Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live

Anayedaiwa kumuua mkewe kwa kumchoma moto aiomba Mahakama apatiwe Line zake za simu

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv.
MFANYABIASHARAKhamis Luwonga maarufu kwa jina la Meshack (38), anayedaiwa kumuua mkewe kwa kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa, Naomi Marijani ameiomba Mahakama ya Hakimu Kisutu kuwa apatiwe Line zake mbili za simu zenye zaidi ya Sh. Milioni 5 kwa ajili ya matumizi ya nyumbani kwake pamoja na kumlipia ada mwanae.

Said ambaye ametinga mahakamani hapo akiwa na pingu miguuni kufuatia hivi karibuni kutoa vitisho mahakamani hapo kwa waandishi wa habari kwamba atawafanya kitu mbaya ametoa maombi hayo leo Agosti 27,2019 mbele ya Hakimu Mkazi, Salum Ally.

Mshtakiwa Said ametoa maombi hayo baada ya Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon kudai kuwa, Kesi hiyo leo imeitishwa kwa ajili ya kutajwa, upelelezi bado haujakamilika,

Baada ya kueleza hayo, Said alinyoosha mkono na kumueleza Hakimu kwamba ana mambo mawili muhimu ikiwemo nakala yake ya Hati ya Mashitaka na Line zake za simu zilizopo kituo cha kati cha Polisi (Central) na kuomba apatiwe line hizo zenye zaidi ya Sh.Mil 5 ili ziweze kutumika kwa matumizi madogo madogo pamoja na kumlipia ada ya mwanae.

"Sitaki simu ila naomba nipatiwe line ambazo nimpatie ndugu yangu atoe hizo hela kwa ajili ya matumizi, ikiwezekana zitolewe hata Polisi wakiwepo,"amedai.

Baada ya kueleza hayo, Wakili Wankyo ameeleza kuwa simu hizo ni sehemu ya upelelezi hivyo kwa sasa itakuwa ngumu kumpatia kwa sababu hawawezi kuamini moja kwa moja kama kweli anahitaji kutoa hizo hela.

Pia ameeleza kuwa kesi hiyo ni ya mauaji na maombi hayo alipaswa kuyawasilisha katika Mahakama husika yenye mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo ambayo ni Mahakamani Kuu na pia kama anahitaji fedha hizo basi atumie njia ya kumuandikia barua Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP).

Kufuatia maelezo hayo, Hakimu Ally alimshauri Said kutumia mbinu ya kuandika barua na kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 10, 2019.

Katika kesi hiyo, mshtakiwa anatuhumiwa kwa kosa moja la mauaji Kinyume cha Sheria ya kanuni ya adhabu namba 196 sura 16 kama kilochofanyiwa marejeo mwaka 2002

Katika kesi hiyo ya muaji namba 4 ya mwaka 2019, mshtakiwa Luwonga ambaye ni Mkazi wa Kigamboni, Dar es Salaam anadaiwa Mei 15, 2019 akiwa Gezaulole eneo la Kigamboni alimuua Naomi Marijani.

Kampeni YA TCRA ya Mnada kwa Mnada yatoa Elimu ya Usajili wa laini kwa kutumia alama za vidole

$
0
0
 Wananchi wakipata huduma ya usajili wa katika banda la vitambulisho vya Taifa (NIDA) katika Viwanja vya Tangamano jijini Tanga.
 Afisa wa TCRA akimuhudumia mwananchi wakati alipotembelea banda la TCRA katika Mnada wa Tangamano jijini Tanga.
 Afisa wa Idara ya Uhamiaji akitoa huduma kwa mwananchi wakati alipotembelea banda la Uhamiaji katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya TCRA katika Viwanja vya Tangamano jijini Tanga.
 Mwananchi akiweka alama za kidole kwa ajili ya usajili wa laini ya simu katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya TCRA katika Viwanja vya Tangamano jijini Tanga.
 Wananchi wakipata huduma za Mawasiliano katika Viwanja vya Tangamano jijini Tanga.
Wananchi wakipata huduma za Mawasiliano katika Viwanja vya Tangamano jijini Tanga.

WAKAZI wa jijini Tanga   na viunga vyake wamejitokeza kwa wingi katika kampeni  ya Mnada kwa Mnada ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Kampuni ya simu, Jeshi la Polisi Kitengo cha Uhalifu Mitandaoni  na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa ajili  ya utoaji wa huduma za usajili wa laini za simu kwa kutumia vitambulisho vya kitaifa na kuhakikiwa na kampuni za simu kwa kuweka alama za vidole kwa laini za simu.

Mkuu wa Kanda ya Kaskazini wa TCRA  Mhandisi Emelda Salum amesema ni fursa kwa wananchi wa wa Tanga kupata huduma kutokana na kuwa na mnyororo wadau wa  mawasiliano. 
Amesema Mnada kwa Mnada utadumu kwa siku tatu katika Viwanja vya Tangamano jijini Tanga ambapo itatoa fursa kwa wananchi wengi kufika kupata huduma za Mawasiliano na usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.

Salum kuwa kampeni ya Mnada kwa Mnada ni kwa ajili ya kutoa elimu ya mawasiliano kwa kushirikiana na wadau katika kujibu changamoto wanazokutanazo katika utumiaji wa mawasiliano nchini.

Salum amesema kuwa wananchi wasio kuwa na Vitambulisho vya NIDA wahakikishe  wanapata katika usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole na huduma nyinginezo za Mawasiliano hayo.
Amesema kuna watu wengine wanatumia mawasiliano ya simu bila kujua ambapo Jeshi Polisi lipo katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ili kuwaelewesha makosa ya jinai ya matumizi ya simu.
Aidha amesema Kampeni hiyo ni endelevu katika kuwafikia ikiwa kuhakikisha kila mwananchi anajisajili laini yake kwa alama za vidole kwa kutumia kitambulisho cha taifa cha NIDA.

Amesema kuwa TCRA iko kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi ili mtumie Mawasiliano kwa usalama kutokana na elimu tunayotoa.

Salum amesema kuwa wananchi wajitokeze katika kujisajili kwa alama za vidole kabla ya Desemba 31.

"TCRA tumejidhatiti katika kuwafikia  wananchi katika utoaji wa elimu za utumiaji wa bidhaa za mawasiliano kwa kutatua changamoto katika huduma hiyo"amesema Salum

RAIS DKT. SHEIN AZUNGUMZA NA BALOZI WA RWANDA NCHINI TANZANIA

$
0
0
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Balozi wa Jamuhuri ya Rwanda Nchini Tanania Eugine Kayihura, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na Rais na kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi Nchini Tanzania, yaliofanyika leo 27-8-2019.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Balozi wa Jamhuri ya Rwanda Nchini Tanzania Eugine Kayihura, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na kuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi Nchini Tanzania, mazungumzo hayo yamefanyika Ikulu Zanzibar leo 27-8-2019.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Rwanda Nchini Tanzania Eugine Kayihura, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na kumuaga baada ya kumaliza muda wake ya kazi Nchini Tanzania, hafla hiyo imefanyika leo 27-8-2019 Ikulu Zanzibar.

/RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na mgeni wake Balozi wa Jamuhuri ya Rwanda Nchini Tanzania Eugine Kayihura , baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika Ikulu Zanzibar leo 27-8-2019, alipofika kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa Kazi Nchini Tanzania.(Picha na Ikulu)

MALINZI AMEIAMIA MAHAKAMA YA KISUTU KUWA ALIIKOPESHA TFF

$
0
0
ALIYEKUWA Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Jamal Malinzi pichani, ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa mwaka 2014 aliikopesha TFF  USD 258,000 na Sh. Milioni 252 na mwaka 2016 aliikopesha TFF USD 50,000 na Sh. Milioni 74 ambapo jumla zilizopo kwenye rekodi ya mahakama ni USD 298,000 na sh.milioni 320.

Aidha Malinzi amedai kuwa, utaratibu wa watu kuikopesha TFF ulikuwepo tokea miaka ya nyuma na kwamba katika kipindi chake walikuwepo  watu mbalimbali ambao walikuwa wakiikopesha TFF, lakini  yeye ndiye Rais wa kwanza kushtakiwa na kufikishwa mahakamani. 

