Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live

WATANZANIA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA YA MFUKO MPYA WA HATIFUNGANI (BOND FUND)

0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, akizindua  Mfuko wa Uwekezaji wa Hatifungani (BOND Fund) wa kampuni ya UTT Amis katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha  Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo, Wanaoshuhudia ni  Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya UTT-AMIS, Bw. Simon Migangala na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) Bw. Nicodemus Mkama
KATIBU Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, Mwenyekiti wa Bodi ya UTT Amis Bw. Casmir Kyuki , Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya UTT-AMIS, Bw. Simon Migangala na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA)Bw. Nicodemus Mkama wakizindua Mfuko wa Uwekezaji wa Hatifungani (BOND Fund) wa kampuni ya UTT Amis katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha  Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
KATIBU Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James akimpongeza Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA)Bw. Nicodemus Mkama mara baada ya uzinduzi wa Mfuko wa Uwekezaji wa Hatifungani (BOND Fund) wa kampuni ya UTT Amis katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha  Julius Nyerere jijini Dar es salaam, wa pili kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya UTT-AMIS, Bw. Simon Migangala na Mwenyekiti wa Bodi ya UTT Amis Bw. Casmir Kyuki. 
 KATIBU Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James akisoma hotuba fupi mbele ya Wageni waalikwa na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa uzinduzi wa Mfuko wa Uwekezaji wa Hatifungani (BOND Fund) wa kampuni ya UTT Amis,uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha  Julius Nyerere jijini Dar es salaam. 
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) Bw. Nicodemus Mkama akizungumza mbele ya Wageni waalikwa na Waandishi wa Habari (hawapo pichani),wakati wa uzinduzi wa Mfuko wa Uwekezaji wa Hatifungani (BOND Fund) wa kampuni ya UTT Amis,uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha  Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
 Waageni waalikwa mbalimali wakifuatilia tukio hilo ndani ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha  Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
 Baadhi ya Wadau wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye hafla hiyo
..........................................................

Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam

KATIBU Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, amezindua mfuko mpya wa uwekezaji wa pamoja ujulikanao kama Mfuko wa Hatifungani (Bond Fund) unaomilikiwa na Kampuni ya UTT-AMIS, wenye lengo la kuwawezesha wawekezaji wadogo na wakubwa kutoka ndani na nje ya nchi kuweka akiba, kukuza mitaji na kipato chao.

Akizindua Mfuko huo Jijini Dar es Salaam, Bw. James ameiagiza Kampuni ya UTT-AMIS kutoa elimu ya kutosha kwa umma ili wananchi wengi zaidi wanufaike na fursa mbalimbali zinazotolewa na Serikali ili kuwawezesha kumiliki uchumi wa chi yao.

Alisema kuwa UTT-AMIS inamiliki mifuko mitano yenye thamani ya sh. bilioni 300 ikiwa na wawekezaji 145,000 pekee ikilinganishwa na idadi kubwa ya watanzania.

“Namba hii ni ndogo na jitihada kubwa inahitajika ili kuwafikia watu wengi zaidi, hivyo nawaelekeza muendelee kutoa elimu kwa wananchi na wadau wengine wote ili mifuko hii iwe chachu ya maendeleo nchini” alisema Bw. James

Alitoa wito kwa mashirika na taasisi mbalimbali kuchangamkia fursa za kuwekeza katika Mfuko huo mpya wa Hatifungani kwa kuwa ni salama na una faida kubwa.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya UTT-AMIS, Bw. Simon Migangala, alisema kuwa mwekezaji anaweza kuwekeza kwenye Mfuko huo mpya kuanzia sh. 50,000.

“Mwekezaji atakaye wekeza sh. 10,000,000 atapata gawio kila mwezi, atakaye wekeza sh. 5,000,000 atapata gawio la mara moja kila baada ya miezi sita wakati watakaowekeza sh. 50,000 na zaidi watapata fursa ya kukuza mitaji yao” alisisitiza Bw. Migangala

Alifafanua kuwa Bond Fund ni uwekezaji wa pamoja uliowazi ambao utawekeza kwenye hatifungani za Serikali, hatifungani za mashirika na uwekezaji katika masoko ya fedha lengo kuu likiwa ni kuwawezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika soko la mitaji

UTT-AMIS inasimamia na kuendesha mifuko mingine mitano ikiwemo Mfuko wa Umoja, Mfuko wa Wekeza Maisha, Mfuko wa Watoto, Mfuko wa Kujikimu na Mfuko wa Ukwasi.

Nae Afisa Mtendaji  Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA),Bw.Nicodemus Mkama amesema kuwa hafla hiyo inaweka historia kubwa katika maendeleo ya Masoko ya mitaji hapa nchini,kwani uzinduzi wa mfuko huo utatoa fursa kwa wawekezaji kuwekeza kwenye dhaman mbalimbali ikiwa ni pamoja na hatifungani za Serikali Kuu na hatifungani za kampuni binafsi.

''Hivyo basi napenda kutumia fursa hii kuipongeza bodi ya Wakurugenzi na Uongozi wa UTT AMIS pamoja na Taasisi na Wadau wote waliohusika katika kufanikisha hatua hii Muhimu",alisema .

Rais Dkt. Magufuli akagua Mradi wa Ujenzi wa Machinjio ya Kisasa Vingunguti

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akukagua eneo la Machinjio ya Ng’ombe na Mbuzi Vingunguti jijini Dar es Salaam mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kukagua ujenzi wa machinjio ya kisasa ambao unasuasua.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na kukagua eneo la Machinjio ya Ng’ombe na Mbuzi Vingunguti jijini Dar es Salaam mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kukagua ujenzi wa machinjio ya kisasa ambao unasuasua. PICHA NA IKULU

RAIS DKT. MAGUFULI AZINDUA RADA MBILI ZA KUONGOZEA NDEGE ZA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE NA UWANJA WA NDEGE WA KIA

0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe kuashiria uzinduzi wa Rada mbili za kuongozea Ndege katika Uwanja wa Ndege wa  Kimataifa wa Julius Nyerere na Uwanja wa Ndege wa  Kimataifa wa KIA katika Sherehe zilizofanyika katika Uwanja wa Ndege wa  Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Viongozi wengine kwenye picha ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Isack Kamwelwe, Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Hamza Johari pamoja na Balozi wa Ufaransa hapa nchini Fredrick Clavier 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na viongozi mbalimbali akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Rada mbili za kuongozea Ndege katika Uwanja wa Ndege wa  Kimataifa wa Julius Nyerere na Uwanja wa Ndege wa  Kimataifa wa KIA katika Sherehe zilizofanyika katika Uwanja wa Ndege wa  Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TCAA) Hamza Johari kuhusu utendaji kazi wa Rada hiyo mpya ya kuongozea ndege.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi wa Ufaransa hapa nchini Fredrick Clavier mara baada ya kuzindua mfumo wa Rada za kuongozea Ndege katika kituo cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua moja ya vitendea kazi katika kituo cha Mfumo wa Rada cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kabla ya kuzindua mfumo wa Rada za kuongozea Ndege katika kituo cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Msanii Hamonize ambaye alitumbuiza kabla ya uzinduzi wa mfumo wa Rada za kuongozea Ndege katika kituo cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Msanii Hamonize ambaye alitumbuiza kabla ya uzinduzi wa mfumo wa Rada za kuongozea Ndege katika kituo cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere 
 Muonekano wa Kituo cha Mfumo wa Rada za kuongozea Ndege katika kituo cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere 
PICHA NA IKULU

DKT MAKAKALA KUFUNGA MAFUNZO YA UONGOZI YA MAAFISA UHAMIAJI

0
0
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Peter Makakala kesho Jumanne tarehe 17 Septemba, 2019 anatarajia kufunga Mafunzo ya Uongozi ya awamu ya nne kwa Maafisa 54 wa ngazi ya Wakaguzi Wasaidizi wa Uhamiaji ambao wamehitimu mafunzo hayo.

