Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

KAMPENI YA MNADA KWA MNADA YA TCRA YAWAFIKIA WAKAZI WA TABORA

$
0
0
WAKATI wa Mkoa wa Tabora na viunga vyake wamejitokeza kwa wingi katika kampeni ya Mnada kwa Mnada ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Kampuni ya simu, Jeshi la Polisi Kitengo cha Uhalifu Mitandaoni na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Idara ya Uhamiaji kwa ajili ya utoaji wa huduma za usajili wa laini za simu kwa kutumia vitambulisho vya kitaifa na kuhakikiwa na kampuni za simu kwa kuweka alama za vidole kwa laini za simu.

Kampeni tangu imeanzishwa imekwenda katika Mikoa 15 lengo kuu ni nchi nzima kufiwa na Kampeni hiyo.

Mwakilishi wa Mkuu wa Kanda ya Kati wa TCRA Joseph Kavishe amesema ni fursa kwa wananchi wa Mkoa wa Tabora katika Uwanja wa Chipukizi na viunga vyake kupata huduma kutokana na kuwa na mnyororo wadau wa mawasiliano. 

Kavishe amesema kuwa Mnada kwa Mnada TCRA ilianzisha ili kutoa fursa ya Wananchi kuhudumiwa hasa wakati huu usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.

Aidha amesema Kampeni hiyo ni kuimarisha ulinzi katika mawasiliano ya simu pamoja kufanya mawasiliano kuwa salama katika nchi.

Amesema kuwa kampeni ya Mnada kwa Mnada ni kwa ajili ya kutoa elimu ya mawasiliano kwa kushirikiana na wadau katika kujibu changamoto wanazokutanazo katika utumiaji wa mawasiliano nchini.

Kavishe amesema kuwa wananchi wasio kuwa na Vitambulisho vya NIDA wahakikishe wanapata katika usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole na huduma nyinginezo za Mawasiliano hayo.

Amesema kuna watu wengine wanatumia mawasiliano ya simu bila kujua ambapo Jeshi Polisi lipo katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ili kuwaelewesha makosa ya jinai ya matumizi ya simu.

Aidha amesema Kampeni hiyo ni endelevu katika kuwafikia ikiwa kuhakikisha kila mwananchi anajisajili laini yake kwa alama za vidole kwa kutumia kitambulisho cha taifa cha NIDA.

Kavishe amesema kuwa TCRA iko kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi ili mtumie Mawasiliano kwa usalama kutokana na elimu tunayotoa.

Hata hivyo amesema kuwa wananchi wajitokeze katika kujisajili kwa alama za vidole kabla ya Desemba 31.

"TCRA tumejidhatiti katika kuwafikia wananchi katika utoaji wa elimu za utumiaji wa bidhaa za mawasiliano kwa kutatua changamoto katika huduma hiyo" amesema Kavishe.

 Wananchi wakiwa katika foleni ya kusajili ili kupata vitambulisho vya Taifa na kuweza kusajil laini kwa alama za vidole.



Wananchi katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada Mkoani Tabora.

TADB yakutana na Wadau wa Pamba na Kahawa mkoani Simiyu

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya maendeleo ya Kilimo (TADB), Japhet Justine akielekeza jambo wakati wa mkutano na Wadau wa Pamba na Kahawa mkoani Simiyu katika kubadilishana uzoefu. 

Benki Ya Maendeleo Ya Kilimo (TADB) yakutana na Wadau wa Pamba na Kahawa mkoani Simiyu katika kubadilishana uzoefu. TADB, inayochagiza maendeleo ya kilimo nchini Tanzania imepata fursa ya kushiriki katika majadialiano juu ya fursa mbalimbali zilizopo katika mazao ya pamba na kahawa na mkakati uliopo katika kuendeleza mazao hayo. Majadaliano hayo yaliyofanyika mkoani Simiyu yakihusisha wadau mbalimbali ikiwemo serikali na pamoja na wadau wa maendeleo yaani shirika la Huduma za Kifedha (FSDT) na Gatsby Foundation wakiwa waandalizi wakuu katika majadiliano hayo.

Mkoa wa Simiyu, ni mojawapo ya mikoa yenye fursa nyingi za kuwekeza pamoja na ari yake ya kuleta maendeleo makubwa mkoani humo, Aidha Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka ameeleza kuwa ‘’Simiyu ina rasilimali nyingi ikiwemo mifugo ya ng’ombe zaidi ya milioni 1.2 na wakazi zaidi ya milioni 1.7 ambao wengi wao wanajishughulisha na kilimo cha pamba, hivyo angependa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo benki ya maendeleo ya kilimo katika kusukuma ajenda hii ya maendeleo mkoani Simiyu na kuona kuwa wakulima wanafaidika kilimo hicho. Kwa maana mapinduzi ya uchumi wa viwanda yanaenda moja kwa moja na maendeleo kaika sekta ya kilimo, kwa kuwa malighafi nyingi zinatoka katika sekta hiyo’’
Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya maendeleo ya Kilimo, Japhet Justine alieleza namna ambavyo benki ya maendeleo ya kilimo ina mkakati ambao umelenga kufanya mapinduzi makubwa ya zao la pamba na kuwawezesha wakulima wa chini wa pamba na kahawa pamoja na vyama vya ushirika (AMCOS) kuhakikisha kuwa wananufaika na kilimo cha pamba na na kuendelea kumiliki thamani ya zao mpaka linapofika kwa mlaji. 

Na sio tu kukusanya mazao kupitia vyama vya msingi na kuuza siku ya kwanza, bali kuanza kufungua mnyororo wa thamini na kushiriki kwenye fursa mbali mbali kabla ya kufikia ngazi kubwa ya masoko. Kwa mwaka 2017 pekee uzalishaji wa pamba ulikuwa tani 120,000, wakati kwa mwaka 2018 uzalishaji uliongezeka hadi Zaidi ya 220,000.  

Benki ya maendeleo ya kilimo kupitia Mkurugenzi Mtendaji wake ilishauriana na wataalam wa zao la pamba haswa pendekezo la kufanya mabadiliko ya pamoja ya kuongeza thamani katika hatua za awali katika chama cha msingi au chama kikuu kwa kuwezesha upatikanaji wa viwanda vya kutofautisha kati ya pamba nyuzi na pamba mbegu katika ngazi ya ushirika. Mabadiliko haya yataongeza tija kwa mkulima na pia kuongeza ajira na pia kubadilisha taswira ya ushirika. Akiongeza bwana Japhet Justine amependekeza Vyama Vya Msingi na Vyama Vikuu vibadilike na kujiendesha kifaida na isiwe kuajiri ya kukusanya mazao pekee. Tunaamini mpango huu ni endelevu kwa maendeleo ya wakulima wote, AMCOS na sekta nzima ya kilimo. 
Akiongelea zao la Kahawa, TADB imefanya mapinduzi makubwa mkoani Kagera. “Tuliweka Bilioni 23 Mwaka 2018 kuwezesha malipo ya awali kwa wakulima zaidi ya laki moja na elfu arobaini na mbili (242,000) na pia tumefanikiwa kufufua viwanda vidogo vya kukoboa kahawa na kuajiri zaidi ya wafanyakazi 5,200. Wakati huo huo tuliweka tena bilioni 7.1 kama sehemu ya kufufua vyama hivi vikuu vya ushirika. 

Mpaka sasa tunaweza kusema mwaka 2019, kama benki ya maendeleo ya kilimo ilivyoweza kuwekeza mkoani Kagera katika zao la kahawa kwa kutumia mfumo huu wa kuziwezesha AMCOS tatu tu na kuzipa sapoti ya uendeshaji na ushauri zaidi wa masoko ili waweze kufaidika na zao lao na kwa kushirikiana na mfumo jumuishi, leo hii wakulima wengi wanafaidika na zaidi ya watu 5000 wameajiriwa wakiwemo zaidi ya wanawake 1000. 

Benki ya maendeleo ya maendelo ya kilimo inawekeza kilimo kuanzia ngazi ya chini na kuwezesha mnyororo wa thamani ya mazao kupitia huduma za mbalimbali za kifedha. 

SERIKALI YAONGEZA BEI YA KUNUNUA MAHINDI

$
0
0
Songea: MKOA wa Ruvuma una ziada ya  chakula tani  zipatazo 269,000  zilizo zalishwa katika msimu wa kilimo  2019 katika maghala yake, huku  pato la mwananchi katika mkoa huo likipanda kutoka shilingi ml 2.1  mwaka 2015 hadi kufikia ml 2,240,000. mwaka 2019 kwa mwaka.

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wik,i wakati akiongea na waandishi wa Habari alipotembelea kituo cha ununuzi wa mahindi cha  wakala wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula NFRA Kanda ya Songea kilichopo eneo la Ruhuwiko mjini Songea.

Alisema, mafanikio hayo yametokana na juhudi kubwa za uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara unaofanywa na wakulima wa mkoa huo ambao wamekuwa wanatumia fursa za kuwepo kwa Ardhi nzuri na mvua zinazo nyesha kwa wingi kuzalisha mazao mashambani.

