Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109604 articles
Browse latest View live

RAIS DKT. MAGUFULI ALIPOZUNGUMZA NA WATENDAJI WA KATA ZOTE TANZANIA BARA LEO IKULU JIJINI DAR


CHMTs KAGERA WAFUNDWA KUJIKINGA DHIDI YA UGONJWA WA EBOLA

0
0
Na Rayson Mwaisemba WAMJW- KAGERA

Timu za uendeshaji huduma za Afya za Halmashauri (CHMTs) za Mkoa wa Kagera zimeelekezwa jinsi ya kujikinga dhidi ya ugonjwa wa Ebola, ikiwa ni moja kati ya mikakati ya Serikali kuwakinga Watumishi wa Sekta ya Afya endapo utaingia nchini.

Hayo yamejiri wakati wa mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kudhibiti magonjwa (Maambukizi) kwa kuzingatia taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC Standard) inayoendelea Mkoani Kagera ikiwa ni moja kati ya mikoa iliyo katika hatari ya kupata ugonjwa wa Ebola.

Katika Mafunzo hayo, Afisa kutoka Kitengo cha Dharura na Maafa Wizara ya Afya Dkt. Alex Sanga amesema kuwa Tanzania ni moja kati ya nchi ambazo zipo katika hatari ya kupata wagonjwa wa Ebola kutokana na mwingiliano mkubwa wa watu na ukaribu na Nchi ya Uganda na Jamhuri ya Demokrasia ya Congo ambazo tayari zimekwishapata janga hilo.

Dkt. Sanga amesema kuwa, taarifa za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinasema kuwa takribani zaidi ya Wagonjwa 2950 wamethibitika kuwa na Ugonjwa wa Ebola, huku zaidi ya Wagonjwa 2000 wakipoteza maisha tokea mlipuko huo ulipojitokeza Agosti 2018, huku Wataalamu wa Afya 131 walipata maambukizi, ambapo 41 kati yao wamepoteza maisha

Aidha, Sanga amesema kuwa Serikali ya Tanzania imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuimarisha utayari wa kukabiliana na tishio la Ugonjwa huo ili kuhakikisha hauingii nchini, ikiwemo kuelimisha jamii njia za kujikinga na Ugonjwa ili kuzuia usiingie nchini, na kutoa Elimu kwa Watoa huduma za Afya juu ya kumuhudumia mtu mwenye dalili za Ebola endapo atatokea.

"Watoa huduma wanatakiwa kuzingatia taratibu za kujikinga na kudhibiti maambukizi (IPC Standard precautions) kwa kadri Miongozo inavyoelekeza wakati wote watoapo huduma kwa Wagonjwa, jambo litalosaidia kuwaepusha kupata maambukizi, au kumsaidia mgonjwa kupata maambukizi mapya wakati wa matibabu” Alisema Dkt. Alex Sanga

Hata hivyo, Dkt. Sanga amesema kuwa, Shirika la Afya Duniani (WHO) inakusudia kuzuia Ugonjwa wa Ebola kwa kuimarisha huduma za uchunguzi na kusaidia nchi zilizo katika hatari ya kupata ugonjwa wa Ebola.

Kwa upande wake Mtaalamu wa Maabara kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi MUHAS Akili Mawazo Mwakabhana amesisitiza umuhimu wa kufuata taratibu na miongozo wakati wa kutoa huduma kwa mgonjwa kuzuia maambukizi mapya kwa Mgonjwa au Mtoa huduma za Afya jambo ambalo litasaidia kupunguza idadi ya Wagonjwa na kuokoa fedha ambazo zingetumika katika matibabu. 

Aliendelea kusisitiza kwa kutoa wito kwa watoa huduma za Afya kuacha kufanya kazi kwa mazoea hali itakayosaidia kuondoa tatizo la usugu wa magonjwa (Wadudu) kutokana na matumizi mara kwa mara ya dawa, ambayo daktari angeweza kuyazuia kwa kufuata miongozo wakati wakutibu ugonjwa.
 Afisa kutoka Kitengo cha Dharura na Maafa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Alex Sanga akieleza namna ya uvuaji wa maski baada ya kumuudumia mgonjwa wa Ebola endapo atatokea, mbele ya Wataalamu wa Sekta ya Afya, wakati wa Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kudhibiti magonjwa kwa kufuata mmiongozo ya (IPC guideline),
 Afisa kutoka Kitengo cha Dharura na Maafa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Alex Sanga akionesha vazi la kujikinga wakati wa kumuudumia mgonjwa wa Ebola endapo atatokea, mbele ya Wataalamu wa Sekta ya Afya, kutoka Halmashauri za Mkoa wa Kagera.
 Baadhi ya Wataalamu wa Sekta ya Afya kutoka Halmashauri mbali mbali za Mkoa wa Kagera wakijipima uelewa kupitia maswali yaliyotolewa na Wizara ya Afya, katika mafunzo ya namna ya kujikinga dhidi ya mmagonjwa ikiwemo ugonjwa wa Ebola endapo utaingia nchini.
 Baadhi ya Wataalamu wa Sekta ya Afya kutoka Halmashauri mbali mbali za Mkoa wa Kagera wakijipima uelewa kupitia maswali yaliyotolewa na Wizara ya Afya, katika mafunzo ya namna ya kujikinga dhidi ya mmagonjwa ikiwemo ugonjwa wa Ebola endapo utaingia nchini.
 Mtaalamu wa Maabara Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikikishi MUHAS Bw. Akili Mawazo Mwakabhana akiendelea na kutoa mafunzo  kwa Wataalamu wa Sekta ya kutoka Halmashauri  za Mkoa wa Kagera wakati wa Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga dhidi ya maambukizi kwa kufuata miongozo ya utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC guideline).
Picha ya Pamoja ikiongozwa na Wataalamu kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto sambamba na Wataalamu wa Sekta ya Afya kutoka Halmashauri za Mkoa wa Kagera baada ya kumaliza mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga na kudhibiti magonjwa Magonjwa ikiwemo ugonjwa wa Ebola kwa kufuata muongozo wa utoaji huduma kwa Wagonjwa (IPC guideline).

