Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110175 articles
Browse latest View live

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LEO SEPTEMBA 19, 2019

$
0
0
KUPATIKANA NA NISHATI YA MAFUTA BILA KIBALI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea na Operesheni, Misako na Doria katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya katika kuzuia na kupambana na uhalifu na kudhibiti uuzaji na usambazaji wa nishati ya mafuta bila kibali.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa kumi na sita [16] kwa tuhuma za kupatikana na kufanya biashara ya nishati ya mafuta aina ya Diesel na Petrol bila kibali.
Katika misako iliyofanyika kuanzia tarehe 17 Septemba, 2019 hadi 19 Septemba, 2019 katika maeneo ya Maghorofani, Uyole, Itezi Jijini Mbeya, Chimala, Igawa na Igurusi Wilayani Mbarali na maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Kyela na Chunya jumla ya watuhumiwa 16 wamekamatwa na jumla ya lita 5,940 za Diesel na lita 20 za Petrol zimekamatwa.
Aidha katika misako hiyo watuhumiwa wamekutwa na madumu 79 na mapipa 06 yenye ujazo tofauti tofauti yanayotumika kuhifadhia mafuta hayo pamoja na mipira ya kuhamishia mafuta.

Watuhumiwa waliokamatwa ni:-
MAJALIWA EDWARD [30] Mkazi wa Mwambene
EDSON KALINGA @ MANGI [32] Mkazi wa Iganzo
HAMIS ANYIMIKE [32] Mkazi wa Mafiati
ISSAH MWAMBELO [33] Fundi Magari na Mkazi wa Sae
KAMBELA HAMAD MWIPOPO [30] Mkazi wa Makunguru
LUGANO MWASALEMBA [18] Mkazi wa Kibonde Nyasi.
DAUD MWASALEMBA [40] Mkazi wa Itezi
SIKUDHANI ANTHONY [35] Mkazi wa Kijiji cha Isyonje
HASHIM DAVID JOSEPH [20] Mkazi wa Mchangani
JUSTINE ADAM [21] Mkazi wa Isyonje
GEORGE MWAKALOBO @ MWADADA [40] Mkazi wa Ipinda
MAJUTO SIMONI [37] Mkazi wa Kapwili
LWITIKO MWAIPOPO [38] Mkazi wa Ipinda
JAKOBO MWAKILEMA [47] Mkazi wa Ipinda
ANGALWISYE ASUBISHI [35] Mkazi wa Chimala 
MWAGAMBO USWEGE [40] Mkazi wa Igurusi
Watuhumiwa watafikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

KUINGIZA BIDHAA NCHINI ZILIZOPIGWA MARUFUKU.

Mnamo tarehe 16/09/2019 majira ya saa 03:30 usiku huko maeneo ya Imezu, Kata ya Inyala, Tarafa ya Tembela, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Askari Polisi waliikamata gari namba T. 667 ADM aina ya Mark II rangi nyeupe na baada ya kuikagua ndani yake ilikuwa na vipodozi vya aina mbalimbali ambavyo ni:-
Carolite dozen 24 na pic 52, 
Betasol pic 90,
Diproson pic 20,
Epiderm pic 30,
White Max boksi 02,
Diana Lotion boksi 02,
Cocoderm pic 12,
Teint Claire pic 06,
Esapharma Dozen 48 na pic 10,
Lemovet Cream Dozen 46 na pic 10,
Clairmen pic 72,
Extra Clair pic 77,
Citrolite Dozen 12 pic 18,
Calorite Dozen 24 na pic 52,
Top Lemon pic 24,
Carats pic 32,
Miki Clair Dozen 4,
Mount Clair Dozen 1,
Bronz Dozen 2,
Clinic Cleare dozen 3,
Bio Claire dozen 1,
Dodo Dozen 1 na pic 2
Carotone pic 6 na
Actif Plup pic 1 
Vyote vikiwa ni vipodozi vilivyopigwa marufuku kuingia nchini.
Mbinu iliyotumika ni dereva asiyefahamika kupita kwa spidi maeneo ya maghorofani kitendo kilichopelekea kutiliwa shaka gari hilo na askari Polisi kisha kuifuatilia gari hiyo na kuikamata ikiwa na vipodozi hivyo. Msako mkali wa kumtafuta dereva wa gari hilo na mmiliki wake unaendelea. 

KUINGIZA BIDHAA NCHINI BILA KIBALI.

Mnamo tarehe 16/09/2019 majira ya saa 03:30 usiku huko maeneo ya Imezu, Kata ya Inyala, Tarafa ya Tembela, Wilaya ya Mbeya Vijijini, askari Polisi waliikamata gari namba T. 667 ADM aina ya Mark II rangi nyeupe na baada ya kupekua ndani yake kulikuwa na vitenge jozi 106 na mabelo 03 ya vitenge ambayo hayajafunguliwa vikiwa vimeingizwa nchini bila kibali. 

Mbinu iliyotumika ni dereva asiyefahamika kupita kwa spidi maeneo ya maghorofani kitendo kilichopelekea kutiliwa shaka na askari Polisi na kuanza kuifuatilia gari hiyo na kuikamata ikiwa imebeba vitenge hivyo. Mtuhumiwa mmoja aitwaye HOBOKELA MWAKYUSI JENGELA [49] Mfanyabiashara na Mkazi wa Sae anashikiliwa kwa mahojiano kuhusiana na bidhaa hizo. Msako wa kumtafuta na kumtia mbaroni dereva na mmiliki wa gari hiyo unaendelea.

Imetolewa na:
[ULRICH O. MATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.






UCHORONGAJI HANDAKI NAMBA 2 LA TRENI YA UMEME,WAFIKIA ZAIDI YA 45%,NI MITA ZAIDI YA 470

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASISISTIZA MAWAZIRI WA SADC KUSIMAMIA MAENDELEO YA TEKNOLOJIA

$
0
0



 Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewataka mawaziri wanaoshughulikia tehama, habari, uchukuzi na hali ya hewa kutoka nchi 16 wanachama wa Jumuiya ya maendeleo ya nchi kusini mwa Afrika (SADC) kusimamia maendeleo ya teknolojia. 





