Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110185 articles
Browse latest View live

MISS TANZANIA KUPATIKANA AGOSTI 23 MWAKA HUU ...MWANUKUZI ATOA NENO

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

MKURUGENZI wa Kampuni ya The Look ambayo inayosimamia mashindano ya urembo nchini (Miss Tanzania) Basila Mwanukuzi Shayo amesema fainali za mashindano hayo yatahitimishwa rasmi Ijumaa ya Agosti 23 mwaka 2019, ukumbi wa Millenium Tower LAPF uliopo Makumbusho jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Mwanukuzi amesema washiriki wapatao 20 kutoka mikoa mbalimbali nchini wapo kambini tangu Agosti 12 mwaka huu wakijiandaa na kinyang'anyiro cha kuwania taji hilo.

"Kufanyika kwa fainali hizi ni hitimisho ya mashindano ya Mikoa ambayo yalifanyika kuanzia mwezi April mwaka huu" ameeleza.

Amesema kwa kipindi walichokuwa kambini washiriki wameshiriki shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kutembelea, kuwafariji na kucheza michezo mbalimbali na watoto katika kituo cha watoto yatima kilichopo Mbezi mwisho jijini Dar es Salaam na kufanya shughuli nyingine za kijamii.

"Washiriki wakiwa kambini wamepata pia nafasi ya kufanya mashindano madogo madogo kwa mujibu wa mashindano ya dunia ambapo walifanya mashindano ya kumtafuta mrembo mwenye kipaji.

"Mrembo mwenye mvuto katika picha, mrembo mwanamitindo, mrembo mwanamichezo na mrembo chaguo la watu, na washindi watatangazwa siku ya tukio" ameeleza Mwanukuzi.

Mashindano hayo yanategemewa kuwa ya aina yake ambapo wananchi wameombwa kujitokeza kwa wingi kujipatia tiketi zao ili kumshuhudia mlimbwende atakayeliwakilisha Taifa katika mashindano ya urembo ya dunia.
 Washiriki wa shindano la Miss Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Mkurugenzi wa Kampuni ya The Look ambayo inayosimamia mashindano ya urembo ya Miss Tanzania nchini, Basila Mwanukuzi Shayo (katikati) akiwa na baadhi ya wadhamini wa shindano hilo pamoja na warembo hao (waliosimama) leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya The Look, Basila Mwanukuzi Shayo (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mashindano ya urembo ya Miss Tanzania yanayotarajiwa kufanyika Ijumaa wiki hii, ambapo ameeleza kuwa maandalizi yapo tayari na mashindano yatakuwa ya aina take, leo jijini Dar es Salaam.


MBUNGE GULAMALI AMPONGEZA RAIS DK.MAGUFULI KUWA MWENYEKITI SADC

$
0
0
Na Ripota Wetu, Michuzi Blogu

MBUNGE Jimbo la Manonga lililopo Igunga mkoani Tabora Seif Gulamali amempongeza Rais John Magufuli kwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na kuufanikisha kuumalizika vema kwa mkutano mkuu wa SADC uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi habari kwa nyakati tofauti Gulamali amesema anampongeza Rais Magufuli na watanzania wote kutokana na lugha ya Kiswahili kuchaguliwa kuwa moja ya lugha itakayotumiwa katika mikutano ya SADC, suala alilosema litazidi kulitangaza taifa la Tanzania.

Amesema kitendo cha Rais Magufuli kuwa Mwenyekiti mpya wa SADC katika mkutano huo kunazidi kuiletea heshima Tanzania ambayo tangu ilipopapata uhuru wake mwaka 1961 imeendelea kuwa kitovu kikuu cha amani miongoni mwa mataifa ya Bara la Afrika na Dunia kwa ujumla. 

"Pamoja na kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa SADC, pia mkutano huo wa wakuu wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo ulifana chini ya uenyeji wake na hotuba yake ikigusia maeneo muhimu kwa ajili ya maendeleo ya jumuiya hiyo.

"Jambo hili litazidi kuhimarisha umoja na mshikamano wa nchi hizo kama alivyokuwa ameligusia katika hotuba yake alipokuwa akifunga mkutano huo,"amesema.

Mbunge huyo amesema kauli ya Rais Magufuli kueleza kuwa Tanzania ipo tayari kutoa ushirikiano unaohitajika kwa wanachama wa SADC ili kuharakisha jitihada za kuleta maendeleo fungamani, linaonesha ni kwa namna gani kiongozi huyo ana kiu ya kuziona nchi zote zilizomo ndani ya SADC zinapiga hatua zaidi za kimaendeleo kama alivyo na kiu hiyo kwa Tanzania .

Amesema pamoja na kuzitaka nchi wanachama kutoa kipaumbele katika suala zima la usalama, amani na utulivu pia alizitaka kuboresha eneo la ukuaji wa viwanda, biashara na utengenezaji wa fursa za kibiashara.

Hili ni jambo muhimu katika uzalishaji wa ajira na maendeleo yake na wananchi kwa ujumla.Ukweli anastahili pongezi kwa kuliona hilii,"amesema Gulamali.

Ameongeza kimsingi mambo mengi ambayo Rais Magufuli amegusia katika hotuba yake hiyo yanaakisi yale anayoendelea kuyafanya hapa nchini ambayo kwa kiasi kikubwa matokeo yake yanaonekana kwa kadri siku zinavyozidi kwenda.

Pia amesema hatua ya Rais Magufuli kuzitaka nchi wanachama wa jumuiya hiyo kuweka mkazo katika usimamizi wa rasimali zake una maana kubwa katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi miongoni mwa nchi wanachama.

Kuhusu lugha ya Kiswahili kuchaguliwa kuwa miongoni lugha rasmi ya nne kutumika SADC, Mbunge huyo amesema ni fahari kwa Tanzania kwani itazidi kulitangaza Taifa na kuzidi kuliletea heshima.

"Tunaamini lugha ya Kiswahili itaendelea kuzungumzwa na nchi nyingi duniani kama ambavyo tumeshuhudia nchi kadhaa zinazungumza lugha hii adhimu,"amesema.

Uhalifu wapungua nchini-Serikali

$
0
0
Serikali imesema katika kipindi cha Januari hadi Juni mwaka huu nchi imeendelea kuwa katika amani na utulivu huku uhalifu ukipungua kwa asilimia 2.2 kwa makosa makubwa ya jinai ukilinganisha na kipindi kama hicho kwa mwaka uliopita hali inayopelekea wananchi kuendelea na shughuli za kiuchumi kwa amani na usalama.

Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati akisoma taarifa ya Serikali mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, iliyohusu Hali ya Ulinzi na Usalama wa Raia na Mali zao kwa Kipindi cha mwezi Januari hadi Juni mwaka huu ikiwemo utekelezaji wa dhana ya Ulinzi Shirikishi.

“Kuanzia Januari hadi Juni ndani ya mwaka huu jumla ya makosa makubwa ya jinai yaliyoripotiwa katika vituo vya polisi nchi nzima yalikuwa 28,252 tofauti na kipindi kama hiki mwaka uliopita ambapo makosa 28,889 yaliripotiwa vituoni, tukiangalia vizuri hesabu zetu ndani ya mwaka huu tumepunguza makosa 637 hii yote inatokana na juhudi za askari wetu na utekelezaji wa dhana ya ulinzi shirikishi” alisema Masauni

Naibu Waziri Masauni ameyataja makosa hayo makubwa ya jinai kuwa ni Makosa dhidi ya binadamu, Makosa dhidi ya Maadili ya Jamii, Makosa ya kuwania mali na Makosa ya Uhalifu wa Kifedha

Akizungumzia makosa ya usalama barabarani Naibu Waziri Masauni amesema kumekuwepo na mafanikio katika kupunguza makosa ya usalama barabarani hali inayochagizwa na usimamiaji wa sheria na kutoa elimu ya usalama barabarani kwa watumiaji wa vyombo vya moto na watembea kwa miguu..

“Takwimu za makosa ya ajali za barabarani katika kipindi cha Januari hadi Juni mwaka huu zinaonesha kuwepo kwa jumla ya makosa 1,610 yaliyoripotiwa ikilinganishwa na makosa 2,200 mwaka uliopita huku takwimu zikiweka wazi makosa 590 kupungua katika vipindi hivyo viwili” alisema Masauni

Alisema kutokana na kupungua kwa makosa ya barabarani hata idadi ya ajali zilipungua hali iliyopelekea kupungua kwa vifo kwani mwaka jana watu 1,051 walifariki tofauti na mwaka huu ambapo kuanzia mwezi Januari mpaka Juni watu 781 walipoteza maisha.

Akizungumza wakati wa kikao hicho Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro alisema mafanikio hayo ya kupungua kwa uhalifu nchini yamechangiwa pia na matumizi ya teknolojia katika kupambana na uhalifu huku akiwaonya wahalifu kutafuta shughuli nyingine ya kufanya.

“Tunatumia vifaa maalumu ikiwepo drones katika kudhibiti uhalifu japo kwasababu za kiintelijinsia hatuwezi kusema ziko ngapi na maeneo gani muhimu tunawaasa wahalifu kuacha mipango yao ya kuvuruga amani ya nchi hii nawahakikishia hawatabaki salama,tunataka wananchi wafanye shughuli zao za kiuchumi” alisema IGP Sirro

Vikao vya Kamati za Bunge zinaendelea jijini Dodoma huku wizara mbalimbali zikiwasilisha taarifa zao kwa kamati hizo huku vikao vya Bunge vikitarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwezi ujao.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, akisoma taarifa ya Hali ya Ulinzi na Usalama nchini mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nje, Ulinzi na Usalama (hawapo pichani),wakati wa kuwasilisha taarifa hiyo leo jijini Dodoma.Kushoto ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu,akitoa ufafanuzi unaohusu utendaji wa Taarifa ya Hali ya Ulinzi na Usalama nchini mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nje, Ulinzi na Usalama (hawapo pichani), wakati wa kuwasilisha taarifa hiyo leo jijini Dodoma.Kulia  ni Naibu Waziri wa wizara hiyo,Mhandisi Hamad Masauni.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akizunguma wakati wa uwasilishaji wa Taarifa ya Hali ya Ulinzi na Usalama nchini mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nje, Ulinzi na Usalama (hawapo pichani), wakati wa kuwasilisha taarifa hiyo leo jijini Dodoma. 

DK.SHEIN AKUTANA NA MRATIBU MKAAZI WA UMOJA WA MATAIFA

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na  Mratibu Mkaazi wa Umoja wa Mataifa Nchini Tanzania Bw.Alvaro Rodrigues leo alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa ajili ya kumuaga Rais baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini.[POicha na Ikulu.] 20/08/2019.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Mratibu Mkaazi wa Umoja wa Mataifa Nchini Tanzania Bw.Alvaro Rodrigues alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kwa ajili ya kumuaga Rais baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini.[POicha na Ikulu.] 20/08/2019.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akifuatana na mgeni wake Mratibu Mkaazi wa Umoja wa Mataifa Nchini Tanzania Bw.Alvaro Rodrigues baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika leo alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa ajili ya kumuaga Rais baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini.[

MWAKILISHI WA UNFPA AKUTANA NA DK.SHEIN

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Mwakilishi wa UNFPA Nchini Tanzania Ms.Jacqueline Mahon alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kwa ajili ya kumsalimia Rais [Picha na Ikulu.] 20/08/2019.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Mwakilishi wa UNFPA Nchini Tanzania Ms.Jacqueline Mahon (katikati)alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kwa ajili ya kumsalimia Rais akiwa na ujumbe aliofuatana nao 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akimsikiliza mgeni wake Mwakilishi wa UNFPA Nchini Tanzania Ms.Jacqueline Mahon wakati wa mazungumzo alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kwa ajili ya kumsalimia Rais
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akifuatana na mgeni wake Mwakilishi wa UNFPA Nchini Tanzania Ms.Jacqueline Mahon baada ya mazungumzo yao alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kwa ajili ya kumsalimiana [Picha na Ikulu.] 20/08/2019.

TCRS KUJA NA MTAALA WA KUWAFUNDISHA BIASHARA WAMACHINGA

$
0
0
Meneja wa TCRS Mkoa wa Morogoro, Rehema Samweli, akizungumza wakati wa semina ya kujadili kuhusu kuanzishwa kwa mataala wa wafanya biashara ndogo ndogo. Picha na Victor Makinda


NA VICTOR MAKINDA: MOROGORO

Taasisi isiyo ya kiserikali iyoshughulika na masuala ya wakimbizi ya Tanzania, TCRS, ipo mbioni kuja na mtaala wa elimu kwa ajili ya kuwafundisha mbinu sahihi za biashara, wafanya biashara ndogo ndogo maaraufu kama machinga.

