Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

Maofisa 513 wa Idara ya Uhamiaji wapandishwa vyeo

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV

Idara ya Uhamiaji nchini imewapandisha vyeo maafisa 513 katika ngazi mbalimbali wakiwemo Marakibu Waandamizi kuwa Makamishina Wasaidizi wa Idara hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana mara baada ya kuwapandisha vyeo Kamishina wa Utawala na Fedha wa Idara ya Uhamiaji Edward Chogero kwa niaba ya Kamishina Jenerali wa Idara ya Uhamiaji alisema kuwa kupandishwa vyeo ni kufanya kazi katika maeneo yao ya kazi.

Alisema kuwa kupanda kwa vyeo huko sio ndio tiketi ya moja kwa moja kwa moja kwani wanaweza kupanda au hata kushushwa kwa vyeo hivyo.Chogero alisema maafisa hao wamekaa kwa muda mrefu bila kupanda hivyo wengine ambao hawajapanda waendelee kujituma katika kazi.

Pia alisema kuwa Makamishina Wasaidizi wawasimamie waliochini yao.
"Mmepandishwa vyeo lakini vinaweza kushuka kutokana na kutokwepo kwa mabadiliko ya kupanda kwa vyeo kifikra na kiutendaji." Alisema chogero

Alisema kuwa vyeo vinahitaji uwajibikaji wa matokeo chanya katika idara ya Uhamiaji katika utoaji huduma bora kwa Wananchi.Naye Kamishina Msaidizi wa Mkoa wa Dar es Salaam aliyepanda cheo Novaita Mrosso alisema kuwa hawatawaangusha wenzake waliopanda cheo katika utumishi wa Idara hiyo.
Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa Idara ya Uhamiaji Edward Chogero kwa niaba ya Kamishina Jenerali wa Idara ya Uhamiaji akimvisha cheo cha Kamishina Msaidizi James Mwanjotile awali alikuwa na cheo Mrakibu Mwandamizi wa Idara hiyo katika katika Hafla iliyofanyika Ofisi za Makao Makuu ya Idara hiyo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa Idara ya Uhamiaji Edward Chogero kwa niaba ya Kamishina Jenerali wa Idara ya Uhamiaji akiwa katika picha ya pamoja na Makamishina wasaidizi mara baada ya kupanda cheo hicho katika katika Hafla iliyofanyika Ofisi za Makao Makuu ya Idara hiyo jijini Dar es Salaam.
Kamishina wa Utawala na Fedha wa Idara ya Uhamiaji Edward Chogero akizungumza na maafisa wa Idara ya Uhamiaji waliopandiswa Vyeo katika Hafla iliyofanyika Ofisi za Makao Makuu ya Idara hiyo jijini Dar es Salaam.
Kamishina wa Udhibiti wa Mipaka Samuel Mahirane akizungumza katika kuwaasa maofisa wa Idara ya Uhamiaji waliopandiswa Vyeo katika Hafla iliyofanyika Ofisi za Makao Makuu ya Idara hiyo jijini Dar es Salaam.

Kamishina Msaidizi wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam Novaita Mrosso akitoa neon la shukrani kwa niaba ya waliopandishwa vyeo mbalimbali Hafla iliyofanyika Ofisi za Makao Makuu ya Idara hiyo jijini Dar es Salaam

RAIS CYRIL RAMAPHOSA WA AFRIKA KUSINI AWASILI NCHINI KWA ZIARA RASMI YA SIKU MBILI

$
0
0
Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusine na mkewe Dkt. Tshepo Motsepe wakiwasili
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius  Nyerere jijini Dar es
salaam usiku huu. Rais Ramaphosa amewasili kwa ziara rasmi ya siku
mbili nchini kabla ya kuhudhuria Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi
Wanachama za Jumuiya ya Maendeleo  ya Kusini kwa Afrika SADC

 Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusine akipokewa na Waziri wa Mambo ya Nje na 

Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius  Nyerere jijini Dar es salaam usiku huu. Rais Ramaphosa
amewasili kwa ziara rasmi ya siku mbili nchini kabla ya kuhudhuria
Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi Wanachama za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini kwa Afrika SADC

 Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini akipeana mikono  na Mkuu wa Wilaya ya

Ubungo Mhe. Kisare Makori alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius  Nyerere jijini Dar es salaam usiku huu. Wengine
kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo,
Mkuu wa Wiklaya ya Kigamboni Mhe. Mhe. Sarah Misafiri na Mkuu wa
Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema. Rais Ramaphosa amewasili kwa ziara
rasmi ya siku mbili nchini kabla ya kuhudhuria Mkutano wa Viongozi
Wakuu wa Nchi Wanachama za Jumuiya ya Maendeleo  ya Kusini kwa Afrika SADC

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini akipeana mikono  na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius  Nyerere jijini Dar es salaam usiku huu. Kushoto
ni Kamanda wa Kanda Mazlumu ya Kipolisi ya Dar es salaam Lazaro
Mambosasa. Rais Ramaphosa amewasili kwa ziara rasmi ya siku mbili
nchini kabla ya kuhudhuria Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi Wanachama

za Jumuiya ya Maendeleo  ya Kusini kwa Afrika SADC 
 Rais Cyril Ramaphosa akiongozana na Waziri wa Mambo ya Nje na

Ushirikiano wa Afrika Mashariki baada ya kupokewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius  Nyerere jijini Dar es salaam usiku huu. Rais Ramaphosa
amewasili kwa ziara rasmi ya siku mbili nchini kabla ya kuhudhuria
Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi Wanachama za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini kwa Afrika SADC