Malinzi amedai hayo leo Agosti 27,2019  mahakamani hapo  wakati akiendelea kutoa utetezi wake dhidi ya kesi inayomkabili ya matumizi mabaya ya madaraka, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji fedha,

Akiongozwa na wakili wake Richard Rweyongeza mbele ya Hakimu Mkazi Maira Kasonde , Malinzi amedai,  fedha hizo alikuwa akiikopesha TFF bila masharti yoyote wala kudai riba na kuongeza kuwa alikuwa akilipwa kadri ambavyo hali ya kifedha ilivyokuwa inaruhusu katika shirikisho hilo ambapo alikuwa analipwa fedha hizi kadiri hali ya kifedha ilivyokuwa inaruhusu pale TFF,  pia nilikuwa nalipwa kwa mafungu yaani kidogo kidogo. 

Amedai Ahamed Mgoyi ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya utendaji ya TFF ni miongoni mwa watu ambao walikuwa wakilikopesha shirikisho hilo kwa muda mrefu na hilo limethibitishwa mahakamani hapo na Shahidi wa sita Daniel Msangi iliyethibitisha na kutambua malipo ya Sh. Milioni 55 ambayo aliikopesha TFF na kulipwa. 

"Na katika maombi ya hati ya risiti tuliomba maelezo ya Mgoyi ili kuona anamdai nani mpaka sasa,  hadi upande wa mashtaka unafunga ushahidi wake,  mimi sikupatiwa hiyo nyaraka kuangalia, " alidai Malinzi. 

Alidai Mgoyi alikuwa akiikopesha TFF kwa kutumia utaratibu aliyokuwa akiufanya yeye wa bila kuweka masharti yoyote. 

Aidha Malinzi alidai kuwa yeye na wenzake walikamatwa Juni 27, 2017 na kulazwa mahabusu ya Polisi siku mbili lakini Juni 29 mwaka huo walipelekwa mahakamani na kunyimwa dhamana. 

"Wakati nakamatwa nilikuwa najiandaa kufanyiwa usahili mimi na wagombea wenzangu tuliokuwa tukigombea nafasi za uongozi TFF ikiwemo urais, " alidai Malinzi. 

Alidai baada ya kunyimwa dhamana,  Julai Mosi, 2017 kikao cha dharura cha kamati ya utendaji ya TFF kiliitishwa na kumkaimisha urais wa TFF Wallace Karia kisha kuvunja kamati ya uchaguzi iliyokuwepo hapo awali na kuundwa nyingine mpya ambayo iliondoa jina lake miongoni mwa wagombea urais. 

"Kwa hiyo Wallace Karia na wagombea wengine walipitishwa kugombea bila jina langu kuwepo,  hata hivyo kwa mujibu wa katiba ya TFF mwenye mamlaka ya kuitisha kikao cha dharura cha kamati ya utendaji wa TFF ni rais hivyo kukaa kwangu mahabusu hakukuniondolea sifa ya kuwa mjumbe wa kikao hicho, kwahiyo kanuni zilivunjwa pamoja na katiba pia ilivunjwa, " alidai Malinzi. 

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mhasibu wa TFF Nsiande Mwanga, Karani Flora Rauya na Selestine Mwesigwa.

Malinzi, Mwesigwa na Nsiande wapo rumande kwa kukabiliwa na mashtaka ya utakatishaji wa fedha kuwa miongoni mwa mashtaka  ambayo kwa mujibu wa sheria hayana dhamana huku Frola akiwa  nje kwa dhamana.

Kutana na Mtanzania wa kwanza kuwa Afisa Mkuu wa Fedha,Tigo Tanzania.

$
0
0
 
 Tigo Tanzania ni kampuni inayoongoza katika kubuni, na kuleta huduma na bidhaa bora zinakata kiu ya watanzania, sasa kutana na Innocent Rwetabura mtanzania wa kwanza kuwa Afisa Mkuu wa Fedha


Historia ya bwana Rwetabura inajieleza yenyewe. Alijiunga na kampuni ya Tigo akiwa na uzoefu mkubwa unaotokana na kutumikia katika nyadhifa mbalimbali za juu katika makampuni mengine katika sekta ya mawasiliano.

Kwa mujibu wa maelezo yake, uhasibu upo katika damu yake. Ndio ni ukweli kwamba uhasibu unaambatana na donge nono, lakini hamasa yake haitokani na malipo au mafao yatokanayo na taaluma hiyo, bali hamasa na msukumo wa kuwa mhasibu mahiri unatokana na ukweli kwamba kazi hii inasisimua kitaaluma.

Safari yake katika sekta ya uhasibu na fedha ilianza pale alipochukuliwa kwenda kufanya kazi mara baada ya kuhitimu kutoka katika chuo kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1998.

Kwa mara ya kwanza kabisa aliingia katika sekta ya ajira kama mhasibu msaidizi wa benki, Citibank. Akiwa na miezi michache tu tangu kuajiriwa, Price water house Coopers (PwC) walimpigia simu ya kutaka kufanya naye kazi na akachukua fursa hiyo. “Japokuwa mazingira na mafao yalikuwa mazuri sana pale Citibank lakini matarajio aliyokuwa nayo kwa kufanyakazi PwC yalikuwa bora zaidi. Nilihitaji kuwa pale ambapo utendaji upo. PwC ilikuwa ni njia yangu ya kuelekea kuwa mhasibu mahiri katika mazingira ambayo yanatoa kiwango cha juu cha utaalamu wa uhasibu,” alisema bwana Rwetabura.

Ni wazi kabisa kwamba bwana Rwetabura ni mtu mwenye malengo makubwa. Ametumikia makampuni mbalimbali akiwa katika nyadhifa mbalimbali kwa miaka mingi. Amefanya kazi na PwC kwa takribani miaka miwili. Baada ya hapo alihamia katika kampuni ya Celtel (ambayo kwa sasa ni Airtel) kama Meneja wa Fedha akitokea kuwa Mkaguzi wa Mahesabu. Alipoanza kazi kama Meneja wa Fedha, kampuni ya Celtel ilikuwa ni ndogo. Kadri ambavyo kampuni hiyo ilivyokuwa inakua, nafasi yake ilipandishwa hadi kufikia kuwa Mdhibiti wa Fedha.

Baada ya mwaka mmoja na nusu, alihamishiwa nchini Sierra Leone akitumikia kampuni hiyo hiyo na katika wadhifa huo huo wa Mdhibiti wa Fedha. Alifanikiwa kupanda vyeo mbalimbali na kufikia ngazi ya Mdhibiti wa Fedha baada ya mwaka mmoja.

Mafanikio yake haya hajayapata pasipokuwa na gharama yoyote. “Sierra Leone ni nchi ambayo ilitokea vita vya wenyewe kwa wenyewe, na kutokana na mtazamo mbaya uliokuwa unasambazwa wakati huo katika vyombo vya habari wakati huo, ilikuwa ni changamoto kwa mke wangu na familia kufwatana na mimi japo kuwa alikuwa akinitembelea mara kwa mara,” Alisema bwana Rwetabura.

Baada ya miaka mitatu, mwaka 2010, bwana Rwetabura aliona kwamba ni wakati mwafaka wa kurudi Tanzania.

Alipowasili, alijiunga na kampuni ya Zantel kama Mkurugenzi wa Fedha. Alishikilia wadhifa huu kwa karibia miaka miwili kabla ya kuhamia katika kampuni ya ulinzi ya G4S. Sababu zilizopelekea kuhama ni kwamba aliahidiwa kuchukua nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji, nafasi ambayo hakupewa.


Baada ya hapo aliachana na kampuni ya ulinzi na kujiunga na kampuni ya Helios Towers japo katika ngazi za chini. Baada ya muda, kampuni hiyo iliamua kuunganisha vitengo vya idara ya fedha na hivyo nafasi yake iliondolewa.


Bwana Rwetabura alipewa muda wa miezi sita kuweka sawa mambo yake. Wakati bado anapangilia hatua inayofwata, kampuni ya mawasiliano ya Tigo Tanzania ilimpigia simu na ilipofika mwaka 2015 safari yake yenye mafanikio na kampuni ya simu ya Tigo Tanzania ilianza rasmi.


Maisha yake katika kampuni ya Tigo


Awali kabisa bwana Rwetabura alishikilia wadhifa wa Mdhibiti wa Fedha katika kampuni ya Tigo. Mwenendo wake binafsi pamoja na taaluma yake ulichangia kwa kiasi kikubwa katika kumteua bwana Rwetabura kushika nafasi ya Afisa Mkuu wa Fedha (CFO). Amekuwa na mafanikio makubwa tangu alipojiunga na kampuni ya Tigo ikiwemo kuongeza ufanisi kwenye matumizi (Operating Expenditure (OPEX) kwa kiwango ambacho kilikuza faida ya kampuni. Timu anayoiongoza ya idara ya Fedha, iliunganisha kwa wakati mifumo ya Tigo na mfumo wa serikali wa ukusanyaji mapato (ERCS), hatua ambayo imesaidia mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kukusanya kodi na ushuru wa bidhaa kielektroniki.

