Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live

APOLLO YAKABIDHI MASHINE YA KUMWAGA LAMI KWA KAMPUNI YA MAYANGA

$
0
0

 Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Wakala wa Usambazaji wa mashine ya kumwaga Lami ya Dynapac Paver Kampuni ya Apollo Heavy Equipment wamekabidhi mashine ya kumwaga lami iliyotengenezwa nchini Ujerumani.

Kampuni hiyo leo wamekabidhi mtambo huo ukiwa ni wa pili kuingia nchini ndani ya mwaka.mmoja.

Mashine hiyo ya kumwaga lami kutoka kampuni ya Dynapac ya nchini Sweden imekabidhiwa kwa Kampuni ya Ukandarasi ya Mayanga inayojihusisha na uuzaji wa vifaa mbalimbali.

Akizungumza baada ya kukabidhi mtambo huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Appolo, Ruben Mwambene amesema wamekuwa mawakala wa kuleta vifaa vyote vinavyotengenezwa na kampuni ya Dynapac kwa miaka mitatu sasa. Amesema, mashine hiyo ya kumwaga lami ni wa pili ndani ya mwaka mmoja na wamekuwa wanauza mashine mpya na vipuli vyake. Mwambene amesema, "Ni miaka mitatu tumekuw mawakala wa kuleta mitambo na vipuli vyake kutoka kampuni ya Dynapac inayopatikana nchini Sweden ambao pia wamesambaa kwenye nchi tofauti duniani"

"Tumekabidhi mashine hii kwa kampuni ya Ukandarasi Mayanga ajili ya ujenzi wa barabara za Musoma na imani kubwa kila kitu kitaenda sawa,"

Amesema, mashine hizo zina ubora mkubwa na imara. Na wameweza kuikabidhi kwa kampuni ya Ukandarasi ya Mayanga kwa ajili ya ujenzi wa barabara za Musoma.
 MKURUGENZI Mtendaji wa kampuni ya Apollo Heavy Equipment Ltd, Reuben Mwambene, akikabidhi mashine ya kuwekea lami kwa mwakilishi wa kampuni ya Ukandarasi ya Mayanga, Arif Salim (kushoto), Dar es Salaam leo kwa ajili ya ujenzi wa barabara za Musoma.
MKURUGENZI Mtendaji wa kampuni ya Apollo Heavy Equipment Ltd, Reuben Mwambene (kulia), akimpa maelezo kuhusu mashine ya kuwekea lami kwa mwakilishi wa kampuni ya Ukandarasi ya Mayanga, Arif Salim (kushoto), wakati akimkabidhi mashine hiyo, Dar es Salaam leo kwa ajili ya ujenzi wa barabara za Musoma.


WATANZANIA WATAWEZESHWA ILI WASHIRIKI KUJENGA UCHUMI-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Tanzania imeendelea kuchukua hatua za makusudi kwa ajili ya kuwawezesha Watanzania washiriki kikamilifu katika kujenga uchumi wa nchi yao, ikiwa ni pamoja na kubadilisha sera na sheria zinazohusisha sekta mbalimbali ikiwemo mafuta, madini, bima na ununuzi wa umma.

Amesema lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha kuwa Watanzania wanapewa kipaumbele kwenye ajira, ununuzi wa bidhaa na huduma zao, uongezaji wa ujuzi na uhaulishaji wa teknolojia kupitia miradi hiyo ya kimkakati inayotekelezwa nchini.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Ijumaa, Septemba 20, 2019) wakati wa akifungaKongamano la Taifa la Ushiriki wa Watanzania katika Miradi ya Kimkakati ya Uwekezaji (Local Content) lililofanyika kwenyeukumbi wa LAPF jijini Dodoma.

“Nyote mtakubaliana nami kuwa ushiriki wa wananchi katika uchumi wa Taifa lao ni suala linalopewa kipaumbele katika nchi nyingi duniani kwa kuwa linachangia katika kukuza uchumi wa nchi husika.”

Amesema Serikali imeendelea kutoa kipaumbele kwenye huduma mbalimbali ikiwemo bima, huduma za benki, sheria na uhandisi. “Vilevile, mikataba mbalimbali ya ujenzi wa miundombinu pia imetoa kipaumbele kwenye ajira za Watanzania pamoja na bidhaa na huduma ambazo zinapatikana hapa nchini.”

Waziri Mkuu amesema Serikaliya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imeweka dhamira ya dhati ya kutekeleza Sera ya Viwanda inayolenga kuipeleka nchi katika uchumi wa kati ifikapo 2025.

Amesema jitihada za makusudi zimeendelea kufanyika ikiwa ni pamoja na kusimamia na kufanikisha utekelezaji wa malengo mbalimbali pamoja na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi 2015/2020.

Pia, Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa miaka mitano 2016/2017/2020/2021 ambao pamoja na mambo mengine una lenga kuimarisha upatikanaji wa stadi zinazohitajika viwandani, na stadi kwa ajili ya shughuli nyingine za uzalishaji na utoaji huduma.Amesema dhana ya ushiriki wa wananchi (Local Content) ni mojawapo ya nyenzo muhimu itakayowezesha Tanzania kufikia lengo la kuwa na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema iwapo bidhaa na huduma za Kitanzania zitatumika kwenye miradi ya kimkakati na uwekezaji unaofanyika hapa nchini viwanda vya ndani vitakua, malighafi zinazopatikana nchini zitapata soko la uhakika, ajira zitaongezeka na hivyo uchumi wa nchi utakua kwa kasi.

“Hakuna nchi yoyote ile duniani inayoweza kupiga hatua kubwa ya kimaendeleo na kufanikiwa bila ya kuweka dhamira na jitihada za makusudi za kuhakikisha kunakuwa na mazingira wezeshi kwa wananchi wake kushiriki ipasavyo kwenye shughuli za kiuchumi.”

Amesema Serikali itaendelea kuchukua hatua madhubuti ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mazingira ya kisera na kisheria yanaboreshwa kwa kuzingatia maslahi ya wananchi wake, hivyo Serikali itafanya kazi kwa karibu na sekta binafsi ili kuhakikisha malengo hayo yanafanikiwa kwa kuwa sekta binafsi ina mchango mkubwa katika kujenga uchumi wa nchi na kutoa ajira kwa Watanzania.

Waziri Mkuu amesema tarehe 21 Julai 2016, wakati alipozindua Kongamo la Taifa la Ushiriki wa Watanzania katika miradi ya kimkakati aliagiza kutengenezwa kwa Mwongozo wa Taifa wa Ushiriki wa Watanzania katika Uwekezaji (National Multi-sector Local Content Guidelienes). Mwongozo huo umekamila na ameuzindua leo pamoja na tovuti ya Miradi ya Kimkakati na Uwekezaji.

Tovuti hiyo, itakuwa na taarifa mbalimbali kuhusu miradi ya kimkakati, fursa zilizopo kwenye miradi hiyo pamoja na mipango na mikakati mbalimbali kuhusu masuala ya ushiriki wa wananchi kwenye miradi hiyo. Pia itawezesha kujenga uelewa wa umma kuhusu ushiriki wa wananchi kwenye miradi ya kimkakati na kufahamu changamoto zinazowakabili Watanzania katika ushiriki kwenye miradi mbalimbali ili kuzipatia suluhisho changamoto hizo.

Hivyo, Waziri Mkuu ameagiza Mwongozo wa Taifa wa Kisekta wa ushiriki wa Watanzania usambazwe kwa wadau mbalimbali ili waweze kufahamu majukumu walionayo katika kuwawezesha Watanzania kushiriki katika uchumi wa nchi. “Tujenge utamaduni wa kufuatilia tovuti ya Serikali ya miradi mikubwa ya kimkakati na uwekezaji ili kutambua fursa za kibiashara.

Kongamano hilo limehudhuriwa na Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilnith Mahenge, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi KiuchumiBeng’i Issa.

