Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110160 articles
Browse latest View live

Majeruhi watatu ajali ya moto Morogoro waruhusiwa

$
0
0
 Daktari Bingwa wa Upasuaji, Dkt.Edwin Mrema akiongea na waandishi wa habari kuhusu hali za majeruhi wa ajali ya moto wanaoendelea kupatiwa matibabu.
 Kutoka kulia ni Shabani Abdalla Omary na Mikidaki Issa ambao ni majeruhi wa ajali ya moto walioruhusiwa leo wakiwa kwenye picha ya pamoja na madaktari na wauguzi waliowahudimia.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo.

MAJERUHI watatu kati ya 11 wa ajali ya moto wanaoendelea kupatiwa matibabu Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wameruhusiwa kutoka hospitalini leo baada ya afya zao kuanza kuimarika.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Daktari Bingwa wa Upasuaji ambaye pia ni mtaalamu wa kutibu majeraha ya moto Dkt. Edwin Mrema, amesema kuwa majeruhi hao wameruhusiwa kwa kuwa afya zao zimeanza kuimarika na kuelekeza kuwa watahitajika kuhudhuria kliniki ya wagonjwa wa nje ili kufuatilia maendeleo ya afya zao.

“Hadi kufikia leo tuna wagonjwa kumi na moja miongoni mwao ni hawa wawili na mmoja ataruhusiwa kesho, hawa wagonjwa tuliwapokea wakiwa katika hali ya hatari zaidi lakini leo tumefikia hatua ya kuwaruhusu kwenda nyumbani maana yake hali ya hatari waliyokuwa nayo imetoka, na sehemu kubwa ya vidonda walivyokuwa navyo vimepona, upumuaji wao ni nzuri na afya zao kwa ujumla zinaruhusu, lakini wataendelea kuja Hospitali kuhudhuria kliniki ya nje” alifafanua Dkt. Mrema.

Pamoja na kufuatilia mwenendo wa matibabu yao, amesema wataendelea kuhudhuria kliniki ya saikolojia ili kuwahimairisha zaidi kifikira. 

Dkt. Mrema amesema wagonjwa wameanza kupatiwa huduma za mazoezi ya viungo (physiotherapy) kwani majeraha ya moto walioyapata yanaweza kusababisha baadhi ya viungo visikae sawa.

Aidha, Dkt. Mrema amesema kuna wagonjwa wawili ambao kutokana na kuugua sana ilibidi kuwafanyia upasuaji kuondoa baadhi ya viungo ili kuokoa maisha yao,lakini kwa sasa hali zao zinaendelea vizuri.

Katika hatua nyingine, mmoja wa majeruhi aliyeruhusiwa Bw. Shabani Abdalla Omary amemshukuru kwa dhati Mh. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwatembelea hospitali hapo pamoja na kuwagharamia gharama zote za matibabu na pia ameshukuru madakrati na wauguzi wa MNH kwa huduma nzuri waliyowapa kipindi chote cha matibabu.

“Namshukuru Rais, alifika kutuona na akatupatia kiasi cha fedha Mungu ambariki sana sina cha kumlipa, lakini pia nawashukuru sana wauguzi na madaktari wa MNH kwa sababu nilivyofika hapa nilikuwa na hali ngumu mno ila kwa sasa naendelea vizuri” amesema Bw. Omary.

VIJANA WAMETAKIWA KUONGEZA THAMANI YA MAZAO YA NAFAKA

$
0
0
 Mratibu wa Shirika lisilokua la kiserikali la INFOY ,Laurent Sabuni

Na  Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha
MRATIBU wa Shirika lisilokua la kiserikali la infoy Laurent amewataka Vijana wa Kitanzania  kuchangamkia fursa ya kuongeza thamani mazao na kuyafungasha katika viwango vya ubora wa hali ya juu ili yaweze kukubalika katika masoko ya ndani ya nje

Sabuni amesema hayo katika mkutano wa wadau kutoka asasi za kiraia zinazojishughulisha na vijana ambazo zinafadhiliwa na The Foundation for Civil Society  ambapo amesema kuwa  wamekua wakitoa mafunzo ya usindikaji wa bidhaa za chakula hususan lishe pamoja namna ya kuzifungasha bidhaa hizo ili kupanua wigo wa fursa kwa vijana.

"Vijana licha ya kujishughulisha na ujasiriamali pia wanapaswa kuongeza thamani ya mazao ya nafaka kama mahindi,ngano na hata mazao ya mifugo kuyachakata na kuyafungasha vizuri na kuyafikisha sokoni yakiwa katika hali nzuri ya kuvutia masoko ya ndani na nje" Alisema Sabuni

Kwa upande wao vijana Fransisca Wilson  amesema kuwa tayari wameanza kutengeneza unga wa lishe kwa kutumia nafaka hivyo kuwasaidia kuinua kipato chao na kuchangia maendeleo katika jamii zao.

Leonard Paulo amesema kuwa mwamko wa vijana katika kuongeza thamani umeongezeka huku changamoto kubwa ikiwa ni mtaji wa kuanzia biashara zao na kununua mazao kwa kulima pamoja na mashine za kuchakata mazao na kutengeneza bidhaa.

 Afisa Vijana na Maendeleo Jiji la Arusha Hanifa Ramadhani alisema kuwa  vijana hao wanapaswa kusindika bidhaa za nafaka na kutengeneza bidhaa mbalimbali ambazo zinahitajika katika jamii badala ya kuacha mazao ya wakulima wakati mwingine yamekua yakiharibika kwa kukosa soko Na pia kutokuongezwa thamani jukumu ambalo inapaswa lifanywe na vijana. 

FUATILIENI MTOTO ALIYEKATWA MKONO MWANANYAMALA: DKT. NDUGULILE

$
0
0
Aliyekuwa mjumbe wa bodi iliyoisha muda wake Dkt. Charles Massambu akipokea cheti cha shukrani kutoka kwa Naibu Waziri Dkt. Faustine Ndugulile.
Kaimu Msajili wa bodi ya Maabara binafsi Dickson Majige akipokea cheti cha shukrani wakati wa uzinduzi huo.
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alipokua akiongea wakati wa uzinduzi wa bodi ya maabara binafsi za afya kwenye ukumbi wa hoteli ya Veta jijini Dodoma
Kaimu Mwenyekiti wa bodi hiyo Prof. Said Abood akitoa neno la shukrani mara baada ya uzinduzi wa bodi ya maabara binafsi za afya ambapo aliahidi kufanya ukaguzi wa kuzibaini maabara ambazo hazijasajiliwa nchini
Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Vivian Wonanji akiongea na washiriki waliohudhuria uzinduzi wa bodi hiyo
Picha ya pamoja mgeni rasmi na wajumbe wa bodi iliyomaliza muda wake

Naibu Waziri Dkt. Faustine Ndugulile akiwa kwenye picha ya pamoja na bodi mpya ya nane ya baraza la maabara binafsi za afya

Baadhi ya wasajili wa mabaraza ya kitaaluma yaliyo chini ya wizara ya afya wakimsikiliza Naibu Waziri(hayupo pichani) wakati wa uzinduzi huo

Msajili wa baraza la maabara binafsi za afya Dominic Fwiling’afu akiongea wakati wa uzinduzi.huo



