Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live

UINGEREZA YAFADHILI MASOMO YA WATUMISHI WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kulia),akimkabidhi Cheti Mtumishi wa Wizara hiyo kutoka Tanzania Bara, Bi. Patricia Mlowe,wakati wa hafla ya kuagwa rasmi kwa ajili ya safari ya kwenda masomoni Uingerezakwa udhamini wa Shirika la Maendeleo la Uingereza (DFID), hafla iliyofanyika jijini Dares Salaam, wa pili kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Amina Shaaban.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kulia),akimkabidhi Cheti Mtumishi wa Wizara hiyo kutoka Zanzibar, Bw. Hamad Said, wakati wa hafla ya kuagwa rasmi kwa ajili ya safari ya kwenda masomoni Uingereza kwa udhamini wa Shirika la Maendeleo la Uingereza (DFID), hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam, wa pili kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Amina Shaaban.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), akimpongeza mtumishi wa Wizara hiyo, Bi. Diana Ulomi, aliyepata fursa ya udhamini wa masomo katika vyuo vikuu nchini Uingereza kwa kiwango cha Shahada ya Uzamili uliotolewa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Uingereza (DFID)
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa nne kulia), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi Amina Shaaban (wa tatu kushoto) Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Uingereza (DFID), Bi. Beth Arthy (wa tatu kulia) na wajumbe wengine kutoka Tanzania na British Council-Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja wa watumishi waliopata fursa ya kwenda kusoma Uinnereza kwa udhamini wa DFID.

**************

Na. Peter Haule, WFM, Dar es Salaam

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amewataka Watumishi wa Wizara hiyo waliopatiwa ufadhili wa masomo na Serikali ya Uingereza kupitia Shirika lake la Maendeleo (DFID) katika vyuo vikuu vya nchi hiyo kusoma kwa bidii ili kuja kulitumikia taifa kwa umahili zaidi katika nyanja za uchumi na uchambuzi wa masuala ya fedha.

Hayo yameelezwa na Waziri huyo wakati wa hafla ya kuwaaga rasmi watumishi watano wa Wizara hiyo waliopata udhamini huo, iliyofanyika katika Ofisi za British Council- Tanzania, jijini Dar es Salaam.

Dkt. Mpango alisema kuwa, miaka miwili iliyopita aliiomba Serikali ya Uingereza kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Uingereza (DFID), wasaidie kusomesha watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango kwenye Vyuo vikuu vya Uingereza, kwa kuwa Wizara ya Fedha katika nchi yeyote ndio nguvu ya fikra katika Serikali, hivyo bila watumishi wenye ujuzi kutakua na wizara dhaifu.

“Ninawasisitiza sana vijana waliopata fursa ya kwenda kusoma Uingereza, wajue dhamana wanayokwenda nayo, watanzania takribani milioni 50 wanaimani nao, wanamatarajio kwamba watakapokwenda huko watazingatia kusoma kwa bidii, ili wakirudi wawe wataalam waliobobea katika masuala ya uchumi na uchambuzi wa masuala yote ya fedha ndani ya Wizara”, alieleza Dkt. Mpango.

Dkt. Mpango alisema kuwa, pamoja na kuiomba Serikali ya Uingereza kutoa mafunzo kwa vijana hao aliwaomba pia iwapatie mafunzo kwa vitendo katika taasisi zinazojihusisha na masuala ya uchumi na fedha nchini humo ili wapate udhoefu.

Alisema anaishukuru Serikali ya Uingereza kwa kukubali ombi hilo na sasa ni timu ya tatu kupelekwa masomoni, awamu ya kwanza na ya pili walipelekwa jumla ya vijana kumi, na sasa tumewaaga rasmi watumishi watano ambao wataenda mwezi ujao na kufikisha idadi ya watumishi 15.

Amewataka watumishi hao wakaitangaze vizuri Tanzania na wakirudi waje kuitumikia Tanzania ili taifa lipate maendeleo yanayotarajiwa baada ya hatua hiyo muhimu ya kuwekeza kwa vijana watanzania katika kupata ujuzi.

Kwa upande wake Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa Uingereza (DFID), Bi Beth Arthy, alisema kuwa tangu mpango huo uanze Serikali yake imekwisha wasomesha wanafunzi kumi katika fani za uchumi na uchambuzi wa masuala ya fedha na idadi ya watumishi watano watakao kwenda kusoma nchini humo itafikisha idadi ya watumishi 15.

Alisema kuwa lengo la hatua hiyo ni kuisaidia Serikali kuimarisha utawala wa fedha, masuala ya usimamizi wa kodi na mifumo ya kifedha.

Aidha amewapongeza waliofanikiwa kufuzu mitihani mbalimbali iliyowawezesha kupata nafasi hizo kwa watumishi wa Wizara hiyo kutoka Tanzania Bara na Zanzibar na kuwataka kufanya bidii kwa kuzingatia masomo ili watakapomaliza masomo yao warudi kulitumikia Taifa la Tanzania.

Watumishi waliopata ufadhili wa masomo kupitia Shirika la DFID ni pamoja na Patricia Mlowe, Diana Ulomi, Alex Mwakisu, Martha Luanda na Hamad Bakar Said.

Kwa upande wa wanufaika kupitia wawakilishi wao, Bi. Diana Ulomi na Hamad Said waliishukuru Serikali ya Uingereza na Wizara ya Fedha na Mipango kwa jitihada za kufanikisha kuwapatia masomo kwa ngazi ya Uzamili ili kuongeza ujuzi wa kulitumikia taifa katika masuala ya uchumi hasa kipindi hiki ambacho Tanzania inaelekea katika uchumi wa kati uliojikita katika Viwanda na wameahidi kusoma kwa bidii ili kufikia malengo hayo.

CHMTs MWANZA ZAAGIZWA KUSIMAMIA MIONGOZO YA KUKINGA NA KUDHIBITI MAAMBUKIZO

$
0
0
Afisa kutoka Kitengo cha Uhakika Ubora wa Huduma Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Chrisogone Justine German akitoa mafunzo kwa Watoa huduma za Afya na Watumishi wa Sekta ya Afya Mkoa wa Mwanza wakati wa Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga dhidi ya magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC sstandard).


Afisa kutoka Kitengo cha Uhakika Ubora wa Huduma za Afya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Joseph Hokororo akifafanua jambo mbele ya Watoa Huduma na Watumishi wa Sekta ya Afya Mkoa wa Mwanza wakati wa Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga dhidi ya, kwa kufuata kanuni za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC standard ).
Afisa kutoka Kitengo cha Dharura na Maafa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Alex Sanga akielekeza umuhimu wakufuata taratibu kwa mgonjwa wakati wa kumuudumia (IPC Standard) kwa Watoa Huduma za Afya na Watumishi wa Sekta ya Afya Mkoa wa Mwanza.
Baadhi ya Watoa huduma za Afya kutoka Halmashauri za Jiji la Mwanza wakifuatilia Mafunzo kwa makini ya jinsi yakujikinga dhidi ya maambukizi kwa kufuata kanuni na taratibu (IPC Standard) wakati wa kumuudumia mgonjwa.

Baadhi ya Watoa Huduma za Afya na Watumishi wa Sekta ya Afya kutoka Halmashauri mbali mbali jijini Mwanza wakifuatilia kwa makini Semina ya mafunzo juu ya njia bora ya namna ya kujikinga dhidi ya magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa (IPC Standard)


Picha ya pamoja ikiongozwa na Maafisa kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakiwa na Watoa huduma kutoka Halmashauri mbali mbali za Mwanza baada ya kumaliza mafunzo ya namna ya kujikinga na kudhibiti magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa Mkoani hapo.

…………………

Na Rayson Mwaisemba WAMJW- MWANZA

Timu za uendeshaji huduma za Afya za Halmashauri (CHMTs) za Mkoa wa Mwanza zimeelekezwa kusimamia miongozo ya kukinga na kudhibiti maambukizi (Magonjwa) wakati wanatoa huduma za Afya kwa Wagonjwa. 

Hayo yamejiri wakati wa Semina ya mafunzo ya njia bora ya namna ya kujikinga na kudhibiti magonjwa (Maambukizi) kwa kufuata kanuni, miiko na taratibu za utoaji huduma kwa mgonjwa, iliyofanyika Jijini Mwanza ikiwa ni moja kati ya mikoa iliyo katika hatari ya kupata ugonjwa wa Ebola.

Kwa upande mwingine mafunzo hayo yametumika kama njia ya kusambaza muongozo mpya wa namna ya kujikinga na kudhibiti maambukizo (IPC Guidline), ambayo yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, ikiwa ni njia ya kuboresha huduma za Afya nchini. 

Katika mafunzo hayo imedaiwa kuwa Tanzania ipo kwenye hatari ya kupata wagonjwa wa Ebola kutokana na mwingiliano mkubwa wa watu na ukaribu na Nchi ya Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo ambako Mlipuko unaendelea.

Inakadiriwa kuwa watu Bilioni 2.5 Duniani wapo katika hatari ya kupata ugonjwa wa Ebola, huku kati yao 60% ikiwa ni watu kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahara, huku nchi za Sudan, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zikiripoti kuwa na maambukizi ya ugonjwa huo ambao ulisnza tangu 1976.

Kulingana na Taarifa kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) inakadiriwa kuwa Wagonjwa 1790 wapoteza maisha tokea mlipuko huo ulipojitokeza Agosti 2018 Wagonjwa 2577 wamethibitika kuwa na Ugonjwa wa Ebola, huku Wagonjwa 1790 wakipoteza maisha tokea mlipuko huo ulipojitokeza Agosti 2018, huku Wataalamu wa Afya 131 walipata maambukizi, ambapo 41 kati yao wamepoteza maisha.

