Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

Muasisi wa Familia kwa Ajili ya Amani ya Dunia Kutua Tanzania Mwezi Huu

$
0
0
Muasisi na Mlezi wa Shirikisho la Familia kwa Ajili ya Amani ya Dunia, Dkt. Hak Ja Han Moon, kutoka Korea anataraiwa kuwasili nchini kwa ajili ya kushiriki tamasha ambalo mgeni rasmi inatarajiwa awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli.

Akizungumza kwa niaba ya Kiongozi Mkuu wa Shirikisho hilo nchini, Stylos Simbamwene, Semeni Kingaru amesema tamasha hilo la Baraka na Upendo, litafanyika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam 31 mwezi huu.

Ujio wa Dkt. Moon utaambatana na wageni wapatao 200 kutoka Korea, Japani, China, Marekani na Uingereza ambapo timu ya maandalizi imeanza kuingia nchini juzi na jana huku wageni 200 wakitarajiwa kuwasili nchini 26 Mwezi huu.

“Watapokewa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Costantine Kanyasu, na kwenda kutembelea mbuga ya wanyama Mikumi, kabla ya Muasisi wa Shirikisho kuwasili na kujiunga nasi kati ya tarehe 28 na 29 mwezi huu,” amesema Kingaru.

Amesema shughuli mbalimbali zitakazofanyika kwenye tamasha hilo zimejikita katika Dira ya Shirikisho ambayo ni kudhibiti mmomonyoko wa maadili. ili kuijenga Tanzania ya kizalendo.

Amesema tamasha hilo litakalojumuisha wanandoa 80,000 linatarajiwa kuripotiwa mubashara na vyombo mbalimbali vya habari nchini, ingawa hakuvitaja. 

Kwa upande wa maandalizi ya tukio hilo nchini, yapo chini ya uratibu wa kiongozi mkuu kitaifa wa Shirikisho hilo, Simbamwene na viongozi wenzake, Kingaru na Neema Elpin.

SIKU YA KUMBUKUMBU YA WAATHIRIKA WA UGAIDI, AGOSTI 21 KILA MWAKA

$
0
0
Picha ya Amaury na Andrew Razafitrimo kutoka Madagaska
wakimkumbuka mama yao ambaye alifariki dunia katika shambulio la ugaidi 14 July 2016.

Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
TANZANIA ikiwa ni nchi mojawapo inayopingana na ugaidi na kuiweka Tanzania kuwa mahali salama pa kuishi leo duniani kote inafanyika kumbukumbu ya waathirika wa ugaidi ambao umewahi tokea duniani kote.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres  katika kumbukumbu ya kuwakumbuka waathirika wa ugaidi duniani kote amesema kuwa "Ninaomba sote tuangalie maisha ambayo yamebadilishwa milele kwa sababu ya ugaidi. Tujitolee kuwaonyesha waathirika wa matukio ya kugaidi kuwa  wao sio peke yao na  jamii ya umoja wa mataifa imesimama katika kumbukumbu hiyo  pamoja nao popote walipo duniani.

Ikiwa mataifa mengi yameathiriwa na ugaidi hata nchini za Afrika Mashariki zinawahanga wa matukio ya ugaidi hasa nchi ya Kenya leo ni kumbukumbu ya kuwakumbuka waathirika wa matukio hayo ambayo yanamaliza wanadamu kwa kiasi mkubwa.

Tuungane kwa pamoja katika kukemea ugaidi unaochukua maisha ya watu wengi na kusababisha yatima, na kuongeza balaa la umasikini  duniani kote.
Waathirika wa matukio ya kigaidi wasifikiri kuwa wapo peke yao dunia kwa ujumla imetenga siku ya leo ya Agosti, 21 kila mwaka kuwakumbuka watu walioathirika na matukio ya ugaidi nchini kote.

 Waathirika wanatakiwa kufarijiwa, kusamehana pamoja na kupewa msaada wa hali na mali, kijamii, kifedha pamoja na kisaikolojia ili kulinda utu wao.

Umoja wa mataifa unaungana na waathirika wote wa matukio hayo ili kuhakikisha  unahaki ya kutoa msaada katika nchi malimali ili kuzuia matukio ya kigaidi yanayoweza kujitokeza katika nchi mbalimbali ili kuchochea amani na upendo.

Katika kumbukumbu ya kuwakumbuka waathirika wa matukio ya ugaidi ni uzingatiaji katika uimarishaji wa wathirika na familia zao jinsi wameweza kukabiliana na kile ambacho kimefanya kubadili uzoefu wa maisha yao ili kusaidia uponyaji wa waathirika pamoja na kupambana kwa nguvu dhidi ya ugaidi.

Vyombo vya usalama hapa nchini vinaonekana kuwa mstari wa mbele katika kukabilia na ugaidi ili kuleta amani katika nchi yetu ikiwa Juni 19, 2019 katika ukurasa wa mitandao ya kijamii wa Umoja wa Mataifa ulipata fununu za kuwepo kwa shambulio la kigaidi nchini na Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) nchini Tanzania, Simon Sirro wakati akizungumza na gazeti la Mwananchi alisema kuwa  jeshi lake lilishapata fununu za shambulio hilo kabla Ubalozi wa Marekani kutoa tahadhari juu ya tukio hilo kupitia tovuti yake Juni 19,2019.

Kuhusu tahadhari iliyotolewa na ubalozi wa Marekani nchini Tanzania Sirro alisema: "hiyo ni taarifa kama taarifa nyingine, inaweza kuwa ya kweli au uongo, lakini sisi kama vyombo vya ulinzi huwa hatupuuzi jambo katika kukabiriana jambo lolote''.

FURSA YA MAFUNZO KAZINI WILAYA YA IRINGA YAKUTANISHA ZAIDI YA WASOMI 514

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiongea na wasomi waliojitokeza ofisini kwake kwa ajili ya kuchangamkia fursa ya mafunzo kanzini inayotewa na serikari ya awamu ya tano
 Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela  akiwa katika akiwa amezungukwa na wasomi walijioteza kuchangamkia fursa ya mafunzo kazini 
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela  akiwa katika akiwa amezungukwa na wasomi walijioteza kuchangamkia fursa ya mafunzo kazini 


NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

ZAIDI ya wasomi mia tano na kumi na nne (514) wamejitokeza katika ofisi za mkuu wa wilaya ya Iringa kuchangamkia fursa iliyotolewa na serikali ya kuwasaidia wasomi kupata mafunzo kazini kwa mwaka mmoja na serikali itagharamia mafunzo hayo kwa kutoa kiasi cha shilingi laki moja na nusu kila mwenzi.


Akizungumza na blog hii Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alisema kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano inayongozwa na Rais Dr John Pombe Magufuli imetenga fedha za kuwasaidia wasomi zaidi ya elfu tano nchi nzima kufanya kazi kwenye taasisi binafsi


“Mheshimiwa Rais ametanga fedha kupitia mfuko wa waziri mkuu kwa ajili ya kuwasaidia wasomi kufanya kazi kwenye mashirika binafsi kwa lengo la kuwasaidia kupata uzoefu kazini ili wakifanya vizuri waweze kusaidiwa na wengine kupata uzoefu ili wakienda kuomba kazi sehemu nyingine wawe na uzoefu” alisema Kasesela


Kasesela alisema kuwa alichokifanya ni kutimiza  ndoto ya Rais Dr John Pombe Magufuli ya kuhakikisha wasomi wote wanakuwa na uzoefu kazini kwa kuwawezesha ili kuwarahisisha kupata ajira pale wanapoenda kuomba kazi kwa kuwa watakuwa tayari wameshafanya kazi kwenye taasisi binafsi kwa mwaka mmoja.


“Ukiangalia Tanzania kada moja tu ya udaktari ndio kata ambayo imekuwa ikipewa mafunzo ya uzoefu kazini hivyo kada nyingine zote hazina mafunzo kazini ndio maana sisi wasaidizi wake tumeanza kutekeleza hili swala kwa nguvu zote” alisema Kasesela


Kasesela alisema kuwa aliitisha zoezi hilo huku akitegemea kuwa angepata wasomi wapatao mia moja tu lakini amekutana na wasomi mia tano na kumi na nne jambo ambalo hakulitarajia kukutana nalo.


“Nimekutana na wasomi wengi sana leo ambao wamesoma vitu tofauti tofauti na wanauwezo wa kufanya kazi hivyo ni jukumu langu kuwatafutia sehemu za kupata mafunzo kazini katika makampuni na mashirika yaliyopo wilaya ya Iringa”alisema Kasesela


Nao baadhi ya wasomi waliofika kwenye zoezi hilo wameipongeza serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dr John Pombe Magufuli ikiwakilishwa vizuri na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela kwa kuanzisha zoezi hilo.