………………..
Na. Catherine Sungura –Dodoma
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee wa Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amemuagiza Msajili wa Baraza la Madaktari la Tanganyika kushirikiana na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania kufuatilia mtoto aliyekatwa mkono baada ya kuhamishiwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa ya Mwananyamala.
Dkt. Ndugulile ametoa maagizo hayo wakati akizindua bodi ya nane ya maabara binafsi za afya kwenye ukumbi wa Veta jijini hapa.
“Nilitegemea baraza la madaktari muwe mmeanza uchunguzi, kwahiyo nakupa maagizo kesi hiyo muanze kufuatilia na kama itathibitika ni uzembe waliohusika wachukuliwe hatua, ndani ya wiki mbili mtuletee majibu ili mimi na Mhe. Waziri tujue tunachukua hatua gani.
Dkt. Ndugulile amesema kwenye mabaraza bado kuna changamoto ya baadhi ya mashauri kuchukuliwa hatua hivyo kama mabaraza ya kitaakluma ni vyema kuangalia ufanisi wa majukumu yao na kuchukulia hatua pale taaluma inapokosewa na waliokosea wachukuliwe hatua.
Dkt. Ndugulile ameitaka bodi hiyo kusimamia usajili wa maabara zote nchini kwani hivi sasa imetokea uanzishwaji wa maabara kiholela zinazotoa huduma kwa wananchi bila ya kusajiliwa hivyo kufanya ukaguzi ili kubaini maabara hizo na kuzichukulia hatua.
“Naomba sheria ifuate mkondo wake ili kubaini wale wote walioanzisha huduma za maabara bila kufuata sheria na taratibu za usajili, tushirikiane kuhakikisha kuwa hakuna taasisi au mtu atakayefungua au kutoa huduma za maabara bila kusajiliwa”. Amesisitiza Dkt. Ndugulile.
Aidha, Naibu Waziri huyo amesema baraza hilo ni chombo muhimu na ndio moyo wa sekta ya afya kwani maabara inatoa muelekeo wa mgonjwa kwa kuthibitisha tatizo, hivyo inahitajika maboresho katika utoaji huduma za maabara.
“Sasa hivi huduma hizi zimekua ni biashara kwani asiliamia 70 ya homa wala sio Malaria ni virusi watu wanakunywa dawa sana pasipo kuzingatia misingi kwani maabara hizi zinatumika kama sehemu ya matibabu na hata upasuaji, mtu anaenda maabara anakaa dakika kumi na tano anaambiwa ana UTI wakati mwingine anaambiwa ana malaria plasi plasi hii maana yake ni nini hili linahitaji ufuatiliaji”. Alisema Dkt. Ndugulile.
Hata hivyo aliitaka bodi hiyo mpya kusimamia ubora wa huduma za maabara ili kuinufaisha jamii na kuhakikisha huduma za afya katika jamii zinaboreshwa kukidhi viwango vitavyotarajiwa na hivyo kuboresha afya na maisha ya watanzania.
Naye Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la maabara binafsi Prof. Said Abood aliahidi kutekeleza maagizo yote waliyopewa na Naibu waziri ikiwemo ya kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kubaini maabara bubu na ambazo hazijasajiliwa pamoja na kuhakikisha maabara zinatoa huduma zinazostahili ili kuweza kumsaidia daktari kumpatia mwananchi huduma stahili.

WIZARA YA AFYA YAPATA BILIONI 26.6 KUTOKA SERIKALI YA UJERUMANI

$
0
0
Na. Catherine Sungura- Dodoma

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesaini mkataba wa makubaliano wa miaka mitatu na serikali ya Ujerumani kwa ajili ya kuimarisha afya ya msingi nchini.

Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Zainabu Chaula alisema kuwa wizara yake imesaini mkataba huo na serikali ya Ujerumani katika kuboresha sekta ya afya katika maeneo manne ambapo sekta hiyo itapata kiasi cha shilingi za kitanzania Bilioni 26.6.

Dkt. Chaula amesema kwamba kwa mwaka huu wameweka makubaliano ili fedha hizo zitolewe kwa wakati mmoja na kuweza kutumia mfumo wa Force Akaunti kama walivyoweza kutumia kwenye ujenzi wa Vituo vya afya na Hospitali za Wilaya na Mikoa katika kuboresha sekta ya afya nchini.

“Tumeanza mahusiano tangu mwaka 1961, kuanzia mwaka 2003 huu ni mkataba wa tano na mkataba wao ni wa miaka mitatu mitatu ambapo umejikita katika kuimarisha afya ya msingi katika halmshauri zetu katika vituo vya afya pamoja na zahanati”.

Dkt. Chaula alitaja maeneo yatakayonufaika na mkataba huo ni uhimarishaji wa taarifa, afya ya mama na mtoto, uzazi wa mpango, bima ya afya kwa akina mama wajawazito pamoja na utawala bora jinsi ya kutumia fedha hizi kulingana na kanuni na taratibu za nchi.

“Huu ni muendelezo wa mkataba wa miradi mingi ambayo tumeifanya katika kuboresha sekta ya afya, kama mnavyokumbuka hadi sasa hivi tumeshafanyia ukarabati wa vituo vingi vya afya ambapo tuna vituo 470 ambavyo vimeshafanyiwa ukarabati tangu mwaka 2017 katika ngazi za zahanati, vituo vya afya na hospitali za wilaya.

Aidha, Dkt. Chaula alisema Serikali iliwekeza shilingi bilioni mia moja na milioni mia tano katika hospitali za halmashauri.

“Zamani hawa wenzetu walikua wakitumia wakandarasi wao na pesa wanakaa nazo hivyo tumekaa nao na kukubaliana kama fedha hizi watazitoa kwa wakati mmoja ili tuweze kuzisimamia kama tulivyofanya kwenye vituo tulivyoanza ili kuweza kutekeleza kwa umakini na kupata matokeo makubwa katika kipindi hiki” . Amesema Dkt. Chaula. 

Kwa upande wa hali ya uzazi, mama na mtoto Katibu Mkuu huyo alisema hivi sasa inakaribia asilimia 80 ya akina mama wajawazito wanajifungulia kwenye vituo vya afya tofauti na zamani ambapo kulikuwa na changamoto kubwa kwani wengi walikua wanajifungulia majumbani kwa asilimia 39 na kufuatia na asilimia 59 hii ni kutokana na kuboreshwa kwa vituo vya afya pamoja na mikakati mbali mbali ya kuhakikisha akina mama wote wanajifungulia kwenye vituo vya afya.
 Mwakilishi Mkazi wa Shirika la giz Dkt. Mike Falke akisaini mkataba wa makubaliano na serikali ya tanzania kupitia wizara ya afya katika kuimarisha afya ya msingi nchini, kushoto ni katibu mkuu wa wizara hiyo Dkt. Zainab Chaula
 Katibu Mkuu Idara kuu Afya Dkt. Zainabu Chaula akisaini mkataba huo wa shilingi bilioni 26.6 kutoka Serikali ya Ujerumani,halfa hiyo ilifanyika kwenye ukumbi wa wizara uliopo mji wa serikali Mtumba.
 Viongozi hao wakibadilishana mikataba hiyo mara baada ya kusaini
Mwakilishi wa Serikali ya Ujerumani.Bi. Vera Rosendahl akizungumza wakati wa kusaini mkataba kati ya nchi yake na Serikali ya Tanzania
Katibu Mkuu Dkt. Zainab Chaula akimuonesha kitabu cha masuala ya mama na mtoto Bi. Vera  Rosendahl mwakilishi kutoka Serikali ya Ujerumani

Viongozi wa Wizara na serikali ya Ujerumani wakati wa mazungumzo ya pamoja katika kuboresha sekta ya afya
 Picha ya pamoja ya Katibu Mkuu Dkt. Zainab Chaula na baadhi ya viongozi wa  giz na serikali ya Ujerumani mara baada ya kusainiana mkataba

MAKAMU WA RAIS ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO UBALOZI WA ZIMBABWE

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitia saini kitabu cha kumbukumbu ya Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Zimbabwe Mzee Robert Mugabe alipofika katika Ubalozi wa Zimbabwe Oysterbay Jijini Dar Es Salaam leo Septemba 12, 2019.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Naibu Balozi wa Zimbabwe Nchini Mhe. Martin Tavenyika alipofika katika Ofisi ya Ubalozi wa Zimbabwe Nchini Tanzanai kwa ajili ya kutia saini kitabu cha kumbukumbu ya Maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Zimbabwe Mzee Robert Mugabe alipofika katika Ubalozi wa Zimbabwe Oysterbay Jijini Dar Es Salaam leo Septemba 12, 2019.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

NEWZ ALERT:RAIS DKT MAGUFULI AMTEUA KAMISHNA DIWANI ATHUMANI KUWA MKURUGENZI MKUU WA IDARA YA USALAMA WA TAIFA, AMWAPISHA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Kamishna Diwani Athuman Msuya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Ikulu Jijini Dar es Salaam, ambaye anachukua nafasi ya Dkt. Modestus Kipilimba.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Kamishna Diwani Athuman Msuya akitia sahihi hati ya kiapo mara baada ya kuapishwa  kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Ikulu Jijini Dar es Salaam, ambaye anachukua nafasi ya Dkt. Modestus Kipilimba
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini hati ya kiapo mara baada ya kumuapisha Kamishna Diwani Athuman Msuya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Ikulu Jijini Dar es Salaam, ambaye anachukua nafasi ya Dkt. Modestus Kipilimba 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi vitendea kazi Kamishna Diwani Athuman Msuya mara baada ya kumuapisha kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Ikulu Jijini Dar es Salaam, ambaye anachukua nafasi ya Dkt. Modestus Kipilimba.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Kamishna Diwani Athuman Msuya akiapa kaipo cha Maadili kwa Viongozi wa Utumishi wa Umma mara baada ya kuapishwa  kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Ikulu Jijini Dar es Salaam, ambaye anachukua nafasi ya Dkt. Modestus Kipilimba. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kumuapisha Kamishna Diwani Athuman Msuya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Ikulu Jijini Dar es Salaam, ambaye anachukua nafasi ya Dkt. Modestus Kipilimba  
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Kamishna Diwani Athuman Msuya mara baada ya kumuapisha kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Ikulu Jijini Dar es Salaam, ambaye anachukua nafasi ya Dkt. Modestus Kipilimba 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na  Kamishna Diwani Athuman Msuya mara baada ya kumuapisha kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Ikulu Jijini Dar es Salaam, ambaye anachukua nafasi ya Dkt. Modestus Kipilimba. Picha na Ikulu



SERIKALI KUWEZESHA WAKALA WA MBEGU ZA KILIMO (ASA) KUONGEZA UZALISHAJI WA MBEGU BORA NA KUIMARISHA SOKO LA ZAO LA NAZI

$
0
0
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe (Mb) akijibu swali bungeni leo tarehe 12 Septemba 2019 wakati wa mkutano wa kumi na sita wa Bunge la miswada Jijini Dodoma.(Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akijibu swali bungeni leo tarehe 12 Septemba 2019 wakati wa mkutano wa kumi na sita wa Bunge la miswada Jijini Dodoma.


Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma


Upatikanaji wa mbegu bora zikiwemo za mahindi ngano, maharage, mpunga, soya, alizeti, mtama, ufuta, viazi mviringo na mbegu za mazao ya bustani kwa msimu wa 2018/19 ulifikia tani 49,040 kati ya hizo tani 38,507 sawa na asilimia 78.6 zilizalishwa nchini na tani 8,361 sawa na asilimia 17 ziliagizwa nje ya nchi na tani 2,171 sawa na asilimia 4.4 ni bakaa ya msimu wa 2017/2018.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe ameyasema hayo leo tarehe 12 Septemba 2019 wakati akijibu swali la Mbunge wa Kasulu Mjini Mhe Daniel Nsanzugwanko mkakati wa serikali katika kutatua uhaba mkubwa wa mbegu hasa za mahindi na maharage ambayo ni mazao ya chakula na namna ambavyo serikali itajikita katika uzalishaji wa mbegu.

Alisema kuwa Mikakati ya Serikali ya kuongeza uzalishaji wa mbegu ni pamoja na kuwezesha Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) kuongeza uzalishaji wa mbegu bora katika mashamba ya Mwele, Dabaga, Mbozi, Msimba, Bugaga na Arusha; kutumia Taasisi za Utafiti wa Kilimo kuzalisha mbegu mama, msingi na zilizothibitishwa ubora na kukodisha maeneo katika mashamba ya ASA kwa kampuni binafsi za mbegu ili kuongeza uzalishaji wa mbegu bora za mazao mbalimbali ikiwemo mahindi na maharage.


Aidha, mikakati mingine ni kuongeza eneo la umwagiliaji katika mashamba ya mbegu ya Msimba, Arusha, Dabaga na mashamba ya Vituo vya Utafiti kutoka hekta 200 hadi 600;kushirikisha taasisi za umma kama Jeshi la Magereza na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kuzalisha mbegu borapamoja na vikundi vya wakulima wadogo kuzalisha mbegu za Daraja la Kuazimiwa ubora.


Mhe Bashe alisema kuwashamba la mbegu la Bugaga lililopo katika Wilaya ya Kasulu lina ukubwa wa hekta 200. Shamba hilo linamilikiwa na ASA na kwa sasa linatumika kuzalishia mbegu bora za mahindi, maharage na alizeti. Aidha, shamba hilo linatumika kuzalisha miche bora ya michikichi, miche ya matunda ya machungwa na maembe.


Pia serikali imeanza kuchimba kisima cha maji katika shamba hilo ili kuwezesha uzalishaji wa mbegu kwa kipiti chote cha mwaka. Vilevile, ASA imejenga kitalu nyumba cha kukuzia miche ya chikichi pamoja na kuandaa bustani ya kukuzia miche hiyo ya michikichi na miche ya matunda.


Aliongeza kuwaMkakati wa Serikali ni kuongeza uzalishaji wa mbegu ambapo Serikali katika mwaka wa fedha 2019/20 imetenga takribani shilingi bilioni 13 kwa ajili ya utafiti wa mbegu kupitia Taasisi ya Utafiti wa Mbegu-TARI na uzalishaji wa mbegu kupitia Wakala wa Mbegu za Kilimo –ASA kwa ajili ya kuzalisha mbegu kwa njia ya umwagiliaji ili kuongeza uzalishaji mara tatu hadi nne zaidi ya sasa. "Aidha, nitumie fursa hii kuzisihi halmashauri kutotumia maeneo yaliyotengwa kwa tafiti za kilimo kwa shughuli zingine ikiwemo kujenga stendi za mabasi" Alikaririwa Mhe Bashe


Kadhalika, Wizara ya Kilimo itaamua kuyaachia maeneo hayo kwa shughuli zingingine baada ya kujiridhisha kwamba maeneo hayo hayana tija kwa shughuli hizo za kilimo.


Naye Naibu waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akijibu swali la mbunge wa viti maalum Zaynab kuhusu serikali kutafuta soko la zao la nazi alisema kuwa Soko la kudumu la zao la nazi lipo nchini kwa sababu kiasi cha nazi kinachozalishwa bado hakikidhi mahitaji ya soko la ndani ya nchi kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya zao hilo ikiwemo ulaji wa madafu na watumiaji wa nazi.


Aidha, mafuta mwali yanayotokana na nazi yanaendelea kupata umaarufu kutokana na uhitaji wake kuwa mkubwa ndani na nje ya nchi, ambayo lita moja inafika hadi Shilingi 40,000/=. Bidhaa kama fagio, mbao, kamba na samani zinazotokana na mti wa mnazi na uwezo wa zao hilo kutunza mazingira huongeza thamani ya zao la minazi.


Alisema kuwa Katika kuimarisha soko la zao la nazi nchini msimu wa mwaka 2018/2019 wakulima wapatao 74 katika mikoa ya Lindi na Mtwara wamefundishwa namna ya kukamua mafuta mwali.


Vilevile, kikundi cha wanachama 50 katika Wilaya ya Bagamoyo kimepewa mashine yenye uwezo wa kukamua lita 500 za mafuta mwali kwa mwaka. Aidha, Serikali inaendelea kuimarisha masoko ya mazao yote ya kilimo likiwemo zao la nazi kwa  kuwaunganisha wakulima na wanunuzi kupitia vyama vya ushirika, masoko ya moja kwa moja na viwanda vidogo  vya kuongeza thamani ya zao la nazi.


Mhe Mgumba amesema, Serikali inaendelea kutoa elimu kwa wazalishaji wa zao la nazi kuendelea kupanda mbegu bora zenye ukinzani dhidi ya magonjwa na zenye tija  kubwa. Tanzania ni nchi ya kumi duniani kwa uzalishaji wa nazi ikiongozwa na nchi ya Indonesia na kwa Afrika ni nchi ya kwanza ambapo huzalisha wastani wa tani 530,000 za nazi kwa mwaka ikifuatiwa na Ghana ambayo huzalisha wastani wa tani 366,183.


Aidha, Serikali inaendelea kuhamasisha kilimo cha minazi nchini ambapo imeanzisha shamba lenye ukubwa wa hekta 54 katika kituo kidogo cha utafiti cha Chambezi Wilaya ya Bagamoyo ili kuzalisha miche bora  ya minazi yenye ukinzani dhidi ya ugonjwa wa kunyong’onyea kwa minazi (Coconut Lethal Disease) na kuisambaza kwa wakulima kwa gharama nafuu.


Aliongeza kuwa Serikali inahamasisha kilimo cha minazi katika maeneo mapya ili kuongeza uzalishaji wa nazi nchini ambapo msimu wa 2018/2019 ilizalisha na kusambaza jumla ya mbegu 11,000 kwa wakulima katika mikoa ya Rukwa na Mwanza. Aidha, Serikali inafanya mazungumzo na Jumuiya ya Asia - Pasific Coconut Community (APCC) ambayo hutunza “germplasm” ya minazi kuwezesha upatikanaji wa mbegu bora za minazi zenye kuongeza tija kwa wakulima.

TOZENI BILI ZA MAJI ZISIZOWAUMIZA WANANCHI-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Maji ifuatilie utendaji wa Mamlaka zilizopewa dhamana ya kusimamia miradi ya maji katika maeneo mbalimbali nchini na ihakikishe kwamba bili wanazotozwa wananchi zinakuwa na uhalisia na si kuwaumiza.

Ametoa agizo hilo baada ya kuibuka wimbi la malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu upandaji wa bili za maji ambao hauna uhalisia kwa sababu Serikali ndiyo inayotoa fedha za miradi hiyo nchini.”Serikali haitakubali wala haitoruhusu mwananchi anatozwa gharama kubwa za maji.”

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Alhamisi, Septemba 12, 2019) Bungeni jijini Dodoma katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu wakati akijibu swali la Mbungewa Viti Maalumu, Mariam Kisangi, aliyetaka kujua kauli ya Serikali kuhusu suala hilo.