Aidha Mkuu wa Mkoa, ametangaza rasmi bei mpya ya mahindi kutoka shilingi 430 hadi 600 kwa kilo na kuwataka wakulima kupeleka mahindi yao kwa NFRA ili kupata bei nzuri, badala ya kuuza kwa wafanya biashara wengine ambao wananunua kwa bei isiolingana na gharama halisi ya uzalishaji.

Mndeme, amemshukuru Rais Dkt John Magufuri na Serikali yake kwa uamuzi wa kuongeza bei ya mahindi kwa wakulima wa mkoa huo kutokana na kutambua thamani ya  kazi zao na pia  itaongeza hamasa ya uzalishaji wa  mazao ya chakula na biashara.
Pia Mndeme alieleza kuwa,Serikali imeongeza mgao wa mahindi Wakala wa Taifa wa hifadhi ya chakula kutoka tani 13,000 mwaka 2018 hadi kufikia tani 25,000  katika msimu 2019  na  uamuzi huo unatokana na serikali kutambua na kuthamini kazi zinazo fanywa na wakulima wa mkoa huo.

Katika hatua nyingine Mkuu wa mkoa alisema, Serikali imeanza  kujenga vihenge na maghala mapya ambayo yatatumika kuhifadhi na kuongeza thamani ya mazao nakutoa wito kwa watu wenye uhitaji wa chakula kwenda Ruvuma kununua mahindi.

Pia alisema, jumla ya watu 600 wamepata vibarua  vya muda na kudumu katika kituo cha wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula wanaofanya kazi mbalimbali, hivyo NFRA imesaidia sana kupunguza tatizo la ajira kwa wananchi wa mkoa wa Ruvuma.

Amewataka wananchi waliobahatika kupata nafasi hizo,kufanya kazi kwa  kujituma na kujiepusha na vitendo vinavyoweza kuharibu mchakato  wa ununuzi wa mahindi, kwani uwepo wa kituo cha kununulia mahindi cha NFRA umesaidia kupunguza ukali wa maisha kwa jamii ya watu wa Ruvuma.

Kwa upande wake,kaimu meneja wa wakala wa Taifa wa hifadhi ya chakula NFRA kanda ya Songea Eva Michael alisema, hadi sasa NFRA imenunua tani 12,000 za mahindi na wanaendelea kupokea mahindi kutoka sehemu mbalimbali ndani ya Mkoa wa Ruvuma.

Alisema, zoezi la ununuzi wa mahindi linafanyika kwa ubora wa hali ya juu ili kupata mahindi safi ambayo yatakidhi vigezo na kuwataka wakulima kupeleka mahindi kwa wingi  kwa NFRA ambao ndiyo wakombozi wa mkulima katika mkoa huo.

Baadhi ya wakulima waliokutwa wakiuza mahindi yao katika kituo hicho,wameishukuru Serikali kwa uamuzi wa kuongeza bei ya mahindi,hata hivyo wameiomba  kudhibiti uuzaji holela wa pembejeo hasa mbolea ambazo zinauzwa kwa bei kubwa.

Rose Mbonde alisema,wakulima wamekuwa wakitekeleza maagizo mbalimbali yanayotolewa na Serikali yao, hata hivyo wengine wanashindwa kulima kutokana na changamoto kubwa ya kupanda kwa pembejeo ambazo zinauzwa kwa bei  ya juu  jambo linalo wakatisha tamaa baadhi ya wakulima.

Michela Hyera, ameiomba Serikali kituo cha Ruhuwiko kiwe cha kwanza  cha kuuzia mahindi kwani kunamazingira mazuri ya wakulima kuleta mahindi yao ikilinganisha na vijijini.

BREAKING NEWS: AVEVA, KABURU KUPEWA DHAMANA

$
0
0
ALIYEKUWA Rais wa Simba Evance Aveva na makamu wake  Nyange Kaburu wamekutwa hawana kesi ya kujibu katika kesi ya  utakatishaji.

Wawili hao walikuwa wanatuhumiwa kwa makosa ya utakatishaji ila upande wa mashtaka umeondoa shtaka hilo na sasa watapatiwa dhamana.

Mamia ya watu wajitokeza kupata mafunzo ya uwekezaji soko la Hisa yanayotolewa kupitia Vodacom

$
0
0



Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar Es Salaam (DSE), Moremi Marwa akizungumza na wanahisa waliojitokeza kupata mafunzo ya uwekezaji kwenye soko la Hisa yaliyotolewa kupitia Vodacom. Mafunzo yalifanyika jijini Dar Es Salaam leo.
Sehemu ya wanahisa waliojitokeza kwenye mafunzo ya uwekezaji kwenye soko la Hisa yaliyolewa na Vodacom, mafunzo yalifanyika jijini Dar Es Salaam leo.

RAIS DKT.SHEIN AKUTANA NA RAIS WA MUUNGANO WA VISIWA VYA COMMORO

$
0
0
Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
ZANZIBAR na Comoro zimeahidi kuendeleza uhusiano na ushirikiano wa kidugu na kihistoria uliopo ambao una lengo la kuzidisha mashirikiano katika sekta za maendeleo kwa manufaa ya pande mbili hizo.

Ahadi hiyo imetolewa leo katika mazungumzo kati ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein alipofanya mazungumzo na Rais wa Comoro Azali Assoumani ambaye yupo Zanzibar kwa mapumziko.

Katika mazungumzo yao viongozi hao kwa pamoja waliahidi kuendeleza uhusiano na ushirikiano wa kihistoria  baina ya pande mbili hizo ambao umeimarika kwa muda mrefu na kuleta manufaa kwa nchi na wananchi wake ambao wana udugu wa damu.

Viongozi hao walieleza kuwa licha ya kuwa ni majirani lakini pia, ni ndugu wa damu hivyo, kuna haja ya kuendeleza uhusiano na ushirikiano wao uliopo kwa manufaa ya nchi zao hasa katika kuendeleza sekta za maendeleo kwa mashirikiano ya pamoja.

Akizungumza kwa upande wake Rais Dk. Shein alimueleza Rais Azali Assoumani kuwa Zanzibar inathamini sana uhusiano huo na ushirikiano uliopo sambamba na kuendeleza Mkataba wa Makubalino uliosainiwa mwaka 2014 na pande mbili hizo kwa lengo la kukuza udugu uliopo.

Rais Dk. Shein alisema kuwa katika Mkataba huo wa Makubaliano masuala mbali mbali yalitiliwa nguvu yakiwemo mashirikiano katika sekta ya afya, elimu, mila na utamaduni pamoja na masuala mengineyo ambayo tayari yameshaanza kufanyiwa kazi na kuleta tija.

Alieleza kuwa mbali ya uhusiano wa kimaendeleo kati ya pande mbili hizo pia, Zanzibar na Comoro zina historia katika kukuza mila na tamaduni sambamba na mafunzo hasa katika elimu ya dini ya Kiislamu ambapo historia inaonesha kwamba wananchi wa Comoro walio wengi wamepata elimu ya dini ya Kiislamu hapa Zanzibar.

Akitolea mfano maelezo hayo, Rais Dk. Shein alisema kuwa miongoni mwa Masheikhe wakuu wa Comoro  akiwemo Marehemu Sheikh Mwinyi Baraka walipata elimu yao ya dini hapa Zanzibar na hatimae kuwa balozi mzuri wa kuitangaza Zanzibar katika uhai wake hadi kufariki kwake mwaka 1988.

Kutokana na umuhimu huo Rais Dk. Shein alieleza hatua alizozichukua katika kuhakikisha katika ziara yake aliyoifanya nchini humo mwaka huo wa 2014 alipata fursa ya kulizuru kaburi la Sheikh Mwinyi Baraka ambaye alikuwa ni mwanachuoni mashuhuri.

Katika kuhakikisha Mkataba wa Makubaliano hayo yaliosainiwa katika ziara ya Rais Dk. Shein nchini Comoro mnamo mwezi Septemba mwaka 2014 yanafanyiwa kazi Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kilitiliana saini Mkataba wa Makubaliano juu ya mashiriikiano na Chuo Kikuu cha Comoro mnamo Januari 19 mwaka 2016.

Aidha, katika mazungumzo hayo, Rais Dk. Shein alieleza juhudi zinazoendelea kuchukuliwa katika kuhakikisha Mkataba huo wa Makubaliano unatekelezwa vyema ikiwa ni pamoja na kufundishwa kwa lugha ya Kiswahili nchini Comoro sambamba na kuwepo kwa kubadilishana uzoefu na utaalamu kati ya Chuo Kikuu cha Comoro na Chuo Kikuu cha (SUZA).

Rais Dk. Shein aliongeza kuwa makubaliano hayo pia, yanaeleza jinsi Chuo Kikuu cha Comoro kitakavyoshirikiana na (SUZA) katika kutoa mafunzo ya lugha ya Kifaransa.

