Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

Airtel Tanzania, Board ya Wakurugenzi na Wafanyakazi wake wamlilia Eng, Dkt Omar Rashid Nundu

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania Plc, bw. Sunil Colaso akimwaga udongo ishara ya kuuaga mwili wa marehemu Omari Rashid Nundu aliyekuwa Mwenyekiti wa bodi ya Airtel Tanzania Plc aliyefariki siku ya Jumatano Septemba 11, 2019. 
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania Plc, bw. Sunil Colaso akisaini kitabu cha maombolezo,alipo hudhuria msibani kwa aliyekua Mwenyekiti wa bodi ya Airtel Tanzania Plc aliyefariki siku ya jumatano Septemba 11, 2019. 

TIRA YAANDA MKUTANO WA WADAU WA BIMA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi TV
MAMLAKA ya Usimamizi wa Shughuli za Bima nchini (TIRA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Bima Tanzania (IIT) wameandaa mkutano wa wadau wa bima ili utakaofanyika mkoani Mwanza mwezi huu ili kujadili maendeleo na changamoto zinazoikabili sekta hiyo, katika kipindi cha mwaka mmoja.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Septemba 12,2019 Kamishina wa TIRA, Tanzania  Dk. Mussa Juma amesema mkutano huo amao hufanyika kila mwaka mwezi huu wa tisa  safari hii mada kubwa itakuwa ni kuinua upenyo wa bima kwa kuongeza wigo wa bima kwa wasiokuwa na bima.

Aidha amesema mada hiyo inamalengo makuwa ya kutoa elimu ya bima kwa jamii na jukwaa kamili kwa ajili ya wadau wa Taasisi na kuongeza mtandao wa kibiashara  kitu kitakachoongeza malengo ya serikali ya awamu ya tano amayo imedhakia nchi kufikia kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.

Dk. Juma amesema, katika mkutano huo, unaotarajiwa kuanza septemba 24 hadi 29, mwaka huu, watakuwa pia watatoa elimu juu ya ufahamu wa bima, kubadirishana maarifa na utaalamu wa bima,kutoka kwa wataalamu wa ndani na nje ya nchi na pia katika wiki hiyo, taasisi ya bima itatoa jukwaa kamili na vifaa muhimu kwa maendeleo, uboreshaji wa maarifa ya ima na mazoezi.

“Katika wiki hiyo tutakuwa na matemezi ya bima, Utoaji Damu utoaji wa tunzo mbali mbali mbali za mwaka kwa washindo mbali mbali pamoja na michezo mbali mbali kiwamo mpira wa miguu na ama mikono”, amesema Dk. Juma

Amesema pia watajadili fursa na changamoto zinazoikabili sekta ya bima nchini pamoja na wajibu wa wasambazaji wa huduma hiyo ya bima.

"Katika mkutano huu Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashantu Kijaji anatarajiwa kuwa mgeni rasmi, hii ni kwa sababu wizara yake ndio yenye dhamana ya usimamizi wa sekta ya fedha na bima ikiwemo, " amesema Dk. Juma.

Naye Katibu wa Taasisi ya Bima Tanzania, Ernest Kilumbi amesema wiki hiyo ya bima ni jukwaa sahihi kwa ajili ya kuanzisha na kuratibu shughuli za bima ikiwamo kutoa elimu, misaada kwa wazee, yatima na watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

"Wiki hii ya bima ni jukwaa kamili kabisa la kuwakutanisha wadau kwa lengo la kupeana taarifa na kuinua upenyo na kuuongeza kwa watu wasiokuwa na bima, " alisema.

Kwa upande wake Mwakilishi wa majaji katika utoaji tuzo za umahiri kwenye sekta ya Bima, Frenk Kitende amesema katika mkutano huo wa TIRA kwa kushirikiana na IIT imeona ni muhimu kuanzisha tuzo hizo ili kuweza kuwatambua na kuzawadi ufanisi kwenye uendeshaji, uongozi na utawala wa wadau katika sekta ya bima.

Amesema walipokea  jumla ya maombi 72 ya wadau kutoka taasisi mbali mbali za bima amapo kati ya hizo maombi 32 yalipitishwa huku 40 yakikataliwa kwa sababu mbalimbali.

"Majaji wote walifanya kazi kwa bidii kubwa kupitia maombi ya washiriki wote na kuhakiki taarifa ziluzowasilishwa, alama za ufaulu zitawekwa kwenye mtandao baada ya sherehe za utoaji tuzo zotakazofanyika Septemba 26 mwaka huu, " amesema. 

 Kamishana wa mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima nchini (TIRA) Dk. Musa Juma akizungumza na waandishi wa habari juu ya mkutano wa wadau mbali mbali wa bima unaotarajiwa kufanyika mkoani Mwanza kuanzia Septemba 24 hadi 29,2019. Mkutano huo umeandaliwa na TIRA kwa kushirikiana na Taasisi ya Bima Tanzania (IIT)  kwa lengo la kujadili maendeleo na changamoto zinazoikabili tasnia ya bima katika kipindi cha mwaka mmoja.
 Katibu wa Taasisi ya Bima Tanzania (IIT) ,  Ernest Kilumbi, akizungumza katika mkutano huo

Mwakilishi wa majaji katika utoaji tuzo za umahiri katika sekta ya Bima,  Frenk Kitende akielezea namna wadau mbali mbali wa tasnia ya Bima watavyopewa tuzo ya kuweza kutambua na kuzawadi ufanisi kwenye uendeshaji, uongozi na utawala wa wadau katika sekta hiyo  katika mkutano huo.
 

Uzinduzi Klabu Ya Wafanyabiashara NBC Dodoma,serikali yawaomba kuchangamkia fursa za Kibiashara.

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Bilinith Mahenge ametoa wito kwa wafanyabishara jijini humo kuhakikisha wanachangamkia fursa za mikopo inayotolewa na taasisi za kifedha ili waweze kunufaika na ongezeko kubwa la fursa za kibiashara zinazoibuka katika jiji hilo ambalo ni makao makuu ya nchi.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa huyo wakati wa hafla ya jioni ya Uzinduzi wa Klabu ya wafanyabiashara ya Benki ya NBC ya mkoa wa Dodoma, Mkurugenzi wa jiji hilo Bw Godwin Kunambi mbali na kuipongeza benki hiyo kwa mabadiliko makubwa ya kihuduma alisema ipo haja ya makusudi kwa wafanyabiashara wa jiji hilo kuitumia vema benki hiyo ili kupata nguvu ya kiuchumi itakayowawesha kufaidi vema fursa ya mabadiliko ya ukuaji wa uchumi katika jiji hilo.

“Dodoma kwasasa kuna utekelezaji wa miradi mikubwa mingi ikiwemo barabara, Stendi ya mabasi ambayo ni kubwa zaidi Afrika Mashariki, upanuzi wa uwanja wa ndege, ujenzi wa viwanja vya mapumziko ambayo vitachochea mzunguko mkubwa wa pesa na ongezeko la watu. Hivyo ni fursa kwa wafanyabiashara kushirikiana vema na benki kama NBC ili kukuza mitaji itayowawezesha kufanya uwekezaji utakaowanufaisha na mabadiliko hayo,’’ alibainisha.

Alitolea mfano umuhimu wa wafanyabiashara hao kuwekeza kwenye sekta ya usafiri ambapo kwasasa serikali jijini humo ipo kwenye mpango wa kuondoa gari ndogo za abiria maarufu kama vipanya kwenye mizunguko ya mjini ili kutoa fursa kwa gari kubwa ‘coaster’ kufanya kazi hiyo.

Akizungumza kuhusu uanzishwaji wa Klabu hiyo, Mkuu wa Kitengo cha wateja wa Kati na Wadogo wa benki ya NBC, Bw Evance Luhimbo alisema pamoja na mambo mengine klabu hizo zinalenga kutoa mafunzo kwa wateja wa benki hiyo kuelewa mabadiliko ya uboreshwaji wa huduma za za benki hiyo, kuwakutanisha pamoja wajadili fursa za kibiashara sambamba na kuwajengea uelewa kuhusu masuala mbalimbali ya kibiashara ikiwemo masuala ya kodi na taratibu za kijiunga na taasisi wadau biashara ili ziwasaidie.

“Benki ya NBC kwasasa ipo kwenye mabadiliko makubwa ya kihuduma kwa wateja wateja wetu na ili mabadiliko haya yaweze kuwafikia wateja wetu ni vema kuwa nao karibu zaidi. Mbali na benki kuwajengea uelewa kama hudua zetu na taasisi wadau ikiwemo Chemba ya biashara, viwanda na kilimo (TCCIA)na Baraza la. Uwezeshaji (NEEC)na nyingine nyingi pia tumekuwa tukipokea maoni kutoka kwa wateja wetu yanayotuwezesha kubuni huduma zinazoendana na uhalisia wa mahitaji yao ya kifedha,’’ alisema.

Awali wakiwasilisha mada kwenye kongamano la uzinduzi wa Klabu hiyo muwakilishi wa TCCIA, Bw Patrick Magai na muwakilishi wa NEEC Bi Nyakao Mturi walitoa wito kwa wafanyabiashara wadogo kuunganisha nguvu ya kimitaji ili wapate nguvu ya pamoja itakayowawezesha kushiriki fursa kubwa za kibiashara ndani na nje ya nchi.

