Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

Sanlam Tanzania ya wapeleka washindi wa mbio Capetown marathon

0
0
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Sanlam kitengo cha bima ya maisha, Khamis Suleiman (Kushoto), akizungumza na waandishi wa habari katika hafla fupi ya kuwazawadia washindi wa mashindano yalioisha hivi karibuni yaitwayo “Life is a Marathon competition” na
kuwapa fursa ya kwenda kushiriki na kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya fainali ya “Sanlam Cape Town Marathon”, katika ofisi za makao makuu ya kampuni hiyo, jiji Dar es Salaam, jana. Kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Sanlam kitengo cha bima Gift Noko.


=========   ========  ======

Kampuni ya Sanlam Tanzania imetoa zawadi kwa washindi wa mashindano yalioisha hivi karibuni yaitwayo “Life is a Marathon competition” na kuwapa fursa ya kwenda kushiriki na kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya fainali ya “Sanlam Cape Town Marathon” yatakayo fanyika tarehe 15 septemba mwaka huu. 

Washindi hao ni Jamia Abdallah na lister Lusulo Pakua. Vile Vile balozi wa Sanalam Maulid Kitenge na wateja wa Sanlam Stephen Mndeme na Innocent Shaku wamepata nafasi ya kushiriki katika mashindano hayo. 

Hatua ya kwanza ya mashindano ya “Life is a Marathon competition” yalihusisha washindani kuwasilisha picha na video zao zikionyesha jinsi watakavyo jiandaa kushiriki katika mashindano hayo, baada ya hapo washindi walichaguliwa na kupitia mazoezi mbali mbali ya kujiandaa. 

Akizungumza katika hafla ilyofanyika ofisi za Sanlam Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Mr Khamis Suleiman, aliwapongeza wachezaji kwa kujituma kwao na kuwasihi kuonyesha juhudi zaidi katika mashindano yanayokuja. 

“Tunafuraha sana kuona jinsi wachezaji hawa walivyofanya vizuri na mkiwa mnajianda kusafiri napenda kuwatia moyo mkafanye vizuri zaidi. Iwe unafanya mazoezi kwa ajili ya mashindano ya mbio au unajifunza kuendesha baiskeIi inabidi uwe na mshirika ambaye atakusaidia kufanikisha malengo yako, na hii ndio ngao yetu hapa Sanlam Tanzania, tumejikita katika kutuoa huduma na bidhaa za kidigitali ambazo zitakusaidia wewe katika hatua zote za maisha.” 

Sanlam ilizindua mashindano ya “Life marathon” tarehe 8 Agosti kwa lengo la kuonyesha umuhimu wa ushirikiano katika kuwezesha watu kufanikisha malengo yao na kuwa na maisha bora, pia ni moja ya njia ya kampuni ya Sanlam kutambua na kuwapongeza wanamichezo mbali mbali nchini Tanzania 

Ikiwa ni mashindano pekee ya marathon yenye daraja la dhahabu barani Africa, Sanlam Cape town marathon huleta pamoja zaidi ya vilabu 23 vya kimataifa na wakimbiaji takribani 15,000 kila mwaka.

WAZIRI LUGOLA ATEMBELEA MRADI WA UJENZI WA MAKAO MAKUU YA UHAMIAJI JIJINI DODOMA

0
0
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akisikiliza maelezo ya Mradi wa Ujenzi wa Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji kutoka kwa Mhandisi David Pallangyo (kulia), wakati wa ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya mradi huo leo, jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya  Ndani ya  Nchi
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akikagua Mradi wa Ujenzi wa Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji wakati wa ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya mradi huo leo, jijini Dodoma.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza baada ya Ukaguzi wa  Mradi wa Ujenzi wa Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji wakati wa ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya mradi huo leo, jijini Dodoma.Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo,Ramadhani Kailima.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akitoka kukagua Mradi wa Ujenzi wa Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji wakati wa ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya mradi huo leo, jijini Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akisalimiana na Wahandisi wa Mradi  wa Ujenzi wa Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji wakati wa ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya mradi huo leo, jijini Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya  Ndani ya  Nchi

SHERIA NDOGO YA FEDHA KUONDOA CHANGAMOTO YA RIBA KWA WADAU

0
0
Na Josephine Majura na Peter Haule, WFM, Dodoma

Serikali imeeleza kuwa Sheria ya Huduma Ndogo za fedha ya mwaka 2018 haina lengo la kuinyima jamii fursa ya kusaidiana kwa njia ya kukopeshana bali inalenga kutatua changamoto zilizopo ikiwemo ya utozaji wa riba kubwa.

Hayo yamesemwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti maalum, Mhe. Lucy Magereli, aliyetaka kujua Sheria ya udhibiti wa taasisi ndogo za fedha imetekelezwa kwa kiasi gani na Serikali haioni Sheria hiyo inainyima jamii kusaidiana.

Dkt. Kijaji alisema kuwa kutokana na changamoto za Sekta ndogo ya Fedha ikiwemo kutoza kiwango kikubwa cha riba na ukosefu wa utaratibu wa kuwalinda walaji na wadau kwa ujumla, Sheria ya  Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018 itaimarisha usimamizi na udhibiti wa sekta hiyo.

“Udhibiti wa sekta ndogo ya fedha unaakisi matarajio na mahitaji ya wadau na hivyo kuongeza kasi ya ukuaji na mchango wake katika sekta nzima ya fedha na uchumi kwa ujumla”, alieleza Dkt. Kijaji.

Alisema kuwa walengwa wa Sheria hiyo wamepewa mwaka mmoja wa mpito baada ya kanuni kutolewa ili waweze kujiandaa kulinganana matakwa ya kanuni hizo ambazo zitaanza kutumika rasmi baada ya kipindi hicho kupita.

Dkt. Kijaji alisema kuwa hadi sasa hakuna taasisi yoyote iliyosajiliwa kupitia Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2018.

Alifafanua kuwa, baada ya Sheria hiyo kutungwa, Serikali ilianza mchakato wa kuandaa kanuni za huduma hiyo zilizolenga madaraja manne ya watoa huduma yaliyoainishwa kwenye Sheria.

Mchakato huo ulihusisha ukusanyaji wa taarifa mbalimbali za walengwa ili kuweza kutengeneza kanuni zilizozingatia hali halisi ya biashara zao pamoja na matakwa ya Sheria. Aidha mchakato wa kuandaa kanuni ulikamilika na hivyo kutangazwa kwenye gazeti la Serikali namba 575 Agosti 2, 2019.

Tigo yazindua Huduma ya ‘Office Internet’ kwa wafanyabiashara wadogo na wakati Tanzania

0
0


Afisa Mkuu wa Tigo Business, Pavan Ramdhani akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya ‘Office Internet’ ikiwalenga wafanyabiashara wadogo na wa kati nchini, ambapo huduma hiyo ina mfumo wa kisasa uliounganishwa na Microsoft
Kaimu mkuu wa mauzo-Nick kazuka akifanua jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya. uzinduzi wa huduma mpya ya ‘Office Internet’ ikiwalenga wafanyabiashara wadogo na wa kati nchini, ambapo huduma hiyo ina mfumo wa kisasa uliounganishwa na Microsoft
Afisa Mkuu wa Tigo Business, Pavan Ramdhani akimkabidhi Router Mkuu wa Idara ya masoko wa Dstv Baraka Shelukindo. mara baada ya uzinduzi wa huduma mpya ya ‘Office Internet’ ikiwalenga wafanyabiashara wadogo na wa kati nchini, ambapo huduma hiyo ina mfumo wa kisasa uliounganishwa na Microsoft.Hafla hiyo ilifanyika katika Makao makuu ya ofisi za Tigo Jijini Dar es salaam.
waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini uzinduzi wa uzinduzi wa huduma mpya ya ‘Office Internet’ ikiwalenga wafanyabiashara wadogo na wa kati nchini, ambapo huduma hiyo ina mfumo wa kisasa uliounganishwa na Microsoft.Hafla hiyo ilifanyika katika Makao makuu ya ofisi za Tigo Jijini Dar es salaam.
Mtaalam bidhaa Tigo Business Brian Swai akifafanua jambo kwa wageni waalikwa uzinduzi wa huduma mpya ya ‘Office Internet’ ikiwalenga wafanyabiashara wadogo na wa kati nchini, ambapo huduma hiyo ina mfumo wa kisasa uliounganishwa na Microsoft.Hafla hiyo ilifanyika katika Makao makuu ya ofisi za Tigo Jijini Dar es salaam.


Ni huduma ya intaneti yenye kasi inayokwenda sambamba na mfumo wa kisasa wa kibiashara kutoka Microsoft


Dar es Salaam: Septemba 12, 2019, Kampuni ya simu ya Tigo, kupitia kitengo chake cha Tigo Business leo imetangaza rasmi uzinduzi wa huduma mpya ya ‘Office Internet’ ikiwalenga wafanyabiashara wadogo na wa kati nchini, ambapo huduma hiyo ina mfumo wa kisasa uliounganishwa na Microsoft . Hatua hii inazidi kuifanya Tigo kuendelea kuwa kinara wa ubunifu kuiwezesha kampuni katika kujitolea kufanya biashara zake kwa malengo.


Sambamba na uzinduzi wa huduma ya ‘Home Internet’ uliyofanywa na Tigo hivi karibuni, huduma ya ‘Office Internet’ inakuja na faida endelevu kwa wateja wenye biashara ndogo na za kati ambao hupendelea huduma za intaneti kwa mkataba. Hii inadhihirisha matumzi bora ya mtandao wa wenye kasi nchini Tanzania wa 4G+.


Afisa Mkuu wa Tigo Business, Pavan Ramdhani, aliwaambia wateja wa Tigo kuwa, kwa sasa wana uwezo wa kutoa huduma bora zinazoendana na wakati kwa kushirikiana na wataalamu wa Microsoft. “Tulifanya kazi kwa ushirikiano wa karibu sana na wateja wetu, ambapo walituonyesha maeneo matatu muhimu yenye changamoto; Muda unaotumika kuunganisha huduma ya intaneti, Kasi ya huduma hiyo na ukosefu wa maana halisi, Matumizi ya intaneti na zana zenye uhusiano na biashara. Tuna furaha kutangaza kuwa, ‘Office Internet ina huduma ya daraja la kwanza iliyounganishwa na mtandao wa Tigo 4G+, wenye watumiaji wengi duniani kote chini ya ushirikiano wa Microsoft.

Huduma hii kwa ujumla wake inatumika bila muunganisho wa waya, kwa maana ya kwamba mteja wetu anatakiwa kuwasha kifaa chake cha Modem au Router. Ofisi ya mteja inaweza kuunganisha vifaa 10 hadi 32 kwenye inteneti kwa mara moja. Microsoft 365 inaruhusu kufanya mambo mbalimbali ikiwamo utumaji wa barua pepe za kibiashara, Kutuma na kuhifadhi ujumbe katika mtandao, Matumizi ya Microsoft katika masuala yote ya kibiashara ikiwamo mikutano ya moja kwa moja mtandaoni


Kujiunga na huduma ya ‘Office Internet’ tembelea duka lolote la Tigo nchini ili kujisajili. Wateja wanaotumia huduma hii watapewa kipaumbele katika huduma kwa wateja. Kwa nyongeza, mteja anaweza pia kupiga 0711100101 au barua pepe Tigobusiness@tigo.co.tz.

KERO YA MAJI YAENDA KUWA HISTORIA MJI WA KISARAWE NA VITONGOJI VYAKE

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Kukamilika kwa mradi wa Kisarawe kutanufausha mji mzima wa kisarawe, eneo la sekta viwanda na vitongoji jirani na mji huo.

Tatizo la Maji kwa Wananchi wa Kisarawe litabaki historia baada ya mradi wa ujenzi wa Tanki la maji lenye ujazo wa lita Milion sita kukamilika.

Mradi huo uliozinduliwa na Makamu wa Rais Mama Samia Hassan Suluhu utawanufaisha wananchu wa eneo la Kisarawe na maeneo ya Viwanda.

Ujenzi wa Mradi huo unasimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) ambao umechukua takribani miezi 12 kukamilika.

Akitoa taarifa ya kukamilika kwa mradi huo ambao kwa sasa mkandarasi anaendelea na kazi ya uunganishaji wa bomba, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii DAWASA, Neli Msuya amesema kwa sasa Mkandarasi sambamba na mafundi kutoka Mamlaka hiyo wanaendelea na maunganisho ya bomba la nchi 16 kutoka Mtambo wa Ruvu juu kuelekea kwenye tanki la Kisarawe.

Amesema, maunganisho ya bom a hilo yanafanyika kwenye mradi wa Kibamba ambapo mafundi wapo katika hatua za mwisho kukamilisha.

Wakazi wa Kisarawe watanufaika na mradi huo ambapo wamekuwa na kero ya maji kwa muda mrefu na kukamilika kwake kutatatua changamoto hiyo pamoja na kuvutia wawekezaji kwenda kuwekeza kwenye maeneo ya viwanda.

Mradi wa Kisarawe unajengwa kwa fedha za ndani za Mamlaka ya Majisafi na Majitaka DAWASA na unagharimu takribani Bilioni 10 za kitanzania.

TULIA TRADITIONAL DANCES FESTIVAL KURINDIMA SEPTEMBA 26 HADI 28 TUKUYU, MBEYA

0
0
*Kila mshiriki kunufaika na mashindano hayo ikiwemo kupata nafasi ya masomo katika chuo cha sanaa Bagamoyo (TASUBA)

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

MASHINDANO ya ngoma za asili yanayojumuisha vikundi mbalimbali kutoka Mikoa ya Tanzania bara na visiwani yajulikanayo Kama "Tulia Traditional Dances Festival" kwa mwaka huu yanatarajiwa kutimua vumbi kuanzia Septemba 26 hadi 28 mwaka huu huko Tukuyu jijini Mbeya.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam balozi wa mashindano hayo na mwigizaji wa filamu nchini Yvonne Cherry maarufu kama Monalisa amesema kuwa kwa mwaka huu vikundi vilivyoomba kushiriki vimekuwa vingi zaidi ukilinganisha na mwaka jana ambapo vikundi 108 kutoka Tanzania bara na visiwani vitashindana.