Akizungumza wakati wa semina ya kujadili uanzishwaji wa mitaala kwa ajili ya wafanyabiashara ndogo ndogo, iliyofanyika juzi mjini Morogoro, Meneja wa TCRS mkoa wa Morogoro, Rehema Samweli, alisema kuwa wao kama taasisi wamefanya tafiti na kubaini mapungufu mengi sambamba na changamoto nyingi zinazo kabili kundi la wafanya biashara ndogo ndogo.

“ Tumefanya utafiti mara tatu katika mikoa ya Morogoro, Dar es Salaam na Dodoma na tumebaini changamoto nyingi zinazo wakabili wafanya biashara ndogo ndogo na hivyo kwa sasa tunakusanya maoni ya wadau mbali mbali ili tuje na mtaala maalumu kuwafundisha wafanya biashara ndogo ndogo mbinu bora za biashara ili waweze kujikwamua wao wenyewe na kuchangia katika pato la Taifa. Alisema Rehema.

Akitaja baadhi ya changamoto zinazowakabili wafanya biashara ndogo ndogo ambazo wamezibaini katika utafiti wao walioufanya kwa ufadhiri wa shirika la TCRS, Dkt Wambuka Rangi, Mtafiti kutoka Chuo Kikuu Huria Tanzania, alisema kuwa changamoto kwa wafanya biashara ndogo ndogo ni kutokuwa na elimu ya kuweka kumbukumbu za biashara zao, ikiwa ni pamoja na kujua kiasi gani kimetumika kununua bidhaa na biadhaa hiyo iuzwe shilingi ngapi ikiwa na mchanganuo wa faida au hasara.

“ Wafanya biashara ndogo ndogo, katika utafiti tulioufanya tumebaini kuwa wengi wao hawajui ni namna gani watapata mikopo ya riba nafuu na hivyo hukopa mikopo yenye riba kubwa ambayo haina tija kwao. Tumebaini kuwa wengi wao hawajui masuala ya afya na usafi wao na mazingira, hawajui sheria ndogo ndogo za miji na majiji, ,hawafanyi utafiti wa kubaini soko gani linahitaji bidhaa gani, hawatumii lugha nzuri ya kumvutia mteja lakini pia tumebaini kuwa hawana nidhamu ya fedha sambamba na elimu ya kujitambua na kujikubali.” Alisema Dkt Wambuka.

Haya na mengine mengi ndiyo masuala hasa yanayotupelekea kuja na mtaala maalumu wa kuwafundisha wafanya biashara ndogo ndogo ili waweze kuwa na elimu na maarifa ya kufanya biashara kwa tija ili waboreshe maisha yao na jamii yao kwa ujumla.

Kwa upande wake mshiriki wa semina hiyo, Chuwa Haruni, ambaye ni mwenyekiti wa kikundi cha wafanyabiashara ndogondogo cha Umoja Group cha mjini Morogoro, alilipongeza wazo hilo la TCRS kuja na mitaala kwa ajili ya kuwafundisha wafanya biashara hizo huku akisema mtaala huo utakuwa ni mkombozi mkubwa kwao.

“ Ni kweli sisi wafanya biashara ndogo ndogo hatuna elimu yoyote ya biashara. Tunafanya biashara pasipo elimu wala ujuzi. Tunahitaji sana elimu juu ya nmna sahihi ya kufanya bisahara ambayo itatupa mwongozo wa kufanya biashara zetu kwa tija.” Alisema Chuwa.

Naye Haji Sajilo Mfanyabisahara ndogo ndogo wa Manispaa ya Morogoro alisema kuwa elimu ya biashara ni muhimu mno kwa wafanya biashara ndogo ndogo kwani wengi wao wanakabiliwa na tautizo la kutotunza kumbukumbu na hivyo wanafanya bishara kwa mazoea huku wakiwa hawajui ipi faida na ipi hasara na mwisho wake kuishia kufilisika,

“ Mtaala huo ni mzuri sana. Ninaomba uje haraka, tena haraka sana. Ni elimu ambayo itatutoa hapa tulipo na kutupeleka hatua nyingine. Mali bila daftari hupotea. Tukifundishwa njia sahihi ya namna ya kutunza kumbukumbu itatujengea uwezo wa kufanya biashara kwa faida na kuzalisha faida. Kwa sasa tunahangaika tu huku tukiwa hatuna mbinu, maarifa na elimu ya biashara ndio sababu unaweza kuona wafanya biashara ndogo ndogo 50 wote wanauza Radio. Ni kwa ajili ya kukosa mbinu na ubunifu hivyo hata biashara zetu ni za kuigana.

Afisa tawala msaidizi Wilaya ya Morogoro, Yahya Mohamed, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya katika semina hiyo, alisema kuwa mtaala huo utawapunguzia kazi wao viongozi kwa kuwa utakuwa umewapa mwanga mkubwa wafanya biashara ndogo ndogo kujua sheria za miji na majiji na hivyo kuwaondolea kazi ya kukimbizana nao kila uchao kwa kuwa wafanya bishara ndogo ndogo wamekuwa ni wakaidi wa sheria.

“Itatusaidia sana sisi kama Wilaya kwa kuwa tutakuwa na wafanya bisahara watakao kuwa na uwelewa wa sheria na taratibu. Lakini pia hii itawaondolea hasara wanazozipata mara kwa mara kwa kutojua namna ya kutunza kumbukumbu na elimu juu ya mikopo. Wazo lenu TCRS ni zuri na sisi kama serikali tunalipongeza na tunaomba mlitekeleze kwa kuwa tija yake ni tija ya Taifa kwa ujumla.” Alisema Yahya.