Akizungumza kwa niaba ya wafanyabiashara hao Bw Ponsian Rweyemela ambaye ni mfanyabiashara jijiji humo pamoja na kuipongeza benki hiyo kwa mabadiliko makubwa ya kiutendaji pia aliiomba benki hiyo pamoja na taaisisi nyingine za kifedha kuongeza idadi ya mashine za kuweka na kutolea fedha (ATM) ilikuendana na ukuaji wa jiji hilo pamoja na ongezeko la watumiaji wa mashine hizo.
Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Bw Godwin Kunambi(kulia-mbele) akifurahia uzinduzi wa rasmi wa Klabu ya wafanyabiashara ya Benki ya NBC ya mkoa wa Dodoma uliofanyika katikati ya wiki jijini humo. Wengine ni baadhi ya wateja na maofisa wa benki hiyo akiwemo Mkurugenzi wa Idara ya wateja wa kati na wadogo Bw Elibariki Masuke.

Kwa Simu Toka London - NASSOR MAHRUKI: MTANZANIA PEKEE KATIKA MASHINDANO YA KIMATAIFA YA KUZUNGUKA DUNIA KWA MASHUA ZA UPEPO

$
0
0
 Picha na Habari za Freddy Macha, London 
 Wangapi tumewahi kusikia mashindano ya kimataifa ya mashua za upepo (“clipper race” )? Mimi sikuyajua hadi nilipomhoji Nassoro Mahruki, Mzanzibari mshiriki wa tukio hilo litakalochukua miezi kumi na moja hadi Agosti 2020. 
Nassoro Mahruki ambaye huendesha shughuli zake za biashara za utalii visiwani Pemba na Unguja, ni Mwafrika Mashariki pekee na anasema alijitayarisha kwa miaka miwili kushiriki. “Yakubidi ufanye mafunzo na kufaulu ...” alisema akinionyesha mashua iitwayo “Zhuhai” ikiongozwa na nahodha Nick Leggatt. Zhuhai ni kati ya vyombo vingine kumi na moja vyenye majina kama “Korea”, “Punta Del Este”, “WTC Logistics”, nk.

Dimba hili lilianzishwa hapa London mwaka 1996. Mwasisi wake, aliyeshatunukiwa heshima ya “Sir” na Malkia Elisabeth wa Uingereza ni Robin Knox Johnson. Bw Johnson alikuwa mwanadamu wa kwanza kuzunguka dunia nzima kwa mashua inayotegemea upepo tu mwaka 1968. Keshafundisha zaidi ya mabaharia 5,000. Kitatange hiki kinahusu kila aina ya changamoto za kimichezo. Kushirikiana na wenzako, dhoruba zenye pepo kali, mvua, barafu, mawimbi nk. Usafiri ulioanzia London Septemba Mosi , 2019 utapitia mabara yote na bahari kubwa zaidi ya sita, Ureno, Uruguay, Afrika Kusini, Australia, China, Marekani, visiwa vya Bermuda, Panama, nk. Watarejea London Agosti 2020. Nilipowasiliana naye leo alikuwa tayari salama Ureno. Nassoro Mahruki aliyevalia bendera za Tanzania, Zanzibar, Pemba alisema mbali ya kupenda michezo ya majini lengo ni kujenga tasnia ya utalii wa majini Tanzania. “Ikiwa washindani wenzangu wako radhi kununua meli ya paundi milioni kumi, hawatashindwa kuja Tanzania kuchezea maji na kutumia dola elfu mbili kwa juma. Ni hela nzuri sana kwa utalii wetu.” Mataifa zaidu ya 40 yamo mwaka huu na Afrika ina nchi nne tu : Tanzania, Nigeria, Misri na Morocco. Tumpe heko na kumwombea dua arejee salama. Fahari yetu. 1.  
Nassoro Mahruki akiwa kazini katika mashua ya Zhuhai yenye mabaharia toka mataifa China, Marekani, Uingereza, Canada, Ufaransa, nk 2.  
Nassoro Mahruki akizungumza kando ya bandari ya Katherine Docks, London, kabla ya kusafiri na mabaharia wenzake Septemba Mosi, 2019. 3.  
Moja ya majengo ya mandhari ya hoteli Mnarani , Nungwi kaskazini ya Zanzibar. Bw Mahruki ameendesha biashara za utalii, Zanzibar na Pemba kwa miaka 23 sasa. Ni mtu anayependa kazi na shughuli azifanyazo. Mchapa kazi na Mjasiria Mali wa mfano. 4. Maelfu ya wakazi wa London waliokuja kushangilia kuondoka kwa washindani wa tukio, la Clipper Race, Jumapili Mosi Septemba, 2019 5.  
Nassoro Mahruki akiwa na nahodha wa mashua husika (“Zhuhai”), Nick Leggatt, mzawa wa Afrika Kusini mwenye uzoefu wa muda mrefu. Keshazunguka dunia kwa mashua hizi mara tatu! 7.  
Mwandishi Freddy Macha nikiwa na Nassoro Mahruki mwenye umri wa miaka 51. Mahruki alijilipia mwenyewe. Washikiri wa mataifa mengine hupata wafadhili wa kibiashara kirahisi ukilinganisha nasi Afrika Mashariki Tazama mahojiano na Nassoro Mahruki - “Kwa Simu Toka London” ( KSTL)

MAADHIMISHO YA SIKU YA MARA YAFUNGULIWA RASMI

$
0
0
     
Maadhimisho ya Siku ya Mara maarufu "Mara Day" yamefunguliwa rasmi tarehe 12 Septemba, 2019 na Mhe. Adam Malima Mkuu wa Mkoa wa Mara, katika uwanja wa Sokoine uliopo Mugumu, wilayani Serengeti. 

Maadhimisho haya yanayo adhimishwa kwa mzunguko kati ya nchi mbili za Tanzania na Kenya hufanyika kila mwaka, ambapo mwaka huu yanafanyika Tanzania katika Mji wa Mugumu wilayani Serengeti kuanzia tarehe 12 hadi 15 Septemba, 2019 yakiongozwa na kauli mbiu "Mimi ni Mto Mara, Nitunze Nikutunze".

 Madhimisho ya Siku ya Mara yanayolenga kuhimiza na kuhamasisha wananchi wanaozunguka bonde la mto Mara kuhifadhi mazingira ya mto, ili kulinda ikolojia ya bonde hilo ambalo ni muhimu kwa utastawi wa mazingira na uchumi wa jamii ya Tanzania na Kenya. Akizungumza katika sherehe za ufunguzi wa maadhimisho Mhe. Malima ambaye pia ni mgeni wa heshima katika sherehe hizo amesema, "ni jukumu la jamii na kizazi cha sasa kuhakikisha kuwa mazingira ya bonde la mto Mara yanaendelea kubaki salama na kustawi kwa mafuaa ya kizazi kilichopo na kijacho". 

Aidha, amewahamasisha  wananchi wa Mkoa wa Mara kuchangamkia fursa zinazotoka na maadhimisho hayo ikiwemo uuzaji wa bidhaa mbalimbali kwenye maonesho yanayoendelea  katika kipindi cha maadhimisho.

Maadhimisho ya Siku ya Mara yanafanyika ikiwa ni utekelezaji wa uamuzi wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Afrika Mashariki la Bonde la Ziwa Victoria, uliofanyika terehe 4 Mei, 2012 jijini Kigali, Rwanda. Kilele cha maadhimisho haya hufanyika tarehe 15 Septemba kila mwaka ambayo pia inawiana na tukio la uhamaji wa wanyama pori kutoka Tanzania kwenda Kenya.

Bw. Eliabi Chodota Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii, akizungumza na wanahabari amesisiza kuwa Serikali ya Tanzania na Kenya zimejidhatiti katika kuhifadhi bonde la mto Mara na kuwaasa wananchi wanaozunguka mazingira ya bonde hilo kuunga mkono jitihada za Serikali.
     
Maadhimisho haya yatakayofanyika kwa siku 4 yanahusisha shughuli mbalimbali ikiwemo zoezi la upandaji miti ambapo, zaidi ya miti 500 itapandwa katika maeneo yanayozunguka bonde hilo. Vilevile yatahusisha uwekwaji wa alama za kuonesha mipaka ya ukomo wa shughuli za binadamu katika bonde hilo, mita kadhaa kutoka ukingo wa mto Mara.

Kwa mara ya kwanza maadhimisho haya yalifanyika tarehe 15 Septemba, 2012 mjini Mulot, Kenya yakiongozwa na kauli mbiu "Mara - Uhai wetu".


Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Dar es Salaam.


Mhe. Adam Malima Mkuu wa Mkoa wa Mara, akihutubia hadhira iliyojitokeza (hawapo pichani) kwenye ufunguzi wa maadhimisho ya Siku ya Mara..
Moja ya banda linaloonesha na kuuza bidhaa za wajasiliamali katika maadhimisho ya siku ya Mara lililopo uwanja wa Sokeine Mugumu, Serengeti.
Watendaji mbalimbali wa Serikali, viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama, na viongozi wa dini wakiwa tayari kumlaki mgeni wa heshima katika sherehe za ufunguzi Mhe. Adam Malima Mkuu wa Mkoa wa Mara .
Meza kuu wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa kabla ya kuanza kwa sherehe za ufunguzi

WFP KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUTAFUTA SOKO LA NAFAKA NJE - BASHE

$
0
0

 Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe akiongea na ujumbe wa Shirika la Chakula Duniani (WFP) wakati alipofanya kikao ofisini kwake Dodoma.
 Mwalikishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani nchini Michael Dunford (wa pili kulia) akiwa timu yake wakati wa mazungumzo kuhusu ushirikiano wa kutafuta soko la mahindi na Naibu Waziri wa Kilimo Husein Bashe (hayupo pichani). Nawasilisha.
 Naibu Waziri wa Kilimo Husein Bashe akifuatilia mazungumzo na ujumbe wa Shirika la Chakula Duniani wakati wa kikao cha kujadili upatikanaji wa soko la mahindi na mtama nchini.
Picha ya pamoja kati ya Naibu Waziri wa Kilimo Husein Bashe (wa sita toka kulia) akiwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani Michael Dunford (wa nne toka kushoto) mara baada ya mazungumzo kuhusu ushirikiano wa kutafuta masoko ya nafaka nchini.

