI KWA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI

$
0
0


Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Selemani Jafo akizungumza alipotembelea katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019. 


Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema kuwa Tamasha la utamaduni na sanaa la nchini za Afrika mashariki litumike kukiuza kiswahili ili na nchini mwanachama wa Afrika Mashariki waweze waongee lugha hii adhimu ambayo sasa ni lugha rasmi katika jumuiya za Afrika. 


Amesema hayo alipotembelea maonesho ya Tamasha la Uatamaduni na Sanaa la nchi za Afrika amashariki al-maalufu kama JAMAFEST linaloendelea kufanyika katika uwa nja wa Taifa jijini Dar es Salaam. "Nimetembelea mabanda mbalimbali na kujionea bidhaa mbalimbali za asili na utamaduni wa maeneo mbalimbali katika nchi za Afrika Mashariki za wajasiriamali wa nchi zote". 

Amesema kuwa wizara ya Tamisemi ni chumvi, Afya, elimu vipo chini ya wizara yake, lakini wizara ya habari utamaduni, Sanaa na Michezo hususani Maafisa Utamaduni wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri wako TAMISEMI, hivyo unaweza kuona kwanini yupo hapa.

Hata amewapongeza wizara ya habari na utamaduni kwa kufanya kazi nzuri pamoja na kuhakikisha tamasha hili linafanyika kama lilivyopangwa na kwa mafanikio makubwa hasa kukidhi kiu ya wananchi wanaohudhuria tamasha hili adhimu. "Sina cha kuficha, nimefurahishwa na mambo yote niliyoyaona hapa uwanja wa Taifa hakina mmejipanga vyema, hongerani sana," amesema.

 Pia amesema kuwa amefurahishwa na maandalizi ya Tamasha la JAMAFEST na amewasihi wananchi kuja kwenda Uwanja wa Taifa kujifunza tamaduni mbalimbali kutoka nchi za Afrika Mashariki. 
Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (mwenye tai nyekundi) akiwa ameongozana na Mkurugenzi wa Michezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Yusuph Singo (wa kwanza kushoto) wakati alipotembelea katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. 

Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Selemani Jafo akimsikiliza mkuu wa kikundi cha kukuna nazi ikiwa washiriki ni washindi katika makundi mbalimbali walioshindanishwa kukuna nazi. Mashindano hayo yanafanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Tanzania katika maonesho ya Tamasha la JAMAFEST. Ikiwa wamepata washindi wa tatu kutoka makundi tofauti wakiwa wananwake wawili pamoja na mwananume mmoja. 
Akina mama wakikuna nazi katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. 
Waziri Jafo akiangalia nazi iliyokunwa vizuri katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. 
Waziri Jafo akitoa neno katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. 

Waziri Jafo akijionea sanaa za mikono katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. 
Mchezo wa mdako ukiendelea katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. 
Mchezo wa bao ukiendelea katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. 
Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Selemani Jafo akiangalia meza na viti vilivyotengenezwa na Mianzi. Yote hayo ni katika tamasha la JAMAFEST linaloendelea kufanyika katika uwanja wa Taiafa jijini Dar es Salaam. 
Waziri Jafo akijionea shughuli za mikono zinazofanywa na wajasiliamali toka katika jumuiya ya Afrika Mashariki katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.

MAJALIWA AWASILI IRINGA KUANZA ZIARA YA KIKAZIMAJALIWA AWASILI IRINGA KUANZA ZIARA YA KIKAZI

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ali Happy wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Iringa kuanza ziara ya kikazi mkoani humo, Septemba 24, 2019. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Iringa, Dkt Abel Nyamahanga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Lugola Atembelea Maonesho ya Utamaduni wa Afrika Mashariki (JAMAFEST)

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akimuuliza swalimshiriki kutoka nchini Uganda wakati waziri huyo alipotembelea kujionea Tamasha la Utamaduni wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki(JAMAFEST) linaloendelea hii leo Septemba 24, 2019 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akiangalia nguo ya batikitoka kwa wajasiriamali wa nchini Tanzania wakati waziri huyo alipotembelea kujionea Tamasha la Utamaduni wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki(JAMAFEST) linaloendelea hii leo Septemba 24, 2019 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akiangalia mkoba
uliotengenezwa kwa kifuu cha nazi toka kwa wajasiriamali wa nchini Tanzania wakati waziri huyo alipotembelea kujionea Tamasha la Utamaduni wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki(JAMAFEST) linaloendelea hii leo Septemba 24, 2019 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akimuangalia MzeeAbdallah Nyangalio fundi cherehani asiye ona wakati waziri huyo alipotembeleakujionea Tamasha la Utamaduni wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki(JAMAFEST) linaloendelea hii leo Septemba 24, 2019 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Picha na WHUSM – Dar es Salaam
24 Septemba, 2019

TIGO Yazindua promosheni ya Tigo Chemsha Bongo,KANDA YA ZIWA

$
0
0


Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Ziwa Uthmaan Madati,akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu gari atakalopewa mshindi wa Tigo chemsha bongo jijini Mwanza, wakati wa ufunguzi wa msimu wa Tigo Fiesta Saizi Yako na bahati nasibu ya Tigo chemsha bongo.

Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Ziwa Uthmaan Madati,akiwasha gari la mfano atakalopewa mshindi wa Tigo chemsha bongo jijini Mwanza, wakati wa ufunguzi wa msimu wa Tigo Fiesta Saizi Yako na bahati nasibu ya Tigo chemsha bongo.

Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Ziwa Uthmaan Madati(katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza, wakati wa ufunguzi wa msimu wa Tigo Fiesta Saizi Yako na bahati nasibu ya Tigo chemsha bongo, kushoto ni Meneja wa Tigo kanda ya Ziwa Daniel Mainoya na Afisa Huduma za Ziada wa Tigo Fabian Felician. 



Mteja wa Tigo kuzawadiwa gari aina ya Renault Kwid na wengine kujishindia mamilioni kama zawadi katika promosheni iliyozinduliwa leo Mwanza,iitwayo Tigo Chemsha Bongo katika msimu wa Tigo Fiesta 2019-Saizi Yako.


Akizungumza na waandishi wa habari,(Septemba 24,2019), wakati wa uzinduzi wa shindano la Tigo Fiesta Chemsha Bongo, ambalo linatafanyia Tanzania nzima katika msimu wa Tigo, Mkurugenzi Tigo Kanda ya Ziwa, Uthmaan Madati, alisema kwa mara ya kwanza, mkoa huo umeweka historia ya kufungua shughuli zote za Tigo Fiesta Saizi Yako 2019

“Tunatambua umuhimu wa tamasha la Tigo Fiesta 2019 Saizi Yako, kwamba si tu linaleta burudani kwa taifa bali linaibua na kukuza vipaji vipya hususan kwa tasnia ya muziki nchini,” alisema Madati.