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI ATEMBELEA MAMLAKA YA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo toka kwa Meneja wa Kitengo cha Sayansi Jinai, Biolojia na Vinasaba Bi. Hadija Saidi Mwema alipotembelea Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali jijini Dar es salaam leo Agosti 20, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wagonjjwa na wafanyakazi katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road wakati akitembelea Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali jijini Dar es salaam leo Agosti 20, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembezwa kukagua sehemu mbali mbali za Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali jijini Dar es salaam alipotembekea leo Agosti 20, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akipata maelezo toka kwa Bw. Kagera Zacharia Ng’weshemi juu ya uendeshaji wa mashine ya kisasa ya kuchambulia na kugundua vinasaba vya aina mbalimbali ikiwemo dawa za kulevya alipotembelea Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali jijini Dar es salaam leo Agosti 20, 2019. Mashine hiyo za aina hiyo katika Afrika zipo Tanzania, Afrika Kusini na Madagascar pekee.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na watumishi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali jijini Dar es salaam alipotembelea leo Agosti 20, 2019. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Esther Hellen Jason na kulia ni MKEMIA Mkuu wa erikali, Dkt. Fidelice Mafumiko.
Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ukiondoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali jijini Dar es salaam ambako Mhe Rais alitembelea leo Agosti 20, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John PombeMagufuli akiongea na watumishi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali jijini Dar es salaam alipotembelea leo Agosti 20, 2019.
Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ukiondoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali jijini Dar es salaam ambako Mhe Rais alitembelea leo Agosti 20, 2019.
Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapongeza kwa kazi nzuri viongozi wa vyombo vya ulinzi na Usalama wa Mkowa wa Dar es salaam wakati wa Mkutano wa 39 wa Wakuu wa nchi za SADC wakati akiwa anaondoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali jijini Dar es salaam alikotembelea leo Agosti 20, 2019.

JAJI MKUU WA TANZANIA AONGOZA ‘SESSION’ IRINGA

$
0
0
Na Lusako Mwang’onda, Mahakama Kuu – Iringa 

Jumla ya mashauri 29 yanatarajiwa kusikilizwa mkoani Iringa katika kikao maalum ‘session’ ya Mahakama ya Rufani chini ya jopo la Wahe. Majaji watatu likiongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Juma. 

Akizungumzia kuhusu kikao hicho ‘session’ mapema Agosti 19, 2019, Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Eddie Fussi amesema kuwa katika kikao hicho kuna jumla ya mashauri ya rufaa za jinai ishirini na tano (25), rufaa za madai mbili (2) na maombi ya madai mawili (2) 

Mhe. Fussi ameongeza kuwa kati ya mashauri hayo ishirini na tisa (29); matatu (3) ni ya zamani (backlogs) na ishirini na sita (26) ni ya muda wa kati na mapya (back stopping). 

Kikao hiki cha Mahakama ya Rufani kilichoanza wiki iliyopita ni cha pili (II) kufanyika ndani ya mwaka huu. Majaji wengine waliopo katika jopo hilo ni pamoja na Mhe. Richard Mziray, Mhe. Rehema Mkuye na Mhe. Ignas Kitusi. 

Kikao hicho kitarajiwa kukamilika Agosti 30 mwaka huu na mara baada ya kukamilika kwa kikao hicho, Mhe. Jaji Mkuu anatarajia kufanya ziara ya kikazi kwenye Mahakama zote za mikoa ya Iringa na Njombe, ambapo atakagua maendeleo ya shughuli mbalimbali za kimahakama na kuzungumza na watumishi. 
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akisaini kitabu cha wageni Agosti 18, 2019 pindi alipowasili mkoani Iringa kuungana na jopo la Majaji watatu katika kikao maalum cha Mahakama ya Rufani ‘session’ kinachofanyika mkoani humo.

Kiwanda cha Kwanza cha Kusafisha Dhahabu Kuanza Octoba Mwaka Huu

HAJI MANARA ATAKA MASHABIKI 60,000 KWA MKAPA SIMBA IKICHEZA DHIDI YA UD SONGO

$
0
0

Na Said Mwishehe, Michuzi TV

MSEMAJI wa timu ya soka ya Simba na Mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Haji Manara amewaomba wanachama, mshabiki na wapenzi wa soka nchini kujitokeza kwa wingi katika mechi yao ya marudiano dhidi ya timu ya UD Songo itachezwa Agosti 25 mwaka hu kuanzia saa 10 jioni katika Uwanja wa Taifa maarufu kwa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mbali na kuwahimiza Wana-Simba na wapenzi wa soka kujitokeza kwa wingi uwanjani kuishangilia Simba ,Manara pia amesema anaiombea dua njema timu za Tanzania ambazo nazo zitakuwa na mechi za marudiano ikiwemo timu ya Yanga ambayo amesema anaamini bado ina nafasi ya kusonga mbele.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam,Manara amewaambia waandishi wa habari kuwa kuhusu maandalizi ya timu yao ya Simba yamekamilika n wachezaji wako tayari kwa mchezo huo na ushindi kwao ni jambo namba moja na si vinginevyo.

"Maandalizi yamekamilika na mechi itachezeshwa na na waamuzi kutoka nchini Rwandwa na viingilio vya mchezo huo ni rafiki kama ilivyo kawaida.Kiingilio kinaanzia Sh.5000, Sh.15,000 na Sh.30,000 wakati Platinum kitakuwa Sh.100,000 na Platinum Plus itakuwa Sh.150,000.

"Tiketi zitaanza kuuzwa kuanzia Alhamisi ya wiki hi kupitia Selcom ambao nao wako tayari kwa kzi hiyo.Kuelekea mchezo huo gari litazunguka katika maeneo mbalimbali yenye mkusanyiko wa watu na tunatarajia kuona mashabiki 60,000 uwanjani na hili kwa Simba sina wasiwasi nalo hata kidogo,"amesema Manara.

Amesisitiza kuwa mashabiki wa Simba ni chachu kubwa ya ushindi wa timu yao na kwamba hata wachezaji wa Simba wakiongozwa na Medie Kagere wamekiri wanapowaona idadi kubwa ya mashabiki uwanjani basi huwa wanapagawa na kuwafanya wacheze kwa moyo wa kujituma ili kushinda mechi.

Hivyo amesema matarajio yao wana Simba watajitokeza kwa wingi kushangilia na ikibidi kuzomea wapinzani wao mwanzo mwisho.

"Nataka kuwaambia msimu uliopita Simba iliongoza kwa kujaza mashabiki wengi uwanjani na matarajio yetu Simba itapata tuzo ya kuingiza mashabiki wengi,"amesema Manara.

Ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa mechi itachezwa muda mzuri na siku nzuri ya Jumapili, hivyo mashabiki watajitokeza kwa wingi uwanjani kuishangilia timu yao."Tunataka mashabiki wa Simba uwanjani hakuna kukaa kimya, muda wote tutashangilia."

