Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

RELI YA SGR KUINUA PATO LA TAIFA KUPITIA SEKTA YA MIFUGO NCHINI

$
0
0
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (kulia) akimuonesha eneo la kushushia na kupakia mifugo la reli ya zamani katika Kata ya Kwala iliyopo Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi Mawasiliano (Uchukuzi na Mawasiliano) Mhandisi Atashasta Nditiye (anayemfuata) .
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (kulia) akipewa maelezo ya ujenzi wa reli ya kisasa SGR na meneja mradi Bw. Mchibya Masanja baada ya kukagua eneo lililotengwa kwa ajili ya mifugo.
*********************

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amesema ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) na ufufuaji wa reli ya zamani ni mkombozi mkubwa kwa wafugaji na wafanyabiara ya mifugo katika kupunguza gharama ya kufikia masoko na namna ya kufikia masoko hayo.

Akizungumza mwishoni mwa wiki, wakati alipotembelea ujenzi wa reli ya SGR pamoja na eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya bandari kavu ambapo pia kuna eneo maalum lilmetengwa kwa ajili ya kushushia na kupakia mifugo katika shamba la kupumzishia mifugo la serikali lililopo katika Kata ya Kwala, Wilaya ya Bagamoyo, Mkoani Pwani Mhe. Ulega alisema ujenzi huo unapaswa kuendelea kuzingatia sekta ya mifugo kadri kazi inavyoendelea kufanyika.

“Reli ya zamani ilikuwa na miundombinu yote inayohusisha mifugo na reli yetu ya kisasa SGR iendelee kuhusisha mifugo na ufufuaji wa reli ya zamani uende sambamba na kujua kwamba malighafi yetu watanzania ni mifugo yetu.” Alisema Mhe. Ulega

Mhe. Ulega amesema ujenzi wa reli hiyo ya kisasa mara utakapokamilika na kuanza kufanya kazi, pato la taifa litakuwa kupitia sekta ya mifugo kwa kuwa mifugo itakuwa inasafirishwa kwa haraka ambapo reli ya mizigo itakuwa na mwendokasi wa Kilometa 120 kwa saa.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye, aliyeambatana na Naibu Waziri Ulega amemuarifu kuwa wizara yake imepata mkopo wa bei nafuu wa Dola za Marekani Milioni 300 kwa ajili ya kufufua reli ya zamani hivyo wizara itahakikisha wakulima na wafugaji wanatumia ipasavyo reli ya kisasa (SGR) pamoja na reli ya zamani.

Mhe. Nditiye amemuomba Naibu Waziri Ulega kufikisha wataalam wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika eneo la bandari kavu lililopo Kata ya kwala wilayani Bagamoyo, ambalo limetengwa maaalum kwa ajili ya mifugo ili wataalam hao watoe muongozo wa michoro ya namna eneo hilo linavyopaswa kuwa ili kuwezesha mifugo hiyo kuwa katika mazingira inayostahili.

Aidha Mhe. Niditiye amemshukuru Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega kwa kuwa na mawazo mazuri ya namna reli hiyo ya kisasa inavyopaswa pia kuwa mkombozi kwa wafugaji kwa kuhakikisha miundombinu yote inayohusu mifugo katika usafirishaji inazingatiwa.

Naye Katibu wa Chama cha Wafugaji Tanzania Bw. Maghembe Makoye ameishukuru serikali kwa ujenzi ya reli ya kisasa kwa kuwa mifugo itakuwa inasafirishwa kwa muda mfupi na kufika katika eneo husika ikiwa na afya njema.

Aidha Bw. Makoye amefafanua kuwa uwepo wa miundombinu ya kupakia na kushushia mifugo iendelee kuzingatiwa katika ujenzi huo kwa kuwa kwa wafugaji mifugo ni uchumi kwao na taifa kwa ujumla.

WAZIRI LUGOLA AKAGUA MRADI WA UJENZI WA JENGO LA MAKAO MAKUU YA ZIMAMOTO JIJINI DODOMA

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na Maofisa wa Zimamoto na Uokoaji (hawapo pichani), wakati wa ziara ya ukaguzi wa Mradi wa Ujenzi wa Makao Makuu ya Zimamoto na Uokoaji jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo,Ramadhani Kailima na Kulia ni Kamishna Jenerali wa Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Ramadhani Kailima (kulia), baada ya kukagua Mradi wa Ujenzi wa Makao Makuu ya Zimamoto na Uokoaji jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza wakati wa ukaguzi wa Mradi wa Ujenzi wa Makao Makuu ya Zimamoto na Uokoaji jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo,Ramadhani Kailima na Kulia ni Kamishna Jenerali wa Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akiongozana na Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Ramadhani Kailima (kulia), baada ya kukagua Mradi wa Ujenzi wa Makao Makuu ya Zimamoto na Uokoaji jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Mbaga: Mfuko wa Hati Fungani kutoa fursa kwa jamii kujikomboa kiuchumi

$
0
0
Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa UTT AMIS, Daudi
Mbaga, akizungumza na waandishi wa habari (hawako pichani)

**********************

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya UTT AMIS inayomilikiwa na Serikali kupitia
Wizara ya Fedha na Mipango, imeanzisha huduma mpya ya
Mfuko wa Hati Fungani ‘Bond Fund’ ili kuiwezesha jamii iweze
kuzifikia fursa za uwekezaji na kujikomboa kiuchumi.

Kuanzishwa kwa mfuko huo kumeongeza idadi ya mifuko na
kufikia sita yote ikisimamiwa na kampuni hiyo iliyoanzishwa
mwaka 2013 ikichukua jukumu ya usimamizi wa Mifuko ya
Uwekezaji wa Pamoja kutoka kwa Dhamana ya Uwekezaji
Tanzania (UTT).

Akiuzungumzia mfuko huo, Mkurugenzi wa Masoko na
Uhusiano wa UTT AMIS, Daudi Mbaga, alisema utatoa fursa
kwa wawekezaji wadogo, wakati kuzifikia fursa za uwekezaji
zilizokuwa zikifikiwa na wawekezaji wachache, wakubwa.

Alifafanua kuwa, baadhi ya bidhaa hizo zinaeleweka kirahisi
ambapo namna ya kuzifikia, kuwekeza ni rahisi lakini wakati
mwingine hazitoi faida shindani kwa wawekezaji.

Alisema mfuko huo utaondoa changamoto ambazo huwakuta
wawekezaji kwenye soko la fedha ambalo lina bidhaa nyingi
zilizobuniwa ili kukidhi mahitaji tofauti ya watumiaji.

“Mbali ya Mfuko wa Hati Fungani, UTT AMIS inasimamia
mifuko mingine ya uwekezajiambayo ni Mfuko wa Umoja,
Wekeza Maisha, Watoto, Kujikimu, Mfuko wa Ukwasi.

“Kuanzishwa kwa Mfuko wa Hati Fungani kumetokana na
mahitaji ya wawekezaji pamoja na uchambuzi wa bidhaa za
kifedha zilizoko kwenye soko la mitaji kwa sasa,” alisema.

Mbaga alisema mfuko huo utawekeza kwenye hati fungani
zilizoorodheshwa katika soko la hisa kwa asilimia 90, asilimia
10 itakuwa kwenye uwekezaji wenye ukwasi mkubwa.

Lengo ni kuwawezesha wawekezaji wanaohitaji kuchukua fedha
kutokana na uwekezaji wao waweze kufanya hivyo, kumfanya
mwekezaji achague kama anapenda kukuza mtaji au kupokea
gawio kila mwezi, kila miezi sita kulingana na hitaji lake.

Alisema kampuni hiyo pia inatoa huduma ya usimamizi wa mali
za kifedha ili kukidhi mahitaji maalum kwa wawekezaji binafsi
wa kipato cha kati, cha juu na taasisi.

Aliongeza kuwa, baadhi ya wawekezaji hasa wadogo ni vigumu
kuwekeza katika baadhi ya bidhaa kwenye soko la fedha, Mfuko
wa Hati Fungani umeratibiwa ili kuondoa changamoto hizo.

“Mwekezaji anapata faida sawa na wawekezaji wakubwa,
akihitaji fedha anauza baadhi ya umiliki wake kwenye mfuko
kwa utaratibu rahisi bila kupoteza faida aliyoipata.

“Mfuko pia unawafaa wawekezaji wakubwa kwani ina faida
shindani, gharama ndogo za kuwekeza, ukwasi wa kutosha,
usalama wa mtaji, hatari ndogo za uwekezaji,” alifafanua.

Alisema mfuko huo hutoa fursa kwa wawekezaji kuwekeza,
kushiriki katika masoko ya mitaji, kufaidika na uwekezaji huo,
umeanzishwa ili kutoa fursa kwa wawekezaji wa kipato cha
chini, kati na kipato cha juu.

Mbaga alisema watu binafsi, kampuni, taasisi, vikundi rasmi
wanaweza kushiriki katika uwekezaji kwenye mfuko huo, lengo
ni kuwafanya wawekezaji wawe na ushiriki mpana kupitia
uwekezaji wa vipande, kuhamasisha utamaduni wa kuweka
akiba kupitia hati fungani na masoko ya fedha.

Mfuko huo unatoa fursa ya uwekezaji rahisi wa muda mrefu
kwa wawekezaji wanaopenda kuwekeza ili kukuza mtaji, kupata
gawio kila mwezi au baada ya miezi sita kama anavyohitaji.

“Kimsingi Mfuko wa Hati Fungani una mipango miwili ya
uwekezaji ili kukidhi matakwa tofauti ya wawekezaji, kuna
mpango wa kukuza mtaji, gawio kila mwezi na gawio kila baada
ya miezi sita.

“Mpango wa kukuza mtaji, gawio la mara kwa mara
halitatolewa kwa wawekezaji badala yake faida iliyopatikana
itarudishwa kwenye uwekezaji wa awali kwa kununua vipande
vitakavyonunuliwa kwa bei ya wakati huo.

“Mpango huo utawafaa wawekezaji wanaohitaji kuweka akiba
kwa malengo maalum mfano kujenga nyumba au wafanyakazi
wenye kipato na wangependa kuwa na fedha ya akiba kama
dharura itatokea au kwa matumizi ya baadae wanaweza
kuchagua mpango wa kukuza mtaji,” alisema.

Mbaga alifafanua kuwa, wawekezaji katika mpango huo
wanaweza kuuza kiasi chochote cha uwekezaji kama watakidhi
vigezo ya mfuko vinavyohusu uuzwaji wa vipande.

