Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

BRELA WATOA MAFUNZO KWA WAFANYABIASHARA WA CHALINZE, WAFANYABIASHARA KUJIPATIA LESENI KWA NJIA YA MTANDAO

$
0
0
Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
WAKALA wa usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) watoa mafunzo kwa wafanyabiashara wa Halmashauri ya Chalinze wapewa mafunzo kwaajili ya kujipatia leseni kwa njia ya mtandao.

Akizungumza na waaandishi wa habari Afisa Biashara mwandamizi kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Boniface Mrema amesema kuwa wafanyabiashara wa halmashauri ya Chalinze wamepewa mafunzo wezeshi kwaajili ya kupata leseni mpya au kurudia kusajili leseni zao za biashara.

"Wafanyabiashara wa halmashauri ya Chalinze wamepewa mafunzo na maafisa wa kutoka Wakala ya Usajili biashara na Leseni (BRELA) ili waweze kupata leseni za biashara zao kwa njia ya mtandao na kuachana na namna ya zamani ambayo ilikuwa ikiwapotezea muda wa kufanya biashara zao". Amesema Mrema.

Nae Afisa Leseni Mwandamizi wa BRELA, Abas Kothema amesema kuwa Tanzania ya Viwanda lazima iwe na mfumo sahihi wa kusajili biashara kwa njia ya mtandao kwani mataifa mengi duniani husajili biashara kwa njia ya mtandao.

Pia amewaasa wafanyabiasha wa Manispaa zilizochaguliwa kwaajili ya kupewa mafunzo wachukue fursa hiyo kwaajili ya kujipatia leseni zao kwa njia ya mtandao na kutokupoteza muda.

Hata hivyo Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa halmashauri ya Chalinze, Lawrence Tsingay ameishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa kuwachagua wafanyabiashara wa Chalinze kuwa wamojawapo kati ya halmashauri zilizochaguliwa kupewa mafunzo ya kujisajili na kujipatia leseni kwa njia ya Mtandao.

Nae Mfanyabiashara Farida Khamis amewashukuru maafisa BRELA kwa kazi wanayoifanya na kuwaelimisha wafanyabiashara wa Chalinze kwani wamewapunguzia muda wa kupanga foleni walipokuwa wakitafuta leseni za biashara zao.
Afisa Leseni Mwandamizi wa BRELA, Abas Kothema akizungumza na wafanyabiashara wa  Manispaa ya Chalinze kwaajili ya kuwajengea uwezo waweze kujipatia Leseni za Biashara kwa njia ya mtandao.

Afisa biashara Mwandamizi kutoka Wizara ya Biashara na Viwanda, Boniface Mrema akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutoa mafunzo kwa wafanyabiashara wa Halmashauri ya Chalinze ambayo yanahusu wafanyabiashara kujipatia Leseni kwa njia ya Mtandao baada ya kuzinduliwa Mwanzoni mwa Oktoba,2019.


Baadhi ya wafanyaiashara wa  Halmashauri ya Chalinze wakisikiliza mafunzo yanayotolewa na BRELA kwaajili ya kuwarahisishia wafanyabiashara hao kujipatia Leseni kwa njia ya Mtandao.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara  Halmashauri ya Chalinze, Lawrence Tsingay akizungumza mara baada ya kupewa mafunzo kwaajili ya kuijipatia Leseni kwa njia ya Mtandao katika mafunzo yaliyofanyika Chalinze leo.
Mfanyabiashara  wa Halmashauri ya Chalinze, Farida Khamis akizungumza mara baada ya kupewa mafunzo ya kujisajiri na kujipatia Leseni kwa njia ya mtandao. Amesema kuwa Mafunzo hayo yamekuja kwa muda muafaka kwani itawarahisishia kujipatia leseni bila kupanga foleni.

KIVULE FOOTBAL CHALLENGE CUP YAANZA KUTIMUA VUMBI

$
0
0
 Mratibu wa mshindano wa Shirika la OCCRI, Rehema Sanga akizungumza na waandishi habari kuhusiana na uratibu mashindano hayo yanayofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Kivule jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
SHIRIKA la Capitalizing Community and Resources Initiative  (OCCRI) limeandaa mashindano ya Kivule Footbal Challenge Cup ikiwa ni lengo ya vijana kutumia fursa za maendelezo zinazowazunguka.

Mratibu wa mashindano hayo Rehema Sanga, amesema ili vijana kuweza kukutana na kuzungumza na masuala ya maendeleo ni michezo kuleta vijana kuwa sehemu moja na ujumbe kufika kirahisi.

Amesema OCCRI imeandaa mashindano ya mpira wa miguu kwa kushirikisha timu 16 za kata ya kivule na kwenye mashindano hayo washiriki watafundishwa ujasiriamali pamoja na kutumia vipaji vyao vya mpira kama sehemu ya ajira kwao.

Rehema  amesema mashindano hayo yatalenga kutoa elimu ya Afya kwa vijana na kuwa na utaratibu wa kupima afya zao kila mara.

Afisa Mtendaji wa Kata ya Kivule Mwanahamis Shaban  ameishukuru OCCRI kwa kuleta michezo katika kata yake na kuja kwa mashindano hayo mshikamano kwa  vijana pamoja na kupata fursa ya kujifunza ujasiriamali na elimu ya afya.

Amesema, dhima ya shirika hilo litachochea maendeleo  kutokana na mshikamano wa michezo pamoja na utengenezaji wa fursa ajira zinazozunguka katika kata hiyo .

Mwanahamis amesema kuelekeaa uchumi wa viwanda  vijana ni sehemu muhimu katika kuhakikisha dhamira ya serikali kufikia uchumi wa kati na lengo kuu ni kuona vijana wanaungana kwa kuanzisha Viwanda na kuweza kuajiri vijana wengine.

Mwenyekiti wa Serikali ya Kivule, Amos Hangaya  amesema kivule ina vijana wenye vipaji hivyo wakitumia vizuri wanaweza kupata ajira  zinazotokana na michezo.

Katika ufunguzi wa mashindano hayo kati ya Stock City ilipata ushindi wa bao moja dhidi ya  Mchikichini lililofungwa kwenye kipindi cha pili cha mchezo huo na kufanya timu hiyo kunyakua pointi tatu

Washindi katika mashindano hayo watapata fedha taslim pmaoja na vifaa vya michezo kwa mshindi wa kwanza hadi wa tatu pamoja na mfugaji bora na kipa bora wa mashindano watapata zawadi.
 Afisa Mtendaji wa Kata ya Kivule, Mwanahamis Shaban akizungumza namna walivyjipanga katika mashindano hayo katika kuchochea ajira katika kata hiyo.
 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kivule, Amos Hangaya akitoa  malezo namna walivyojimarisha katika sekta ya michezo katika maeneo yao.
 Afisa Mtendaji wa Kata ya Kivule Mwanahamis Shaban akipiga mpira kuashiria uzinduzi wa mechi kati ya Stock City na Mchikichini
 Mratibu wa mshindano wa Shirika la OCCRI Rehema Sanga akiwa katika picha ya pamoja na  timu katika mashindano ya Kivule Footbal Challenge Cup
 Mashabiki 
 Timu ya Stock City wakijindaa na mechi katika mashindano ya Kivule Footbal Challenge Cup
Timu ya mchikichini wakijiandaa katika mashindano ya Kivule Footbal Challenge Cup.

TAYOA YAWEKA WAZI MKAKATI WA KUKUZA KUENDELEZA VIPAJI VYA VIJANA NCHINI

$
0
0
Na Mwandishi Wetu 
MKURUGENZI wa Shirika la Vijana la TAYOA Peter Masika amesema kuwa asilimia kubwa ya Watanzania ni vijana na hivyo ni muhimu kuwapa nafasi ya kuonesha na kuendeleza vipaji vyao ili kutengeneza ajira kwao na kwa wengine. 

Pia ni vema wakapewa fursa ya kuonesha kazi zao za kiubunifu kwenye vyombo mbalimbali vya habari kwani hiyo itawapa hamasa ya vijana kupenda kujitegemea, uzalendo, maendeleo na kuongeza kasi ya mafanikio ya kuondokana na umaskini wa kipato na usio wa kipato kwa kufanya kazi kwa juhudi ili kuleta maendeleo yao na ya jamii zao kupitia Vijanatz Talent Show. 

Masika amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati akitoa shukrani zake kwa vyombo vya habari nchini kwa mchango wao mkubwa ukiwemo wa kuandika habari za TAYOA na hatimaye kufanikiwa kuendelea kutekeleza malengo yake na hasa ya kuhakikisha kijana wa kitanzania anajitambua, anajiendeleza, anatafuta fursa za kujiajiri pamoja na kutoa elimu inayohusu afya. 

" TAYOA tumekubaliana na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari kuhamasisha vijana kujitegemea na kujifunza kutoka kwa vijana wengine waliofanikiwa katika mazingira magumu zaidi ya wanayoishi. Nia ya shirika letu ni kuibua vipaji vya vijana na kuwasaidia kufikia ndoto zao kupitia teknolojia na mabadiliko ya fikra, tabia, uongozi, uzalendo, ujasiriamali ili waweze kutengeneza ajira mpya au wawe wanaajirika. 

"Pia kupitia Vijanatz Talent Show, TAYOA inatatafuta vijana wenye vipaji vya ubunifu, mawazo yenye tija kwa Taifa na ulimwengu na sio kulenga tasimia ambazo zimezoeleka kwenye utafutaji wa vipaji has kwenye sanaa ya musiki na filamu,"amesema Masika. 

Ameongeza kwamba ili kuondokana na mkwamo wa kimaendeleo ni lazima sekta binafsi na ya umma zifanye kazi kwa pamoja kuibua na kuvikuza vipaji vya ubunifu na kuvibadilisha kuwa fursa na ajira. Alieleza Mungu huwaga vipaji kwa uwiano katika nchi zote duniani. 

"Hivyo ni juu yetu sisi waafrika kuwatambua wale wenye vipaji, tuwapende na kuwaendeleza ili wawe chachu na watengeneze fursa mpya na ajira kwa wengine, kwani kama wote tungekuwa wakurugenzi, je ni nani angeandaa chakula au kulima mazao ya vyakula,"amefafanua. 