Sambamba na hayo, Rais Dk. Shein alimpongeza Rais Azali Assoumani kwa uwamuzi wake wa kuja kupumzika Zanzibar, na kumueleza kuwa Zanzibar ni salama. “Karibu sana Zanzibar jisikie uko nyumbani kwani Zanzibar ni sehemu salama ya kupumzika”,alisisitiza Dk. Shein.

Nae Rais wa Muungano wa Visiwa vya Comoro Azali Assoumani alimpongenza Rais Dk. Shein kwa kumkaribisha vizuri Zanzibar jambo ambalo alisema huo ni utamaduni uliojengeka kwa watu wa pande mbili hizo ukiwa ni urithi wa Waasisi wao.

Rais Assoumani alimueleza Rais Dk. Shein kuwa Comoro na Zanzibar zina mambo mengi ya kushirikiana licha ya yale yaliotiwa saini ambayo tayari yameshaanza kutekelezwa na kuanza kuleta manufaa.

Alieleza kuwa wananchi wa Comoro wanafarajika na uhusiano na ushirikiano mwema uliopo kati yao na ndugu zao wa Zanzibar hasa ikizingatiwa kwamba wapo Wakomoro waliozaliwa Zanzibar wananchi Comoro na wale waliozaliwa Comoro ambao wanaishi Zanzibar.

Rais Assoumani alieleza kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwemo Zanzibar ina mambo mengi ya kushirikiana hasa ikizingatiwa ukaribu na udugu uliopo baina ya pande mbili hizo na kueleza kuwa kuchaguliwa kwa Rais John Pombe Magufuli kuwa Mwenyekiti mpya wa (SADC) kutazidi kujenga mustakbali mwema wa nchi mbili hizo.

“Sisi ni ndugu wa damu hivyo, kuna haja ya kufanya kazi kwa pamoja”,alisema Rais Assoumani na kusisitiza kuyafanyia kazi yale yote yaliotiwa saini katika Mkataba wa Makubaliano kati ya Zanzibar na Comoro mnamo mwaka 2014.

Katika maelezo yake, Rais Azali Assoumani alimuhakikishia Rais Dk. Shein kuwa nchi yake pamoja na wananchi anaowaongoza wataendelea kuthamini udugu wa kihistoria uliopo na kuzidisha uhusiano na ushirikiano wao.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na mgeni wake Rais wa Muungano wa Visiwa vya Comoro Mhe. Azali Assoumani wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa ajili ya kusalimiana leo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na mgeni wake Rais wa Muungano wa Visiwa vya Comoro Mhe. Azali Assoumani wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kwa ajili ya kusalimiana
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akifuatana na mgeni wake Rais wa Muungano wa Visiwa vya Comoro Mhe. Azali Assoumani baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika leo alipofika Ikulu Mjini Zanzibar .(Picha na Ikulu) 

DC Katambi ampongeza Rais Magufuli kwa kutekeleza ilani ya CCM ndani ya muda mfupi

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe Patrobas Katambi akiwa na viongozi wa Kamati ya Siasa ya Wilaya hiyo sambamba na watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo.

Charles James, Michuzi TV

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe Patrobas Katambi amemshukuru Rais Dk John Magufuli kwa namna alivyotekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi ndani ya kipindi kifupi. 

DC Katambi amesema Rais Magufuli amefanya mambo makubwa kwenye afya, elimu, miundombinu na miraidi ya maendeleo na kuwataka Watanzania kuzidi kumuombea.

Amesema zawadi pekee ambayo imekua Watanzania wanaweza kumpatia Rais Magufuli kutokana na utendaji kazi wake basi ni kufanya kazi kwa bidii, kuwa wazalendo na kuweka maslahi ya Taifa mbele.

" Hakuna Taifa lolote duniani ambalo limefanikiwa bila kufanya kazi siri yao kubwa kuwa na umoja wa kitaifa, mshikamano na upendo hivyo ni vema Watanzania tukawa na upendo na Serikali yetu hii ambayo inafanya kazi usiku na mchana kutuletea maendeleo.

" Lakini jambo lingine na kubwa la kumpatia Rais Magufuli ni kumwaga kura nyingi sana mwakani kwenye uchaguzi Mkuu kwa sababu kwa haya mambo makubwa anayofanya Reli ya Kisasa, Bwawa ka Umeme, Ndege, Ubanaji wa matumizi na kuzuia ufisadi vyote hivyo vinatosha kumfanya asiangaike kuomba kura," Amesema DC Katambi.

Akizungumza mbele ya kamati ya siasa ya Wilaya hiyo, DC Katambi amewaahidi kuendelea kusimamia kwa upana maslahi ya umma na mtumishi yeyote atakwenda kinyume na maagizo na kasi ya Rais Magufuli hatosita kumchukulia hatua.

Amesema kwenye maeneo ya kuchukua hatua ataendelea kuchukua hatua bila kumuonea mtu.

" Lazima tugombane tunavyoona mtu hafati misingi ya utumishi ya umma na niwaambie watendaji na watumishi wote waliopo ndani ya Wilaya hii sitomchekea mtu hakuna udugu wala urafiki kwenye mali za umma. Kwa viongozi wenye kasoro mimi sina unafiki. Kabla sijatumbuliwa mimi mwingine atakua amesagwa kabisa," Amesema DC Katambi.

WEKENI MIKAKATI THABITI KUDHIBITI UHALIFU-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Wakuu wa Polisi katika nchi za Mashariki mwa Afrika waweke mikakati thabiti ya kukabiliana na magenge yote ya uhalifu unaovuka mipaka ili wahalifu hao wasipate mahali salama pa kufanya uhalifu bila mkono wa dola kuwafikia.

Pia, Waziri Mkuu amewataka viongozi hao wadumishe ushirikiano baina yao ili waimarishe utendaji bila kujali mipaka ya nchi zao kwa sababu wahalifu wanatumia sana udhaifu wa kukosekana ushirikiano madhubuti miongoni mwa nchi hizo.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Alhamisi, Septemba 19) wakati akifunguaMkutano Mkuu wa 21 wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi Mashariki mwa Afrika (EAPCCO), uliofanyika kwenye ukumbi wa AICC, jijini Arusha. Amefungua mkutano huo kwa niaba ya Rais Dkt. John Magufuli.

Amesema mfumo wa uhalifu duniani kwa sasa unachukua sura mpya kufuatia kukua kwa teknolojia hususani ya habari na mawasiliano, uhuru wa watu na bidhaa kuvuka mipaka pamoja na kuondolewa vikwazo vingi hususani visivyo vya kiforodha, hivyo kumewezesha kuwepo kwa fursa ya maendeleo kwani bidhaa na watu husafiri kwa wepesi na haraka zaidi hivyo kufanya ukanda huo na dunia kwa ujumla kuwa kama kijiji kimoja.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema maendeleo hayo kwa upande mwingine yameleta athari za kiusalama kwani wahalifu nao wanatumia fursa hiyo kuimarisha magenge yao ya uhalifu unaovuka mipaka, mfano biashara ya dawa za kulevya.

“Uhalifu mwingine ni wizi wa magari, ujangili, utoroshaji madini na biashaa haramu ya binadmu, ugaidi utengenezaji na uuzaji wa bidhaa bandia na uharamia katika maziwa na baharini, utakatishaji wa pesa zinazotokana na uhalifu huo na vitendo vya rushwa.”

Waziri Mkuu amesema ushirikiano unahitajika katika kuzuia uhalifu ikiwemo mafunzo kwa watendaji hasa kwa makosa yanayovuka mipaka, operesheni za pamoja, upelelezi wa pamoja na ubadilishanaji wa taarifa za kiintelijensia ili kuyasaka, kuyabaini na kuyakamata magenge ya watuhumiwa wanaofanya makosa katika nchi moja na kwenda kujificha katika nchi nyingine.

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema kwamba anatambua katika jukumu lao la kutekeleza sheria bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo zinahitaji kufanyiwa kazi ili waweze kufikia lengo lao la kiutendaji kwa haraka zaidi.

Waziri Mkuu amezitaja baadhi ya changamoto hizo ni pamoja na utashi wa kisiasa.“Ili kutokomeza uhalifu wa aina yoyote utashi wa kisiasa unahitajika sana. Lengo ni kuvipatia nguvu vyombo vya dola katika kusimamia sheria. Niwatake wanasiasa wengine tutoe ushirikiano kwa vyombo hivi ili viwe na meno kwa kutunga sheria zitakazo wawezesha kuafanya kazi zao ipasavyo”

Changamoto nyingine aliyoitaja Waziri Mkuu ni utofauti wa sheria baina ya nchi zao. Amesema iwapo sheria zao zitabaki kuwa tofauti, wataendelea kutoa mwanya kwa wahalifu. “Wahalifu wataendelea kufanya uhalifu nchi moja na kukimbilia nchi nyingine ambapo sheria haiwabani, lakini sheria zikiwa zinafanana watakosa pa kukimbilia.”

Waziri Mkuu amesema suala la vita dhidi ya rushwa lazima lisimamiwe kwa nguvu zote kwani kama hatua madhubuti hazitachukuliwa katika kuimarisha uadilifu, vitendo vya rushwa vitashamiri na kusababisha kuimarika kwa magenge ya uhalifu kwa vile wahalifu watakua na uhakika wa kukwepa mkondo wa sheria.