Akitoa taarifa hiyo Mjini Morogoro, Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Mrakibu Mwandamizi Alhaji Ally Mtanda amesema kuwa Mafunzo hayo yatafungwa na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Peter Makakala katika Chuo cha Magereza cha Gereza Kuu Kingolwira – Morogoro.

Sherehe hizo za ufungaji wa mafunzo hayo zitahudhuriwa na Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu (CI -Znz), Kamishna wa Uhamiaji, Utawala na Fedha Edward Peter Chogero (CI - A&F), Kamishna wa TRITA, Maurice Kitinusa (CI - TRITA), Afisa Uhamiaji Mkoa Morogoro, Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji Angela Mathew Shija (ACI) pamoja na Wakuu wa Vitengo mbalimbali kutoka Ofisi ya Uhamiaji Makao Makuu.

KIKAO CHA CHA SHIRIKISHO LA WAKUU WA MAJESHI YA POLISI (EAPCCO ) KINAENDELEA JIJINI ARUSHA

0
0


Na Vero Ignatus,Arusha

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro amesema kuwa bado ukanda wa Mashariki mwa Afrika unakabiliwa na matishio ya kiusalama ambayo ni usafirishaji haramu wa binadamu, utoroshwaji wa madini

,ujangili na makosa ya kimtandao, makosa ambayo wahalifu wa kimataifa hutumia kutengeneza fedha kwaajili ya kuendelea kufanya makosa makubwa zadi hasa ya ugaidi.
IGP Sirro ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa kikao cha siku mbili cha Kamati Tendaji ya Shirikisho la Wakuu wa Majeshi ya Polisi (EAPCCO) leo kinachoendelea Jijini Arusha ambapo (IGP) Sirro amesema matukio ya kigaidi yanatokea maeneo mbalimbali duniani ni kiashiria tosha kuwa kuwa nchi Bara la Afrika bado haziko salama

“Kama mnavyojua yamekuwepo matukio ya aina hiyo katika Nchi nyingi duniani na kwa upande wa bara la Afrika baadhi ya mataifa yamekuwa wahanga wa matukio haya zikiwemo nchi za Nigeria,Algeria,Somalia,Msumbuji ,Kenya n.k.’’Alisema IGP

Amesema kumekuwepo kwa matukio ya aina mbalimbali katika nchi nyingi
Duniani na kwa upande wa Bara la Afrika baadhi ya mataifa yamekuwa
wahanga wa matukio hayo ikiwemo nchi za Nigeria, Algeria, Somalia,
Msumbiji na Kenya.

Amesema japokuwa kwa sasa inaonyesha kunautulivu lakini taarifa za
kiitelejensia zinaonyesha kuwa matishio ya vikundi vya ugaidi bado
yapo na yanaendelea kujiimarisha na kufungua seli maeneo mbalimbali
ndani na nje ya mpaka “Magaidi kila siku wanatafuta mianya ya kufanya matukio ya kigaidi ili kujitapa huku wakitaka kuimarisha dunia kuwa wapo na wap imara ,hivyo hakuna nchi iliyo salama lazima kuwe na uwezo wa kubaini na kuzuia matukio haya”

Amewataka wakuu hao kuhakikisha wanabuni mikakati ya utendaji na
utatuzi wa changamoto za uhalifu wa kimtandao (Cyber Crimes)
yanayotokana na mabadiliko ya kukua kwa teknilojia ya habari na
mawasiliano ikiwemo uboreshaji wa oparesheni zao sambamba na kukusanya uchakataji wa taarifa za kiitelejensia.

Awali Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Nchini, Robert Boaz
alisema nchi 13 zimeshiriki mkkutano huo kasoro nchi ya Comoro na
kusisitiza kuwa wataalam hao watajadiliana mbinu mbalimbali kwa
kutumia teknolojia kwaajili ya kukabiliana na vitendo vya uhalifu

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya Uratibu ya EAPCCO na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini Sudani,Gedion Kimilu amesema kuwa anatambua kazi kubwa inayofanywa na shirikisho hilo ya kupambana na vitendo mbalimbali vya uhalifu haswa Ugaidi na kuwahisi wajumbe hao kuendelea kuwa na mikakati ya pamoja ya kiitelejensia ya kupambana na uhalifu kwani uhalifu mwingi unafanywa kwa mbinu za kiteknolojia.

Pia watajikita zaidi katika mbinu za kuongeza ushirikiano na kukabilia
na mbinu za uhalifu ikiwa ni pamoja na kubadilishana watuhumiwa sambamba na kufanya oparesheni za pamoja katika kuleta matokeo chanya.

Aidha Jeshi la polisi Tanzania ambalo linaenda kuwa mwenyekiti wa EAPPCO kwa kipindi cha mwaka mmoja ujao limeahidi kuendeleza ushirikiano na nchi wananchama kwa wote katika kuhakikisha eneo lao linakuwa mahali salama pa kuishi,sambamba kwa kushirikiana na INTERPOL makao makuu na Ofisi za INTERPOL za Nairobi kuwa watendelea kubaki wamoja kwa lengo la kuvumbua mbinu mbalimbali za kuzuia uhalifu na wahalifu wabainike mapema,ili wakamatwe kabla hawajatekeleza nia yao.

WATUHUMIWA WANNE WA KESI YA UTEKAJI WA MO DEWJI BADO WANATAFUTWA

0
0

Na Karama Kenyunko, Michuzi Blog.

UPANDE wa Mashitaka katika kesi ya kuongoza genge la uhalifu na utakatishaji umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa bado inaendelea kuwatafuta washitakiwa wanne wanaodaiwa kumteka Mfanyabiashara, Mohammed Dewji maarufu MO.

Awali Mahakama hiyo ilitoa hati ya kuwakamata washitakiwa hao ambao ni Henrique Simbine, Daniel Manchice, Issac Tomo na Zacarious Junior wote raia wa Msumbiji na Phila Tshabalala ambaye ni raia  wa Afrika Kusini.

Mshitakiwa mmoja ambaye ni dereva taksi na Mkazi wa Tegeta, Mousa Twaleb (46) tayari alishafikishwa mahakamani hapo na kusomewa mashitaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amemueleza Hakimu Shaidi kuwa upelelezi wa kesi hiyo  haujakamilika na kwamba walitoa  hati ya kuwakamata washitakiwa hao, lakini bado hawajawapata hivyo wanaendelea kuwatafuta na wataieleza mahakama hatua waliyofikia.

Baada ya kueleza hayo, Wakili wa Utetezi,  Robert Mtakula ameuomba upande wa mashitaka kuongeza jitihada za kuwatafuta kwa kuwa mshitakiwa mmoja yupo ndani kwa muda mrefu.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi Septemba 30, 2019.

Washitakiwa hao wakikamatwa wataunganishwa katika kesi hiyo kujibu mashitaka mawili ya  kumteka nyara MO kwa nia ya kumuhifadhi kwa siri na kumuweka maeneo ambayo ni hatari na kuongoza genge la uhalifu.

Mapema ilidaiwa Mei Mosi, 2018 na Oktoba 10, mwaka huo huo, katika maeneo ya jiji la Dar es Salaam na Johannesburg Afrika Kusini, kwa makusudi washitakiwa wote kwa pamoja waliendesha genge la uhalifu.

