Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

Waziri Jafo alipongeza Jiji la Dodoma kwa kubuni miradi ya Maendeleo

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo ameziagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanaweka mikakati ya kubuni miradi ambayo itawasaidia katika kujiwekea vitega uchumi na kukuza mapato katika Halmashauri zao ili kuachana na utegemezi katika Serikali.

Ameyasema hayo leo wakati wa utiaji wa saini Miradi ya Ujenzi wa majengo mawili ya vitega uchumi vya Halmashauri ya Jiji la Dodoma uliofanyika katika Viwanja vya Nyerere Square, Jijini Dodoma.

Mhe Jafo amesema Halmashauri zote nchini zinatakiwa kuwa wabunifu, kujipanga na kuweka mikakati ya kuondokana na unyafuzi wa mapato kwa kuanzisha miradi ambayo itasaidia kuongeza mapato na kuleta maendeleo kwa jamii.

Amesema kuwa kama Halmashauri zote zingekuwa wabunifu na kuamua kujitoa katika utendaji kazi kusingekuwa na unyafuzi wa mapato bali zingejikita katika kubuni na kuibua miradi ya maendeleo ili kujikwamua kiuchumi na kujiongezea vitega uchumi vitakavyoleta maendeleo katika Halmashauri zao

“ Kusipokuwa na ubunifu, kujitoa katika utendajikazi wa watumishi wa Halmashauri, hali ya unyafuzi wa mapato itaendelea na bado Halmashauri nyingi zitakuwa ni tegemezi kwa Serikali, hivyo ninaziagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanabuni vitega uchumi ili waweze kujitegemea kwa kutumia mapato yao ya ndani ” Anasisitiza Mhe.Jafo

Mhe. Jafo amezitaka Halmashauri zote nchini kuiga mfano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kubuni Miradi ya Maendeleo kwa ajili ya vitega uchumi na kuondokana na utegemzi kwa Serikali.

Amefafanua zaidi kuwa watumishi wa Serikali za Mitaa nchini kuacha kufanyakazi kwa maigizo, kwa kujionyesha kwenye mitandao bali wafanyekazi kwa weledi lengo likiwa ni kuwahudumia wananchi maskini na kulipeleka taifa katika uchumi wa kati

“Kuna watu nchi hii wamezoea maigizo, hivyo kwa wale ambao wapo chini ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kuacha kufanyakazi kwa maigizo bali watu wafanyekazi kwa weledi ili kufikia mallengo ya Serikali.” Amesisitiza Mhe. Jafo

Amesema watu wasipende kujionyesha kwenye mitandao kuwa wanafanyakazi , bali wafanye kazi kwa ajili kulitumikia taifa hasa wananchi maskini kwa kuwa nchi hii inabadilika na kinachohitajika ni maendeleo ya Taifa.

Amewasii vijana waliopewa dhamana ya uongozi nchini kufanyakazi kwa bidii na maarifa waliyonayo na kuacha kufanyakazi kwa maigizo, lengo likiwa ni kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli katika kufikia uchumi wa kati.

Amewapongeza Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kuweza kutumia Makusanyo ya Fedha za Ndani kwa ajili ya ujenzi wa vitega uchumi lengo kubwa ni kutoa unyafunzi wa mapato na kupunguza utegemezi kwa Serikali.

Aidha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Bilinith Mahenge amesema kuwa kupitia miradi hiyo Wananchi wa Mkoa wa Dodoma watapata fursa ambazo zitawasaidia kuongeza kipato na kukuza uchumi wa Dodoma utaongezeka .

Dk Gwajima awataka Watanzania kutumia Bima ya Afya iliyoboreshwa

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughurikia afya Dk. Doroth Gwajima,akizungumza na watumishi wa kituo cha afya cha Chamwino Ikulu alipofanya ziara ya kukagua utoaji huduma za afya kwa wateja wenye kadi za CHF iliyoboreshwa.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughurikia Afya Dk.Doroth Gwajima,akiwaonyesha kadi ya CHF iliyoboreshwa wananchi waliofika katika kituo cha Afya cha Chamwino Ikulu alipofanya ziara ya kukagua utoaji huduma za afya kwa wateja wenye kadi za CHF iliyoboreshwa huku akiwahimiza zaidi ili wajiunge na wapate huduma iliyobora.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughurikia Afya Dk.Doroth Gwajima,akizungumza na baadhi ya wananchi waliofika katika kituo cha Afya cha Chamwino Ikulu alipofanya ziara ya kukagua utoaji huduma za afya kwa wateja wenye kadi za CHF iliyoboreshwa huku akiwahimiza zaidi ili wajiunge na wapate huduma iliyobora.


Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughurikia afya Dk. Doroth Gwajima, amewataka watumishi wa afya kote nchini kuacha kuwabagua au kutowapa kipaumbele wateja wanaotumia kadi za bima ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa kwa kuwahudumia watu wenye fedha mkononi kwanza.

Dk. Gwajima ameyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na watumishi wa kituo cha afya cha Chamwino Ikulu alipofanya ziara ya kukagua utoaji huduma za afya kwa wateja wenye kadi za CHF iliyoboreshwa wilayani hapo.

Amewataka watumishi wa afya kuwapa kipaumbele wagonjwa wanaotumia kadi hizo ili kuweza kuongeza idadi ya watu wanaotumia mfumo huo nchini.Dk Gwajima Amewataka watumishi kote nchini kuendelea kuhamasisha matumizi ya kadi hizo ili kuongeza idadi ya watu wanaotumia mfumo huo hapa nchini na watu wengi waweze kujiunga.Amesema hivi sasa kadi za CHF iliyoboreshwa imefanyiwa marekebisho makubwa na serikali hali ambayo inamwezesha mgonjwa kupata huduma katika hospitali yoyote hadi ngazi ya mkoa.

Pia amewataka watumishi wa afya nchini kutoa huduma zenye ubora ili kuweza kuwavutia wananchi kujiunga na mifumo hiyo ya bima ya afya ya jamii.“Kama tusipotoa huduma bora hivi vituo vyetu tulivyojenga nchi nzima vitakuwa havina maana lazima sisi kama watumishi wa afya tubadilike ili kuweza kuwavutia wananchi kuja katika vituo vyetu kupata huduma ya afya”

“Sitaki kusikia baada ya siku hizi 14 kuwa kuna kituo kimeshindwa kutuma taarifa zake au mifumo inakataa kwani kila kituo kinatakiwa kutuma taarifa zake za wateja waliohudumiwa ili kuweza kurejeshewa fedha zake ambazo zitatumika katika mahitaji mbalimbali ya eneo hilo”amesema Dkt Gwajima.

Naye mganga mfawidhi wa kituo cha afya Chamwino, Dk. Zipora Mfugale amesema kuwa wamejipa kuhakikisha kuwa wanaongeza idadi ya watu wanaotumia mfumo wa CHF iliyoboreshwa.

MWENYEKITI WA BODI DAWASA AWAONDOA HOFU WAKAZI WA MKURANGA

$
0
0

Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange  akiangalia mafundi wa DAWASA wakiwa wanaunganisha mabomba kabla ya kuyalaza, ziara ya Mwenyekiti wa Bodi ilikua sambamba na wajumbe pamoja Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja.

Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara yake kutembelea miradi inayosimamiwa na DAWASA na kuzungumzia hatua mbalimbali ilipofikia na kuwaondoa hofu wakazi wa maeneo ya Mkuranga baada ya kukaa bila maji safi kwa kipindi kirefu.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumzia mradi wa maji wa Mkuranga wenye thamani ya  Bilion 5.5 unaotarajia kukamilika ndani ya miezi nane kuanzia sasa na utahudumia wananchi 25,000 ambapo maji yatasambazwa katika Vitongoji mbalimbali vya Wilaya ya Mkuranga.
Msimamizi wa mradi wa maji Mkuranga  kutoka DAWASA, Mhandisi John Kirecha akielezea ramani ya mradi wa Maji Mkuranga kuanzia kwenye chanzo cha maji Kulungu kuelekea kwenye tanki la maji la ujazo wa Lita Milioni 1.5 leo wakati wa ziara ya mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange pamoja na wajumbe wa bodi hiyo. 



Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange akiyajaribu maji kwa kuyaonja kutoka kwenye kisima kilichopo Mkuranga kitakachohudumia wakazi wa maeneo hayo.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

MWENYEKITI wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange amewaondoa hofu wakazi wa Mkuranga na kuwataka kuwa na subira kwani kero ya maji inakaribia kumalizika.

Hayo ameyasema wakati wa ziara yake katika mradi wa maji wa Mkuranga ulioanza kutekelezwa hivi karibuni ukiwa umefikia kwenye hatua ya ujenzi wa tanki la maji na ulazaji wa mabomba.

Mwamunyange amesema, kulikuwa na changamoto zilijitokeza katika mradi huo ila kwa sasa zimeshapatiwa ufumbuzi na wakandarasi wameshaingia kazini.

“Napenda kusema hakuna udanganyifu katika mradi wa Mkuranga ila kulikuwa na changamoto zilijitokeza na kwa sasa zimeshapatiwa uchambuzi na wakandarasi wameingia kazini kuendelea na kazi,”amesema Mwamunyange.

Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema mradi huu ni moja kati ya miradi sita iliyosainiwa hivi karibuni ukiwa na thamani ya Bilion 5.5 na inatarajia kukamilika ndani ya miezi nane kuanzia sasa.

Luhemeja amesema, kukamilika kwa mradi huu utahudumia wananchi 25,000 ambapo maji yatasambazwa katika Vitongoji mbalimbali vya Wilaya ya Mkuranga.

“Katika mradi huu kutakuwa na ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa Lita Milion 1.5 ambapo litasambaza maji katika maeneo mbalimbali na zoezi la ulazaji wa mabomba linaendelea kwa sasa na wameangalia ubora wa mitaro kwa kuchimba urefu wa mita 1.5 na mabomba yote ni mapya.

"Hatutarajii kuona kuna changamoto ya upotevu wa maji katika mradi huu, kwani mabomba yote ni mapya pia tumeangalia ubora wa mitaro kwa kuchimba mita 1.5 kwenda chini na utakamailika ndani ya muda wa miezi nane tokea sasa,"amesema.

Msimamizi wa mradi huo kutoka DAWASA, Mhandisi John Kirecha ameweka wazi kuwa wameweza kufuata taratibu mbalimbali za kitaalamu kabla ya kuendelea na ujenzi ambapo walichukua sampo ya mchanga eneo la ujenzi wa tanki na kupeleka DIT na wakapata ushauri wa kuchimba urefu wa Mita 2.5 kwenda chini.


Pia, ameeleza kuwa watafunga Booster itakayosaidia kusafirisha maji kwa kasi kuelekea kwenye tanki la maji la Mwanambaya lenye ujazo wa Lita 100,000 litakalotumika kama tanki la akiba ( reserve).


Mradi wa Mkuranga unatarajiwa kukamilika mapema 2020, na utahudumia Mkuranga na vitongoji vyake, maeneo ya Viwanda Kisemvule, Vikindu na wananchi wa maeneo hayo wamefurahi kuja kwa mradi huo kutoka chanzo cha Maji Kulungu ambapo wamekaa na shauku ya kupata maji safi na salama kwa muda mrefu.

RUBY AFUNGUKA

MHE. WAZIRI MKUU ATEMBELEA BANDA LA TANZANIA LA MAONESHO YA TICAD 7

$
0
0

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akisalimiana na Bi. Edda Magembe, Afisa Ubalozi wa Tanzania nchini Japan alipotembelea banda la maonesho ya vivutio vya utalii wa Tanzania jijini Yokohama, Japan tarehe 28 Agosti 2019. Mhe. Waziri Mkuu yupo nchini Japan akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Mkutano wa Saba wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika (TICAD 7) utakaofanyika kuanzia tarehe 28 hadi 30 Agosti 2019. Maonesho hayo yanaenda sambamba na mkutano huo ambao umetoa fursa kwa nchi za Afrika kujitangaza kwenye masuala ya vivutio vya utalii, uwekezaji na biashara.
Mhe. Waziri Mkuu akisalimiana na mmoja wa washiriki kwenye banda la maonesho la Tanzania. Maonesho hayo yanafanyika sambamba na Mkutano wa Saba wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika (TICAD 7)

Mhe. Waziri Mkuu akiangalia moja ya kipeperushi kuhusu maeneo ya vivutio vya utalii vilivyopo nchini alipotembelea banda la Tanzania kwenye Mkutano wa TICAD 7 unaofanyika jijini Yokohama, Japan
Mhe. Waziri Mkuu akiangalia moja ya bidhaa zinazopatikana nchini alipotembelea banda la Tanzania
Mhe. Waziri Mkuu kwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi wakiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa maonesho kwenye banda la Tanzania yanayoendelea sambamba na Mkutano wa Saba wa TICAD

RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN AKUANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA RWANDA ANAYEMALIZA MUDA WAKE NCHINI TANZANIA

$
0
0

 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Balozi wa Jamuhuri ya Rwanda Nchini Tanania Eugine Kayihura, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na Rais na kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi Nchini Tanzania, yaliofanyika leo 27-8-2019.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Balozi wa Jamhuri ya Rwanda Nchini Tanzania Eugine Kayihura, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na kuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi Nchini Tanzania, mazungumzo hayo yamefanyika Ikulu Zanzibar leo 27-8-2019.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Rwanda Nchini Tanzania Eugine Kayihura, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na kumuaga baada ya kumaliza muda wake ya kazi Nchini Tanzania, hafla hiyo imefanyika leo 27-8-2019 Ikulu Zanzibar.

/RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na mgeni wake Balozi wa Jamuhuri ya Rwanda Nchini Tanzania Eugine Kayihura , baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika Ikulu Zanzibar leo 27-8-2019, alipofika kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa Kazi Nchini Tanzania.(Picha na Ikulu)

TUZO ZA "TANZANIA ELIMU AWARDS" KUTOLEWA AGOSTI 31 MWAKA HUU MLIMANI CITY JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Wanafunzi, walimu na wadau mbalimbali wanaoshiriki kuiinua sekta ya elimu kupata tuzo hizo

KWA mara ya kwanza Kampuni ya Elimu Solutions Tanzania imeandaa tuzo za Tanzania Elimu Awards zitakazotolewa  Agosti 31 mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam huku mgeni rasmi akitegemewa kuwa Waziri wa nchi ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Seleiman Jaffo (Mbunge.)

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Elimu Solution nchini Neithan Swedi amesema kuwa jukumu la kusaidia sekta ya elimu ni la kwetu zote, na serikali imeonesha mfano kwa kushiriki vyema katika sekta ya elimu na mwaka huu shule za serikali zimeingia katika shule kumi bora zilizofanya vizuri zaidi katika mitihani ya kidato cha sita.

Amesema kuwa wameanzisha utoaji tuzo za Tanzania Elimu Awards kwa walimu, wanafunzi na wadau wa sekta hiyo Afrika Mashariki na hiyo ni katika kuendeleza na kusimamia sekta hiyo muhimu katika ujenzi wa taifa na kueleza kuwa ni muhimu kuendeleza sekta hiyo ili iendelee kuwa kiwanda cha kuzalisha vijana wa kitanzania ambao ndio taifa la kesho.

Kwa upande wake msimamizi wa miradi kutoka Elimu Solutions Tanzania Peter Godian amesema kuwa katika kuenzi na kuheshimu jitihada za wanafunzi, walimu, shule, serikali na taasisi mbalimbali kampuni hiyo kwa mara kwanza imeandaa tuzo hizo ili kuleta motisha ili kuipeleka sekta hiyo mbele zaidi.