WAKAGUZI WA MIFUMO YA UZALISHAJI DAWA NA VIFAA TIBA (GMP) KWA NCHI ZA SADC WAPEWA SOMO

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk Zainab Chaula akifungua mafunzo ya wakaguzi wa Mifumo ya uzalishaji Dawa na Vifaa tiba (GMP) kwa nchi wanachama wa SADC ambapo Tanzania ndiyo mwenyeji Wakufunzi wa mafunzo hayo wanatoka Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA),Adam Fimbo.Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Habour View  jijini jijini Dar es salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA),Adam Fimbo akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wakaguzi wa Mifumo ya uzalishaji Dawa na Vifaa tiba (GMP) kwa nchi wanachama wa SADC ambapo Tanzania ndiyo mwenyeji Mafunzo hayo yanafanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Habour View jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk Zainab Chaula akiteta jambo na Mratibu wa Mradi wa SADC Medicines Reguratory Harmonisation Project (SMRHP) Bi. Sakhile Dube Mwedzi(kulia
Mratibu wa Mradi wa SADC Medicines Reguratory Harmonisation Project (SMRHP) Bi. Sakhile Dube Mwedzi(kulia) akizungumza katika uzinduzi wa mafunzo hayo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba TMDA Bi. Gaudensia Simwanza akimkaribisha kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo ili kuzungumza na washiriki wa mafunzo hayo.
Picha ya pamoja
Washiriki wa mafunzo ya wakaguzi wa Mifumo ya uzalishaji Dawa na Vifaa tiba (GMP) kwa nchi wanachama wa SADC ambapo Tanzania ndiyo mwenyeji Wakufunzi wa mafunzo hayo wakimsiliza kwa makini Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk Zainab Chaula.(Picha zote na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

UMOJA WA WAZAZI CCM SHINYANGA WATOA TAMKO KUMPONGEZA RAIS MAGUFULI

$
0
0
Umoja wa wazazi CCM mkoa Shinyanga umetoa tamko la kumpongeza Rais John Magufuli kutokana na kutekeleza ipasavyo ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kutetea haki za wanyonge pamoja na kuiletea nchi mafanikio makubwa ya kimaendeleo.

Tamko la umoja huo wa wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga, limetolewa leo Agosti 14, 2019 kwenye kongamano la umoja huo, ambao limehudhuriwa na wajumbe kutoka wilaya ya Kishapu, Kahama, Shinyanga vijijini, na manispaa ya Shinyanga, ambalo limefanyika kwenye ukumbi wa CCM mkoa, huku mgeni rasmi akiwa mjumbe wa NEC Gaspar Kileo. 

Akisoma tamko hilo, Katibu wa Umoja wa Wazazi mkoa wa Shinyanga Masanja Salu, amesema wanampongeza Rais John Magufuli kwa kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM ipasavyo, ambapo ndani ya miaka minne tangu alipoingia madarakani amefanya mambo makubwa ikiwamo kuiletea nchi maendeleo.

 “Sisi Umoja wa Wazazi mkoa wa Shinyanga tunatoa tamko la kupongeza Rais John Magufuli kwa kutekeleza ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi kwa asilimia 100, ambapo ndani ya miaka yake minne tu akiwa madarakani amefanya mambo makubwa sana katika nchi yetu, hivyo lazima tumpongeze na kumuombea pia,”amesema Salu. 

“Mambo ambayo ameyafanya Rais wetu na anapaswa kupongezwa ni pamoja na kudhibiti mafisadi, rushwa, mishahara hewa, utoroshwaji wa makinikia, upotevu wa mapato, kaboresha mikataba mibovu ya madini, elimu bure, ujenzi wa madaraja, miundombinu ya barabara, reli ,huduma za afya, ununuaji wa ndege, na makazi ya watumishi,”amefafanua Salu. 

Naye mgeni rasmi kwenye kongamano hilo la kumpongeza Rais John Magufuli mjumbe wa halmashauri kuu Taifa mkoani Shinyanga (NEC) Gaspar Kileo, akipokea tamko la pongezi hizo kwa niaba ya Rais Magufuli, ameupongeza umoja huo wa wazazi CCM mkoani humo kwa kutambua kazi kubwa ambayo anaifanya rais Magufuli.

Amesema mbali na pongezi hizo, lakini zawadi pekee ambayo wanapaswa kumpa Rais John Magufuli, ni kumpatia ushindi wa kishindo kwa asilimia 100 kwenye changuzi zote kuanzia serikali za mitaa mwaka huu, pamoja na uchaguzi mkuu ujao mwaka 2020,wapinzani wasiweze kupata hata kiti kimoja cha ushindi waambulie zero.

