Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

ENSULO, PROMISE NI ZAIDI YA MAPINDUZI BONGOMOVIE

$
0
0
Wahitimu wa mafunzo maalum ya uzalishaji filamu wakitambulisha rasmi filamu walizotengeneza kurushwa rasmi kwenye King'amuzi cha Dstv.


     Na.Khadija seif, Michuzi TV
WAHITIMU wa mafunzo maalum ya uzalishaji filamu chini ya programu ya Kampuni ya Multichoice talent factory wajipanga kuleta mapinduzi kwenye soko la filamu duniani.

Akizungumza na waandishi wahabari wakati wa kutambulisha rasmi filamu mbili zilizotengenezwa na wahitimu hao, Wilson Nkya amesema wanapongeza uongozi wa Multichoice kwa kuendelea kukuza vipaji vya vijana wenye ndoto za kufanya vitu vikubwa katika sekta ya filamu.

"Mafunzo tuliyotapata yameweza kutupa akili na maarifa jinsi gani tunateweza kutengeneza filamu bora zenye kujenga jamii na kutumia vitu asilia  vya kutambulisha utamaduni Kama vile maporomoko ya maji,ngoma za asili na vitu vyenye upekee ,"

Aidha ameeleza pia kwa kipindi chote cha mafunzo wameweza kuandaa filamu mbili Ensulo pamoja na promise ambazo zitarusha hivi karibuni kupitia King'amuzi cha dstv kupitia Maisha magic bongo.

Na pia miongoni mwa wahitimu hao Janet Moshi amesema pamoja na kupatiwa na mafunzo hayo bado wanania ya dhati kubadilisha soko la filamu kuanzia utengenezwaji wa miswada (Script) ,kuongoza filamu pamoja kutengeneza picha jongefu.

" Wasanii na waongozaji (directors) wanatakiwa kujifunza kutengeneza filamu kwa kutumia bajeti ndogo pamoja na kutumia vitu ambavyo vinaweza kueleweka kwa urahisi kwa watazamaji".

RAIS MAGUFULI NA WAZIRI MKUU MAJALIWA NI KAMA CHRITIANO RONALDO NA LIONEL MESSI

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye moja ya hafla hivi karibuni jijini Dar.


Na Said Mwishehe,Michuzi TV 

SITAKI kukupotezea muda msomaji wa makala haya, naomba tu uelewe mapema leo hii nimeamua kujikita kuzungumzia muunganiko wa kazi kati ya Rais Dk.John Magufuli na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. 

Ndio kuna kitu nataka kuzungmza kuhusu viongozi wangu hawa wawili ambao nawapenda kwa nafasi sawa huku nikitambua kila mmoja na nafasi yake na mamlaka yake kwa mujibu wa Katiba ya Nchi yetu. 

Nikiri ni mara kadhaa nimeandika makala au chambuzi kuhusu utendaji kazi wa Rais Dk.John Magufuli.Nimeandika sana kuhusu Rais wetu. 

Nimeandika kuhusu mambo ya msingi ambayo anayasimamia katika kuhakikisha Taifa la Tanzania linasonga mbele.Niahidi kadri nitakavyopata nafasi na uhai nitaandika tu.Nasisitiza nitaandika kuhusu Rais wangu, kikubwa nifuate sheria na taratibu zilizopo. 

Kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa nikiri kwamba sijawahi kuandika chochote tangu amekuwa katika nafasi hiyo.Nazugumzia kuandika makala au uchambuzi kuhusu Waziri Mkuu.Kweli sijawahi. 

Hata hivyo kwa kuandika habari zinazohusu Waziri Mkuu, namshukuru Mungu kwani kazi hiyo nimekuwa nikiifanya sana tena kwa nyakati tofauti.Kuna tofauti kati ya kuandika habari na makala au kuandika habari na uchambuzi. 

Kwa leo naomba niandike kuhusu Waziri Mkuu.Navutiwa na utendaji wake wa kazi, navutiwa na namna ambavyo anatimiza majukumu yake kwa nafasi yake ya Waziri Mkuu. 

Ukweli Waziri Mkuu Kassim Majaliwa unajua namna ya kufanya kazi zako, unajua kutekeleza majukumu yako, unajua kuwasimamia walio chini yako.Waziri Mkuu wewe ni jembe.Tena ni jembe la kazi. 

Tangu Rais Dk.Magufuli alivyokuteua nafasi hiyo umekuwa makini kwa kila ambacho unakifanya.Unajua namna ya kuhakikisha Serikali ya Awamu ya Tano inakwenda vizuri.Kweli Waziri Mkuu uko vizuri. 

Nimekuwa nikifuatilia ziara zako, nimekuwa nikifuatilia maagizo yako na kubwa zaidi nimekuwa nikifuatilia misimamo yako.Kuna wakati huwa najifikirisha ujinga. 

Ndio nafikiri ujinga kwasababu kadri navyokutafakari nakosa majibu ya moja kwa moja wewe ni wa aina gani.Hata hivyo jibu langu la moja kwa moja nalipata kuwa wewe unastahili kuwa Waziri Mkuu na Rais wetu mpendwa hakukosea kukuteua katika nafasi hiyo. 

Kwa kuwa nimeamua kuandika kuhusu wewe, leo nataka nikuambie jambo.Iko hivi baada ya Rais Magufuli kushinda uchaguzi Mkuu na kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaia, kitendawili kikabaki nani atakuwa Waziri Mkuu wake. 

Kila Mtanzania alitaka kufahamu nani atakuwa Waziri Mkuu.Tunafahamu Dk.Magufuli akiwa katika harakati za kuutaka urais hakuwa na makundi, hivyo haikuwa rahisi kujua nani atakuwa nani baada ya kushinda kiti cha urais. 

Wakati tunasubiri nani atakuwa Waziri Mkuu, nakumbuka nilipata nafasi ya kwenda mkoani Mbeya na nilifikia wilayani Mbalali katika mji mdogo wa chimala. 

Sikumbi tarehe, wala mwezi ila nakumbuka nilikuwa na rafiki yangu ambaye ni Mwandishi Mwandamizi wa gazeti la Majira.Anaitwa David John. 