Hata hivyo ameeleza kufurahishwa na moyo ulionyesha wahariri kwa kukubali kutoa kipaumbele kwenye habari za vipaji ambayo vinaweza kutengeza ajira zinazowalenga vijana na kuleta maendeleo tokana na ndoto zao. Alisema kupitia maonyesho mbalimbali ya vipaji vya vijana (Vijanatz Talent Show), asasi ya TAYOA ikishirikiana na wahariri wanategemea kufungua hazina ya vipaji iliyo ndani ya vijana wa kike na wa kiume kupitia Tehama, fikra chanya, malezi bora na tabia nzuri. 



“Mashindano hayo ya vipaji vya vijana Tanzania yatazingatia kanuni zifuatazo; moja, kujenga uwezo wa ubunifu kwa vijana kwa kuwawezesha waone changamoto zinazowazunguka kama fursa na hivyo kuwashaa tamaa ya kupata maendeleo kupitia ubunifu na mawazo chanye ili kubadilisha hali inayowazunguka. Pili, kuzingatia weledi katika shughuli zote wanazofanya ikiwemo kuhakikisha wanafanyakazi kwa bidii, uaminifu, uzalendo na kwa ufanisi na ufasaha kwa kila fursa wanayoipata. 

"Tatu, kuwawezesha vijana kuondokana na mazingira hatarishi kwa kuwajengea uwezo wa kutumia rasilimali binafsi na za kijamii na kubadili mitazamo isiyo na tija Nne, kuimarisha uwajibikaji kwa kuwawezesha kutimiza majukumu yao huku wakizingatia uaminifu, uadilifu na uwazi. Tano, kukuza ushirika wa vijana kwa kuhamasisha ushirikiano kati ya vijana wenye vipaji na wenzao ili kutengeneza fursa na ajira mbalimbali kwenye mazingira wanayoishi,"amesema. 

Kuhusu maono ya TAYOA ,Masika amesema ni kuona vijana wa kike na kiume wenye uwezo wa kujimudu na kujitejemea ambao wanaoishi maisha bora na wenye afya njema. Katika miaka 20 tangu kuanzishwa kwake, shirika hilo limeweza kutoa huduma ya ushauri wa kiafya kwa vijana na watu wazima wapatao milioni 3.5 kupitia huduma za simu za bila malipo kwenda namba 117. 

Pia amesema asasi hiyo imekuwa ikitoa huduma za upimaji wa virusi vya Ukimwi na uwezeshwaji kiuchumi ikiwalenga wasichana na wavulana balehe hasa wanaotoka maeneo ya vijijini na kusisitiza TAYOA imewajengea uwezo wa kutumia Tehama kwa manufaa chanya kupitia tovuti ya vijanatz ambayo hutoa mafunzo na taarifa za ajira kila siku ambazo pia zinapatiakana kupitia simu za kiganjani. 

Hata hivyo amesema kutokana na kupungua kwa hamasa ya usomaji kwa vijana, TAYOA imejikita kutengeneza taarifa za kitaalam na mafunzo kupitia sauti na picha zilizorekodiwa katika studio zake na kuzitumia katika kuwajengea vijana uwezo, stadi mbalimbali na taaluma muhimu katika maisha yao. 

"TAYOA inaamini kwa kupitia fursa hii mpya ya Vijanatz Talent Show, vijana wa kike na kiume wataonyesha vipaji vyao vya kiubunifu ambavyo vinatatua matatizo yanayowazunguka na kuleta mapinduzi makubwa kwa kizazi kijacho cha vijana kwa Afrika inatarajiwa kuwa na nguvu kazi ya vijana kubwa Zaidi duniani kwa miaka ijayo. 

"Kupitia makubaliano ya ushirikiano TAYOA na wahariri watafuatilia vipaji hivyo vya vijana na kuonyesha jinsi juhudi binafsi na moyo wa kupenda kujitegemea unavyoweza kutatua matatizo na kutengeneza fursa za ajira na utajiri kwa jamii yetu ambapo vijana wataweza kuiweka Tanzania katika ramani ya dunia, kuwa kati ya nchi zinazojitegemea na zenye mchango maalum duniani kupitia rasilimali watu na asilia. 

"Kwa sasa asasi ya TAYOA inatekeleza miradi miwili ambapo mradi moja unawalenga vijana wa kike katika wilaya kumi za mikoa ya Morogoro(Ulanga, Kilombero na Malinyi), Dodoma (Kondoa, Kongwa, Bahi na Mpwapwa) na Singida Singida MC, Singida DC nas Iramba),"amesema Masika 

Ameeleza kuwa kama sehemu ya utekelezaji wa mradi TAYOA inatarajia kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa wasichana walio katika umri wa kubalehe na wanawake vijana 11,000 kutoka kaya masikini zilizopo chini ya TASAF. Katika wilaya hizi wasichana wengine zaidi ya 113,445 watafikiwa na huduma mbalimbali za afya na kinga dhidi ya VVU na UKIMWI. Mradi huu unatekelezwa chini ya uangalizi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia wazee wa watoto na AMREF kwa ufadhili wa Global Fund. 

Amefafanua kuwa katika mikoa saba ya Mwanza, Geita, Shinyanga, Kagera, Simiyu, Mara na Kigoma, TAYOA inafanya kazi Kwa kushirikiana na Intrahealth chini ya udhamini wa watu wa Marekani kupitia CDC kutekeleza afua zinazolenga kutoa huduma za tohara kwa wanaume hususani wale wenye umri kati ya miaka 25 hadi 29. Mwaka huu TAYOA ina lengo la kufikia jumla ya watu 48,000. Huduma za Tohara zinalenga kupunguza uwezekano wa wanaume kupata maambukizi ya VVU. 
Mkurugenzi wa Shirika la Vijana la TAYOA Peter Masika(anayepiga makofi) akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa TAYOA Balozi Charles Sanga, baadhi ya wahariri na vijana wakati wa uzinduzi wa programu ya kuibua na kuendeleza vipaji vya vijana nchini.
Mkurugenzi wa Shirika la Vijana la TAYOA akizungumza wakati wa kikao maalum cha kutoa shukrani kwa vyombo vya habari kutokana na mchango wao mkubwa wa kuandika habari za shirika hilo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Vijana la TAYOA Balozi Charles Sanga akifafanua jambo na hasa kuhusu umuhimu wa vijana kutengeneza mazingira ya kutumia fursa zilizopo nchini kujitegemea na kujenga utamaduni wa kuwa wazelendo kwa nchi yetu.
Mkurugenzi wa Shirika la Vijana la TAYOA Peter Masika akifafanua jambo wakati wa kikao hicho.

TBS yatoa Elimu kwa wagizaji bidhaa, Mawakala wa Forodha

$
0
0
Na Chalila Chibuda
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limetoa elimu kwa waangizaji wa bidhaa na mawakala wa forodha nchini ili kuwawezesha wafanyabiashara kufanya biashara zenye tija kwa taifa bila kuathiri taratibu na sheria za nchi. 

Akifungua semina hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Dkt. Yusuf Ngenya, jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Upimaji na Ugezi wa shirika hilo, Johanes Maganga, alisema washirika hao watapatiwa kuhusiana na taratibu za uingizaji wa bidhaa nchini pamoja na usajili wa maghala ya kuhifadhi bidhaa za chakula na vipodozi.

Maganga alitaja maeneo mengine ambayo walipatia elimu kwamba ni   kuhusu taratibu za kufanya maombi kwa njia ya mtandao (OAS) pamoja na kujadili changamoto zinazoikabili sekta hiyo, hususan kwenye masuala ya viwango na mifumo ya udhibiti ubora.

Wadau hao walipatiwa elimu hiyo jijini Dar es Salaam jana kupitia semina waliyoandaliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS). 

Kwa mujibu wa Maganga wengine walioshiriki semina hiyo ni wawakilishi kutoka Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI) na Baraza la Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), wawakilishi kutoka Shirikisho la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC), Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT), Chama cha Mawakala wa Forodha Tanzania (TAFFA) na wadau wengine.

Maganga alisema, ili kutimiza majukumu ya shirika hilo ni muhimu kwa umma wa Watanzania kwenda sambamba na mikakati mingine ya kitaifa. 

Alisema shirika hilo limeendelea kutoa semina kama hizo kwa waagizaji wa bidhaa mbalimbali zitokazo nje na mawakala wa forodha katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Tanga.

"Lakini tumepanga kufanya semina kama hii katika Mkoa wa Mbeya hivi karibuni," alisema. Alifafanua kwamba kwa kuzingatia kifungu cha 36 cha sheria ya viwango Na: 2 ya mwaka 2009, Serikali ilipitisha kanuni ya udhibiti wa shehena kupitia notisi ya Serikali Na: 405 ya Desemba 25, 2009.

Alisema kanuni hizo ziliipa TBS mamlaka ya kudhibiti ubora wa bidhaa zinazoingia nchini kabla ya kusambazwa kwenye soko la ndani.

Kwa mujibu wa Maganga, Februali mwishoni, mwaka 2012 ndipo shirika lilianzisha mfumo wa ukaguzi wa bidhaa kabla ya kusafirishwa kuja nchini (PVoC) kama mpango wa kudhibiti ubora wa bidhaa katika nchi zinakotoka, ambao unasaidia kutatua changamoto zinazokuwepo wakati bidhaa zinapokuwa zinakaguliwa baada ya kufika nchini.

Alitaja changamoto hizo kuwa ni mabadiliko ya mifumo ya uondoshaji wa shehena bandarini kwa kutumia mfumo wa kielektroni, hasara  ambazo wafanyabiashara walikuwa wanapata kutokana na kuharibiwa kwa bidhaa zinazopatikana kutokidhi viwango, hasara kwa Serikali kupitia matumizi ya fedha za kigeni katika kuagiza bidhaa hizo na athari kwa mazingira wakati wa uteketezaji wa bidhaa zilizofeli vipimo.  

Akitoa mada kwenye semina hiyo, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Bidhaa baada ya kuwasili nchini, Athuman Kissumo, aliwaeleza washiriki kuhusiana na faida za uamuzi wa Serikali kurejesha TBS majukumu yaliyokuwa yakisimamiwa na iliyokuwa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA).

Hiyo ni kutokana na mabadiliko ya sheria ya fedha ya mwaka 2019 ambayo yameleta mabadiliko katika sheria ya viwango Na: 2 ya mwaka 2009, ambapo majukumu ya kudhibiti ubora na usalama wa chakula na vipodozi yanafanywa na shirika hilo.

Alitaja huduma zinazotolewa na shirika hilo kwa sasa kuwa ni usajili wa jengo, kusimamia masuala ya usalama na ubora wa chakula na vipondozi na upimaji wa bidhaa za vyakula na vipodozi kwa lengo la kudhibiti ubora.
Majukumu mengine ni utoaji wa leseni au cheti cha TBS kwa bidhaa za chakula na vipodozi na usajili wa bidhaa za vyakula na vipodozi vinavyotoka nje ya nchi.