Hayo ameyasema leo Septemba 19, 2019 wakati akizindua mkutano wa mawaziri hao, ambao ulitanguliwa na majadiliano yaliyowakutanisha makatibu wakuu na viongozi wa juu wanaoshughulikia sekta hizo kutoka nchi wanachama ambao walikaa kwa siku tatu kabla ya baraza la mawaziri lililoanza juzi. 
Kati ya maagizo hayo ni pamoja na kushughulikia masuala ya mtandao, mkakati wa posta kuurejesha katika teknolojia ya sasa, kuondoa vikwazo vya kibiashara kati ya nchi na nchi, maendeleo kiteknolojia. 
Katika hotuba yake, amesema mkutano huo ni wa kwanza kisekta baada ya mkutano wa awali. 
“Ni matarajio yetu kuwa mkutano huu utajadili utekelezaji wa mikakati mbalimbali, programu na miradi kama ilivyoainishwa kwenye mpango mkakati elekezi wa maendeleo ya sadc wa mwaka 2015 mpaka 2030. 
“Pamoja na mpango kabambe wa maendeleo ya miundombinu wa mwaka 2019 mpaka 2023 utajadili na kufanya tathmini na kuja na njia mbadala ya utekelezaji uchumi kikanda ili kuharakishwa,” alisema.
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa SADC wa Sekta ya TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa wanakutana kwa siku mbili kuanzia leo Septemba 19-20, 2019 jijini Dar es Salaam. Picha zote na Matokeo Chanya+. Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhandisi Isack Kamwelwe akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa SADC wa Sekta ya TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa wanakutana kuanzia leo Septemba 19-20, 2019 jijini Dar es Salaam. Nae Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe amesema mkutano huo umewakutanisha wataalamu wa tehama, hali ya hema, uchukuzi na mawasiliano kutoka nchi wanachama pamoja na wakuu wa taasisi na mashirika pamoja na viongozi waliopo katika sekta binafsi nchi za SADC. Amesema katika majadiliano wote kwa pamoja wanazo changamoto mbalimbali wanazoshabihiana katika hali ya hewa, miundombinu mbalimbali ambayo inarudisha nyuma nchi kujikomboa kiuchumi na kuwa wana mjadala wa pamoja katika kuzileta nchi kiuchumi kwa manufaa ya wananchi wa ukanda huu. “Kipindi cha asubuhi tumeshaanza na tumeendelea na mjadala wajumbe walileta hoja mbalimbali kushuhghulikia reli, majanga na hali ya hewa, manufaa ya teknolojia ya habari na mawasiliano katika kuboresha uchumi na maisha ya wana SADC. “Aidha wataalamu kutoka sekta za kibenki maendeleo ya Afrika na Benki ya Maendeleo ya Afrika Kusini wameelezea uwezo wao katika kusaidia ujenzi na uboreshaji wa miundombinu katika sadc, lakini pia maeneo mengine yaliyoangaziwa ni pamoja na ushirikishwaji wa wanawake na sekta binafsi,” amesema Kamwelwe.
Mkurugenzi wa Miundombinu wa SADC, Mapolao Mokoena amesema mkutano huo utaweza kusaidia uelewa wa watendaji wa Serikali kujua njia ya kupita katika kuifanya jumuiya ifikie malengo yake hasa katika miundombinu.
Mawaziri wa SADC wa Sekta ya TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa wanakutana kwa siku mbili kuanzia leo Septemba 19-20, 2019 jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akiwa na Mkurugenzi wa Miundombinu wa SADC, Mapolao Mokoena (kushoto).
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhandisi Isack Kamwelwe (wa kwanza kushoto) akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (katikati) pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Sekta ya Uchukuzi Bw. Leonard Chamriho.
Mawaziri wa SADC wa Sekta ya TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa wanakutana kwa siku mbili kuanzia leo Septemba 19-20, 2019 jijini Dar es Salaam. Meza kuu.
Meza kuu wakiendelea na majadiliano.
Mawaziri wa SADC wa Sekta ya TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa wakiuliza maswali wakati wa majadiliano.
Majadiliano yakiendelea...
Mawaziri wa SADC wa Sekta ya TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa wanakutana kwa siku mbili kuanzia leo Septemba 19-20, 2019 jijini Dar es Salaam.
Cathbert Kajuna 19:11 (2 hours ago) to amichuzi, othmanmichuzi, me ....TUMIE HII KUNA MAREKEBISHO YA JINA LA WAZIRI MKUU.... WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASISISTIZA MAWAZIRI WA SADC KUSIMAMIA MAENDELEO YA TEKNOLOJIA
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa SADC wa Sekta ya TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa wanakutana kwa siku mbili kuanzia leo Septemba 19-20, 2019 jijini Dar es Salaam. Picha zote na Matokeo Chanya+. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akiwa na Mkurugenzi wa Miundombinu wa SADC, Mapolao Mokoena (kushoto).

JENISTA MHAGAMA AKABIDHI VYETI MAHAFALI YA PILI YA PROGRAMU YA MWANAMKE KIONGOZI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Mahafali ya Tatu ya Programu ya Mwanamke Kiongozi yamefanyika leo kwa Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama  kuwapatia vyeti washiriki 20 waliohitimu mafunzo hayo kutoka kampuni mbalimbali.

Mahafali ya mwaka huu yamebeba  ujumbe unaosema “Mustakabali wa Ajira ya Wanawake kwa Wakati Ujao: Je Sera za Mahali pa Kazi zipo tayari? Na yamekuwa yanaandaliwa na Chama cha Waajiri Nchini (ATE).

Akizungumza na wahitimu wa mafunzo hayo, Jenista amesema  ATE wamekuwa na mchango mkubwa katika kujenga uwezo wa rasilimali watu ambao watashiriki kukuza na kuboresha uchumi wa taifa letu na serikali imejipanga vizuri kuhakikisha tunafanya kazi pamoja kwa kuhakikisha kuwa tunawajengea uwezo vijana ili wapate ujuzi wa aina mbali mbali utakaowawezesha kufikia maendeleo endelevu kuelekea Uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Amesema, kwa moyo wa dhati kabisa anayo furaha kuwapongeza ATE kwa kufanikiwa kuandaa kwa mara ya pili mfululizo Mkutano wa Mwaka wa Uongozi kwa Wanawake na kuzitaka Taasisi mbalimbali za kibiashara na Wadau mbalimbali nchini kuungana ili kuhakikisha programu hii inakuwa endelevu kwa kuwahamasisha wanawake wengi kushiriki mafunzo haya.

Pia, ameupongeza uongozi wa ATE ambao wameshirikiana na Shirikisho la Vyama vya Waajiri Nchini Norway (NHO) pamoja naUN Global Compact Network Tanzania (UNGCN) kwa kuandaa mkutano huu kwa ustadi wa hali ya juu na ninaamini utaleta mafanikio makubwa kwa manufaa ya wanawake wengi wenye ndoto za kuwa viongozi nakupelekea matokeo chanya kwa taifa letu kwa ujumla

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa ATE Jayne Nyimbo amesema Mwaka 2019 ulioambatana na Mahafali ya Tatu ya Programu ya Mwanamke Kiongozi kama ambavyo ulifanya hivi tulipofanya tukio kama hili mwaka uliopita.

Jayne amelishukuru shirika la UN Global Compact Network Tanzania (UNGCN) ambao mwaka huu wameshirikiana kwa pamoja kuandaa tukio hilo na kuhakikisha linafanikiwa kwa ubora wa hali ya juu.

Aidha, Shukrani zao pia zinakwenda kwa wawezeshaji kutoka Chuo cha ESAMI ambao wamekuwa wakishirikina nao katika kutoa mafunzo haya kwa washiriki wote ambao wamehitimu rasmi na kutunukiwa vyeti vyao.

Jayne amezipongeza  kampuni ambazo zimefanikisha kupeleka  wafanyakazi wao katika Awamu ya Tatu ya mafunzo ya programu hiyo yenye lengo la Kuwajengea uwezo wanawake kwa ajili ya kushika nafasi za juu za uongozi na kuwapa Uwezo wa kuingia kwenye Bodi mbalimbali na kushiriki katika kutoa maamuzi yenye tija 

ambapo wanawake kadhaa waliohitimu tayari wamefanikiwa kupata nafasi za juu za
uongozi na pia kuwa wawakilishi kwenye bodi mbalimbali huku mchango wao ukionekana dhahiri.
Mkurugenzu Mtendaji wa ATE Dr Aggrey Mlimuka ameeleza kuwa Kwa kipindi cha toka mwaka jana wamefanikiwa kuanzisha Alumni ya programu  ya Mwanamke Kiongozi kwa malengo ya kutengeneza mtandao thabiti wa wanawake ambao Watashirikiana kutimiza malengo yao ya kushika nafasi za juu za uongozi na kuwa Wakurugenzi wa bodi mbalimbali kwa kushirikishana nafasi hizo, kujadiliana mambo mbalimbali ya uongozi, kuchochea uwepo wa sera zinazoshirikisha wanawake katika uongozi na jinsi ya kuandaa wanawake wengine kwa ajili ya uongozi na pia kuwekeana ufadhili pale unapohitajika kwa ajili ya wao kushika nafasi mbalimbali za uongozi.

Amesema kama Chama cha Waajiri wameandaa na kuhifadhi taarifa zote (data) juu ya wanawake hao waliohitimu toka awamu ya kwanza na kutoa rai kwa makampuni wanachama na wasio wanachama kuwasiliana na nao pindi wanapohitaji wakurugenzi wa bodi kwani programu hii imewajengea uwezo wa kumudu nafasi hizo kwa ufanisi wa hali ya juu.

Zifuatazo ni kampuni mbalimbali ambazo zimeleta wananyakazi wao katika mafunzo haya ni Legal and Human Right Centre ,Equinor Tanzania, Songas Gas Ltd, Social Action Trust Fund (SATF), National Housing Corporation (NHC), Barclays Bank Tanzania, TOL Gases, Grumeti Reserves na  wao wenyewe ATE.
 Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama akizungumza wakati wa mahafali ya  pili ya programu ya mwanamke Kiongozi yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam kwa wanawake 20 kutoka makampuni mbalimbali wakitunukiwa vyeti.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Nchini (ATE) Dr Aggrey Mlimuka akizungumzia programu ya mwanamke wa wakati ujao na kuzitaka makampuni kuwafuata pindi wanapohitaji wakurugenzi kwenye mahafali yaliyofanyika Leo Jijini Dar es Salaam
 Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama akikabidhi vyetu kwa baadhi ya wahitimu wa programu ya mwanamke Kiongozi yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam kwa wanawake 20 kutoka makampuni mbalimbali wakitunukiwa vyeti.
 Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama akikabidhi vyetu kwa baadhi ya wahitimu wa programu ya mwanamke Kiongozi yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam kwa wanawake 20 kutoka makampuni mbalimbali wakitunukiwa vyeti.
 Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama akikabidhi vyetu kwa baadhi ya wahitimu wa programu ya mwanamke Kiongozi yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam kwa wanawake 20 kutoka makampuni mbalimbali wakitunukiwa vyeti.

