Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live

SPIKA NDUGAI AMUAPISHA RASMI MTATURU KUWA MBUNGE SINGINDA MASHARIKI

$
0
0
Spika wa Bunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai, leo Jumanne September 3, 2019 amemuapisha Ndugu Miraji Mtaturu kuwa Mbunge wa Singida Mashariki.

Mtaturu amechukua nafasi iliyoachwa na Tundu Lissu kupitia chama cha CHADEMA aliyevuliwa Ubunge  mnamo Juni 28 mwaka huu kwa kupoteza sifa za kuwa mbunge wa Jimbo.

Wakati  shughuli za kumuapisa Mh.Mtaturu, Wabunge wa CHADEMA wamesusia tukio hilo kwa kugoma kuingia ukumbini .

Wakati Mtaturu akichukua nafasi yake, Ndugai amesema jimbo hilo sasa limepata mwakilishi halali

SERIKALI YARIDHISHWA NA MAENDELEO YA UJENZI WA DARAJA LA MAGARA

$
0
0
Muonekano wa hatua za ujenzi wa Daraja la Magara lenye urefu wa mita 84 ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 75, utagharimu zaidi ya shilingi Bilioni 12 na unatarajiwa kukamilika mwezi Februari 2020, Mkoani Manyara.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga, ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa Daraja la Magara lenye urefu wa mita 84 na barabara za maingilio KM 4.

Katibu Mkuu Mwakalinga, amesema kuwa daraja hilo linajengwa na mkandarasi M/s China Railway Seventh Group kwa muda wa miezi ishirini na sita (26)  na kuongeza kuwa daraja hilo ni kiungo muhimu kwani litaunganisha Wilaya ya Mbulu na Makao Makuu ya Mkoa wa Manyara.

Amefafanua pia daraja hilo litaunganisha hifadhi ya Taifa ya Manyara na Tarangire kupitia Mayoka pamoja na kuunganisha mashamba makubwa ya mpunga na miwa yaliyopo ng'ambo ya pili ya Mto na masoko ya Babati, Arusha na kwingineko kwa vipindi vyote vya mwaka.

Katibu Mkuu ameyazungumza hayo katika eneo la Magara, mkoani Manyara ambapo pamoja na mambo mengine alipokea taarifa ya mradi kutoka kwa Mshauri Elekezi M/S Crown Tech Consult na kukagua hatua za ujenzi wa daraja hilo na kusisitiza kwa mkandarasi kukamilisha daraja hilo kwa mujibu wa mkataba.

"Nimeridhishwa na kazi zilizofanyika mpaka sasa, naomba Meneja wa TANROADS endelea kusimamia daraja hili likamilike kwa muda uliopangwa", amesisitiza Arch. Mwakalinga.

Ameongeza kuwa ujenzi wa daraja hilo la Magara utachochea ukuaji wa utalii na uchumi  katika mkoa wa Manyara na Taifa kwa ujumla. Arch. Mwakalinga, ametoa wito kwa wananchi wa Magara kuendelea kutoa ushirikiano kwa mkandarasi ikiwa ni pamoja na kutojihusisha na vitendo vya wizi wa vifaa vinavyotumika katika ujenzi wa Daraja.

"Nitoe wito kwa wananchi wa maeneo haya kuwa daraja pamoja na miundombinu yake ni mali ya umma hivyo ni jukumu la wananchi kuilinda na kuitunza", amesema Arch. Mwakalinga.

Naye Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Manyara Eng. Bashiri Rwesingisa, amemueleza Katibu Mkuu huyo kuwa ujenzi wa daraja hilo unatarajia kukamilika mwezi Februari mwakani na unagharimu kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 12.

Eng. Rwesingisa ameendelea kueleza kuwa hatua za mradi mpaka sasa zimefikia asilimia 75 na kazi nyingi zimefanyika ikiwemo kuweka mihimili ya chuma kwa ajili ya kubeba zege la juu la Daraja limekamilika asilimia 100. Ameongeza kuwa katika mradi huo mkandarasi atatakiwa kuhakikisha mazingira ya Mto Magara yanakuwa salama hii ikiwa ni pamoja na kupanda miti ili kuufanya mto huo usihame.

Daraja la Magara lipo umbali wa KM 21 kutoka Mbuyu wa Mjerumani katika barabara kuu ya Babati - Arusha ili kuwezesha kuvuka mto Magara katika barabara ya Mkoa ya Mbuyu wa Mjerumani - Mbulu yenye urefu wa KM 49.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Arch. Elius Mwakalinga, akitoa maelekezo kwa Mkandarasi wa Kampuni ya M/S China Railyway Seventh Group anayejenga Daraja la Magara lenye urefu wa mita 84 na barabara za maingilio KM 4 kwa kiwango cha lami, wakati alipotembelea na kukagua hatua za maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo, Mkoani Manyara.
Meneja wa Wakala wa Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Manyara Eng. Bashiri Rwesingisa, akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Arch. Elius Mwakalinga, wakati alipotembelea na kukagua hatua za maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Magara lenye urefu wa mita 84 na barabara za maingilio KM 4 kwa kiwango cha lami, Mkoani Manyara.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Arch. Elius Mwakalinga, akitoa maelekezo kwa Mshauri Elekezi kutoka Kampuni ya Crown Tech Consult anayesimamia ujenzi wa Daraja la Magara lenye urefu wa mita 84 na barabara za maingilio KM 4 kwa kiwango cha lami, wakati alipotembelea na kukagua hatua za maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo, Mkoani Manyara.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Arch. Elius Mwakalinga, akielekea kukagua hatua za ujenzi wa Daraja la Magara lenye urefu wa mita 84 na barabara za maingilio KM 4 kwa kiwango cha lami ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 75 na unatarajiwa kukamilika mwezi Februari 2020, Mkoani Manyara.

WAKULIMA WATAKIWA KUENZI MBEGU ZA ASILI

$
0
0
Na Woinde Shizza - Globu ya Jamii, Arusha

Katibu tawala mkoa wa Arusha, Richard Kwitega amewataka wakulima kote nchini kuyaenzi matumizi  ya mbegu za asili ili kuepuka tishio la kutoweka kwa mbegu hizo kutokana na mwingiliano wa matumizi ya mbegu mpya zinazoonekana kushamiri kwa wingi kwa wakulima. 

Rai hiyo ameitoa mwishoni mwa wiki katika maonyesho  ya mbegu na vyakula vya asili yaliyoandaliwa na Mtandao wa Vikundi vya Wakulima MVIWATA na kufanyika kwa siku moja wilayani Karatu, ambapo wakulima kutoka mikoa mbalimbali nchini walifanya maandamano na kuonyesha mbegu za mazao mbalimbali ya asili. 

Aidha alisema changamoto nyingine inayoikumba mfumo huo wa mbegu usio rasmi ni pamoja na kutofika kwa wakulima kwa wakati kutokana na uratibu na usambazaji  usio wa uhakika hivyo kupelelekea wakulima kutumia mbegu za kisasa katika kilimo .