Mpango wa gawio kila mwezi hutokana na mahitaji ya kifedha
ya mwekezaji na anavyochagua kwenye fomu ya maombi ya
kuwekeza kwenye mfuko.

Wawekezaji ambao wanahitaji kuchukua faida kila mwezi
mfano wastaafu wanaopata fedha zao za mkupuo, kuwekeza
kwenye mfuko wanashauriwa kupokea gawio kila mwezi ili
wapate kipato cha kuishi bila kupoteza fedha walizopata.

Mbaga alisema wawekezaji wengine wanaopata fedha nyingi
kwa mara moja mfano wachimba madini wadogo, wanaweza
kuchagua kupata gawio kila mwezi ili waweze kuendesha
shughuli zao bila kuathiri mtaji walioupata.

Pia wawekezaji watakaojiunga na mpango huo wanaweza kuuza
vipande kidogo au vyote ili mradi wawe wamekidhi vigezo vya
mfuko vinavyohusu uuzwaji wa vipande vya mfuko.

Wawekezaji wanaopata fedha nyingi kwa msimu kama
wakulima wa mazao mbalimbali, wanaweza kuchagua gawio la kila miezi sita ili waweze kupata fedha wakati wa kuandaa mashamba yao, kulima na kuvuna ili waweze kuendesha
shughuli zao, kufuata msimu bila kupoteza mtaji.

Akizungumzia gharama za kuwekeza, Mbaga alisema hakuna
gharama yeyote wakati wa kujiunga au kujitoa kwenye Mfuko
wa Hati Funganui, wawekezaji wataruhusiwa kununua, kuuza
vipande kwa thamani halisi ya kipande itakayokuwepo.

“Wawekezaji wote wa ndani na nje ya Tanzania kama Sheria ya
Soko la Mitaji na Dhamana inavyoruhusu, wanaweza kuwekeza
kwenye mfuko huu,” alifafanua.

Kuhusu ununuzi wa vipande, alisema vinaweza kununuliwa siku
yoyote ya kazi isipokuwa kipindi cha kufunga vitabu ambacho
hakitazidi siku saba za kazi.

Alisema kuanzia Septemba 16, mwaka huu hadi Oktoba 16,
mwaka huu, itakuwa kipindi cha mauzo ya awali hivyo ni vizuri
Watanzania wakachangamkia fursa hiyo.

Kiwango cha chini kitakuwa sh. 50,000 na thamani halisi ya
kipande itakuwa sh. 100 ambapo maombi ya kununua vipande
yanaweza kuwakilishwa katika tawi lolote la Benki ya CRDB;
ofisi za madalali waliosajiliwa wa Soko la Hisa la Dar es
Salaam; Ofisi za Shirika la Posta au Wakala yoyote
atakayeteuliwa na UTT AMIS.

“Uwekezaji katika mfuko huu kwa wawekezaji walio nje ya
Tanzania, awasiliane na ofisi za madalali waliosajiliwa wa Soko la Hisa la Dar es Salaam au ofisi za UTT AMIS ili kupata taarifa na muongozo zaidi.

Anaongeza kuwa, thamani ya mwanzo ya kipande itakuwa sh.
100. Thamani ya kuuza na kununua kipande itakuwa sawa na
thamani halisi ya kipande bila gharama yoyote.

Kiwango cha chini kitakuwa sh. 50,000 na hakuna ukomo
kwenye kiwango cha juu, hiyo ni fursa kwa kila Mtanzania
ambapo baada ya muda wa mauzo ya awali, mwekezaji anaweza
kuwekeza kuanzia sh. 5000, mara nyingi kadri awezavyo.

Malipo ya mauzo ya vipande yanaweza kufanywa kwa fedha
taslimu au hundi ya benki itakayolipwa kwenye akaunti ya
Mfuko wa Hati Fungani iliyopo Benki ya CRDB.

“Wawekezaji wanaweza kwenda kwenye tawi lolote la Benki ya
CRDB na kufanya malipo. Pia malipo yanaweza kufanyika kwa
kupitia M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money,” alisema.

Mbaga alisema kiwango cha chini cha uwekezaji wakati wa
mauzo ya mwanzo kwa Mpango wa Kukuza Mtaji ni vipande
500. Kwa kuwa thamani ya mwanzo ya kipande ni sh. 100,
thamani ya chini ya vipande, mauzo itakuwa sh. 50,000.

Kuhusu mpango wa gawio kila mwezi, kiwango cha chini cha
uwekezaji wakati wa mauzo ya mwanzo kwa mpango wa gawio
kila mwezi ni vipande 100,000, thamani ya mwanzo ya kipande
sh. 100, thamani ya chini ya vipande katika mauzo itakuwa sh.
10,000,000.

Mpango wa gawio kila miezi sita, kiwango cha chini cha
uwekezaji wakati wa mauzo ya mwanzo kwa Mpango wa gawio
kila miezi sita ni vipande 50,000, thamani ya mwanzo kwa
kipande sh. 100, thamani ya chini ya vipande katika mauzo
itakuwa sh. 5,000,000.

Alitoa wito kwa Watanzania wote ndani na nje ya nchi
akiwahimiza wawe sehemu ya uwekezaji katika mfuko huo
mpya kwani una faida nyingi, hawapaswi kuwa na hofu.

WAZIRI MKUU AWASIMAMISHA KAZI WATUMISHI SABA

$
0
0
WAZIRI MKUU AWASIMAMISHA KAZI WATUMISHI SABA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi watumishi saba katika halmashauri mbili za wilaya ya Kilombero kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha zaidi ya sh. bilioni 1.3 za makusanyo ya mapato ya ndani.

Mbali na kuwasimamisha kazi watumishi hao, pia Waziri Mkuu ameagiza watumishi hao warejeshe fedha hizo ndani ya siku tatu kabla hajamaliza ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro. Watumishi hao ni Reina Mrema ambaye anadaiwa kuchukua kiasi cha sh. milioni 298, Haile Njitango milioni 73, Linus Mdembo kiasi cha sh. milioni 2 kwa kushirikiana na mtendaji huyo wa Kata.

Waziri Mkuu amewasimamisha kazi watumishi hao leo (Jumapili, Septemba 15, 2019) wakati akiongea na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero pamoja na watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara, akiwa katika siku ya pili za ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro.

Kuhusu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Fransis Ndulane ambaye aliingiziwa sh. milioni tano katika akaunti yake binafsi, Waziri Mkuu ameagiza azirudishe mara moja na amkabidhi stakabadhi ya kuonesha kuwa amerejesha fedha hizo kabla hajamaliza ziara yake mkoani hapa.

Amesema “Mkoa mzima wa Morogoro umekuwa na tatizo la upotevu wa mapato, fedha zinakusanywa zinapita mikononi mwa watu hazifiki benki, hii ni shida, hatutavumilia.”

Waziri Mkuu amesema kwa mujibu wa taarifa ya mkaguzi wa hesabu za serikali (CAG) kipindi cha mwaka 2016 hadi juni 2019, Katika mji wa Ifakara makusanyo yalikuwa ni bilioni 2.7 ambapo fedha iliopelekwa bank ni shilingi bilioni 1.9 na kwamba kiasi cha shilingi milioni 727 hazijulikani zilipoenda. 

Amesema katika mitambo kumi ya ukusanyaji wa mapato iliokaguliwa imeonyesha kiasi cha shilingi milioni 348 zilizokusanywa hazikupelekwa bank na hivyo kuishia mikononi mwa watu.

Waziri Mkuu amesema katika uchunguzi huo ilibainika kuwa fedha hizo ziliingizwa katika akaunti mbalimbali za watumishi wa halamshauri hizo kutoka kwa mtendaji wa Kata ya Viwanja 60 katika Mji wa Ifakara aitwaye Gregory Midas.

Hata hivyo Waziri Mkuu ameagiza Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA katika halmashauri ya Mji wa Ifakara, John Mvanga ambaye ndiye alibaini kuwepo na ubadhilifu wa fedha hizo na badae kusimamishwa kazi, arejeshwe kazini mara moja na asibugudhiwe.

“Mlimsimamisha kazi kwa sababu mlijua amegundua madudu yenu, lakini haisaidi, arejeshwe kazini naagiza apewe ulizi wakutosha.”

Kwa upande wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero, Waziri Mkuu amesema zaidi ya sh. milioni 600 hazijulikani zilipo huku kiasi cha shilingi milioni 98.5 zikidaiwa kuingizwa katika akaunti za watumishi wa halamshauri hiyo bila maelezo yeyote.

Waziri Mkuu amewataja watumishi hao kuwa ni Devid Onyango aliyechukua kiasi cha milioni 51, Elakada Kanongole milioni 36, Fork Karunde milioni 8 na Charlse Chali milioni 2.5.Amesema kati ya milioni hizo 600 kampuni ya Kilombero Plantation LTD (KPL) ambao wanadaiwa kiasi cha shilingi milioni 531 ambazo hazikuingizwa katika mfumo huo.

UJENZI WA SGR NA KUFUFUA RELI YA ZAMANI UTAINUA SEKTA YA MIFUGO NA KUMKOMBOA MFANYABIASHARA-ULEGA

$
0
0

***************
NA MWAMVUA MWINYI,PWANI

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi ,Abdallah Ulega ameeleza ,ujenzi wa reli ya kisasa ya standard gauge (SGR) pamoja na kufufuliwa kwa reli ya zamani, utainua sekta ya mifugo kwa kumpunguzia mfanyabiashara wa mifugo gharama za usafirishaji na upatikanaji wa soko la uhakika.

Aidha amebainisha kuwa, reli hiyo itakuwa sababu ya kubeba nyama ya kutosha kuingiza katika uwekezaji mkubwa wa kiwanda cha kuchakata mifugo na mazao eneo la Ruvu.

Akionyeshwa eneo litakaposhushwa mifugo kwenye reli mpya ya kisasa,na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano mhandisi Atashasta Nditie ,naibu waziri huyo wa Mifugo na Uvuvi ,Ulega alisema reli hiyo ni chachu ya maendeleo na mkombozi kwa wafugaji.

Alieleza, wafugaji na wafanyabiashara wa mifugo wana gharama za kuweza kufikia masoko lakini mradi huu mkubwa wa usafiri wa reli unaenda kuweka historia kwa watanzania.

“Ombi ni kuhakikisha miundombinu ya reli ya zamani irejee katika mazingira yake na reli mpya kuzingatie mifugo na mazao “:SGR imewekewa mkazo na Rais dkt .John Magufuli ,itakuwa chachu ya kuinua sekta ya mifugo kuitoa Bara kuileta sokoni.”