 Aidha amesema ushindi huo ndiyo itakuwa zawadi kubwa kwa Rais John Magufuli ikisindikiza tamko lao la pongezi, huku akiwataka pia wajitokeze kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura, na kuhamasisha majirani zao, ndugu, jamaa na marafiki, ili waweze kupiga kura na kuipatia ushindi huo mnono CCM. Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga Salum Abdalah Simba akizungumza wakati Umoja huo ukitoa tamko la kumpongeza rais John Pombe Magufuli kwa kutekeleza kikamilifu ilani ya CCM. Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog Katibu wa Umoja wa Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga Masanja Salu akisoma Tamko la umoja wa wazazi mkoa wa Shinyanga la kumpongeza Rais John Magufuli kwa uchapakazi wake wa kutekeleza ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi kwa asilimia 100. Katibu wa Umoja wa wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga Masanja Salu, mkono wa kulia akimkabidhi tamko la kumpongeza Rais John Magufuli, mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa NEC mkoani Shinyanga Gaspar Kileo kwa niaba ya Rais ambapo atamfikishia tamko lao. Kitabu chenye tamko la Umoja wa Wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga la kumpongeza Rais John Magufuli kwa kutekeleza ipasavyo ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Mjumbe wa halmashauri kuu taifa (NEC) Gaspar Kileo akiteta jambo na mwenyekiti wa umoja wa wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga Salum Abdala Simba,kwenye kongamano la kupongeza utendaji kazi wa Rais John Magufuli kwa kutekeleza ilani ya CCM kwa asilimia 100. Mjumbe wa halmashauri kuu Taifa (NEC) Gaspar Kileo, akizungumza mara baada ya kupokea Tamko la umoja wa wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga la kumpongeza Rais John Magufuli kwa kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM kwa asilimia 100 ndani ya miaka minne tu. Mjumbe wa halmashauri kuu Taifa (NEC) Gaspal Kileo, akiwa asa wajumbe wa umoja huo wa wazazi CCM mkoa wa Shinyanga kuwa licha ya pongezi hizo, bali wanatakiwa wampatie zawadi Rais John Magufuli ya ushindi wa kishindo kwenye chaguzi zote kuanzia Serikali za mitaa hadi uchaguzi mkuu ujao mwaka 2020. Mchungaji Elias Madoshi kutoka kanisa la FPCT Shinyanga akipongeza utendaji kazi wa Rais John Magufuli. Shekhe Alhaji Ibrahimu Ramadhani akipongeza utendaji kazi wa Rais John Magufuli. Wajumbe wa Umoja wa wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye Kongamano la kumpongeza Rais John Magufuli la kutekeleza ipasavyo ilani ya uchaguzi ya CCM ndani ya miaka yake Minne akiwa madarakani. Wajumbe wakiwa kwenye Kongamano la kumpongeza Rais John Magufuli. Wajumbe wa umoja wa wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye Kongamano la kumpongeza Rais John Magufuli la kutekeleza ipasavyo ilani ya CCM ndani ya miaka yake Minne akiwa madarakani. Wajumbe wakiwa kwenye Kongamano la kumpongeza Rais John Magufuli. Wajumbe wa umoja wa wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye Kongamano lao la kumpongeza Rais John Magufuli la kutekeleza ipasavyo ilani ya CCM. Wajumbe wakiwa kwenye Kongamano la kumpongeza Rais John Magufuli. Wajumbe wa umoja wa wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye Kongamano lao la kumpongeza Rais John Magufuli la kutekeleza ipasavyo ilani ya CCM. Wajumbe wakiwa kwenye Kongamano la kumpongeza Rais John Magufuli. Wajumbe wa umoja wa wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga wakipiga picha na MNEC Gaspar Kileo mara baada ya kupokea tamko lao la kumpongeza Rais John Magufuli. wajumbe wakiendelea kupiga picha. Wajumbe wa umoja wa wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga wakiserebuka huku wakibeba tamko lao la kumpongeza Rais John Magufuli. Wajumbe wakendelea kuserebuka.Awali mjumbe wa halmashauri kuu Taifa (NEC) Gaspal Kileo mkono wa kulia akiingia ukumbini kwenye Kongamano la umoja wa wazazi CCM mkoa wa Shinyanga la kumpongeza Rais John Magufuli, kushoto ni mwenyekiti wa wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga Salum Abdala Simba. Mjumbe wa halmashauri kuu Taifa (NEC) Gaspar Kileo akiwasili kwenye ukumbi wa CCM Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kupokea Tamko la kumpongeza Rais John Magufuli lililoandaliwa na umoja wa wazazi CCM Mkoani humo, ambapo amepokelewa na viongozi wa umoja huo, huku akiwa ameshikana mkono na katibu wa umoja wa wazazi mkoa wa Shinyanga Masanja Salu. Askofu Josephat Musira wa kanisa la TMRC- Ndembezi Shinyanga mjini, akimwombea Rais John Magufuli, pamoja na makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, na waziri mkuu Kassim Majaliwa na wateule wake wote wakiwamo mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya, Mungu awajalie afya njema na kuendelea kuchapa kazi ya kutumikia wananchi na kuleta maendeleo ya taifa. Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

NIMR YATOA MSAADA MUHIMBILI KWA MAJERUHI WA AJALI YA MOTO WA MAFUTA

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV

Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR) imetoa msaada wa vifaa tiba katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kusaidia majeruhi wa ajali ya Moto wa mafuta iliyotokea Agasti 9 mkoani Morogoro.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Profesa Yunus Mgaya amesema kuwa wameguswa kama taasisi na kuona umuhimu wa kutoa vifaa tiba kwa ajili ya majeruhi hao,

Amesema kuwa wadau wadau wameguswa na janga hilo na kuona umuhimu wa kusaidia vifaa tiba kwa ajili ya wagonjwa kwa wana mahitaji ya ziada katika kuokoa maisha yao.

“Tumetoa msaada kama taasisi katika kuhakikisha tunashiriki kwa pamoja katika kuwasaidia majeruhi waliobaki hospitalini kuweza kupona na kuendelea na majukumu yao ya uzalishaji mali” amesema Mkurugenzi Mkuu wa NIMR Profesa Mgaya.