"Kuna vikundi vinatoka Mikoa ya Dodoma,  Kigoma, Kilimanjaro, Tanga, Kagera, Mwanza, Mtwara, Njombe, Lindi, Dar es Salaam na Songwe na watazamaji zaidi ya 1500 wanakadiriwa kushuhudia ngoma hizi na kubwa zaidi kwa mwaka huu kipengele cha chakula cha asili kimeongezwa ambapo kila kikundi kishiriki kitakuja na akina Mama wawili ambao watapika vyakula vya asili ili wahudhuriaji  wapate kufahamu vyakula vyetu vya asili na kuuenzi utamaduni wetu" ameeleza Monalisa.

Kuhusiana na zawadi zitakazotolewa kwa washindi hao Dotto Bernad Bwakeya maarufu kama Ditto amesema kuwa, watakaoshiriki katika mashindano hayo wote ni washindi na watapewa zawadi ili kupongezwa kwa juhudi zao;

"Mshindi wa kwanza atakayeibuka kidedea atazawadiwa pikipiki 22 yaani pikipiki moja kwa kila mwanakikundi, mshindi wa pili atapata fedha taslimu shilingi milioni moja kwa kila mwanakikundi, mshindi wa tatu atapata shilingi laki saba kwa kila mwanakikundi na kila siku kikundi kilichoshiriki kitapata fedha taslimu shilingi laki nne na hiyo ni pamoja na baadhi ya washindi kupata nafasi ya masomo katika chuo cha sanaa Bagamoyo" ameeleza Ditto.

Amesema kuwa kwa mwaka huu nafasi 40 zimetengwa ambapo baadhi ya washindi watadhaminiwa kusoma cha sanaa (TASUBA) kilichopo Bagamoyo na kusoma kozi fupi na wenye vigezo watadhaminiwa kusoma ngazi za cheti na Astashahada ili wakimaliza wajitengenezee nafasi na fursa kwao na kwa vijana wengine.

Mwasiti Almas nyota wa muziki wa Bongo Fleva amesema kuwa; kwa mwaka huu taasisi ya Tulia Trust imeshirikiana na ubalozi wa China ili kufanikisha tamasha hilo pekee linaloendeshwa nchini ambapo ubalozi wa China umetoa pikipiki 22 zitakazotolewa kwa washindi wa kwanza kwenye tamasha hilo.

Taasisi ya Tulia Trust iliyo chini ya Naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania  Dkt. Tulia Ackson ilianzishwa mwaka 2015 ikiwa na malengo ya kuwasaidia watu watu walio hatarini hasa akina mama, walemavu, wazee pamoja na kupambana na magonjwa na umaskini.
 Mabalozi wa mashindano ya ngoma za asili yajulikanayo kama "Tulia Traditional Dances Festival" wakiwa wameshika fulana maalumu iliyobeba dhima ya mashindano hayo, kulia ni Yvonne Cherry (Monalisa,) Mwasiti Almas (kushoto) na katikati  Dotto Bernad Bwakeya (Lameck Ditto.) Leo jijini Dar es Salaam.
 Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva Dotto Bernad Bwakeya maarufu kama Ditto (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mashindano hayo ambapo amesema kuwa washiriki wote ni washindi na zawadi watakazopewa ni pongezi kutokana na juhudi zao, leo jijini Dar es Salaam.
 Msanii wa muziki wa Kizazi kipya Mwasiti Almas akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mashindano hayo na kueleza kuwa taasisi hiyo na ubalozi wa China umeshirikiana kwa ukaribu zaidi katika kufanikisha malengo ya mashindano hayo, leo jijiji Dar es Salaam.
Yvonne Cherry maarufu kama Monalisa (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mashindano hayo ya ngoma za asili yanayotarajiwa kufanyika mapema mwezi huu ambapo amesema kuwa zaidi ya watazamaji 1500 wanakadiriwa kushuhudia mashindano hayo, leo jijini Dar es Salaam.

WASANII KUTOKA INDIA KUJA KUREKODI FILAMU NA MUZIKI NCHINI

0
0

BODI ya Utalii nchini imeendelea na jitihada zake za kuhakikisha sekta ya utalii inakua na kuchangia uchumi wa taifa ambapo sasa wanaenda kutekeleza mkakati wa kutumia muziki na filamu kwa kuwatumia watayarishaji na wacheza filamu kutoka kampuni maarufu ya kutengeneza filamu ya 3rd Rock Multimedia ya nchini India inayotengeneza filamu za Bollywood ambao watakuja nchini  kutengeneza video na filamu za wasanii wa India katika mazingira ya Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati akiwapokea wageni hao mwenyekiti wa bodi ya utalii jaji Thomas Mihayo amesema kuwa wageni hao wamekuja kuangalia maeneo ya kupiga picha na kurekodi video ambayo watakuja kuyafanyia kazi mwezi Agosti mwaka huu na kueleza kuwa kampeni hiyo imelenga kuvuna watalii wengi katika soko la India ambalo ni miongoni mwa masoko muhimu sana nchini huku mikakati ya kuhakikisha watalii wengi zaidi wanazidi kumiminika nchini utazidi kusimamiwa.

Amesema kuwa ujio wa mtayarishaji wa filamu Raj Suri Harvinder Sigh na mmiliki na mwongozaji video kutoka kampuni ya 3rd Rock Multimedia Amandeep Sighn ni fursa kubwa hasa kwa kutangaza mandhari na vivutio vya Tanzania kupitia filamu za Boolywood, hivyo ni vyema wasanii wa Tanzania wakatumia vyema fursa hiyo katika kujitangaza.

Jaji Mihayo amesema kuwa mkakati huo utaendelea kuitangaza nchi na vivutio vilivyomo katika soko la India kwa kuonesha filamu na picha katika televisheni na mitandao yao ya kijamii itasaidia kutangaza utalii wa Tanzania.

Amandeep Sighn ameeleza kufurahishwa na mazingira ya Tanzania na kusema kuwa yanafaa katika kazi zao. Amesema kuwa mwezi Oktoba watakuja wasanii 40 kutoka India ambao watajumuisha wanamuziki na waigizaji ili waweze kupata kitu tofauti na kuutangazia ulimwengu vivutio vinavyopatikana Tanzania.

WAZIRI MKUU AIAGIZA WIZARA YA MAMBO YA NJE IFUATILIE FEDHA ZA MIRADI NANE

0
0
*Ataka Watanzania wachangamkie soko la nafaka nchi za SADC

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ifuatilie kwa karibu miradi nane iliyowasilishwa na kuombewa fedha za ufadhili kupitia mkutano wa saba wa TICAD uliofanyika Agosti 28-30, 2019 jijini Yokohama, Japan.

“Kupitia Mkutano wa Saba wa Kimataifa wa Tokyo Kuhusu Maendeleo ya Afrika (TICAD 7), Serikali ya Japan imetenga kiasi cha dola za Marekani bilioni 20 kwa kipindi cha miaka mitatu kwa ajili ya nchi za Afrika. Ninaielekeza Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ishirikiane kwa karibu na Wizara zenye dhamana kuratibu vema utekelezaji wa miradi nane ya maendeleo ambayo tayari imewasilishwa kupitia TICAD 7,” amesema.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, Septemba 13, 2019) katika hotuba yake aliyoitoa wakati wa kuahirisha Mkutano wa 16 wa Bunge jijini Dodoma. Bunge limeahirishwa hadi Novemba 5, mwaka huu.

Amesema fedha hizo zimetengwa ili kuziwezesha nchi za Afrika zitekeleze miradi ya kimkakati ya maendeleo itakayoleta mageuzi ya kiuchumi. “Kiasi hicho kitatolewa ili kuendeleza miradi mbalimbali katika sekta za elimu, afya, kilimo, maji, nishati, ujenzi wa maeneo maalumu ya viwanda na miundombinu ya usafiri na usafirishaji.”

Amesema lengo la Serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha Tanzania inanufaika na fedha hizo zilizotengwa na Serikali ya Japan ili iweze kufikia uchumi wa kati unaoongozwa na viwanda ifikapo mwaka 2025.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka Watanzania watumie fursa ya upungufu wa nafaka katika nchi za Kusini mwa Afrika kwa kuzalisha zaidi mazao hayo ikiwa ni pamoja na kujiwekea akiba zaidi.

Amesema hali ya usalama wa chakula katika ukanda wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), imetetereka kutokana na athari mbalimbali ikiwemo ukame katika upande wa magharibi wa ukanda, mvua zilizokithiri, mafuriko na vimbunga vya IDAI na Kenneth pamoja na wadudu waharibifu wa mazao na magonjwa.

“Athari hizo zimesababisha uzalishaji wa nafaka kama mahindi, mtama, mpunga, ngano na ulezi ndani ya SADC upungue kwa asilimia 14 kutoka tani milioni 42.6 mwaka 2018 hadi tani milioni 36.8 mwaka 2019. Hata hivyo, Tanzania na Afrika Kusini kwa kipindi hicho zilizalisha ziada ya mazao hayo ambayo yanakadiriwa kukidhi mahitaji kwa mwaka 2019/2020,” amesema.

Waziri Mkuu amesema kuwa Agosti 29-30, mwaka huu, Wizara ya Kilimo iliratibu mkutano na wadau mbalimbali wenye kujihusisha na uzalishaji na biashara ya nafaka ili kujadili fursa zilizopo katika mazao ya nafaka, changamoto wanazokabiliana nazo na kutafuta utatuzi wake.

“Ninaigiza Wizara husika ihakikishe inashirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ili kutumia vema fursa ya uwepo wa masoko ya nafaka kwenye ukanda huu wa SADC na hivyo, kukidhi mahitaji katika ukanda sambamba na kuboresha biashara na maisha ya wananchi wa vijijini,” amesema.

Pia ameitaka wizara hiyo iendelee kuhamasisha uzalishaji wa mazao hayo kwa wingi ili nchi iweze kujitosheleza kwa chakula na kuwa na ziada.
 Spika wa Bunge Job Ndugai akiongozwa kutoka kwenye ukumbi wa Bunge baada ya kuahirisha Mkutano wa 16 wa Bunge la 11, jijini Dodoma, Septemba 13, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisoma hotuba yake ya kuahirisha Mkutano wa 16 wa Bunge la 11 ,  Bungeni jijini Dodoma, Septemba 13, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Viti Maalum, Bernadeta Mushashu, Bungeni jijini Dodoma, Septemba 13, 2019.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Kuteuliwa, Janeth Masaburi kwenye jengo la utawala la Bunge jijini Dodoma, Septemba 13, 2019.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na wabunge, Bungeni jiini Dodoma, Septemba 13, 2019. Kutoka kushoto ni Naibu Waziri , Ofisi ya Rais TAMISEMI na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara, Waziri wa Madini na Mbunge wa Bukombe, Doto Biteko, Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Msukuma na wa pili kulia ni Waziri wa Nishati na Mbunge wa Chato, Dkt.  Medard Kalemani.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akielekekea kwenye eneo la kusomea hotuba yake ya kuahirisha Mkutano wa 16 wa Bunge la 11, Bungeni jijini Dodoma, Septemba 13, 2019.




SERIKALI YATOA ONYO UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

0
0
*Yawataka wadau wajiepusha na vitendo vya rushwa, uvunjifu wa amani

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wadau watakaoshiriki katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa wahakikishe wanajiepusha na vitendo vya rushwa na uvunjifu wa amani kwani Serikali haitasita kuchukua hatua pale itakapothibitika vitendo hivyo kufanyika.

Waziri Mkuu amesema wadau hao mbalimbali kutoka katika Vyama vya Siasa, Taasisi za Serikali na Zisizo za Serikali na wananchi ni vema wakahakikisha wanasoma na kuelewa kanuni na miongozo ya uchaguzi huo ili waweze kushiriki ipasavyo.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Ijumaa, Septemba 13, 2019) , wakati akiahirisha mkutano wa 16 wa Bunge la 11, Bungeni jijini Dodoma. Waziri Mkuu amewataka Watanzania wote wenye sifa washiriki uchaguzi huo kwani ni haki yao ya msingi.

“Natoa wito kwa Watanzania wote wenye sifa wajiandikishe katika orodha ya wapiga kura, wachukue fomu za kugombea nafasi mbalimbali na kushiriki kupiga kura kwani hiyo ni haki yao ya kikatiba kwa kuzingatia misingi ya demokrasia.”

Mbali na wadau hao, pia, Waziri Mkuu amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama vishiriki kikamilifu katika kuhakikisha wananchi wanafanya uchaguzi kwenye mazingira ya amani na utulivu bila kubugudhiwa.

Waziri Mkuu amewataka Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa uchaguzi huo wahakikishe wanazielewa kanuni na miongozo ilitoyotolewa ili waweze kutoa tafsiri sahihi wakati wa kusimamia uchaguzi huo.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewahimiza Wakuu wa Mikoa na Wilaya waratibu vizuri shughuli za uchaguzi kwenye maeneo yao na wahakikishe uwepo wa ulinzi na usalama wakati wote wa uchaguzi hasa kipindi cha kampeni na wakati wa kupiga kura.