Pia, Waziri Mkuu amesisitiza kuwa ustawi wa nchi zao katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na kijamii utategemea hali ya usalama, amani na utulivu, hivyo katika ukanda wao wa Afrika Mashariki wanategemea sana utekelezaji madhubuti wa mipango na mikakati watakayojiwekea.

Kwa upande wake, Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Simon Sirro ambaye leo amekabidhiwa uenyekiti wa EAPCCO, amesema atashirikiana vizuri na viongozi wenzake ili kuhakikisha hali ya amani na utulivu vinaendelea kuwepo kwenye nchi zao.

Pia, IGP Sirro ametumia fursa hiyo kuwashukuru marais wa nchi hizo kwa ushirikiano wanaowapa hali inayowawezesha kutimiza majukumu yao ipasavyo. Amekabidhiwa uwenyekiti wa shirikisho hilo na Mkuu wa Jeshi la Polisi la Sudan na Mwenyekiti wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi Mashariki mwa Afrika anayemaliza muda wake, Luteni Jenerali Adil Mohammed.

Shirikisho hilo linaundwa na nchi 14 ambzo ni Tanzania, Burundi, Jamuhuri ya Kimokrasi ya Congo (DRC), Djibouti, Kenya, Sudan, Sudan ya Kusini, Somalia, Rwanda, Uganda, Shelisheli, Comoro, Eritrea na Ethiopia. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akihutubia kwenye ufunguzi wa Mkutano wa 21 wa Wakuu wa Polisi wa Nchi za Mashariki mwa Afrika (EAPCCO), katika ukumbi wa AICC Arusha, Septemba 19, 2019. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa ameshika ngao, aliyokabidhiwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Simon Sirro, kwa niaba ya Rais Magufuli, kwenye ufunguzi wa Mkutano wa 21 wa Wakuu wa Polisi wa Nchi za Mashariki mwa Afrika (EAPCCO), uliyofanyika katika ukumbi wa AICC Arusha, Septemba 19, 2019. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipeana mkono na Mkuu wa Jeshi la Polisi la Kongo DRC, kwenye ufunguzi wa Mkutano wa 21 wa Wakuu wa Polisi wa Nchi za Mashariki mwa Afrika (EAPCCO), uliyofanyika katika ukumbi wa AICC Arusha, Septemba 19, 2019. 
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akifafanuliwa jambo na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Simon Sirro, katika ufunguzi wa Mkutano wa 21 wa Wakuu wa Polisi wa Mashariki mwa Afrika, kwenye ukumbi wa AICC Arusha, Septemba 19, 2019.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Simon Sirro, akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa 21 wa Wakuu wa Polisi wa Mashariki mwa Afrika, kwenye ukumbi wa AICC Arusha, Septemba 19, 2019. 
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Simon Sirro, akiwa teyari kupokea bendera ya Wenyekiti wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi wa Nchi za Mashariki mwa Afrika (EAPCCO) kwenye ufunguzi wa Mkutano wa 21 wa Wakuu wa Polisi wa nchi hizo, katika ukumbi wa AICC Arusha, Septemba 19, 2019.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Simon Sirro, akikabidhiwa bendera ya Wenyekiti wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi wa Nchi za Mashariki mwa Afrika (EAPCCO) kutoka wa Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Mkuu wa Jeshi la Polisi Sudan, Abdi Mohammed Bashir, kwenye ufunguzi wa Mkutano wa 21 wa Wakuu wa Polisi wa nchi hizo, katika ukumbi wa AICC Arusha, Septemba 19, 2019. 
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Simon Sirro, akiwa ameshika bendera ya Wenyekiti wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi wa Nchi za Mashariki mwa Afrika (EAPCCO), baada ya kukabidhiwa Wenyekiti huo na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Mkuu wa Jeshi la Polisi Sudan, Abdi Mohammed Bashir, kwenye ufunguzi wa Mkutano wa 21 wa Wakuu wa Polisi wa nchi hizo, katika ukumbi wa AICC Arusha, Septemba 19, 2019. 
 PMO_2235 Mkuu wa Jeshi la Polisi Sudan, Abdi Mohammed Bashir na Mwenyekiti wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi wa Nchi za Mashariki mwa Afrika (EAPCCO) aliyemaliza muda wake, akizungumza, kwenye ufunguzi wa Mkutano wa 21 wa Wakuu wa Polisi wa Nchi za Mashariki mwa Afrika (EAPCCO), katika ukumbi wa AICC Arusha, Septemba 19, 2019.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Simon Sirro (katikati), wakitoka kwenye ukumbi wa AICC Arusha, katika ufunguzi wa Mkutano wa 21 wa Wakuu wa Polisi wa Nchi za Mashariki mwa Afrika (EAPCCO) Septemba 19, 2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipeana mkono na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Simon Sirro, baada ya kutoka kwenye ukumbi wa AICC Arusha, katika ufunguzi wa Mkutano wa 21 wa Wakuu wa Polisi wa Nchi za Mashariki mwa Afrika (EAPCCO) Septemba 19, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Dkt.Mpango azitaka Benki kufikisha huduma vijijini

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA), uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania, jijini Dar es salaam. katika hotuba yake, Dkt. Mpango alisema kuwa Tafiti zinaonyesha Kuwa upanuzi wa huduma shirikishi za fedha unaweza kuongeza pato ghafi la taifa kwa kati ya asilimia 10 mpaka 15 kwa mwaka. Kutokana na tafiti hizo, asilimia 28 ya watanzania bado hawajafikiwa kabisa na huduma za kifedha, pia katika asilimin 65 ya waliofikiwa na huduma hizo, ni asilimia 17 tu wanaozipata kupitia mabenki, hivyo kuyataka mabenki kufikisha huduma zake kwenye maeneo ya vijijini na kuwafikia watanzania wengi zaidi.
Mwenyekiti wa Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA), Abdulmajid Nsekela, akizungumza katika Mkutano wa Umoja huo, uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania, jijini Dar es salaam. ambapo alisema kuwa mabenki yataendelea kuwa mdau mkubwa wa maendeleo kwa kuwawezesha watanzania wengi zaidi kupata huduma za kifedha.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (wa tatu kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Kanuni za Mwenendo za Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA) pamoja na Mwenyekiti wa Umoja huo ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wa pili kulia) katika Mkutano wa Umoja wa Mabenki, uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania, jijini Dar es salaam. Kushoto ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Florance Luoga na kulia ni Waziri wa Viwanja na Biashara, Innocent Bashungwa.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (wa pili kushoto) akipokea zawadi maalumu kutoka kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA) ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (katikati) na Makamu wake, Sanjay Rughani, baada ya uzinduzi rasmi wa Kanuni za Mwenendo za Umoja wa Mabenki Tanzania, uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania, jijini Dar es salaam. Kulia ni Waziri wa Viwanja na Biashara, Innocent Bashungwa na kushoto ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Florance Luoga.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Mwenyekiti wa Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA), Abdulmajid Nsekela, Makamu wake, Sanjay Rughani pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Mabenki Tanzania, Tusekelege Mwaikasu-Jounde, wakikabidhi zawadi ya ngoma maalum kwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Florance Luoga, baada ya uzinduzi rasmi wa Kanuni za Mwenendo za Umoja wa Mabenki Tanzania, uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania, jijini Dar es salaam. 




WANUFAIKA WA HUDUMA YA MSAADA WA KISHERIA WAFUNDWA

$
0
0
Na Raya Hamad –WKS  
Mashirikiano ya pamoja  kutoka kwa wanufaika wa huduma ya msaada wa  kisheria na watoaji huduma hio ndio chachu itakayopelekea  utekelezaji mzuri wa majukumu ya Idara ya Msaada wa Kisheria katika kuleta ufanisi wa majukumu ya kazi zao

Mkurugenzi wa Idara ya Msaada wa Kisheria Bi Hanifa Ramadhan Said ameyasema hayo kwenye mkutano uliowashirikisha baadhi ya wanufaika wa msaada wa kisheria uliofanyika katika ukumbi wa mkutano Wizara ya Katiba na Sheria Mazizini
Bi Hanifa amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  imeanzisha Idara ya Msaada wa Kisheria ili kuratibu utoaji na upatikanaji wa huduma ya kisheria kwa wananchi wote bila ya kujali uwezo wa kifedha kwa mtaka huduma

Aidha Bi Hanifa amewashukuru wanufaika hao waliopatiwa msaada kutoka vituo vinavyotoa huduma za msaada wa  sheria kwa kukubali kufuata taratibu na kutoa mashirikiano pale wanaposhughulikiwa malalamiko yao jambo ambalo linarahisisha kupata haki zao stahiki kwa muda muafaka
Pia  ametoa pongezi za dhati kwa watoaji wa huduma ya msaada wa Kisheria kwa kuwapokea na kuwashughulikia matatizo yao  wananchi  bila upendeleo jambo ambalo limepelekea kutokuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wanufaika waliofika katika vituo vyao