TFF WALINILIPA FEDHA KIHALALI-MALINZI

0
0
Ushahidi upande wa utetezi wa kesi inayomkabili aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Jamal Malinzi umeendelea leo kwa utetezi wake mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Malinzi amedai kuwa fedha alizolipwa na TFF, alilipwa kihalali.

Akiongozwa na Wakili wa utetezi Richard Rweyongeza mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Maira Kasonde, Malinzi alidai kuwa dola za Marekani 2,400 alizolipwa na TFF ilikuwa ni malipo baada ya kuhudhuria mkutano wa FIFA nchini Mexico, Mei 16, 2016, ambapo wakati anaenda katika mkutano huo alitumia fedha zake mfukoni, hivyo aliporudi nchini alilipwa fedha hizo.

Amedai kuwa, malipo ya dola za kimarekani 7,000 anazodaiwa kujipatia kwa njia ya udanganyifu, alilipwa kilahalali na TFF, baada  ya kuchukua fedha yake mikononi kumlipa Kocha wa timu ya vijana kiasi cha dola 7,000.

" TFF walinilipa dola za kimarekani 7,000 kwa sababu niliikopesha TFF na kumlipa mshahara kocha wa timu ya taifa ya Serengeti Boys, Kim Paulsen, kipindi hicho TFF haikuwa na fedha " alidai Malinzi.

Malinzi amedai hata dola za kimarekani 10,000 alizolipwa na TFF, alilipwa kihalali kwa sababu aliikopesha TFF  ambazo alitoa mfukoni mwake kwa ajili ya kuilipia timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 walikuwa wanacheza na timu ya vijana ya Misri na hiyo ilikuwa Juni 16, 2016.

"Nilikuwa natoa fedha zangu mfukoni kuwalipa wachezaji halafu baadaye fedha zikipatikana TFF inanilipa, hivyo niseme tu fedha hizo nilipewa kihalali na TFF na wala sikujipatia kwa njia ya udanganyifu kama jinsi shtaka la 26 linavyoeleza kuwa nilijipatia fedha hizo kwa njia ya udanganyifu" amedai Malinzi.

Mshtakiwa huyo ameendelea  kujitetea kuwa katika kipindi cha mwaka 2014 hadi 2016, ameikopesha  TFF kiasi cha Sh 320 milioni.

"Katika kipindi changu, walikuwepo  watu mbalimbali ambao walikuwa wakiikopesha TFF, lakini mimi ndio Rais wa kwanza wa TFF ambaye nilikamatwa na kufikishwa Mahakamani" alidai Malinzi

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mhasibu wa TFF Nsiande Mwanga, Karani Flora Rauya na Celestine Mwesigwa.

Malinzi, Mwesigwa na Nsiande wako rumande kwa kukabiliwa na mashtaka ya utakatishaji wa fedha kuwa miongoni mwa mashtaka  ambayo kwa mujibu wa sheria hayana dhamana huku Flora akiwa  nje kwa dhamana.

RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK. SHEIN AKABIDHIWA TUZO YA SINEMA ZETU

0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akikabidhiwa Tuzo ya Sinema Zetu na Waziri wa Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar Mhe. Balozi Ali Karume katika hafla hiyo iliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar leo.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiangali CD za Michezo ya Wasanii wa Zanzibar zilizoshinda katika mashindano ya Tuzo ya Senima Zetu,Tanzania, baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar Mhe. Balozi Ali Karume, hafla hiyo imefanyika Ikulu Zanzibar.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na kuwapongeza Wasanii wa Zanzibar kwa ushindi waliopata katika mashindano ya Sinema Zetu,walipofika Ikulu Zanzibar leo, kushoto kwa Rais Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Issa Haji Gavu na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ndh Salum Maulid wakiwa na Wasanii wa Filamu Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar na Uongozi wa Wasanii wa Filamu Zanzibar waliosimama , waliokaa kulia kwa Rais Waziri wa Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Ali Karume,Bi. Maryam Hamdani Mwenyekiti wa Baraza lac Sanaa Zanzibar na Bi. Khadija Ibrahim Dau (Bi.Hawa) Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wasanii wa Filamu Zanzibar na kushoto Naibu Waziri wa Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Lulu Msham Abdalla, Mshauri wa Rais Masuala ya Sanaa na Utamaduni Mhe. Chimbeni Kheri na Katibu Mkuu Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Ndg Omar Hassan King.
(Picha na Ikulu Zanzibbar)

mawakala 12 wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) wahukumiwa kulipa faini ya sh.Millioni moja kila mmoja ama kwenda jela miaka 20

0
0
Na Karama Kenyunko, globu ya Jamii.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewahukumu mawakala 12 wa Shirika la Ndege Tanzania  (ATCL) kulipa faini ya sh.Millioni moja kila mmoja ama kwenda jela miaka 20 baada ya kukiri kosa la kulisababishia  Shirika hilo hasara ya zaidi ya Sh. Milioni kumi.

Pia washtakiwa hao wote wameamriwa kulipa fidia ya Sh10,874,280 na mahakama pia imeamuru zana ambazo walizitumia katika kusababisha hasara ambazo ni simu kumi na tatu na Laptop sita zitaifishwe na kuwa mali ya serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

Akisoma Hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mwandamizi, Salum Ally amesema amezingatia hoja zilizotolewa na pande zote mbili, ule wa mashtaka na Utetezi baada ya washtakiwa hao kukiri makosa yao.

Washtakiwa hao waliohukumiwa  ni Fabian Ishengoma, Adamu Kamara, Marlon Masubo, Alexander Malongo, Tunu Kiluvya, Jobu Mkumbwa, Mohamed Issa, Godfrey Mgomela, Absalom Nyusi na Janeth Lubega. Mary semakweli Janet Lubega.

Mapema kabla ya kusomwa kwa adhabu Hakimu Ally aliuliza upande wa mashtaka kama walikuwa na chochote cha kusema, ambapo wakili wa serikali Mwandamizi, Wankyo Simon aliiomba Mahakama itoe adhabu kali kwa washtakiwa ili iwe fundisho kwao na kwa wengine wenye tabia kama hiyo. Pia aliiomba mahakama iamuru laptop na simu za mkononi zilizotumika katika kuisababishia serikali hasara zitaifishwe na kuwa mali ya serikali. Aidha aliiomba mahakama washtakiwa hao kulipa fidia ya hasara waliyoisababishia ATCL.