Alisema tamasha hilo pia linasaidia katika kutoa elimu ya ujasiriamali lakini pia kutoa fursa mbali mbali kwa vijana.

Aidha Mkurugenzi huyo alitumia nafasi hiyo kuishukuru serikali ya mkoa kwa ushirikiano wake wakati wote wa tamasha hilo na mengine mengi na kwamba hilo limesaidia kuendesha shughuli hizo kwa ufanisi lakini pia kwa kujiamini. Katika hatua nyingine, Madata aliarifu kwamba kwenye shindano hilo, wanatoa zawadi za kila siku ikiwemo Sh 50,000 mpaka 100,000 na Sh 1 Milioni moja kila wiki.

“Katika kipindi cha miezi mitatu wakati kampeni hiyo ikiwa inaendelea, tutapata mshindi ambaye ataweza kujishindia gari lenye thamani ya Sh 23 milioni.,” alisema. Kwenye suala zima la usalama, Madata alisema wanashirikiana kwa ukaribu mkubwa na serikali huku akiwasihi wateja wa mtandao wa Tigo kujisajili kwa alama za vidole.

Katika hatua nyingine, Afisa Huduma za Ziada, Fabian Felician, alielezea kwamba msimu huu Tigo imeamua kushirikisha wateja wake wote kwa kuandaa maswali rahisi hususan yanayowahusu wasanii wa ndani. “Lengo la kufanya hivi ni kudhihirisha umuhimu na mchango wa wateja wetu na pia kutambua aina ya huduma tunazozitoa,” alisema Felician


Mathalan, Meneja wa Tigo, Kanda ya Ziwa, Daniel Mainoya alisema promosheni hiyo inaenda sambamba na msimu wenyewe ambao ni Tigo Fiesta 2019-Saizi Yako, kwa maana ya wasanii na burudani. Tigo Fiesta itafungua pazia mkoa wa Mwanza, Septemba 28,2019 katika viwanja vya CCM Kirumba.

BALOZI GETRUDE MONGELLA AFUNGUA TAMASHA LA 14 LA JINSIA 2019

$
0
0
Balozi Getrude Mongella ambaye ni Rais wa Kwanza wa Bunge la Afrika (PAP) na Katibu Mkuu wa Mkutano wa Nne wa wanawake duniani uliofanyika mwaka 1995 Beijing China amefungua Tamasha la 14 la Jinsia 2019 leo Jumanne Septemba 24,2019 katika viwanja vya TGNP Mtandao Mabibo Jijini Dar es salaam.


Akizungumza wakati wa kufungua Tamasha hilo litakalodumu kwa muda wa siku nne (Septemba 24 hadi 27,2019),Balozi Mongella maarufu 'Mama Beijing' amesema ili kujenga Tanzania ya Viwanda ni lazima wanawake na wanaume washiriki.

Balozi Mongella pia amehamasisha umuhimu wa wanawake kushirikishwa katika utengezaji wa Ilani za uchaguzi za vyama vya siasa ili kuhakikisha masuala ya wanawake yanaingizwa kufikia usawa wa kijinsia.

"Huu msemo wa Wanawake wakiwezeshwa wanaweza mimi nasema hii ni dhambi...hatupaswi kuwa omba omba...Sisi wanawake tunaweza tunachotaka ni vikwazo vinavyotukwamisha viondolewe njiani,tunataka wanawake washiriki kwenye utengenezaji wa ilani za uchaguzi ili Rais atakayegombea apewe na kubeba ajenda zinazohusu wanawake",alisema Balozi Mongella.

"Tuone masuala yanayotuhusu wanawake ni sehemu ya ajenda na uchaguzi utakapopita iwe rahisi kwa tutakayemchagua kuwa Rais kumuomba akimbizane na ajenda za wanawake na asipofanya hivyo atakuwa hajatekeleza Ilani",

Hata hivyo aliipongeza serikali kwa kutekeleza ajenda za Mkutano wa Beijing mfano Sera ya elimu bure hali inayosababisha ongezeko la watoto wa kike kwenda shule na imeondoa kikwazo cha watoto kukosa elimu.Aidha Balozi Mongella amewataka wanasiasa kuepuka Rushwa huku akieleza kuwa Wanasiasa wanaohonga 'rushwa' ili wapate uongozi wanabaka siasa.

Naye Mgeni Maalumu kutoka serikalini,Naibu Waziri - Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alisema Ukatili wa Kijinsia ni janga jipya linaloitia doa nchi ya Tanzania hivyo kuwaomba wadau wote kuungana kutokomeza hali hiyo.

"Hatuwezi kufikia usawa wa kijinsia katika taifa kama tunaendelea kuwa na matukio ya ukatili ya kijinsia ambayo nyuma yake yana sura ya mila,desturi,umaskini na ukosefu wa elimu.Naomba tuvunje ukimya na tuepuke kumaliza kesi zinazohusu masuala ya ukatili kwa kuyamaliza kienyeje",alisema Dkt. Ndugulile.

Dkt. Ndugulile alitumia fursa hiyo kuwahamasisha wanawake kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2020 na uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 24,2019.Akielezea kuhusu Tamasha la 14 la Jinsia 2019,Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao,Lilian Liundi alisema linahudhuriwa na wadau mbalimbali wa haki za wanawake kutoka ndani na nje ya Tanzania likiongozwa na mada kuu 'Wanaharakati wa jinsia mbioni kubadili dunia'.

"Tamasha hili lina umuhimu wa kipekee kwani tunaendelea kusherehekea maadhimisho ya miaka 25 ya TGNP tangu ianzishwe mwaka 1993 na kidunia tumeanza kusherehekea maadhimisho ya miaka 25 ya Azimio na Mpangokazi wa Beijing ambapo kilele chake ni mwaka 2020",alisema Liundi.
Balozi Getrude Mongella akifungua Tamasha la 14 la Jinsia 2019 katika viwanja vya TGNP Mtandao Mabibo Jijini Dar es salaam leo Jumanne Septemba 24,2019. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Balozi Getrude Mongella akifungua Tamasha la 14 la Jinsia 2019 katika viwanja vya TGNP Mtandao Mabibo Jijini Dar es salaam leo Jumanne Septemba 24,2019.

