Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live

Serikali yajipanga kufufua Shirika la uvuvi la Taifa

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia sekta ya Uvuvi Dk. Rashidi Tamatama,akizungumza na wadau wakati wa warsha ya uzinduzi wa zoezi la kupitia na kuandaa mpango mpya kabambe wa uvuvi uliofanyika leo jijini Dodoma
Muwakilishi kutoka shirika la FAO Bw.Fred Kafeo,akisoma taarifa wakati wa warsha uzinduzi wa zoezi la kupitia na kuandaa mpango mpya kabambe wa uvuvi uliofanyika leo jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Uvuvi wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw.Emmanuel Bulayi,akiongea na wadau wakati wa warsha uzinduzi wa zoezi la kupitia na kuandaa mpango mpya kabambe wa uvuvi uliofanyika leo jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia sekta ya Uvuvi Dk. Rashidi Tamatama,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kuzindua warsha wa zoezi la kupitia na kuandaa mpango mpya kabambe wa uvuvi uliofanyika leo jijini Dodoma.
Kaimu Meneja Mkuu Shirika la Uvuvi Tanzania TAFICO Bi. Esther Mulyila wakati wa warsha ya uzinduzi wa zoezi la kupitia na kuandaa mpango mpya kabambe wa uvuvi uliofanyika leo jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia sekta ya Uvuvi Dk. Rashidi Tamatama akiwa katika picha ya pamoja na wadau baada ya kuzindua warsha ya uzinduzi wa zoezi la kupitia na kuandaa mpango mpya kabambe wa uvuvi uliofanyika leo jijini Dodoma.



SERIKALI  imesema iko katika michakato wa kulifufua Shirika la Uvuvi la Taifa (TAFICO) ambalo  litajiwekeza katika uvuvi wa samaki kwenye ukanda wa bahari kuu.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia sekta ya Uvuvi Dk. Rashidi Tamatama  wakati wa warsha ya uzinduzi wa zoezi la kupitia na kuandaa mpango mpya kabambe wa uvuvi.

Amesema malengo ya serikali ya kuifufua TAFICO inatarajia kuwa na tija kubwa kutokana na mipango iliyopo katika kuiendeleza sekta hiyo.

“Mipango yetu ni kuhakikisha hii sekta unakuwa na serikali inafanya michakato ya kuifufua TAFICO na Mambo mazuri yanakuja” amesema Dkt Tamatama.

Amebainisha mpango mpya kabambe wa uvuvi unaelekeza sekta kusimamia, kuhifadhi na kulinda ili sekta hiyo itoe mchango mkubwa kwenye lishe kwa mtu moja moja na usalama wa chakula na kuelekeza sekta ili itoe mchango kwa uchumi,

 Amesema mpango  uliozinduliwa mwaka 2002,  ulimalizika mwaka 2015 na mafanikio ya mpango ule upande wa pwani kuna maboresho makubwa ya uvuvi wakati wa mradi uliojenga mialo nyingi na kukopesha zana za kuvulia vikundi mbalimbali vya uvuvi, pia kuna mradi mwingine wa benki ya dunia.

Kwa upande wake kaimu Meneja Mkuu wa TAFICO, Ester Mulyila, amesema Shirika hilo linatazamiwa kufufuliwa hivi karibuni na menejimenti ya kufufua shirika hilo waliteuliwa kuanza taratibu za kufufua shirika. 

Amesema TAFICO ilianzishwa 1974 wakati wa serikali ya awamu ya kwanza, ili kuendeleza shughuli za uvuvi  makao makuu Dar es salaam na ilifanya kazi Pwani yote ya Tanzania kuanzia Tanga,mpaka Mtwara ziwa Victoria.

Lingine ni Tanganyika Nyasa kubwa mpaka mwaka 1996 ikijihusisha na uvuvi hasa  wa kambamiti ilikuwa na meli, viwanda vya kutengeneza mashua za mbao na chuma, mitambo ya kuzalisha barafu, maghara ya kuhufadhia samaki.

Amebainisha mwaka 2008 wizara ya maliasili na utalii ilikuwa na dhamana ya uvuvi iliuza vitu vinavyohamishika kwa taratibu za serikali msajili wa hazina, lakini mali zisizohamishika zilibaki viwanja na majengo vilibaki kwa matumizi ya serikali.

Serikali ya awamu hii.imeongeza nguvu ya kutaka kufufua shirika waraka wa baraza la mawaziri imeelekeza shirika hilo kufufuliwa, lengo kuwezesha serikali kunufaika na raslimaliza zake za uvuvi hasa zilipo uchumi wa bahari kuu una ukubwa wa eneo la kilomita za mraba 223,000  ikiwa ni sawa na robo ya Tanzania nchi kavu.

MAANDALIZI YA UFUNGUZI WA EAPCCO GAMES KASARANI NAIROBI KENYA

$
0
0
Wanamichezo wa timu za Jeshi ya Polisi Tanzania wakiwa katika mazoezi ya mwisho kabla ya ufunguzi wa mashindano ya michezo ya Wakuu wa Majeshi ya Polisi kwa Nchi za Kanda ya Afrika Mashariki 2019 (EAPCCO GAMES), michezo inatarajiwa kufunguliwa rasmi Agosti 27,2019 katika kiwanja cha Kasarani Jijini Nairobi nchini Kenya.
Naibu Kamishna wa Polisi, DCP Ahmada Khamis akizungumza na wanamichezo wa timu za Jeshi la Polisi Tanzania zinazoshiriki katika michezo ya Wakuu wa Majeshi ya Polisi kwa Nchi za Kanda ya Afrika Mashariki 2019 (EAPCCO GAMES). Michezo hiyo inatarajiwa kufunguliwa Agosti 27, 2019 siku ya jumanne katika kiwanja cha Kasarani Jijini Nairobi nchini Kenya.
Wanamichezo wa timu za Jeshi ya Polisi Tanzania wakiwa katika hali ya morali kabla ya kuingia uwanja wa Karasani kwa mazoezi ya mwisho kabla ya ufunguzi wa mashindano ya michezo ya Wakuu wa Majeshi ya Polisi kwa Nchi za Kanda ya Afrika Mashariki 2019 (EAPCCO GAMES), michezo inatarajiwa kufunguliwa rasmi Agosti 27,2019 katika kiwanja cha Kasarani Jijini Nairobi nchini Kenya.
Wanamichezo wa timu za Jeshi ya Polisi Tanzania wakipita mbele ya jukwaa kuu kwa mazoezi ya mwisho (rehearsal) kabla ya ufunguzi wa mashindano ya michezo ya Wakuu wa Majeshi ya Polisi kwa Nchi za Kanda ya Afrika Mashariki 2019 (EAPCCO GAMES), michezo inatarajiwa kufunguliwa rasmi Agosti 27,2019 katika kiwanja cha Kasarani Jijini Nairobi nchini Kenya. Picha Na Jeshi la Polisi.

MKUU WA MKOA WA SHINYANGA AONGOZA MAMIA YA WAOMBOLEZAJI MAZISHI YA KAKA WA MBUNGE AZZA HILAL HAMAD

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack ameongoza mazishi ya kaka wa Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga, Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) Abel Bulugu Kaheza (52) aliyefariki dunia siku ya Alhamis Agosti 22,2019 jijini Dar es salaam akisumbuliwa na kansa ya koo.

Mazishi hayo yamefanyika leo Jumatatu Agosti 26,2019 katika kijiji cha Jomu kata ya Tinde wilaya ya Shinyanga ambapo mamia ya waombolezaji wameshiriki mazishi hayo. 

Akitoa salamu za pole na rambirambi,Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack amesema : 

"Kwa niaba ya serikali na wakuu wote wa wilaya wapo hapa,Mhe.Azza tunakupa pole sana,viongozi wote wa serikali wapo hapa kwa ajili ya kukuunga mkono na kukupa pole kwa msiba huu mkubwa,tunajua wote tumeguswa lakini hatuna namna,tungekuwa na uwezo tungeweza kusema aendelee kubaki lakini kwa kuwa hatuna uwezo tumwachie Mungu",amesema Telack. 

"Namuomba mwenyezi Mungu awape subira katika wakati huu mgumu lakini kikubwa tuendelee kumwombea marehemu kwa mwenyezi Mungu. Siku zote tunasema,msiba uunganishe watu,lakini msiba usichonganishe familia",ameongeza Telack. 

Mhubiri katika ibada ya mazishi alikuwa Mchungaji wa Kanisa la AICT Tinde William Shinyanga huku kiongozi wa ibada akiwa ni Nuhu Manoni kutoka kanisa la AICT Tinde. 

Abel Bulugu Kaheza alizaliwa Julai 1,1967 na amefariki dunia Agosti 22,2019 wakati akiendelea kupatiwa matibabu ya kansa ya koo katika hospitali ya Lugalo jijini Dar es salaam. 
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack akimpa pole Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga, Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) kwa kufiwa na kaka yake Abel Bulugu Kaheza leo nyumbani kwake kijiji cha Jomu kata ya Tinde wilaya ya Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akiteta jambo na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack nyumbani kwa Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga, Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) aliyefiwa na kaka yake Abel Bulugu Kaheza. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akimpa pole Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga, Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM) kwa kufiwa na kaka yake Abel Bulugu Kaheza.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga,Mabala Mlolwa akimpa pole kwa kufiwa na kaka yake Abel Bulugu Kaheza.
Mbunge wa jimbo la Msalala,Mhe Ezekiel akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack wakati wa msiba wa Abel Bulugu Kaheza.
Viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga wakiwa katika msiba wa Abel Bulugu Kaheza leo nyumbani kwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad.
Mbunge wa jimbo la Msalala,Mhe Ezekiel akiwapa pole wafiwa.
Jeneza lililobeba Mwili wa marehemu Abel Bulugu Kaheza likitolewa ndani kwa ajili ya ibada na waombozaji kuaga mwili huo.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack na wakuu wa wilaya wakiwa wamesimama wakati mwili wa marehemu Abel Bulugu ukitolewa ndani na kuwekwa nje kwa ajili ya ibada na waombolezaji kuuaga.Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha akifuatiwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko,wa kwanza kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kishapu, Mhe. Nyabaganga Talaba.
Mchungaji wa Kanisa la AICT Tinde William Shinyanga akiendesha ibada ya mazishi ya marehemu Abel Bulugu Kaheza nyumbani kwa Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad leo katika kijiji cha Jomu kata ya Tinde wilaya ya Shinyanga.
Mchungaji wa Kanisa la AICT Tinde William Shinyanga akiongoza ibada ya mazishi ya Abel Bulugu Kaheza (ambaye ni kaka wa Mbunge Azza Hilal) leo nyumbani kwa Mbunge Azza Hilal Hamad katika kijiji cha Jomu kata ya Tinde halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Kiongozi wa ibada ya mazishi ya Abel Kaheza, Nuhu Manoni kutoka kanisa la AICT Tinde akizungumza wakati wa ibada ya mazishi nyumbani kwa Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad leo katika kijiji cha Jomu kata ya Tinde wilaya ya Shinyanga.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad (mwenye kiremba cheusi katikati) akiwa kwenye ibada ya mazishi ya kaka yake Abel Bulugu Kaheza.
Ndugu wa marehemu Abel Bulugu Kahiza wakiwa kwenye ibada ya mazishi ya marehemu Abel Bulugu Kaheza.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack akitoa salamu za pole na rambirambi kufuatia kifo cha Abel Bulugu Kaheza.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack akitoa salamu za pole na rambirambi kufuatia kifo cha Abel Bulugu Kaheza.
Mbunge wa jimbo la Msalala,Mhe Ezekiel akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya wabunge 9 wa mkoa wa Shinyanga.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga,Mhe. Mabala Mlolwa akitoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Abel Bulugu Kaheza.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack( watatu kutoka kushoto akiwa msibani. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha akifuatiwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko,wa kwanza kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kishapu, Mhe. Nyabaganga Talaba.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack akiaga mwili wa marehemu Abel Bulugu Kaheza.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akiaga mwili wa marehemu Abel Bulugu Kaheza


Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akiaga mwili wa marehemu kaka yake,Abel Bulugu Kaheza.




Mazishi ya mwili wa marehemu Abel Bulugu Kaheza yakiendelea leo Tinde.




Ibada wakati wa mazishi ya marehemu Abel Bulugu Kaheza ikiendelea.




Ndugu wakiweka mchanga katika kaburi la marehemu Abel Bulugu Kaheza




Ndugu wakiweka mchanga katika kaburi la marehemu Abel Bulugu Kaheza




Ndugu wakiweka mashada ya maua katika kaburi la marehemu Abel Bulugu Kaheza




Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga,Mhe. Abdalah Simba na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga,Mhe. Mabala Mlolwa wakiweka shada la maua katika kaburi la marehemu Abel Bulugu Kaheza




Mkuu wa wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha akiweka shada la maua katika kaburi la Abel Bulugu Kaheza.




Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akiweka shada la maua katika kaburi la Abel Bulugu Kaheza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack.




Mbunge wa Jimbo la Solwa, Mhe. Ahmed Salum akiweka shada la maua katika kaburi la Abel Bulugu Kaheza.




Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Mhe. Hoja Mahiba akiweka shada la maua katika kaburi la Abel Bulugu Kaheza.




Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakiongozwa na mwenyekiti wa halmashauri hiyo Ngasa Mboje wakiweka shada la maua katika kaburi la Abel Bulugu Kaheza.




Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakiweka shada la maua katika kaburi la Abel Bulugu Kaheza.




Mchungaji wa Kanisa la AICT Tinde William Shinyanga akiweka shada la maua katika kaburi la Abel Bulugu Kaheza.


Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

WAZIRI MHAGAMA AFUNGUA WARSHA YA WADAU KUJADILI FURSA ZA BOMBA LA MAFUTA –DODOMA

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, bunge, kazi, vijana, ajira na watu wenye ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku moja ya majadiliano ya wadau kuhusu ushiriki wa Watanzania katika miradi ya kimkakati (Local content) katika sekta ya uziduaji mkoani Dodoma iliyofanyika tarehe 26 Agosti, 2019.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, bunge, kazi, vijana, ajira na watu wenye ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akisalimiana na mmoja wa washiriki wa warsha hiyo Bi. Mariagorete Charles mara baada ya ufunguzi wa warsha hiyo Agosti 26, 2019.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia sera, bunge, kazi, vijana, ajira na watu wenye ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Bilinith Mahenge mara baada ya kufungua warsha ya majadiliano ya wadau kuhusu ushiriki wa Watanzania katika miradi ya kimkakati (Local content) katika sekta ya uziduaji mkoani Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Bilinith Mahenge pamoja na sehemu ya washiriki wa warsha hiyo wakifuatilia mada kutoka kwa mwezeshaji Bi. Mariagorete Charles kutoka katika mradi wa EACOP (hayupo pichani) wakati wa warsha hiyo.
Sehemu ya washiriki wa warsha hiyo wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, bunge, kazi, vijana, ajira na watu wenye ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipokuwa akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo.
Mwasilishaji wa mada kuhusu mradi ya bomba la mafuta – EACOP Bi. Mariagorete Charles akiwasilisha mada wakati wa warsha hiyo kwa washiriki wa warsha iliyofanyika Agosti 26, 2019 Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia sera, bunge, kazi, vijana, ajira na watu wenye ulemavu Mhe.Jenista Mhagama  akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Bilinith Mahenge

*****************

NA.MWANDISHI WETU

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama amefungua warsha ya siku moja ya majadiliano ya wadau kuhusu ushiriki wa Watanzania (Local content) katika sekta ya uziduaji mkoani Dodoma.

Warsha hiyo imewakutanisha pamoja wawakilishi zaidi ya 100 wa makundi mbalimbali kutoka Wilaya zote za Mkoa wa Dodoma ili kujadili mikakati na maendeleo ya utekelezaji wa dhana ya ushiriki wa Watanzania katika fursa za miradi ya kimkakati ikiwemo mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Hoima nchini Uganda kwenda Tanga, Tanzania na sekta ya madini kwa ujumla.

Akizungumza wakati wa kufungua warsha hiyo leo Agosti 26, 2019 katika ukumbi wa Kilimanjaro Hazina Mjini Dodoma Waziri Mhagama aliwataka viongozi wa maeneo ambako bomba litapita wawahamasishe wananchi kuchangamkia fursa zitakazokuwepo katika utekelezaji wa mradi huo na kujiletea maendeleo.

“Ni wakati sahihi sasa kuitumia fursa hii ya miradi mikubwa ambayo inalenga kunufaisha wananchi kwa kuzingatia kuwa ajira zitazalishwa kwa wazawa hivyo mjiandaae kikamilifu katika kuupokea mradi huu,” alieleza Mhagama.

Waziri Mhagama aliongezea kuwa, Sheria ya Mafuta imeweka wazi kwamba watanzania na kampuni za kitanzania zinatakiwa zipewe kipaumbele wakati wa ununuzi. Serikali inaamini kwamba Sekta binafsi ina mchango mkubwa katika kuinua uchumi wa nchi. Hivyo ni matarajio kwamba Mkandarasi wa mradi atazingatia matakwa ya Sheria hii na pale ambapo kampuni za kitanzania hazina uwezo basi ziingie ubia na kampuni za nje ili kuongeza ujuzi wa uzalishaji na utoaji wa huduma.

Alifafanua kuwa, kwa kuzingatia dhamira ya Serikali ya awamu ya Tano kuona Watanzania wanamiliki uchumi wao, hivyo wataendelea kuwahamasisha watanzania kushiriki katika miradi Mikubwa ya kimkakati na katika miradi mbalimbali.

“Serikali kupitia Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchu Kiuchumi imejipanga kuweka mazingira wezeshi kwa watanzania ikiwa ni pamoja na kutengeneza Sera na Sheria na miongozo inayotoa kipaumbele kwa watanzania kupata fursa za ajira, kushiriki kwa kutoa huduma, uuzaji wa bidhaa na utoaji wa huduma kwenye miradi inayotekelezwa hapa nchini hasa katika sekta ya uziduaji,”alisisitiza Mhagama.

Mradi wa EACOP ni moja kati ya miradi mikubwa ambao una manufaa mengi kwa nchi yetu na kueleza kuwa, bomba hili la mafuta ghafi litakuwa na urefu wa km 1443 kati ya hizo km 296 zitakuwa nchini Uganda na km 1147 zitakuwa Tanzania. Hii ni fursa kubwa kwa watanzania kwa kuwa 80% ya mradi huu utapita Tanzania.

Aidha alibainisha mikoa itakayopitiwa na mradi huo ikiwemo Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Manyara na Tanga na kufafanua kuwa bomba hilo litapita katika wilaya 24, Kata 134 na vijiji zaidi ya 180 na kutoa wito kwa wananchi kujiandaa na kuhakikisha wanaandaa mazingira wezeshi katika kushiriki fursa zitakazotokana na uwepo wa mradi huo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Bilinith Mahenge alipongeza jitihada zinazoendelea katika kuhamasisha na kutoa elimu kwa jamii juu ya ushiriki wa Watanzaia katika fursa ya mradi bomba la mafuta na kuahidi kuzimamia kikamilifu ili kuhakikisha jamii inashiriki kwa uhakika.



“Kipekee ninapongeza juhudi zinazoendelea katika kuhakikisha wananchi wanajikwamua kiuchumi kwa kuzingatia ujio wa miradi hii ya kimkakati nchini hivyo hatuna budi kuendelea kutoa rai kwa Watanzania wote kuchangamkia fursa hizi,”alisema Dkt. Mahenge.

WAZIR WA MAMBO YA NJE PROF. KABUDI ATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA ULIOPO TOKYO NCHINI JAPAN

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akitoa maelekezo kwa Kaimu Balozi wa Tanzania Tokyo,Japan Bw. John Kambona akiwa na Afisa Ubalozi Bi. Edda Magembe. August 26,2019.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwasili katika Ubalozi wa Tanzania uliopo Tokyo,Japan. Katikati ni Kaimu Balozi wa Tanzania Nchini Japan Bw. John Kambona akifuatiwa na Bi. Edda Magembe Afisa Ubalozi. August 26,2019. 

Kaimu Balozi wa Tanzania Nchini Japan Bw. John Kambona (katikati) akitoa ufafanuzi wa jambo kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) mara baada ya kuwasili katika Ubalozi wa Tanzania uliopo Tokyo,Japna anayefuatia ni  Bi. Edda Magembe Afisa Ubalozi. August 26,2019.  
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa anaingia katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania uliopo Tokyo,Japan. August 26,2019.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika moja ya Maktaba ya vitabu iliyopo katika Ubalozi wa Tanzania - Tokyo,Japan. August 26,2019.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akikagua aina  ya vitabu vilivyopo katika Maktaba ya Ubalozi wa Tanzania Nchini Japan. August,26,2019.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika ofisi ya Balozi wa Tanzania Nchini Japan. August 26,2019.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiongoza kikao kazi cha ujumbe wa Tanzania uliopo Yakohama Nchini Japan kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika 2019 (TICAD7 YOKOHAMA 2019). August 26,2019.