Alibainisha kupuungua kwa uhifadhi wa mbegu unaosababishwa na ukame hivyo ambapo amewataka wakulima kutumia maonyesho hayo kupanua wigo kwa wakulima ila kutatua changamoto hizo za utumiaji na upatikanaji wa mbegu za asili.

mratibu wa MVIWATA Mkoa wa Arusha, Richard Masandika amesema kuwa kupitia mradi wao wa kilimo endelevu sheria ya mbegu ya mwaka 2016 imekuwa kikwazo kikubwa kwa wakulima katika kutekeleza mfumo wa mbegu za asili na kuitaka serikali itazame upya sheria hiyo ili matumizi ya mfumo usio rasimi yaweze kutambulika na kufufua matumaini mapya kwa mkulima.

Amesema kuwa wadau wa kilimo endelevu waliamua kuwasaidia wakulima kupunguza kero ya upatikanaji wa mbegu kwa kufufua mfumo wa matumizi  ya mbegu za asili ambao wakulima wengi wanazitumia kwa kuhamasisha uhuru wa Mbegu 

Alisema kuwa serikali inazitambua mbegu za asili kupitia wadau Wa mbegu za asili 

 Mwenyekiti wa mviwata John Safari ameiomba serikali kutambua mfumo wa mbegu usio rasimi ili wakulima wapate uhuru wa matumizi yanayokubalika kwani sheria za mbegu hapa nchini hajitambui mbegu za asili kwani zinawasidia katika kilimo na kupunguza garama za mbegu

 Baadhi ya wananchi waliohudhuria maonyesho hayo ya mbegu za asili wamepongeza hatua ya kuandaa maonyesho hayo ya mbegu za asili na wameiomba serikali kuzitambua mbegu za asili na kuziwekea sheria na kuweka katika mfumo ulio rasmi kwani mbegu hizo hazitumii gharama kubwa kama mbegu nyingine.

Dkt. Kalemani: Mwanakijiji kuweka umeme ni lazima si hiari

$
0
0
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani,( katikati) akikata utepe kushiria
kuwasha umeme katika moja ya shule za msingi katika Kijiji cha Saja,
wilayani ya Wanging’ombe mkoani Njombe.

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani,( kulia) akiwa ameshika mkuki
huku amevaa mavazi maalum baada ya kusimikwa kuwa Chifu wa Kijiji
cha Ihalula, kutoka kwa mmoja wa wazee wa kimila( aliyesimama kulia),
baada kuwasha umeme katika kijiji hicho kilichopo Halmashauri ya Wilaya
ya Njombe mkoani Njombe.


Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani,( wa pili kulia) akitoa maelekezo
baada ya kutembelea chumba kujifungulia akina mama wajawazito katika
Kituo cha Afya cha Ihalula, katika halmashauri ya wilaya ya Njombe,
mkoani njombe,baada ya kuwasha umeme katika zahanati hiyo.


Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani,( kushoto) akigana na Mbunge
wa Wanging’ombe, Gerson LWENGE( kulia) baada ya kuwasha umeme
katika Kijiji cha Itombololo, wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe.
***************

Na Zuena Msuya, Njombe

Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani, amesema zoezi la mwakijiji
yeyote kuunganishiwa umeme ni lazima siyo hiari kwa kuwa kila mtanzania
hasa walio vijijini wanamudu gharama ya kuunganishiwa umeme kutokana
na kiwango cha gharama kilichopangwa na serikali.

Dkt.Kalemani alisema serikali imetumia fedha nyingi kugharamia
utekelezaji wa Mradi wa Usambazaji wa Umeme vijijini(REA) ili uweze
kuwafikia wananchi wote walioko vijijini ambao wanatakiwa kuchangia kiasi
kidogo cha fedha ili kuunganishwa na huduma hiyo.

Dkt.Kalemani alisema hayo wakati akiwasha umeme katika vijijini vinne
ambavyo ni Ihalula, Itombololo, Itowo na Saja vilivyopo katika Halmashauri
ya Wilaya Njombe na Wanging’ombe mkoani Njombe, Septemba 2,2019.

Kwa mujibu wa Dkt.Kalemani, Serikali iliangalia hali ya uchumi kwa
wananchi wake wote hasa wanaoishi Vijijini na kujiridhisha kuwa kila
mlengwa anauwezo kwa kuchangia shilingi 27,000/= ikiwa ni gharama
nafuu ya kuunganishiwa umeme kwa kuwa gharama zingine za kutekeleza
mradi huo zinalipwa na serikali.

Alifafanua kuwa zoezi kuunganisha umeme kwa kila nyumba ya mwanakijiji
anaeishi kijijini ni lazima kwa sababu Mradi wa Usambaji Umeme Vijijini(
REA) unaunganisha nyumba za aina zote na maeneo yote ya vijijini bila
kujali itikadi za Kisiasa, Imani za Dini, wala Kabila.

Aliendelea kusisitiza kuwa, hapo baadaye serikali itafanya zoezi la kukagua
nyumba moja baada ya nyingine zilizopo vijijini kufuatilia zoezi la
uunganishwaji wa umeme kwa wanavijiji, na endapo watabaini kuwa
mwakijiji ameshindwa kuunganisha huduma hiyo bila sababu ya msingi,
basi itamlazimu kuuza mifugo au mazao ili kupata shilingi 27,000/= ikiwa ni
gharama ya kunganisha umeme kwa lazima.

“Zoezi la kuweka umeme katika kila nyumba vijijini ni lazima siyo hiari
kama mnavyodhani, serikali imetumia fedha nyingi kutekeleza mradi wa (
REA),pia ni nia ya kuwasogezea huduma bora na za msingi kwa
maendeleo ya wananchi wake, ambao na wao watachangia gharama
ndogo: Sasa usipoweka umeme tutakuja kuuza chochote unachozalisha
nyumbani kwako tukulipie huduma hii”. Alisema Dkt.Kalemani.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari Amtambulisha Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu

$
0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw.Bernad Patrick( kulia) akizungumza na watumishi wa wizara hiyo kituo cha Dar es Salaam wakati alipokuwa akimtambulishwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Susan Mlawi (kushoto) mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kituo cha Dar es Salaam wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu wa wizara hiyo Bw.Bernad Patrick (hayupo pichani) wakati alipokuwa anatambulishwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Susan Mlawi (hayupo pichani) mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw.Bernad Patrick akizungumza na watumishi wa wizara hiyo kituo cha Dar es Salaam wakati alipokuwa akimtambulishwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Susan Mlawi mapema hii leo jijini Dar es Salaam.Picha na WHUSM – Dar es Salaam

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AMUWAKILIOSHA RAIS MAGUFULI KUAGA MWILI WA KADUMA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo Sept 03,2019 amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe magufuli kwenye Shuhuli ya kuaga Mwili wa Mwanasiasa Mkongwe Nchini Marehemu Ibrahim kaduma.

Katika salam zake za pole kwa Wanafamilia, wafiwa na Watanzania wote kwa Ujumla, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amewaomba kuwa na Subira na Uvumilivu katika kipindi hiki cha Maombolezo na kumuomba Mwenyezi Mungu kuwapa nguvu na Moyo wa Subira.