 Washiriki na Wageni mbalimbali waalikwa wakiwa wanafutuatilia mahafali hayo
Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Jenista Mhagama(katikati) akiwa ameambatana na Mwenyekiti wa Bodi wa Chama cha Waajiri Nchini (ATE) Jayne Nyimbo (Kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa ATE Dr Aggrey Mlimuka (Kushoto) akiwasili kwenye mahafali ya  programu ya mwanamke Kiongozi yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam kwa wanawake 20 kutoka makampuni mbalimbali wakitunukiwa vyeti.

Lazima dhahabu ya mgodi wa serikali iuzwe hapa nchini - Biteko

$
0
0
Na Issa Mtuwa – Biharamulo Kagera. 
Waziri wa Madini Doto Biteko ameagiza mgodi wa dhahabu wa Mistamigold unaomilikiwa na Shirika la madini la Taifa STAMICO kuanzia Mwezi Desemba 2019 dhahabu inayozalishwa mgodini hapo iuzwe kwenye masoko ya dhahabu ya hapa nchini hususani kwenye soko la Biharamulo.
Biteko amesema hayo leo tarehe 19/09/2019 alipotembelea mgodi huo uliopo wilaya ya Biharamulo. Amesema aiwezekani serikali ihimize dhahabu yote iuzwe kwenye masoko ya ndani wakati mgodi wa serikali dhahabu yake inazwa Ususwi.
“Naagia kuanzia Desemba mwaka huu, dhahabu yote inayo zalishwa katika mgodi huu iuzwe kwenye masoko ya ndani, mara baada ya mkataba wenu kuisha mwezi Novemba. Kwa kufanya hivyo gharama isiyo ya lazima mtaiepuka.” amesema Biteko.
Wakati huo huo Biteko amemuagiza Afisa Madini Mkazi mkoa wa Kagera Mhandisi Lucas Mlekwa kuzifuta leseni 159 ambazo haziendelezwi ili zigawiwe kwa wanaohitaji kuendeleza leseni hizo na serikali ipate mapato yake.
Awali, akitoa taarifa ya madini mkoa wa Kagera Mhandisi Mlekwa pamoja na mambo mengine alimwambia Waziri kuwa kuna changamoto nyingi kwenye mkoa wake pamoja na nyingine ni uwepo wa leseni nyingi zisizo endelezwa. 
Ameongeza kuwa kila anapo jaribu kufanya mawasiliano na wamiliki wa leseni hizo ili waendeleze hawapatikani. 
Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa mgodi wa STAMIGOLD  Mhandisi Gray Shamika amemueleza Waziri jinsi mgodi unavyo endeshwa na kwa sasa wanajiendesha wenyewe kwa kugharamia gharama zote ikiwemo kulipa mishara ya watumishi na kulipa wazabuni. Amesema taarifa za kijiolojia zinaonyesha kuwa mgodi bado utaendelea kuishi pamoja na uwepo wa  changamoto mbalimbali zikiwemo za madeni.
Akitoa taarifa yake kwa Waziri Mhandisi Shamika amesema, kwa sasa Mgodi upo kwenye utaratibu kuanzisha mradi wa kuchenjua Visusu (Tailings) mradi utakao upa uhai wa mgodi hadi miaka 7-10 ijayo. Kuhusu kupunguza gharama za uzalishaji Shamika amesema mgodi umepunguza gharama za uzalishaji kutoka 1800 hadi 940 kwa wakia (Ounce) moja.
Kufuatia taarifa hiyo, Waziri Biteko ameupongeza uongozi na wafanyakazi wote kwa hatua hiyo na kuwaomba kuendela kupunguza gharama hiyo angalau kufikia 800 kwa wakia. 
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Brigadia Jenerali Silvester Ghuliko amesema wako teyari kutekeleza maagizo ya Waziri na walisha anza kujipanga kutekeleza maagizo hayo hususani kuanza kuuza dhahabu katika soko la ndani mara baada ya mkataba wa kuuza dhahabu nje kumalizika mwezi Novemba mwaka huu. 
Akimkaribisha Waziri wa Madini, Katibu Tawala wa Wilaya ya Biharamumo ambae ni Kaimu Mkuu wa Wilaya hiyo Agness Alex amemwambia waziri hali halisi ya sekta ya madini wilayani humo pamoja na changamoto mbalimbali ikiwemo deni la Halmashauri yake kwa mgodi huo. 
Kufuatia hoja hiyo ya deni la Halmashauri, Biteko amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Biharamulo Ionde Ng’ahala kutuma timu ya wahasibu wake kwenda STAMIGOLD kukaa na uongozi kupitia deni hilo na kuhakiki na kukubaliana namna ya kulipa deni hilo.
 Waziri wa Madini Doto Biteko wa nne kulia akitembelea eneo la uzalishaji katika mgodi wa STAMIGOLD. Wa tatu kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Biharamumo ambae ni Kaimu Mkuu wa Wilaya Agness Alex na wa pili kulia  ni meneja Mkuu wa Mgodi Mhandisi Gray Shamika.
 Waziri wa Madini Doto Biteko wa tatu kulia akimsikiliza Kamishna wa Tume ya Madini Dkt. Athanas Machiyeki  wakiwa kwenye eneo la Mgodi wa STAMIGOLD.

MADAM RITA AJIVUNIA MIAKA 10 , ASEMA BSS NI KAMA GANDA LA NDIZI

$
0
0
    
   Na.Khadija Seif, Michuzi TV

JAJI Mkuu wa shindano la kusaka vipaji vya kuimba (BSS) Rita paulsen a.k.a Madam Rita amesema bado shindano hilo ni ganda la ndizi kwa vijana wenye nia ya kufikia mbali kwenye sekta muziki.

Madam Rita ameeleza kitu kikubwa hasa kinachomsukuma kila mwaka kuendelea kujitolea kusaidia vijana ni kutokana na wengi wao kuonyesha nia, jitihada na malengo yao kufika mbali na kuwa wasanii wazuri kama wengine au hata kuzidi uwezo wao.

"Wapo wasanii ambao tunajivunia uwepo wapo na tunajitoa kifua mbele kuona ni zao letu la (Bss ) Kama Kala Jeremiah, Mina Atick, Leah Moudy, Jumanne Iddi, Haji, Pascal Cassian ,Walter Chilambo, Kayumba, Frida Amani, Peter msechu ambao wengi tuliwatoa mikoani na kuwafungulia njia ya kuonyesha vipaji vyao kwa watanzania,"


Licha ya kuwepo kwa mafanikio mengi ambayo amepata lakini bado anakumbana na kasumba ya baadhi ya watu kuchukulia shindano hilo kama nguvu ya soda kwa washindi kutosikika kwa kipindi fulani au hata kutoonekana Tena kwenye taswira ya muziki pamoja na kukatishwa tamaa na kupigwa vita kwa baadhi ya watu.

" Shindano hili lipo kwa ajili ya kukusaidia kutafuta mashabiki wa awali ambapo Kama msanii mwenyewe hatoonyesha ujuzi zaidi ya kile wanachokiona mashabiki inakua ni kazi bure kwani naamini ukishikwa mkono na wewe inabidi umpe moyo yule aliekushika.

"Kuna baadhi wapo na wanaendelea na muziki vizuri kutokana na jitihada zao za kupigania kile ambacho wanakiu nacho na wengine hawaendelei pengine kwa sababu tofauti tofauti mtu wa kusimamia kazi zake anakua sio mzoefu,starehe kupita kiasi ameshakua maarufu anajisahau nini anatakiwa kufanya wakati huo"


Pia Madam Rita amesema kwa sasa msimu wa 10 wa Bss umerudi tena kwa kishindo huku majaji wapya wakiwa ni wakongwe kwenye Muziki wa Bongofleva.