Katika hatua nyingine Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi na Watu Wenye Ulamavu Jenista Mhagama alitembelea Hospitali ya Taifa kuangalia huduma inayotolewa majeruhi wa ajali ya Moto wa mafuta iliyotokea Agasti 9 mkoani Morogoro.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Profesa Yunus Mgaya akimkabidhi msaada wa vifaa tiba Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Lawrence Museru kwa ajili ya majeruhi wa ajali ya moto wa mafuta uliotekea Agasti 9 mkoani Morogoro.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Koleta Njelekela akikabidhi shemu ya msaada wa Sprite kwa Afisa wa Mapokezi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi na Watu Wenye Ulamavu Jenista Mhagama (katikati) akizungumza wakati alipotembelea wodi ya majeruhi wa ajali ya moto wa mafuta uliotekea Agasti 9 mkoani Morogoro. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Profesa Yunus Mgaya watatu kutoka kushoto ni Dkt. Elisha Osati.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Profesa Yunus Mgaya akisalimiana na Daktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Elisha Osati wakati walipkwenda kuwajulia hali majeruhi wa ajali ya moto wa mafuta uliotekea Agasti 9 mkoani Morogoro
Watendaji wa NIMR wakiwa katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Lawrence Museru 
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Profesa Yunus Mgaya akisaini kitabu cha Wageni Katika Ofisi ya Mkuruenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Lawrence Museru wakati alipokwenda kutoa msaada.
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi na Watu Wenye Ulamavu Jenista Mhagama akisaini kitabu cha Wageni Katika Ofisi ya Mkuruenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Lawrence Museru wakati alipokwenda kuangalia hali za majeruhi wa ajali ya moto wa mafuta uliotekea Agasti 9 mkoani Morogoro.

RC NDIKILO AANZA ZIARA YA VIWANDA 14 AMBAPO 13 ATAWEKA JIWE LA MSINGI NA KIMOJA ATAKIKAGUA

$
0
0

MKUU wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo ameanza ziara ya kutembelea viwanda 14 ikiwa ni sehemu ya viwanda 1,192 vilivyojengwa mkoani humo.

Katika ziara hiyo, mkuu huyo wa mkoa ataweka mawe ya msingi katika viwanda 13 na kimoja atakikagua ujenzi wake.

Hayo yalisemwa mjini Kibaha na Katibu Tawala wa mkoa (RAS) Pwani Theresia Mbando alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya ziara ya kikazi itakayofanywa na mkuu wa mkoa huo.

"Jumla ya viwanda vilivyojengwa kati ya hivyo vikubwa ni 56, vya kati 85, vidogo ni 350 na vidogo sana ni 701 vikiwa vimejengwa kwenye wilaya za mkoa huu".

Akizungumzia juu ya Ziara hiyo anasema kuwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Magufuli la ujenzi wa viwanda ili kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo 2025.

Alisema, viwanda hivyo viko kwenye hatua mbalimbali za ujenzi huku vingine vikiwa vimeanza uzalishaji ambavyo ni Lake Steel, Shafa Investment na Super Meals.

TRC KUCHOCHEA UKUAJI UCHUMI WA NCHI ZA JUMUIYA YA MAENDELEO YA KUSINI MWA AFRIKA - SADC

$
0
0
Shirika la Reli Tanzania – TRC limeonekana kuwa chachu ya kukuza uchumi kwa kuendeleza sekta ya miundombinu ya reli nchini katika maadhimisho ya maoneshoya 4 ya wiki ya viwanda ya jumuiya ya maendeleo ya kusini mwa Afrika - SADC ambayo inajumuisha nchi 16 katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha Julius Nyerere - JNICC jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania – TRC Ndugu Masanja Kungu Kadogosa amesema kuwa ni fursa kubwa kwa TRC kushiriki katika maadhimisho ya SADC kwa kuonesha na kuelezea huduma zitolewazo na maendeleo ya miradi, ambayo ni mradi mkubwa wa ujenzi ya reli ya kisasa - SGR unaoendelea pamoja na uboreshaji wa reli ya kati Dar – Isaka ambapo itasaidia nchi za jirani kupitisha mizigo kirahisi na haraka zaidi.

“SADC ni soko kubwa na ni sehemu muhimu kwa taifa” amesema Ndugu Masanja Kadogosa.

Ndugu Kadogosa alizungumzia mradi mkubwa unaoendeleawa reli ya kisasa – SGR ambao kwa sasa umefikia asilimia 64.4 na kusema kuwa mradi huo umezingatia vitu mbalimbali ikiwemo mapishano ya barabara ya magari na reli, njia za watembea kwa miguu pamoja na wanyama, vilevile kuweka uzio pembezoni mwa reli ili kuepusha madhara yatakayoweza kutokea.

“Reli hii itajengewa uzio kulia na kushoto kwa asilimia mia moja na shughuli za wananchi za kiuchumi na kijamii zitaendelea kama kawaida” alisema Mkurugenzi Ndugu Masanja Kadogosa.

Ndugu Kadogosa alisema kuwa Usafiri wa Reli ambao ni imara utakabiliana na changamoto ya ushindani wa usafirishaji wa bidhaa za ndani na nje, kuleta chachu ya maendeleo katika uzalishaji na kupunguza gharama za usafiri.

“usafiri wa reli ni nafuu zaidi na unapunguzo asilimia 70 mpaka 60” alisema Ndugu Kadogosa.Hata hivyo ndugu Kadogosa alisema kuwa TRC ina mpango mzuri wa kushirikiana na Mamlaka ya Bandari Tanzania kujenga bandari kavu ambayo itasaidia pia nchi jirani ikiwemo Congo kufikisha mizigo ikitokea nchi za nje, na pia shirika la reli limekuwa na juhudi ya kuwa na uhusiano wa karibu na nchi ya Congo kwa kuwa wamekuwa wakishirika vyema katika usafirishaji wa mizigo.


Vilevile Ndugu Kadogosa amewakaribisha mabalozi wa Tanzania kutoka nchi mbalimbali kesho Agosti 15 katika maadhimisho hayo ambapo watapata fursa ya kutembelea na kujua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa – SGR, mradi ambao unatekelezwa kwa fedha za ndani za watanzania, aidha mabalozi hao watafanya ziara kwenye daraja jipya la Salenda linaloendelea pamoja na kuona mradi wa ufuaji umeme wa Mwalimu Julius Nyerere.