Kaimu Balozi wa Tokyo - Japan Bw. John Kambona akiwa anatoa maelezo kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) na baadhi ya ujumbe uliopo Yakohama, Japan kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika 2019 (TICAD7 YOKOHAMA 2019). August 26,2019.

Baadhi ya wajumbe waliopo Yakohama-Japan kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika 2019 (TICAD7 YOKOHAMA 2019) wakiwa katika kikao kazi cha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi(hayupo Pichani). August 26,2019.



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi amewasili jijini Yokohama, Japan tarehe 26 Agosti kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 7 wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika (Tokyo International Conference on African Development-TICAD 7) utakaofanyika kuanzia tarehe 28 hadi 30 Agosti 2019.


Mkutano huu wa Saba utatanguliwa na kikao cha Maafisa Waandamizi wakiwemo Makatibu Wakuu na Mabalozi tarehe 25 na 26 Agosti 2019 ukifuatiwa na kikao cha Mawaziri tarehe 27 Agosti, 2019 na utahitimiswa na Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali tarehe 28 hadi 30 Agosti 2019. Kauli mbiu ya Mkutano huu ni “Kuendeleza Maendeleo ya Afrika kupitia Watu, Teknolojia na Uvumbuzi”.


Mkutano wa Saba pamoja na mambo mengine unatoa fursa ya kupanga mikakati ya ushirikiano na agenda za kimaendeleo zitakazotelezwa kati ya Japan na Afrika kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo kuanzia mwaka 2019 hadi 2021.


Agenda za mkutano wa mwaka huu zinalenga kujadili mageuzi ya kiuchumi na kuboresha mazingira ya uwekezaji kwa kukuza sekta na uvumbuzi. Pia kuimarisha usalama na ustahimilivu endelevu kwenye jamii pamoja na kuendeleza jitihada za kuimarisha amani na usalama barani Afrika. Agenda za Mkutano wa Saba zinaenda sambamba na agenda 2063 ya Umoja wa Afrika, Agenda 2030 ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa na maazimio mengine ya kimataifa kama Mkataba wa Paris kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa.


Kutokana na mchango wa sekta binafsi katika maendeleo ya kiuchumi barani Afrika, Mkutano wa TICAD 7 umeandaa ratiba maalum itakayozishirikisha taasisi binafsi na za umma kwenye majadiliano ya kibiashara yatakayofanyika tarehe 29 Agosti 2019. Lengo la majadiliano hayo ni kuwaleta pamoja wadau mbalimbali wakiwemo Viongozi wa Serikali wamiliki wa Kampuni, wafanyabiashara na wawekezaji ili kujadili kwa pamoja masuala mbalimbali ya kukuza baishara, uwekezaji na utalii kati ya Japan na Afrika.


Kadhalika  wakati wa mkutano wa saba nchi zote za Afrika zimepatiwa nafasi ya kushiriki katika shughuli mbalimbali kwa lengo la kutangaza fursa za biashara, uwekezaji na vivutio vya utalii za nchi husika. Tanzania kupitia Bodi ya Utalii (TTB) imejipanga kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini wakati wa mkutano huo.


Mkutano wa Saba wa TICAD utahitimishwa kwa Wakuu wa Nchi kupitisha Azimio la Yokohama na Mpango Kazi wa utekelezaji wa Azimio hilo. Serikali ya Japan ilianzisha jukwaa la majadiliano kati yake na nchi za Afrika mwaka 1993 kwa ajili ya kujadili maendeleo na nchi hizo.


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungao wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa ataongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano huo akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.



Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Yokohama, Japan.

26 Agosti 2019


Serikali kukarabati Shule kongwe ya Galanos, Milioni 696 zatengwa

$
0
0
Serikali imetoa zaidi ya shilingi milioni 696 kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya shule kongwe ya sekondari Galanos iliyopo mkoani Tanga.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknlolojia William Ole Nasha alipotembelea shule hiyo kukagua maendeleo ya ukarabati wa miundombinu ambapo amesema fedha hizo zimetolewa kupitia mradi wa Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R) katika mpango unaolenga kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia katika shule hiyo kongwe.

Ole Nasha amesema fedha hizo ni sehemu ya fedha zilizopelekwa katika shule kongwe nchini ambazo zinafanyiwa ukarabati mkubwa lengo likiwa ni kuzirudisha katika hadhi yake ya awali ili ziwe na mazingira mazuri yanayomwezesha mwanafunzi kujifunza na kufaulu vizuri

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri huyo amemtaka Mkurugenzi wa Jiji la Tanga, Daudi Mayeji kufuatilia kwa karibu sababu zilizopelekea kukiukwa kwa masharti ya mkataba wa muongozo wa ukadiriaji majenzi (BOQ) ambao ulielekeza kuwekwa chuma katika varanda za madarasa zinazoruhusu hewa na badala yake yamewekwa matofali ya kuchoma.

“Galanos tumeleta fedha zaidi ya shilingi milioni 696 kwa ajali ya kukarabati miundombinu, baada ya kukagua maendeleo ya ukarabati nimegundua kuna mapungufu makubwa ya kimakusudi, Mfano kwenye madarasa kulitakiwa kuwekwe chuma lakini badala ya kuweka chuma wameweka matofali ya kuchoma bila hata kufuata taratibu wa kufanya mabadiliko” amesema Ole Nasha.

Amesema inashangaza kwani Mhandisi alishiriki katika uandaaji wa BOQ hiyo na ni mmoja wa walioshauri kuwekwa kwa chuma lakini katika utekelezaji wa BOQ hiyo iliyopitishwa amebadili maelekezo, hata baada ya kamati ya ujenzi kumkatalia na kumtaka kufata BOQ inavyotaka lakini bado aliendelea na utaratibu wa kuweka matofali hayo badala ya chuma.

“Ndio maana nimemwelekeza Mkurugenzi wa Jiji afuatilie kwanini kuna ukiukwaji wa makusudi wa kuacha kufuata BOQ na nimemwelekeza achukue hatua kwa yeyote anayehusika kubadilisha maelekezo ya BOQ” amesisitiza Ole Nasha

Mkurugenzi wa Jiji la Tanga, Daudi Mayeji ameahidi kufatilia suala hilo la uwekwaji wa matofali badala ya chuma na kwamba atachukua hatua kwa wale wote waliohusika katika kubadili maelekezo yaliyopo katika mkataba wa ukadiriaji majenzi (BOQ).
Mabweni ya Shule ya Sekondari Galanos ambayo yapo kwenye ukarabati

 Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe William Ole Nasha akikagua mabweni ya Shule ya Sekondari Galanos iliyopo jijini Tanga wakati alipofanya ziara yake

BENKI ZA BIASHARA NCHINI ZASHAURIWA KUANZISHA HUDUMA YA UHIFADHI WA DHAMANA NA USIMAMIZI WA UWEKEZAJI KATIKA MASOKO YA MITAJ, OFISA MTENDAJI MKUU CMSA ATOA PONGEZA BENKI YA I&M

$
0
0




Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Nicodemus Mukama, akibonyeza kitufe wakati wa uzinduzi wa Huduma ya Usimamizi wa Dhamana na Uwekezaji ya Benki ya I&M  jijini Dar es Salaam Agosti 26.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya I&M  Baseer Mohammed (kulia) akiteta jambo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Nicodemus Mukama.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya I&M , Baseer Mohammed (kulia) akiteta jambo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Nicodemus Mukama.

Mkuu wa Idara ya Wateja wa RejaReja Benki ya I&M  Lilian Mtali.

Meza Kuu.

Baadhi ya maofisa wa Benki ya I&M

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya I&MBank , Baseer Mohammed, akizungumza katika uzinduzi wa Huduma ya Usimamizi wa Dhamana na Uwekezaji.

Baadhi ya wageni waalikwa.

Meneja Msaidizi wa Huduma ya Usimamizi wa Dhamana na Uwekezaji Benki ya I&M , Frank Bunuma, akizungumza kuhusu Huduma ya Usimamizi wa Dhamana na Uwekezaji iliyozinduliwa na benki hiyo.



OFISA Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana(CMSA) Nicodemus Mkama ametoa mwito kwa benki za biashara kuanzisha huduma ya Uhifadhi wa Dhamana na Usimamizi wa Uwekezaji katika masoko ya mitaji kwani hatua hiyo ni muhimu na itazisaidia benki hizo kuongeza idadi ya wawekezaji na hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi yetu.

Aidha amezishauri benki zote hapa nchini kutumia fursa zilizopo katika sekta ya masoko ya mitaji ikiwemo kuuza dhamana kwa umma na hatimaye kuorodheshwa katika soko la hisa la Dar es Salaam ili kuongeza mitaji yao.

Mkama amesema hayo leo Agosti 26 jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma ya uhifadhi wa dhamana na usimamizi wa uwekezaji wa Benki ya I&M ambapo ametumia nafasi hiyo kueleza hiyo ni uthibitisho sekta ya fedha ina wadau wengi wanaounga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano.

Amesema hatua hiyo itasaidia utekelezaji wa agizo la Serikali kwa benki zote za biashara pamoja na benki za wananchi kutimiza matakwa ya kisheria ya kuwa na mtaji wa kutosha ili kuweza kujiendesha kibiashara. Aidha,ametoa mwito kwa kampuni za bima kutumia fursa zilizopo katika sekta ya masoko ya mitaji ili kuongeza mitaji yao.

Amesisitiza hiyo itaziwezesha kampuni za bima hapa nchini kuwa na uwezo wa kushindana na kampuni za nje zinazotoa huduma ya bima (underwriting risks) hapa nchini. Vile vile, natoa wito kwa mifuko ya hifadhi ya jamii na taasisi za fedha kuunga mkono malengo na azma ya Serikali ya kujenga uchumi wa Viwanda kupitia masoko ya mitaji nchini.

Akizungumzia Benki ya I&M,Mkama amesema kuwa benki hiyo amesema imefanikiwa kupata leseni kutoka kwa Mamlaka hiyo ya kutoa huduma ya uhifadhi wa dhamana na usimamizi wa uwekezaji kwa mujibu wa kanuni za masoko ya mitaji na dhamana za mwaka 2006.