"Dullysykse, Lady Jjay Dee  watakuwa nasi pamoja Kama majaji wapya katika msimu huu wa 10 wa shindano hili tutegemee vipaji vingi na vizuri,"

Aidha Rita amefafanua mikoa watakayofika kufanya usahili ni Arusha Septemba 28 hadi 29, Mwanza Oktoba 4 hadi 5 , Mbeya Oktoba 10, Dodoma Oktoba 17 na huku Mkoa wa Dar es salaam ikiwa ni 23, 24 na 25 Oktoba mwaka huu.

"Na vipindi vitaonekana katika King'amuzi cha startimes kupitia  chaneli ya ST Swahili.

TADB NA NMB WATEKELEZA AZMA YA SERIKALI YA KUPANUA HUDUMA BORA ZA KIFEDHA KWA WAKULIMA WADOGO

$
0
0
Benki Ya Maendeleo Ya Kilimo Tanzania (TADB) ikishirikiana na NMB zatimiza azma ya serikali katika kupanua wigo wa huduma za kifedha pamoja na mikopo kwa wakulima wadogo nchini wanaojishughulisha na mazao mbali mbali kama miwa, kahawa, korosho na pamba.

Wakizungumza katika mkutano wa wanahabari uliofanyika jijini Dar es Salaam, mkutano uliokuwa na lengo la kurasimisha mikopo kwa wakulima wapatao 2997 wa zao la korosho  iliyoyolewa hivi karibuni, ambayo iligharimu zaidi ya shilingi Bilioni 9.3.

Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Japhet Justine alisema “tulianzisha huduma ya kutoa dhamana ya mikopo kwa wakulima wadogo ambao wasingeweza kukopesheka kirahisi na mabenki ya biashara. Siku hadi siku huduma hii imeleta mapinduzi makubwa. Kwa kushirikiana na NMB pekee tumetoa jumla ya mikopo Bilioni 14.3 kwa AMCOs 32, zenye wakulima 14310.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa kurasimisha mikopo kwa wakulima wadogo wapatao 2997 wa zao la korosho, iliyofanyika jana jijini Dar es salaam. Mikopo hiyo inatolewa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ikishirikiana na NMB, ambayo inagharimu zaidi ya shilingi Bilioni 9.3. Wengine pichani toka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NMB, Filbert Mponz, Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Japhet Justine pamoja na Meneja Mahusiano na Mawasiliano wa TADB, Chaba Rhuwanya

Akielezea muundo wa huduma ya mikopo ya dhamana Mkurugenzi Mtendaji wa TADB alisema “Ubunifu huu wa mikopo ya dhamana umesaidia mabenki kuwakopesha wakulima wengi  zaidi. Hadi sasa tumekwisha kutoa zaidi ya billion 19.7 kwa mabenki manane ambayo tuna mikataba nao ya gurantee scheme. Lengo letu ni kuongeza mikopo ya kwenye kilimo kutoka 8.7% kama ilivyo sasa hadi kufika 15% kwa miaka mitano ijayo” .

Na kuongeza kuwa benki ya TADB inaamini mfumo wa dhamana utaongeza chachu na kutoa fursa kwa mabenki mengine zaidi kuongeza huduma za mikopo kwa ajili ya kutatua changamoto zilizopo katika kilimo, na kuongeza wigo wa uzalishaji na masoko. 

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe , alifurashishwa na ubunifu mkubwa unaofanywa na benki ya TADB katika kuchachusha maendeleo ya kilimo nchini alisema “TADB ndio benki inayobeba dhamana ya Serikali kukopesha wakulima, ili benki za biashara ziweze kukopesha wakulima wengi zaidi inahitaji taasisi inayoweza kubeba hiyo dhamana na ndio mana TADB chombo muhimu sana kwetu”

Naibu waziri huyo, alitoa wito kwa mabenki nchini kutatua changamoto za uwekezaji katika miundombinu ya mazao ikiwemo upatikanaji wa ghala za kuhifadhia mazao, kuwa iwapo tutaongeza mikopo na kuwajengea uwezo AMCOs wataweza kufufua maghala yao kwa kuyaboresha yakatumika kibiashara. Vile vile Mhe. Bashe alisisitiza mabenki kuangalia namna ya kupunguza gharama za mikopo ikiwemo kutoa riba nafuu.

Nae Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NMB, Ndugu Filbert Mponzi akifunga mkutano huo wa wana habari walisema “tuna Imani kubwa na TADB, ushirikiano wetu umeleta mafanikio mazuri. Ushirikiano huu wa kumuhudumia mkulima umeongeza wigo wa huduma zetu na hadi sasa tumetoa mikopo kwa jumla ya AMCOs 32, zenye wakulima 14310”.

JUKWAA LA FIKRA LA TANO LA ITV& MWANANCHI COMMUNICATION KIZENGA HALL KIJITONYAMA DAR ES SALAAM


Tanzania, Poland zakubaliana kuongeza ushirikiano katika biashara

$
0
0

Serikali ya Tanzania na Serikali ya Poland zimekubaliana kuongeza ushirikiano katika biashara, na kuwataka wafanyabiashara kutoka nchi zote mbili kuchangamkia fursa mbalimbali za biashara.
Makubaliano hayo yalifanyika Jijini Dar es Salaam jana (Septemba 20, 2019) ambapo serikali ya Tanzania iliwakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi ili hali Poland iliwakilishwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Marcin Przydacz.
Akiongea na waandishi wa habari mara baada ya makubaliano hayo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi amesema kuwa lengo la makubaliano hayo ni kukuza ushirikiano uliopo kati ya nchi hizi.
"Kwa sasa, tunashirikiana na Poland katika maeneo kadhaa ikiwa ni pamoja na biashara ambayo takwimu zinaonesha kwamba biashara kati ya Tanzania na Poland zimepanda kutoka milioni 77.7 mwaka 2016 mpaka milioni 124.5 mwaka 2017. Bidhaa za Tanzania zinazouzwa Poland ni pamoja na chai, kahawa na tumbaku. Tanzania inanunua Poland bidhaa mbalimbali kama tairi za magari, vifaa vya maabara na vifaa vya umeme," alisema Prof. Kabudi  
Prof. Kabudi aliongeza kuwa, fursa za biashara baina ya nchi hizi mbili bado ni nyingi na imekubaliwa kuwa balozi zetu na taasisi zingine za Serikali zetu zitumike kuongeza ushirikiano katika biashara. "Kwa hili, tunawaomba wafanyabishara wetu kuchangamkia fursa mbalimbali za biashara," Aliongeza Prof. Kabudi

Kwa mujibu wa Waziri Kabudi, Tanzania na Poland zinashirikiana kwenye miradi mikubwa miwili. Mradi wa kwanza ni wa kiwanda cha kuunganisha trekta, kilichopo Kibaha ambao unatekelezwa kwa mkopo wa riba nafuu kutoka Serikali ya Poland. Kupitia mradi huu, jumla ya trekta 2400 zinaunganishwa nchini kupitia kampuni ya URSUS ya Poland. Tayari trekta 875 zimeshaunganishwa. Mradi huu utaongeza uzalishaji kwenye sekta ya kilimo na kuleta mapinduzi ya kilimo kutoka kutumia jembe la mkono kwenda kutumia trekta.

Mradi mwingine ni ule wa kujenga maghala ya kuhifadhia nafaka ambapo jumla ya maghala 8 yanajengwa katika kanda zote zinazohifadhi chakula nchini. Mradi huu utaongeza uwezo wa Serikali wa kuhifadhi nafaka kutoka tani 250,000 kwa sasa hadi tani 500,000. 

Katika hatua nyingine, tumekubaliana pia kutoa fursa ya elimu ambapo watanzania sasa watapata fursa ya kwenda kusomaPoland ambapo fursa nyingi zitatolewa katika fani ya udaktari wa aina mbalimbali, uhandisi, sayansi, Tehama, kilimo na maeneo mengine. 


Prof. Kabudi aliongeza kuwa, Tanzania imeendelea kuvutia watalii kutoka nchi ya Poland. Kila mwaka, watalii wapatao 12,000 wamekuwa wakitembelea visiwa vya Zanzibar kwa ndege zinazotoka miji mbalimbali ya Poland moja kwa moja mpaka Zanzibar. Idadi ya watalii inaendelea kuongezeka kutoka watalii 12,241 mwaka 2017 hadi watalii 18, 853 mwaka 2018.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland, Marcin Przydacz amesema kuwa Serikali yake itaendelea kuwahimiza Wapoland kuja kuwekeza nchini kwa wingi na hasa kwenye maeneo ya uzalishaji wa dawa, kilimo hususan katika uongezaji wa thamani ya mazao ya kilimo, uzalishaji wa mashine za viwandani na uzalishaji wa bidhaa za viwandani.