“Kazi kubwa ya CFO ni kulinda na kusimamia rasilimali za wanahisa na kuhakikisha maslahi yao yanalindwa na kufwatwa. Jukumu hili linajumuisha kiwango kikubwa cha uwekaji wa mikakati, utekelezaji, usimamizi na uendeshaji wa shughuli zote za kifedha za kampuni ikiwepo kuandaa bajeti na kusimamia utekelezaji wake,” alisema bwana Rwetabura

“Wakati mwingine CFO anajiona kama mpinzani wa Mkurugenzi Mtendaji na wakati huo huo, mshirika muhimu. CEO na timu yake ya biashara wanaweza kuja na wazo, Ili wazo hilo litekelezwa CFO anakiwa kukubaliana nalo au kuja na wazo mbadala ambalo ni bora zaidi. Kwa muda mrefu CFO wameokuwa wakionekana kama wapinzani. Lakini kwa sasa CFO wameanza kubadilika na kushirikiana na mfumo mzima kwa lengo la kuleta matokeo chanya kwa manufaa ya kampuni na wanahisa,” Aliongeza.

Ni dhahiri kuwa, mazingira ya usimamizi wa fedha yanabadilika sana na ni muhimu kukidhi viwango vilivyowekwa duniani. Matumizi ya teknolojia za kisasa ni muhimu katika kuongeza ufanisi na kubaini viashiria vya hatari kwa wakati.

“Tunapaswa kuendana na kasi hii ya mabadiliko kama tunataka kusonga mbele. Kwa mfano, taarifa zetu za fedha zinapaswa kukidhi viwango vya utoaji wa taarifa za kifedha vya kimataifa. (International Reporting Standards)Kwa hiyo, kuwa na timu yenye weledi sio tu katika idara ya fedha lakini pia katika kampuni nzima ni jambo la muhimu.” alisema 

BARA LA AFRIKA LATAKA KUWEZESHWA KUJITEGEMEA

$
0
0


Nchi za Bara la Afrika Tanzania ikiwemo zimesema wakati umefika sasa kwa Nchi zilizoendelea kuisaidia Afrika kujitegemea na kuliwezesha kutumia rasilimali zake yenyewe kwa maendeleo ya watu wake badala ya kulifanya Bara hilo kama eneo la kupata malighafi ya kuhudumia viwanda za nchi zilizoendelea.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Prof. Palamagamba John Kabudi ameyasema hayo baada ya kushiriki Mkutano wa Mawaziri wa Maandalizi ya Mkutano wa Saba wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika (TICAD 7) uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Pacifico jijini Yokohama, Japan.

Ameongeza kuwa mkutano huo pamoja na mambo mengine umesisitiza umuhimu ya uwepo wa miundombinu ambayo inaunganisha Nchi za Kiafrika ili kuliwezesha bara la Afrika kuwa na miundo mbinu ya usafirishaji imara na zenye kuleta tija kwa wote.

Aidha Prof. Kabudi ameongeza kuwa ni mkutano huo pia umeazimia kuzitaka nchi zilizoendelea kuongeza fedha zaidi kwa ajili ya kutoa huduma za kijamii hususani katika nyanja za afya hususani katika kupambana na malaria,kifua kikuu na ukimwi sambamba na Afrika kuwajibika kuchukiua hatua zote za kuhakikisha uwepo wa utawala bora,usalama na Amani.

Akifungungua mkutano huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Mhe. Kono Taro amezipongeza nchi za Afrika kwa kupiga hatua katika maendeleo kupitia ushirikiano na Japan na kwamba nchi yake itaendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na nchi hizo ili kuziwezesha kufikia malengo ikiwemo mapinduzi ya viwanda.

Mhe. Taro amesema kuwa, ushirikiano kati ya Afrika na Japan kupitia mpango wa TICAD umeendelea kuimarika tangu kuanzishwa kwa mpango huo mwaka 1993 na kwamba ni matarajio yake Mktano wa Saba utakuwa wa tija zaidi kwa pande hizo mbili.

“Nawakaribisha Mawaziri wenzangu Yokohama ambapo maandalizi ya mkutano wa saba wa kimataifa wa Tokyo kuhusu maendeleo ya Afrika yanaendelea. Jukumu letu ni kupitia na kupitisha rasimu ya Azimio la Yokohama na Mpango kazi wake ili hatimaye litunufaishe sote pale litakapopitishwa na Wakuu wa nchi” alisema Mhe. Taro.

Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Mkutano huo, Mhe. Sameh Shoukry ameipongeza Japan kwa kuendelea kuandaa mikutano hiyo ambayo ina nia ya kuifikisha Afrika katika mapinduzi ya viwanda na kuondokana na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa ajira kwa vijana na nyingine nyingi.

Kwa upande wake, Naibu Mwenyekiti wa Kamishenii ya Umoja wa Afrika ambao ni miongoni mwa waandaaji wenza wa Mkutano wa Saba wa TICAD, Bw. Kwesi Quartey amesema kuwa, mkutano huo unafanyika wakati Umoja wa Afrika unaendelea kutekeleza agenda 2063. Agenda hiyo pamoja na mambo mengine inalenga kuziwezesha nchi za Afrika kufikia maendeleo ya hali ya juu kwenye sekta mbalimbali zikiwemo afya, elimu, teknolojia na miundombinu. 

Kadhalika Mkurugenzi wa Kituo cha Huduma za Kanda ya Afrika kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Afrika, Bw. Lamin Manneh alisema kuwa ushirikiano kati ya Afrika na Japan kupitia TICAD umekuwa na mchango mkubwa kwenye maendeleo ya Bara la Afrika.

Mkutano wa Saba pamoja na mambo mengine unatoa fursa ya kupanga mikakati ya ushirikiano na agenda za kimaendeleo zitakazotelezwa kati ya Japan na Afrika kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo kuanzia mwaka 2019 hadi 2021.

Agenda za mkutano wa mwaka huu zinalenga kujadili mageuzi ya kiuchumi na kuboresha mazingira ya uwekezaji kwa kukuza sekta na uvumbuzi. Pia kuimarisha usalama na ustahimilivu endelevu kwenye jamii pamoja na kuendeleza jitihada za kuimarisha amani na usalama barani Afrika. Agenda za Mkutano wa Saba zinaenda sambamba na agenda 2063 ya Umoja wa Afrika, Agenda 2030 ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa na maazimio mengine ya kimataifa kama Mkataba wa Paris kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa.
  
Mkutano huu ambao umewashirikisha Mawaziri kutoka nchi za Afrika, na wadau mbalimbali wa maendeleo unafanyika ikiwa ni maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali utakaofanyika kuanzia tarehe 28 hadi 30 Agosti 2019.

SIMANJIRO YAZINDUA SOKO LA MADINI

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara mhandisi Zephania Chaula akishiriki kukata utepe na wadau wa madini kwenye uzinduzi wa soko la madini ya vito Orkesumet.
Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara mhandisi Zephania Chaula akizungumza kwenye uzinduzi wa soko la madini ya vito Mji mdogo wa Orkesumet.
Matukio mbalimbali kwenye uzinduzi wa soko la madini ya vito Mji mdogo wa Orkesumet Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara
…………………..
MKUU wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, mhandisi Zephania Chaula amezindua soko la madini ya vito kwenye mji mdogo wa Orkesumet.

Soko hilo litatumika kuuza na kununua madini ya vito ikiwemo Ruby, Green Tomarine, Green Gainet, Tanzanite na mengineyo.

Mhandisi Chaula akizungumza wakati akizindua soko hilo, amewataka wafanyabiashara na wachimbaji wa madini kutumia soko hilo kuuza madini na kulipa kodi ya serikali. 

Chaula alisema serikali imelenga kuondoa ukiritimba kwenye sekta ya madini hivyo wachimbaji na wanunuzi watumie fursa hiyo kwa kuuza na kununua madini kwenye soko hilo. 

“Baada ya kumaliza uzinduzi wa soko hilo la madini Orkesumet tutazindua soko lingine Mirerani hivyo kuwa na masoko mawili kwenye mkoa wa kimadini wa Simanjiro hiyo ni hatua kubwa mno,” alisema mhandisi Chaula. 

Aliwataka wafanyabiashara na wachimbaji kutumia masoko hayo kulipa kodi kwani ndizo zinazotumika kwenye maendeleo mbalimbali ya jamii. 