Nimeamua kumtaja mwandishi huyu si kwasababu ya kutaka kumpa sifa au umaarufu.Hana sifa ya kuwa maarufu au kuwa na sifa ila anabaki kuwa mwandishi makini na anayejua kutimiza majukumu yake. 

Tukiwa Mbeya tunaendelea na majukumu yetu, tukapata nafasi ya kusikia Rais atatangaza jina la Waziri Mkuu ambalo litapelekwa bungeni kwa ajili ya kupigiwa kura na wabunge. 

Hivyo wakati tukisubiri nani atapendekezwa katika nafasi hiyo , tukiwa katika moja ya mgawa,baadhi ya wananchi waliamua kutaja baadhi ya wabunge ambao wanadhani wangeweza kupendekezwa na Rais kushika nafasi hiyo ya Waziri Mkuu. 

Binafsi nilitaja jina la Kassim Majaliwa.Baada ya kutaja jina hilo kukaibuka mjadala.Huyu mwandishi wa Majira David John akawa anakubaliana nami kuhusu Kassim Majaliwa lakini akawa ananiambia hataiweza nafasi hiyo kwasababu ni mpole.Ndivyo alivyokuwa anamtafsiri kwa wakati huo. 

Nadhan alikuwa anaangalia haina ya Kassim Majaliwa ambaye kimuonekano ni mpole lakini kiutendaji yuko makini na mkali. 

Nilimwambia David John , sawa Kassim Majaliwa anaweza kuwa mpole lakini nafasi ya Waziri Mkuu inaweza kumbadilisha na akaimudu vema. 

Hicho ndicho ambacho kimenifanya leo hii niandike makala haya.Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameimudu nafasi hiyo.Nimekuwa nikimfuatilia hatua kwa hatua.Yuko vizuri sana. 

Hata hivyo nimekuwa nikijiuliza Rais Magufuli alifikiria nini hadi kuamua Kassim Majaliwa awe Waziri Mkuu wake. Aliona mbali sana.Rais Magufuli wewe uliona mbali sana kuamua kumchagua Kassim Majaliwa. 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa sasa yuko mkoani Morogoro katika ziara ya kikazi.Watendani na viongozi wazembe wanaipata freshi.Wanakiona cha mtema kuni. 

Tayari Mkurugenzi na Mkuu wa Wilaya ya Malinyi wako pembeni.Madudu ambayo amekutana nayo Waziri Mkuu aliamua kuchukua hatua kwa nafasi yake kimamlaka na mengine akaacha kwa Rais.Kama unavyojua tena Rais Magufuli hana muda wa kuvumilia mambo ya hovyo.Ametengua nafasi za viongozi hao. 

Kama kuna muungano mzuri na wenye tija katika kutenda kazi ya kuwatumikia Watanzania basi ni huu unaoneshwa na Rais pamoja na Waziri Mkuu.Katika soka huwa nawafananisha na wachezaji maalufu duniani ambao ni Christiano Ronaldo na Lionel Mess.Wachezaji hao kila mmoja anakuwa uwanjani acha kabisa.Ni mafundi wanaojua kutafuta ushindi kwa ajili ya timu zao. 

Hadi leo ni ngumu kujua nani zaidi kati ya Mess na Ronaldo.Kwa utendaji kazi wa Rais Magufuli na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa hawana tofauti na wachezaji hao. 

Wanajua wanachokifanya kuhakikisha Tanzania inashinda katika mapambano ya kiuchumi na hatimaye kuwa na maendeleo.Wanahakikisha wanashinda katika kurudisha nidhamu kwa watendani wa umma. 

Ingekuwa ni wanasoka basi ningesema Rais ni Mess na Waziri Mkuu ni Ronaldo.Sio mfano mzuri kwa wazee wangu hawa lakini nia yangu ni kujaribu kuwaelezea kwa namna ambavyo huenda watu wakanielewa.Niombe msamaha kwa kutoa mfano huo.Sina nia mbaya. 

Pia najua baada ya Rais Magufuli kuamua kuwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa vyovyote vile kuna mambo walizungumza na kukubaliana.Sina hakika walizungumza nini lakini leo hii naomba nieleze kitu.Nataka kuwaza kile ambacho walikubaliana. 

Huenda hawakuzungumza mambo mengi lakini moyo wangu eti unaniaminisha kuwa Rais Magufuli na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa walipokutana kwa mara ya kwanza baada ya mazungumzo yao ya kuhusu Tanzania mpya wakamalizia na wimbo huu;Tuimbe wote tena mkono ukiwa umeweka kifuani na itapendeza ukiwa upande unaokaa moyo. 

Tuanze kuimba; 


KIITIKIO(1) 

Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote 
Nchi yangu Tanzania jina lako ni tamu sana 
Nilalapo nakuota wewe 
niamkapo ni heri mama we! 
Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote 

UBETI WA KWANZA 

Tanzania Tanzania ninapokwenda safirini kutazama maajabu, biashara nayo makazi 
Sitaweza kusahau mimi mambo mema ya kwetu kabisa 
Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote 


KIITIKIO(MARA 1) 

Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote 
Nchi yangu Tanzania jina lako ni tamu sana 
Nilalapo nakuota wewe 
niamkapo ni heri mama we! 
Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote 


UBETI WA PILI 

Tanzania Tanzania watu wako ni wema sana, 
Nchi nyingi zakuota nuru yako hakuna tena, 
Nawageni wakukimbilia ngome yako imara kweli we, 
Tanzania Tanzania heri yako ni kwa mataifa 

KIITIKIO 

Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote, 
Nchi yangu Tanzania jina lako ni tamu sana, 
Nilalapo nakuota wewe, 
niamkapo ni heri mama we! 
Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote, 


UBETI WA TATU 

Nchi nzuri Tanzania, karibu wasio kwao, 
Wenye shida na taabu hukimbizwa na walowezi, 
Tanzania yawakaribisha mpigane kiume chema we, 
Tanzania Tanzania mola awe nawe daima. 