Kuhusu kushangilia timu zingine, Manara amewaomba Watanzania kujitokeza kusapoti timu ya KMC na Azam ambao wanatangulia kucheza mechi zao na ni vema uwapa hamasa na kuzishangilia timu hizo na Wana Simba na watanzania wote wajitokeze kwa wingi kushangilia timu hiyo.

Pia amesema ni ngumu kwake kuipenda Yanga na hajawahi kuipenda lakini kwenye mechi yao ya marudiano anaiombea dua ili ishinde kwani kufanya vizuri kwa timu hiyo ni mafanikio kwa nchi yetu.

BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 20. 08. 2019

WHY NAFASI YA MANARA?...MSEMAJI WA SIMBA KWA SASA NI HAJI SANDE RAMADHAN MANARA

$
0
0

*Ni majibu ya Manara baada ya kuibuka tetesi za kuondolewa usemaji wa Simba

Na Said Mwishehe,Michuzi Blogu

MSEMAJI wa Klabu ya Simba Haji Manara amewaambia mashabiki na wapenzi wa soka nchini Tanzania kwamba kwa sasa yeye ndio Msemaji wa klabu hiyo na wala hakuna mwingine huku akieweka wazi hata hivyo hatakaa katika nafasi hiyo milele.

Manara amesema hayo leo jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari wakati anazungumzia mechi yao ya marudiano dhidi ya timu ya UD Songo itakayochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Jumapili ya wiki hii.

Baada ya kuzungumzia mechi hiyo na maandalizi ambayo wameyafanya,ukafika wakati wa maswali ambapo Mwandishi wa Michuzi Blogu alitaka kufahamu kuhusu nafasi ya Manara hasa baada ya kuwepo kwa tetesi zinazodai nafasi yake imechukuliwa na mtu mwingine.

Hivyo wakati anajibu swali hilo Manara alianza kwa kujibu hivi "Why Manara. Kwanini ,Why Manara na kama nafasi Simba mbona zimetangazwa nyingi tu iweje kwa Manara.

"Ngoja niwaambie kwa sasa Msemaji wa Klabu ya Simba ni Haji Sande Ramadhan Manara.Mimi ndio msemaji wa Simba na wala hakuna mwingine,"amesema Manara.

Wakati anajibu swali hilo Manara alionesha kuzungumza kwa utulivu na umakini mkubwa huku akifafanua licha ya kuwa yeye ndio Msemaji wa Simba lakini hatakaa milele katika nafasi hiyo na hilo amekuwa akilieleza mara kwa mara.

"Hata hivyo sijui kwanini watu wanazungumzia sana kuhusu nafasi yangu. Why ? Niwaambie ndugu zangu waandishi wa habari hakuna mtu mkubwa ndani ya Simba zaidi ya Simba yenyewe.Simba ni kubwa kuliko mtu yoyote.

"Najua kuna siku atakuja mwingine na akitoa wana Simba naomba tumpe ushirikiano mkubwa kama ambavyo mmekuwa mkinipa mimi,"amesema Manara.

Ametumia nafasi hiyo kueleza wazi anachofurahi zaidi hana tatizo lolote na uongozi wa Simba na wala hajaaambiwa chochote na ndio maana anaendelea kuchapa kazi na wanaoweka maneno mitandaoni wafahamu bado yupo yupo sana katika nafasi hiyo ya usemaji.

Kwa siku kadhaa sasa kwenye mitandao ya kijamii kumekuwepo na tetesi nyingi zinazodai kuwa Manara ameondolewa kuwa Msemaji wa Simba na badala yake atapewa kitengo cha hamasa. Ambapo katika hilo Manara amesema kuna mambo ya ajabu, kwani tetesi za uongo zinawekwa mitandaoni halafu viongozi wa Simba ndio wanatakiwa kujibu.

"Haya zaidi ya swali hili kuna tetesi gani nyingine za huko mitandaoni nizijibu? Aliuliza Manara kwa kujiamini huku akisisitiza yeye ndio Msemaji wa Simba.

FURSA YA MAFUNZO KAZINI WILAYA YA IRINGA YAKUTANISHA ZAIDI YA WASOMI 514

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiongea na wasomi waliojitokeza ofisini kwake kwa ajili ya kuchangamkia fursa ya mafunzo kanzini inayotewa na serikari ya awamu ya tano
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa katika akiwa amezungukwa na wasomi walijioteza kuchangamkia fursa ya mafunzo kazini
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa katika akiwa amezungukwa na wasomi walijioteza kuchangamkia fursa ya mafunzo kazini 


NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Zaidi ya wasomi mia tano na kumi na nne (514) wamejitokeza katika ofisi za mkuu wa wilaya ya Iringa kuchangamkia fursa iliyotolewa na serikali ya kuwasaidia wasomi kupata mafunzo kazini kwa mwaka mmoja na serikali itagharamia mafunzo hayo kwa kutoa kiasi cha shilingi laki moja na nusu kila mwenzi.

Akizungumza na blog hii Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alisema kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano inayongozwa na Rais Dr John Pombe Magufuli imetenga fedha za kuwasaidia wasomi zaidi ya elfu tano nchi nzima kufanya kazi kwenye taasisi binafsi

“Mheshimiwa Rais ametanga fedha kupitia mfuko wa waziri mkuu kwa ajili ya kuwasaidia wasomi kufanya kazi kwenye mashirika binafsi kwa lengo la kuwasaidia kupata uzoefu kazini ili wakifanya vizuri waweze kusaidiwa na wengine kupata uzoefu ili wakienda kuomba kazi sehemu nyingine wawe na uzoefu” alisema Kasesela 

Kasesela alisema kuwa alichokifanya ni kutimiza ndoto ya Rais Dr John Pombe Magufuli ya kuhakikisha wasomi wote wanakuwa na uzoefu kazini kwa kuwawezesha ili kuwarahisisha kupata ajira pale wanapoenda kuomba kazi kwa kuwa watakuwa tayari wameshafanya kazi kwenye taasisi binafsi kwa mwaka mmoja.