LIVE: MAPOKEZI YA RAIS WA AFRIKA KUSINI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM


WAKAZI WA PANDE NA MLINGOTINI WASEMA CHONDE CHONDE WAONANE USO KWA USO NA RAIS.DK.MAGUFULI KUJUA HATMA YA FIDIA ZAO

$
0
0





NA MWAMVUA MWINYI,BAGAMOYO

WAKAZI wa kijiji cha Pande na Mlingotini ,Bagamoyo mkoani Pwani ambao walitakiwa kuhama kupisha mradi wa bandari mpya ya Bagamoyo wamemuangukia Rais dk.John Magufuli aone umuhimu wa kwenda kutoa kauli yake ya mwisho,kuhusu hatma ya fidia zao na eneo wanalopaswa kuhamia.

Wamedai ni zaidi ya miaka saba tangu wafanyiwe tathmini na kuahidiwa watahamishwa eneo jingine lakini imekuwa ni hadithi inayowaacha katika sintofahamu.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti ,juu ya suala hilo wakati mbunge wa jimbo la Bagamoyo, alhaj dk.Shukuru Kawambwa alipofanya ziara yake ya jimbo na kupeleka mrejesho wa kusitishwa kwa ujenzi wa Bandari kavu kwa sasa ,walimueleza wanamtaka Rais na sio mtu mwingine.

Wakazi akiwemo mzee Rajabu Wading’ola na Matata alisema ,serikali ione uchungu ,iangalie nafsi zao zinavyohangaika kwa muda mrefu .

“Ni kama tumesuswa ,hatuna msaada ,eneo hili lilishajengwa shule watoto wetu wanasoma ,kuna msikiti,zahanati, “alieleza Wading’ola.

“Baadhi ya watu walilipwa fidia lakini wengine hawajalipwa huku wengine wakiwa wamepunjwa fidia zao kwa kulipwa kidogo fedha ambazo hazitoshi kununulia maeneo mengine” Matata alisema.

Aidha alitaja changamoto nyingine ni ufugaji holela wa ng’ombe unaofanywa na wamang’ati ambapo mifugo hiyo imekuwa ikila mazao yao huku kukiwa hakuna msaada wowote kisheria.

Kwa upande wake mbunge wa Jimbo la Bagamoyo Dk Shukuru Kawambwa alipokea agizo na malalamiko hayo kutoka kwa wananchi na kudai atalishughulikia kuhakikisha anafanikiwa.

Aliwaambia, serikali imesitisha ujenzi wa Bandari kavu Bagamoyo baada ya kubaini mwekezaji kuweka masharti magumu ya kimkataba na kuonekana kubana maslahi ya watanzania na nchi kijumla.

“Serikali isingeweza kukubali masharti yanayobana uchumi wetu,haiwezekani baada ya ujenzi huo ,Tanzania kutoruhusiwa kujenga na kuendeleza bandari nyingine kuanzia Tanga mpaka Mtwara na pia kushindwa kukusanya kodi katika bandari hiyo, “:-kutokana na masharti hayo serikali isingeweza kukaa kimya “,serikali inajua changamoto mliyonayo na inafanyia kazi” 

Kawambwa alifafanua, kijiji cha Pande kina kaya 2,200 sawa na watu 16,500 ambao walitakiwa kuhama eneo hilo.

Alisema, jambo hilo limekuwa ni changamoto kubwa ,wananchi hawamuelewi hivyo kuna haja ya suala hilo kufikia mwisho.

SPIKA NDUGAI AONGOZA KAMATI YA FEDHA NA MIPANGO, KAMATI YA SIASA ZIARA YA KIKAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA MANYONI

$
0
0
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akiangalia mkorosho uliopandwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Rehema Nchimbi tarehe 18 Januari, 2018 wakati alipotembela Shamba la korosho lilipo katika kijiji cha Masigati Wilayani Manyoni Mkoani Singida. Spika Ndugai alioongoza kamati ya Fedha na Mipango na Kamati ya siasa ya halmshauri ya Wilaya ya kongwa kwa ajili ya kujifunza na kubadilishana uzoefu na Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni tukio lililofanyika leo Wilayani Manyoni Mkoani Singida.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akimsikiliza Bwana Nyuki, Ndg. Ramia Konyo wakati alipotembelea kiwanda cha asali kilichopo Wilayani Manyoni Mkoani Singida. Spika Ndugai yuko Wilayani Manyoni kwa ziara ya kikazi ya siku moja
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akipokea zawadi ya asali kutoka kwa Bwana Nyuki, Ndg. Ramia Konyo (kushoto) wakati alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Wilayani Manyoni Mkoani Singida. Kulia ni Mbunge wa Manyoni Mashariki, Mhe. Daniel Mtuka.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (kulia) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Mhe. Rahabu Mwagisa wakati alipowasili katika Ofisi ya Wilayani hiyo katika ziara ya kikazi ya siku moja Manyoni Mkoani Singida. Kushoto ni Mbunge wa Manyoni Mashariki, Mhe. Daniel Mtuka na Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe. Deogratius Ndejembi (wa pili kushoto)
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa pili kushoto) akisalimiana na Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni wakati alipowasili kwa ziara ya kikazi ya siku moja Wilayani Manyoni Mkoani Singida. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Mhe. Rahabu Mwagisa na kushoto ni Mbunge wa Manyoni Mashariki, Mhe. Daniel Mtuka
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni na kamati ya Fedha na Mipango na kamati ya siasa ya halmshauri ya Wilaya ya kongwa kabla ya ziara ya kikazi ya siku moja Manyoni Mkoani Singida. Kulia kwake ni Mbunge wa Manyoni Mashariki, Mhe. Daniel Mtuka
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa pili kulia) akimsikiliza Msimamizi wa Mradi wa korosho Wilaya ya Manyoni, Ndg. Paul Lenjima wakati alipotembelea Shamba lililopo katika kijiji cha Mkwese Wilayani Manyoni Mkoani Singida. Spika Ndugai alioongoza kamati ya Fedha na Mipango na Kamati ya siasa ya halmshauri ya Wilaya ya kongwa katika ziara ya kikazi ya siku moja kwa ajili ya kujifunza na kubadilishana uzoefu, Kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Mhe. Rahabu Mwagisa, Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe. Deogratius Ndejembi (kulia kwake) na Mbunge wa Manyoni Mashariki, Mhe. Daniel Mtuka (mwenye kofia ya CCM)
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (mwenye kofia) akiangalia Shamba lililopo katika kijiji cha Masigati Manyoni Mkoani Singida. Spika Ndugai alioongoza kamati ya Fedha na Mipango na Kamati ya siasa ya halmshauri ya Wilaya ya kongwa katika ziara ya kikazi ya siku moja kwa ajili ya kujifunza na kubadilishana uzoefu