Wakati wa Uhai wake Marehemu Ibrahim Kaduma aliwahi kuwa Mwanasiasa pamoja na kupitia ngazi mbali mbali za Uongozi hapa nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa Heshima za Mwisho mbele ya Jeneza lenye Mwili wa Mwanasiasa Mkongwe Nchini Marehemu Ibrahim Kaduma katika Kanisa la KKKT Makongo Juu leo Sept 03,2019 ambapo Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye Msiba huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisani kitabu cha kumbukumbu ya maombolezo kufuatia kifo cha Mwanasiasa Mkongwe nchini Marehemu Ibrahim Kaduma alipowasili katika Kanisa la KKKT Makongo Juu kwa ajili ya kumuwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye Shuhuli ya kuaga Mwili wa Mwanasiasa huyo leo Sept 03,2019. Kushoto ni Dkt. Alex Malasusa Askofu wa KKKT Dayosis ya Mashariki na Pwani.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimfariji, Mjane wa Marehemu Marehemu IBrahim Kaduma katika Kanisa la KKKT Makongo Juu, jijini Dar es salaam leo Sept 03,2019.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Dkt. Alex Malasusa Askofu wa KKKT Dayosis ya Mashariki na Pwani alipowasili katika Kanisa la KKKT Makongo Juu kwa ajili ya kumuwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye Shuhuli ya kuaga Mwili wa Mwanasiasa Mkongwe Marehemu IBrahim Kaduma leo Sept 03,2019.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na kuwapa pole Baadhi ya Wajukuu na Vitukuu vya Mwanasiasa Mkongwe Nchini Marehemu IBrahim Kaduma wakati wa shuhuli ya kuaga Mwili wa Mwanasiasa huyo leo Sept 03,2019 katika kanisa la KKKT Makongo Juu, Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye Msiba huo.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AMUWAKILIOSHA RAIS MAGUFULI KUAGA MWILI WA KADUMA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo Sept 03,2019 amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe magufuli kwenye Shuhuli ya kuaga Mwili wa Mwanasiasa Mkongwe Nchini Marehemu Ibrahim kaduma.

Katika salam zake za pole kwa Wanafamilia, wafiwa na Watanzania wote kwa Ujumla, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amewaomba kuwa na Subira na Uvumilivu katika kipindi hiki cha Maombolezo na kumuomba Mwenyezi Mungu kuwapa nguvu na Moyo wa Subira.

Wakati wa Uhai wake Marehemu Ibrahim Kaduma aliwahi kuwa Mwanasiasa pamoja na kupitia ngazi mbali mbali za Uongozi hapa nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa Heshima za Mwisho mbele ya Jeneza lenye Mwili wa Mwanasiasa Mkongwe Nchini Marehemu Ibrahim Kaduma katika Kanisa la KKKT Makongo Juu leo Sept 03,2019 ambapo Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye Msiba huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisani kitabu cha kumbukumbu ya maombolezo kufuatia kifo cha Mwanasiasa Mkongwe nchini Marehemu Ibrahim Kaduma alipowasili katika Kanisa la KKKT Makongo Juu kwa ajili ya kumuwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye Shuhuli ya kuaga Mwili wa Mwanasiasa huyo leo Sept 03,2019. Kushoto ni Dkt. Alex Malasusa Askofu wa KKKT Dayosis ya Mashariki na Pwani.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimfariji, Mjane wa Marehemu Marehemu IBrahim Kaduma katika Kanisa la KKKT Makongo Juu, jijini Dar es salaam leo Sept 03,2019.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Dkt. Alex Malasusa Askofu wa KKKT Dayosis ya Mashariki na Pwani alipowasili katika Kanisa la KKKT Makongo Juu kwa ajili ya kumuwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye Shuhuli ya kuaga Mwili wa Mwanasiasa Mkongwe Marehemu IBrahim Kaduma leo Sept 03,2019.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na kuwapa pole Baadhi ya Wajukuu na Vitukuu vya Mwanasiasa Mkongwe Nchini Marehemu IBrahim Kaduma wakati wa shuhuli ya kuaga Mwili wa Mwanasiasa huyo leo Sept 03,2019 katika kanisa la KKKT Makongo Juu, Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye Msiba huo.

CHMTs KAGERA WAFUNDWA KUJIKINGA DHIDI YA UGONJWA WA EBOLA

$
0
0
Na Rayson Mwaisemba WAMJW- KAGERA

Timu za uendeshaji huduma za Afya za Halmashauri (CHMTs) za Mkoa wa Kagera zimeelekezwa jinsi ya kujikinga dhidi ya ugonjwa wa Ebola, ikiwa ni moja kati ya mikakati ya Serikali kuwakinga Watumishi wa Sekta ya Afya endapo utaingia nchini.

Hayo yamejiri wakati wa mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kudhibiti magonjwa (Maambukizi) kwa kuzingatia taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC Standard) inayoendelea Mkoani Kagera ikiwa ni moja kati ya mikoa iliyo katika hatari ya kupata ugonjwa wa Ebola.

Katika Mafunzo hayo, Afisa kutoka Kitengo cha Dharura na Maafa Wizara ya Afya Dkt. Alex Sanga amesema kuwa Tanzania ni moja kati ya nchi ambazo zipo katika hatari ya kupata wagonjwa wa Ebola kutokana na mwingiliano mkubwa wa watu na ukaribu na Nchi ya Uganda na Jamhuri ya Demokrasia ya Congo ambazo tayari zimekwishapata janga hilo.

Dkt. Sanga amesema kuwa, taarifa za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinasema kuwa takribani zaidi ya Wagonjwa 2950 wamethibitika kuwa na Ugonjwa wa Ebola, huku zaidi ya Wagonjwa 2000 wakipoteza maisha tokea mlipuko huo ulipojitokeza Agosti 2018, huku Wataalamu wa Afya 131 walipata maambukizi, ambapo 41 kati yao wamepoteza maisha

Aidha, Sanga amesema kuwa Serikali ya Tanzania imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuimarisha utayari wa kukabiliana na tishio la Ugonjwa huo ili kuhakikisha hauingii nchini, ikiwemo kuelimisha jamii njia za kujikinga na Ugonjwa ili kuzuia usiingie nchini, na kutoa Elimu kwa Watoa huduma za Afya juu ya kumuhudumia mtu mwenye dalili za Ebola endapo atatokea.

"Watoa huduma wanatakiwa kuzingatia taratibu za kujikinga na kudhibiti maambukizi (IPC Standard precautions) kwa kadri Miongozo inavyoelekeza wakati wote watoapo huduma kwa Wagonjwa, jambo litalosaidia kuwaepusha kupata maambukizi, au kumsaidia mgonjwa kupata maambukizi mapya wakati wa matibabu” Alisema Dkt. Alex Sanga

Hata hivyo, Dkt. Sanga amesema kuwa, Shirika la Afya Duniani (WHO) inakusudia kuzuia Ugonjwa wa Ebola kwa kuimarisha huduma za uchunguzi na kusaidia nchi zilizo katika hatari ya kupata ugonjwa wa Ebola.

Kwa upande wake Mtaalamu wa Maabara kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi MUHAS Akili Mawazo Mwakabhana amesisitiza umuhimu wa kufuata taratibu na miongozo wakati wa kutoa huduma kwa mgonjwa kuzuia maambukizi mapya kwa Mgonjwa au Mtoa huduma za Afya jambo ambalo litasaidia kupunguza idadi ya Wagonjwa na kuokoa fedha ambazo zingetumika katika matibabu. 

