Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

INRODUCING GNAKO X FANY - WEKA


Dodoma FC kuivaa Lipuli kesho, Kocha Makata atamba kuibuka na ushindi

$
0
0

Charles James, Michuzi TV

TIMU ya Soka ya Dodoma Jiji Fc,inatarajia kushuka dimbani kesho kucheza  mchezo wa kirafiki dhidi ya Lipuli ya Mkoani Iringa,mtanange unaotarajiwa kufanyika katika uwanja wa Jamhuri Jijini hapa.

Huu unakuwa mchezo wa pili wa kirafiki ambapo hivi karibuni timu hiyo ilicheza na Mbeya City ya Mkoani Mbeya na timu hizo kutoka sare ya kutofungana.

Dodoma Jiji Fc inatarajiwa kukata utepe wa Ligi daraja la kwanza kwa kucheza na Reha Fc mchezo unaotarajiwa kufanyika Septemba 14 mwaka huu katika uwanja wa Jamhuri Jijini hapa.

Akizungumza Jijini hapa, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mbwana Makata alisema mchezo huo ni maandalizi kwa ajili kukipima kikosi chake.

" Tumepanga kucheza Michezo nane ya kujipima nguvu kabla hatujaanza Ligi, tunaamini kupitia Michezo hii tutaona mapungufu na kuyafanyia kazi, lengo letu ni kuhakikisha tunafanya vema na kuipandisha timu Ligi Kuu.

" Hamasa ni kubwa sana kwa wachezaji, tuwaombe mashabiki wetu kujitokeza kwa wingi, wao ni sehemu yetu na wingi wao ndio chachu ya sisi kufanya vizuri,"alisema.

Makata ambaye amewahi kuzifundisha timu kadhaa za Ligi daraja la kwanza na Ligi Kuu,alisema wamepanga kucheza Michezo nane ya kirafiki kabla ya kuanza kwa Ligi daraja la kwanza.
Kocha wa Dodoma FC, Mbwana Makata Akizungumza na wachezaji wake katika mazoezi ya Timu hiyo yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri

Damu Salama Kanda ya Mashariki yawashukuru wakazi Dar Es Salaam kwa uchangiaji Damu Dar es Salaam

$
0
0
Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS) Kanda ya Mashariki umewashukuru wakazi wa jiji la Dar es Salaam na maeneo ya jirani kwa namna walivyojitokeza kuchangiaji damu kwa ajili kuwasaidia wagonjwa wenye uhitaji ikiwemo majeruhi wa ajali ya moto iliyosababishwa na lori la mafuta lililopinduka na kulipuka eneo la Msamvu Mkoani Morogoro ambapo watu zaidi ya 90 wameripotiwa kufariki dunia na wengine kujeruhiwa.

Sambamba na shukrani hizo Mpango huo umeendelea kuwakumbusha wananchi umuhimu wa kuchangia damu huku ukiwahimiza kuendelea kuchangia damu zaidi ili kuokoa maisha ya wagonjwa wenye uhitaji wa damu waliopo kwenye vituo mbalimbali vya afya hapa nchini.

Akizungumza wakati wa hitimisho la zoezi la uchangiaji damu lililofanyika kwa siku tatu mfululizo kwenye viunga vya stendi ya mabasi ya Mbagala jijini Dar es Salaam ili kusaidia majeruhi hao, Muhamasishaji Jamii kutoka NBTS, Bi Mariamu Juma alisema shukrani hizo zinafuatia mafanikio makubwa yaliyopatikana wakati wa zoezi hilo muhimu lililoandaliwa na NBTS kwa kushirikiana na benki ya Exim Tanzania.

“Kwa kweli muitikio ulikuwa wa kuridhisha na tumefanikiwa kukusanya chupa takribani 155 kulingana na malengo yetu hivyo tunawashukuru sana wakazi wa Mbagala na vile vile tunawashukuru sana Benki ya Exim Tanzania ambao ni washirika wetu wakubwa kwa kujitoa kwao kwa hali na mali hadi kufanikisha zoezi hili pamoja na wakazi wa Dar es Salaam kwa ujumla wanaoendelea kuchangia damu kwenye vituo vingine ikiwemo ikiwemo Hospitali ya Taifa Muhimbili.’’ Alisema.

Tangu kutokea kwa ajali hiyo ya moto mkoani Morogoro imeshuhudiwa idadi kubwa ya wakazi wa Dar es Salaam na kwinginepo nchini wakiguswa na kuitikia wito wa kuchangia damu kwa majeruhi hao ambapo imearifiwa kuwa bado kuna uhitaji wa damu huku jamii ikiendelea kuhamasishwa kujitolea zaidi ili kuokoa maisha ya wagonjwa wenye uhitaji.

“Watanzania wasisubiri kuuguliwa na ndugu ndio wakumbuke kuchangia damu na mazao ya damu wanatakiwa kuwa na tabia ya kuchangia damu mara kwa mara ili itumike kuwatibu wagonjwa na si tu majeruhi wa ajali bali pia kuna makundi mengine yenye uhitaji mkubwa wa damu ambayo ni pamoja na wagonjwa wa saratani, watoto, kina mama wajawazito na wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji’’ alisema.
Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kwenye viunga vya Stendi ya mabasi ya Mbagala jijini Dar es Salaam wakifuata taratibu ili kuchangia damu kwa ajili ya majeruhi wa ajali ya moto iliyosababishwa na lori la mafuta lililopinduka na kulipuka eneo la Msamvu Mkoani Morogoro ambapo watu zaidi ya 70 walifariki dunia na wengine kujeruhiwa. Zoezi hilo la siku tatu lilikamilika mwishoni mwa wiki, kwa uratibu wa benki ya Exim Tanzania kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS).

DKT. KAZUNGU: WADAIWA SUGU WA BENKI YA TIB WATAKIWA KUREJESHA FEDHA

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TIB, Bw. Charles Singili (kulia) akimuongoza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu (kushoto) kuangalia baadhi ya viongozi wa Benki hiyo kwa nyakati tofauti wakati wa ziara ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/19 katika taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango ili kujua changamoto na njia za kuzitatua kwa mwaka wa fedha 2019/20.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu (katikati), akisalimiana na mmoja wa wateja wa Benki ya TIB, wakati wa ziara ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/19 katika taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango ili kujua changamoto na njia za kuzitatua kwa mwaka wa fedha 2019/20, kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TIB, Bw. Charles Singili.



Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu (kushoto) akiwa na mwenyeji wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TIB, Bw. Charles Singili (kulia) alipofanya ziara katika Benki hiyo jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/19 katika taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango ili kujua changamoto na njia za kuzitatua kwa mwaka wa fedha 2019/20.


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TIB, Bw. Charles Singili (kulia), akieleza kuhusu utoaji mikopo ya mitaji katika miradi ya Serikali na watu binafsi, wakati wa Mkutano na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu (kushoto), katika Ofisi za Benki hiyo jijini Dar es Salaam. 


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu (kushoto), akiangalia machapisho ya Benki ya TIB na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bw. Charles Singili akitoa maelezo, wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu huyo iliyolenga katika utekelezaji wa bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/19 kwa taasisi hiyo ili kujua changamoto na njia za kuzitatua kwa mwaka wa fedha 2019/20.


Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Christopher Nkupama (kulia) na Mtaalam wa Mipango kutoka Wizara hiyo, Bw. Msabaha Msabaha, wakifuatilia mkutano kati ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Khatibu Kazungu na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TIB, Bw. Charles Singili (hawapo pichani), jijini Dar es Salaam.
(Picha na Peter Haule, WFM, Dar es Salaam)

*************

Na. Peter Haule, WFM, Dar es Salaam

Serikali imeitaka Benki ya TIB kuhakikisha inawafuatilia kwa karibu wadaiwa sugu wote wa Benki hiyo ili waweze kurejesha fedha wanazodaiwa ili kuongeza ukwasi wa taasisi.

Hayo yameelezwa jijiji Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu, alipofanya ziara katika Benki hiyo ikiwa ni sehemu ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2018/19 katika taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Fedha na Mipango ili kujua changamoto na njia za kuzitatua kwa mwaka wa fedha 2019/20.

Dkt. Kazungu amesema, wadaiwa sugu wanaodaiwa na Benki ya TIB warejeshe fedha walizochukua ili kuongeza ukwasi wa Benki hiyo na kuendelea kukidhi vigezo vya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inavyoviangalia katika kudhibiti taasisi za kibenki nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TIB, Bw. Charles Singili, alisema kuwa ni vizuri watu wazingatie mikataba wanayoingia na Benki wakati wa kukopa fedha, kwa kujenga nidhamu ya matumizi ili kuzitumia katika lengo husika na kukuza uchumi wa mlengwa hatimaye kuzirudisha kwa wakati ili kutoa fursa kwa wengine kunufaika na mikopo hiyo.

“Benki ya TIB ni taasisi ya Serikali na ni ya kisera, imeundwa mahususi kwa ajili ya kuchochea maendeleo ya uwekezaji wa ndani ya nchi hususani katika kufanikisha utekelezaji wa miradi ya Serikali na miradi ya sekta binafsi”, alieleza Bw. Singili.