Waziri Mkuu amewasihi wabunge na madiwani wawahamasishe wananchi ili watumie haki yao ya kidemokrasia ya kuchagua na kuchaguliwa. “Natoa rai kwenu mhakikishe mnashiriki kikamilifu katika shughuli zote za uchaguzi huo.”

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unatarajiwa kufanyika tarehe 24 Novemba 2019. Uchaguzi huo unafanyika kila baada ya miaka mitano kwa lengo la kukidhi matakwa ya Ibara ya 8 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, inayoelekeza kuwa Mamlaka na Madaraka ya Serikali yanatokana na wananchi.

Kuhusu uboreshaji wa daftari la wapiga kura, Waziri Mkuu amesema tarehe 18 Julai 2019 Serikali ilizindua zoezi hilo mkoani Kilimanjaro na kuongeza kuwa uboreshaji huo, unahusisha wapiga kura waliotimiza umri wa miaka 18 na wale watakaotimiza umri huo wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020.

“Makundi mengine yatakayohusika ni wapiga kura waliohamia katika kata au jimbo jingine la uchaguzi, waliopoteza kadi au kuharibika, wanaohitaji kurekebisha taarifa zao; mfano majina ambayo hapo awali yalikuwa yamekosewa pamoja na kuwaondoa wapiga kura waliopoteza sifa kama vile kufariki dunia.”

Amesema kwa sasa zoezi hilo tayari limekamilika katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Simiyu, Mara na Mwanza (isipokuwa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba). Zoezi hilo linaendelea kutekelezwa chini ya kaulimbiu isemayo Kadi Yako, Kura Yako, Nenda Kajiandikishe.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisoma hotuba yake ya kuahirisha Mkutano wa 16 wa Bunge la 11 ,  Bungeni jijini Dodoma, Septemba 13, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WALIOZEMBEA AJALI YA MOTO WACHUKULIWE HATUA-MAJALIWA

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezielekeza mamlaka husika ziwachukulie hatua za kinidhamu watu wote ambao hawakutekeleza majukumu yao ipasavyo kufuatia tukio la ajali ya moto iliyotokea Agosti 11, 2019 mkoani Morogoro na kusababisha vifo vya watu 104, majeruhi pamoja na uharibifu wa mali.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Ijumaa, Septemba 13, 2019) , wakati akiahirisha mkutano wa 16 wa Bunge la 11, Bungeni jijini Dodoma. Bunge limeahirishwa hadi tarehe 3, Novemba mwaka huu.

“Baada ya tukio hilo la kusikitisha tarehe 12 Agosti 2019niliunda Kamati Maalumu kwa lengo la kufanya uchunguzi wa kina kuhusu ajali hiyo iliyosababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa mali.”

“Lengo lilikuwa kufahamu chanzo cha ajali, mazingira baada ya ajali na hatua gani zichukuliwe kuzuia matukio kama haya sambamba na kuwawajibisha wale wote ambao hawakutekeleza wajibu wao ipasavyo kabla na baada ya ajali kutokea.”

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwashukurumadaktari na wahudumu wa Hospitali ya Rufaa ya Morogoro na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili nawadau wote ambao walishiriki kuokoa maisha ya waathirika wa ajali hiyo tangu ilipotokea.

“Nawasihi Watanzania wenzangu tujifunze kutokana na ajali hiyo iliyotokea Morogoro na hivyo kuepuka mikusanyiko ya aina hiyo katika maeneo ya ajali. Aidha, tujenge nyoyo za huruma na kuwa wepesi wa kutoa msaada kwa waathirika wa ajali badala ya kutumia kama fursa za kujinufaisha isivyo halali.” 

Makatibu Wakuu Watembelea Uwanja Wa Taifa Kuona Maandilizi Kuelekea Tamasha la JAMAFEST

0
0
Mwenyekiti wa Kamati ya maandlizi ya Tamasha la nne la Utamaduni wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST), Joyce Fisoo akifafanua jambo kwa wajumbe wa kikao cha Makatibu Wakuu cha kupitia taarifa ya maandalizi ya tamasha hilo mapema hii leo Septemba, 13 jijini Dar es Salaam, tamasha hilo linatarajia kufanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 21 hadi 28, Septemba 2019.
Makatibu Wakuu na wajumbe wakiendelea na kikao cha kupitia taarifa ya maandalizi ya Tamasha la nne la Utamaduni wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) linalotarajia kufanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 21 hadi 28, Septemba 2019.





Katibu Mkuu wa Wizara Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Susan Mlawi akifafanua jambo kwa wajumbe wa kikao cha Makatibu Wakuu cha kupitia taarifa ya maandalizi ya Tamasha la nne la Utamaduni wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) linalotarajia kufanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 21 hadi 28, Septemba 2019.
Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza (katikati) akifafanua jambo kwa wajumbe wa kikao cha Makatibu Wakuu cha kupitia taarifa ya maandalizi ya Tamasha la nne la Utamaduni wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) mapema hii leo Septemba, 13 jijini Dar es Salaam, tamasha hilo linatarajia kufanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 21 hadi 28, Septemba 2019.
Katibu Mkuu wa Wizara Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Susan Mlawi akiwaongoza Makatibu Wakuu na baadhi ya viongozi kutembelea baadhi ya miundombinu itakayotumika katika Tamasha la nne la Utamaduni wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) linalotarajia kufanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 21 hadi 28, Septemba 2019.
Katibu Mkuu wa Wizara Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Susan Mlawi akiwaelekeza Makatibu Wakuu na baadhi ya viongozi baadhi ya miundombinu itakayotumika katika Tamasha la nne la Utamaduni wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) linalotarajia kufanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 21 hadi 28, Septemba 2019.

Katibu Mkuu wa Wizara Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Susan Mlawi (katikati) akiwaongoza Makatibu Wakuu na baadhi ya viongozi kutembelea baadhi ya miundombinu itakayotumika katika Tamasha la nne la Utamaduni wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) linalotarajia kufanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 21 hadi 28, Septemba 2019.
Meneia wa Uwanja wa Taifa, Nsajigwa Gordon akitoa maelekezo kwa Makatibu Wakuu na baadhi ya viongozi juu ya nyasi bandia katika uwanja wa Uhuru wakati Makatibu Wakuu hao walipokwenda kutembelea baadhi ya miundombinu itakayotumika katika Tamasha la nne la Utamaduni wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) linalotarajia kufanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 21 hadi 28, Septemba 2019.
Moja ya eneo litakalotumika katika Tamasha la nne la Utamaduni wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST), linalotarajia kufanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 21 hadi 28, Septemba 2019.Picha na WHUSM – Dar es Salaam

SERIKALI KUONGEZAWATUMISHI TRA KWA HATUA ILI KUENDELEZA UFANISI

0
0
Farida Ramadhani, WFM, Dodoma
Serikali imeeleza kuwa ili Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) iweze kufanya kazi zake kwa ufanisi inahitaji watumishi takribani 7000 wa kada mbalimbali za kiutumishi.
Hayo yamebainishwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Tunza Malapo, aliyetaka kujua ni watumishi wangapi wanahitajika na TRA ili iweze kufanya kazi kwa ufanisi.
Dkt. Kijaji alisema kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania haina upungufu mkubwa kama inavyoelezwa, kwa kuwa idadi ya watumishi wa TRA walioajiriwa ni 4,751 kati ya 7000 wanaohitajika hivyo kufanya upungufu kuwa asilimia 28 tu.
Alisema jitihada za kukamilisha idadi ya watumishi wa Mamlaka hiyo kufikia 7000 zinafanywa kwa hatua, lengo likiwa kuongeza ufanisi wa kiundendaji na kuendelea kuleta matokeo chanya katika maendeleo ya nchi.
Alifafanua kuwa tangu Serikali ya Awamu ya Tano imeingia madarakani imejitahidi kwa kiwango kikubwa kukabiliana na suala hilo, tayari imeajiri watumishi 692 na katika mwaka wa fedha 2019/20 Mamlaka hiyo imeweka Bajeti ya kuajiri watumishi takribani 150.

ECLAT FOUNDATION LATUMIA BILIONI 6 KWA MIRADI YA JAMII

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, mhandisi Zephania Chaula watatu kushoto na viongozi wa shirika la ECLAT Foundation na Upendo Society wakipongezana baada ya uzinduzi wa shule ya msingi Kimelok Kijiji cha Kimotorok Kata ya Loiborsiret.
Mkuu wa wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, mhandisi Zephani Chaula (katikati) akikagua miundomnbinu ya shule ya msingi Kimelok ambayo majengo yamejengwa na kukarabatiwa na shirika la ECLAT Foundation.
Wanafunzi na wazazi wa shule ya msingi Kimelok Kijiji cha Kimotorok Kata ya Loiborsiret Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakishuhudia makabidhiano ya miundombinu ya shule yao ambapo shirika la ECLAT Foundation lilitumia shilingi milioni 267 kujenga na kukarabati kisha kuikabidhi serikali.
…………………..
Na.Joseph Lyimo,Simanjiro

SHIRIKA lisilo la kiserikali la ECLAT Foundation la Emboreet Wilayani Simanjiro, limetumia shilingi bilioni 6 katika kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo kwa jamii kwenye mikoa ya Manyara, Arusha, Mtwara na Kigoma. 

Mwenyekiti wa ECLAT Foundation, Peter Toima aliyasema hayo wakati akiikabidhi serikali miundombinu ya shule ya msingi Kimelok ya kijiji cha Kimotorok kata ya Loiborsiret kwa mkuu wa wilaya ya Simanjiro Mhandisi Zephania Chaula. 

Toima alikabidhi madarasa mapya na mengineyo yaliyokarabitiwa, nyumba mpya ya walimu na matundu 32 ya vyoo ambayo yamesababisha shule hiyo kuwa na muonekano mpya kwa gharama ya sh267 milioni. 

Alisema katika kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi, ECLAT Foundation na shirika la Upendo la Ujerumani wamefanya hayo kuisaidia serikali kwenye mikoa tofauti nchini. 

Alisema wamefanikisha miradi ya maendeleo ya elimu, maji na kuwezesha kiuchumi miradi ya vikundi, kwa kutumia fedha hizo kwa ushirikiano mkubwa wa shirika la Upendo la Ujerumani. 

“Tumefanya haya kwenye maeneo mbalimbali nchini ikiwemo wilaya za Simanjiro Manyara, Monduli na Ngorongoro Arusha, Kakonko Kigoma na Tandahimba mkoani Mtwara,” alisema Toima. 

Ofisa miradi wa ECLAT Foundation, Bakiri Angalia alisema kwa siku tatu mfululizo wataikabidhi serikali shule ya msingi Kimelok, shule ya msingi Nadoilchukini na Lengijape ya Lorkisalie ambazo wamejenga miundombinu au kukarabati. 

Mkuu wa wilaya ya Simanjiro, Zephania Chaula aliipongeza ECLAT Foundation kwa kufanikisha ujenzi wa miundombinu wa shule hiyo ya Kimelok ya Kimotorok. 

“Tunawapongeza ECLAT Foundation na Upendo, sisi hatuna ubaguzi wa shirika lolote lile kwa hiyo mashirika mengine tunawakaribisha mlete maendeleo kwenye wilaya yetu ya Simanjiro,” alisema Chaula. 

Mkazi wa kijiji cha Kimotorok, Namnyaki Isaya alisema hatua ya shirika la ECLAT Foundation ni kubwa katika kufanikisha mwanga wa elimu kwa wananchi wa wilaya ya Simanjiro. 

Alisema mashirika kama hayo ndiyo yanatakiwa kuungwa mkono kwani yanajitoa kuhakikisha kuwa wananchi wanapata maendeleo kupitia miradi kama hiyo. 

WAZIRI WA KILIMO MHE JAPHET HASUNGA AICHARUKIA TUME YA TAIFA YA UMWAGILIAJI ATOA MAAGIZO MAZITO

0
0
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji katika ukumbi wa ofisi ndogo za wizara ya kilimo Jijini Dodoma, leo tarehe 13 Septemba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji katika ukumbi wa ofisi ndogo za wizara ya kilimo Jijini Dodoma, leo tarehe 13 Septemba 2019.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akizungumza wakati wakati wa kikao kazi kilichoitishwa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga kukutana na watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji katika ukumbi wa ofisi ndogo za wizara ya kilimo Jijini Dodoma, leo tarehe 13 Septemba 2019. 


Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameipa wiki moja Tume ya Taifa ya umwagiliaji kutengeneza mikakati ya kutengeneza mabwawa ya kukinga maji ya mvua ili kuwasaidia wakulima kuwezesha kilimo cha umwagiliaji kukua.

Mhe Hasunga ameyasema leo tarehe 13 Septemba 2019 katika ukumbi wa ofisi ndogo za wizara ya kilimo Jijini Dodoma alipokuwa akizungumza kwenye kikao kazi na watumishi wa Tume huyo. 

Waziri Hasunga amesema kuwa wizara hiyo ina matarajio ya kutumia fursa ya mradi mradi wa umeme wa maporomoko ya maji ya Mto Rufiji (RHPP) utakaozalisha megawati 2115, kea ajili ya kilimo cha umwagiliaji ambapo inatajwa kuwa kuna zaidi ya Hecta 150,000 zinazofaa kea ajili ya umwagiliaji.

Mhe Hasunga amewataka watendaji hao wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kuhakikisha kuwa wanampatia mipango na mkakati wa namna gani baada ya umeme kuzalishwa katika eneo lile, yale maji yatatumika yote katika umwagiliaji na hecta zote zile zianze uzalishaji.

‘’Ninawapa wiki moja hakuna muda mwingine wa kufanya hivyo kwa sababu niliwapa mienzi minne hamjafanya hivyo’’ Alisema Mhe Hasunga.Aidha, Waziri Hasunga ametoa siku tatu kumpatia taarifa za utendaji kazi wa miradi ya umwagiliaji katika mikoa minne yaani Tabora, Katavi, Rukwa, na Songwe iwapo kuna miradi inayofanya kazi na isiyofanya kazi. 