Pia, Waziri Przydacz ameahidi kuwa Serikali yake itaendeleea kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano inayooongozwa na Mhe. Rais Magufuli ya kutafuta suluhisho la changamoto ya uhaba wa maji inayokabili wananchi sehemu mbalimbali nchini. 


Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland Mhe. Marcin Przydacz. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na

Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) pamoja na baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland Mhe. Marcin Przydacz (hayupo pichani)

 Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland Mhe. Marcin Przydacz pamoja na ujumbe alioambatana nao wakimsikiliza Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb)(hayupo pichani)
Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland Mhe. Marcin Przydacz wakiwa katika mazungumzo katika Ofisi ndogo za Wizara  ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akimkabidhi zawadi ya picha ya kuchora ya Mlima Kilimanjaro Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland Mhe. Marcin Przydacz mara baada ya mazungumzo rasmi waliyoyafanya kaaika ofisi neogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam.

News Alert: Vigogo wa upinzani Ileje wahamia CCM

$
0
0
Na Daniel Mwambene Ileje
Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa hapa nchini  vigogo wanne wa vyama vya siasa vya upinzani wilayani Ileje vimepoteza majembe yake baada ya kuhamia CCM ili kuijenga Tanzania mpya kama walivyosema.
Waliokabibdhi kadi zao za vyama vya awali kwa Katibu wa CCM Mkoa wa Songwe na kupewa kadi mpya za kijani ni pamoja na Ndg.Pitirosi Mshani aliyekuwa Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Itumba ambayo ni Makao Makuu ya Wilaya ya Ileje.
Wngine ni Ndg.Francis Mbembela aliyegombea udiwani kata ya Isongole 2015 kupitia ACT Wazalendo akitokea CHADEMA ambako aliwahi kuwa kiongozi pia,Eliamu Kibona pia (CHADEMA) alikuwa ni mjumbe wa Serikali ya Kijiji cha Itumba pamoja na mama Dale Kaonga aliyekuwa tishio upande wa wanawake kisiasa akitokea CHADEMA.
Wakizungumza mara baada ya kupokelewa na Katibu wa Mkoa wageni hao waliahidi kukitumikia chamaa hiki na kuhakikisha kinashinda kwa kishindo katika uchaguzi huu.
“Kazi zinazofanywa na Awamu hii haziwezi kupingwa kwa lolote kwani zinalenga kuwakomboa watanzania,yeyote anayepinga matokeo ya kazi hizi atakuwa anapingana na Mungu”Alisema Ndg.Eliamu Kibona.
Akizungumza na wajumbe wa kikao kwenye Ukumbi wa CCM wilayani humo(maarufu kama Kimwaga) Bi.Mecy Moleri aliwataka wanachama wa CCM kuungana na wanachama hao wapya katika kazi mbalimbali za chama ikiwemo mipango ya ushindi katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu.
Naye,Diwani wa Kata ya Itumba Mhe.Mohamed Mwala alifurahia kupokea wageni hao akisema hakika chama kimepata majembe ya kazi.
 Makatibu wa matawi  CCM Wilaya ya Ileje wakifurahia baada ya kuwapokea wageni toka upinzani.
 Wajumbe wa Kikao (makatibu wa matawi) wakisikiliza maneno toka kwa Pitirosi Mshani (hayupo pichani) mara baada ya kupewa nafasi ya kujieleza ambpo alisema amerudi nyumbani baada ya kuwa upinzani tangu 1993.

 Ndugu Francis Mbemebela (kushoto) akisalimiana  na Katibu wa CCM Mkoa wa Songwe Bi.Mecy Morell mara baada ya kupokelewa akitokea ACT wazalendo

Vigogo wa upinzani Ileje walihamia CCM wa kuoka kulia ni Pitirosi Mshani (CHADEMA), Francis Mbembela ACT Wazalendo(aliyevaa tai),Eliamu Kibona(CHADEMA)Na Bi.Dela Kaonga (CHADEMA). Vigogo hao waliohamia CCM hapa wakipokea nasaha toka kwa Mwenyekiti wa  CCM Wilaya Ileje Ndg.Hebron Kibona(hayupo pichani). 

Petrobena East Africa Limited, BASF Tanzania Limited team up to spread pesticides to farmers countrywide

$
0
0
Petrobena East Africa Limited and BASF Tanzania Limited have signed an agreement under which the two companies will cooperate and ensure that pesticides reach peasants countrywide and in time.

Speaking after signing the accord, BASF’s Senior Marketing Officer, East African Zone, Mr. Lincholn Asembo, said Tanzanian smallholder farmers lose their crops to pests for lack of right pesticides or for having no pesticides at all. The agreement between the two firms, he said, would go a long way in solving that problem. 
“We hope this agreement will be a timely catalyst in the nation’s efforts to solve the age-old problem of pesticides countrywide because Petrobena is an important and a longtime stakeholder in promoting Tanzania’s agricultural revolution and has experience and a big distribution network. 
"We are happy to work together to increase agricultural productivity in Tanzania,” Mr. Asembo said. 

He said Tanzania’s agriculture faces multiple challenges that demand clear-cut solutions. 

“One of those challenges is the timely delivery of right pesticides, fertilizers and other farm inputs to farmers. We hope our joint effort will go a long way in solving farmers’ problems and promoting agricultural productivity in this country,” he explained. 

 The agreement was signed after a short training of Petrobena’s field staff in the best ways of using BASF products. The Managing Director of Petrobena East Africa Limited, Mr. Peter Kumalilwa, welcome the agreement, saying his company will be the sole distributor the pesticides and assured farmers of timely pesticides and fertilizers. 

 “We welcome this agreement that enables us to work with this international company in solving problems besetting Tanzania’s agriculture. BASF makes world-class pesticides. If the pesticides will be properly used, they will liberate the farmers from recurrent inadequate harvests,” he said. 

 Mr. Kumalilwa said the joint efforts of the two companies will contribute fittingly to the government’s ambition to increase agricultural productivity and transform smallholders into producers of quality raw materials for local industries and of surplus crops for export. 

 Petrobena East Africa Ltd has demonstration farms where it trains farmers and also distributes fertilizers and other products produced by Yara, a Norwegian multinational corporation.

Kampuni za Petrobena na BASF zaungana kusambaza viuatilifu kwa wakulima nchini

$
0
0
Kampuni ya Petrobena inayosambaza pembejeo za kilimo nchini, imeungana na BASF Tanzania Limited kusambaza n viatilifu na madawa vyenye ubora kwa wakulima ili kuongeza tija katika uzalishaji mazao nchini. 

Kampuni mbili hizo  zimetiliana saini mjini hapa makubaliono ya kuwa na ushirikiano huo baada ya mafunzo kwa maafisa kilimo wa kampuni ya Petrobena juu ya matumizi bora ya madawa ya kilimo yanayotengenezwa na BASF, ambayo ni kampuni ya kimataifa inayotengeneza viatilifu na aina nyingine za madawa ya kilimo. 

 Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya makubaliano hayo, Afisa Mkuu Mauzo wa BASF kanda ya Afrika ya Mashariki, Bw.Lincholn Asembo, ameyaeleza makubaliano hayo kuwa ni chachu katika kuboresha uzalishaji mazao nchini Tanzania. 

 “Kampuni ya PETROBENA imekuwa ni mdau mkubwa katika kuchagiza mapinduzi ya kilimo Tanzania, hivyo ushirikiano huu utasaidia kuinua uzalishaji na kukuza kipato cha wakulima kupitia kilimo,” amesema Bw. Asembo.

 Amesema kilimo nchini Tanzania kimekuwa kikikabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo wadudu waaribifu wa mazao, na kuongeza kuwa viutilifu kutoka BASF vinalenga kuondoa tatizo hilo. “Tunayofuraha kufanya kazi na Petrobena kwani ndio kampuni pekee ambayo itasambaza viuatilifu vyenye ubora wa hali ya juu nchini Tanzania. 