Balozi Getrude Mongella akisalimiana na Naibu Waziri - Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa kufungua Tamasha la 14 la Jinsia 2019 katika viwanja vya TGNP Mtandao Mabibo Jijini Dar es salaam leo Jumanne Septemba 24,2019. 
Naibu Waziri - Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza wakati wa ufunguzi wa Tamasha la 14 la jinsia mwaka 2019. 
Awali Balozi Getrude Mongella (kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP Mtandao,Asseny Muro wakifurahia jambo wakati akiwasili katika viwanja vya TGNP Mtandao kwa ajili ya kufungua Tamasha la 14 la jinsia mwaka 2019. 
Meza kuu wakiwa wamesimama baada ya Balozi Getrude Mongella kuwasili katika viwanja vya TGNP Mtandao jijini Dar es salaam. 
Washiriki wa Tamasha la 14 la Jinsia 2019 wakiendelea na burudani wakati Balozi Getrude Mongella akiwasili katika viwanja vya TGNP Mtandao kwa ajili ya kufungua tamasha hilo. 
Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP Mtandao,Asseny Muro akizungumza wakati wa ufunguzi wa Tamasha la 14 la jinsia mwaka 2019.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao,Lilian Liundi akizungumza wakati wa ufunguzi wa Tamasha la 14 la jinsia mwaka 2019.
MC wakati wa ufunguzi wa Tamasha la 14 la Jinsia 2019 ambaye ni Mwanachama wa TGNP Mtandao Ulu Mallya akitoa maelekezo mbalimbali wakati wa sherehe hizo za ufunguzi wa tamasha.

Sehemu ya wageni waalikwa wakati wa tamasha hilo.
Spika Mstaafu wa Bunge la Tanzania,Anne Makinda akizungumza wakati wa ufunguzi wa Tamasha la 14 la jinsia mwaka 2019.
Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Anders Sjoberg akizungumza wakati wa ufunguzi wa Tamasha la 14 la jinsia mwaka 2019.
Waziri Mkuu Mstaafu Tanzania,Joseph Sinde Warioba akizungumza wakati wa Tamasha la 14 la jinsia mwaka 2019. 
Washiriki wa Tamasha la 14 la jinsia mwaka 2019 wakicheza muziki. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

WAZIRI KANGI LUGOLA ATOA POLE KWA MKUU WA MAJESHI NCHINI

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akisaini kitabu cha maombolezo ya kmifo cha Nelson Mabeyo, mtoto wa Mkuu wa Majeshi nchini, Jenerali Venance Mabeyo, nyumbani kwa Mkuu wa Majeshi, Msasani jijini Dar es Salaam, leo Septemba 24, 2019.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia) akizungumza na Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali Robert Mboma, nyumbani kwa Mkuu wa Majeshi, Jenerali Venance Mabeyo, Msasani jijini Dar es Salaam, leo Septemba 24, 2019, walipokwenda kuhani msiba wa mtoto wa Mkuu wa Majeshi, Nelson Mabeyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akizungumza na Mwanasiasa Mkongwe na aliyewahi kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Prof. Philemon Sarungi, wakati walipokwenda nyumbani kwa Mkuu wa Majeshi, Jenerali Venace Mabeyo, Msasani jijini Dar es Salaam, leo Septemba 24, 2019, walipokwenda kuhani msiba wa mtoto wa Mkuu wa Majeshi, Nelson Mabeyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akimpa pole Mkuu wa Majeshi nchini, Jenerali Venance Mabeyo, wakati alipokwenda kuhani msiba wa mtoto wa Mkuu wa Majeshi, Nelson Mabeyo, Msasani jijini Dar es Salaam, leo Septemba 24, 2019. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

WAZIRI KAIRUKI AIPA SIKU SABA TIC KUWAFIKIA WAWEKEZAJI WAZAWA

$
0
0
 Meneja wa Kiwanda cha kutengeneza Kahawa cha Wilaya ya Mbinga (MCCCO) Mhandisi Rabbian Uromi akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki kuhusu mitambo ya kutengeneza mifuko (magunia) ya kuhifadhia kahawa katika kiwanda hicho kilichopo Mkoani Ruvuma wakati wa ziara yake Septemba 23, 2019.

Serikali yaipongeza kampuni ya usambazaji ya Route Pro kwa uwezeshaji vijana wa kuwapatia pikipiki 30

$
0
0

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,Ajira na Vijana ,Anthony Mavunde (kushoto) akimkabidhi pikipiki, Peter Mushi mkazi wa Makole Jijini Dodoma moja ya kampuni iliyotolewa na kampuni ya usambazaji ya Route Pro kwa ajili ya uwezeshaji wa vijana kibiashara.

.Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,Ajira na Vijana ,Anthony Mavunde (kushoto) akijaribu kuendesha moja ya pikipiki zilizotolewa kwa ajili ya kuwezesha vijana na Kampuni ya Route Pro Katika hafla iliyofanyika Dodoma,kushoto ni Meneja Uendeshaji wa Kampuni hiyo Jaja Mbazila ,Kulia ni Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo,Duane Edward na nyuma ni baadhi ya vijana watakaonufaika na msaada huo

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,Ajira na Vijana ,Anthony Mavunde akimkabidhi Augustine Dotto moja ya pikipiki iliyotolewa na Kampuni ya Route Pro.

Meneja Mkuu wa Kampuni ya usambazaji Bidhaa ya Route Pro akikabidhi funguo za pikipiki zilizotolewa kwa ajili ya kuwawezesha vijana kibiashara kwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Ajira na Vijana Anthony Mavunde wakati wa hafla hiyo iliyofanyika jijini Dodoma Katika viwanja vya Nyerere Square



Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi,Vijana na Ajira),Antony Mavunde, ameipongeza kampuni ya kitanzania ya usambazaji bidhaa ya Route Pro kwa ubunifu wake utakaowezesha vijana kupata ajira ambapo imetoa pikipiki 30 kwa vijana kutoka mikoa ya Dodoma, Dar es Salaam, Arusha, Moshi na Singida ambapo pia itawapatia mafunzo ya biashara.

Mavunde, alitoa pongezi hizo katika hafla ya kampuni ya Route Pro, kukabidhi pikipiki 10 kwa vijana wa mkoani Dodoma iliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square jijini humo.