Kilimo cha umwagiliaji kimekuwa kikisisitizwa na serikali kwani ni kilimo kisichotegemea mvua hivyo kuwa na matarajio ya kuvuna mazao kwa wingi.

Umwagiliaji ni mtindo wa kilimo wa kupeleka maji kwa mimea shambani pasipo mvua ya kutosha, hutumiwa katika maeneo yabisi au wakati mvua ni kidogo. Katika nchi baridi unatumiwa pia kwa kusudi la kulinda mazao dhidi ya jalidi.

Ni kilimo ambacho kinasaidia sana, kwa mfano nchi ya Misri tangu zamani inategemea mto Naili katika shughuli zake za umwagiliaji wa mazao.

HOTUBA YA WAZIRI MKUU YA KUAHIRISHA MKUTANO WA 16 WA BUNGE LEO JIJINI DODOMA

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisoma hotuba yake ya kuahirisha Mkutano wa 16 wa Bunge la 11 , Bungeni jijini Dodoma, Septemba 13, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akielekekea kenye eneo la kusomea hotuba yake ya kuahirisha Mkutano wa 16 wa Bunge la 11, Bungeni jijini Dodoma, Septemba 13, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wabunge, Bungeni jiini Dodoma, Septemba 13, 2019. Kutoka kushoto ni Naibu Waziri , Ofisi ya Rais TAMISEMI na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara, Waziri wa Madini na Mbunge wa Bukombe, Doto Biteko, Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Msukuma na wa pili kulia ni Waziri wa Nishati na Mbunge wa Chato, Dkt. Medard Kalemani
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Kuteuliwa, Janeth Masaburi kwenye jengo la utawala la Bunge jijini Dodoma, Septemba 13, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Viti Maalum, Bernadeta Mushashu, Bungeni jijini Dodoma, Septemba 13, 2019
Spika wa Bunge Job Ndugai akiongozwa kutoka kwenye ukumbi wa Bunge baada ya kuahirisha Mkutano wa 16 wa Bunge la 11, jijini Dodoma, Septemba 13, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