Wengine ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Salum Shamte, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Dkt. Festus Limbu pamoja na viongozi mbalimbali wa sekta ya umma na binafsi, wafanyabiashara, wanatlaaluma, watafiti, asasi za kiraia na vikundi mbalimbali vya wajasiriliamali. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizindua mwongozo wa Taifa wa ushiriki wa wananchi katika uwekezaji na tovuti ya miradi ya mikakati, kwenye Kongamano la Kitaifa la Ushiriki wa Watanzania katika Miradi ya Kimkakati, lililofanyika katika ukumbi wa LAPF jijini Dodoma. Septemba 20.2019
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa ameshika kitabu cha mwongozo wa Taifa wa ushiriki wa wananchi katika uwekezaji, baada ya kuzindua mwongozo huo, kwenye Kongamano la Kitaifa la Ushiriki wa Watanzania katika Miradi ya Kimkakati, lililofanyika katika ukumbi wa LAPF jijini Dodoma. Septemba 20.2019.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mwenyekiti wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Dkt. Festus Limbu, wakati akiwasili kwenye ukumbi wa LAPF jijini Dodoma, kufunga Kongamano la Kitaifa la Ushiriki wa Watanzania katika Miradi ya Kimkakati. Septemba 20.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Mwenyekiti wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Dkt. Festus Limbu, akizungumza na washiriki, kwenye Kongamano la Kitaifa la Ushiriki wa Watanzania katika Miradi ya Kimkakati, lililofanyika katika ukumbi wa LAPF jijini Dodoma. Septemba 20.2019.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Binilith Mahenge, akizungumza na washiriki, kwenye Kongamano la Kitaifa la Ushiriki wa Watanzania katika Miradi ya Kimkakati, lililofanyika katika ukumbi wa LAPF jijini Dodoma. Septemba 20.2019. 
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu,Jenista Mhagama, akizungumza na washiriki, kwenye Kongamano la Kitaifa la Ushiriki wa Watanzania katika Miradi ya Kimkakati, lililofanyika katika ukumbi wa LAPF jijini Dodoma. Septemba 20.2019. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akihutubia kwenye Kongamano la Kitaifa la Ushiriki wa Watanzania katika Miradi ya Kimkakati, lililofanyika katika ukumbi wa LAPF jijini Dodoma. Septemba 20.2019.

RAIS DKT MAGUFULI AFANYA UTEUZI NA MABADILIKO YA VIONGOZI MBALIMBALI LEO

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amemteua Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha, Lootha Sanare, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kuchukua nafasi ya Dkt. Steven Kebwe ambaye uteuzi wake umeteguliwa.


Akitangaza uteuzi na utenguzi huo leo Septemba 20, 2019 Katibu mkuu kiongozi  Balozi Mhandisi John Kijazi, ameeleza kuwa Rais amefanya uteuzi na mabadiliko kadhaa.

Aidha Rais Magufuli amemteua Musa Masele ambaye alikuwa msaidizi wa mkuu wa mkoa wa Geita, kuwa mkuu wa Wilaya ya Malinyi, Mkoani Morogoro.

Mbali na teuzi hizo pia Rais amefanya mabadiliko ambapo, Mkuu wa Wilaya ya Tarime Charles Kabeho, amehamishiwa wilaya ya Chato na Mkuu wa Wilaya ya Chato Msafiri Mtemi amehamishiwa Wilaya ya Tarime. 

Aidha, Rais Magufuli amefanya uteuzi wa mabalozi 12 watakaowakilisha Tanzania nchi mbalimbali, katika uteuzi huo wamo pia Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Benson Bana na aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Dk Modestus Kipilimba.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akisoma majina ya viongozi mbalimbali walioteuliwa ama waliobadilishwa vituo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 20, 2019 PICHA NA IKULU

RAIS DKT SHEIN AONGOZA KIKAO CHA KAMATI MAALUM CCM ZANZIBAR

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akikaribishwa na Wajumbe wa Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar,[Picha na Ikulu.] 20/09/2019. 
Baadhi ya Wajumbe wa Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa akiendesha kikao cha siku moja kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar,[Picha na Ikulu.] 20/09/2019.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akikaribishwa na Wajumbe wa Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar,[Picha na Ikulu.] 20/09/2019. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akiendesha kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar (kulia)Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdalla Juma Saadala,[Picha na Ikulu.] 20/09/2019.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiendesha kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.[Picha na Ikulu.] 20/09/2019.





Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdalla Juma Saadala mara alipowasili katika viwanja vya Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar alipohudhuria katika Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar kilichofanyika leo,[Picha na Ikulu.] 20/09/2019.

NEWZ ALERT: MAHAKAMA KUU YAMSIMAMISHA FATMA KARUME KAZI ZA UWAKILI KWA MUDA

$
0
0
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imemsimamisha kwa muda Wakili wa kujitegemea Fatma Karume kufanya kazi za uwakili, baada ya upande wa Serikali kulalamikia matamshi aliyoyatoa katika kesi ya kikatiba ya kupinga uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Adelardus Kilangi.

 Katibu Mwenezi wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu alifungua kesi ya kikatiba Mahakamani hapo akipinga uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Adelardus Kilangi

Aidha Jaji Kiongozi Dkt, Eliezer Feleshi ameitupilia mbali kesi hiyo akisema kwamba, imemjumuisha Rais na kwa msimamo wa Mahakama Kuu kufanya hivyo ni kinyume cha sheria

Tutawaletea habari kamili hivi punde.

Timu ya Kakoi yatinga robo Fainali michuano ya Chemchem CUP 2019

$
0
0


Mwandishi wetu,Arusha 

Timu ya soka ya Kakoi ya wilaya ya Babati mkoa wa Manyara,imefanikiwa kuingia robo fainali katika michuano ya Chemchem CUP ambayo inafanyika wilayani Babati baada ya jana timu ya Kazamoyo kushindwa kutokea uwanjani . 

Katika michuano hiyo, ambayo inaendelea katika eneo la Mdori, jumla ya timu 20 za soka zinashiriki na timu nne za mpira wa pete ambapo kiasi cha sh 70 milioni zimetolewa na Taasisi ya uhifadhi ya Chemchem kuendesha michuano hiyo. Timu ya Kakoi amefanikiwa kutinga robo fainali baada ya kujipatia pointi tatu jana na kufanya kuongoza kundi lake, ambapo awali iliitandika timu ya Kona Mbaya magori 5-0. 

Wafungaji katika mchezo huo, walikuwa ni Devis Severine ambaye alifunga magori matatu , Shaban Jabu gori moja na Buzuka Amani gori moja. 

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Katibu wa michuano hiyo, Beno Alfred alisema michuano hiyo, inashirikisha jumla ya timu kutoka vijiji 10, ambavyo vinaunda jumuiya ya jamii ya uhifadhi ya wanyamapori ya Burunge. 

"katika michuano hiyo, kuna makundi manne ambapo timu mbili kutoka kila kundi zinasonga mbele kwa ajili ya kuingia robo fainali. Mratibu wa michuano hiyo wa Taasisi ya Chemchem ambayo imewekeza shughuli za kitalii katika hifadhi hiyo, Walter Pallanyo, alisema kiasi cha milioni 4.5 kinatarajiwa kutolewa kama zawadi kwa washindi. 

Pallangyo alisema timu zote ambazo zinashiriki, zilipewa jezi na mipira kwa ajili ya michuano hiyo ambayo hufanyika kila mwaka. "lengo la michuano hiyo ni kuwashirikisha vijana katika vita dhidi ya ujangili lakini pia kujua thamani ya uhifadhi wa maeneo yao kwa shughuli za kitalii"alisema 

Timu ya Manyara ndio ilitwaa ubingwa katika michuano ya Chemchem mwaka jana. Timu za mpira wa pete ambazo zinashiriki ni timu ya Mwada, Mdori, Walimu na Ngolei

UJENZI WA MAHANDAKI YATAKAYOPITISHA RELI YA KISASA – SGR KATIKA MILIMA YA KILOSA WAZIDI KUNOGA

$
0
0
Mafundi wakiendelea na Ujenzi wa mahandaki yatakayopitisha reli ya kisasa katika milima ya Kilosa mkoani Morogoro
*************************************

Maendeleo ya ujenzi wa reli ya kisasa kwa kipande cha awamu ya pili Morogoro -Makutopora Singida wazidi kunoga umefikia zaidi ya 15% , ujenzi huu unaambatana na ujenzi wa Mahandaki 4 yatakayokuwa na jumla ya urefu wa Kilomita 2.6

Maendeleo ya ujenzi wa mahandaki washika kasi katika Milima ya Kilosa ambapo zaidi ya Mita 470 kati ya Mita 1030 zimechorongwa katika handaki namba 2, ujenzi wa handaki hilo umefika 45% hivi karibuni Septemba 2019.