Amesema kuwa tuzo hizo TEA  zinajumuisha tuzo 32 kutoka vipengele vikuu 11 zikiwemo tuzo kwa wanafunzi Bora wakike na kiume kwa shule za msingi na sekondari pamoja na vipengele mbalimbali vikiwemo walimu bora, shule bora, na tuzo ya heshima.

Amesema kuwa washindi watapatikana kupitia takwimu zitakazopatikama kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu na wanaamini itachangia katika kuchangia utamaduni wa kutunza na kutambua mchango wa wasomi, wabunifu na wadau wa sekta ya elimu na kuzidi kuwapa faraja na moyo wa kuendelea kufanya kazi na kukuza sekta adhimu ya elimu.
  Mkurugenzi Mtendaji wa  Elimu Solutions Tanzania Neithan Swedi akizungumzia kuhusu utoaji wa Tuzo zijulikanazo kama Tanzania Elimu Awards zitakazotolewa na Kampuni hiyo zitakazofanyika Agosti 31, 2019 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Msimamizi wa Miradi kutoka Elimu Solutions Tanzania Peter Godian na Kulia ni Afisa Masoko wa  Elimu Solutions Tanzania Catherine Ndosi.
 Msimamizi wa Miradi kutoka Elimu Solutions Tanzania Peter Godian akisoma tuzo zitakazotolewa  na kampuni ya Elimu Solutions Tanzania kwenye hafla ya utoaji wa Tuzo zijulikanazo kama Tanzania Elimu Awards zitakazofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Masoko wa  Elimu Solutions Tanzania Catherine Ndosi na kushoto ni  Mkurugenzi Mtendaji wa  Elimu Solutions Tanzania Neithan Swedi.
 Afisa Masoko wa  Elimu Solutions Tanzania Catherine Ndosi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kapuni hiyo ilivyojipanga kutekeleza utoaji wa tuzo hizo wakati wa kutangaza utoaji wa tuzi zijulikanazo kama Tanzania Elimu Awards

Airtel Africa crosses the 100 million subscribers milestone

$
0
0
Nairobi, August 28, 2019: Airtel Africa, a leading telecommunications services provider with operations in 14 countries across Africa, today announced that it has crossed the 100 million customers mark across its operations. Airtel Africa is the second-largest mobile operator in Africa by a number of active subscribers.
Commenting on this milestone achievement, Raghunath Mandava, Airtel Africa’s Chief Executive Officer, said: “I am delighted to report that Airtel Africa has crossed the 100 million subscriber mark. This achievement is a testament to the hard work of our employees and a clear reflection that customers value our network, service offerings and customer experience. The positive momentum we have seen in customer acquisition further underpins our medium-term aspirations for revenue and profit growth. I would like to take this opportunity to thank all the teams that have worked hard to get us here.”
Airtel Africa’s footprint is characterized by low but increasing mobile connectivity, with a unique user penetration at 43%, highlighting the potential for growth across its footprint.
The company believes in enhancing connectivity and digitizing the countries in which it operates and has invested to expand its network footprint and number of 4G sites to enhance network capabilities and support its future business growth.
A combination of an under-penetrated telecom market, a young addressable population, and rising smartphone affordability, along with low data penetration and an underbanked population, will drive the growth opportunities for the data and mobile money segments moving forward.

About Airtel Africa
Airtel Africa is a leading provider of telecommunications and mobile money services, with a presence in 14 countries in Africa, primarily in East Africa and Central and West Africa.
Airtel Africa offers an integrated suite of telecommunications solutions to its subscribers, including mobile voice and data services as well as mobile money services both nationally and internationally. The Group aims to continue providing a simple and intuitive customer experience through streamlined customer journeys.


Kampeni ya TCRA ya Mnada kwa Mnada yatoa Elimu ya Usajili wa laini kwa kutumia alama za vidole

$
0
0
 Wananchi wakipata huduma ya usajili wa katika banda la vitambulisho vya Taifa (NIDA) katika Viwanja vya Tangamano jijini Tanga.
 Afisa wa TCRA akimuhudumia mwananchi wakati alipotembelea banda la TCRA katika Mnada wa Tangamano jijini Tanga.
 Afisa wa Idara ya Uhamiaji akitoa huduma kwa mwananchi wakati alipotembelea banda la Uhamiaji katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya TCRA katika Viwanja vya Tangamano jijini Tanga.
 Mwananchi akiweka alama za kidole kwa ajili ya usajili wa laini ya simu katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ya TCRA katika Viwanja vya Tangamano jijini Tanga.
 Wananchi wakipata huduma za Mawasiliano katika Viwanja vya Tangamano jijini Tanga.
Wananchi wakipata huduma za Mawasiliano katika Viwanja vya Tangamano jijini Tanga.

WAKAZI wa jijini Tanga   na viunga vyake wamejitokeza kwa wingi katika kampeni  ya Mnada kwa Mnada ambapo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikishirikiana na Kampuni ya simu, Jeshi la Polisi Kitengo cha Uhalifu Mitandaoni  na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa ajili  ya utoaji wa huduma za usajili wa laini za simu kwa kutumia vitambulisho vya kitaifa na kuhakikiwa na kampuni za simu kwa kuweka alama za vidole kwa laini za simu.

Mkuu wa Kanda ya Kaskazini wa TCRA  Mhandisi Emelda Salum amesema ni fursa kwa wananchi wa wa Tanga kupata huduma kutokana na kuwa na mnyororo wadau wa  mawasiliano. 
Amesema Mnada kwa Mnada utadumu kwa siku tatu katika Viwanja vya Tangamano jijini Tanga ambapo itatoa fursa kwa wananchi wengi kufika kupata huduma za Mawasiliano na usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.

Salum kuwa kampeni ya Mnada kwa Mnada ni kwa ajili ya kutoa elimu ya mawasiliano kwa kushirikiana na wadau katika kujibu changamoto wanazokutanazo katika utumiaji wa mawasiliano nchini.

Salum amesema kuwa wananchi wasio kuwa na Vitambulisho vya NIDA wahakikishe  wanapata katika usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole na huduma nyinginezo za Mawasiliano hayo.
Amesema kuna watu wengine wanatumia mawasiliano ya simu bila kujua ambapo Jeshi Polisi lipo katika Kampeni ya Mnada kwa Mnada ili kuwaelewesha makosa ya jinai ya matumizi ya simu.
Aidha amesema Kampeni hiyo ni endelevu katika kuwafikia ikiwa kuhakikisha kila mwananchi anajisajili laini yake kwa alama za vidole kwa kutumia kitambulisho cha taifa cha NIDA.

Amesema kuwa TCRA iko kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi ili mtumie Mawasiliano kwa usalama kutokana na elimu tunayotoa.

Salum amesema kuwa wananchi wajitokeze katika kujisajili kwa alama za vidole kabla ya Desemba 31.

"TCRA tumejidhatiti katika kuwafikia  wananchi katika utoaji wa elimu za utumiaji wa bidhaa za mawasiliano kwa kutatua changamoto katika huduma hiyo"amesema Salum

WANANCHI DAR WAANDAMANA UBALOZI WA AFRIKA KUSINI ULIOPO TANZANIA KUISHINIKIZA SERIKALI YA NCHI HIYO KUIACHIA HARAKA NDEGE WANAYOISHIKILIA, POLISI WAIMARISHA ULINZI

$
0
0
Mmoja wa Waandamanaji akiwa amebeba bango lake nje ya Ubalozi wa Afrika Kusini uliopo nchini Tanzania leo,wakiishinikiza Serikali ya Afrika Kusini kuiachia ndege ya Tanzania  ambayo wanaishikilia kwa siku kadhaa sasa. 

Na Said Mwishehe,Michuzi TV


TUNATAKA ndege  yetu...tunataka ndege yetu...Mandela anahujumiwa ...tunataka ndege yetu...! Hivyo ndivyo walivyokuwa wanaimba Watanzania walioamua kufanya maandamano katika Ubalozi wa Afrika Kusini uliopo nchini Tanzania wakiishinikiza Serikali ya Afrika Kusini kuiachia ndege ya Tanzania ambayo wanaishikilia kwa siku kadhaa sasa.