Bw. Singili alisema kuwa, Benki ya TIB ilianzishwa ili kukabiliana na uhitaji wa mitaji ya muda mrefu kwa kuwa benki nyingi nchini ni za kibiashara na mitaji inayotoa kwa wateja wake ni ya muda mfupi.

Alisema kuwa mikopo inayotolewa na benki hiyo inaendana na ajenda ya Serikali ya kuboresha miundombinu wezeshi pamoja na uwekezaji kwenye viwanda, hivyo ajenda hiyo haiwezi kufikiwa kwa mikopo ya mitaji ya muda mfupi.

“Ukitazama Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka mitano 2016/17 hadi 2020/21 kwa fedha iliyopangwa kwa ajili ya kutekeleza mpango huo haiwezi kupatikana kutokana na makusanyo ya kodi pekee hivyo kuna kila sababu kwa taasisi hii kama Benki ya Maendeleo kuangalia njia mbadala hususani kupitia kwenye masoko ya mitaji ili kusaidia juhudi za Serikali katika upatikanaji wa fedha hizo”, aliongeza Bw. Singili.

Bw. Singili ameahidi kuyafanyia kazi maagizo ya Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Kazungu, hususani katika kukabiliana na mikopo chechefu kwa kuongeza nguvu katika kuwafuatilia wadaiwa sugu.

Aidha amempongeza Naibu Katibu Mkuu huyo, kwa kufanya ziara za kiutendaji katika taasisi yake, kwa kuwa zinasaidia katika kubadilishana mawazo na kujua matarajio na changamoto za taasisi katika mtazamo wa pamoja wa kuzitatua.

MKURUGENZI MTENDAJI WA BENKI YA CRDB AMTEMBELEA MKURUGENZI WA MANISPAA YA KINONDONI, JIJINI DAR LEO

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akisalimiana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Aron Kagurumjuli,  alipomtembelea ofisini kwake leo Agosti 20, 2019. 
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Aron Kagurumjuli (wa pili kulia) akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kulia) aliyembatana na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki hiyo, Tully Esther Mwambapa pamoja na Mkuu wa Taasisi za Serikali wa Benki ya CRDB, Dkt. Bennett Bankobeza, walipomtembelea ofisini kwake, Magomeni jijini Dar es salaam leo Agosti 20, 2019.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Aron Kagurumjuli, juu ya mahusiano ya kibiashara baina ya Benki na Manispaa ya Kinondoni.

Ziara ya Biteko Lindi Kampuni ya Indiana yajisalimisha

$
0
0
Waziri wa Madini Doto Biteko kushoto akimueleza Bob Adam kulia mmoja wa wakurugenzi wa Kampuni ya Indiana kutoka Austaria utaratibu wa kufuatwa katika kufanya ushirika (Ubia) kati ya Kampuni ya Ndani na ya nje ya nchi alipokwenda kuzungumza na Waziri kuhusu ushirika wao na Kampuni ya Ngwena Ltd.
Waziri wa Madini Doto Biteko kushoto akimsikiliza Bob Adam kulia mmoja wa wakurugenzi wa Kampuni ya Indiana kutoka Austaria wakati wa mazungumzo yao ofisini kwake jijini Dodoma. Kulia ni Katibu wa Waziri wa Madini Kasongi Kungulu na Godluck Sekozo kutoka Ngwena Ltd.
Viongozi mbalimbali wa Wizara ya Madini wakishiriki kikao cha Waziri wa Madini Doto Biteko alieshika kidevu na Mkurugenzi wa Indiana Bob Adam kushoto kwa waziri ofisini kwa waziri wa madini Jijini Dodoma. Kutoka kulia kwa waziri ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango Augustine Ollal, Mkurugenzi wa huduma za sheria Edwin Igenge na Kamishna msaidizi (Local Content) Terence Ngole. 



Na Issa Mtuwa Dodoma

Kufuatia ziara aliyofanya Waziri wa Madini Doto Biteko mkoani Lindi na Mtwara hususani wilaya ya Nachingwea na kuibua sintofahamu juu ya Kampuni ya Ngwena Ltd kuhusu ushirika wake na Kampuni ya Indiana kutoka Australia, suala hilo limefanya Uongozi wa Kampuni ya Indiana kupitia Mkurugenzi wake Bob Adam kuja nchini kukutana na Waziri wa Madini ili kujadili kuhusu ushirika wao na Ngwena Ltd.

Leo Agosti 19, 2019 Waziri Biteko amekutana na kuzungumza na mkurugenzi huyo kuhusu ushirika wao wa kuunganisha kampuni hizo bila kuijulisha wizara. 

Waziri Biteko amembana mwekezaji huyo kwa hoja tatu zilizopelekea kutopatika majibu ya moja kwa moja kutokana na kuto kuwepo kwa mwakilishi wa upande wa pili wa wa kampuni ya Ngwena Ltd. 

Hoja hizo ambazo waziri Biteko alitaka kufahamu kutoka kwa kampuni ya Indiana ni; mosi, makubaliano kati ya Indiana na Ngwena hayana taarifa kwa Wizara, ni kwa nini waliamua kuunganisha bila kuijulisha Wizara wakati kampuni moja ni ya Kitanzania na nyingine ni ya kigeni Mbili, Wizara inataka kuona makubaliano yao ya kimaslahi (fair deal) baina ya pande zote ili pia wizara ijue serikali inafaidikaje? Na tatu, kampuni husika zinatunzaje shehena kubwa ya sampuli za madini bila kuijulisha Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) ambayo ndio yenye dhamana ya utunzaji? 

Aidha, waziri Biteko aliendelea kuibana kampuni hiyo ya Indiana kupitia mkurugenzi wake huyo kwa kumuuliza uhusika wake katika kampuni ya Ngwena Ltd huku Mkurugenzi wa huduma za Sheria wa Wizara ya Madini Edwin Igenge akimhoji ni tangu lini ushirika wake na Ngwena ulianza? Je, ni kabla au baada ya marekebisho ya Sheria ya Mwaka 2017? 

Akitoa majibu kwa baadhi ya hoja na maswali, Bob Adam amesema Indiana ndio inayomiliki Ngwena Ltd na kufadhili kifedha na masuala mengine. Kuhusu kabla au baada ya marekebisho ya sheria ya 2017 Adam hakuwa na uhakika wa moja kwa moja na alisema mpaka arejee kwenye nyaraka ili ajiridhshe.

“Kampuni yetu ndio inayo miliki Ngwena Ltd kwa maana Indiana inamiliki 60% ya hisa zote na ndio maana ninasema Indiana inamiliki Ngwena,” amesema Bob Adam.

Kutokana na hoja tatu za msingi kutopatiwa majibu ya kuridhisha kwa kukosekana kwa Uongozi wa Ngwena Ltd katika kikao hicho, Waziri Biteko ametaka kupangwa kwa tarehe nyingine huku akimtaka Adam kurudi tena nchini akiwa na uongozi wa Ngwena Ltd ili kufahamu kiundani juu ya makubaliano yao kwani mpaka sasa kampuni inayotambuliwa na wizara ni Ngwena Ltd na siyo Indiana. 

Wiki iliyopita Waziri wa Madini alifanya ziara mkoani Lindi wilaya ya Nachingwea na kutembelea eneo la Nditi ambalo kampuni ya Ngwena Ltd imewekeza, moja ya mambo aliyokutana nayo ni uwepo wa makubaliano (Joint-Venture) kati ya kampuni ya Ngwena Ltd na Indiana kutoka Australia kinyume cha sheria na uwepo wa shehena kubwa ya sampuli za madini zilizohifadhiwa kinyume cha sheria. 

WAGANGA WAKUU WA MIKOA NA.HALMASHAURI IMARISHENI LISHE-DKT NDUGULILE

$
0
0
Na.Catherine Sungura,WAMJW-Dodoma

Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri nchini wametakiwa kuweka mikakati ya kuimarisha hali ya lishe katika ngazi ya jamii ili kupunguza hali ya udumavu kwa jamii.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya, Maendleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile kwenye kikao kazi cha Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri unaofanyika jijini hapo.

Dkt. Ndugulile amesema kuwa ili kuwe na taifa lisilo na kiwango cha chini cha hali ya lishe waganga wakuu hao lazima wapange mikakati ambayo itaanzia ngazi ya jamii ili wananchi waweze kuelewa umuhimu wa lishe bora na inayostahili kwa familia hivyo wanapaswa kufanya kazi kwa weledi ili mikakati hiyo ifanikiwe.

Hata hivyo alisisitiza watoa huduma kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kuimarisha huduma za afya katika maeneo yao ili wananchi wanaoenda kupata huduma wapate huduma hizo kwa haki na usawa" na katika hili ni vyema mwananchi anayekuja kupata huduna ni vyema aridhike na huduma anayopata katika vituo vyetu vyote nchini”.Alisema Dkt. Ndugulile.

Aidha, Dkt. Ndugulile aliwataka waganga wakuu hao kusimamia utendaji wa kazi katika maeneo yao ili kuweza kutoa huduma bora za afya kwa jamii“inasikitisha kuona mama mjamzito anafariki kwenye kituo cha afya kwa ajili ya uzembe au kutokupata huduma sahii jambo hili halikubariki”.