Hata hivyo, Serikali ya Tanzania tayari imekwisha kuchukua hatua mbalimbali za kuimarisha utayari wa kukabiliana na tishio la Ugonjwa huo ili kuhakikisha hauingii nchini, ikiwemo kuelimisha jamii njia za kujikinga na Ugonjwa ili kuzuia usiingie nchini, na kutoa Elimu kwa Watoa huduma za Afya juu ya kumuhudumia mtu mwenye dalili za Ebola endapo atatokea.

Katika mafunzo hayo, Watoa huduma wameaswa kuzingatia taratibu za kujikinga na kudhibiti maambukizo (IPC Standard precautions) kwa kadri Miongozo inavyoelekeza wakati wote wa kutoa huduma kwa Wagonjwa, jambo litalosaidia kuwaepusha kupata maambukizi, au kumsaidia mgonjwa kupata maambukizi mapya wakati wa matibabu.

Akitoa mafunzo hayo, Afisa kutoka Kitengo cha Uhakiki Ubora Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Joseph Hokororo amesema kuwa Watoa Huduma za Afya wapo katika hatari kubwa za kupata maambukizi ya ugonjwa huu, endapo hawatofuata miongozo na taratibu za utoaji huduma kwa kadri ya muongozo huu

“Mara kwa mara ni muhimu kuwa na tahadhari wakati unahudumia Wagonjwa, hususan kunawa mikono kabla na baada ya kutoa huduma kwa wagonjwa na wasio wagonjwa kwani Watoa huduma mpo kwenye hatari kubwa sana yakupata maambukizo” alisema Dkt. Joseph Hokororo.

Ameendelea kusema kuwa, Shirika la Afya Duniani (WHO) inakusudia kuzuia Ugonjwa wa Ebola kwa kuimarisha huduma za uchunguzi na kusaidia nchi zilizo katika hatari ya kupata ugonjwa wa Ebola.

Pia alisisitiza kuwa Dunia imekumbwa na tatizo la Usugu wa vimelea vya magonjwa ambukizi dhidi ya dawa (antimicrobial resistance), hivyo amesisitiza juu ya umuhimu mkubwa wa kufuata taratibu za kutoa huduma (IPC Standard) ili kusaidia kutokomeza vimelea hivyo. 

Akitoa mafunzo kwa Watoa Huduma za Afya, juu ya namna ya kukinga maambukizi wakati wa kujifungua, Afisa kutoka Kitengo cha Uhakiki Ubora Wizara ya Afya Dkt. Chrisogone German amesema kuwa ni muhimu kwa Watoa huduma kufuata viwango vya kukinga na kudhibiti maambukizo (IPC Standard) ili kudhibiti ya ugonjwa wakati wa kutoa huduma ikiwemo kuhakikisha kunawa mikono kabla ya kufanya kazi za kuhudumia wagonjwa.

Aliendelea kusisitiza kuwa, si jambo zuri kwa Watoa huduma za Afya, kufanya mambo kwa mazoea, hali inayopelekea kufanya kazi kwa mazoea na kujikuta kunasambaa maambukizi kutoka kwa mtu anaepokea huduma za Afya au kinyume chake

HOSPITALI YA SEKOU TOURE YASAIDIWA MATUNDU NANE YA VYOO

$
0
0


NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

HOSPITALI ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza, Sekou Toure imekabidhiwa matundu manane ya vyoo kati ya 20 ili kukabiliana na changamoto ya uhaba wa vyoo na kuweza kumudu idadi kubwa ya wagonjwa na wasindikizaji wanaofika hospitalini hapo huduma ya matibabu.

Matundu hayo manane ya vyoo vilivyogharimu sh. 20,304,800, vimejengwa na Taasisi ya The Desk & Chair Foundation (TD&CF) Tawi la Tanzania kwa ufadhili wa Charty Walfare Aid ya Australia.

Akikabidhi vyoo hivyo kwa uongozi wa hospitali hiyo jana Mwenyekiti wa TD &CF, Alhaji Sibtain Meghjee alisema taasisi hiyo inafanya shughuli za kijamii kwenye sekta za maji, elimu na afya iliguswa na changamoto ya uhaba wa matundu ya vyoo inayoikabili hospitali hiyo ya rufaa ya Mkoa wa Mwanza.

Alisema hospitali ya Sekou Toure iliyojengwa miaka ya 70 ikiwa kituo cha afya ilikuwa na matundu manne tu ambayo hayakidhi mahitaji na kwa kutambua umuhimu wa afya bora kwa jamii inayohudumiwa hapo iliamua kujenga matundu manane kati ya 20, ambapo matundu 12 yajengwa baadaye ili kumudu kuhudumia watu zaidi ya 500 kwa siku. 

Meghjee alisema dhamira ya taasisi hiyo ni kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha afya za wananchi na kuwaepusha na maradhi ya kuambukiza na kuwafanya kuwa na afya bora kuelekea uchumi wa kati wa viwanda, sababu bila afya njema ni vigumu kufikia ndoto hiyo.

“Nina furaha kuwafahamisha awamu ya kwanza ya ujenzi wa matundu 8 ya vyoo umekamilika na niko tayari kuvikabidhi vianze kutumika vikiwa na vifaa vya usafi, tenki la maji la ujazo wa lita 5000.Awamu ya pili ya ujenzi utaanza wiki sita baadaye ukihusisha matundu 12 ili kukamilisha 20 yakiwemo ya watu wenye ulemavu, watumishi na wazee wa jinsia zote,”alisema.

Mwenyekiti huyo wa TD & CF alisema ili vyoo hivyo vidumu aliuataka uongozi wa hospitali hiyo kusimamia kwa dhati ili mundombinu yake isiharibiwe kwa sababu yampo maeneo mengi waliyosaidia kujenga vyoo miundombinu yake imehabiriwa.

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo wa vyoo, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Sekou Toure Dk. Bahati Msaki, alisema inahudumia watu 500 hadi 700 kwa siku hivyo msaada huo umekuja muda muafaka kwa sababu namba ya wahitaji ni kubwa.

“Kwa niaba ya Bodi na uongozi wa hospitali tunashukuru sana The Desk & Chair kwa msada huu wa vyoo matundu 8 ambayo yamegharibu fedha nyingi.Bado taasisi hii inaendelea kujenga mengine 12 ili kukamilisha matundu 20, ili kukidhi mahitaji makubwa ya wagonjwa na wasindikizaji pamoja na watumishi”alisema Dk. Bahati.

Aliongeza kuwa taasisi hiyo imefanya mambo mengi kwenye hospitali hiyo kwa kujenga jengo la kupumzikia wananchi wanaokuja kuona waagonjwa pamoja na vyoo matundu saba, lakini pia imejenga vyoo matundu manne kwenye jengo la kuhifadhia maiti.

Hata hivyo, mbali na changamoto ya uhaba wa matundu ya vyoo kwa wagonjwa wan je, pia wodi nyingi zina changamoto hiyo na kuomba watu wengine wenye kuguswa na hali hiyo kuiga mfano wa The Desk & Chair ili kusaidia kujenga miundombinu ya vyoo hospitalini hapo.

Kwa mujibu wa Dk. Bahati Hospitali ya Sekou Toure ambayo ilijengwa kwenye miaka 70 miundombinu yake ya vyoo ililenga kuhudumia watu 50 ambapo sasa kulingana na hadhi yake inahudumia watu 700 na hivyo kuwa na mahitaji makubwa ya ya matundu ya vyoo.

BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA-AfDB KULIG'ARISHA JIJI LA DODOMA KWA BARABARA ZA KISASA HUDUMA ZA JAMII

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (wa pili kulia) na Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB, Bw. Alex Mubiru wakibadilishana hati za mikataba ya mkopo wenye masharti nafuu wa dola 180m, sawa na sh. bilioni 414 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), kwa ajili ya ujenzi wa barabara za pete (ring road) ama mzunguko kwa kiwango cha lami umbali wa kilometa 110.2 na uboreshati wa miundombinu katika Jiji la Dodoma, Makao Makuu ya nchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (wa pili kulia) akizungumza jambo mbele ya waandishi wa wahabari (hawapo pichani) baada ya kusaini makubaliano ya mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa dola 180m, sawa na sh. bilioni 414 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), kwa ajili ya ujenzi wa barabara za pete (ring road) ama mzunguko kwa kiwango cha lami umbali wa kilometa 110.2 na uboreshati wa miundombinu katika Jiji la Dodoma, Makao Makuu ya nchi. Kulia kwake ni Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB, Bw. Alex Mubiru.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (wa pili kulia) na Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB, Bw. Alex Mubiru wakitia saini makubaliano ya mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa dola 180m, sawa na sh. bilioni 414 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), kwa ajili ya ujenzi wa barabara za pete (ring road) ama mzunguko kwa kiwango cha lami umbali wa kilometa 110.2 na uboreshati wa miundombinu katika Jiji la Dodoma, Makao Makuu ya nchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (wa pili kulia) na Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB, Bw. Alex Mubiru wakitia saini makubaliano ya mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa dola 180m, sawa na sh. bilioni 414 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), kwa ajili ya ujenzi wa barabara za pete (ring road) ama mzunguko kwa kiwango cha lami umbali wa kilometa 110.2 na uboreshati wa miundombinu katika Jiji la Dodoma, Makao Makuu ya nchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (wa pili kulia) na Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB, Bw. Alex Mubiru wakitia saini makubaliano ya mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wa dola 180m, sawa na sh. bilioni 414 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), kwa ajili ya ujenzi wa barabara za pete (ring road) ama mzunguko kwa kiwango cha lami umbali wa kilometa 110.2 na uboreshati wa miundombinu katika Jiji la Dodoma, Makao Makuu ya nchi.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini-TANROADS, Mhandishi Patrick Mfugale, akiwaeleza wanahabari kuhusu michoro ya mradi wa ujenzi wa barabara za mzunguko katika Jiji la Dodoma ambao Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) umetoa mkopo wenye masharti nafuu wa dola 180m, sawa na sh. bilioni 414 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), kwa ajili ya kuutekeleza katika kipindi cha miaka miwili ijayo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (wa pili kulia) walioketi mbele akizungumza jambo mbele ya waandishi wa wahabari (hawapo pichani) kabla ya kusaini makubaliano ya mikataba miwili ya mikopo yenye masharti nafuu yenye thamani ya dola 180m, sawa na sh. bilioni 414 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), kwa ajili ya ujenzi wa barabara za pete (ring road) ama mzunguko kwa kiwango cha lami umbali wa kilometa 110.2 na uboreshati wa miundombinu katika Jiji la Dodoma, Makao Makuu ya nchi. Kulia kwake ni Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB, Bw. Alex Mubiru.
Tukio la kusaini makubaliano ya mikataba miwili ya mikopo yenye masharti nafuu yenye thamani ya dola 180m, sawa na sh. bilioni 414 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), kwa ajili ya ujenzi wa barabara za pete (ring road) ama mzunguko kwa kiwango cha lami umbali wa kilometa 110.2 na uboreshati wa miundombinu katika Jiji la Dodoma, Makao Makuu ya nchi, lililofanyika katika ukumbi wa Hazina Jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Fedha za Nje Bw. John Rubuga (Kushoto) akiwa na maafisa waandamizi wa Wakala wa Barabara Nchini-TANROADS, wakifuatilia kwa makini hotuba za viongozi wa Wizara na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) wakati wa halfa fupi ya kusaini mikataba miwili ya mikopo ya dola milioni 180 kwa ajili ya ujenzi wa barabara za pete (ring road) ama mzunguko kwa kiwango cha lami umbali wa kilometa 110.2 na uboreshati wa miundombinu katika Jiji la Dodoma, Makao Makuu ya nchi, lililofanyika katika ukumbi wa Hazina Jijini Dar es Salaam.


Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam

Jiji la Dodoma na vitongoji vyake, hivi karibuni litabadilika mwonekano wake na kuwa la viwango vya kimataifa baada ya Benki ya Maendeleo ya Afrika, AfDB kuipatia Tanzania mikopo yenye masharti nafuu ya dola milioni 180 sawa na shilingi bilioni 414 kwa ajili ya ujenzi wa barabara za pete (ring road) kwa kiwango cha lami na uboreshaji wa miundombinu katika Jiji hilo.

Makubaliano ya mikopo hiyo yametiwa saini Jijini Dar es Salaam kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, kwa upande wa Serikali, na Meneja Mkazi wa Benki hiyo hapa nchini, Bw. Alex Mubiru.

Akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini mikopo hiyo, Bw. Doto James, amefafanua kuwa mradi utahusisha Ujenzi wa barabara ya mzunguko wa njia nne zenye urefu wa km 110.2 kwa kiwango cha lami kutoka Nala – Veyula – Ihumwa – Matumbulu.

Alisema mikopo hiyo pia inahusisha uboreshaji wa upatikanaji wa miundombinu ya huduma za kijamii ikiwemo huduma za maji na vituo vya afya; Ukarabati wa barabara za mchepuko; na Utekelezaji wa mikakati ya usalama wa barabarani katika mji wa Dodoma itakayotekelezwa katika kipindi cha miaka miwili” alifafanua Bw. James

”Kupitia Mikataba hii, Benki ya Maendeleo ya Afrika itatoa kiasi cha dola za Marekani milioni 138 kupitia dirisha la Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB Window) na dola za Marekani milioni 42 zitatolewa kupitia mfuko wa Africa Growing Together Fund (Mfuko wa Serikali ya China unaosimamiwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika)” alisisitiza Bw. James

Aliishukuru Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali za uwekezaji katika miundombinu ya usafiri itakayoiwezesha Tanzania kufikia azma yake ya kuwa kitovu cha biashara na usafirishaji katika Ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika.

“Uwekaji saini wa Mikataba hii miwili itaongeza kiasi cha fedha ambacho kimetengwa na Benki kwa ajili ya miradi ya ujenzi wa barabara nchini Tanzania, kutoka dola za Marekani milioni 858.16 hadi dola za Marekani bilioni 1.038, sawa na takribani sh. trilioni 2.39”, aliongeza Bw. James

Alisema Barabara hiyo inaungana na barabara ya Cape hadi Cairo inayojulikana kama the Great North Road Highway yenye urefu wa km 10,228 inayopita katika nchi nane ambazo ni Afrika ya Kusini, Zimbabwe, Zambia, Tanzania, Kenya, Ethiopia, Sudan na Misri na ni barabara ya ukanda wa kati (central corridor) inayounganisha Tanzania na nchi jirani za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda na Uganda.

Alidokeza pia kuwa Benki hiyo ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), imeonesha utayari wa kufadhili ukarabati wa barabara ya Bagamoyo–Pangani-Tanga kwa kiwango cha lami na Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa-Msalato, utakaojengwa mkoani Dodoma ambapo tayari maandalizi yameanza.

Kwa upande wake, Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(AfDB), Bw. Alex Mubiru, alisema kukamilika kwa mradi huo kutaiunganisha Dodoma na mikoa mingine ikiwemo Arusha, Iringa, Singida, na Dar es salaam na kwamba utasaidia kupunguza msongamano wa magari katikati ya Jiji la Dodoma kwa sababu magari yanayokwenda kwenye maeneo hayo yatapita pembezoni mwa Jiji.

“Benki ya Maendeleo ya Afrika pamoja na washirika wake tutatoa asilimia 84 ya gharama za mradi ambazo ni dola za Marekani Milioni 215 wakati Tanzania itatoa asilimia 16 na baadae mwaka huu tutatoa kiasi kingine cha msaada wa takriban dola milioni 7.2 ambazo zitatumika kwa ajili ya kuimarisha mazingira kwa kupanda miti kwenye eneo la mradi” alisema Bw. Mubiru.

Aliongeza kuwa hivi sasa Benki yake inajiandaa kutoa mkopo kwa ajili ya miradi miwili muhimu ukiwemo mradi wa uboreshaji wa barabara kutoka Bagamoyo-Pangani-Tanga-Horohoro/lunga, Lunga – Mombasa-Malindi pamoja na ujenzi wa uwanja wa ndege wa Kimataifa-Msalato, miradi ambayo Bodi ya Benki hiyo inatarajia kuipitisha mwishoni mwa mwaka 2019.

Meneja Mkazi huyo wa AfDB nchini alisema matukio haya yote yanatokea kwa sababu Benki yake ina imani na kupongeza mafanikio makubwa ya Serikali ya Tanzania katika kuimarisha maendeleo ya watu wake na kwamba Benki hiyo iko tayari kuhakikisha azma hiyo inafikiwa.

UVCCM Tabora Mjini Wachangia Damu Waathirika wa ajali ya Moto Morogoro

$
0
0
Na, Editha Edward-Tabora 

Umoja wa vijana wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Tabora mjini(UVCCM) wamejitokeza na kuungana na baadhi ya watanzania kuendelea kuchangia Damu kwa ajili ya majeruhi wa ajali ya moto iliyotokea huko mkoani Morogoro 

Taasisi hii ni ya pili kwa mkoa wa Tabora kujitokeza kuchangia Damu kwa ajili ya majeruhi wa ajali hiyo ya moto, ambapo hapo awali chama cha bodaboda na bajaji mkoa wa Tabora ndicho kilichoanza kufanya zoezi hilo ambalo tayari waliweza kukabidhi chupa za Damu miamoja katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili

Kwa upande wa Mwenyekiti wa UVCCM Tabora mjini Ibrahimu Songoro amesema wameguswa na tukio hilo la ajali ya moto hivyo Wamefanya uamuzi wa kujitolea Damu kwa watanzania wenzao waliofikwa na tukio hilo

"Watanzania ni wamoja na sisi vijana wa chama cha Mapinduzi ni wamoja pia tunatakiwa kujali Maisha ya mtu na kujali uthamani wa utu wa vijana wetu nchi nzima kwa hiyo vijana waliopata matatizo na janga la moto mkoani Morogoro tunajiona ni kama sisi matatizo hayo ni ya kwetu na ndio maana leo tumechukua jukumu letu lakuchangia Damu kwa hiari Ili kuweza kusaidia maisha ya wenzetu wanaohangaika kwa kukosa Damu"Amesema Songoro.
 Pichani  ni benki za damu zilizotolewa na vijana wa UVCCM Tabora mjini.
Pichani ni mmoja wa  vijana wa UVCCM Tabora akitoa Damu kwa ajili ya ajali ya moto iliyotokea mkoani Morogoro.
 Pichani ni vijana wa UVCCM  Tabora mjini wakiwa na tayari wametoa  Damu.

GAMBO ATAKA UFUMBUZI CHANGAMOTO ZA MIPAKA KATI YA TANZANIA NA KENYA BADALA YA KUSHINDANA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akifungua kikao cha Uimarisha Mpaka wa Kimataifa kati ya Tanzania na Kenya leo tarehe 19 Agosti 2019 kinachoendelea mkoani Arusha. Wa tatu kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mathias Kabundugulu na wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani Wizara ya Ardhi Hamdoun Mansoor.Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akizungumza na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mathias Kabundugulu wakati wa ufunguzi wa kikao ha Uimarishaji mpaka kati ya Tanzania na Kenya kinachoendelea mkoani Arusha leo tarehe 19 Agosti 2019. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Ujumbe wa Kenya Justa Nkoroi.Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akitoka katika kikao cha Uimarishaji mpaka kati ya Tanzania na Kenya kinachoendelea mkoani Arusha baada ya kukifungua leo tarehe 19 Agosti 2019. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mathias Kabundugulu na wa pili kushoto ni Mkuu wa Ujumbe wa Kenya Justa Nkoroi.Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiwa katika picha ya pamoja kati ya ujumbe wa Tanzania na Kenya unaoshiriki kikao cha Uimarishaji mpaka kati ya nchi hizo mbili. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)



………………………..