Lengo kubwa la kampuni yetu ni kumwinua mkulima kwa kuongeza tija kwenye kilimo kwa kutumia viuatilifu bora kutoka BASF”, amesema Bw. Asembo 
Ameeleza kuwa kampuni ya PETROBENA inamtandao mkubwa na uzoefu katika usambazaji wa mbolea hivyo haitakuwa ngumu kwao kusambaza viuatilifu ambavyo vitamsaidia mkulima kuongeza tija katika shughuli yake ya kilimo. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya PETROBENA, Bw.Peter Kumalilwa, ameishukuru kampuni ya BASF kwa kukubali kufanyakazi na kampuni yao ili kwa pamoja kushiriki katika kuimarisha mapinduzi ya kilimo nchini. 
 “Tunafuraha kuanza kufanya kazi na kampuni kubwa ya kimataifa ya BASF yenye kutengeneza viuatilifu vyenye viwango vya hali ya juu ambavyo vikitumiwa vizuri vitakuwa ni mkombozi wa mkulima. 

Lengo la serikali sasa hivi ni kuinua tija katika kilimo ili wakulima wauze malighali bora kwa viwanda nchini na ziada isafirishwe nje ili kuliingizia taifa fedha ya kigeni,”amesema Bw.Kumalilwa 


Kwa kuwa Petrobena ndiyo itakuwa msambazaji mkuu wa viatilifu vya BASF nchini na ina uzoefu na weledi wa kuwahudumia wakulima, ameeleza Bw Kumalilwa, basi mkulima atakuwa na uhakika wa kupata mbolea na viuatilifu kwa wakati na pia kupata elimu ya kutumia vitu hivyo. 



 Kampuni ya PETROBENA pamoja na kusambaza pembejeo za kilimo pia hutoa mafunzo kwa wakulima kupitia mashamba darasa ili kukuza uelewa wa wakulima juu ya matumizi sahihi ya pembejeo za kilimo ikiwemo viuatilifu na mbolea kutoka Kampuni ya Yara.

Waziri Mpina awataka wafugaji kuongeza uzalishaji wa maziwa nchini

$
0
0
Waziri wa Mifugo na  Uvuvi Luhaga Mpina amewataka wafugaji kuongeza uzalishaji wa maziwa nchini ili kuchochea uwekezaji katika Tasnia ya Maziwa.

Hayo amesema jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na  waandishi wa habari kuelekea siku ya unywaji maziwa shuleni Duniani itakayoadhimishwa Septemba 25 mwaka huu  mkoani Iringa.

Mpina amesema kuwa ni mikakati ya serikali kuhakikisha kuwa uzalishaji wa maziwa unaongezeka kutoka lita bilioni 2.7 hadi kufika lita bilioni 7 kwa mwaka ifikapo 2020.

Amesema kuwa  malengo ya serikali ifikapo mwaka 2025 kila shule ya msingi iwe na  programu za kunywa maziwa shuleni na kila mtanzania awe anakunywa angalau  lita 100 kwa mwaka.

Kwa sasa kuna shule 25 tu ambazo zinatekeleza Programu ya unywaji maziwa shuleni na  kunufaisha jumla ya wanafunzi16.849 kwenye wilaya za Njombe, Mbeya na Wangingo'mbe.
Programu hizi zinaendeshwa kwa ushirikiano na  Mamlaka za Serikali za Mitaa, Viwanda vya kusindika maziwa, wazazi na wafadhili mbalimbali.

Waziri Mpina ametoa pia rai kwa wananchi kunywa maziwa na bidhaa za maziwa ili kuchochea maendeleo ya Tasnia ya Maziwa.

Maadhimisho ya Siku ya Unywaji Maziwa shuleni yanatarajiwa kufanyika mkoani Iringa uwanja wa Samora. Kauli Mbiu ya Maadhimisho haya ni Glasi moja ya maziwa kila siku kwa afya na  Elimu bora.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Kupanga Mpina akizungumza na waandishi habari kuhusiana maadhimisho ya Siku ya unywaji wa Maziwa yatakayofanyika mkoani Iringa.

Ecobank kuboresha mifumo yake ya Kibenki

$
0
0
ECOBANK Tanzania leo Septemba 20 imetangaza kufanya maboresho ya uendeshaji wa huduma kwa kimfumo wa kiteknolojia ili kuweza kukidhi mahitaji ya wateja na kutoa huduma iliyobora zaidi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkuu wa kitengo cha biashara Ecobank Respige Kimati  amesema kuwa benki hiyo ipo kwenye mchakato wa kuboresha mfumo wake wa kibenki kutoka mfumo wa Flexcube 7 walioutumia kwa miaka saba na kwenda kwenye mfumo bora zaidi wa kiteknolojia wa Flexcube 12.

Amesema kuwa kuanzia Septemba 23 mwaka huu  akaunti namba za wateja zitabadilika kutoka tarakimu 16 hadi tarakimu 10 na wateja watakuwa huru kufanya huduma za kifedha kwa kutumia akaunti namba zao za awali.

Amesema sababu za kubadilisha mfumo huo ni kuongezeka kwa wateja na  mahitaji kutoka kwa wateja yamekuwa mengi na ili kuboresha kiwango katika mifumo hiyo wameona ni vyema wakabadilisha mfumo wa kiteknolojia ili kuweza kutoa huduma bora zaidi kwa wateja.

Aidha amesema kuwa benki hiyo ambayo ni sehemu ya Ecobank group inayowafanya kazi katika nchi  ya zaidi ya 30 Afrika wamebadilisha mfumo huo ili kutoa huduma kieletroniki faafu zaidi bila huduma za kifedha kusumbua, na hatua hiyo isaidia katika kutoa huduma kwa teknolojia  zaidi mahali popote.

Kwa upande wake mmoja wa wateja wanaotumia kutoka benki hiyo  Violet Mfinanga amesema kuwa hatua iliyochukuliwa na benki hiyo ni muhimu sana na wao kama wateja wanaamini itaenda kutatua changamoto katika mifumo ya kifedha .


Violet amezishauri taasisi nyingine kutumia mifumo hiyo kwa kuwa itaokoa muda na kiuchumi itasaidia kurahisisha kufanya miamala mingi ya kifedha kwa muda mfupi.
 Mkuu wa kitengo cha Biashara Ecobank Tanzania Respige Kimati akizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo waliofika kwenye kikao cha kujadili maboresho ya mifumo ya Kibenki ya Ecobank yatakayoanza Septemba 23, 2019 yaliyofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu wa kitengo cha masoko na mawasiliano Ecobank Tanzania, Furaha Sumalu akiwakaribisha wateja waliofika kwenye kikao cha kujadili maboresho ya mifumo ya Kibenki ya benki hiyo yatakayoanza Septemba 23, 2019 kilichofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wateja wakichangia mada pamoja na kuuliza maswali kuhusu maboresho huduma za Ecobank yatakayoanza Septemba 23, 2019  yatakayofanikisha huduma kufanyika kwa haraka na kidijitari utaoanza kutumika Septemba 23, 2019.
Afisa wa Malipo ya kidigitali Ecobank Tanzania, Brown Kessy(kushoto) akijibu maswali ya wateja wa benki hiyo wakati wa kikao kilichowakutanisha wafanyakazi wa Banki hiyo na baadhi ya wateja kujadili maboresho ya mifumo ya Kibenki ya Ecobank yalichofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Serena leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa kitengo cha Biashara Ecobank Tanzania Respige Kimati.
Baadhi ya wateja wa Ecobank pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo wakifuatilia mada

BREAKING NEWS: VIGOGO WA SIMBA WAGONGA MWAMBA KUPATA DHAMANA

$
0
0
Zoezi la aliyekuwa rais wa club ya Simba Evans Aveva na Makamu wake Godfrey Nyange Kaburu limegonga mwamba kufuatia Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kuwasilisha kusudio la kukata rufaa kupinga uamuzi mahakamani hiyo kuondoa mashtaka ya utakatishaji.

Hatua hiyo imekuja wakati washtakiwa hao walipopandishwa mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba kwa ajili ya kukamilisha masharti ya dhamana ili waweze kuachiwa huru.