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

RAIS DKT MAGUFULI AMPOKEA MGENI WAKE RAIS RAMAPHOSA IKULU JIJINI DAR LEO.

$
0
0
President Cyril Ramaphosa and Spouse Dr Tshepo Motsepe arrive at the State House received by President of the United Republic of Tanzania, President John Pombe Magufuli for the State Visit held today, 15 August 2019, in Dar es Salaam in the United Republic of Tanzania. 

This is the first State Visit by President Ramaphosa since assuming office in May 2019. The visit will allow the two leaders to discuss bilateral, continental and global issues, and to reaffirm their commitment to further cooperate closely on multilateral issues between the two countries.

South Africa and Tanzania enjoy strong fraternal, historical as well as excellent political, economic and social relations which were cemented during the period of the liberation struggle. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akizungumza jambo na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mh. Cyril Ramaphosa,mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam leo.Rais Ramaphosa amewasili hapa nchini jana jioni kwa Ziara ya Kitaifa ya siku 3 na baada ya hapo atahudhuria Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika Jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwakaribisha wageni wao Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mh. Cyril Ramaphosa na mkewe Dkt. Dk Tshepo Motsepe, Ikulu Jijini Dar es Salaam leo. Rais Ramaphosa amewasili hapa nchini jana jioni kwa Ziara ya Kitaifa ya siku 3 na baada ya hapo atahudhuria Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika Jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mh. Cyril Ramaphosa na mkewe Dkt. Tshepo Motsepe wakikabidhiwa maua ikiwa ni ishara ya upendo ya kuwakaribisha nchini,mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar na kupokewa na Rais Dkt John Pome Magufuli .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama pamoja na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mh. Cyril Ramaphosa wakati nyimbo za Mataifa hayo mawili zikipigwa katika hafla fupi ya mapokezi kwenye viunga vya Ikulu leo jijini Dar.
Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mh. Cyril Ramaphosa akikagua gwaride la heshima mara baada ya kuwasili katika viunga vya Ikulu,leo jijini Dar .

Vodacom ilivyoshiriki maonesho ya Nane nane mkoani simiyu na jijini Arusha

$
0
0


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akimkabidhi tuzo Mkuu wa mauzo wa kanda ya Kaskazini wa Vodacom Tanzania, Brigita Stephen baada ya kampuni hiyo kuibuka mshindi wa kampuni bora upande wa mawasiliano kanda ya kaskazini katika maonyesho ya Nane Nane yaliyofanyika jijini Arusha, hivi karibuni, kushoto kwa Ulega ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (mwenye kofia). Kampuni ya Vodacom Tanzania inaendelea kuboresha huduma zake kuwa za kidijitali ili kuwawezesha Watanzania kwenda sambamba na maendeleo ya ulimwengu.
Mtaalamu wa mauzo wa Vodacom Tanzania Mandela Seth, akiwapa maelezo ya kutumia kifaa cha intaneti (modem) wateja waliotembelea banda la Vodacom katika viwanja vya nane nane Nyakabindi mkoani Simiyu hapo jana. katika maonyesho ya nane nane mwaka huu kampuni ya Vodacom imewandalia wateja wao huduma za kidigatili ikiwemo vifaa mbali mbali vya intaneti na simu.
Wakazi wa Bariadi mkoani Simiyu wakipatiwa huduma mbalimbali kwenye banda la Vodacom katika viwanja vya nane nane Nyakabindi mkoani Simiyu hapo jana. katika maonyesho ya nane nane mwaka huu kampuni ya Vodacom imewandalia wateja wao huduma za kidigatili ikiwemo vifaa mbali mbali vya intaneti na simu.

Waitara awakumbusha Wakurugenzi kutekeleza maelekezo ya kununua zana za kufundishia watoto wa madarasa ya awali

$
0
0
Naibu Waziri Tamisemi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Mwita Waitara amewakumbusha Wakurugenzi kutekeleza maelekezo ya kununua zana za kufundishia kwa watoto wa madarasa ya awali ili waweze kujifunza kwa vitendo na kukuza ubongo wao.

Waitara alisema kuwa, zana hizo ni muhimu na kwamba zinamsaidia mtoto kujifunza kwa njia rahisi na salama na kumuongezea uelewa katika elimu ya malezi na makuzi.

Alisema tayari serikali ilishatoa maelekezo kwa wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanatenga fedha kwa ajili ya kununua zana za kufundishi kwa wanafunzi wa madarasa ya awali, kwa sababu zina hizo zinasaidia kupanua uelewa wa watoto katika masuala ya elimu, malezi na makuzi.