Kikao kazi cha waganga wakuu wa mikoa na halmashauri mwaka huu kinafanyika jijini hapa ambapo kilifunguliwa na mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Suleiman Jafo na kauli mbiu ya kikao hicho ni “Uwajibikaji ni nguzo muhimu katika utoaji huduma bora za afya kuelekea uchumi wa kati na utakua wa siku tano.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Dkt. Faustine Ndugulile
Picha ya pamoja

Jafo afungua mkutano wa Waganga Wakuu Nchini, Atoa maagizo kwa Katibu Mkuu TAMISEMI

$
0
0
Charles James, Michuzi TV

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kufanya uchunguzi katika Wilaya ya Bumbuli ambapo Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo alisimamishwa.

Mhe Jafo ameyasema hayo katika Kikao kazi cha Waganga wakuu wa Mikoa na Halmashauri nchini kilichofanyika leo jijini Dodoma ambapo kinalenga kufanya tathimini ya utekelezaji wa Afya wa mwaka uliopita.

Amesema Wizara ya TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Afya itahakikisha kuwa pamoja na Uwekezaji mkubwa inaoufanya katika Sekta hiyo ni lazima wahakikishe pia wanawalinda watumishi wake.

" Mimi Niwapongeze sana ndugu zangu madaktari mnafanya kazi kubwa sana katika kuwatumikia wananchi wetu, kama Wizara hatutokubali kuona mtu yeyote anawagandamiza, nyinyi ni nguza kubwa na mnastahili sifa na heshima kwa utumishi wetu.

" Ni kweli tumejenga vituo vingi vya Afya na Hospitali Nchi nzima vilivyogharimu Bilioni 385. Lakini pia ni jukumu letu kuwajengea watumishi wetu mazingira rafiki ya kufanya kazi zao kwa weledi, niwaahidi lazima tuwalinde," amesema Waziri Jafo.

Aidha amemuagiza Katibu Mkuu pia kuhakikisha watumishi saba wa Kituo cha Afya Ipogoro kilichopo Manispaa ya Iringa waliokua wameondolewa kazini kurudishwa mara moja na tayari ameshaunda Timu inayofanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha watumishi hao kuondolewa katika Kituo chao cha kazi.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndugulile amewataka madaktari kuongeza ubunifu na kujituma zaidi katika vituo vya vya kazi.

Amesema wao kama wataalamu wana jukumu la kuhakikisha wanazuia Watanzania kutokuugua na kuwataka kuwa suluhishi na siyo walalamikaji.

" Madaktari tunapaswa kuongeza ubunifu, mfano juzi kuna mmoja kanipigia simu ananiambia Hospitali yake haina Thermometer sasa kama kifaa kidogo hicho anashindwa kununua mpaka Serikali Kuu ije kuna maana gani ya yeye kuwa kwenye nafasi hiyo? Kwani Hospitali haina mapato?.

" Ni lazima tubadilike, na ninafikiri ni vema mkutano ujao tuitaje Mikoa iliyofanya vizuri na kuipa zawadi lakini pia ile iliyofanya vibaya nayo itajwe," Amesema Dk Ndugulile.

Nae Rais wa Chama Cha Madaktari Nchini ameipongeza Serikali chini ya Rais Dk John Magufuli kwa namna ilivyoboresha vituo vya Afya jambo ambalo linawafanya sasa wao ndio wawe na deni kwa Mhe Rais LA kutoa huduma bora kwa wananchi

Wakazi Manispaa Ya Tabora Wapigwa Marufuku Shughuli Za Kibinadamu Katika Bwawa La Igombe

$
0
0
Na, Editha Edward-Tabora 

Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Tabora mjini imefanya ukaguzi katika vyanzo vya maji katika Bwawa la Igombe linalotoa huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wa manispaa ya tabora na kubaini uhalibifu katika baadhi ya maeneo ya vyanzo hivyo kutokana ba Shughuli mbalimbali za kibinadamu ikiwemo uvuvi na kilimo cha mbogamboga kinachodaiwa Kutumia viutatilifu ambavyo ni hatari kwa binadamu 

Mkuu wa wilaya ya Tabora mjini Komanya Erick ameambatana na Wajumbe wa kamati hiyo ambapo wamekagua vyanzo hivyo vya maji na kupiga marufuku wakazi wa manispaa ya Tabora mjini wanaofanya Shughuli za kibinadamu ambazo wanafanya pembezoni mwa Bwawa hilo

Pamoja na hayo Komanya ametoa maagizo mbele ya kamati ya ulinzi kuwa wananchi wote ambao wamelima kando ya bwawa hilo wanatakiwa kufyeka mbogamboga pamoja na mazao mengine na kusafisha eneo hilo eneo liweze kuwa Wazi

"Natoa maagizo kwa mtendaji wa eneo hili ikifika kesho saa kumi na mbili jioni narudi kukagua hii Shughuli ya kilimo cha matango inayoendelea hapa na Shughuli zingine ni marufuku na ninaomba eneo hili ni la vyanzo vya maji tu Siyo Shughuli za kibinadamu tena na ninaomba viongozi muendelee kutoa elimu kwa Kushirikiana na TUWASA kuwa hili Siyo eneo la Shughuli za kibinadamu kwani mnasababishia watu wanapata maradhi ya kibinadamu kutokana na kumwagilizia mazao yenu madawa ya kemikali na mvua zikinyesha madawa yote yanaishia kwenye bwawa marufuku "Amesema Komanya

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya maji safi mjini Tabora TUWASA Mhandisi Joel Rugemalila amesema athari zinazojitokeza kutokana na Shughuli hizo za kibinadamu kama za kuchoma moto na kumwagilia dawa katika mimea ambayo imelimwa pembezoni na bwawa hilo ambapo mvua zikinyesha madawa yote yanatiririkia ndani ya bwawa hilo hivyo inaleta madhara makubwa kwa watumiaji

"Shughuli za kibinadamu pembezoni mwa bwawa hili zinasababisha madhara makubwa kwani ule udogo unakuwa tifutifu ambapo wanachoma kwa hiuo mvua zikinyesha uchafu wote unaishia kwenye bwawa na madhara yake yanapunguza kina cha bwawa ukishapunguza kina cha bwawa kinapunguza uwezo wa bwawa kutohudumia watu huduma ya maji kwa hiyo inakuwa ya shida sana" Amesema Rugemalila

Aidha bwawa la Igombe ndilo tegemeo kubwa kwa wakazi wa manispaa ya tabora na kwa sasa linakadiriwa kutoa huduma ya maji safi kwa wananchi wa manispaa hiyo zaidi ya laki tatu na nusu.
 pichani ni kamati ya ulinzi na usalama  iliyoambata na mkuu wa wilaya ya Tabora mjini Komanya Erick katika ukaguzi wa bwawa la Igombe.
 Pichani ni Bwawa la Igombe  ambalo ndilo chanzo cha maji  linalotegemewa na wakazi wa Tabora mjini zaidi ya wakazi laki tatu na nusu.
 Pichani ni kilimo cha matango ambacho kimelimwa karibu na bwawa la Igombe ambapo mkuu wa wilaya ameagiza mimea hiyo ifyekwe.
Pichani ni kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Tabora mjini wakikagua eneo la bwawa la Igombe.

RAIS WA ZANZIBAR DK.SHEIN AZINDUA JUMUIYA YA WASTAAF NA WAZEE ZANZIBAR

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akikapidhiwa Cheti cha Shukrani na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wastaaf na Wazee Zanzibar (JUWAZA) Ndg. Masururu Saadun Ferouz, wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Jumuiya hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar , kulia Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe.Maudline Castico.(Picha na Ikulu)
BAADHI ya Wanachama wa Jumuiya ya Wastaaf na Wazee Zanzibar wakifuatilia hutba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, wakati wa Uzinduzi wa Jumuiya yao uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.(Picha na Ikulu).

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Jumuiya ya Wastaaf na Wazee Zanzibar (JUWAZA) uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.(Picha na Ikulu).
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wastaaf na Wazee Zanzibar (JUWAZA) Ndg. Masururu Saadun Ferouz akizungumza na kutowa neno la shukrani kwa mgeni rasmin Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.(Picha na Ikulu)
BAADHI ya Wanachama wa Jumuiya ya Wastaaf na Wazee Zanzibar (JUWAZA) wakiitikia dua ikisoma na Mwanachama wa Jumuiya hiyo Sheikh Gharib Bakari Seif kutoka Kijiji cha Gana Wilaya ya Kati Unguja, baada ya kumalizika kwa hafla hiyo iliofanyika katika ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni Zanzibar.(Picha na Ikulu).

*******************

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Braaza la
Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein ameitaka jamii
kuzingatia umuhimu wa kuwaheshuimu na kuwatendea
wema wazee, kwa kutambuwa kuwa ni misingi muhimu
ya silka, malezi na utamaduni wa Wazanzibari.

Dk. Shein amesema hayo leo katika ufunguzi wa
mkutano mkuu wa Jumuiya ya Wazee na Wastaafu
Zanzibar (JUWAZA), uliofanyika katika ukumbi wa
Sheikh Idris Abdul wakil, Kikwajuni mjini hapa.