Wananchi hao wameamua kwenda kwenye Ubalozi huo leo Agosti 28,mwaka huu wa 2019 kati ya saa nne na saa tano asubuhi huku wengine wakionekana kuwa na hasira kali wakiwa na mabango.

Wakiwa kwenye ubalozi huo Watanzania hao walikuwa wanapaza sauti ya kutaka ndege hiyo kuachiwa haraka na kinachofanywa na Afrika Kusini ni kuihujumu Tanzania pamoja na kumhujumu Mandela.

Wakati wakiwa katika ubalozi huo wananchi hao walikuwa wameshika mabango yanayoshinikiza ndege hiyo kuachiwa.

Baadhi ya wananchi wamehoji waliokuwepo kwenye ubalozi huo walikuwa wanahoji inakuaje suala la mtu binafsi linaigharimu Serikali ya Tanzania. Wengine wamesema inashangaza kuona marafiki wa Tanzania kwa miaka mingi ambao  ni Afrika Kusini wakiahiriki kurudisha nyuma maendeleo ya Tanzania.

Akizungumza akiwa eneo la tukio Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amesema sio sahihi kwa  wananchi hao kwenda katika ubalozi huo,hivyo amesema watu watatu  ambao ni vinara wa maandamano hayo wanawashikilia kwa sasa

"Hata kama walikuwa na haki ya kuandamana hapaswi kufanya hivyo kwasababu ni kinyume na sheria,waache suala hilo lishughulikiwe na Serikali kwa utaratibu unaofaa kwani tayari maofisa wa ngazi za juu wanaendelea kulishughulikia,"amesema Mambosasa.

Hata hivyo eneo hilo nilikuwa limeimarishwa na ulinzi qmbapo Kikosi cha Kutuliza Ghasia(FFU)walikuwa eneo la ubalozi huo wakisimamia usalama.Polisi waliamua kuwatawanya wananchi waliokwenda katika ubalozi huo.

Watanzania hao ambao walionekana kuwa na hasira kutokana  na ndege yao kushirikiwa nchini Afrika Kusini kwa siku kadhaa waliuzunguka waliamua mazingira Ubalozi huo huku waiomba vyombo za kutaka ndege inayoshikilliwa kuachiwa haraka.
 Baadhi ya Wananchi wakiwa wameandamana nje ya ubalozi Ubalozi wa Afrika Kusini uliopo nchini Tanzania kabla ya kutawanywa na jeshi la Polisi,wakiishinikiza Serikali ya Afrika Kusini kuiachia ndege ya Tanzania ambayo wanaishikilia kwa siku kadhaa saa.

Waandamana kushinikiza ndege iliyokamatwa iachiwe

$
0
0
Mamia Waandamana Jijini Dar es Salaam kushinikiza Ndege iliyokamatwa Kuachiwa 

Na.Mwandishi Maalum –Dar es Salaam. 

Katika hali isiyo ya kawaida mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wameandamana kuelekea katika Ubalozi wa Afrika ya Kusini nchini kushinikiza kuachiwa kwa ndege ya ATCL inayoshikiliwa Jijini Johanesberg Afrika ya Kusini kwa amri ya Mahakama. 

Maandamano hayo ambayo hayakufahamika yametokea upande gani wa Jiji yaliwashirikisha watu mbalimbali wakiwemo waliojitambulisha kama wanafunzi wa vyuo vya elimu ya Juu pamoja na wananchi wa kawaida waliodai wamechoshwa na vitendo vya kuihujumu serikali ya awamu ya Tano. 

Mabango mbalimbali waliyobeba waaandamanaji hao yalionyesha kusikitishwa na kitendo cha kushikiliwa kwa ndege ya Tanzania nchini Afrika ya Kusini , nchi ambayo uhuru wake umepatikana kwa msaaada wa Tanzania kwa kuwasaidia makazi na hata vifaa waliokua wapigania uhuru wa nchi hiyo. 

Mmoja wa waandamanaji hao ambaye hakutaka kutaja majina yake , akiongea kwa uchungu alisema Afrika ya Kusini imekua nchi isiyo na shukrani kabisa kwa kitendo cha kuikamata ndege ya ATCL ambalo ndilo kwanza linatoka katika hali ya kuwa taabani. 

“Tumekuja hapa kuwaambia wenzetu wa Afrika ya Kusini kwamba uungwana sio tu kulipa fadhila kwa aliyekusaidia, bali hata matendo tu yanatosha, haiwezekani sisi tumewasaidia wapate uhuru leo hii hawana hata aibu wanakamata ndege yetu tena kwa sababu zisizokua na msingi” Alisema mmoja wa waandamanaji hao. 

Mingoni mwa mabango waliyobeba yalisomeka ‘Turudishieni ndege yetu na sisi tuwarudishie makaburu uhuru wao maana mmeshindwa kuwa wasataarabu’ lingine lilisomeka ‘ Waafrika ndio maana tunadharaulika duniani kwa kufanya mambo ya hovyo. 

Kwa upande wake Sadik Ramadhan aliyekua anazungumza kwa jazba alisema waafrika ya kusini ni rafiki zetu kitendo cha kushirikiana na mzungu mmoja kuihujumu Tanzania ni kitendo ambacho hakikubaliki kabisa, alisema Rais Ramaphosa alipokuwa nchini kwenye mkutano wa SADC aliwahakikishia watanzania kwamba undugu wa nchi hizi utaendelea na hakuna hata mtu mmoja wa kuuvunja. 

Aidha alisema lengo la maandamano hayo ya amani ni kumtaka Balozi atoke na aeleze ni hatua gani zinazoendelea za kuhakikisha ndege ya watanzania inarudi kwani imenunuliwa kwa kodi za wananchi tena wananchi masikini wanaopambana kuinua nchi yao. 

Huku wakiimba wimbo kwamba wamemsaliti mzee Mandela waandamanaji hao walisema inatia uchungu sana kuona taifa lililosaidiwa na Tanzania ndio sasa linakua mstari wa mbele kuhujumu mali zake jambo ambalo wamesema halikubaliki. 

Maandamano hayo ambayo yalizua taharuki kwa takriban nusu saa, yalizimwa na Jeshi la polisi kwa kuwataka waandamanaji hao kuondoka kwa madai suala hilo linaendelea kushughulikiwa kwa mujibu wa sharia na taratibu za kidiplomasia. 

Baada ya kuamriwa kuondoka waandamanaji walitawanyika wakiendelea kuimba kwamba ujume umefika na kilichobaki wanasubiria ndege yao na kama haitaachiwa watafanya ubalozi huo ushindwe kutekeleza kazi zake za kila siku kwani wataandamana mpaka kieleweke. 

Kwa upande wake kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa alipofika kwenye ubalozi huo aliwataka waandamanaji kufuata sharia na kutojichukulia sharia mkononi kwani wanaweza kushitakiwa, aidha Jeshi la Polisi liliwatia nguvuni baadhi ya waandamanaji hao. 

Hadi maandamano hayo yanavunjwa hakuna kiongozi yeyote wa ubalozi huo aliyejitokeza kusikiliza hoja za waandamanaji bali walijifungia ndani huku baadhi ya wafanyakazi wakionekana kuchungulia madirishani kuona nini kinaendelea , na wengine wakipiga picha kwa kutumia simu zao za kiganjani. 
 Picha mbalimbali zikiwaonyesha waandamanaji walioandamana katika Ubalozi wa Afrika ya Kusini kushinikiza kuachiwa kwa ndege ya Shirika la ATCL inayoshikiliwa Jijiji Johanesberg nchini Afrika ya Kusini.


  

Jeshi la Polisi likitoa Maelekezo kwa waandamanaji walioandamana katika Ubalozi wa Afrika ya Kusini kushinikiza kuachiwa kwa ndege ya Shirika la ATCL inayoshikiliwa Jijiji Johanesberg nchini Afrika ya Kusini.