“nimefarijika na michango iliyotolewa leo hii kutoka kwenu hakuna hata mmoja aliyelalamika kuwa hakutendewa haki wakati alipotaka huduma ya msaada wa Kisheria na mmeona mafanikio yake hivyo msisite kuwafahamisha na wengine pale wanapopata matatizo hasa wanapodai haki zao za msingi wasiyamalize kienyeji au kuona muhali  bali wafuate taratibu  vituo hivi vipo kwa ajili yenu”alisisitiza

 Hata hivyo ameomba kutosita kutoa maoni ama ushauri  kwa Idara ya Msaada wa Kisheria  ili kuenda sambamba na kasi ya maendeleo kwani lengo la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ni kukuza ustawi wa wananchi wake katika nyanja zote za maisha kwa kuwahudumia na kuwaletea maendeleo na kuwaondolea uzito wa maisha yao ya kila siku

Bi Hanifa ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  kwa kuweza kufanikisha kupatikana Sera, Sheria na Kanuni inayosimamia sekta nzima ya msaada wa kisheria

Wakitoa mada kuhusu huduma za msaada wa kisheria watoa mada na uchambuzi wa vifungu vya kanuni  katika mafunzo hayo wanasheria  ndugu Amour Omar Mbwana  na ndugu Omar Haji Gora wamesema huduma za msaada wa Kisheria  zinajumuisha ushauri wa kisheria, uwakilishi mahakamani au katika mabaraza, kutoa elimu ya kisheria, pamoja na kutayarisha nyaraka za kisheria na taarifa kuhusiana na mambo ya kisheria

Aidha wamefafanua baadhi ya vifungu kwa watu wasiokuwa na sifa ya kupatiwa msaada wa kisheria kuwa ni pamoja na kampuni, shirika, taasisi ya umma, Jumuiya ya kiraia , Jumuiya isiyokuwa ya kiserikali au mtu mwengine wa kisheria .

Msisitizo pia umewekwa kuwa watoaji  wa msaada  wa kisheria hawatatoa huduma za msaada wa kisheria kuhusiana na kesi za madai zikiwemo masuala yanayohusu ulipaji wa kodi, ulipaji wa madeni na katika kesi za ufilisi na kutoweza kulipa madeni

Nao washiriki wa mafunzo hayo wametoa shukurani zao  kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kuanzisha Idara ya Msaada wa Kisheria  na kuomba idara hio kuendelea kutoa elimu na kuielimisha jamii ili waweze kuifahamu na kuona umuhimu wa kufikisha malalamiko yao pale wanapohitaji usaidizi wa huduma ya msaada wa kisheria

Washiriki hao  wamezungumzia kuwa utaratibu huo wa kuwasaidia kisheria wananchi wasiokuwa na uwezo Serikali inastahili kupongezwa kwa sababu wamo wananchi wengi wanyonge wenye vilio vya muda mrefu, lakini hawana pa kuvipeleka kutokana na unyonge.

A Wameeleza kuwa jambo la muhimu kwa Taasisi inayohusika na Utoaji wa Huduma za msaada wa Kisheria kuhakikisha wasiokuwa na uwezo ndio wanaonufaika na utaratibu huo na kuomba kufanywa kila liwezekanalo kuwazuia wale wenye uwezo wa kujisimamia ama kuendesha kesi ili waweze kupata haki zao wenyewe kutojingia katika utaratibu huo na kuwazuia walengwa.

Wamesema kwamba wamo wananchi wengi ambao uwezo wao na mwamamko wa kupigania haki zao ni mdogo, huku baadhi ya wananchi hao wanashindwa na hata nauli ya kuwawezesha kufika mahakamani, hivyo uamuzi huo ni jambo la kupongezwa kwa sababu umelenga hasa kuwakomboa wenye mahitaji.
Mkurugenzi Idara ya Mswaada wa Kisheria Zanzibar Bi Hanifa Ramadhan Said akifungua mafunzo kwa wanufaika wa huduma ya Mswaada wa Kisheria kutoka Taasisi tofauti

DAWASA YATOA ONYO KWA WAHUJUMU MIUNDOMBINU YA MAJI

$
0
0
MAMLAKA ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) leo Septemba 19 imekagua miundombinu ya maji katika Mikoa ya kihuduma ya Mtaa wa Dovya, Bunju na kushuhudia wananchi wakihujumu maji kwa kutengeneza mabwawa ya umwagiliaji na kusababisha hasara kwa wateja halali waliounganishwa na wanaolipa bili.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua miundombinu ya maji katika kata ya Bunju mtaa wa Dovya jijini humo meneja mapato wa DAWASA Edger Zawayo amesema kuwa bado wanaendelea  miundombinu ya DAWASA na wamethibitisha mabwawa wanayotumia kustawisha mazao yao ni ya DAWASA na wamiliki wa mabwawa hayo wamekimbia.

Amesema kuwa kila mwananchi awe mlinzi wa mwenzake kwa kutoa taarifa kwenye ofisi za Serikali za mitaa na ofisi za DAWASA zilizokaribu ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

"Ukikutwa unahujumu miundombinu ya maji faini ni kuanzia shilingi milioni tano hadi hamsini, hivyo ni vyema wananchi wakatumia fedha hizo kufanya shughuli za maendeleo ikiwemo kupata huduma hiyo ya maji kwa halali kabisa" Ameeleza Zawayo.

Kwa upande wake Afisa mtendaji wa mtaa wa Dovya Clara Kiriho amewaasa wananchi wa Dovya juu wa wizi wa maji wanaoufanya na kutumia maji hayo kumwagilia bustani badala yake wafuate taratibu maalumu na kupata huduma hiyo ya maji kwa uhalali.

Amesema kuwa wananchi wote wanaohitaji huduma ya maji ofisi zipo kila mahali ni vyema wakafuata taratibu na kulipa bili na sio kuhujumu maji kwa wateja halali na kuwasababishia hasara. 


 Meneja Mapato wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Edger Zawayo(kulia) akimsikiliza Mtendaji wa mtaa wa Dovya Clara Kiriho alipokuwa anatolea ufafanuzi wa matumizi ya kiwanja hicho kinacholimwa Mbogamboga na wananchi wanaoiba maji ya Mamlaka hiyo katika mtaa wa Dovya kata ya Bunju jijini Dar es Salaam leo.
 Mtaalamu wa Mambo ya Mita kutoka Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Da es Salaam (DAWASA) Mohammed Mwakimila kionesha mambomba ya maji yaliyokuwa yanaunganishwa kwenye bomba la Mamlaka hiyo na kuelekezwa kwenye kisima na kumwagilia mbogamboga wakati wa ziara ya kushtukiza kwenye shamba lililopo kata mtaa wa Dovya kata ya Bunju jijini Dar es Salaam.
 Mtendaji wa mtaa wa Dovya Clara Kiriho (katikati) akitolea ufafanuzi kwa Meneja Mapato wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Edger Zawayo (kulia) walipokuwa waangalia mbogamboga zilivyostawi kwenyeshamba hilo lililokuwa linatumia maji ya wizi ya DAWASA.
Meneja Mapato wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Edger Zawayo akikagua mambomba yanayotumiwa na na wananchi hao kama niya DAWASA au la mara baada ya kufanya ukaguzi wa kustukiza kwenye shamba hilo na kukuta wizi wa maji kwa kiasi kikubwa katika mtaa wa  Dovya kata ya Bunju jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya visima vya maji vinavyotumika kuhifadhia maji ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Da es Salaam (DAWASA) vilivyokutwa katika shamba la mbogamboga katika mtaa wa  Dovya kata ya Bunju jijini Dar es  Salaam leo.
Shamba la Mbogamboga likiwa limenawili kwa kutumia maji ya wizi ya DAWASA.

RAIS DKT.SHEIN AMEWAAPISHA WAKUU WA MIKOA IKULU LEO

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Mhe.Ayoub Mohamed Mahmoud kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja hafla leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar kabla Ayoub alikuwa Mkuu wa Mkoa wa mjini Magharibi.(Picha na Ikulu)
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Mhe.Hassan Khatib Hassan kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar kabla alikuwa Mkoa wa Kusini Unguja.
 Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe.Omar Othman Makungu (kushoto) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Issa Haji Ussi(Gavu) na Naibu Waziri Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa n a Idara Maalum za SMZ Shamata Shaame Khamis,(kulia) wakiwa katika hafla ya kuapishwa Wakuu wa Mikoa Kusini na Mjini Magharibi leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar.
 Baadhi ya Viongozi mbali mbali waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa kwa Viongozi ambao ni Wkuu wa Mikoa naRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar. (Picha na Ikulu).

TEGESHA YAWAUMIZA KICHWA WATHAMINI FIDIA NYAMONGO

$
0
0
Na Munir Shemweta, WANMM NYAMONGO
Zoezi la uthamini kulipa fidia kwa wananchi wa Nyamongo wilaya ya Tarime mkoa wa Mara kupisha upanuzi wa Mgodi wa Dhahabu North Mara kwa ajili ya ujenzi wa Bwawa la Maji Taka limekumbwa na changamoto kufuatia baadhi ya wananchi kujenga nyumba ama kuongeza sehemu za nyumba zao maarufu kama ‘Tegesha’ ili kujipatia faida kupitia thamani ya fidia.