APANDISHWA KIZIMBANI KWA KUJIFANYA AFISA USALAMA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Mkazi wa Buguruni, Thomas Mgoli (37) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  akikabiliwana na kesi ya Uhujumu Uchumi yenye mashtaka matatu likiwemo la kujifanya Afisa Usalama wa Taifa anayetaka kumsaidia aliyekuwa Rais wa TFF, Jamal Malinzi.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Kelvin Mhina na wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi akisaidiana na wakili wa serikali mwandamizi Wankyo Simon, amedai kuwa, katika shtaka la  kwanza imedaiwa, katika tarehe tofauti kati ya Desemba 1, 2017 na Agosti 2019 katika eneo la Mahabusu ya Keko, huko Temeke, mshtakiwa alijifanya kama Mtumishi wa Umma aliyeajiriwa kitengo cha Usalama wa Taifa (TISS)

Katika shtaka la pili imedaiwa kuwa, kati ya Agusti 17 na 29,2019 katika maeneo tofauti ndani ya jiji la Dare es Salaam,  mshtakiwa kwa njia ya kudangaya alijipatia  Sh. 280,500 kutoka kwa Lucy Ngongoseki kupitia  namba mbili za simu tofauti za mtandao wa Airtel akijifanya kuwa yeye Afisa Usalama kutoka TISS  anayetaka kusaidia kesi namba 213/2017 ya Uhujumu Uchumi inayomkabili Jamal Malinzi katika mahakama ya Kisutu kwa ajili

Aidha katika kosa la   mwisho imedaiwa, siku na mahali hapo, mshtakiwa alijipatia fedha kiasi cha sh 280,500 huku akijua kuwa fedha hizo ni zao la kosa tangulizi  la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu

Hata hivyo,  baada ya kusomewa mashitaka hayo, Hakimu Mhina alisema mahakama  hiyo haina mamlaka ya  kumpatia mshitakiwa dhamana, pia haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya Uhujumu Uchumi hivyo mshtakiwa atakwenda rumande.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa kesi hiyo basdo haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 4, 2019.

Mwesigwa: Malizi alikuwa akiikopesha TFF

$
0
0

Na Zaynab Nyamka, Globu ya Jamii
ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Celestine Mwesigwa ameanza kujitetea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo amedai aliyekuwa rais wa TFF, Jamal Malinzi alikuwa akiikopesha TFF na kwamba hakuhusika kwenye mchakato wa kumtoa aliyekuwa Mkurugenzi mpya wa Fedha na Mipango.

Mwesigwa amekiri kwamba mara ya mwisho Malinzi aliikopesha TFF Sh milioni 15 ili kulipia matangazo ya moja kwa moja ya  mechi ya Serengeti Boys iliyokuwa ikichezwa hapa  nchini kupitia Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

Mwesigwa amedai hayo leo Septemba 20,2019  mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde wakati akijitetea mahakamani hapo.

Akiongozwa na Wakili wake, Richard Rweyongeza, Mwesigwa amedai mkataba wa udhamini ulionesha kuwa michezo inapochezwa ndani ya Tanzania mechi zioneshwe moja kwa moja kwenye chaneli ambazo wananchi wanaweza kuangalia bila kulipia.

Amedai walikuwa hawalipi chochote endapo Azam Pay TV ikionesha mechi hizo lakini wananchi walipaswa kulipia hivyo, walilazimika kuonesha kupitia TBC

Ameendelea kudai kuwa TBC walituomba kuonesha mechi hivyo tuliomba masafa kwa Azam ili kuwapa TBC kurusha matangazo ya moja kwa moja ambao walitukubalia lakini ndani ya saa 24, TBC walituambia hawarushi matangazo bila kulipwa Sh milioni 15," alidai Mwesigwa.

"Wakati wanatuambia tuwalipe akaunti yetu haikuwa na fedha tuliandaa hundi lakini hatukuweza kuwapa TBC kwani haikuwa na fedha. Tulimpigia rais na kutuambia kuwa atatupa fedha ili kuondoa aibu ya taifa."

Amedai walichukua fedha hizo na kupeleka benki ya DTB ndipo mechi hiyo ilirushwa moja kwa moja na kwamba Malinzi ni miongoni mwa wafadhili waliokuwa wakiisaidia TFF kwenye shughuli mbalimbali za timu za taifa.
Amedai Malinzi na wafadhili wengine walikuwa wakilipwa baada ya kupata fedha kwenye mashindano, fedha kutoka kwa wafadhili ambao ni CAF na Shirikisho la Mpira duniani (FIFA) na endapo hali ya kifedha inapokuwa nafuu.

Mwesigwa alidai vyanzo vya mapato vya TFF ni mashindano, ufadhili na udhamini na kwamba CAF na FIFA wanatoa fedha baada ya kupeleka ripoti ya ukaguzi wa fedha ya msimu uliopita.

"Malinzi alikuwa akitupa fedha endapi tutashindwa  kumlipa mkaguzi wa hesabu wa TFF ambaye anachaguliwa na FIFA," alidai.

Mwesigwa amedai aliyekuwa Mkurugenzi wa Fedha na Mipango, Edger Masoud ajira yake ilikoma baada ya kushindwa kufanya kazi vizuri hivyo, walivunja mkataba na TFF kwa kushirikiana na FIFA walifanya mchakato wa kumpata Mkurugenzi mpya hivyo, walitoa matangazo na kupata majina ya watu watatu.

Alidai majina hayo yalipelekwa kamati ya ajira chini ya Mwenyekiti wake Warace Karia wakati huo, ambapo walichambua majina hayo na kumpata Aziza Mwanja.

Mwesigwa pia alidai hawakuhusika katika matumizi mabaya ya madaraka na badala yake walifuata taratibu zilizowekwa na shirikisho hilo.

Mbali na Malinzi na Mwesigwa  washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mhasibu wa TFF, Nsiande Mwanga na Karani Flora Rauya.

Katika kesi  hiyo ya jinai namba 213 ya mwaka 2017 washitakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka 20 yakiwamo ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa fedha wa Dola za Marekani 173,335