KAYA 970 KATA YA KIBADA WAUNGANA KUCHIMBA MTARO WA KUPITISHA MAJI KUNUSURU MAKAZI YAO

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, Globu ya jamii
KAYA 970 zilizopo katika mtaa wa Kiziza na Nyakale Kata ya kibada wilayani kigamboni jijini Dar es Salaam zimeungana kutafuta ufumbuzi wa changamoto ya maji kujaa katika makazi yao kwa kutengeneza mtaro wa kupitisha maji pindi mvua zinaponyesha ili kunusuru makazi yao.

Ili kukamilisha mradi wa uchimbaji wa mtaro uliowashirikisha wananchi kujenga hadi kukamilika kwake zinatarajia kutumika kwa shilingi  ya Bilioni moja au Bilioni 1.2.

Akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea baadhi ya mitaro katika eneo la kiziza na nyakale kuangalia maendeleo ya ujenzi wa mtaro ulipofikia,Mwenyekiti wa mradi wa mitaro kata ya Kibada, Nazzar Nicholaus alisema ulianza kutengenezwa januari 2018 na kasi ya ujenzi unaenda vizuri.

Nicholas ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo ya wananchi kwa Rais Magufuli,alisema ilikukamilisha mradi wote wa ujenzi wa mtaro wananchi wamekubaliana kushirikiana kwa kujitolea fedha,vifaa na Nguvu kazi.

"Ili kufanikisha mradi huu tunahitaji mkono mrefu na mkono mrefu tunazungumzia serikali.Hata hivyo wananchi tumeamua kuunga mkono juhudi za serikali za kutatua kero za wananchi chini ya Rais mpendwa Dk.John Magufuli kwa kuanza kuitatua kero hii," aliongeza

"Wakati wa kipindi cha mvua ndipo wananchi wa maeneo haya wanakuwa katika wakati mgumu Kutokana na maji kutuama katika makazi yetu hali inayofikia wanafunzi kushindwa kwenda shule na wafanyakazi kushindwa kwenda kwenye majukumu yao hivyo kwa umoja wetu tumeamua kutatua kero hii," alisema Nicholas

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Kibada,Amin Sambo alisema mradi huo ulianza mwaka 2005 chini ya wizara ya Ardhi ambapo wananchi wa eneo hilo walipoona mradi huo umesimama ndipo walipoamua kushirikiana kwa pamoja na kuamua kutengeneza moja ya Mtaro mkubwa ambao utapitisha maji kiurahisi n miitado midogo kuunganishwa kwa mtaro huo mkubwa.

"Tunautengeneza mtaro huo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, tumeamua kuchangishana na kutengeneza mtaro huo nia yetu ni kumsaidia Rais Magufuli kwa kutumia rasiliamari zetu wenyewe tulizonazo," alisema na kuongeza

"Tayari kazi imeanza na hadi sasa kuna kampuni moja ijulikanayo kwa jina la Plasisco imejitolea kutupatia Makaravati mawili ambayo yatatandikwa katika mtaro huo," amesema.

Wakati huo huo Mwenyekiti wa Mtaa WA Kiziza kata ya Kibada ,Adinani Simba amesema tatizo la maji katika eneo hilo lilianza siku nyingi mvua zinaponyesha na kuathiri nyumba nyingi na watu kushodwa kutoka kwenda kufanya shughuli zao.

Ame1sema katika eneo hilo 1kuna mitaro kama minne ambayo inahitajika kutengenezwa lakini 1wananchi wa eneo hilo wameamua kushirikiana na kutengeza mtaro mmoja mkubwa utakaopitisha maji kutoka katika mtaro mingine.
Kazi ya kuchimba mtaro ikiendelea katika Kata ya Kibada wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam ili kunusuru kaya 970 ambazo zimekuwa na changamoto ya maji kujaa wakati wa mvua za masika
Sehemu ya mtaro huo unaoendelea kuchimbwa kwa nguvu za wananchi wa Kata ya Kibada wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Mradi wa kuchimba Mtaro Kibada wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam, Nizzar Nicholaus akizungumzia kasi ya ujenzi wa mtaro huo unaojengwa kea lengo la kunusuru makazi ya wananchi wa eneo hilo.
Ofisa Mtendaji Kata ya Kibada, Salome Ngonyani akizungumza baada ya ziara ya kukagua mtaro unaochimbwa na wananchi wa Kata hiyo kwa ajili ya kunusuru makazi yao.

Benki Ya NBC Yaandaa Kongamano La Kibiashara Kwa Ajili Ya Wateja Wake Dodoma

$
0
0
  Benki ya NBC imeratibu kongamano maalum la kibiashara kwa ajili ya wateja wake wadogo na wakati jijini Dodoma ambalo pamoja na mambo mengine lililenga kuwaongezea wateja hao hao uelewa kuhusiana na mabadiliko ya kihuduma na fursa za kiuwezeshaji kutoka benki hiyo.

Akizungumza wakati wa kongamano hilo lililofanyika hivi karibuni jijini humo, Meneja Ukuzaji wa Biashara Kitengo cha biashara ndogondogo na za kati wa Benki hiyo, Bw Jonathan Bitababaje alisema kufuatia uboreshwaji mkubwa wa huduma za benki hiyo ambazo zinaendana na kasi ya kiteknolojia na fursa za kiuchumi kumekuwa na hitaji kubwa kwa wateja hao kujengewa uelewa ili waweze kwenda sambamba na mabadiliko hayo.

“NBC kwasasa tumefanya mabadiliko makubwa ya kihuduma yanayoendana na kasi ya kiteknolojia na ukuaji wa uchumi na tumeona kuwa mabadiliko haya yatakuwa na tija zaidi kwa wateja wetu hasa wadogo na wakati ikiwa tu tutawajengea uelewa wa kutosha ili waweze kwenda sambamba mabadiliko haya badala ya kuwa changamoto,’’ alibainisha.

Alisema mbali na kuwajengea uelewa kuhusu huduma za benki hiyo,kupitia kongamano hilo washiriki waliweza kutoa maoni yao ikiwa ni mrejesho wa huduma wanazopata kutoka benki hiyo, hatua aliyosema itasaidia taasisi hiyo kuboresha zaidi huduma hizo sambamba na kubuni huduma mpya zinazoendana na mahitaji ya wateja hao.

Aidha katika kongamano hilo la siku moja, mbali na masuala ya kibenki washiriki walipata fursa ya kusikiliza na kuchangia mada kutoka kwa wawakilishi wa taasisi nyingine ikiwemo Chemba ya biashara, viwanda na kilimo (TCCIA)na Baraza la Uwezeshaji (NEEC) ambao walielezea fursa mbalimbali za kibiashara ndani na nje ya nchi ikiwemo nafasi ya taasisi hizo katika kuwaunganisha wafanyabiashara na wenzao kutoka nje ya nchi.

“ Kwa kushirikiana na benki ya NBC tumekuwa tukishirikiana mambo mengi yanayolenga kuwasaidia wafanyabiashara wetu na hivi karibuni tunatarajia kuwasafirisha wafanyabiashara kwenda nchini China kwa ajili ya safari ya kibiashara ya siku kumi ambapo wahusika watalipa gharama ya kiasi cha Dola za Kimarekani 2500 tu ambayo itagharamia mahitaji yao yote ya msingi ikiwemo nauli ya kwenda na kurudi, gharama za chakula na huduma nyingine ikiwemo ya wakalimani,’’ alisema Bw Patrick Magai, Meneja Maendeleo Viwanda kutoka TCCIA.

Wakizungumza wakati wa kongamano hilo lililofutiwa na Uzinduzi wa Klabu wa Wafanyabiashara ya Benki hiyo mkoani humo, baadhi ya washiriki walisema pamoja na huduma za kifedha ipo haja ya taasisi za kifedha hapa nchini kuongeza ushirikiano zaidi na wafanyabiashara hao pindi wanapotafuta zabuni kubwa zenye kuhitaji dhamana kutoka taasisi hizo.

“Pia ipo haja kwa taasisi za fedha nchini kutambua baadhi ya changamoto zinazotukabili wateja wao kwenye biashara zetu kwa kubuni huduma zinazotambua changamoto zetu ikiwemo kuangalia namna ya kushirikiana nasi pindi tunapokabiliwa na changamoto ya ucheleweshwaji wa malipo yetu kutoka kwa wateja wetu,’’ alisema mmoja wa wafanyabiashara hao ambae ni Mkandarasi, Dr Steven Masangia.


Meneja Ukuzaji wa Biashara Kitengo cha biashara ndogondogo na za kati wa Benki hiyo, Bw Jonathan Bitababaje akiwasilisha mada kuhusiana na huduma za benki hiyo wakati wa Kongamano la kibiashara lililoandaliwa na Benki hiyo kwa ajili ya wateja wake wadogo na wa kati mkoani Dodoma lilillofanyika hivi karibuni jijini humo.


Maofisa waandamizi wa Benki ya NBC wakichangia mada kwenye kongamano hilo.
Maofisa waandamizi wa Benki ya NBC wakichangia mada kwenye kongamano hilo.
Maofisa waandamizi wa Benki ya NBC wakichangia mada kwenye kongamano hilo.
Baadhi ya wateja wa benki ya NBC wakichangia mada wakati wa kongamano hilo.
Baadhi ya wateja wa benki ya NBC wakichangia mada wakati wa kongamano hilo.
Baadhi ya wateja wa benki ya NBC wakichangia mada wakati wa kongamano hilo.
Baadhi ya wateja wa benki ya NBC wakichangia mada wakati wa kongamano hilo.
Muwakilishi kutoka Baraza la Uwezeshaji (NEEC) Bi Nyakao Mturi akiwasilisha mada wakati wa Kongamano hilo.

SAYANSI NA UTAFITI INA MCHANGO MKUBWA KUELEKEA UCHUMI WA KATI-DKT.MSANGI

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI
OFISA Utafiti Mkuu kiongozi kutoka Tume ya Sayansi na teknolojia ,Dkt Bakari Msangi amesema katika kuelekea kwenye uchumi wa kati ,sayansi na utafiti ina mchango mkubwa kufikia adhma na malengo hayo.

Ameeleza, kuelekea uchumi wa kati ,ikumbukwe kwamba uchumi wa viwanda unategemea zaidi viwanda vya malighafi za kilimo ,uvuvi na mifugo.