……………….
Shukrani
  • Mheshimiwa Spika, awali ya yote hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutujalia afya njema na kutuwezesha kuhitimisha shughuli zote zilizopangwa kwenye mkutano huu wa 16 wa Bunge lako tukufu.
  • Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kuendelea kuliongoza Bunge hili tukufu kwa umahiri mkubwa, ukisaidiwa na Mheshimiwa Naibu Spika na Waheshimiwa Wenyeviti wa Bunge. Aidha, niwashukuru sana Wenyeviti na Wajumbe wa Kamati zote za Kudumu za Bunge kwa kazi nzuri waliyoifanya ya kupokea na kuchambua taarifa, Maazimio na Miswada mbalimbali iliyowasilishwa kwenye Kamati hizo.
  • Mheshimiwa Spika, nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipowashukuru Waheshimiwa Wabunge wenzangu kwa michango mizuri mliyoitoa wakati wa mijadala ya hoja mbalimbali zilizowasilishwa na Serikali kwenye Mkutano huu ambayo ninaamini itasaidia sana kuboresha utekelezaji wa mipango ya Serikali. 
Salamu za Pole
  • Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii kuwapa pole Watanzania wenzangu waliopoteza ndugu, jamaa na marafiki na wengine kupata ulemavu kutokana na ajali ya lori la mafuta iliyotokea tarehe 10 Agosti 2019 mjini Morogoro na kupoteza maisha ya watu 104. Tunamuomba Mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi na awape nafuu majeruhi wapone haraka.
  • Mheshimiwa Spika, baada ya tukio hilo la kusikitisha tarehe 12 Agosti 2019 niliunda Kamati Maalumu kwa lengo la kufanya uchunguzi wa kina kuhusu ajali hiyo iliyosababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa mali. Lengo lilikuwa kufahamu chanzo cha ajali, mazingira baada ya ajali na hatua gani zichukuliwe kuzuia matukio kama haya sambamba na kuwawajibisha wale wote ambao hawakutekeleza wajibu wao ipasavyo kabla na baada ya ajali kutokea. Tayari kamati hiyo imekamilisha majukumu yake na mamlaka husika zimeelekezwa kuchukua hatua za kinidhamu kwa wale wote ambao hawakutekeleza majukumu yao ipasavyo.
  • Mheshimiwa Spika, niwashukuru madaktari na wahudumu wa Hospitali ya Rufaa ya Morogoro na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na wadu wote ambao walishiriki katika kuokoa maisha ya wahanga wa ajali hiyo tangu ilipotokea. Nawasihi Watanzania wenzangu kujifunza kutokana na ajali hiyo iliyotokea Morogoro na hivyo kuepuka mikusanyiko ya aina hiyo katika maeneo ya ajali. Aidha, tujenge nyoyo za huruma na kuwa wepesi wa kutoa msaada kwa wahanga wa ajali badala ya kutumia ajali hizo kama fursa za kujinufaisha isivyo halali. 
  • Mheshimiwa Spika, natumia fursa hii kutoa pole kwa familia, ndugu na jamaa wa marehemu Mohammed Dahman, mwanahabari nguli wa Idhaa ya Kiswahili ya Ujerumani (DW) aliyekuwa Balozi mzuri wa lugha ya Kiswahili ambaye alifariki tarehe 02 Agosti 2019 huko Ujerumani. Aidha, natoa pole kwa familia ya marehemu Ibrahimu Kaduma aliyefariki tarehe 31 Agosti 2019 huko nchini India alikokwenda kwa ajili ya matibabu. Marehemu Kaduma aliyekuwa mfuasi mkubwa wa falsafa za Mwalimu Julius Nyerere hasa za ujamaa na kujitegemea, atakumbukwa pia kwa kuitumikia nchi yetu katika nyadhifa mbalimbali ikiwemo uwaziri wa Mambo ya Nje. 
  • Mheshimiwa Spika, nitoe pole pia kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kutokana na kifo cha Dkt. Omary Nundu, aliyewahi kuwa Waziri wa Uchukuzi na Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel, kilichotokea tarehe 11 Septemba 2019. Kadhalika, nitoe pole kwa wadau wa michezo kwa kuondokewa na Bw. Ramadhan Nasib, aliyewahi kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) tarehe 29 Agosti 2019 na pia kwa kuondokewa na shabiki wa Taifa Stars Bw. Christopher Rupia, ambaye alipoteza uhai wakati alipokwenda kuishuhudia na kuiunga mkono Taifa Stars ikicheza dhidi ya Burundi tarehe 8 Septemba 2019. Mungu aziweke roho za marehemu mahala pema. Amina!
  • Mheshimiwa Spika, tarehe 6 Septemba 2019, Tanzania ilipokea kwa mshtuko mkubwa kifo cha Rais Mstaafu na Baba wa Taifa la Zimbabwe Mheshimiwa Robert Gabriel Mugabe kilichotokea huko Singapore alikokwenda kwa ajili ya matibabu. Nami niungane na Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoa salamu za pole kwa Mheshimiwa Emmerson Mnangagwa, Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe, Familia ya Mzee Robert Gabriel Mugabe, Wananchi wa Zimbabwe, Waafrika na wale wote walioguswa na msiba huu.
  • Mheshimiwa Spika, nyote mtakubaliana nami kuwa Mzee Robert Gabriel Mugabe, alikuwa ni miongoni mwa viongozi jasiri, shupavu na mwanamajumui wa Afrika (yaani Pan Africanist) aliyekataa ukoloni kwa vitendo. Tanzania tutaendelea kumkumbuka sana Mzee Mugabe kwa mchango wake mkubwa katika kuhakikisha Mwalimu Nyerere anaenziwa ipasavyo na Umoja wa Afrika, kutokana na mchango wake kwenye harakati za ukombozi na kujenga mtangamano wa Waafrika.
  • Mheshimiwa Spika, itoshe tu kusema kwamba Mzee Mugabe alimheshimu sana Mwalimu Nyerere hata kufikia hatua ya kuandika kitabu mwaka 2015 kiitwacho “Julius Nyerere, Ahsante sana, Thank You Mwalimu”. Kitabu hicho kimebeba simulizi nyingi kuhusu Mwalimu Nyerere na Tanzania. Tuendelee kumuomba Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahala pema. Amina!
Pongezi
  • Mheshimiwa Spika, naomba niungane na Waheshimiwa Wabunge wenzangu kumpongeza Mheshimiwa Miraji Jumanne Mtaturu, Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, kwa kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo hilo kufuatia uchaguzi mdogo uliofanyika hivi karibuni ambapo alipita bila kupingwa, karibu sana sisi Wabunge tunakuhakikishia kukupa ushirikiano katika kuwatumikia Watanzania wenzetu. 
SHUGHULI ZA BUNGE
Maswali na Majibu
  • Mheshimiwa Spika, wakati wa Mkutano huu, Waheshimiwa Wabunge wamepata fursa ya kuuliza maswali ya msingi 123 na maswali 217 ya nyongeza ambayo yalijibiwa na Serikali. Pia, maswali 6 ya Papo kwa Papo yaliulizwa na kujibiwa na Waziri Mkuu.
Miswada ya Sheria
  • Mheshimiwa Spika, kwa upande mwingine, Waheshimiwa Wabunge walipata fursa ya kujadili na kupitisha Miswada minne iliyowasilishwa na Serikali katika Mkutano huu. Miswada ya Sheria iliyojadiliwa na kupitishwa na Bunge lako tukufu katika Mkutano huu ni kama ifuatavyo:
  1. Muswada wa Sheria ya Serikali Mtandao wa Mwaka 2019;
  1. Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na.4) wa Mwaka 2019;
  1. Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na.5) wa Mwaka 2019; na
  1. Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na.6) wa Mwaka 2019.
Maazimio ya Bunge
  • Mheshimiwa Spika, kupitia Mkutano huu, Bunge lako tukufu lilijadili na kuridhia maazimio nane kama ifuatavyo:
  1. Azimio la Kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa SADC na kuendesha vyema Mkutano wa 39 wa Jumuiya hiyo uliofanyika Dar es Salaam, Tanzania;
  1. Azimio la Kuridhia Mkataba wa Minamata Kuhusu Kupunguza kwa kadiri iwezekanavyo Matumizi ya Zebaki ifikapo Mwaka 2030;
  1. Azimio la Kuridhia Itifaki ya pamoja ya ziada ya Nagoya – Kuala Lumpur kuhusu Uwajibikaji Kisheria na Fidia kwa Madhara yanayoweza kutokea kutokana na matumizi ya Bioteknolojia ya Kisasa katika kutekeleza Itifaki ya Cartagena;
  1. Azimio la Kuridhia Itifaki ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika kuhusu Kulinda Hakimiliki za Wagunduzi wa Aina Mpya za Mbegu za Mimea;
  1. Azimio la kuridhia Mapendekezo ya Ubadilishaji Hadhi sehemu ya eneo la Pori la Akiba la Selous kuwa Hifadhi ya Taifa ya Nyerere;
  1. Azimio la kuridhia Mapendekezo ya Ubadilishaji Hadhi Sehemu ya eneo la Pori la Akiba la Kigosi kuwa Hifadhi ya Taifa ya Kigosi; 
  1. Azimio la kuridhia Mapendekezo ya Ubadilishaji wa Hadhi Sehemu ya eneo la Pori la Akiba la Ugalla kuwa Hifadhi ya Taifa ya Mto Ugalla; na
  1. Azimio la Kuridhia Itifaki ya Marrakesh inayowezesha Upatikanaji wa Kazi zilizochapishwa kwa Watu Wasioona, Wenye Uoni Hafifu au Ulemavu Unaofanya Mtu Kushindwa Kusoma ya Mwaka 2013.
  • Mheshimiwa Spika, nawashukuru sana Waheshimiwa Mawaziri na Naibu Mawaziri kwa kazi nzuri ya kuwasilisha Miswada na Maazimio yaliyojadiliwa katika Mkutano huu pamoja na kutoa ufafanuzi kuhusu hoja mbalimbali zilizoibuliwa na Waheshimiwa Wabunge. Kadhalika, nimpongeze Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na Wataalamu wake kwa kazi nzuri ya kuandaa miswada hiyo. 
DIPLOMASIA YA UCHUMI
  • Mheshimiwa Spika, kabla ya kuhitimisha Mkutano huu, ningependa kutumia fursa hii japo kwa uchache kuzungumzia na kutoa ufafanuzi kuhusu baadhi ya masuala muhimu yaliyojiri katika kipindi hiki hususan utekelezaji wa diplomasia ya uchumi.
  • Mheshimiwa Spika, Tanzania imeendelea kufanya vizuri katika Kimataifa. Ukweli wa hili unajidhihirisha katika matokeo ya Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC); Ushiriki wa Tanzania katika Mkutano wa Saba wa Kimataifa wa Tokyo Kuhusu Maendeleo ya Afrika (TICAD 7) na juhudi za Serikali katika kujenga miundombinu wezeshi ya kiuchumi kwa lengo la kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji na biashara na hivyo, kurahisisha utekelezaji wa dhana ya diplomasia ya uchumi. 
Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC
  • Mheshimiwa Spika, kama itakavyokumbukwa, tarehe 3 Septemba, 2019 Bunge lako tukufu lilipitisha Azimio la Kumpongeza Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa SADC na kuendesha vyema Mkutano wa 39 wa Jumuiya hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam, tarehe 17 na 18 Agosti, 2019.
  • Mheshimiwa Spika, miongoni mwa mafanikio ya Uenyekiti wa Tanzania kwenye Mkutano huo ni kitendo cha Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC kupitisha matumizi ya Kiswahili kuwa lugha rasmi ya nne katika Jumuiya ya Maendeleo Kusini wa Afrika sambamba na lugha ya Kiingereza, Kifaransa na Kireno. Kwa kuanzia lugha ya Kiswahili itatumika katika mikutano ya Wakuu wa Nchi na Serikali na Baraza la Mawaziri.
  • Mheshimiwa Spika, Tanzania inaendelea kujivunia historia ya lugha ya Kiswahili hususan matumizi yake wakati wa harakati za ukombozi wa Kusini mwa Afrika na pia kuwa miongoni mwa lugha rasmi za Umoja wa Afrika. Nitoe wito kwa wadau wote wa Kiswahili nchini, watumie vyema fursa hii kutengeneza ajira kupitia huduma za ukalimani, ufundishaji na masuala mengine yenye kuhusisha matumizi ya lugha hii adhimu yenye kuakisi utamaduni wa Mwafrika. Naiagiza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kujipanga vizuri ili kuchangamkia fursa hiyo muhimu.
  • Mheshimiwa Spika, katika hotuba yake ya kupokea Uenyekiti wa SADC, Mheshimiwa Rais pamoja na mambo mengine alisisitiza umuhimu wa kuimarisha umoja na kuongeza biashara ndani ya Jumuiya sambamba na kukuza viwanda kwa kushiriki katika mnyororo wa thamani ndani ya ukanda wa SADC. 
  • Mheshimiwa Spika, kwa msingi huo, nitoe wito kwa Bunge lako tukufu, wadau wa sekta binafsi na Watanzania kwa ujumla wamuunge mkono Mheshimiwa Rais akiwa Mwenyekiti wa SADC ili aweze kutimiza malengo ya kujenga Mazingira Wezeshi kwa ajili ya Maendeleo Endelevu na Jumuishi ya Viwanda, Kukuza Biashara na Ajira ndani ya SADC.
  • Mheshimiwa Spika, taarifa kuhusu hali ya usalama wa chakula katika ukanda wa SADC, imeonesha kutetereka kutokana na athari mbalimbali ikiwemo ukame katika upande wa magharibi wa ukanda, mvua zilizokithiri, mafuriko na vimbunga vya IDAI na Kenneth pamoja na wadudu waharibifu wa mazao na magonjwa. 
  • Mheshimiwa Spika, athari hizo zimesababisha uzalishaji wa nafaka kama mahindi, mtama, mpunga, ngano na ulezi ndani ya SADC kupungua kwa asilimia 14 kutoka tani milioni 42.6 mwaka 2018 hadi tani milioni 36.8 mwaka 2019 sambamba na kupanda kwa bei. Hata hivyo, Tanzania na Afrika Kusini kwa kipindi hicho zilizalisha ziada ya mazao hayo ambayo yanakadiriwa kukidhi mahitaji kwa mwaka 2019/2020.
  • Mheshimiwa Spika, natambua pia kuwa tarehe 29 na 30 Agosti 2019, Wizara ya Kilimo iliratibu Mkutano na Wadau mbalimbali wenye kujihusisha na uzalishaji na biashara ya nafaka. Aidha, pamoja na kupongeza juhudi hizo zenye lengo la kujadili fursa zilizopo katika mazao ya nafaka, changamoto pamoja na utatuzi wake, nitumie fursa hii kuelekeza Wizara husika ihakikishe inashirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ili kutumia vema fursa ya uwepo wa masoko ya nafaka kwenye ukanda huu wa SADC na hivyo, kukidhi mahitaji katika ukanda sambamba na kuboresha biashara na maisha ya wananchi wa vijijini. Aidha, ni muhimu kuendelea kuhamasisha uzalishaji wa mazao hayo kwa wingi ili tuweze kujitosheleza kwa chakula na kuwa na ziada.
Mkutano wa TICAD 7
  • Mheshimiwa Spika, katika mwendelezo wa utekelezaji wa diplomasia yetu ya kiuchumi, tarehe 28 hadi 30 Agosti 2019, nilimwakilisha Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Mkutano wa Saba wa Kimataifa wa Tokyo Kuhusu Maendeleo ya Afrika. Serikali imeendelea kutumia majukwaa na mikutano ya namna hii kusukuma ajenda mbalimbali za maendeleo kwa lengo la kuimarisha shughuli za kiuchumi na kijamii kwa maslahi ya Watanzania.
  • Mheshimiwa Spika, kupitia Mkutano wa saba wa TICAD, Serikali ya Japan imetenga kiasi cha Dola za Marekani bilioni 20 kwa kipindi cha miaka mitatu kwa nchi za Bara la Afrika. Lengo ni kuziwezesha nchi hizo kutekeleza miradi ya kimkakati ya maendeleo itakayoleta mageuzi ya kiuchumi. Kiasi hicho kitatolewa ili kuendeleza miradi mbalimbali katika sekta za elimu, afya, kilimo, maji, nishati, ujenzi wa maeneo maalumu ya viwanda na miundombinu ya usafiri na usafirishaji. 
  • Mheshimiwa Spika, ninaielekeza Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ishirikiane kwa karibu na Wizara zenye dhamana kuratibu vema utekelezaji wa miradi nane ya maendeleo ambayo tayari imewasilishwa kupitia TICAD 7 kwa ajili ya kujadiliwa na kupatiwa fedha za ufadhili. Lengo ni kuhakikisha nchi yetu inanufaika na fedha zilizotengwa na Serikali ya Japan kwa ajili ya nchi za Afrika katika kufikia uchumi wa kati unaoongozwa na viwanda ifikapo mwaka 2025. 
  • Mheshimiwa Spika, sambamba na Mkutano wa saba wa TICAD, ujumbe wa Tanzania ulitumia vema fursa ya Mkutano huo kufanya mazungumzo na viongozi wa nchi mbalimbali, wakuu wa mashirika ya kimataifa na kitaifa, taasisi na makampuni mbalimbali. Mazungumzo na viongozi na wadau hao wa maendeleo yamekuwa na tija katika kusukuma ajenda za kuendeleza biashara na uwekezaji katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii. Baadhi ya maeneo yaliyopewa kipaumbele ni uwekezaji kwenye viwanda vya nguo na nyuzi, sukari, sekta ya uvuvi, elimu, nishati pamoja na uboreshaji wa sekta ya afya ikiwemo kuimarisha huduma za uchunguzi wa kisasa wa magonjwa na matengenezo ya vifaa tiba.
  • Mheshimiwa Spika, Serikali ya Japan na wadau wengine wa maendeleo wameridhishwa na kusifu namna Mheshimiwa Rais wetu, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, anavyosimamia mwenendo wa uchumi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo hususan ile inayotekelezwa kwa kushirikiana na nchi hiyo. Aidha, Tanzania na Japan zinaendelea na mashauriano kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kipaumbele ikiwemo kuendeleza Jiji la Dodoma pamoja na kuharakisha utekelezaji wa miradi ya kuboresha barabara; ukarabati wa bandari ya Kigoma na mradi wa maji Zanzibar.
Uimarishaji wa Mazingira ya Biashara na Uwekezaji
  • Mheshimiwa Spika, ikumbukwe kwamba Tanzania imeanza kutekeleza Mpango wa Kuboresha Mfumo wa Udhibiti wa Biashara nchini (Blueprint on Regulatory Reforms For Improved Business Environment) na Mpango Kazi wa Utekelezaji wake tangu Julai mosi, 2019. Aidha, sote tunatambua kuwa lengo la blueprint ni kujenga mazingira wezeshi ya biashara na uwekezaji ambapo kupitia Mkutano wa 15 wa Bunge la 11 jumla ya kodi na tozo 54 ziliondolewa.
  • Mheshimiwa Spika, sambamba na hilo, Serikali imeunda Timu ya Wataalamu ambayo inafanya uchambuzi wa changamoto zilizobainishwa kwenye taarifa mbalimbali na kuandaa mapendekezo ya marekebisho ya sheria husika. Aidha, kama nilivyoeleza katika hotuba yangu ya bajeti, Ofisi ya Waziri Mkuu inakamilisha mapitio na uandaaji wa Sera mpya ya Uwekezaji nchini. Hivyo, nitoe rai kwa wadau wote kutoa maoni yao kuhusu mapitio ya Sera ya Uwekezaji hasa kupitia tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu ya www.pmo.go.tz na ile ya Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) ya www.tpsftz.org.  
  • Mheshimiwa Spika, kwa upande mwingine, nitumie fursa hii kumpongeza tena Mheshimiwa Rais kwa hatua za makusudi anazochukua kuhakikisha anaimarisha shughuli za biashara na uwekezaji kupitia ziara za kitaifa za viongozi rafiki kutoka mataifa mbalimbali sambamba na makongamano ya kibiashara na uwekezaji.
  • Mheshimiwa Spika, kati ya Agosti na Septemba 2019, Mheshimiwa Matalema Cyril Ramaphosa, Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini na Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Jamhuri ya Uganda walifanya ziara rasmi za Kiserikali nchini Tanzania. Vilevile, ziara hizo muhimu ziliambatana na makongamano ya biashara na uwekezaji kati ya wafanyabiashara wa Tanzania na nchi hizo.
  • Mheshimiwa Spika, niungane na Mheshimiwa Rais kusisitiza kuwa makongamano ya namna hiyo yamekuwa na mchango mkubwa katika kubaini na kutumia fursa za biashara na uwekezaji zinazopatikana nchini lakini pia kushughulikia changamoto za kibiashara na uwekezaji zinazokabili pande husika.
  • Mheshimiwa Spika, katika hatua nyingine ya kuimarisha biashara na uwekezaji Mheshimiwa Rais wetu mpendwa tarehe 22 Agosti 2019, jijini Dar es Salaam, alikutana na Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje. Kupitia mkutano huo, Mheshimiwa Rais aliwafahamisha Mabalozi kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuimarisha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini na wajibu wa Mabalozi katika kuvutia uwekezaji nchini, kutafuta masoko ya bidhaa na mazao yetu na kutangaza utalii. Nami niungane tena na Mheshimiwa Rais kusisitiza kuwa utendaji wa wawakilishi wetu nje, utaendelea kupimwa kwa idadi na matokeo ya uwekezaji na biashara walizovutia nchini.
  • Mheshimiwa Spika, mwaka 2001 Robert Kiyosaki, mwandishi maarufu wa vitabu aliwahi kuandika nami ninamnukuu: “The size of your success is measured by the strength of your desire; the size of your dream; and how you handle disappointment along the way.” Mwisho wa kunukuu. Kwa tafsiri isiyo rasmi ya Kiswahili, mwandishi huyu anajaribu kueleza kuwa ukubwa wa mafanikio yako hupimwa kwa kiwango cha utashi, ndoto zako na namna unavyokabiliana ama kukatishwa tamaa wakati ukitekeleza malengo yako.
  • Mheshimiwa Spika, nukuu hii kwa kiasi kikubwa inaakisi dhamira ya Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuhakikisha anajenga misingi ya uchumi wa kisasa wa Taifa linalojitegemea pamoja na uwezeshaji wa wananchi kiuchumi bila kutetereka kutokana na kauli za kubeza zinazotolewa na baadhi ya watu wachache wasioitakia mema nchi hii.
Ujenzi wa Miundombinu Wezeshi
  • Mheshimiwa Spika, juhudi hizo za Mheshimiwa Rais zinakwenda sambamba na ujenzi wa miundombinu wezeshi ikiwemo ya usafiri na usafirishaji, nishati pamoja na maendeleo ya Jamii. Napenda kutumia fursa hii kutaja japo kwa uchache baadhi ya miradi inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi mahiri wa Mheshimiwa Rais kwa lengo la kuchochea uwekezaji, kujenga uchumi imara, shindani na wenye kujitegemea. 
Mosi:    Kuongeza Bajeti kwa ajili ya mikopo ya Elimu ya Juu kutoka Shilingi bilioni 186.48 mwaka 2010 hadi Shilingi bilioni 424 mwaka 2018/2019 sawa na ongezeko la asilimia 44.1 sambamba na ongezeko la wanafunzi wanaonufaika na mikopo ya Elimu ya Juu kutoka wanafunzi 72,035 mwaka 2009/2010 hadi kufikia 122,754 mwaka, 2018/2019 sawa na ongezeko la asilimia 58.7;