Ulega ambae pia ni mbunge wa jimbo la Mkuranga alielezea, lengo jingine la ziara hiyo ni kutazama maendeleo ya ujenzi wa reli ya kisasa na kufunganisha na sekta ya mifugo,ya matarajio ya miundombinu ya reli hiyo kuwa rafiki kubebea mifugo .

Naye Nditie alisema, reli ya zamani iliharibika lakini kwasasa kupitia jitihada za serikali ya awamu ya tano imeshaanza kufufuliwa .

Alisema, wamepata mkopo nafuu fedha za Kimarekani milioni 300 kwa ajili ya kufufua reli hiyo na wameanza na maeneo korofi ili kuhakikisha mizigo yote iwe inapitia kwenye reli hiyo na baadae katika reli ya standard gauge.

Nditie alielezea, ikumbukwe kwamba reli hizo zinakwenda sambamba kwa asilimia 70.

Awali meneja mradi ,SGR LOTI, mhandisi Machibya Masanja alisema reli hiyo itakuwa na stesheni nne ikiwemo Soga,Pugu,Ruvu,Ngerengere na kituo cha mizigo na pia itakuwa mahsusi kwa ajili ya mifugo.

Akishukuru kwa niaba ya wafugaji, katibu wa chama cha wafugaji nchini ,Maghembe Makoe aliainisha kuwa miundombinu ya reli hiyo itatambua mifugo na kutatua changamoto za usafiri kwa mfanyabiashara wa mifugo.

KONGAMANO LA SIKU YA MTO MARA LAFANA

$
0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Simaakifuatilia majadiliano katika Kongamano la ‘Siku ya Mto Mara’ linaloendelea Mugumu – Sengereti Mkoani Mara. Kongamano hilo linaongozwa na kauli mbiu isemayo Nitunze Nikutunze. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Malima.

*****************************

Na Ibrahim Mdee, Mara.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Simamwishoni mwa wiki ameshiriki katika kongamano la mto Mara linalofanyika Mugumu Wilaya ya Serengeti.

Katika kongamano hilo Naibu Waziri Sima amekuwa Mwenyekiti katika mjadala uliohusu Utunzaji wa Mazingira na uhifadhi wa Ikolojia ya Mto Mara.Naibu Waziri Sima amesema kuwa maadhimisho ya siku ya mto Mara ni jitihada zaviongozi wakuu wa nchi zetu mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Kenya kwa upande mwingine. “Ushirikiano wao ndio unaendeleza jitihada hizi za kuutunza mto huu muhimu” Sima alisisitiza.

Akizungumzia Malengo ya Siku ya Mto Mara Sima ameainisha kuwa ni kukutanishajamii za pande zote mbili za nchi, kuona na kutambua faida za uhifadhi wa mto Mara kwa kuzingatia wajibu wa kila mmoja, kwa kuwa imebainika Bonde hilo linakabiliwa na Changamoto kubwa za uharibifu wa mazingira zitokanazo na shughuli zisizoendelevu za kibinadamu ikiwa ni pamoja na kilimo, ufugaji na uvuvi.

“Hivyo kwa kutambua Changamoto hizi ni lazima wananchi wapewe taarifa sahihi za uharibifu na wajibu wao katika uhifadhi wa mto mara, Uharibifu ukiendelea kuna hatari ya Kupoteza ikolojia nzima ya mto Mara, hivyo mto utakauka na kusababisha atharikubwa kwa jamii na wanyama katika hifadhi yetu ya Serengeti na Maasai Mara huko Kenya” Sima alifafanua.

Imebanika kwamba takribani watu milioni 1.3 wanategemea uwepo wa bonde la Mto Mara katika shughuli za kilimo, uvuvi na ufugaji. Hata hivyo kumekuwa na ongezeko kubwa la idadi ya watu ambalo halina uwiano na matumizi ya bonde la mto Mara, hivyo kuongezeka kwa idadi ya watu kumeongeza uharibifu wa uoto wa asili.

Aidha, imeelezwa kuwa katika siku za hivi karibuni kumekuwepo na gugu vamiziambalo linaathiri mimea ya asili hasa majani ambayo yanasaidia kuhifadhi uoto wa asili ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya tabia nchi ambayo yanachangia katika uharibifu wa Mazingira katika bonde la mto Mara.

Katika majadiliano hayo imedhihirika kuwa uharibifu mkubwa Uko uwanda wa juu(upstream) maeneo ya Kenya na uwanda wa chini (downstream) na Ili kukabiliana na hali hiyo imependekezwa kuanzishwa kwa chanzo cha kudumu cha Fedha kwa ajili ya kushughulikia uhifadhi wa bonde la Mara.

Pia, watafiti wa mazingira ikiwemo taasisi za elimu kuendelea kufanya tafiti zinazoweza kuibua njia sahihi za uhifadhi wa bonde la mara ikiwa ni pamoja na ushirikishwaji wa jamii inayoishi kandokando ya mto Mara.

Kongamano hilo limeenda sambamba na uwasilishaji wa mada zinazotilia mkazoumuhimu wa uhifadhi wa bonde la Mto Mara, na kuongozwa na kauli mbiu isemayo “Nitunze Nikutunze”

Waziri Dkt. Mwakyembe Awapongeza Wazee wa Kimasai kwa Kudumisha Mila na Desturi.

$
0
0

Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison
Mwakyembe (Katikati Mwenye suti Nyeusi) akikaribishwa na vijana wa
kimasai kwa wimbo maalum alipowasili kwa ajili ya kufunga serehe za kimila leo Jijini Arusha.
Mwenyekiti wa Viongozi wa Ukoo wa Wamasai Bw. Isack Lekisongo
akiongea jambo wakati wa ufungaji wa sherehe za kimila zilizofanywa na kabila hilo leo Jijini Arusha.
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison
Mwakyembe akiongea na Wazee wa Kimasai wakati wa kufunga sherehe za kimila za kabila hilo leo Jijini Arusha.
Baadhi ya Viongozi na Wazee wa Kimila wa kabila la Wamasai
wakifuatilia shughuli mbalimbali zilizokuwa zikifanywa wakati wa kufunga sherehe za kimila za kabila hilo leo Jijini Arusha.
Vijana wa kimasai wakicheza ngoma za kiutamaduni ikiwa ni ishara
ya kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na
Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Hayupo katika picha) katika shughuli za kufunga sherehe za kimila leo Jijini Arusha.
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison
Mwakyembe (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa
Serikali na Wazee wa kimila wa kabila la Wamasai katika shughuli ya kufunga sherehe za kimila leo Jijini Arusha.

(Picha na Lorietha Laurence-WHUSM,Arusha).

********************************

Na Lorietha Laurence-WHUSM,Arusha

Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe
awapongeza wazee na viongozi wa kimila wa kabila la kimasai kwa kuendeleza na kuhifadhi mila na desturi.

Hayo ameyasema leo Ngaramtoni, Jijini Arusha wakati wa kufunga
mafunzo ya kimila kwa vijana wa kimasai na kueleza kuwa mafunzo hayo
ni muhimu katika kumjenga kijana kuwa mtu mwenye maadili na kuheshimika kwa jamii yake.

“Mafunzo haya mliyoyapata kutoka kwa viongozi wenu na Wazee wa
kimila yanawajenga kuwa rai wema na wenye maadili katika kujenga taifa letu ” Dkt. Mwakyembe

Aidha aliongeza kwa kueleza kuwa Wizara inaunga mkono juhudi
zinazofanywa na Wazee wa Kimasai kwa kuhakikisha mila na desturi ya
mtanzania inatunzwa na kuendelezwa kwa ajili ya vizazi vijavyo.
Pia Dkt. Mwakyembe ameahidi kushirikiana kwa karibu na Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi katika
kuhakikisha maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli za mila yanahifadhiwa vizuri bila kuingiliwa na watu.

Vilevile aliwapongeza viongozi wa Jeshi la Tanzania kwa kuruhusu
maeneo ya kijeshi ambayo ni ya kihistoria kuendelea kutumika ajili ya
masuala ya kimila na kuzitaka taasi nyingine ambazo zina maeneo hayo kuiga mfano huo .

Naye Mwenyekiti wa Viongozi wa Ukoo wa Wamasai Bw. Isack Lekisongo
ameiomba serikali kulinda, kuhifadhi na kuendeleza mila na desturi za
jamii mbalimbali za kitanzania ili kupunguza madhara yanayoletwa na utandawazi.

“Ni muhimu kwa serikali yetu kutilia mkazo suala la kuhifadhi na
kuendeleza mila za jamii mbalimbali zilizopo nchini ili kuwa na taifa
lenye kuheshimu na kudumisha tamaduni zake” Bw. Isack Lekisongo

Anazidi kueleza kuwa kupitia mafunzo hayo yanayotolewa kwa vijana
yanawasaidia kujitambua,kuheshimu wakubwa na wadogo pamoja na
kuachana na tabia zisizofaa ikiwemo matumizi ya madawa ya kulevya.

Shughuli hizo za kimila za kimasai zilifunguliwa tarehe 6 Julai 2019 kwa
vijana kutoka katika sehemu mbalimbali za Tanzania pamoja na nchi
jirani ya Kenya ambao walipewa mafunzo kwa muda wa siku 100 na
kuhitimishwa tarehe 15 Septemba 2019 huku Dkt. Mwakyembe Waziri
mwenye dhamana ya utamaduni akiwa ndiye mgeni rasmi.