“Kwa zoezi hili limetusaidia kwa kiasi kikubwa kupata uzoefu na kutusaidia kupata elimu ya mafunzo kazini na kusaidia njia rahisi ya kupata ajira kwa kuwa wasomi wanavyoenda kuomba kazi sehemu mbalimbali” alisema Kasesela

Wasomi hao walimpongeza Rais Dr John Pombe Magufuli kwa hatua aliyoichukua kuwatafutia njia mbadala ya kupata ajili kwa wasomi wengi ambao wapo mtaani hawana ajira. 

GGML yazindua Mafunzo maalum kwa Wahitimu wa Vyuo Vikuu 2019/2020.

$
0
0
Kama sehemu ya jitihada za kuwanyanyua na kuwajengea uwezo vijana wa kitanzania wapate ujuzi wa vitendo na kupata ajira kwa urahisi,Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGML) kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu,Ajira,Vijana na Watu wenye Ulemavu,Taasisi ya Sekta Binafsi(TPSF) pamoja na  Umoja wa Waajiri nchini Tanzania(ATE) wamezindua tena awamu nyingine ya kujenga uwezo na kusaidia  wahitimu wa vyuo vikuu.
Mkurugenzi Mtendaji wa GGML Bw. Richard Jordinson(anayezungumza) akitoa hotuba ya kuzindua mafunzo ya wahitimu wa Vyuo Vikuu kwa mwaka 2019/2020.Kushoto kwake ni Mgeni rasmi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Geita Bi Janeth Mobe na mwakilishi wa Umoja wa Waajiri nchini Tanzania Bw Danny Sora Tandasi(Kulia)
Mpango huu unawalenga wahitimu wapya kutoka Vyuo Vikuu nchi Tanzania katika taaluma mbalimbali ambao hupewa fursa ya kufanya kazi ndani ya Mgodi wa Dhahabu Geita (GGML) kwa muda wa mwaka mmoja ili kupata ujuzi wa vitendo husika ambao utawajengea uwezo wa kujiamini  kabla ya kupata ajira rasmi.
Mwakilishi wa Serikali kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Geita Bi Janeth Mobe akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua program ya mafunzo ya vitendo kwa wahitimu wa vyuo Vikuu nchini ambayo inafadhiliwa na Mgodi wa Dhahabu Geita(GGML)


Akizungumza kuhusu Program hiyo,Mkurugenzi Mtendaji wa GGML Bw. Richard Jordinson amesema; “Serikali na Wadau wengine wamekubaliana kuanzisha program hii ya wahitimu wa vyuo vikuu nchi nzima ambayo itatoa fursa kwa wahitimu vijana kupata ujuzi katika maeneo ya kazi ili kuweza kuhusianisha masomo ya darasani pamoja na uzoefu wa vitendo kwenye maeneo ya kazi jambo ambalo ni muhimu sana katika soko la ajira kwa sasa”.

Bw Jordinson alisema kuwa Mgodi wa Dhahabu Geita (GGML) ni Kampuni Raia,inayounga mkono jitihada za Serikali kuakisi mitaala inayofundishwa vyuoni pamoja na mahitaji ya ujuzi katika soko la ajira ili kuwasaidia vijana waendelee kuwa na mchango chanya kwenye jamii yao.

“Uhusiano kati ya nadharia na vitendo ni muhimu kwa wahitimu vijana wanapofanya kazi na kushindana katika soko la Ajira. Kupitia Program hii,thamani ya wahitimu vijana katika soko la ajira itaongezeka na kuwa na tija katika safari yao ya ajira ndani ya Mgodi wa Dhahabu Geita(GGML) au kwingineko,”aliongeza Bw Jordinson.


Mwaka jana,Ofisi ya Waziri Mkuu,Ajira,Vijana na Watu wenye ulemavu ilianzisha Mwongozo wa Kitaifa wa Mafunzo kwa Wahitimu wa Vyuo Vikuu kwa lengo la kuisaidia nchi kufikia kwa urahisi malengo ya uchumi wa pato la kati kama inavyoongozwa na Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025.

Mwaka 2018/2019, Program ya Mafunzo kwa Wahitimu wa Vyuo Vikuu ndani ya Mgodi wa Dhahabu Geita(GGML) ilitoa ajira 7 kwa wahitimu 22 waliokuwa katika mafunzo hayo.Maeneo yaliyopewa kipaumbele yalikuwa Jiolojia,Uchimbaji,Uchakataji madini,Rasilimali Watu,Sheria,Jamii,Usalama na Mazingira.Faida nyingine ya program hiyo ni kutengeneza idadi ya wahitimu wenye vipawa ili Kampuni inapohitaji wahitimu wenye sifa zinazohitajika iwe rahisi kuwapata nafasi zinapotokea.
“Tunakusudia kuacha alama yenye thamani katika Mji wa Geita pamoja na Tanzania kwa ujumla ambapo kusudio letu ni kuhakikisha uwekezaji wetu wa moja kwa moja kupitia mafunzo hayo tunayoyatoa na ajira tunazotengeneza,tunaendelea kuzalisha mapato na kulipa Kodi zinazohitajika.Tunajivunia sana kuwa sehemu ya wadau wanaofanikisha program hii ili kuleta maendeleo endelevu ya uchumi kutoka kwenye shughuli zetu za uchimbaji dhahabu,” alihitimisha  Bw. Jordinson.
Naye Mwakilishi wa Serikali kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Geita Bi Janeth Mobe aliipongeza GGML kwa kuendeleza program hiyo na kuwataka vijana waitumie fursa hiyo kwa maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.
“Mafunzo yenu ni muhimu sana katika kusaidia nia ya serikali kutimiza ndoto ya viwanda na uchumi wa pato la kati,zingatieni kwa umakini mkubwa fursa hii ili iweze kuleta tija na manufaa yaliyokusudiwa hasa kwenye soko la ajira baada ya kumaliza mwaka wenu wa mafunzo kwa vitendo ndani ya Mgodi wa Dhahabu Geita,”alisisitiza Bi Janeth
Kwa upande wake,mnufaika wa program hiyo mwaka huu Bi Diana Ngungi alisema kuwa amefarijika sana kupata fursa ya kupata mafunzo baada ya kuhitimu elimu yake ya Chuo Kikuu.
“Ninayo kila sababu ya kuipongeza GGML kwa kunipatia fursa hii na ninaahidi kuitumia ipasavyo kwa ajili ya kujifunza zaidi kabla sijapata ajira ya kudumu,”alisema Bi Diana.

Mhini ang’ara mashindano ya dunia kuogelea

$
0
0
Na Mwandishi wetu
Dar es Salaam. Nahodha wa timu ya Taifa ya kuogele ya waogeleaji chipukizi (Junior), Dennis Mhini ameng’ara katika mashindano ya Dunia yanayoendelea mjini Budapest, Hungary baada ya kuongoza katika kundi la kwanza mchujo.

Dennis ambaye ni mwanafunzi wa shule ya St Felix ya Uingereza, aling’ara katika shindano ya mita 100 katika mtindo wa Backstroke kwa kutumia muda wa 1.04,27 na kuwashinda waogeleaji wengine kutoka mataifa mbalimbali katika kundi la kwanza.

Aliweza kuwapita waogeleaji kutoka nchi za Albania ambayo iliongozwa na Ared Ruci, Madagascar iliyowakilishwa na Mandresy Rajaonson na Nigeria iliyokuwa chini ya muogeleaji, Adewole Adekoya.

Katika kundi hilo pia Dennis aliwachapa waogeleaji, Humza Khaliq wa Pakistan, Tsitocina Razanatefy (Madagascar), Amar Altub ali Altub wa Sudani na Mtanzania mwenzake, Isam Sepetu.

Matokeo ya kuongoza katika hatua ya mchujo yametoa faraja kwa Tanzania katika kuendeleza mchezo huo pamoja na changamoto ya kukosa bwawa la kuogelea la kisasa la mchezo huo.

Waogeleaji wa Tanzania wamekuwa na kilio cha kupata bwawa la mita 50 la kisasa kwa kipindi kirefu na kushindwa kuzoea vifaa vya kisasa.

Mabwawa mengi ambayo yanamilikiwa na taasisi binafsi (zaidi shule za kimataifa) yana urefu wa mita 25 na kukosa vifaa vya kisasa kama ‘diving block’ (kifaa kinachutumiwa na waogeaji kuchupa) na touchpad ambayo inatumika kwa ajili ya kurekodi muda.