“Ukosefu wa ajira kwa vijana ni moja ya changamoto inayolikabili taifa letu, ili kukabiliana nalo Serikali imekuwa ikitoa kipaumbele kushirikiana na wadau wanaonyesha nia ya kusaidia kubuni mipango endelevu ya kuwezesha ajira kwa vijana , kama ilivyofanya kampuni ya Route Pro, kwa kutoa mafunzo ya biashara kwa vijana wetu,Tutaendelea kutoa ushirikiano mkubwa kufanikisha suala hili,” alisema Mavunde.

Kampuni ya Route Pro, itatoa pikipiki 30 kwa vijana sambamba na kuwapatia elimu ya biashara na usambazaji bidhaa pia itawapatia elimu ya kutumia vifaa vya teknolojia ya kisasa vya kusaidia kuratibu usambazaji na taarifa.Vijana hao pia itawaunganisha na wadau wake katika biashara na wazalishaji wengine na kushirikiana nao kusambaza bidhaa za wateja katika masoko mkakati ambao utawanufaisha vijana hao na kampuni kwa kugawana faida itakayopatikana nusu kwa nusu.

Akiongea katika zoezi la kuwachagua vijana hao, Meneja Uendeshaji wa kampuni ya Route Pro, Jaja Mbazila, alisema kampuni hiyo imepata walengwa wa kushirikiana nao katika mpango huu, kutokana na rekodi yake ya vijana ambao imewahi kufanya nao kazi katika miradi yake mbalimbali ya usambazaji bidhaa katika siku za nyuma na imewachagua waliokuwa wanafanya kazi kwa bidii na wenye malengo ya kukua kibiashara.

“Tumelenga kuwawezesha vijana wenye bidii ya kazi na kujituma kupata fursa kuwa na biashara zao,tumefanya nao kazi kwa karibu katika miaka iliyopita na wameonyesha kuwa na nia ya kufanya vizuri biashara ya usambazaji”,alisema Mbazila.

Aliongeza kuwa mbali na kuwapatia pikipiki,RoutePro itawapatia vijana hao kiasi cha shilingi 100,000/- kila mmoja ziwasaidie kuanzia kazi.

Baada ya miezi 24, pikipiki hizo zitakuwa mali yao kwa ajili ya kuwasaidia katika shughuli za usambazaji,ingawa watakaopenda kufanya kazi katika mpango huu wa Route Pro wa kuwezesha vijana watajiunga tena katika mpango wa miaka 2 na kupatiwa tena tena pikipiki mpya.

Route Pro ni kampuni ya Kitanzania yenye uzoefu mkubwa wa biashara ya usambazaji wa bidhaa,kwa hivi sasa inazo pikipiki zaidi ya 250 za usambazaji nchini kote,na inatumia teknolojia ya kisasa za kupata taarifa za mauzo kwa ajili ya kuzifanyia uchambuzi.

DKT.NCHIMBI ATAKA CHANJO YA SURUA -RUBELLA IFIKE ASILIMIA 100

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi akizungumza wakati akiongoza kikao cha mafunzo kwa Wajumbe wa Kamati ya Afya ya Msingi (PHC) Mkoa wa Singida yaliyohusu kampeni shirikishi ya Surua-Rubella yaliyofanyika mjini hapa leo. Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Singida (RAS) Dkt. Angelina Lutambi.
Dkt.Khalid Ng’ombo kutoka Mari’e Stops Tanzania akichangia jambo.
Wajumbe wa kamati hiyo wakifuatilia mafunzo.
Wajumbe wa kamati hiyo wakifuatilia mafunzo.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Ernest Mugetta akizungumza kwenye kikao hicho.
Wajumbe wa kamati wakichukua maelezo ya mafunzo hayo.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida (RAS) Dkt.Angelina Lutambi akichangia jambo.
Mtaalamu wa Jinsia na Utetezi kutoka Shirika la World Vission Tanzania, Tumain Fred akizungumzia kuhusu watumishi kushiriki kampeni hiyo ya chanjo.
Mratibu wa Afya ya Uzazi na Mtoto Mkoa wa Singida, Christoweru Barnabas akitoa mada.
Mratibu wa Huduma ya Chanjo Mkoa wa Singida, Jadil Mhanganonya akitoa mada kwa wajumbe wa kamati hiyo.
Mwakilishi wa Meneja Mradi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la USAID- Boresha Afya-EGPAF, Dkt. Nicholaus Njoka akichangia jambo kwenye mafunzo hayo.
Afisa Tathmini na Ufuatiliaji wa Shirika la Sema, Jacob Kanka akichangia jambo katika mafunzo hayo.


Na Dotto Mwaibale, Singida

MKUU wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ametaka mkoa huo kutoka katika asilimia 98 ya kampeni ya chanjo ya surua rubella na polio ya mwaka 2014 kitaifa na kufikia asilimia 100 mwaka 2019.

Kauli hiyo aliitoa katika kikao cha mafunzo kwa wajumbe wa kamati ya afya ya msingi (PHC) Mkoa wa Singida yaliyohusu kampeni shirikishi ya Surua- Rubella na polio yaliyofanyika mkoani hapa jana.

Alisema suala hilo la chanjo si la mchezo ni la kitaaluma halitakiwi kuathiriwa hivyo wao kama mkoa waikatae asilimia hiyo ya 98 na kufikia asilimia 100.

“Sisi katika chanjo ya kitaifa ya mwaka 2014 tulifanya vizuri lakini mwaka huu tuikatae asilimia hiyo tufikie asilimia 100” alisema Dkt. Nchimbi.

Dkt.Nchimbi alisema bila ya kuwa na afya hakuna litakaloweza kufanyika hasa katika kipindi hiki ambacho taifa letu linaingia kwenye uchumi wa kati wa viwanda.

Alisema magonjwa hayo ya surua rubella na polio ambayo yanaenezwa kwa hewa hayabagui jinsia ya mtu, taaluma yake, utaifa wake, uongozi wake na fedha zake hivyo ni muhimu kila mmoja wetu kuzingatia kampeni hiyo ili kumuunga mkono Rais Dkt. John Magufuli katika kuboresha sekta ya afya nchini.

Dkt. Nchimbi alitumia nafasi hiyo kuwaomba viongozi wa dini ambao ni wajumbe wa kamati hiyo kuiombea kampeni hiyo na kwenda kuwahimiza waumini wao kuwapeleka watoto wao kwenye chanjo hiyo itakayofanyika kitaifa kuanzia Oktobata 15/19 2019 kwa kuwapeleka watoto wao wenye umri wa miaka mitano kushuka chini.

Aliongeza kuwa kampeni ya chanjo hiyo haina itikadi ya chama chochote ni kampeni ya watu wote walio Tanzania na Mkoa wa Singida.