Na Munir Shemweta, WANNM ARUSHA

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amewataka wajumbe wanaoshiriki kikao cha Uimarishaji mpaka wa kimataifa kati ya Tanzania na Kenya kutumia kikao hicho kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa changamoto za mipaka badala ya kushindana.

Mrisho Gambo alitoa kauli hiyo leo tarehe 19 Agosti 2019 wakati wa kufungua kikao cha cha muendelezo wa Uimarishaji mipaka ya kimataifa baina ya Tanzania na Kenya kinachoendelea jijini Arusha.

Alisema, anafarijika sana kuona utatuzi wa changamoto za mipaka ya kimataifa kati ya Kenya na Tanzania unafanywa na nchi husika bila kushirikisha mataifa ya nje na kusema kuwa hiyo inaonesha ni jinsi gani nchi hizo zinavyoweza kukaa pamoja kwa kujiamini na kupata ufumbuzi wa masuala yake.

Aliwataka wajumbe wa kikao cha nchi hizo mbili kutafuta ufumbuzi wa changamoto za mipaka ya kimataifa kati yao kwa kukubaliana na kuzingatia tamaduni za nchi hizo sambamba na miongozo ya viongozi wa nchi husika.

Aidha, Mkuu huyo wa mkoa wa Arusha aliwataka washiriki kudumisha pia mahusiano ya kijamii wakati wa majadiliano yao kwa kuwa wananchi wanaoishi mipakani wana mahusiano mazuri ya kindugu na kusisitiza kuwa hali hiyo itadumisha umoja na mshikamano uliopo kati ya nchi hizo.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mathias Kabundugulu alisema kikao hicho cha siku tano ni muendelezo wa vikao vya uimarishaji mipaka ya kimataifa katika maeneo mbalimbali ya mipakani ikiwa na lengo la kuondoa changamoto kama ilivyoelekezwa na Umoja wa Afrika (AU).

Kwa mujibu wa Kabundugulu, Kikao hicho kitapokea taarifa ya ukaguzi wa kipande cha mpaka cha kilomita 128 kutoka eneo la Ziwa Natron hadi Namanga mkoani Arusha ambapo lengo ni kuimarisha mpaka huo hadi Tarakea mkoani Kilimanjaro na baadaye Jasini mkoani Tanga.

Kwa upande wake Mkuu wa Ujumbe kutoka Kenya Justa Nkoroi alisema kikao hicho ni muhimu kwa mustakabali wa nchi za Tanzania na Kenya katika kuangalia changamoto za alama za mipaka ya kimataifa iliyowekwa wakati wa ukoloni na kubainisha kuwa ana imani kikao hicho kutatatua changamoto zilizopo na hatimaye kukamilisha kazi hiyo ndani ya muda uliopangwa na Umoja wa Afrika mwaka 2022.

Tayari jumla ya Kilomita 172 kutoka ziwa Victoria hadi Loliondo mkoani Arusha zimeimarishwa kwa kuwekwa alama (Pillars) za mipaka kati ya Tanzania na Kenya kwa umbali wa mita zisizozidi mita 100 ili zionekanane kwa urahisi na wananchi wanaoendesha shughuli zao katika maeneo ya mipakani.

BALOZI DKT SLAA ATEMA CHECHE

MOBISOL KUTUMIA NISHATI YA JUA KUFIKIA UCHUMI WA KATI WA VIWANDA

$
0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
KAMPUNI ya usambazaji wa huduma  za vifaa vinavyotumia umeme unaotokana na nishati ya jua (Mobisol), wamesema kuwa nchi haiwezi kufikia uchumi wa kati wa viwanda bila Kuwa na umeme wa uhakika katika maeneo mengi ya nchi.

Hayo yamebainishwa  na Meneja Mauzo wa Mobisol Kanda ya Pwani,  Wesley Muyenze wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya mafaniko na mikakati ya kampuni hiyo na kuongezea wateja wanaotumia nishati ya jua ambapo kwa sasa wana wateja 100,000.


Muyenze amesema kuwa kwa sasa watanzania wengi wanauelewa juu ya matumizi ya umeme wa solar hali iliyochangia  kampuni hiyo kupata wateja zaidi 100,000 na kuwahudumia watu  500,000.

Alisema umeme wa jua ni chanzo mbadala cha nishati majumbani , pia nishati hii inaweza kuinua uchumi wa nchi kupitia sekta ya Viwanda na nchi nyingi tayari zimeachana na vyanzo vya kuzalisha nishati ya umeme vilivyozoeleka kama  makaa ya mawe.

Alisema,”nchi haiwezi kufikia uchumi wa viwanda bila Kuwa na umeme wa uhakika katika maeneo mengi ya nchi hivyo kama kampuni watahakikisha wanawafikia wananchi hasa waliopo vijijini ili waweze kuwa na uwezo wa kuzalisha malighafi,”

Muyenze alisema, anawashukuru watanzania ambao wanaotumia nishati ya jua kutoka kampuni ya Mobisol  na wapo baadhi yao wameachana na nishati ya umeme inayotokana na vyanzo vilivyozoeleka.

"Hata hivyo kutokana na kuongezeka kwa wateja katika kampuni yetu,  tumeamua kutoa zawadi ambapo mteja akinunua mtambo wa W 40 anapata betri na paneli bure kabisa, kwahiyo niwaombe watanzania na wateja wetu wafike madukani kwetu ili waweze kununua bidhaa zetu na kujipatia zawadi hizo, " alisema. 

Aidha alisema anatambua kuwa  kuwahudumia wateja zaidi ya 500,000 si kazi ndogo na kuongeza kuwa hali hiyo imetokana na kukua kwa uelewa wa wananchi juu ya matumizi hayo  ya nishati ya umeme unatokana na jua. 

Naye Mteja wa mitambo ya umeme  inayouzwa katika kampuni hiyo kutoka Tarime,  Sophia Simon alisema mitambo inayouzwa na kampuni hiyo ni imara na tangu ainunue haijawai kuzima hata kama mvua inanyeshe wiki nzima. 

Sophia amesema, bidhaa za Mobisol ni nzuri sana na za uhakika ila ametoa ombi kwa kampuni hiyo kupunguza gharama ili kila mwananchi mwenye uhitaji aweze kuipata na kuitumia kwani wapo wengi ila wanashindwa kuwa nazo kutokana na gharama kuwa juu.

Kampuni hiyo pia wamekuwa na utaratibu wa kutoa mtambo wa umeme wa nishati ya jua kwa mkopo wa miaka mitatu utakaomuwezesha mteja kulipa kidogo kidogo ndani ya muda huo.

MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA CHUO KIKUU CHA TAIFA ZANZIBAR HAYA HAPA

$
0
0

CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA ZANZIBAR TANGAZO KWA WAOMBAJI WA CHUO MWAKA WA MASOMO 2019/2020 

CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA ZANZIBAR (SUZA) KINAPENDA KUWAJULISHA WAOMBAJI WAKE WOTE KWA MWAKA WA MASOMO 2019/2020 KUWA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA CHUO KWA NGAZI YA SHAHADA YA KWANZA (DEGREE) YAMESHATOKA NA YANAPATIKANA KATIKA TOVUTI YA CHUO www.suza.ac.tz. AIDHA MWANAFUNZI ANAWEZA KUANGALIA KAMA AMECHAGULIWA AU HAKUCHAGULIWA KUPITIA AKAUNTI YAKE YA MAOMBI NA KUPITIA BARUA PEPE YAKE (EMAIL) ALIYOTUMIA WAKATI WA MAOMBI. KWA WALE AMBAO HAWATOYAONA MAJINA YAO, FURSA YA KUOMBA TENA.

KWA DIRISHA LA PILI (AMBALO LINAANZA TAREHE 21/08 HADI 29/08/2019) ITATOLEWA KWA KOZI AMBAZO ZITATANGAZWA KUPITIA TOVUTI HIYO. KWA WAOMBAJI AMBAO WAMECHAGULIWA CHUO ZAIDI YA KIMOJA (MULTIPLE SELECTIONS) IKIWEMO SUZA, WANAOMBWA WATHIBITISHE CHUO WANACHOKITAKA KWA KUTUMIA KODI MAALUMU (CONFIRMATION CODES) .

WATAKAZOTUMIWA NA TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA (TCU), KWA AMBAE ATASHINDWA KUFANYA HIVYO, AFIKE CHUONI KWA MSAADA ZAIDI. SUZA INAWASISITIZA WAOMBAJI WOTE AMBAO HAWAKUCHAGULIWA KWA AWAMU YA KWANZA KUFANYA MAOMBI TENA KWA AWAMU YA PILI KWA PROGRAMU WANAZOWEZA KUZISOMA KULINGANA NA SIFA ZAO. 

TANBIHI TANGAZO HILI LINAWAHUSU WAOMBAJI WA SHAHADA YA KWANZA TU (DEGREE). KWA WAOMBAJI WA CHETI NA STASHAHADA WANAOMBWA WASUBIRI HADI CHUO KITAKAPOTOA TANGAZO. SUZA INAWATAKIWA MAFANIKIO MEMA WAOMBAJI WOTE. 
AHSANTE.

WAZIRI NDALICHAKO AWAASA WANAFUNZI WALIOPATA UFADHILI WA MASOMO YA ELIMU YA JUU NCHINI CHINA KUWA MABALOZI WAZURI

$
0
0
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi waliopata ufadhili wa masomo nchini China. Hafla hiyo imefanyika katika Ofisi za Ubalozi wa China Jijini Dar es Salaam.