Juhudi, maarifa na Upendo kupandisha TAA hadhi – DG Ndyamukama

$
0
0
Katibu wa Sheria wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania
(TAA), Elias Mwashiuya (kushoto), akilishwa keki na watumishi waliostaafu waIdara ya Uhandisi na Huduma za Ufundi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifacha Julius Nyerere (JNIA), katika hafla ya kuwaaga baada ya kustaafu hivikaribuni Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania
(TAA), Mhandisi Julius Ndyamukama, akiongea na watumishi walioudhuria haflaya kuwaaga watumishi wa Idara ya Uhandisi na Huduma za Ufundi wa Kiwanjacha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), waliostaafu hivi karibuni jijiniDar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere
(JNIA), Paul Rwegasha akimkabidhi mmoja wa Watumishi waliostaafu wa Idaraya Uhandisi na Huduma za Ufundi wa JNIA, Mhandisi Bertha Kipenda zawadi yavifaa vya mazoezi katika hafla ya kuwaaga iliyofanyika hivi karibuni Jijini Dar esSalaam.
Kaimu Meneja wa Idara ya Uhandisi na Huduma za Ufundi wa
Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Mhandisi Diana
Munubi (kushoto), akimkabidhi zawadi picha ya ua Ernest Kevela (wa kwanzakulia) katika hafla ya kuwaaga wastaafu wa Idara hiyo iliyofanyika hivi karibuniJijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania
(TAA), Mhandisi Julius Ndyamukama (kushoto), akimkabidhi zawadi ya ngao,Theobald Benigius wa Idara ya Uhandisi na Huduma za Ufundi katika Kiwanjacha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) katika sherehe ya kuwaagaWastaafu baada ya kustaafu kwa mujibu wa sheria na taratibu za Utumishi waUmma.
Watumishi kutoka Idara na vitengo mbalimbali vya Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), wakiserebuka kwa kucheza muziki katikahafla ya kuwaaga watumishi wenzao wa Idara ya Uhandisi na Huduma za Ufundiwaliostaafu hivi karibuni.

*******************



Na Bahati Mollel, TAA JUHUDI, maarifa na upendo ndio vigezo vitatu vilivyotajwana Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
Tanzania, (TAA), Mhandisi Julius Ndyamukama kuwa ni
chachu ya kuipandisha hadhi taasisi hiyo.

Mhandisi Ndyamukama ametoa rai hiyo juzi katika
sherehe ya kuwaaga Watumishi waliostaafu kwa mujibu
wa sheria wa Utumishi wa Umma wa Idara ya Uhandisi na
Huduma za Ufundi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa
cha Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam.

Amesema kwa sasa hadhi ya taasisi hiyo imeshuka mbele
ya uso wa nchi na jamii na kusababisha baadhi ya kazi
ilizokuwa ikizifanya zamani, sasa kupewa taasisi nyingine.

“Nashauri tupendane na tuchape kazi kwa bidii, kwani
sura yetu kama TAA hapo katikati imedorora, kwani
tumepoteza kazi nyingi, hivyo tukitaka kurudisha hadhi
yetu itahusu kusukumana, nitaomba mnivumilie, lakini
lengo likiwa ni kutaka kurudisha TAA ya zamani ingawa
najua wapo, ambao hawataki hivyo,” amesema Mhandisi
huyo.

Hatahivyo, amewashukuru watumishi wenzake kwa
kumpokea vizuri tangu kuteuliwa kwake kuongoza taasisi
hiyo, takribani miezi sita iliyopita, ambapo amekiri
kubobea zaidi katika masuala ya ujenzi wa barabara,
lakini sasa kwa muda mfupi aliokaa ameweza kwenda
sambamba na wataalam wa viwanja vya ndege kwa
kujifunza masuala yote muhimu ya viwanja hivyo.

“Wengi wamenisaidia kuelewa hii kazi, kwani nilikuwa
nikitegemea Watumishi wote waniongoze na kunifundisha,
na sasa naelewa kazi za aviation, ila la msingi nasisitiza
hapa tupendane na tuchape kazi kama wenzetu
wanaostafu leo (juzi) kwa mujibu wa taratibu na sheria za
utumishi wa umma,” amesema.

Pia ameweka angalizo kwa Watumishi wote kuwa muda
wote atakaokuwepo hapo kama Mkurugenzi Mkuu,
atalazimika kuwasumbua na kuwasukuma, ili sura ya TAA
ambayo hapo katikati imedorora kwa kupoteza kazi
nyingine mbele ya wananchi na taifa, ing’are tena.

Akiwapongeza wastaafu hao amewataka kuendelea
kufanya kazi wawapo majumbani mwao, ili kuimarisha
afya ya mwili na akili.

“Ninawapongeza sana Wastaafu wote bado mna nguvu ya
kufanyakazi pamoja na kustaafu, muwe mnapitapita
sehemu mbalimbali kuendelea na kazi zenu maana
mmestaafu, lakini hamjachoka, bado ‘you’re retired but not tired’” pia nawapongeza sana walioandaa shughuli hii, ambayo imefana sana”, amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa JNIA, Paul Rwegasha
amesema watumishi hao walikuwa na nidhamu kubwa na
kufanya kazi kwa bidii, pasipo kuchoka wala kuwa na
malalamiko, ambapo amewataka watumishi wengine
kuiga mfano huo uliotukuka.

Lakini, pia amewataka Wastaafu hao kuendelea kufanya
mazoezi, kwani wamekuwa wakifanya kazi ngumu
wawapo katika kituo chao cha kazi cha JNIA.

“Wote nikiwaangalia mlikuwa mkifanyakazi kwa bidii hadi
usiku mwingi, hivyo mnahitajika kuendelea kufanya
mazoezi ya viungo asubuhi na jioni na mkifanya hivi
mtafikisha ule umri wa ahadi wa miaka 120 (Mwanzo sura
ya 6), ile mingine ya miaka 80 ni ya Mfalme Daudi ila hii
120 ni ya Mwenyezi Mungu mwenyewe, mlikuwa mkiwahi
shuttle kuwahi kazini lakini sasa muamke na kufanya
mazoezi,” amesema.

Naye Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Idara ya Uhandisi na
Huduma za Ufundi, Mhandisi, Alex Kalumbete amesema
wastaafu hao walikuwa na uvumilivu mkubwa katika
utumishi wa umma kutokana na kazi ngumu walizokuwa
wakifanya za kiuhandisi.

Kaimu Meneja Uhandisi na Huduma ya Ufundi JNIA,
Diana Munubi amesisitiza upendo uendelee kuwepo baina ya watumishi kama vile wastaafu hao walivyokuwa wakiuenzi wakati wa utumishi wao wote wa umma.

Mmoja wa wastaafu hao, Bw. Theobald Benigius kwa
niaba ya wenzake ameishukuru TAA kwa kuwezesha
kufanya kazi vizuri hadi utumishi wao kukoma kwa
kustaafu, na amewaomba watumishi wenzake kuwa
wavumilivu na tabia njema, kwani wataweza kustaafu
vizuri.


RAIS DKT MAGUFULI :SERIKALI KUENDELEZA MAHUSIANO MAZURI KATI YAO NA MADHEHEBU YA DINI NCHINI

$
0
0




WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee wa Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga akizungumza wakati wa Jubilee ya miaka 25 Uaskofu wa Askofu wa Jimbo Katoliki la Tanga Anthony Banzi ambapo Waziri huyo alimuwakilisha Rais Dkt John Magufuli iliyofanyikaa kwenye Kanisa la Mtakatifu Anthony wa Paduo wa Chumbageni Jijini Tanga 
Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Kadinali Polycarp Pengo akizungumza wakati wa Jubilee hiyo leo 
Askofu wa Jimbo Katoliki la Tanga Anthony Banzi akizungumza wakati wa Jubilee hiyo 
Askofu wa Jimbo Katoliki la Tanga Mhashamu Anthony Banzi akiwasha mishumaa 25 ikiwa ni sherehe yake ya Jubilee ya miaka 25 ya Uaskofu wa Jimbo la Tanga jana kwenye ibada iliyofanyika kwenye kanisa la Mtakatifu wa Paduo Jijini Tanga ambayo ilihudhuriwa na Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa, Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella,mkuu wa wilaya ya Tanga Tobias Mwilapwa, Kadinali Pengo, maaskofu, mapandre na masista
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tangaa ambaye alimwakilisha Rais Dkt John Magufuli kushoto akimpongeza Askofu wa Jimbo Katoliki la Tanga Mhashamu Anthony Banzi wakati wa ibada ya Jubilee ya kutimiza miaka 25 ya Uaskofu
Askofu wa Jimbo Katoliki la Tanga Mhashamu Anthony Banzi kushoto akisalimia na Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa 
RAIS Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamini Mkapa kulia akiwa na Mkewe Mama Anna Mkapa na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella wakiwa kwenye Kanisa la Mtakatifu Anthony wa Paduo Chumbageni Jijini Tanga wakiwa kwenye Jubilee ya miaka 25 ya Uaskofu
Sehemu ya mapande wakiwa kwenye Jubilee ya miaka 25 ya Uaskofu Askofu wa Jimbo Katoliki la Tanga Mhashamu Anthony Banzi
Askofu wa Jimbo Katoliki la Tanga Mhashamu Anthony Banzi akiingiaa kanisani
Sehemu ya waumini kutokaa maeneo mbalimbali mkoani Tanga wakiwa kwenye Jubilee hiyo
Sehemu ya waumini kutokaa maeneo mbalimbali mkoani Tanga wakiwa kwenye Jubilee hiyo

Rais wa Dkt John Magufuli amesema kwamba serikali ina kila sababu ya kuendeleza mahusiano mzuri kati yao na madhehabu ya dini nchini kwa sababu kazi wanayoifanya haina mbadala wake kwenye jamii.

Hayo aliyasema leo kwenye hotuba yake iliyotolewa na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati alipomwakilisha kwenye Jubilee ya miaka 25 Uaskofu wa Askofu wa Jimbo Katoliki la Tanga Anthony Banzi.

Jubilee hiyo ilikwenda sambamba na ibada iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Kadinali Mstaafu Policapy Pengo, Maaskofu, Mapadre, Masista na watawa,Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamini Mkapa na Mkewe wakiwemo pia viongozi wa serikali wa sasa na wastaafu

Alisema kwamba anaamini kwa pamoja wanaweza kujenga na kuendelea kuimarisha amani na umoja uliopo hapa nchini kwa wakishirikiana na kuongeza kasi ya watawezesha watanzania kupata maendeleo.

“Baba Askofu sisi kama serikali tutatimiza wajibu wetu kutengeneza mazingira mazuri kwa madhehebu ya dini kutekeleza wajibu wake kwani uhuru wa kuabubdu uliopo nchini unaheshimuwa na kutekelezwa kwa vitendo.

Aidha alisema pia wataendelea kushirikiana na kusaidia na madhehebu ya dini kwenye upande wa shughuli zenu za huduma za kiuchumi na kijamii wanazofanya watafanya hivyo kwa kutambua mchango wao muhimu unaotolewa na huduma hizo kwa maendeleo ya nchi na ustawi wa watu wake.

“Maombi yangu kwamba msiwaruhudu watu waovu kutumia fursa hiyo muhimu…tunapopata taarifa za kutumika kinyume hatutasumbuka sana wakati wote viongozi wa dini na serikali wana jukumu la ulezi na kuhakikisha wananchi wanaishi kwa amani umoja upendo na mshikamano.
Waziri Ummy alisema kwamba licha ya utofauti za dini, kabila rangi au vyama Rais Dkt Magufuli anasema tofauti hizo hatuna budi kuishi nazo na wasiziache zikawa nyufa za uhasama ambao sio zitaligawa taifa bali linaweza kulimonyony’oa hata kanisa.