Katika utetezi kwa niaba ya washtakiwa, Wakili Benedict Inshabakaki amedai washtakiwa hao ni wakosaji wa kwanza na kwa kuwa wamekiri mashtaka yao wenyewe tunaomba wapunguziwe adhabu kwa kuwa awajaisumbua mahakama na vile vile ni vijana wadogo ambao wanafamilia zinazowategemea na pia ni nguvu kazi ya kesho.

Wakili Inshababakaki ameendelea kudai kuwa, Wateja wake hao wamekaa ndani kwa zaidi ya miezi nane, hivyo watakuwa wamejifunza na wanajutia hivyo, tunaomba walipe faini na siyo kifungo gerezani.

"Licha ya washtakiwa kuonesha kujutia kitendo hicho cha kuisababishia ATCL hasara natoa adhabu ya kila mshtakiwa kulipa faini ya Sh. Milioni moja ama kwenda jela miaka 20, pia wanatakiwa kulipa fidia ya hasara hiyo kwa ATCL mahakama pia inaamuru zana zilizotumika katika kusababisha hasara ambazo ni Simu 13 na Laptop sita zitaifishwe kuwa Mali ya serikali na kama washtakiwa hamjaridhika na hukumu, rufaa iko wazi" amesema Hakimu Ally.

Katika keai hiyo washtakiwa hao walikuwa wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kwa kuisababishia serikali hasara ya Sh10,874,280.

TMA kutatoa utabiri wake wa msimu wa Mvua za Vuli kwa kipindi cha Oktoba, Novemba hadi Disemba

0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Dk. Agnes  Kijazi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu utabiri wa mvua za vuli,  Octoba hadi Desemba (OND) unatarajiwa kutangazwa kesho mara baada ya kufungua semina ya wanahabari inayofanyika leo Septemba 2, 2019 kwenye makao makuu ya Mamlaka ya Hali ya hewa (TMA) Ubungo Plaza jijini Dar es salaam .
 Mchambuzi wa utabiri wa hali Hali ya Hewa nchini, kutoka TMA Abubakari Lungo, akiwaeleza waandishi wa Habari namna  utabiri unavyofanyika wakati wa warsha ya siku moja ya mundelezo wa taarifa ya hali ya hewa juu ya utabiri mvua za vuli, iliyofanyika leo Sepemba 2,2019 katika Makao Makuu ya Mamlaka ya Hali ya Hewa TMA, Ubungo jijini Dar es Salaam
 Mkurugenzi wa Huduma za utabiri, Hamza Kabelwa, akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari juu ya utabiri wa mvua za vuli unaotarajiwa kutangazwa kesho, pembeni yake ni ameneja wa huduma za utabiri Samwel Mbuya.

Na Karama Kenyunko,  Michuzi TV,

MAMLAKA  ya Hali ya Hewa nchini (TMA), kesho Septemba 3, 2019 itatoa utabiri wake wa msimu wa Mvua za Vuli kwa kipindi cha Oktoba, Novemba hadi  Disemba mwaka huu.

 Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi amesema hayo leo wakati akifungua warsha ya siku moja kwa waandishi wa Habari iliyofanyika katika Makao Makuu ya TMA, Ubungo jijini Dar ea Salaam.

 Amesema, kwa kuzingatia umuhimu wa taarufa za hali ya hewa, mamlaka  haina budi kutoa taarifa zake mapema na kwa wakati ili ziweze kufikia wananchi wote na sekta husika kwa ajili ya kuwawezesha kuchukua hatua stahiki ikiwemo kuepukana na majanga yanayoweza kusababishwa na mvua kwa kuwa matumizi ya taarifa za hali ya hewa kwa jamii katika shughuli zetu za kila sik ni ya muhimu.

Amesema, TMA, imekuwa ikahakikisha inakutana na wanahabari ambao ni daraja muhimu kati ya taasisi zetu za serikali na wananchi wote kwa ujumla katika kuwapa warsha mbali mbali za kujadili mwelekeo wa msimu wa Mvua na kuongeza kuwa Serikali ya Awamu ya tano inatambua vyema mchango wa huduma za hali ya hewa nchini na umuhimu wa kuwafikia wananchi kwa wakati.

Dkt, Kijazi Amesema, lengo la warsha ya lei ni kujadili Mwelekeo wa Msimu wa Mvua za vuli kwa kipindi cha Oktoba hadi Disemba mwaka huu na kujadili athari zinazoweza kujitokeza, hivyo wataalamu wameandaa rasimu ya mwelekeo huo na viashiria vilivyopelekea kupatikana kwa utabiri huu, Aidha amesema kutokana na maoni ya wanahabari na wadau wengine kuhusu lugha inayotumika kuwasilisha taarifa za hali ya hewa.

Mamlaka kwa kushirikiana na Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) na taasisi zingine ikiwemo BAKIZA na vyuo vikuu, imeweza kutafsiri baadhi ya maneno kwa lugha ya Kiswahili hivyo kupitia warsha hiyo wanahabari wamepata fursa ya kuona baadhi ya misamiati ya hali ya hewa iliyo katika lugha ya Kiswahili kwa lengo la kutoa maoni kabla haijaanza kutumika rasmi.

"Lugha ya kiswahili itasaidia wananchi kwa wingi, kuelewa utabiri wa hali ya hewa pale unaposomwa kwabi wakati mwingine imesheheni maneno ya kisayansi na yasiyo rahisi kueleweka na jamii,," amesema Dkt.kijazi

TUZO YA MCHEZAJI, KIPA NA KOCHA BORA WA FIFA KUTOLEWA SEPTEMBA 23 MWAKA HUU

0
0
Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Shirikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA) linatarajiwa kutoa Tuzo za Mchezaji Bora, Golikipa Bora na Kocha Bora wa msimu wa 2018 - 2019, Septemba 23 mwaka huu.

TUZO ZA MCHEZAJI BORA WA MSIMU,
Wanaowania ni Virjil Van Dijk, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.

VIRJIL VAN DIJK anawania Tuzo hiyo kwa mafanikio aliyoyapata msimu uliopita akiisaidia Liverpool kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League) msimu uliopita, na alishinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ulaya (UEFA).