Aliendelea kusisitiza kwa kutoa wito kwa watoa huduma za Afya kuacha kufanya kazi kwa mazoea hali itakayosaidia kuondoa tatizo la usugu wa magonjwa (Wadudu) kutokana na matumizi mara kwa mara ya dawa, ambayo daktari angeweza kuyazuia kwa kufuata miongozo wakati wakutibu ugonjwa.
 Afisa kutoka Kitengo cha Dharura na Maafa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Alex Sanga akieleza namna ya uvuaji wa maski baada ya kumuudumia mgonjwa wa Ebola endapo atatokea, mbele ya Wataalamu wa Sekta ya Afya, wakati wa Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kudhibiti magonjwa kwa kufuata mmiongozo ya (IPC guideline),
 Afisa kutoka Kitengo cha Dharura na Maafa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Alex Sanga akionesha vazi la kujikinga wakati wa kumuudumia mgonjwa wa Ebola endapo atatokea, mbele ya Wataalamu wa Sekta ya Afya, kutoka Halmashauri za Mkoa wa Kagera.
 Baadhi ya Wataalamu wa Sekta ya Afya kutoka Halmashauri mbali mbali za Mkoa wa Kagera wakijipima uelewa kupitia maswali yaliyotolewa na Wizara ya Afya, katika mafunzo ya namna ya kujikinga dhidi ya mmagonjwa ikiwemo ugonjwa wa Ebola endapo utaingia nchini.
 Baadhi ya Wataalamu wa Sekta ya Afya kutoka Halmashauri mbali mbali za Mkoa wa Kagera wakijipima uelewa kupitia maswali yaliyotolewa na Wizara ya Afya, katika mafunzo ya namna ya kujikinga dhidi ya mmagonjwa ikiwemo ugonjwa wa Ebola endapo utaingia nchini.
 Mtaalamu wa Maabara Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikikishi MUHAS Bw. Akili Mawazo Mwakabhana akiendelea na kutoa mafunzo  kwa Wataalamu wa Sekta ya kutoka Halmashauri  za Mkoa wa Kagera wakati wa Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga dhidi ya maambukizi kwa kufuata miongozo ya utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC guideline).
Picha ya Pamoja ikiongozwa na Wataalamu kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto sambamba na Wataalamu wa Sekta ya Afya kutoka Halmashauri za Mkoa wa Kagera baada ya kumaliza mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kudhibiti magonjwa Magonjwa ikiwemo ugonjwa wa Ebola kwa kufuata muongozo wa utoaji huduma kwa Wagonjwa (IPC guideline).

PACHA ALIYETENGANISHWA NA MWENZIE AFARIKI DUNIA MUHIMBILI

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

IKIWA zimepita siku nne tangu mapacha Merryness na Anosia kurejea nchini kutoka nchini Saudi Arabia walikofanyiwa upasuaji mmoja wa pacha hao amefariki dunia jana usiku katika hospitali ya taifa Muhimbili.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa huduma za upasuaji wa hospitali hiyo Dkt.Suphian Baruan amesema kuwa Anisia amesema kuwa pacha huyo amefariki dunia wakati wakimpatia matibabu.

Amesema kuwa tangu walivyorejea nchini Anisia alionekana kuwa na tatizo na wakaanza kumfanyia uchunguzi ikiwa ni pamoja na kumpatia matibabu.

Daktari wa upasuaji wa watoto Petronilla Ngilino amesema kuwa wakati wakiendelea kumfanyia uchunguzi Anasia alianza kutapika hali iliyowashtua na mama wa mtoto huyo aliwaeleza hali hiyo ilianza tangu walivyokuwa kwenye ndege na alikuwa akiishiwa nguvu.

"Tulifanya uchunguzi pamoja na kumwekea maji kwa kuwa yalikuwa yanapungua, pia tulizuia matapishi yasiingie kwenye mfumo wa hewa lakini baada ya uchunguzi tukabaini ana tatizo kwenye tumbo utumbo ulijikunja" ameeleza Dkt. Ngilino.

Mapacha hao walizaliwa Januari 29, 2018 katika Zahanati ya mtakatifu. Thereza Omukajungutu Wilayani Misenyi na kusafirishwa Mkoani Bukoba kabla ya kuletwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili wakiwa wameungana kuanzia kifuani hadi miguuni ambapo mfalme Salman wa Saudi Arabia alidhamini upasuaji kupitia Serikali.

Mwili wa marehemu Anisia unategemewa kusafirishwa hadi Mkoani Bukoba kwa mazishi.

BENKI ZATAKIWA KUBORESHA HUDUMA KUVUTIA TAASISI ZA UMMA

$
0
0
Na. Peter Haule na Josephine Majura, WFM, Dodoma

Serikali imeitaka Benki ya TPB na Benki nyingine nchini kuboresha mifumo ya huduma na bidhaa zao ili kuvutia Watumishi pamoja na Taasisi za Umma kutumia huduma zao.

Hayo yameelezwa bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipokuwa akijibu swali la Msingi la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Jacqueline Msongozi, aliyetaka kujua kwa nini Watumishi na shughuli zote za Serikali zisitumie huduma za kibenki kupitia Benki ya Serikali ya TPB.

Dkt. Kijaji alisema kuwa, kwa mujibu wa Sera, Sheria, Kanuni, taratibu na miongozo iliyopo ya uchumi huria, Serikali haina mamlaka ya kumlazimisha Mtumishi au Taasisi ya Umma kutumia huduma za benki yoyote ikiwemo Benki ya TPB.

“Kwa kuzingatia misingi ya nguvu ya soko, Benki ya TPB imefanikiwa kujitangaza na kuimarisha huduma na hivyo kuvutia baadhi ya Taasisi za Serikali na Mashirika ya Umma kutumia bidhaa zake”, alieleza Dkt. Kijaji.

Dkt. Kijaji alisema huduma za Benki ya TPB zinazotumiwa na Taasisi za Serikali ni pamoja na akaunti ya muda maalumu, akaunti ya biashara, malipo kwa njia ya mtandao, kubadilisha fedha za kigeni, kukusanya mapato ya Serikali, kulipa mishahara ya Watumishi, mikopo kwa Watumishi, kulipa pensheni za Wastaafu pamoja na mikopo kwa Wastaafu wanaolipwa pensheni zao na Serikali.

Alisema kuwa baada ya biashara huria ya Sekta ya Fedha na kupitishwa kwa sheria ya Benki ya Taasisi ya fedha kuanzia mwaka 1991, Wawekezaji mbalimbali walifungua benki binafsi nchini na hivyo matumizi ya huduma na bidhaa za benki kuanza kuamliwa na nguvu ya soko ikiwa ni pamoja na huduma na bidhaa za Benki za Serikali.

Akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Madaba Mhe. Joseph Mhagama, kuhusu wafanyabiashara kushindwa kufanyabiashara kwa kukosa mitaji ili hali kuna Benki ya Serikali ya TPB, Dkt. Kijaji alisema kuwa Benki hiyo ina mfumo wa kuwasaidia Wajasiriamali kwa kuwapa mafunzo na mikopo iliyo na riba nafuu.

Aidha Benki ya TPB kwa kushirikiana na Benki ya Kilimo Tanzania imetoa mikopo ya takribani Sh. bilioni 431 kwa Wakulima katika maeneo ambayo Benki ya Kilimo haina matawi, hivyo kusadifu dhima ya Serikali ya kuwafikia Wananchi wake katika kuwasaidia kukuza uchumi wao.

BENKI ZATAKIWA KUBORESHA HUDUMA KUVUTIA TAASISI ZA UMMA

$
0
0
Na. Peter Haule na Josephine Majura, WFM, Dodoma

Serikali imeitaka Benki ya TPB na Benki nyingine nchini kuboresha mifumo ya huduma na bidhaa zao ili kuvutia Watumishi pamoja na Taasisi za Umma kutumia huduma zao.