“Mnaona pale tunajenga hospitali ya wilaya ya Simanjiro, awali hatukuwa nayo ila kupitia makusanyo ya ndani yanayotokana na kodi zenu na usimamizi wa Rais John Magufuli hivi sasa tumekamilisha hospitali,” alisema mhandisi Chaula. 

Mwenyekiti wa chama cha wachimbaji madini mkoa wa Manyara (Marema) Justin Nyari alimpongeza mkuu huyo wa wilaya na ofisi ya madini kwa kuhakikisha soko hilo linafanikishwa kuanzishwa ili kutimiza agizo la Rais John Magufuli. 

Nyari alisema wanamuomba mkuu huyo wa wilaya kupeleka salamu zao kwa mkuu wa Mkoa huo Alexander Mnyeti ili azifikishe kwa Rais John Magufuli kwani anawapenda na kuwapa kipaumbele wachimbaji na sekta ya madini kwa ujumla. 

Kaimu ofisa madini mkazi mkoa wa kimadini wa Simanjiro mhandisi Castro Maduwa alisema wamejipanga kuvuka lengo la makusanyo ya kodi ya sh6 bilioni kwa mwaka wa fedha wa 2019/2020.

Maduwa alisema mwaka jana 2018/2019 walipangiwa wakusanye sh1.5 bilioni lakini wakakusanya sh2.8 bilioni hivyo kuvuka lengo. 

Katibu wa CCM wa wilaya ya Simanjiro Ally Kidunda alisema ilani ya uchaguzi wa CCM inazidi kutekelezwa kwa vitendo Simanjiro. 

Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Sendeu Laizer alipongeza hatua hiyo kwani itaongeza tija kwa wachimbaji na wanunuzi wa madini Simanjiro.

KAMATI YAPONGEZA UTEKELEZAJI MIRADI YA BARABARA

$
0
0
Muonekano wa hatua ya ujenzi wa barabara ya Mtwara-Mnivata KM 50 kwa kiwango cha lami. Ujenzi wa barabara hiyo umefikia zaidi ya asilimia 50 na utagharamu zaidi ya shilingi bilioni 89.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, walipokuwa wakikagua moja ya ujenzi wa barabara ya kimkakati ya Mtwara-Mnivata yenye urefu wa KM 50, wakati kamati hiyo ilipotembelea mradi huo, Mkoani Mtwara.
Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa, akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), mjini Dodoma.Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mheshimiwa Selemani Kakoso, akitoa maelekezo na ushauri kwa Viongozi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano pamoja na Watendaji wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), mara baada ya kupokea taarifa ya Utekelezaji wa Wakala huo, mjini Dodoma.
……………………………..

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeupongeza Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), kwa utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa madaraja makubwa na barabara ya kuunganisha mkoa kwa mkoa kupitia mtandao wa barabara nchini.

Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji ya Wakala huo ilyowasilishwa kwa Wajumbe wa Kamati jijini Dodoma, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Selemani Kakoso, amesema kuwa kupitia utaratibu huo hata barabara zilizosahaulika nchini zinaweza kunufaika kwa kuwa na maendeleo ya kiuchumi kutokana na uwepo wa miradi hiyo.

“Naipongeza Serikali kupitia TANROADS kwa kufikiria kuunganisha mikoa kupitia barabara hususan katika mikoa ya Katavi, Rukwa, Kigoma na Kagera. Mikoa hii ilionekana kama imesahaulika lakini sasa inaonekana kupata maendeleo kutokana na uwepo wa miradi ya barabara ambayo inatekelezwa”, amesema Mhe. Kakoso.

Aidha, Ameutaka Wakala huo kuendelea kuziangalia na kuzipa kipaumbele barabara za kimkakati ambazo zina maslahi mapana katika maendeleo na ukuaji wa uchumi wa nchi.

Ametaja miradi hiyo kama barabara ya Mtwara- Mnivata, Katavi- Kigoma na Kasulu – Kagera ambayo kwa pamoja ikikamilika itaunganisha mikoa hiyo na mikoa jirani na hatimaye kufungua fursa za kiuchumi kwa wananchi. 

Mwenyekiti Kakoso, ameusisitiza Wakala huo kuendelea na uboreshaji wa viwanja vya ndege hususan katika ujenzi wa majengo ya abiria ambayo yanaendana na wingi wa abiria pamoja na kujenga uzio katika viwanja vya ndege ambavyo havina uzio lengo likiwa ni kuweka usalama katika viwanja hivyo.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa, amesema kuwa Serikali itaendelea kutekeleza ujenzi na ukarabati wa barabara, madaraja na mizani.

Amefafanua kuwa hadi kufikia Juni, 2019 Wakala umefanikiwa kujenga kituo cha mizani cha Kurasini ambacho kimejengwa kwa ajili ya kuhakiki uzito wa magari yanayotoka bandarini na kuweka CCTV Kamera katika mzani huo.

Kwandikwa, ameongeza kuwa Wakala umeendelea na kazi za ujenzi na ukarabati wa miradi mbalimbali ya viwanja vya ndege ambapo hatua za utekelezaji zilizofikiwa kwa baadhi ya miradi zinaridhisha. 

Amesema kuwa hadi kufikia Juni, 2019 ujenzi wa Jengo la abiria katika Kiwanja cha ndege wa Songwe umefika asilimia 77 na ukarabati na ujenzi wa Jengo la kuongozea ndege na mizigo katika Kiwanja cha Ndege cha Mwanza umefika asilimia 93. 

“Sisi kama Serikali tutaendelea kuboresha viwanja vingine vya ndege, tunajua wananchi wanahitaji maendeleo kupitia sekta ya anga, hivyo hatuna budi kuboresha viwanja hivi, amesisitiza Kwandikwa.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imepokea taarifa ya TANROADS ambayo imeainisha majukumu ya Wakala huo kwa mwaka wa Fedha 2018/19 na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi na ukarabati wa barabara kuu, barabara za mikoa, madaraja na viwanja vya ndege.

WIZARA YA AFYA,MLOGANZILA KUSHIRIKIANA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA

$
0
0
Mhandisi Akaniwa Msengi (wa kwanza kushoto) akifafanua jambo kuhusu mtambo wa liquid oxygen.
Mhandisi Msengi akiwaelezea wataalam wa Hospitali ya Mnazi mmoja Zanzibar jinsi mtambo wa oxygen mbadala unavyofanya kazi. Ujumbe wa wataalam hao umetembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila ili kujifunza matumizi ya oxygen kwa wagonjwa.





Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Tiba kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Timothy Wonanji (katikati) akizungumza na baadhi ya viongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila mara baada ya kutembelea hospitalini hapo.
Mhandisi wa Hospitali ya Mloganzila, Happymark John (wa kwanza kushoto) akielezea jinsi tanki la kuhifadhi maji linavyofanya kazi.
……………………….

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto imesema itaendelea kushirikiana na Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila katika kuhakikisha inatatua changamoto zilizopo ili kuendelea kuboresha utoaji wa huduma za fya.

Kauli hiyo nimetolewa na Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Tiba kutoka Wizara ya Afya Dkt. Timothy Wonanji mara baada ya kutembelea Hospitali ya Mloganzila ili kuangalia utoaji wa huduma, miundominu na changamoto zilizopo.

“Nawapongeza kwa utendaji wenu wa kazi nahidi tutaendelea kushirikiana katika kuhakikisha Hospitali ya Mloganzila inafikia malengo yake na wananchi wanaendelea kupata huduma bora’’amesema Dkt. Wonanji.

Katika hatua nyingine, Ujumbe wa wataalam kutoka Hospitali ya Mnazi mmoja Zanzibar umetembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila ili kujifunza matumizi ya oxygen kwa wagonjwa.

Mkurugenzi wa Uuguzi Hospitali ya Mnazi mmoja Zanzibar, Haji Nyonje Tandu amesema ujumbe huo umehusisha viongozi wa ngazi mbalimbali kwa lengo kujifunza jinsi oxygen inavyopatikana, matumizi yake kwa wagonjwa na kuona namna mitambo inavyozalisha na kusambaza.

“Tumekuja kujifunza kwenu ili tuendelee kuboresha utoaji huduma za afya kwa wananchi kwani hospitali yetu ina matumizi makubwa ya oxygen ikiwa ni wastani wa mitungi 45 kwa siku, hivyo inatupasa kuendelea kujifunza zaidi’’amesema Bw. Haji Nyonje Tandu.