Mpaka sasa wataalamu wanaendelea na hatua za ujenzi wa handaki hilo ambazo ni kuchoronga na kuimarisha kuta za handaki kwa kufunga nondo (reinforcement work) na kuweka zege kali (shotcrete application) ambapo hivi sasa kazi kubwa inayofanyika ni kuchimba Mita tatu kwenda chini ndani ya handaki ili kukamilisha urefu wa Mita 9.6 za handaki katika Kazi ya Uchorongaji wa Mahandaki iliyozinduliwa rasmi na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Atashasta Nditiye mapema Julai 22, 2019.

Sambamba na kazi kuanza rasmi baada ya maandalizi ya uchorongaji kukamilika katika eneo ambalo handaki namba 2 linajengwa. Katika hatua nyingine wahandisi wanaendelea na maandalizi ya uchorongaji wa handaki namba 1 litakalokuwa na urefu wa Mita 424, mahandaki haya yote yataunganishwa na Madaraja marefu ili kuepusha athari za mto Mkondoa ambao umekuwa ukiathiri miundombinu ya reli za zamani mara kwa mara.

Kukamilika kwa ujenzi wa Handaki namba mbili kati ya mahandaki 4 yanayojengwa eneo la Kilosa kutalifanya Hanadaki hilo kuwa la kwanza kwa urefu hapa Tanzania. Ujenzi wa Mahandaki katika eneo la Kilosa unatokana na Jiografia ya eneo lenye milima mingi na uwepo wa mto Mkondoa.

Usanifu huu wa ujenzi wa reli ya kisasa -SGR unaondelea nchini, kutokana na changamoto za kijiografia utakua chachu wa kuilinda miundombinu ya reli ili isipate madhara hasa katika kipindi cha mvua kali.

BALOZI SEIF AWATAKA MAWAZIRI WA SADC KUYAPA UZITO MAAZIMIO YA MKUTANO

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akipata maelekezo kuhusu mfumo wa matumizi ya simu za mezani kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) wakati wa kutembelea mabanda mbalimbali kabla ya kufunga mkutano wa Mawaziri wa sekta za Tehama, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) leo Ijumaa Septemba 20, 2019.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wa pili (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri wa Sekta za Tehama, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewakutoka Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) mara baada ya kufunga mkutano huo leo Ijumaa Septemba 20, 2019.(PICHA NA MAELEZO)


MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi amewataka Mawaziri wa Sekta za TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa katika Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) kuyapa uzito maazimio yaliyofikiwa katika mkutano wao kuleta ustawi wa Maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wananchi wa Ukanda huo.

Akifunga Mkutano wa Mawaziri wa SADC wa sekta za TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa leo Ijumaa (Septemba 20, 2019) Jijini Dar es Salaam, Balozi Seif alisema ajenda na maazimio ya mkutano mkutano huo ni maeneo muhimu yatakayoweza kuharakisha kasi ya ukuaji wa uchumi na biashara kiuchumi katika ukanda wa SADC.

Balozi Idd alisema miongoni mwa maeneo muhimu yaliyojadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na ukuaji wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ambayo kwa sasa ukuaji wake umekuwa ni sehemu muhimu katika maendeleo ya kiuchumi ndani ya Jumuiya hiyo ikienda sambamba Mpango Mkakati Wa Maendeleo wa ya Miundombinu ya Kikanda jumuiya hiyo wa mwaka 2019-2023.

Aidha Balozi alisema malengo ya Tanzania ni kuhakikisha Jumuiya hiyo inakuwa na mshikamano na nguvu ya pamoja katika kuondoa na kukabiliana na vikwazo mbalimbali vinavyosababisha ukuaji hafifu wa maendeleo ya kiuchumi katika SADC vikwazo vya biashara ya mipakani vilivyopo baina ya Nchi na Nchi ndani ya Jumuiya hiyo.

“Mkutano huu umekuwa muhimu kwa ustawi wa Jumuiya ya SADC, wananchi wa mataifa yetu wanatarajia kupata unafuu na kutengeneza fursa mbalimbali za kiuchumi ikiwemo masoko, biashara na ajira na kwa kufanya hivi tutatekeleza Mipango Mikakati tuliyojiwekea katika kuinua uchumi wa mataifa yetu ndani ya Jumuiya” alisema Balozi Idd.

Kwa mujibu wa Balozi Seif alisema sekta za TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hali pia zina mchango mkubwa katika kuleta mageuzi ya uzalishaji mali na ufanyaji biashara ndani ya Jumuiya ya SADC na hivyo kuzitaka Nchi wanachama kuweka mkazo katika kubuni mipango madhubuti itakayowahakikishia inakuza na kuimarisha miundombinu iliyopo.

Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe alisema katika Mkutani huo, Mawaziri wa sekta hizo wamekuwa na majadiliano mapana yaliyoweza kujadili kwa kina changamoto mbalimbali zilizopo katika Nchi wananchama wa Jumuiya hiyo na kuweka mipango madhubuti kwa ajili ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili.

Aliitaja moja ya changamoto hiyo kuwa ni pamoja na vikwazo vya ufanyaji biashara katika mipaka baina ya Nchi hizo na kueleza kuwa kwa pamoja wamejipanga kuhakikisha kuwa wananachi wa Mataifa hayo wanakuwa na fursa ya kutembeleana na kuweza kufanya biashara baina yao bila vikwazo vya kisheria na kisera.

“Mkutano huu umekuwa muhimu sana kwa manufaa ya wananchi wetu kwani umeweza kuweka mikakati ya pamoja itakayosaidia wananachi wetu kupata unafuu wa gharama katika mfumo mzima wa ufanyaji biashara uliopo katika jumuiya yetu” alisema Waziri Kamwelwe.

Kamwelwe alisema mkutano huo pia ni sehemu muhimu iliyowapa fursa wajumbe wa kuweka mikakati ya pamoja ya njia bora zitakazowezesha kuzinufaisha Nchi wanachama kuweza kutumia fursa za ukuaji wa teknolojia katika kutengeneza fursa ya ukuaji wa sekta za kijamii na kiuchumi ndani ya jumuiya hiyo.

Viwanja vya Ndege kuchochea Utalii Nyanda za Juu Kusini

$
0
0


Katibu Kata ya Nduli mkoani Iringa, Wilbert Chale (kulia) akipata
maelezo ya uboreshaji wa viwanja mbalimbali vya Ndege vilivyopo chini ya
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania kutoka kwa Ofisa Uhusiano wa
Mamlaka hiyo, Bahati Mollel, alipotembelea banda la maonesho ya Karibu UtaliiKusini yaliyofunguliwa leo na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano waTanzania, Dkt. Tulia Akson yanayofanyika kwenye viwanja vya Kihesa-Kilolo
Afisa Usalama wa Kiwanja cha Ndege cha Iringa, Miyaga Juma
(kushoto) akisikiliza maswali ya Meneja wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga wa
Mkoa wa Iringa, Rosalia Makwaya, alipotembelea banda la maonesho la
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) ya Karibu Utalii Kusini
yanayofanyika kwenye Viwanja vya Kihesa-Kilolo.
Watumishi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA)
wakiwa mbele ya banda la maonesho ya Karibu Utalii Kusini, ambayo
yamezinduliwa leo na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Tulia Akson.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Albert Chalamila (wa pili kulia) na
Katibu Tawala Mkoa wa Songwe, David Kafulila (kulia), wakimsikiliza KaimuMeneja wa Kiwanja cha Ndege cha Iringa, Lydia Mwenisongole (watatu kulia),akitoa maelezo kuhusiana na viwanja vya ndege wakati walipotembelea banda lamaonesho la Mamlaka hiyo la Karibu Utalii Kusini, yaliyozinduliwa leo na NaibuSpika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Akson.
Kaimu Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Iringa, LydiaMwenisongole (wa pili kulia) na Meneja wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA)
mkoa wa Iringa, Haji Usantu (kulia) wakimsikiliza mgeni rasmi wa maonesho yaKaribu Utalii Kusini yaliyozinduliwa leo na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri yaMuungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Akson.
Mhandisi Astelius John (kushoto) akimfafanulia jambo Afisa
Biashara wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) mkoa wa Iringa, Winfrida
Kihange, alipotembelea banda la Maonesho la Mamlaka ya Viwanja vya NdegeTanzania (TAA) ya Karibu Utalii Kusini yaliyozinduliwa leo na Naibu Spika waBunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Akson.