LIONEL MESSI na yeye anawania Tuzo hiyo kwa kuisaidia Barcelona kutwaa taji la Ligi Kuu Soka nchini Hispania (La Liga) pamoja na Kiatu cha dhahabu katika Ligi hiyo.

CRISTIANO RONALDO Nyota huyo alishinda taji la La Liga na Italian Super Cup kwa mara ya kwanza akiwa na Juventus ya Italia, pamoja na hayo alishinda UEFA Nation League na Ureno.
 KOCHA BORA WA FIFA MSIMU WA 2018-2019

Wanaowania Tuzo ya Kocha Bora wa FIFA ni Jurgen Klopp, Pep Guardiola & Mauricio Pochettino.

MAURICIO POCHETTINO aliiongoza Tottenham Hotspurs katika Fainali ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League) msimu uliopita licha yakufungwa na Liverpool bao 2-0 katika mchezo wa Fainali ya Michuano hiyo.

PEP GUARDIOLA yeye ameiongoza Manchester City kutwaa taji la Ligi Kuu Soka nchini Uingereza (Premier League) msimu uliopita pamoja na kutwaa taji la FA Cup, na Kombe la Ligi pamoja na Ngao ya Hisani.

JURGEN KLOPP Kocha wa Liverpool  ameisaidia timu hiyo kutwaa Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League) msimu uliopita na kumaliza nafasi ya pili katika Ligi Kuu Soka nchini Uingereza (English Premier League) akiachwa Points moja na Man City ambao walikuwa Mabingwa.
TUZO YA GOLIKIPA BORA WA MSIMU

Wanaowania Tuzo hiyo ni Kipa Alisson Becker, Marc-Andŕe Ter Stegen na Ederson Santana de Moraes

ALISSON BECKER ameitumikia  Liverpool na Brazil kwa mafanikio, ikiwa kutwaa Tuzo ya Kipa Bora wa Copa America msimu uliopita ambapo Brazil walitwaa taji hilo.

EDERSON SANTANA DE MORAES yeye ameisaidia Manchester City kutwaa kwa mara nyingine taji la Ligi Kuu Uingereza (EPL) msimu wa 2018-2019.

MARC-ANDRE TER STEGEN
akiwa na Barcelona ameisaidia kutwaa taji la Ligi Kuu nchini humo (La Liga) na kufika hatua ya Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA CHAMPIONS LEAGUE).
TUZO YA GOLI BORA LA FIFA MSIMU HUU

Wanaowania Tuzo hiyo, Lionel Messi, Juan Fernando Quintero na Daniel Zsori

LIONEL MESSI anawania tuzo hiyo katika bao lake la Ligi dhidi ya Real Betis, 17 March 2019.

JUAN FERNANDO QUINTERO, Nyota wa Kimataifa wa Colombia anayecheza River Plate,  yeye anawania Tuzo hiyo kwa bao lake alilofunga dhidi ya  Racing Club mnamo 10 February 2019.

DANIEL ZSÒRI Mshambuliaji wa Debrecen FC na Romania anawania Tuzo hiyo katika bao lake dhidi ya Ferencváros TC mnamo 16 February 2019).

MAHAKAMA YA TANZANIA YAENDELEA KUTOA MAHAKAMA INAYOTEMBEA

0
0
Mtaalam Mwezeshaji kutoka Benki ya Dunia, Bw. Waleed Malik akitoa maelezo kuhusu Mahakama Inayotembea inavyofanya kazi, wakati wa mafunzo kwa vitendo kwa watumishi wanaofanya kazi kwenye Mahakama hiyo, yaliyofanyika leo kwenye Kituo cha Mafunzo na Habari kilichopo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam. (Wa pili kulia) ni Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania,Mhe Katarina Revocati(wa tatu kwanza kushoto) ni Msaidizi wa Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Upendo Ngitiri, (wa pili kushoto) ni Mkurugenzi wa Menejimenti ya Mashauri wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Nkya, (wa tatu kushoto) ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya DaresSalaam. (Wa nne kushotoni Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Bw. Leonard Magacha na watano ni Naibu Msajili Mwandamizi Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Messeka Chaba.


Msajili Mkuu wa Mahakama Tanzania, Mhe. Katarina Revocat akifungua mafunzo kwa vitendo kuhusu Mahakama Inayotembea kwa baadhi ya watumishi wa Mahakama ya Tanzania, yaliyofanyika leo katika Kituo cha Mafunzo na Habari kilichopo, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Bw. Kalege Enock (aliyenyoosha kidole) akiwaonyesha baadhi ya viongozi wa Mahakama ya Tanzania na watumishi wanaofanya kazi katika Mahakama Inyotembea moja ya kifaa kilichopo ndani ya gari la Mahakama hiyo, wakati wa mafunzo kwa vitendo yaliyofanyika leo katika Kituo cha Mafunzo na Habari kilichopo katika Mahakama Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.
Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revokati (katikati)akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Mahakama ya Tanzania wanaofanya kazi katika Mahakama Inayotembea(Makao Makuu) mara baada ya kufungua mafunzo kwa vitendo kwa watumishi hao. (Kushoto wa kwanza) ni Mkuu wa Kitengo cha Maboresho ya Mahakama ya Tanzania (JDU), Mhe. Zahra Maruma, (wa pili kushoto) ni Mkurugenzi wa Menejimenti ya Mashauri wa Mahakama ya Tanzania,Mhe. Eva Nkya na (Watatu kushoto) ni Mtaalam Mwezeshaji kutoka Benki ya Dunia, Bw. Waleed Malik. Kulia wa kwanza ni Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mhe. Kelvin Mhina, wa pili kushoto ni Naibu Msajili Mwandamizi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Messeka Chaba na (wa tatu kulia) ni Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Bw. Leonard Magacha.

(Picha na Mary gwera na Magreth Kinabo )


KAMISHNA WA OPERESHENI NA MAFUNZO CP LIBERATUS SABAS, AMEFANYA UKAGUZI WA UTENDAJI KAZI KATIKA OFISI ZA MARINE JIJINI DAR.