Mtaalamu wa Jinsia na Utetezi kutoka Shirika la World Vission Tanzania, Tumaini Fred aliomba wakati wa kampeni hiyo watumishi wapewe muda wa nusu saa kwa ajili ya kuwapeleka watoto wao kupata chanjo kwani uzoefu umeonesha watoto wao hawakupatiwa chanjo kutokana na wazazi wao kukosa muda wa kuwapeleka.

Katika kampeni ya mwaka huu Mkoa wa Singida umelenga kuwafikia watoto 225,586 kwa chanjo ya Surua-Rubella na pia watoto 119,198 watapatiwa chanjo dhidi ya polio kwa njia ya sindano.

VOA: Viongozi wa mataifa 150 wahudhuria mkutano wa 74 wa umoja wa mataifa

VOA: DUNIANI LEO SEPT 24, 2019 2

BBC SWAHILI: DIRA YA DUNIA

DC KOROGWE MHE. KISSA KASONGWA AZINDUA WIKI YA USIKILIZWAJI, UTOAJI HUDUMA NA UTATUZI WA KERO ZA WANANCHI KATIKA WILAYA YA KOROGWE

$
0
0
Wakati wa  uzinduzi wa wiki ya usikilizwaji,utoaji huduma na utatuzi wa kero za wananchi wilayani Korogwe, Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe. Kissa G. Kasongwa amekemea watumishi wote wa Serikali ambao wanatabia ya kutowasikiliza na kuwahudumia wananchi vizuri pale wanapokwenda katiaka ofisi zao na kuongeza kuwa wananchi ndio mabosi wa wahusika wote serikalini. 

Alisema kama yeye Mkuu wa Wilaya wa Korogwe anatoa kiti chake ofisini na kukaa nje katika eneo la kuegeshea magari ili kuwasikiliza wananchi kwa unyenyekevu wote.

Mhe. Kasongwa alitoa rai kwa watumishi wote wa idara na taasisi, kuwa waende wawasikilize wananchi na kuto watolea maneno mabaya na kuwahimiza kufanya kazi kwa bidii na weredi ili kufikisha azma ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kutaka kuwafikia wananchi wanyonge.

Taasisi mbalimbali zitatoa huduma katika wiki hii, ikiwa ni pamoja na Mfuko wa Fidia kwa wafanyakazi (WCF) , PSSSF, NHIF, NSSF, NIDA, RITA, PCCB, TRA, Damu Salama, Jeshi la zima moto, Benki mbalimbali ikiwa ni pamoja na NMB na CRDB, Kampuni za Simu ikiwa ni pamoja na Halotel, TTCL, Mawakili wanaotoa msaada wa kisheria pamoja na taasisi mbalimbali
Mhe. Kissa G. Kasongwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe akizindua rasmi wiki ya usikilizwaji,utoaji huduma na utatuzi wa kero za wananchi wilayani hapo kuanzia tarehe 21 - 24 Septemba 2019, katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Wilaya Korogwe tarehe 21.09.2019
 Viongozi wa Dini wakifungua kwa maombi wiki ya usikilizwaji,utoaji huduma na utatuzi wa kero za wananchi
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Korogwe Bi. Rehema Bwasi akitoa maelezo ya chimbuko la wiki ya usikilizwaji,utoaji huduma na utatuzi wa kero za wananchi katika Wilaya hiyo.
Mbunge wa Korogwe mjini Mhe. Mary Chatanda akitoa sakamu zake kwa wananchi wakati wa uzinduzi wa  wiki ya usikilizwaji,utoaji huduma na utatuzi wa kero za wananchi wilayani Korogwe.
Mbunge wa Korogwe Vijijini Mhe. Timotheo Mzava akitoa salamu zake kwa wananchi wakati wa uzinduzi wa  wiki ya usikilizwaji,utoaji huduma na utatuzi wa kero za wananchi wilayani Korogwe.
 Mwenyekiti wa CCM Korogwe vijijini Bw. Nassoro Malingumu akitoa salamu zake wakati wa  wiki ya usikilizwaji,utoaji huduma na utatuzi wa kero za wananchi  wilayani Korogwe
 Mwenyekiti wa CCM Korogwe mjini  Bw. Immanuel Chale akitoa salamu zake wakati wa  wiki ya usikilizwaji,utoaji huduma na utatuzi wa kero za wananchi wilayani Korogwe
 Wananchi mbalimbali wakiwa katika uzinduzi wa wiki ya usikilizwaji,utoaji huduma na utatuzi wa kero za wananchi
Waananchi mbalimbali kutoka Wilayani Korogwe wakipata huduma wakati wa  wiki ya usikilizwaji,utoaji huduma na utatuzi wa kero za wananchi.

BALOZI WA BURUNDI NCHINI TANZANIA AHUDHURIA TAMASHA LA JAMAFEST JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

Balozi wa Burundi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Gervais Abayeho (kulia) akisalimiana na wacheza ngoma kutoka nchini Burundi waliokuja kushiriki katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Balozi wa Burundi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Gervais Abayeho (kulia) akisalimiana na wacheza ngoma kutoka nchini Burundi waliokuja kushiriki katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
 Balozi wa Burundi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Gervais Abayeho na viongozi alioambatana nao akisalimia wananchi waliofika katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Wacheza ngoma kutoka nchini Burundi wakitoa burudani katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Wacheza ngoma kutoka nchini Burundi wakitoa burudani katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Wacheza ngoma kutoka nchini Burundi wakitoa burudani katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Balozi wa Burundi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Gervais Abayeho (kulia) akiwa pamoja na wacheza ngoma kutoka nchini Burundi waliokuja kushiriki katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Geita wazinduliwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa

$
0
0

 Mkurugenzi wa Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk.Tausi Kida akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri mara baada ya kuwasili kwenye uwanja Kahangalala mjini Geita kwa ajili ya kushiriki kwenye ufunguzi wa Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu yaliofanyika sambamba na uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji wa mkoa wa Geita ulioandaliwa na ESRF kwa ufadhili wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Geita Mjini, Joseph Kasheku (kulia) maarufu kama Musukuma mara baada ya kuwasili kwenye uwanja Kahangalala mjini Geita kwa ajili ya kushiriki kwenye ufunguzi wa Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu yaliofanyika sambamba na uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji wa mkoa wa Geita ulioandaliwa na ESRF kwa ufadhili wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP). Katikati ni Mkurugenzi wa Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk.Tausi Kida
 Mkurugenzi wa Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk.Tausi Kida na Prof. Godwin Mjema ambaye ni mmoja wa watu waliofanikisha kuandaa mwongozo wa uwekezaji wa mkoa wa Geita wakielekea kwenye eneo maalum lililotengwa mara baada ya kuwasili kwenye uwanja Kahangalala mjini Geita kwa ajili ya kushiriki kwenye ufunguzi wa Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu yaliofanyika sambamba na uzinduzi wa mwongozo wa uwekezaji wa mkoa wa Geita ulioandaliwa na ESRF kwa ufadhili wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).
 Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi, Robert Gabriel akitoa salamu na kuwakaribisha wageni wakati sherehe za ufunguzi wa Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu yaliyofanyika katika uwanja wa Kahangalala mjini Geita.
  