RAIS DKT. SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA WIZARA YA BIASHARA NA VIWANDA ZANZIBAR

$
0
0
Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameeleza kuwa nia ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kuhakikisha sauti za Wajasiriamali zinasikika na zinafanyiwa kazi ili kufikia malengo waliyoyakusudia.

Rais Dk. Shein aliyasema, Ikulu mjini Zanzibar alipokutana na uongozi wa Wizara ya Biashara na Viwanda wakati ilipowasilisha Mpango Kazi wa Julai 2018 hadi Juni 2019 sambamba na Mpango Kazi wa Utekelezaji kwa mwaka 2019/2020.

Alieleza kuwa matajiri walio wengi duniani walianza na ujasiriamali hivyo ni vyema wajasiriamali wakapewa kipaumbele katika shughuli zao wanazozifanya ili waweze kupata mafanikio na kufikia malengo yao waliyoyakusudia ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha kikamilifu katika maonesho ya kibiashara ya ndani na nje ya nchi.

Alieleza kuwa mbali ya matajiri hao duniani, hata hapa Zanzibar matajiri walio wengi wameanza na ujasiriamali hivyo, si jambo la busara kuwabeza  na badala yake ni vyema wakapema kipaumbele na mashirikiano ya kutosha. 

Aidha, Rais Dk. Shein alisisitiza haja ya kuwasaidia wajasiriamali ili na wao waweze kuwa wafanyabiashara wakubwa na kufikia malengo waliojiwekea jambo ambalo limeiibua Serikali katika kuhakikisha inawatekelezea matakwa yao na kuwashirikisha kikamilifu

Pamoja na hayo Rais Dk. Shein alitumia fursa hiyo kutoa pongezi kwa uongozi wa Wizara ya Biashara na Viwanda kwa kuwasilisha vyema Mpango Kazi wao na kueleza kuwa utendaji wao pamoja na wafanyakazi wa Wizara hiyo ndio uliopelekea kupata mafanikio 

Hivyo, Rais Dk. Shein aliutaka uongozi huo kuongeza kasi na kufanya kazi kwa bidii ili mafanikio zaidi yaendelee kupatikana katika kuimarisha sekta hiyo ambayo ina umhimu katika kuimarisha uchumi na kukzua sekta za kijamii.

Rais Dk. Shein alipongeza mafanikio makubwa yaliopatikana katika Wizara hiyo chini ya uongozi wa Waziri wake Balozi Amina Salum Ali ambaye amefanya juhudi kubwa ya kuiimarisha Wizara hiyo katika uongozi wake kwa mashirikiano ya pamoja na watendaji wake.

Dk. Shein aliutaka uongozi wa Wizara hiyo kuendelea kumsaidia Waziri wao huyo kila mmoja kwa wakati wake na nafasi yake kwa lengo la kuimarisha sekta ya biashara na viwanda kwani azma ya Serikali ni kuhakikisha Zanzibar inakuwa kwenye ramani ya viwanda.

Alieleza matumaini ya kuimarika kwa zao la mwani ambapo tayari kuna aina nne za mwani hapa Zanzibar na kueleza kuwa hatua hiyo itapelekea kupata mafanikio mazuri ya zao hilo ikiwa ni pamoja na mchakato wa kujenga kiwanda cha mwani huko Chamanangwe Pemba.

Alieleza kuwa Zanzibar ina historia kubwa ya kulima mazao mbali mbali yakiwemo ya viungo vya chakula kwa muda mrefu, hivyo ni vyema mazao hayo yakaimarishwa ikiwa ni pamoja na kuwashajiisha wakulima kuyalima vikiwemo viungo kama pilipili hoho.

Rais Dk. Shein alisisitiza haja ya kulima kwa wingi kwa viungo vya chakula kwa sababu vimekuwa vikipendwa sana nje ya nchi hivyo ni vyema kilimo hicho kikaimarishwa.

Aidha, alieleza kufarajika kwake na uongozi wa Wizara hiyo kwa kutumiwa alama ya ubora ya Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS) katika bidhaa mbali mbali zinazozalishwa ndani na nje ya nchi huku akieleza azma ya Zanzibar kuwa nchi ya viwanda.

Makamo wa Pili wa Rais  wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd alitoa pongezi kwa uongozi huo na kuzipongeza juhudi za Waziri Balozi Amani Salum Ali za kuhakikisha  maendeleo yanapatikana katika sekta ya viwanda na biashara ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa  Mamlaka inayosimamia Viwanda vidogo vidogo na Vya Kati (SMIDA).  

Nae Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee aliipongeza kazi nzuri ya uwasilishaji iliyofanywa na Wizara hiyo huku akisisitiza haja kwa uongozi huo kuendeleza mashirikiano na uadilifu.

Mshauri wa Rais wa Zanzibar Pemba Dk. Maua Abeid Daftari kwa upande wake alitoa pongezi kwa Shirika la Biashara la Taifa (ZSTC) kwa kuendeleza zao la mchaichai kisiwani Pemba kwani wananchi wengi wamehamasika na kuomba wasaidiwe kuwekewa vinu karibu na sehemu wanazoishi. 

Mapema Waziri wa Biashara na Viwanda Balozi Amina Salaum Ali akiwasilisha muhtasari wa utekelezaji Mpango Kazi wa Wizara hiyo alisema katika kipindi cha mwaka 2018/2019 jumla ya tani 218,911 za chakula muhimu ukiwemo mchele, sukari na unga wa ngano zilikuwepo kwa ajili ya matumizi ya soko la ndani na kuifanya Zanzibar kuendelea kuwa na chakula cha kutosha cha aina hizo katika kipindi chote.

Alieleza kuwa sensa ya viwanda iliyofanyika mwaka 2016 ilionesha idadi ya viwanda imeongezeka  ambapo sukari imeongezeka kutoka tani 677 iliyozalishwa mwaka 2017 hadi tani 3,339 kwa mwaka 2018 sawa na ongezeko la asimilia 79.7 na uzalishaji wa unga wa ngano nao uliongezeka kutoka tani 25,196 mwaka 2017 hadi tani 26,963 mwaka 2018.

Balozi Amina alieleza kuwa katika kipindi cha mwaka 2018/2019, Shirika la Biashara la Taifa limenunua karafuu tani 211.34 kwa jumla ya TZS Bilioni 2.9 ambapo pia uzalishaji wa mafuta ya mimea ulifikia kilo 40,955.3 kwa jumla ya TZS bilioni 1.5.

Alieleza kuwa Serikali inaendelea kununua karafuu kulingana na Sera ya Serikali ya kununua kwa bei ya asilimia 80 ya bei ya kuuzia nje hata hivyo, msimu mdogo wa karafuu kwa mwaka 2018/2019 ulipelekea kupungua kwa tani za ununuzi wa karafuu.

Kwa bajeti ya mwaka 2019/2020, alisema Wizara inakusudia kuimarisha maabara za ZBS zilizopo Amani pamoja na kuimarisha miundombinu, vifaa vya ukaguzi wa magari, kuliendeleza eneo la Nyamanzi sambamba na kuongeza vifaa kwa ajili ya matamasha.

Alieleza kuwa Wizara hiyo kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Indonesia inatarajia kufanya mafunzo ya ukulima wa mwani ulio na tija na kuanza maandalizi ya kuanzisha kiwanda cha kusarifu mwani huko Chamanangwe kisiwani Pemba.

Balozi Amina, alieleza mpango wa Wizara wa kusimamia program maalum ya wajasiriamali inayopata msaada kutoka mfuko maalum wa Nchi za Falme za Kiarabu pamoja na mchango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

Alisisitiza kuwa ili kurahisisha ufanyaji biashara hapa Zanzibar, Wizara itaandaa mfumo maalum wa Tehama ambao utatoa taarifa na huduma muhimu za usajili, uwekezaji na leseni au vibali vinavyotakiwa kwa wawekezaji na wafanyabiashara.  