Pia inadaiwa Oktoba 11, mwaka jana maeneo Hoteli ya Colloseum  wilayani Kinondoni Dar es Salaam, Twaleb pamoja na watu wengine ambao hawapo mahakamani, walimteka nyara MO kwa nia ya kumuhifadhi kwa siri na kumuweka maeneo ambayo ni hatari.

Pia inadaiwa Julai 10, mwaka jana maeneo ya Mbezi Beach wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, Twaleb alitakatisha fedha ambazo ni Sh 8,000,000 wakati akijua fedha hizo ni kosa la kushiriki genge la uhalifu na makosa ya kupanga.

MO alitekwa nyara Oktoba 11, mwaka jana alfajiri maeneo ya Hoteli ya Colloseum wakati akienda kufanya mazoezi na alipatikana Oktoba 20, mwaka huo huo katika eneo la Gymkhana.

KIKOSI CHA WACHEZAJI 25 WAITWA KUJIANDAA NA SUDAN CHAN

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Kaimu Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa Tanzania Ettienne Ndayiragije ameita kikosi cha Wachezaji 25 kwa ajili ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Sudan.

Kikosi hichi kinatarajia kuingia kambini kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo wa Kufuza CHAN mwaka

Wachezaji walioitwa ni Golikipa Juma Kaseja (KMC),Metacha Mnata (Yanga) na Said Kipao (Kagera Sugar).  Kwa upande wa safu ha ulinzi ni Haruna Shamte (Simba), Gadiel Michael (Simba), Mohamed Hussein (Simba), Kelvin Yondani (Yanga) Boniface Maganga (KMC) na Erasto Nyoni (Simba).

Wachezaji wengine, ni Iddy Mobi (Polisi Tanzania), Bakari Nondo (Coastal Union), Jonas Mkude (Simba),  Bakari Majogori (Polisi Tanzania), Mohamed Issa (Yanga), Iddy Selemani (Azam), Mudathir Yahya (Azam) na Salum Abubakar (Azam)

Wengine ni Frank Domayo (Azam), Mzamiru Yassin (Simba),  Shaban Idd (Azam), Ayoub Lyanga (Coastal Union), Abdull Aziz Makame (Yanga), Hassan Dilunga (Simba), Miraji Athuman (Simba) na Feisal Salum (Yanga).

Kikosi hichi kitaingia kambini kikiwa na kumbukumbu ya ushindi walioupata dhidi ya Kenya baada ya kutoka nao sare kwenye michezo miwili na kuwaondosha kwa mikwaju ya penati.

TIGO YANG'ARISHA MKUTANO WA MAWAZIRI NCHI ZA SADC WA SEKTA YA TEHAMA, HABARI, UCHUKUZI NA HALI YA HEWA

0
0


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng Isack Kamwelwe kipata maelekezo kutoka kwa mfanyakazi wa kampuni ya Tigo juu ya huduma mbalimbali zitolewazo na kampuni hiyo mara baada ya kutembelea banda la kampuni hiyo wakati wa mkutano wa mawaziri (Tehama) nchi wanachama wa SADC unaoendelea. Kampuni ya simu ya Tigo ni mtoa huduma ya WI-FI ya Bure katika wa mkutano huo.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng Isack Kamwelwe akifanya usajili upya wa laini ya simu kwa mfumo wa alama za vidole wakati alipotembelea banda la Tigo wakati wa mkutano wa mawaziri (Tehama) nchi wanachama wa SADC unaoendelea. Kampuni ya simu ya Tigo ni mtoa huduma ya WI-FI ya Bure katika wa mkutano huo. 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la utangazaji (TBC) Ayub Rioba akifanya usajili upya wa laini ya simu kwa mfumo wa alama za vidole wakati alipotembelea banda la Tigo wakati wa mkutano wa mawaziri (Tehama) nchi wanachama wa SADC unaoendelea. Kampuni ya simu ya Tigo ni mtoa huduma ya WI-FI ya Bure katika wa mkutano huo. 
Mtaalamu wa mifumo ya mawasiliano (Tehama) Benjamin Sabuka akipata maelekezo kutoka kwa mfanyakazi wa kampuni ya Tigo juu ya huduma mbalimbali zitolewazo na kampuni hiyo mara baada ya kutembelea banda la kampuni hiyo wakati wa mkutano wa mawaziri (Tehama) nchi wanachama wa SADC unaoendelea. Kampuni ya simu ya Tigo ni mtoa huduma ya WI-FI ya Bure katika wa mkutano huo 

MRADI WA UBORESHAJI WA RELI YA KATI – TIRP DAR ES SALAAM ISAKA WAFIKIA 40%

0
0
Mradi wa Uboreshaji wa Reli ya Kati – TIRP Dar es Salaam – Isaka wafikia 40% tangu kuanza utekelezaji wake mwezi Juni 2018
Mashine zinazotumika katika uboreshaji wa reli hiyo zikiendelea na kazi kwenye la reli Kati ya – TIRP Dar es Salaam – Isaka ambapo umefikia asilimia 40% tangu kuanza utekelezaji wake mwezi Juni 2018

Mradi wa Uboreshaji wa Reli ya Kati – TIRP Dar es Salaam – Isaka wafikia 40% tangu kuanza utekelezaji wake mwezi Juni 2018. Mradi huo unahusisha uboreshaji wa miundombinu ya reli ikiwemo Makalavati, tuta la reli, Madaraja makubwa na madogo na kuweka mifumo ya kisasa ya mawasiliano na uendeshaji wa treni kuanzia Dar es Salaam hadi Isaka urefu wa Kilometa 970.

Lengo la mradi wa Uboreshaji wa Reli ya Kati ( TIRP) ni kuiwezesha reli ya zamani (Meter Gauge) kutoa huduma ya usafiri wa abiria na mizigo kwa ufanisi na uhakika kutokana na uchakavu wa miundombinu ya reli ya ‘Meter Gauge’ yenye umri wa zaidi ya miaka mia moja (100) tangu ilipojengwa wakati wa ukoloni.

Kazi inayofanyika ni kuimarisha tuta kwa kuondoa kokoto za zamani na kuweka kokoto mpya, kuimarisha Makalavati, Madaraja makubwa na madogo, lakini pia wahandisi wanaendelea na kazi kubwa ya kuiunganisha reli Dar es Salaam – Isaka kwa kutumia mashine ya ‘Mobile Flash Butt plant’ na kuifanya reli kuwa moja (contionus welded rail), mashine hiyo ina uwezo wa kuzalisha joto kali lenye uwezo wa kuunga vipande viwili vya reli kwa muda wa sekunde 120.

Kutumika kwa teknolojia hii mpya ya kuunganisha reli itqsaidia treni za abiria na mizigo kwenda mwendokasi hadi Kilometa 75 kwa saa tofauti na hapo awali ambapo treni zilikuwa zikienda Kilometa 30-35 kwa saa, hii itasaidia kupunguza muda wa safari na kusaidia kuendelea kwa kasi kwa shughuli nyingine za kiuchumi.

Faida nyingine ni kuongezeka kwa uwezo wa treni za mizigo kubeba mzigo mkubwa zaidi.Aidha Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu kutoka TRC Mhandisi Maizo Mgedzi ameeleza kwa undani mabadiliko yanayotarajiwa kupatikana mara baada ya mradi huu kukamilika, amesema kuwa mwendokasi wa treni utaongezeka sambamba na uwezo wa kubeba mizigo.