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limekubali kuwa na ushirikiano na Wizara ya Kilimo katika kutafuta soko la uhakika la mazao ya mahindi na mtama nje ya nchi.
Kauli hii imetolewa jana na Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe mara baada ya kufanya mazungumzo ofisini kwake na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani Michael Dunford.

Bashe amebainisha kuwa Wizara ya Kilimo ina mkakati wa kuhakikisha mahindi na mtama unaozalishwa nchini unapata soko la uhakika ili kuinua uchumi wa wakulima
“Wizara inataka kutumia uzoefu wa Shirika la Chakula Dunia katika kuyafikia masoko ili mazao ya wakulima wetu yaweze kupata bei nzuri katika soko la Afrika” alisema Naibu Waziri

Amewahakikishia WFP kuwa wizara imejipanga kuona uzalishaji wa mahindi na mtama unaongezeka na kuzingatia kiwango cha ubora kinachotakiwa na soko la nje.
Aliongeza kuwa kwa sasa serikali kupitia Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko na Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) wamewezeshwa ili wanunue na kuhifadhi nafaka kwa wingi na kwa kuzingatia viwango vya kimataifa.

“Ni lengo la wizara kuhakikisha wakulima nchini wanaunganishwa na fursa za masoko ya mazao yao ili uchumi wa nchi uendelee kukua kwa kasi kupitia sekta ya kilimo” alisema Bashe
Naibu Waziri Bashe alisema mkakati wa wizara katika kipindi cha miaka mitatu ijayo ni kuona Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko inakuwa na uwezo wa kuhifadhi kisasa nafaka tani 520,000 tofauti na ilivyo sasa ambapo tani 120,000 zinahifadhiwa,hivyo kuwa na uwezo wa kuuza nje.

Kwa upande wake mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani Michael Dunford amesema wanahitaji kununua zaidi ya tani 50,000 za mahindi toka Tanzania kwa ajili ya kusaidia nchi za Uganda na Sudan Kusini.
Dunford alisema kutokana na uzalishaji mzuri ulipo Tanzania kwenye zao la mahindi unatoa fursa ya soko la uhakika endapo vigezo vya ubora unaotakiwa na Shirika la Chakula Duniani utazingatiwa ikiwa ni pamoja na kupunguza tatizo la sumukuvu.

Ameishauri wizara ya kilimo kutumia uzoefu na teknolojia ya kisasa uliopo WFP katika kudhibiti upotevu wa mazao baada ya mavuno ili wakulima wapate ufanisi katika uzalishaji.
“Tanzania inapoteza asilimia 30 ya mazao ya wakulima baada ya mavuno kutokana na kukosekana kwa uhifadhi bora na teknolojia ya kisasa” alisema Dunford

Katika kuhakikisha ushirikiano huu unafikiwa,Dunford alisema Shirika la Chakula Duniani linahudumia chakula kwa watu zaidi ya milioni 150 duniani wenye uhitaji katika maeneo yenye migogoro na majanga ,hivyo Tanzania inayo fursa ya kupata soko la nafaka .
Makubaliano yamefikiwa kuwa wataalam wa wizara ya Kilimo na wale wa Shirika la Chakula duniani watakutana mapema mwezi Octoba mwaka huu kukamilisha agenda muhimu za ushirikiano.

MAKAMU WA RAIS MHE SAMIA SULUHU HASSAN ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO UBALOZI WA ZIMBABWE

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitia saini kitabu cha kumbukumbu ya Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Zimbabwe Mzee Robert Mugabe alipofika katika Ubalozi wa Zimbabwe Oysterbay Jijini Dar Es Salaam leo Septemba 12, 2019.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Naibu Balozi wa Zimbabwe Nchini Mhe. Martin Tavenyika alipofika katika Ofisi ya Ubalozi wa Zimbabwe Nchini Tanzanai kwa ajili ya kutia saini kitabu cha kumbukumbu ya Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Zimbabwe Mzee Robert Mugabe alipofika katika Ubalozi wa Zimbabwe Oysterbay Jijini Dar Es Salaam leo Septemba 12, 2019.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

WAZIRI MKUU AZINDUA MFUMO WA UENDESHAJI BUNGE KIDIGITALI

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizindua mfumo wa uendeshaji Bunge kidigitali, katika ukumbi wa Msekwa, Bungeni jijini Dodoma, Septemba 12, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa na Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai (kulia) wakiangalia mfumo wa uendeshaji Bunge kidigitali, baada ya kuzinduliwa, katika ukumbi wa Msekwa, Bungeni jijini Dodoma, Septemba 12,  2019. 
 Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, akizungumza na Wabunge, baada ya uzinduzi wa mfumo wa uendeshaji Bunge kidigitali, Bungeni jijini Dodoma, Septemba 12, 2019.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Wabunge, kwenye uzinduzi wa mfumo wa uendeshaji Bunge kidigitali, Bungeni jijini Dodoma, Septemba 12, 2019. 

WASIMAMIZI WA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA SIMIYU WAAPISHWA, WAASWA KUZINGATIA SHERIA, KANUNI NA MIONGOZO KUEPUSHA MALALAMIKO

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Wasimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019 kutoka katika Halmashauri sita za Mkoa wa Simiyu wameapishwa Septemba 12, 2019 Mjini Bariadi, ambapo Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amewataka wazingatie sheria, kanuni, taratibu na miongozo katika uchaguzi huo ili kuepusha malalamiko yasiyo ya lazima.

Sagini amesema wasimamizi hao  wanapaswa kutambua kuwa wamepewa jukumu zito ambalo linahitaji umakini wa hali ya juu na utulivu wa akili, hivyo ni vema wakasoma na kuzipitia tena sheria, kanuni na miongozo ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa walizopewa ili wazielewe na waweze kufanya kazi bila kubabaika.

“Kumbukeni kuwa Uchaguzi huu unaweka msingi na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 hivyo ni imani yangu kuwa kila mmoja wenu atakahakikisha anazingatia sheria, kanuni,miongozo na taratibu zilizotolewa ili kuepusha malalamiko yasiyo ya lazima; matarajio yangu ni kwamba mtaishi viapo mlivyoapa leo” alisema Sagini.

Aidha, Sagini amewataka wasimamizi hao kujiepusha na ushabiki wa kisiasa kwa kuwa wao kama wasimamizi ni waamuzi, hivyo hawapaswi kwa namna yoyote kujihusisha na masuala ya ushabiki wa vyama vya kisiasa, ili waaminiwe kuwa wanaweza kutoa haki; watakaobainika kujihusisha na itikadi za kisiasa watachukuliwa hatua za kinidhamu.

Akizungumza mara baada ya kuwaapisha wasimamizi hao, Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio amewataka wasimamizi hao kuishi viapo vyao na kuhakikisha wanafanya majukumu yao kwa uadilifu na kwa mujibu wa sheria kwa sababu watakapokiuka sheria , kanuni na taratibu wataiingiza serikali kwenye gharama.

Kwa upande wao wasimamizi wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa mkoani Simiyu mwaka 2019 wamesema watahakikisha wanatekeleza wajibu na majukumu waliyopewa kwa mujibu wa sheria, kanuni, taratibu na miongozo kama walivyoelekezwa.

“Tunashukuru kwa kuaminiwa katika jukumu hili nyeti la Kitaifa, tunaamini kama tulivyoelekezwa kama wasimamizi tutasimamia yale tunayopaswa tutafanye kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu na tutaviishi viapo vyetu tulivyoapa siku ya leo na kutimiza wajibu wetu kama watumishi wa Umma” alisema Wilbert Siogopi msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi.

“Tunaahidi kwamba tutakitekeleza kiapo tulichoapa leo, tunafahamu kuwa kazi hii ngumu lakini kama mlivyotuasa tukiamua kwa dhati kabisa tukapitia sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya uchaguzi tutafanya kazi inayotarajiwa” alisema Bi . Amina Mbwambo msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Halmashauri ya Wilaya ya Itilima.

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unatarajiwa kufanyika Novemba 24, 2019 nchini kote ambapo katika Mkoa wa Simiyu utahusisha  Vijiji 470, Mitaa 92 na Vitongoji 2652.
 Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Eng. Wilbert Siogopi Makala akila kiapo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio(kushoto), zoezi ambalo limefanyika Septemba 12, 2019 Mjini Bariadi na kushuhudiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini.
 Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Pelagia  Daudi Sogoti akila kiapo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio(kushoto), zoezi ambalo limefanyika Septemba 12, 2019 Mjini Bariadi na kushuhudiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini.
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini,(kushoto walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na Wasimamizi wa chaguzi wa Serikali za Mitaa baada ya wasimimizi hao kuapishwa ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio(kushoto), zoezi ambalo limefanyika Septemba 12, 2019 Mjini Bariadi na kushuhudiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini.
 Bi . Amina Mbwambo msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Halmashauri ya Wilaya ya Itilima akizungumza kwa niaba ya wenzake  mara baada ya kuapishwa ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio(kushoto), zoezi ambalo limefanyika Septemba 12, 2019 Mjini Bariadi na kushuhudiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini.
 Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio(kushoto) akizungumza na wasimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mara baada ya kuwaapisha Septemba 12, 2019 Mjini Bariadi na kushuhudiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini.
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanna Sagini akizungumza na wasimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mara baada ya kuwaapisha Septemba 12, 2019 Mjini Bariadi.
 Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Joyce Thomas Ndunguru akila kiapo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio(kushoto), zoezi ambalo limefanyika Septemba 12, 2019 Mjini Bariadi na kushuhudiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini.
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Bariadi, Bw. Melkizedeck Humbe akitoa neno kwa wasimamizi wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao waliapiswa Septemba 12, 2019  Mjini Bariadi na   Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio na kushuhudiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini.