Hayo yameelezwa bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipokuwa akijibu swali la Msingi la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Jacqueline Msongozi, aliyetaka kujua kwa nini Watumishi na shughuli zote za Serikali zisitumie huduma za kibenki kupitia Benki ya Serikali ya TPB.

Dkt. Kijaji alisema kuwa, kwa mujibu wa Sera, Sheria, Kanuni, taratibu na miongozo iliyopo ya uchumi huria, Serikali haina mamlaka ya kumlazimisha Mtumishi au Taasisi ya Umma kutumia huduma za benki yoyote ikiwemo Benki ya TPB.

“Kwa kuzingatia misingi ya nguvu ya soko, Benki ya TPB imefanikiwa kujitangaza na kuimarisha huduma na hivyo kuvutia baadhi ya Taasisi za Serikali na Mashirika ya Umma kutumia bidhaa zake”, alieleza Dkt. Kijaji.

Dkt. Kijaji alisema huduma za Benki ya TPB zinazotumiwa na Taasisi za Serikali ni pamoja na akaunti ya muda maalumu, akaunti ya biashara, malipo kwa njia ya mtandao, kubadilisha fedha za kigeni, kukusanya mapato ya Serikali, kulipa mishahara ya Watumishi, mikopo kwa Watumishi, kulipa pensheni za Wastaafu pamoja na mikopo kwa Wastaafu wanaolipwa pensheni zao na Serikali.

Alisema kuwa baada ya biashara huria ya Sekta ya Fedha na kupitishwa kwa sheria ya Benki ya Taasisi ya fedha kuanzia mwaka 1991, Wawekezaji mbalimbali walifungua benki binafsi nchini na hivyo matumizi ya huduma na bidhaa za benki kuanza kuamliwa na nguvu ya soko ikiwa ni pamoja na huduma na bidhaa za Benki za Serikali.

Akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Madaba Mhe. Joseph Mhagama, kuhusu wafanyabiashara kushindwa kufanyabiashara kwa kukosa mitaji ili hali kuna Benki ya Serikali ya TPB, Dkt. Kijaji alisema kuwa Benki hiyo ina mfumo wa kuwasaidia Wajasiriamali kwa kuwapa mafunzo na mikopo iliyo na riba nafuu.

Aidha Benki ya TPB kwa kushirikiana na Benki ya Kilimo Tanzania imetoa mikopo ya takribani Sh. bilioni 431 kwa Wakulima katika maeneo ambayo Benki ya Kilimo haina matawi, hivyo kusadifu dhima ya Serikali ya kuwafikia Wananchi wake katika kuwasaidia kukuza uchumi wao.

RC MAKONDA ATIMIZA NDOTO ZA WAJANE,AKABIDHI MUSWADA WA SHERIA YA MIRATHI KWA WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo September 03 ametimiza ndoto za Wajane kwa kukabidhi Muswada wa Mapendekezo ya Mabadiliko ya Sheria ya Mirathi kwa Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dkt. Augustine Mahiga kwaajili ya Kufanyiwa maboresho na kufikishwa Bungeni.

Akikabidhi Muswada huo mapema leo Mjini Dodoma RC Makonda amesema ndani ya Muswada huo ameainisha mapendekezo ya kubadilishwa kwa Sheria kandamizi ambazo zimekuwa mwiba na Mateso kwa Wajane kwa muda wa miaka mingi.

Aidha RC Makonda amesema Miongoni mwa Sheria kandamizi anazopendekeza zifanyiwe mabadiliko ni Sheria ya Kiserikali ya Mirathi ya Mwaka 1865, Sheria ya Mirathi ya Kimila ya Mwaka 1963 na Sheria ya Mirathi ya Kidini ya Mwaka 1963 kwakuwa zimepitwa na Wakati na zimekuwa na Mapungufu mengi ya Kisheria.

RC Makonda amevitaja baadhi ya vipengele anavyopendekeza vifanyiwe maboresho ni pamoja na kipengele cha kumpa uhalali Mke wa marehemu kushiriki katika vikao vya mgawanyo wa mali, mjane kupewa haki ya kurithi na kusimamia mali za marehemu, Mjane kutoondolewa kwenye nyumba wala Mali kuhamishwa, Usawa wa watoto katika kumiliki mali za marehemu bila kujali jinsia pamoja haki ya mtoto wa nje ya Ndoa kurithi Mali.

Vifungu vingine ambavyo RC Makonda ameeleza kuwa ni kandambizi kwa Mjane ni pamoja na kipengele kinachoruhusu Mjane kurithiwa na kile kinachomnyima Mwanamke haki ya kurithi ardhi ya ukoo.

Pamoja na hayo RC Makonda amesema chimbuko la muswada huo ni mapendekezo yaliyotokana na Kongamano la Wajane zaidi ya 5,181 alilohitisha mwezi April Ukumbi wa Mlimani City ambapo katika kongamano hilo alipokea Kero na Malalamiko yaliyomlazimu kuunda kamati iliyoshirikisha Wadau na Wataalamu mbalimbali kutoka Serikalini na Asasi za Kiraia.

Kwa upande wake Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dkt. Augustine Mahiga amesema kuwa alichokifanya RC Makonda kupigania haki za wajane ni Ushujaa wa hali ya Juu na ameweka historia ya Jambo ambalo halijawahi kufanyika ambapo amemuahidi kufanyia maboresho ya haraka na kuwasilisha Bungeni.


KATIBU MSAIDIZI CPA KANDA YA AFRIKA AKUTANA NA MWAKILISHI WA SPIKA WA PAKISTAN MJINI ZANZIBAR

$
0
0
Katibu Msaidizi wa Chama cha Mabunge Jumuiya ya Madola (CPA) Kanda ya Afrika, Ndg. Said Yakubu (kulia) akisalimiana na Mwakilishi Maalum wa Spika wa Pakistan, Ndg. Shandana Gulzar Khan ambae pia ni mgombea wa nafasi ya Uenyekiti wa dunia wa Wabunge wanawake wa Jumuiya ya Madola. Shandana Gulzar Khan ni mmoja kati ya wageni maalum waalikwa katika Mkutano wa Chama cha Mabunge Jumuiya ya Madola unaoendelea Mjini Zanzibar.
Katibu Msaidizi wa Chama cha Mabunge Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika, Ndg. Said Yakubu (kulia) akizungumza na Mwakilishi Maalum wa Spika wa Pakistan, Ndg. Shandana Gulzar Khan ambae pia ni mgombea wa nafasi ya Uenyekiti wa dunia wa Wabunge wanawake wa Jumuiya ya Madola. Shandana Gulzar Khan ni mmoja kati ya wageni maalum waalikwa katika Mkutano wa Chama cha Mabunge Jumuiya ya Madola unaoendelea Mjini Zanzibar.
Katibu Msaidizi wa Chama cha Mabunge Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika, Ndg. Said Yakubu (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mwakilishi Maalum wa Spika wa Pakistan, Ndg. Shandana Gulzar Khan ambae pia ni mgombea wa nafasi ya Uenyekiti wa dunia wa Wabunge wanawake wa Jumuiya ya Madola. Shandana Gulzar Khan ni mmoja kati ya wageni maalum waalikwa katika Mkutano wa Chama cha Mabunge Jumuiya ya Madola unaoendelea Mjini Zanzibar.