Nimeamua kuweka mashairi wa wimbo huo nikiamini mengi ambayo yanafanywa na viongozi hao utaona yanauhusiano mkubwa na yaliyomo katika mashairi ya wimbo huo.Ndio.Soma beti moja baada ya nyingine.Kisha changanua kisha tafsri matendo ya viongozi hao katika kuwatumikia Watanzania.Inatosha kwa leo. 

KWA HERUFI KUBWA KAMA VIPI TUWASILIANE KWA 0713833822

Malinzi aieleza mahakama kuwa alikuwa akilipwa fedha kwa taratibu za uendeshaji wa TFF

$
0
0
Na Mwandishi wetu, Globu ya Jamii
ALIYEKUWA Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Jamal Malinzi ameieleza mahakama ya hakimu mkazi  kisutu  kuwa alikuwa akilipwa fedha na TFF kwa taratibu za uendeshaji wa shirikisho hilo na wala hajawahi kujaza fomu ya madai ya ulipwaji wa fedha  na wala hajawahi kutoa maelekezo ya jinsi ya upokeaji wa fedha hizo.

Malinzi ameeleza hayo leo Septemba 18,2019 mbele ya Hakimu Mkazi Maira Kasonde  wakati akijibu maswali ya wakili  wa serikali kutoka Takukuru Leonard Swai.

Amedai kuwa fedha hizo zililipwa kupitia kwa Shadi wa 10 Hellen Ushahidi wa 12 Miriamu Zayumba na nyingine zilikuwa zikiingizwa kwenye akaunti.

Amedai katika shtaka la 16-25 inaonyesha kuwa alilipwa fedha na TFF, lakini  fedha hizo zililipwa kwa utaratibu na sio kweli kwamba aliwahi kutoa maelekezo ya upokeaji wa fedha hizo na kuongeza kudai kuwa, hundi na vocha zilizotolewa mahakamani ni baadhi kwani kuna zingine hazikuletwa mahakamani kama ushahidi.

Akiendelea kutoa ushahidi alidai aliwahi kufadhili mbio za wabunge (bunge marathon) kwa mika 7 toka miaka1997 hadi 2004 kuutangaza mchezo wa ngumi,mchezo wa golfu  pamoja na kujenga uwanja.

Amedai wakati anafadhili mbio hizo, Spika wa wakati huo pamoja na mwenyekiti wa bunge hawakumbuki ila anayemkumbuka ni  kiongozi wa timu hiyo  marehemu Joeli  Bendera na baadae alifuatiwa na William Ngeleja na kwamba fedha zilitoka Cargo Star na nyaraka za kumkabidhi fedha Bendera  na Ngeleja zipo Cargo Star.

"Fedha  hizo kwenye risiti zilikuwa zikiandikwa kulipwa mkopo na  nyingine marejesho ya mkopo na wala sikuwahi kumkabidhi mtu yoyote nyaraka za malipo" amedai 

Malinzi bado anaendelea kuhojiwa kutokana na ushahidi wake wa utetezi, kesi hiyo itaendelea kesho

Mbali na Malinzi, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni aliyekuwa Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa, Mhasibu wa TFF, Nsiande Mwanga na Karani Flora Rauya.

Katika kesi  hiyo ya jinai namba 213 ya mwaka 2017 washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 20 yakiwamo ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa fedha wa Dola za Marekani 173,335.

WANANCHI BUNJU WAIBA MAJI NA KUJITENGENEZEA BWAWA LA UMWAGILIAJI

$
0
0
Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) imeendelea na zoezi la ukaguzi wa miundo mbinu ya maji katika Mikoa ya  kihuduma ya DAWASA  ambapo katika mtaa wa Bunju A katika kata ya Bunju wamegundua uhujumu mkubwa wa miundombinu ya maji inayofanywa na wananchi.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanya ukaguzi huo Meneja Mapato wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Edger Zawayo amesema kuwa zoezi la kupambana na watu wanaochezea miundombinu ya maji linaendelea na katika eneo hilo la Bunju A, wamekuta Bomba lililokuwa linaenda kwa mteja limehujumiwa katikati na maji hayo kutumika katika kilimo cha mbogamboga.

"Kama tulivyoona maji yaliyohujumiwa katikati kutoka kwenye bomba la mteja yameelekezwa katika bwawa na wanatumia pampu kumwagilia mchicha, nyanya na migomba kama tunavyoona hapa." ameeleza Zawayo.

Amesema kuwa mtandao wa DAWASA umesambaa katika jiji hilo hivyo ni vyema wakaenda kwenye ofisi husika ili wapate kuunganishwa na huduma hiyo na sio kuhujumu na kuwakosesha wananchi wengine huduma.

"Ofisi za DAWASA zimesambaa kila sehemu ndani ya jiji la Dar es Salaam hivyo ni vyema kila mwananchi mwenye uhitaji wa maji aje kulipia na atapata huduma hiyo, haipendezi kuhujumu huduma ya maji ambayo mteja ameilipia hali inayowapelekea wateja wengine  kununua maji baada ya wananchi wasio wema kuhujumu huduma hiyo." Amesema  Zawayo

Aidha amesema kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa kwa yeyote atakayebainika amehujumu miundombinu ya maji kwa namna yoyote ile.

Kwa upande wake Afisa mtendaji wa mtaa wa Bunju A katika kata ya Bunju Maombi Lameck amesema kuwa baadhi ya wananchi wamekuwa sio waaminfu baada ya kuhujumu miundombinu ya DAWASA kwa kukata mabomba ya wateja na kuelekeza maji katika bwawa ambalo hutumika katika kilimo cha mbogamboga.