Akizungumza katika kiwanda cha kuchakata maziwa cha Tanga Fresh, wakati wa mafunzo ya vitendo kwa baadhi ya waandishi wa habari kanda ya Mashariki na watafiti, yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na teknolojia kwa ufadhili wa shirika la kimataifa la maendeleo la Sweden (SIDA ),Msangi alisema sayansi na utafiti ndio nguzo kwa wawekezaji wenye viwanda kuwahakikisha uzalishaji wa malighafi wanazozitegemea.

"Inasaidia ni wapi tunapata malighafi ya kutosha,kwasababu haina maana sana kuanzisha uzalishaji mfano wa ngano ya chapati wakati ngano mnayozalisha ni kidogo"

" Ni lazima mtafiti atafute ngano inayozalisha kwa wingi kwa mwaka mzima ili kumsaidia mwekezaji huyo azalishe kwa tija"alifafanua Msangi.

Nae kaimu mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa mifugo Tanzania ofisi ya Kanda, Zabron Nziku aliwataka wafugaji kubadilika kwa kufuga kisasa na kitaalamu .

Alielezea, wafugaji wakiweza kupanda aina bora za malisho,kuweka mabanda na kutumia utaalamu ya upandaji miche ya majani bora kwa ng'ombe kutoka katika taasisi hiyo basi wataongeza tija katika maziwa .

Awali meneja wa vyanzo vya maziwa Tanga Fresh, Nadomana Nyanga alibainisha ,kwa kushirikiana na Taasisi ya mifugo ya TALIRI wapo katika program ya kuangalia namna ya kuweza kuwalipa wafugaji kwa wanaozalisha kwa ubora.

"Zimbambwe wanafanya hivi, hivyo kwa Tanzania tukianza italeta maendeleo chanya kwa mfugaji ili afanye biashara ambayo ni endelevu"

Nadomana alisema kwasasa wanasindika lita 120,000 lakini wanazalisha lita 30,000 hadi 50,000 za maziwa kwa siku,kiwango kisichokidhi matakwa yao kutokana na uwezo wa wafugaji kupeleka maziwa kuwa mdogo.

Alifafanua kwamba, tukielekea katika uchumi wa kati inakadiriwa kila mtanzania hunywa maziwa lita 47 kwa mwaka na kutegemewa kufikia lita 100 kwa kipindi hicho kama ilivyo nchi ya Kenya.

Baadhi ya wafugaji Muheza ,Tanga akiwemo Sidori Charles alisema ,wana changamoto ya uhifadhi wa chakula cha kiangazi kwa ng'ombe ila kwa kupata elimu ameelewa ufugaji ng'ombe ni sayansi.

WASANII WASHAURIWA KUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII KUPITIA KAZI ZAO ZA SANAA

$
0
0
Na Khadija Seif, Globu ya Jamii
RAIS wa Zanzibar, Dr. Mohammed Shein anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la 'Utalii Kusini' lililoandaliwa na balozi wa hifadhi za utalii Nangasu Warema .

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Warema amesema Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika septemba 20 hadi 22 mwaka huu.

Amesema lengo la Tamasha hilo ni kukuza utalii wa kusini na kuhamasisha wawekezaji  kujitokeza kwa wingi ili kuboresha mazingira ya vivutio vya nchi ya Tanzania.

"Lengo la tamasha hili kukuza utalii wa kusini  kama mikoa mingine inavyopewa thamani kutokana na vivutio vilivyopo," amesema Warema.

Kwa upande wake Miss wa Tanzania 2018, Queen Elizabeth Makune amesema watanzania wanapaswa kutangaza vivutio vya utalii ili kujitangaza zaidi katika nchi za kigeni.

"Mkoa wa Kusini  umekuwa na vivutio mbalimbali vya kuwavutia watalii,
ifike mahali watanzania watangaze utalii  kwa manufaa ya nchi yetu,"
amesema Queen Elizabeth.

Msanii wa filamu za bongo nchini, Rose Ndauka amemalizia kwa kuwashauri wasanii kutangaza utalii wa nchi yao kupitia kazi wanazozifanya kwa lengo la kuongeza kipato katika sekta ya utali

RC PWANI AWAONYA WANAOWANYANYASA WAFANYAKAZI WAO

$
0
0
NA VICTOR MASANGU, PWANI
WAWEKEZAJI wa sekta ya viwanda wametakiwa kuhakikisha wanazingatia sheria na taratibu zote za kazi na kuachana na vitendo vya kuvunja sheria za nchi kwa kuamua kuwanyanyasa wafanyakazi wao kwa kuwanyima haki zao za msingi ikiwemo kuwapatia huduma ya matibabu, pamoja na kuwapatia maslahi yao kama inavyotakiwa bila ya kuwa na vitisho vyovyote ili kutumiza azma ya serikali ya kuwa na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja kwa ajili ya uwekeji wa jiwe la msingi katika kiwanda cha kutengenezea vifungashio (WANDE PRINTING) vitumikavyo katika sekta ya chakula,kilimo,viwanda, afya, ujenzi pamoja na viwanda ambacho kinajengwa katika eneo la kata ya Pangani Wilayani Kibaha na kuwaasa watendaji na mamlaka zinazohusika kuwapa ushirikiano wa kutosha wawekezaji hao bila ya ubaguzi na ubinafsi wowote.

Ndikilo alisema kwamba serikali ya awamu ya tano lengo lake kubwa ni kuendelea kushirikiana bega kwa wawekezaji mbali mbali wa ndani na nje ya nchi kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Rais Dk Jojn Pombe ,Magufuli hivyo wafanyakazi wanatakiwa kupewa haki zao stahiki bila ya kuonewa hasa katika suala la vitendea kazi pindi wanapokuwa katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

“Katika Mkoa wa Pwani kwanza nashukuru kwa sasa tunaendelea kushirikiana na wawekezaji wazawa ambao wamekuwa na nia ya kuendelea kuwekeza katika sekta ya viwanda katika maeneo mbali mbali. Lakini kila siku Rai yangu kubwa ni kuwapa haki zao zote waafanyakazi kwani wao ndio wapo mstari wa mbele katika kuzalisha bidhaa, kwa hivyo katika hili naomba sana kwa wawekezaji kuliangalia kwa jicho la tatu.”alisema Ndikilo.

Aidha Mkuu huyo aliipongeza Benki ya Azania kwa kuweza kuonyesha uzalendo kwa kushirikiana bega kwa bega na serikali ya awamu ya tano katika kuwapa sapoti na kuwawezesha mikopo wawekezaji ikiwemo kiwanda hicho kwa lengo la kuweza kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo kwa wananchi kupitia sekta ya viwanda.

Kwa upande wake mmoja wa wawekezaji wazawa katika kiwanda hicho John Obach akisoma risala kwa mgeni rasmi kwa niaba viongozi wenzake amebainisha kuwa ujenzi wa mradi huo umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 6.6 na kwamba wanatarajia kutoa ajira zaidi ya 300 ambazo zitaweza kuwasaidia wananchi kujikwamua kiuchumi na kuondokana na wimbi la umasikini.

Naye Mkurugenzi wa Azania Benki Charles Itembe ambao ndio wamewezesha kwa kiasi kikubwa ujenzi wa mradi huo wa kiwanda amesema kwamba lengo lao kubwa ni kuunga mkono sera ya Rais wa awamu ya tano Dr. John Pombe Magufuli ya kuwa na uchumi wa viwanda na kuahidi kuendelea kushirikiana na wawekezaji wengine katika kuinua sekta ya viwanda.

“Sisi kama taasisi ya kifedha Azania Benki nia na madhubmuni yetu makubwa ni kuhakikisha tunaaunga sera ya Rais wetu wa awamu ya tano Dk , John Pombe Magufuli katika kuwa na Tanzania ya viwanda, kwa hivyo ndio maana tumeamua kuwawezesha wenzetu wa kiwanda hiki cha kutengenezea vifungashio ili kuleta mapinduzi ya kuwa na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Pia liongeza kwa sasa wataendelea kutoa sapoti kwa wadau wa maendeleo pamoja na serikali katika kuhakikisha wananchi wanapata fursa mbali mbali za ajira kupitia miradi ya ujenzi ywa viwanda ambavyo vinajengwa katika maeneo tofauti lengo ikiwa ni kuondokana na wimbi la umasikini na jukikwamua kiuchumi.
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo wa kulia akipeana mkono na Mwenyekiti wa makampuni ya Global Packaging na Wande Printing Joseph Wasonga mara baada ya kumalizika kwa zoezi la uwekaji wa jiwe la msingi katika kiwanda cha kutengenezea vifungashio kilichojengwa Wilayani Kibaha.
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akikagua moja ya bidhaa ambazo zinazalishwa katika kiwanda cha Wande Printing ambacho kinatengeneza vifungashio wakati alipofanya ziara yake ya kikazi kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la msingi katika kuwanda hicho.
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarit Ndikilo akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbali mbali wa serikali, viongozi wa kiwanda hicho pamoja na wadau mbali mbali wa maendeleo ikiwemo Mkurugenzi wa benki ya Azania kulia kwake Charles Itembe.
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akisalimiana na viongozi mbali mbali wa serikali ambao walifika kwa ajili ya kushuhudia halfa ya uwekaji wa jiwe la msingi katika kiwanda hicho cha vifungashio.
 Mwenekano wa moja ya mitambo iliyopo katika kiwanda cha kutengeenzea vifungashio ambacho kinatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni Wilayani Kibaha.
 Mwenyekiti wa makampuni ya Global Packaging na Wande Printing Joseph Wasonga akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani juu ya mwenendo mzima katika uzalishaji wa kiwanda hicho cha kutengenezea vifungashio.
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akisalimiana na Mwenyekiti wa makampuni ya Global Packaging na Wande Printing Joseph Wasonga mara baada ya kutoa neno la utambulisho katika halfa hiyo ya uwekaji wa jiwe la msingi.(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)

SERIKALI HAITAMFUMBIA MACHO MKURUGENZI WA HALMASHAURI AMBAYE HATATENGA FEDHA ZA MIKOPO KWA WALEMAVU

$
0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Tv ,Arusha
KATIBU Mkuu wa ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamuhanga amezitaka halmashauri zote nchini ambazo bado zinasuasua katika kutekeleza sheria ya kutoa asilimia kumi ya mapato ya ndani kwa ajili ya vikundi vya walemavu, vijana na wanawake.