“Yako maeneo ambayo mamlaka zilizopewa dhamana ya kusimamia miradi ya maji kumejitokeza wimbi la mabadiliko ya kuhusu kupanda kwa bei za bili, mfano wilayani Maswa mkoani Simuyu bei imeongezeka kutoka sh. 5,000 hadi 28,000 kwa mwezi.”

“Bei hizo hazina uhalisia na hakuna sababu ya mamlaka kuzoza bei kubwa kiasi hicho na kuwafanya wananchi washindwe kumudu kulipia bili zao, wakati Serikali ndio imetoa fedha za kugharamamia uanzwishwaji wa miradi hiyo na haijadai kurudishiwa fedha hizo.”

Waziri Mkuu amesema Wizara ya Maji kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) ifuatilie bei za bili wanazotozwa wananchi ili kujiridhishwa kwamba zinazingatia uwezo wa wananchi wengi kuzilipa hasa wale wa vijijini.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amewaagiza Wakuu wa Mikoa, Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Maafisa Kilimo na Maafisa Biashara kote nchini wasimamie katika masoko yote na wajirishe iwapo vipimo vinavyotumika ni sahihi kwani lumbesa haikubaliki.

Ametoa agizo hilo wakati akijibu swali la Mbungewa Jimbo la Mlalo, Rashid Shangazi aliyetaka kupata kauli ya Serikali kuhusu hatua zilizochukuliwa katika kudhibiti unyonyaji wanaofanyiwa wakulima kupitia ufungaji wa mazao unaozidi viwango.

Waziri Mkuu amesema wanunuzi wa mazao mbalimbali lazima wafuate sharia, kanuni na taratibu za manunuzi ya mazao husika. “Maafisa Kilimo wasimamie biashara hiyo na waendeshe operesheni kwenye maeneo ya masoko ili kujirishana vipimo vinavyotumika.”

Amesema ni muhimu zaidi kutumia mizani ambayo haina utata ili kuwawezesha wakulima kuweza kunufaika kutokana na kilimo na kwamba suala la waununuzi kutumia vipimo visivyosahihi kama lumbesa halikubaliki.

Akijibuswali la Mbunge wa Sumve, Richard Ndasa aliyetaka kupata kauli ya Serikali kuhusu kuhusu suala la ununuzi wa zao la pamba, Waziri Mkuu amesema Serikali imelifanyia kazi suala hilo na tayari zaidi ya tani 200,000 zimeshanunuliwa ambayo ni sawa na asilimia 80.

Waziri Mkuu amewahakikishia wakulima wa zao la pamba kwamba pamba yote iliyosailia majumbani itanunuliwa. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akijibu maswali, Bungeni jijini Dodoma, Septemba 12.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kushoto) Bungeni jijini Dodoma, Septemba 12.2019. Katikati ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, George Simbachawene. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, katika viwanja vya Bunge, jijini Dodoma, Septemba 12.2019.


WALIOKUWA WAFANYAKAZI NA WATEJA WA BENKI YA FBME KULIPWA AMANA

$
0
0
Na Peter Haule na Josephine Majura, WFM, Dodoma
SERIKALI imeeleza kuwa itawalipa waliokuwa wateja na wafanyakazi wa Benki ya FBME baada ya taratibu za kisheria na majadiliano na Cyprus yatakapo kamilika hivi punde.
Hayo yamesemwa Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), wakati akijibu maswali ya Mhe. Jaku Ayoub, aliyetaka kujua Benki ya FBME ipo katika hali gani na ni lini italipa wateja amana zao.
Dkt. Kijaji alisema kuwa wateja wa Benki ya FBME waliokuwa na amana ya milioni 1.5 Serikali imewalipa kwa zaidi ya asilimia 83 ya wateja wote, asilimia 17 iliyobaki ni ya wateja ambao hawajajitokeza kuchukua amana hizo.
“Bodi ya Bima ya Amana (Deposit Insurance Board- DIB) ilianza zoezi la kulipa fidia kwa mujibu wa sheria kwa waliokuwa na amana katika benki hiyo kuanzia Novemba, 2017 na bado zoezi hilo linaendelea”, alieleza Dkt. Kijaji.
Alisema kuwa hadi kufikia Septemba 9, 2019 jumla ya kiasi cha Sh. milioni 2,404.2 kimelipwa kwa wateja 3426 kama fidia ya bima ya amana, ambapo kiasi hicho ni sawa na asilimia 55.9 ya kiasi chote kilichotarajiwa kulipwa kama fidia ya bima ya amana kwa wateja wote 6,628 waliopo Tanzania na wateja waliopo nje ya nchi (Tanzania International Banking Depositors- TIB)
Aidha jumla ya Sh. milioni 2,401.2 zimelipwa, ikiwa ni asilimia 83.3 ya lengo la kulipa jumla ya Sh. milioni 2,882.6 kwa wateja waliopo Tanzania tu.
Naibu Waziri huyo wa Fedha na Mipango, amempongeza Mwanasheria na Wakili Mkuu wa Serikali pamoja na Benki Kuu ya Tanzania kwa kuhakikisha amana za wateja FBME ambao wako ndani na nje ya nchi zinabaki salama na kuzipata baada ya taratibu za kisheria kukamilika.
Dkt. Kijaji aliongeza kuwa, Sheria ya Benki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006 imeipa Benki Kuu ya Tanzania- BOT, mamlaka ya kutoa leseni, kutunga kanuni, kusimamia benki zote zinazochukua amana za wateja na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya benki zinazoendesha biashara bila kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo iliyopo.
 Kwa ujumla Benki Kuu imepewa mamlaka ya kusimamia na kudhibiti benki na taasisi za fedha ili kuhakikisha kuwa amana za wateja zinakuwa salama na pia kuna usalama, utulivu na uthabiti wa sekta ya fedha na uchumi.
Benki ya FBME Ltd ilifutiwa leseni ya kufanya biashara hapa Tanzania na Benki Kuu ya Tanzania Mei 8, 2017 kutokana na tuhuma za kujihusisha na biashara ya kutakatisha fedha nchini Marekani.
Benki  Kuu nchini Tanzania iliiteua Bodi ya Bima ya Amana- DIB kuwa mfilisi wa Benki ya FBME, hivyo kwa sasa  benki hiyo haiendeshi shughuli zozote za kibenki hapa nchini.

DIAMOND PLATINUMZ APEWA UBALOZI WA PARI MATCH TANZANIA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Msanii wa muziki wa Kizazi kipya Nasib Abdul ‘Diamond Platinumz’ ameteuliwa na kutambulishwa leo kama balozi wa Kampuni ya michezo ya kubashiri Pari March Tanzania.

Mkurugenzi muendeshaji wa Parimatch Tanzania 
Tumaini Maligana amesema wamechukua hatua ya uthubutu na kumchagua Diamond kama balozi wetu kwa dhana hii (Burudani),yeye ni mtu ambaye amepambana na ameweza, Ila kikubwa ni kwamba huwezi ongelea burudani Tanzania bila kumtaja Diamond.

Kama balozi atasaidia kutoa uelewa kwa wachezaji maana hasa ya kubeti ili wote tuweze kufurahi na kucheza kistarabu.

Maligana amesema kwa msaada toka kwa Bodi Ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania ambao wamekua mstari wa mbele katika kuhakikisha wanasimamia na kuhimiza kubeti kistarabu kupitia kampeni yao ya Makinika kijana, wanaahidi kuwaunga mkono katika hili kwa manufaa ya watu wote na kwa wateja wetu.

Amesema kuwa, kuna  Ofa na Promosheni zinakuja, Kama bado hujawa Mwanafamilia wa Parimatch Huu ni wakati wa kuungana nasi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Msanii Diamond amesema anachofahamu ni kwamba kwa upande wa Pari Match Kubeti sio ajira ni burudani,na ndio maana wameweka mkazo katika kubeti kistarabu.

Akitolea mfano wa burudani, Diamond amesema ukienda kwenye show ya mziki unakua na kinywaji na utatokelezea basi hata ukitazama mpira, weka mkeka wako kuongeza msisimko na shangwe .

Amesema, yeye na menejimenti yake wamedhamiria kuwapeleka washindi wale wanaopata donge nono kwenda kushuhudia mechi nje ya nchi na sio kuishia kubeti tu.

“Mimi na Menejimenti yangu tunasafiri sana, na tulikua tunajadili namna ya kuwasapoti washindi hao na kuonelea kuwapeleka kushuhudia mechi hizo nje ya nchi hasa wale waliopata donge nono na sio kuishia kubeti tu,”amesema Diamond.