Amesema jamii imekumbwa na vitendo vya udhalilishaji
na unyanyapaa dhidi ya wazee, huku kukiwa na watu
ndani ya familia wanaowadharau wazee wao kwa

kuwatukana pamoja na kuwahusisha na imani za
kuwashirikina na dhana za kuhusika na vitendo viovu,
ikiwemo uchawi na wanga.

Alisema kuna baadhi ha vijana mbali na kusomeshwa
vyema na wazee wao, wamekuwa wakiwadharau wazee
kwa kigezo kuwa hawaendani na hadhi walizonazo,
mambo yanayochangia na kuwafanya wazee kukosa
amani, matunzo, misaada na haki wanazostahiki.

“Haki ya kuheshimiwa na kutunzwa ni ya msingi kwa kila
mzee, vijana wana wajibu wa kuwapa wazee wao haki zao
kwani huo ni wajibu wao”, alisema.

Aliitaka jamii kuendelea kuwaheshimu wazee kutokana
na mambo mbali mbali makubwa waliyolifanyia Taifa na
kusisistiza haja ya kuendelea kuwatunza an kuwaenzi ili
kupata fursa ya kuchota hekima na busara kutoka kwao.

Alisema nchi zote zinazoendelea zimekuwa na utamaduni
wa kuwaenzi na kuwathamni wazee na wastaafu na
kuwatumia ipasavyo, hususan pale kunapohitajika
ushauri wa mambo mbali mbali, kutokana ana maarifa,
hekima na uzoefu wao katika masuala ya kimaisha.

Aidha, alisema ni muhimu kuzingatia suala la kuwatunza
wazee kuwa limetiliwa mkazo katika mafunzo ya Dini
zote, ikiwa ni hatua maalum katika kuwatendea wema.

Dk. Shein alisema katika kudhihirisha dhamira njema ya
Serikali katika kuyashughulikia masuala ya wazee, mara
baada ya Mapinduzi matukufu ya 1964, Rais wa kwanza
wa Zanzibar, hayati Abeid Amani Karume alianzisha
ujenzi wa nyumba za wazee kwa lengo la kuwahifadhi,
hususan wale waliokosa uwezo na watu wa kuwahudumia.

Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekuwa
ikiendeleza utaratibu wa kuwapa hifadhi na
kushughulikia changamoto mbali mbali zinazowakabili
wazee, kwa kutambuwa kuwa huo ni wajibu wake wa
msingi.

“Lazima tuwathamini wazee wetu, tuwaheshimu na
tuwahifadhi kwa kusikiliza shida zao na kuzitafutia
ufumbuzi kwa kadri ya uwezo wetu”, alisema Dk Shein.

Aidha, alibainisha kuwa wajibu wa kuyashughulikia
masuala yanayowahusu waze ni hatua ya utekelezaji wa
Ilani ya CCM ya uchaguzi mkuu wa 2015 – 2020, kama
ilivyoainishwa katika Ibara ya 135,

Dk. Shein alieleza taarifa ya Idadi ya watu na
iliofanyiika mwaka 2012 imebainishwa kuwepo zaidi ya
wazee 53, 311 wenye umri wa kuanziza miaka 60, hatua
iliyoifanya Serikali kuanzisha Wizara ya Kazi,
Uwezeshaji, wazee, wanawake na watoto baada ya
kutambua thamani yao.

Aidha, alisema Serikali ilianzisha Sera ya Hifadhi ya
Jamii mnamo mwaka 2014, kwa lengo la kusimamaia
wazee wote nchini, ikiwemo wenye umri wa kuanzia
miaka 70 na kuendelea na kuwapatia posho la shilingi
20,000 kila mwezi.

“Serikali itaendelea kuyaimarisha makaazi yao na
kuhakikisha kuwa wazee hao wanapewa huduma zote
muhimu wanazostahili, zikiwemo za chakula, matibabu,
maji safi na salama pamoja na ulinzi wa maisha yao”,
alisema.

Dk. Shein aliweka wazi malengo ya serikali ya kuwapatia
wazee hao mazingira bora zaidi ya kuishi ikiwa pamoja
an kuwaandalia ziara za kuzitemebelea sehemu mbali
mbali za kihistoria na za maendeleo.

Alisema amefurahishwa sana mafanikio makubwa
yaliopatikana kupitia JUWAZA kutokana na kazi kubwa
ya kuwaunganissha wazee kwa lengo la kuimarisha hali
zao kiafya, kiuchumi na ustawi bora wa maisha yao.

Akigusia maomba mbali mbali yaliowasilishwa kwake, Dk.
Shein alisema Serikali inalifanyia kazi ombi la kuongeza
kiwango cha posho ya Pensheni jamii na kuahidi
kulitolea uamuzi kutegemea na wakati husika.

Sambamba na hilo, Dk. Shein alisema ni jambo zuri
kuwepo kwa sheria, itakayozingatia mambo mbali mbali
ya wazee, huku akionyesha imani kubwa aliyonayo ya
Rais ajaye kuendelea na ataratibu wa utoaji wa Pensheni
jamii kwa kuzingatia kuwa atakuwa na uelewa mpana wa
Ilani ya CCM.

Aidha, Dk. Shein alikubali kuwa mlezi wa Jumuiya ya
Wazee na Wastaafu (JUWAZA) pamoja na kuunga
mkono rai ya uanzishaji wa mfuko maaalum, ili kusaidia
shughuli mbali mbali za kuendeleza Jumuiya hiyo.

Katika hatau nyengine, Dk. Shein alipokea Cheti cha
Uongozi bora kutoka JUWAZA pamoja kupokea Kadi ya
Uanachama wa Jumuiya hiyo.

Nae, Waziri wa Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee,
Wanawake na watoto Modline Castico, alisema kuwepo
kwa mswada wa sheria kuhusiana na utoaji wa Pensheni
jamii, umewafanya wazee kufurahia jambo hilo, kwa
kuzingatia kuwa utawahakikishia ulinzi wa haki zao,
sambamba na kuondokana na vitendo vya udhalilishaji.

Alisema Wizara hiyo itaendelea na juhudi zake za
kupigania na kuimarisha haki na ustawi bora wa maisha
ya wazee nchini.

Mapema, akisoma Risala ya Jumuiya hiyo, Amour Haji
Nassor aliiomba Serikali kuangalia uwezekano wa
kuongeza kiwango cha Posho la Pensheni jamii kwa
wastani wa asilimia hamsini ya kima cha chini cha
mshahara, kabla ya kumaliza kwa awamu ya saba ya
Uongozi.

Aidha, alipongeza juhudi kubwa zinazochukuliwa na
Serikali katika kuwapatia wazee huduma mbali mbali za
kijamii, ikiwemo suala la afya bora , akibainisha juhudi
hizo zimefanikiwa kuimarisha hali zao.

MITAMBO YA KUNYANYULIA MIZIGO YA UJENZI WA MRADI WA JN HPP YAZINDULIWA RASMI FUGA.

$
0
0
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Atashasta Nditiye(wa pili kutoka kushoto) akiambatana na Msemaji Mkuu wa Serikali,Dkt.Hassan Abbasi (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi mtendaji wa TAZARA-Zambia, Mhandisi.Bruno Chingandu (wa kwanza kulia) na Meneja wa TAZARA ,Mkoa wa Tanzania, Fuadi Abdallah wa pili kulia wakiwa katika uzinduzi wa mitambo ya kunyanyulia mizigo stesheni ya Fuga.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Atashasta Nditiye(wa pili kutoka kushoto) akivaa kofia kujiandaa kuwasha moja ya mitambo ya kunyanyulia mizigo ya ujenzi wa mradi wa Umeme JN HPP iliyopo katika Stesheni ya Fuga, wa kwanza kushoto ni Meneja wa TAZARA ,Mkoa wa Tanzania, Fuadi Abdallah.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Atashasta Nditiye, akiendesha moja ya mitambo ya Kunyanyulia mizigo iliyoko katika stesh
eni ya Fuga wakati wa ufunguzi wa mitambo hiyo hapo jana Agosti 19, 2019.
Wafanyakazi wa Stesheni ya Fuga wakishuhudia uwezo wa mtambo aina ya Raech Stacker wa kunyanyua mizigo mizito katika stesheni ya Fuga uliozinduliwa jana na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Atashasta Nditiye.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Atashasta Nditiye, akitelemka kutoka kwenye moja ya mtambo wa kunyanyulia mizigo mara maada ya kuuzindua hapo jana katika Stesheni ya Fuga itayotumika kopokea na kusafirisha mizigo kwenda mradi wa Umeme JN HPP.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Atashasta Nditiye, akipata maelezo fulani kutoka kwa Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi wakati wa uzinduzi wa mitambo ya kunyanyulia mizigo ya ujenzi wa mradi wa umeme JN HPP uliofanyika katika Stesheni ya Fuga.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Atashasta Nditiye, akipata maelezo fulani kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya usambazazi mitambo ya kunyanyulia mizigo ya Eristic (t) Investment Company, Hassan Kipussi katika uzinduzi wa mitambo hiyo uliofanyika katika Stesheni ya Fuga jana Agosti 19, 2019.