 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na baadhi ya wanafunzi waliopata ufadhili wa masomo nchini China wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi hao iliyofanyika Jijini Dar es Salaam

 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiteta jambo na Balozi wa China nchini Wang Ke.
 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akimkabidhi Balozi wa China nchini Wang Ke zawadi ya picha inayoonesha baadhi ya wanyama wanaopatikana katika hifadhi za Tanzania.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa China nchini Tanzania pamoja na wanafunzi waliopata ufadhili wa masomo nchini China.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako amewaasa wanafunzi waliopata ufadhili wa masomo ya Elimu ya juu nchini China kuwa mabalozi wazuri wa Tanzania nchini humo.
Waziri Ndalichako amesema hayo Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi hao iliyofanyika katika ofisi za ubalozi wa China nchini.
Jumla ya wanafanzi 61 wamepata ufadhili wa masomo kwa shahada za  uzamili na uzamivu katika fani za Afya, Uhandisi, Utabibu , TEHAMA na Mazingira.

Article 2

$
0
0

Mafundi wa DAWASA Mkoa wa Kawe wakiendelea na zoezi la ulazaji wa mabomba ya inchi 6 kwa umbali wa Kilomita 3 kutoka tanki la Changanyikeni lenye uwezo wa kuhifadhi lita 6,000,000, ili kuhudumia wakazi zaidi ya 500 wanaoishi katika kata ya Kibululu.

Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii
WANANCHI wa eneo la Kibululu Goba watafaidika na mradi wa maji wa Changanyikeni baada ya kukamilika kwa ulazaji wa mabomba.

Kazi ya ulazaji wa mabomba inaendelea chini ya mafundi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam DAWASA.
Mafundi wa DAWASA Mkoa wa Kawe wameendelea kulaza mabomba ya inchi 6 kwa umbali wa Kilomita 3 kutoka tanki la Changanyikeni lenye uwezo wa kuhifadhi lita 6,000,000.

Kukamilika kwa mradi huo utawezesha kuhudumia wakazi zaidi ya 500 wanaoishi katika kata hiyo.

Wananchi wa kata ya Kibululu watafaidika na mradi huo mpyabaada ya kukaa kwa kipindi kirefu bila ya kupata maji safi na kwao ni neema na cherekoo.

MABALOZI WA TANZANIA WATEMBELEA MIRADI YA MAENDELEO ZANZIBAR

$
0
0
Mabalozi wakisiliza maelezo kuhusu ujenzi wa uwanja mpya wa ndege Zanzibar (Tereminal 3), kutoka kwa Mratibu wa Mradi huo Bw. Yasiri Costa. 
Mabalozi wakiwasili eneo la mradi wa ujenzi wa barabara ya Kitope hadi Mkokotoni katika kiwango cha lami yenye urefu wa kilomita 31. Barabara hiyo hadi kukamilika kwake itagharimu jumla ya shilingi za Bilioni 58.6. 
Mabalozi wakiwa Wameambatana na watumishi wa Wizara wakitembelea eneo la mradi wa ujenzi wa barabara 
Ujenzi wa daraja ukiendelea katika barabara ya Kitope-Mkokotoni 
Mabalozi wakiwa eneo la ujenzi wa bandari ya mafuta iliyopo Mnangapwani walipotembele eneo la mradi huo Agosti 19, 2019. 
Balozi Ramadhani Mwinyi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, (katikati; ambaye pia aliongoza ujumbe wa mabalozi katika ziara) akitoa maelezo kwa Mabalozi waliopotembelea mradi wa ujenzi wa jengo la makazi na biashara (Shopping mall) unaotekelezwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

Jumla ya mabalozi 42 wanaoiwakilisha Tanzania maeneo mbalimbali Duniani wapo nchini, ambapo pamoja na mambo mengine wametembelea miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali.

Wakiwa Zanzibar Mambalozi wametembelea mradi wa ujenzi wa jengo la biashara na makazi (shopping mall), uwanja mpya wa ndege (terminal 3), ujenzi wa mradi wa nyumba za makazi Fumba, ujenzi wa mradi wa barabara ya kilomita 31 (Kitope hadi Mkokotoni) na ujenzi wa bandari ya mafuta iliyopo eneo la Mnangapwani.

Mabalozi wamendelea kuridhishwa na kufahishwa na namna Serikali zote mbili (Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Muungano) zilivyo jidhatiti kutekeleza miradi mikubwa ambayo itachagiza kasi ya ukuaji wa uchumi na kuboresha maisha ya wananchi. 
Mabalozi wakisikiliza maelezo kuhusu mradi wa ujenzi wa jengo la makazi na biashara (Shopping mall) lililopo eneo la Mapinduzi square, Michenzani kutoka kwa mtaalam na msimamizi wa mradi huo
Mabalozi wakitembelea maeneo mbalimbali yanayouzunguka maradi kuona shughuli zinazondelea katika eneo hilo
Mabalozi wakiwasili katika jengo la Makubusho ya Kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar lililopo eneo la Michenzani, ambapo walipata fursa ya kufahamu kwa undani historia na taarifa mbalimbali kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar
Mabalozi wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa Jengo la Makumbusho ya Kumbukumbu ya Mapinduzi na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki walipotembelea jengo hilo Agosti 19, 2019. 
Balozi Ramadhani Mwinyi Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akisalimiana na wafanyakazi wa mradi wa ujenzi wa uwanja mpya wa ndege wa Zanzibar, alipoongoza ujumbe wa mabalozi katika ziara ya mradi huo Agosti 19, 2019.

SPIKA WA BUNGE, MHE. JOB NDUGAI AKUTANA NA BALOZI WA RWANDA NCHINI TANZANIA

$
0
0

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Mhe. Eugene Kayihura alipomtembela leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Balozi huyo alimtembelea Spika Ndugai kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa nchini Tanzania.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Mhe. Eugene Kayihura alipomtembela leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Balozi huyo alimtembelea Spika Ndugai kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa nchini Tanzania.


Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Mhe. Eugene Kayihura alipomtembela leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Balozi huyo alimtembelea Spika Ndugai kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa nchini Tanzania.


Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akiagana na Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Mhe. Eugene Kayihura alipomtembela leo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma. Balozi huyo alimtembelea Spika Ndugai kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa nchini Tanzania.


Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai (kushoto) akisalimiana na Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Mhe. Eugene Kayihura leo katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma. Kulia ni Katibu wa Spika, Ndg. Said Yakubu, Balozi huyo alimtembelea Spika Ndugai (hayupo kwenye picha) kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa nchini Tanzania.


Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai (kushoto) akifurahia jambo na Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Mhe. Eugene Kayihura leo katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma. Kulia ni Katibu wa Spika, Ndg. Said Yakubu, Balozi huyo alimtembelea Spika Ndugai (hayupo kwenye picha) kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa nchini Tanzania.

Benki ya Maendeleo TIB yawapiga msasa Wataalam 150 wa Maandiko ya Miradi ya Maendeleo

$
0
0
Wataalam kutoka Benki ya Maendeleo TIB imetoa darasa kuhusu maandiko ya miradi ya maendeleo yenye kukopesheka (bankable projects) kwa wataalam wa maandiko kutoka mikoa minne inayojumuisha mikoa ya Mtwara, Lindi, Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani.

Mafunzo hayo yaliongozwa na Mkurugenzi wa Mipango na Mikakati, Bw. Patrick Mongella kwa kusaidiana na Meneja Uendelezaji Biashara, Bw. Joseph Chilambo na Meneja Miradi Maalum, Bw. Derick Moshi.
Mkurugenzi wa Mipango na Mikakati wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. Patrick Mongella akitoa utambulisho wa Programu Maalum na Huduma za Fedha za Benki ya Maendeleo TIB.
Meneja Uendelezaji Biashara wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. Joseph Chilambo akiwasilisha mada kuhusu Huduma za Fedha kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo na Maandilizi yake kwa wataalam wa maandiko kutoka mikoa ya Mtwara, Lindi, Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani.
Meneja Miradi Maalum wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. Derick Moshi akitoa elimu kuhusu Uchambuzi wa Miradi ya Maendeleo kwa wataalam wa maandiko kutoka mikoa ya Mtwara, Lindi, Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani.
Wataalam wa maandiko kutoka mikoa ya Mtwara, Lindi, Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani wakifuatilia kwa makini mafunzo kuhusu maandiko ya miradi yenye kukopesheka (bankable projects).

MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR BALOZI IDD AANZA ZIARA MKOANI SHINYANGA , AKEMEA MAKUNDI NDANI YA CCM KUELEKEA KWENYE UCHAGUZI

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ambaye pia ni Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, ameanza ziara ya siku tano mkoani Shinyanga, kuangalia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ambapo pamoja na mengine amekemea kuwepo na makundi ndani ya chama hicho.

Ziara ya Makamu huyo wa pili Zanzibar imeanza leo Agosti 19 wilayani Kahama kwa kutembelea Jimbo la Msalala, na kukagua utekelezeaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM katika jimbo hilo, ambapo kesho atakuwa jimbo la Ushetu na Kahama Mji. Akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Buganzo kata ya Ntobo halmashauri ya Msalala wilayani Kahama Mkoani Shinyanga, amekemea kuwepo na makundi ndani ya Chama Cha Mapinduzi CCM hasa kuelekea kwenye kipindi cha uchaguzi na kutaka kusiwepo na makundi hayo. Amesema kuwepo kwa makundi ndani ya CCM, kuelekea kwenye kipindi hiki cha uchaguzi ni hatari, ambapo kutawagawa na kuwafanya kushindwa kupata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi na kuwapa nafasi wapinzani. 