Amesema ili kuhakikisha wanatenga fedha zisiopungua asilimia 100 au zaidi kwa ajili ya kusaida vikundi na kubainisha kuwa serikali haita mfumbia macho mkurugenzi yeyote wa halmashauri ambaye atashidwa kutekeleza sheria hii ya kutenga fedha hizi kwa ajili ya kutoa mikopo kwa makundi haya.

Haya ameyasemwa katibu Mkuu wa ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamuhanga wakati alipotembelea kikundi cha watu wenyeulemavu cha Tumaini Ushiriki kilichopo wilayani Longido mkoani hapa ambapo alipata fursa ya kujionea mambo mbalimbali yanayofanywa na kikundi hicho ikiwemo unenepesha wa mbuzi kwa ajili ya kuwauza .

Amesema hii ndio njia pekee itakayosaidia serikali kuwawezesha wananchi wake kiuchumi na kuhahikisha wanainua kipato chao wanatengeneza ajira na wanakuza uchumi wa mwananchi na serikali kwa ujumla ili nchi yetu iweze kufikia viwango vya uchumi wa kati.

Hata hivyo ameungamkono kikundi Tumaini Ushiriki kikundi ambacho kinafanya kazi ya kunenepesha mbuzi kwa ajili ya kuwauza cha watu wenye ulemavu kwa kununua mbuzi moja ambaye aliwakabidhi kituo cha watoto yatima cha Namanga

Kwa upande wake katibu wa chama cha watu wenye ulemavu wilayani Longido ambaye pia ni mwanachama wa kikundi cha Tumaini Ushiriki, Emanuel Taraiya amesema ameiomba serikali kutenga bajeti kwa ajili ya kuwapa elimu watu wenye ulemavu.

Amesema wasikae ndani watoke nje wapaze sauti ili serikali iweze kutoa asilimia za fedha ambazo wametengewa kwa ajili ya mikopo ambayo itaweza kuwasaidia kwani walemavu wengi wamekuwa hawajui haki zao .

Kwa upande wake katibu wa kikikundi cha Tumaini Ushiriki Kitoitoi Ole Ndwati amesema kuwa kikundi chao kinafanya kazi ya kunenepa mifugo kwa ajili ya kuiuza katika masoko mbalimbali ,alisema kuwa kikundi chao kinaakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upande wa masoko kutokana na ushuru wa mifugo kupamba kwa kiasi kukubwa hali inayowafanya kukosa wateja wa kununua mifugo yao.

Amesema kuwa changamoto inayowakabili ni masoko pamoja na mazingira magumu ya kufanyia kazi, mitaji yao kuwa midogo, kauli au lugha chafu wanazotolewa na watu ambao sio walemavu hivyo ameiomba serikali kuwasaidia kutatua changamoto hizo ili nao waweze kufanya biashara na kunufaika.

Naye mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Longido mebainisha kuwa swala la kutoa mikopo kwa walemavu lazima atekeleze sheria ya kutenga fedha hizo kwa ajili ya kuwapatia kundi maalumu ambalo ni wanawake vijana na watu wenye ulimavu.

UWEZO WA WATALAAM KUWASHA VIFAA VYA KUSAIDIA KUSIKIA WAFIKIA 100%

$
0
0

Uwezo wa watalaam wazalendo kuwasha vifaa vya kusaidia kusikia (cochlear implants) watoto waliopandikizwa vifaa hivyo ambao walizaliwa wakiwa hawasikii sasa umeongezeka kufikia 100% huku kiwango cha kufanya upasuaji wenyewe kikifikia 90%.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kaimu Mkurugenzi Huduma za Upasuaji, Hospitali ya Taifa Muhimbili, (MNH) Dkt. Sufiani Baruani amesema baada ya upasuaji watoto hawa husubiri kipindi cha mwezi mzima ili waweze kuwashiwa vifaa husika. 

“Katika kuwasha vifaa hivyo, tulikua tukitegemea watalaam kutoka nje, lakini kwa sasa tunafurahi kuwa eneo hilo nalo tayari tumeliweza kwa 100% na leo tutafanya wenyewe bila kusaidiwa” amesema Dkt. Baruani. 

Ameongeza kuwa hatua hii inaashiria kuwa sasa huduma hizi nchini zitafanyika katika mfumo endelevu unaowezesha watalaam wa ndani kufanya wenyewe bila kutegemea watalaam wa nje. 

“Tangu kuanzishwa kwa huduma hii nchini Juni, 2017 wagonjwa 30 wamepandakizwa vifaa hivyo kati yao watoto ni 29 na mtu mzima mmoja. Huduma hii imekua ikitolewa kwa kushirikiana na madaktari bingwa wa upasuaji kutoka nchini Misri ambapo mwanzoni watalaam wazalendo walikua wakisaidia lakini hivi sasa watalaam wanafanya wenyewe kwa 90%” amesisitiza Dkt. Baruani.

Amesema upandikaji wa wagonjwa 30 uliofanyika ndani ya miezi 26 ni sawa na 60% ya wagonjwa 50  waliopelekwa nje ya nchi katika kipindi cha miaka 13 tangu Serikali ilipoanza kupeleka wagonjwa hao mwaka 2003 hadi 2016.

Amebainisha kuwa mpaka sasa, Serikali imetumia kiasi cha Tshs. 1.1 bilioni kuhudumia wagonjwa 30 kwa gharama ya Tshs. 37 milioni kwa mgonjwa mmoja na kama wangeenda nje ya nchi ingegharimu Tshs. 3 bilioni sawa na Tshs. 100 milioni kwa kila mgonjwa hivyo kuokoa Tshs. 1.89 bilioni.

Dkt. Baruani amesisitiza kuwa Hospitali imehakikisha utoaji wa huduma hizi unazingatia mahitaji na uwezo halisi wa mgonjwa anayehitaji huduma hii ambapo kwa sasa inagarimu mgonjwa kiasi cha Tshs. 37 milioni gharama hii ni kubwa kwa kuwa kifaa vya usikivu pekee yake kinagharimu kiasi cha Tshs. 31 milioni kwa mgonjwa mmoja na upasuaji Tshs. 6 milioni.
 Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Dkt. Sufian Baruani(katikati) akitoa taarifa leo kuhusu uwezo wa watoa huduma wazalendo kuwasha vya vifaa vya kusikia kuongezeka hadi 100%. Pembeni yake ni Madaktari Bingwa wa Upasuaji wa Pua, Koo na Maskio, Dkt. Aveline Kahinga na Dkt. Shaban Mawala.
 Wa pili kushoto, aliyekaa ni Bw. Waisai Wambura (55) akifurahi mara tu baada ya kuwashiwa kifaa alichopandikizwa (cochlear implant) na kusikia tena upya sauti. Bw. Wambura alipoteza uwezo wa kusikia ukubwani sasa anaweza kusikia tena.
 Bw. Waisai Wambura akiongea jambo na waandishi wa habari mara tu baada ya kusikia tena sauti. 
Mmoja wa watoto akielekezwa kupokea sauti mara tu baada ya kuwashiwa kifaa alichopandikizwa mwezi mmoja uliopita.

Benki ya Exim Yazindua Kampeni Kuhamasisha Matumizi ya Huduma Salama za Kifedha

$
0
0
Benki ya Exim Tanzania leo imezindua kampeni maalum inayolenga kuhamasisha wateja wake kuhusiana na matumizi ya mtiririko wa huduma maalumu za kiusalama kwenye masuala ya fedha zinazotolewa na benki hiyo.

Kupitia mtoririko huo imebainishwa kuwa wateja wa benki hiyo wanapata huduma mbalimbali ikiwemo huduma ya usafirishaji wa fedha kwa usalama (Cash-In-Transit service), huduma ya kiusalama ya malipo (Host to host services), huduma za kisasa za hundi (Corporate Cheque Capture service) pamoja na huduma ya kuweka (deposit) pesa kwenye akaunti ya benki hiyo wakati wowote kwa kutumia mashine ya kuwekea fedha (Cash Deposit Machines services). 

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam leo Mkuu wa Idara ta Masoko na Mahusiano wa benki hiyo Bw Stanley Kafu alisema kupitia huduma hizo wateja wa benki hiyo hawahitaji tena kupanga foleni kwenye matawi ya benki hiyo ili kupata huduma za kifedha au hata kuhofia muda wa kufungwa kwa huduma za benki hiyo kwa kuwa wanaweza kupata huduma wakiwa kwenye maeneo ya kazi. 

“Huduma hizi ni sehemu ya mkakati wa benki ya Exim Tanzania kutoa huduma kwa wateja bila kubanwa na muda wa kazi au umbali wa kijiografia.,’’ alisema Kafu 

Akifafanua kuhusu huduma ya usafirishaji wa fedha kwa usalama (Cash-In-Transit service), Kafu alisema inamuondolea mteja hatari (risk) ya kuibiwa, kuvamiwa, kunyang’anywa pesa wakati anazitoa ofisini kwake kupeleka benki kwa kuwa atapatiwa huduma ya kusafirisha fedha hizo kuelekea na kutoka benki kwa kutumia usafiri maalumu ukiwa na walinzi wenye mafunzo maalum ya kulinda fedha. 

“ Kupitia huduma yetu ya Host- to- Host service, mteja wetu anaruhusiwa kutumia matawi yetu yote Tanzania nzima kupokea malipo yake ya invoices kutoka kwa wateja wake wote nchi nzima. Huduma hii ni kwa wateja ambao wanatoa na kupokea hundi nyingi kutoka kwa watu mbalimbali kama vile vyuo vikuu, mashule, viwanda, kampuni za usafirishaji, kumpuni za clearing and forwarding, biasahara za mitandaoni, shughuli kama hoteli na utalii.’’ alitaja 

Aidha akizungumzia huduma ya ‘corporate cheque capture’ Kafu alisema hudumahiyo inayotumia ‘scanner’ inamuwezesha mteja kuweka hundi zake (deposit cheque) wakati wowote bila kutembelea tawi lolote la benki. 

“Hakuna haja ya kupanga foleni tena, huduma ipo ofisini au nyumbani kwako. Huduma hii ni maalumu kwa wateja wote wenye biashara ambazo zinapokea hundi (cheque) kwa wingi kila siku bila kujali ni shilingi za kitanzania ama dola za kimarekani, au inatoka benki gani hapa Tanzania. Hapa tunahusisha biashara kama za usafirishaji, mashirika ya bima, wauza magari au pikipiki na vipuli, maduka ya jumla, mawakala wa gesi, pamoja na viwanda mbalimbali.’’ Alitaja. 