(Picha na Idara ya Habari-MAELEZO)

**************

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe.Atashasta Nditiye
amazindua Rasmi Vifaa vya Kunyanyulia Makontena ya Mizigo na Vifaa vizito vya utekelezaji wa ujenzi wa Mradi mkubwa wa umeme wa Julius Nyerere Hydro Power Project (JN HPP).

Akizungumza jana katika stesheni ya fuga, Waziri Nditiye alisema kuwa Serikali imenunua vifaa hivyo ambavyo ni Reach Stacker 2 zenye uwezo wa kunyanyua tani 45, Mobile crane yenye uwezo wa tani 15 na Forklift 2 zenye uwezo wa tani 5 na zimegharimu Tzs Bilioni 3.5.

“Vifaa hivi vimenunuliwa na Serikali ili kuiwezesha TAZARA kutekeleza majukumu iliyopewa ya upokeaji makontena ya mizigo mizito ya ujenzi wa bwawa la kufua umeme la JN HPP, katika mto Rufiji, mradi utakozalisha Megawati 2,115 na kuiwezesha Tanzania kufikia uchumi wa viwanda”, Naibu Waziri Nditiye.

Aidha, Waziri Nditiye alisema kuwa Serikali itaendelea kuishika mkono TAZARA ili kuhakikisha inafanya kazi ufanisi mkubwa kwenye utekelezaji wa mradi wa kufua umeme JN HPP na ndiyo maana imetoa Tsh. Bilioni 10 ili kununua Traction Motors 42 kwa ajili ya vichwa saba vya treni za masafa marefu na sogeza ambazo zitaanza kuwasili mwezi oktaoba.

Waziri Nditiye aliongeza kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inawahakikishia wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia (TAZARA)kuwa itaendelea kulipa mishahara yote kwa kipindi chote cha mwaka wa fedha 2019/2020 na tayari imetanga kiasi cha shilingi bilioni 14.9 zimetengwa.

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia
(TAZARA) alisema kuwa ni jambo kubwa na heshima kwa Mamlaka hiyo kupewa majukumu ya kupoea mizigo ya utekelezaji wa ujenzi wa Mradi wa Umeme JN HPP.

“Napenda kusema kuwa Serikali ya Tanzania, Chini ya Rais Dkt.John Pombe
Magufuli, ilituamini na kutupatia kiasi cha Shilingi Bilioni tano ili kukarabati stesheni ya Fuga kwa kujenga Stendi ya kupokea na kusafirisha mizigo, kununua vifaa vitakavyosaidia kunyanyua mizigo hiyo kwa ufanisi mkubwa”, Mhandisi. Bruno Chingandu.

Mhandisi Chingandu alisema kuwa vifaa hivyo viyakuwa na uwezo mkubwa wa kutosheleza mahitaji ya kupokea mizigo ya ujenzi wa mradi mkubwa wa kihistoria wa kufua umeme wa JN HPP, kwani tani kati ya 5 mpaka 45 zitanayanyuliwa na vifaa hivyo.

Aidha, Mhandisi Chingandu alisema kuwa Serikali imetekeleza kwa vitendo ununuzi wa Traction motor 42 kwa ajili ya treni ya masafa marefu kwa kutoa Tsh.Bilioni 10, hivyo itaiwezesha TAZARA kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa na kuliwezesha Shirika hili kurejera tena katika utendaji mkubwa.

Naye Meneja wa TAZARA Mkoa wa Tanzania, Fuad Abbdalah, alisema kwamba Serikali imewapatia Fedha za ujenzi na ununuzi wa vifaa ni heshima kubwa kwaShirika hilo kwani limeingia kwenye historia ya mageuzi ya Serikali ya Awamu yaTano.

“Leo tunashuhudia kitendo kikubwa cha kuzindua hizi mashine tano za kunyanyulia mizigo mizito ya ujenzi wa Mradi wa kihistoria wa JN HPP, Mashine hizi zina uwezo mkubwa wa kunyanyua Tani 5 mpaka 45, uwezo stahiki kabisa kuhudumia mizigo yote inayohitajika kwenye mradi wa umeme mto Rufiji”; Fuad Abbdalah, Meneja TAZARA mkoa wa Tanzania.

Fuad aliongeza kuwa Serikali imeliamini Shirika hilo na Rais wa Jamhuri ya
Muungano ameahidi kurudisha uafanisi wa utendaji wake na katika ziara yake yakwenda kuzindua Mradi wa umeme JN HPP alisema atahakikisha anashirikiana naRais wa Zambia ili kurudisha heshima ya TAZARA.

Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi alisema Serikaliimetekeza ukarabati wa stesheni ya kupokea na kushushia mizigo ya Fugaitayosaidia ujenzi wa Mradi wa Umeme wa JN HPP kufanikiwa kwa haraka Zaidi.

“Tunatekeleza Uboreshaji huu wa Stesheni ya Fuga, tumeleta mitambo ya kisasamikubwa kabisa ambayo imedhaminiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano waTanzania kwa ajili ya kuhudumia ujenzi wa bwawa la kufua umeme JN HPP, kwahiyo mitambo hii imefika, inafanya kazi na inasambazwa na Kampuni ya kizawa”,Dkt.Abbasi.

MWENGE WA UHURU KUZINDUA MIRADI YA MAENDELEO YENYE THAMANI ZAIDI YA BILIONI 1 MKOANI SINGIDA

$
0
0


Na Dotto Mwaibale, Singida

MWENGE wa Uhuru unaotarajiwa kuwasili wilayani Ikungi mkoani Singida kesho asubuhi utazindua miradi ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya sh. bilioni 1.162 .

Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya hiyo Edward Mpogolo (pichani) wakati akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu ukimbizaji wa mwenge wa Uhuru katika wilaya yake.

Mpogolo alisema mara baada ya kuwasili kwa mwenge huo na kupokelewa Kijiji cha Mkiwa patazinduliwa madarasa mawili ya Shule ya Msingi Darajani na kisha kuelekea kutembelea mradi wa upimaji wa virusi vya na elimu ya uchaguzi wa Serikali za mitaa uliopo katika Kijiji cha Issuna.

" Baada ya kutembelea mradi huo wa kijiji cha Issuna watakwenda kuweka jiwe la msingi ujenzi wa mnara wa kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere utakao jengwa Ikungi mjini" alisema Mpogolo.

Alisema baada ya hapo watakwenda kuweka jiwe la msingi wa mtandao wa maji Kijiji cha Ighuna pamoja na kutembelea mapambano dhidi ya dawa za kulevya Kituo cha Polisi cha Puma.

Aliongeza kuwa baada ya hapo watakwenda kukagua ujenzi wa Kituo cha Afya cha Sepuka na kufuatiwa na usomaji wa risala ya utii eneo la mkesha wa mwenge Uwanja wa Ofisi ya Mtendaji Kata ya Sepuka.

Mpogolo amewaomba wananchi wa wilaya hiyo kujitokeza kwa wingi kuupokea mwenge huo na kushuhudiwa miradi hiyo itakapo kuwa ikizinduliwa.

BRIGEDIA JENERALI, MKEREMY AIPONGEZA TFS KWA UTENDAJI WAKE

$
0
0
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Brigedia Jenerali Mbaraka Mkeremy amesema taasisi hiyo inafanya kazi kubwa kuhakikisha inasimamia rasilimali za misitu zilizopo ili ziwe endelevu kwa kizazi cha sasa na kijacho. 

Brigedia Jenerali Mkeremy ameyasema hayo akiwa kwenye Msitu wa Hifadhi ya Mazingira asili ya Kalambo ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kutembelea maeneo ya hifadhi za misitu na mashamba ya miti ya serikali.

Amesema uamuzi wa serikali kuupandisha hadhi msitu wa Kalambo kuwa msitu wa hifadhi ya mazingira asili ni jitihada za kuhakikisha maporomoko ya mto huo yanahifadhiwa na kusimamiwa ipasavyo.

Brigedia Jenerali Mkeremy amesema ni wakati sasa kwa watanzania kuanza kuwa na utamaduni wa kutembelea hifadhi hiyo ili kujionea maajabu ya maporomoko hayo.

Amesema , “Eneo hili linavutia na zuri kwa utalii, nitowe wito kwa Watanzania wakiwa katika siku za mapumziko na sikukuu kutembelea na kushuhudia maajabu ya maporomoko haya ambayo yameshatangazwa na Shirika la Umoja wa Matifa la Elimu, Sayansi, na Utamaduni (Unesco) kuwa ni urithi wa dunia.” 

“Niwapongeze TFS kwa ujenzi wa ngazi zenye urefu wa mita 1,277 zinazoshuka hadi kwenye maporomoko haya yanayomwaga maji ziwa Tanganyika. Nimeambiwa kuwa katika ngazi za kushuka chini kwenye maji kuna “view point” tatu, ya kwanza unapotoka kwenye maji imepewa jina la Mheshimiwa waziri wa Maliasili na Utalii n “Kigwangala view point” napendekeza katika “view point” ya pili ambayo ni ya kwanza unapoteremka ngazi iitwe Dos Santos View point na ya tatu inayofuatia iitwe, “Mkeremy view point,” amesema 

Kwa upande wake Kamishna Mhifadhi wa Misitu Profesa Dos Santos Silayo amesema TFS imeweka mikakati kadhaa katika kuhakikisha misitu yake inaingiza mapato ya kutosha kupitia huduma za utalii sambamba na kuuza mazao ya misitu.