Mkurugenzi Manispaa ya Sumbawanga apita masokoni kuhamasisha vikundi kuomba mikopo

$
0
0
Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga James Mtalitinya ameendelea kuwahamasisha vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kuhakikisha wanajiunga katika vikundi ili kuweza kupata fursa ya kupewa mikopo ili kuweza kujiajiri hali itakayopelekea kupunga wimbi la wasio na ajira na hatimae kujiongezea kipato.

Amesema kuwa moja ya majukumu ya Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga ni kutoa mikopo ya asilimia 10 kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu na kuongeza kuwa katika mwaka wa fedha 2018/2019 halmashauri ilitoa shilingi milioni 253 na kusisitiza kuwa bado kuna milioni 32 zilizovuka mwaka ambapo kwa mwaka wa fedha 2019/2020 halmashauri inatakiwa kutoa shilingi milioni 230.

“Kufikia Mwezi wa 10 tarehe 15 tunategemea kutoa kiasi cha shilingi milino 120 ikiwa ni makusanyo ya robo ya kwanza kwa maana ya Julai – Septemba, kwahiyo tunaomba wananchi wa bangwe pamoja na wananchi wa Sumbawanga wajiunge katika vikundi visivypongua watu watano mpaka kumi halafu waainishe shughuli wanayofanya na waje waombe mkopo wa kiasi chochote, tutawakagua na baada ya hapo tutawapatia mkopo,” alimalizia.

Ameyasema hayo wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo walipokuwa wakitembelea masoko yaliyopo katika mji wa Sumbawanga ili kujionea hali halisi ya maendeleo ya biashara na kujua changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wananchi katika masoko hayo.

Rais Magufuli atekeleza 79% ya ahadi za barabara katika mji wa Namanyere Rukwa

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo amesifu juhudi za Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuhakikisha anatekeleza ahadi zake alizoahidi kipindi cha kampeni baada ya kutembelea barabara zinzoendelea kujengwa katika mji mdogo wa Namanyere, Wilayani Nkasi na kuona kasi ya ujenzi wa barabara hizo ikiendelea vizuri.

Amesema kuwa ahadi ya mheshimiwa rais ni kujenga barabara zenye jumla ya kilometa tano katika mji na mpaka kufikia mwezi Disemba mwaka 2019 zitakuwa zimefikia jumla ya kilometa 3.95 ambayo ni sawa na asilimia 79 ya utekelezaji wa ahadi zake na hivyo kumtaka mkandarasi nayeendelea na ujenzi wa barabara ya kilometa moja afanye haraka kumalizia ujenzi huo ili wananchi waweze kutumia barabara ambazo zimefungwa kwa muda wa mwaka ili kupisha ujenzi.

“Huyu mkandarasi anayejenga kilometa moja kwa kiwango cha lami kazi yake inasuasua kwasababu mradi huu ulipaswa kukamilika mwezi wa sita mwaka huu na sasa ni mwezi wa tisa, kazi haijakamilika lakini pia kuna kero ambazo zipo ndani ya barabara hizi, kuna vivuko vimewekwa vya muda na kwengine hakuna, watu wanapata shida kuvuka mitaro kwenda kufanya biashara zao lakini pia kwenye matolea ya barabara kuna vifusi, hivyo nakupa siku 12 utoe vifusi na ujenge vivuko kwenye mitaro,” Alisisitiza.

Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa ujenzi wa barabara hizo ili kutimiza ahadi za Mheshimiwa Rais Mratibu wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijiji Tanzania (TARURA) Mkoa wa Rukwa Mhandisi Boniface William alisema kuwa mbali na kujitahidi kuhakikisha barabara hizo zinajengwa kwa wakati lakini kumekuwa na changamoto ya ufinyu wa bajeti pamoja na upatikanaji wa malighafi za ujenzi wa barabara hizo hasa kokoto.

“katika utekelezaji wa hii miradi kumekuwa na changamoto mbalimbali, changamoto mojawapo ni ufinyu wa bajeti, fedha tunayotengewa kulingana na hali halisi ya ‘site’ unakuta ile fedha ni kidogo kiasi kwamba kama ile barabara ya salala ilikuwa tutengeneze kilometa moja lakini kwa milioni 350 tulishindwa kutengeneza kilometa moja kwahiyo tukaweza kutengeneza mita 700 pekee, tatizo jingine ni malighafi kwa maana ya kuwa na chanzo kimoja cha kokoto katika mkoa, hii inachelewesha kazi,” Alisema.

Katika hatua nyingine, Mh. Wangabo wakati alipomaliza kutrembelea barabara zenye jumla ya kilometa moja katika manispaa ya Sumbawanga amewataka wakandarasi wazawa wanaopewa kazi za ujenzi na TARURA kuhakikisha wanaheshimu na kuzingatia masharti ya mikataba ili kufanya kazi kwa wakati na kuongeza kuwa ikiwa wakandarasi hao hawataonyesha uaminifu katika kazi hizo ndogo itakuwa vigumu kwao kupewa miradi mingine mikubwa.

Katika mwaka wa fedha wa 2019/2020 Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Wilaya ya Nkasi wametengewa bajeti ya shilingi milioni 500 wakati TARURA upande wa Manispaa ya Sumbawanga wametengewa bajeti ya shilingi milioni 460 ili kuendelea kukamilisha ujenzi wa barabara katika kutimiza ahadi za Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo (wa tatu toka kushoto) akiwa na wataalamu mbalimbali wakati wa ukaguzi wa barabara zilizopo chini ya usimamizi wa Wakala wa barabara za Mjini na Vijijini Tanzania (TARURA) katika mji wa Namanyere katika Wilaya ya Nkasi.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo (wa pili toka Kushoto) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule (kushoto) Mratibu wa TARURA Mkoa wa Rukwa Mhandisi Boniface William ( wa pili toka kulia) pamoja na Mkurugenzi wa manispaa ya Sumbawanga James Mtalitinya (kulia) wakitembea wakati wa ukaguzi wa barabara zilizopo chini ya usimamizi wa Wakala wa barabara za Mjini na Vijijini Tanzania (TARURA) katika mji wa Sumbawanga, Wilayani Sumbawanga.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo pamoja na Wataalamu wengine wakikagua mitaro katika moja ya barabara za mji wa Sumbawanga. 

TAARIFA KWA UMMA

SUPER MAZEMBE ‘BADO INADUNDA’

$
0
0
 Na Moshy Kiyungi, Tabora

Hauwezi kuamini bendi iliyoanzishwa zaidi ya miongo minne iliyopita, bado ipo inapiga muziki. Bendi hiyo ni ya Orchestra Super Mazembe iliyojipatia umaarufu mkubwa katika nchi za Afrika ya Mashariki na Kati, ikiwa na  makao yake makuu Nairobi, Kenya.

Historia inaeleza kuwa kabla ya kuitwa Super Mazembe, ilikuwa na mizizi katika kundi la Super Vox, iliyoundwa mwaka 1967, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ikiongozwa na Mutonkole Longwa Didos.

Mwaka 1974 Super Vox ikahamishia makazi yake katika jiji la Nairobi nchini Kenya, ambako ndiko walikobadili jina la bendi kuwa Orchestra Super Mazembe. Kwa mujibu wa Mutokole, alisema kuwa bendi yao ilikuwa ikitoa burudani za muziki wa Soukous katika kumbi mbalimbali za jijini humo, kibao chao kikubwa walichoanza nacho wakakiimba kwa lugha adhim ya Kiswahili ni wa Shauri yako.

Vibao vingine maarufu vilivyotamba wakati huo ni pamoja na Loboko, Kayembe, Nabimakate, Atia Joe, Samba, Bwana Nipe Pesa na Kasongo. Super Mazembe ilihesabiwa kama moja ya bendi za Kikongo wakati wa ‘dhahabu’ nchini Kenya.

Ikiwa nchini humo bendi hiyo ilikumbana na bendi zingine zilizokuwepo jijini humo za Les Mangelepa, Baba Gaston, Orchestra Virunga, Orchestra Moja One, Les Knoirs na zingine nyingi, ambazo nazo zilikuwa na wanamuziki wengi waliokuwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (zamani Zaire).

Kama makundi mengi ya kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yaliyojikita katika nchi za  ya Afrika Mashariki, Super Mazembe ilikuwa tishio kwa jinsi ilivyokuwa imeenea wanamuziki waliokuwa mahiri kila idara.

Baadhi ya wanamuziki wa bendi hiyo ambao kila mara walikuwa wakiingia na kutoka, ni pamoja na Mutonkole Longwa Didos, Lovy Longomba, Kasongo wa Kanema, Kilambe na Katele Aley waliokuwa watunzi na waimbaji.

Lovy aliacha bendi hiyo mwaka 1981, alianzisha vikundi vya Super Lovy na baadae Bana Likasi. Lovy alikuwa ni mwana wa Vicky Longomba, aliyekuwa mwanamuziki mkongwe katika bendi ya T.P.OK.Jazz iliyokuwa ikiongozwa na Franco Luambo Makiadi.