Wathamni katika zoezi hilo walibaini tofauti kubwa katika uthamini walioufanya awali na pale walipoenda kwa mara ya pili kwa ajili ya uhakiki ambapo ilibainika baadhi ya vyumba katika nyumba zilizofanyiwa uthamini kuwa wazi baada ya waliokuwa wakiishi kuondoka baada ya kuthaminiwa.

Imeelezwa kuwa lengo wananchi wanaofanya ujanja wa ‘Tegesha’ ni kujipatia posho ya makazi ambayo kwa kawaida hutolewa kama fidia kwa wamiliki kulingana na idadi ya vyumba kwenye nyumba ya mmiliki.

Kwa mujibu wa Wathamini wa zoezi hilo, mbali na wamiliki walioathirika na zoezi hilo kulipwa gharama nyingine kama vile nyumba na mazao pia hulipwa posho ya makazi kwa kipindi cha miezi 36 lengo kumuwezesha mpangaji kupata mahali pa kuishi kabla ya kuanza zoezi la kuondolewa.

Mwandishi wa Gazeti hili alishuhudi moja ya nyumba iliyopo kitongoji cha Kigonga A katika kijiji cha Matongo ikiwa na vyumba ishirini na moja wakati nyumba hiyo ilistahili kuwa na vyumba vitatu na baadhi ya vyumba havina hata madirisha.

Mthamni Mkuu wa Serikali Evaline Mugasha ambaye alitembelea baadhi ya nyumba hizo kukagua maendeleo ya kazi ya uthamini katika eneo hilo aliweka wazi kuwa Ofisi yake inafanya kazi kwa kufuata sheria ya Uthamini na hatua kali zitachukuliwa kwa mtu atakayeonekana kufanya udanganyifu kwa kwa lengo la kujipatia kipato.

Kwa mujibu wa Mugasha, zoezi la uthamini katika eneo la Nyamongo linalohusisha vitongoji vitatu katika kijiji cha Matongo limekuwa likifanyika kwa uwazi na kushirikisha pande zote wakati wa kuorodhesha mali na kufafanua kuwa hata mwananchi asiyeridhika na uthamini katika eneo lake hupewa fomu maalum ya kujaza lengo likiwa kutoa haki.

‘’Tumeona watu walihamisha magodoro, vitanda na mizigo mingine lengo ni kupata posho ya makazi ili kujipatia faida na cha kushangaza baadhi ya wapangaji hawajui hata choo cha nyumba wanayoishi kilipo, ofisi yangu haitavumilia vitendo hivyo kila mtu atalipwa anachostahili’’ alisema Mugasha.

Mthamini kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Lazaro Magumba alieleza kuwa wakati zoezi la uthamini kumekuwa na changamoto hasa wakati wa kukagua mali za wananchi kutokana na baadhi yao kuwa na dhana ya kujipatia utajiri kupitia mradi huo ambapo hufanya maendelezo ya kuegesha maarufu kama ‘tegesha’ ili kulipwa fedha nyingi.

‘’ Wananchi wanajenga nyumba zilizopangana na hakuna hata nafasi na wakati wa uthamni usiku kucha watu wanahamisha vyombo, magodoro na wengine hata wanyama ili ionekane ni makazi halali’’ alisema Lazaro.

Alisema wanachokifanya wao ni kukagua kwa awamu kwa lengo la kujiridhisha kama kweli walionekana wakati wa uthamini kama ni wakazi halali ama walienda kutegesha.

Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Matongo wilayani Tarime mkoa wa Mara ambao hawakupenda majina yao yawekwe wazi kutokana na sababu za kiusalama walikiri kuwepo mchezo huo wa Tegesha lakini walidai hufanywa na watu wasio wakazi wa muda mrefu katika kijiji hicho bali walienda kwa lengo la kujipatia faida kupitia zoezi hilo.

Kwa mujibu wa wakazi hao, baadhi ya wananchi kutoka nje ya kijiji hicho walinunua nyumba ama maeneo kwa wenyeji na kuongeza vyumba na kuwakodisha watu kuishi ili kuvizia zoezi la uthamini wa fidia wapate faida.

Kwa muda mrefu wananchi wa Nyamongo wilaya ya Tarime mkoa wa mara hasa wale wanaoishi vitongoji vinavozunguka Mgodi wa Dhahabu wa North Mara wamekuwa wakilalamikia uchafuzi wa mazingira hasa maji yanayovuja kutoka Mgodi huo kuwa yana sumu inayoathiri afya zao jambo lililomlazimu Rais John Pombe Magufuli wakati wa ziara yake katika eneo hilo kuagiza kufanyika utafiti ili kubaini ukweli huo.
  Mthamini Mkuu wa Serikali Evaline Mugasha akiwa katika chumba kilichojengwa maarufu kama Tegesha katika kijiji cha Matongo wilaya ya Tarime mkoa wa Mara wakati akikagua kazi ya uthamini wa fidia inayofanywa na Ofisi yake katika eneo la Nyamongo kupanua mgodi wa Dhahabu wa North Mara kupisha ujenzi wa bwawa la maji taka juzi.
 Mthamini Mkuu wa Serikali Evaline Mugasha akionesha moja ya chumba kilichojengwa maarufu kama Tegesha katika kijiji cha Matongo wilaya ya Tarime mkoa wa Mara wakati akikagua kazi ya uthamini wa fidia inayofanywa na Ofisi yake katika eneo la Nyamongo kupanua mgodi wa Dhahabu wa North Mara ili kupisha ujenzi wa bwawa la maji taka juzi.
Mthamini Mkuu wa Serikali Evaline Mugasha (Wa pili kushoto) akiongozana na timu ya uthamini katika kijiji cha Matongo wilaya ya Tarime mkoa wa Mara wakati akikagua kazi ya uthamini wa fidia inayofanywa na Ofisi yake katika eneo la Nyamongo kupanua mgodi wa Dhahabu wa North Mara ili kupisha ujenzi wa bwawa la maji taka juzi. (PICHA NA WIZARA YA ARDHI)

NI MUHIMU KUWEKEZA KWENYE TEHAMA-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema ili kuleta maendeleo endelevu ya viwanda, kuongeza biashara na kutengeneza ajira, nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) zinapaswa kuwekeza katika uunganishaji na uwianishaji wa viwango mbalimbali vya TEHAMA.

Amesema hatua hiyo itasaidia kutatua changamoto za maendeleo ya miundombinu na muingiliano wa mawasiliano nje ya mipaka ya nchi na kikanda. “Changamoto hizo zinajumuisha maunganisho ya njia kuu za mawasiliano kati ya nchi jirani, kuyafanya mawasiliano ya kikanda yabaki ndani ya kanda, maunganisho ya kuvuka mipaka ya nchi, upangaji wa bei pamoja na uwianishaji wa viwango.”

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Alhamisi, Septemba 19, 2019) wakati akifungua Mkutano wa Pamoja wa Mawaziri wa SADC wa sekta ya TEHAMA, uchukuzi na hali ya hewa pamoja na kongamano maalumu la Mawaziri, unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu amesema kwa kipindi hiki, nchi wanachama zinapaswa kuhakikisha kuwa utekelezaji unalenga katika teknolojia zinazochipukia kwenye utoaji wa huduma za posta sambamba na kuanzisha huduma na bidhaa mpya ambazo zitakidhi mahitaji ya sasa ya wateja na kuhamasisha biashara mtandao.

“Katika kufanikisha hili, ni muhimu kufanya tathmini ya utekelezaji wa Mkakati wa Posta wa SADC wa mwaka 2017-2020 ambao uliridhiwa mwezi Septemba, 2017.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema ili kufikia mtangamano wa kikanda kuhusua miundombinu ya usafiri na usafirishaji, mkutano huo unapaswa kuzungumza namna gani nchi wanachama zinaweza kuwianisha sera, viwango, mifumo ya sheria katika maeneo ya barabara, reli, usafiri wa anga, usafiri wa majini, pamoja na hali ya hewa.

Waziri Mkuu amesema kuna haja ya kuboresha miundombinu muhimu ya usafirishaji, utaratibu wa ugavi na usafirishaji wa vitu na huduma pamoja na kuwezesha kutoa mizigo kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine ndani ya kanda. “Hivyo, nawaomba katika mkutano wenu mjadili maeneo haya na kuja na mapendekezo ya suluhisho ili kutatua vikwazo mbalimbali.”

“Tanzania imeweza kuboresha miundombinu ya bandari pamoja na mifumo ya uendeshaji ili kusaidia nchi za SADC ambazo hazipakani na bahari nazo ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Jamhuri ya Zambia, Jamhuri ya Malawi pamoja na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki za Jamhuri za Uganda, Rwanda na Burundi.”