“Tunazirefusha njia za kupishana kwahiyo tutaweza kupitisha treni ya urefu wa Mita 600 badala ya Mita 400, tunaiongezea uwezo reli Dar – Isaka ya uwezo wa kubeba mizigo kutoka tani 14 – 18.5, kutoka mwendokasi wa Kilometa 30 hadi 75 kwa saa, pia abiria akipanda itakuwa raha mustarehe hakutakuwa na kurukaruka kwa sababu reli itakua imeiungwa vizuri kwa kutumia mashine ya umeme,alisema Maizo

Waziri Mkuu azitaka mamlaka za Mto Mara kuwa na usimamizi madhubuti wa mazingira

0
0
WAZIRI Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa amezitaka mamlaka zinazosimamia Bonde la Mto Mara kwa Nchi za Tanzania na Kenya kuwa na usimamizi madhubuti wa mazingira ya bonde la mto huo na matumizi ya rasimali katika sekta zote za kiuchumi na kijamii ili kuleta tija kwa jamii.

Akisoma hotuba kwa niaba ya Waziri Mkuu, Waziri wa Maji, Prof Makame Mbarawa amesema wananchi zaidi ya milioni mbili wanategemea kuendesha maisha yao kupitia bonde la mto Mara.

Ametaja changamoto zinazokabili sekta ya maji hususani kwa upande wa rasimali za maji kuwa ni uvamizi wa wafugaji kwenye maeneo ya vyanzo vya maji, uvamizi wa wakulima kwa ajili ya shughuli za kilimo, ukataji wa miti kwa ajili ya kuni, mkaa na ujenzi wa nyumba mjini, umwagiliaji usiokua endelevu pamoja na uhaba wa kumbukumbu na takwimu sahihi kuhusiana na vyanzo vya maji kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kiuchumi na maendeleo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima amesema maadhimisho ya siku ya Mara mwaka huu yamefanyika kwa ufanisi mkubwa kwa kuwa mwaka huu kuliandaliwa warsha iliyojenga kueleza na kujadili changamoto na kuzitafutia ufumbuzi wake.

Maafisa Habari Wajengewa Uwezo Uandishi Habari za Kiserikali

0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akiwasilisha mada kuhusu uandishi wa habari za Kiserikali wakati wa mafunzo kwa Maafisa Habari na Mwasiliano wa Serikali na taasisi zake leo jijini Dodoma.Mafunzo hayo ya siku tano yameandaliwa kwa ushirikiano baina ya Idara ya Habari – MAELEZO na Cham cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) kwa lengo la kuwajengea uwezo maafisa hao.Afisa Habari toka Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, Daud Nyingo akichangia mada wakati wa mafunzo wakati wa mafunzo kwa Maafisa Habari na Mwasiliano wa Serikali na taasisi zake leo jijini Dodoma.Mafunzo hayo ya siku tano yameandaliwa kwa ushirikiano baina ya Idara ya Habari – MAELEZO na Cham cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) kwa lengo la kuwajengea uwezo maafisa hao.Afisa Uhusiano wa Tume ya Nguvu za Atomiki, Angela Msangi akijibu swali walilopewa wakati wa mafunzo kwa Maafisa Habari na Mwasiliano wa Serikali na taasisi zake leo jijini Dodoma. Mafunzo hayo ya siku tano yameandaliwa kwa ushirikiano baina ya Idara ya Habari – MAELEZO na Cham cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) kwa lengo la kuwajengea uwezo maafisa hao.

Baadhi ya Maafisa Habari wa Serikali na taasisi zake wakijadiliana katika makundi mara baada ya kusikiliza mada toka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi (hayupo pichani) wakati wa mafunzo kwa Maafisa Habari na Mwasiliano wa Serikali na taasisi zake leo jijini Dodoma.Mafunzo hayo ya siku tano yameandaliwa kwa ushirikiano baina ya Idara ya Habari – MAELEZO na Cham cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) kwa lengo la kuwajengea uwezo maafisa hao. (Picha na Idara ya Habari – MAELEZO)

Mahakama ya kimataifa yaanza kusikiliza shauri la aliyekua waziri wa mipango wa nchini Rwanda

0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha 

Mahakama ya kimataifa inayoshughulikia masuala yaliyosalia ya mahakama za makosa ya jinai, imeanza kusikiliza shauri la aliyekuwa waziri wa mipango wa nchini Rwanda Augustin Ngirabatware aliyehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa makosa matano likiwepo la kuhusika na mauaji ya Kimbari.

Shauri lililosomwa katika mahakama hiyo iliyopo Arusha , pamoja na mambo mengine linaeleza kuwa watu waliotoa ushahidi dhidi ya Ngirabatware walishawishiwa ili waseme uongo mahakamani.

Mmoja wa mashahidi hao ameiambia mahakama kuwa wakati anatoa ushahidi miaka 10 iliyopita, alikuwa amehukumiwa kifungo cha kunyongwa na hivyo alishawishiwa atoe ushahidi wa uongo mahakamani ili apunguziwe adhabu.

Mwaka 2012, Ngirabatware alihukumiwa kifungo cha miaka 35 Jela na mahakama ya kimataifa ya mauaji ya Kimbari ya nchini Rwanda baada ya kukutwa na hatia ya kuhusika katika mauji ya kimbari kwa kushirikiana na kundi la mauaji ya halaiki la nchini humo Interahamwe , pamoja na kosa la ubakaji.

Mwaka 2014, Mahakama ya rufaa ya Rwanda ilimpunguzia adhabu ya kifungo kutoka miaka 35 hadi 30 baada ya kuondoa kosa la ubakaji ,kifungo ambacho anakitumikia hadi sasa.Hukumu ya kesi ya Ngirabatware inatarajiwa kutolewa baada ya kukamilika kwa shauri hilo siku ya tarehe 27 ya mwezi huu.

RAIS MAGUFULI: WASIMAMIZI WA MIRADI YA SERIKALI TUMIENI VIFAA VYA VIWANDA VYA NDANI

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Wakurugenzi Wakuu wa Pipe Industries Co. Limited Bw,. Seif a, Seif na Nassor A. Seif baada ya kufunua pazia kuashiria kufunguliwa rasmi kwa kiwanda chao cha kutengeneza mipira na mabomba ya plastiki eneo la Vingunguti jijini Dar es salaam leo Septemba 16.

Na Paschal Dotto-MAELEZO

RAIS Dkt. John Magufuli amewataka watendaji wanaosimamia miradi ya Serikali kutumia vifaa vinavyozalishwa na viwanda vya ndani ili kuinua sekta ya viwanda na kuongeza ajira kwa watanzania wanaofanya kazi katika viwanda hivyo.

Akizungumza katika uzinduzi wa kiwanda cha kutengeneza mabomba ya plastiki cha Pipe Industirial Co.Ltdleo (Septemba 16, 2019) Jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli amesema kuwa Serikali inatekeleza miradi mingi mkubwa katika sekta mbalimbali ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, maji na sekta ya umwagiliaji ambayo yote hiyo inatumia mabomba ya kusafarisha maji.

“Miradi yote inayotekelezwa na Serikali inahitaji matumizi ya mabomba kwa asilimia 100, kwa hiyo ni lazima tutumie mabomba yanayotengenezwa nchini, sijasema tusiagize pengine lakini lazima tuwe wazalendo ili kuinua sekta yetu ya viwanda kwa kulinda viwanda vyetu vya vinavyozalisha bidhaa mbalimbali hapa nchini” alisema Rais Magufuli.