Amesema kuwa hiyo ni hatua muhimu katika maendeleo ya masoko ya mitaji nchini, kwani benki ya I&M inakuwa ni benki ya saba kati ya benki za bishara 40 zinazofanya shughuli zake hapa nchini, kupata idhini ya kutoa huduma ya Uhifadhi wa Dhamana na Usimamizi wa Uwekezaji katika masoko ya mitaji na dhamana hapa nchini.

Ametumia nafasi hiyo kutumia fursa hiyo kuipongeza bodi ya wakurugenzi na uongozi wa Benki ya I&M pamoja na taasisi na wadau wote waliohusika katika kufanikisha hatua hiyo muhimu na kwamba masoko ya mitaji ni sehemu muhimu katika sekta ya fedha nchini. Sekta hii inasaidia upatikanaji wa mitaji ya muda mrefu kwa ajili ya kugharamia shughuli za maendeleo.

Amefafanua masoko ya mitaji hujumuisha uuzaji wa hisa za kampuni (shares), hatifungani za kampuni (Corporate Bonds), hatifungani za Serikali Kuu (Government Bonds), hatifungani za Serikali za Mitaa (Municipal Bonds), na vipande katika Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja (Collective Investment Schemes).

Mkama amesema hivyo masoko ya mitaji husaidia pia kurekebisha kiwango cha ukwasi na mfumuko wa bei katika uchumi. Aidha, sheria na taratibu za masoko ya mitaji zinazitaka kampuni zilizopo katika masoko ya mitaji kujiendesha kwa uwazi wa hali ya juu na kwa kufuata kanuni za utawala bora. Matokeo ya masharti haya ni kwamba mara nyingi kampuni hizo hufanya kazi kwa ufanisi na kwa kuwa taarifa zao za fedha ziko wazi ni rahisi kwa serikali kukusanya kodi stahiki.

Amesema huduma ya uhifadhi wa dhamana na usimamizi wa uwekezaji ni huduma inayotolewa na benki za biashara na ili kutoa huduma hii ni lazima kupata leseni kutoka Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) na kwamba wanaopata leseni hiyo hutoa huduma hiyo kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

Pia amesema Uhifadhi wa Dhamana na Usimamizi wa Uwekezaji hutoa huduma za utunzaji wa dhamana: akaunti za dhamana za wawekezaji huifadhiwa na kusimamiwa kwa umakini na benki za biashara (custodians) ikiwa ni pamoja na kukusanya taarifa za siku kwa siku kuhusu thamani halisi ya dhamana hizo.

Mkama ametaja nyingine ni utunzaji wa mapato ambapoo wawekezaji hupatiwa taarifa kuhusu faida za uwekezaji wao ikiwa ni pamoja na kuwekewa gawio au riba kwenye akaunti zao pale uwekezaji wao unapokuwa umepata faida. Ukamilishaji wa miamala ya dhamana kwa kuhakikisha miamala ya dhamana inakamilika vizuri, kwa uhakika na kwa wakati kulingana na maelekezo ya mwekezaji na matakwa ya sharia, kanuni na taratibu zote.

Pia Utoaji wa taarifa kwa maana ya kutengeneza taarifa mbalimbali kuhusu uwekezaji husika kama vile muhtasari, salio la akaunti na taarifa za siku. Pia kutengeneza taarifa atakazohitaji mwekezaji kuhusu uwekezaji wake na utunzaji wa fedha ili kuwezesha uwekezaji zaidi, utunzaji wa fedha ni muhimu. Utunzaji wa fedha unahusisha kuwa na taarifa moja ya fedha kutokana na vyanzo vyote vya mwekezaji, kusaidia uamuzi wa uwekezaji na dhamana husika, kufanya uwekezaji, kuratibu fedha kutokana na uwekezaji na kuratibu mtiririko wa fedha

“Kwa huduma hii wawekezaji huwakilishwa katika mikutano mikuu ya mwaka ya kampuni walizowekeza dhamana zao, na hivyo kupata fursa ya kushiriki katika maamuzi yote ya kampuni hizo. Kwa ujumla, huduma hii ni muhimu kwani inarahisisha uwekezaji katika masoko ya mitaji na hivyo kuchangia kupanuka kwa uwekezaji unaoleta ongezeko la ajira.

“Aidha huduma hii inachangia kuongezeka kwa idadi ya wawekezaji wa kigeni na hivyo kuchangia kuongezeka kwa akiba hapa nchini; kuongezeka kwa mapato kwa njia ya kodi kwa Serikali; na kuinua kipato cha watanzania kwa ujumla. Ni matumaini yangu kuwa, ninyi mliohudhuria hafla hii, na hasa waandishi wa habari mtaendelea kushirikiana na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) katika kutoa elimu kwa umma kuhusu huduma ya Uhifadhi wa Dhamana na Usimamizi wa Uwekezaji”,

Amesema kuwa kadiri Taifa letu linavyosonga mbele katika utekelezaji wa Sera ya Uchumi wa Viwanda, mahitaji ya fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo hususani miundombinu yanaongezeka. Serikali na kampuni binafsi zinaweza kujipatia fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo kwa njia ya kuuza hisa, hatifungani na bidhaa zingine za masoko ya mitaji. Ili kufanikisha azma hiyo kunahitajika kuwepo kwa benki nyingi za biashara zinazotoa huduma ya Uhifadhi wa Dhamana na Usimamizi wa Uwekezaji.

Amoengeza hatua hiyo ni muhimu kwani inachangia kuongezeka kwa uwekezaji na hivyo kuchochea ukuaji wa Uchumi wa Viwanda hapa nchini. Hivyo anao ujasiri wa kueleza benki ya I&M imekuja katika wakati muafaka. Pia leseni hiyo ya benki ya I&M kwa ajili ya kutoa huduma ya Uhifadhi wa Dhamana na Usimamizi wa Uwekezaji ni mojawapo wa kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli katika kuifanya Tanzania ya viwanda na uchumi wa kati. Benki I&M Hongereni Sana.

Pia amesema huduma ya uhifadhi wa dhamana na usimamizi wa uwekezaji inawezesha na kurahisisha biashara kwa wawekezaji wa kigeni katika soko la hisa. Itakumbukwa kwamba katika mwaka wa fedha 2014/1015, Kanuni za Masoko ya Mitaji na Dhamana (Wawekezaji wa Kigeni) za 2003 zilirekebishwa ili kuruhusu ushiriki wa bila kikomo wa wawekezaji wa kigeni katika soko la hisa.

Hivyo watoa huduma ya Uhifadhi wa Dhamana na Usimamizi wa Uwekezaji ndio wanaoweza kuingia mikataba na wageni kwa ajili ya kutoa huduma hiyo. Kwa sababu hiyo, inatarajiwa kuwa kuongezeka kwa huduma hiyo kutaongeza biashara katika soko la hisa inayohusisha wawekezaji wa nje ya nchi.

Pia amesema benki ya I&M ina uhusiano mzuri na benki washirika katika nchi mbalimbali kama vile Kenya ambao wanatoa huduma kama hii. Pia inao uzoefu wa zaidi ya miaka kumi katika masoko ya mitaji na hivyo kutawezesha wawekezaji wa Afrika ya Mashariki na kwingineko kuweza kuingia Tanzania kirahisi.

JAJI MKUU ATAKA VIPIMO VYA DNA KUTUMIKA KATIKA KESI

$
0
0
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.Prof.Ibrahim Hamis Juma,akikagua ujenzi wa jengo la mahakama ya mwanzo Makete wilayani Makete,akiwa katika ziara ya kikazi kwenye mikoa ya Njombe na Iringa
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.Prof.Ibrahim Hamis Juma akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Njombe mara baada ya kuwasili mkoani humo kuanza ziara ya Kikazi.
………………

Na Lydia Churi- Mahakama Njombe 

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma leo ameanza ziara ya kikazi katika mikoa ya Iringa na Njombe na kutaka kuwepo kwa matumizi ya vipimo vya vinasaba (DNA) katika kesi za mauaji, ubakaji na unajisi kwa watoto ili kurahisisha uendeshaji wa kesi hizo na kusaidia haki kupatikana kwa wakati.

Akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka alipomtembelea ofisini kwake, Jaji Mkuu amesema matumizi ya vipimo vya DNA katika kesi yatasaidia haki kupatikana ambapo aliyetenda kosa atatiwa hatiani na asiyetenda kosa ataachiwa mapema.

“Kipimo cha DNA husaidia kuthibitisha kosa lililofanyika lakini bahati mbaya, kwa uzoefu wetu hatuoni matumizi ya kipimo hicho”, alisema Jaji Mkuu.

Alisema kutokutumika kwa kipimo cha DNA Mahakamani, mshtakiwa huweza kuachiwa huru kutokana na kukosekana kwa ushahidi. 

“Eneo hili tumeona huweza kusababisha mtuhumiwa kuachiwa huru kwa sababu sisi tunaangallia zaidi ushahidi” alisisitiza Jaji Mkuu.

Alisema wakati mwingine Jaji au Hakimu huweza kuona wazi kuwa mshtakiwa alistahili kutiwa hatiani lakini ushahidi unapokosa uzito mtuhumiwa huachiwa huru.

Akifafanua, Jaji Mkuu Alisema kesi kama hizi huchukua muda mrefu na kusababisha wakati mwingine ushahidi muhimu kufifia kiasi kwamba kesi inapofika mahakamani lile joto la ushahidi lililoonekana wakati wa tukio huweza kupotea.

Alisema kutokana na kukua kwa sayansi na Teknolojia hivi sasa hatua kubwa imefikiwa katika matumizi ya kipimo cha DNA na kurahisisha sana. Akitolea mfano wa kesi ya ubakaji au unajisi kwa watoto wadogo alisema badala ya kumuhoji mtoto mdogo mahakamani, kipimo hiki huweza kutumika ili kuthibitisha kosa lililofanyika.

Alisema Serikali kwa kushirikiana na Mahakama hawana budi kuifanyia kazi changamoto hii ili kila raia anayetenda kosa atiwe hatiani na asiye na kosa aachiwe huru mapema hata katika hatua ya upelelezi wa kesi husika. 

Wakati huo huo, Jaji Mkuu alisema suala la ujazaji wa fomu za taarifa ya Daktari yaani PF 3 halizingatiwi kwa kuwa fomu hizo hazijazwi kwa ufasaha na hivyo huweza kusababisha mtuhumiwa kuachiwa huru wakati mwingine. 

“Fomu hii inayo maeneo muhimu ya kujazwa na hasa yanayohitaji vipimo na endapo itajazwa kwa ufasaha itasaidia sana katika kuhakikisha mtu anayetenda kosa anatiwa hatiani”, alisema. 