Mkurugenzi wa Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk.Tausi Kida akitoa taarifa kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ya mwongozo wa uwekezaji wa mkoa wa Geita iliyoandaliwa na taasisi yake kwa ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa na Maendeleo (UNDP) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu uliofanyika sambamba na uzinduzi wa mwongozo huo kwenye uwanja wa Kahangalala mjini Geita.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua Mwongozo unaoonyesha fursa za uwekezaji katika mkoa wa Geita wakati alipofungua Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu kwenye uwanja wa Kahangalala mjini Geita. Wengine pichani kutoka kushoto ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, Waziri wa Madini, Doto Biteko, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi, Robert Gabriel na kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Geita, Alhaj Said Kalidushi.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha Mwongozo unaoonyesha fursa za uwekezaji katika mkoa wa Geita mara baada ya kuuzindua wakati alipofungua Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu kwenye uwanja wa Kahangalala mjini Geita. Wengine pichani kutoka kushoto ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, Waziri wa Madini, Doto Biteko, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi, Robert Gabriel na kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Geita, Alhaj Said Kalidushi.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Waziri wa Madini, Mh. Doto Biteko (wa pili kushoto) Mwongozo unaoonyesha fursa za uwekezaji katika mkoa wa Geita mara baada ya kuuzindua wakati alipofungua Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu kwenye uwanja wa Kahangalala mjini Geita.Wanaoshuhudia tukio hilo ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi, Robert Gabriel (wa pili kulia) na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Geita, Alhaj Said Kalidushi (kulia).
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi, Robert Gabriel (wa pili kulia) Mwongozo unaoonyesha fursa za uwekezaji katika mkoa wa Geita mara baada ya kuuzindua wakati alipofungua Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu kwenye uwanja wa Kahangalala mjini Geita.
 Msanii wa muziki wa Injili nchini Emmanuel Mbasha akitoa burudani wakati wa hafla ya uzinduzi wa Maonyesho ya Pili ya Tekinolojia ya Dhahabu na Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa wa Geita uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kahangalala mjini Geita.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na meza kuu katika picha ya pamoja na wadau wa ESRF na UNDP mara baada ya kuzindua Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu yaliyoenda sambamba na uzinduzi wa Mwongozo unaoonyesha fursa za uwekezaji katika mkoa wa Geita katika hafla iliyofanyika kwenye uwanja wa Kahangalala mjini Geita.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na meza kuu katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa GGM mara baada ya kuzindua Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu yaliyoenda sambamba na uzinduzi wa Mwongozo unaoonyesha fursa za uwekezaji mkoa wa Geita katika hafla iliyofanyika kwenye uwanja wa Kahangalala mjini Geita.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na meza kuu katika picha ya pamoja na kamati ya maandalizi mara baada ya kuzindua Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu yaliyoenda sambamba na uzinduzi wa Mwongozo unaoonyesha fursa za uwekezaji katika mkoa wa Geita hafla iliyofanyika kwenye uwanja wa Kahangalala mjini Geita.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na meza kuu katika picha ya pamoja na viongozi wa CCM wa mkoa wa Geita mara baada ya kuzindua Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu yaliyoenda sambamba na uzinduzi wa Mwongozo unaoonyesha fursa za uwekezaji katika mkoa huo hafla iliyofanyika kwenye uwanja wa Kahangalala mjini Geita.
 Mkurugenzi wa Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk.Tausi Kida na Mkuu wa Idara ya maarifa na Ubunifu wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Margareth Nzuki (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na mdau wa Geita wakati sherehe za ufunguzi wa Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu yaliyofanyika katika uwanja wa Kahangalala mjini Geita.
 Mkurugenzi wa Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk.Tausi Kida katika picha ya kumbukumbu na Mkuu wa mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri wakati sherehe za ufunguzi wa Maonyesho ya Tekinolojia ya Dhahabu yaliyofanyika katika uwanja wa Kahangalala mjini Geita.
 Kutoka kushoto ni Meneja wa Data wa ESRF, John Kajiba, Mkurugenzi wa Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk.Tausi Kida, Mkuu wa mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri pamoja na wabunge wa viti maalum wa mkoa wa Geita wakiwa kwenye picha ya pamoja.

Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Geita umezinduliwa jana tarehe 22 Septemba 2019 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa wakati wa Maonyesho ya Teknolojia ya Dhahabu kwenye Uwanja wa Kalangalala Mjini Geita. Zaidi ya watu 1000 walishiriki uzinduzi huo, ikijumuisha viongozi mbalimbali wakiwamo Mawaziri, Wabunge, Wakuu wa Mikoa na Madau wa Madini.

Katika uzinduzi huo Waziri Mkuu alibainisha jitihada mbalimbali ambazo Serikali imefanya kuhakikisha Madini yananufaisha Nchi na Watu wake.

Waziri Mkuu Majaliwa amewaonya watoroshaji Madini na kusema Serikali ipo makini na imejidhatiti vya kutosha na kwamba haitokuwa na huruma nao. Aidha alisema kwa wale wasiotaka kuelewa na kuacha kutorosha madini Serikali itashughulika nao.

Kwa upande wake, Waziri wa Madini Doto Biteko amesema kwa sasa Serikali na Makampuni yanayomiliki migodi wanaheshimiana kwani Makampuni hayo yanatii magizo na kufuata sheria za nchi.

Waziri Doto amesema kabla ya kufunguliwa kwa masoko ya madini nchini makusanyo ya dhahabu yalikuwa kilo 101 kwa mwezi lakini baada ya masoko kufunguliwa makusanyo yameongezeka na kufikia kilo 1,974 hivi sasa.

Akizungumza mbele ya Waziri Mkuu, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Mbaga Kida, alisema ESRF chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na kwa kushirikiana na Serikali imekuwa ikiandaa Miongozo ya Uwekezaji katika Mikoa kwa lengo la kuchambua na kuainisha fursa za uwekezaji zilizopo katika mikoa husika ili kuwavutia wawekezaji.