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

Mbunge David Mathayo aendea na ziara jimboni kwake

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Same Magharibi wilayani Same Mkoani Kilimanjaro dakta Mathayo D.Mathayo ametenga Zaidi ya shilingi million mia moja kwa ajili ya kuibua vipaji na kuimarisha michezo katika jimbo hilo.

Mbunge huyo ambae ameanza kugawa mipira katika kila kata kwa ajili ya maandalizi ya mashinda hayo yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi mapema mwezi ujao yatashindanisha timu za wanawake kwa upande wa mpira wa pete na wanaume kwa upande wa mpira wa miguu.

Akizungumza na wananchi wa kata zote 20 anazotembelea Mathayo amesema katika kila kata watashindana vijiji kwa vijiji kwa mtindo wa marudiano mara tatu tatu ili aweze kupatikana mshindi kwa upande wa wanawake na wanaume.

“Nataka mshindane kila kijiji na kijiji na kijiji kitakachoshinda kwenye kila kata,kitapata zawadi ya shilingi milioni mbili kwa timu ya wanawake na shilingi milioni mbili kwa timu ya wanaume”alisema Mathayo

Mathayo amesema ametenga shilingi milioni themanini taslim kwa ajili ya timu zitakazoibuka  kidedea katika kila kata.

“Ndugu zangu michezo ni afya michezo ni ajira leo namkabidhi mhe diwani hii mpira lakini asiigawe mpaka nitakapoleta jezi ili muanze mashindano hayo mkiwa na jezi zinazotofautina au mnataka kucheza kienyeji”alihoji Mathayo

Mathayo pia amekuwa akigawa mipira katika shule za msingi na sekondari katika kata mbalimbali jimboni kwake.
Mbunge wa jimbo la Same Magharibi akitoa somo kwa wananchi wa kata ya Same Mjini,Kisiwani na Stesheni kwa njia ya mabango kuhusu kazi kubwa zilizofanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais Magufuli.
Mbunge wa jimbo la Same Magharibi Dakta Mathayo David Mathayo akiwakabidhi Mwenyekiti wa mji mdogo wa Same Eliamini Mkongo na diwani wa viti Maalum CCM Halima Mgonja fedha Taslim kwa ajili ya maendeleo mbalimbali katika kata hiyo kama alivyoahidi wakati akiomba ridhaa ya kuwaongoza wananchi wa Jimbo hilo kwa awamu ya tatu.

MAKATIBU MEZANI WA CPA WAFANYA MKUTANO WA MWAKA

$
0
0
Menyekiti wa Chama cha Makatibu Mezani cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola (SoCATT), ambaye pia ni Katibu wa Bunge la Zambia, Ndugu Cesilia Mbewe akizungumza katika Mkutano wa Mwaka wa chama hicho uliofanyika katika Hoteli ya Madinat Al Bahr Visiwani Zanzibar. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho, Ndugu Michael Sialai na kushoto ni Katibu Mezani wa Bunge la Zambia, Ndugu Elsio Simpamba
Wajumbe wa Chama cha Makatibu Mezani cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola (SoCATT), wakiwa katika Mkutano wa Mwaka wa chama hicho uliofanyika katika Hoteli ya Madinat Al Bahr Visiwani Zanzibar.

DK.SHEIN AKUTANA NA UONGOZI WA WIZARA YA UJENZI,MAWASILIANO NA USAFIRISHAJI.

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji katika mkutano wa utekelezaji wa  mpango kazi wa Mwaka wa Fedha kwa kipindi cha Julai  2018-Juni 2019 na mpango kazi wa mwaka 2019-2020 uliofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,[Picha na Ikulu.] 03/09/2019.
 Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji Mhe.Sira Ubwa Mamboya (katikati) alipokuwa akisoma muhtasari  wa utekelezaji wa  mpango kazi wa Mwaka wa Fedha kwa kipindi cha Julai  2018-Juni 2019 na mpango kazi wa mwaka 2019-2020 wa Wizara hiyo katika mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,(kushoto) Naibu Waziri wa Wizara hiyo  Mohamed Ahmed Salum  na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Kaimu Katibu Kiongozi Salum Maulid Salum (kulia)
 Baadhi ya Viongozi wa Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji wakiwa katika mkutano wa utekelezaji wa  mpango kazi wa Mwaka wa Fedha kwa kipindi cha Julai  2018-Juni 2019 na mpango kazi wa mwaka 2019-2020 uliofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) [Picha na Ikulu.] 03/09/2019.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji katika mkutano wa utekelezaji wa  mpango kazi wa Mwaka wa Fedha kwa kipindi cha Julai  2018-Juni 2019 na mpango kazi wa mwaka 2019-2020 uliofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,[Picha na Ikulu.] 03/09/2019.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Kaimu Katibu Kiongozi Salum Maulid Salum (kulia) alipokuwa akichangia katika mkutano wa  utekelezaji  wa  mpango kazi wa Mwaka wa Fedha kwa kipindi cha Julai  2018-Juni 2019 na mpango kazi wa mwaka 2019-2020 uliofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,(katikati) Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji Mhe.Sira Ubwa Mamboya na Naibu wake Mohamed Ahmed Salum [Picha na Ikulu.] 03/09/2019.

Tigo yazindua huduma ya kwanza na ya kipekee ya Home Internet

$
0
0
Wateja wa Kampuni ya mawasiliano,Tigo, kwa mara ya kwanza watapata fursa ya kufurahia huduma Home Internet yenye kasi ya 4G+ majumbani mwao. Huduma hii ni ya kwanza na ya kipekee Tanzania, yenye ubunifu wa hali ya juu itakayowafanya wateja wafurahie intaneti ya 4G+ kwa kutumia vifaa vya Router au Modem.

Kampuni ya simu ya Tigo imezindua rasmi huduma hiyo ambayo itatatua changamoto ambazo watumiaji wa mitandao ya simu hususan wale wa majumbani wamekuwa wakikabiliana nazo.

Kupitia huduma hiyo, wateja wa kampuni ya Tigo sasa watapata fursa ya kupanga na kuchagua ni jinsi gani watatumia huduma ya intaneti, ikiwemo kununua vifurushi, kuongeza na kuangalia salio kupitia simu zao za mkononi.

“Mrejesho kutoka kwa wateja wetu umeonyesha kwamba kuna umuhimu wa uwepo wa huduma rahisi na ya uhakika ya mtandao wa intaneti majumbani. Hata hivyo, uzoefu katika matumizi ya huduma ya mtandao wa intaneti majumbani kwa wateja ni jambo lenye umuhimu mkubwa sana kwetu,” ameeleza Mkuu wa kitengo cha Biashara cha Kampuni ya Tigo, Tarik Boudiaf.

“Zama zile za mteja kusumbuka kutumia simu yake ya mkononi kama modem au kuhamisha line inayotumika kwenye modem au router ili kupata huduma ya intanet zimekwisha pita kitambo. Zama za kununua kifurushi ama kuongeza au kuangalia salio la laini inayotumika kwenye modem au router kwa kutumia kifaa kingine, ni jambo ambalo humpa mteja usumbufu, nazo zimekwisha pita kitambo,” ameongeza Boudiaf.

Kupitia huduma hii iliyozinduliwa na Tigo, wateja sasa wanaweza kupangilia matumizi yao ya huduma ya intaneti kwa kuunganisha vifaa vya modem na router kutumia Tigo Pesa App.