Bodi ya Michezo Nchini imeweka mikakati ya kuwasajili wachezaji wote wanaocheza michezo ya kubashiri, ambapo itasaidia katika kutambua umri sahihi wa mshiriki na kucheza kwa ustaarabu.
 Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Nasib Abdul ‘Diamond Platinumz’ akizungumza na waandishi wa habari wakati wa utambulisho wake kama Balozi wa Kampuni ya Kubashiri ya Pari Match uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Nasib Abdul ‘Diamond Platinumz’ akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Pari Match Na Menejimenti ya Wasafi wakati wa hafla ua kumtambulisha kama Balozi wa Kampuni ya Kubashiri Pari Match Tanzania leo Jijini Dar es Salaam

MAFUNZO YA MAPISHI NA UKARIMU KUFANYIKA ZANZIBAR

$
0
0
 Makamo Meneja Mkuu wa Taasisi ya China NATIONAL RESEARCH INSITITUTE OF FOOD AND FERMENTATION INDUSTIES COPORATION LTD Bw.Dong Wei Hong akitoa taarifa ya mafunzo kwa mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Issa Haji Ussi (Gavu) leo katika Ufunguzi wa Mafunzo ya Upishi na Ukarimu yatayoendeshwa na Wakufunzi kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China katika ukumbi wa Idris Abduwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar,[Picha na Ikulu.] 11/09/2019.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Issa Haji Ussi (Gavu) alipokuwa akifungua Mafunzo ya Upishi na Ukarimu kwa Taasisi za Serikali na Binafsi leo ambayo yatayoendeshwa na Wakufunzi kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China katika ukumbi wa Idris Abduwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar.

 Washiriki wa Mafunzo ya Upishi na Ukarimu kutoka Taasisi za Serikali na Binafsi wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Issa Haji Ussi (Gavu) (hayupo pichani) alipokuwa akifungua mafunzo hayo yatayoendeshwa na Wakufunzi kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China,hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Idris Abduwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar
Balozi Mdogo wa Jamhuri ya Watu wa China aliyepo Zanzibar Mhe.XIE XIAOWU (kulia) akicheza ngoma ya Msewe iliyopigwa na kikundi cha Sanaa cha Taifa katika Ukumbi wa Idris Abduwakil Kikwajuni Mjini Zanzibar wakati wa ufunguzi wa mafunzo Mapishi na Ukarimu yaliyofunguliwa leo na kuendeshwa na Wakufunzi kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China, [Picha na Ikulu.] 11/09/2019,

WANANCHI UKONGA WAASWA KUTOA VINYONGO VYAO MAHAKAMA INAYOTEMBEA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv 

HAKIMU Mkazi wa Mahakama ya Ukonga, Faudhia Hamza ametoa wito kwa wananchi wenye dukuduku, malalamiko ama vinyongo mioyoni mwao juu ya mambo yote ya kimahakama kujitokeza katika Mahakama inayotembea kutoa shida zao. 

Wito huo umetolewa leo Septemba 12,2019 wakati akiendesha kesi katika mahakama inayotembea eneo la Chanika jijini Dar Salaam na kuongeza kuwa, Mahakama hiyo itakuwa ikitoa huduma kila alhamisi katika eneo la ofisi ya serikali ya mtaa ya chanika. 

"Ninawaomba wananchi wote nchini mnapoiona hii gari ya mahakama inayotembea msiikimbie wala kufikiri kuwa sasa mtafungwa hapana, huu ni ukombozi wenu jitokezeni ili kutatua matatizo hasa yanayohusiana na madai, mirathi na ndoa" Amesema Hakimu Hamza. 

Ameongeza kuwa katika jamii watu wamekuwa wakikaa na vitu katika mioyoni ambavyo vinawapelekea kuchukua maamuzi magumu ikiwamo kujinyonga kutokana na kukosa ushauri ama elimu ila mahakama hii inayotembea ipo kwa ajili ya wananchi, inapokea kesi, vinyongo, madukuduku na malalamiko waliyonayo wananchi na kuwashauri kwa mujibu wa sheria na taratibu zake. 

Kwa upande wa Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala,Martha Mpaze amesema mahakama hii inayotembea imejikita kusikiliza kesi za madai, talaka na Mirathi kwa kutoa usuluhishi zaidi na kwamba utakuwa akitoa maamuzi ndani ya siku 30. 

Amesema wamesogeza huduma hizo karibu na Mwananchi ili kuhakikisha haki inatendeka kwa usawa, urahisi na kwa wakati na kwamba awali huduma hizo zilikuwa zikitolewa katika Mahakama ya Mwanzo ya Ukonga lakini kutokana na umbali na nguzo ya tatu ya mahakama ya kuwa karibu na Mwananchi. 

Huduma hii ya mahakama inayotembea iliyoanzishwa mwaka huu 'mahakama mtaani kwako' kwa sasa inafanyakazi katika Mkoa wa Dar es Salaam na Mwanza. 

Kwa upande mkazi mmoja wa Chanika ambaye ni Katibu wa CCM, Yahaya Rajabu aliishukuru mahakama kwa kusogeza mahakama mtaani kwani itasaidi wananchi kupata uelewa wa sheria kwa kuwa wengi wanakabiliwa na changamoto nyingi hasa migogoro ya talaka na wana kuwa njia panda hawajui nini cha kufanya lakini ushauri na elimu inayotolewa na mahakama hiyo itawapa dira jinsi ya kukabiliana nazo. 

WIZARA YAWAPIGA MSASA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII TABORA KUPUNGUZA VITENDO VYA UKATILI

$
0
0
 Mkurugenzi Msaidizi Familia kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Tausi Mwilima akizungumza na maafisa Maendeleo ya Jamii na Waratibu wa Madawati ya Jinsia na Watoto kutoka Halmashauri za Wilaya na Miji kutoka Mkoa wa Tabora wakati akifungua kikao kazi ya kuwajengea uwezo maafisa hao kuhusu masuala ya elimu ya malezi kwa familia.
 Afisa Maendeleo ya Jamii wa mkoa wa Tabora Bw. Panin Kerika akitoa neno la ukaribisho kwa Mkurugenzi Msaidizi Familia kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Tausi Mwilima(wa pili kulia) wakati wa kikao kazi cha kuwajengea uwezo Maafisa Maendeleo ya Jamii na waratibu wa Madawati ya Jinsia na Watoto kutoka Halmashauri za Wilaya na Miji kutoka Mkoa wa Tabora kuhusu masuala ya elimu ya malezi kwa familia.
 Afisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Emmanuel Burton akielezea hali ya ukatili nchini wakati wa kikao kazi cha kuwajengea uwezo Maafisa Maendeleo ya Jamii na waratibu wa Madawati ya Jinsia na Watoto kutoka Halmashauri za Wilaya na Miji kutoka Mkoa wa Tabora kuhusu masuala ya elimu ya malezi kwa familia.
 Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Violeth Mulyalya akielezea kuhusu wajibu wa wazazi au walezi katika malezi wakati wa wa kikao kazi cha kuwajengea uwezo kuhusu Maafisa Maendeleo ya Jamii na Waratibu wa Madawati ya Jinsia na Watoto kutoka Halmashauri za Wilaya na Miji kutoka Mkoa wa Tabora masuala ya elimu ya malezi kwa familia.
 Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Bi. Frida Edward akichangia mada wakati wa kikao kazi cha kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya elimu ya malezi kwa familia kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii na Waratibu wa Madawati ya Jinsia na Watoto kutoka Halmashauri za Wilaya na Miji kutoka Mkoa wa Tabora.
 Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Bw. Mabula Bugumba akichangia mada wakati wa wa kikao kazi cha kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya elimu ya malezi kwa familia kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii na waratibu wa Madawati ya Jinsia na Watoto kutoka Halmashauri za Wilaya na Miji kutoka Mkoa wa Tabora.
Baadhi ya Maafisa Maendeleo ya Jamii na Waratibu wa MAdawati ya Jinsia na Watoto kutoka Halmashauri za Mkoa wa Tabora wakti wa kikao cha kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya elimu ya malezi kwa familia. Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW

Na Mwandishi Wetu Nzega
Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii imetoa elimu kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii na Waratibu madawati ya Jinsia na Watoto mkoa wa Tabora ili kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya elimu ya malezi kwa familia ili kukabiliana na vitendo vya kikatili katika jamii.

Akifungua kikao kazi cha Maafisa na Waratibu hao leo wilayani Nzega mkoani Tabora Mkurugenzi Msaidizi Familia kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bi. Tausi Mwilima amesema kuwa malengo ya kuwa na kikao kazi hicho ni kuwajengea uwezo Maafisa na waratubu hao ili waweze kufikisha elimu ya malezi na makuzi katika jamii.