BARABARA YA KISONGO BYPASS KUFUNGUA FURSA ZA KIUSALAMA UWANJA WA NDEGE ARUSHA

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Sifael Kulanga akimkabidhi rasmi eneo la mradi wa ujenzi wa barabara ya Kisongo bypass Mkandarasi wa Ujenzi wa barabara hiyo Lang Shang ambaye ni mhandisi wa barabara wa kampuni ya Snohydro ya China kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara nje kidogo ya jiji la Arusha leo picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha.Mstahiki Meya wa jiji la Arusha Kalist Lazaro Buhay akisikiliza taarifa kutoka kwa kaimu mkurugenzi Sifael Kulanga wakiwa pamoja na Mhandisi wa barabara wa Snohydro Lang Shang mara baada ya makabidhiano hayo ya ujenzi wa barabara ya kisongo bypass nje kidogo ya jiji la Arusha picha na Ahmed Mahmoud Arusha

Baadhi ya Maofisa kutoka jiji la Arusha na Kampuni ya ujenzi ya Snohydro wakifuatilia makabadhiano hayo mara baada ya kutembelea eneo la mradi wa ujenzi wa barabara ya kisongo bypass wenye urefu wa kilimeta 3,44 picha na Ahmed Mahmoud Arusha

Picha ya pamoja mara baada ya kukagua eneo la ujenzi wa barabara ya Kisongo bypass itakayogharimu kiasi cha billion 4.106 hadi kukamilika mwezi januari mwakani picha na Ahmed Mahmoud Arusha.

*****************

Na Ahmed Mahmoud Arusha


Halmashauri ya Jiji la Arusha limepata Fedha za nyongeza kiasi cha bilion 4,106 kwa ajili ya ujezi wa barabara ya kisongo Bypass yenye urefu wa kilometa 3.44 kupitia fedha za mradi wa TSCP inayoratibiwa na benki ya dunia chini ya Ofisi ya Raisi Tamisemi

Mradi huo ambao tarehe 27 mwezi huu umekabidhi na Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa Mkandarasi Kampuni ya Ujenzi ya Snohydro ya nchini china utatekelezwa kwa muda wa miezi minne hadi Januari mwakani.

Akizungumza mara baada ya kuukabidhi mradi huo kwa kampuni hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Sifael Kulanga ambaye pia ni Mwanasheria wa jiji hilo amesema kuwa mradi huo ni wanyongeza na utatekelewa ndani ya miezi minne.

Alisema kuwa mradi huo utasaida sana kuondoa changamoto za msongamano katikati ya jiji la Arusha na una manufaa ya moja kwa moja kwa wananchi na utasaidia usalama kwenye uwanja mdogo wa ndege badala ya kukata katikati ya uwanja barabara hiyo itasaidia kuchepuka pembezoni mwa uwanja.

“Barabara hii ina umuhimu mkubwa sana katika uwanja wetu wa ndege na maeneo ya shule ya sekondari na itafungua fursa kwa wanaowahi katikati ya jiji kutoka stand kubwa ya mabasi ya mkoani inayotarajiwa kujengwa Olasit”

Kwa upande wake Mhandisi wa barabara wa kampuni ya Snohydro watakaojenga barabara hiyo Lang Yang Shang alisema kuwa wataifanya kazi hiyo ndani ya muda uliopangwa na kwa viwango vilivyowekwa na kwa ubora.

Alisema kuwa barabara hiyo na udogo ulipo hautawapa tabu kuikamilisha ndani ya wakati hivyo kuweza kukamilika bila kuwepo vikwazo vyovyote hivyo kuomba ushirikiano wakati wote wa ujenzi huo.

Awali akitoa taarifa ya mradi huo Mhandisi Agustini Mbuya alisema kuwa barabara hiyo ni muunganiko wa bypass na itarahisisha mchepuko na kusaidia usalama na kuishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kutenga fedha hizo.

Alisema kuwa mradi huo utaanza ujenzi rasmi tarehe 11 mwezi ujao na leo ndio makabidhiano kwa jiji kumkabidhi rasmi mkarandari kwa ajili ya Ujenzi huo wa barabara

Nae Mstahiki meya wa jiji la Arusha Kalist Lazaro alisema kuwa Barabara hiyo ni sehemu ya mkataba uliosainiwa wiki iliyopita na utakuwa kielelezo cha kueleza jinsi utekelezaji wa ilani ya uchaguzi kwa wananchi mwaka ujao jinsi serikali ilivyotekeleza miradi.

WAAJIRI SERIKALINI WATAKIWA KUMALIZA ZOEZI LA UHAKIKI WA VYETI VYA WATUMISHI

$
0
0
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumzia utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuhusiana uadilifu na uwajibikaji kwa watumishi wa umma.

**************

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt.
Laurean Ndumbaro amewataka Wakuu wa Taasisi za Umma na Maafisa
Utumishi nchini kumaliza zoezi la uhakiki wa vyeti vya Watumishi wa
Umma vya ufaulu wa kidato cha Nne, cha Sita na Ualimu kwani ofisi yake
imekuwa ikipokea taarifa za uwepo wa watumishi wachache wenye vyeti
vya kughushi katika baadhi ya halmashauri na taasisi za umma.

Dkt. Ndumbaro ametoa maelekezo hayo ikiwa ni sehemu ya msisitizo wa
utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliyoyatoa wakati akizindua Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwezi Novemba, 2015 ambapo
alielekeza utumishi wa umma nchini uwe wa uadilifu, unaowajibika na
wenye sifa stahiki.

Dkt. Ndumbaro amefafanua kuwa uwepo wa taarifa za watumishi wenye
vyeti vya kughusi mpaka sasa unaashiria kuwa kuna baadhi ya Wakuu wa
Taasisi na Maafisa Utumishi hawajalipa uzito unaostahili zoezi la
kuwaondoa watumishi wenye vyeti vya kughushi.

“Mpaka sasa bado tunapata taarifa za baadhi ya watumishi wenye vyeti
vya kughushi kuendelea na utumishi wa umma katika baadhi ya
halmashauri na taasisi, hivyo inatulazimu kuwasilisha vyeti vyao Baraza la
Mitihani kwa ajili ya uhakiki badala ya kuendelea na utekelezaji wa
majukumu mengine ya kitaifa,” Dkt. Ndumbaro amesisitiza.

Sanjari na hilo, Dkt. Ndumbaro amewataka watumishi wa umma nchini
kuwajibika kwa Serikali na wananchi pindi wanapofuata huduma katika
taasisi zao ili kujenga mahusiano mazuri kati ya Serikali na wananchi.

Dkt. Ndumbaro ametoa wito kwa Wakuu wa Taasisi kuhakikisha
wanasimamia nidhamu mahala pa kazi ili watumishi wa umma waweze
kutumia muda wao wa kazi vizuri kwa kutoa huduma bora kwa umma.

SERIKALI YAZINDUA UJENZI WA VIVUKO VIPYA VYA BUGOROLA-UKARA, CHATO-NKOME

$
0
0
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Eng. Japhet Maselle (wa tatu kushoto) akimuongoza Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng. Warioba Sanya (katikati), kwenda kuzindua ujenzi wa vivuko viwili vipya vya Bugorola-Ukara Wilaya ya Ukerewe na Chato nkome Wilaya ya Chato. Uzinduzi huo ulifanyika jana katika karakana ya Songoro Marine Boartyard Ltd iliyoko Ilemela, jijini Mwanza.
Eng. Warioba Sanya kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akizindua ujenzi wa kivuko kipya cha Chato-Nkome (wilaya ya Chato) kinachojengwa na Kampuni ya Songoro Marine Boatyard Ltd ya jijini Mwanza, kwa gharama ya Tshs Bilioni 3.1 fedha inayotolewa na Serikali ya Tanzania. Kivuko hicho kitakuwa na uwezo wa kubeba tani 100 yaani abiria 200, magari 10 na mizigo. Ujenzi wa kivuko hiki utakamilika ndani ya Wiki 40.
Eng. Warioba Sanya kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akizindua ujenzi wa kivuko kipya cha Bugorola-Ukara (Wilaya ya Ukerewe) kinachojengwa na Kampuni ya Songoro Marine Boatyard Ltd ya jijini Mwanza, kwa gharama ya Tshs Bilioni 4.2 fedha inayotolewa na Serikali ya Tanzania. Kivuko hicho kitakuwa na uwezo wa kubeba tani 100 yaani abiria 300, magari 10 na mizigo. Ujenzi wa kivuko hiki utakamilika ndani ya Wiki 40.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Eng. Japhet Maselle (kushoto) akimpongeza Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng. Warioba Sanya (kulia) baada ya kukamilisha uzinduzi wa ujenzi wa vivuko vipya viwili kwa ajili ya maeneo ya Chato-Nkome (Chato) na Bugorora-Ukara (Wilaya ya Ukara) Mkoa wa Mwanza. Uzinduzi huo ulifanyika jana katika karakana ya Songoro Marine Boatyard Ltd, Ilemela jijini Mwanza.