“Nimefurahi kuongoza katika ‘heat’ yangu na kuitangaza nchi. Ni kazi kubwa sana kufikia hatua hii, kwangu mimi ni historian a hasa ukizingatia kuwa tunafanya mazoezi kwenye mabwawa ambayo hayalingani na haya ya kisasa na kulazimika kuja mapema Hungary ili kupata fursa ya kutumia mabwawa haya japo kwa siku mbili,” alisema Dennis.
Dennis Mhini akipozi mara baada ya kuibuka wa kwanza katika kundi la mchujo la kwanza (heat 1) katika mashindano ya Dunia ya Vijana yanayofanyika mjini Budapest, Hungary.
Muogeleaji wa Tanzania, Dennis Mhini akimaliza kwa kishindo na kuibuka wa kwanza katika kundi la mchujo la kwanza (heat 1) katika mashindano ya Dunia ya Vijana yanayofanyika mjini Budapest, Hungary.

Waziri Kabudi afungua rasmi kikao kazi maalum cha Mabalozi wanaowakilisha Tanzania nchi mbalimbali za nje

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi amewataka Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje kuongeza jitihada katika kuhamasisha wawekezaji, wafanyabiashara na watalii kuja nchini ikiwa ni utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi. 
Waziri Kabudi ameyasema hayo tarehe 20 Agosti 2019 wakati akifungua rasmi  kikao kazi maalum cha Mabalozi kinachofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere  jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 20 hadi  23 Agosti 2019.
Mhe. Waziri Kabudi alisema kuwa, Mabalozi ambao wana jukumu kubwa la kusimamia maslahi ya Tanzania kwenye nchi mbalimbali duniani, wameendelea kufanya kazi nzuri katika  kuhakikisha dhana ya diplomasia ya uchumi inafikiwa na kwamba matokeo ya jitihada hizo ni pamoja na kuongezeka kwa watalii, wawekezaji na wafanyabiashara nchini. Pia kumekuwa na ongezeko la fursa za ufadhili wa masomo na ajira kwa Watanzania kwenye nchi mbalimbali.
“Hii ni mara yangu ya kwanza kukutana nanyi Waheshimiwa Mabalozi tangu niteuliwe na Mhe. Rais kwenye wadhifa huu. Nazipongeza jitihada zenu katika utekelezaji wa diplomasia ya uchumi kwani matokeo tunayaona kwa biashara kuongezeka hapa nchini watalii na hata wawekezaji. Hivyo nataka mwongeze jitihada zaidi ili nchi yetu ifikie azma yake ya kuwa nchi ya uchumi wa kati na viwanda ifikapo mwaka 2025” alisema Mhe. Kabudi”.
Aidha, Mhe. Waziri Kabudi alitoa rai kwa Mabalozi kuendelea kuwahamasisha Watanzania waishio nje (Diaspora) kujiandikisha na kuanzisha jumuiya zao ili kwa namna moja au nyingine na wao washiriki kuchangia maendeleo hapa nchini.
Akizungumzia changamoto mbalimbali zinazowakabili Mabalozi hao ikiwa ni pamoja na uchakavu wa baadhi ya majengo ya balozi, Mhe. Kabudi alieleza kuwa Wizara inaendelea kutafuta suluhisho la kudumu kwa changamoto hizo.
Akizungumza kwa niaba ya Mabalozi, Kiongozi wa Mabalozi hao, Mhe. Naimi Aziz, Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia alipongeza jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuanzisha na kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo Mabalozi walipata fursa ya kuitembelea. Alisema kuwa, miradi hiyo ni chachu ya maendeleo katika kuifikisha Tanzania kwenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025. 
"Tunaipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuanzisha miradi mikubwa ya kimkakati. Tumepata fursa ya kuiona miradi hiyo ikiwemo ile ya ujenzi wa barabara, reli na umeme. Kimsingi miradi hii inalenga kumwondolea umaskini Mtanzania kwa vile pamoja na mambo mengine itarahisha usafirishaji na kumwezesha mkulima kusafirisha kwa urahisi mazao yake kutoka sehemu moja kwenda nyingine kupitia miundombinu hiyo", alisema Balozi Aziz.
Pia aliipongeza Serikali kupitia Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kuandaa na kufanikisha Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kufanyika nchini kwa mafaniko makubwa.
Mhe. Prof. Paramagamba Kabudi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akitoa hotuba ya ufunguzi wa kikao kazi cha Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania sehemu mbalimbali duniani. Kikao hicho kinafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam Agosti 20,2019. Lengo la kikao hicho ni kujadili masula mbalimbali yanayohusu utekelezaji wa diplomasia ya uchumi. 
Katibu Mkuu  Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe akizumgumza kwenye kikao na Mabalozi wa wanaoiwakilisha Tanzania sehemu mbalimbali duniani. 

Mabalozi na Watendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia hotuba ya ufunguzi iliyo kuwa ikitolewa na  Waziri Mhe. Prof Kabudi (Hayupo pichani).
Sehemu ya Watendaji wa Wizara wakifuatilia kikao
Mabalozi wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi Wakuu wa Wizara mara baada ya ufunguzi wa kikao kazi cha Mabalozi
Viongozi Wakuu wa Wizara wakiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi Wanawake
Viongozi Wakuu wa Wizara  wakiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiao wa Afrika Mashariki mara baada ya ufunguzi wa Kikao kazi maalum.
Mhe. Naimi Aziz Balozi wa Tanzania Addis Ababa, Ethiopia akitoa hutuba kwenye ufunguzi wa Kikoa kazi cha Mabalozi kinachoendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam

TEDxOYSTERBAY YAKUTANISHA WADAU KUJADILI MAENDELEO NA CHANGAMOTO MBALI MBALI

$
0
0

Kongamano la kuongeza maarifa la TEDx Oysterbay, liilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na kuwakutanisha wadau kutoka nyanja mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi, ambapo walipata fursa ya kusikiliza mada na kubadilishana mawazo na uzoefu kuhusiana na masuala ya ubunifu, mapinduzi ya teknolojia,michezo na mada nyinginezo nyingi zenye kuelimisha zilizotolewa na wataalamu.Kampuni ya bia Tanzania (TBL) ilikuwa mmoja wa wadhamini wa kongamano hilo.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada wakati wa kongamano la TEDx Oysterbay lililofanyika katika ukumbi wa The Little Theatre jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wakibadilishana mawazo wakati wa kongamano hilo
Baadhi ya washiriki wakifurahi katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kongamano hilo

MBATIA ATUMIA JUBILEI YA MIAKA 25 PA PADRE KESSY KUSHAURI JAMBO SADEC

$
0
0
Askofu wa Jimbo la Katoliki la Same,Mhashamu Rogathe Kimario akiongoza ya misa takatifu ya Jubilei ya fedha ya miaka 25 ya Padri Thomas Salekio Kesyy iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Yohani Mtume ,Parokia ya Iwa-Kirua Vunjo mkoani Kilimanjaro.
Mbunge wa Jimbo la Vunjo ,James Mbatia alikuwa miongoni mwa waumini walioshiriki Ibada hiyo ,ambapo Padri Thomas Kessy ni kaka yake mkubwa .
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika Ibada ya Misa ya takatifu ya Jubilei ya fedha ya miaka 25 ya Padri Thomas Kessy .
Padri Thomas Kessy akizungumza wakati wa ibada hiyo.
Baadhi ya ndugu wa Padri Thomas Kessy wakishiriki ibada hiyo.
Mbunge wa jimbo la Vunjo ,James Mbatia akitoa hotuba yake wakati wa ibada ya Misa takatifu ya Jubilei ya fedha ya kaka yake Padri Thomas Kessy .
Askofu wa Jimbo la Katoliki la Same,Mhashamu Rogathe Kimario akimkabidhi Padri Thomas Kessy sululu na vitu vingine vilivyotolewa kanisani hapo kama kumuunga mkono.
Baada ya kumalizika kwa misa hiyo ,shughuli ilihamia nyumbani kwa familia hiyo eneo la Kirua Vunjo wilaya ya Moshi.
Padri Thomas Kessy akiwaongoza ndugu zake kufungua Champegne wakati wa hafala fupi ya pongezi kwa Padri Thomas Kessy kufikisha miaka 25 ya utume.
Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia akiwawekea wageni waalikwa kinywaji cha Champegne wakati wa hafla hiyo
Padri Thams Kessy akikata ndafu katika hafla hiyo.
Padri Thomas Kessy akimlisha kipande cha ndafu  Askofu wa Jimbo la Katoliki la Same,Mhashamu Rogathe Kimario.
Baadhi ya wageni wakiwa katika hafla hiyo.
Wageni wakicheza muziki na Padri Thomas Kessy katika hafla hiyo hiy iliyofanyika nyumbani kwa familia ya Mbatia.