Bi. Tausi ameongeza kuwa lengo la Kitini cha elimu ya malezi ya familia ni muhimu kwani uwapa wazazi na walezi uelewa na jinsi ya kuendeleza malezi na makuzi yenye matokeo chanja kwa watoto ili kujenga jamii yenye kuwajibika na uzalendo.

Amesisitiza kuwa jukumu la kwanza la malezi na makuzi kwa mtoto ni la mzazi au mlezi katika familia hivyo wazazi au walezi wana wajibu mkubwa wa kuzingatia wanawapa watoto wao malezi na makuzi bora.

Aidha Bi. Tausi ameeleza kuwa Waratibu wa Madawati ya Jinsia na Watoto katika Halmashauri wanajukumu kubwa kufuatilia na kuhakikisha changamoto za malezi na makuzi zinatatuliwa katika jamii na wazazi wanapata elimu sahihi ya kusaidia kuwajengea uelewa juu ya suala la malezi ya familia.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Tabora Bw. Panin Kerika amesema kuwa suala la elimu ya malezi kwa familia ni muhimu na la msingi ambapo linasaidia katika utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto wenye lengo la kutokomeza ukatili kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2022.

Naye Afisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bw. Emmanel Burton amesema kuwa Wizara iliamua kuwa na Kitini cha elimu ya malezi kwa familia kutokana na kuongezeka kwa vitendo vya ukatili katika familia hivyo elimu juu ya malezi na makuzi itasaidia kupunguza vitendo vya ukatili vinavyofanywa katika familia.

Mmoja wa Mratibu wa Dawati la Jinsia na Watoto Wilaya ya Tabora Bi. Faiza Hassan amesema kuwa masuala ya elimu ya malezi kwa familia ni muhimu sana kwa familia kwani familia nyingi zimekuwa zikifanya vitendo vya kikatili bila kujua kama ni vitendo vya ukatili kwa watoto wao.

Naye Mratibu wa Dawati la Jinsia na Watoto Wilaya ya Uyui Bw. Godwin Masaka amesema kuwa elimu ya malezi kwa familia itawasaidia Waratibu wa Madawati ya Jinsia na Watoto kuwajengea uwezo wa kwenda katika jamii kuwapatia elimu hiyo ili kuimarisha misingi ya malezi na makuzi katika familia.


WFP KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUTAFUTA SOKO LA NAFAKA NJE-BASHE

$
0
0
 Naibu Waziri wa Kilimo Husein Bashe akiongea na ujumbe wa Shirika la Chakula Duniani (WFP) wakati alipofanya kikao ofisini kwake Dodoma.
 Mwalikishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani nchini Michael Dunford (wa pili kulia) akiwa timu yake wakati wa mazungumzo kuhusu ushirikiano wa kutafuta soko la mahindi na Naibu Waziri wa Kilimo Husein Bashe (hayupo pichani). Nawasilisha.
 Naibu Waziri wa Kilimo Husein Bashe akifuatilia mazungumzo na ujumbe wa Shirika la Chakula Duniani wakati wa kikao cha kujadili upatikanaji wa soko la mahindi na mtama nchini.
Picha ya pamoja kati ya Naibu Waziri wa Kilimo Husein Bashe (wa sita toka kulia) akiwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani Michael Dunford (wa nne toka kushoto) mara baada ya mazungumzo kuhusu ushirikiano wa kutafuta masoko ya nafaka nchini.

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limekubali kuwa na ushirikiano na Wizara ya Kilimo katika kutafuta soko la uhakika la mazao ya mahindi na mtama nje ya nchi.
Kauli hii imetolewa jana na Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe mara baada ya kufanya mazungumzo ofisini kwake na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani Michael Dunford.

Bashe amebainisha kuwa Wizara ya Kilimo ina mkakati wa kuhakikisha mahindi na mtama unaozalishwa nchini unapata soko la uhakika ili kuinua uchumi wa wakulima
“Wizara inataka kutumia uzoefu wa Shirika la Chakula Dunia katika kuyafikia masoko ili mazao ya wakulima wetu yaweze kupata bei nzuri katika soko la Afrika” alisema Naibu Waziri

Amewahakikishia WFP kuwa wizara imejipanga kuona uzalishaji wa mahindi na mtama unaongezeka na kuzingatia kiwango cha ubora kinachotakiwa na soko la nje.
Aliongeza kuwa kwa sasa serikali kupitia Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko na Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) wamewezeshwa ili wanunue na kuhifadhi nafaka kwa wingi na kwa kuzingatia viwango vya kimataifa.

“Ni lengo la wizara kuhakikisha wakulima nchini wanaunganishwa na fursa za masoko ya mazao yao ili uchumi wa nchi uendelee kukua kwa kasi kupitia sekta ya kilimo” alisema Bashe
Naibu Waziri Bashe alisema mkakati wa wizara katika kipindi cha miaka mitatu ijayo ni kuona Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko inakuwa na uwezo wa kuhifadhi kisasa nafaka tani 520,000 tofauti na ilivyo sasa ambapo tani 120,000 zinahifadhiwa,hivyo kuwa na uwezo wa kuuza nje.

Kwa upande wake mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani Michael Dunford amesema wanahitaji kununua zaidi ya tani 50,000 za mahindi toka Tanzania kwa ajili ya kusaidia nchi za Uganda na Sudan Kusini.
Dunford alisema kutokana na uzalishaji mzuri ulipo Tanzania kwenye zao la mahindi unatoa fursa ya soko la uhakika endapo vigezo vya ubora unaotakiwa na Shirika la Chakula Duniani utazingatiwa ikiwa ni pamoja na kupunguza tatizo la sumukuvu.

Ameishauri wizara ya kilimo kutumia uzoefu na teknolojia ya kisasa uliopo WFP katika kudhibiti upotevu wa mazao baada ya mavuno ili wakulima wapate ufanisi katika uzalishaji.
“Tanzania inapoteza asilimia 30 ya mazao ya wakulima baada ya mavuno kutokana na kukosekana kwa uhifadhi bora na teknolojia ya kisasa” alisema Dunford

Katika kuhakikisha ushirikiano huu unafikiwa,Dunford alisema Shirika la Chakula Duniani linahudumia chakula kwa watu zaidi ya milioni 150 duniani wenye uhitaji katika maeneo yenye migogoro na majanga ,hivyo Tanzania inayo fursa ya kupata soko la nafaka.
Makubaliano yamefikiwa kuwa wataalam wa wizara ya Kilimo na wale wa Shirika la Chakula duniani watakutana mapema mwezi Octoba mwaka huu kukamilisha agenda muhimu za ushirikiano.


MAKONDA ATEMBELEA CLOUDS FM,ATOA NENO

$
0
0
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda mapema leo alipotembelea kituo cha Clouds FM kupitia kipindi cha XXL, alisema kuwa siku ya kwanza kupata taarifa kuwa amechaguliwa kuwa Mkuu wa Mkoa alikuwa anatoka Hospitali ya Mwananyamala kukagua wadi za watoto.

“Nakumbuka siku hiyo nilikuwa nimetoka Mwananyamala Hospital kuangalia wodi za kina-mama wajawazito ambao wapo Mwananyamala na sehemu za 'Operation Room' sio rafiki kwao, hivyo nilienda kuangalia namna gani tunaweza kuziboresha nikiungana na wadau wengine.

Baada ya hapo nikarudi nyumbani, lakini wakati nipo seating room na kijana mmoja aitwae  Rey wa hapa @cloudstv ndiyo akaniambia Mh naona hapa umechaguliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, kiukweli sio kitu ambacho nilikuwa natarajia hivyo kilinishtua sana, kwani kutoka kuwa mkuu wa Wilaya mpaka mkuu wa mkoa halikuwa jambo ambalo linawezekana sana kwangu” 

Anaendelea kuelezea Mkuu wa mkoa wa Dar, Paul Makonda, namna ambavyo yeye anaweza kutofautisha kazi yake na maisha ya familia. 

“Mimi ni Baba mzuri kwa familia yangu pia ni mume mzuri na mke wangu anafahamu hilo, siwezi kupeleka stress za kazini nyumbani kuna baadhi ya mambo huwezi ku- share na mke wako kama hana hekima ya ki- Mungu, maana utayasikia kwenye saloon, hivyo kiapo ambacho niliapa mwenyewe hivyo mambo ya kazi yanabaki kazini na nikirudi nyumbani nakuwa baba na mme bora.” 