Kuhusu huduma ya mashine ya kuweka fedha (Cash Deposit Machine), Kafu alisema , inamsaidia mteja kuweka (deposit) pesa kwenye akaunti ya benki hiyo wakati wowote bila kutembelea tawi la benki ambapo mteja akishaweka pesa katika mashine hiyo anapata risiti ambayo inaonyesha kuwa pesa tayari imeshaingia kwenye akaunti, na kisha mteja anaweza kuendelea kufanya miamala kama vile kutoa (withdraw) au kutuma malipo mbalimbali. 

“ Mashine hii inafanya kazi masaa 24 siku saba za wiki hivyo hakuna haja ya kupanga foleni tena, huduma ipo ofisini au kiwandani kwako. Huduma hii inamuondolea mteja risk (hatari) na wasiwasi wa kuibiwa, kuvamiwa, kunyang’anywa pesa wakati anazitoa ofisini kwake kupeleka benki.’’ Alisema. 

Aliongeza kuwa benki hiyo itaendelea kubuni huduma za kisasa zaidi ambazo si tu zinaokoa muda kwa wateja hao bali pia kuwahikikia usalama wao na fedha zao ili kwenda sambamba na kauli mbui ya benki hiyo inatosema “ Exim Tupo Kazini Leo Kwa Ajili Ya Kesho.

JESHI LA POLISI LAKAMATA MADUMU 859 YA MAFUTA

$
0
0


Kamanda wa polisi mkoani Pwani,Wankyo Nyigesa akiwaonesha waandishi wa habari mafuta yaliyokamatwa Bagamoyo.

Na Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo
JESHI la Polisi mkoani Pwani, limekamata madumu 859 ya mafuta ya kula yanayodaiwa kutolipiwa ushuru, yenye thamani takriban milioni 50, huko Chemchem kata ya Magomeni Bagamoyo.

Akithibitisha kuhusu tukio hilo, kamanda wa polisi mkoani hapo,Wankyo Nyigesa amesema ,madumu hayo yalikuwa yakisafirishwa na Christopher Emmanuel (32).

Alieleza kuwa, Christopher aliyasafirisha madumu hayo kupitia gari yake namba T.621 BCG aina ya fuso baada ya kukwepa kulipa ushuru kwenye moja ya bandari bubu Bagamoyo.

"Tunachunguza risiti zake za malipo kwani pia zina TIN namba tofauti, tunamshikilia mtu huyu pamoja na aliyeshirikiana nae kutoa Hassan Saidi mpemba huyu mkazi wa Bagamoyo."

Wankyo amesema, huo ni usafirishaji haramu na kutia hasara Taifa kwa kukwepa kulipa ushuru ama kodi,hivyo amewaasa wananchi kuacha biashara za magendo.

Kamanda huyo amefafanua, wafanyabiashara wanapaswa kulipa ushuru kwa maendeleo ya Taifa na sio kutaka faida kwa njia za mkato.

Amebainisha hawatawaachia nafasi wakwepa ushuru na kudhibiti mianya ya kukwepa ushuru kwenye bandari zote bubu kwakuwa zinafahamika.

SERA YA KILIMO KUPITIWA UPYA

$
0
0

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akiongoza kikao cha menejimenti ya wizara yake kinachofanya ukumbi wa wizara jijini Dodoma kuhusu maandalizi ya sera mpya ya kilimo ya mwaka 2019.
 Sehemu ya wajumbe wa Menejimenti,Taasisi na Bodi za Mazao zilizopo chini ya wizara ya kilimo wakifuatilia kikao kazi cha Waziri wa Kilimo leo jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akishiriki kikao cha menejimenti ya wizara kinachofanyika ukumbi wa Kilimo IV jijini Dodoma.

WIZARA wa Kilimo Japheti Hassunga leo amekutana na Menejimenti ya wizara,wakuu wa Taasisi na Wenyeviti wa Bodi za Mazao zilizopo chini ya Wizara. 

Lengo la mkutano huu wa siku mbili unaofanyika katika ukumbi wa wizara Jijini Dodoma ni kujadili maandalizi ya sera mpya ya kilimo ya mwaka 2019 na kuondoa mapungufu yaliopo katika sera ya mwaka 2013.

Akiongea katika kikao kazi hicho Waziri Hasunga ameeleza umuhimu wa kuwa na sera mpya ya kilimo ni kufanya kilimo kuwa na tija na cha kibiashara ,hivyo kuleta maendeleo makubwa katika sekta ya kilimo

“Tunataka sera mpya ya kilimo ilenge kukifanya kilimo kuwa shughuli kuu ya kiuchumi itakayochangia kukuza uchumi wa nchi na kuongeza ajira” alisisitiza Waziri Hasunga.

Waziri Hasunga amebainisha kwamba sera mpya inatakiwa kukamilika kabla ya mwisho wa mwaka huu ili kutoa fursa kwa Bunge kutunga sheria na kanuni za kilimo.

Aidha katika mkutano huu wizara ya kilimo itajadili na kupitia taarifa ya utekelezaji wa shughuli kwa mwaka 2018/2019 na kuweka mkakati madhubuti wa utekelezaji mipango utendaji kazi ya wizara kwa mwaka 2019/2020.

Kikao hicho kinahudhuriwa na Manaibu Waziri Hussein Bashe na Omary Mgumba,Katibu Mkuu Mhandisi Mathew Mtigumwe na Naibu Katibu Mkuu 

Imeandaliwa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Kilimo-DODOMA

TANCOAL YATAKIWA KULIPA DENI LA DOLA MILIONI 10.4

$
0
0
Na Greyson Mwase, Dodoma

TUME ya Madini imeitaka kampuni ya kuzalisha makaa ya mawe nchini ya TANCOAL kulipa deni la Dola za Marekani 10,408,798 ambalo ni kwa kipindi cha Septemba, 2011 hadi Juni, 2019 na kuacha kupotosha umma wa watanzania.

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 16 Septemba, 2019 jijini Dodoma na Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya kwenye mkutano wake na waandishi wa habari kufuatia taarifa za upotoshaji ambazo zimekuwa zikichapishwa na kampuni ya TANCOAL kupitia tovuti ya www.miningreview.com tarehe 03 Septemba, 2019 na kusambazwa kwenye mitandao mingine ya kijamii.

Mkutano huo ulihudhuriwa na Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula, Mkurugenzi wa Ukaguzi na Biashara ya Madini, Dkt. Venance Mwase, Mkurugenzi wa Huduma za Tume, William Mtinya, Meneja wa Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Gift Kilimwomeshi, Meneja wa Leseni, Mhandisi Ramadhani Lwamo na Kaimu Meneja wa Utafiti na Sera, Andendekisye Mbije. 

Profesa Manya alifafanua kuwa, kampuni ya TANCOAL kupitia taarifa yake ilidai kuwa, Wizara ya Madini kupitia Tume ya Madini imeanza kuitoza TANCOAL tozo ya mrabaha kwenye gharama za usafirishaji wa makaa ya mawe kutoka mgodini hadi kwa mtumiaji wa mwisho wa ndani na nje ya nchi.

Aliongeza kuwa, kampuni ya TANCOAL ilidai kulazimishwa kuuza makaa ya mawe kwa wateja wenye leseni za biashara ya madini hali itakayoongeza gharama za makaa ya mawe.

Profesa Manya alisema kuwa TANCOAL imekuwa ikilipa tozo ya mrabaha kwa kuzingatia thamani ya madini yakiwa yadi ya Kitai bila kujumuisha gharama za usafirishaji kwenda kwa wateja jambo ni kinyume na Sheria ya Madini ya Mwaka 2010.

“Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 kifungu cha 87 (6) kinaelekeza namna ya kukokotoa mrabaha kwa kuzingatia thamani ya madini sokoni (kwa mtumiaji wa mwisho) ambayo inajumuisha gharama za usafirishaji hadi kwa mteja (Gross Value). Utaratibu huu wa malipo umekuwa ukifuatwa na kampuni nyingine zote zinazochimba ama kuuza makaa ya mawe isipokuwa TANCOAL,” alisema Profesa Manya.

Aliongeza kuwa, pamoja na kuelimishwa mara kwa mara juu ya namna ya kukokotoa malipo ya mrabaha kwa mujibu wa Sheria ya Madini ya Mwaka 2010, TANCOAL imekuwa ikikaidi kulipa mrabaha kwa kuzingatia msingi huo.

Alisema kuwa, utaratibu ambao kampuni ya TANCOAL inautumia kwa kuwauzia wateja wa makaa ya mawe katika yadi ya Kitai badala ya kusafirisha wenyewe au kutumia wafanyabiashara wa madini walioidhinishwa (Mineral Brokers or Dealers) unakwenda kinyume cha Sheria. Kifungu cha 18 (1) cha Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 kinakataza mtu au kampuni yeyote isipokuwa mmiliki halali wa leseni ya madini au mfanyakazi wa wamiliki wa leseni hizo: kumiliki, kusafirisha au kuuza madini bila kuwa na kibali cha kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria.

Alifafanua kuwa, kutokana na Kampuni ya TANCOAL kulalamikia Madai ya Mrabaha inayotakiwa kulipa Serikalini, iliundwa Timu maalum kwa ajili ya kuhakiki deni la mrabaha unaojumuisha usafirishaji wa makaa ya mawe kwa kwa kipindi cha Septemba, 2011 hadi Juni, 2014 ambayo yalikuwa hayajalipwa pamoja na kufanya upembuzi wa madai ya mrabaha ambao TANCOAL inatakiwa kulipa Serikalini kwa kipindi cha Septemba 2011 hadi Juni, 2019.

Alisema kuwa katika upembuzi na uchambuzi wa takwimu za mauzo na usafirishaji wa makaa ya mawe uliofanyika, imebainika kuwa TANCOAL inatakiwa kulipa USD 1,103,594 ikijumuisha na adhabu ya asilimia 50 kwa kipindi cha Septemba 2011 hadi Juni 2014. TANCOAL inapaswa kulipa USD 9,305,205 ikijumuisha na adhabu ya asilimia 50 kwa kipindi cha Julai 2014 hadi Juni 2019. Jumla ya malipo ni USD 10,408,798 kwa kipindi cha Septemba, 2011 hadi Juni, 2019.

Naye Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula akizungumza katika mkutano huo aliitaka kampuni ya TANCOAL kutopandisha bei ya makaa ya mawe kwa wateja na badala yake kuuza kulingana na bei elekezi zinazotolewa na Tume ya Madini kila mwezi.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya (katikati) akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani kwenye mkutano wake na vyombo vya habari uliofanyika leo tarehe 16 Septemba, 2019. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula na kushoto ni Mkurugenzi wa Ukaguzi na Biashara ya Madini, Dkt. Venance Mwase.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula (kulia) akifafanua jambo katika mkutano huo.