“Ukiangalia Tanzania kada moja tu ya udaktari ndio kata ambayo imekuwa ikipewa mafunzo ya uzoefu kazini hivyo kada nyingine zote hazina mafunzo kazini ndio maana sisi wasaidizi wake tumeanza kutekeleza hili swala kwa nguvu zote” alisema Kasesela

Kasesela alisema kuwa aliitisha zoezi hilo huku akitegemea kuwa angepata wasomi wapatao mia moja tu lakini amekutana na wasomi mia tano na kumi na nne jambo ambalo hakulitarajia kukutana nalo.

“Nimekutana na wasomi wengi sana leo ambao wamesoma vitu tofauti tofauti na wanauwezo wa kufanya kazi hivyo ni jukumu langu kuwatafutia sehemu za kupata mafunzo kazini katika makampuni na mashirika yaliyopo wilaya ya Iringa”alisema Kasesela

Nao baadhi ya wasomi waliofika kwenye zoezi hilo wameipongeza serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dr John Pombe Magufuli ikiwakilishwa vizuri na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela kwa kuanzisha zoezi hilo.

“Kwa zoezi hili limetusaidia kwa kiasi kikubwa kupata uzoefu na kutusaidia kupata elimu ya mafunzo kazini na kusaidia njia rahisi ya kupata ajira kwa kuwa wasomi wanavyoenda kuomba kazi sehemu mbalimbali” alisema Kasesela

Wasomi hao walimpongeza Rais Dr John Pombe Magufuli kwa hatua aliyoichukua kuwatafutia njia mbadala ya kupata ajili kwa wasomi wengi ambao wapo mtaani hawana ajira.

WAZIRI MPINA AVIPAISHA VIWANDA VYA MAZIWA NCHINI

$
0
0
Serikali imesema itaendelea kulinda viwanda vya kuzalisha maziwa nchini ili kukuza soko la ndani na kuhakikisha viwanda hivyo vinazidi kujiimarisha kibiashara kwa kuvipa msamaha wa tozo mbalimbali na kuongeza tozo kwa bidhaa ya namna hiyo inayotoka nje ya nchi.

Kauli hiyo imetolewa leo (20.08.2019) na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina jijini Dodoma kwenye kikao cha kutoa taarifa ya tathmini ya sekta ya mifugo ya mwaka 2016/2017 hadi 2031/2032 kwa kamati ya kudumu ya bunge ya Kilimo, mifugo na Maji ili kujionea namna sekta hiyo inavyochangia ukuaji wa pato la taifa.

“Nataka niseme tuliamua kwa nia njema kupandisha tozo za maziwa kutoka nje kutoka Shilingi 150 hadi Shilingi 2,000 kwa nia ya kuwalinda wazalishaji wa ndani, wizara tukafanya hivyo ili kuona wazalishaji wetu wanavyofanya kazi, sasa hivi kampuni za ndani kila wanachozalisha kwa siku kinanunuliwa chote kutokana na kwamba waliokuwa wakiagiza maziwa kutoka nje waliyo wengi wameshindwa.” Amesema Waziri Mpina.

Akizungumzia kuhusu chanjo za mifugo ili kuhakikisha inakuwa na afya bora na kutoa matokeo mazuri yakiwemo ya upatikanaji wa maziwa, Waziri Mpina amesema serikali itaendelea kuhakikisha inazalisha chanjo za kutosha na kwamba haitaiachia sekta binafsi kuendelea kuzalisha chanjo hizo ili iziweze kupatikana kwa bei nafuu na zenye ubora unaotakiwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Kilimo, Mifugo na Maji Mhe. Mahmoud Mgimwa amesema Mpango Kabambe wa Mifugo nchini (TLMP) wa mwaka 2017/2018 hadi 2021/2022 uliozinduliwa na wizara hiyo, ukifanikiwa utakuwa na faida kwa wafugaji huku akitaka uwepo mkakati wa upatikanaji wa fedha ili kuhakikisha mpango huo unatekelezwa kama ulivyokusudiwa bila kutegemea wafadhili.

“Ni vyema sasa ikafika wakati serikali ikajielekeza kupanga bajeti ambayo inawiana na mipango tunayoipanga ili mipango hiyo iweze kutekelezwa isije ikatokea moja ya nchi jirani ikanufaika na mipango hiyo kutokana na sisi kushindwa kutekeleza na wao wakachukua wazo wakalifanyia kazi.” Amesema Mhe. Mgimwa

Kikao cha kutoa taarifa ya tathmini ya sekta ya mifugo na utekelezaji wa Mpango Kabambe wa Mifugo nchini (TLMP) kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kimehudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel.

ZIARA YA MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR BALOZI SEIF YAJA NA NEEMA KWA WAKULIMA WA TUMBAKU KAHAMA

$
0
0
Awali Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa madarasa, Bweni na Matundu ya vyoo katika shule ya Sekondari Ulowa. 
 Serikali mkoani Shinyanga imewatoa wasiwasi wakulima wa zao la Tumbaku katika halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama juu ya uuzaji wa tumbaku kilo milioni mbili ambayo imebaki na kusema kwamba wanunuzi wapo na itanunuliwa yote.

Hayo yamebainishwa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo Agosti 20.2019 katika viwanja vya shule ya Msingi Kangeme kata ya Ulowa halmashauri ya Ushetu wakati wa ziara ya Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ambaye pia ni mlezi wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga.

 Telack amesema serikali inaendelea kufanya jitihada ili kuhakikisha kwamba wakulima hao wa tumbaku wanapata mnunuzi na tayari kampuni ya British American imekwishapatiwa kibali na itaanza kununua tumbaku hiyo hivi karibuni. "Kutokana na changamoto iliyojitokeza hapo awali ya ununuzi wa zao la Tumbaku kutokana kampuni ya TLTC kusitisha ununuzi wa zao hili, serikali sikivu iliendelea kutafuta wanunuzi na tayari kampuni ya Alliance itanunua asilimia 10 ya tumbaku hiyo pamoja na kampuni ya British American ambapo yenyewe itanunua tumbaku yote itakayobaki",amesema Telack. 

"Naagiza pia acheni kukata miti hovyo kwa ajili ya kuchomea tumbaku zenu ,nilishasema muwe mnakata matawi na siyo miti kama mnavyofanya hivi sasa na mkiendelea na hali hii nitasitisha ulimaji wa zao la tumbaku kwa sababu hatutaki tuishi kwenye hali ya jangwa,"ameongeza. 