Aidha alisema kwamba matumaini ya waumini wa Jimbo Katiloki la Tanga na wananchi ni kwako Mhashamu Banzi na sio ya kiroho peke yake hivyo atambue kwamba wanayomatarajio chini ya uongozi wake kanisa katoliki linaweza kuendelea kutoa huduma huduma za kijamii kama walivyfanya huko nyuma.

“Wana tanga wanayo matumaini makubwa kwa sababu wanathamin i na kutambua manufaa makubwa yanayofanya kwenye harakati za kujilete maendeleo kutokana na kazi kubwa mnayoifanya kuwapa maendeleo kutokana na kazi kubwa”Alisema

Waziri Ummy alisema kwamba Rais Magufuli ataendelea kutambua na kuthamani mchango wa viongozi wa dini nchini hususani kwenye suala la kuliombea Taifa ili liendelea kuwa na amani na utulivu uliopo ili kuwawezesha wananchi kushiriki kwenye shughuli za kimaendeleo.

Hata hivyo alisema kwamba Serikali ya awamu ya tano itaendelea kuunga mkono juhudu za makanisa na viongozi wa dini kwenye kujenga amani ya nchi na kuleta ustawi wa Taifa ikiwemo kujenga masikilizano endelevu kati ya taasisi za dini na serikali.

“Niwaambie ndugu zangu maaskofu kwamba Rais Dkt Magufuli anasema ataendeleza ushirkiano uliopo kati ya serikali na Kanisa Katoliki pia kuunga mkono shughuli za kanisa kwenye kutoa huduma za jamii hususani elimu,afya na nyengine”Alisema.

Awali akitoa salamu za kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani ,Balozi wa Papa nchini Askofu Mkuu Marek Solczriski alisema kuwa mchango wa askofu Banzi ni mkubwa kwa kanisa na uhudumu wake wa kazi za kanisa umekuwa ni kichocheo cha maendeleo .

“Nakuombea katika kipindi hiki cha kusherehekea maadhimisho ya miaka 25 kiwe sababu za Baraka kwako na jimbo zima la Tanga na Mungu aendelee kukulinda na kukuongoza”alisema Mwakilishi huyo.

Serikali yatakiwa kufanyia marekebisho fomu za uchaguzi Serikali za Mitaa

$
0
0
Charles James, Michuzi TV

SERIKALI imetakiwa kuzielekeza mamlaka husika kufanya maboresho katika fomu za uteuzi, upigaji kura na matokeo ya uchaguzi hususani fomu za matokeo ya uchaguzi kutaja jina la kituo cha kupiga kura.

Wito huo umetolewa na Mtandao wa Uangalizi wa Uchaguzi Tanzania (TACCEO) na Jukwa la Sera wakati wakitoa maoni yao kuhusiana na uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Akizungumza katika mkutano na wandishi wa habari, Mwenyekiti wa TACCEO, Martina Kabisama amesema wadau wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wanapaswa kutoa msaada na ushirikiano ili kuhakikisha watu wenye ulemavu wanashiriki kikamilifu katika uchaguzi.

Pia amemtaka Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI kukasimu mamlaka ya kutoa vibali vya kuangalia uchaguzi na kuendesha elimu ya mpiga kura jwa msimamizi wa uchaguzi ngazi ya halmashauri.

" Baada ya uchaguzi, Waziri mwenye dhamana azielekeze halmashauri zote nchini kuandaa na kutoa taarifa ya uchaguzi wa serikali za mitaa kwa umma ikiainisha pamoja na masuala mengine ya upigaji kura, matokeo, ushiriki wa makundi maalum (vijana, walemavu na wanawake).

" Pia sanduku la kupigia kura liwekwe mahali ambapo watu wenye mahitaji maalum wanaweza kulifikia kwa urahisi," Amesema Kabisama.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Uangalizi wa Uchaguzi Tanzania, Martina Kabisama akizungumza na wandishi wa habari jijini Dodoma leo wakati wakitoa tamko kuhusu kanuni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

ELIMU NI URITHI PEKEE KWA WATOTO - RAIS MSTAAFU DKT. KIKWETE

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

RAIS mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa urithi pekee kwa watoto ni elimu ambayo itawasaidia na kuwafaa kwa baadaye, na ili kufanikisha hilo lazima kuwe na  ubunifu pamoja na kuboresha mitaala ya elimu ambayo itawaongoza kuyafikia malengo yao.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika mahafali ya 16 ya shule ya msingi Hekima Waldorf iliyopo Goba Kinzudi Kikwete amesema kuwa elimu inayotolewa lazima ijibu mahitaji ya ajira na elimu inayotolewa kwa kizazi  cha sasa lazima iendane na soko la dunia kwa wakati huu na hata miaka 50 ijayo na hiyo ni pamoja na kuboresha mitaala itakayowaongoza vijana katika kutimiza ndoto zao.

Kikwete amewahimiza wanafunzi kusoma kwa bidii kwa kuwa jinsi maendeleo ya sayansi na teknolojia yanavyozidi kukua ndivyo waliopambana kusoma watakavyonufaika.

"Wekeni malengo yenu mbele na piganieni ndoto zenu ili muweze kuyafikia malengo yenu, na ninawapongeza wazazi kwa juhudi wanazoonesha katika kuhakikisha mnapata elimu bora kabisa, pamoja na uongozi wa shule ambao daima umehakikisha mnapata maarifa tosha na yenye tija" ameeleza Kikwete.

Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa shule hiyo Emmanuel Mzengi amesema kuwa elimu inayotolewa na shule hiyo ni ile inayoendana na mazingira halisi yanayoendana na soko la ajira, na hiyo ni pamoja na kuwafundisha wanafunzi maadili na tabia njema.

Mzengi amesema kuwa ushirikiano uliopo baina ya walimu, wanafunzi pamoja na wazazi umekuwa nguzo muhimu katika kufanikisha kukidhi malengo ya kielimu. Pia ameishukuru serikali na Wizara ya elimu kwa kutambua ubora na utofauti wanaouonesha katika kuwafundisha watoto kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla.

Amesema kuwa elimu hiyo ya kiwaldorf imesambaa katika nchi zaidi ya 120 duniani na kinachowavutia wengi ni namna watoto wanavyolelewa na kufunzwa kwa kuzingatia akili, fikra, utashi na nguvu ya kutenda kwa weledi.

Awali alisoma historia ya shule hiyo Mwalimu. Stephen Chambo amesema kuwa kuanza kwa elimu ya Kiwaldorf mwaka 1997 ulipokelewa vizuri na viongozi pamoja na wadau wa serikali hapa nchini na Hekima imekuwa shule pekee ambayo imekuwa na utaratibu wa kuwaendeleza walimu pamoja na wafanyakazi sambamba na kuandaa warsha na makongamano mbalimbali ya kielimu.

Amesema kuwa daima wamekuwa wakizingatia kauli mbiu yao ya "Learning With Love" ambayo inaendelea kujenga hamasa ya kujifunza na kudumisha upendo wa kweli katika utoaji elimu na malezi, na amewahakikishia wazazi kuwa wanafunzi wanaotoka katika shule hiyo wameiva kielimu na kimalezi na hivyo kuwa waadilifu kiasi cha kutambulika kwa urahisi katika kundi la watoto.
 Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akisoma hotuba yake leo katika mahafali ya 16 ya shule ya msingi Hekima Waldorf iliyopo Goba Kinzudi wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam,ambapo aliupongeza uongozi wa shule hiyo  kwa kazi nzuri ya kuelimisha watoto. 
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kikabidhi vyeti  kwa mwanafunzi  wakati wa Mahafali ya 16 ya darasa la saba ya shule ya msingi Hekima Waldorf iliyopo Goba Kinzudi wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Mwenyekiti wa Bodi ya shule ya Msingi Hekima Waldorf,Augustino  Mbogella akisoma historia fupi ya shule hiyo.


 Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa shule ya Hekima Waldorf  na baadhi ya wageni waalikwa mwishoni wa shughuli za mahafali hayo.

(Picha zote na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)





WAZIRI KAMWELWE AZIKARIBISHA NCHI WANACHAMA WA SADC KUTUMIA BANDARI YA DSM ,ASEMA IKO TAYARI KUPOKEA MIZIGO MKUBWA

$
0
0
Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack
Kamwelwe(kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Bandari Tanzaznia (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko (kulia)
kuhusu kutua kwa Meli kubwa ya mizigo ya MV Grand Duke kwenye gati
jipya namba 0 katika Bandari ya Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA)wakiongoza baadhi ya magari kutoka kawenye meli kubwa ya mizigoya magari MV Grand Duke baada ya kutua hapo jana kwenye gati jipyanamba 0 ya Bandari ya Dar es Salaam.
Gari likitoka kwenye meli kubwa ya mizigo ya magari MV Grand
Duke baada ya kutua hapo jana kwenye gati jipya namba 0 ya Bandari ya
Dar es Salaam.
Meli kubwa ya mizigo ya magari MV Grand Duke ikiwa katika
bandari ya Dar es Salaam mara baada ya kutua hapo jana kwenye gati
jipya namba 0 ya Bandari hiyo ambalo ukarabati wake unaelekea mwisho.

************************************

Na Paschal Dotto-MAELEZO
15-09-2019.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe
amezikaribisha Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini MwaAfrika (SADC) kutumia bandari ya Dar es Salaam mara baada ya ukarabati wake hasa gati namba sifuri kuanza kupokea mizigo.

Akizungmza Jijini Dar es Salaam alipotembelea kuona meli kubwa ya Mizigo yaMagari ya kampuni ya Meli ya Mv Grand Duke iliyotua bandarini hapo leo , WaziriKamwelwe amefurahishwa kuona meli hiyo kubwa yenye urefu wa mita 200 na uwezo wa kubeba magari 6,000 ambapo imetua ikiwa na magari 1,347 imedhihirisha uwezo wa bandari hiyo kwamba iko tayari kupokea mizigo mikubwa.

“Tuko hapa kuwahabarisha Watanzania, na Nchi Wanachama wa Jumuiya yaMaendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC), kwamba ukarabati wa Bandari ya Dar esSalaam unaenda vizuri ikiwa ni pamoja na kukamilika kwa gati namba moja, mbilina hili gati namba sifuri liko mwishoni na limeanza kupokea meli kubwa za Mizigo kama mnavyoona hapo, hiyo ni meli ya mizigo ya magari yenye uwezo mkubwasana”, Waziri Kamwelwe.