Maombi ametoa rai kwa wananchi wote wa Bunju A na Manispaa ya Kinondoni kwa ujumla kuacha mara moja tabia ya kuhujumu miundombinu ya DAWASA na miundombinu mingine ya Serikali kwa kuwa wanakwamisha maendeleo kwa kiasi kikubwa na yeyote atakayebainika anahujumu miundombinu hiyo kwa namna yeyote ile atachukuliwa hatua kali za kisheria.
 Meneja Mapato wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Edger Zawayo akionesha bwawa lililojanzwa na baadhi ya wananchi wa mtaa wa Bunju A kutoka kwenye Bomba la DAWASA kwa ajili ya umwagiliaji wa Mbogamboga zinazolimwa eneo hilo.
 Mtaalamu wa Mambo ya Mita kutoka Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Da es Salaam (DAWASA) Mohammed Mwakimila akionesha moja ya bomba lililokuwa linaenda kwa mteja likiwa limehujumiwa na maji hayo kwa kujaza bwawa na kutumika katika kilimo cha mbogamboga katika mtaa wa Bunju A kata ya Bunju jijini Dar es Salaam leo.
 Meneja Mapato wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Edger Zawayo akionesha bomba la pili lililokatwa na kuelekenzwa kwenye Bwawa kwa ajili ya kutunza maji ya kumwagilia Mbogamboga zinazolimwa na kumkosesha mwenye bomba hilo maji eneo hilo la Bunju A kata ya Bunju jijini Dar es Salaam .
 Baadhi ya mabomba yaliyokuwa yanatumika kuvutia maji kutoka kwenye bwawa hilo lililokuwa linatunzia maji ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA)
 Muonekano wa Bwawa la lililojazwa maji ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) mara baada ya wananchi wasiowaaminifu kukata bomba la Mamlaka hiyo na kulielekezea kwenye bwawa hilo kwa ajili ya umwagiliaji wa Mbogamboga zinazolimwa eneo hilo.
 Meneja Mapato wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Edger Zawayo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanya ukaguzi wa kustukiza kwenye shamba hilo na kukuta wizi wa maji kwa kiasi kikubwa katika mtaa wa Bunju A kata ya Bunju jijini Dar es Salaam leo.
 Afisa mtendaji wa mtaa wa Bunju A katika kata ya Bunju Maombi Lameck akizungumza na waandishi wa habari pamoja na kuwaasa wananchi wa eneo hilo kuacha tabia za wizi wa maji kwani watashughulikiwa mara baada ya kujione wizi wa Maji ya DAWASA katika shamba hilo.
Shamba la Nyaya likiwa limestawi karibu na bwawa lililokuwa linahifadhi maji ya wizi ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA).

TAMASHA LA NNE LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI - UTAMADUNI FESTIVAL (JAMAFEST2019) SEPTEMBA 21 hadi 28

$
0
0
MAHALI: Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam - Tanzania. HAKUNA KIINGILIO TAREHE: 21 hadi 28 Septemba, 2019 NCHI ZINAZOSHIRIKI : Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na South Sudan

WAZIRI UMMY MWALIMU NA RC MAKONDA WATINGA TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE

Benki ya NBC yazidi kutanua huduma zake kupitia Shirika la Posta

$
0
0
  Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya uwakala wa huduma za kibenki na Shirika la Posta nchini ili kupanua wigo wa huduma za benki hiyo sambamba na kurahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha hasa maeneo ya vijijini.

Hatua hiyo inatajwa kuwa itaongeza wigo wamtandao wa utoaji huduma za kifedha kwa njia ya kijiditi huku ikienda sambamba na azma ya serikali ya kupanua ushiriki wa wananchi katika shughuli za kifedha (financial inclusion).

Akizungumza katika hafla ya utiaji saini mkataba wa kutoa huduma za kubeki kati ya Posta na NBC jijini Dar es Salaam leo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe alisema kupitia mtandao wa ofisi za Shirika la Posta nchini lenye mtandao wa matawi 370, kutaiwezesha Benki ya NBC kuwafikia maelfu ya wananchi nchi nzima katika utoaji wa huduma zake za kibenki kwa gharama nafuu.

“Ushirikiano huu kati ya NBC na Posta utawezesha ukusanyaji wa kodi na maduhuli ya serikali kwa urahisi zaidi. Kwani ulipaji wa kodi na ukusanyaji wa maduhuli ya serikali yatafanyika katika mazingira salama na rafiki kwa wananchi kupitia ofisi za Posta. Wafaidikaji wa ushirikiano huu kati ya NBC na Posta sio tu wateja bali watakuwepo wastaafu, wanafunzi, wakulima, wazazi, na wafanyabiashara.’’ Alisema

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi alisema ushirikiano huo utawawezesha kutumia mifumo ya kidijitali na wingi wa ofisi za posta katika kutoa huduma za kibenki nchi nzima.

“Kwa sasa NBC ina mawakala wapatao 2,000 na hivyo kuungana na Shirika la Posta, kupitia mtandao wa ofisi zake 370, kutatuwezesha kuongeza idadi ya wananchi watakaofikiwa na huduma za kibenki kwa ukaribu.’’ alisema

Aliongeza kuwa ushirikiano huo, ni utekelezaji wa maelekezo ya serikali kwa mabenki ya kupeleka huduma ya kifedha kwa wananchi hasa walioko mikoani na vijijini. Kwa upande wake Posta Masta Mkuu, Hassan Mwang'ombe alisema kwa kuanza shirika hilo na NBC wataanza kutoa huduma katika ofisi 99 zilizo maeneo mbalimbali nchini.

“Huduma hizi ni zile zote za kibenki, kukusanya mapato ya serikali, kuhamisha na kutuma fedha, kufungua akaunti pamoja na huduma nyingine za kibenki.