Pia, uongozi huo ulieleza juhudi inazozichukua kwa wafugaji wa nyuki kwa kuwapa mafunzo maalum  wafugaji  hao sambamba na kusimamia vyema ufugaji huo kwa lengo la kupata asali yenye ubora na viwango vinavyohitajika kitaifa na kimataifa. 

Uongozi huo pia, ulimpongezi Rais Dk. Shein kwa utaratibu mzuri alioweka wa mikutano hiyo inayojadili Mpango Kazi wa Mawizara huku wakitumia fursa hiyo kueleza sifa inazozipata Zanzibar kutoka kwa wageni wanaokuja kuitembelea kutokana na amani, utulivu, upendo pamoja na maendeleo yaliopo. 

Uongozi huo pia, ulizitaja bidhaa zilizizothibitishwa ubora na kupatiwa alama ya ubora ya (ZBS) kwa mwaka 2018/2019 ni maji ya kunywa ya (Zan Aqua), mchele (Tulip) unaozalishwa nchini Pakistan, mchele wa (Ikram), unga wa sembe (Mwangaza), Mikate ya slesi, maji ya kunywa (Pure life) na (Uhai), mafuta ya nazi na mifuko.

 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar ,wakati wa mkutano wa Utekelezaji wa Bajeti na Mpango Kazi wa Wizara hiyo juazia mwezi  wa Julai 2018 hadi Juni 2019, uliofanyika ukumbi wa Ikulu Zanzibar , kushoto kwa Rais Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi na kulia kwa Rais Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee.(Picha na Ikulu)
 WAZIRI wa Biashara na Viwanda Zanzibar Mhe. Balozi Amina Salum Ali akiwasirisha mutasari wa Utekelezaji wa Bajeti na Mpango Kazi wa Wizara yake kwa mwezi wa Julai 2018 hadi Juni 2019, kulia Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Abdulhamid Yahya Mzee na kushoto Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Mhe. Hassan Khamis Hafidh, uliofanyika ukumbi wa Ikulu Zanzibar ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, hayupo pichani.
 MKURUGENZI wa Taasisi ya Viwango Zanzibar  (ZBS)  Ndg .Khatib Mwadin  akijibu swali wakati wa mkutano wa Utekelezaji wa Bajeti ya Mpango Kazi kwa mwezi Julai 2018 hadi Juni 2019, uliofanyika ukumbi wa Ikulu Zanzibar, ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, (hayupo pichani  kulia Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara Zanzibar (ZSTC) Dk. Said Seif Mzee
 NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar Bi. Khadija Khamis Rajab wa kwanza kushoto akisoma taarifa ya Utekelezaji Bajeti na Mpango Kazi ya Wizara yake kwa mwezi wa Julai 2018 hadi Juni 2018, wakati wa mkutano huo uliofanyika Ukumbi wa Ikulu Zanzibar ukiongozwa na Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein.
 BAADHI ya Watendaji wa Idara za Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar wakifuatilia taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti na Mpango Kazi kwa Wizara yao kwa mwezi wa Julai 2018 hadi Juni 2019, mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.
 MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) Ndg Maalim Kassim Suleiman, akizungumza wakati wa mkutano wa Utekelezaji wa Bajeti na Mpango Kazi wa Wizara ya Biashara na Viwanda kwa mwezi wa Julai 2018 hadi Juni 2019, uliofanyika ukumbi wa Ikulu Zanzibar, ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, hayupo pichani.
 MSHAURI wa Rais Pemba Mhe.Dk. Maua Abeid Daftari  akizingumza wakati wa mkutano wa Utekelezaji  wa Bajeti na Mpango Kazi  wa Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar uliofanyika ukumbi wa Ikulu Zanzibar, ukiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein. Hayupo pichani.
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi akizungumza wakati wa mkutano wa Utekelezaji wa Bajeti na Mpango Kazi wa Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar kwa mwezi Julai 2018 hadi Juni 2019, uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.(Picha na Ikulu) 


WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKUTANA NA WAZIRI MKUU WA MAURITIUS, PRAVIND KUMAR

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu wa Mauritius, Pravind Kumar kabla ya mazungumzo yao  kwenye  Ukumbi wa Maonyesho wa Pacifico Yokohama nchini Japan, Agosti 28, 2019. Wote wawili wako Japan kuhudhuria Mkutano wa  Saba wa Tokyo International Conference on Africa Development -TICAD 7.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na Waziri Mkuu wa Mauritius, Pravind Kumar kwenye ukumbi wa Maonyesho wa Pacifico Yokohama nchini Japan, Agosti 28, 2019. Wate wawili wanahudhuria Mkutano wa Saba wa Tokyo International Conference on Africa – TICAD 7.  Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi.


 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na Waziri Mkuu wa Mauritius, Pravind Kumar kwenye ukumbi wa Maonyesho wa Pacifico Yokohama nchini Japan, Agosti 28, 2019. Wate wawili wanahudhuria Mkutano wa Saba wa Tokyo International Conference on Africa – TICAD 7.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi (wa pili kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na maofisa kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Japan,   Hifadhi za Taifa Tanzania(TANAPA) na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) wakati alipotembelea banda la maonyesho la Tanzania kwenye Ukumbi wa Maonyesho wa Pacifico Yokohama nchini Japan, Agosti 28, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na maofisa kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Japan,   Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na Bodi ya Utalii Tanzania  (TTB) wakati alipotembelea  banda la maonyesho la Tanzania kwenye Ukumbi wa Maonyesho wa Pacifico Yokohama nchini Japan, Agosti 28, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MBUNGE SAME MAGHARIBI ATEKELEZA ILANI YA CCM JIMBONI KWAKE

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Same Magharibi mkoani Kilimajaro,Dk.Mathayo David Mathayo akimkabidhi Afisa elimu Kata, Ruth Kisaka Mifuko 250 ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na mabweni katika kata ya Msimbo wilayani Same, ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015-2020.
Mbunge wa jimbo la Same Magharibi mkoani Kilimajaro,Dk. Mathayo David Mathayo akimkabidhi fedha taslim Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mshewa, Anastazia Clement kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya kata hiyo ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015-2020.
Mbunge wa jimbo la Same Magharibi mkoani Kilimajaro,Dk.Mathayo David Mathayo akimkabidhi fedha taslimu diwani wa CCM kata ya Mhezi wilayani Same John Kiure kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya kata hiyo.
Mbunge wa jimbo la Same Magharibi mkoani Kilimajaro,Dk.Mathayo David Mathayo akihutubia wananchi. 
MBUNGE wa Jimbo la Same Magharibi CCM, Dk. Mathayo David Mathayo amewaomba wananchi wa Jimbo la Same Magharibi kumuunga mkono na kumuombea afya njema Rais John Magufuli ili aweze kuendelea kuiongoza Tanzania izidi kupata maendeleo na kurudisha nidhamu katika sekta mbalimbali nchini.

Dk.Mathayo ametoa kauli hiyo katika siku ya kwanza ya ziara yake ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020 kama alivyoahidi wakati akiomba ridhaa ya kuwaongoza wananchi wa jimbo hilo ambapo akizungumza na wananchi wa kata za Msindo,Mshewa na Mhezi, Mathayo amesema serikali ya awamu ya tano imeonesha mafanikio lukuki katika Nyanja mbalimbali.

Aidha Mbunge huyo amekabidhi vifaa mbalimbali alivyoahidi katika kata hizo zikiwemo Fedha, saruji na mabomba ya kusambazia maji huku akitoa rai kwa uongozi wa kila Kata kuhakikisha vifaa hivyo vinatumika ndani ya kipindi cha miezi mitatu.

Katika Kata ya Msindo Dk. Mathayo ametoa fedha ,mifuko ya saruji,mabomba ya maji,ambapo katika kata ya Mshiwa amekabidhi mifuko ya saruji na fedha taslimu kwa ajili ya shughuli za marendeleo kiasi cha shilingi milioni 13 laki 9 na Zaidi ya shilingi million tisa katika kata ya Mhezi Zaidi ya shilingi milioni tisa na mifuko ya saruji.