Na Dixon Busagaga.
MWENYEKITI wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) ambaye pia ni Mwenyekiti wa taifa wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, amewapa neno wakuu wa nchi 16 zinazounda Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), katika mkutano ujao kufikiria kuja na ajenda ya pamoja ya sera moja ya elimu inayofanana.

Mbatia amesema kuwa kama itakuwapo dhamira ya pamoja ya kuwa na sera hiyo ya elimu kwa wanachama wa SADC, kunaweza kubadili sura ya Afrika na mageuzi makubwa yakaonekana kwa miaka 20 yakisadifu mfumo wa elimu wa nchi za Ulaya.

Mbatia ametoa kauli hiyo mara  baada ya kumalizika kwa ibada ya misa takatifu ya Jubilee ya fedha ya miaka 25 ya Padri Thomas Salekio Kessy, iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Yohani Mtume, Parokia ya Iwa-Kirua Vunjo, mkoani Kilimanjaro.

Ibada hiyo iliongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Same, Mhashamu Rogathe Kimario, akisaidiwa na Msimamizi wa Jimbo Katoliki la Moshi na Wakili wa Askofu, Deogratius Matiika.

“Kwa mfano, majuzi nilisikia na kusoma baadhi ya maandiko kwamba watu wa Namibia wao wanasema mfano mwanafunzi anayetoka Tanzania na amemaliza kidato cha sita na akienda kwao, kupata Chuo Kikuu kule ni shida, kwa sababu Namibia wao mfumo wao ni mgumu, wao elimu zao wanamalizia kidato cha nne. Unajiuliza hivi silabasi zetu zimeundwa namna gani, nawashauri wakuu wa nchi wanachama ni vizuri tukawa na sera moja ya SADC katika masuala ya elimu,”alisema

Mwaka huu, Tanzania imekuwa mwenyeji wa mkutano wa 39 wa SADC ikiwa imepita miaka 16, tangu mkutano kama huo kufanyika kwa mara ya mwisho mwaka 2003 chini ya utawala wa Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa.

Kuhusu Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika, kuweka mikakati ya kuziwezesha nchi wanachama kufikia malengo ya kuelekea kwenye ukuaji wa uchumi wa kati utakaokuwa maendeleo ya viwanda, Mbatia alisema:

“Mimi nina ushauri kwa SADC, pamoja na mambo ya viwanda na mambo mengine yote ambayo ni muhimu, wakuu wa nchi 16 wajitahidi sana kuhakikisha nguvu kazi ya SADC ambayo ni vijana, wanapata elimu ambayo ni ujuzi na wanaweza kuzalisha kwenye viwanda, wanaweza kuondoa masuala ya umasikini, njaa, watu wakawa na afya njema lakini penda tusipende ni lazima tuangalie je mifumo yetu ya elimu ikoje,”alieleza

Alisema malengo hayo yanatekelezeka, lakini sharti nchi wanachama wawe wamejiandaa vizuri na kwa utafiti alioufanya, bado kuna kazi kubwa mbele ya safari, na akashauri zaidi kuwa malengo hayo yasiwe ya maneno, yaende kwenye vitendo zaidi.

DKT.CHAULA AMPONGEZA MHE.RAIS KWENYE SEKTA YA AFYA

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto 
Dkt. Zainab Chaula.

Na.Catherine Sungura, WAMJW-Dodoma

KATIBU Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa uwekezaji mkubwa aliouweka katika sekta ya afya nchini.


Dkt. Chaula ameyasema hayo jana wakati wa mahojiano na kituo cha runinga cha Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1) wakati wa taarifa ya habari baada ya Mhe. Rais kutembelea Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali iliyopo jijini Dar es Salaam.


Katika mahojiano hayo Dkt. Chaula alisema kuwa Serikali ya awamu ya tano sio kwamba imewekeza tu kwa mamlaka ya maabara ya mkemia mkuu wa serikali bali katika sekta yote ya afya kwa kuboresha huduma za afya kwa upande wa miundombinu, dawa, vifaa na vifaa tiba katika hospitali pamoja na taasisi zake.


Kwa upande kwa mamlaka ya maabara ya mkemia mkuu wa serikali alisema kuwa serikali kupitia wizara ya afya imefanya jitihada kubwa za kusogeza huduma za mamlaka hiyo katika kanda zote nchini na hivi karibuni inatarajia kuwa na kanda nyingine jijini Dodoma.


“Sisi hapa kwa afrika mashariki, Tanzania tunaongoza kwa kuwa na mitambo ya uchunguzi ya kisasa vya kufanya utambuzi wa miili na tuna imani tutapokea hata vinasaba kutoka nchi za jirani pale panapotokea mkanganyiko hususani kwenye kesi za jinai,ajali,sumu,madawa ya kulevya pamoja na kemikali.


Dkt. Chaula alisema mitambo hiyo ya kisasa inatoa majibu ndani ya siku saba tofauti na zamani ambapo sampuli thelathini na tano zilichukua mwezi kuthibitisha ila kwa sasa wanachukua sampuli hadi mia mbili.


Hata hivyo katibu Mkuu huyo amewashauri watanzania kupenda na kujenga mazoea ya kutumia taasisi za serikali zilizopo nchini hususani mamlaka ya mkemia mkuu wa serikali pale panapotokea mkanganyiko kwa kisheria au utambuzi wa vinasaba mbalimbali.

DKT. KALEMANI AIFAFANULIA KAMATI YA BUNGE UUNGANISHWAJI UMEME WATEJA VIJIJINI

$
0
0
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kuhusu umeme vijijini, mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, katika kikao kilichofanyika Dodoma, Agosti 20, 2019.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kuhusu umeme vijijini, mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, katika kikao kilichofanyika Dodoma, Agosti 20, 2019. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Amos Maganga akiwasilisha taarifa ya maendeleo na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umeme vijijini kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, katika kikao kilichofanyika Dodoma, Agosti 20, 2019.


Viongozi na wataalamu wa Wizara ya Nishati na Taasisi zilizo chini yake, wakiwa katika kikao kilichohusisha uwasilishaji taarifa ya maendeleo na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umeme vijijini kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, kilichofanyika Dodoma, Agosti 20, 2019.

Na Veronica Simba – Dodoma
WAZIRI wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ameieleza Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuwa idadi ya  wanaounganishiwa umeme vijijini kupitia miradi mbalimbali inayoendelea ni ya awali na itakuwa ikiongezeka kadri wananchi husika watakavyokuwa wakilipia gharama yake ambayo ni shilingi 27,000 tu.

Alieleza hayo leo, Agosti 20, 2019 jijini Dodoma, wakati akijibu hoja iliyoibuliwa na wajumbe kadhaa wa Kamati hiyo walioonesha wasiwasi wao kuwa idadi ya wananchi wanaounganishiwa umeme vijijini ni ndogo.

“Kinachofanyika hivi sasa ni kupeleka miundombinu ya umeme katika maeneo mbalimbali vijijini na kuunganisha wateja wa awali. Wengine wataendelea kuunganishwa kwa wakati wao kadri wanavyolipia,” alifafanua Waziri.

Aidha, kuhusu agizo la serikali kwa wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini, kutumia vifaa vya ndani ya nchi, Waziri ameieleza Kamati husika kuwa msimamo huo unatokana na matumizi ya vifaa vya ndani kuwa na tija zaidi kuliko vinavyoagizwa kutoka nje ya nchi.

Akifafanua, alieleza kuwa kuagiza vifaa nje ya nchi ni gharama kubwa ukilinganisha na kutumia vifaa vya ndani. Pia, alisema, ni rahisi zaidi kwa serikali kusimamia na kudhibiti ubora wa vifaa vya ndani kuliko vinavyotengenezwa nje ya nchi. Vilevile, aliongeza kuwa muda unaotumika kupata vifaa vinavyotengenezwa ndani ya nchi tangu siku vinapoagizwa ni mdogo kulinganisha na ule unaotumika kuagiza na kuletewa vifaa hivyo kutoka nje ya nchi.

Waziri pia alizungumzia katazo lililotolewa na serikali kuhusu wananchi vijijini kulipia nguzo ambapo alisema uamuzi huo ulifikiwa ili kuwapunguzia gharama wananchi hao ambao wengi kipato chao ni kidogo.