0
0
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo Liberatus Sabas, aliekaa katika Boti ya Polisi Wanamaji akiwa amelejea baada ya kumaliza kukagua vipenyo hatarishi na vinavyotumiwa na wahalifu wa majini. ( PICHA NA JESHI LA POLISI).
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo Liberatus Sabas, akiwasili katika ofisi za Kikosi cha Askari Wanamaji cha Jeshi la Polisi katika ofisi zao zilizopo jijini Dar es Salaam na kushoto kwake ni SP Benedict Nyagabona.
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo Liberatus Sabas, akipata maelekezo utendaji kazi wa Askari Polisi wanamaji kutoka kwa Kamanda wa Kikosi cha Askari wanamaji Tanzania ACP Evince Mwaijage baada ya kuwasili ofisini hapo.

RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK. SHEIN AKABIDHIWA TUZO YA SINEMA ZETU

0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akikabidhiwa Tuzo ya Sinema Zetu na Waziri wa Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar Mhe. Balozi Ali Karume katika hafla hiyo iliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar leo
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akikabidhiwa Cheti cha Kutambua Mchango wake mkubwa katika kukuza Sanaa ya Filamu Zanzibar iliotolewa na Chama Cha Wasanii Waigizaji Zanzibar, akikabidhiwa na Waziri wa Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar Mhe. Balozi Ali Karume hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar leo, 2-9-2019.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiangali CD za Michezo ya Wasanii wa Zanzibar zilizoshinda katika mashindano ya Tuzo ya Senima Zetu,Tanzania, baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar Mhe. Balozi Ali Karume, hafla hiyo imefanyika Ikulu Zanzibar.
RAIS wa Zanzibaer na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na kuwapongeza Wasanii wa Zanzibar kwa ushindi waliopata katika mashindano ya Sinema Zetu,walipofika Ikulu Zanzibar leo, kushoto kwa Rais Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Issa Haji Gavu na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ndh Salum Maulid wakiwa na Wasanii wa Filamu Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Zanzibar na Uongozi wa Wasanii wa Filamu Zanzibar waliosimama , waliokaa kulia kwa Rais Waziri wa Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Ali Karume,Bi. Maryam Hamdani Mwenyekiti wa Baraza lac Sanaa Zanzibar na Bi. Khadija Ibrahim Dau (Bi.Hawa) Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wasanii wa Filamu Zanzibar na kushoto Naibu Waziri wa Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Lulu Msham Abdalla, Mshauri wa Rais Masuala ya Sanaa na Utamaduni Mhe. Chimbeni Kheri na Katibu Mkuu Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Ndg Omar Hassan King.(Picha na Ikulu)

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MAAFISA WATENDAJI WA KATA WA NCHI NZIMA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli,Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora) Mhe. George Mkuchika, Rais wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Suleiman Jaffo, Katibu Mkuu Ikulu Dkt. Moses Kusiluka, Katibu Mkuu Utumishi Dkt. Laurian Ndumbaro,Katibu Mkuu TAMISEMI Mhandisi Nyamhanga na Naibu Katibu Mkuu Utumishi Dkt. Francis Michael katika picha ya pamoja na Maafisa Watendaji wa Kata baada ya kukutana na kuzungumza nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata chakula cha mchana na Maafisa Watendaji wa Kata wa nchi nzima baada ya kukutana na kuzungumza nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Maafisa Watendaji wa Kata wa nchi nzima wakati wa chakula cha mchana baada ya kukutana na kuzungumza nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Maafisa Watendaji wa Kata wa nchi nzima alipokutana nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Maafisa Watendaji wa Kata wa nchi nzima baada ya kukutana na kuzungumza nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora) Mhe. George
Mkuchika, Rais wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Suleiman Jaffo,Katibu Mkuu Ikulu Dkt. Moses Kusiluka, Katibu Mkuu Utumishi Dkt.Laurian Ndumbaro, Katibu Mkuu TAMISEMI Mhandisi Nyamhanga na Naibu Katibu Mkuu Utumishi Dkt. Francis Michael katika picha ya pamoja na Maafisa Watendaji wa Kata wa Mkoa wa Lindi baada ya mkutano wao Ikulu ijini Dar es salaam leo Septemba 2, 2019

PICHA NA IKULU

MAHAKAMA KUU YAKATAA KUTOA AMRI KWA SPIKA YA KUTOMUAPISHA MBUNGE MTEULE WA SINGIDA MASHARIKI

0
0
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es salaam, imekataa kutoa amri kwa spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya kutomuapisha Mbunge Mteule wa singida mashariki Miraji Mtaturu (CCM) kwa kuwa inaweza kuharibu maamuzi kesi ya msingi.

Jaji Sirilius Matupa amesema hayo leo Septemba 2, 2019 usiku huu, baada ya kusikiliza kusikiliza kesi ya Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu dhidi ya Spika wa Bunge kuhusu kutetea ubunge wake wa jimbo la Singida Mashariki kwa zaidi ya Massa 10.

Kesi hiyo iliyoanza kusikilizwa saa 4 asubuhi mbele ya Jaji Sirilius Matupa ambapo Lissu aliwakilishwa na Mawakili wanne, Kiongozi wa jopo akiwa Peter Kibatala na kwa upande wa Spika na Mwanasheria Mkuu uliwakilishwa na Mawakili 15, waliokuwa wakiongozwa na Wakili Mkuu wa Serikali Dk. Clement Mashamba.

Kabla ya kuahirishwa kwa kesi hiyo Jaji Matupa amesema, kuna wabunge wengi walishawahi kuapishwa lakini baada ya kesi kuisha walitolewa bungeni na kupatiwa wenye haki hivyo kutoa maamuzi ya haraka kwa hoja zilizotolewa na pande zote mbili zinaweza kuharibu kesi ya msingi. Pia amesema inatakiwa kupatikana muda wa kuweza kuchambua hoja zote kwa makini zilizowasilishwa ili maamuzi sahii yaweze kupatikana.

"Siwezi kutoa kwa sasa uamuzi wa kuzuia kuapishwa kwa huyo mbunge, hata akiapishwa sio tatizo uamuzi ukitolewa anaweza kuvuliwa ubunge wake pamoja na kiapo chake, hivyo uamuzi wangu nitautoa Septemba 9, mwaka huu, " amesema Jaji Matupa.