Waziri Mkuu amesema kuwa nchi wanachama wa SADC zinapaswa kuboresha mifumo ya reli kwa kuzingatia Mpango Mkakati Elekezi wa Maendeleo wa Kikanda wa mwaka 2015-2063 pamoja na Mpango Kamambe wa Maendeleo ya Miundombinu wa Kikanda wa mwaka 2019-2023.

Amesema kati ya miradi mikubwa inayotekelezwa hapa Tanzania, ni pamoja na ujenzi wa reli ya kisasa ya mwendo kasi inayojengwa katika ukanda wa kati pamoja na ukarabati wa Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) ambayo inaunganisha nchi wanachama wa SADC. “Hivyo, katika ukarabati uliofanyika wa TAZARA, umeongeza uwezo wa reli hiyo kusafirisha mizigo kutoka tani 88,000 mwaka 2014/2015 hadi tani 220,000 mwaka 2017/2018.”

Mkutano huo unahudhuriwa na Mawaziri wa Sekta ya TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa kutoka nchi za Angola (4), Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (2), Msumbiji (1) Zambia (3), Afrika Kusini (2), Lethoto (1), Zimbabwe (2) na Tanzania inawakilishwa na Mawaziri watano na Naibu Waziri Mmoja, akiwemo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe ambaye ndiye Mwenyekiti wa Mkutano huo. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akihutubia kwenye Mkutano wa Mawaziri wa Nchi za SADC wa masuala ya Tehama, Uchukuzi, Habari na Hali ya Hewa. Septemba 19.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Mwakilishi wa Katibu Mkuu SADC, Mapalao Makuena, akizungumza kwenye Mkutano wa Mawaziri wa Nchi za SADC wa masuala ya Tehama, Uchukuzi, Habari na Hali ya Hewa. Septemba 19.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe, wakati akiwasili kwenye ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam, kufungua Mkutano wa Mawaziri wa Nchi za SADC wa masuala ya Tehama, Uchukuzi, Habari na Hali ya Hewa. Septemba 19.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Mrakibu Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Gabriel Mukungu, wakati akiangalia mfumo wa unaorahisisha mawasiliano kwa vyombo vya usafiri (Traffic Information System - TIMS), kabla ya kufungua Mkutano wa Mawaziri wa Nchi za SADC wa masuala ya Tehama, Uchukuzi, Habari na Hali ya Hewa, uliyofanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Septemba 19.2019.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia mfumo wa unaorahisisha mawasiliano kwa vyombo vya usafiri(Traffic Information System - TIMS), kabla ya kufungua Mkutano wa Mawaziri wa Nchi za SADC wa masuala ya Tehama, Uchukuzi, Habari na Hali ya Hewa, uliyofanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Septemba 19.2019.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Injinia James Kilaba, nje ya ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam, kabla ya kufungua Mkutano wa Mawaziri wa Nchi za SADC wa masuala ya Tehama, Uchukuzi, Habari na Hali ya Hewa. Septemba 19.2019.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia gari maalum la mtambo wa usimamizi wa masafa, nje ya ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam, kabla ya kufungua Mkutano wa Mawaziri wa Nchi za SADC wa masuala ya Tehama, Uchukuzi, Habari na Hali ya Hewa. Septemba 19.2019. Kulia ni Mhandisi Mwandamizi, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Victor Kweka.

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mwakilishi wa Katibu Mkuu SADC, Mapalao Makuena (katikati), , nje ya ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam, baada ya kufungua Mkutano wa Mawaziri wa Nchi za SADC wa masuala ya Tehama, Uchukuzi, Habari na Hali ya Hewa. Septemba 19.2019. Kulia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Paramagamba Kabudi, nje ya ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam, baada ya kufungua Mkutano wa Mawaziri wa Nchi za SADC wa masuala ya Tehama, Uchukuzi, Habari na Hali ya Hewa. Septemba 19.2019. 


MWILI WA MWANDISHI WA HABARI MKONGWE GODFREY DILUNGA WAAGWA KWA HESHIMA DAR, KUZIKWA KESHO MORO

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

MWILI wa aliyekuwa mwandishi wa habari mkongwe nchini Gofrey Dilunga aliyefariki dunia Septemba 17 mwaka 2019 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili umeagwa leo katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam na kusafirishwa kuelekea mjini Morogoro ambapo utapumzishwa kwenye nyumba yake ya milele.

Akizungumza kwa niaba ya Serikali Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa Serikali haitasahau mchango wa marehemu Dilunga hasa katika kuitumia vyema kalamu yake kwa manufaa ya taifa kwa ujumla.

Dkt. Mwakyembe amesema kutokana na mchango wake mkubwa katika taifa Rais Dkt. John Joseph Magufuli, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassani na waziri Mkuu Kassimu Majaliwa wametuma salamu zao za rambirambi kwa ndugu, jamaa, marafiki na wanahabari wote.

" Kuna vikao vya dharura vinavyoendelea ila nimelazimika kuja hapa kutokana na mchango wake,na kutokana na umuhimu Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu wamenituma kuja kutoa salamu zao za rambirambi" ameeleza Dkt. Mwakyembe.

Kwa upande wake Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole amesema kuwa mchango wa marehemu katika taifa na chama hicho ni mkubwa na daima alikuwa mstahimilivu aliyetumia kalamu yake vyema kwa manufaa ya taifa kwa ujumla.

Amesema kuwa waandishi wa habari hawana budi kufuata nyayo zake ili kuweza kulipeleka taifa mbele zaidi na hiyo ni kwa kutumia vyema kalamu zao.

Akisoma wasifu wa marehemu Mkurugenzi wa Kampuni ya Jamhuri Deudatus Balile amesema kuwa marehemu alianza kusumbuliwa na maradhi ya tumbo kuanzia julai mwaka huu kabla ya kupelekwa hospitali ya taifa Muhimbili ambapo umauti ulimkuta.

Balile amesema kuwa marehemu ameacha watoto watatu na mjane mmoja na kueleza kuwa kampuni hiyo itamsomesha mtoto wa kwanza wa marehemu hadi elimu ya juu na amewaomba wanajamii wengine kuendelea kuwashika mkono watoto wa marehemu na mjane huyo.

Viongozi mbalimbali wa kisiasa na serikali wamejitokeza kuaga mwili wa mwandishi huyo wakiongozwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe.

Pia alikuwepo Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas, Mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais Ikulu Gerson Msigwa, na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole.

Wengine ni Mbunge wa Mtama Nape Nnauye, Waziri Mstaafu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe, wabunge, viongozi wa taasisi mbalimbali na wanahabari.
Waziri wa Habari ,Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk.Harrison Mwakyembe akizungumza wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari Godfrey Dilunga leo Septemba 19 katika  viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam
Waziri wa Habari ,Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk.Harrison Mwakyembe akimsalimia Mke wa aliyekuwa mwandishi wa habari wa gazeti la Jamhuri  Godfrey Dilunga .
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Gerson Msigwa akimpa mkono wa pole  Mke wa aliyekuwa Mwandishi wa Habari Godfrey Dilunga katika viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa kuaga mwili wa Mwandishi huyo.
Mbunge wa Viti Maalum Amina Mollel akizungumza wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari Godfrey Dilunga 
Mbunge wa Viti Maalum Amina Mollel akimpa mkono wa pole Mke wa marehemu Godfrey Dilunga akisalimiana na 
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe akizungumza wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari Godfrey Dilunga .
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk.Harrison Mwakyembe akimuonesha kitu aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari Godfrey Dilunga ,Kushoto ni Mbunge wa viti maalum Amina Mollel,Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt Hassan Abbasi,na kulia ni Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe na Meya wa Ilala Omari Kumbilamoto.
Sanduku  lililobeba mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari maarufu Godfrey Dilunga likishushwa viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam tayari kwa kuagwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Gerson Msigwa(kulia) akisalimiana na Kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe  baada ya kukutana viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari Godfrey Dilunga .Wa kwanza kulia ni Meya wa Ilala Omary Kumbilamoto 
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Gerson Msigwa(kushoto)akiwa na waombolezaji wengine kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam 