Aidha amewataka wakulima hao wa tumbaku kutumia vyema pesa ambazo watazipata kutokana na mauzo ya tumbaku, kwa kuzifanyia shughuli za maendeleo ikiwemo kujenga nyumba za kisasa na kusomesha watoto wao. Kwa upande wake, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ambaye pia ni mlezi wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga, amesema serikali ya Tanzania itawasaidia wakulima wa tumbaku ili kuhakikisha tumbaku yao inanunuliwa.

Awali akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa, amesema kuwa shauku kubwa ya wakulima wa tumbaku wa kata ya Ulowa, ni kujua hatma ya uuzaji wa tumbaku yao iliyobaki yenye kiasi cha kilo milioni mbili na kumuomba mkuu wa Mkoa awapatie ufafanuzi wakulima hao juu ya suala hilo  Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd ambaye pia ni mlezi wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga akiwatoa wasiwasi wakulima wa zao la tumbaku katika halmashauri ya wilaya ya Ushetu kuwa serikali yao itahakikisha inawasaidia wakulima na kuhakikisha tumbaku yao inanunuliwa yote. Picha zote na Annastazia Paul,Picha na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akizungumza na wananchi wa kata ya Ulowa halmshauri ya Ushetu wilayani Kahama ambao ni wakulima wa zao la tumbaku na kuwatoa wasiwasi kuwa tumbaku yao iliyosalia kilo Milioni 2 itanunuliwa yote.  Awali Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa, alimuomba mkuu wa mkoa Zainab Telack kuwatoa wasiwasi wakulima wa zao la Tumbaku juu ya hatma ya ununuzi wake mara baada ya kampuni ya awali iliyokuwa ikinunua zao hilo kusitisha ununuzi.  Mbunge wa Viti maalumu mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad akisoma taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Jimbo la Ushetu kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo hilo Elias Kwandikwa,ambapo alisema asilimia kubwa ya miradi ya maendeleo imetekelezwa ikiwamo ya huduma za afya , ujenzi wa zahanati, kituo cha afya , hospitali ya wilaya pamoja na unuaji wa vifaa tiba.  Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi Iddi, akiwataka wananchi wa kata ya Ulowa kuwa wawe wanachangia shughuli mbalimbali za maendeleo na siyo kutegemea kila kitu wafanyiwe na serikali, huku akitoa Shilingi Milioni Moja kwa ajili ya ununuzi wa saruji mifuko 50 ili kukamilisha ujenzi wa bweni katika shule ya Sekondari Ulowa.  Wananchi wa Kata ya Ulowa halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.  Wananchi wa Kata ya Ulowa halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.  Wanachama wa CCM wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Kangeme Kata ya Ulowa- Ushetu wilayani Kahama. 
Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimsalimia mmoja wa wanafunzi katika shule ya Sekondari Ulowa Leticia Tungu (15) ambaye anasoma kidato cha kwanza. Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akiwasisitiza wanafunzi wa shule ya sekondari Ulowa kusoma kwa bidii hasa masomo ya Sayansi ili waje kuwa tegemeo katika familia zao pamoja na taifa kwa ujumla kwa kupata watalaamu ambao watailetea maendeleo nchi. Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini,Mhe. Jumanne Kishimba akisoma taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM ya Jimbo hilo, kuwa changamoto kubwa ambayo wanakabiliana nayo ni ubovu wa miundombinu ya barabara hasa za mjini. Mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini Jumanne Kishimba akikabidhi Taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Kwa Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, ambaye pia ni mlezi wa CCM Mkoa wa Shinyanga. Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Donald Magesa akiwaapisha wanachama wapya watano wa Chama cha Mapinduzi CCM, ambao wamekihama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Picha zote na Annastazia Paul,Picha na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

JIJI LA ARUSHA LASAINI MKATABA MDOGO NA KAMPUNI YA CHINA MRADI UJENZI WA BARABARA

$
0
0
Na Jusline Marco-Arusha

Halmashauri ya Jiji la Arusha imesaini mkataba mdogo wa Addendum na kampuni ya SINOHYDRO CONSTRUCTION LTD kutoka China ikiwa ni kazi ya nyongeza ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Kisongo bypass hadi Olasiti yenye urefu wa kilomita 3.442 itakayo gharimu fedha za kitanzania shilingi bilioni 4.1

Ujenzi wa barabara hiyo ya Kisongo upo chini ya mradi wa TANZANIA STRATEGIC CITIES PROJECT (TSCP)-AF2 ambapo unahitajika kukamilika ndani ya miezi minne kuanzia 11 Septemba 2019 hadi 11 Januari 2020.

Akizungumza wakati wa utiaji wa saini hiyo Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dkt. Maulid Suleimani Madeni amemsisitiza mkandarasi wa miradi huo kufanya kazi kwa ubora na kwa muda uliopangwa ili mradi huo ukawe faida kwa wananchi wa maeneo hayo.
 Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Arusha akikabidhiana mkataba na kiongozi wa kampuni ya SINOHYDRO CONSTRUCTION LTD kutoka nchini China.
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Dkt. Maulid Suleimani Madeni akisaini mkataba mdogo(Addendum) wa ujenzi wa barabara ya Kisongo bypass
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Mhe. Kalisti Lazaro akiweka sahihi katika mkataba mdogo(Addendum) wa ujenzi wa barabara hiyo ya Kisongo bypass

RC MAKONDA AUNGANA NA WATANZANIA KUMPONGEZA RAIS DKT MAGUFULI KWA KUWA MWENYEKITI WA SADC

$
0
0
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa anaungana na watanzania wote kumpongeza Rais wa Jamhuri ya kwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Aftika (SADC).

Magufuli amerithi mikoba ya kiti cha Uwenyekiti wa SADC kutoka Kwa mtangulizi wake Rais wa Namibia, Dr. Have Geingob na atadumu na cheo hicho Kwa mwaka mmoja. 

Makonda amesema kuwa anaungana na Watanzania wote kumpa pongezi Magufuli kutokana na kuaminiwa Kwa utendaji wake wa kazi. 

"Kwetu Sisi tunaona fahari Kwa kiongozi wetu kupewa jukumu la kuongoza nchi 16 zilizo ndani ha SADC ni matokeo ya uzalendo nasi tunapaswa kuendeleza uzalendo Kwa vitendo.