Aidha Jaji Matupa alisema hakubaliani na hoja ya Serikali ya kumtaka Wakili Magai ambaye ndio aliyeshuhudia kiapo cha Lissu kuja mahakamani kwani yeye alifanya kushuhudia tu. 

Wakili wa mleta Maombi, Peter Kibatala ndiye alikuwa wa kwanza kuwasilisha hojabzake wakati wa usikilizwaji ambapo amedai hatua zilizochukuliwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai kutangaza kuwa jimbo analoliongoza Lissu la Singida Mashariki lipo wazi lilifanyika bila haki ya Lissu kusikilizwa na pia mchakato wa kumvua Lissu ubunge haukuwa shirikishi kwani hakuwahi kutaarifiwa rasmi sababu za yeye kutenguliwa ubunge wake bali alisikia barabarani. 

"Spika anatekeleza majukumu yake kwa kuongozwa na kanuni za Bunge, katiba pamoja na kupitia maamuzi ya Maspika waliopita, hata hivyo kanuni hizo zinamtaka kutoa uamuzi kwa kuzingatia haki bila upendeleo," ameeleza Kibatala. 

Wakili Kibatala aliongeza kuwa, mbunge asipoudhuria vikao kwa mujibu wa kanuni upewa adhabu, hivyo alihoji ni adhabu gani inayotolewa bila ya kumpatia mtu haki yake ya kumsikiliza kwanza, na kumuomba Jaji aangalie matilio waliyompatia kwani kupatia Jaji, kwani Lissu ameadhibiwa bila ya kupewa haki yake ya kusikilizwa.

Aidha wakili Kibatala katika hoja sake, ameiomba Mahakama hiyo itoe amri kwa Spika Ndugai kusimamisha kwa muda kuapishwa kwa mbunge mteule Miraji Mtaturu hadi kesi hiyo itakapomalizika kusikilizwa mahakamani na kuongeza kudai kuwa wakati Lissu anakwenda mahakamani ratiba za Bunge zilikuwa bado hazijapangwa hivyo kilichotangulia ni maombi ya Lissu na ratiba ndio ikafuatia. 

"Kikao cha Bunge kinaanza kesho na kabla ya kuanza lazima Spika awaapishe kiapo cha uadilifu wabunge wapya, hivyo tunaiomba Mahakama itoe amri ya kumzuia Spika kwa muda kumuapisha Mtaturu wakati mashauri yaliyopo mahakamani yatakaposikilizwa mbele yake Jaji ili tusiweze kupoteza maana ya kesi hii, " ameeleza Kibatala. 

Amedai kuwa kama mchakato wa kuapishwa kwa mbunge huyo utaruhusiwa kuendelea utafanya kazi ya mahakama kuwa ngumu. 

Wakijibu hoja hizo, wakili wa Serikali Mkuu, Aboubakary Mrisha amedai kuwa hati ya kiapo iliyowasilishwa mahakamani hapo inamapungufu kwani kimsingi Mleta maombi (Lissu) hajaonyesha ni kwa sababu zipi haki zimepotea, hivyo maombi hayo hayana msingi wa Mahakama kuyasikiliza na kudai kuwa maombi yaliyowasilishwa mahakamani hapo na aya zilizoendolewa kwenye hati ya kiapo ni maoni yao kwamba hayakidhi vigezo kwa kuwa vinahitajika kuangaliwa kwa umoja wake.

Wakili Mrisha ameendelea kudai kuwa mapungufu mengine yapo katika kipengele cha Allute Mughwai ambaye kiapo chake amekielezea kuwa kina aya nane wakati si kweli.

Katika Maombi ya ya Lissu yaliyofunguliwa ja kaka yake Alute Mughwai chini ya hati ya dharura, dhidi ya Spika wa Bunge la Tanzania na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), anaomba mahakama kibali cha kufungau shauri la maombi maalum kwa lengo la kupata amri mbalimbali kuhusiana na uamuzi huo wa kuvuliwa ubunge.

Amri hizo kwa mujibu wa hati ya maombi na hati ya maelezo yake ni pamoja na mahakama kumwamuru Spika Ndugai awasilishe mahakama taarifa ya kumvua ubunge, aliyoitoa bungeni, ili iweze kuupitia na kisha iamuru kuutengua na kuutupilia mbali.

Nyingine ni mahakama imwamuru Spika ampatie yeye Lissu nakala ya taarifa ya kumvua ubunge pamoja na itoe amri ya kusitishwa kuapishwa kwa mbunge mteule Mtaturu .

KANISA LA WAADVENTISTA WASABATO WAZINDUA CHUO KIKUU CHA AFYA NCHINI RWANDA,RAIS KAGAME AWAPONGEZA

0
0
Rais wa Rwanda Mh,Paul Kagame akiwa sambamba na Mwenyekiti wa Kanisa la Waadventista Wasabato Ulimwenguni Pr.Teddy Wilson kwa pamoja wakisoma maandishi yaliyoandikwa kwenye jiwe la msingi,mara baada ya kuzinduliwa rasmi kwa chuo hicho leo mjini Kigali,nchini Rwanda.
Picha ya pamoja mara baada ya kufanyika kwa tukio hilo la uzinduzi
Mandhari ya chuo kikuu cha afya nchini Rwanda kinavyoonekana mara baada ya kuzinduliwa rasmi leo mjini Kigali,nchini humo.


Mwenyekiti wa Kanisa la Waadventista Wasabato Ulimwenguni Pr.Teddy Wilson amezindua chuo kikuu cha Afya nchini Rwanda kwa lengo la kutoa fursa ya elimu ya afya kwa wanafunzi wa Mashariki ya kati  ya Afrika. 

Hafla fupi ya uzinduzi wa chuo hicho cha afya kinachomilikiwa na kanisa la Waadventista wasabato mashariki kati mwa Afrika, limefanyika leo mjini Kigali ambapo Teddy Wilson amesema elimu bora siyo jengo bali ni huduma bora inayotolewa ndani ya majengo hayo huku akisema chuo hicho licha ya kutoa elimu ya afya inatoa huduma ya kiroho. 