Rais Magufuli alisema kuwa viwanda vinavyojengwa nchini vitakuwa na faida nyinyi kwa wananchi na kwa Serikali kwa ujumla ikiwemo, upatikanaji wa ajira, ambapo Serikali itakusanya kodi ambazo zitatumika katika ujenzi wa barabara, ununuzi wa Ndege, ununuzi wa madawa, pamoja na uuzaji wa bidhaa zinazoenda nje zitakazoifanya Serikali kupata fedha za kigeni.

AIdha Rais Magufuli alisema katika kuhakikisha sekta ya Viwanda imekua, Serikali imechukua hatua mbalimbali ikiwemo kufufua viwanda vuilivyokufa, kuondoa urasmu katika taasisi zinazohusika na viwanda kama TBS, TFDA, NEMC, OSHA na Taasisi zinginezo ili kuwawezesha wawekezaji kuja kuwekeza kwa wingi nchini.

“Serikali imefanya yote hayo kwenye Taasisi husika, lakini pia imeweza kupunguza utitiri wa kodi kwa wafanyabiashara na kwa wenye viwanda, kwa mwaka huu wa fedha tumefuta tozo zipatazo 54 ambazo zingekuwa zinakwamisha juhudi za Serikali za kuwa na viwanda vya kutosha”, Rais Magufuli.

Rais Magufuli amesema kuwa kiwanda cha Pipe Industirial Co.Ltd Jijini Dar es Salaam ni kiwanda ambacho kinatumia teknolojia ya kisasa kuzalisha mabomba ambapo uwekezaji wake umetumia Bilioni 120 kwa wawekezaji kujenga kiwanda hicho.

“Nimefurahi kusikia kwamba wakati wa awamu ya kwanza ya ujenzi wa kiwanda hiki watu wapatao 215 wamepata ajira, ambapo awamu ya pili itakapokamilika kiwanda hiki kitaweza kuzalisha mabomba ya kusafirisha gesi, mafuta na nyaya za umeme na kitaajili watu wapatao 500 hii ni hatua kubwa katika kutekeleza azma ya Serikali ya kuifanya Tanzania kuwa na uchumi wa kati wenye viwanda”, Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli, alisema kuwa Sekta ya viwanda ni Sekta muhimu kwa nchi yoyote duniani, kwani Takwimu za Shirika la Biashara Duniani (WTO) zinaeleza kuwa asilimia 70 ya biashara ya kimataifa kwa mwaka 2018 bidhaa za viwandani zilichukua nafasi kubwa na kuwa na thamani ya dola za kimarekani Trilioni 12.41 ikifuatiwa na bidhaa ya mafuta asilimia 15, bidhaa za kilimo asilimia 10 na bidhaa nyinginezo asilimia 5 na thamani yake ni dola trilioni 5.

Kwa upande wake Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa, alisema kuwa Serikali kupitia Wizara hiyo inalenga kuwasaidia wafanyabiashara kuzalisha kwa kulenga masoko yote ndani na nje ya nchi ili kuinua sekta hiyo muhimu nchini.

“Kiu ya Serikali ya Awamu ya Tano, ni kuona Tanzania hatuzalishi tu kwa soko la ndani, bali tunazalisha kwa ajili ya masoko ambayo Tanzania ni mwanachama wa jumuiya mbalimbali, kwa hiyo uzalishaji katika viwanda vyetu ni vizuri ukalenga masoko ya Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC), Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika(SADC) na Soko la Pamoja la Nchi Huru za Afrika (AU)”, Waziri Bashungwa.

WANANCHI NGORONGORO WAASWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA KUKUZA UCHUMI KWA KUBADILI UTAMADUNI WA ASILI KUWA UTALII

0
0
Na Jusline Marco-Arusha

Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mhe.Mfaume Taka amewataka wananchi kuchangamkia fursa za kukuza uchumi kwa kubadili utamaduni wa asili kuwa utalii wa utamaduni ili kuzidi kuwavutia wageni wengi.

Mhe.Taka amayesema hayo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya tamasha la utalii wa utamaduni lijulikanalo kama tamasha la utalii wa utamaduni wa Masai Ngorongoro linalotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Amesema wilaya ya Ngorongoro iliweka mpango huo kwa muda mrefu baada ya kuona kuna haja ya wananchi wilayani humo kunufaika na mila na desturi zao ambazo zimetunzwa kwa muda mrefu kwa kuzibadili ili kuwezakuingiza kipato kwa wananchi.

Amesema, wilaya hiyo tayari imeshirikiana na kila mdau ambae atakuwa tayari kutangaza utamaduni wa makabila yaliyopo ili kuuenzi na kuwa kivutio bora zaidi kwa wageni hasa watalii kutoka nchi za nje wanaopenda kuona na kujifunza vitu vya asili.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya Trace Hills Mgema Mhina,amesema kampuni hiyo kwa kushirikiana na wilaya ya Ngorongoro imeandaa tamasha hilo ambalo litajumuisha maonesho ya mila na desturi za makabila yaliyomo katika wilaya hiyo wakiwemo Wamaasai, Wasonjo,Watindiga na Wamang’ati.

Vilevile amesema katika tamasha hilo kutakuwa na maonesho ya mavazi ya asili,mitindo ya nywele, mapambo ya asili, michoro ya asili, vyakula ,ngoma za asili za makabila hayo,kampuni za utalii, bidhaa za utamaduni ili watu mbalimbali wakiwemo wageni waweze kujifunza zaidi.

Aidha ameongeza kuwa malengo ya tamasha hilo ni kukuza utalii na utamaduni wa makabila hayo na kutambulisha kitaifa na kimataifa, kukuza uchumi kwa wananchi wa Ngorongoro na nchi kwa ujumla jambo ambalo litaweza kutuza mazingira ya hifadhi .

Naye Mzee wa Kabila la Kimaasai Wiliam Ole Seki amesema Wilaya ya Ngorongoro ndio mahali pekee ambapo mila na desturi za makabila bado zinaenziwa kwa kiasi kikubwa bila kuingiliwa na tamaduni za makabila mengine au nchi nyingine.Tamasha hilo la utalii wa utamaduni Wilayani Ngorongoro linatarajiwa kufanyika Septemba 18 hadi 20 katika kiwanja cha Waziri Mkuu Wasso Loliondo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo watalii.
Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mhe.Mfaume Taka akiwa na viongozi wengine akiwemo kiongozi wa kimila Mzee wa Kabila la Kimaasai Wiliam Ole Seki Wilayani humo

OFISI YA MAKAMU WA RAIS YAADHIMISHA SIKU YA TABAKA LA OZONI DUNIANI KWA KUTOA MAFUNZO KWA MAFUNDI MCHUNDO WANAOSHUGHULIKIA MAJOKOFU NA VIYOYOZI

0
0
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira kuutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi Kemilembe Mutasa akiongea na Mafundi wanaohudumia gesi za majokofu na viyoyozi wakati wa warsha ya mafunzo kuadhimisha siku ya tabaka la ozoni Duniani iliyofanyika katika Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Chang;ombe jijini Dar E s Salaam.
Mgeni Rasmi katika Warsha ya siku moja ya maaadhimisho ya siku ya ozone Duniani Bibi Vaileth Fumbo akiongea na Washiriki wa warsha hiyo ambayo ilifanyika katika Chuo cha VETA jijini Dar Es Salaam. Washiriki wa warsha hiyo ni Mafundi wa gesi za majokofu na viyoyozi

Sehemu ya Washiriki wa warsha ya mafunzo ya maadhimisho ya siku ya ozoni Duniani wakimskiliza Mgeni Rasmi (hayupo pichani) warsha hiyo ilifanyika katika Chuo cha mafunzo ya Ufundi –VETA Chang’ombe

Washiriki wa warsha hiyo wakipatiwa mafunzo juu ya utunzaji wa gesi iliyotolewa kwenye jokofu na baadaye kuweza kutumiwa tena (badala ya kuacha isambae hewani na kuharibu tabaka la hewa). Gesi hiyo inatunzwa na kifaa kiitwacho recovering unit.