Kuhusu kesi za Mirathi, Jaji Mkuu alisema eneo hili lina changamoto kwa kuwa kesi hizi pia huchukua muda mrefu zaidi hivyo elimu haina budi kutolewa hasa kwa wananchi wanaoishi maeneo ya vijijini. Alisema wananchi wanatakiwa kufahamu kuwa kila mtu anapaswa kujitahidi kutafuta chake badala ya kutegemea cha marehemu.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Njombe alimpongeza Jaji Mkuu wa Tanzania kwa kujitoa kwake katika kuhakikisha Mahakama inatoa mchango mkubwa kwenye maendeleo ya nchi na pia alimpongeza kwa kuendeleza ushirikiano na Mihimili ya Serikali na Bunge.

Aidha, Mhe. Ole Sendeka ameahidi kushirikiana kwa karibu zaidi na Mahakama ya Tanzania inapotekeleza majukumu yake ya msingi ya utoaji wa haki kwa wakati. 

Katika ziara iliyoanza leo, Jaji Mkuu ametembelea Mahakama ya wilaya ya Makete na kuzungumza na watumishi wa Mahakama hiyo lakini pia alipata nafasi ya kukagua ujenzi wa jengo la Mahakama ya Mwanzo Makete.

SERIKALI YAWAOMBA WADAU WA USAFIRI MIKOA YA KASKAZINI KUTOA MAONI YAO ILI KUIBORESHA RASIMU MPYA YA HUDUMA YA USAFIRI NCHINI

$
0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Tv ,Arusha

SERIKALI imewaomba wadau wa huduma ya usafirishaji mikoa ya Kanda ya Kaskazini ya Arusha,Kilimanjaro na Manyara kutoa maoni yao kwa ajili ya maboresho ya rasimu mpya ya huduma za usafirishaji nchini ili kuboresha kanuni za usafirishaji na yatafanyiwa kazi.

Rai hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Hagnes Chitukulo, alipokuwa akifungua kikao cha siku moja cha kujadili rasimu mpya ya kuboresha huduma ya usafiri iliyowasilishwa na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi kinachoshirikisha wadau wa huduma ya usafiri ambao ni wamiliki wa mabasi, daladala, malori ,madereva, makondakta, bajaji ,taxi.

Chitukulo, amesema Serikali inatayaka kutunga sheria mpya ya huduma za usafiri, hivyo imeaandaa rasimu na kuipeleka kwa wadau ili watoe maoni ya kuiboresha na waweze kuboresha huduma za usafiri nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma ya uchukuzi, Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Haron Kisaka amesema rasimu hiyo mpya inalenga kuboresha huduma ya vyombo vya usafiri .

Amesema Wizara imetoa kanuni mpya za huduma ya usafirishaji na sasa rasmu hiyo inapelekwa kwa wadau ili waweze kuitolea maoni ili baadae itengenezwe sheria za usafiri wa ardhini ,ambazo sasa zitasimamiwa na LATRA.

Amesema Serikali imeanzisha mamlaka ya kusimamia huduma za usafiri wa ardhini ambayo ni LATRA inayochukua nafasi ya Sumatra ,ambayo ilikuwa inadhibiti huduma za usafiri wa barabara, leri na anga

Amesema kulingana na mabadiliko hayo wamiliki wa mabasi kuanzia sasa watakuwa wakitumia mfumo wa Kielektoroniki kutoa tiketi za mabasi na lengo ni kuboresha huduma na kuondoa wapiga debe kwenye vituo vya mabasi ambao wamekuwa ni kero.

Kisaka amesema kuwa tayari yapo baadhi ya mabasi yameshaanza kutumia mfumo wa kutoa tiketi za abiria za kielektroniki na mfumo huo ni mzuri .

Kisaka, amesema sheria mpya namba 3/2019 inayodhibiti vyombo vyote vya usafiri nchini inawashirikisha, wamilikio, madereva,makondakta, magari ya kukodi yaani Taxi,bajaji

Katika hatua nyingine wadau wamegomea kikao hicho na kimemalizika bila maafikiano kutokana na kutokuelewana kati ya wadau na Serikali kutokana na hoja za wadau kutaka kupewa muda zaidi ili wakaisome rasimu hiyo .
Wadau wamedai kuwa wamechelewa kupata nakala za rasimu hiyo hivyo inawawia vigumu kuijadili kwa kuwa hawajaipitia na kuelewa na hivyo kusisitiza wapewe muda zaidi .

Huku upande wa Serikali ukisisitiza kuwa wanatakiwa kutoa maoni kwa kuwa tayari rasimu imeletwa kwao hivyo hawana budi kiuijadili na kuwataka watenganishe changamoto zao na utendaji kwa kuwa serikali itarejesha rasimu hiyo ili waweze kuipitia.

Kisaka, amesisitiza kwamba baadhi ya vyama vya watoa huduma walipokea rasimu hizo muda wa siku nne zilizopita kabla ya kikao hicho kulingana na kumbu kumbu zilizopo hivyo anawashangaa kudai hawajapata nakala hizo .

Mwenyekiti wa AKIBOA,Loken Masawe, akichangia ameomba wadau wa huduma ya usafirishaji kuwapa muda zaidi ili waisome rasimu hiyo wailewe waweze kutoa maoni yao ,na wasilazimishwe kwani hawana ugomvi na serikali .

Kwa upande wake mmiliki wa mabasi ya Mtei,Mwenyekitio wa TABOA Mkoa wa Arusha, Felix Mtei, rasimu ilichelewa kuwafikia wahusika ,wamiliki na madereva walitakiwea kufafanuliwa maeneo yanayowagusa.

Amesema kuwa kwa minajili hiyo wadau tunatakiwa walione suala hilo kwa Hivyo wanahitaji muda zaidi ili wafafanuliwe kisheria kuweza kujadili suala hilo kuweza kutoa maoni yao kuboresha rasimu hiyo kwa uwazi na muda.

SERIKALI YAZINDUA UJENZI WA VIVUKO VIPYA VYA BUGOROLA-UKARA, CHATO-NKOME

$
0
0
SERIKALI imezindua rasmi ujenzi wa vivuko vipya viwili vya kisasa vitakavyotoa huduma ya kusafirisha abiria, mizigo na magari kati ya Bugorola-Ukara Wilaya ya Ukerewe Mkoa wa Mwanza na Chato-Nkome Wilaya ya Chato mkoani Geita.

Uzinduzi wa ujenzi huo umefanyika jana mkoani Mwanza katika eneo la karakana ya Kampuni ya Songoro Marine Transport Boatyard Ltd, inayojenga vivuko hivyo ambapo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe pamoja na taasisi mbali mbali zilizo  chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Mhandisi Japhet Maselle alisema Serikali imeamua kujenga vivuko hivyo kutokana na kuwapo kwa uhitaji mkubwa wa huduma ya vivuko kwa wananchi wa maeneo hayo.
Mhandisi Maselle alisema kivuko cha Bugorola-Ukara kinajengwa na Kampuni ya Songoro Marine Transport Boatyard Ltd kwa gharama ya Tsh bilioni 4.2 na kile cha Chato- Nkome kinagharimu Tsh bilioni 3.1

“Vivuko vyote vinagharimu jumla ya Tsh bilioni 7.3 fedha zinazotolewa na Serikali ya awamu ya tano, chini ya uongozi mahiri wa Jemedari, Rais wetu, Mhe. Dkt. John Joseph Pombe Magufuli, na kwa mujibu wa mikataba tuliyoingia na kampuni hii ni kwamba vivuko hivi vitajengwa kwa miezi 10, hata hivyo namuagiza mzabuni akamilishe ujenzi wa vivuko hivi kwa chini ya muda huo”.

Kivuko cha Bugorola-Ukara kitakuwa na na vipimo vya urefu wa mita 39, upana mita 10 na kitaelea ndani ya maji kati ya mita 0-7 hadi 1.0, pia kitakuwa na uwezo wa kubeba tani 100 yaani abairia 300, magari 10 na mizigo, vile vile kivuko cha Chato-Nkome kitakuwa kitakuwa na vipimo vya urefu wa mita 37, upana mita 10 na kitaelea ndani ya maji kati ya mita 0-7 hadi 1.0, pia kitakuwa na uwezo wa kubeba tani 100 yaani abairia 200, magari 10 na mizigo.

Vivuko hivi vitafungwa injini mbili kila kimoja, HP 350 kwa kivuko cha Bugorola-Ukara na HP 300 kwa kivuko cha Chato-Nkome na vitaendeshwa na mifumo miwili ya usukani ambapo mmoja utakuwa ni wa dharura. Lengo la serikali ni kuimarisha usalama majini na usafiri wa uhakika ndio maana vivuko hivi vinajengwa kwa mabati maalum ya daraja la kwanza ‘grade A marine’ 

Naye Mkurugenzi  Mtendaji wa Kampuni ya Songoro Marine Transport Boatyard  Ltd, Major Songoro aliipongeza Serikali kwa kuiamini kampuni yake na kuipatia zabuni za kujenga vivuko hivyo huku akiahidi kuvikabidhi mapema mwezi Februari badala ya Aprili kama ilivyo kwenye mkataba. 

Kwa upande wa Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Warioba Sanya alisema ujenzi wa vivuko hivyo ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Dk. John Magufuli ya kutaka kuboresha   na kuimarisha usalama wa abiria na vyombo vya majini ndani ya Ziwa Victoria.
“Hapa kinachotekelezwa ni ahadi ya rais wetu na ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), hatutaki yale yalitokea Bugorola yatokee tena, sote tunajua mahitaji yaliyopo pale Bugorola ingawa kuna kivuko cha MV Sabasaba kinafanya kazi pale”.