Profesa Silayo amesema miongoni mwa mikakati hiyo ni kuvitangaza vivutio vya utalii ekolojia vilivyopo kwenye misitu ya mazingira asilia iliyo chini ya taasisi hiyo.

“Utalii ekolojia na biashara ya mazao ya misitu na nyuki ni nguzo ya utendaji kazi wa taasisi yetu, tunafanya kila liwezekanalo kuimarisha maeneo ya Maporomoko ya Kalambo ili yaweze kutusaidia kuongeza tija katika jukumu letu la ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali, kuongeza mauzo ya nje na fedha za kigeni kupitia huduma za utalii na uuzaji wa mazao ya nyuki,” amesema Profesa Silayo

Aidha, Profesa Silayo amewashukuru wananchi wa kata ya Mpimbwe kwa kukubali kutoa sehemu ya ardhi yao kwa ajili ya mlima ya Mpimbe ili iwe kiunganishi (corridor) kati ya msitu wa Maporomoko ya Mto Kalambo na Msitu wa Hifadhi wa Kalambo, ambayo sasa umeunganishwa na kuwa Msitu wa Hifadhi ya Mazingira Asili.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Brigedia Jenerali Mbaraka Mkeremy akiwa na Kamishna Mhifadhi wa Misitu Profesa Dos Santos Silayo katika Msitu wa Hifadhi ya Mazingira asili ya  Kalambo ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kutembelea maeneo ya hifadhi za misitu na mashamba ya miti ya serikali. 
Maporomoko yaliyo katikaMsitu wa Hifadhi ya Mazingira asili ya  Kalambo.

POLISI IRINGA WAMSHIKILIA MWANAMKE ALIYEKUTWA AKIWA KIFUA WAZI, UNGO KATIKA PAA LA NYUMBA YA MCHUNGAJI

$
0
0
Na Datus Mahendeka, Jeshi la Polisi

JESHI la Polisi Mkoa wa Iringa linamshikilia na kumhoji mwanamke Kabula Masunga(41), anayedaiwa kufanya ushirikiana baada yakukutwa kwenye paa la nyumba ya Mchungaji Jeremia Charles saa 11 alfajiri.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa Juma Bwire amesema leo Agosti 20,2019 kuwa mwanamke huyo anatuhumiwa kufanya ushirikina huo eneo la Isele Ilula wilayani Kilolo mkoani Iringa na kusababisha taharuki kwa wakazi wa maeneo hayo.

Amefafanua mwanamke huyo ambaye ni mpagani na mkazi wa Morogoro alikutwa akiwa katika mazingira hayo akiwa amejifunga mavazi ya rangi nyekundu na nyeusi lakini kifua aliacha wazi.

"Pia alikutwa akiwa na ungo uliyofungwa kitambaa ya rangi nyeusi na nyekundu.Amekutwa pia na pembe la ng'ombe na alijifunga hirizi mikononi. Mwanamke huyo alikuwa na wenzake wanne inaodaiwa alikuwa anasafiri nao kwa kutumia ungo,"amesema . 

Kamanda Bwire amesema kwa sasa wanaendelea kumhoji zaidi ili kufahamu lengo la kufanya ushirikina huo.

Waziri Kabudi afungua rasmi kikao kazi maalum cha Mabalozi

$
0
0



Waziri Kabudi afungua rasmi kikao kazi maalum cha Mabalozi

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi amewataka Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje kuongeza jitihada katika kuhamasisha wawekezaji, wafanyabiashara na watalii kuja nchini ikiwa ni utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi.

Waziri Kabudi ameyasema hayo leo tarehe 20 Agosti 2019 wakati akifungua rasmi kikao kazi maalum cha Mabalozi kinachofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere kuanzia tarehe 20 hadi 23 Agosti 2019.

Mhe. Waziri Kabudi alisema kuwa, Mabalozi ambao wana jukumu kubwa la kusimamia maslahi ya nchi kwenye nchi mbalimbali duniani, wameendelea kufanya kazi nzuri katika katika kuhakikisha dhana ya diplomasia ya uchumi inafikiwa na kwamaba matokeo ya jitihada hizo ni pamoja na kuongezeka kwa watalii, wawekezaji na wafanyabiashara nchini. P.ia kuongezeka kwa fursa za ufadhili wa masomo na ajira kwa Watanzania kwenye nchi mbalimbali

“Hii ni mara yangu ya kwanza kukutana nanyi Waheshimiwa Mabalozi tangu niteuliwe na Mhe. Rais kwenye wadhifa huu. Nazipongeza jitihada zenu katika utekeelzaji wa diplomasia ya uchumi kwani matokeo tunayaona kwa biashara kuongezeka hapa nchini watalii na hata wawekezaji. Hivyo nataka mwongeze jitihada Zaidi ili nchi yetu ifikie azma ya kuwa nchi ya uchumi wa kati na viwanda ifikapo mwaka 2025” alisema Mhe. Kabudi”.

Aidha, Mhe. Waziri Kabudi alitoa rai kwa Mabalozi kuendelea kuwahamasisha Watanzania waishio nje (Diaspora) kujiandikisha na kuanzisha jumuiya zao ili kwa namna moja au nyingine na wao washiriki kuchangia maendeleo hapa nchini.

Akizungumzia changamoto mbalimbali zinazowakabili Mabalozi hao ikiwa ni pamoja na uchakavu wa baadhi ya majengo ya balozi, Mhe. Kabudi alieleza kuwa Wizara inaendelea kutafuta suluhisho la kudumu kwa changamoto hizo.

Akizungumza kwa niaba ya Mabalozi, Kiongozi wa Mabalozi hao, Mhe. Naimi Aziz, Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia alipongeza jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuanzisha na kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo Mabalozi walipata fursa ya kuitembelea. Alisema kuwa, miradi hiyo ni chachu ya maendeleo katika kuifikisha Tanzania kwenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Tunaipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuanzisha miradi mikubwa ya kimkakati. Tumepata fursa ya kujionea miradi hiyo ikiwemo ile ya ujenzi wa barabara, reli na umeme. Kimsingi miradi hii inalenga kumwondolea umaskini Mtanzania kwa vile itarahisha usafirishaji na kumwezessha mkulima kusafirisha kwa urahisi mazao yake kutoka sehemu moja kwenda nyingine kupitia miundombinu hiyo.

Pia aliipongeza Serikali kupitia Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kufanikisha Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kufanyika nchini kwa mafaniko makubwa.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam
20 Agosti 2019
Mhe. Prof. Paramagamba Kabudi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akitoa hotuba ya ufunguzi wa kikao kazi cha Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania sehemu mbalimbali duniani. Kikao hicho kinafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam Agosti 20,2019oLengo la kikao hicho ni kujadili masula mbalimbali yanayohusu utekelezaji wa diplomasia ya uchumi.
Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe akizumgumza kwenye kikao na Mabalozi wa wanaoiwakilisha Tanzania sehemu mbalimbali duniani.
Mabalozi na Watendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia hotuba ya ufunguzi iliyo kuwa ikitolewa na Waziri Mhe. Prof Kabudi (Hayupo pichani).
Sehemu ya Watendaji wa Wizara wakifuatilia kikao

Mabalozi wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi Wakuu wa Wizara mara baada ya ufunguzi wa kikao kazi cha Mabalozi
Viongozi Wakuu wa Wizara wakiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi Wanawake
Viongozi Wakuu wa Wizara wakiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiao wa Afrika Mashariki mara baada ya ufunguzi wa Kikao.
Mhe. Nahimu Azizi Balozi wa Tanzania Addis Ababa, Ethiopia akitoa hutuba kwenye ufunguzi wa Kikoa kazi cha Mabalozi kinachoendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam Mabalozi wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi Wakuu wa Wizara mara baada ya ufunguzi wa kikao kazi cha Mabalozi
Viongozi Wakuu wa Wizara wakiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi Wanawake
Viongozi Wakuu wa Wizara wakiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiao wa Afrika Mashariki mara baada ya ufunguzi wa Kikao.
Mhe. Nahimu Azizi Balozi wa Tanzania Addis Ababa, Ethiopia akitoa hutuba kwenye ufunguzi wa Kikoa kazi cha Mabalozi kinachoendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam 

HOSPITALI YA SEKOU TOURE YAMTUNUKU CHETI MWENYEKITI THE DESK & CHAIR

$
0
0
Mwenyekiti wa The Desk & Chair Foundation (TD & CF) Alhaji Sibatin Meghjee (kulia) akimkabidhi hati ya kamabidhiano ya vyoo nane kati ya 20, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza, Sekou Toure Dk. Bahati Msaki (kushoto) jana.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza, Sekou Toure Dk. Bahati Msaki (kulia) akifungua mlango wa moja ya vyoo vilivyokabidhiwa jana na taasisi ya The Desk & Chair Foundation (TD & CF) tawi la Tanzania.Nyuma ni Mwenyekiti wa taasisi hiyo alhaji Sibtain Meghjee.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza, Sekou Toure Dk. Bahati Msaki (kushoto) akifungua bomba na kwenye sinki la maji nje ya vyoo vilivyokabidhiwa jana na taasisi ya The Desk & Chair Foundation (TD & CF) tawi la Tanzania.Kulia ni Mwenyekiti wa taasisi hiyo alhaji Sibtain Meghjee.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza, Sekou Toure Dk. Bahati Msaki (kushoto) akifungua bomba na kwenye sinki la maji nje ya vyoo vilivyokabidhiwa jana na taasisi ya The Desk & Chair Foundation (TD & CF) tawi la Tanzania.Kulia ni Mwenyekiti wa taasisi hiyo alhaji Sibtain Meghjee.