“Katika kuimarisha shirika kibiashara na kurahisisha wananchi wapate huduma kwa ukaribu shirika tayari linashirikiana taasisi kadhaa ikiwemo Benki ya Posta, Necta, MSD, Tanesco, NIC, mifuko ya hifadhi ya jamii, mashirika na makampuni mbalimbali,” alisema.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta nchini Luteni Kanali Mstaafu Dk. Haroun Kondo alisema kulingana na mageuzi ya kimfumo na maboresho mbalimbali yanayofanywa sasa na shirika hilo, yatatoa nafasi bora kwa taasisi na makampuni mbalimbali kuvutiwa kuweka ofisi au kuingia ubia wa kutoa huduma au uwakala wa huduma zake.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (wa kwanza kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Luteni Kanali Mstaafu Dk. Haroun Kondo (wa pili kulia) na Mkurugenzi wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kushoto) wakifurahia uzinduzi wa uwakala wa huduma za kibenki kati ya Shirika la Posta na NBC ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha hasa maeneo ya vijijini. Hafla hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kulia) na Posta Masta Mkuu, Hassan Mwang'ombe (kushoto) wakisaini mikataba ya ushirikiano katika utoaji huduma za kubeki kati ya Shirika la Posta na Benki ya NBC ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha hasa maeneo ya vijijini.
Mkurugenzi wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kulia) na Posta Masta Mkuu, Hassan Mwang'ombe (kushoto) wakionesha mikataba ya makubaliano ya utoaji huduma za kubeki kati ya Shirika la Posta na NBC ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha hasa maeneo ya vijijini. Anaeshuhudia Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (katikati). Hafla hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kulia) na Posta Masta Mkuu, Hassan Mwang'ombe (kushoto) wakijipongeza mara baada ya kusaini mikataba ya makubaliano ya utoaji huduma za kubeki kati ya Shirika la Posta na Benki ya NBC ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha hasa maeneo ya vijijini. 

BANDARI KAVU YA ISAKA KUONGEZEWA UWEZO KUPITIA MRADI WA UBORESHAJI WA RELI YA KATI DAR - ISAKA

$
0
0

Mradi wa Uboreshaji reli ya kati Dar - Isaka umepelekea kuongeza uwezo wa kupokea, kuhifadhi na kupakua mizigo Bandari Kavu ya Isaka, Uboreshaji huo unaendelea hivi sasa na matarajio ya kukamilika kwa mradi mwaka 2021.

Lengo la kuboresha bandari Kavu ya Isaka ni kuongeza ufanisi wa utoaji huduma za usafirishaji  mizigo kati ya Dar es Salaam, maeneo ya nyanda za Kaskazini na nchi jirani za Rwanda, Congo na Burundi ambazo zimekuwa zikitumia bandari kavu ya Isaka kusafirisha mizigo.

Mradi wa Uboreshaji wa Reli ya Kati unatekelezwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa lengo la kuboresha reli ya kati kutoka Dar es Salaam hadi Isaka yenye urefu wa KM 970. Reli hii ilijengwa zaidi ya miaka 100 na Mkoloni, ili kuleta ufanisi wenye tija kwa TRC, kuhakikisha uwepo wa usafiri wa uhakika, haraka na kuaminika wa treni utakaoziunganisha Bandari ya Dar es Salaam na Bandari Kavu ya Isaka.

Maafisa wanaondaa Gazeti la Reli na Matukio TRC walifika  eneo ya Stesheni ya Isaka mkoani Shinyanga, eneo ambalo Mradi wa wa uboreshaji  wa reli kati - TIRP unaishia kwa awamu ya kwanza na kuzungumza na Meneja Mradi wa TIRP kipande cha Itigi – Isaka Mhandisi Benard Mbonde ambaye amesema kuwa reli zilizopo eneo la Stesheni zinatarajiwa kurefushwa na kuongeza njia za kupishania ndani ya Bandari kavu, njia zitakazokuwa zikipitisha treni kwa ajili ya kupakua na kupakia mizigo hivyo eneo hilo litaweza kupokea treni nyingi zaidi za mabehewa ya mizigo.

Aidha Mhandisi Mbonde ameeleza kuwa kufunga njia kwa Saa 72 kumekuwa na manufaa makubwa katika utekelezaji wa mradi huo kwani kasi ya uboreshaji imeongezeka, amesema kuwa kabla ya kupewa muda wa saa 72 kazi zilikuwa zikisuasua lakini mara baada ya kupewa muda wa saa 72 wameweza kufanya kazi kwa kasi kubwa na ufanisi.

“Nashukuru uongozi wa  Shirika la Reli Tanzania, unaoongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa TRC Ndugu Masanja zkungu Kadogosa kwa maamuzi ya busara na yenye kuleta tija kwa TRC na maslahi ya taifa".

Aliongeza kuwa "kabla ya kupata saa 72 wakandarasi walikua na uwezo wa kutandaza reli umbali wa Mita 200 pia katika uboreshaji wa tuta wakandarasi walikua wanasuasua, lakini baada kupata Saa 72 wakandarasi wameweza kuondoa reli ya zamani na kuweka reli mpya kipande cha zaidi ya Kilometa 30 na mpango wa saa 72  ulianza rasmi tarehe 12 Julai 2019, hivyo TRC imeweza kufanya kazi kubwa ndani ya muda mfupi” amesema Mhandisi Mbonde

Bandari kavu ya Isaka ilisajiliwa mwezi Septemba Mwaka 1999 kwa lengo la kuisogeza Bandari ya Dar es Salaam karibu na nchi za Rwanda, Burundi, DRC(Congo) na Uganda.

Kukamilika kwa Mradi wa uboreshaji wa reli ya kati kutawawezesha wafanyabiashara kusafirisha mizigo yao kwa haraka na kwa kiwango kikubwa kutoka bandari ya Dar es Salaam hadi Bandari kavu ya Isaka na hatimaye kwenda nchi jirani za Rwanda, Congo na Burundi.


Kutokana na haya yanayoendelea  katika uboreshaji wa miundombinu ya Reli,  TRC inawakumbusha watanzania kuendelea kuunga mkono Juhudi zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Jemedali, Rais Dkt. John Pombe Magufuli, katika ulinzi wa miundombinu ya Reli kwa maana ya kuwa Reli hizi ni mali za watanzania na zinaboreshwa na kujengwa kwa fedha za watanzania .


UJUMBE WA DKT. NDUMBARO KWA MAAFISA UTUMISHI NA WAAJIRI NCHINI

$
0
0
Ujumbe wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro kwa Waajiri na Maafisa Utumishi nchini alioutoa akiwa katika ziara ya kikazi Wilayani Sengerema.