Familia ya mzee huyo takriban wote wamepitia mambo ya muziki akiwemo Awilo Longomba, Watoto wa Lovy Longomba wakiongozwa na Christian Lovy, ambao waliunda kikundi chao  cha Longombas, ambacho ni maarufu nchini Kenya.

Kasongo wa Kanema naye aliondoka katika bendi hiyo mapema miaka ya 1980, akaenda kujiunga katika bendi ya Orchestra Virunga, iliyokuwa ikiongozwa na Samba Mapangala. Kwa upande wa washika ala za muziki alikuwepo Bukasa wa Bukasa ‘Bukalos’ aliyekuwa kiongozi wa wapiga magitaa. Bukalos alitangulia mbele za haki mwaka 1989.

Aidha alikuwepo mcharazaji wa mwingine wa gitaa Kayembe Miketo, ambaye alifariki dunia mwaka 1991. Muungurumishaji wa gitaa zito la besi alikuwa Mwanza wa Mwanza Mulunguluke ‘Atia Jo’, aliyefariki dunia mwaka 2006. Komba Kasongo Songoley aliyekuwa ikilicharaza gitaa, yeye alifariki mwaka 1990.

Drums zilikuwa zikicharazwa na Kitenge Ngoi wa Kitombole na Musa Olokwiso Mangala. Orchestra Super Mazembe ilitamba kwa nyimbo zao zingine za Mwana Mazembe, Longwa Mukala Musi, Ouma ya mwaka 1980, Banamama ya mwaka 1983, Samba ya mwaka 1978, Okova, Mbanda ya Mobange na Mwana Nyau.

Kama zilivyo wahi kuanguka bendi zingine, halikadhalika Super Mazembe aliondoka kwenye sura ya muziki mwaka 1985 baada ya baadhi ya wanamuziki wake kuokoka na wengine kufariki dunia. Lakini habari zilizopatikana hivi karibuni toka Nairobi, zimeeleza kwa Super Mazembe imerejea tena ulingoni, baada ya baadhi ya wanamuziki wake walio hai, kuizindua upya.

Makala hii imeandaliwa kwa msaada wa mitandao mbalimbali.
Mwandaaji anapatikana kwa namba: 0713331200, 0736331200, 0784331200 na 0767331200.

MESS CHENGULA AWATAKA VIJANA KUZINGATIA NIDHAMU NA JUHUDI MAZOEZINI ILI KUFIKIA MAFANIKIO

$
0
0
Mdau wa michezo mkoani Iringa Mess Chengula akiwasalimia wachezawa timu mbili zilizokuwa zimeingia fainali ya mashindano ya UVCCM CUP Kata ya Mkwawa yaliyofanyikia katika chuo cha mkwawa mkoani Iringa
Mdau wa michezo mkoani Iringa Mess Chengula akimkabidhi kapteni wa timu ya Donbosco fc ambayo imeibuka bingwa wa mashindano ya UVCCM CUP Kata ya Mkwawa kwa ushindi wa penat 5-3 dhidi ya Don south baada ya sare ya 1-1 katika uwanja wa chuo cha Mkwawa kwa kijinyakulia ng’ombe mmoja.
Mdau wa michezo mkoani Iringa Mess Chengula akiwa na wadau na viongozi wa CCM kata ya mkwawa wakifauatilia fainali ya mashindanohayo.
Mdau wa michezo mkoani Iringa Mess Chengula akimkabidhi kapteni wa timu ya Don south ambao waliibuka kuwa washindi wa pili.

NA FREDY MGUNDA, IRINGA
VIJANA manispaa ya Iringa wametakiwa kuzingatia nidhamu na juhudi katika mazoezi kwa lengo la kufikia mafanikio katika michezo na kukuza zaidi vipaji walivyojaliwa na mwenyezi mungu.


Hayo yamesemwa na mdau wa michezo mkoani Iringa Mess Chengulawakati wa fainali ya mashindano ya UVCCM CUP Kata ya Mkwawa,iliyofanika katika uwanja wa chuo kikuu cha Mkwawa na kuhudhuliwa na wapenzi wengi wa mpira wa miguu mkoani Iringa.


Chengula alisemakuwa Mkoa wa Iringa umebarikiwa na vipaji vingi vya mpira wa miguu kwa kuwa amefanikiwa kuwaona vijana wengi waliokuwawanacheza fainali ya mashindano ya UVCCM CUP Kata ya Mkwawa na ameahidi kuhakikisha ataendelea kusaidia michezo ndani ya mkoa wa Iringa.


“Nimefarijika sana baada ya kuona vijana walivyokuwa na vipaji vya kusakata kabumbu maana nimebarikiwa kwa kuwaonakwamacho yangu vijina walivyokuwa wamechangamka kusakata soka uwanjani hapa chuo cha Mkwawa” alisema Chengula


Chengula amewataka wadau mbalimbali kuandaa mnashindano mbalimbali ambayo yanakuwa yanawakusanya vijana wapenda michezo na kuwawekasehemumojaambayo inakuwa inabarisha mtazamo kwenye akili za watu ambao wanakuwa wanahudhuria michezo hiyo.


“Kwanza nimpongeze diwani wa kata ya Mkwawapamojana viongozi wa chama cha mapinduzi (CCM) kwa kuwaunganisha vijana pamoja na kuwaweza kuwa na lugha moja ya kimichezo na kuweza kubarishana mawazo ya kimaendeleo walipokuwa viwanjani” alisema Chengula


Aidha Chengula alisema kuwa michezo inaleta chachu kwa vijana kwenda kumchagua kiongozi wanayemtaka katika serikali za mitaa ambazo hivi karibuni utafanyika nchi nzina hivyo zoezi la kuwakusanya vijana pamoja linaleta picha nzuri ya uchaguzi.


“Rais wa Dr John Pombe Magufuli amewafundisha uzalendo wa kufanya kazi nakujitegemea na kufanya kazi kwa uhuru na ndivyo wananchi wote tunatakiwa kufanya kazi kwa kujituma na kujitafutia mali zetu wenyewe” alisema Chengula


Naye Mdhamini wa Mashindano Amiri Zakaria Kalinga ambaye ndiye diwani wa kata ya Mkwawa alisema kuwa lengo la mashindano hayo ni kuwaunganisha vijana kuwa wamoja na kutambua kuwa michezo ni ajira namichezoinaimarisha kuwa na afya njema.


“mashindano ya UVCCM CUP Kata ya Mkwawa yameshirikisha timu za kata ya mkwawa kwa kuendeleza kuwaunganisha kuwa wamoja kamaambaovyotupo hivi sasa” alisema Kalinga


Kalinga alisemakuwakata ya Mkwawa ina viwanja vingi ambavyo sio bora kama viwanja vya chuo kikuu kwa ubora hivyo tunatakiwa kutafuta wadau kuhakikisha tunatengeneza viwanja vyetu wenyewe.


Na katika fainali hiyo Timu ya Donbosco fc imeibuka bingwa wa mashindano ya UVCCM CUP Kata ya Mkwawa kwa ushindi wa penat 5-3 dhidi ya Don south baada ya sare ya 1-1 katika uwanja wa chuo cha Mkwawa kwa kijinyakulia ng’ombe mmoja.

Huku mshindi wa pili Don south na Mshindi wa tatu Dream team kutoka ikonongo kwa penati 5-4 baada ya sare tasa dhidi ya hoho fc ya itamba wote walipata mbuzi moja moja.

MC HAMMER ALIVYOTESA MAREKANI

$
0
0
Na Moshy Kiyungi, Tabora.
Mwanamuziki MC Hammer alijipatia umaarufu mkubwa kwa kazi yake ya muziki wa Hip hop nchini Marekani.

Alianza kufanya muziki mwishoni mwa miaka ya 1980 hadi katikati ya 1990, wakati huo haikuwa rahisi watu kushindwa kujitokeza kwenye onesho la ngoma zake kali ambao alikuwa akiimba na kunengua jukwaani.

Baada ya kuzaliwa miaka 57 iliyopita, alipewa jila Stanley Kirk Burrell, ambaye mpaka sasa anakumbukwa kwa kusaidia kwa kiasi kikubwa kuupeleka muziki wa dunia nzima na watu wakafurahia.

Aidha anakumbukwa kutokana na aina ya muziki aliyokuwa akiifanya nchini mwake Marekani na kutamba duniani kote.

Licha ya kuwa mwanamuziki, MC Hammer ni maarufu wa Hip hop ama muziki wa kufokafoka pia amewahi kuwa mnenguaji, mtayarishaji wa muziki ma mjasiriamali katika muziki.

Ni kijana miongoni mwa vijana  wa Kimarekani mwenye asili ya Afrika ambao walitumia muda wao mwingi kufungua na kuweka milango ya muziki kulekea katika faidakubwa tofauti na ilivyokuwa awali.

MC Hammer alianza kufanya muziki mwishoni mwa miaka ya 1980 hadi katikati ya 1990, wakati huo ilikuwa ngumu watu kushondwa kujitokeza kwenye shoo yake kutokana na ngoma kali ambazo alikuwa akiimba, alijaza sana kwenye shoo zake.

Wakati huo ilikuwa kama umeenda disco kujirusha halafu DJ eti asipige wimbo wake, vijana wa mjini ‘wanamfanyizia’ DJ huyo.

Vijana wengi wa enzi hizo walikuwa wakimuiga sana kwa kuimba, wengine waliona ni fahari kumuiga kwa mavazi hata uchezaji wake.