“Ila watu wanatakiwa kujua tu kuwa siku zote mimi nimekuwa nikieleza mambo yanayoendana na uwepo wa jamii yetu hivyo utaona kutoa kwangu kibari kwa wachungaji kwenda kuhubiri sehemu za kumbi za starehe nafahamu kabisa wazi kuwa katika maisha ya siku hizi kuna watu wengi huwa wanakwenda Club wakiwa na mawazo yao kule sasa wakikutana na neno la Mungu wanaweza kupona, ila sijamlazimisha Mtumishi yoyote kuhubiri kwenye Club," Alisema Paul Makonda Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda mapema leo alipotembelea kituo cha Clouds FM kupitia kipindi cha XXL

MDAHALO KUHUSU KODI KWA SKULI ZA SEKONDARY KANDA YA UNGUJA WAFANYIKA ZANZIBAR

$
0
0
 Afisa Uhusiano ZRB Makame Khamis Mohamed akizungumza machache katika Mdahalo kuhusu Kodi kwa Skuli za Sekondary Kanda ya Unguja uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar SUZA Kampasi ya Vuga Zanzibar.Ikiwa ni Shamra shamra za kutimia miaka 20 ya Bodi ya Mapato Zanzibar.
 Afisa Elimu ZRB Raya Suleiman Abdalla akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Mdahalo kuhusu Kodi kwa Skuli za Sekondary Kanda ya Unguja uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar SUZA Kampasi ya Vuga Zanzibar. Ikiwa ni Shamra shamra za kutimia miaka 20 ya Bodi ya Mapato Zanzibar.
 Kiongozi wa Majaji Mussa Said Salum akizungumza machache katika Mdahalo kuhusu Kodi kwa Skuli za Sekondary Kanda ya Unguja uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar SUZA Kampasi ya Vuga Zanzibar.Ikiwa ni Shamra shamra za kutimia miaka 20 ya Bodi ya Mapato Zanzibar. PICHA NA YUSSUF SIMAI /MAELEZO ZANZIBAR.
 Mwanafunzi Kutoka Skuli ya Sekondary Umoja Uzini Zalha Bakari Omar akiwasilisha mada katika Mdahalo kuhusu Kodi kwa Skuli za Sekondary Kanda ya Unguja uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar SUZA Kampasi ya Vuga Zanzibar.Ikiwa ni Shamra shamra za kutimia miaka 20 ya Bodi ya Mapato Zanzibar.
 Mwanafunzi Kutoka Skuli ya Sekondary ya Biashara Mombasa Haidar Suleiman Rashid akiwasilisha mada katika Mdahalo kuhusu Kodi kwa Skuli za Sekondary Kanda ya Unguja uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar SUZA Kampasi ya Vuga Zanzibar.Ikiwa ni Shamra shamra za kutimia miaka 20 ya Bodi ya Mapato Zanzibar.
Baadhi ya Walimu na Wanafunzi kutoka Skuli za Sekondary walioshiriki kuhusu Kodi kwa Skuli za Sekondary Kanda ya Unguja uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar SUZA Kampasi ya Vuga Zanzibar. Ikiwa ni Shamra shamra za kutimia miaka 20 ya Bodi ya Mapato Zanzibar.

DC Kongwa awataka wakulima kuunda ushirika kukuza sekta ya Kilimo

$
0
0
Charles James, Michuzi TV

KATIKA kuhakikisha Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma inapiga hatua kutoka kufanya kilimo cha kujitegemea na kufanya kilimo cha uchumi, Mkuu wa Wilaya hiyo amewataka wakulima kuunda ushirika wao.

DC Ndejembi amesema sehemu yoyote ambayo watu wamefanikiwa kimaendeleo ni kwa sababu waliamua kuungana na kushirikiana.

Hayo ameyasema katika uzinduzi wa uuzaji wa matrekta ya kilimo wilayani humo uliofanywa na Kampuni ya Loan Agro ambao ni wauzaji wa matrekta ya John Deere sambamba na Mabenki washirika ikiwemo Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) na Benki ya NMB.

" Niwaase wakulima wote wakubwa tuthubutu, tuanzishe ushirika wetu huu ndio utatusaidia kuwa na mawasiliano mazuri na wenzetu wa mamlaka ya hali ya hewa, watu wa mbegu bora na watafiti wa Ardhi hapa ndipo tutakapoona faida ya kilimo, bila ushirikiano huo ni ngumu kufanya kilimo cha uchumi.

Haya mabenki ambayo tunayalalamiki kuwa wana riba kuwa siku tukiwa na ushirika wetu wao ndio watakua wakitufuata na kutuomba tuchukue mikopo kwao kwa riba nafuu," Amesema DC Ndejembi.

Amesema ni wakati sasa pia kwa wakulima wa wilaya hiyo kuanza kulima zao la korosho ikiwa ni muendelezo wa kampeni yao kama wilaya ya kuondoka njaa 

" Korosho ni zao la thamani sana kwa sababu ni la kudumu hivyo uthaminishwaji wake una thamani sana katika kukopesheka na mabenki na unakua rahisi, " Amesema DC Ndejembi.

Kwa upande wake Afisa Biashara wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini, Willy Lyumi amesema Benki yao itaendelea kuwa pamoja na Wakulima katika kuhakikisha wanapiga hatua kutoka kufanya kilimo cha kujitegemea na kufanya kilimo chenye faida kiuchumi.

Amesema leo la Benki ya TADB ni kubadilisha aina ya kilimo cha mazoea ambacho kinafanywa na Wakulima wengi nchini lakini pia kuhakikisha Nchi inakua na chakula cha kutosha.

" Sisi tunatoa mikopo kwa wakulima mbalimbali lengo likiwa kukuza kilimo ambacho sisi kama TADB tunaamini ndio uti wa mgongo wa Taifa letu katika kukua kiuchumi.

" Tunafahamu dhamira ya Serikali yetu ya awamu ya tano chini ya Dk John Magufuli imejipanga kuifanya Nchi yetu kuwa Nchi yenye uchumi wa kati na Kilimo ni mojawapo ya sekta muhimu katika kufikia malengo hayo, na sisi kwa kutambua dhamira hiyo njema ya Mhe Rais ndio maana tunahakikisha wakulima wananufaika na Benki hii ambayo ni mahususi kwa ajili yao," Amesema Lyumi.

Aidha amewataka wakulima kutoogopa kukopa na kuwahakikishia kuwa wao kama Benki inayojali maslahi ya wakulima inatoa ushauri kwa mkulima yeyote anayeenda kuomba mkopo kabla ya kumpatia hiyo ni katika kumfanya mkulima afaidike na uwepo wa Banki ya Maendeleo ya Kilimo.

Nae Margret Julius ambaye ni Afisa Mauzo Mkuu wa Kampuni ya Loan Agro amemhakikishia DC Ndejembi kuwa watauza matrekta hayo kwa bei nafuu ambayo kila mkulima ataimudu lakini pia upatikanaji wa vifaa vyake utakua rahisi na wa bei nafuu.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa (katikati), Mhe Deo Ndejembi akikata utepe kuashiria kuzindua uuzaji wa matrekta ya kilimo wilayani Kongwa leo.

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe Deo Ndejembi akizungumza wakati wa uzinduzi wa uuzaji wa matrekta ya kilimo katika eneo la Kibaigwa wilayani humo leo
 Afisa Biashara kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Nchini (TADB), Willy Lyumi akizungumza katika uzinduzi huo ambapo ameahidi Benki hiyo kuendeleza ushirikiano na Wakulima katika kukuza sekta ya Kilimo
 Baadhi ya wakulima wa Wilaya ya Kongwa waliojitokeza katika hafla ya uzinduzi wa uuzaji wa matrekta ya kilimo wilayani Kongwa.

WALIOKUWA WAFANYAKAZI NA WATEJA WA BENKI YA FBME KULIPWA AMANA

$
0
0
Na. Peter Haule na Josephine Majura, WFM, Dodoma

SERIKALI imeeleza kuwa itawalipa waliokuwa wateja na wafanyakazi wa Benki ya FBME baada ya taratibu za kisheria na majadiliano na Cyprus yatakapo kamilika hivi punde.

Hayo yamesemwa Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), wakati akijibu maswali ya Mhe. Jaku Ayoub, aliyetaka kujua Benki ya FBME ipo katika hali gani na ni lini italipa wateja amana zao.

Dkt. Kijaji alisema kuwa wateja wa Benki ya FBME waliokuwa na amana ya milioni 1.5 Serikali imewalipa kwa zaidi ya asilimia 83 ya wateja wote, asilimia 17 iliyobaki ni ya wateja ambao hawajajitokeza kuchukua amana hizo.

“Bodi ya Bima ya Amana (Deposit Insurance Board- DIB) ilianza zoezi la kulipa fidia kwa mujibu wa sheria kwa waliokuwa na amana katika benki hiyo kuanzia Novemba, 2017 na bado zoezi hilo linaendelea”, alieleza Dkt. Kijaji.