……………………

Utafiti wa kisayansi katika tabaka la ozoni katika karne ya ishirini ulithibitisha kumong’onyoka kwa tabaka hilo kutokana na kulundikana angani kwa kemikali aina ya chloroflourocarbons (CFCs), halons, methyl choroform, methyl bromide, carbon tertrachoridena nyinginezo. Hayo yalisemwa na Mkuu wa Chuo cha VETA– Chang’ombe Bi Vaileth Mfumbwa wakati wa warsha ya mafunzo kwa Mafundi mchundo wanaoshughulikia majokofu na viyoyozi ikiwa ni maadhimisho ya siku ya tabaka la ozoni Duniani iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais, iliyofanyika katika Chuo cha VETA-Chang’ombe jijini Dar Es Salaam.

Aliongeza kuwa Kemikali hizi hutumika katika majokofu, viyoyozi, vifaa vya kuzimia moto, ushafishaji chuma, utengenezaji wa magodoro, madawa na manukato ya kupulizia, ufukizaji wa udongo katika vitalu vya tumbaku na mashamba ya maua na ufukizaji wa mazao katika maghala kabla ya kusafirishwa nje ya nchi. Matumizi ya kemikali hizi yapo kwa wingi katika nchi zilizoendelea na zinazoendelea, kama Tanzania.

Akimkaribisha Mgeni Rasmi, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mazingira Bi Kemilembe Mutasa alisema kuwa , Kitaifa maadhimisho ya mwaka huu ya Siku ya Kimataifa ya Hifadhi ya Tabaka la Ozoni yanafanyika jijini Dar es Salaam ambapo Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira kwa kushirikiana na Wakufunzi wa Chuo cha Ufundi Dar es salaam wamepanga kutoa mafunzo kwa vitendo kwa mafundi mchundo wanaohudumia majokofu na viyoyozi kuhusu njia bora za kuhudumia vifaa hivyo; kutoa elimu jinsi ya kutumia vitambuzi vya gesi; na kubadilisha tekinolojia zinazotumia kemikali haribifu kwa tabaka la Ozoni kwa kemikali mbadala.

“Katika maadhimisho haya, tunakumbushwa kuwa katika Mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Monteral uliofanyika nchini Rwanda mwaka 2016, nchi wanachama zilikubaliana kupunguza uzalishaji na utumiaji wa kemikali jamii ya Hydrofluorocarbons (HFCs) ambazo pia hujulikana kama R-143a kwa jina la biashara na kukubaliana kuzuia ongezeko la joto la dunia kwa nyuzi joto 0.5 (0.5 degrees Celsius)” alisema Bi. Mutasa



Warsha hiyo ya mafunzo ya siku moja imekua chachu kwa Mafundi Mchundo wanaoshughulikia majokofu na viyoyozi kwa kufundishwa njia mbalimbali za kiutaalamu za kutumia wanapokua katika shughuli zao za kila siku. Mafunzo hayo yalitolewa na Wakufunzi wa Chuo cha Ufundi-VETA Chang’ombe jijini Dar Es Salaam.

SERIKALI KUENDELEA KUJUMUISHA MASUALA YA WATU WENYE ULEMAVU KATIKA MIPAGO NA BAJETI NGAZI YA WIZARA

0
0
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Watu wenye Ulemavu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Filbert Kawemwamwa. wa akieleza umuhimu wa ujumuishwaji wa masuala ya watu wenye ulemavu katika mipango na bajeti ngazi ya wizara wakati wa kikao cha Menejimenti ya wizara hiyo na , viongozi kutoka SHIVYAWATA na Shirika la Kimataifa la ADD, leo jijini Dodoma, tarehe 16 Septemba, 2019, kushoto kwake ni Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge), Parkshard Mkongwa.
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge), Parkshard Mkongwa akieleza umuhimu wa ujumuishwaji wa masuala ya watu wenye ulemavu katika mipango na bajeti ngazi ya wizara wakati wa kikao cha Menejimenti ya wizara hiyo na , viongozi kutoka SHIVYAWATA na Shirika la Kimataifa la ADD, leo jijini Dodoma, tarehe 16 Septemba, 2019, kulia kwake ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Watu wenye Ulemavu wa Ofisi hiyo, Filbert Kawemwamwa.
Baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia kikao cha Menejimenti ya wizara hiyo na , viongozi kutoka SHIVYAWATA na Shirika la Kimataifa la ADD, wakati wa kujadili namna ya ujumuishwaji wa masuala ya watu wenye ulemavu katika mipango na bajeti ngazi ya wizara leo jijini Dodoma, tarehe 16 Septemba, 2019.
Mwenyekiti wa SHIVYAWATA, Ummy Ndeliyanaga, akieleza umuhimu wa ujumuishwaji wa masuala ya watu wenye ulemavu katika mipango na bajeti ngazi ya wizara wakati wa kikao cha Menejimenti ya wizara hiyo na , viongozi kutoka SHIVYAWATA na Shirika la Kimataifa la ADD, leo jijini Dodoma, tarehe 16 Septemba, 2019.
Mkurugenzi wa Programu, Shirika la Kimataifa la ADD, Rose Tesha, akieleza umuhimu wa utetezi wa pamoja wa masula ya watu wenye ulemavu wakati wa kikao cha Menejimenti ya wizara hiyo na , viongozi kutoka SHIVYAWATA na Shirika la Kimataifa la ADD, leo jijini Dodoma, tarehe 16 Septemba, 2019.
Baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia kikao cha Menejimenti ya wizara hiyo na , viongozi kutoka SHIVYAWATA na Shirika la Kimataifa la ADD, wakati wa kujadili namna ya ujumuishwaji wa masuala ya watu wenye ulemavu katika mipango na bajeti ngazi ya wizara leo jijini Dodoma, tarehe 16 Septemba, 2019.
Mkalimani kwa kutumia lugha ya alama, Edna James, akieleza umuhimu wa utetezi wa pamoja wa masula ya watu wenye ulemavu wakati wa kikao cha Menejimenti ya wizara hiyo na , viongozi kutoka SHIVYAWATA na Shirika la Kimataifa la ADD, leo jijini Dodoma, tarehe 16 Septemba, 2019.
Baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Watu wenye Ulemavu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Filbert Kawemwamwa. wakati wa kikao cha Menejimenti ya wizara hiyo na , viongozi kutoka SHIVYAWATA na Shirika la Kimataifa la ADD, wakati wa kujadili namna ya ujumuishwaji wa masuala ya watu wenye ulemavu katika mipango na bajeti ngazi ya wizara leo jijini Dodoma, tarehe 16 Septemba, 2019.

………………….


Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) imewahakikishia watu wenye ulemavu nchini kupitia Shirikisho la Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) kuwa itaendelea kujumuisha masuala ya watu wenye ulemavu katika mipango na bajeti kwa ngazi ya Wizara ili kuweza kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata huduma bora na stahiki.