“Napenda kuwaambia wana CCM kwenye uchaguzi huu wa serikali za mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu ujao ushindi ni lazima, hivyo naomba kusiwepo na makundi ya aina yoyote ndani ya chama, pamoja na kutoweka wagombea wasio na sifa, bali pitisheni watu wanaokubalika kwa wananchi na waleta maendeleo,” amesema Balozi Iddi.

 “Pia makatibu wa CCM ambao mna tabia ya kupitisha wagombea wenu wasio na sifa kwa sababu ya kufahamiana,naomba tabia hiyo muiache, kwani katika Serikali hii ya awamu ya tano tunataka washinde wagombea ambao wana sifa, waaminifu na wenye kuwatumikia wananchi kuwaletea maendeleo,”ameongeza Balozi Iddi. 

Aidha amesema ili ushindi huo uweze kupatikana ni lazima watu wajitokeze kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura, pamoja na kwenda kupiga kura siku ya uchaguzi, na kuchagua wagombea wa CCM, ambao ndiyo wenye kupigania maslahi ya wananchi. Katika hatua nyingine amewataka watanzania kudumisha amani pamoja kuuenzi Muungano, ili nchi iweze kuwa amani, kwa sababu bila amani nchi haiwezi kukua kimaendeleo kamwe.

 Naye mbunge wa Jimbo la Msalala Ezekiel Maige, akisoma taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi CCM jimboni humo kuanzia (2016-19),amesema jumla ya shilingi Bilioni 41.4 zimetumika kwenye utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, ambapo hadi kufikia (2020) asilimia 90 ya ahadi zitakuwa zimetekelezwa. 

Amesema miradi iliyotekelezwa ni ujenzi wa vituo vya afya, zahanati, ununuzi wa vifaa tiba, miradi ya maji, umeme ,pamoja na miundombinu ya barabara, huku miradi mingine ikiendelea kutekelezwa. Na Marco Maduhu - Malunde1 blog TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Buganzo kata ya Ntobo halmashauri ya Msalala na kukemea kuwepo na makundi ndani ya CCM hasa kuelekea kwenye kipindi cha uchaguzi, na kuwataka wawe kitu kimoja ili ushindi uweze kupatikana kwa kushinda viti vyote. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, ambaye pia ni mlezi wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga, akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Buganzo Kata ya Ntobo halmashauri ya Msalala, nakuwataka watanzania wadumishe Amani pamoja na kuuenzi Muungano. Mbunge wa Jimbo la Msalala Ezekiel Maige akisoma taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha mapinduzi CCM kwa kipindi kuanzia (2016-19) na kusema jumla ya Shilingi Bilioni 41.4 zimetumika kwenye utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Mbunge wa Jimbo la Msalala Ezekiel Maige, akimuomba Makamu huyo wa Pili wa Rais Zanzibar kutoa msukumo Serikalini ili kufanikisha ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha lami kutoka Kahama kwenda Geita. Mbunge wa jimbo la Msalala Ezekiel Maige akikabidhi taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM kwa Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi mara baada ya kumaliza kuisoma. Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Shinyanga Azza Hilal Hamad, akimuahidi mlezi wa chama hicho Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Balozi Seif Ali Iddi kuwa ataendelea kushirikiana na wabunge mkoani humo kuendelea kuitekeleza ilani ya uchaguzi kwa kwaletea maendeleo wananchi zikiwamo huma za kiafya. Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, akielezea namna serikali mkoani humo inavyoendelea kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kushirikiana na wabunge. Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa, akimuahidi Makamu Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ambaye pia ni mlezi wa CCM Mkoa wa Shinyanga, kuwa maelekezo yote atakayo yatoa atayasimamia ili chama kiendelee kuwa imara. Wananchi wa kijiji cha Buganzo Kata ya Ntobo halmashauri ya Msalala wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi. Wananchi wa kijiji cha Buganzo Kata ya Ntobo halmashauri ya Msalala ,wakiwa na Madiwani kwenye mkutano wa hadhara wa Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi. Wananchi wa kijiji cha Buganzo Kata ya Ntobo halmashauri ya Msalala wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi. Wanachama wa CCM wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwenye kijiji cha Buganzo Kata ya Ntobo halmashauri ya Msalala. Wanachama wa CCM wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwenye kijiji cha Buganzo Kata ya Ntobo halmashauri ya Msalala. Wanachama wa CCM wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwenye kijiji cha Buganzo Kata ya Ntobo halmashauri ya Msalala. Awali Makamu wa Rais wa Pili Zanzibar Balozi Seif Ali Idd akiweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa jengo la CCM Tawi la Buganzo. Makamu wa Rais wa Pili Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi kiasi cha Shilingi milioni moja Taslimu mwenyekiti wa CCM tawi la Buganzo Lukas Shitungulu kwa ajili ya ukalimishaji wa jengo la ofisi la Chama kwenye tawi hilo. Wanachama watano wa Chadema kwenye kijiji hicho ya Buganzo- Ntobo wakirudi CCM. Getruda Boniphace aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema kijiji cha Buganzo, ambaye amejiunga CCM, amesema sababu za kurudi CCM kuwa alikuwa amepotea na kuamua kuunga juhudi za Rais John Magufuli. Burudani za ngoma zikitolewa kwenye mkutano wa hadhara wa Makumu huyo wa pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwenye kijiji cha Buganzo Kata ya Ntobo- Msalala. Awali Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwasili kwenye uwanja wa ndege Buzwagi wilayani Kahama Tayari kwa ziara mkoani Shinyanga ya kuangalia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi CCM kwenye majimbo yote mkoani humo. Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akisalimiana na mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa mara baada ya kushuka kwenye ndege kuanza ziara mkoani Shinyanga. Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd akisalimia na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, mara baada ya kushuka kwenye ndege tayari kwa ziara yake mkoani humo. Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Solwa Ahmed Salum ambaye alifika kwenye uwanja wa ndege Buzwagi wilayani Kahama kwa ajili ya kumpokea na kumkaribisha mkoani Shinyanga, wapili kushoto ni mbunge wa jimbo la msalala Ezekiel Maige. Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

MSD KUJENGA KITUO CHA MAUZO NA USAMBAZAJI DAWA SIMIYU

$
0
0
Mkurugenzi mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Laurean Bwanakunu akitoa neno la utangulizi katika mkutano wa tathmini ya utendaji kazi wa Bohari ya Dawa(MSD) unaofanyika Mjini Bariadi mkoani Simiyu kwa siku tatu na lengo likiwa ni kujenga ushirikiano na kufanya kazi kwa timu, Agosti 19, 2019.
Katibu Tawala wa mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akifungua mkutano wa tathmini ya utendaji kazi wa Bohari ya Dawa(MSD) unaofanyika Mjini Bariadi mkoani Simiyu kwa siku tatu na lengo likiwa ni kujenga ushirikiano na kufanya kazi kwa timu, Agosti 19, 2019.
Katibu Tawala wa mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akifungua mkutano wa tathmini ya utendaji kazi wa Bohari ya Dawa(MSD) unaofanyika Mjini Bariadi mkoani Simiyu kwa siku tatu na lengo likiwa ni kujenga ushirikiano na kufanya kazi kwa timu, Agosti 19, 2019.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Bohari ya Dawa(MSD), Victoria Mwanri Elangwa akitoa taarifa katika mkutano wa tathimini ya utendaji kazi wa Bohari ya Dawa(MSD) unaofanyika Mjini Bariadi mkoani Simiyu kwa siku tatu na lengo likiwa ni kujenga ushirikiano na kufanya kazi kwa timu, Agosti 19, 2019.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, bw. Jumanne Sagini (wanne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wakurugenzi wa idara mbalimbali na mameneja wa kanda wa Bohari ya Dawa nchini(MSD) mara baada ya kufungua mkutano wao wa siku tatu, Agosti 19, 2019 ambao unafanyika kwa siku tatu Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya wakurugenzi wa idara mbalimbali na mameneja wa kanda wa Bohari ya Dawa nchini(MSD) wakiwa katika mkutano wao wa siku tatu,uliofunguliwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, bw. Jumanne Sagini Agosti 19, 2019 ambao unafanyika Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya wakurugenzi wa idara mbalimbali na mameneja wa kanda wa Bohari ya Dawa nchini(MSD) wakiwa katika mkutano wao wa siku tatu,uliofunguliwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini Agosti 19, 2019 ambao unafanyika Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya wakurugenzi wa idara mbalimbali na mameneja wa kanda wa Bohari ya Dawa nchini(MSD) wakiwa katika mkutano wao wa siku tatu,uliofunguliwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, bw. Jumanne Sagini Agosti 19, 2019 ambao unafanyika Mjini Bariadi Mkoani Simiyu..



……………………..

Na Stella Kalinga, Simiyu RS

Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya dawa (MSD) Laurean Bwanakunu amesema Bohari ya dawa inatarajia kuanza ujenzi wa kituo cha mauzo na usambazaji dawa mkoani Simiyu ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa mkoa wa Simiyu na mikoa jirani.



Bwanakunu ameyasema hayo Agosti 19,2019 katika ufunguzi wa mkutano wa tathmini ya utendaji kazi wa menejimenti na mameneja wa kanda wa bohari ya dawa nchini.

lengo likiwa ni kujenga ushirikiano na kufanya kazi kwa timu.

Bwanakunu amesema wameamua kufanyia mkutano wa tathimini mkoani Simiyu ili kuweza kujionea eneo la ujenzi wa kituo cha mauzo ya dawa ikiwa ni moja ya kuongeza wigo mpana wa utoaji huduma.

“Tutakuwa na mkutano wa siku tatu hapa Simiyu kwa ajili kufanya tathmini ya utendaji kazi ulivyokuwa kwa mwaka mzima, tutawafanyia tathmini wakurugenzi wote na wenyewe watamfanyia Mkurugenzi Mkuu; lakini pia tutatumia fursa hii kutembelea mahali tulipoamua kujenga bohari kwa kuwa tunatarajia kujenga bohari hapa Simiyu”alisema Bwanakunu.