"Tuna jukumu la kuendeleza uzalendo ambao uliachwa na Mwalimu Julius Kambarange Nyerere ambaye ni mmoja wa waasisi wa Jumuiya hii kwa kuwasaidia wengi kupata Uhuru, hatuna bundi kuungana na kiongozi wetu ambaye Kwa sasa ana jukumu la kuendeleza Yale yaliyoachwa na waasisi hasa malengo yake makubwa yamekuwa ni kutotoa kwenye Lindi la umaskini.

"Kama ambavyo amesema kuwa Mataifa yetu si maskini na namna jitihada zilivyotumika kuwatoa wengi kwenye utumwa hizo ndizo zitatumika kuyatoa Mataifa yetu kwenye dimbwi la umaskini kama alivyosema kwenye hotuba yake, ni wakati wetu wa kuungana na kumpa sapoti,".

MAGAZETI YA LEO JUMATANO AGOSTI 21,2019

TAASISI ZA MIFUGO NA UVUVI ZATAKIWA KUTOA GAWIO SERIKALINI

$
0
0
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Joelson Mpina ( katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu Mkuu Sekta ya Mifugo Prof.Elisante Ole Gabriel (kulia) na Mkurugenzi Mkaazi wa Taasisi binafsi ya TRADEMARK East Africa baada ya majadiliano yenye lengo la kuboresha mifumo ya ukusanyaji mapato ya serikali kwa njia ya kielektroniki yaliyofanyika Wizarani jijini Dodoma leo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (mifugo) Profesa Elisante Ole Gabriel( katikati) akiongea na wataalam na wawakilishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi( hawapo pichani) kwenye kikao cha kujadili uboreshaji wa mifumo ya ukusanyaji wa mapato ya serikali  kwa kuahirikiana na Trademark East Africa kwenye ukumbi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mtumba jijini Dodoma leo. (19/8/2019)

KATIBU Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof.Elisante Ole Gabriel amezitaka taaisisi zilizo chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuimarisha ukusanyaji wa mapato kwa njia ya kielekroniki ili kuweza kutoa gawio serikalini.

Katibu Mkuu Prof.Gabriel ameyasema hayo jijini Dodoma leo (19.8.2019) wakati akifungua kikao cha majadiliano kati ya wataalamu wa sekta za Mifugo na uvuvi na wataalam kutoka taasisi binafsi ya Trade Mark East Africa yenye lengo la kusaidia uboreshaji wa mifumo ya ukusanyaji wa mapato ya serikali kwa njia ya kielekroniki.

Prof.Gabriel alisema kuwa lengo la kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya serikali ni kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli katika jitihada zake za kuinua uchumi na kuleta maendeleo nchini.

Akitolea mfano wa upotevu wa mapato ya serikali hususan kwenye Sekta ya Mifugo, Prof.Gabriel alisema kwenye mnada wa Maswa ulikuwa ukikusanya kiasi cha Shilingi 756,000 kwa siku lakini baada ya kuweka udhibiti kwa kupeleka wasimamizi mapato yaliongezeka na kufikia shilingi 7,028,000 kwa siku.

Kwa upande wa mnada wa Halmashauri ya Bariadi,mkoani Simiyu,Prof.Gabriel alisema baada ya udhibiti mapato yaliongezeka kutoka shilingi mil.2.5 hadi mil. 3 kwa siku na kufikia shilingi 14,950,000 kwa siku.

Aidha Katibu Mkuu aliwataka wataalam hao baada ya kuwa na mifumo imara ya ukusanyaji wa mapato, pia kufikiria na kuona njia nyingine za kuongeza wigo wa ukusanyaji mapato, akitolea mfano utalii kwenye sekta za Mifugo na Uvuvi nchini.

Prof.Gabriel aliiahidi taasisi hiyo yenye makao yake makuu jijini Nairobi nchini Kenya kuwa Wizara yake iko tayari kutoa ushirikiano wa hali na mali ili kufanikisha azma hiyo ya kuziba mianya ya upotevu wa mapato ya serikali.

Kabla ya kumalizia na kuashiria ufunguzi rasmi wa kikao kazi hicho, Prof.Gabriel alisisitiza suala la elimu kwa umma kuhusu matumizi ya mifumo hiyo kuwa ni muhimu sana kutolewa hususan kwa wafugaji na wavuvi ambao ndio wadau wakuu wa sekta za mifugo na uvuvi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkaazi wa Taasisi hiyo nchini, Bw.John Ulanga alimshukuru sana Katibu Mkuu na wataalamu wake kwa kuonyesha utayari wa kushirikiana nao na kusema haijawahi kutokea katika taasisi zote walizofanya nazo kazi kuona utayari na ushirikiano kama walioupata kwa wizara ya mifugo na uvuvi.

Ili kufanikisha azma hiyo.Bw.Ulanga alisisitiza kuwepo na utayari wa kubadilika fikra katika utendaji ndani ya Wizara na taasisi zake vinginevyo mifumo hiyo haitakuwa na faida yoyote.

Wakichangia hoja wakati wa uwasilishwaji wa mada kutoka taasisi binafsi ya Trade Mark East Africa wataalam wa wizara ya mifugo waliipongeza taasisi hiyo na kuitaka kujitahidi kutumia changamoto walizokutana nazo kwenye taasisi nyingine kuboresha mifumo ya wizara ili kurahisisha matumizi ya mifumo hiyo.

Naye Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Sekta ya Mifugo, Bw.Amosy Zephania akihitimisha kikao hicho aliishukuru taasisi hiyo kwa kuonyesha nia ya kuisaidia wizara na kuahidi ushirikiano wa hali ya juu.

Alisema kwa kuwa wizara ilishaanza mchakato wa kuwa na mifumo hiyo basi ni vema taasisi hiyo ikashirikiana kwa haraka ili kufanikisha malengo ya wizara ya kuokoa fedha nyingi zinazopotea kwa kukosekana kwa mifumo ya udhibiti wa ukusanyaji mapato ya serikali.

RC MAKONDA AWATAKA WATANZANIA KUTUMIA FURSA ZA SADC.

$
0
0
Mkuu wa mkoa Mh.Paul Makonda akizungumza jambo na Naibu Waziri Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde wakati wa kufungwa kwa mkutano wa 39 wa SADC,mwishoni mwa wiki jijini Dar.
Viewing all 110185 articles
Browse latest View live




Latest Images