Akiongea wakati wa kikao kazi kuhusu ushawishi na utetezi pamoja na ujumuishwaji wa masuala ya watu wenye ulemavu katika mipango na bajeti ngazi ya wizara, kilicho washirikisha Menejimenti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, viongozi kutoka SHIVYAWATA na Shirika la Kimataifa la ADD, leo jijini Dodoma, tarehe 16 Septemba, 2019, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Watu wenye Ulemavu wa Ofisi hiyo, Filbert Kawemwamwa amebainisha kuwa lengo la kikao hicho ni kuibua mikakati ya ujumuishaji, usimamizi na utekelezaji wa masuala watu wenye ulemavu nchini.

“Katika kuhakikisha kuwa mipango na bajeti ngazi ya wizara zinajumuisha masuala ya watu wenye ulemavu tutaendelea kukutana na wizara nyingine saba za kisekta ili kuweza kuhakikisha mipango ya maendeleo yao inaweza kuwafikia watu wenye ulemavu hasa walio vijijini, kwa kuzingatia Sera ya Taifa ya Maendeleo na Huduma ya Watu wenye Ulemavu ya Mwaka 20014” amesistiza Kawemwamwa

Awali akiongea katika kikao hicho Mwenyekiti wa Shirikisho la Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Ummy Ndeliyanaga, ameshukuru kwa jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya Tano, inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli katika kuboresha huduma za msingi za watu wenye Ulemavu nchini, hata hivyo amebainisha kuwa wanazo hoja za msukumo kumi ambazo anaamini utekelezaji wake ukikamilika zitaboresha huduma na maendeleo kwa watu wenye ulemavu nchini.

“Tayari serikali kupitia ofisi ya Waziri Mkuu imeshaunda madawati ya watu wenye ulemavu katika wizara na taasisi zake tunaomba majukumu ya maofisa hao yapitiwe upya, pia uanzishwaji wa mchakato wa uundwaji wa mfuko wa Kitaifa wa watu wenye Ulemavu, masuala mengine ni kuanzishwa kwa rejista ya watu wenye ulemavu, kupitia sheria ya watu wenye ulemavu, Makakati wa ufukiwaji wa 3% ya watu wenye ulemavu kwenye kila taasisi inayo ajiri watu kuanzia 20” amesema Ndeliyanaga

Ameongeza kuwa wanaomba serikali isisimamie ukamilishwaji wa mchakato wa uandaaji wa taarifa ya utekelezaji wa mkataba wa umoja wa mataifa wa haki za watu wenye Ulemavu, pamoja na kuwaelekeza waajiri wote kuandaa na kuwasilisha taarifa ya mwaka ya hali ya ajira kwa watu wenye ulemavu katika taasisi zao, pia ukamilshawaji wa mwongozo wa viwango vya ufikikaji wa miundo mbinu, Mipango ya Kisekta pamoja na Baraza la ushauri la watu wenye ulemavu kuhakikisha linafanya kazi kikamilifu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Programu, Shirika la Kimataifa la ADD, Rose Tesha, amefafanua kuwa shirika hilo limeamua kuunga juhudi za serikali za kuwahudumua watu wenye Ulemavu kwa kuwezesha SHIVYAWATA kukutana na wizara za kisekta ili kuweza kuhakikisha kuwa wanaweza kuzitetea vizuri fursa na haki za watu wenye ulemavu hapa nchini.

Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) iliundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Tangazo kwenye gazeti la Serikali Na.144 la mwezi Aprili, 2016. Pamoja na majukumu mengine Ofisi hiyo inajukumu la kusimamia utekelezaji wa sera, sheria, AMiongozo, Kanuni na Viwango vya Ubora katika utoaji wa huduma za watu wenye ulemavu nchini.

MATISHIO YA KIUSALAMA,MAGENGE YA UHALIFU BADO YAENDELEA KUSUMBUA UKANDA WA MASHARIKI MWA AFRIKA

0
0
Wakati mkutano mkuu wa 21 wa mwaka wa wakuu wa polisi wa nchi za ukanda wa mashariki mwa Afrika (EAPCCO)ukitarajiwa kufanyika wiki hii jijini Arusha, imeelezwa kuwa bado kuna matishio ya kiusalama ambapo magenge ya uhalifu bado yameendelea kusumbua katika ukanda huo yakiwemo vitendo vya ugaidi na mafunzo ya kihafidhina.

Hayo yamebainishwa jijini Arusha na mkuu wa jeshi la polisi nchini Simon Sirro wakati akifungua kikao cha siku mbili cha kamati tendaji za EAPCCO kitakachofuatiwa na mkutano mkuu wa 21 wa mwaka wa wakuu wa polisi kutoka katika nchi 14 wanachama wa shirikisho hilo ambapo wajumbe hao ambao ni wataalamu wa masuala ya upelelezi,sheria,mafunzo,kuzuia vitendo vya kigaidi na jinsia wanategemewa kuja na matokeo chanya yatakayojenga agenda za mkutano huo wa 21. 

IGP Siro amesema matukio ya kigaidi yanayotokea maeneo mbalimbali duniani ni kiashiria tosha kwamba na nchi za ukanda huo pia hazipo salama.

Awali kamisha mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai nchini Robert Boaz amesema katika mkutano huo wa siku mbili wajumbe wa kamati hizo watapata fursa ya kujadili mbinu mbalimbali za mikakati ya kukabiliana na uhalifu ambapo mkuu wa sekretarieti ya RB Nairobi Gidion Kimilu amesema bara la afrika linashuhudia kuibuka kwa uhalifu mpya wa kimtandao unaoletwa na teknlogia haswa kwa vijana ambao asilimia kubwa hawana ajira

Tangu kuanzishwa kwa shirikisho la wakuu wa polisi wa nchi za mashariki mwa afrika agenda kuu imekuwa ni Kuimarisha usalama,Amani na utulivu kwa raia na mali miongoni mwa nchi washirika.

WAZIRI MKUU AWASIMAMISHA KAZI WATUMISHI WANANE ULANGA

0
0
*Aagiza wafikishwe mahakamani kujibu tuhuma za ubadhilifu wa sh bilioni tatu

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi watumishi wanane wa halmashauri ya wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro na kuagiza wafikishwe mahakamani kujibu tuhuma za ubadhilifu wa zaidi ya sh. bilioni tatu za mapato ya ndani.

Amesema watumishi wa umma wanawajibu wa kufanya kazi kwa bidii, maarifa na ubunifu. “Nawasihi nyote muache kufanya kazi kwa mazoea, mbadilike na kuenenda sawa na matakwa na maelekezo ya Serikali ya Awamu ya Tano na anayejiona hatoshi ajiondoe.” 

Waziri Mkuu amewasimamisha kazi watumishi hao leo (Jumatatu, Septemba 16, 2019) wakati akizungumza na watumishi na madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Ulanga kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo uliopo mjini Mahenge.

Watumishi hao kuwa ni pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Yusuph Semguruka ambaye kwa sasa amehamishiwa TAMISEMI, Rajabu Siriwa (mwekahazina), Stanley Nyange, Jonson Mwenyembole, Isack Mwansokope, Said Majaliwa, Charles Steven na Hezron Lopa.

Pia, Waziri Mkuu ametumia kikao hicho kumrejesha kazini na kumpandisha kuwa mkuu wa Idara ya Ukaguzi wa Ndani, Agustine Mwaria ambaye awali alikuwa akikaimu nafasi na kuibua ubadhilifu huo. Baada ya kuibua ubadhilifu huyo mtumishi huyo alisimamishwa kazi.

Waziri Mkuu amewataka watumishi hao wazingatie sheria, kanuni na taratibu za kiutumishi pamoja na kujiepusha na vitendo vya wizi kwa sababu wanaoathirika baada ya wao kuchukuliwa hatua za kisheria ni wenza wao na watoto.