WAZIRI KALEMANI AKUTANA NA WAZALISHAJI BINAFSI WA UMEME NCHINI

$
0
0

Na Veronica Simba – Dar es Salaam
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani, amekutana na wazalishaji binafsi wa umeme nchini na kujadiliana masuala mbalimbali ya kuboresha zaidi sekta hiyo, ikiwa ni mwendelezo wa kutekeleza kwa vitendo azma ya serikali kutambua mchango wao na kuwawezesha.
Mkutano huo ulifanyika Septemba 19 jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa pia na Naibu Waziri Subira Mgalu, Katibu Mkuu Dkt Hamisi Mwinyimvua, Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu Mhandisi Leonard Masanja, viongozi pamoja na wataalamu wengine mbalimbali kutoka wizarani na taasisi zilizo chini yake.
Akifungua mkutano huo, Waziri Kalemani alisema serikali itaendelea kutambua na kuthamini mchango wa wazalishaji hao wa umeme na itaendelea kuwajengea mazingira wezeshi ili wakue na kuzalisha zaidi kusudi lengo la kufikia uchumi wa kati na wa viwanda liweze kufikiwa.
“Nishati ndiyo injini ya uchumi wa viwanda. Pasipo umeme wa uhakika na wa kutosha, hakuna viwanda. Hivyo basi, pamoja na serikali kuanzisha na kutekeleza miradi mikubwa ya umeme, tungali tunahitaji mchango wenu pia ili tuzalishe umeme wa kutosha kwa ajili ya viwanda na matumizi mengine nchini.”
Aidha, akifunga mkutano husika, Waziri alitaja mambo kadhaa muhimu yatakayozinufaisha pande zote mbili, serikali na wawekezaji kwa kuzingatia manufaa ya wananchi na taifa kwa ujumla.
Aliwataka wadau wa sekta hiyo kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Baraza la Mazingira la Taifa (NEMC) na wengineo, kupitia upya masharti ya utoaji leseni na kuyaboresha ili kuwajengea wawekezaji mazingira rafiki zaidi ya uwekezaji lakini pasipo kukiuka sheria.
Vilevile, Waziri alielekeza kuwa taasisi zinazohusika na utoaji vibali, ziache tabia ya urasimu wa kutumia muda mrefu katika kushughulikia barua za mapendekezo kutoka kwa wawekezaji. Alitaka uwepo utaratibu wa kujibu barua hizo ndani ya kipindi cha mwezi mmoja lakini kwa kuzingatia sheria.
Aidha, alitoa maelekezo kwa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), kutangaza utaratibu wa upatikanaji ruzuku inayotolewa na serikali kwa wawekezaji hao na kuwashindanisha waombaji kwa uwazi kulingana na sifa zao ili kuepusha upendeleo.
Waziri pia alielekeza kwamba maeneo yote mahsusi ya uwekezaji katika sekta ya umeme jadidifu yabainishwe na kuwekwa wazi, ili watu wayajue na kwenda kuwekeza.
Kuhusu suala la gharama za umeme, Waziri alielekeza kuwa inapaswa bei zinazotolewa na wawekezaji binafsi ziwiane na za serikali ili kuwawezesha wananchi wote kunufaika na huduma hiyo pasipo malalamiko kuwa wengine wanapendelewa. “Mathalani, gharama iliyowekwa na serikali kuunganisha umeme kwa wananchi vijijini ni shilingi 27,000 tu; nanyi inabidi mjipange ili mtoze bei inayowiana na hiyo,” alisisitiza.
Kwa upande wake, Naibu Waziri Mgalu aliunga mkono yale yote yaliyoelekezwa na Waziri na akatilia mkazo kuwa taasisi za REA na TANESCO zihakikishe zinaweka utaratibu wa kufanya mapitio ya miradi mbalimbali ya umeme jadidifu inayotekelezwa nchini, hususan katika maeneo ambayo hayafikiwi na gridi ya taifa,  ili kujiridhisha na maendeleo yake.
Naye Juma Shamte ambaye ni Mwakilishi wa wanachama wa Umoja wa Wazalishaji Binafsi wa Umeme Tanzania (Tanzania Independent Power Producers Association – TIPPA), alimshukuru Waziri Kalemani na serikali kwa ujumla kwa jitihada ambazo zimekuwa zikifanyika katika kutambua mchango wao na kuendelea kuwajengea mazingira wezeshi ya uwekezaji.
Awali, ilielezwa kuwa hadi sasa, idadi ya wanachama hai waliojiandikisha na kutambulika rasmi na serikali kama wazalishaji binafsi wa umeme nchini, inafikia 110 na kwamba kiasi cha umeme wanachozalisha kinafikia megawati 18 ambapo huingizwa kwenye gridi ya taifa na kiasi kingine hutumika kuhudumia wateja moja kwa moja.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akiongoza kikao baina yake na wazalishaji binafsi wa umeme nchini, jana Septemba 19, 2019 jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu na kulia kwake ni Katibu Mkuu Dkt Hamisi Mwinyimvua.
 Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu, akizungumza wakati wa mkutano wa Waziri wa Nishati na wawekezaji binafsi wa umeme (hawapo pichani), uliofanyika Dar es Salaam, Septemba 19, 2019.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Dkt Hamisi Miwnyimvua akizungumza wakati wa mkutano wa Waziri wa Nishati (kulia) na wawekezaji binafsi wa umeme (hawapo pichani), uliofanyika Dar es Salaam, Septemba 19, 2019.
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (katikati), akiongoza kikao baina yake na wazalishaji binafsi wa umeme, kilichofanyika Septemba 19, 2019 jijini Dar es Salaam.
 Mwakilishi wa wanachama wa Umoja wa Wazalishaji Binafsi wa Umeme Tanzania (Tanzania Independent Power Producers Association – TIPPA), Juma Shamte akizungumza wakati wa mkutano wa Waziri wa Nishati na wawekezaji binafsi wa umeme (hawapo pichani), uliofanyika Dar es Salaam, Septemba 19, 2019.
 Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Leonard Masanja akizungumza wakati wa mkutano wa Waziri wa Nishati na wawekezaji binafsi wa umeme uliofanyika Dar es Salaam, Septemba 19, 2019.
 Kutoka kushoto ni Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu Mhandisi Leonard Masanja, Kamishna Msaidizi wa Nishati Jadidifu Edward Ishengoma na Kamishna Msaidizi wa Umeme Mhandisi Innocent Luoga, wakifuatilia mkutano wa Waziri wa Nishati na wawekezaji binafsi wa umeme uliofanyika Dar es Salaam, Septemba 19, 2019.
 Sehemu ya wataalamu kutoka wizarani wakifuatilia mkutano wa Waziri wa Nishati na wawekezaji binafsi wa umeme uliofanyika Dar es Salaam, Septemba 19, 2019.

Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (katikati), Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu (kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Dkt Hamisi Mwinyimvua (kushoto), wakifuatilia hoja zilizokuwa zikiwasilishwa na wawekezaji binafsi wa umeme (hawapo pichani) wakati wa kikao baina yao (wawekezaji) na Waziri kilichofanyika Septemba 19, 2019 jijini Dar es Salaam.

VODACOM TANZANIA YAFANYA MKUTANO WA MWAKA WA WANAHISA WAKE JIJINI DAR

$
0
0
 

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Vodacom Tanzania Plc, Bw. Ali Mufuruki (katikati) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa mwaka wa wanahisa wa Vodacom uliofanyika jijini Dar Es Salaam leo. Wengine pichani ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Hisham Hendi (kushoto) na Mkurugenzi wa Fedha Jacques Marais.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Vodacom Tanzania Plc, Hisham Hendi akibadilishana mawazo na Mkurugenzi, Bi. Margaret Ikongo kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa wanahisa wa Vodacom Tanzania Plc uliofanyika leo jijini Dar Es Salaam

 Sehemu ya wanahisa waliojitokeza kwenye mkutano wa mwaka wa Vodacom Tanzania Plc uliofanyika jijini Dar Es Salaam leo.


Mkuu wa Mipango na Uwekezaji wa Vodacom Tanzania Plc, Hilda Bujiku akizungumza na wanahisa waliohudhuria mkutano mkuu wa mwaka wa wanahisa wa Vodacom Tanzania jijini Dar Es Salaam leo.

DKT. CHEGENI AONGOZA MAZUNGUMZO NA CHAMA CHA WABUNGE CHA KUPAMBANA NA MALARIA CHA UINGEREZA NA UJERUMANI JIJINI DODOMA

$
0
0

 Katibu wa Chama cha Wabunge cha Kupambana na Malaria na Magonjwa yaliyokuwa hayapewi Kipaumbele Tanzania (TAPAMA) ambae alimuwakilisha Spika Ndugai, Mhe. Dkt. Raphael Chegeni (Kushoto) akiongozana na Kiongozi wa msafara wa Chama cha Wabunge kutoka Uingereza na Ujerumani, Ndg. Jeremy Lefroy baada ya kutembelea Ukumbi wa Bunge Bungeni Jijini Dodoma. 
 

 Katibu wa Chama cha Wabunge cha Kupambana na Malaria na Magonjwa yaliyokuwa hayapewi Kipaumbele Tanzania (TAPAMA), Mhe. Dkt. Raphael Chegeni akizungumza na Wabunge kutoka Chama cha Wabunge cha Kupambana na Malaria na Magonjwa yaliyokuwa hayapewi Kipaumbele Tanzania (TAPAMA) na Chama cha Wabunge kutoka Uingereza na Ujerumani katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma. Dkt. Chegeni alimuwakilisha Spika Ndugai katika mazungumzo hayo
 Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge cha Kupambana na Malaria na Magonjwa yaliyokuwa hayapewi Kipaumbele Tanzania (TAPAMA), Mhe. Riziki Lulida akizungumza jambo wakati wa kikao cha hicho na Chama cha Wabunge kutoka Uingereza na Ujerumani katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
 Mbunge kutoka Uingereza, Mhe. Dkt. Paul William akizungumza jambo wakati wa mazungumzo ya Chama cha Wabunge cha Kupambana na Malaria na Magonjwa yaliyokuwa hayapewi Kipaumbele Tanzania na Chama cha Wabunge kutoka Uingereza na Ujerumani katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
Katibu wa Chama cha Wabunge cha Kupambana na Malaria na Magonjwa yaliyokuwa hayapewi Kipaumbele Tanzania (TAPAMA), Mhe. Dkt. Raphael Chegeni (kulia) akipokea zawadi ya kikombe kwa niaba ya Spika Ndugai kutoka kwa Kiongozi wa msafara wa Chama cha Wabunge kutoka Uingereza na Ujerumani, Ndg. Jeremy Lefroy baada ya kutembelea Ukumbi wa Bunge Bungeni Jijini Dodoma. 

 Katibu wa Chama cha Wabunge cha Kupambana na Malaria na Magonjwa yaliyokuwa hayapewi Kipaumbele Tanzania (TAPAMA), Mhe. Dkt. Raphael Chegeni (mbele wanne kulia) katika picha ya pamoja na Wabunge kutoka Chama cha Wabunge cha Kupambana na Malaria na Magonjwa yaliyokuwa hayapewi Kipaumbele Tanzania (TAPAMA) na Chama cha Wabunge kutoka Uingereza na Ujerumani katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma. (PICHA NA OFISI YA BUNGE)
Viewing all 110175 articles
Browse latest View live




Latest Images