MC Hammer alitamba wakati wake na vibao  vikali vya U Can’t Touch This na 2 Legit 2 Quit.  Vibao hivyo vilitamba na kummfanya afahamike miongoni mwa wapenda muziki duniani.

Safari ya MC Hammer katika muziki ilianzia mwanzoni mwa miaka ya 1980, pale alipoona ana rap mitaani na katika kumbi zisizo na hadhi, akaamua kukopa dola 20,000 (Shilingi Milioni 45.8 za Kitanzania)  akaanzisha lebo ya Bust it Production, ikiwa na studio yake.

Baada ya kuwa na uwezo wa kurekodi kazi zake, MC Hammer alifanikiwa kutenganeza albamu yake ya kwanza iitwayo Feel Power ya mwaka 1986.

Albamu hiyo ilirekodiwa mwaka 1986 na kuachiwa mwaka uliofuatia wa 1987 akitumia studio yake mwenyewe, Nyingine ilikuwa ikiitwa Oaktown Records chini ya mtayarishaji Felton Pilate.

Albamu hiyo iliuza zaidi ya nakala 60,000 ka ilisambazwa na City Hall Records. MC Hammer pia aliachia singo yake iitwayo “Ring Em”, ambayo iklifanya vizuri wakati huo na kuzidi kumpa jina.

Kuanzi hapo studio kibao zikawa zinataka kufanya kazi na MC Hammer lakini yeye aliamua kuingia mkataba na studio ya Capital Records wa kurekodi albamu yake nyingine huku akikunja dola Milioni 1.7 ambazo sawa na Shilingi bilioni 3.9.

Fedha hizo alizopata MC Hammer aliamua kuwekeza katika mambo mbalimbali ikiwemo kampuni ya mavazi mbalimbali na biashara nyingine ili aweze kujiongezea kipato mbali na muziki.

Akiwa na Capitalm Records, mwaka 1989, MC Hammer aliachia albamu ya Let’s Get It Started, iliyouza nakala million mbili huku ikiwa na vibao vikali kama Pump It Up, Turn This Murtha Out, Let’s Get Started na They Put Me in The Mix.

Baadhi ya albamu zingine za MC Hammer ni Please Hammer, Don’t Hurt ‘Em ya mwaka 1990, Too Legit to Quit ya mwaka 1991,  New Venture ya mwaka 1992, The Funky Heahunter ya mwaka 1994, Inside Out ya mwaka 1995 na Too Tight ya mwaka 1996.

MC Hummer aliendelea kutoa albamu mbalimbali lakini singo yake ya mwisho aliitoa mwaka 2014, ikiitwa All in My Mind, aliyoimba na kundim lake la zamani la Oakland, wakimshirikisha Mistah F.A.B

Miaka hiyo ya 1990, MC Hammer aliigeukia dini na kuwa muhubiri wa dini ya Kikristo na kuendesha kipindi chake cha M.C. Hammer and Friends.

Aidha kuna mradi wake wa Katuni za televisheni ziitwazo Hmmerman, zilitoka mwaka 1991 na amewahi kuwa na kipindi chake cha kuzungumzia maisha kilichoitwa Hammertime mwaka 2009.

MC Hammer bado anapanda kimuziki, lakini wajuvi wa mambo wamesema hawezi kurejea enzi zake za zamani.


Makala hii imeandaliwa kwa msaada wa mitandao.
Mwandaaji anapatikana kwa namaba: 0784331200 na 0767331200.

Serikali yamkana Musiba, Waziri Lugola amuonya kuacha kuiongelea Serikali

$
0
0
Charles James, Michuzi TV
SERIKALI imemuonya Mwanaharakati huru, Cyprian Musiba kuacha mara moja kufanya harakati zake kwa kuwaaminisha Watanzania kuwa Serikali inamtuma kufanya hivyo.

Onyo hilo limetolewa leo jijini Dodoma na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe Kangi Lugola wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya kiusalama nchini.

Waziri Lugola amesema Musiba amekua akijaribu kuwaonesha na kuwaaminisha watanzania kwamba pengine Serikali imemtuma hivyo yeye kama Waziri mwenye dhamana ya mambo ya ndani ya Nchi anawahakikishia wananchi kwamba Serikali haiwatumi wanaharakati hao.

Amesema anafahamu kuwa wapo wanaharakati nchini wanaofanya harakati zao lakini amewaonya kuacha kufanya uwanaharakati unaopitiliza wa kuwaaminisha wananchi kuwa sisi viongozi tunabariki uwanaharakati wao.

" Nimuonye huyu Musiba kuacha kuhusisha harakati zake na Serikali au asiwaaminishe Watanzania kuwa Rais anamtuma, Serikali hatuwezi kufanya kazi kwa kuwatuma wanaharakati kutusemea.

" Kwa sababu imefikia hata wakati fulani viongozi wa Dini wanaandika waraka wakijaribu kumzungumzia huyu Musiba wanavyomuona na vitendo vyake kwamba wanadhani Serikali inabariki mambo yake. Niwahakikishie sisi hatujamtuma na tunamuonya mara moja kuacha harakati zake hizo," Amesema Waziri Lugola.

Amesema pamoja na kwamba Serikali haimtumi Musiba na kueleza kuwa Jeshi la Polisi likibaini kuwa anaendelea kujiwasilisha katika mazingira yanayoashiria kuwajengea hofu watanzania kwamba maneno anayoyasema anatumwa na Serikali basi watamchukulia hatua kali.

" Ninarudia akiendelea kujitanabaisha kwamba anatumwa na Serikali basi tutamchukulia hatua kali sana bila kuangaliana usoni wala kuoneana huruma," Amesema Mhe Lugola.

Amemtaka Musiba kutovuka mipaka yake na kama anafanya uwanaharakati basi asijishughulishe na mambo ya Serikali.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe Kangi Lugola akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma kuhusu hali ya kiusalama nchini

SERIKALI YA KUBORESHA TBC KUFIKIA VIWANGO VYA KIMATAIFA

$
0
0
Anitha Jonas – WHUSM
Serikali ya ahidi kuendelea kuboresha Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kwa kuhakikisha linakuwa na muonekano bora kama mashirika ya Kimataifa.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dodoma na Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza wakati wa  Semina ya kuwajengea uwezo wabunge  kuhusu mpango wa serikali wa kuboresha mfumo wa Visimbusi kwa kutaka kuanzisha utaratibu wa kununua kifaa maalum kitakachobeba kifurushi ambacho kinaitwa ‘’CAM’ kifaa hicho kitatumika badala ya kununua zaidi ya kisimbusi kimoja.Semina hiyo iliandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa wabunge wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii.

 ‘’Na serikali inampango endelevu wa kuboresha TBC na kuifanya ya kisasa zaidi na ndiyo maana tangu serikali ya awamu ya tano iingie madarakani imekuwa ikiongeza Bajeti ya Maendeleo kwa Shirika hilo na lengo ni kuifanya iwe yenye bora zaidi,’’alisema Shonza.

Akiendelea kuzungumza katika Semina hiyo Mheshimiwa Shonza alitoa wito kwa wanasiasa wote wa vyama vya upinzani  kujitokeza na kukitumia chombo cha TBC kwani shirika hilo ni la umma na halina ubaguzi kwa wanachama wa upinzani kama inavyosemekana kwani linaendeshwa kwa kodi za wananchi.

Kwa upande Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Huduma na Maeneleo ya Jamii Mhe.Peter Serukamba  alitoa rai kwa uongozi wa TBC kuhakikisha unatumia wapiga picha wenye weledi wakati wa uandaaji wa Makala za utalii kwa ajili ya Chaneli ya Utalii ya TANZANIA SAFARI CHANELI  kama chaneli nyingine za wadau wa utalii. 

Halikadhalika nae Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe.Juma Nkamia alitoa angalizo kwa uongozi wa TCRA kufuatilia kwa umakini Maudhui ya Redio za Kijamii kwani redio hizo zisipofuatiliwa kwa karibu zinaweza kuleta changamoto hivyo ni vyema waweke mkakati madhubuti wa kufuatilia vituo hivyo.
 Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akitoa wito kwa wanasiasa kutoka vyama vya upinzani kutumia Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kutangaza maendeleo leo jijini Dodoma wakati wa Semina ya kuwajengea uwezo wabunge wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu mpango wa serikali kuboresha mfumo wa visimbusi na kuleta mfumo wa matumizi ya ‘’CAM’’ kwa televisheni ,kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Nicholaus William.

 Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe.Peter Serukamba  akitoa maelekezo kwa uongozi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kuzingatia ubora katika uandaaji wa Makala za Chaneli ya Utalii ya SAFARI wakati wa Semina ya wabunge wa kamati hiyo (hawapo pichani) leo Jijini Dodoma,kushoto ni Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza.
 Mkuu wa Kitengo cha Leseni Mhandisi Andrew Kisaka kutoka Mamlaka ya Mawaliano Tanzania akitoa semina kuhusu mpango wa serikali kuboresha mfumo wa visimbusi na kuleta mfumo wa matumizi ya ‘’CAM’’ kwa televisheni ambapo mteja hata lazimika kununua kisimbusi zaidi ya kimoja ilikupata kifurushi bali atanunua kifaa hicho na kukiweka katika kisimbusi aina yoyote.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania Dkt.Ayoub Rioba akitoa semina kwa wabunge wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu umuhimu wa shirika hilo kuzingatia maudhui ya kitanzania zaidi badala ya mudhui ya mataifa mengine leo jijini Dodoma katika semina ya kuwajengea uwezo wabunge kuhusu mpango wa serikali kuboresha mfumo wa visimbusi na kuanzisha matumizi ya teknolojia ya  matumizi ya ‘CAM’.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe.Juma Nkamia (katikati) akitoa angalizo kwa uongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kufuatilia maudhui ya redio za jamii kwani nyingi zimekuwa na changamoto ya maudhui wakati wa semina Semina ya kuwajengea uwezo wabunge wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu mpango wa serikali kuboresha mfumo wa visimbusi na kuleta mfumo wa matumizi ya ‘’CAM’’ kwa televisheni iliyofanyika leo Jijini Dodoma.      