************
NA BALTAZAR MASHAKA

Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza, Sekou Toure imemtunuku na kumkabidhi cheti Mwenyekiti wa Taasisi ya The Desk & Cair Foundation (TD &CF), Alhaji Sibtain Meghjee kwa a kutambua mchango wake wa kusaidia jamii.

Alhaji Meghjee alikabidhiwa cheti hicho jana na Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Dk. Bahati Msaki muda mfupi baada ya hafla ya kukabidhi matundu nane ya vyoo kwenye hospitali hiyo yaliyotolewa na The Desk & Chair Foundation na kugharimu sh. zaidi ya sh. milioni 20.3.
Akimkabidhi cheti hicho Dk Bahati alisema, Alhaji Meghjee kupitia taasisi hiyo amejitoa na kufanya mambo mengi kwenye jamii na kujenga miundombinu ya jengo la kupumzikia pamoja na vyoo matundu saba kwa ajili wananchi wanaokuja kuona wagonjwa kwenye hospitali hiyo.

Pia amejenga vyoo matundu manne kwenye jengo la kuhifadhia maiti ikiwa ni pamoja na kutoa msaada waa manteki ya kuhifadhia maji, madawa na vifaa tiba pamoja na mgodoro kwa ajili ya wagonjwa.

“Tutakuwa ni wezi wa wafadhila tusipoenzi na kutambua mchango wa Alhaji Meghjee na taasisi yake katika kusaidia jamii ikiwemo hospitali hii na wapokea huduma wake.Hivyo tunamkabidhi cheti hiki ikiwa ni kumbukumbu yake kwa mazuri aliyotufanyia hospitali ya Sekou Toure,”alisema Dk.

Kwa upande wa alhaji Meghjee alishukuru kwa cheti hicho na kuahidi kitakuwa chachu ya kuendelea kusaidia jamii.

“Najisikia faraja kwa kupata zawadi hii ambayo itakuwa chachu ya kuendelea kusaidia jamii katika sekta mbalimbali kwa kushirikiana na serikali kuhakikisha wananchi wanatimiza ndoto zao,”alisema.

Vodacom Tanzania Foundation yatoa milioni 303 kuwezesha Safari ya kuifanya Dodoma kuwa ya kijani

$
0
0
Taasisi isiyo ya kiserikali ya Vodacom Tanzania Foundation (VTF) leo imesaini mkataba wa makubaliano na WWF (World Wide Fund for Nature) ili kuchangia milioni 303 kwa ajili ya mradi wa “kijanisha Dodoma” ambao umeratibiwa na ofisi ya makamu wa rais kwa kushirikiana na WWF. Hafla hiyo ya usainishaji ilifanyika leo katika ofisi za WWF jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na Afisa wa Mazingira kutoka ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dr Thomas Bwana aliyemwakilisha Mgeni rasmi naibu katibu mkuu katika Wizara hiyo Mheshimiwa Balozi Joseph Sokoine.. 

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Dr Bwana amesifu mpango wa Vodacom Tanzania Foundation na WWF (World Wide Fund for Nature) kupambana na hali ya mabadiliko ya tabia nchi. Pia aliongeza kuwa amefurahi namna makampuni na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yanavyoungana kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu namba 13 juu ya hali ya hewa. 

“Kutokana na asilimia 80 ya watu kutegemea mazingira na maliasili kwa ajili ya kutengeneza kipato, kulinda maliasili ni jambo muhimu litakalochochea mafanikio ya kufikia mpango wa maendeleo ya kiuchumi. Serikali imeweka mikakati kwa ajili ya kupambana na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi nchini Tanzania pamoja na kuhakikisha kuwa jamii inamifumo ya kukabiliana na mabadiliko haya, jambo linalofanya tufurahie ushirikiano huu.” 

Aidha Dk Bwana aliongeza kuwa serikali ina mpango wa kupanda miti milioni 280 kila mwaka ili kuunga mkono mpango wa taifa wa kusimamia na kupanda miti kwa ajili kuifanya nchi yetu kuwa ya kijani. 

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation Rosalynn Mworia, amesema kuwa wamefurahia kuingia ubia na WWF ili kutekeleza mpango huo ambao unawiana na mpango mkakati wa VTF kwa mwaka 2019/21 ambao umejikita katika kuchochea hatua za kudhibiti mabadiliko ya tabia nchi. 

Kama kampuni ya Vodacom, maono yetu ni kuwaunganisha watu ili kuleta maendeleo Tanzania, tuna matumaini ya kuunda jamii ya kidijitali, tukilenga kujenga uchumi jumuishi na kufanya kazi katika sayari ambayo athari zetu ni ndogo. Mradi huu umejidhatiti katika kuifanya Dodoma kuwa ya kijani lakini tunatumaini uwepo wa ongezeko la hatua za kisasa dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi kutoka ufahamu na uhamasishaji wa jamii,” alisema Mworia. 

Akizungumzia ushirikiano huo, Mkurugenzi mkazi wa WWF Tanzania, Dr Amani Ngusaru amesema kuwa mfuko huo utaelekezwa kuunga mkono juhudi za serikali katika kuufanya mji wa Dodoma kuwa kijani kwa kupanda miti 100,000 kwa mwaka wa kwanza na kutengeneza bustani ndani ya mji mkuu pamoja na kuongeza ufahamu na kuhamasisha jamii kwa kuwapa mafunzo makundi ya vijana na wanawake katika uzalishaji na matumizi ya mifuko ya plastiki mbadala na kusimamia taka kama shughuli ya kuwawezesha kiuchumi. 

Tumejidhatiti kuunda miradi endelevu ambayo itasaidia kudhibiti changamoto za kimazingira na kijamii nchini Tanzania. Tunaishukuru Vodacom Tanzania Foundation kwa kutuunga mkono katika kutekeleza mpango huu. Athari za mabadiliko ya tabia nchi zinaonekana katika maeneo mbalimbali nchini, hivyo kurejesha mfumo wa ikolojia na kulinda maliasili ni njia mahususi ya kuzuia madhara yenye uwezo wa kuharibu maisha ya watu na utekelezaji wa mradi huu utakuwa ni hatua kubwa sana katika kushughulikia changamoto hizo,” aliongeza Dr Ngusaru. 

Mradi huo uliopewa jina “kuishi kwa amani na mazingira asili” utaanza rasmi mwezi Septemba mwaka huu na utatekelezwa kwa kushirikiana na ofisi ya makamu wa rais – mazingira, halmashauri ya jiji la Dodoma na taasisi ya huduma za misitu (TSF).




Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation, Rosalynn Mworia (kulia) pamoja na Mkurugenzi mkazi wa WWF Tanzania, Dr Amani Ngusaru (kushoto) wakisaini makubaliano yenye thamani ya Shilingi za Kitanzania 303 milioni kwa ajili ya mradi wa “kijanisha Dodoma” ambao umeratibiwa na ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na WWF. Wanaoshuhudia ni Afisa wa Mazingira kutoka ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dk Thomas Bwana (katikati), Meneja ruzuku na mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation, Sandra Oswald (kulia) na Meneja Washirika na Maendeleo wa WWF Dk Severine Kalonga. Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation imedhamiria kuisaidia serikali katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zitokanazo na athari za mabadiliko ya tabia nchi ili kuwezesha mazingira endelevu (sustainable environment) pamoja na maendeleo.



Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation, Rosalynn Mworia (kulia) akibadilishana mkataba na Mkurugenzi mkazi wa WWF Tanzania, Dr Amani Ngusaru (kushoto) ambao una thamani ya Shilingi za Kitanzania 303 milioni kwa ajili ya mradi wa “kijanisha Dodoma” ambao umeratibiwa na ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na WWF. Anayeshuhudia ni Afisa wa Mazingira kutoka ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dk Thomas Bwana. Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation imedhamiria kuisaidia serikali katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zitokanazo na athari za mabadiliko ya tabia nchi ili kuwezesha mazingira endelevu (sustainable environment) pamoja na maendeleo.

Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation, Rosalynn Mworia (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Shilingi za Kitanzania 303 milioni, Mkurugenzi mkazi wa WWF Tanzania, Dr Amani Ngusaru (kushoto), kwa ajili ya kudhmaini mradi wa “kijanisha Dodoma” ambao umeratibiwa na ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na WWF. Anayeshuhudia ni Afisa wa Mazingira kutoka ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dk Thomas Bwana (katikati). Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation imedhamiria kuisaidia serikali katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zitokanazo na athari za mabadiliko ya tabia nchi ili kuwezesha mazingira endelevu (sustainable enviroment) pamoja na maendeleo. 