WAZIRI SIMBACHWENE AFUNGUA MKUTANO WA 5 WA KISAYANSI JUU YA UTUNZAJI ENDELEVU WA MAZINGIRA

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. George Simbachawene ameziagiza Mamlaka zote za Serikali Nchini  kuanzia Mamlaka za Mikoa mpaka mamlaka za Vijiji kuweka utaratibu wa kutumia ardhi kwa ajili ya kuhifadhi misitu ili kuweza kutunza mazingira  . Ameyasema hayo jijini Arusha wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 5 wa Kisayansi juu ya utunzaji endelevu wa Mazingira ambapo alikua Mgeni Rasmi.

Amesema kuwa Elimu izidi kutolewa kwa Wananchi ili kuweza kupata uelewa zaidi juu ya maeneo ya uhifadhi wa misitu ambayo yametengwa.. Aliyataja maeneo hayo kuwa ni Serengeti-Ngorongoro, Ziwa Manyara, East Usambara, Jozani Chwaka-Zanzibar na Gombe-Masito-Ugalla. Alisema kuwa maeneo hayo yametengwa kuwa maeneo ya hifadhi kwa sababu ya ikolojia na bayonuai iliyopo katika maeneo hayo. Kwa sasa maeneno hayo yanapata changamoto kwa kuvamiwa na shughuli za Binadamu hivyo kusababisha uharibifu katika maeneo hayo ya hifadhi.

Alisema kuwa ni vema kila  Mtanzania kujua umuhimu wa mazingira na hivyo kuweza kulinda na kuhifadhi maeneo maalumu yaliyotengwa kwa ajili ya hifadhi, na pale yalipoharibiwa basi parejelezwe kwani kwa kufanya hivyo ni kutunza mazingira.  

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. George amefungua Mkutano huo wa 5 wa Kisayansi juu ya utunzaji endelevu wa Mazingira ambao umeandaliwa na Baraza la Usimamizi wa hifadhi ya Mazingira (NEMC) na umefanyika katika kumbi za Mikutano za AICC jijini Arusha.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mheshimiwa George Simbachawene akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 5 wa kisayansi  juu ya utunzaji endelevu  wa Mazingira ulioandaliwa na Baraza la usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira (NEMC)  jijini Arusha.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mheshimiwa George Simbachawene akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira (NEMC) Dkt Gwamaka Mafwenga wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 5 wa kisayansi  juu ya utunzaji endelevu  wa Mazingira uliofanyika katika kumbi za AICC jijini Arusha.
 Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa  Mkutano wa 5 wa kisayansi  juu ya utunzaji endelevu  wa Mazingira ambaye Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mheshimiwa George Simbachawene (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Mkutano huo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mheshimiwa George Simbachawene akiongea jambo na Mwenyekiti wa Kamati  ya kudumu ya  Bunge ya Viwanda , Biashara na Mazingira Mh. Suleiman Saddiq wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 5 wa kisayansi  juu ya utunzaji endelevu  wa Mazingira uliofanyika katika kumbi za AICC jijini Arusha.

Airtel Africa crosses the 100 million subscribers milestone

$
0
0
Airtel Africa, a leading telecommunications services provider with operations in 14 countries across Africa, today announced that it has crossed the 100 million customers mark across its operations. Airtel Africa is the second largest mobile operator in Africa by number of active subscribers.

Commenting on this milestone achievement, Raghunath Mandava, Airtel Africa’s Chief Executive Officer, said: “I am delighted to report that Airtel Africa has crossed the 100 million subscriber mark. 

This achievement is testament to the hard work of our employees and a clear reflection that customers value our network, service offerings and customer experience. 

The positive momentum we have seen in customer acquisition, further underpins our medium-term aspirations for revenue and profit growth. I would like to take this opportunity to thank all the teams that have worked hard to get us here.”

Airtel Africa’s footprint is characterized by low but increasing mobile connectivity, with a unique user penetration at 43%, highlighting the potential for growth across its footprint.

The company believes in enhancing connectivity and digitizing the countries in which it operates and has invested to expand its network footprint and number of 4G sites to enhance network capabilities and support its future business growth.

A combination of an under-penetrated telecom market, a young addressable population and rising smartphone affordability, along with low data penetration and an underbanked population, will drive the growth opportunities for the data and mobile money segments moving forward.

WAZIRI MKUU AMWAKILISHA MAGUFULI KATIKA MKUTANO WA TICAD 7

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiwa katika picha ya pamoja na viongozi waku wa Nchi za Afrika na Japan katika ufunguzi wa Mkutano wa Saba wa Tokyo International Conference on Africa Development (TCAD 7) uliofanyika kwenye Ukumbi wa hoteli ya Pacifico Yokohama nchini Japan, Agosti 28, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Rais waTogo,  Faure Gnassingbe (kulia)  wakipiga makofi katika ufunguzi wa Mkutano wa Saba wa Tokyo International Conference on Africa Development (TCAD7) uliofunguliwa na Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe kwenye Ukumbi wa hoteli ya Pacifico  Yokohama nchini Japan, Agosti 28, 2019. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na viongozi  Wakuu wa Nchi za Afrika wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa  Saba wa  Tokyo International Conference on Africa Development (TCAD7) uliofunguliwa na Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe kwenye Ukumbi wa hoteli ya Pacifico  Yokohama nchini Japan, Agosti 28, 2019. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi (kushoto) wakisikiliza hotuba ya  ufunguzi wa  Mkutano wa  Saba wa Tokyo International Conference on Africa Development (TCAD7) uliofunguliwa na Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe kwenye Ukumbi wa hoteli ya Pacifico  Yokohama nchini Japan, Agosti 28, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Bella apeleka usiku wa masauti Nefaland Jumamosi

$
0
0
Na Mwandishi wetu

Dar es Salaam.  Mwanamuziki nyota wa muziki wa dansi nchini, Christian Bella na bendi yake ya Malaika, wameibuka na wimbo mpya ujulikanao kwa jina la Pacha ambao utatambulishwa Jumamosi kwenye hotel ya Nefaland ya Magomeni Kagera.

Bella ambaye alianza kutamba na wimbo wake, Yapo Wapi Mapenzi akiwa na bendi ya Akudo Impack, ameweza kuliteka soko la muziki wa dansi kwa nyimbo zake mbalimbali ambazo bado zinapendwa katika muziki wa dansi.

Nyimbo hizo ni Nani Kama Mama,  Nishike, Nashindwa, Msaliti, Usilie, Niende Wapi, Nakuhitaji, Rudi, Pambe na Boss ambaye alimshirikisha mrembo, Hamisa Hassan Mobetto.

Mbali ya nyimbo hizo, pia Bella ameweka historia katika muziki wa dansi nchini kwa kuweza kumshirikisha mwanamuziki nyota barani Afrika, Ngiana Makanda maarufu kwa jina la Werrason katika wimbowake wa Moyo.

Pia Bella ameweza kumshirikisha nyota nyingine ya muziki Wa dansi, Fally Ipupa ujilikanao kwa jina Starehe. Mbali na Fally Ipupa na Werrason, Bella pia amemshirikisha mwanamuziki wa Bongo Fleva, John Makini katika wimbo wake wa Niende Wapi.

Mratibu wa onyesho hilo, Bakari Seif alisema kuwa onyesho hilo litaanza saa 2.00 jioni ili kutoa nafasi kwa mashabiki wa muziki wa dansi nchini kupata burudani inayoendana na kiingilio chao.

Alisema kuwa wanatarajia kupata shoo yenye ubora wa aina yake kwani Bella na wanamuziki wenzake wamejiandaa vilivyo.

“Hili ni onyesho maalum kwa mashabiki wa muziki wa dansi ambao wamekuwa wakimsubiri kwa hamu Christian Bella na bendi yake ya Malaika. Kwa mara ya kwanza, Bella ataimba nyimbo zake zote anazotamba nazo,” alisema Seif.