Serikali inaendelea kusajili vyama na vilabu vya michezo kwa wanawake

$
0
0
Na Shamimu Nyaki –WHUSM
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza amesema kuwa Serikali inaendelea kusajili Vyama na Vilabu vya michezo ikiwemo vya soka la wanawake ili kuimarisha maendeleo ya mchezo huo chini.

Mhe.Shonza ameyasema hayo leo Bungeni Jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mhe.Devotha Minja (Viti Maalum) aliyeuliza Je ni upi mkakati wa Serikali wa kuhamasisha soka kwa wanawake katika ngazi za Mikoa na Wilaya kuwa na timu za soka kwa wanawake kama ilivyo kwa wanaume ?

“Serikali imekuwa ikiandaa program mbalimbali za kukuza na kuendeleza soka la wanawake ikiwemo michezo ya UMITASHUNTA na UMISETA na  kuanzishwa kwa shule za michezo ambazo zinadahili wanamichezo wa kike ambao moja kati ya michezo inayofundishwa ni mpira wa miguu”amesema Mhe.Shonza.

Akijibu maswali ya nyongeza ya Wabunge Mhe.Shonza ameongeza kuwa Serikali inaendelea kuhamasisha wafadhili na wadhamini mbalimbali kufadhili na kudhamini soka la wanawake nchini.

Aidha Mhe.Shonza amesema kuwa mafunzo mbalimbali ya ukocha na uamuzi wa mpira wa miguu kwa wanawake yameendelea kutolewa,sasa tunawaamuzi wanaotambulika na Shirikisho la Mpira wa Miguu duniani (FIFA)

Halikadhalika Mhe.Shonza amesema kuwa Serikali inaendelea kuwahamasisha wanawake kujihusisha katika kucheza mpira wa miguu kwa kuwa ni mchezo maarufu na kwamba unatoa fursa ya ajira kwa mtoto wa kike.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akijibu maswali leo Bungeni Jijini Dodoma.

UTITIRI WA DECODER MWISHO DECEMBER MWAKA HUU - TCRA

JOSE CHAMELEONE MWANAMUZIKI TAJIRI UGANDA

$
0
0
Na Moshy Kiyungi, Tabora.

Jose Chameleone yaelezwa kuwa ndiye anayeongoza kwa utajiri miongoni mwa wanamuziki nchini Uganda, akikadiriwa kuwa na utajiri unaofikia Shilingi bilioni 1.5 kwa fedha za Tanzania.

Chameleon anamiliki mijengo ya bei mbaya ya kukodisha (Apartments),iitwayo Daniella Villas, jijini Kampala, studio yake iitwayo Leon Island, ambapo imejijengea umaarufu mkubwa nchini mwake Uganda. Mwanamuziki huyo ametajwa na takwimu za kifedha kuwa ana utajiri wa zaidi ya Dola za Marekani milioni 5.

Katika orodha ya mali zake, pia anamiliki ufukwe uitwao Coco Beach, uliopo Barabara ya Entebbe nchini humo. Jose Mayanja Chameleone, pia ana mikataba minono na kampuni zinazomtumia kutangaza bidhaa na huduma zake. Moja kati ya mikataba yake iliyowahi kumtajirisha ni ile ya MTN na simu za Android.

Jose Chameleone ambalo ni jina la kisanii, alipozaliwa mwaka 1976, wazazi wake walimpa jina la Joseph Mayanja, ambalo siyo geni miongoni mwa wapenzi na washabiki wa muziki wa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati. Chameleone alianza muziki mwaka 1996, kipindi hicho akiwa ‘DJ’ katika ukumbi wa usiku wa Missouri uliopo Kampala.

Moja kati ya nyimbo zake za kwanza ulikuwa wa "Bageya", aliomshirikisha msanii kutoka Kenya Redsan. Albamu yake ya kwanza ilitolewa nchini Kenya mwaka wa 1999. Tangu wakati huo aliachia albamu kadhaa zikiwa pamoja na "Bageya" ya mwaka wa 2000, "Mama Mia" mwaka wa 2001, "Njo Karibu" mwaka wa 2002, "The Golden Voice" mwaka wa 2003, "Mambo Bado" mwaka wa 2004 na "Kipepo" mwaka wa 2005.

Aidha alishirikiana na mwanamuziki mwenzake Bebe Cool, lakini baadaye waliibuka kuwa na upinzani mbaya. Mtindo wa muziki anaocheza Chameleone ni mchanganyiko wa muziki wa tamaduni wa Kiganda, rumba ya Kati ya Afrika, Zouk na ragga. Jose Chameleone ni mwanachama wa Jamii ya Mwanamuziki, muungano wa wanamuziki ambao hutumia umaarufu na mali zao kusaidia kuondoa umaskini na kujenga kampeni za mwamko wa Virusi Vya Ukiwi VVU.

Amezitembelea nchi nyingi za ng'ambo kufanya maonesho yake zikiwemo Marekani, Uingereza na Sweden miongoni mwa mengine. Ikumbukwe kuwa wimbo wa Kipepeo ulikuwa haukauki vinywani mwa watu wazima pamwe na watoto wadogo, wakisikika wakitamka Kipepo, Kipepeo, wimbo ambao ulitungwa na kuimbwa na mwanamuziki huyo Jose Chameleone.

Aidha jina alifanya ‘kufuru’ baada ya kuachia vibao vya Jamila, Bei Kali, Mama Rhoda na nyingine nyingi vilivyo muongezea umaarufu zaidi. Ngoma zake zingine ambazo zimewahi kutikisa kwenye soko la muziki Barani Afrika ni ‘Wale Wale’, ‘Nkoleki’, ‘Vale Vale’, ‘Dorotia’, ‘Tubonge’, ‘Agatako’ na ‘Pam Pam’.

Mpaka mwaka 2013, tayari alikuwa na albamu 12. Miongoni mwa matukio yaliyowahi kumpa umaarufu mkubwa ni kuvunja rekodi ya kuingiza mashabiki wengi kwenye Uwanja wa Kriketi wa Lugogo. Katika onesho hilo lililopachikwa jina la ‘Tubonge Live’, takribani mashabiki 40,000 walizama ndani kushuhudia.

Licha ya kufanya vizuri nchini mwake, kazi za Chameleon zimekuwa zikitesa nje ya mipaka ya nchi hiyo. Jose Mayanja kutokana na ubunifu wake amekuwa akiishi maisha ya kifahari, ambapo mwenyewe alithibitisa kuwa muziki unalipa. Kali zaidi ni pale aliponunua jozi mbili za viatu vya kisasa vilivyomgharimu kiasi cha zaidi ya milioni 40.

Chameleone na familiya yake wanaishi kwenye jumba lao la kifahari lenye gharama za takriban Shilingi milioni 17, nje kidogo ya jiji la Kampala. Aidha anamiliki Coco Beach, iliyopo ufukweni mwa Ziwa Victoria, kukiwa na vivutio vya burudani vyenye thamani Shilingi milioni 27.

Jose pia anamiliki magari ya kifahari aina ya Cadillac Escalade, BMW, Premio, Toyota Ipsum, Landcruiser VX, Mercedes Benz yenye thamani Shilingi milioni 270.

Chameleone amewekeza kwenye miradi mingine mikubwa inayomuongezea kipato ikiwa ni pamoja na kumiliki mjengo wa kupangisha ‘Apartment’ katika mji wa Arizona, nchini Marekani, jumba la kifahari katika vilima vya Sekuku jiji la Kampala na nyumba nzuri sana aliyoinunua kwa bei ‘ndefu’ mjini wa Kigali, Rwanda.

Mwaka 2013, alitajwa kuwa mmoja kati ya wasanii sita matajiri Afrika. Awali wasanii Bebe Cool na Navio, walijitangaza kuwa ndiyo matajiri nchini Uganda, ndipo Chameleone alipoibuka na kuanza kuanika mali zake. Jose alikerwa zaidi aliposikia watu wanasema kuwa aliongopa kutamka kuwa alimpa mkewe gari aina ya Range Rover katika sikukuu ya Wapendanao.

“Haijalishi mimi kumnunulia Daniella Range Rover lakini yeye ana lake na langu lipo, watu wanapaswa kuamini kuwa mimi ni mwanamuziki tajiri na mwenye mali kibao,” alijigamba Chameleone

Akifanya mahojiano na kituo kimoja cha redio, Chameleone alikanusha tetesi kuwa Range Rover walilodai ni lake, lilikuwa la promota wa muziki aitwaye Sipapa.Jinsi mafanikio yake yalivyokuwa yakitiririka mithiri ya maji mtoni, nguli huyo aliwahi kutuhumiwa kwamba hutumia nguvu za giza katika kutengeneza jina lake na hatimaye kupata utajiri alionao.

Mahasimu wake walidai kuwa umaarufu na utajiri wake barani Afrika umetokana na ‘ndumba’. Aliyekuwa wa kwanza kumtuhumu Chameleone kutumia nguvu za giza ni mkali wa muziki wa raga, Badman Denzo. Badman alisema amekuwa ‘akinyunyiza’ ili kufanikisha malengo yake kimuziki.