“Kwa uhalisia, umeme vijijini unatolewa bure kwa wananchi na gharama zake kuchukuliwa na serikali. Hata hiyo 27,000 wanayolipa ni gharama za ushuru wa thamani tu ambayo ni asilimia 18 ya gharama husika. Sasa ukimlipisha mwananchi huyo nguzo itarudisha tatizo palepale, hivyo nasisitiza tena kwamba wananchi wa vijijini hawatakiwi kulipia nguzo.”

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Amos Maganga, ameieleza Kamati hiyo kuwa, tangu kuanzishwa kwake, REA imetekeleza miradi mbalimbali ikiwemo Miradi ya Awali, Mradi wa Kupeleka Umeme Vijijini Awamu ya Kwanza (REA I), Awamu ya Pili (REA II) na Awamu ya Tatu (REA III).

Amesema kuwa kukamilika kwa miradi hiyo mwaka 2021, kutawezesha vijiji vyote 12,268 vya Tanzania Bara kufikiwa na miundombinu ya umeme.

Katika kikao hicho, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ilikuwa ikipokea taarifa ya maendeleo na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya REA pamoja na changamoto inazokabiliana nazo.

Wengine walioshiriki kikao hicho ni Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara, Haji Janabi pamoja na viongozi mbalimbali wa Wizara na Taasisi zilizo chini yake.

TWENDE PAMOJA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA –DKT NDUGULILE

$
0
0
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile (katikati) akizungumza na vyombo vya habari leo Jijini Dodoma kuhusu Kampeni ya Kitaifa ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia, kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Jinsia Bi. Mboni Mgaza na kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Jinsia Bw. John Mapunda.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

Na Anthony Ishengoma WAMJW
NAIBU Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa mtoto wa kike uzidi kukua kiuchumi kulingana na muda anaokaa shuleni akiongeza kuwa mwanamke anavyozidi kujiendeleza kielimu upunguza uwezekano wa kuwa na idadi kubwa ya watoto na na kufanyiwa vitendo vya kikatili.

Dkt. Ndugulile amesema hayo leo Jijini Dodoma wakati wa akiitambulisha Kampeni mpya ya Kitaifa ya kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto ijulikanayo kama Twende Pamoja inayolenga kushirikisha wanaume na wanawake kwa lengo la kutoa elimu kwa jamii kupitia mbinu anwai.

Aidha Dkt. Ndugulile amesisitiza kuwa kuwepo kwa elimu bure nchini kwa kiasi kikubwa kumepunguza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake ikiwemo mimba na ndoa za utotoni pamoja na uwepo wa Sheria inayotoa adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela kwa anayebainika kufanya vitendo hivyo.

Dkt. Ndugulile ametaja wastani wa watoto kwa mwanamke wa Tanzania kuwa watano hivyo kadri msichana anavyokaa shuleni anapunguza uwezekano wa wa kuzaa watoto wengi lakini pia akasema uwezi ukalinganisha kipato cha Msichana wa kidato cha nne na yule wa Darasa la Saba.

Akizungumzia kuhusu kauli mbiu ya kampeni hiyo Dkt. Ndugulile ameviambia vyombo vya habari kuwa yeye kama Naibu Waziri anachukizwa na vitendo vya ukatili dhidi ya Wanawake hivyo akachukua fursa hiyo kuhamasisha pia wanaume wengine nchini kuchukia vitendo hivyo akiitaja kauli mbiu ya Kampeni hiyo kuwa ni ''Ukatili wa Kijinsia Tanzania sasa basi’’.

Akizungumzia hali ya ukatili wa kijinsia Nchini Dkt. Ndugulile amesema taarifa ya hali ya Uhalifu nchini ya Mwaka 2017 inaonesha kuwa jumla ya watu 41,416 waliofanyiwa ukatili wa kijinsia walitoa taarifa kwenye vituo vya polisi ikilinganishwa na watu 31,996 waliofanya hivyo mwaka 2016.

Dkt. Ndugulile ameyataja baadhi ya matukio ya ukatili yaliyotolewa taarifa kuwa ni ubakaji, vipigo, matusi, ulawiti, kutupa watoto, ukeketaji na kuwapa mimba wanafunzi na kuongeza kuwa kati ya mataukio hayo 41,416 yaliyotolewa taarifa mwaka 2017 matukio 27,703 sawa na asilimia 67 yalifanywa dhidi ya wanawake na watoto.


Dkt. Ndugulile ameongeza kuwa asilimia 40 ya wanawake wa umri kati ya miaka 15-49 wamefanyiwa ukatili wa kimwili au kingono mara moja au zaidi katika kipindi hicho cha maisha wakati wanawake asilimia 20 wenye umri miaka 15-49 wamefanyiwa ukatili wa kimwili katika kipindi cha miezi 12 iliyopita.

Dkt. Ndugulile amefafanua kuwa Wizara ianshirikiana na wasanii katika kufikisha ujumbe na amemtaja Msanii Nurdin Bilal Maarufu SHETTA kuwa amejitolea kuwa Balozi wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto na atataumia jukwaa la Sanaa kuelimisha jamii kwa kutumia mziki wake na mitandao ya kijamii.

''Ni matarajio yangu kwamba kampeni hii ya Kupinga Ukatilili wa Kijinsia Kitaifa italeta mabadiliko makubwa kupitia jumbe mbalimbali zilizoandaliwa kupitia muziki, machapisho, nyimbo, shuhuda na Semina zitakazokuwa zinaendelea kutolewa kwenye majukwaa mbalimbali kipindi cha kampeni’’. Alihitimisha Dkt. Ndugulile.

MAJERUHI 32 KATI YA 47 WA JANGA LA MOTO MOROGORO WAMEFARIKI DUNIA MUHIMBILI

$
0
0

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

MAJERUHI 32 kati ya 47 wa ajali ya moto iliyotokea Agosti 10 mwaka huu Mkoani Morogoro wamefariki dunia hadi kufikia asubuhi ya leo, huku wagonjwa waliobaki hospitalini hapo ni 15 ambapo wagonjwa13 wapo chumba cha wagonjwa mahututi na wawili ambao ni wanawake wapo wodi ya kawaida (Sewahaji.)

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkuu wa kitengo Cha mawasiliano ya umma wa hospitali ya taifa Muhimbili Aminiel Aligaesha amesema kuwa kumekuwa na maswali mengi katika mitandao ya kijamii kuhusiana na hali za wagonjwa hao hasa kutokana na namna wanavyopoteza maisha licha ya kupelekwa katika hospitali hiyo.

"Janga hili limegusa jamii na taarifa tunatoa kila asubuhi ili jamii isiseme tunaficha, na tunapenda kuwataarifu watanzania kuwa serikali kwa kushirikiana na hospitali ya taifa Muhimbili imetumia fedha, utaalamu, ujuzi na rasilimali katika kuokoa maisha ya wenzetu 32 waliopoteza maisha, na hatuangalii mtu ameungua kiasi gani huduma zote zitatolewa bila kuangalia ni kiasi gani ameungua" ameeleza Aligaesha.

Daktari bingwa wa upasuaji kutoka hospitali ya taifa Muhimbili Dkt. Edwin Mrema amesema kuwa katika ajali ya moto kitu cha kwanza kinachoangaliwa ni kuzuia moto usitokee na kuleta madhara zaidi.

"Lazima jamii ifahamu kuhusiana na kuungua moto, katika janga hili wengi wameathirika katika mfumo wa upumuaji, figo na kupata vidonda katika asilimia kubwa ya mwili hali inayopelekea kuathirika kwa urahisi vijidudu kutokana na ngozi yao kuwa wazi, na wagonjwa wetu waliungua katika mazingira ya wazi hivyo wakaanza kuathirika palepale na walipoteza maji kwa kiasi kikubwa na chembembe nyingine za protein na chumvi" ameeleza. 

Amesema kuwa majeruhi hao wameungua kwa asilimia kubwa na wana uhitaji mkubwa wa tiba zaidi."Majeruhi waliungua moto katika eneo la wazi na kuathirika kwa kuunguza ngozi na kibaya zaidi kuvuta moshi wa kemikali iliyowafanya kuwa katika hali hatarishi" ameongeza.

Pia daktari bingwa wa magonjwa ya upasuaji Laurean Rwanyuma amesema kuwa wagonjwa wengi walioletwa katika hospitalini hapo walikuja wakiwa wameungua kati ya asilimia 70 hadi 100 na kuathirika sana katika mfumo wa upumuaji kutokana na moshi waliovuta.