Nae Rais wa Rwanda Mh.Paul Kagame amesema kwa kutambua huduma mbalimbali zinazotolewa na kanisa hilo, Serikali yake itaongeza ardhi kwa chuo hicho pamoja na fedha, huku akipongeza Makanisa ya Waadventista wasabato nchini humo kwa kuadhimisha miaka 100 ya utoaji huduma ya kijamii na kiroho nchini Rwanda,kwani huduma walizozitoa zimekuwa na matokeo makubwa katika kuleta maendeleo hasa katika sekta ya afya na elimu. 

Awali akiwasilisha taarifa fupi ya chuo hicho Mwenyekiti wa jimbo la Afrika Mashariki na kati mchungaji,Dkt  Blasous Luguri alieleza kuwa mpaka  kukamilika kwa ujenzi wa chuo hicho, kitasaidia kutoa mchango mkubwa wa elimu ya afya nchini humo. 

Uzinduzi wa chuo hicho umeshuhudiwa na viongozi wa Serikali ya Rwanda akiwemo Waziri wa Afya nchini humo Diana Lumba, Waziri wa Elimu Eugene Tamura pamoja na viongozi mbalimbali wa kanisa la Waadventista wasabato divisheni ya Afrika. 

MAJALIWA AZUNGUMZA NA MSHAURI WA MASUALA YA AFYA WA JAPAN

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mshauri Maalum wa Masuala ya Afya wa Taasisi ya Tokushukai General Incorporated ambayo iko chini ya serikali ya Japan , Bw. Akio Egawa kwenye uwanja wa ndege wa Narita nchini Japan kabla ya kuondoka kurejea nyumbani baada ya kukamilisha ziara yake ya kikazi nchini humo, Septemba 2, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na wafanyakazi wa hoteli ya Yokohama Bay nchini Japan alikokuwa amefikia wakati alipoondoka kurejea nyumbani baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi, Septemba 2, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI HASUNGA ARIDHIA OMBI LA KUWAPATIA ARDHI VIJANA WALIOHITIMU MAFUNZO NCHINI ISRAEL

0
0
 Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza na vijana waliohitimu mahafali ya mafunzo ya Kilimo ya Agro Studies yaliyofanyika jijini Jerusalem nchini Israel, leo tarehe 2 Septemba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na vijana watanzania waliohitimu mahafali ya mafunzo ya Kilimo ya Agro Studies yaliyofanyika jijini Jerusalem nchini Israel, leo tarehe 2 Septemba 2019.

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Jerusalem,Israel
SERIKALI imeridhia ombi la vijana 45 waliohitimu masomo ya Kilimo nchini Israel la kuwapatia ardhi kwa ajili ya kuwekeza kwenye sekta ya Kilimo.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 2 Septemba 2019 wakati akizungumza na vijana hao wakati wamahafali ya mafunzo ya Kilimo ya Agro Studies yaliyofanyika jijini Jerusalem nchini Israel na kuwatunuku vyeti vya kuhitimu wanafunzi 45 kutoka Tanzania.

Amesema kuwa serikali ya Tanzania ina ardhi nzuri yenye rutuba ambayo haijaguswa kwa ajili ya kilimo hivyo huo ni muda mwafaka kwa vijana hao kupatiwa ardhi kwa ajili ya kuonyesha kwa vitendo waliyofundishwa wakati wa masomo yao nchini Israel.

Alisema kuwa ni wakati muafaka kwa wanafunzi hao kutumia ujuzi walioupata wa kujifunza mbinu bora na teknolojia za kisasa za kuendeleza kilimo cha umwagiliaji ili kutoa elimu ya kilimo hicho nchini mwao pindi watakaporejea.

Amesema kuwa nafasi hizo za masomo ya kilimo nchini Israel zimetoa fursa kwa wataalam hao kuongeza ufanisi katika Sekta ya kilimo hivyo watakaporejea nchini wanapaswa kukibadilisha kilimo kuwa na tija zaidi.

Aidha, amesema kuwa, tatizo kubwa la Sekta ya Kilimo nchini ni uzalishaji mdogo usiokuwa na tija ambapo wakulima hutumia nguvu kubwa lakini matokeo yanakuwa madogo. hivyo, amesisitiza kuwa, watakaporejea nchini Tanzania wanatakiwa kutoa elimju kwa wakulima ya kuzingatia mbinu bora za kilimo, matumizi sahihi ya pembejeo, mbolea na pia kutumia mbegu bora ili kuweza kumnufaisha mkulima.

Aliongeza kuwa mabadiliko ya tabianchi yanaathiri kwa kiasi kikubwa Sekta ya Kilimo hivyo ni muhimu kilimo cha umwagiliaji kikaanza kutumika maeneo mbalimbali ya nchi kwa sababu ya uwepo wa vyanzo vya maji vya kutosha na sio kuendelea kutegemea kilimo cha mvua ili kupambana na hali hiyo.
“Hadi sasa eneo linalotumika kwa kilimo cha umwagiliaji ni hekta 475,000 na Mkakati wa Serikali ni kufikia hekta milioni moja ifikapo mwaka 2035,”amesema Mhe Hasunga.

Hata hivyo, Waziri Hasunga amesema kuwa ataiomba Serikali ya Israel kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuendeleza bonde la mto rufiji kwa kuwekeza katika kilimo cha umwagiliaji ili wakulima wengi waachane na kilimo cha kutegemea mvua kama ilivyo sasa.

Serikali yaombwa kurekebisha mtaala Wa elimu ufundi stadi

0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Tv ,Arusha 

Serikali imetakiwa kuboresha mazingira ya elimu ya ufundi stadi pamoja na kufanya marekebisho ya mtaala Wa elimu ya ufundi stadi kwani mtaala huo ni Wa zamani na unawapa changamoto kubwa walimu wanaofundisha shule hiyo.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Wa shule ya msingi ya Healsun  ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa taasisi ya Elimu  ya Sinoni Edward Laiza wakati akisoma hotuba yake katika mahafali ya nne ya kidato cha saba ya shule hiyo.

Alisema kuwa mtaala wa elimu ya ufundi stadi haujaboreshwa tangu ulipotugwa mwaka 1984, hivyo unawapa tabu sana ya kupata vitendea Kazi ikiwemo vitabu vya kufundishia masomo mbalimbali  .