Pili:    Kuendelea na ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kimataifa kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza na Kigoma na kisha kufikisha kwenye mipaka ya nchi za Burundi na Rwanda, kwa fedha zetu wenyewe. Ujenzi wa Kilometa 300 kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro upo katika hatua nzuri na kilometa 412 kutoka Morogoro hadi Makutupora nao unaendelea vizuri. Gharama za ujenzi kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma zitafikia shilingi trilioni 7.062;
Tatu:    Kuendelea na upanuzi wa bandari zetu za Dar es Salaam, Mtwara na Tanga ambao utagharimu shilingi Trilioni 1.2;
Nne:    Kukamilika kwa ujenzi wa meli mbili za Mv. Iringa na Mv. Ruvuma, ambazo zinatoa huduma katika Ziwa Nyasa. Kuendelea na ukarabati wa meli mbili za Mv. Victoria na Mv. Butiama pamoja na ujenzi wa meli mpya kwa ajili ya Ziwa Victoria kwa zaidi ya shilingi bilioni 172.3;
Tano:    Kuendelea na ujenzi wa Ubungo Interchange kwa shilingi bilioni 247 na barabara ya njia nane kutoka Dar es Salaam hadi Chalinze kwa gharama ya shilingi bilioni 140;
Sita:    Ujenzi wa Daraja la Kigongo – Busisi unaotarajiwa kugharimu shilingi bilioni 699.2;
Saba:    Kuendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kuzalisha umeme, ikiwemo kutumia gesi yetu asilia na ujenzi wa mradi mkubwa wa kuzalisha umeme wa maji wa Megawati 2,115 (Nyerere Hydro Power Project) kwa shilingi trilioni 6.5 katika maporomoko ya mto Rufiji; na
Nane:    Kukamilika kwa ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere kwa gharama ya shilingi bilioni 722, na upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kilimajaro kwa thamani ya shilingi bilioni 91. Aidha, tunaendelea na ukarabati wa viwanja takriban 11 vya ndege sehemu mbalimbali nchini, ikiwemo Mwanza (bilioni 90); Mtwara (shilingi bilioni 46); Shinyanga (shilingi bilioni 49.2); Sumbawanga (shilingi bilioni 55.9); Musoma (shilingi bilioni 21), Songea (shilingi bilioni 21) na Iringa (shilingi bilioni 39);
  • Mheshimiwa Spika, maboresho katika sekta ya usafiri wa anga na mengine yanayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano yamekuwa na matokeo makubwa katika kuitangaza na kuimarisha heshima ya Tanzania kwa Jumuiya ya Kimataifa. Kwa mfano, tumeendelea kupokea fursa ya kuwa wenyeji wa matamasha ya kimataifa ya utamaduni, wachezaji na wasanii maarufu akiwemo muigizaji wa sinema wa Marekani, Will Smith ambaye amekuja nchini zaidi ya mara mbili. 
  • Mheshimiwa Spika, Watanzania wote wanatambua tukio lililotokea hivi karibuni la kushikiliwa kwa Ndege yetu aina ya Airbus 220-300 huko Afrika Kusini. Napenda kutumia nafasi hii kulipongeza jopo la Wanasheria wazalendo wa Kitanzania wakiongozwa na Dkt. Damas Daniel Ndumbaro, Mbunge wa Songea Manispaa kwa jitihada zao za kupigania kurejeshwa kwa Ndege yetu hapa nchini, bila kuwasahau Watanzania walioonesha kukerwa kwa tukio lile. TANZANIA ITAJENGWA KWANZA NA WATANZANIA WENYEWE.
  • Mheshimiwa Spika, tarehe 21 hadi 28 Septemba 2019, Tanzania itakuwa mwenyeji wa Tamasha la Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki lijulikanalo kama Jumuiya ya Afrika Mashariki Utamaduni Festival (JAMAFEST). Rai yangu kwa waandaaji na wadau wa tasnia ya ubunifu na ujasiriamali ni kutumia vema fursa ya uwepo wa Tamasha hilo lenye kukutanisha viongozi, wabunifu, wajasiriliamali na wasanii kuhamasisha masoko ya bidhaa za wabunifu na wajasiriamali kwa lengo la kuleta maendeleo endelevu ya masoko ya bidhaa hizo.
  • Mheshimiwa Spika, kwa upande mwingine nitumie pia fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Dkt. Hamis Kigwangalla (Mb.), Waziri wa Maliasili na Utalii, Ubalozi wa Tanzania nchini China, Watendaji wa Wizara na Bodi ya Utalii nchini kwa kufanikisha Makubaliano na Mtandao maarufu nchini China (BAIDU). Lengo la makubaliano hayo ni kuongeza idadi ya Wachina wanaotembelea vivutio vyetu vya utalii kutoka 32,773 msimu uliopita hadi 100,000. 
  • Mheshimiwa Spika, Tanzania ndiyo nchi pekee kutoka Afrika iliyofanikiwa kuingia katika mpango wa BAIDU ujulikanao kama “Wonder Planet”. Vilevile, ndiyo nchi ya kwanza kutembelewa na timu inayoandaa mpango huo. Mpango wa Wonder Planet, una lengo la kutembelea nchi saba ili kuona vivutio vilivyopo kwenye nchi hizo na kuvitangaza kwa wateja wa mtandao huo wasiopungua milioni 700.
  • Mheshimiwa Spika, tuna kila sababu ya kujivunia mafanikio yaliyopatikana kwa kipindi hiki. Waswahili husema “huwezi kuwasha taa, halafu ukaifunika”. Hivyo basi, tunaeleza mafanikio haya ili wananchi watambue kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha inashirikiana nao katika kujenga Taifa lenye uchumi imara, shindani na wenye kujitegemea. Kwa lugha nyingine, mipango endelevu tuliyojiwekea, sera maridhawa na usimamizi makini vinatupa matumaini kuwa lengo tulilojiwekea linatimia pasi na shaka.
  • Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia muktadha huo, niwaombe Watanzania wenzangu kuendelea kumuomba Mwenyezi Mungu awajalie viongozi wetu hekima na busara ili waendelee kuliongoza Taifa letu kwa haki, kuondoa uovu, kujenga umoja na mshikamano, kudumisha amani katika nchi yetu pamoja na kuimarisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
  • Mheshimiwa Spika, napenda pia kutoa wito kwa wawekezaji kutumia fursa ya uwepo wa mazingira mazuri ya uwekezaji na biashara, miundombinu wezeshi, upatikanaji wa malighafi na rasilimali watu kwa ajili ya kujenga viwanda mbalimbali hususan vya kuchakata mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi na malighafi nyinginezo zinazopatikana nchini.
KILIMO
Hali ya Chakula
  • Mheshimiwa Spika, hali ya uzalishaji wa mazao ya chakula nchini imeendelea kuwa toshelevu. Kwa mfano, katika msimu wa kilimo wa 2018/2019 uzalishaji ulifikia takriban tani milioni 16.41 ikilinganishwa na mahitaji ya tani milioni 13.84. 
  • Mheshimiwa Spika, hivi sasa wafanyabiashara wa mazao ya chakula wanaendelea kusafirisha na kuuza mazao hayo ndani na nje ya nchi. Serikali inawahimiza wananchi wote kuhifadhi chakula cha kutosha kwa ajili ya matumizi ya nyumbani hususan wakati huu tunapoingia kwenye msimu mpya wa kilimo kwa mwaka 2019/2020.
Maandalizi ya Msimu wa Kilimo
  • Mheshimiwa Spika, katika kipindi hiki cha kuanzia Septemba 2019 maeneo mengi ya nchi yetu huanza kupata mvua za vuli ambazo ni ishara ya kuanza kwa msimu mpya wa kilimo. Serikali inahakikisha pembejeo za kilimo ikiwemo mbegu bora, mbolea na viuatilifu kwa ajili ya msimu huu mpya wa kilimo zinapatikana.
  • Mheshimiwa Spika, nitumie nafasi hii kuiagiza Wizara ya Kilimo ihakikishe inasimamia ipasavyo mawakala waliopewa jukumu la kusambaza pembejeo kwa wakulima ili ziwafikie kwa wakati na kwa bei inayohimilika na ubora unaohitajika.
Upatikanaji wa Masoko ya Mazao
  • Mheshimiwa Spika, nawapongeza wakulima kwa kuitikia wito wa Serikali katika kuongeza uzalishaji wa mazao mbalimbali ya kilimo hasa yale ya biashara kama vile pamba, tumbaku, kahawa na korosho. 
Pamba
  • Mheshimiwa Spika, mabadiliko ya bei ya pamba katika soko la dunia yaliyosababishwa na mgogoro wa kibiashara kati ya mataifa makubwa yameporomosha bei ya pamba katika soko la dunia kinyume na matarajio kuwa bei ingeongezeka. Katika kukabiliana na hali hiyo, Serikali imechukua hatua zifuatazo:
Mosi:    Kusimamia makubaliano kati ya Benki Kuu na Benki zilizotoa mikopo kwa kampuni zinazonunua pamba kulingana na mahitaji yao ya mitaji ya kununua pamba ili pamba yote inunuliwe kwa wakati;
Pili:    Kuhamasisha makampuni kupeleka fedha kwa ajili ya malipo ya wakulima na kulipia pamba iliyopimwa ghalani na iliyobaki mikononi mwa wakulima.
Tatu:    Kudhibiti udanganyifu kupitia mizani, malipo ya wakulima na makato ya pembejeo katika maeneo yaliyobainika kutokea kwa vitendo hivyo.
  • Mheshimiwa Spika, hivi sasa, wanunuzi wote wamepewa maeneo yote yenye Pamba na tayari wameshapewa fedha kwa ajili ya kulipia pamba yote. Natoa wito kwa Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wasimamie manunuzi haya ili wakulima walipwe malipo yao stahiki.
Tumbaku
  • Mheshimiwa Spika, hadi kufikia tarehe 31 Agosti, 2019 mauzo ya tumbaku za mkataba yalikuwa yamekamilika. Jumla ya kilo milioni 60.59 zenye thamani ya Dola za Marekani milioni 92.79 zilinunuliwa. Kiasi hicho, ni sawa na asilimia 105.7 ya lengo la kuzalisha kilo milioni 57.31 za tumbaku ya mkataba. 
  • Mheshimiwa Spika, hata hivyo, tathmini ya masoko imeonesha uwepo wa tumbaku ya ziada kiasi cha kilo milioni 12.22 ambazo zilizalishwa nje ya mkataba katika maeneo mbalimbali. Serikali inaendelea na majadiliano na makampuni ya ununuzi kwa lengo la kuhakikisha tumbaku yote inanunuliwa.
Korosho
  • Mheshimiwa Spika, katika msimu wa 2018/2019 jumla ya tani 224,964 za korosho ghafi zenye thamani ya shilingi bilioni 729.90 zilikusanywa. Kati ya hizo, tani 222,825 zilikusanywa na Serikali. Aidha, korosho zilizolipwa ni tani 197,547 na Serikali inakamilisha malipo ya kiasi kilichobaki cha tani 25,278. Hivi sasa, korosho yote imenunuliwa na inasafirishwa. Aidha, baada ya zoezi hilo Bodi ya Mazao Mchanganyiko itarudi kulipa madeni yaliyobaki kwa wakulima na wenye maghala.
  • Mheshimiwa Spika, kuelekea msimu ujao wa ununuzi wa korosho, Serikali imeandaa mikakati ya kuhakikisha upatikanaji wa masoko ya uhakika. Jitihada zinazofanywa na Serikali hivi sasa ni:-
Moja:    Kuvutia uwekezaji katika viwanda vya kubangua korosho nchini;
Mbili:    Kupanua soko la korosho kwa kuhamasisha ujenzi wa viwanda vya kutengeneza bidhaa nyingine zitokanazo na korosho zikiwemo siagi, maziwa, mvinyo na sharubati;
Tatu:    Kuendelea kujenga maghala ya mfano na yenye viwango kwa ajili ya kuhifadhia korosho katika maeneo ya kimkakati;
Nne:    Kusimamia uuzwaji wa korosho inayozalishwa nchini kwa wakati ili kutumia fursa ya korosho ya Tanzania ambayo inazalishwa kipindi ambacho hakuna korosho nyingine katika soko la dunia; na
Tano:    Kuimarisha mifumo ya ununuzi wa korosho kwa lengo la kuvutia wanunuzi wengi zaidi kutoka ndani na nje ya nchi;
  • Mheshimiwa Spika, hivi karibuni, msimu wa korosho utaanza na wakulima wataarifiwa kuhusu utaratibu mzima wa uuzaji. Aidha, Serikali itatoa nafasi ya kwanza ya ununuzi kwa wenye viwanda nchini. Hivyo, ni vema sasa waandae mahitaji yao kwa msimu huu na kuyawasilisha kwenye mamlaka husika ili kuwahakikishia malighafi ya kutosheleza mahitaji ya viwanda vyao.
  • Mheshimiwa Spika, kama mtakavyoona, Serikali inafanya kazi kubwa ya kuimarisha masoko ya mazao ndani na nje. Kwa msingi huo, naielekeza Wizara ya Viwanda na Biashara na Wizara ya Kilimo kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuhakikisha wanasimamia upatikanaji wa masoko mapya ya mazao mbalimbali. 
  • Mheshimiwa Spika, wizara hizo, zinapaswa kuzingatia maelekezo mahsusi yaliyotolewa na Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipokutana na Mabalozi wanaoiwakilisha nchi yetu. Aidha, taasisi zinazohusika na utafutaji wa masoko ikiwemo Soko la Bidhaa (TMX), TanTrade na Bodi zote za Mazao zijikite katika kutafuta masoko ya mazao yanayozalishwa nchini. 
UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA
  • Mheshimiwa Spika, tarehe 24 Novemba 2019, nchi yetu itafanya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao hufanyika kila baada ya miaka mitano. Lengo la uchaguzi huo ni kukidhi matakwa ya Ibara ya 8 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, inayoelekeza kuwa Mamlaka na Madaraka ya Serikali yanatokana na wananchi. 
  • Mheshimiwa Spika, wakati tukielekea kwenye uchaguzi huu, napenda kusisitiza mambo yafuatayo:
Moja:    Kuwasihi Waheshimiwa Wabunge na Madiwani kuhamasisha wananchi watumie haki yao ya kidemokrasia ya kuchagua na kuchaguliwa. Natoa rai kwenu kuhakikisha mnashiriki kikamilifu katika shughuli zote za uchaguzi huo;
Pili:    Kuwahimiza Wakuu wa Mikoa na Wilaya waratibu shughuli za uchaguzi katika maeneo yao na kuhakikisha uwepo wa ulinzi na usalama wakati wote wa uchaguzi hasa kipindi cha Kampeni na wakati wa kupiga kura. Vyombo vya ulinzi na usalama vishiriki kikamilifu kuhakikisha wananchi wanafanya uchaguzi katika mazingira ya amani na utulivu bila kubughudhiwa; na
Tatu:    Kuwahimiza Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kuhakikisha wanazielewa Kanuni na miongozo ilitoyotolewa ili waweze kutoa tafsiri sahihi wakati wa kusimamia uchaguzi huo na kuhakikisha unafanyika kwa ufanisi mkubwa kwa mujibu wa Sheria.
  • Mheshimiwa Spika, natoa wito kwa Watanzania wote wenye sifa wajiandikishe katika orodha ya wapiga kura, wachukue fomu za kugombea nafasi mbalimbali na kushiriki kupiga kura kwani hiyo ni haki yao ya kikatiba kwa kuzingatia misingi ya demokrasia. 
  • Mheshimiwa Spika, pia, nitoe rai kwa wadau mbalimbali watakaoshiriki katika uchaguzi wakiwemo Vyama vya Siasa, Taasisi za Serikali na Zisizo za Serikali na Wananchi kusoma na kuzielewa Kanuni na miongozo ya uchaguzi kwa kuhakikisha wanajiepusha na vitendo vyovyote vya rushwa na uvunjifu wa amani. Serikali haitasita kuchukua hatua pale itakapothibitika vitendo hivyo kufanyika kinyume cha Kanuni na Sheria nyingine za nchi. 
UBORESHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA
  • Mheshimiwa Spika, kwa upande wa uboreshaji wa daftari la wapiga kura, tarehe 18 Julai 2019 Serikali ilizindua zoezi hilo mkoani Kilimanjaro. Uboreshaji huo, unahusisha Wapiga Kura waliotimiza umri wa miaka 18 na wale watakaotimiza umri huo wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020.
  • Mheshimiwa Spika, makundi mengine yatakayohusika ni wapiga kura waliohamia katika kata au jimbo jingine la uchaguzi, waliopoteza kadi au kadi zao zimeharibika, wanaohitaji kurekebisha taarifa zao; mfano majina ambayo hapo awali yalikuwa yamekosewa pamoja na kuwaondoa wapiga kura waliopoteza sifa kama vile kufariki.
  • Mheshimiwa Spika, kwa sasa zoezi hilo tayari limekamilika katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Simiyu, Mara na Mwanza (isipokuwa Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba). Zoezi hilo linaendelea kutekelezwa chini ya kaulimbiu isemayo Kadi Yako, Kura Yako, Nenda Kajiandikishe.
  • Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii kuwapongeza wananchi wote wanaoendelea kujitokeza kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Aidha, nitoe rai kwa wananchi ambao bado hawajajiandikisha, wafanye hivyo ili watimize haki yao ya Kikatiba. Kwa upande wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, nirudie maelekezo niliyoyatoa wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo kwa waandikishaji kutoa kipaumbele kwa makundi maalumu ikiwemo wazee, wajawazito na watu wenye ulemavu ili wasikae kwenye foleni kwa muda mrefu.
MICHEZO
  • Mheshimiwa Spika, katika nyanja ya michezo naomba nitoe pongezi za dhati kwa timu ya Taifa ya Wanawake chini ya Umri wa Miaka 20 (maarufu kama Tanzanite) kwa kutwaa kombe la mpira wa Miguu kwa Nchi za COSAFA huko Port Elizabeth, Afrika ya Kusini. Aidha, naipongeza timu ya kandanda ya Taifa Stars kwa kufanikiwa kuiondoa Harambee Stars katika mashindano ya CHAN 2020. Kadhalika, kwa kuiondoa Burundi na kufanikiwa kuingia hatua ya makundi ya kufuzu Kombe la Dunia huko Doha, Qatar 2022. Hatua hii ni nzuri na muhimu kwani inaiweka timu yetu katika nafasi nzuri kushiriki fainali za mashindano hayo. Timu ya Taifa itarudi dimbani kupambana na Sudan tarehe 22 Septemba, 2019 kwenye Uwanja wa Taifa. Kama kawaida yetu twenda tukaujaze Uwanja wetu na kuishangilia kwa nguvu timu yetu ya Taifa.
  • Mheshimiwa Spika, vilevile, navipongeza vilabu vya Azam, Malindi na Yanga kwa kufanikiwa kusonga mbele kuingia hatua ya pili katika michuano ya vilabu ya Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF). Aidha, kwa vilabu vya KMC, KMKM na Simba, ambavyo vimeondolewa katika hatua ya mwanzo kabisa, vichukulie hali hiyo kama changamoto ya kujitathmini na kujiandaa kwa ajili ya michezo ya ndani na mashindano yajayo ya kimataifa badala ya kutumia muda mrefu kujadili kuhusu kutolewa kwao mapema.
  • Mheshimiwa Spika, kwa upande wa masumbwi, bendera ya Tanzania imeendelea kupeperushwa vyema kufuatia wana masumbwi wengine wawili wa Kitanzania kufanya vizuri katika medani za kimataifa. Nitumie nafasi hii kuwapongeza mwanamasumbwi Abdallah Shaaban Pazi maarufu Dulla Mbabe kwa kufanikiwa kutwaa ubingwa wa dunia wa WBO baada ya kumpiga kwa KO kwenye raundi ya tatu mpinzani wake Mchina anayejulikana kwa jina la Zulipikaer Maimaitiali. 
  • Mheshimiwa Spika, nampongeza pia mwanamasumbwi mwingine wa kitanzania Bruno Tarimo maarufu vifua viwili kwa kumnyoosha mpinzani wake Mserbia, Scheka Gurdijeljac kwenye pambano la ubingwa wa dunia lililofanyika mwanzoni mwa mwezi huu huko Serbia. Hongereni sana wanamichezo wetu na endeleeni na moyo huo wa kizalendo mliouonesha katika kuipeperusha vema bendera ya Taifa letu. 
  • Mheshimiwa Spika, nimpongeze pia Mrembo wetu Miss Tanzania 2019, Miss Sylvia Sebastian Bebwa pamoja na Queen Anthony Magese na Greatness Amos Nkuba walioshika nafasi ya pili na ya tatu. Tunamtakia matayarisho mema Miss Tanzania ili akapeperushe vema Bendera ya Taifa letu nchini Uingereza kwenye mashindano ya Mrembo wa Dunia (Miss World) ambako pia ataitangaza nchi yetu na vivutio vya utalii tulivyonavyo. Aidha, naitaka Wizara kuendelea kuratibu vizuri shughuli za michezo, utamaduni na sanaa ili zilete ufanisi wa hali ya juu na pia kuweka msisitizo sambamba na kuwa na mikakati ya kuendeleza michezo ikiwemo shuleni, vituo maalumu vya michezo sambamba na kuwa na mifumo mizuri ya upatikanaji wa fedha za kuendesha vilabu nchini.
HITIMISHO
  • Mheshimiwa Spika, wakati nikielekea kuhitimisha hotuba yangu napenda kukupongeza pamoja na Bunge lako tukufu kwa heshima kubwa tuliyoipata kama nchi ya kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 50 wa Chama cha Mabunge cha Jumuiya ya Madola, Kanda ya Afrika (CPA) uliofanyika huko Zanzibar tarehe 2 Septemba 2019.
  • Mheshimiwa Spika, kufanikiwa kwa mkutano huo ni ishara tosha ya utekelezaji mzuri wa diplomasia yetu ya mabunge yaani parliamentary diplomacy ambayo pamoja na mambo mengine inalenga kusaidia kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania, kuingiza fedha za kigeni na kutoa fursa kwa wanyabiashara nchini kufanya biashara zao hususan zile za utoaji huduma (service delivery).
  • Mheshimiwa Spika, nami niungane nawe kutoa rai kwa wafanyabiashara na Watanzania wenzangu kwa ujumla kuchangamkia fursa hizi adhimu tunazozipata kwa kuaminiwa na mataifa mbalimbali kwani licha ya kuja kwetu, mataifa mengine pia yangetamani kuzipata kutokana na mchango wake katika kuinua kipato cha wananchi kupitia biashara za huduma.
  • Mheshimiwa Spika, nihitimishe hotuba yangu kwa kumshukuru Katibu wa Bunge na watendaji wa Ofisi ya Bunge kwa kazi kubwa ya kuratibu vikao vya mkutano huu. Aidha, niwashukuru watendaji wa Serikali kwa kufanikisha shughuli zilizopangwa na Bunge lako tukufu kwa weledi na ufanisi mkubwa. 
  • Mheshimiwa Spika, kipekee, niwashukuru wanahabari kwa kufikisha habari kuhusu mkutano huu kwa wananchi. Nivishukuru pia vyombo vya ulinzi na usalama kwa huduma wanazozitoa kwa washiriki wa Bunge hili bila kuwasahau madereva waliotuhudumia wakati wote tukiwa hapa Bungeni. 
  • Mheshimiwa Spika, pamoja na kuwatakia safari njema Waheshimiwa Wabunge, niwaombe mnaporejea majimboni kwenu muendelee kuwahamasisha wananchi kuhusu umuhimu wa kushiriki ipasavyo kwenye uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa. Aidha, waendelee kuiunga mkono Serikali kwenye jitihada zake za kujenga uchumi imara, wenye ushindani na kujitegemea.
  • Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, sasa naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu liahirishwe hadi tarehe 05 Novemba, 2019 siku ya Jumanne saa tatu kamili asubuhi litakapokutana tena katika ukumbi huu Jijini Dodoma.
  • Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.