Mtangazaji wa Clouds TV  na Clouds Redio Simon Simalenga(kushoto) akizungumza jambo mbele ya waandishi wengine wa wahabari waliofika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam 
Sehemu ya waandishi wa habari nchini wakiwa katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaa n kuaga mwili wa mwandishi wa habari Godfrey Dilunga .Kuanzia kushoto ni Jamal Hashim, Emmanuel Mbuguni na Idd Mkwama
Mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari Dodfrey Dilunga ukishushwa katika gari baada ya kufika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam 
Jeneza la mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari wa gazeti la Jamhuri Godfrey Dilunga ukishushwa katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuuga kabla ya kuanza safari ya kuusafirsisha mkoani Morogoro kwa ajili ya maziko yanayotarajia kufanyika kesho
Waombolezaji wakiweka vizuri jeneza lililobeba mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari wa gazeti la Jamuri marehemu Godrey Dilunga 
Baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa nchini wakiwa katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa nwandishi wa habari nchini Godfrey Dilunga
Waombolezaji wakiwa wamesimama kwa ajili ya maombi wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari Godfrey Dilunga
Baadhi ya waombolezaji waliofika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam kuaga mwili wa Godfrey Dilunga wakiwa wamesiamama wakati wa ibada maalum 
Waombolezaji wakiwa wamesimama wakati wa ibada maalum ya kumuombea aliyekuwa mwandishi wa habari maarufu nchini Godfrey Dilunga
Sehemu ya waombolezaji wakiwa wamesimama wakati wa shughuli za kuaga mwili wa mwandishi Godfrey Dilunga katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa wa Kampuni ya Jamhuri inayochapisha gazeti la Jamhuri Deodatus Balile akizungumza wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa mwandishi wa gazeti hilo Goddrey Dilunga .Mwii wa marehemu Dilunga umeagwa leo viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam  
Mwenyekiti wa Kamati ya Kamati ya Mazishi ya aliyekuwa mwandishi wa habari Godfrey Dilunga, Thomson Kasenyenda akitoa ufafanuzi na maelezo kwa waombolezaji waliofika kuaga mwili wa marehemu Dilunga 
Katibu wa Jukwaa la  Wahariri Tanzania(TEF) Nevill Meena akizungumza mbele ya waombolezaji waliofika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam kuaga mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari Godfrey Dilunga 
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Afrika Group Media inayosimamia kituo cha Luninga cha Chanel Ten na kituo cha Redio cha Magic FM Jaffary Haniu akitoa salamu za pole wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari wa gazeti la Jamhuri Godfrey Dilunga ambaye ameagwa leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam 
Mhariri Mkuu wa Gazeti la Mtanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Jukwaa la Wahariri wa Habari Tanzania (TEF)Kulwa Karedia(kushoto) akizungumza leo Septemba 19,2019 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam wakati wa kuaga mwili wa mwandishi Godfrey Dilunga 
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania(TAMWA) Joyce Shebe ambaye pia ni Mhariri wa Clouds Redio na Clouds TV akitoa neno wakati wa kuaga mwili wa marehemu Godfrey Dilunga aliyefariki dunia Septemba 17 mwaka huu .Dilunga ameagwa leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam 
Baadhi ya waombolezaji wakiwemo viongozi wa Serikali, viongozi wa vyama vya siasa na wadau wa tasnia ya habari wakiwa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam wakati wa kuaga mwili wa mwandishi mkongwe Godfrey Dilunga aliyefariki dunia Septemba 17 mwaka huu.Marehemu Dilunga anatarajiwa kuzikwa kesho mkoani Morogoro
Meya wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam Omary Kumbilamoto akizungumza mbele ya waombolezaji waliofika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini kwa ajili ya kuaga mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari mkongwe nchini Godfrey Dilunga ambaye amefariki dunia Septemba 17, 2019 
Katibu wa Itikadi na Uenezi- CCM Hamphrey Polepole akitoa salamu za pole kwa niaba ya chama hicho wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mwandishi wa habari Godfrey Dilunga aliyeagwa leo  katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk.Harrison Mwakyembe(kulia) akisalimiana na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje  na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe 
Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika picha ya pamoja katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam baada ya kuaga mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari wa gazeti la Jamhuri, Godfrey Dilunga 


EAC DECLARES FRIDAYS AS ‘AFRIKA MASHARIKI FASHION DAY’

$
0
0
EAC Secretariat
East African Community Secretariat, Arusha, Tanzania, 19th September, 2019:  The East African Community has declared Fridays as ‘Afrika Mashariki Fashion Day’ during which East Africans will wear attires manufactured in the region.

The 36th Extra-Ordinary Sectoral Council on Trade, Industry, Finance and Investment (SCTIFI) further declared the 1st Week of September an ‘Afrika Mashariki Fashion Week’ to be held annually as a Trade Fair and Exhibition of EAC designed textiles and garments.

The SCTIFI urged EAC Partner States that produce cotton to set up national cotton lint buffer stock mechanisms to ensure all year-round availability of locally produced cotton lint to spinning mills.

The Ministerial Session of the 36th SCTIFI which was chaired by Rwanda’s Minister for Trade and Industry, Ms. Soraya M. Hakuziyaremye, approved the Final Draft Cotton, Textile and Apparels (CTA) Strategy and the Implementation Roadmap.

In her opening remarks, Ms. Hakuziyaremye said that for the EAC region to reap maximum benefits from the African Continental Free Trade Area (AfCTA), it was imperative to enhance the region’s productive capacity. Ms. Hakuziyaremye called for urgent implementation of a number of outstanding EAC Summit decisions and directives especially in the textile, leather and automotive industries, in addition to resolving Non-Tariff Barriers.

She reminded the Ministers that AfCTA Summit had directed that the implementation of the agreement should commence by 1st July, 2020 necessitating EAC Partner States to conclude their Tariff Offers by the agreed dates.

Other Ministers present at the meeting were Hon. Jean Marie Niyokindi (Minister for Trade and Industry, Burundi), Hon. Peter Munya (Minister for Industry, Trade and Cooperatives, Kenya), Hon. Kafabusa Michael (Minister of State for Trade and Industry, Uganda), Hon. John Dor Majok (Deputy Minister of Finance and Planning, South Sudan), and Hon. Innocent Bashungwa (Minister for Industry and Trade, Tanzania).

The Ministers called on Partner States to give priority to the implementation of the Cotton, Textiles and Apparels (CTA) Strategy by providing budgets for the activities, as relevant to specific countries, in the 2020/2021 Financial Year.

The SCTIFI directed the Standards Committee to assess and advise on feasibility of the Pre-shipment Verification of Conformity (PVoC) of all imports of textiles and ready-made garments (RMGs) into the region, as a measure to control illicit imports of worn out or used textiles and garments.

The meeting further approved the Draft Leather and Leather Products Sector Strategy and the Implementation Roadmap, and urged Partner States to give priority to the implementation of the Strategy by including the activities, as relevant to each country, in the next Financial Year’s national budgets.

The Council was informed of case studies of investment in the leather and leather products in Vietnam and Ethiopia. Due to government support, Vietnam had become the second largest footwear exporter after China exporting more than 1 billion pairs of shoes and accounting for 7.4 per cent of global supply.

Ethiopia, on the other hand, has recently emerged as a world-class player in leather footwear due to its low cost skilled labour, improvements in the quality of its raw material supply, the stable business climate, and the establishment of special economic zones. The country is attracting an increasing number of investors who use the country as a production site targeting the EU and US markets. Shoes from Ethiopia are also increasingly gaining popularity in East Africa.

On Non-Tariff Barriers (NTBs), the SCTIFI directed Partner States to eliminate all the outstanding NTBs from the EAC Time Bound Programme. The Ministers further directed the Secretariat to always schedule a one day session of Ministers with the East African Business Council and other Private Sector stakeholders before every SCTIFI to deliberate on issues of concern to the private sector including NTBs.

The recommendations of these engagements would then be escalated to the Council of Ministers and eventually the Summit. It was noted that among the causes of NTBs include: non-harmonisation of excise duty amongst Partner States; lack of a common framework for harmonisation of local content; multiple trade facilitation agencies; persistent stays of application; non-implementation of recommendations from studies and verification missions, and; non-recognition of standards quality marks.

On AfCTA, the SCTIFI agreed on a time-frame of 10 years for Category A products and 13 years for Category B products to be adopted by the EAC for tariff liberalization for the AfCTA as a customs union. Category A products refer to non-sensitive products to be liberalized first. Category B products, on the other hand, will be liberalized from the 6th year after the commencement of tariff dismantling.

The 19th Ordinary Summit of the EAC Heads of State held in February 2018 in Kampala, Uganda, with regard to promoting Cotton, Textiles, Apparels and Leather industries in the region and make the region more competitive and create jobs, decided to prioritize the development of competitive domestic and textile and leather sectors to provide affordable, new and quality options of clothing and leather products to EAC citizens. The Summit directed the Council of Ministers to put in place mechanisms that support textiles and leather manufacturing in the region.

In fulfilment of the Summit directive, the EAC Secretariat received support from TradeMark East Africa (TMEA) to facilitate the development of Regional Strategic Plans for (i) Cotton, Textiles and Apparels Strategy (CTA) and (ii) Leather and Leather Products Sectors. The two strategies were presented at country consultative workshops in the months of December 2018 and January 2019. Inputs from the workshops were incorporated and considered at Experts Group Meetings held in February 2019. Technical feedback from the experts group meetings were incorporated into the strategies which were then validated and adopted in April 2019 in Dar es Salaam, Tanzania.

The EAC Deputy Secretary General in charge of Productive and Social Sectors, Hon. Christophe Bazivamo, represented the Secretary General.

SUPER MODEL MIRIAM ODEMBA KATIKA THE TRENDY SHOW

HABARI ZA UMOJA WA MATAIFA KUTOKA NEW YORK LEO

TBC: LAINI MILIONI TANO TU ZA SIMU ZASAJILIWA HADI SASA

VOA SWAHILI: Duniani Leo September 19, 2019

Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images