*************************



Na Mwandishi Wetu
UBORESHAJI wa miundombinu ya viwanja vya ndege na barabara kwa Nyanda za Juu Kusini kutachangia kukuza utalii kutokana na kuwa na vivutio vingi zaidi.Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano waTanzania, Dkt. Tulia Akson alipozindua maonesho ya Karibu Utalii Kusini yanayofanyika kwenye Viwanja vya Kihesa-Kilolo, ambapo yanashirikisha taasisi za umma na watu binafsi.

Hatahivyo, Dkt. Akson amesema tayari amepata taarifa kuwa kuna matengenezomakubwa ya kiwanja cha ndege cha Iringa, ili kiweze kuhudumia ndege kubwa zaidi ya Bombardier ambayo inabeba abiria 72.

“Nimesikia hapa mkuu wa mkoa amesema kiwanja chetu cha hapa Iringa kitafanyiwa upanuzi mkubwa wa barabara ya kutua na kuruka ndege, na pia viwanja vya mikoa ya Mbeya, Mpanda, Songea na Katavi vyote vitaboreshwa zaidi,” amesema Dkt. Akson.

Lakini, amewataka wakazi wa Nyanda za Juu Kusini kuwa wabunifu kwa kuvutia watalii kutembelea vivutio vilivyopo, ikiwemo milima mingi, Hifadhi za Taifa za Ruaha, Mikumi, Udzungwa, Katavi na Kitulo; Kimondo cha Mbozi, Maporomoko ya Maji ya Kalambo na Ziwa Ngosi.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli kwa kufanikisha upanuzi wa jengo la abiria na ukarabati wa barabara ya kutua na kuruka kwa ndege ya kiwanja hicho.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi PatrickMfugale amesema barabara ya kwenda kwenye Hifadhi ya Ruaha itaboreshwa, pamoja na Kiwanja cha ndege cha Iringa nacho kipo kwenye mchakato wa maboresho hayo.

Waandishi wa Habari Wapewa Semina Fupi kuelekea Tamasha la JAMAFEST

$
0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk. Hassan Abbasi (katikati) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa semina maalum kwa waandishi kuelekea Tamasha la Utamaduni wa Afrika Mashariki (JAMAFEST) litakaloanza kesho 21 Septemba katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa maandalizi ya tamasha hilo Bi. Joyce Fissoo na kulia Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari, Rodney Thadeus.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk. Hassan Abas akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa semina maalum kwa waandishi kuelekea Tamasha la Utamaduni wa Afrika Mashariki (JAMAFEST) litakaloanza kesho 21 Septemba katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya maandalizi ya Tamasha la Utamaduni wa Afrika Mashariki (JAMAFEST) Bi. Joyce Fissoo akieleza historia ya tamasha hilo kwa waandishi wa habari wakati wa semina maalum kwa waandishi kuelekea Tamasha la Utamaduni wa Afrika Mashariki (JAMAFEST) litakaloanza kesho 21 Septemba katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia semina maalum kwa waandishi
kuelekea Tamasha la Utamaduni wa Afrika Mashariki (JAMAFEST) litakaloanza kesho 21 Septemba katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Picha na WHUSM – Dar es Salaam

Kampuni ya Vodacom yalipa Zaidi ya TZS bilioni 54.5 kama gawio kwa Wanahisa

$
0
0

· Vodacom yatoa taarifa ya ongezeko la faida kwa mwaka kufikia TZS billioni 90.2


 Kampuni ya mawasiliano ya simu za mikononi inayoongoza Tanzania, Vodacom Tanzania PLC imetangaza faida ya mwisho wa mwaka ya kiasi cha TZS bilioni 90.2 kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ulioishia mwezi Machi mwaka huu.

Wakati huo huo Kampuni ya Vodacom ambayo ina mtandao wenye kasi zaidi nchini inajivunia thamani iliyojitengenezea katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni ikiwemo TZS bilioni 54.5 ambazo zimelipwa kama gawio kwa wanahisa.

Ongezeko hili limechangiwa na kuongezeka kwa mapato yatokanayo na huduma ambayo yanafikia TZS bilioni 1018.9, ambayo yamesababishwa na kukua na kuimarika kwa mapato yatokanayo na huduma za M-pesa, ununuzi wa Intaneti (Bando) na mapato yatokanayo na ujumbe wa simu. Kampuni ya Vodacom imepata wateja wapya wapatao milioni 1.2 katika mwaka huu wa fedha jambo ambalo linaongeza idadi yake ya wateja kufikia milioni 14.1.

Katika mwaka huu wa fedha kampuni ya Vodacom ilifanya uwekezaji mkubwa wa zaidi ya TZS bilioni 171.4 sawa na (asilimia 16.7% ya Mapato) katika kupanua mtandao wake, kuongeza maeneo yanayopata mtandao wa 4G katika miji mikubwa nchini, kuongeza uwezo na kuboresha mtandao kuweza kutoa huduma ya data ya kiwango cha juu kwa wateja.

Wakati huo Shilingi bilioni 59 zimewekezwa katika mishahara, mafunzo na maendeleo ya wafanyakazi wake wa kudumu wapatao 548 pamoja na kutoa ajira isiyo ya moja kwa moja kwa zaidi ya Watanzania 127,000.

Akiongea katika mkutano mkuu wa mwaka wa kampuni ya Vodacom leo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni ya Vodacom bwana Ali A. Mufuruki amesema, “Kampuni ya Vodacom vile vile inajivunia uwekezaji wake katika jamii ambao una thamani ya jumla ya shilingi trilioni 1.1, ambazo ni fedha zilizochangiwa katika uwezeshaji wa jamii kupitia kodi, ada za udhibiti katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita ambapo malipo ya zaidi ya Shilingi trilioni 0.4 yalifanyika katika mwaka 2019 peke yake.”

“Ukuaji katika sekta ya mawasiliano imekuwa wa pole pole katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni. Tukiwa kama watendaji muhimu katika sekta hii, tunajivunia kuwa chanya katika ukuaji wa sekta hii,” alihitimisha bwana Mfuruki. 


OFISI YA MAKAMU WA RAIS YATANGAZA KANUNI MPYA ZA TAKA HATARISHI ZA MWAKA 2019

$
0
0
Ofisi ya Makamu wa Rais imefanya mapitio ya kanuni na kuandaa Kanuni mpya za Usimamizi wa Taka Hatarishi za mwaka 2019 kwa kuzingatia masharti ya Sheria ya Usimamizi wa Mazingira zilizotangazwa katika gazeti la Serikali na kupewa G.N 676 . Hayo yamesemwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Injinia Joseph Malongo alipokua akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam.