WIZARA YAWEZESHA UANZISHAJI VIKUNDI VYA MALEZI NZEGA

0
0
Mkurugenzi Msadizi Familia kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Tausi Mwilima akizungumza na wanachama wa kikundi cha malezi cha Happy kilichopo Kata ya Nzega Magharibi katika mpango wa uanzishwaji wa Vikundi vya Malezi na Elimu ya Malezi kwa Familia.
Mkurugenzi Msadizi Familia kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Tausi Mwilima akikabidhi bango kitita la kufundishia Elimu ya Malezi kwa familia kwa Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Mji wa Nzega Bi. Mwajuma Kisoma mara baada ya kutoa mafunzo ya elimu ya familia kwa kikundi cha malezi cha Happy.
Mkurugenzi Msadizi Familia kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Tausi Mwilima akikabidhi Kitini cha Elimu ya Malezi kwa familia kwa Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Mji wa Nzega Bi. Mwajuma Kisoma mara baada ya kutoa mafunzo ya elimu ya familia kwa kikundi cha malezi cha Happy.

Mkurugenzi Msadizi Familia kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Tausi Mwilima akishuhudia Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Mji wa Nzega Bi. Mwajuma Kisoma akikabidhi Kitini cha Elimu ya Malezi kwa familia kwa Katibu wa kikundI cha Malezi ya Happy Bi. Neema Nogigwa mara baada ya kutoa mafunzo ya elimu ya familia kwa kikundi cha malezi cha Happy.


Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Emmanuel Burton akieleza vyanzo vya ukatili kwa wanachama wa kikundi cha malezi cha Amani kilichopo Kata ya Nzega Magharibi katika mpango wa uanzishwaji wa Vikundi vya Malezi na Elimu ya Malezi kwa Familia.




Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Emmanuel Burton akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa kikundi cha malezi cha Amani mara baada ya kutoa mafunzo ya elimu ya familia kwa kikundi hicho.

Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW

…………………

Na Mwandishi Wetu Nzega

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii imewezesha uanzishwaji wa vikundi vya malezi katika Kata mbili za Halmashauri ya Mji wa Nzega mkoani Tabora.

Akizungumza katika Kata ya Nzega Magharibi Mkurugenzi Msaidizi Familia kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Tausi Mwilima amesema lengo la kuanzishwa kwa vikundi vya malezi katika jamii ni kuisaidia jamii kupata elimu sahihi ya malezi ili kuondokana na vitendo vya kikatili.

Bi. Tausi amesema kuwa jamii inawajibu wa kuhakikisha kuwa watoto wanapata malezi bora ambayo yatamuweka mbali na vitendo vya ukatili ambapo kwa sehemu kubwa vimekuwa vikiwaharibu watoto hasa kisaikolojia.

Ameongeza kuwa Serikali katika kuhakikisha vikundi hivyo vinapata nguvu ya kutekeleza wajibu wao imekuja na Kitini cha Malezi ya Familia ambacho kitawasaidia kupata nyenzo muhimu za namna ya kuwapa malezi bora watoto katika jamii.

Bi. Tausi amesisitiza kuwa vikundi vya malezi vitasimama vizuri basi watoto wetu watapata malezi bora na kuwezesha kuwa na taifa lenye kuwajibika katika kuwajenga watoto katika malezi.

“Vitendo vingi vya ukatili kwa Wat’s katika vinafanywa na wazazi/walezi na watu wa karibu hivyo tunahitaji elimu ya malezi ili kuhakikisha knatokomeza vitendo hivi” alisema Bi. Tausi

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii na Mratibu wa Dawati la Jinsia na Watoto Halmshauri ya Mji wa Nzega Bi. Mwajuma Kisoma amesema kuwa vikundi vya malezi ni nyenzo muhimu katika kuhakikisha watoto wanapatiwa malezi bora ambayo yatasaidia kuondokana na vitendo vya ukatili katika jamii.

Ameongeza kuwa wanachama wa vikundi vya malezi wanatakiwa kuwa mabalozi kwa wanajamii ambao hawajapata elimu ya malezi ya familia kuzuia ukatili dhidi ya watoto nchini.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kikundi cha Malezi cha Happy Mtaa wa Utemile Kata ya Nzega Magharibi Bi. Rebeca Madafu amesema kuwa mafunzo ya elimu ya malezi itasaidia kuondokana na vitendo vya ukatili katika familia kwani mara nyingi familia zimekuwa zikifanya vitendo vya ukatili bila kujua kama wanawakatili watoto.

Wakati huo huo akizungumza na kikundi cha Malezi cha Amani Kata ya Nzega Mashariki Shule ya Sekondari Nzega Afisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Emmanuel Burton amesema kuwa wazazi na walezi wanawatakiwa kuwalinda na kuwafundisha stadium za kuwalinda ili kuondokana na vitendo vya ukatili katika maeneo mbalimbali.