Malengo ya Serikali ni kufanya ukarabati wamagati nane ambapo mpaka sasa gati namba moja na gati namba mbili yako kwenye matumizi mara baada ya kukamilikana sasa meli zinaendelea kutoa huduma kama kawaida, gati namba sifuri ambalo ni maalum kwa meli za mizigo ya magari linaendelea na ukarabati lakini asilimiakubwa liko vizuri.

Waziri Kamwelwe alisema kuwa mara baada ya gati hilo kukamilika Tanzaniaitakuwa na uwezo mkubwa wa kupokea mizigo ya magari laki 6 kwa mwaka, lakinipia bandari hiyo inabeba tani milioni 17 kwa mwaka huku malengo ya Serikali ikiwa ni kufikia tani milioni 25 ifikapo mwaka 2021.

“Malengo yetu ni kufikia tani milioni 25 kwa mwaka tofauti na tani za sasa milioni17, kwa hiyo Nchi Wanachama wa SADC, bandari hii sasa inafanya kazi vizuri, kwahiyo majirani zetu kutoka SADC, DRC, Malawi, Zambia na nchi zingine za ukandahuu wa Kusini mwa Afrika wanakaribishwa sana kutumia bandari ya Dar es Salaam” Alisisitiza Waziri Kamwelwe.

Waziri Kamwelwe alisema Serikali itaendelea kufanya kazi kwa kushirikiana nawafanyabiashara kutoka Nchi Wananchama wa SADC ili maeneo ambayo yanachangamoto ziweze kutatuliwa haraka.

“Serikali imewekeza fedha nyingi katika ukarabati huo, kwa hiyo itahakikisha kuwa inaipa bandari hii mizigo ya kutosha na hasa kutoka kwa Nchi Wanachama wa SADC, ili kuwawezesha kupata huduma rahisi za usafirishaji” alisema Kamwelwe.

kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari, Mhandisi DeusdeditKakoko, alisema kuwa gati jipya namba sufuri limeanza kufanya kazi kwa kupokeameli kubwa ya Mv Grand Duke ambayo imetua jana na mzigo wa magari 1347.

“ Hili gati ni Jipya ni kati ya magati nane ambayo yanajengwa, lenyewe
limejengwa kwa zege kama mnavyoona, lina uwezo wa kubeba magari 10,000 kwa wakati mmoja kutoka uwezo wa kubeba magari 2,500 ambao tulikuwa nao hapo mwanzo, lakini pia lina urefu wa mita 320 kwa hiyo ni gati kubwa na hii meli ina urafu wa mita 200 kwa hiyo kuna mita 120 zimebakia kwenye gati hili”, Alisema Mhandisi Kakoko.

Gati hilo ambalo ni la kisasa Zaidi litakuwa na taa ambazo zitawezesha kufanyikakazi usiku na mchana hapo bandarini, na makabidhiano ya gati hilo yatafanyikakesho ambapo Mkandarasi ataikabidhi Mamlaka ya Bandari (TPA).

Aidha, Mhandisi Kakoko alisema kuwa meli ya Abiria ziwa nyasa imeingia kwenyemajaribio ya mwezi mmoja ambapo mwezi ujao inatarajiwa kukabidhiwa kwaMamlaka hiyo ili kuanza kuhudumia wananchi wa maeneo hayo.

Sherehe ya Uzinduzi wa Jezi mpya za Timu ya Green

$
0
0

Mkuu wa Kombania ya Muziki Meja Nimroad Kitinya akipokea Udhamini wa Jezi kutoka Kwa Mwakilishi wa Smart Gin Forgiver Tito wakati wa Sherehe ya Uzinduzi wa Jezi mpya za Timu ya Green Warriors inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza katika hafla  iliyofanyika Club 361 Mwenge Jijini Dar Es Salaam .
Baadhi ya Wachezaji wakiwa wamevalia Jezi za Ugenini Nyeusi na Nyumbani Za Kijani wakizionyesha kwa Wadau katika Hafla iliyofanyika Club 361 Mwenge Jijini Dar es Salaam.


JAJI CHANDE AWAPA SOMO WANASHERIA WACHANGA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv.
JAJI Mstaafu wa Mahakama Kuu Tanzania, Mohamed Chande Othman amesema pamoja na kuwa na idadi kubwa ya mawakili nchini wapatao 6750, bado watu wengi wa mikoani wamekuwa wakikosa uwakilishi wa mawakili wa kujitegemea huku wengi wakitajwa kujazana mijini.

Amesema kwa makadirio ya Tanzania yenye watu zaidi ya milioni 58, wakili mmoja anahudumia watu 82,857 wakati Afrika Kusini ambao inalingana kwa kiasi kikubwa na idadi ya watu wakili mmoja anahudumia watu 2,500.

Jaji Chande ameyasema hayo wakati akitoa mhadhara (Lecture) wa Jukumu la wanasheria chipukizi kwa umma na mwelekeo wa sekta ya sheria Tanzania kwa wanasheria wachanga jijini Dar es Salaam walipokutana pamoja kujadiliana mambo mbali mbali ikiwemo kuhamasisha wanasheria wachanga ambao bado hawajasajiliwa na wale waliosajiliwa kufanya kazi kwa weledi.

Jaji Chande amewaambia wanasheria hao kuwa mawakili wanatakiwa kwenda kufanya kazi vijijini na kama maofisa wa mahakama wakasaidie katika utoaji haki na kuongeza kuwa, asilimia 70 za kesi nchini zipo Mahakama za Mwanzo lakini wananchi wanajiwakilisha wenyewe.

Amewaambia kuwa wakiwa kama wanasheria vijana wanapaswa kuhakikisha wanafikia wananchi waliopo vijijini ili kuwasaidia katika masuala yao ya kisheria na kusaidia mahakama katika utoaji haki kwa haraka zaidi kwani mawakili wengi wamekuwa wakiishia kufanya kazi mijini kuliko vijijini.

Pia amewataka kuhakikisha kuwa wanafanya kazi kwa kuafuata maadili yao kwa kuwa wakweli na kuepuka vitendo vya rushwa na kuhakikisha wanalinda utawala wa sheria na haki za msingi, uhuru na wajibu.

" Katika Mkoa wa Lindi, kuna wakili mmoja huku mawakili nane wakiwa katika Mkoa wa Katavi, 20 mkoani Ruvuma, 29 Kigoma na 38 wapo mkoani Mara.

Aidha Jaji Chande amesema kuna baadhi ya mikoa takribani saba ya Tanzania Bara haina Mahakama Kuu kama vile, Lindi, Katavi, Morogoro, Simiyu, Manyara, Pwani, Singida and Songwe huku Wilaya 28 zikiwa hazina Mahakama za Wilaya kama vile Mkinga.

"Kutokuwepo kwa mahakama ni kikwazo kikubwa katika utoaji wa haki na masuala ya sheria hususani kwa mawakili wachanga. Hivyo, tutaendelea kuishauri serikali kuharakisha ujenzi wa miundombinu ya mahakama ili watu waweze kupata haki zao natambua kuna mchakato wa mahakama wa kuhakikisha kila wilaya inakuwa na mahakama," amesema Jaji Chande.

Amefafanua kuwa katika ripoti ya dunia ya mwaka 2019 kuhusu utoaji haki inaonesha watu milioni 230 wanaoishi katika mazingira mbalimbali wanakosa haki huku watu bilioni 1.5 wanashindwa kutatua matatizo yanayowakabili yanayohusu haki na watu bilioni 4.5 wametengwa na fursa zitolewazo na sheria na inaonesha kutokuwepo kwa usawa au ufikishaji sawa wa haki kwa wote na ukosefu mkubwa wa uwakilishi wa kisheria.

Jaji Chande amesema katika miaka mitano iliyopita zaidi ya asilimia 50 ya mawakili wamepokelewa nchini kufanya kazi hivyo, anaamini wataendelea kubadilisha muundo na taasisi ya sheria.

Kwa upande wake Balozi Juma Mwapachu amesema serikali imefanya jitihada kubwa katika kuimarisha miundombinu ya mahakama lakini bado watu wengi wana uhitaji wa kusaidiwa katika masuala ya utoaji haki.

"Wanasheria wachanga wanatakiwa kujua wanaisaidiaje jamii katika masuala ya sheria pamoja na kupigania haki za binadamu, uhuru wa kuongea na katiba" amesema.

Naye, Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za binadamu (TDHRC), Onesmo Olengurumwa amesema ni wakati wa mawakili kuhakikisha wanakwenda vijijini kuwasaidia wananchi waliowengi ambao hawajui masuala ya sheria.

Amesema, wanasheria wanapaswa kuwa na wito na uelewa mkubwa katika kuendesha kesi zenye maslahi kwa umma na zile za ki mkakati zaidi.

Olengurumwa ameongeza kuwa, kwa sasa kuna changamoto kubwa kwa mawakili kurundikana mijini, kwani nchini kuna mawakili wapatao 8000 lakini nusu ya hao wako mijini hivyo wanapaswa kujua wameitwa katika kazi hivyo kusaidia watu wote.

Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Mohammed Othman Chande akitoa Lecture kwa wanasheria wachanga kuhusu majukumu yao kwa jamii na taaluma hiyo wakati wa sherehe ya majadiliano baina ya wanafunzi hao iliyofanyika katika chuo cha sheria jijini Dar es Salaam.
Balozi Juma Mwapachu akizungumza na wanasheria wachanga wakati wa sherehe ya majadiliano baina ya wanafunzi wa sheria, iliyofanyika mijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa haki za binadamu (TDHRC), Onesma Olengurumwa akizungumza wakati wa sherehe ya majadiliano baina ya wanafunzi hao iliyofanyika katika chuo cha sheria jijini Dar es Salaam.
Picha ya Pamoja
Naibu Mkuu wa Taasisi, Fedha na Utawala wa chuo cha sheria (TLS) William Pallangyo akimkabishi Balozi Mwapachu jarida la takwimu za sheria wakati wa sherehehiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam.