………………………

Na TEMESA

SERIKALI imezindua rasmi ujenzi wa vivuko vipya viwili vya kisasa vitakavyotoa huduma ya kusafirisha abiria, mizigo na magari kati ya Bugorola-Ukara Wilaya ya Ukerewe Mkoa wa Mwanza na Chato-Nkome Wilaya ya Chato mkoani Geita.

Uzinduzi wa ujenzi huo umefanyika jana mkoani Mwanza katika eneo la karakana ya Kampuni ya Songoro Marine Transport Boatyard Ltd, inayojenga vivuko hivyo ambapo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe pamoja na taasisi mbali mbali zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Mhandisi Japhet Maselle alisema Serikali imeamua kujenga vivuko hivyo kutokana na kuwapo kwa uhitaji mkubwa wa huduma ya vivuko kwa wananchi wa maeneo hayo.

Mhandisi Maselle alisema kivuko cha Bugorola-Ukara kinajengwa na Kampuni ya Songoro Marine Transport Boatyard Ltd kwa gharama ya Tsh bilioni 4.2 na kile cha Chato- Nkome kinagharimu Tsh bilioni 3.1

“Vivuko vyote vinagharimu jumla ya Tsh bilioni 7.3 fedha zinazotolewa na Serikali ya awamu ya tano, chini ya uongozi mahiri wa Jemedari, Rais wetu, Mhe. Dkt. John Joseph Pombe Magufuli, na kwa mujibu wa mikataba tuliyoingia na kampuni hii ni kwamba vivuko hivi vitajengwa kwa miezi 10, hata hivyo namuagiza mzabuni akamilishe ujenzi wa vivuko hivi kwa chini ya muda huo”.

Kivuko cha Bugorola-Ukara kitakuwa na na vipimo vya urefu wa mita 39, upana mita 10 na kitaelea ndani ya maji kati ya mita 0-7 hadi 1.0, pia kitakuwa na uwezo wa kubeba tani 100 yaani abairia 300, magari 10 na mizigo, vile vile kivuko cha Chato-Nkome kitakuwa kitakuwa na vipimo vya urefu wa mita 37, upana mita 10 na kitaelea ndani ya maji kati ya mita 0-7 hadi 1.0, pia kitakuwa na uwezo wa kubeba tani 100 yaani abairia 200, magari 10 na mizigo.

Vivuko hivi vitafungwa injini mbili kila kimoja, HP 350 kwa kivuko cha Bugorola-Ukara na HP 300 kwa kivuko cha Chato-Nkome na vitaendeshwa na mifumo miwili ya usukani ambapo mmoja utakuwa ni wa dharura. Lengo la serikali ni kuimarisha usalama majini na usafiri wa uhakika ndio maana vivuko hivi vinajengwa kwa mabati maalum ya daraja la kwanza ‘grade A marine’ 

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Songoro Marine Transport Boatyard Ltd, Major Songoro aliipongeza Serikali kwa kuiamini kampuni yake na kuipatia zabuni za kujenga vivuko hivyo huku akiahidi kuvikabidhi mapema mwezi Februari badala ya Aprili kama ilivyo kwenye mkataba. 

Kwa upande wa Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Warioba Sanya alisema ujenzi wa vivuko hivyo ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Dk. John Magufuli ya kutaka kuboresha na kuimarisha usalama wa abiria na vyombo vya majini ndani ya Ziwa Victoria.

“Hapa kinachotekelezwa ni ahadi ya rais wetu na ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), hatutaki yale yalitokea Bugorola yatokee tena, sote tunajua mahitaji yaliyopo pale Bugorola ingawa kuna kivuko cha MV Sabasaba kinafanya kazi pale”.

Aliongeza kuwa Serikali imekusudia kuwawezesha wakandarasi wa ndani ili kusudi kodi za watanzania ziweze kubaki hapa nchini kwa watanzania wenyewe. Mkoa wa Mwanza sasa upo katika mkakati maalumu wa kuwa kituo cha uchumi katika nchi za Afrika Mashariki, ndio maana tunataka kampuni hii iwezeshwe na kuwa mahiri ili iweze kujenga meli kubwa hapa hapa jijini Mwanza. Hivyo nawaagiza viongozi wa kampuni hii kujenga vivuko hivi kwa ufanisi na kasi kubwa.

YAMETIMIA YA UKARABATI WA SHULE YA MSINGI KIHESA IRINGA

$
0
0
Diwani wa kata ya Kihesa Jully Sawani akiongea na mwandishi wa habari wa blog hii ofisini kwake.

Na Fredy Mgunda, Iringa
MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati ametakiwa kutimiza ahadi ya kukarabati shule ya msingi Kihesa kama alivyowaahidi wakazi wa kata ya kisheza wakati wa mkutano wa hadhara uliyofanyika katika shule hiyo.

Akizungumza na blog diwani wa kata ya Kihesa Jully Sawani amemuomba mbunge huyo kutimiza ahadi aliyoitoa kwa lengo la kuhakikisha wanaboresha sekta ya elimu katika kata hiyo.

“Naomba nimpongeze bwana Jose Mgongolwa kwa kusaidia kukarabati baadhi ya majengo ya madarasa kwa msaada wake wa kukarabati madarasa hayo katika shule ya msingi Kihesa” alisema Sawani

Kwa upande wake Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati amesema kuwa atatimiza ahdi hiyo mwezi wa tisa akitoka bungeni na kila kitu kipo sawa.

“Utaratibu wa sasa ukiomba pesa kwa wadau unatakiwa kutoa account ya Halmashuri ili kila kitu kinapitia kwenye ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri hivyo tayari wadau tayari wameshazitoa na zipo halmashuri” alisema Kabati 

Aidha Kabati amesema anamifuko ya saruji zaidi ya mia saba kwa lengo la kukamilisha ahadi zote alizoahidi katika shule mbalimbali mkoani Iringa.

Mwezi wa tisa naanza kutekeleza ahdi zote kwa kuwa pesa ninazo hivyo ni jukumi la mkurugenzi kuninunulia mifuko hiyo ya sariji ili nianze kutimiza ahadi zote.

Watu saba wafikishwa kortini kwa kukutwa na mnyama kakakuona

$
0
0

Na, Editha Edward-Tabora 

Watu saba wamepandishwa Kizimbani hii leo katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Tabora wakikabiliwa na nyara ya Serikali za mnyama aina ya kakakuona katika kijiji cha Sogolo tarafa ya Usoke Wilayani Urambo mkoani Tabora 

Wayuhumiwa hao wamefikishwa mahakamani ambapo wameanza kusomewa shitaka linalowakabili katika shauri la uhujumu uchumi la namba 53 la mwaka 2019 

Akisoma shitaka hilo mbele ya hakimu mkazi mkoa Wa Tabora Joktan Rushwela, watuhumiwa hao wote saba wamedaiwa kukutwa na mnyama Huyo kakakuona bila kuwa na kibali cha Mkurugenzi mkuu Wa idara ya wanyama pori kinyume na kifungu cha 86(1) na (2) cha sheria namba 5 ya uhifadhi wanyamapori ya mwaka 2009

Aidha katika shitaka hilo upande wa jamhuri umebainisha kuwa watuhumiwa hao walinaswa na mtego mkali uliowekwa na maafisa wa mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori TAWA mkoa wa Tabora mnamo tarehe 20 mwezi wa kumi mwaka huu katika kijiji cha Sogolo wilayani Urambo wakiwa katika harakati za kutaka kumuuza kwa bei ya Shilingi milioni hamsini 

Hata hivyo maelezo hayo yaliyowasilishwa katika shauri hilo la uhujumu uchumi mnyama huyo kaka kuona mwenye thamani halisi ya Shilingi milioni mbili na laki mbili ambapo ni sawa na Dola za kimarekani 960,na watuhumiwa hao imedaiwa walikuwa wakimmiliki ambavyo Siyo halali huku wakitafuta soko la kwenda kumuuza.
Pichani ni mnyama kakakuona.

 Pichani ni watuhumiwa Saba wanaokabiliwa na shitaka la uhujumu uchumi la kukamatwa na nyara za serikali aina mnyama kakakuona.