RAIS MAGUFULI AFUNGUA KIWANDA CHA PIPE INDUSTRIES DAR ES SALAAM

LEO NI SIKU YA KUZALIWA KAMANDA MKUU WA FFU UGHAIBUNI AKA NGOMA AFRICA BAND RAS EBRAHIM MAKUNJA

$
0
0
 Siku ya leo 19 September ndio siku ya kuzaliwa mkuu wa bendi ya Ngoma Africa aka FFU ya kule Ujerumani, mwanamuziki Ebrahim Makunja aka kamanda Ras Makunja aka mkuu wa viumbe wa ajabu "Anunnaki Aliens" alizaliwa mjini Dar-es-Salaam,
Akiwa mtoto wa kwanza wa kiume wa Bw.Jumanne Saleh Makunja Ngayonga (RIP) na Bi.Moza Hassan Seifu Mpili (Mama Makunja),
Mwanamuziki Kamanda Ras Makunja ni mtunzi na mwimbaji  mahili wa muziki wa dansi leo ndio Happy Birthday yake.
MICHUZI TV NA  MICHUZI BLOG KWA PAMOJA TUNASEMA HERI YA KUZALIWA KAMANDA NA MLEZI WETU WA HIARI!!!
Unaweza kuburudika na kusherekea naye katika kambi yao FFU-Ughaibuni 

PROF. KABUDI AKUTANA NA UJUMBE WA HISPANIA, WAAHIDI KUSAIDIA MIRADI MBALIMBALI IKIWEMO SOKA

DKT TULIA AENDELEA KUCHANGIA MASUALA YA ELIMU MKOANI MBEYA,AZINDUA CHUMBA 'TULIA TRUST COMPUTER LAB'

$
0
0
September 18, 2019 Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson amefanya uzinduzi wa chumba cha Kompyuta  kilichopewa jina la 'TULIA TRUST  COMPUTER LAB ' kilichopo katika Shule ya Sekondari Samora Machel iliyopo mkoani Mbeya ili kuwawezesha Wanafunzi kuweza kujifunza masomo ya computer kwa vitendo ili kuendana na teknolojia iliyopo sasa.

Awali Dr. Tulia aliwezesha shule hiyo kupata  Kompyuta  tano za kuanzia, na baadaye aliwahidi kuwaongezea  Kompyuta nyingine pamoja na mashine za kuchapisha mitihani na kutolea copy.

Katika hotuba yake Dkt. Tulia amesema ”Kwakweli nimekutana na maajabu makubwa sana kwa hii hatua mliyofikia ya kujenga chumba hiki kizuri na kikubwa ingawa zimetajwa baadhi ya changamoto ikiwemo uchache wa Computer kwakuwa wanafunzi ni wengi, mimi niahidi tu kwamba nitaleta Computer nyingine hapa ili kuweza kumudu idadi ya wanafunzi”

“Nimeelezwa pia watoto wote hapa kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita wanakaa mitaani ambapo ni changamoto kwao, kwenye hili niseme tutatafuta wadau na ikiwezekana tuanze kujenga mabweni kwa ajili ya watoto hawa lakini napenda tuanze na mabweni ya watoto wa kike kwasababu hawa changamoto zao ni kubwa zaidi ukilinganisha na wakiume ingawa tungetamani tujenge yote hivyo kwa kuanza tutaanzia hapo”-Dr. Tulia Ackson
Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson (katikati ) akikata utepea kuashiria uzinduzi wa chumba cha Komyuta kilichopewa jina la TULIA TRUST kilichopo katika Shule ya Sekondari Samora Machel iliyopo mkoani Mbeya, ili kuwawezesha Wanafunzi kujifunza masomo ya kompyuta kwa vitendo ili kuendana na teknolojia iliyopo sasa.
Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson (katikati ) akiwasalimia wanafunzi wa Shule ya Sekondari Samora Machel iliyopo mkoani Mbeya, alipowasili kuzindua chumba cha Komyuta kilichopewa jina la TULIA TRUST 
Picha ya pamoja


SERIKALI INATEKELEZA MIRADI YA UJENZI WA MADAMPO YA KISASA NCHINI KUWEZESHA WANANCHI KUPATA ENEO LA KUTUPIA TAKA NGUMU

$
0
0
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Suleimani Jafo akizungumza wakati wa ziara yake kwenye dampo la Kisasa la Jiji la Tanga kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
AZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Suleimani Jafo katikati akitembelea dampo la kisasa la Jiji la Tanga leo wakati wa ziara yake kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa na Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Suleimani Jafo kushoto akitembelea dampo la kisasa la Jiji la Tanga leo wakati wa ziara yake kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa na Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji akifuatiwa na Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji
Muonekano wa dampo la kisasa la Halmashauri ya Jiji la Tanga

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Suleimani Jafo amesema serikali inatekeleza mradi wa ujenzi wa madampo ya kisasa kwenye majiji mbalimbali hapa nchini ili kuwezesha wananchi kupata eneo la kutupia taka ngumu ambazo zimekuwa zikizalishwa. 

Aliyasema hayo leo wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa kwenye Halmashauri ya Jiji la Tanga ambapo pia alitembelea dampo la kisasa linalojengwa eneo la Mabokweni Jijini humo huku akionyeshwa kuridhishwa na ujenzi huo.Alisema madampo hayo ya kisasa yatakuwa na msaada mkubwa ya kuondosha changamoto ya taka ngumu ambazo zinazalishwa kwenye maeneo mbalimbali na kukosa eneo la kuhifadhi

“Madampo haya yamekwisha kujengwa na kukamilika majiji nchini likiwemo Jiji la Arusha lengo likiwa kuhakikisha taka ngumu zinazozalishwa ziweze kufika eneo la dampo lililokuwa sahihi zaidi”Alisema Waziri Jafo.

“Kwa kweli niwashukuru Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji umekuwa wa mfano nchi nzima pamoja na watendaji wako na madiwani mmefanya kazi kubwa na nzuri sana huwaga sipendi kusifu vitu vya hovyo lakini kwa hili mnastahili Pongezi”Alisema

“Sipendi kusifu vitu vya hovyo lakini Tanga jiji mnastahili Pongezi mmetoa fedha bilioni 6 kwa ajili ya mradi huu mpaka sasa kati ya Bilioni 9 niwapongeze dampo hili ni la kipekee ambalo lenye ekari 75 zote mmeliwekea ukuta wa kisasa kama ule wa mererani wengine wachovu hawawezi kufanya hivyo”Alisema

Waziri huyo aliwataka viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam waenda kujifunza Tanga ili waone namna wanavyotekeleza miradi iliyopo kwenye maeneo yao na kuweza kuleta tija kubwa na ufanisi kama ulivyokuwa mradi huo.