Aliongeza kuwa Serikali imekusudia kuwawezesha wakandarasi wa ndani ili kusudi kodi za watanzania ziweze kubaki hapa nchini kwa watanzania wenyewe. Mkoa wa Mwanza sasa upo katika mkakati maalumu wa kuwa kituo cha uchumi katika nchi za Afrika Mashariki, ndio maana tunataka kampuni hii iwezeshwe na kuwa mahiri ili iweze kujenga meli kubwa hapa hapa jijini Mwanza. Hivyo nawaagiza viongozi wa kampuni hii kujenga vivuko hivi kwa ufanisi na kasi kubwa.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Eng. Japhet Maselle (wa tatu kushoto) akimuongoza Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng. Warioba Sanya (katikati), kwenda kuzindua ujenzi wa vivuko viwili vipya vya Bugorola-Ukara Wilaya ya Ukerewe na Chato nkome Wilaya ya Chato. Uzinduzi huo ulifanyika jana katika karakana ya Songoro Marine Boartyard Ltd iliyoko Ilemela, jijini Mwanza.
 Eng. Warioba Sanya kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akizindua ujenzi wa kivuko kipya cha Chato-Nkome (wilaya ya Chato) kinachojengwa na Kampuni ya Songoro Marine Boatyard Ltd ya jijini Mwanza, kwa gharama ya Tshs Bilioni 3.1 fedha inayotolewa na Serikali ya Tanzania. Kivuko hicho kitakuwa na uwezo wa kubeba tani 100 yaani abiria 200, magari 10 na mizigo. Ujenzi wa kivuko hiki utakamilika ndani ya Wiki 40.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Eng. Japhet Maselle (kushoto) akimpongeza Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng. Warioba Sanya (kulia) baada ya kukamilisha uzinduzi wa ujenzi wa vivuko vipya viwili kwa ajili ya maeneo ya Chato-Nkome (Chato) na Bugorora-Ukara (Wilaya ya Ukara) Mkoa wa Mwanza. Uzinduzi huo ulifanyika jana katika karakana ya Songoro Marine Boatyard Ltd, Ilemela jijini Mwanza. 


Wachezaji 40 waitwa Kambini Timu ya Taifa ya Wanawake Twiga Stars

$
0
0
Kocha wa Timu ya Taifa ya Wanawake Bakari Shime ametaja Kikosi cha Wachezaji 40 watakaoingia Kambini kujiandaa na mashindano mbalimbali.

Kambi itaanza rasmi Agosti 30,2019 mpaka Septemba 21,2019.

Wachezaji walioitwa

Najat Abas (JKT)
Tausi Abdallah (Mlandizi)
Zubeda Mgunda (Simba)
Stumai Abdallah (JKT)
Wema Richard (Mlandizi)
Enekia Kasonga (Alliance)
Vailet Thadeo (Simba)
Fatuma Issa (Evergreen)
Vailet Singano (Simba)
Happy Hezron (JKT)
Janeth Christopher (Mlandizi)
Eva Wailes (Ruvuma)
Amina Ally (Simba)
Diana Lucas (Ruvuma)
Asha Hamza (Kigoma)
Pheromena Daniel (Mlandizi)
Opa Clement (Simba)
Herieth Shija (Mash Academy)
Donisia Minja (JKT)
Joyce Fredy (Tanzanite)
Janeth Shija (Simba)
Masha Omari (Panama)
Ester Mabanza (Alliance)
Anastazia Nyandago (Panama)
Rahabu Joshua (Alliance)
Dotto Tossy (Simba)
Neema Charles (Panama)
Lucia Mrema (Panama)
Wande Mahona (Tabora)
Fumukazi Ally (JKT)
Emeliana Mdimu (Makongo Sec)
Protasia Mbunda (Ruvuma)
Irene Kisisa (Kigoma)
Shamimu Ally (Ruvuma)
Joyce Meshack (Makongo Sec)
Thadea Hamdani (Yanga)
Rukia Hussein (Tanzanite)
Aisha Masaka (Alliance)
Agnes Palangyo (Tanzanite)
Angel Joseph (Arusha)

Viongozi wa Vijiji na Halmashauri watakiwa kutenga fedha za kuunganisha umeme

$
0
0
Na Hafsa Omar, Rukwa
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amewaagiza viongozi wa Serikali za Vijiji na Halmashauri kote nchini, kutenga  fedha kwa ajili ya kulipia gharama za kuunganisha umeme kwenye  Taasisi za Umma na hivyo kuboresha huduma za kijamii katika maeneo yao.

Alitoa agizo hilo Agosti 26, 2019, akiwa katika Kijiji cha Mkinga na Mkomolo wilayani Nkasi Mkoa wa Rukwa wakati  akizungumza na wananchi wa vijiji hivyo kabla ya kuwasha umeme kwenye Vijiji husika.

 Dkt Kalemani aliwaambia viongozi hao  kuwa,  umeme unapofika kwenye maeneo yao, umekuwa ukisambazwa  kwenye nyumba za wananchi na wanazisahau taasisi za umma hivyo ni muhimu kwa Taasisi hizo kupewa kipaumbele..

“Niwaombe viongozi wa Serikali za Vijiji, Mwenyekiti wa Halmashauri na Mkurugenzi mtenge fedha kwa ajili ya kuunganisha umeme kwenye taasisi za umma, kama umeme upo jambo la kwanza kwenye vijiji ni kuunganisha umeme kwenye Zahanati au Shule.” Alisema Dkt Kalemani.

Aidha, Dkt Kalemani aliwaagiza wakandarasi wa umeme vijijini, kuajiri vibarua wengi ili kazi ya usambazaji umeme ifanyike kwa kasi na wananchi pamoja na taasisi mbali mbali za umma zipate umeme wa uhakika na  kwa haraka.

Alitoa msisitizo kuhusu kuajiri vijana kutoka maeneo ambayo kazi za usambazaji umeme zinafanyika ili kutoa ajira kwa wakazi wa maeneo hayo ya vijijini, “nimeshapiga marufuku vibarua wa kutoka maeneo ya mbali, kazi za hapa zifanywe na vibarua kutoka eneo hili, Mwenyekiti wa kijiji simamia hili.” Alisema Dkt Kalemani.

Vile vile, Dkt Kalemani aliwahamasisha wananchi wa vijiji hivyo kujenga viwanda vya kukoboa na kusaga nafaka ili kuboresha maisha yao na kutunza miundombinu ya umeme ili wanufaike na nishati hiyo ambayo itakuwa ni mkombozi wa maisha yao, “mtunze miundombinu ya umeme msikate nyaya, msichome moto nguzo, wala msiibe transfora.”alisisitiza.

 Pia, Dkt. Kalemani alitoa agizo kwa TANESCO kudhibiti suala la uwepo wa vishoka kwa  kubandika katika ofisi za Tanesco, majina ya wakandarasi wote wenye vigezo vya kufanya kazi za wiring kwenye makazi ya wananchi.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kufika katika Kijiji cha Mkinga wilayani Nkasi ili kukagua kazi ya usambazaji umeme na kuwasha rasmi umeme kwenye Kijiji hicho.
 Baadhi ya wananchi katika Kijiji cha Mkomolo wilayani Nkasi, wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani mara baada ya kufika Kijijini hapo ili kukagua kazi ya usambazaji umeme na kuwasha rasmi umeme kwenye Kijiji hicho.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa pili kushoto) akifurahi mara baada ya kukata utepe, kuashiria uwashaji rasmi umeme  katika Kijiji cha Mkinga wilayani Nkasi. Wa Pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Said Mtanda.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akizungumza na wananchi  katika Kijiji cha Mkinga wilayani Nkasi baada ya kufika kijijini hapo kukagua kazi ya usambazaji umeme na kuwasha rasmi umeme kwenye Kijiji hicho.

FILAMU ZILIZOINGIA SOKONI BILA KIBALI ZAINGIA MATATANI

$
0
0
Kaimu Katibu Mkuu wa bodi ya Filamu Tanzania, Dkt. Kiagho Kilonzo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo na kutoa onyo kwa wasambazaji pamoja na wazalishaji wa filam nchini kwenda kusajili katika bodi ya filam hapa nchini. Kushoto ni Afisa Utamaduni wa bodi ya filamu nchini, Clerence cheles.
Kaimu Katibu Mkuu wa bodi ya Filam Tanzania, Dkt. Kiagho Kilonzo akionesha waandishi wa habari  filamu ambazo zimekamatwa mtaani kwa kutokusajiliwa katika bodi ya filam nchini na kutoa onyo kwa wasambazaji pamoja na wazalishaji wa filam nchini kwenda kusajili katika bodi ya filamuhapa nchini. Kulia ni Mkuu wa Idara ya utawala bodi ya Filamu nchini, Abdallah Amanzi.
Kaimu Katibu Mkuu wa bodi ya Filam Tanzania, Dkt. Kiagho Kilonzo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo na kutoa onyo kwa wasambazaji pamoja na wazalishaji wa filam nchini kwenda kusajili katika bodi ya filam hapa nchini.Kushoto ni Afisa Utamaduni wa bodi ya filamu nchini, Clerence cheles.

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
FILAMU kumi zimekamatwa zikiwa sokoni huku zikiwa hazijapitia hatua mbalimbali zikiwemo ukaguzi wa miswada ya filamu hizo pamoja na uhakiki wa filamu hizo baada ya kutengenezwa na kutokuwa na daraja maalumu linaoonesha rika husika la kuangalia filamu hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kaimu katibu mkuu wa bodi ya filamu nchini Dkt. Kiagi Kilonzo amesema kuwa filamu hizo zimekamatwa zikiuzwa kinyume na taratibu.

"Ili filamu iingie sokoni lazima zipitie hatua mbalimbali, ikiwemo kuleta muswada katika bodi ya filamu ili uweze kupitiwa, uhakiki baada ya kutengenezwa kwa filamu husika ili iweze kupangiwa daraja maalumu la rika la kuangalia kutokana na maudhui ya filamu husika" ameeleza Dkt. Kilonzo.

Amesema kuwa baada ya filamu hizo kukamatwa wahusika wameitwa kwa maridhiano zaidi huku akieleza kuwa kuna filamu nyingi zinazouzwa kinyemela na hatua za kisheria zitachukuliwa kwa watakaokiuka ikiwemo kulipa faini na kifungo. 

"Kifungu cha 20 cha kanuni inayosimamia masuala ya filamu inafafanua kuwa mtu yeyote anayetengeneza picha jongefu nchini kwa maonesho ya hadhara lazima akabidhi kwa bodi ya filamu hiyo ili iweze kupitiwa na kupangiwa daraja na yeyote atakayekiuka sheria na kanuni zilizopangwa atapambana na mkono wa sheria ambapo mzalishaji, msambazaji na muuzaji atakayekwenda na  kinyume cha sheria atatakiwa kulipa faini ya shilingi milioni moja kwa kila kosa na akikaidi atapelekwa mahakamani ambako akishindwa kesi atalipa faini ya shilingi milioni tano, au kifungo cha miaka mitano au vyote kwa pamoja" ameeleza.

Vilevile amesema kuwa mafunzo na elimu yanaendelea kutolewa kwa wauzaji, wasambazaji, wazalishaji na wasanii katika maeneo mbalimbali ili waweze kufanya kazi zao kwa kuzingatia sheria zilizowekwa.