Dkt.Kikwete mgeni rasmi marathon ya kuchangia watoto wenye ugonjwa wa moyo

$
0
0

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
RAIS Mstaafu Awamu ya Nne Dkt.Jakaya Kikwete kuwa mgeni rasmi wa Brazuka Marathon zitazokafanyika Septemba 15 viwanja vya Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mratibu wa Marathon hizo  Nasikiwa Berya amesema kuwa fedha zitapatikana katika mashindano hayo zitakwenda kwa ajili ya kusaidia watoto wa chini ya miaka mitano  wenye matatizo ya moyo.


Amesema kuwa kwa mujibu wa Taasisi  Moyo ya Jakaya Kikwete( JKCI) kuna watoto 512 wenye matatizo ya Moyo hivyo kama watanzania tunawajibu wa kusaidia watoto hao kuweza kusaidia katika matibabu.

Berya amesema kuwa watanzania wajitokeze kujisajili katika mbio hizo za kilomita Tano, Kumi pamoja na Kumi na Tano  ambapo kilomita tano watajisajili kwa sh.5000, Kilomita 10 sh.10000 pamoja na kilomita 15 sh.15000.


Amesema katika  kuwa mbio hizo wanatarajia kukusanya milioni 100 ambazo zitasaidia kutoa matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo wanaotoka katika familia zisizojiweza katika kugharamia matibabu hayo.

Berya amesema kuwa watanzania wanaweza kuchangia katika  namba ya simu ya TTCL ambao wamekuwa wadhamini katika marathon hizo

Balozi wa Mbio hizo ni Msanii Hamis Mwijuma MwanaFA amesema  kuwa kama jamii tunawajibu wa kusaidia watoto hawa ambao  kila mtoto anakipaji chake hivyo hawahitajiwi kuachwa.


Kwa upande wa Afisa Mahusiano na Mawasiliano wa Coca Cola Victor Biyemerwa amesema kama wadau wameguswa  na kuona wa wajibu wa kushiriki marathon ikiwa ni pamoja na kudhamini.
 Mratibu wa Mrazuka Marathon Nasikiwa Berya akizungumza na waandishi habari  kuhusiana na marathon ya kuchangia watoto wenye matatizo ya Moyo yatayofanyika jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa Marathon kwa ajili ya kuchangia watoto wenye matatizo ya moyo Hamis Mwijuma ‘MwanaFA’ akizungumza na waandishi habari kuhusiana na ushiriki katika marathon hizo.
Afisa Mahusiano na Mawasiliano wa Coca Cola Victor Biyemerwa akizungumza kuhusiana na udhamini katika marathon.

Jiji la Dodoma kujenga Hoteli ya Nyota Nne na Kitega Uchumi kwa Bilioni 69

$
0
0
Charles James, Michuzi TV

HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imesaini mikataba ya ujenzi wa miradi ya kimkakati yenye thamani ya shilingi bilioni 69.29 katika jitihada zake za kuelekea kujitegemea kimapato.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi alipokuwa akitoa maelezo mafupi ya miradi ya kimkakati ya ujenzi wa hoteli ya Jiji la Dodoma na jengo la kitega uchumi la Jiji katika hafla ya utiaji saini mikataba miwili ya miradi ya uwekezaji..

Kunambi amesema Halmashauri ya Jiji itasaini mkataba wa ujenzi wa Hoteli ya Jiji la Dodoma (Dodoma City Hotel) itakayojengwa katika mtaa wa Nyerere na Mkandarasi Stecol Coorporation (China) kwa gharama ya shilingi bilioni 9.995. 

Amesema kuwa hoteli hiyo itakayokuwa na hadhi kati ya nyota tatu na nyota nne, itakuwa na ghorofa 11 ikiwa na kumbi za mikutano, mgahawa mkubwa, vyumba vya kulala na maegesho ya magari.

Mkataba wa pili aliutaja kuwa ni ujenzi wa jengo la kitegauchumi la Jiji (Government City Complex) litakalojengwa katika Mji wa Serikali – Mtumba. Jengo hilo litajengwa na na Mkandarasi Mohamed Builders Ltd kwa gharama ya shilingi bilioni 59.3. 

“Jukumu la Halmashauri ya Jiji ni kujenga makao makuu ya nchi. Hivyo, awamu ya kwanza litajengwa jengo la ghorofa sita litakalokuwa na mgahawa, sehemu za taasisi za kifedha, na kumbi za mikutano zenye ukubwa tofauti na ‘apartments kwa gharama ya shilingi bilioni 18’” amesema Kunambi.

Utiaji saini wa mikataba hiyo umeshuhudiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge, Meya wa Jiji la Dodoma Prof Mwamfupe pamoja na Wakuu wa Wilaya za Dodoma na Wananchi wa Jiji hilo.
 Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi (kulia) Meya wa Jiji hilo Profesa Mwanfupe (wa pili kulia) wakisaini mkataba wa kuanza kwa ujenzi wa Hosteli ya Dodoma City Hotel yenye hadhi ya Nyota Nne na Wakandarasi kutoka Kampuni ya Stecol Cooperation ya China.
 Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma (kulia), Godwin Kunambi, Meya wa Jiji hilo, Profesa Mwanfupe (katikati) na Mkandarasi kutoka Kampuni ya Mohamed Builders wakisaini mkataba wa kujenga mradi wa jengo la kitega uchumi litakalogharimu Sh Bilioni 59
 Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi akizungumza wakati wa kutiliana saini na wakandarasi watakaojenga mirado miwili ya kimkakati, Hoteli ya Nyota Nne na Jengo la Kitega Uchumi
Baadhi ya wananchi wa Jiji la Dodoma waliojitokeza kushuhudia utiliaji saini huo

DKT. MAHIGA AKUTANA NA ASASI YA UTAWALA WA SHERIA YA IRELAND JIJINI DODOMA

$
0
0
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akisikiliza maelezo ya Naibu Balozi wa Ireland nchini mhe. Bronagh Carr walipofanya mazungumzo ofisini kwake katika mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akisalimiana na Naibu Balozi wa Ireland nchini Mhe. Bronagh Carr alipowasili ofisini kwake kwa ajili ya mazugumzo na Asasi ya Utawala wa Sheria ya ireland yaliyofanyika jijini Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akisikiliza maelezo ya wageni wake walipokutana ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na ugeni wa Asasi ya Utawala wa Sheria ya Ireland uliomtembelea ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akiwa na Mhe. Jaji Ailleen Donolley wa Mahakama Kuu ya Irelandambaye amekuja nchini na Asasi ya Utawala wa Sheria ya Ireland uliomtembelea mhe. Waziri ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akiwa na Mhe. Jaji Ailleen Donolley wa Mahakama Kuu ya Ireland na Mary Rose Gearty Mwendesha Mashtaka nchini Ireland ambao wamekuja nchini na Asasi ya Utawala wa Sheria ya Ireland uliomtembelea mhe. Waziri ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma.

*************

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt Augustine Mahiga amekutana na asasi
isiyo ya kiserikali ya Utawala wa Sheria ya nchini Ireland ofisini kwake katika mji wa Serikali Mtumba ulioko Jijini Dodoma.

Ugeni huo ambao uliongozwa na Naibu Balozi wa Ireland nchini Bi. Brognagh Carr ulijumuisha Jaji Ailleen Donolley wa Mahakama Kuu ya Ireland, Mary Rose Gearty Mwendesha Mashtaka nchini Ireland, Kate Mulkerrins Mkuu wa Idara ya Sheria katika Jeshi la Polisi nchini Ireland. Ugeni huo pia uliambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanawake katika Sheria na Maendeleo Afrika tawi la Tanzania (WiLDAF) Anna Kulaya.

Katika mazungumzo yao wamezungumzia namna ya kuangalia jinsi ambavyo wanaweza kutumia ujuzi na utaalamu wao katika kusaidia Mahakama nchini, kuona vyanzo vya matatizo ya kijamii nchini na jinsi ya kusaidia kukakabiliana navyo na kwa pamoja kuja na mpango wa kukabiliana na matukio ya ukatili wa kijinsia nchini.

Ujumbe huo pua umejadili maeneo ambayo pande hizo mbii zinaweza
kushirikiana katika harakati za kukabiliana na vitendo cya ukatili wa kijinsia na upatikanaji wa haki za kijinsia nchini.