Tafiti Saba zilizofanywa na JKCI kuwasilisha nchini Zambia

$
0
0
Na Ales Mbilinyi – JKCI
Tafiti saba za magonjwa ya moyo zilizofanywa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) zinatarajiwa kuwasilishwa katika mkutano wa wanasayansi, madaktari bingwa na wahudumu wa afya wanaotoka katika nchi za ukanda wa Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika utakaofanyika wiki ijayo nchini Zambia.

Tafiti hizo ambazo zimefanyika mwaka jana na mwaka huu ni kuhusu mwenendo wa mapigo ya moyo kwa mgonjwa, wagonjwa wenye moyo ambao uwezo wake wa kufanya kazi umepungua jinsi wanavyozingatia matibabu kama walivyoshauriwa na madaktari, shinikizo la damu na tatizo la kisukari.

Tafiti nyingine zitakazowasilishwa ni upungufu wa nguvu za kiume katika jamii, uelewa wa sababu hatarishi za magonjwa ya moyo katika jamii, magonjwa matatu kwa pamoja yaani moyo na figo kushindwa kufanya kazi na upungufu wa damu mwilini.

Akizungumza kuhusu tafiti hizo Mkuu wa Kitengo cha Utafiti wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Pedro Pallangyo alisema tafiti hizo zimefanyika katika mkoa wa Dar es Salaam kwa kipindi cha miaka miwili na na kwa wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi hiyo.

“Tumekuwa tukifanya tafiti mbalimbali kuhusu magonjwa ya moyo ambazo zinatusaidia kufahamu wagonjwa wetu pamoja na wananchi wanaotuzunguka wanakabiliwa na matatizo gani katika afya za moyo na hii inatusaidia kuweza kuboresha huduma zetu”,.

Akizungumza kuhusu mkutano huo wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza Dkt. Pedro alisema kwa upande wa magonjwa ya moyo utawasaidia kubadilishana matokeo ya huduma za matibabu wanazozitoa hasa tafiti zinazofanywa katika nchi mbalimbali ili kuboresha huduma zinazotolewa kwa wagonjwa. Kwa upande wake Afisa uuguzi wa JKCI Jalack Milinga ambaye alishiriki katika kufanya tafiti hizo alisema kwake ni mara ya kwanza kuhudhuria mkutano huo ambao utamsaidia kuongeza ujuzi katika utoaji wa huduma kwa wagonjwa wa moyo lakini pia kubadilishana uzoefu na wauguzi wenzake watakaoshiriki katika mkutano huo.

“Utafiti wangu uliangalia jinsi ya uzingatiaji wa unywaji wa dawa za moyo kwa wagonjwa ambao mioyo yao haifanyi kazi vizuri. Hivyo naamini ushiriki wangu katika mkutano huu utaniwezesha kupata mbinu mpya za kusimamia jukumu la kuwasaidia wagonjwa wetu kuzingatia matibabu ili kupata matokeo bora ya tiba”, alisema Jalack.

Naye daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa JKCI Smita Bhalia alisema ushiriki wa wataalamu kutoka Tanzania umelenga kutoa matokeo ya utafiti uliofanywa hapa nchini na kuonesha baadhi ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza jinsi yanavyoweza kusababisha magonjwa ya moyo ama magonjwa ya moyo yanavyoweza kupelekea mtu kupata magonjwa mengine yasiyo ya kuambukiza.

Malengo ya mkutano huo ni kwa nchi washiriki kutoka ukanda wa Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika kuona jinsi ya kushirikiana katika kufanya tafiti za ndani, kuwa na njia bora na za kisasa za matibabu ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza na kuwa na mbinu mpya za kuweza kuzia magonjwa hayo.

Mkutano huo ambao hufanyika kila mwaka unatarajia kufayika mjini Living stone nchini Zambia kuanzia tarehe tano hadi saba mwezi ujao ambapo mwaka jana mkutano kama huo ulifanyika jijini Nairobi nchini Kenya. 
  Mkuu wa Kitengo cha Utafiti kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Pedro Pallangyo akiwaeleza wafanyakazi wa Taasisi hiyo (hawapo pichani) kuhusu tafiti saba za magonjwa ya moyo zilizofanywa na Taasisi hiyo ambazo zitawasilishwa katika mkutano wa kimataifa wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza utakaofanyika wiki ijayo nchini Zambia.
 Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Happiness Swai akiwaeleza wafanyakazi wa Taasisi hiyo (hawapo pichani) kuhusu utafiti wa shinikizo la damu na tatizo la kisukari uliofanywa na Taasisi hiyo ambao ni moja ya tafiti saba za magonjwa ya moyo ambazo zitawasilishwa katika mkutano wa kimataifa wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza utakaofanyika wiki ijayo nchini Zambia.
Wataalamu wa Afya kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambao walifanya tafiti saba za magonjwa ya moyo ambazo zitawasilishwa katika mkutano wa kimataifa wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza utakaofanyika wiki ijayo nchini Zambia wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzielezea tafiti hizo kwa wafanyakazi wa Taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam. Picha na JKCI

RC MAKONDA ATOA NENO KWA SHERIA YA MIRATHI YA MWAKA 1865 INAYOTUMIKA HADI SASA

$
0
0

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema kuwa baada ya kukutana na wajane zaidi ya 5000 Aprili mwaka huu na kusikiliza kero zao kamati iliyoundwa kushughulikia kero hizo imegundua kuwa sheria zinazotumika katika suala zima la mirathi ni kandamizi na za muda mrefu hivyo hazina budi kubadilishwa ili wajane na wagane wapate haki zao kwa urahisi.

Kufuatia suala hilo Makonda amesema kuwa wanatarajia kuwasilisha muswada wa mapendekezo ya  mabadiliko ya sheria ya mirathi na sheria ya ndoa kwa waziri wa katiba na sheria ili ziweze kufanyiwa marekebisho na hiyo ni kutokana na sheria hizo kupitwa na wakati na kuonekana kuwa kandamizi kwa wanawake pindi waume zao wanapofariki.

Makonda amesema kuwa miongoni mwa sheria kandamizi zinazotakiwa kufanyiwa mabadiliko ni sheria ya kiserikali ya mirathi ya mwaka1865 ambayo ilichukuliwa kutoka nchini India, Sheria ya mirathi ya kimila ya mwaka1963, sheria ya watoto na sheria ya mirathi ya kidini ya mwaka1963 ambazo kimsingi zimeonekana kuwa na mpungufu makubwa ikiwemo kumhesabu mwanamke Kama sehemu ya mali na kuchanganya msimamizi wa mali na mrithi na sheria nyingine kuonekana zimepitwa na wakati.

Aidha Makonda amevitaja vipengele vilivyopendekezwa kufanyiwa maboresho ni pamoja na kumpa uhalali mke wa marehemu kushiriki katika vikao vya mgawanyo wa mali, mjane kupewa haki ya kurithi na kusimamia mali za marehemu, mjane kutoondolewa kwenye nyumba na mali kutohamishwa hadi maamuzi ya mahakama yatakavyotolewa, usawa wa watoto katika kumiliki mali za marehemu bila kujali jinsia pamoja haki ya mtoto wa nje ya ndoa kurithi mali.

Vifungu vingine ambavyo vimeelezwa kuwa ni kandamizi kwa wajane ni pamoja na kile kinachoruhusu mjane kurithiwa na  kumnyima mjane haki ya  kurithi ardhi ya ukoo.

Makonda amesema kuwa hayo yote ni chimbuko la kongamano la wajane zaidi ya 5000 lililofanyika mwezi April mwaka huu ambapo katika kongamano hilo alipokea kero na malalamiko mbalimbali kutoka kwa wajane jambo lililopelekea kuunda kamati iliyoshirikisha wadau na wataalamu mbalimbali kutoka serikalini na asasi za kiraia ambao waliopitia malalamiko hayo na kutoka na mapendekezo hayo.

Mapendekezo hayo yatapelekwa kwa Waziri wa katiba na sheria ambaye atapeleka muswada bungeni ili sheria hizo ziweze kujadiliwa na kubadilishwa ili wajane na wagane wapate haki zao za msingi.
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images