WIZARA YA NISHATI YAWASILISHA TAARIFA YA MAENDELEO NA UTEKELEZAJI WA WA MIRADI KAMATI YA BUNGE YA NISHATI

$
0
0
Waziri wa Nishati, Mhe. Medard Kalemani akizungumza katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Nishati ambapo Wizara yake iliwasilisha Taarifa ya Maendeleo na Utekelezaji wa Miradi ya REA, kikao hicho kilifanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma, pembeni yake ni Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati wakiwa katika kikao cha Kamati hiyo ambapo walipokea Taarifa ya Maendeleo na Utekelezaji wa Miradi ya REA kutoka Wizara ya Nishati, kikao hicho kilifanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati, Mhe. Dunstun Kitandula akifuatilia jambo katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma, pembeni yake ni Katibu wa Kamati hiyo, Felister Mgonja.

SHAHIDI WA SITA KESI YA UCHOCHEZI INAYOMKABILI MBOWE, WENZAKE ATOA USHAHIDI WAKE, AWATETEA POLISI

$
0
0
Na Karama Kenyunko

SHAHIDI wa sita wa upande wa Jamuhuri katika kesi ya tuhuma za uchochezi inayowakabili viongozi tisa wa Chadema akiwemo Mwenyekiti wake Freeman Mbowe, ameieleza Mahakama video iliyoangaliwa mahakamani kama sehemu ya ushahidi wake, hakukuwa na mahali ambapo panaonesha askari polisi wakishambuliwa na wafuasi wa chama hicho.

Pia amedai katika mkutano huo wa kumnadi aliyekuwa mgombea wa ubunge wa Jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam Salum Mwalimu hakukuwa na wafuasi wa Chadema waliokuwa wanahutubiwa ambao walikuwa wameshika silaha.

Shahidi huyo Koplo Charles amedai hayo leo Agosti 20,mwaka 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu alipokuwa akijibu maswali ya Wakili wa utetezi Peter Kibatala.

Amedai katika ushahidi wake huo wa video ambao mahakamani hapo umepokelewa kama kielelezo namba tano, hakuona wafuasi wa Chadema waliokuwa kwenye mkutano huo uliyofanyika Februari 16,mwaka 2019 katika viwanja vya Buibui na Mwananyamala Kinondoni wakiwashambulia askari polisi.

Shahidi huyo alipoambiwa aeleze ni njia gani Mbowe aliitumia kuongoza mapambano ya kudai haki amedai kuwa yeye hafahamu ila mpelelezi ndiyo anafahamu njia aliyoitumia amedai kuwa ni sahihi.

Imeelezwa kuwa Mbowe katika mkanda huo aliyouonesha mahakamani alitamka kuwa 'Hawataki fujo na hawatafanya fujo na hata kumuua inzi tunataka amani'.Akiendelea kujibu maswali ya Kibatala, Koplo Charles alidai hajawahi kumpa mpelelezi wa kesi hiyo mkanda huo wa video ili autumie kuwahoji washtakiwa.

Akijibu swali la maandamano kuonekana kwenye mkanda huo, amedai unaonesha maandamano hayo kutoka uwanjani hadi Kinondoni Mkwajuni, ambapo aliishia kupiga picha hapo kutokana na fujo zilizokuwa zinaendelea.

"Nilikuwa napiga picha nikiwa kwenye gari la OCD na sijui kama kwenye gari hilo OCD alikuwepo, mimi dereva alinitoa tu pale na kunirudisha kituoni," alidai Koplo Charles

Akielezea kuhusu ni mshtakiwa gani kati ya hao aliyesema waandamane, amedai Mbowe ndiyo alihamasisha wafuasi hao waandamane.Pia, shahidi huyo amedai kuwa katika mkanda huo aliyouonesha mahakamani hakumuonesha Mbunge wa Kawe Halima Mdee akiwahamasisha wafuasi hao kumpiga mawe Magufuli.

"Maneno aliyoyatoa Halima Mdee katika mkutano huo yalisababisha hisia za chuki dhidi ya wananchi, Rais na Serikali yao,lakini hajui kama kumchukia Rais ni kosa la jinai," amedai 

Shahidi huyo alipoambiwa aeleze maneno ya uchochezi yaliyotolewa na viongozi wengine amedai hayakumbuki kwa sababu yaliongelewa kwa urefu, lakini amesisitinza kuwa walitamka maneno ya uchochezi na kuiomba Mahakama nafasi nyingine ya kuonesha mkanda huo kwa lengo la kujikumbisha.

Upande wa mashtaka uliwakilishwa na mawakili wa Serikali wa Kuu, Faraja Nchimbi, Dkt.Zainabu Mango na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon na Wakili wa Serikali, Jackline Nyantori.

Mbali ya Mbowe washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Katibu Mkuu Taifa, Dk. Vincent Mashinji , Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Taifa, Zanzibar, Salum Mwalimu, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Katibu Mkuu Taifa, Vicent Mashinji na Mbunge wa Kawe Halima Mdee.

Wengine ni Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko na Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya.

Washitakiwa wanakabiliwa na mashitaka 13 likiwemo la kula njama, ambapo wote wanadaiwa kuwa, Februari 1 na 16, mwaka jana, Dar es Salaam walikuĺa njama ya kutenda kosa la kufanya mkusanyiko usio halali na kukiuka tamko kutawanyika.

'ALIYEKUWA MWENYEKITI SIMBA ALINIELEZA ALIVYOTOA DOLA ZAKE 32,316.64 KUNUNUA NYASI BANDIA'

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Michuzi TV

SHAHIDI wa kesi inayowakabili viongozi wa Simba, ambaye ni Mchunguzi Mkuu kutoka TAKUKURU Frank Mkilanya, amedai kuelezwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya usajili wa Klabu ya Simba Zackaria Hanspoppe kuwa alitumia fedha zake binafsi dola 32,316.64 kulipa malipo ya awali wakati wa ununuzi wa nyasi bandia za klabu hiyo.

Ameyaeleza hayo leo Agosti 20,mwaka 2019, wakati anatoa ushahidi wake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba.Ushahidi huo ni katika kesi inayowakabili waliokuwa viongozi wa klabu hiyo.

Akiongozwa na Wakili wa Serikali kutoka Takukuru Leonard Swai, Shahidi huyo alipewa maelezo na Hanspope kuwa katika ununuzi wa nyasi hizo yeye binafsi ndiye alianzisha mchakato wa ununuzi wa nyasi hizo na kufanya mawasiliano kati ya mnunuzi na muuzaji.

"Nilihusika kuandika maelezo ya Hanspoppe, kesi ilianza kufunguliwa kabla ya kuandika maelezo yake kwani mshitakiwa alikuwa hajapatikana, baada ya kupatikana ndio maelezo yake yakachukuliwa na hayo ndiyo alinieleza"alidai Mkilanya

Alidai katika maelezo hayo, mshitakiwa huyo pia alimueleza walinunua nyasi hizo kutoka kwa wakala aliyemtaja kwa jina la Hamis kutoka nchini China ambaye alinunua nyasi hizo kutoka Kampuni ya Ninah Trading Company.

Alidai, hundi ya manunuzi ya nyasi inaonesha zilinunuliwa kwa dola 109,499 ambapo Hanspoppe baada ya kupata hundi hiyo alifanya malipo ya awali ya dola 32,316.64 kwa fedha zake binafsi.

Mkilanya alidai,mshitakiwa huyo alimueleza kuwa hundi hiyo baadaye alimkabidhi aliyekuwa rais wa klabu hiyo Evance Aveva na kuna siku wakala (Hamisi) alikuja nchini na kumpa fedha taslimu dola 15,000.

Aliendelea kwa kueleza Hanspoppe alimueleza wakala huyo kwasasa aliyefanikisha ununuaji wa nyasi hizo amefariki.

Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa Agosti 22 mwaka huu.Mshitakiwa mwingine katika kesi hiyo ni aliyekuwa Makamu wa rai wa klabu hiyo Godfrey Nyange maarufu Kaburu.

Washitakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka 10 ikiwemo kula njama, kughushi, kuwasilisha nyaraka za kughushi, kutoa maelezo ya uongo na utakatishaji wa fedha.

Katika mashitaka la kughushi linawakabili washitakiwa wote, anadaiwa katika tarehe hizo hizo kwa pamoja walighushi hati ya malipo ya kibiashara ya Mei 28, 2016 wakionyesha kwamba nyasi bandia zilizonunuliwa na Simba zinathamani ya dola 40,577 sawa na zaidi ya Sh milioni 90 huku wakijua kwamba sio kweli.

Pia katika mashitaka mengine inadaiwa Aveva, Nyange na Hans Poppe kati ya Machi 10 na Septemba 30, 2016 waliwasilisha nyaraka za uongo kuonyesha Simba imenunua nyasi bandia zenye thamani ya Dola za Kimarekani 40,577.
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images