Altanabaisha kuwa kanuni hizo, zilionekana kuwa na mapungufu kadhaa hivyo kupelekea kuandaliwa kwa kanuni zingine. Mapungufu yaliyojitokeza ni kama vile Kifungu cha 133(1) na (3) cha Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004, kinampa mamlaka Waziri mwenye dhamana ya mazingira kutoa vibali vya kuingiza, kusafirisha nje ya nchi, kusafirisha ndani ya nchi au kupitisha taka hatarishi nchini. Hata hivyo Kanuni za mwaka 2009 zilitoa mamlaka hayo kwa Waziri na kwa Mkurugenzi wa Mazingira. Katika Kanuni mpya za mwaka 2019, mamlaka ya kutoa vibali yamebaki kwa Waziri mwenye dhamana ya mazingira tu akishauriwa na Mkurugenzi wa Mazingira. 

Kanuni za mwaka 2009 hazikuweka bayana masharti ya kuzingatiwa na mmiliki wa kibali. Suala hili limezingatiwa katika Kanuni mpya za mwaka 2019. Uwepo wa masharti ya mmiliki wa kibali itarahisisha kufuatilia wa mwenendo wa uzingatiaji wa masharti yaliyoainishwa katika kibali cha usimamizi wa taka hatarishi pamoja na masuala ya hifadhi na usimamizi wa mazingira kwa ujumla wake. 

Aidha alisema kuwa , kanuni za mwaka 2009 hazikuipa NEMC jukumu la kushughulikia maombi ya vibali kama sehemu ya mamlaka yake ya kusimamia uzingatiaji na utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira na Kanuni zake. Kanuni mpya za mwaka 2019 zimeandaliwa kwa kuzingatia Makundi ya aina za Taka Hatarishi kulingana na Mkataba wa Basel ambapo vyuma chakavu ni miongoni mwa taka zinazoweza kuwa hatarishi kwa kutegemea maeneo vinakochukuliwa au vinakohifadhiwa au jinsi vinavyosafirishwa hasa pale vinapochanganywa kutoka maeneo tofauti.

“Kanuni za mwaka 2019 zimeweka adhabu kali zaidi ukilinganisha na Kanuni za mwaka 2009 kwa makosa ya kutokuwa na kibali cha kusimamia taka hatarishi nchini. Adhabu hizo ni faini kuanzia milioni tano hadi bilioni kumi au kifungo kisichozidi miaka kumi na mbili au vyote kwa pamoja” alisema Injinia Malongo.

Ofisi ya Makamu wa Rais ina wajibu wa kusimamia Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira hapa nchini kwa mujibu kwa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya Mwaka 2004 na Kanuni zake. Kanuni hizi pia zinapatikana katika Tovuti ya Ofisi ya Makamu wa Rais ambayo ni www.vpo.go.tz na ile ya NEMC ambayo ni www.nemc.or.tz

WAZIRI WA KILIMO TANZANIA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA KILIMO WA ZIMBABWE

$
0
0
Waziri wa Kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na Waziri wa Kilimo wa Zimbabwe Kamanda wa jeshi jeshi la anga Perrance Shiri, leo tarehe 20 Septemba 2019 katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mtaa wa Posta Jijini Dar es salaam. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Sehemu ya wataalamu wa Kilimo wa Zimbabwe wakifatilia mkutano huo leo tarehe 20 Septemba 2019 katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mtaa wa Posta Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na Waziri wa Kilimo wa Zimbabwe Kamanda wa jeshi jeshi la anga Perrance Shiri, leo tarehe 20 Septemba 2019 katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mtaa wa Posta Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na Waziri wa Kilimo wa Zimbabwe Kamanda wa jeshi jeshi la anga Perrance Shiri, leo tarehe 20 Septemba 2019 katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mtaa wa Posta Jijini Dar es salaam.


Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma

Waziri wa Kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) leo tarehe 20 Septemba 2019 amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo wa Zimbabwe Kamanda wa jeshi jeshi la anga Perrance Shiri.

Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mtaa wa Posta Jijini Dar es salaam.Akizungumza mara baada ya mkutano huo Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga amesema kuwa miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na kuongeza ushirikiano katika sekta ya kilimo baina ya Zimbabwe na Tanzania.

Alisema kuwa nchi zote mbili zina uzoefu katika sekta ya kilimo hivyo uzoefu huo unapaswa kuhuishwa katika nchi zote mbili ili kuwa na tija ya kilimo na kuimarisha usalama wa chakula.

Mhe Hasunga alisema kuwa ujumbe wa wataalamu wa Kilimo kutoka nchini Zimbabwe ukiongozwa na Waziri wao wa Kilimo umeiomba serikali ya Tanzania kuwaongezea Tani 70,000 ili kufikia Tani 100,000 waweze kurudi nazo nchini Zimbabwe

Katika kikao hicho Waziri Hasunga amesema kuwa wamekubaliana wataalamu wa wizara ya Kilimo wa Zimbabwe na Wataalamu wa Kilimo wa Tanzania wakutane katika kikao kazi kujadiliana namna bora ya kufanya biashara hiyo.

“Jana wameshuhudia treni ya kwanza ikiondoka kuelekea Zimbabwe ikiwa imebeba Tani 1200 za mahindi na wanategemea Tani 17,000 za awali ambazo wamechukua ziwasili mapema iwezekanavyo” Alisisitiza Mhe Hasunga

Kwa upande wake Waziri wa Kilimo wa Zimbabwe Kamanda wa jeshi la anga Perrance Shiri amesema kuwa lengo la ziara yake nchini Tanzania ni pamoja na kufuatilia utekelezaji wa mauzo ya mahindi kutoka Tanzania kuelekea Zimbabwe.

Pia amemuomba waziri wa kilimo wa Tanzania kuwa na ushirikiano wa pamoja kwenye sekta ya kilimo hususani katika zao la mpunga na mazao mengine.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Magufuli aliingia makubaliano na Rais wa Zimbabwe Mhe Emmerson Mnangagwa kuwa Tanzania itaiuzia Zimbabwe tani 700,000 za mahindi kufuatia nchi hiyo kukabiliwa na upungufu wa chakula.

RAIA WA CHINA TANZANIA WASHEREKEA MIAKA 70 TANGU KUANZISHWA KWA JAMHURI YAO

$
0
0

 Balozi wa China nchini Wang Ke akizungumza katika hafra ya miaka 70 ya nchi ya China amesema kuwa kipindi chote cha miaka 70 nchi hiyo imepitia vipindi kadhaa katika kulitoa taifa kutoka hali ya chini hadi kujenga uchumi imara ambapo kwa sasa China ni nchi ya pili duniani kiuchumi pamoja uzalishaji kwa ujumla.

Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi akizungumza wakati wa sherehe za miaka 70 ya china
Baadhi ya washiriki.

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
LEO Septemba 19, 2019 raia wa China kupitia ubalozi wa China nchini umesherehekea miaka 70 tangu kuanzishwa kwa jamhuri wa watu wa China ambapo wameishukuru Tanzania kwa kuendelea kuwa na mahusiano bora ya kidiplomasia kwa miaka 55 sasa.

Akizungumza katika hafla hiyo Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi amewapongeza raia wa china kwa kudumisha jamhuri hiyo ambapo imewanufaisha wananchi wengi ambapo kwa miaka hiyo 70 wamefanya mapinduzi makubwa kwa uchumi na kuwa kati ya nchi tano zenye watu wengi zaidi na moja kati ya nchi ambazo zina uchumi mkubwa na imara duniani.

Profesa Kabudi amesema kuwa China imekuwa nchi yenye gunduzi nyingi ambazo pia husaidia mataifa mengine hasa katika sekta za viwanda, biashara na teknolojia na wamekuwa wakiishawishi Tanzania katika kuyafikia malengo yao ya maendeleo ya mwaka 2025.

Hata hivyo amesema kuwa wanaposherekea miaka 70 ya tangu kuanzishwa kwa jamhuri hiyo pia wanasherekea miaka 55 ya mahusiano bora ya kidiplomasia baina ya nchi hizo mbili, amesema kuwa nchi hizo zimekuwa zikishirikiana kwa ukaribu zaidi na mahusiano hayo yamekuwa mahusiano ya kindugu na ametoa pongezi kwa marais wa nchi hizo mbili wameendelea kudumisha mahusiano bora ya kidiplomasia

Kwa upande wake Balozi wa China nchini Wang Ke amesema kuwa kipindi chote cha miaka 70 nchi hiyo imepitia vipindi kadhaa katika kulitoa taifa kutoka hali ya chini hadi kujenga uchumi imara ambapo kwa sasa China ni nchi ya pili duniani kiuchumi pamoja uzalishaji kwa ujumla.