“Lengo letu ni kuhakikisha kuwa kila mteja wa Tigo nchini ambaye atahitaji kutumia huduma yetu ya Home Internet anaunganishwa muda wote bila vikwazo vyovyote,” ameongeza Boudiaf.
Kwa mujibu wa Boudiaf, huduma hii mpya iliyozinduliwa kwa mara ya kwanza nchini ni sehemu tu ya jitihada za kampuni ya Tigo ya kutoa huduma zinazojali maslahi ya wateja katika kuwapa uzoefu endelevu wa kijiditali kupitia mtandao wenye kasi zaidi wa 4G+.

Uzinduzi wa huduma hii mpya umeshuhudiwa pia na Meneja huduma za intaneti wa kampuni ya Tigo, Mkumbo Myonga, ambaye amewahakikishia wateja kupata huduma bora na rahisi wanapojuanga na huduma ya Home Internet.

Ili kujiunga na kufurahia huduma hiyo ya Home Internet, wateja wa Tigo wanaweza kununua modem au router katika maduka ya Tigo yaliyopo nchi nzima. Wateja wa Home internet wanaweza kuwasiliana na kitengo cha huduma kwa wateja wakati wowote, yani masaa 24 kwa siku.

Ili kufurahia huduma hiyo, wateja wa kampuni ya mawasiliano Tigo wanaweza kununua kwa urahisi vifurushi vya Home Internet kwa kutumia Tigo Pesa App, au kwa kutembelea tovuti ya; internet.tigo.co.tzau pia kwa kupiga *147*00# ili kujiunga mwenyewe au kununulia ndugu, jamaa na marafiki kifurushi cha Home Internet.

Wateja wa Tigo watapata huduma hiyo ya Home Internet kulingana na thamani ya fedha zao kwa kununua kifurushi cha wiki au mwezi, kwa kuanzia Tsh15,000 kwa GB12 kwa siku 7 hadi Tshs120,000 kwa GB200 kwa mwezi mmoja.

Vifaa hivyo vitapatikana kwa urahisi kwa bei ya rejareja ya Sh150,000 kwa Modem na Sh250,000 kwa Routers, ambapo mteja wa Tigo akinunua atapata na kifurushi cha bure cha intaneti cha mwezi mmoja cha GB40 na GB100.
Meneja Huduma za Intaneti Mkumbo Myonga akiwaelezea waandishi wa habari,jinsi gani Mteja anaweza kuangalia salio, kununua kifurushi kwa kupitia Tigo Pesa App katika uzinduzi wa huduma ya kipekee ya Home Internet, Kushoto kwake ni Afisa Mkuu wa Biashara, Tarik Boudiaf.
Mkuu wa Bidhaa na Huduma kutoka Tigo, David Umoh akimkabidhi Home Internet Router Mtangazaji wa Clouds Tv, Abdallah Kamelo, katika uzinduzi wa huduma ya kwanza na ya kipekee ya Home Internet kutoka Tigo, Katikati ni Afisa Mkuu wa Biashara, Tarik Boudiaf

Matukio Katika Picha Bungeni Leo

$
0
0
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Agustine Ndugai akitoa taarifa ya kuanza kutumia mfumo wa Tehama badala ya badala ya mfumo wa makaratasi katika kuwasilisha orodha ya shughuli za bunge wakati wa Mkutano wa 16 wa Bunge, Kikao cha Kwanza leo jijini Dodoma tarehe 3 Septemba 2019.
Mbunge wa Singida Mashariki, Mhe. Miraji Mtaturu akila kiapo mbele ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Agustine Ndugai wakati wa Mkutano wa 16 wa Bunge, Kikao cha Kwanza leo jijini Dodoma tarehe 3 Septemba 2019. Mbunge wa Singida Mashariki, Mhe. Miraji Mtaturu akisalimiana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenyeulemavu, Mhe. Jenista Mhagama mara baada ya kula kiapo wakati wa Mkutano wa 16 wa Bunge, Kikao cha Kwanza leo jijini Dodoma tarehe 3 Septemba 2019. Kutoka kulia ni Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Adeladus Kilangi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe(kulia), Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako(kushoto) na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (katikati) wakifurahia jambo wakati wa Mkutano wa 16 wa Bunge, Kikao cha Kwanza leo jijini Dodoma tarehe 3 Septemba 2019. Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile akijibu swali wakati wa Mkutano wa 16 wa Bunge, Kikao cha Kwanza leo jijini Dodoma tarehe 3 Septemba 2019. Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elias Kwandikwa akifafanua jambo walipokuwa akijibu swali katika Mkutano wa 16 wa Bunge, Kikao cha Kwanza leo jijini Dodoma tarehe 3 Septemba 2019. Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ulinzi, Mhe. Mussa Hassan Zungu akiwasilisha Azimio la Bunge la kupmpongeza Mhe. Rasi Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa SADC na kuendesha vyema Mkutano wa 39 wa Jumuiya hiyo wakati wa Mkutano wa 16, Kikao cha Kwanza leo jijini Dodoma tarehe 3 Septemba 2019. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Boniphace Simbachawene (aliyesimama) akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Bumbuli mkoani Tanga ambaye pia ni Waziri wa Zamani wa Ofisi hiyo, Mhe. Januari Makamba (wapili kushoto) walipokutana katika Kikao cha Kwanza cha Mkutano wa 16 wa Bunge leo jijini Dodoma tarehe 3 Septemba 2019. Kulia ni Mbunge wa Kibaha, Mhe. Sylivester Koka. Mbunge wa Singida Mashariki, Mhe. Miraji Mtaturu akiuliza swali la nyongeza wakatiwa kikao cha kwanza cha Mkutano wa 16 wa Bunge leo tarehe 3 Septemba 2019 jijini Dodoma. Mbunge huyo ameapishwa leo baada ya kupita bila kupingwa katika uchaguzi mdogo uliofanyika kutokana na nafasi kuwa wazi baada ya aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo kukosa sifa ya kuendelea na Ubunge. Baadhi ya wananchi wa Jimbo la Singida Mashariki waliomsindikiza Mbunge wao Mhe. Miraji Mtaturu kushuhudia hafla ya kuapishwa kwake wakipunga mikono baada ya kutambulishwa Bungeni katika Mkutano wa 16 wa Bunge kikao cha kwanza leo tarehe 3 Septemba 2019 jijini Dodoma. Mhe. Mtaturu amesindikizwa na zaidi ya wananchi 200 kutoka jimboni kwake. (Picha na Idara ya Habari – MAELEZO)

Serikali Kusomesha Madaktari Bingwa 365 kwa Ajili ya Kusambazwa Maeneo yenye Uhaba

$
0
0
Na Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma. 

Jumla ya madaktari bingwa 365 wanatarajia kuhitimu mafunzo kuanzia mwaka wa wasomo 2019/2020, 2020/2021 na 2021/2022 ambao watasambazwa kwenye hospitali mbalimbali nchini kulingana na uwiano wa wataalamu waliopo pamoja na kuzingatia maeneo yenye uhaba mkubwa.

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile amesema hayo leo Bungeni Jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Sonia Jumaa Magogo juu ya mkakati wa Serikali wa kuongeza Madaktari Bingwa nchini.

"Serikali inaendelea kuimarisha huduma za kibingwa katika ngazi mbalimbali za huduma nchini ikiwa ni pamoja na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili," amesema Dkt. Ndugulile.