"Tayari tumeshatoa maelekezo kwa wakurugenzi wote nchini kuhakikisha wanatenga fedha kwa ajili ya kununua vifaa vya elimu changamshi kwa madarasa ya awali ili waweze kupata elimu bora ya malezi na makuzi," alisema Waitara.

Anaongeza kuwa Mtoto anapotumia zana za kujifunzia kuanzia darasa la awali, anaelewa zaidi kuliko yule ambaye hajatumia kabisa, hivyo basi wakurugenzi wanapaswa kuhakikisha kuwa, zana hizo zinakuwepo ili watoto waweze kupata elimu bora.

Aliongeza kuwa,elimu bora inaanzia darasa la awali, kwa wanafunzi kuwa na vifaa vya kujifunzia hali ambayo imewafanya kutoa maelekezo hayo ili kuhakikisha wanaboresha utoaji wa elimu nchini.

Alisema kutokana na hali hiyo,serikali utaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali nchini ili kuhakikisha kuwa, elimu inayotolewa inakidhi viwango, hali ambayo itasaidia wanafunzi wanaomaliza kuingia kwenye soko la ushindani la ajira.

Kwa mujibu wa mwongozo uliotolewa na Taasisi ya Elimu Tanzania wa mwaka 2016, ulibainisha baadhi ya zana zinazohitajika katika madarasa la awali ambazo ni pamoja na kibao fumbo, bao, karata, dadu, domino, chati ya mchezo wa ngazi na nyoka, drafti, vihesabio na midoli, kadi za herufi, kadi za namba, kadi za picha, vipande vya mbao, kanda za video, runinga, redio.

Baadhi ya picha za kutengeneza zinazofaa kufundishwa kwa watoto wa madarasa ya awali

TUTAIMARISHA BIASHARA ZA MAZAO KATIKA NCHI YA SADC-WAZIRI HASUNGA

$
0
0
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb)


Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam

Serikali imesema kuwa imejipanga kuimarisha biashara ya mazao ya Kilimo na mengineyo kwa nchi wanachama wa SADC ili kuwanufaisha wakulima katika nchi hizo.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo Leo tarehe 15 Agosti 2019 wakati akizungumza Mubashara (Live) kwenye kipindi cha Clouds 360 kilichorushwa na Clouds TV wakati wa mkutano wa 39 wa wakuu wa nchi 16 wanachama wa SADC katika ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Center.

Amesema kuwa zaidi ya watanzania Milioni 50 nchini wanategemea chakula hivyo lazima kubadili mbinu za uzalishaji katika mazao ya kilimo kwa kuongeza tija kupitia teknolojia mpya ili kuwa na uzalishaji mkubwa na wenye tija.

Mhe Hasunga alisema kuwa Malighafi zinazohitajika zaidi ya Asilimia 66 zinatokana na mazao ya Kilimo hivyo ukamilisho wa serikali ya viwanda unaungwanishwa kwa ukaribu na sekta ya kilimo.

Waziri huyo wa Kilimo Mhe Hasunga, alisema Mkutano wa SADC ni fursa kwa wakulima wa Tanzania kwa kuwa wageni wote waliowasili na watakaoendelea kuwasili watahitaji kula vizuri hivyo mkutano huo ni sehemu ya kuimarisha na kutangaza masoko ya mazao mbalimbali hususani vyakula vya asili.

Aidha, Utoshelevu wa chakula nchini ni asilimia 119 ukilinganisha na mwaka jana ambapo ilikuwa asilimia 124 hivyo serikali imefungua mipaka ya kuuza mazao nje ya nchi lakini pia ni lazima kuwa na kumbukumbu muhimu za taarifa zote za usafirishaji wa mazao.

Mhe Hasunga alisema kuwa ni wakati wa nchi za Afrika Mashariki na nchi zote za SADC kuanza kutumia masoko ya ndani ya nchi katika mazao ya Kilimo na mengineyo kuliko kutegemea kuagiza katika nchi zingine nje ya Afrika.

Alisema kuwa kufanya hivyo kutaimarisha masoko ya mazao mbalimbali nchini hivyo kuwaimarisha wakulima katika Kilimo chao na kuwa na kipato kikubwa kinachokidhi mahitaji ya kula mkulima ikiwa ni pamoja na uimara wa ucumi wa nchi.

WANAWAKE 7,648 WAKEKETWA MKOANI SINGIDA

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi wa utetezi dhidi ya mila potovu na udhalilishaji wa kijinsia uliofanyika wilayani humo mkoani Singida juzi. Mradi huo unasimamiwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Save Children for Central Tanzania (SMZZT). Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Evalyen Lyimo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la Kiserikali la Save Mother and Children for Central Tanzania (SMZZT)Evalyen Lyimo akitoa taarifa ya utendaji katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa utetezi dhidi ya mila potovu na udhalilishaji wa kijinsia uliofanyika wilayani Ikungi mkoaniSingida juzi. Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hiyo, Haika Massawe na Mkuu wa Wilaya hiyo, Edward Mpogolo.

Na Dotto Mwaibale, Singida

JUMLA ya wanawake na watoto 7, 648 katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida wamekeketwa katika kipindi cha kuanzia mwaka 2016 na 2018 imefahamika.

Hayo yalielezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilokuwa la kiserikali la Save the Mother and Children of Central Tanzania (SMCCT), Evalyene Lyimo katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa utetezi dhidi ya mila potofu ya ukeketaji na udhalilishaji uliofanyika hivi karibuni wilayani Ikungi mkoani hapa.