Amesema kuwa hali za maisha kwa wananchi zimeendelea kuimarika na hiyo ni pamoja na kuendeleza amani, na sio vita pamoja na  kuweka mbele zaidi shughuli za maendeleo ili kuweza kuondokana na umaskini.

Wang Ke amesema kuwa mwaka huu pia wanasherekea miaka 55 ya mahusiano bora ya kiplomasia baina ya Tanzania na China na kueleza kuwa nchi hizo zimekuwa zikishirikiana kwa karibu katika kuhakikisha maendeleo na huduma muhimu zinawafikia wananchi, na amehaidi kuendeleza mahusiano hayo yataendelea kudumishwa.

Pia Wang Ke amempongeza Balozi wa kwanza wa Tanzania nchini China na Waziri Mkuu mstaafu  Dkt.Salim Ahmed Salim kwa kupewa medali ya heshima ya urafiki wa kidiplomasia iliyotolewa na Rais wa China Xi Jinping mapema wiki hii, Wang amesema kuwa balozi Salim ni rafiki mzuri kwao na alikuwa na miaka 27 pekee alipoanza kuiwakilisha Tanzania nchini humo.

Amesema wataendelea kushirikiana na Tanzania pamoja na nchi nyingine za Afrika ili kuweza kuyafikia malengo ya maendeleo ya mwaka 2063.

Sherehe hizo pia zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda, Naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Tulia Ackson, Waziri wa katiba Balozi Augustine Mahiga, makamu wa chama cha mapinduzi (CCM) Philip Mangula, viongozi wastaafu pamoja na mabalozi.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, afungua Kongamano la Kitaifa la Ushiriki wa Watanzania katikaMiradi ya Kimkakati. Septemba 20.2019

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akihutubia kwenye Kongamano la Kitaifa la Ushiriki wa Watanzania katika Miradi ya Kimkakati, lililofanyika katika ukumbi wa LAPF jijini Dodoma. Septemba 20.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizindua mwongozo wa Taifa wa ushiriki wa wananchi katika uwekezaji na tovuti ya miradi ya mikakati, kwenye Kongamano la Kitaifa la Ushiriki wa Watanzania katika Miradi ya Kimkakati, lililofanyika katika ukumbi wa LAPF jijini Dodoma. Septemba 20.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Mwenyekiti wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Dkt. Festus Limbu, wakati akiwasili kwenye ukumbi wa LAPF jijini Dodoma, kufunga Kongamano la Kitaifa la Ushiriki wa Watanzania katika Miradi ya Kimkakati. Septemba 20.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


Mwenyekiti wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Dkt. Festus Limbu, akizungumza na washiriki, kwenye Kongamano la Kitaifa la Ushiriki wa Watanzania katika Miradi ya Kimkakati, lililofanyika katika ukumbi wa LAPF jijini Dodoma. Septemba 20.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).




Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Binilith Mahenge, akizungumza na washiriki, kwenye Kongamano la Kitaifa la Ushiriki wa Watanzania katika Miradi ya Kimkakati, lililofanyika katika ukumbi wa LAPF jijini Dodoma. Septemba 20.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu,Jenista Mhagama, akizungumza na washiriki, kwenye Kongamano la Kitaifa la Ushiriki wa Watanzania katika Miradi ya Kimkakati, lililofanyika katika ukumbi wa LAPF jijini Dodoma. Septemba 20.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).




Maafisa Mawasiliano Serikalini Watakiwa Kuitangaza Miradi ya Serikali

$
0
0
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa –TAMISEMI,Mhandisi Joseph Nyamhanga akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo kwa Maafisa Habari na Mwasiliano wa Serikali na taasisi zake leo jijini Dodoma. Mafunzo hayo ya siku tano yaliandaliwa kwa ushirikiano baina ya Idara ya Habari – MAELEZO na Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) kwa lengo la kuwajengea uwezo maafisa hao. Kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa TAGCO Bi. Saraha Kibonde Msika na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO, Bw. Jonas Kamaleki.
Makamu Mwenyekiti wa TAGCO Bi. Saraha Kibonde Msika akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo kwa Maafisa Habari na Mwasiliano wa Serikali na taasisi zake leo jijini Dodoma. Mafunzo hayo ya siku tano yaliandaliwa kwa ushirikiano baina ya Idara ya Habari – MAELEZO na Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) kwa lengo la kuwajengea uwezo maafisa hao.
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa –TAMISEMI,Mhandisi Joseph Nyamhanga akiteta jambo na Makamu Mwenyekiti wa TAGCO Bi.Saraha Kibonde Msika wakati wa hafla ya kufunga mafunzo kwa Maafisa Habari na Mwasiliano wa Serikali na taasisi zake leo jijini Dodoma. Mafunzo hayo ya siku tano yaliandaliwa kwa ushirikiano baina ya Idara ya Habari – MAELEZO na Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) kwa lengo la kuwajengea uwezo maafisa hao. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO, Bw. Jonas Kamaleki.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo kwa Maafisa Habari na Mwasiliano wa
Serikali na taasisi zake wakipokea vyeti vya ushiriki wa mafunzo kutoka mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa –TAMISEMI, Mhandisi Joseph Nyamhanga wakati wa hafla ya kufunga mafunzo hayo leo jijini Dodoma. Mafunzo hayo ya siku tano yaliandaliwa kwa ushirikiano baina ya Idara ya Habari – MAELEZO na Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) kwa lengo la kuwajengea uwezo maafisa hao.
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa –TAMISEMI,Mhandisi Joseph Nyamhanga akiwa katika picha ya pamoja na Sekretarieti iliyoandaa mafunzo kwa Maafisa Habari wa Serikali mara baada ya kufunga mafunzo hayo leo Jijini Dodoma. Kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa TAGCO Bi. Saraha Kibonde Msika na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO, Bw. Jonas Kamaleki. Mafunzo hayo ya siku tano yaliandaliwa kwa ushirikiano baina ya Idara ya Habari – MAELEZO na Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) kwa lengo la kuwajengea uwezo maafisa hao. (Picha na Idara ya Habari – MAELEZO)
Mwakilishi wa washiriki wa mafunzo kwa Maafisa Habari na Mwasiliano wa
Serikali na taasisi zake, Bw. Benton Nholo akitoa neno la shukrani kwa niaba yawenzake wakati wa hafla ya kufunga mafunzo hayo leo jijini Dodoma. Mafunzo hayo ya siku tano yaliandaliwa kwa ushirikiano baina ya Idara ya Habari – MAELEZO na Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) kwa lengo la kuwajengea uwezo maafisa hao.



*****************************



Na Lilian Lundo – MAELEZO, Dodoma.

Maafisa Mawasiliano Serikalini wametakiwa kuitangaza miradi mbalimbali
inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano kwa wananchi.

Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhandisi. Joseph Nyamhanga alipokuwa akifunga mafunzo ya siku ya tano ya Uandishi wa Habari za Serikali kwa Usahihi kwa Maafisa Mawasiliano wa Serikali, leo Jijini Dodoma.

“Serikali ya Awamu ya Tano imefanya mambo makubwa sana ikiwemo ujenzi wa barabara za lami, madaraja, reli ya kisasa, ujenzi wa vituo vya afya na hospitali,utoaji wa elimu bila malipo, ununuzi wa ndege mpya pamoja na ujenzi wa jengo la tatu la abiria Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere”.Amesema Nyamhanga.

Amesema, Maafisa Mawasiliano wanalo jukumu la kutangaza miradi hiyo na mingine mingi inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Idara (Habari) Jonas Kamaleki amesema mafunzo hayo ya siku tano yamehusisha uandishi wa kimkakati ya uandishi wa habari za Serikali kwa usahihi, namna ya kutengeneza taarifa za redio na televisheni pamoja na matumizi ya mitandao ya kijamii.