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WABUNGE KUTOKA BUNGE LA UJERUMANI

$
0
0
 Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (katikati) akizungumza na Wajumbe wa Chama Marafiki wa Wabunge wa Afrika Mashariki kutoka Bunge la Ujerumani (kulia) waliotembelea Bunge la Tanzania kwa lengo la kuimarisha uhusiano baina ya pande zote mbili Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni baadhi ya Wabunge wa Bunge la Tanzania waliohudhuria kikao hicho
 Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge Marafiki wa Afrika Mashariki kutoka Bunge la Ujerumani Mhe. Manfred Todtenhausen (wa kwanza kushoto) akimueleza jambo Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (katikati) wakati wa ziara yao katika Bunge la Tanzania yenye lengo la kuimarisha uhusiano baina ya pande zote mbili.
 Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge Marafiki wa Afrika Mashariki kutoka Bunge la Ujerumani Mhe. Manfred Todtenhausen (kulia) akimueleza jambo Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (katikati) wakati wa ziara yao katika Bunge la Tanzania yenye lengo la kuimarisha uhusiano baina ya pande zote mbili.
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (katikati) akiagana na Kaimu Balozi wa Ujerumani hapa nchini Joerg Herrera mara baada ya kunzungumza na Wajumbe wa Chama Marafiki wa Wabunge wa Afrika Mashariki kutoka Bunge la Ujerumani. Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Mhe. Manfred Todtenhausen. PICHA NA BUNGE

RAIS DKT MAGUFULI AFUNGUA KIWANDA CHA PIPE INDUSTRIES ENEO LA VINGUNGUTI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe akiwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa pamoja na Wakurugenzi Wakuu wa Pipe Industries Co. Limited Bw,. Seif A. Seif na Nassor A. Seif pamoja na viongozi na wadau wengine pazia kuashiria kufunguliwa rasmi kwa kiwanda chao cha kutengeneza mipira na mabomba ya plastiki eneo la Vingunguti jijini Dar es salaam leo Septemba 16. 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Wakurugenzi Wakuu wa Pipe Industries Co. Limited Bw,. Seif a, Seif na Nassor A. Seif baada ya kufunua pazia kuashiria kufunguliwa rasmi kwa kiwanda chao cha kutengeneza mipira na mabomba ya plastiki eneo la Vingunguti jijini Dar es salaam leo Septemba 16. 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo ya kazi za uzalishaji za Pipe Industries Co. Limited akiwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa pamoja na Wakurugenzi Wakuu wa kiwanda hicho Bw,. Seif A. Seif na Nassor A. Seif pamoja na viongozi na wadau wengine pazia kuashiria kufunguliwa rasmi kwa kiwanda chao cha kutengeneza mipira na mabomba ya plastiki eneo la Vingunguti jijini Dar es salaam leo Septemba 16. 2019 PIHA NA IKULU

RC MWANRY AWALINGANISHA WALIMU NA SILAHA YA KATYUSHA ILIYOTUMIWA KWENYE VITA YA PILI YA DUNIA NA ILIYOKUWA MUUNGANO WA KISOVYETI

$
0
0
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said-TABORA
MKUU wa Mkoa wa Tabora Mhe. Aggrey Mwanry amewalinganisha walimu na silaha aina ya Katyusha iliyotumiwa na majeshi ya Muungano wa Kisovyeti (Soviet Union) au Urusi wakati wa vita Kuu ya Pili ya Dunia kwa vile huwa hawashindwi katika jambo lolote.
Mhe. Mwanry ameyasema hayo leo Septemba 16, 2019 Mkoani Tabora wakati akifungua Kongamano la Walimu la “Amsha Amsha na Mwalimu Bank”  lililoandaliwa na Mwalimu Commercial Bank kwa lengo la kutoa elimu ya fedha ikiwa ni pamoja na kujenga hamasa kwa walimu kutumia huduma za benki hiyo ambayo kwa kiasi kikubwa inamilikiwa na walimu nchini.
“Katyusha ni silaha iliyotumiwa na majeshi ya Muungano wa Kisovyeti (Soviet Union) au Urusi kwenye vita Kuu ya Pili ya Dunia,  na iliwapatia mafanikio makubwa katika mapambano hayo, na mimi walimu wangu Mkoani Tabora huwa nawalinganisha na silaha ya Katyusha kwani huwa hawashindwi kitu, wamenisaidia sana katika kampeni mbalimbali za maendeleo hapa Tabora ikiwemo ile ya upandaji miti ambayo imefanikiwa.” Alisema.
Alisema kwa niaba ya serikali Mkoani Tabora na wananchi wa Mkoa wa Tabora na Walimu kwa ujumla wako tayari wanaikaribisha benki ya Biashara ya Mwalimu mkoani humo ikiwa ni pamoja na kutumia huduma zake.
“Wameona isiwe tu kazi ya kufundisha darasani bali wameona wanasweza kutengeneza kitu kinachoitwa Benki ya biashara ya Mwalimu, umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu, ukienda benki wao hawaangalii hivi mnavyofikiria wanaangalia umeingiza kiasi gani na utachukua kiasi gani na umekopa shilingi ngapi na utarudisha kiasi gani nawapongeza kwa kuwa na chombo hiki.” Alisema.
Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank, Bw. Richard Makungwa alisema, moja ya mikakati ya benki hiyo kwa sasa ni kuhakikisha inawafikmia walimu nchi nzima na wameanza kwa kongamano kama hilo mkoani Kigoma kwa nia ya kutoa elimu ya fedha lakini pia kujenga hamasa kwa walimu kutumia huduma za benmi hiyo ambayo inamilikiwa na walimu kwa kiasi kikubwa.
“Benki yetu sasa ina miaka mitatu tangu ianze shughuli zake, benki hii ni mali yenu, tumieni huduma za benki yenu, tayari tuna matawi mawili Dar es Salaam, na tumefungua ofisi kwenye mikoa ya Morogoro, Mwanza na Mbeya na tunakusudia kufanya hivyo kadri muda unavyokwenda na ndio maana tuko hapa leo kuamsha amsha mwalimu na benki yenu.” Alifafanua Bw. Makungwa ambaye alifuatana na Kaimu Mkuu wa Biashara na Masoko, Bi. Leticia Ndongole na Mkurugenzi wa Fedha Bw. Selemani Kijori.
Aidha washiriki nao wamepongeza hatua ya uongozi wa benki kuwafikia huko mikoani na kushauri kuwa benki lazima iwe karibu na wateja wake ili kujenga kuaminiana.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey Mwanry, akifungua kongamano la walimu la "Amsha Amsha na Mwalimu Bank" Mkoani humo kwenye ukumbi wa Chama cha Walimu Septemba 16, 2019. Kongamano hilo lililoandaliwa na Mwalimu Bank, lililenga kutoa elimu ya fedha kwa walimu ikiwa ni pamoja na kutoa hamasa kwa walimu kuitumia benki hiyo ambayo asilimia kubwa ya wanahisa wake ni walimu.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank Plc, Bw. Richard Makungwa.(kulia), akitoa hotuba yake kwenye kongamano hilo. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey Mwanry na Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Mkoa wa Tabora, Bw.Norbert Pandisha.
  Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey Mwanry, akifungua kongamano la walimu la "Amsha Amsha na Mwalimu Bank" Mkoani humo kwenye ukumbi wa Chama cha Walimu Septemba 16, 2019. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank Plc, Bw. Richard Makungwa.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank Plc, Bw. Richard Makungwa.(kulia), akitoa hotuba yake kwenye kongamano hilo. 
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank Plc, Bw. Richard Makungwa.(kulia), akitoa hotuba yake kwenye kongamano hilo. 
  Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank Plc, Bw. Richard Makungwa.(kulia), akitoa hotuba yake kwenye kongamano hilo. 
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey Mwanry (kulia) na Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Mmoani Tabora (WCT), Bw. Norbert Pandisha, wakimsikiliza Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Bw.Aron Masalu, (kushoto), wakati akitoa hotuba yake kwenye kongamano hilo. 
 Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Mmoani Tabora (WCT), Bw. Norbert Pandisha
 Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Bw.Aron Masalu
 Baadhi ya walimu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Aggrey Mwanry (hayupo pichani).
 Kaimu Mkuu wa Biashara na Masoko Mwalimu Commercial Bank Plc. Bi. Leticia Ndongole akitoa elimu ya fedha kwa washiriki.
 Mshiriki akizungumza kwenye kongamano hilo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank Plc. Bw. Richard Makungwa (kulia), akiwa na Kaimu Mkuu wa Biashara na Masoko wa benki hiyo. Bi. Leticia Ndongole wakisikiliza maoni ya washiriki.

 Washiriki wakiwa kwenye kongamano hilo.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank Plc. Bw. Richard Makungwa (katikati), akijadiliana jambo na Kaimu Mkuu wa Biashara na Masoko wa enki hiyo na Afisa Uhusiano, Bw. Said Rajabu wakati wa kongamano hilo.
  Washiriki wakiwa kwenye kongamano hilo.
 Washiriki wakiwa kwenye kongamano hilo.


 Baadhi ya washiriki wakisikiliza hotuba ya Mkuu wa Mkoa.
 Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Mkoa wa Tabora, Bw.Norbert Pandisha, (wapili kulia), Katibu wa CWT Mkoa wa Tabora, Bw.Aron Masalu (watatu kulia), Mkurugenzi wa Fedha wa MCB, Bw.Selemani Kijori (kushoto) na Kaimu Mkuu wa Biashara na Masoko, Bi. Leticia Ndongole.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey Mwanry (kulia), akifurahia jambo na Afisa Uhusiano wa benki hiyo, Bw. Michael Kachala

SERIKALI KUENDELEA KUJUMUISHA MASUALA YA WATU WENYE ULEMAVU KATIKA MIPAGO NA BAJETI NGAZI YA WIZARA

$
0
0
Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) imewahakikishia watu wenye ulemavu nchini kupitia Shirikisho la Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) kuwa itaendelea kujumuisha masuala ya watu wenye ulemavu katika mipango na bajeti kwa ngazi ya Wizara ili kuweza kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata huduma bora na stahiki.