Akifungua mkutano huu, Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amesema maboresho ya usambazaji wa dawa yaliyofanywa na Bohari ya Dawa (MSD) yameongeza upatikanaji wa dawa mkoani Simiyu ambapo kwa sasa upatikananji wa dawa ni zaidi ya asilimi 88.

Aidha, Sagini ametoa wito kwa Taasisi zote za Umma zinazohitaji maeneo kwa ajili ya kujenga Ofisi zao kufika mkoani Simiyu, ambapo amewahakikishia upatikanaji wa maeneo lengo likiwa ni kuendelea kusogeza huduma mbalimbali karibu na wananchi.

Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Bohari ya Dawa(MSD), Bibi. Victoria Elangwa amesema uwepo wa kituo cha kusambaza dawa Simiyu kutapunguza umbali kwa Mkoa wa Simiyu na mikoa ya Mara na Shinyanga kupata huduma za Bohari ambazo kwa sasa zinapatikana Mwanza.

Ameongeza kuwa ujenzi wa Kituo hicho unatarajia kuanza mara moja kwa kuwa tayari wataalam wameshaanza kushughulikia masuala ya ukamilifu wa mazingira na baada kukamilisha kazi hiyo atatafutwa mkandarasi kwa ajili ya kuanza ujenzi.

Mastaa wa Gospel kupamba uzinduzi album ya Mariam Kilyenyi Dar

$
0
0
Kwa mara nyingine, mwimbaji wa nyimbo za Injili anayetikisa nchini Mariam Kilyenyi anatarajia kuachia albamu yake ya video inayoitwa Hakimu wa Haki katika uzinduzi utakaopambwa na waimbaji lukuki.

Uzinduzi huo unatarajia kufanyika Jumapili ya Septemba 29, 2019 kwanzia saa saba mchana katika kanisa la uamsho Pentecoste church kwa mchungaji Lilian Kadodo, Ubungo Shekilango.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mariam aliwataja baadhi ya waimbaji watakaomsindikiza kuwa ni DR Tumaini Msowoya Bahati Bukuku,Madame Ruth, Edson Mwasabwite Joyce Ombeni, Robert mwanja, Sarah Mghamba, Loyce Nducha Tumaini Njole, Stephania Masawe na Eddah Mwampagama.

Wengine ni Agnes Nkungwe, Elizabeth Shimanje,Jamuhury Zacharia, Tumaini Mwasubila, Hafsa kazinja,Magreth Sembuche Kisa ludutu Glory Moses ,Biver Kasigala, Surprise France silvia Alexander ,Neema Mahhu na Pst Grace Rendi 

Aliwataja wengine kuwa ni w Dk Donald Kisanga, Stellah Joel,Alfonce Mutema, Daudi Nyigo, Yasinta Kadawele huku mwimbaji Jack Mgaza kutoka South Africa akiwa mmoja kati ya wageni maalum walioalikwa sambamba kabsaaaa na Agnese bilama kutokea Arusha.

Aliwataka wakazi wa Dar es Salaam na viunga vyake vyoooote kutokosa uzinduzi huo na kupata kazi yake mpya aliyofanikiwa kuiweka kwenye video.

Alitaja baadhi ya nyimbo zilizo kwenye albamu hiyo kuwa ni pamoja na Natafuta Mshauri, Agano Langu, Hakimu wa Haki, Pam Pam tukuza, Chereko leo, Ameshinda ,Laana imegeuka Baraka, Mapambazuko na Ushindi Lazima.

Mariam alisema japo ni gharama kubwa ya uandaaji wa muziki pamoja na kusambaza kazi hiyo lakini amefanikiwa kukamilisha albamu yake kwa mfumo wa video.
Mwimbaji wa Injili Mariam Kilyenyi pichani anatarajia kuzindua album yake ya Video hivi karibuni.

WATAFITI AKIOLOJIA WANAKABILIWA NA UKOSEFU WA VIFAA

$
0
0

NA DENIS MLOWE, IRINGA

WANAFUNZI wanaofanya mafunzo kwa vitendo kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Akiolojia juu ya utafiti wa masuala ya kihistoria wanakabilwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa vifaa.

Akizungumza wakati wa kuadhimisha miaka 128 tangu ushindi wa Chifu Mkwawa dhidi ya askari wa Kijerumani na kufanyika katika eneo lilipojengwa mnara wa kumbukumbu eneo la Lugalo katika wilaya ya Kilolo,Mwanafunzi wa Mwaka wa pili chuoni hapo, Amani Kalwani alisema kuwa changamoto hizo zinatokana na kutokuwepo kwa vifaa vya kufanyia utafiti.

Alisema kuwa utafiti wanaofanya ni kuhusu masalia ya vita lengo kubaini vitu vilivyotumika katika mapigano na njia zilizotumika katika vita hiyo baina ya askari wa chifu Mkwawa na askari wa Kijerumani ambapo walipigana vita eneo la Lugalo na kukutana na changamoto zikiwemo ukosefu wa vifaa vya uchunguzi.

Alisema kuwa changamoto nyingine ni ukosefu wa huduma za jamii zikiwemo maji safi na salama, umeme, huduma za afya ambapo wanafata zaidi ya km 25 Iringa mjini hali ambayo inafanya suala la utafiti kuwa mgumu zaidi.

Kalwani alisema kuwa changamoto nyingine wanayokumbana nayo katika utafiti huo ni suala zima la posho ya kujikimu hali inayowakabili wanafunzi wengi walioko katika utafiti huo na kutoa wito kwa bodi ya mikopo kutoa posho linganifu kwa wanafunzi wote.

Alisema kuwa kuna haja kubwa ya bodi ya mikopo kuangalia kwa umakini suala ya posho ya kujikimu kwani wanafunzi wengine wanapata hela kidogo hali inayofanya asilimia kubwa kufanya utafiti kwa kujitolea licha ya utafiti huo kuwa faida kwa taifa hasa katika masuala ya historia.

“Kutambua mafunzo na mchango wa utafiti ipo haja ya bodi ya mikopo iweke ulinganifu wa posho za kujikimu kama ilivyo katika kada ya ualimu hali itakayosaidia wanafunzi wengi kufanya vyema katika utafiti wanaofanya” alisema

Kwa upande wake, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kitivo cha Akiolojia, Dk Frank Masele, alisema kuwa utafiti wa mwaka jana ulifanyika bila kuwa na vifaa vya kisasa hali iliyomlazimu utafiti wa mwaka huu kutumia fedha za kujikimu kupata mashine moja ya kufanyia utafiti kwa lengo la kubaini mabaki yaliyotumika katika vita kati ya Askari wa chifu Mkwawa na askari wa kijerumani.

Alisema kuwa utafiti huo unafanyika katika mazingira magumu kwa wanafunzi na kulazimika kuishi katika nyumba moja kwa kuchangishana ili kuweza kuwapatia mafunzo kwa vitendo juu ya kuitambua historia ya nchi katika harakati za ukombozi.

Dk. Masela alisema kuwa maadhimisho hayo yanatumika kutoa elimu kwa jamii inayozunguka kutambua juu ya historia za mashujaa na utafiti huo utafanyika kwa miaka 3 ingawa changamoto kubwa ya wanafunzi wanayopata ni ukosefu wa fedha.

Alisema kuwa kuwe na fungu la kutosha la kuwawezesha wanafunzi kuweza kufanya utafiti kwani kuna mazingira magumu ya ufundishaji hasa somo la Akiolojia ambalo asilimia kubwa mazingira yake makubwa ni porini ambapo wanakumbana na vitu hatarishi mbalimbali ikiwemo nyoka wenye sumu kali;.

Alisema kuwa katika utafiti wanaofanya kwa mwaka jana ambao walikuwa hawana vifaa walifanikiwa kupata masalia 14 ya maganda ya risasi yaliyotumika katika vita na mwaka huu kwa wiki mbili wamefanikiwa kupata masalia 6 hali ambayo wanatarajia kupata vitu vingi zaidi.

Alisema kuwa utafiti wanaofanya mwaka huu wanatarajia kuangalia njia mbalimbali zilizotumika katika vita baina ya Askari wa Chifu Mkwawa na Askari wa Kijerumani na ukubwa wa eneo la vita ambalo walitumia kupigana mwaka na Mkwawa kupata ushindi mwaka 1891.

Naye mkuu wa wilaya ya Iringa, Asia Abdalah alisema kuwa ifike wakati sehemu zote zenye vivutio ziweze kuleta faida kwa serikali wa watalii kutembelea na kuleta mapato. 

Alisema eneo la Lugalo muhimu kuzungushiwa uzio ili ifike wakati watu waweze kulipa kiingilio na kuleta mapato kwa wilaya na taifa kwa ujumla kuliko ilivyo sasa
Mkuu wa wilaya ya Iringa, Asia Abdalah akifanya utafiti wa kuangalia masalia ya Vita Kati ya askari wa chifu Mkwawa na askari wa kijerumani.




Mkuu wa wilaya ya Iringa, Asia Abdalah akizungumza wakati wa maadhimisho ya Miaka128 tangu ushindi wa chifu Mkwawa dhidi ya askari wa kijerumani. 

INSTITUTE OF SOCIAL WORK: SELECTED STUDENTS FOR BACHELOR DEGREE PROGRAMS 2019/20 INTAKE

Saa 48 nilizoishi ndani ya SADC

$
0
0
Na Hafidh Kido

WIKI tatu zilizopitita sikuwa na uelewa wowote kuhusu Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa kushirikiana na Idara ya Habari (MAELEZO), ililazimika kutoa semina za siku tatu kwa wanahari mkoani Morogoro.