Aidha, Afisa Habari wa Halmashauri ya Bahi, Benton Nollo amesema mafunzo hayo yamekuwa muhimu sana kwao kama Maafisa Mawasiliano wa Serikali, amemuahidi Rais wa Jamhuri ya Muungano kuitangaza vyema miradi inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano.

Mafunzo hayo yameandaliwa na Chama cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali (TAGCO) kwa kushirikiana na Idara ya Habari (MAELEZO) ambapo imehusisha zaidi ya Maafisa Mawasiliano kutoka Taasisi na Idara za Serikali, Wizara, Mikoa na Halmashauri za Wilaya.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA APONGEZA UBUNIFU WA MIFUMO YA FEDHA NA KUDHIBITI MAKOSA YA BARABARANI

$
0
0
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akifafanua jambo alipokuwa akielezewa namna mifumo ya kielektroniki ya kukusanya maduhuli ya Serikali wa GePG, Mfumo wa Usimamizi wa Makosa Barabarani (TMS) na Mfumo wa Taarifa za Mali zilizopote (Los Report System) inavyofanya kazi ,kutoka kwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Dkt. Gabriel Mukungu katika banda la Serikali Na. 26 kwenye Mkutano wa Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wa Sekta ya Tehama, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa, Jijini Dar es Salaam


Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Dkt. Gabriel Mukungu (kulia) akimuelezea Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mhe Felix Lyaviva (katikati) namna watuhumiwa wa makosa ya barabarani wanaokamwatwa kupitia Mfumo wa Usimamizi wa Makosa Barabarani (TMS) kwanavyotumia Mfumo wa Kielektroniki wa Ukusanyaji Maduhuli ya Serikali (GePG) katika banda la Serikali Na. 26 kwenye Mkutano wa Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wa Sekta ya Tehama, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa, unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam

Watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakijiandaa kumpokea Waziri Mkuu, Mhe. Kasim Majaliwa (hayupo pichani) katika banda la Serikali Na. 26 la mifumo ya kielekroniki ya kukusanya maduhuli ya Serikali, Mfumo wa Usimamizi wa Makosa Barabarani (TMS) na Mfumo wa Taarifa za Mali zilizopotea (Los Report System) kwenye Mkutano wa Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Kusini mwa Afrika (SADC) wa Sekta ya Tehama, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa, Jijini Dar es Salaam.

****************************



Na Farida Ramadhani, WFM, Dar es Salaam

Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa ametembelea banda la Serikali Na. 26 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) na kujionea namna mifumo ya kielektroniki ya kukusanya maduhuli ya Serikali wa GePG unaosimamiwa na Wizara ya Fedha na mfumo wa Jeshi la Polisi wa kudhibiti wasiolipa faini za barabarani (TMS) inavyofanya kazi.

Waziri Mkuu amefanya tukio hilo kabla ya kufungua rasmi Mkutano wa Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wa Sekta ya Tehama, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa, unaofanyika Jijini Dar es Salaam.

Aliwapongeza wabunifu wa mifumo hiyo ambayo kwa sasa inasaidia Serikali kupata mapato yake kwa wakati pamoja na kupunguza makosa ya barabarani ambayo yamekuwa yakiongeza ajali na kupunguza nguvu kazi ya Taifa.

Alisema uwekezaji katika Sekta ya Tehama ni muhimu kwa nchi wanachama wa SADC ili kudhibiti uhalifu wa mtandaoni pamoja na kusimamia matumizi ya fedha za umma.

Naye Mkuu wa Uendeshaji wa Mfumo wa GePG kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Basil Baligumya, alisema Wizara imeshiriki mkutano huo ili kuzionesha nchi mbalimbali zinazoshiriki mkutano huo namna Tanzania imepiga hatua katika maendeleo ya teknolojia hususani katika usimamizi wa fedha na ukusanyaji mapato ya Serikali kupitia mfumo wa GePG.

Bw. Basil alisema mfumo huo unadhibiti fedha za umma, umeongeza makusanyo na uwazi katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali, pamoja na kuongeza usahihi wa taarifa za mapato.

“Mfumo huu umerahisisha ulipaji wa huduma mbalimbali za umma na kupunguza gharama nyingi ambazo zilikua zikiambatana na ukusanyaji wa mapato ya Serikali”, alisema.

Alisema kwa kuwa kubadilishana uzoefu ni miongoni mwa malengo ya mkutano huo, wako tayari kujifunza mbinu mpya za kuendeleza mifumo nchini pamoja na kuzielekeza nchi zitazokuwa tayari kujifunza namna ya kutengeneza mifumo ya kusimamia mapato ya nchi zao.

Kwa nyakati tofauti, washiriki mbalimbali waliotembelea banda hilo wameipongeza Serikali kwa kuanzisha mifumo hiyo ambayo itasaidia kudhibiti ubadhilifu wa fedha za umma, kukusanya mapato ya serikali kwa wakati pamoja na kudhibiti makosa ya barabarani.

Washiriki hao wamewapongeza watumishi wote walioshiriki katika kutengeneza mifumo hiyo kwani wameonesha uzalendo wa dhati kwa kuiwezesha Serikali kuweza kisimamia mapato yake kwa wakati.

MAAFISA HABARI SERIKALINI WAAPA KUTOMWANGUSHA RAIS MAGUFULI

$
0
0
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa –TAMISEMI,Mhandisi Joseph Nyamhanga akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo kwa Maafisa Habari na Mwasiliano wa Serikali na taasisi zake leo jijini Dodoma. Mafunzo hayo ya siku tano yaliandaliwa kwa ushirikiano baina ya Idara ya Habari – MAELEZO na Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) kwa lengo la kuwajengea uwezo maafisa hao. Kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa TAGCO Bi. Saraha Kibonde Msika na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO, Bw. Jonas Kamaleki.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo kwa Maafisa Habari na Mwasiliano wa Serikali nataasisi zake wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa –TAMISEMI, Mhandisi Joseph Nyamhanga aliyekuwa mgeni rasmi wakati wa hafla ya kufunga mafunzo hayo leo jijini Dodoma. Mafunzo hayo ya siku tano yaliandaliwa kwa ushirikiano baina ya Idara ya Habari – MAELEZO na Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) kwa lengo la kuwajengea uwezo maafisa hao.

**************************



Na Lilian Lundo – MAELEZO, Dodoma

Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini wameahidi kuitangaza miradi mbalimbali na kutomwangusha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli. Wameyasema hayo leo (Ijumaa) wakati wa kufunga mafunzo ya siku tano yaliyolenga kuwanoa katika kuandika kwa usahihi na umakini habari za Serikali.

Akifunga mafunzo hayo, Katibu Mkuu wa TAMISEMI, Mhandisi Joseph Nyamhanga, alimewataka maafisa hao kuitangaza miradi mbalimbali ya Serikali ya Awamu ya Tano kwa wananchi.

“Serikali ya Awamu ya Tano imefanya mambo makubwa sana ikiwemo ujenzi wa barabara za lami, madaraja, reli ya kisasa, ujenzi wa vituo vya afya na hospitali, utoaji wa elimu bila malipo, ununuzi wa ndege mpya pamoja na ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere pale Dar es Salaam”.Amesema Mhandisi Nyamhanga.

Amesema, Maafisa Mawasiliano wanalo jukumu la kutangaza miradi hiyo na mingine mingi inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano.
Akifungua mafunzo hayo mapema wiki hii, Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi aliwaeleza washiriki hao kuwa Rais Magufuli anataka kuona taasisi zote za umma zikitangaza kwa wakati na usahihi majumu waliyopewa kuyafanya.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Afisa Habari wa Halmashauri ya Bahi, Dodoma, Bw. Benton Nollo amesema mafunzo hayo yamekuwa muhimu sana kwao na amemuahidi Rais Rais Magufuli kuwa hawatamwangusha na watatoka Dodoma wakiwa wameiva zaidi na wataboresha utendaji wao.

Mafunzo hayo yaliandaliwa na Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) kwa kushirikiana naIdara ya Habari (MAELEZO).