Alisema kuwa hadi kufikia Septemba 9, 2019 jumla ya kiasi cha Sh. milioni 2,404.2 kimelipwa kwa wateja 3426 kama fidia ya bima ya amana, ambapo kiasi hicho ni sawa na asilimia 55.9 ya kiasi chote kilichotarajiwa kulipwa kama fidia ya bima ya amana kwa wateja wote 6,628 waliopo Tanzania na wateja waliopo nje ya nchi (Tanzania International Banking Depositors- TIB)

Aidha jumla ya Sh. milioni 2,401.2 zimelipwa, ikiwa ni asilimia 83.3 ya lengo la kulipa jumla ya Sh. milioni 2,882.6 kwa wateja waliopo Tanzania tu.

Naibu Waziri huyo wa Fedha na Mipango, amempongeza Mwanasheria na Wakili Mkuu wa Serikali pamoja na Benki Kuu ya Tanzania kwa kuhakikisha amana za wateja FBME ambao wako ndani na nje ya nchi zinabaki salama na kuzipata baada ya taratibu za kisheria kukamilika.

Dkt. Kijaji aliongeza kuwa, Sheria ya Benki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006 imeipa Benki Kuu ya Tanzania- BOT, mamlaka ya kutoa leseni, kutunga kanuni, kusimamia benki zote zinazochukua amana za wateja na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya benki zinazoendesha biashara bila kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo iliyopo.

Kwa ujumla Benki Kuu imepewa mamlaka ya kusimamia na kudhibiti benki na taasisi za fedha ili kuhakikisha kuwa amana za wateja zinakuwa salama na pia kuna usalama, utulivu na uthabiti wa sekta ya fedha na uchumi.

Benki ya FBME Ltd ilifutiwa leseni ya kufanya biashara hapa Tanzania na Benki Kuu ya Tanzania Mei 8, 2017 kutokana na tuhuma za kujihusisha na biashara ya kutakatisha fedha nchini Marekani.

Benki Kuu nchini Tanzania iliiteua Bodi ya Bima ya Amana- DIB kuwa mfilisi wa Benki ya FBME, hivyo kwa sasa benki hiyo haiendeshi shughuli zozote za kibenki hapa nchini.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb)

UFATILIAJI NA USIMAMIZI MAKINI WAIFANIKISHA TASAF

$
0
0
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema ufuatiliaji pamoja na usimamizi makini wa Watendaji wa Ofisi yake katika kuratibu matumizi sahihi ya fedha zinazotekeleza Miradi ya Kijamii ndio uliopelekea kufanikisha vyema kwa Miradi ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania {TASAF}.

Amesema Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ambayo ndio inayoratibu shughuli zote za Tasaf kwa upande wa Zanzibar imelazimika kuchukuwa hatua hiyo ili kulinda Heshima itakayotoa ushawishi kwa Wafadhili wa Mpango huo kuendelea kuunga mkono katika utoaji wa Mikopo zaidi.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati wa Mazungumzo yake ya Timu ya Waratibu Wakuu wa Majimbo 36 yanayounda Taifa la Nigeria waliowasili Zanzibar kwa ziara ya Siku mbili kuja kujifunza kutokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika mpango wa kuhudumia Kaya Maskini Nchini Tanzania.

Ameeleza kwa vile Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania {TASAF} unatoa huduma katika pande zote mbili za Tanzania, Serikali zote mbili ile ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zinalazimika kufuatilia mwenendo mzima wa fedha zinavyotumika katika Miradi ya Tasaf ili kufikia lengo.

“ Serikali ililazimika kufanya uchambuzi yakinifu na kujiridhisha katika mwenendo wa wa matumizi ya Miradi ya Tasaf ili kuepuka upotevu ambao ungegharimu machungu kwa wasimamizi wa Miradi hiyo”. Alisisitiza Balozi Seif.

Amesema ipo Miradi mingi ya Kijamii katika maeneo mbali mbali ya Visiwa vya Unguja na Pemba Mjini na Vijijini iliyoleta ukombozi kwa Wananchi walio wengi baada ya kupata msukumo uliotokana na uanzishwaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania katika Awamu tofauti uliojikita kuhudumia moja kwa moja miradi hiyo.

Balozi Seif amesema ipo haja kwa Wafadhili wa Miradi ya Kijamii akatolea Mfano Benki ya Dunia pamoja na Taasisi nyengine za Kimataifa za misaada ya Maendeleo kuendelea kuongeza ufadhili wao kwa vile lengo la uanzishwaji wa Miradi ya Kijamii limefanikiwa vyema.

Hata hivyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema hatua hiyo ya Wafadhili ni muhimu kwa vile inaweza kusaidia kuondoa mkwamo kwa baadhi ya Changamoto zinazotokana na Miradi inayoanzishwa hasa katika Sekta za uzalishaji kupitia Vikundi vya ujasiri amali.

Balozi Seif ameishauri Timu hiyo ya Waratibu Wakuu wa Majimbo ya Nigeria kwamba katika kuimarisha Miradi na huduma za Kijamii ipo haja ya Mataifa ya Afrika kuzidi kushirikiana katika kubuni mbinu na njia za pamoja katika kuendeleza Miradi hiyo itakayoleta ustawi na Maisha bora kwa Waafrika walio wengi.

Amesema mfano ulioonyeshwa na Timu hiyo ya Waratibu Wakuu wa Majimbo 36 ya Taifa la Nigeria wa kufika Tanzania kujifunza mwenendo wa uendeshaji wa Miradi ya Kijamii ni mwanzo wa kuigwa kwa Mataifa mengine yanayotekeleza Miradi kama hiyo Barani Afrika.

Mapema Mratibu wa Washirika wa Sekta za Kijamii kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais wa Nchini Nigeria Bwana Gyangyang Limave ameishukuru na kuipongeza Tanzania kwa umakini wake iliyonao wa kuhakikisha Bara la Afrika linaendelea kuimarika Kiuchumi na Ustawi.

 Byangyang amesema msimamo wa Tanzania katika kustawisha maisha ya Wananchi wake ni mfano wa kuigwa na Mataifa mengine Duniani yaliyoanza mpango wa kuimarisha Taasisi za Kijamii.

Amesema Serikali ya Nigeria katika muelekeo wake wa kustawisha Maisha ya Wananchi wake tayari imeshaanzisha Taasisi inayoratibu na kusimamia kasuala ya Kijamii mnamo Mwaka 2016.

 Gyangyang Limave amemueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba zaidi ya Dola za Kimarekani Bilioni 1.3 zimetolewa na Serikali Kuu katika kuimarishaji wa Kaya Maskini Nchini humo.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kushoto akisalimiana na Mratibu wa Washirika wa Sekta za Kijamii kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais wa Nchini Nigeria Bwana Gyangyang Limave wakati akijiandaa kuzungumza na Timu ya Waratibu Wakuu wa Majimbo 36 ya Taifa la Nigeria waliofika Zanzibar kujifunza Mpango Maalum wa uendeleshaji wa Miradi ya Tasaf.
 Balozi Seif Kulia akizungumza na Timu ya Waratibu Wakuu wa Majimbo 36 ya Taifa la Nigeria waliofika Zanzibar kujifunza Mpango Maalum wa uendeleshaji wa Miradi ya Tasaf.
 Balozi Seif katikati waliokaa vitini akiwa katika picha ya pamoja na Timu ya Waratibu Wakuu wa Majimbo 36 ya Taifa la Nigeria pamoja na Watendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania {TASAF} Bara na Zanzibar.
 Balozi Seif akibadilishana mawazo na Waratibu Wakuu wa Majimbo 36 ya Taifa la Nigeria mara baada ya kupiga picha za ukumbusho wa uwepo wao Visiwani Zanzibar.
Balozi Seif akiagana na Kiongozi wa Timu ya Waratibu Wakuu wa Majimbo 36 yanayounda Taifa la Nigeria Naibu Mkurugenzi wa Taasisi inayosimamia masuala ya Ustawi wa Jamii Bwana Ortutu baada ya mazungumzo yao. Picha na – OMPR – ZNZ.

MAVUNDE AKUTANA NA WAENDESHA BODA BODA NA BAJAJI,ASIKILIZA CHANGAMOTO ZAO

$
0
0

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira ,ambaye pia ni  Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini,Mh Anthony Mavunde leo amekutana na Waendesha Boda Boda wa jimbo hilo na kusikiliza changamoto zao mbalimbali  walizonazo kwenye shughuli zao za kila siku . 

Mh Mavunde alisikiliza changamoto za Waendesha Boda boda na Bajaj na baadaye kuwakabidhi vifaa vya usalama wakati wakiendesha vifaa vyao vya moto (Safety Jackets) 600  pamoja na mafuta (OIL) dumu la lita 1 kwa watu  600 kutoka Kampuni ya Mafuta ya MOGAS.




Viewing all 110160 articles
Browse latest View live




Latest Images