Amesema kuwa wanajitahidi kupambana kuokoa maisha ya wagonjwa hao kwa kuhakikisha hawapati baridi, wanapata dripu za maji pamoja na dawa za kupunguza maumivu."Wagonjwa wengi wameathirika kwenye mapafu na wapo kwenye mashine ya oksijeni kwa kuwa hata ubongo unahitaji pia" ameeleza Rwenyuma.

Amesema kuwa serikali kwa kushirikiana na wafanyakazi wanapambana kuokoa maisha ya wagonjwa hao hasa kuwakinga wasishambuliwe na wadudu na wanaendelea kupambana kuokoa maisha yao.

"Kuna wengine wameungua kwa asilimia 80 bado tunapambana Ila kuna wengine waliungua chini ya asilimia 50 pia wapo hospitalini hapo na wanaendelea kupata tiba.

Kuhusiana na tetesi za uhaba na kuwepo wa uhaba wa wataalamu na vifaa tiba hospitalini hapo hali inayopelekea wagonjwa wengi kupoteza maisha Daktari Rwanyuma amesema kuwa wataalamu na vifaa vipo lakini tatizo kubwa lililojitokeza ni wagonjwa kuungua kwa asilimia kubwa na wengine kuungua kwa asilimia 100.
Daktari bingwa wa upasuaji  katika Hospitali ya Taifa Muhimbili,Laurean Rwanyuma (katikati) akizungumza na waandishi wa habari   leo kuhusu vifo na hali za majeruhi wa janga la moto lilitokea Agosti 10 Mkoani Morogoro, baada ya Lori la mafuta kulipuka,ambapo amesema majeruhi 32 kati ya 47 wa ajali hiyo wamefariki Dunia hadi kufikia asubuhi ya leo Agosti 21,2019. Majeruhi wengine 15 wanaendelea kupatiwa matibabu na kati ya hao 13 wamelazwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU). Kulia ni daktari bingwa wa upasuaji Edwin Mrema na kushoto ni Ofisa uhusiano na mawasiliano kwa umma wa hospitali hiyo, Aminiel Aligaesha.

WAZIRI UMMY AIPONGEZA WHO KWA KUSAIDIA KUDHIBITI EBOLA NCHINI KONGO

$
0
0


Na WAMJW- Brazzaville 

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amelipongeza Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo kwa juhudi inazofanya kwa pamoja katika kudhibiti ugonjwa wa Ebola. 

Waziri Ummy amesema hayo leo wakati akiwasilisha taarifa ya mkakati wa kukabiliana na ugonjwa wa Ebola katika mkutano wa 69 wa Shirika la Afya Duniani (WHO) unaojumuisha Mawaziri wa Afya kutoka nchi mbalimbali za Afrika unaoendelea jijini Brazzaville nchini Jamhuri ya Kongo. 

Aidha, Waziri Ummy amempongeza Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt. Tedros Adhanom kwa kutangaza Ebola kuwa janga la Kimataifa, na kuongeza kuwa Tanzania imefaidika na msaada wa WHO ambao umeiwezesha nchi kujenga uwezo wa utayari wa kukabiliana na ugonjwa huo iwapo utaingia nchini. 

Waziri Ummy amesema kumekua na uboreshaji wa mpango mkakati wa Ebola uliofanyika Mwezi Machi Mwaka 2019 ambao umelenga kuimarisha ufuatiliaji wa mgonjwa maeneo ya mipakani, kujenga uwezo wa watumishi wa afya kumtambua mgonjwa na kutoa matibabu, kununua vifaa vya kujikinga (PPE) na uratibu huu wa kukabiliana na Ebola umeshirikisha sekta mbalimbali zaidi ya Afya. 

Pamoja na hayo, Waziri Ummy ametaja maeneo ambayo WHO isaidie ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa rasilimali fedha kwa ajili ya kutekeleza mpango mkakati wa kukabiliana na Ebola, kuimarisha ufuatiliaji katika ngazi ya jamii na kufanya mazoezi zaidi ya kupima utayari wa nchi. 

Pia Waziri Ummy alitaka kujua chanjo ya ugonjwa Ebola inachukua muda gani kuanza kufanya kazi baada ya mtu kuchanjwa ambapo majibu yalitolewa kuwa chanjo hiyo inaanza kufanya kazi baada ya siku kumi huku muda wake wa kumkinga mtu ukiwa bado katika utafiti. 

Vile vile Waziri Ummy alitaka kupata ufafanuzi kuwa chanjo hiyo ni kwa ajili ya aina gani ya virusi vya Ebola na ufafanuzi ulitolewa kuwa chanjo hiyo ni kwa ajili ya kirusi cha Zaire ambacho kwa sasa ndicho kinachosababisha mlipuko wa Ebola nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo.

JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA YA WASHIKILIA WATU 13

$
0
0
JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAWASHIKILIA WATU KUMI NA TATU (13) KWA TUHUMA ZA KUJIHUSISHA NA MAKOSA MBALIMBALI YA KIUHALIFU YALIYOTENDEKA KATIKA MAENEO MBALIMBALI MKOANI MWANZA.

TUKIO LA KWANZA
KWAMBA TAREHE 20.08.19 10:00 HRS MTU MMOJA AITWAYE SAMWEL JOHN @ MTUMWA, MIAKA 26, MSUKUMA, MKAZI WA KIJIJI CHA MIGOMBANI - LUHAMA WILAYANI SENGEREMA ALIUAWA KWA KUSHAMBULIWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE KWA KUTUMIA FIMBO NA MAWE NA KUNDI LA WAHALIFU (WANANCHI) WALIOJICHUKULIA SHERIA MKONONI WAKATI ALIPOKUA AMEHIFADHIWA KATIKA OFISI YA MWENYEKITI WA SERIKALI YA KIJIJI CHA BULYAHIRU AKISUBIRI KUPELEKWA KITUO CHA POLISI BAADA YA KUKAMATWA KWA TUHUMA ZA WIZI WA MKUNGU MMOJA WA NDIZI.

HATUA HIYO YA MAUAJI ILITOKEA BAADA  YA MWENYEKITI WA KIJIJI HICHO KUJARIBU KUWAZUIA WATU HAO AMBAO WALIANZA PIA KUMSHAMBULIA ALIPOWASILIANA NA   POLISI ILI WAFIKE KUMCHUKUA NA POLISI WALIPOFIKA WALIANZA KUSHAMBULIWA NA HIVYO KULAZIMIKA KUMUOKA MWENYEKITI HUYO BAADA YA MTUHUMIWA KUWA AMEUAWA.

KATIKA KUMUOKOA MWENYEKITI  HUYO ASKARI NO D 9777 SGT JUMA ALIJERUHIWA KWA JIWE KICHWANI, NA MWENYEKITI BENJAMINI KAHITIRA ALIUMIA KWENYE PAJI LA USO NA WATU WAWILI AMBAO NI DORICA MAJINGO ALIJERUHIWA KWA RISASI KWENYE PAJA LA MGUU WA KULIA NA MUSA MANGE ALIJERUHIWA KWENYE GOTI LA KUSHOTO KWA RISASI BAADA YA KUWA WANAWASHAMBULIA ASKARI POLISI KWA MAWE.  MAJERUHI WALIPELEKWA HOSPITALI YA WILAYA SENGEREMA KWA MATIBABU NA HALI ZAO ZINAENDELEA VIZURI.

JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAWASHIKILIA WATU 11 KUHUSIANA NA TUKIO HILO, AIDHA KAZI YA KUWATAFUTA WATU WENGINE AMBAO WAMEHUSIKA KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE BADO INAENDELEA. 

JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINATOA ONYO KWA WANANCHI WENYE TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI  WAACHE TABIA HIYO KWANI NI KOSA LA JINAI. AIDHA, KWA YEYOTE ATAKAYEBAINIKA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI HATUA STAHIKI ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA DHIDI YAKE.




TUKIO LA PILI
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LAFREDRICK S/O CHENGULA, MIAKA 32, MFANYABIASHARA, MNGONI, MKAZI WA MBEZI – DAR ES SALAAM ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUJIPATIA FEDHA KWA NJIA YA UDANGANYIFU (UTAPELI) KUTOKA KWA MFANYABIASHARA/MUWEKEZAJI   WA MADINI AITWAYE MOHAMED MUNNOO, MIAKA 35, RAIA WA MAURITIUS AMBAYE, WALIMTAPELI DOLLA ELFU SITINI (US$ 60,000) SAWA NA TSHS 138,000,000/=, FEDHA ZA KITANZANIA, KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI.