Picha ya Pamoja

MBARAWA ATOA MIEZI MITATU KWA MAMLAKA ZOTE ZINAZOKADIRIA BEI YA MAJI KUFUNGA DIRA YA MAJI KWA WATEJA WAO

$
0
0
Waziri wa Maji, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Mb) akikata utepe kuzindua rasmi mradi wa maji wa Kijiji cha Shilima, Kata ya Kikubiji, Wilaya ya Kwimba, Mkoani Mwanza.
Waziri wa Maji, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Mb) akifungua bomba la maji la mradi wa Shilima wakati wa uzinduzi wa mradi huo Septemba 14, 2019.
Baadhi ya wananchi waliofika kushuhudia uzinduzi wa mradi wa maji wa Shilima.
Waziri wa Maji, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Mb) (mbele katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi waliohudhuria uzinduzi wa mradi wa maji Shilima.

*****************************

Mamlaka za maji zinazotumia bei za kukadiria (flat rates) kote nchini zimepewa miezi mitatu kuhakikisha zinawafungia dira za maji wateja wao wote ili kila mteja alipe gharama ya maji kwa kiasi alichotumia.

Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa (Mb) alitoa agizo hilo Septemba 14, 2019 alipokuwa akizindua mradi wa maji wa Kijiji cha Shilima Kata ya Kikubiji, Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza. 

Waziri Mbarawa alisema Serikali imetenga Bilioni moja kusaidia mamlaka za maji ambazo hukadiria matumizi ya maji wateja wake badala ya kutumia dira ya maji ili kuepuka kumbebesha mteja mzigo usiyo kuwa wake. 

Waziri Mbarawa vilevile ameziagiza mamlaka za maji za mikoa kuhakikisha zinadhibiti upotevu wa maji kwani maji mengi yanapotea kabla ya kufika kwa wananchi sambamba na kuongeza mtandao wa maji ili kuwaunganisha wananchi wengi zaidi.

Akizungumzia mradi wa maji wa Shilima, Profesa Mbarawa alisema ujenzi wake ni utekelezaji wa Sera ya Maji pamoja na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi inayoelekeza kuwapatia huduma ya majisafi na salama kwa asilimia 85 wakazi wote waishio vijijini ifikapo mwaka 2020.

Aliongeza kuwa uzinduzi wa mradi huo ni awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mradi wa maji katika Vijiji vya Shilima, Mhande na Izizimba.

Alibainisha kwamba mradi wa maji wa Shilima ulianza kutekelezwa mwaka 2013 na ulitakiwa kukamilika katika kipindi cha miezi sita. Hata hivyo, kutokana na udhaifu wa Mkandarasi aliyekuwa anautekeleza pamoja na usimamizi mbovu haukuweza kukamilika kwa wakati. 

Waziri Mbarawa aliwapongeza wote walioshiriki kwenye ujenzi wa mradi kwa namna mbalimbali na kwa ushirikiano waliotoa kwa kipindi chote cha ujenzi wake hadi unakamilika kwa wakati kama alivyokuwa ameelekeza.

Akizungumzia ujenzi wa mradi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza (MWAUWASA) ambaye alikuwa msimamizi mkuu wa ujenzi, Mhandisi Anthony Sanga alisema walizingatia agizo la Waziri Mbarawa na kwamba mradi huo ulikamilka tarehe 25 Agosti, 2019 kabla ya muda uliyokuwa umeelekezwa.

Kwa upande wake Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kwimba, Mhandisi Boaz Matundalo alisema kuwa Kijiji cha Shilima kina wakazi wapatao 7,526 ambapo mradi huu wenye magati 35 una uwezo wa kuhudumia wakazi 8.750 ikiwa ni wastani wa watu 250 kwa kila gati.

Waziri Mbarawa tarehe 3 Julai, 2019 akiwa katika ziara ya kikazi Wilayani Kwimba alitoa ahadi ya kukamilisha mradi huo kwa kutumia wataalamu wa ndani kwa kuhakikisha wananchi wa Kijiji cha Shilima wanapata maji katika kipindi cha miezi miwili, yaani hadi kufikia tarehe 3 Septemba, 2019, ahadi ambayo hata hivyo ilikamilika tarehe 25 Agosti, 2019 siku tisa kabla ya tarehe ya makubaliano.

NDIKILO-WAWEKEZAJI WAJALI MASLAHI YA WAFANYAKAZI

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA

WAWEKEZAJI mkoani Pwani wametakiwa kujali maslahi ya wafanyakazi ili kuwapa hamasa ya kufanya kazi na kuwafanya kama sehemu ya familia ya wamiliki wa miradi ya uwekezaji. 

Hayo yalisemwa na mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo wakati akiweka jiwe la msingi kwenye kiwanda cha vifungashio vya plastiki cha Wande Printing and Pakaging Co Ltd kilichopo wilayani Kibaha na kusema kuwa wawekezaji wanapaswa kuwafanya wafanyakazi wao kama watu wa familia moja.

Ndikilo alieleza,baadhi ya wawekezaji wameshindwa kufanikiwa kutokana na kutojali maslahi ya wafanyakazi jambo ambalo linasababisha miradi mingi kukwama na kushindwa kufikia malengo waliyojiwekea na kujikuta wakipata hasara.

“Natoa agizo kwa wawekezaji wote ndani ya mkoa wa Pwani kuhakikisha wanawalipa vizuri wafanyakazi wao na kuwafanya sehemu ya familia yao kwani kuwa karibu na wafanyakazi itasaidia wafanye kazi kwa moyo na kuwa na bidii ya kufanya kazi,”alisema Ndikilo.

“Kwa upande wa taasisi wezeshi zikiwemo zinazotoa huduma za umeme, maji na miundombinu lazima ziwe karibu wawekezaji na kuwasaidia wapunguze au kuondoa changamoto ili kuunga mkono serikali katika jitihada za kuifanya nchi kuwa ya viwanda na uchumi wa kati,”alisema Ndikilo.

Naye Mkurugenzi wa benki ya Azania Charles Itembe alisema kuwa benki hiyo ni ya kizalendo na inaunga mkono jitihada za serikali za kuhimiza ujenzi wa viwanda ili kukuza uchumi wa wananchi na nchi kw akutoa mikopo kwa watu mbalimbali wakiwemo wawekezaji.

Meneja uendeshaji John Wande alisema wanazalisha vifungashio vya plastiki kwa ajili ya bidhaa za viwandani,kilimo na sekta ya afya ambapo waliona kuwa kuna changamoto kubwa za upatikanaji wa vifungashio bora kwa ajili ya bidhaa .

Hadi sasa kimetoa ajira kwa watu 60 na baadaye itafikia ajira ya watu 350 na kiwanda hicho kina thamani ya shilingi bilioni 6.6 na kinatarajia kuanza kazi baada ya wiki mbili.

Naye mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa kampuni hiyo Joseph Wasonga alisema kuwa wamekuwa wakishirikiana na serikali kwa kuanzisha viwanda mbalimbali kwa ajili ya kutoa ajira na kukuza uchumi na kuisaidia jamii inayoizunguka kiwanda hicho. 



TATIZO LA BARABARA IFAKARA MLIMBA KUWA HISTORIA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema changamoto ya barabara ya kutoka Ifakara hadi Mlimba iliyokuwa inawakabili wananchi wa maeneo hayo kwa muda mrefu imepatiwa ufumbuzi baada ya Serikali kupanga kuijenga kwa kiwango cha lami.

Amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imedhamiria kuboresha miundombinu ya barabara nchini ikiwemo barabara ya kutoka Ifakara hadi Mlimba yenye urefu wa km. 126.5.

Waziri Mkuu aliyasema hayo jana jioni (Jumapili, Septemba 15, 2019) wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Matangini, Mlimba wilayani Kilombero.

“Serikali imedhamiria kuimarisha barabara katika maeneo mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na ujenzi wa barabara ya Ifakara-Mlimba kwa kiwango cha lami lengo likiwa ni kurahisisha usafiri pamoja na kukuza uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla.”

Alisema Serikali inatambua umuhimu wa barabara hiyo kwa ajili ya kuboresha maendeleo ya wananchi na kwamba itajengwa kwa kiwango cha lami, hivyo aliwataka wananchi hao waendelee kuiamini Serikali yao.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alimuagiza Kaimu Ofisa Elimu Mkoa wa Morogoro, Jackson Mpankuli ahakikishe amepeleka walimu katika shule ya msingi Matangini na Mwangazaambazo zinakabiliwa na upungufu wa walimu.

Waziri Mkuu alisema hadi Sepetemba 30 mwaka huu kiongozi huyo awe ameshawahashimia walimu katika shule husika. Waziri Mkuu alitoa agizo hilo baada ya Mbunge wa Jimbo la Mlimba, Suzan Kiwanga kulalamikia upungufu wa walimu hao.

Mbunge huyo alisema katika jimbo kuna tatizo kubwa la upungufu wa walimu hali inayosababisha baadhi ya wazazi kukodi walimu kwa ajili ya kuwafundisha watoto wao, hivyo Waziri Mkuu aliagiza walimu wahamishiwe katika shule ndani ya wiki mbili.

Akizungumza na wananchi katika eneo la Mchombe alipokuwa njiani kuelekea Mlimba, Waziri Mkuu aliwataka wazazi, walezi na viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro kuhakikisha wanadhibiti ongezeko la mimba kwa watoto wa shule.

“Lazima kuwalinda watoto wa kike ili wasipate mimba kwani watashindwa kuendelee na masomo, hivyo watashindwa kutimiza ndoto zao. Viongozi simamieni utekelezaji wa sheria kwa kuwachukulia hatua wote waliowapa mimba wanafunzi.”

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Mbunge wa jimbo la Kilombero, Lijualikali na Mbunge wa Mlimba, Suzan Kiwanga waliiomba Serikali iwasaidie ujenzi wa barabara za kutoka Ifakara hadi Mlimba na barabara ya Ifakara hadi Kidatu ambayo ujenzi wake unasuasua.