Ameongeza kuwa vitendo vya ukatili kwa watoto vimekuwa vikiiongezeka katika familia na Jamii hivyo kuwepo na umuhimu kuongeza nguvu katika malezi kwa watoto.

Naye Mwenyekiti wa Kikundi cha Malezi cha Amani Bw. Denson Butendeli ameishukuru Wizara kwa kutoa elimu ya malezi kwa kikundi chao na amehaidi kuwa wataitumia elimu hiyo kutengeneza mtandao na vikundi vingine na kuendelea kuelimisha jamii kuhusu malezi bora kwa familia.

katika zoezi hili jumla ya vikundi vya malezi viwili vya Happy na Kikundi cha Malezi cha Amani kutoka Kata ya Nzega Magharibi vimeanzishwa katika Halmashauri ya Mji wa Nzega kwa lengo la kutoa elimu ya malezi ngazi ya Jamii na familia.

SERIKALI KUJENGA MTO MSIMBAZI

0
0

Serikali kupitia Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) kwa kushirikiana na Benki ya Dunia na Shirika la Maendeleo la Uingereza (DFID) inatekeleza mradi wa Tanzania Urban Resilience Programme (TURP) ambao umelenga kuzisaidia Halmashauri na Serikali Kuu katika kukabiliana na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi. Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mh. George Simbachawene alipokua akijibu swali la Mbunge wa Temeke Mh. Ally Mtulia lililouliza Je ni lini Serikali itajenga Mto Msimbazi?.

Waziri Simbachawene aliongeza kuwa Mradi huu ukitekelezwa utaleta manufaa makubwa katika Jiji la Dar es Salaam ambapo utaokoa maeneo yaliyo hatari kwa mafuriko na kuyafanya salama kwa maendeleo ya jiji, utapendezesha jiji kwa kuweka maeneo mazuri ya maegesho ya magari (Dar Central Park, First of its Kind in Tanzania and East Africa), maeneo kwa ajili ya shughuli za umma kama mikutano na matamasha na kubadilisha eneo la Mto Msimbazi linalokumbwa na mafuriko kuwa eneo linalofaa kwa ajili ya michezo na lenye manufaa ya kiikolojia kwa jiji la Dar es Salaam. 

Naye Mbunge wa Jimbo la Wingwi kutoka Zanziba Mh. Juma Kombo Wawi, aliuliza Je, Serikali haioni ni busara kuondoa suala la uvuvi wa Bahari kuu kwenye orodha ya mambo ya Muungano ili kuisaidia Zanzibar kujiendesha yenyewe na kuweza kusaidia uchumi wa Zanzibar. 

Akijibu swali Hilo Waziri Simbachawene alisema kuwa Bunge lilipitisha Sheria ya Territorial Sea and Exclusive Economic Zone Act, 1989 iliyoanzisha Maeneo ya Bahari yaitwayo Bahari ya Ndani (Inner Sea), Bahari ya Kitaifa (Territorial Sea) na Eneo la Uchumi la Bahari (Exclusive Economic Zone – EEZ). Chimbuko la Sheria hii ni Sheria ya Kimataifa ya Bahari (The United Nations Convention on the Law of the Sea (UNCLOS), ya Mwaka 1982 inayotoa fursa sawa kwa nchi duniani kugawana rasilimali za bahari zilizopo kwenye maji (water column) na pia kwenye sakafu ya bahari (seabed). 

Mheshimiwa Spika, Tanzania iliridhia na kuanza kuitekeleza Sheria hii mwaka 1985. Hivyo, jukumu la kusimamia shughuli za uvuvi kwenye maji yaliyo katika Bahari ya Ndani (Inner Sea) na Bahari ya Kitaifa (Territorial Sea) ya Tanzania Bara hutekelezwa kupitia Sheria ya Uvuvi Na. 22 ya Mwaka 2003, na upande wa Zanzibar Sheria ya Uvuvi Na. 7 ya Mwaka 2010. Ili kutekeleza Sheria ya mwaka 1989 hususan katika kusimamia rasilimali za uvuvi zilizopo kwenye eneo la ukanda wa uchumi wa bahari ya Tanzania (EEZ) lenye ukubwa wa kilomita za mraba 223,000, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) zilikubaliana kwa pamoja kuunda Taasisi (Mamlaka) ya Muungano yenye wajibu wa kusimamia uvuvi wa eneo hilo la Uchumi la Bahari na pia Bahari Kuu kwa meli zenye kupeperusha Bendera ya Tanzania alisema Simbachawene.

Akihitimisha alisema kuwa, Uvuvi wa Bahari Kuu unatambulika Kimataifa kupitia Sheria ya Kimataifa ya Bahari ya mwaka 1982 hata katika mikutano mbalimbali ya kimataifa Tanzania huwakilishwa kama Nchi.

Watu 10 Washikiliwa na Jeshi la Polisi Kagera kwa Tuhuma za wizi wa Mtihani Darasa la Saba.

0
0
Kamanda wa Polisi Mkoani Kagera. Revocatus Malimi akitoa taarifa kwa wanahabari.

Watu 10 Wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Kagera kwa Tuhuma za wizi wa Mtihani Darasa la Saba, Tukio hilo limetokea Wilayani Ngara Mkoani Kagera Tarehe 12 Septemba likiwahusisha Walimu watano na Wasimamizi watano akiwemo Mkuu wa Shule Husika, Shule ya Msingi Kumnazi.

WAZIRI JAFO AUPONGEZA UONGOZI WA HALMASHAURI WILAYA YA MBULU

0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akipokea taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Hudson Kamoga wakati wa ziara yake ya kikazi Wilayani humo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akizungumza wakati akikagua ujenzi wa Hospital ya Wilaya ya Mbulu inayoendelea kujengwa Wilayani hapo
Muonekano wa baadhi ya majengo ya Hispital ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu yanayoendelea kujengwa Wilayani hapoWaziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akiagana na viongozi wa Halmashauri ya Mbulu wakati wa ziara yake Wilayani humo.

………………….

Nteghenjwa Hosseah, Dongobesh

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amepongeza Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu kwa usimamizi makini wa ujenzi wa Hospital ya Wilaya inayoendelea kujengwa katika kata ya Dongobesh.

Waziri Jafo ametoa pongezi hizo baada ya kutembelea eneo linapojengwa Hospital ya Wilaya na kuridhishwa na hatua iliyofikiwa katika ujenzi huo ukiacholia mbali changamoto walizokutana nazo wakati wa ujenzi.

Hakina Mbulu nimewaelewa Hospital ya Wilaya inavutia mmejenga majengo mazuri yenye ubora unaotakiwa na mmezingatia maagizo tuliyotoa katoka ujenzi wa hospital hizi za Wilaya

Mmenifurahisha ingawa majengo yenu hayajakamilika lakini nimeziskia changamoto mzilokutana nazo na namna mlivyokabiliana nazo kwa sababu hazikua kikwazo cha kukwamisha kazi hii mmeweza kuzitatua na ujenzi ukaendelea kama kawaida.

“Mbulu mmewapita hata Halmashauri zingine ambazo hawakuwa na changamoto zozote nyie mmekabiliana na changamoto za kutosha lakini bado kazi yenu imekua nzuri na inayopendeza hongereni sana na muendelee na kazi hii nzuri kwenye miradi mingine” Alisema Jafo.

Pia Waziri Jafo amempongeza Mbunge wa Halmashauri ya Mbulu Mhe. Flatei Massay kwa jitihada zake anazozifanya za kutetea wananchi na kuhakikisha wanapata miradi ya maendeleo.

Mbunge wenu anawapenda sana watu wa Mbulu anapambana kuhakikisha miradi mingi ya maendeleo inawafikia wananchi wake na kuleta maendeleo katika Jimbo la Mbulu Vijijini alisema Jafo.

Msidhani kuwa miradi hii imekuja kwenu kwa bahati tu kuna jitihda kubwa zimefanyika mpaka mkapata fedha za ujenzi wa Jengo la Halmashauri , mkajengewa kituo cha Afya Dongobesh na zadi mkapata tena Tsh Bil 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa hospital za Wilaya hii ni miradi mingi sana kwa Halmashauri moja kuipata katika kipindi chwa mwaka mmoja wa fedha.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mbuli Mhe. Chelestino Mofugo amesema pamoja na changamoto walizokutana nazo wakati wa ujenzi, Wananchi wa Dongobesh wametoa ushirikiano wa kutosha wakati wote wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

“Mhe. Waziri Jafo napenda ufahamu kuwa wananchi wa Dongobesh ndio waliotupa hili eneo bure kabisa kwa ajili ya ujenzi wa Hospital ya Wilayah ii inaonyesha utayari wa hali ya juu ya wananchi hawa kuipokea Halmashauri ya Wilaya kuhamia katika eneo hili na hili limetusaidia sana katika kufanikisha ujenzi wa hospital yetu hii unayoiona” alisema Mhe. Mofugo.

Akisoma Taarifa ya ujenzi wa Hospital ya Wilaya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbulu Hudson Kamoga alisema changamoto kubwa liyokutana nayo wakati wa kuanza ujenzi ni pamoja ni miamba migumo ya eneo la hospital pamoja na kuwa na maeneo oevu ambayo kwa kiasi kikubwa yalirudisha nyumba kasi ya ujenzi.

“Hii changamoto ya kukutana na mwamba mgumu ilitulazimu kutafuta milipuko na wataalam wa kuilipua ili kutoa huo mwamba lakini tulijitahidi kadiri ya uwezo wetu kulifanyia kazi kwa haraka na kufanikiwa kuondoa mwamba huo kisha ujenzi ukaendelea” alisema Kamoga.

Pia Kamoga aliotoa ombi maalumu kwa Waziri Jafo kuwa wanaomba kupatiwa Mhandisi wa Halmashauri au mafunzi mchundo ili awasaidie katika kusimamia miradi ya ujenzi kwa kuwa aliyepo sasa anazidiwa na kazi na endapo inatokea anapata dharura kazi zote za ujenzi zinasimama kwa muda kusubiri amalize dharura yake ili ahakiki ubora wa kazi.

Ujenzi wa hospital ya Wilaya ya Mbulu umefikia asilimia 80 na ni moja wapo ya hospital za Wilaya 67 zinazoendelea kujengwa Nchi Nzima.

DAWASA WAKABIDHI MRADI WA MAJI WA MANEROMANGO KWA RUWASA

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam DAWASA wamekabidhi vifaa vya mradi wa maji wa Kisima kwa Mamlaka ya maji Vijijini RUWASA kwa ajili ya kuutekeleza kwenye Mji wa Kisarawe.

Mradi huo utapeleka maji kwenye Shule ya Sekondari Maneromango na kutatua tatizo la maji kwa wanafunzi na walimu wa shule hiyo.

Akizungumza baada ya kupokea vifaa, Mkuu wa Shule ya Sekondari Maneromango Pili Jabir ameishukuru Mamlaka ya Dawasa kwa kuweza kuwapelekea maji kwenye shule yao kwani wamekuwa na adha ya maji kwa muda mrefu.

Amesema kumekuwa na kero ya maji katika shule hiyo na wanafunzi wamekuwa wanaenda kuchota maji kwenye visima vya wanakijiji kitu kinachopelekea kutopata muda toshelezi wa masomo.

" Napenda kuwashukuru Dawasa kwa kutuletea mradi huu, utawasaidia wanafunzi kuepukana na shida ya maji safi na salama iliyokuwa kwa muda mrefu na utawasaidia kupata muda mwingi wa kujisomea,"amesema Pili.

Kwa upande wa Mhandisi wa RUWASA Wilaya ya Kisarawe, Ally Nzwenge amesema wamepokea mradi huo wa kupeleka maji kwenye Shule ya Sekondari Maneromango na wanaahidi kuufanyia kazi ili kuondoa kero ya maji kwa wanafunzi.

"Mradi huu tutautekeleza kulingana na usanifu uliokuwa tayari umeshafanywa na Dawasa na wanashukuru sana kwa kuwakumbuka wanafunzi hao,"

Nzwenge amesema, kukamilika kwa mradi huu kutaondoa magonjwa ya mlipuko yaliyokuwa yanawakuta wanafunzi kwa kukosa maji safi na salama na pia utawasaidia kupunguza muda mwingi wa kwenda kuchota maji vijiji vya jirani.

Makabidhiano ya mradi huo yamefanywa na Mhandisi Lilian Masirago ukishuhudiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii Neli Msuya na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Maneromango Pilo Jabir.

Vifaa hivyo vilikabidhiwa kwa Mwalimu Mkuu ambavyo ni pamoja na mabomba, mita ya kusoma maji, pampu, tanki lenye ujazo wa lita 10,000 na vingine vitakavyotumika kwenye mradi huo.
Mhandisi kutoka DAWASA Lilian Masirago na Mhandisi wa RUWASA Wilaya ya Kisarawe, Ally Nzwenge wakisaini makabidhiano ya mradi wa maji wa Shule ya Sekondari Maneromango utakaotatua changamoto ya maji kwa muda mrefu. Makabidhiano hayo yameshuhudiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii Neli Msuya (wa pili kushoti)na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Maneromango Pili Jabir (wa kwanza kushoto) na wafanyakazi wengine wa Mamlaka hiyo.
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Jamii Neli Msuya akimkabidhi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Maneromango Pili Jabir vifaa vya ujenzi wa mradi wa maji utakaosaidia kutatua kero ya maji kwenye shule hiyo kwa muda mrefu. Wengine ni wafanyakazi wa DAWASA na RUWASA.
Mabomba yatakayotumika kusambaza maji kwenye mradi wa maji wa Shule ya Sekondari Maneromango Kisarawe.
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live




Latest Images