Nyota huyo alidai kuwa Chameleon amekuwa akitembelea Tanzania mara kwa mara kwa lengo la kukutana na waganga wake.Badman aliyasema hayo wakati alipokuwa akihojiwa na kituo cha televisheni cha NBS. Nyota huyo aliyewahi kutamba na kibao ‘Big Mouth By Far’ alimtaja Chameleone pale alipoambiwa amtaje msanii mmoja anayetumia nguvu za giza.

“Nina uhakika Chameleone anatumia uchawi, huwa anapata mambo hayo kutoka Tanzania, niliwahi kumkuta Dar es Salaam”. alidai Denzo. Chameleone aliposikia shutuma hizo, alikanusha vikali huku akisistiza kuwa jitihada zake ndiyo msingi wa mafanikio yake.

Jose aliongeza kusema kwa waliomtaja kuwa ni mchawi, walilenga kumchafua na kulifuta jina lake kwenye soko la muziki. Chameleone ambaye ni kaka wa mastaa wa muziki Uganda, Palaso na Weasel, alisema yeye ni muumini mzuri wa dini ya Kikiristo, si rafiki wa shetani na kuongeza kuwa uchawi hauna ‘dili’.

Miongoni mwa matukio yaliyowahi kumpa umaarufu mkubwa Jose Chameleone, ni kuvunja rekodi ya kuingiza mashabiki wengi kwenye Uwanja wa Kriketi wa Lugogo. Katika onesho hilo iliyopachikwa jina la ‘Tubonge Live’, takribani mashabiki 40,000 walizama ndani ya ukumbi.

Jose Chameleone aliwahi kuwepo kwenye orodha ya Wanamuziki matajiri Afrika, akiwa ni mwimbaji pekee aliyeiwakilisha Uganda kwenye hiyo orodha hiyo. Sehemu ya utajiri wake unatoka kwenye biashara za nyumba na viwanja, pia mauzo ya simu za mkononi zenye jina lake na makampuni makubwa ya kibiashara. Jose aliazimia kufanya onesho kubwa December 2014, ambalo kiingilioni kilikuwa Shilingi milioni moja za Uganda,ambako gari lake jipya aina ya Range Rover ya mwaka 2013, ambalo lilonekana kwa mara ya kwanza kwenye onesho hilo.

Mwanamuziki huyo Jose Chameleone, alinunua jozi moja ya viatu kwa kulipa dola elfu 12 na nusu, wakati huohuo wengine wakadai eti anajionyesha kuwa ‘anazo’. Lakini Chameleone alisema ameamua kuizawadi miguu yake!

Mwimbaji huyo wa wimbo wa ''Wale wale, waliobarikiwa na mungu'', alisema siyo majivuno kamwe bali ni njia yake ya kumshukuru Mungu kwa kumjalia na kumpa uwezo kama huo. Wimbo huo tayari umetazamwa na watu zaidi ya milioni moja laki tatu katika mtandao wa Youtube.

Alipokuwa ziarani nchini Kenya, aliwaacha watu vinywa wazi baada ya kuweka mtandaoni picha ya viatu vyake aina ya Nike Air Mag, ambavyo jozi hiyo alinunua kwa dola 12,500 za Kimarekani. Ilifahamika kuwa Chameleone kanunua viatu kwa jozi moja kwa pesa sawa na milioni moja na laki tatu za Kenya au karibu milioni 26 za Tanzania.

Tambo za Chameleon zlipelekea baadhi ya mahasidi wake kumnanga eti nafuja pesa. Lakini mwenye aliwapa ushauri kuwa ikiwa wao hawawezi kutoa dola elfu 12 mia tano kununua kiatu, basi waende kwa Wachina wanaouza viatu bei rahisi sana...wasimuonee sooo, wakanunue viatu saizi yao mali ya Wachina.

Mwenyewe alisema anajipa raha, ''jifurahishe ungali hai'', Chameleone alijigamba. Alifafanua kuwa anarudishia shukran miguu yake kwa kusimama naye na kumuwezesha kufika alipo sasa. Chameleone alikumbusha kuwa miaka zaidi ya minane iliyopita, angelikuwa Kiwete kutokana na ajali mbaya. Sasa amepona na pesa ziko ''kwanini nisishukuru miguu yangu?

Ikumbukwe kwamba Jose Chameleone alijirusha kutoka ghorofa ya tatu katika hoteli ya Impala jijini Arusha, na kusababisha kuumia vibaya ikiwa ni pamoja na kuvunjika miguu yote.

Walinzi wa hoteli hiyo walikimbilia eneo aliloangukia baada ya kusikia kishindo, wakamkuta akiwa hawezi kuinuka. Hata hivyo haikueleweka mara moja sababu zilizomfanya mwanamuziki huyo kujirusha.

Baada ya tukio hilo wenyeji wake ambao walikuwa ni Clouds FM, waliokuwa wamemualika kwa ajili ya shughuli ya Fiesta ya Tanga, walilazimika kufanya utaratibu wa kumpeleka hospitali.

Taarifa zilipomfikia baba yake huko Uganda, alikodi Ndege ambayo ilituwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa KIA kwa ajili ya kumbeba Jose Chameleone, akapelekwa kwao na kulazwa katika hospitali moja ya nchini Uganda.

Kuumia kwa Chameleone kulisababisha ashindwe kufanya onesho katika tamasha la Fiesta jijini Tanga, ambako kulikuwa na Wasanii wengi wa Tanzania, yeye ndiye angelikuwa mgeni rasmi.

Jose Chameleone amekuwa akitunga na kuimba nyimbo kwa lugha za Kiswahili, Luganda na Kiingereza. Jose anaelezwa kuwa amebadilisha sura ya muziki nchini mwake Uganda, hususan kwa kufanya muziki wa asili kukubalika kwa sehemu nyingi ulimwenguni. Baadhi ya mambo yanayothibitisha utajiri wa nyota huyo ni makadirio ya ujumla ya utajiri wake unaofikia Shilingi bilioni 1.5 kwa fedha za Tanzania.

Pamoja na utajiri huo, alisema bado anazisaka pesa kwani bila ya kuwa na tamaa ya kusaka mafanikio zaidi, ndoto huenda zisitimie. Mayanja alisisitiza kuwa, baada ya kumiliki nyumba, magari na Akaunti iliyonona benki, sasa ana ndoto za kumiliki Chopa yake ‘Helikopta’.

Sababu ni kwamba amekuwa akikodi Chopa mara kadhaa kwenda katika matamasha au kama alivyofanya wakati alivyomuoa mkewe Daniela Atim. Jose Chameleone anaweza kuonekana jeuri na mtata mbele ya mashabiki wake, lakini kuna kitu kimoja ambacho wengi wanaweza wasiwe wanafahamu.

Chameleone ni baba anayeipenda familia yake na anayewajibika kuiweka katika mazingira mazuri kadri awezavyo. Chameleone ana mke na watato wanne. Mtoto wa kwanza ni wa kike anaitwa Ayla Mayanja Onsea, aliyempata wakati akiwa kwenye mahusiano na Dorotia. Katika ndoa yake na Daniella, wamepata watato watatu, Abba Marcas Mayanja akiwa wa kwanza kwenye ndoa yao, Alfa Mayanja na Alba Shyne Mayanja. Kati ya watoto walinaswa na mitandao ya kijamii wakiendesha gari la kifahari katika jiji la Kampala licha ya umri wao kuwa mdogo.

Mwaka 2005 na 2006 Jose alitayarisha mlio wa mziki ambao ulitumika kwa wimbo wa mwanamziki nguli Joseph Haule, maarufu kwa jina Professor J. Wimbo huo unaitwa “Nikusaidieje”. Jose Chameleone akatumia ujanja kwa kuiba beat ile, akaitumia kwenye mziki wake wa Bombo Crat, ambayo ilifanya vyema nchini Uganda. Baada ya mwenye mali Porofessor J. kugundua kuwa kaibiwa, akawasiliana na Chameleone. Majibu ya aliyopewa ni kumuomba msamaha akaahidi kulipa dola za Kimarekani 2400.

March 2017 watayarishaji filamu wa Marekani, katika filamu moja wakaomba kutumia beat ya P-funk Majani ya ‘Nikusaidieje’. Lakini wakataka kwanza wawasiliane na muhusika wa mziki huo. Sintofahamu ikatokezea ni nani aonwe kati ya Jose Chameleon wa Bombocrat, au Profesa J wa ‘Nikusaidieje’. Baada ya Chameleone kubaini kuna ‘dili’ hilo, alikwea Pipa kwenda Marekani, akakutana na wahusika, wakasaini mkataba wa maisha, na kwamba atalipwa milele kutokana na mauzo ya filamu ile.

Jose alipewa kianzio cha malipo cha dola za Kimarekani 50,000 ambazo ni sawa na Shilingi milioni 120 za Tanzania. Jose Chameleone aliingia katika orodha ya wanamuziki walioibukia katika siasa baada ya kutangaza rasmi kuwa atawania kuwa Meya. Mayanja alitangaza nia ya kushindana na Erias Lukwago kugombea kiti hicho cha Umeya wa jiji la Kampala.

Hivi karibuni Chameleon alijiunga na Harakati ya nguvu za watu “People Power Movement”. Kundi la linaloongozwa na mwanamuziki mwenzie aliyeibukia katika siasa, Bobi Wine.

Huyu ndiye Joseph Mayanja ‘Jose Chameleone’

Kila la heri katika harakati zako za muziki na siasa.

Makala hii imeandaliwa kwa msaada mkubwa wa mitandao.
Mwandaaji anapatikana kwa namba: 0713331200, 0784331200, 0736331200 na 0767331200
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images