Akiongea wakati wa kikao kazi kuhusu ushawishi na utetezi pamoja na ujumuishwaji wa masuala ya watu wenye ulemavu katika mipango na bajeti ngazi ya wizara, kilicho washirikisha Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, viongozi kutoka SHIVYAWATA na Shirika la Kimataifa la ADD, leo jijini Dodoma, tarehe 16 Septemba, 2019, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Watu wenye Ulemavu wa Ofisi hiyo, Filbert Kawemwamwa amebainisha kuwa lengo la kikao hicho ni kuibua mikakati ya ujumuishaji, usimamizi na utekelezaji wa masuala watu wenye ulemavu nchini.

“Katika kuhakikisha kuwa mipango na bajeti ngazi ya wizara zinajumuisha masuala ya watu wenye ulemavu tutaendelea kukutana na wizara nyingine saba za kisekta ili kuweza kuhakikisha mipango ya maendeleo yao inaweza kuwafikia watu wenye ulemavu hasa walio vijijini, kwa kuzingatia Sera ya Taifa ya Maendeleo na Huduma ya Watu wenye Ulemavu ya Mwaka 20014” amesistiza Kawemwamwa

Awali akiongea katika kikao hicho Mwenyekiti wa Shirikisho la Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Ummy Ndeliyanaga, ameshukuru kwa jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya Tano, inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli katika kuboresha huduma za msingi za watu wenye Ulemavu nchini, hata hivyo amebainisha kuwa wanazo hoja za msukumo kumi ambazo anaamini utekelezaji wake ukikamilika zitaboresha huduma na maendeleo kwa watu wenye ulemavu nchini.

“Tayari serikali kupitia ofisi ya Waziri Mkuu imeshaunda madawati ya watu wenye ulemavu katika wizara na taasisi zake tunaomba majukumu ya maofisa hao yapitiwe upya, pia uanzishwaji wa mchakato wa uundwaji wa mfuko wa Kitaifa wa watu wenye Ulemavu, masuala mengine ni kuanzishwa kwa rejista ya watu wenye ulemavu, kupitia sheria ya watu wenye ulemavu, Makakati wa ufukiwaji wa 3% ya watu wenye ulemavu kwenye kila taasisi inayo ajiri watu kuanzia 20” amesema Ndeliyanaga

Ameongeza kuwa wanaomba serikali isisimamie ukamilishwaji wa mchakato wa uandaaji wa taarifa ya utekelezaji wa mkataba wa umoja wa mataifa wa haki za watu wenye Ulemavu, pamoja na kuwaelekeza waajiri wote kuandaa na kuwasilisha taarifa ya mwaka ya hali ya ajira kwa watu wenye ulemavu katika taasisi zao, pia ukamilshawaji wa mwongozo wa viwango vya ufikikaji wa miundo mbinu, Mipango ya Kisekta pamoja na Baraza la ushauri la watu wenye ulemavu kuhakikisha linafanya kazi kikamilifu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Programu, Shirika la Kimataifa la ADD, Rose Tesha, amefafanua kuwa shirika hilo limeamua kuunga juhudi za serikali za kuwahudumua watu wenye Ulemavu kwa kuwezesha SHIVYAWATA kukutana na wizara za kisekta ili kuweza kuhakikisha kuwa wanaweza kuzitetea vizuri fursa na haki za watu wenye ulemavu hapa nchini.

Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) iliundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Tangazo kwenye gazeti la Serikali Na.144 la mwezi Aprili, 2016. Pamoja na majukumu mengine Ofisi hiyo inajukumu la kusimamia utekelezaji wa sera, sheria, AMiongozo, Kanuni na Viwango vya Ubora katika utoaji wa huduma za watu wenye ulemavu nchini.
 Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge), Parkshard Mkongwa akieleza umuhimu wa ujumuishwaji wa masuala ya watu wenye ulemavu katika mipango na bajeti ngazi ya wizara wakati wa kikao cha Menejimenti ya wizara hiyo na , viongozi kutoka SHIVYAWATA na Shirika la Kimataifa la ADD, leo jijini Dodoma, tarehe 16 Septemba, 2019, kulia kwake ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Watu wenye Ulemavu wa Ofisi hiyo, Filbert Kawemwamwa.
 Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Watu wenye Ulemavu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Filbert Kawemwamwa. wa akieleza umuhimu wa ujumuishwaji wa masuala ya watu wenye ulemavu katika mipango na bajeti ngazi ya wizara wakati wa kikao cha Menejimenti ya wizara hiyo na , viongozi kutoka SHIVYAWATA na Shirika la Kimataifa la ADD, leo jijini Dodoma, tarehe 16 Septemba, 2019, kushoto kwake ni Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge), Parkshard Mkongwa.
 Baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia kikao cha Menejimenti ya wizara hiyo na , viongozi kutoka SHIVYAWATA na Shirika la Kimataifa la ADD, wakati wa kujadili namna ya ujumuishwaji wa masuala ya watu wenye ulemavu katika mipango na bajeti ngazi ya wizara leo jijini Dodoma, tarehe 16 Septemba, 2019.
 Mwenyekiti wa SHIVYAWATA, Ummy Ndeliyanaga, akieleza umuhimu wa ujumuishwaji wa masuala ya watu wenye ulemavu katika mipango na bajeti ngazi ya wizara wakati wa kikao cha Menejimenti ya wizara hiyo na , viongozi kutoka SHIVYAWATA na Shirika la Kimataifa la ADD, leo jijini Dodoma, tarehe 16 Septemba, 2019.
 Mkurugenzi wa Programu, Shirika la Kimataifa la ADD, Rose Tesha, akieleza umuhimu wa utetezi wa pamoja wa masula ya watu wenye ulemavu wakati wa kikao cha Menejimenti ya wizara hiyo na , viongozi kutoka SHIVYAWATA na Shirika la Kimataifa la ADD, leo jijini Dodoma, tarehe 16 Septemba, 2019.
 Baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia kikao cha Menejimenti ya wizara hiyo na , viongozi kutoka SHIVYAWATA na Shirika la Kimataifa la ADD, wakati wa kujadili namna ya ujumuishwaji wa masuala ya watu wenye ulemavu katika mipango na bajeti ngazi ya wizara leo jijini Dodoma, tarehe 16 Septemba, 2019.
 Mkalimani kwa kutumia lugha ya alama, Edna James, akieleza umuhimu wa utetezi wa pamoja wa masula ya watu wenye ulemavu wakati wa kikao cha Menejimenti ya wizara hiyo na , viongozi kutoka SHIVYAWATA na Shirika la Kimataifa la ADD, leo jijini Dodoma, tarehe 16 Septemba, 2019.
 Baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Watu wenye Ulemavu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Filbert Kawemwamwa. wakati wa kikao cha Menejimenti ya wizara hiyo na , viongozi kutoka SHIVYAWATA na Shirika la Kimataifa la ADD, wakati wa kujadili namna ya ujumuishwaji wa masuala ya watu wenye ulemavu katika mipango na bajeti ngazi ya wizara leo jijini Dodoma, tarehe 16 Septemba, 2019.

SERIKALI YACHUKIZWA NA MGONGANO WA DC, DED MALINYI

$
0
0
*Waziri Mkuu aelekeza weledi wao kiutendaji uchunguzwe

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amechukizwa na mgongano uliopo kati ya Mkuu wa Wilaya ya Malinyi, Majura Kasika na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo Mussa Mnyeti, hivyo kumuelekeza Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora kwenda kuchunguza weledi wa utendaji kazi wao.

“Ni aibu Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli amewateua vijana wawe viongozi lakini leo hadi wananchi wa kawaida wanajua mgongano wenu maofisini. Ni aibu Mkuu wa Wilaya ya Mkurugenzi mnagombana tena wakati mwingine mnagombania miradi, mmesahau kutekeleza majukumu yenu.”

Waziri Mkuu ametoa maelekezo hayo leo (Jumatatu, Septemba 16, 2019) wakati akizungumza na watumishi wa wilaya ya Malinyi pamoja na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Toboa, akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro.

Amesema Serikali imewapa nafasi hiyo ili wakasimamie maendeleo ya wananchi na inapeleka fedha kwa ajili ya kuboresha maendeleo ya jamii kama kuimarisha huduma za afya, elimu, maji na miundombinu ya barabara lakini wao wanagombania miradi na mingine wanaichakachua.

Waziri Mkuu amesema mbali na CAG na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora kwenda kuchunguza utendaji wa viongozi hao, pia ameuelekeza uongozi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wakakague miradi ya ujenzi inayotekelezwa kwenye wilaya hiyo kama ubora wake unalingana na thamani halisi.” Baada ya kupata majibu ya uchunguzi na kubaini kiini cha tatizo ndani ya wilaya hii hatua zitachukuliwa.”

Awali, Mbunge wa Jimbo la Malinyi, Dkt. Haji Mponda alimweleza Waziri Mkuu kwamba kwenye wilaya hiyo kuna matatizo ya mahusiano kati ya Serikali na Halmashauri jambo linalosababisha kukwama kwa shughuli za maendeleo.

Mbunge huyo alisema kutoelewana kwa viongozi wa wilaya hiyo Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi kumesababisha mgawanyo mkubwa kuanzia katika Baraza la Madiwani hadi kwa wananchi mitaani, hivvyo alimuomba Waziri Mkuu awasaidie katika. Kilipatia ufumbuzi suala hilo.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema kuwepo kwa mabango mengi kwenye mikutano ya hadhara ya viongozi wakuu kunadhihirisha wazi kwamba watendaji wa Halmashauri hawawatembelei wananchi katika maeneo yao na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili.

“Watendaji hamuendi kuwatembelea wananchi na kusikiliza matatizo yao, haiwezekana wawe wanawasubiri viongozi wa juu na kuwasilisha kero zao kwa njia ya mabango, sasa jipangeni haya mabango yote mtakuja kuyajibu kwa sababu katika mabango yao hakuna hoja hata moja inayomuhusu Waziri Mkuu zote ni za ngazi ya halmashauri.”

Waziri Mkuu amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imeelekeza nguvu kubwa katika kuwatumikia wananchi na kutatua kero zao, hivyo itasimamia kuhakikisha kila mtumishi anawajibika kwa kiwango kinachostahili.

Mapemaalipowasili wilayani Malinyi, Waziri Mkuu aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi linalojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa kwa gharama ya sh. bilioni 3.9. Ujenzi huo ulianza 29/11/ 2017 na utakamilika 29/09/ 2019. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi, baada ya kukagua na kuweka jiwe la msingi, la jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi, mkoani Morogoro, Septemba 16.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images