Dkt. Kida alisema mpaka sasa ESRF imesaidia Mikoa 17 kuandaa Miongozo ya Uwekezaji ambapo mikoa 11 imekamilisha na Mikoa 6 iko katika hatua mbalimbali na kuongeza kuwa ESRF itaendelea kuandaa Miongozo ya Uwekezaji katika mikoa iliyobaki kuanzia mwezi wa kumi mwaka.

Alisema kazi hii ya Uandaaji wa Miongozo ya Uwekezaji imeweza kuibua fursa nyingi kwenye Mikoa husika zikiwa katika sekta na ngazi zote.

"Kwa mfano mheshimiwa Waziri hapa Geita kuna fursa kubwa katika sekta ya madini hasa uchimbaji na uongezaji thamani wa madini ya dhahabu kwa wawekezaji wadogo, wa kati na wakubwa. Fursa nyingine zipo katika sekta ya viwanda, kilimo, ufugaji, uvuvi, ujenzi, utalii, na huduma. Maelezo ya kina juu ya fursa hizo yapo kwenye Mwongozo wa Uwekezaji ambao utauzindua leo hii”alisema Dkt. Kida.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa ESRF Miongozo hii ya Uwekezaji ngazi ya Mikoa itachangia katika Mwongozo wa Uwekezaji wa Taifa na kwamba ESRF  itaendelea kushirikiana na mikoa katika utekelezaji wa miongozo hii kwa kusaidia kufanya upembuzi yakinifu (feasibilty studies), kuandaa Miongozo ya Biashara (Business Plans) kwa baadhi ya fursa ambazo mikoa itapenda kuwekeza, na kunadi fursa zilizopo kwenye Miongozo.

Aidha Kida alishukuru wataalamu wa ESRF walioshiriki kuandaa mwongozo huo na kuufanikisha. Aliwataja kwa majina waliofanikisha kuwa ni pamoja na Margareth Nzuki, Dk Oswald Mashindano, Prof. Godwin Mjema; Doris Lyimo na Mussa Mayala Martine.

Mkurugenzi wa ESRF aliwapongeza pia viongozi wa Mkoa wa Geita kwa jitihada zao za kuuweka wazi mkoa huo na kuwataka wadau wote kuhakikisha Mwongozo huo unatumika ipasavyo ili kuleta matokeo yaliyo kusudiwa katika mkoa wa Geita na Taifa kwa ujumla.

VOA SWAHILI: ULINZI MKALI KILA KONA JIJINI NEW YORK WAKATI WA MKUTANO WA UMOJA WA MATAIFA

WAFUGAJI KUNUFAIKA NA UWEKEZAJI MRADI WA KIWANDA CHA MBOLEA

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi ( Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel( wa kwanza kulia) akijadili jambo na wageni kutoka nchini slovakia mara baada ya kuwasilisha mada kuhusu nia yao ya kuwekeza kwenye mradi wa kutengeneza mbolea nchini Tanzania katika ukumbi wa Wizara Mtumba jijini Dodoma. (24/9/2019)
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel akiwakaribisha na kuwaahidi ushirikiano wawekezaji wa kampuni ya ROKOSAN kutoka Jamhuri ya Watu wa Slovakia, waliofika wizarani kwa lengo la kuwasilisha mada ya uwekezaji wa mradi wa kiwanda cha kutengeneza mbolea kwa kutumia malighafi zitokanazo na mifugo  katika ukumbi wa Wizara Mtumba jijini Dodoma leo. (24/9/2019)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi(Mifugo), Prof. Elisante Ole Gabriel akiwa kwenye picha ya pamoja na wageni kutoka Jamhuri ya watu wa Slovakia, wawakilishi wa mradi huo nchini Tanzania pamoja na wawakikishi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mara baada ya kikao kifupi katika ukumbi wa Wizara Mtumba jijini Dodoma leo (24/9/2019).

WAFUGAJI nchini mbioni kunufaika baada ya wawekezaji kuja na nia ya kuwekeza kwenye mradi utakaohitaji malighafi kutoka kwenye mifugo zikiwemo kwato,pembe,kinyesi na manyoya ambazo zitakuwa zikinunuliwa kama malighafi nyingine ili kutumika kwenye kiwanda cha kutengenezea mbolea.

Lengo la serikali  ni kuendelea kufungua milango kwa wawekezaji wote wenye nia ya kuwekeza kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo sekta ya mifugo nchini.Miradi kama hii itasaidia kuhamasisha wananchi kuendelea kufuga kwa wingi na kwa tija baada ya kuona fursa za uwekezaji zikiongezeka.

Hayo yamesemwa leo (24/9/2019), na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Profesa Elisante Ole Gabriel wakati akiwakaribisha wawekezaji wa kampuni ya ROKOSAN inayojihusisha na utengenezaji wa mbolea kwa kutumia malighafi zitokanazo na mifugo kutoka Jamhuri ya watu wa Slovakia kwenye makao makuu ya Wizara hiyo eneo la mtumba jijini Dodoma.

Alisema wawekezaji walio tayari kuwekeza wanakaribishwa na  wizara inawaahidi ushirikiano wa hali ya juu kwenye sekta ya mifugo kwa ajili ya  kuinua hali za wafugaji wetu hapa nchini, kuongeza ajira, pia kuongeza ukusanyaji wa kodi kupitia bidhaa mbalimbali zikiwemo zile zitokazo viwandani.

Katibu Mkuu alisema viongozi wa serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt.John Pombe Joseph Magufuli wanahitaji uwekezaji wenye matokeo ya haraka na yenye tija kwa taifa ndio maana wizara yake iko tayari kutoa ushirikiano pale mwekezaji anapoonyesha nia ya kuwekeza kwenye sekta ya mifugo nchini.

Aidha Katibu Mkuu aliwahakikishia kuwa Tanzania ni mahali salama na sahihi kwa  uwekezaji huo kutokana na rasilimali kubwa ya mifugo iliyopo nchini ambapo idadi ya ng,ombe ni takribani milioni.32.2 mbuzi mil.20,kondoo 5.5, kuku mil.79.1 na punda zaidi ya laki 6.