"Tunapata tabu sana kupata vitabu pamoja na vitendea Kazi vingine kwa sababu  mtaala huu haujarekebishwa tangu mwaka 1984, hivyo tunaiomba serikali kupitia mtaala huu na kuubadilisha ili tuweze kufundisha watoto kulingana na mtaala unaoenda na wakati kufanikisha Sera hii ya viwanda " alisema 

Alisema kuwa iwapo ufundi ukipewa kipaumbele itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo la ajira hapa nchini kwani ,wanafunzi wengi wanao maliza katoka shule hizi za ufundi watakuwa na ujuzi Wa kutosha Wa vitendo ambao watakuwa wametoka nao mashuleni  na wataweza kujiajiri wenyenyewe na sio kutegemea ajira za serikalini.

Kwa upande wake  mgeni rasmi katika Mahafali hayo Mwenyekiti Wa umoja Wa wazazi mkoa wa Arusha,  Daudi Hezron Mbise aliwatala wanafunzi hao kuzingatia na kuyafuata yale yote ambayo wamefundishwa na walimu wao ,huku akiwasihi kuhishika sana elimu na kuendelea kusoma  kwani kwa dunia ya sasa hivi elimu ndio kila kitu.

"Najua mmefundishwa vyema na walimu wenu sasa kazingatieni yote mliofundishwa darasani na hata nje ya darasani ,pia napenda kuwasisitiza wazazi kufuatilia maendeleo ya watoto wao mashuleni na sio kuwaachia walimu tu,  kwani ukifuatilia maendeleo ya mtoto kama yupo chini utajua jinsi ya kumkazania  mtoto wako.

Haya ni mahafali ya nne ya darasa la saba tangu kuanzishwa kwa shule hii mwaka 2014 na jumla ya wanafunzi 15 wamemaliza masomo yao ya darasani la saba  ,pia shule hii ina sekondari ya ufundi stadi inayofundisha masomo ya ufundi stadi lakini pia shule hii ya msingi  inatarajia kuanza kufundisha masomo ya ufundi stadi ili kuwasaidia wanafunzi .

Mkurugenzi Wa shule ya msingi ya Healsun ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu Wa taasisi ya Elimu ya Sinoni Edward Laiza akisoma hotuba katika mahafali ya darasa la saba katika shule hiyo
wanafunzi Wa shule ya sekondari ya ufundi stadi Healsun wakionesha wazazi wao hawapo pichani ufundi waliofundishwa darasani kwa vitendo 

Mkuu wa jeshi la uokoaji afanya mabadiliko ya makamanda wa mikoa hapa nchini

DC ARUSHA AZINDUA AWAMU YA NNE YA MAFUNZO KUHUSU MATUMIZI YA MFUMO WA MANUNUZI YA UMMA KWA NJIA YA MTANDAO (TANePS)

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Mh. Gabriel Daqqaro, akizungumza wakati wa ufunguzi wa awamu ya nne ya mafunzo kuhusu Mfumo wa TANePS jijini Arusha.

PPRA YAENDELEA KUTOA MAFUNZO KUHUSU MFUMO WA TANePS

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mh. Gabriel Daqqaro, amefungua awamu ya nne ya mafunzo kuhusu matumizi ya Mfumo wa Manunuzi ya Umma kwa Njia ya Mtandao (TANePS) kwa wataalam wa manunuzi na Tehama kutoka taasisi nunuzi. 

Akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo wapatao 172 kutoka taasisi nunuzi 65, Mh. Daqqaro alipongeza jitihada za Serikali kwa kuanzisha mfumo huo mpya wa TANePS unaosimamiwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma - PPRA kwa kuwa utasaidia kupunguza malalamiko na kero zilizokuwa zinaelekezwa kwenye sekta ya manunuzi ya umma ikiwemo kukabiliana na vitendo vya rushwa,  kupunguza gharama na muda wa michakato ya manunuzi.

Mkuu huyo wa Wilaya aliongeza kuwa Mfumo huo utaisaidia Serikali kuokoa fedha nyingi ambazo zinaelekezwa kwenye sekta hiyo ya manunuzi, na kutoa wito kwa wadau wote wa manunuzi ya umma kutoa ushirikiano wa dhati ili mfumo huo ufanye kazi. 

 Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Mhandisi Leonard Kapongo akifafanua jambo kwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Mh. Gabriel Daqqaro, kabla ya Ufunguzi wa awamu ya nne ya mafunzo ya TANePS, jijini Arusha
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Mh. Gabriel Daqqaro, akizungumza wakati wa ufunguzi wa awamu ya nne ya mafunzo kuhusu Mfumo wa TANePS jijini Arusha.
 Baadhi ya washiriki wakiwa kwenye mafunzo kwa vitendo kuhusu matumizi ya mfumo wa TANePS

BUNGE KUANZA KUTUMIA MFUMO WA DIGITAL KUWAPA WABUNGE NYARAKA

0
0
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, amesema kuwa hivi karibuni Bunge hilo kuacha kutumia mfumo unaotumika sasa wa kuwapa Wabunge nyaraka mbalimbali, kwa kuhamia katika mfumo wa Digitali wa kuwawekea nyaraka hizo kupitia simu zao za mikononi.

Spika Ndugai ametoa kauli hiyo leo Bungeni jijini Dodoma, wakati wa kikao cha kwanza cha Mkutano wa 16 wa Bunge la 11, ambapo amesema katika Afrika Mashariki, Tanzania pekee ndiyo ambayo Bunge lake bado linatumia mfumo wa karatasi.

Spika Ndugai amesema kuwa "sisi ndiyo Bunge pekee Afrika Mashariki ambao tunaendekeza Makaratasi mengi, wenzetu hawatumii, tunaanza na hii 'Order Paper' halafu tutaenda kidogo kidogo"

"Mpaka tufike hatua dawati la Mbunge liwe safi, naombeni mhakiki simu zenu na barua pepe, tunaanza kuwapatia nyaraka." ameongeza Spika Ndugai.
Leo Septemba 03, 2019 mkutano wa Bunge la 16 umeanza jijini Dodoma, ambapo Miraji Mtaturu aliapishwa kuwa Mbunge wa Singida Mashariki, akirithi nafasi ya Tundu Lissu.
Viewing all 109604 articles
Browse latest View live




Latest Images