Ameendelea kusema kuwa katika mwaka 2017/2018, Wizara kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo, ilitenga kiasi cha shilingi bilioni 2 zilizotumika kwa ajili ya kusomesha madaktari bingwa 125 wa fani za kipaumbele katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) ambao wanatarajia kumaliza 2020/2021.

Aidha, katika mwaka 2018/2019, Serikali ilitenga kiasi cha Shilingi bilioni 1.8 ili kuendelea kugharamia mafunzo ngazi ya kibingwa katika kada mbalimbali za afya 127 katika Chuo cha MUHAS.

Dkt. Faustine amesema, katika mwaka 2019/2020, Wizara imetenga jumla ya shilingi 1,844,617,090 kwa ajili ya kugharamia mafunzo ya wataalamu bingwa katika fani za vipaumbele.

"Kutokana na uhaba uliopo kwenye hospitali za Rufaa za Mikoa, Wizara itahakikisha fedha hii inatumika vyema katika kusomesha wataalamu wanaotoka kwenye maeneo yenye uhaba mkubwa," amesema Dkt. Ndugulile.

Aidha, wizara kupitia hospitali za rufaa ngazi ya Taifa na Taasisi za nje zitaendelea kuendesha kambi za udaktari bingwa hapa nchini, kwa lengo la kusogeza huduma za kibingwa na kujenga uwezo wa wataalamu.

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile 

Mwenge wa Uhuru wazindua Kituo cha Uzalishaji Umeme Jua,

$
0
0
*Power Corner yapongezwa katika maendeleo ya wananchi 

Na Chalila Kibuda, MICHUZI TV.

WANANCHI wa Kijiji cha Mgambo kilichopo Kata ya kitunda Wilaya ya Sikonge Mkoani Tabora wamesema kuwa kupata umeme kumeongeza fursa ya ajira katika kijiji hicho.

Umeme huo umetekelezwa na kampuni ya Power Corner uliogharimu zaidi ya bilioni moja na kuunganisha kaya 195.

Wamesema kuwa hivi sasa kijiji cha kitunda kinafurahia huduma hiyo ya umeme jua na kwakweli umewezesha vijana kuweza kujiali kwa kujishughuli na mambo mbalimbali ya uzalishaji.

Hayo aliyasema kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Mzee Ali wakati wa kuzindua mradi wa umeme jua unao zalishwa na kampuni ya power corner 

Akizungumza kwaniaba ya Wananchi wezake Mzungu Maji ya Soda, alisema wanaipongeza sana Serikali kwa kushirikiana na Kampuni ya Power Corner ambao ndio watekelezaji wa mradi kwani hivi wanakunywa maji baridi,nyama safi ambazo zinahifadhiwa kwenye friji,ukikinganisha na awali.

Pia alisema mradi huo wameupokea kwa mikono miwili na kwakweli hawakutegemea kulingana na historia yake kwani awali walikuwa wanatumia umeme wa sola ya kawaida za kufunga wenyewe ambao pia ulikuwa hauna nguvu kama ulivyo huo uliozinduliwa mwenge wa Uhuru.

"Nataka niwaeleze ndugu waandishi wa Habari leo vijana wetu wanatengeneza Simu hapahapa pindi zinapoharibika,wachomeleaji wamerahisishiwa,saluni zinafunguliwa kwakweli mambo mazuri sana." Alisema Anthon Lukas.

Lukasi aliongeza kuwa ujio wa Umeme umeongeza chachu kwa wananchi kuweza kufanya kazi lakini pia umeimarisha usalama katika makazi ya watu ukilinganisha na huko nyuma.

Naye mkazi mwingine John Bernard Fundi Simu alisema awali walikuwa wanalazimika kwenda Sikonge kutengeneza lakini hivi sasa kwakweli wanafurahia ujio wa Umeme jua huo.

Naye Meneja Mradi Kanda ya Magharibi Kutoka Kampuni hiyo ya Power Corner Erick Francis akizungumzia mradi huo alisema Kampuni imepata ushirikiano mkubwa Kutoka mamlaka za Serikali katika kung'amua vijiji stahiki vya kupata huduma ya umeme.

Alisema kuwa mradi huo uliazishwa rasmi mwanzoni mwa mwezi machi 2018 ambao unauwezo wa kuzalisha kilo-whatts 20 kwa kijiji cha Mgambo na umeme wenye uwezo kilo-whatts 28kwa vijini vya mkola na Mwenge.

Kwaupande wake kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa Mzee Ali akizungumzia mradi ,kwanza alipongeza Serikali kwa kuweka Mazingira wezeshi kwa Kampuni ya Power Corner na kufikia hatua ya kuwapatia umeme wananchi.

"Nawaomba ndugu zangu wa Kijiji hiki cha Mgambo muweze kuulinda mradi huu ambao naamini umeleta fursa kubwa kwenu katika kuongeza uzalishaji Mali na kujiongezea kipato." Alisema Ali.

Alisema kuwa mradi ni mzuri na kwakuwa ameridhishwa na kiwaKanda ha ujenzi wake na Fedha ilitotumika hivyo ameuzindua rasim kupitia Mwenge wa Uhuru.

 kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Mzee Mkongea Ali akikata utepe wakati wa uzinduzi wa kituo cha uzalishaji wa umeme jua katika kijiji cha Mgambo wilaya ya Sikonge mkoani Tabora.
 Mwenge wa uhuru ukiwa katika kituo cha uzalishaji umeme jua wa unaotekelezwa na kampuni ya Power Corner.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Mzee Mkongea Ali akizungumza katika uzinduzi wa kituo cha kuzalisha umeme cha  Power Corner katika kijiji cha m, Mgambo wilayani Sikonge.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akitoa salamu wakati wa uzinduzi wa kituo cha uzalishaji wa umeme wa jua wa Power Corner katika kijiji Mgambo wilyani Sikonge mkoani Tabora.
 Meneja wa Mauzo Kanda ya Magharibi Erick Francis akizungumza na waandishi wa habar mara baada ya mwenge wa uhuru kuzindua mradi wa kituo cha uzalishaji umeme jua katika kijiji cha Mgambo wilayani Sikonge mkoani Tabora.
 Watendaji wa Kampuni ya  Power Corner wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa kituo cha kuzalisha umeme jua wa kampumni hiyo.
 watendaji wa kampuni ya power corner wakiwa katika kibao cha uzinduzi wa kituo cha uzalishaji umeme jua mara baada ya kuzindua kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa Mzee Mkongea Ali katika kijiji cha Mgambo wilaya ya Sikonge mkoani Tabora.
 Mhandisi Umeme wa Kampuni ya Power Corner Deogratias Hyera akimpa maelezo .Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Mzee Mkongea Ali kuhusiana na mtambo wa kuzalisha umeme jua katika kijiji mgambo wilaya ya Sikonge mkoani Tabora.
 Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Phares Magiri akiteta jambo na watendaji wa kampuni ya Power Corner mara baada ya uzinduzi wa kituo cha uzalishaji umeme jua katika kijiji cha Mgambo wilayani Sikonge mkoani Tabora.
Fundi Selemala Fidelis Onesmo akionesha umahiri wa kutelezesha mbao baada ya kupata umeme katika kijiji cha Mgambo wilaya ya Sikonge mkoani Tabora.
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live




Latest Images