TUKIO HILO LILITOKEA TAREHE 19.04.109, BAADA YA MFANYABIASHARA HUYO WA MADINI RAIA WA MAURITIUS  KUKUTANA NA WATU HAO (MATAPELI ) WALIOJIFANYA NI M,AAFISA WA SERIKALI NA KUMPELEKA KWENYE OFISI MBALIMBALI ZA KUUZA MADINI YA DHAHABU. AIDHA BAADA YA KUPEWA TAARIFA HIZO RAIA HUYO WA MAURITIUS  ALIELEKEZWA KUWEKA PESA KWENYE ACCOUNT YA MMOJA WAO KATIKA EQUITY BENKI TAWI LA MWANZA YENYE NAMBA 3007211416820 FAMM AMTL CO.LTD, ILI AWEZE KUPATIWA MADINI YA DHAHABU YENYE UZITO WA KILOGRAMU 7.

HATA HIVYO BAADA YA MATAPELI HAO KUINGIZIWA KIASI HICHO CHA FEDHA WALITOROKA, UFUATILIAJI ULIWEZESHA KUWAKAMATA WATUHUMIWA WAWILI. NA BAADAE KIONGOZI WAO NAE AMEKAMATWA AKITOKEA NCHI JIRANI. 

IMETOLEWA NA:-
Muliro J. MULIRO-ACP
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA
21 AGOSTI 2019.

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MRATIBU MKAZI WA UN

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimina na Mratibu Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa hapa Nchini Bw. Alvaro Rodriguez wakati Bw. Alvaro alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Jijini Dar Es Salaam leo Agost 21,2019 kwa ajili ya kumuaga Makamu wa Rais baada ya kumaliza kipindi chake cha Uwakilishi hapa nchini. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mratibu Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa hapa Nchini Bw. Alvaro Rodriguez wakati Bw. Alvaro alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Jijini Dar Es Salaam leo Agost 21,2019 kwa ajili ya kumuaga Makamu wa Rais baada ya kumaliza kipindi chake cha Uwakilishi hapa nchini .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 

=========
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali ya Tanzania itaendelea kuunga mkono mageuzi ya mfumo wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa kwenye maeneo mbalimbali yaliyoafikiwa. 


Amesema Tanzania itaendelea na mpango wa pili wa Maendeleo wa Msada wa Umoja wa mataifa ambao unatekelezwa sambamba na Dira ya Zanzibar ya 2020 pamoja na awamu ya pili ya mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano wa Taifa (F2016,2021 FYDP2) wenye lengo la kuisaidia Tanzania kufikia Uchumi wa kati ifikapo Mwaka 2025. 

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo Agost 21, 2019 Ofisini kwake Ikulu Jijini Dar Es Salaam wakati alipokutana na kufanya Mazungumzo na Bw. Alvaro Rodriguez Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa ayefika Ofisini kwake kwa ajili ya kumuaga Baada ya kumaliza kipindi chake cha Uwakilishi hapa Nchini. 

Aidha Makamu wa Rais amemshukuru Bw. Alvaro kwa Ushirikiano na Uhusiano Mzuri alioujenga baina ya Tanzani na Umoja wa Mataifa katika kipindi chake chote alichokuwepo hapa Nchini kwa kusukuma Agenda za Nchi na kuiletea mafaniko katika Sekta mbalimbali na kumtakia kila la heri na kazi njema katika kituo chake kipya cha kazi, ambapo Bw. Alvaro ameteuliwa kuwa Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Nchini Uturuki. 

Wakati huo huo Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa hapa Nchini Bw. Alvaro ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuwasilisha Taarifa za mapitio ya Hiyari (VNR) ya Utekelezaji wa Maelengo ya Maendeleo Endelevu ya Mwezi Julai 2019 kwa kuwainisha Mafanikio, Changamoto na mbinu bora za kukabiliana nazo pamoja na kujifunza.

UN YAIPONGEZA TANZANIA KWA MATUMIZI MAZURI YA RASILIMALI

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akutana na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa,anaye maliza muda wake hapa Nchini Tanzania Bw. Alvaro Rodriguez .kwa ajili ya kumuaga Waziri Mkuu ofisini kwake .Magogoni jijini Dar es Salaam.leo Agosti 21.2019
UMOJA wa Mataifa (UN) umeipongeza Serikali ya Tanzania kwa namna inavyotumia vizuri rasilimali zake za ndani na hivyo kuiwezesha kutekeleza shughuli mbalimbali za kimaendeleo sambamba na kupunguza utegemezi kutoka nje.

Pongezi hizo zimetolewa leo (Jumatano, Agosti 21, 2019) na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa, Bw. Alvaro Rodriguez alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ofisini kwa Waziri Mkuu Magogoni jijini Dar es Salaam.

Mratibu huyo Mkazi wa Umoja wa Mataifa ambaye alikwenda kumuaga Waziri Mkuu, amesema kuwa Tanzania imeendelea kutumia vizuri mapato yake ya ndani kwa kuimarisha miundombinu na huduma za kijamii kama ujenzi wa hospitali na vituo vya afya.

“Katika kipindi changu cha miaka mitano ambacho nimefanya kazi Tanzania, nimeshuhudia mabadiliko makubwa ya kimaendeleo yanayofanywa na Serikali, ikiwemo kuimarika kwa mahusiano kati ya Serikali na Umoja wa Mataifa na taasisi zake nchini.”

Katika hatua nyingine, Bw. Rodriguez ameisifu Serikali ya Tanzania kwa namna ilivyoweza kuandaa na kuendesha vizuri mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika Agosti 17 na 18 mwaka huu.

Mbali na kuisifu Serikali pia kiongozi huyo amevipongeza vyombo vya habari kwa jinsi vilivyoshirikiana na Serikali kuripoti matukio mbalimbali ya mkutano huo. “Nawapongeza na wananchi kwa ushirikiano walioutoa kwa Serikali wakati wote wa mkutano wa SADC.”

Kwa upande wake, Waziri Mkuu amemshukuru kiongozi kwa pongezi alizozitoa ambazo ni ishara kwamba anatambua jitihada zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli katika kutumia vizuri rasimali zake.

Waziri Mkuu amesema “maelezo yaliyotolewa na Bw. Rodriguez yanaakisi kauli za Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwamba Tanzania si nchi masikini na inayo uwezo wa kutoa misaada kutokana na rasilimali nyingi ilizonazo. Watanzania waendelee kuiunga mkono Serikali yao.”

Pia, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kumpongeza kiongozi huyo kwani alikuwa kiungo kizuri kabaina ya Serikali ya Tanzania na Umoja wa Mataifa. Pia atakumbukwa sana kutokana na mambo mengi aliyoyafanya kipindi cha utumishi wake nchini Tanzania.

Awali, Waziri Mkuu alikutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Afrika Kusini, Mheshimiwa Balozi Thamasanqa Dennis Mseleku ambaye alikwenda kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kufanya kazi nchini Tanzania.

Waziri Mkuu alimpongeza Balozi huyo kwa ushirikiano na mchango alioutoa kwa Serikali ya Tanzania katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo zikiwemo za kiuchumi, elimu, afya, maendeleo ya jamii pamoja na kuimarisha uhusiano baina ya nchini mbili hizo.

Kwa upande wake, Mheshimiwa Balozi Mseleku ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano mkubwa uliompatia katika kipindi chake cha utumishi akiwa nchini na kwamba alitamani aendelee kubaki Tanzania.

DKT.CHAULA AMPONGEZA RAIS KWENYE SEKTA YA AFYA

$
0
0
Na.Catherine Sungura, WAMJW-Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa uwekezaji mkubwa aliouweka katika sekta ya afya nchini.

Dkt. Chaula ameyasema hayo jana wakati wa mahojiano na kituo cha runinga cha Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1) wakati wa taarifa ya habari baada ya Mhe. Rais kutembelea Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali iliyopo jijini Dar es Salaam.

Katika mahojiano hayo Dkt. Chaula alisema kuwa Serikali ya awamu ya tano sio kwamba imewekeza tu kwa mamlaka ya maabara ya mkemia mkuu wa serikali bali katika sekta yote ya afya kwa kuboresha huduma za afya kwa upande wa miundombinu, dawa, vifaa na vifaa tiba katika hospitali pamoja na taasisi zake.

Kwa upande kwa mamlaka ya maabara ya mkemia mkuu wa serikali alisema kuwa serikali kupitia wizara ya afya imefanya jitihada kubwa za kusogeza huduma za mamlaka hiyo katika kanda zote nchini na hivi karibuni inatarajia kuwa na kanda nyingine jijini Dodoma.