Pia Suzan alitumia fursa hiyo kuishukuru Serikali kwa kutenga fedha kwa ajili ya upembuzi yakinifu kwa barabara ya Ifakara-Mlimba na baadae kuwekwa lami kwa awamu na kusema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano ikiahidi kitu inatekeleza

Waziri Mkuu anaendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro ambapo anatarajiwa kutembelea Halmashauri za wilaya ya Ulanga na Malinyi kukagua miradi ya maendeleo ukiwemo mradi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya na kuzungumza na wananchi pamoja na watumishi.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiongea na wananchi wa Mbingu, Kata ya Igima, wilayani Kilombero, mkoani Morogoro Septemba 15.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwasalimia wananchi wa Kata ya Mchombe, wilayani Kilombero, kwenye mkutano wa hadhara, Septemba 15.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwahutubia wananchi wa Kata ya Mrimba, wilayani Kilombero, kwenye mkutano wa hadhara, Septemba 15.2019

WAZIRI NDALICHAKO AITAKA BENKI YA BIASHARA YA MWALIMU KUBUNI MBINU ZA KUWAVUTIA WATEJA

$
0
0
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza wakati wa kufunga kongamano la Walimu wilayani Kasulu mkoani Kigoma
.Baadhi ya walimu wa Mkoa wa kigoma wakifiatilia hotuba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolijia Prof. Joyce Ndalichako wakati akifunga Kongamano la Walimu lililoandaliwa na Benki ya Biashara ya Walimu, Kasulu mkoani Kigoma.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akisalimiana na mmoja wa mwalimu aliyeshiriki Kongamano la Walimu lililoandaliwa na Benki ya Biashara ya Mwalimu, Kasulu Mkoani Kigoma.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako akiteta jambo na Mkurugenzi wa Benki ya Biashara ya Mwalimu Richard Makungwa wakati wa hafla ya kufunga Kongamano la walimu lililoandaliwa na benki hiyo Kasulu, Mkoani Kigoma
Mkurugenzi wa Benki ya Biashara ya Mwalimu Richard Makungwa akizungumza wakati wa hafla ya kufunga Kongamano la walimu lililoandaliwana Benki hiyo Kasulu, Mkoani Kigoma

…………….
Na Editha Karlo,michuzi tv,Kigoma


Waziri wa Elimu sayansi na Teknolojia Prof,Joyce Ndalichako ameutaka uongozi wa Benki ya biashara ya Mwalimu MCB BANK kuboresha huduma za kifedha ikiwemo kuweka vivutio na masharti rafiki ambayo yatawawezesha walimu nchini kukopa fedha ili kukuza vipato vyao.

Prof,Ndalichako ametoa wito huo wakati akifunga Kongamano la walimu
wilayani Kasulu Mkoani Kigoma na kusisitiza kuwa matarajio ya serikali ni kuona benki ya biashara ya mwalimu inakuwa rafiki kwa walimu nchini kwa kuondoa adha na vikwazo ambavyo kwa muda mrefu walimu wamekuwa wakikabiliana Navyo katika taasisi mbalimbali za kifedha.

“Benki ya Biashara ya Mwalimu iwe na ahueni kwa mwalimu anapokuwa ni mteja katika kufanya hivyo walimu wengi watahamasika kujiunga na benki hii, kupitishia mishahara pamoja na hata kuchukua mikopo”

Aidha ameutaka uongozi wa Benki hiyo kusimamia vizuri fedha iliyokwisha wekezwa na walimu ili kuwavutia walimu wengine ambao bado hawajajiunga na kusisitiza kasi ya uanzishwaji wa ofisi za benki hiyo katika mikoa yote nchini iongezeke ili kuwavutia wateja.

” Nafahamu kwamba tayari mnatoa huduma kidijitali na mnashirikiana na Benki ya Posta kutoa huduma katika maeneo ambayo hamna ofisi na lakini ni muhimu mkaharakisha uanzishwaji wa ofisi zenu kila mkoa ili kurahisisha upatikanaji wa huduma,,

Waziri Ndalichako pia amewaasa walimu nchini kuwa na Utamaduni wa kujiwekea akiba pindi wanapopata mishahara yao ili iwasaidie kuanzisha miradi mingine ya kiuchumi ambayo itakuwa mkombozi wa maisha yao pindi wanapostaafu.

“”Walimu tambueni akiba ni kile kitu unachokiweka kwanza kabla ya kuanza matumizi, lakini watu wengi wanadhani akiba ni bakaa baada ya matumizi kwa utaratibu huo kamwe hakutakuwa na kitu kinachobaki,,

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Mwalimu Richard Makungwa
amesema benki hiyo ime endelea kujiimarisha katika kusogeza huduma kwa wateja wake nakwamba tayari imeanzisha ofisi zake katika baadhi ya mikoa nchini ikiwemo MBEYA MOROGORO na MWANZA huku ishirikiana na Benki ya Posta kutoa huduma kwa wateja ambao bado mikoa yao haijafikiwa.

Amesema katika benki hiyo mwalimu mmoja mmoja anamiliki hisa takribani asilimia 35.28 huku chama cha walimu na kampuni yao wakimiliki takribani asilimia 16.17.

” ukiangalia utakubaliana nami kuwa chombo hiki ni cha walimu na madhumuni yake ni kuwaletea maendeleo wao wenyewe ndiyo maana tukasema lazima tuwafikia walimu popote walipo ,,alisema Mkurugenzi huyo.

Naye mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanali Simon Anange amesema mara nyingi watumishi wanakosa nidhamu ya fedha na kutumia zaidi ya kile anachopata na kusisitiza kuwa ni vizuri walimu wakawa na utaratibu wa kujiwekea akiba ili pindi wanapostaafu waweze kuishi maisha ambayo wanaishi wakiwa kazini.

Nae mwalimu mstaafu aliyeshiriki kongamano hilo Kalist Tarimo ameishukuru Benki ya Biashara ya Mwalimu kwa kufanya Kongamano hilo ili kutoa elimu kwao lakini pia ameishaiuri benki hiyo kuwana na ofisi katika kila Wilaya ili walimu waweze kutumia huduma za benki hiyo.

Kongamano hilo limeandaliwa na Benki ya Biashara ya Mwalimu na limeshirikisha walimu kutoka Mkoa wa Kigoma.

NAIBU WAZIRI KANYASU AWAFUNDA WAZAZI WENYE WATOTO WALIOHITIMU DARASA LA SABA

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Geita mjini, Mhe.Constantine Kanyasu amewahimiza wazazi wenye watoto waliomaliza darasa la saba mwezi huu nchini  wahakikishe wanawalinda watoto hao wasijiingize katika makundi yasiyofaa.

Akizungumza kwenye mahafali ya saba ya wanafunzi 69 waliomaliza darasa la saba katika shule ya msingi ya Waja Springs ya mkoani Geita,Mhe.Kanyasu amewataka wazazi wawe mstari wa mbele katika malezi bora ya watoto wao

.Aidha, Mhe.Kanyasu amewataka pia wahitimu hao wakawe mfano bora katika jamii kwa kuwa kuwasaidia wazazi wao kwa kufanya kazi za majumbani badala ya kuacha kazi zote zifanywe na Wafanyakazi wa ndani

Katika hatua nyingine, Mhe. Kanyasu ameipongeza shule hiyo kwa kufanya vizuri katika mitihani ya Taifa na  kuufanya mkoa wa Geita kuwa miongoni mwa  mkoa inayokuwepo kwenye tano bora kitaifa.

Pia, Mhe.Kanyasu amewataka wanafunzi hao watumie muda mwingi kujisomea vitabu vya hadithi badala ya kutumia muda mwingi kuangalia Televisheni hasa vipindi visivyofaa

Katika hatua nyingine, Mhe.Kanyasu ameuhakikishia Uongozi wa shule hiyo kutafuta ufumbuzi wa tatizo la barabara iinayoelekea katika shule hiyo pamoja tatizo maji machafu wakati mvua ikinyesha . 

Kwa upande wake Meneja wa Shule hiyo, Mhandisi.Chacha Wambura amewaasa wazazi kujiepusha kuwapatia simu watoto wao ili wasiweze kuingia katika vishawishi katika kipindi hili kifupi walichohitimu masomo yao.

" Wazazi jiepusheni kuwapa simu zenu hawa watoto, hii mitandao ya kijamii inawapelekea watoto kuanza kuangalia mambo yasiyofaa " alisisitiza Wambura.

Aidha, Amewataka Wahitimu hao waache kuzitumia simu za wazazi wao pindi wakiwa majumbani badala yake wasome vitabu kama walivyokuwa wakifundishwa shuleni

Naye, Janeth Ndibalema ambaye ni mzazi wa mhitimu wa darasa la saba, Amesema malezi ya watoto kwa sasa yamekuwa na changamoto nyingi kutokana na wazazi kuacha jukumu la malezi kwa Wasichana wa kazi  hali  inatopelekea watoto wengi kuharibikiwa.

Kufuatia hali hiyo, Ndibalema ametoa wito kwa wazazi kutenga muda kukaa na watoto wao badala ya kujikita kwenye majukumu ya kazi ili kuwasaidia watoto wao kujiepusha kufanya mambo yasiyofaa yatakayowafanya wasiweze kuendelea na shule.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akimkabidhi cheti, Janeth Ibrahim miongoni mwa wanafunzi  aliyehitimu darasa la saba katika shule ya msingi ya Waja Springs wakati wa mahafali ya saba yaliyofanyika katika shule hiyo  iliyopo mkoani Geita.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akivishwa  skafu na  Sara Keneth ambaye ni wanafunzi wa darasa la sita  katika shule ya msingi ya Waja Springs wakati  Naibu Waziri huyo alipowasili katika shule hiyo akiwa mgeni rasmi katika mahafali  ya saba ya darasa la saba yaliyofanyika mkoani Geita.
 Wahitimu wa darasa la saba wa shule ya msingi ya WAJA Springs wakiwa pamoja na wanafunzi wenzao wakiimba wimbo wa taifa mara baada ya mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu kuwasili katika shule hiyo kwa ajili ya mahafali ya darasa la saba 
 Wanafunzi wa shule ya msingi ya Waja Springs wakiimba ikiwa ni ishara ya kuwaaga wenzao wahitimu wa darasa la saba katika mahafali yaliyofanyika katika shule hiyo mkoani Geita.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akimkabidhi zawadi mwanafunzi bora aliyekuwa akifanya vizuri kwenye masomo yake, Charles Zungu kwenye mahafali ya darasa la saba katika shule ya msingi ya Waja Springs iliyopo mkoani Geita.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi, wamiliki wa shule pamoja na wazazi wa wanafunzi waliohitimu darasa la saba katika mahafali ya saba ya katika shule ya msingi ya Waja Springs iliyopo mkoani Geita

WAZIRI MKUU AWEKA JIWE LA MSINGI JENGO LA HALIMASHAURI MALINYI

$
0
0
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiweka jiwe la msingi, wa jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi, mkoani Morogoro, Septemba 16.2019.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwasalimia  na Mkuu wa Wilaya ya Malinyi, Majura Kasika, kwenye jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi, mkoani Morogoro, Septemba 16.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi, baada ya kukagua na kuweka jiwe la msingi, la jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi, mkoani Morogoro, Septemba 16.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images