WIZARA YA ELIMU KUWAKUTANISHA WADAU WA ELIMU ILI KUJADILI MASUALA YA ELIMU NCHINI

$
0
0
Waziri wa Eimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amefungua na kushiriki Mdahalo juu sekta ya Elimu uliofanyika jijini Dar es Salaam.Mjadala huo ulioandaliwa na Mwanachi Communications Ltd ( MCL) kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ulihusisha majadiliano juu ya uwezeshaji vijana katika kukuza maarifa na ujuzi mahususi.
Akifungua mdahalo huo Waziri Ndalichako amesema Serikali ya awamu ya Tano imewekeza kiasi kikubwa cha rasilimali ili kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji katika ngazi zote za elimu ili vijana wanaosoma wapate mafunzo katika mazingira yatakayowawezesha kuwa mahiri katika fani wanazosomea.
Prof. Ndalichako ameongeza kuwa katika ngazi ya elimu ya ufundi na elimu ya juu serikali inaboresha maabara na karakana na kuweka vifaa vya kisasa ili mafunzo kwa vitendo yafanyike kwa tija na kulingana na mazingira ya sasa. Aidha ametolea mfano wa maktaba ya kisasa inayojengwa katika Chuo Kikuu cha Teknolojia Mbeya (MUST) itakayokuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 2,500 kwa mara moja ambayo inagharimu fedha za ndani zaidi ya shilingi bilioni 11.

Ndalichako amewashukuru MCL kwa kufungua njia ya kuwa na mijadala ya wazi juu ya maendeleo ya elimu na kuahidi kuandaa mjadala mwingine wa Elimu utakaohusisha wadau. Pia amepongeza washiriki kwa kutoa maoni ambayo yana tija katika kuboresha elimu, huku akisisitiza kuwa elimu yetu inaandaa vijana mahiri ambao wanashiriki kujenga taifa.

“Humu ndani tumesikia fikra mahiri zinazotokana na vijana ambao wanasoma hapa hapa nchini na mitaala ni hii hii, hivyo tujiamini kuwa elimu yetu ni bora na inawezesha vijana kuwa mahiri katika fani mbalimbali,” alisema Ndalichako.

Ndalichako amesisitiza juu ya uboreshaji elimu ya ufundi ambapo amesema katika mwaka huu wa fedha vyuo vipya vya VETA 25 vinajengwa kwa shilingi bilioni 40.

Aidha amesema Vyuo 54 vya maendeleo ya wanachi vimeboreshwa na kuwekewa vifaa na tayari vitatoa vijana zaidi ya ….. wenye ujuzi.

Ndalichako pia amesema Serikali kupitia VETA inaendelea na programu ya kutambua na kurasimisha ujuzi kwa vijana ambapo amesema mwaka huu zaidi ya vijana 10,000 watapatiwa mafunzo kutokana na ujuzi walio nao na kupatiwa vyeti vya kurasimisha ujuzi huo. Amesema lengo la kurasimisha ni kuwatambua, kuwapa stadi na kuwaongezea ujuzi vijana walioko katika maeneo mbalimbali ambao wamekuwa wakifanya kazi za ujuzi bila vyeti.

Awali, akizungumza katika mjadala huo Mkurugenzi Mtendaji wa MCL, Francis Nanai amemshukuru Waziri Ndalichako na Viongozi wa wizara kwa kukubali kushiriki mjadala na kupokea maoni. Amesema wao kama sekta binafsi wanalo jukumu la kushirikiana na serikali katika kusukuma mbele maendeleo kulingana na eneo lao la biashara.

Akiongea katika Mjadala huo, Prof. Lughano Kusiluka ambaye ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe amesema Vyuo Vikuu vinaandaa mitaala kulingana na uhitaji wa soko na mahitaji ya wakati. Amewaasa vijana pia kuona umuhimu wa kutumia elimu wanayopata na vipaji walivyo navyo kubuni biashara na kujiajiri badala ya kusubiri ajira.

Kusiluka amesema Vyuo vikuu vina programu za kukuza bunifu za wanafunzi na kuziendeleza kuwa biashara kupitia Vituo Atamizi na kambi za ujasiriamali.

Naye mmoja wa washiriki, Abel Nyengo ameiomba Serikali kuhakikisha kila kijana aliyeko katika chuo anapata nafasi ya mafunzo kwa vitendo.

“Nishauri serikali kuwa mafunzo kwa vitendo iwe ni lazima na ipewe umuhimu mkubwa katika kutahini wanafunzi badala ya kutegemea mitihani,” alisema Nyengo.

Wananchi na wadau mbalimbali wametoa maoni mengi juu ya mada hiyo wakihusisha mitaala, utoaji elimu na ujuzi.

VITONGOJI SITA VYAFUTWA BAGAMOYO KUTOSHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI YA MITAA

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI,PWANI


VITONGOJI Sita vilivyopo maeneo ya uwekezaji kata ya Zinga pamoja na RAZABA kata ya Makurunge eneo la serikali alilopewa mwekezaji BAKHRESA kwa ajili ya uwekezaji wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani vimefutwa kwa mujibu wa sheria na havitoshiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na uchaguzi mkuu 2020. 

Vitongoji hivyo ni Kikonga ,Kasiki ,Pande ,Mkunguni, Mbegani vilivyopo kata ya Zinga eneo la EPZA na RAZABA kata ya Makurunge .

Akizungumza katika baraza la madiwani, Bagamoyo mkuu wa wilaya hiyo, Zainab Kawawa aliwaasa madiwani na viongozi kwenye maeneo hayo wasijiingize katika ushabiki wowote kutokana na maamuzi hayo ya serikali ambayo ni ya msingi na yenye nia njema.

Alieleza ,vitongoji hivyo vimefutwa na Tume ya Uchaguzi ,na mchakato huo ulianzia chini ,msije kukosoa na kupingana na serikali na kushirikiana na wananchi ambao wameshaanza kunung'unika .

"Uchaguzi unatarajiwa kuwa Novemba 24 mwaka huu, madiwani mtoe ushirikiano katika maandalizi ya uchaguzi huo ,ili kupata viongozi bora,"

"Msipange safu ,kwani itasababisha kupata viongozi wasio bora,tunataka uchaguzi uwe huru na wa haki na usio na chembe ya rushwa"alifafanua Zainab .

Nae msimamizi wa uchaguzi , wilaya ya Bagamoyo, Malboard Kapinga alieleza kwamba, uchaguzi huo hautohusisha vitongoji hivyo sita kutokana na wananchi kulipwa fidia kwenye maeneo ambayo yapo katika uwekezaji na walitakiwa kuondoka.

Kapinga alibainisha ,bajeti ya uchaguzi itagharimu takriban milioni 200 ambapo serikali kuu itatoa milioni 163 na halmashauri milioni 54 na hadi sasa serikali kuu imeshatoa milioni 119 na halmashauri milioni 27.

"Elimu ya uraia tunatarajia kuendelea kuitoa mwezi octoba katika maeneo yote vitongoji 167 na vijiji nane na vifaa vya uchaguzi vimeanza kuandaliwa"aliweka bayana.

Awali diwani wa viti maalum kata ya Yombo Elizabeth Shija alilitaka kundi la wanawake kujitokeza kushiriki kugombea nafasi mbalimbali za uchaguzi na kuwaasa kuthubutu bila uoga ili kufikia 50 kwa 50.

Diwani wa kata ya Yombo ,Muhammed Usinga alisema wamejipanga na tayari wamehamasisha wanaCCM kuanzia ngazi ya tawi kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wakazi.

Alisema ,hakuna asiyekosa macho ama kusikia ,utekelezaji wa ilani ya CCM umetekelezeka kwa asilimia kubwa chini ya Rais dkt.John Magufuli na hakuna wakumpinga kutokana na juhudi zake za kuinua maendeleo na uchumi kijumla.

Usinga ,aliwaomba wananchi wasifanye makosa katika uchaguzi huo na uchaguzi mkuu 2020 ,wachague CCM ili kuendelea kula matunda .
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live




Latest Images