“Tunataka wengine waige utendaji wa Jiji la Tanga Mkurugenzi Mayeji wewe ni mkurugenzi Supa sana ...Jiji la Dar es Salaam tumewapa fedha kwa ajili ya ujenzi wa machinjia vingunguti,soko la magomeni,soko la kisutu,kuimarisha ufukwe wa coco beach lakini hata hizo ambazo zimefanyika ni kwa ajili ya mikimiki watu wanataka mpaka Waziri uenda ndio watekeleze”Alisema

Aidha alisema hiyo sawa kabisa lazima viongozi waliopewa dhamani ya kusimamia mikoa, wilaya kila huku akieleza kwamba haipendezi mpaka waziri aende akasimamie mchakato wa manunuzi.

“Leo Dar kila mradi lazima watu wagombane ujenzi wa stendi ya Mbezi Luis watu wanaogomba jinsi ya kumpata nani mkandarasi ili aweze kujenga..leo hii pale Coco Beach watu wanagombania ni ubabaishaji tu kila mtu anakuja na mkandarasi wake mkononi lakini Tanga ukija kila mradi umesimaia vizueri”Alisema

Hata hivyo alisema kwamba Mkurugenzi Jiji la Tanga umekuwa wa mfano bora wa kuigwa yeye na watendaji wake ,meya na baraza la madiwani wa Tanga ni la mfano wea kuigwa kwenye maeneo mengo kwa maana mnatekeleza wajibu wenu ipasavyo.

BBC SWAHILI: DIRA YA DUNIA JUMATANO 18.09.2019


WAZIRI MWAKYEMBE AFUNGA MKUTANO WA MANAIBU WAZIRI WA SADC JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Mchezo Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza wakati akifunga mkutano wa Mkutano wa Mawaziri wa SADC wa Sekta ya TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa wanaokutana kuanzia Septemba 16-18, 2019 jijini Dar es Salaam. Na unatarajia kumalizika Septemba 19-20, 2019. Picha zote na Matokeo Chanya+.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Mchezo Dkt. Harrison Mwakyembe na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Sekta ya Uchukuzi Bw. Leonard Chamriho wakifuatilia wakati wa kufunga mkutano wa Mkutano wa Mawaziri wa SADC wa Sekta ya TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa wanaokutana kuanzia Septemba 16-18, 2019 jijini Dar es Salaam. Na unatarajia kumalizika Septemba 19-20, 2019.
Manaibu waziri wa wa SADC wa Sekta ya TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa wakifuatilia.

NEWS ALERT: SERIKALI YATANGAZA AJIRA MPYA 477 AFYA

$
0
0

SERIKALI imetangaza ajira mpya kwa watumishi 477 kwa kada ya Afya ambao watawasaidia kwenye mamlaka za Serikali za Mitaa kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Tanga Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Suleiman Jafo (pichani) alisema kwamba Tamisemi imepata kibali cha ajira ya watumishi hao Julai 12 mwaka huu na utekelezaji wake ulianza Julai 22 mwaka huu kwa kutangaza nafasi hizo.

Alisema kwamba walitangaza nafasi hizo kwa kutumia mfumo wa kieletroniki wa maombi ya kazi kwa ajili ya waombaji wenye sifa kuomba nafasi hizo ambapo maeneo 14 walikuwa wakihitaji watumishi waweze kuwasaidia kwenye mamlaka za serikali za mitaa.


Alisema kwamba eneo la kwanza ni kupata madaktari daraja la pili ambao walihitajika 44,tabibu daraja la pili 100 ,tabibu msaidizi 19,Afisa Muuguzi daraja la pili 5,afisa muunguzi msaidizi daraja la pili 33,muunguzi daraja la pili 119,tenkolojia daraja la pili upande wa maabara 3.

Aidha alisema kwamba maeneo mengine ni teknolojia msaidizi wa maabara 4,teknolijia daraja la pili kuhusu dawa wanne, teknolojia daraja la pili upande wa mionzi 44,mtoa tiba kwa vitendo daraja la pili 1,Afisa afya mazingira daraja la pili 8,Afisa Afya Mazingira msaidi daraja la pili 29 .

Waziri Jafo alisema kwamba nafasi nyengine ni wahuduma wa afya 64 huku akieleza kwamba zoezi la uchambuzi huo lilianza Agosti 12 mwaka huu hadi 28.8,2019 ambapo jumla ya waombaji wote walikuwa 20237.

Alieleza kwamba kati yao waliomba wenye sifa ni 2644 na waombaji 17593 hawakuwa na sifa za kuajiriwa kwa mujibu wa tangazo la ajira kutokana na sababu mbalimbali kama ikiwemo uchambuzi wa sifa ambao ulizingatia mambo sita .

Alisema jambo la kwanza ni uwepo wa nakala ya kidati cha nne au sita, pili uwepo wa nakala za cheti cha taaluma na tatu uwepo wa nakala ya cheti cha kuzaliwa, uwepo wa nakala ya cheti cha usajili kamili au leseni ya kufan ya kazi inayotolewa na mabaraza ya kitaalamu.

Aidha alisema pia kwamba lazima uwepo wa nakala ya vyeti v ya kidato cha nne au sita na uwepo wa nakala ya cheti cha nacte kwa waombaji wote wa ngazi za cheti na diploma kwa waombaji wote ya koazi husika kwa waliomaliza septemba 2015 na kuendelea.

Alisisitiza kwamba hivyo vilikuwa miongoni mwa vigezo kwa waombaji hao 17593 wengine waliowasilisha taarifa zao zikiwa na mapungufu ya hapa na pale wakati wanafanya uchambuzi kwenye baadhi ya changamoto kulikuwa na waombaji wengi.