Semina ile si tu ilinifungua masikio lakini iliniongezea uelewa mpana juu ya jumuiya hii muhimu kwa maendeleo ya Tanzania na nchi nyingine wanachama.

Siku wiki zikakatika, ikafika Agosti na kuanza mchakamchaka wa shughuli za SADC katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam. Wiki ya nne ya viwanda, mikutano ya makatibu wakuu, mawaziri na hatimaye ikafika siku yenyewe ya Agosti 17 na 18. Mkutano wa wakuu wa nchi na serikali wa SADC.

Nilifika nyuma ya ukumbi na kukaguliwa, baadaye nilianza kutembea kutokea usawa wa Uwanja wa Gymkhana kilipo kituo cha polisi. Kulia na kushoto kwangu kulikuwa kumepambwa na mabango makubwa yanayoonyesha utajiri wa mbuga za wanyama na hifadhi za taifa, milima, mabonde na maporomoko ya maji tulivyo navyo nchini.

Kisiwa cha Zanzibar, wanyama kama Mbega na wengine adimu wanaopatikana bara hili tu lililobarikiwa kila utajiri. Nilijihisi kama naingia mlango wa peponi. Mwili ulinisisimka vinyweleo vikanisimama. Nilitamani dunia nzima ijue kuna nchi inaitwa Tanzania na leo ina ugeni kutoka nchi 16 za Afrika.

Nje ya ukumbi nilifurahishwa na ngoma za asili, zilikuwa zimepangiliwa kwa namna ya kipekee kuvutia kila mtazamaji, kinamama na kinababa wa Kimaasai walikuwa wakinema na kuruka kwa sauti zao za kupendeza na kuvutia.

Utasema ni Twiga waliotoroka mbugani, kinamama wa Kimaasai walikuwa wakichezesha shanga walizozizungusha shingoni utasema wanapeta mahindi. Wao hawaruki hawasogei, wanainua visigino na kuvirudisha, mchezo huo ulileta taswira nzuri ya mtibwiriko wa maungo na kelele za polepole lakini zinazofuatana za shanga mwilini mwao. Huku sauti nzito za kiume zikiunguruma kama Simba mzee, zikisikika kwa nyuma kama kuwagombesha wakinamama wanaolalamika kwa sauti tamu na nyororo.

Ratiba ilionyesha shughuli zinaanza saa mbili asubuhi, kwa kawaida sipendi kuwa wa mwisho katika mambo ya msingi. Saa moja kasoro robo nilikuwa ukumbini, moja kwa moja nilifululiza chumba cha habari gorofa ya kwanza upande wa kushoto. Nilijikuta peke yangu, sikushangaa kwa kuwa dhamira yangu haikutaka niwe wa mwisho.

Baada ya kujipanga nilijitoma ukumbini, upande wa juu tulipopangiwa wanahabari. Mwili ulisisimka kwa kuona siku imewadia kuweka historia. Ni historia katika uandishi wa habari kuripoti tukio kubwa namna hiyo. Sikuwahi kufanya hivyo kabla.

Wakati tukipewa semina na Profesa Palamagamba Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika ukumbi wa Mikumi miezi kadhaa kabla ya tukio hili, nilivutiwa na mwanahabari mkongwe Deodatus Balile namna alivyoelezea kwa madaha mkutano wa SADC uliofanyika kwa mara ya kwanza nchini mwaka 2003, ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

Nilimuona kama aliyeshushwa duniani moja kwa moja bila kuzaliwa, nami nikaweka ahadi Mungu anipe pumzi na afya ili nipate cha kuwaelezea wanahabari wenzangu miaka 16 ijayo namna nilivyoshiriki mikutano ya SADC hatua kwa hatua.

Nilitia mguu wangu eneo la wanahabari saa mbili kasoro, nikaanza kuwaona viongozi wastaafu wakiwasili, alianza Mzee Benjamin Mkapa, akafuata Mzee Jakaya Kikwete kisha akaja Mzee Ali Hassan Mwinyi. Walikaa pamoja wakizungumza na kucheka, ishara nzuri kwa wageni.

 Saa nne kamili asubuhi viongozi wa kitaifa wa nchi 16 za jumuiya hii wakaanza kuingia mmoja baada ya mwingine, alianza mwenyeji Rais Dk. John Magufuli wakafuatia viongozi wengine mmoja mmoja kwa mpangilio wa kupendeza. Walisimama kwa muda wakitizama bendera ndogo zilizopangwa mshazari mbele ya meza zao.

Walipangiwa kukaa kwenye viti vya rangi ya maziwa vilivyodariziwa kwa vitambaa vya mahmeli, juu ya meza kulikuwa na vibakuli vidogo vyenye lawalawa za kuwapumbaza wasichoke kuendesha mkutano. Kila mmoja alipangiwa seti ya vifaa maalum vya kufasiri lugha.

Meza yao ilipendeza kweli maana chini kulitandazwa mashada ya maua kuanzia mwanzo hadi mwisho wa meza yenye urefu yapata futi 30, imepindwa kidogo kuleta taswira ya mwezi mchanga ili kuwafanya watazamaji wawaone vizuri.

Marais walikuwa 11 wakiongozwa na Rais Dk. John Magufuli (Tanzania), Rais Cyril Ramaphosa (Afrika Kusini), Rais Edgar Lungu (Zambia), Rais Dk. Hage Geingob (Namibia), Rais Emmerson Mnangagwa (Zimbabwe), Rais    João Lourenço (Angola), Rais Filipe Nyusi (Msumbiji), Rais Danny Faure (Ushelisheli) na Rais Azali Assoumani (Comoro).

Wengine ni Rais Andry Rajoelina (Madagascar), Rais Felix Tshisekedi (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo - DRC), Makamu wa Rais Everton Herbert Chimulirenji (Malawi), Waziri Mkuu Tom Thabane (Lesotho), Waziri Mkuu Ambrose Mandvulo Dlamini (Eswatini), Waziri wa Mambo ya Nje Unity Dow (Botswana) na Waziri wa Mambo ya Nje Nandi Botha (Mauritius).

Baada ya kuimbwa wimbo wa SADC ukafuata wimbo ya AU kisha ukaimbwa wa Tanzania, nilitamani niitoe sauti yangu yote ili ukumbi mzima ujue kuna mtanzania anaitwa Hafidh Kido anaimba wimbo wa taifa lake.

Cheche za machozi zilinitoka pembezoni mwa macho kwa furaha, nilikuwa nimeukumbatia moyo wangu uliofuatisha mdundo wa Brass Band ya Polisi kwa madaha. Hakika kuwa mtanzania kwenye jumuiya hii ya SADC ni heshima kubwa.

Baada ya hapo zilifuata taratibu za kiitifaki na ukafika wasaa wa Rais Magufuli kukabidhiwa kijiti cha uenyekiti kutoka kwa Rais Geingob wa Namibia. Kilikuwa kipindi cha amani na usikivu wa hali ya juu, kila mmoja alitaka kusikia mwenyekiti mpya atasema nini.

Kama ilivyo kawaida yake, Rais Magufuli ni mkweli na hapendi kupamba maneno. Alieleza alivyoumizwa na alivyofurahishwa ndani ya SADC. Akaahidi kuyabadili yaliyomuumiza ndani ya mwaka mmoja, ikiwa atapewa ushirikiano wa kweli.

Siku ya kwanza ikaisha, vikao vya ndani vikahamia Ikulu ya Dar es Salaam. Siku iliyofuata kama kawaida nikawahi nafasi yangu ndani ya ukumbi. Ulijaa kama jana (Jumamosi Agosti 17, 2019).

Kilichonidhihirikia kuwa leo (Jumapili Agosti 18, 2019) ndio tunaikamilisha safari ya mwezi mzima katika hekaheka za SADC ni pale nilipomuona dada yangu Zamaradi Kawawa ambaye alikuwa mwenyekiti wetu kwa upande wa wanahabari kupitia kamati ya kuratibu mkutano huu, ambaye pia ni Naibu Mkurugenzi wa MAELEZO, alikuwa akiingia ukumbini huku akicheza kwa furaha.

Katika maisha yangu tangu nimjue dada Zamaradi sikuwahi kumuona akicheza, alionyesha kazi imekamilika salama na sasa tumekabidhiwa rasmi jukumu la kuiandika vema SADC ikiwa imerejea nyumbani, Dar es Salaam.

Kikao cha kufunga hakikuwa kirefu, itifaki zilifuata kama kawaida na kilipofika kipindi cha kutoa hotuba ya ufunguzi sote tulikaa kimya kumsikiliza mwenyekiti atakuwa na yapi ya kutuambia. Alipoanza kwa kusalimia kwa lugha ya Kiswahili, nilimuonyesha alama ya dole mwanahabari mwenzangu aliyekaa upande wa kushoto ukumbini; ishara ya kuwa Kiswahili kimekubaliwa kuwa lugha rasmi ya nne ya SADC.

Ni kweli, baadaye Mwenyekiti Rais Magufuli aliueleza umma wa wana SADC kuwa Kiswahili kimepitishwa kwa kauli moja kuwa lugha ya nne ya SASDC. Kila mtu alifurahi, hapo ndipo nilipoamini lugha hii ni lugha ya ukombozi.

Mwisho baada ya kufunga, nilitaka kuwahi kuandika stori ili niitume gazetini Jamvi la Habari. Kwa mara nyingine nikakutana na uso wa bashaha wa Dada Zamaradi akiwa amesimama pembeni ya mlango akiwagongea ‘ngumi’ wanahabari wote waliokuwa wakipita kutoka nje. Ushindi! Hakika ulikuwa ni ushindi wetu sote.

Mwandishi wa makala haya ni  Hafidh Kido ambaye ni Mhariri wa gazeti la Jamvi la  Habari
Viewing all 110130 articles
Browse latest View live




Latest Images