Filamu zilizokamatwa katika msako huo Ni pamoja na Mbwiga, Unaibiwa, Mwanaume wa Dar, Chumba cha kati, Jadu, Adui, Ndumba, Mama Kisheti,  Tukutane Dar na Sarah Dikonko.

Uboreshaji sekta ya mawasiliano ya simu kuwapa wateja tija

$
0
0
TANZANIA inashuhudia ukuaji mkubwa wa maendeleo ya kiteknolojia ambao unaonekana wazi katika ongezeko la idadi ya watu waliounganishwa na mawasiliano kutumia huduma za intaneti. Kiini cha mabadiliko hayo ni teknolojia ya simu za mkononi, ambayo imewezesha kuwaunganisha watu na kutoa huduma za intaneti kuliko ilivyowahi kuwa hapo awali. 

Ni ukweli pia usiopingika kuwa kampuni za mawasiliano ya simu za mkononi ndizo muhimili mkuu wa mabadiliko na teknolojia hii. Uwekezaji mkubwa unaoendelea katika miundombinu ya mitandao ya simu na huduma ni ushahidi wa ushiriki wao katika kufikia malengo ya maendeleo ya nchi.

Kwa mfano, katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, kampuni moja tu Tigo Tanzania imewekeza takribani shilingi za kitanzania trilioni moja katika kuhakikisha kuwa miundombinu yake inakuwa ya kidijitali na bora zaidi  ikiwa ni njia ya kuboresha huduma zake lakini pia kuhakikisha inachangia harakati za nchi kufikia lengo la kuwa na uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2025.

Tigo Tanzania imejipambanua kuwa inafanya kazi katika kujenga maisha ya kidijitali nchini Tanzania na utendaji kazi wao hadi leo unaonesha nia yao ya dhati kufanikisha hilo. Ikumbukwe kuwa Tigo ni kampuni ya kwanza nchini Tanzania kuzindua teknolojia ya 3G, 4G, na 4G+. Wateja wa Tigo mara zote wamekuwa ndio wa kwanza kutumia mtandao wenye kasi zaidi ambao hutokana na maendeleo na maboresho ya teknolojia.

Licha ya kuanza kwa mabadiliko haya ya kidijitali, wataalamu wametahadharisha uwepo wa changamoto mbalimbali katika sekta ya mawasiliano ya simu za mkononi ambazo zinahatarisha viwango vya uwekezaji na ukuaji wake,  jambo ambalo litaathiri huduma zitolewazo kwa wateja, biashara kwa ujumla na hata pato la serikali kutokana na sekta hii. 

Moja ya changamoto kubwa ambayo imekuwa ikigusiwa zaidi ni ile wingi wa kampuni za mawasiliano katika soko la mawasiliano ya simu za mkononi nchini Tanzania. Soko la Tanzania hivi sasa lina kampuni nane za mawasiliano ya simu. 

Wataalumu wa uchumi na teknolojia wanaeleza kuwa, kuimarisha soko itakuwa njia ya kuhakikisha sekta hii inakuwa bora na yenye tija zaidi na njia mojawapo muhimu ya kufanya hivyo ni kuunganisha japo kampuni mbili kati ya zilizopo sasa na kufanya kampuni chache kuwa na mtaji mkubwa zaidi, uwekezaji zaidi na ubora zaidi wa huduma ambao pia utashusha bei na kupandisha ubora. 

Moja ya kampuni ambazo zimechukua ushauri huu kwa vitendo na kuonyesha kusudio la kuungana ili kuboresha huduma na uwekezaji ni Tigo na Zantel. Kwa kuunganisha huduma, kampuni hizi zinaamini kuwa wateja kutoka kwenye kampuni hizo mbili wataweza kupata mtandaoa ambao ni imara na ulioenea zaidi, na pia watafurahia huduma zote ambazo zinatolewa na makampuni hayo, ikiwa ni pamoja na mtandao wa Tigo wa 4G na 4G+.

Hii itamaanisha utoaji wa huduma bora kwa wateja wote, uwekezaji bora, gharama nafuu na pato zaidi kwa nchi yetu. Ni matumaini ya watumiaji wengi za simu za mkononi kuwa uimarishaji wa soko hilo kwa mbinu hizi na nyingine u karibu na utawapa nafuu na tija zaidi.

KAMPUNI YA TANGA CEMENT YATANGAZA KUPATA FAIDA YA UENDESHAJI YA SHILINGI BILIONI 14.9

$
0
0
Na Ripota Wetu, Michuzi Tv
KAMPUNI ya Tanga Cement (TCPLC) imetangaza kupata faida ya uendeshaji ya Sh.bilioni 14.9 kwa kipindi cha mwaka kinachoishia Desemba 31,mwaka 2018 kutoka hasara iliyotokana na uendeshaji ya Sh.bilioni 10.99 kwa mwaka 2017.
Akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa wanahisa wa Kampuni hiyo Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Tanga Cement, Lau Masha amesema pia kuwa utendaji wa mwaka 2018 umesaidia kupunguza hasara baada ya kodi ya shilingi billion 11.3 kutoka shilingi bilioni 26.3 kwa mwaka 2017.

“Mauzo ya kundi letu yalipanda kwa asilimia 25 na kufika shilingi bilioni 214.9 kutoka shilini bilioni  171.8 zilizopatikana kwa mwaka uliopita wakati faida ghafi kwa mwaka iliongezeka kwa asilimia  91 na kuwa Sh.bilioni 56.2 kutoka Sh.bilioni 29.4 zilizopatikana mwaka uliopita,” amesema.

Ameongeza kuwa ukuaji wa biashara ulijikita katika ukuuaji wa simenti na secta ya ujenzi nchini Tanzania.

 Matumaini miundombinu chini ya mipango ya dira ya maendeleo ya Serikali ya mwaka 2025
Pamoja na hayo mwenyekiti huyo amesema kutokana na Tanzania kuwa soko la pili kwa ukubwa kwa masuala ya ujenzi Afrika Mashariki, uzalishaji wa simenti unatarajiwa kuongezeka hivyo Kampuni yao imejipanga kuhakikisha inanufaika na ukuaji huo katika soko la Kanda.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Reinhardt Swart amesema, kampuni iliongeza uzalishaji kwa kipindi chote hiki cha mwaka na kuweza kuzalisha mapato ya ziada kutokana na mauzo ya klika ya ziada iliyozalishwa.

Mkurugenazi huyo ameongeza kuwa mkataba wao na Kampuni ya reli Tanzania (TRC) umewawezesha kupata mabehewa zaidi ambayo yapo kwa ajili ya usafirishaji katika maeneo yao ya kimikakati ya usambazaji. Unafuu huo unapunguza gharama za kuhifadhi na usafirishaji huku ukuupa nguvu usafiri wa reli na usambazaji nchini Tanzania.

“Ingawa kushuka kwa thamani ya fedha na riba tunayolipa kutokana na mkopo tuliochukua kwa ajili ya mtaji wa uwekezaji mpya wa kinu namba mbili (TK2) vimeendelea kubakia kuwa matumizi ya gharama kubwa, hasara baada ya kodi kwa mwaka 2018 ilipungua,” ameongeza Mkurugenzi huyo.

Pamoja na mafanikio hayo kampuni haikutangaza gawio la mpito kwa wanahisa wake kwa mwaka 2018 kutokana sababu zilizoelezwa mahali hapo kuwa ni hali iliyotokana na utendaji wake wa kifedha kwa mwaka 2017 hivyo bodi kuamua kutumia busara kutotangaza gawio la mwisho ili fedha iliyopo kutumika katika shughuli za utendaji na kulipia madeni.
Mwenyekiti wa Bodi Tanga Cement, Lau Masha (wa nne lushoto), alizungumza wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa wanahisa wa kampuni hiyo jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Reinhardt Swart na baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Tanga Cement.

WAZIRI MKUU ATEMBELEA KIWANDA CHA KUTENGENEZA MITAMBO YA UMEME CHA TOSHIBA NA MAKUMBUSHO YA SAYANSI YA KAMPUNI HIYO NCHINI JAPAN

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Bibi Ririko Tanabe kuhusu historia ya kampuni ya Toshiba ya Japan wakati alipotembelea makumbusho ya Sayansi ya kampuni hiyo, Agosti 27, 2019.
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akipata maelezo kutoka kwa  Bibi Ririko Tanabe   kuhusu redio ya kwanza  ilitengenezwa na kampuni ya Toshiba kwenye miaka ya 1930, wakati alipotembelea Makumbusho ya Sayansi ya Kampuni ya Toshiba nchini Japan, Agosti 27, 2019. (
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa  Bibi Ririko Tanabe   kuhusu redio ya kwanza ya kucheza santuri iliyotengenezwa na kampuni ya Toshiba kwenye miaka ya 1930, wakati alipotembelea Makumbusho ya Sayansi ya kampuni ya Toshiba nchini Japan, Agosti 27, 2019.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na ujumbe wake wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi na watumishi wa Makumbusho ya Sayansi ya Kampuni ya kampuni ya Toshiba nchini Japan baada ya kutembelea makumbusho hiyo, Agosti 27, 2019. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa kiwanda cha kutengeneza mitambo ya  kuzalisha umeme cha Tsurumi kinachomilikiwa na kampuni ya Toshiba nchini Japan wakati alipotembelea kiwanda hicho, Agosti 27, 2019. Kushoto ni Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Japan, John Kambona.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na ujumbe wake wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wafanyakazi wa Kiwanda cha kutengeneza mitambo ya kuzalisha umeme cha Tsurumi kinachomilikiwa na kampuni ya Toshiba nchini Japan baada ya kutembelea kiwanda hicho, Agosti 27, 2019. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama chombo muhimu kinachounda  mitambo ya kuzalisha umeme wa maji na gesi (turbine) wakati alipotembelea kiwanda cha kutengeneza mitambo ya kuzalisha umeme cha Tsurumi kinachomilikiwa na Kampuni ya  Toshiba nchini Japan, Agosti 27, 2019. Wapili kulia ni Meneja Mkuu wa kiwanda hicho, Shinya Fujitsuka. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

VETA YAANZA KUTOA MAFUNZO RASMI KWA MAFUNDI WA SIMU ZA MKONONI NCHINI

$
0
0

Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Kipawa Dickson Mkasanga akizungumza na wanafunzi wa kozi ya ufundi wa simu za mkononi wakati wa ufunguzi rasmi wa mafunzo hayo katika chuo cha VETA Kipawa.
Mratibu wa kozi ya Ufundi wa Simu za Mkononi Ricky Sambo akitoa maelezo kuhusu utaratibu wa uendeshaji wa kozi hiyo.


Picha ya pamoja.

MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kupitia chuo cha VETA Kipawa imeanza kutoa mafunzo ya Ufundi wa Simu za Mkononi kwa lengo la kuandaa mafundi bora wa simu za mkononi nchini.

Akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa mafunzo hayo Agosti 26, 2019, Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Kipawa Dickson Mkasanga alisema mafunzo hayo yanalenga kuandaa mafundi wa simu za mkononi wenye ujuzi na  weledi watakaofanya kazi zao kwa mujibu wa sheria na kutoa huduma zenye viwango na ubora.

Alisema mafunzo hayo yanatolewa kwa ushirikiano na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ambapo wahitimu wa kozi hiyo watapatiwa vyeti vitakavyowawezesha kusajiliwa na kupewa leseni ya kufanya kazi za ufundi wa simu za mkononi inayotolewa na TCRA.

Alisema chuo chake pamoja na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) zilishirikishwa na TCRA kubaini uhitaji wa kozi hiyo, umahiri wa mafundi wanaohitajika sokoni na kutengeneza mtaala kwa ushirikiano na wadau mbalimbali na kwamba chuo chake kimejipanga kutoa mafunzo hayo kwa kiwango cha juu.

“Chuo hiki kitatumia rasilimali zake za kisasa na utaalamu wa walimu wake ili kuhakikisha mafunzo haya yanatolewa kwa umahiri na weledi wa hali ya juu”.Alisema

Aliwasihi wanafunzi wa kozi hiyo kuonesha ushirikiano na kufuata taratibu za mafunzo katika hatua zote ili kuwawezesha kupata ujuzi uliokusudiwa na kuwa mahiri katika kutoa huduma za ufundi wa simu za Mkononi.

Naye Mratibu wa kozi hiyo Ricky Sambo alisema mafunzo hayo yamepangwa kutolewa kwa hatua tatu kuanzia hatua ya awali (Basic Mobile Phone Technician) kwa wiki nne, hatua ya kati (Intermediate Mobile Phone Technician ) kwa wiki sita na hatua ya juu(Advanced Nobile Phone Technician ) kwa wiki mbili.

Kwa mujibu wa Sambo, TCRA imetoa ufadhili wa ada kwa wanafunzi 60  kusoma kozi ya awali huku VETA ikitoa waalimu na vifaa vya kuendesha kozi hiyo.

Desemba 2018, Serikali iliagiza kusajiliwa na kupatiwa leseni kwa mafundi wanaotoa huduma za matengenezo ya simu za mkononi ili kuhakikisha huduma wanazozitoa kwa wananchi zinakuwa na viwango stahiki.

WAZIRI SIMBACHAWENE AIELEZEA YA KAMATI BUNGE MCHAKATO WA TATHMINI YA ATHARI KWA MAZINGIRA

$
0
0
Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) leo Agosti 27, 2019 imewasilisha taarifa zake mbili kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira jijini Dodoma.

Taarifa zilizowasilishwa ni ya Utekelezaji wa Maazimio ya Bunge yanayohusiana na majukumu ya Wizara yaliyotokana na Mapendekezo ya Kamati hiyo katika taarifa yake ya mwaka iliyowasilushwa katika Mkutano wa Bunge wa Februari 2019.

Kamati hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Suleiman Sadik pia imepokea taarifa ya Mazingira kwa ajili ya kujijengea uelewa kuhusu Tathmini ya Athari ya Mazingira (TMA). 
 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. Suleiman Sadik (kushoto) akiongoza Kikao cha Kamati jijini Dodoma kilichopokea taarifa za Ofisi ya Makamu wa Rais.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingia) Mhe. George Simbachawene akifafanua jambo wakati wa Kikao cha Kamati Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira.
 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingia) Mhe. Mussa Sima akizungumza wakati wa Kikao cha Kamati Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira kilichofanyika jijini Dodoma.
 Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira wakifuatilia Kikao cha Kamati hiyo na Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dodoma.
 Kuanzia kushoto Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingia) Mhe. George Simbachawene, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingia) Mhe. Mussa Sima, Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Profesa William Mwegoha na Mkurugenzi wa Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Samuel Gwamaka wakifuatilia kikao hicho.
Wajumbe wa Kamati pamoja wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais wakimsikiliza Mkurugenzi wa Baraza la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Samuel Gwamaka (aliyesimama) wakati akifafanua jambo


TUZO ZA "TANZANIA ELIMU AWARDS" KUTOLEWA AGOSTI 31 MWAKA HUU

$
0
0
* Wanafunzi, walimu na wadau mbalimbali wanaoshiriki kuiinua sekta ya elimu kupata tuzo hizo

KWA mara ya kwanza Kampuni ya Elimu Solutions Tanzania imeandaa tuzo za Tanzania Elimu Awards zitakazotolewa  Agosti 31 mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam huku mgeni rasmi akitegemewa kuwa Waziri wa nchi ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Seleiman Jaffo (Mbunge.)

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Elimu Solution nchini Neithan Swedi amesema kuwa jukumu la kusaidia sekta ya elimu ni la kwetu zote, na serikali imeonesha mfano kwa kushiriki vyema katika sekta ya elimu na mwaka huu shule za serikali zimeingia katika shule kumi bora zilizofanya vizuri zaidi katika mitihani ya kidato cha sita.

Amesema kuwa wameanzisha utoaji tuzo za Tanzania Elimu Awards kwa walimu, wanafunzi na wadau wa sekta hiyo Afrika Mashariki na hiyo ni katika kuendeleza na kusimamia sekta hiyo muhimu katika ujenzi wa taifa na kueleza kuwa ni muhimu kuendeleza sekta hiyo ili iendelee kuwa kiwanda cha kuzalisha vijana wa kitanzania ambao ndio taifa la kesho.

Kwa upande wake msimamizi wa miradi kutoka Elimu Solutions Tanzania Peter Godian amesema kuwa katika kuenzi na kuheshimu jitihada za wanafunzi, walimu, shule, serikali na taasisi mbalimbali kampuni hiyo kwa mara kwanza imeandaa tuzo hizo ili kuleta motisha ili kuipeleka sekta hiyo mbele zaidi.

Amesema kuwa tuzo hizo TEA  zinajumuisha tuzo 32 kutoka vipengele vikuu 11 zikiwemo tuzo kwa wanafunzi Bora wakike na kiume kwa shule za msingi na sekondari pamoja na vipengele mbalimbali vikiwemo walimu bora, shule bora, na tuzo ya heshima.

Amesema kuwa washindi watapatikana kupitia takwimu zitakazopatikama kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu na wanaamini itachangia katika kuchangia utamaduni wa kutunza na kutambua mchango wa wasomi, wabunifu na wadau wa sekta ya elimu na kuzidi kuwapa faraja na moyo wa kuendelea kufanya kazi na kukuza sekta adhimu ya elimu.
  Mkurugenzi Mtendaji wa  Elimu Solutions Tanzania Neithan Swedi akizungumzia kuhusu utoaji wa Tuzo zijulikanazo kama Tanzania Elimu Awards zitakazotolewa na Kampuni hiyo zitakazofanyika Agosti 31, 2019 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Msimamizi wa Miradi kutoka Elimu Solutions Tanzania Peter Godian na Kulia ni Afisa Masoko wa  Elimu Solutions Tanzania Catherine Ndosi.
 Msimamizi wa Miradi kutoka Elimu Solutions Tanzania Peter Godian akisoma tuzo zitakazotolewa  na kampuni ya Elimu Solutions Tanzania kwenye hafla ya utoaji wa Tuzo zijulikanazo kama Tanzania Elimu Awards zitakazofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Masoko wa  Elimu Solutions Tanzania Catherine Ndosi na kushoto ni  Mkurugenzi Mtendaji wa  Elimu Solutions Tanzania Neithan Swedi.
 Afisa Masoko wa  Elimu Solutions Tanzania Catherine Ndosi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kapuni hiyo ilivyojipanga kutekeleza utoaji wa tuzo hizo wakati wa kutangaza utoaji wa tuzi zijulikanazo kama Tanzania Elimu Awards

MANYARA WACHANGIA DAMU AJALI YA MOROGORO

$
0
0
JAMII yatakiwa kuwa na mwamko wa kuchangia damu ili kuwasaidia wahitaji waliopo kwenye hospitali mbalimbali nchini, wakiwemo wanawake wenye ujauzito na majeruhi wanaopata ajali.

Mwenyekiti wa jumuiya ya umoja wa vijana wa CCM (UVCCM) mkoani Manyara, Moses Komba ameyasema hayo wakati akielezea mpango wao wa kuchangia damu ya kuwasaidia majeruhi wa ajali iliyotokea Morogoro.

Komba amesema umoja huo unawaomba wananchi kuwa na tabia ya kujitokeza kuchangia damu kwa ajili ya kuwasaidia wahitaji mbalimbali. 

Amesema viongozi, wanachama na vijana wa chama chao wanapaswa kuchangia damu ili kuokoa maisha ya majeruhi waliopata ajali ya moto mkoani Morogoro. 

"Tunapaswa kuchangia damu kwani huu ndiyo utamaduni wa Watanzania kushirikiana wakati wa shida na raha bila kujali dini, kabila, rangi, itikadi ili kuonyesha umoja wetu kwa kusaidia ndugu zetu," alisema Komba. 

Katibu wa UVCCM mkoani Manyara, Daniel Muhina alisema wamepata uniti 58 za chupa za damu na wanaendelea na uchangiaji damu hadi Agosti 31. 

Muhina alisema shughuli za uchangiaji damu zinaendelea mkoa mzima ambapo mjini Babati ni kwenye ofisi za CCM Bagara na halmashauri ya wilaya ya Babati ni kituo cha afya Magugu. 

Alisema sehemu nyingine ni ofisi ya CCM ya wilaya ya Hanang', hospitali ya wilaya ya Mbulu, kituo cha afya Orkesumet wilayani Simanjiro na hospitali ya wilaya ya Kiteto. 

Mmoja kati ya vijana hao, Carol Gisimoy amesema wanaungana na watanzania wengine nchini katika kuwasaidia kuchangia damu majeruhi wa ajali hiyo ya Morogoro. 

Agosti 10 mwaka huu ajali ya lori la mafuta ilitokea Msamvu mkoani Morogoro ambapo watu 101 walifariki dunia na majeruhi 12 wamelazwa hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam. 

Baadhi ya wanachama wa UVCCM Mjini Babati Mkoani Manyara wakishiriki kuchangia damu kwenye ofisi ya CCM Tawi la Bagara.
Viewing all 110028 articles
Browse latest View live




Latest Images