Asasi ya Utawala wa Sheria inaundwa na wanasheria wa nchini Ireland inafanya kazi ya kukuza utawala wa sheria katika nchi zinazoendelea kwa kutumia ujuzi na wanasheria wa nchi hiyo kuhakikisha upatikanaji haki duniani na kuwezesha wananchi kuishi katika jamii ambazo hazikabiliwi na matatizo ya kutokuwa na usawa, rushwa na migogoro

PROF KABUDI AELEZEA KUSUDIO LA NCHI ZA AFRIKA KUTAKA NCHI ZILIZOENDELEA KULIWEZESHA BARA LA AFRIKA KUJITEGEMEA KWA KUTUMIA RASILIMALI ZAKE

WAZIRI WA MAMBO YA NJE, PROF. PALAMAGAMBA JOHN KABUDI ASHIRIKI MKUTANO WA MAWAZIRI WA TICAD JIJINI YOKOHAMA, JAPANA

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Mhe.Kono Taro (mwenye tai ya rangi ya chungwa) akifungua rasmi Mkutano wa Mawaziri wa maandalizi ya Mkutano wa Saba wa Kimataifa kuhusu Mandeleo ya Afrika (TICAD 7) . Ufunguzi huo umefanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Pacifico jijini Yokohama, Japan tarehe 27 Agosti 2019. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (wa tatu kushoto kwenye meza nyeupe) akifuatilia ufunguzi wa Mkutano wa TICAD wa Mawaziri uliofanyika Yokohama, Japan tarehe 27 Agosti 2019 
Mkutano ukiendelea





MKUTANO WA MAWAZIRI WA MAANDALIZI YA MKUTANO WA SABA WA TOKYO KUHUSU MAENDELEO YA AFRIKA (TICAD 7) WAFANYIKA JIJINI YOKOHAMA, JAPAN


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi leo tarehe 27 Agosti 2019 ameshiriki Mkutano wa Mawaziri wa Maandalizi ya Mkutano wa Saba wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika (TICAD 7) uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Pacifico jijini Yokohama, Japan.


Mkutano huo pamoja na mambo mengine unatarajiwa kupitia na kupitisha rasimu ya Azimio la Yokohama na Mpango Kazi wa Utekelezaji wa Azimio hilo litakalowasilishwa kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali utakaoanza tarehe 28 hadi 30 Agosti 2019 kwa ajili ya kuridhiwa.


Akifungungua mkutano huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Mhe. Kono Taro amezipongeza nchi za Afrika kwa kupiga hatua katika maendeleo kupitia ushirikiano na Japan na kwamba nchi yake itaendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na nchi hizo ili kuziwezesha kufikia malengo ikiwemo mapinduzi ya viwanda.


Mhe. Taro alisema kuwa, ushirikiano kati ya Afrika na Japan kupitia mpango wa TICAD umeendelea kuimarika tangu kuanzishwa kwa mpango huo mwaka 1993 na kwamba ni matarajio yake Mkutano wa Saba utakuwa wa tija zaidi kwa pande hizo mbili.


“Nawakaribisha Mawaziri wenzangu Yokohama ambapo maandalizi ya mkutano wa saba wa kimataifa wa Tokyo kuhusu maendeleo ya Afrika yanaendelea. Jukumu letu ni kupitia na kupitisha rasimu ya Azimio la Yokohama na Mpango kazi wake ili hatimaye litunufaishe sote pale litakapopitishwa na Wakuu wa nchi” alisema Mhe. Taro.


Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Mkutano huo, Mhe. Sameh Shoukry ameipongeza Japan kwa kuendelea kuandaa mikutano hiyo ambayo ina nia ya kuifikisha Afrika katika mapinduzi ya viwanda na kuondokana na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa ajira kwa vijana na umaskini.


Kwa upande wake, Naibu Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika ambao ni miongoni mwa waandaaji wa Mkutano wa Saba wa TICAD, Bw. Kwesi Quartey amesema kuwa, mkutano huo unafanyika wakati Umoja wa Afrika unaendelea kutekeleza agenda 2063. Agenda hiyo pamoja na mambo mengine inalenga kuziwezesha nchi za Afrika kufikia maendeleo ya hali ya juu kwenye sekta mbalimbali zikiwemo afya, elimu, teknolojia na miundombinu.


Kadhalika Mkurugenzi wa Kituo cha Huduma za Kanda ya Afrika kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Afrika, Bw. Lamin Manneh alisema kuwa ushirikiano kati ya Afrika na Japan kupitia TICAD umekuwa na mchango mkubwa kwenye maendeleo ya Bara la Afrika. Aliongeza kuwsema kuwa, Shirika lake ambalo linasimamia maendeleo linaridhishwa na ushirikiano uliopo kati ya Japan na Afrika ambao kwa kiasi kikubwa umefanikiwa.


Mkutano wa Saba wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Ushirikiano na Afrika pamoja na mambo mengine unatoa fursa ya kupanga mikakati ya ushirikiano na agenda za kimaendeleo zitakazotelezwa kati ya Japan na Afrika kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo kuanzia mwaka 2019 hadi 2021.


Agenda za mkutano wa mwaka huu zinalenga kujadili mageuzi ya kiuchumi na kuboresha mazingira ya uwekezaji kwa kukuza sekta na uvumbuzi. Pia kuimarisha usalama na ustahimilivu endelevu kwenye jamii pamoja na kuendeleza jitihada za kuimarisha amani na usalama barani Afrika. Agenda za Mkutano wa Saba zinaenda sambamba na agenda 2063 ya Umoja wa Afrika, Agenda 2030 ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa na maazimio mengine ya kimataifa kama Mkataba wa Paris kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa.


Mkutano huu ambao umewashirikisha Mawaziri kutoka nchi za Afrika, na wadau mbalimbali wa maendeleo unafanyika ikiwa ni maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali utakaofanyika kuanzia tarehe 28 hadi 30 Agosti 2019.


Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Yokohama, Japan.

27 Agosti 2019.

RC MAKONDA AFANIKISHA MATIBABU YA MGONJWA ASHIRAFU, UVIMBE ULIOMTESA MUDA MREFU SASA WAPONA.

$
0
0
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, leo amemtembelea kijana aitwaye Hamza Ashiraf ambaye hivi karibuni alimsaidia kwa kumsafirisha kutoka nyumbani kwao Bukoba na kumleta jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi juu ya uvimbe wake kwenye paji la uso, ambapo ameridhishwa na maendeleo yake baada ya kufanyiwa upasuaji.

Makonda ametumia wasaha huo kuwashukuru madaktari wote walioshiriki kumfanyia upasuaji na kmwezesha hali yake kurejea kwenye matumaini zaidi tofauti na alivyokuwa mwanzo wakati anamuona.

“Ninapomuona leo Ashiraf akiwa katika hali hii kiukweli siamini macho yangu kwani nilivyomkuta mwanzo wakati nachukua hatua ya haraka ya kumsafirisha kuja kupatiwa matibabu ukweli sasa nikimuona nahisi mabadiliko yake ni kama mbingu na aridhi

hivyo sina budi kuendelea kutoa shukurani zangu kwa madakitari wote,” alisema Makonda.SIKU chache zilizopita kijana Ashiraf akiwa kwao Bukoba, alijitokeza hadharani kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii akiomba msaada wa matibabu ya tatizo lake la uvimbe uliojitokeza kwenye eneo la uso wake.

Lakini kwa kudra za Mwenyenzi Mungu,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh.Makonda alijitoa kumsaidia na mara moja akamfanyia utaratibu wa ndege ya kumfikisha jijini Dar es Salama na mara moja akaelekeza apelekwe katika hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi zaidi jambo ambalo tayari limeshafanyika na kwamba siku chache zijazo atafanyiwa upasuaji mkubwa ambao utapelekea sehemu kubwa ya uso wake kutoka.

Taarifa kutoka kwa Dkt Bingwa wa upasuaji wa Macho na masikio Edwin Lyombo, amesema, wakati Ashiraf anatolewa Bukoba tayari alikuwa ameshaanza kufanyiwa matibabu lakini Haya kuwa mazuri.

“Nitoe shukurani nyingi kwa Mh Makonda kwa moyo wake wa kujitolea kama huu, kwani endapo watu wengi Zaidi watapatikana kujitolea hapa nchini kusaidia watu wenye matatizo makubwa kama haya basi uwezokano wa kupunguza Malachi makubwa kama haya utaleta tija,” alisema Lyombo.

Ashiraf yeye ameendelea kutoa shukurani zake kwa Makonda kwa kumwezesha kumfikisha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

“Niendelee kutoa shukurani zangu kwa Mh Makonda kwa kuendelea kutoa mahitaji yote hadi muda huu ambapo leo naonekana mpya tena.,” alisema Ashiraf
Viewing all 110173 articles
Browse latest View live




Latest Images