Awali,Mkuu wa wilaya ya Ulanga, Ngollo Malenya alisema wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto wa ubadhilifu wa fedha za umma hali inayosababisha kuwepo kwa mpasuko kati ya watumishi na Baraza na Madiwani. Alisema watumishi wanaotekeleza majukumu yao ipasavyo wanaandamwa. 

WAZIRI KAMWELWE AFUNGUA MKUTANO WA MAWAZIRI WA SADC JIJINI DAR ES SALAAM

0
0


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhandisi Isack Kamwelwe akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa SADC wa Sekta ya TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa wanaokutana kuanzia leo Septemba 16, 2019 jijini Dar es Salaam. Picha zote na Matokeo Chanya+. 

=======  =========  =========
 NCHI za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), zipo katika mkakati wa kuwa Mfumo Satelaiti ambapo utawezesha taarifa za nchi hizo kudhibitiwa katika ukanda huo bila kuvuka mipaka.
 
 Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhandisi Isack Kamwelwe wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mawaziri wa SADC wa Sekta ya TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa waliokutana jijini Dar es Salaam. Waziri Kamwelwe ameema kwa muda mrefu nchi za SADC zimekuwa zikitumia mfumo wa Satelaiti ambao unahitaji taarifa kwenda katika nchi za Ulaya na Marekani ndio zirudi nchini na kumfikia muhusika hivyo wanataka kuondokana na utaratibu huo. 
 
Amesema maofisa hao waandamizi watatumia mkutano huo kujadili na kuja na ubunifu ambao utarahisisha kila nchi mwanachama kusimamia mawasiliano yake bila kutegemea uthibiti kutoka nje ambao sio salama kwa nchi na watuamiaji. 
 
“Mkutano huu huu wa siku tano wa sekta ya Tehama, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa ni mwanzo mzuri wa nchi za SADC kuweka mazimgira salama katika mfumo wa ke wa taarifa na mawasiliano ya inteneti kwani tupo kwenye mkakati wa ujenzi wa Satelaiti ya pamoja hivyo kuachana na mifumo ya zamani,” alisema. Kwa upande wake Mkurugenzi wa Miundombinu SADC, Mapolao Mokoena amesema mkutano huo utaweza kusaidia uelewa wa watendaji wa Serikali kujua njia ya kupita katika kuifanya jumuiya ifikie malengo yake hasa katika miundombinu. Mokoena alisema baadhi ya nchi zimeonesha uthubutu katika ujenzi wa miundombinu akitolea mfano wa Tanzania hivyo kuzitaka nchi zingine ziongeze jitihada katika eneo hilo ambalo ni muhimu katika kukuza uchumi wan chi husika.
 
 “SADC ina program yake ya kuendelea miundombinu katika sekta zote hivyo mkutano huu ni mwanzo mzuri wa utekelezaji huo ni imani yangu kuwa tutaweza kufikia mazimio yenye tija kwa kila nchi mwanachama,” alisema. Mkurugenzi huyo ambaye alimuwakilisha Katibu Mkuu wa SADC, Dk.Stergomena Tax alisema sekta ya Tehama, Bahari, Uchukuzi na Hali ya Hewa ni sekta muhimu katika kukuza uchumi hivyo ni vema kila nchi kuwekeza katika eneo hilo.



Mawaziri wa SADC wa Sekta ya TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa pamoja na wageni waalikwa wakifuatilia uzinduzi.
Mkurugenzi wa Miundombinu SADC, Mapolao Mokoena amesema mkutano huo utaweza kusaidia uelewa wa watendaji wa Serikali kujua njia ya kupita katika kuifanya jumuiya ifikie malengo yake hasa katika miundombinu.






Mawaziri wa SADC wa Sekta ya TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa pamoja na wageni waalikwa wakifuatilia uzinduzi.


Viongozi wakifuatilia kwa makini.
Meza kuu.
Mawaziri wa SADC wa Sekta ya TEHAMA, Habari, Uchukuzi na Hali ya Hewa wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhandisi Isack Kamwelwe akicheza ngoma mara baada ya kumaliza kufungua mkutano.

Burudani ya Ngoma.

MTOTO WA NAIBU WAZIRI WA ARDHI DAVID NA SANDRA WALIVYOMEREMETA JIJINI MWANZA

0
0
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula akiwa na mtoto wake David Mabula (wa tatu kushoto) na mkewe Sandra Ndiwu wakisikiliza maelekezo kwa makini wakati wa hafla ya kuwapongeza kufunga ndoa. Hafla hiyo ilifanyika ukumbi wa Malaika Beach Resort jijini Mwanza mwishoni mwa wiki. 
David Mabula na mke wake Sandra Ndiwu wakiwasili katika ukumbi wa Malaika Beach Resort jijini Mwanza kwa ajili ya sherehe ya kupongezwa baada ya kufunga ndoa takatifu katika Kanisa Katoliki la St Joseph Kirumba Mwanza mwishoni mwa wiki. 
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akifurahia jambo na Sandra Ndiwu (Mke wa mtoto wake) wakati wa hafla ya kusheherekea kufunga ndoa takatifu kwa mtoto wake David iliyofanyika ukumbi wa Malaika Beach Resort jijini Mwanza mwishoni mwa wikli. Mbunge wa Jimbo la Urambo Magreth Sitta akimvisha Khanga Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula kwa niaba ya Wabunge wenzake wakati wa hafla ya kumpongeza mtoto wa Mhe Dkt. Mabula aliyefunga ndoa na Sandra Ndiwu mwishoni mwa wiki. Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dorothy Mwanyika akisalimiana na Masajili wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba Stela Tullo wakati wa hafla ya kumpongeza mtoto wa Mhe Dkt Angeline Mabula aliyefunga ndoa mwishoni mwa wiki. Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Ardhi Tutubi Mangazeni. Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dorothy Mwanyika (Kushoto) akiongoza watumishi wa Wizara yake kwenda kutoa zawadi wakati wa hafla ya kumpongeza mtoto wa Mhe Dkt Angeline Mabula aliyefunga ndoa mwishoni mwa wiki. Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara yake wakati wa hafla ya kumpongeza mtoto wa Mhe Dkt Angeline Mabula aliyefunga ndoa mwishoni mwa wiki jijini Mwanza. David Mabula mtoto wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza wakati wa hafla ya kumpongeza kwa kufunga ndoa na Sandra Ndiwu mwishoni mwa wiki. Wengine pichani ni watoto wa mhe Dkt Angeline Mabula. Aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mecky Sadick akifurahia jambo na Sandra Ndiwu (Mke wa mtoto wa Mhe Dkt Angeline Mabula) wakati wa hafla ya kumpongeza mtoto wa mhe Dkt Angeline Mabula kwa kufunga ndoa mwishoni mwa wiki jijini Mwanza. Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akiwaongoza Wabunge wenzake wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika picha ya pamoja na Naibu Wake Dkt Angeline Mabula (aliyekaa) wakati wa hafla ya kumpongeza mtoto wa Naibu Waziri Mhe. Dkt Mabula kwa kufunga ndoa mwishoni mwa wiki jijini Mwanza Mbunge wa Jimbo la Urambo mkoani Tabora Magreth Sitta akizungumza kwa niaba ya Wabunge wenzake wakati wa wa hafla ya kumpongeza mtoto wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula kwa kufunga ndoa mwishoni mwa wiki jijini Mwanza Bendi ya Twanga Pepeta ikitumbuiza wakati wa hafla ya kumpongeza Mtoto wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula kwa kufunga ndoa mwishoni mwa wiki.(PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live




Latest Images