Alisema pia uwepo wa waombaji wachache kwa kada ya mionzi wakati waliotangaza walikuwa wakihitaji watu wa mionzi 44 lakini walioomba walikuwa 46 lakini kati ya hao waombaji 25 ndio walikuwa wana sifaa na 19 waombaji walikuwa wamepungukiwa na sifa pia uwepo idadi kubwa ya waombaji wasiokidhi vigezo.

“Niwapongeze waombaji wote waliopata nafasi na nisistiza maekelezo yafuatayo kuripoti kwenye vituo vya kazi kwa muda wa siku kumi na nne kuanza leo hii na wale ambao watashindwa kufanya hivyo nafasi zao zitajazwa na waombaji wengine haraka sana”Alisisitiza.

Hata hivyo aliwakumbusha kuhakikisha wakati wa kuripiti wanakwenda na vyeti halisi vya kidato cha nne,sita ,chuo kikuu,nacte na vyeti halisi vya usajili wa baraza la kitaalumu ambao watapaswa kuwasilisha kwa mwajiri kabla ya kupata barua ya ajira.

“Lakini pia niseme kwamba kuripoti na transcript pekee bila kuwa na cheti halisi hatopokelewa hivyo ni muhimu waliotangazwa waende na vyeti vyao halisi na watakaoshindwa kuwasilisha vyeti watakuwa wamekosa sifa”Alisema

Hata hivyo aliwataka waombaji waliopata nafasi za ajira watambue kwamba hawatakuwa na nafasi wa kubadilisha vituo vyao vya kazi huku akisisitiza kwamba watakaoshindwa kuripoti nafasi zao zitajazwa na watu wengine.

Waziri huyo alisema kwamba watawapeleka kwenye maeneo yenye changamoto ya watumishi ambao wameomba na kutokupata fursa wasisite kuomba tena huku akiwataka wakurugenzi kuwapokea na kuhakiki vyeti vyao ikiwemo kuwapatia mafunzo .

BADO HATUJANUFAIKA NA BIASHARA YA ZIWA VICTORIA -ULEGA

$
0
0

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amesema ni vyema shughuli za uvuvi zikarasimishwa ili wavuvi waweze kunufaika kupitia sekta hiyo kwa kupata mikopo kutoka katika taasisi za kifedha pamoja na kuchangia kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii.

Naibu Waziri Ulega amesema hayo Wilayani Muleba Mkoani Kagera wakati wa kikao na wawakilishi kutoka taasisi za kifedha, mifuko ya hifadhi ya jamii pamoja na baadhi ya wavuvi wa wilaya hiyo, ambapo amesema sekta ya uvuvi nchini zikiwemo shughuli zinazofanywa kwenye Ziwa Victoria bado hazijatoa mchango wa kutosha katika pato la taifa.

“Jumla ya thamani ya biashara ya mazao ya samaki kwa mwaka mmoja kwa Ziwa Victoria katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda inakadiriwa kuwa Shilingi Trilioni 6 wakati Tanzania inapata Shilingi Trilioni 1.6 wakati inamiliki eneo kubwa la ziwa ilhali Uganda na Kenya zinazomiliki eneo dogo zinapata Shilingi Trilioni 4.4 tafsiri yake ni kwamba bado hatujanufaika vya kutosha na Ziwa Victoria” Amesema Mhe. Ulega

Kufuatia hali hiyo Naibu Waziri Ulega ametaka shufghuli za uvu vi ziweze kurashimishwa na wavuvi waweze kupata mikopo ile kukuza sekta hiyo ambayo imekuwa ikitegemewa katika kuchangia pato la taifa na mtu mmoja mmoja.

Katika ziara hiyo pia Naibu Waziri Ulega ametembelea kijiji cha Mulela kilichopo Kata ya Kishanda na kutoa ahadi ya Shilingi Milioni Mbili kukarabati josho la kijiji hicho pamoja na kuwataka wananchi kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. John Magufuli ambaye amekuwa anakusanya mapato ili kumletea mwananchi maendeleo kwa kuboresha huduma mbalimbali za jamii.

Imetolewa: Kitengo cha Mawasiliano serikalini
Wizara ya Mifugo na Uvuvi
19.09.2019

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme stembelea NFRA kanda ya Songea

$
0
0
 Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme kushoto akisaidiana na baadhi ya vibarua kusafisha mahindi alipotembelea Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula NFRA  kanda ya Songea kuangalia zoezi la ununuzi wa mahindi linavyoendelea ambapo hadi kufikia mwishoni mwa wiki NFRA tayari  imenunua tani zaidi ya 12,000  za mahindi kutoka kwa wakulima.
 Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme wa pili kushoto na kaimu meneja wa wakala wa Taifa wa Hifadhi ya chakula NFRA kanda ya Songea Eva Michael wa kwanza kushoto wakifanya kazi ya kusafisha mahindi yaliyoletwa na wakulima katika kituo kikuu cha kununulia mahindi eneo la Ruhuwiko mjini Songea wakati Mkuu wa mkoa alipotembelea kituo hicho kwa ajili ya kuangalia zoezi la ununuzi wa zao hilo linavyofanyika,ambapo Mkuu huyo wa mkoa alitangaza bei rasmi ya mahindi kuwa shilingi 600 kwa kilo.

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme akikusanya mahindi kabla ya kuwekwa kwenye magunia alipotembelea kituo cha kununua mahindi cha Wakala wa Taifa wa hifadhi ya chakula NFRA kanda ya Songea ambapo alitangaza kuwa Serikali  kupitia NFRA kununua zao hilo kwa shilingi 600 na kuwataka wakulima wa mkoa huo kupeleka mahindi yao NFRA ili wanufaike na bei hiyo. Picha na Muhidin Amri

VIWANJA VINAUZWA MWANZA

$
0
0

Viwanja vinauzwa bei nafuu kabisa.

Je wewe unahitaji kiwanja kwa ajili ya makazi au biashara?

kama jibu ni ndio basi wahi sasa ujipatie kiwanja au viwanja.

Viko sehemu nzuri Umeme na maji yapo.

Mahali Vilipo - Usagara - Mwanza karibu na NGASSECO ENGLISH MEDIUM.

Bei ni nafuu sana karibu na bure.

Kwa maelezo zaidi piga simu 0687 702 510 au 0755 563 538
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images