Prof.Gabiel aliongeza kuwa uwekezaji huo nchini Tanzania utakuwa na manufaa sio kwa watanzania tu bali hata kwa wawekezaji wenyewe kwa kuwa soko  la bidhaa la ndani ya nchi ni kubwa, Afrika ya Mashariki pia lipo,bila kusahau nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Akizungumzia mradi huo wa kiwanda cha kutengeneza mbolea kwa kutumia malighafi zitokanazo na mifugo zikiwemo kwato, pembe, manyoya na kinyesi,Prof.Gabiel alisema itakuwa ni faraja kwa wadau wa sekta kuona hakuna kinachotupwa kutoka kwenye mifugo bali kinaongezewa thamani na kuwa bidhaa.

Profesa Gabriel aliongeza kuwa hata kwenye Mpango Kabambe wa Kuendeleza  Sekta ya Mifugo nchini (TLMP) umeelekeza jinsi mnyororo wa kuongeza thamani malighafi zitokanazo na mifugo zitakavyoleta tija kuelekea uchumi wa viwanda nchini.

Kwa upande.wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya ROKOSAN Dkt. Stefan Szoke alisema anashukuru kwa mwitikio wa serikali wa kuonyesha ushirikiano katika hatua za awali za uwekezaji wa mradi huo.

Dkt. Szoke alisema baada ya kufuatilia masuala ya uwekezaji waligundua kuwa Tanzania ni nchi yenye fursa kubwa za uwekezaji kutokana na rasilimali na mazingira mazuri yaliyopo katika sekta ya mifugo na kusisitiza kuwa nia yao ni kuanzisha miradi yenye manufaa kwa haraka mara baada ya kukamilisha taratibu husika.

Akitolea mfano nchi za Ulaya ambako pia wamewekeza miradi ya aina hiyo, Dkt.Szoke alisema licha ya wafugaji kunufaika kwa kuuza malighafi hizo zitokanazo na mifugo, wakulima nao wamekuwa wakinufaika kwa kupata mbolea yenye ubora na kwa gharama nafuu.

Akifafanua faida nyingine ya mradi huo alisema kuwa gharama za uzalishaji zikipungua hata bei ya mazao sokoni  hupungua hivyo kumfanya mwananchi kumudu bei za bidhaa mbalimbali ziwemo za vyakula ambayo ni muhimu kwa afya zao.

TAMASHA LA JAMAFEST KUZINDULIWA SEPTEMBA 22 JIJINI DAR

$
0
0
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kufungua Tamasha utamaduni na Sanaa JAMAFEST la nchi za Afika Mashariki jijini Dar es Salaam.

Tamasha lenye lengo la kuunganisha nchi za Afrika Mashariki kupitia sanaa na utamaduni litazinduliwa jijini Dar es Salaam Septemba 22,2019 katika uwanja wa Taifa jijini.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hasan Abbas amesema  wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati wa semina ya kuwajengea Uwezo kwajili ya kulipoti na kutoa taarifa mbalimali za Tamasha la Jamafest leo jijini Dar es Salaam.

 Amesema kuwa  tamasha hilo la Utamaduni na sanaa la Jumuiaya ya Afrika Mashariki litatanguliwa na matembezi ya 

litazinduliwa Jumapili na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Magufuli kuanzia saa nane katika viwanja vya Taifa jijini Dar es Salaam.

Amasema tamasha hili litakalohusisha nchi za jumuiya ya Afrika mashariki litafanya maonesho ya utamaduni wa nchi za Afrika Mashariki ambapo kila nchi itaonesha sanaa na tamaduni zao.

Nae Mwenyekiti wa maandalizi wa tamasha la Jamafest, Joyce Fisoo amasema kuwa tamasha hilo litahudhuliwa na washiriki kutoka Kenya  612, Uganda 201, Burundi 179, Rwanda 125 na zaidi ya watanzania elfu moja kuhudhulia tamasha hilo.

MABINGWA NGUMI KUPONGEZWA NA MASHABIKI OKTOBA 4

$
0
0
MABINGWA wa mgumi za kulipwa nchini walioibuka na ushindi wanatarajia kushiriki katika sherehe za kupongezwa na mashabiki wao Oktoba Nne Club 361Mwenge Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Mwandishi wa Habari hizi Mratibu mkuu wa Pambano la kuwapongeza mabondia hao Selemani Semunyu alisema mipango imekamilika ikiwemo mabondia watakaocheza ingawa maombi ni mengi ya mabondia wengi kutaka kushiriki kuonyesha furaha yao na kuwaunga mkono mabondia hao.

Amewataja miongoni mwa mabingwa  hao ni  Abdalah Pazi ,Tonny Rashidi ,Bruno Vifua Viwili na  Nassib Ramadhani kwa pamoja na bondia yeyote binhwa na wameletea taifa heshma kubwa  wadau na mashabiki hakuna budi kuwapongeza.

" Serikali na Wabunge wamewapongeza lakini wadau na mashabiki sasa huu ndio wasaa wa kuwapongeza hata kama kuna zawadi ya kuwapa hii ndio sehemu moja lakini sie tunawapongeza kwa pambano" Alisema Semunyu.

Pambano hili pia litatumika kupata mabondia watakaowania mikanda mwezi Desemba ambapo litafanyika pambano funga mwaka.


" Watakaofanya vizuri katika pambano hili wataweza kupata nafasi katika pambano la mwezi wa 12 ambapo historia ya Ngumi nchini kwa  kipindi cha hivi karibuni utawekwa " Alisema Semunyu.

Pia amewashukuru kamisheni ya ngumi za kulipwa kutoa kibali wadhamini Smart Gin na kuomba wadhamini wengine kujitokezo kwa wingi ili kufanikisha kurejesha hadhi ya mchezo wa ngumi nchini.

Kwa upande wake mratibu wa kiufundi wa mapambano hayo Yassin Abdalah  Ustaadh aliwataja mabondia watakaosindikiza sherehe hiyo kuwa ni issa nampechehe  (Dsm) vs alli hamisi  (morogoro )

Ibrahim Makubi (Dsm)vs abdallah kingolwira  ( morogoro )Maganga kulwa (mbagala) vs Said Sudi (M'nyamala) )Hashimu msungo vs Epson john Lewis Salumu omari vs ramadhani chicho

Ameongeza kuwa mapambano yanaweza kuongezeka kutokana na  mabondia wengine kitafuta nafasi ya kutaka kishiriki Desemba lakini wengine nao wanatala kushiriki kuonuesha furaha ya ushindi huo

" Mapambano ya surprize kibao  mabingwa watakuwepo  na wasanii wa kutumbuiza njoo tuwapongeze mabondia wetu walioshinda mikanda tule tunywe tupige nao picha," alisema Ustaadhi.
Viewing all 110129 articles
Browse latest View live




Latest Images