“Sisi hapa kwa afrika mashariki, Tanzania tunaongoza kwa kuwa na mitambo ya uchunguzi ya kisasa vya kufanya utambuzi wa miili na tuna imani tutapokea hata vinasaba kutoka nchi za jirani pale panapotokea mkanganyiko hususani kwenye kesi za jinai,ajali,sumu,madawa ya kulevya pamoja na kemikali.

Dkt. Chaula alisema mitambo hiyo ya kisasa inatoa majibu ndani ya siku saba tofauti na zamani ambapo sampuli thelathini na tano zilichukua mwezi kuthibitisha ila kwa sasa wanachukua sampuli hadi mia mbili.

Hata hivyo katibu Mkuu huyo amewashauri watanzania kupenda na kujenga mazoea ya kutumia taasisi za serikali zilizopo nchini hususani mamlaka ya mkemia mkuu wa serikali pale panapotokea mkanganyiko kwa kisheria au utambuzi wa vinasaba mbalimbali.

TWENDE PAMOJA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA –DKT NDUGULILE

$
0
0

Na Anthony Ishengoma WAMJW 

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa mtoto wa kike uzidi kukua kiuchumi kulingana na muda anaokaa shuleni akiongeza kuwa mwanamke anavyozidi kujiendeleza kielimu upunguza uwezekano wa kuwa na idadi kubwa ya watoto na na kufanyiwa vitendo vya kikatili. 

Dkt. Ndugulile amesema hayo leo Jijini Dodoma wakati wa akiitambulisha Kampeni mpya ya Kitaifa ya kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto ijulikanayo kama Twende Pamoja inayolenga kushirikisha wanaume na wanawake kwa lengo la kutoa elimu kwa jamii kupitia mbinu anwai. 

Aidha Dkt. Ndugulile amesisitiza kuwa kuwepo kwa elimu bure nchini kwa kiasi kikubwa kumepunguza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake ikiwemo mimba na ndoa za utotoni pamoja na uwepo wa Sheria inayotoa adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela kwa anayebainika kufanya vitendo hivyo. 

Dkt. Ndugulile ametaja wastani wa watoto kwa mwanamke wa Tanzania kuwa watano hivyo kadri msichana anavyokaa shuleni anapunguza uwezekano wa wa kuzaa watoto wengi lakini pia akasema uwezi ukalinganisha kipato cha Msichana wa kidato cha nne na yule wa Darasa la Saba. 

Akizungumzia kuhusu kauli mbiu ya kampeni hiyo Dkt. Ndugulile ameviambia vyombo vya habari kuwa yeye kama Naibu Waziri anachukizwa na vitendo vya ukatili dhidi ya Wanawake hivyo akachukua fursa hiyo kuhamasisha pia wanaume wengine nchini kuchukia vitendo hivyo akiitaja kauli mbiu ya Kampeni hiyo kuwa ni ”Ukatili wa Kijinsia Tanzania sasa basi’’. 

Akizungumzia hali ya ukatili wa kijinsia Nchini Dkt. Ndugulile amesema taarifa ya hali ya Uhalifu nchini ya Mwaka 2017 inaonesha kuwa jumla ya watu 41,416 waliofanyiwa ukatili wa kijinsia walitoa taarifa kwenye vituo vya polisi ikilinganishwa na watu 31,996 waliofanya hivyo mwaka 2016. 

Dkt. Ndugulile ameyataja baadhi ya matukio ya ukatili yaliyotolewa taarifa kuwa ni ubakaji, vipigo, matusi, ulawiti, kutupa watoto, ukeketaji na kuwapa mimba wanafunzi na kuongeza kuwa kati ya mataukio hayo 41,416 yaliyotolewa taarifa mwaka 2017 matukio 27,703 sawa na asilimia 67 yalifanywa dhidi ya wanawake na watoto. 

Dkt. Ndugulile ameongeza kuwa asilimia 40 ya wanawake wa umri kati ya miaka 15-49 wamefanyiwa ukatili wa kimwili au kingono mara moja au zaidi katika kipindi hicho cha maisha wakati wanawake asilimia 20 wenye umri miaka 15-49 wamefanyiwa ukatili wa kimwili katika kipindi cha miezi 12 iliyopita. 

Dkt. Ndugulile amefafanua kuwa Wizara ianshirikiana na wasanii katika kufikisha ujumbe na amemtaja Msanii Nurdin Bilal Maarufu SHETTA kuwa amejitolea kuwa Balozi wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto na atataumia jukwaa la Sanaa kuelimisha jamii kwa kutumia mziki wake na mitandao ya kijamii. 

”Ni matarajio yangu kwamba kampeni hii ya Kupinga Ukatilili wa Kijinsia Kitaifa italeta mabadiliko makubwa kupitia jumbe mbalimbali zilizoandaliwa kupitia muziki, machapisho, nyimbo, shuhuda na Semina zitakazokuwa zinaendelea kutolewa kwenye majukwaa mbalimbali kipindi cha kampeni’’. Alihitimisha Dkt. Ndugulile.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile (katikati) akizungumza na vyombo vya habari leo Jijini Dodoma kuhusu Kampeni ya Kitaifa ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia, kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Jinsia Bi. Mboni Mgaza na kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Jinsia Bw. John Mapunda. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW 

TBS kufanya msako kwenye viwanda vya kuzalisha nondo nchini

$
0
0

SHIRIKA la viwango Tanzania limepanga kufanya msako kwenye viwanda vyote za kuzalisha nondo nchini ili kujiridhisha kama nondo zinazozalishwa zinazikidhi viwango vya ubora wa nondo.

Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa ukaguzi huo uliofanywa kwenye maeneo ya Kawe, Buguruni, Mwenge na Tegeta mwishino juzi, Mkaguzi wa TBS, Mhandisi Donard Manyama,  alisema katika ukaguzi wao wamebaini kuwepo kwa nondo nyingi zisizokidhi viwango kwenye matumizi ya ujenzi.

"Ukaguzi wetu umebaini kuwepo udanganyifu katika uzalishaji wa nondo kuanzia unene, urefu na madaraja vyote hivyo hakuna ukweli jambo hili ni hatari kama litafumbiwa macho," alisema Mhandisi Manyama

Alisema kiwango halisi cha urefu wa nondo huwa ni ujazo husiopungua futi 40, lakini zilizopo sokoni baadhi zina futi 39 hadi 34, huku unene yaani ujazo wa kipenyo halisi ni  mm 18, lakini zilizopo sokoni nyingi ni ujazo 9 hadi 6.
 
Alizungumzia pia kuhusu udanganyifu unaofanywa na wafanyabiashara kuuza bei moja kati ya nondo za daraja la BS 300 na 500, Mhandisi Manyama alisema kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Kwa upande wake Mhandisi Nyabuchweza Methusel alisema ukaguzi huu umetoa matokeo hasi ambayo TBS wanaona kama changamoto kwao na kwamba  yasipodhibitiwa mapema yanaweza kuzalisha majanga ya hatari kwa majengo kuporomoka.

Mhandisi Methusel alisema hatua hiyo italazimu kila mzalishaji wa nondo kuanza kutekeleza matakwa ya sheria ya viwango ambayo inamtaka kila mzalishaji kuweka jina la kampunii, ujazo na urefu kwa kila nondo inayozalishwa.

Mmoja wa mafundi ujenzi, Patrick Jacob, alipongeza hatua kazi kubwa inayofanywa na shirika hilo kuhakikisha nondo ambazo hazikidhi viwango zinaondolewa kwenye soko hapa nchini.

Tigo yazindua mtandao wa 4G Mwanga

$
0
0

Meneja Mauzo wa Tigo Mkoa wa Kilimanjaro,Tryphone Kamugisha,akikata utepe kwa pamoja na Kaimu Afisa Mtendaji wa mji Mdogo wa Mwanga, Hassan Msuya, wakikata utepe kwenye mnara wa Mawasiliano ya simu kuashiria kuanza rasmi kutumika kwa huduma ya mtandao wenye kasi ya 4G kwa wilaya ya Mwanga .
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Mawasiliano ya Simu za Mkononi ya Tigo wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa mji mdogo wa Mwanga mara baada ya kufanyika uzinduzi wa mtandao wa kasi wa 4G katika mji wa Mwanga.
Wakazi wa Mwanga . na wafanyakazi wa Tigo wakifuatilia uzinduzi wa uzinduzi wa mtandao wa kasi wa 4G katika mji wa Mwanga. 
Wateja wakipata huduma mara baada ya kufanyika uzinduzi wa mtandao wa kasi wa 4G katika mji wa Mwanga.
Wateja wakipata huduma mara baada ya kufanyika uzinduzi wa mtandao wa kasi wa 4G katika mji wa Mwanga.
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live


Latest Images