“Kuanzia Januari hadi mwezi Oktoba 2018 jumla ya wanafunzi 37 wa Shule ya Sekondari wilayani humo walibainika kuwa na mimba huku wanawake na watoto 7,648 wakiwa wamekeketwa katika kipindi cha mwaka 2016 hadi 2018” alisema Lyimo.

Akizungumzia mradi huo Lyimo alisema ulianza mwaka 2017 hadi mwaka jana na kuwa katika kipindi hicho umetoa elimu juu ya madhara yatokanayo na mila potofu na udhalilishaji wa kijinsia kwa wakazi wapatao 15,000.

Akichangia jambo katika hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo aliwata viongozi wa madhehebu ya dini na mangariba wastaafu kushiriki kikamilifu vita dhidi ya vitendo hivyo.

Alisema utekelezaji wa masuala ya mila kwa mambo ya maendeleo ni jambo jema lakini inapokuwa kinyume kama masuala hayo ya ukeketaji inakuwa ni changamoto kubwa kwa jamii pia ni kinyume na haki za binadamu.

“Tuna taarifa kuwa ukeketaji wa sasa wanafanyiwa watoto wadogo na wachanga ambao hawawezi kukataa au kujihami na vitendo hivyo serikali haitaweza kuvumilia kuona vikiendelea na mtu yeyote atakaye baanika anavifanya atachukuliwa hatua kali” alisema Mpogolo.

SANGARA WANUFAIKA NA MRADI WA MAJI

$
0
0
Mkurugenzi wa shirika la WaterAid Tanzania, Abel Dugange akizungumza kwenye uzinduzi huo wa mradi wa maji Sangara.
Mkuu wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, Elizabeth Kitundu akipiga (katikati) makofi baada ya kumtwisha ndoo ya maji kichwani mama wa Kijiji cha Sangara Kata ya Riroda.
Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini Vrajilal Jituson akielezea namna mfumo wa utiaji maji kwenye mradi huo.
Mkurugenzi wa operesheni wa shirika la Habitat for Humanity, Cyrus Watuku akizungumza na waandishi wa habari kwenye uzinduzi huo.

……………….

WANANCHI 650 wa Kijiji cha Sangara Kata ya Riroda Wilayani Babati Mkoani Manyara, waliokuwa na changamoto ya ukosefu wa maji, wameondokana na kero hiyo baada ya mradi wa maji wa gharama ya sh229 milioni kuzinduliwa. 

Mradi huo wa wenye miundombiu ya kilomita 3.4 unaotoa maji lita 352,800 kwa siku sawa na lita 14,700 kwa saa, unatumia mfumo wa malipo kabla ya huduma kwa njia ya elekrtoniki.

Mkurugenzi wa shirika la WaterAid Tanzania, Abel Dugange akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi huo alisema waliingia makubaliano ya kutekeleza mradi huo mwaka jana na Halmashauri ya wilaya ya Babati, shirika la Habitat for Humanity, kampuni ya eWater na taasisi ya fedha ya Unit Trust of Tanzania (UTT-MFI).

Dugange alisema kabla ya kutekeleza mradi huo hali ya upatikanaji wa maji kwenye kijiji hicho ilikuwa asilimia 20 tofauti na lengo la Taifa la asilimia 85 ya huduma za maji vijijini.

“Mradi huu umelenga kuhamasisha ubunifu na kuvutia sekta binafsi kuwekeza katika ujenzi wa miundombinu na uendeshaji wa miradi ya maji ili kurahisisha upatikanaji wa huduma endelevu na hakika ya maji safi na salama vijijini,” alisema.

Mkuu wa wilaya ya Babati, Elizabeth Kitundu akizindua mradi huo kwa niaba ya mkuu wa mkoa huo Alexander Mnyeti aliwataka wakazi wa eneo hilo kuutunza ili uwe endelevu. Kitundu alisema lengo la serikali ni ifikapo mwaka 2020 asilimia 85 ya waliopo vijijini wawe wamepata maji safi na salama na mwaka 2025 iwe asilimia 95 na mwaka 2030 iwe asilimia 100.

Mbunge wa jimbo la Babati Vijijini, Vrajilal Jituson alisema mradi huo ni wa mfano kwani umeanzia Babati kisha wilaya za Korogwe mkoani Tanga na Arumeru mkoani Arusha zikafuata.

Jituson alisema mchotaji anaokoa muda kwani anaweza chota hata usiku na hauhitaji muuzaji wa maji kuwepo katika kituo.“Inaongeza usalama wa fedha kutopotea inayotokana na huduma ya maji, imeongeza nidhamu ya matumizi ya maji na hata tone moja linalipiwa,” alisema Jituson.

Mkazi wa kijiji hicho Magdalena Bayo alisema awali walikuwa wanachota maji umbali mrefu kwenye visima na makorongo ila mradi huu umewasaidia kwani upo karibu nao. 

“Mradi ni mzuri yaani kama vocha ya simu unaingiza tokeni maji yanatoka kadiri unavyolipia ndivyo unavyopata maji na hatutembei umbali mrefu kama awali unaamka alfajiri unapambana na foleni,” alisema.

ASKOFU ATAKA RAIS MAGUFULI AENDELEE KUUNGWA MKONO

$
0
0
Na Dotto Mwaibale, Singida

ASKOFU mstaafu wa Kanisa la Pentekoste (FPCT) la Singida Kati, Dkt.Paul Samwel (pichani) amewahimiza Watanzania kuunga jitihada zinazofanywa na Rais Dkt.John Magufuli za kuiletea nchi maendeleo.

Aliyasema hayo hivi karibuni katika hafla ya makabidhiano ya kituo cha kupima uoni na usikivu kwa wanafunzi wa shule za sekondari na msingi ziliopo mkoani hapa ambapo kituo hicho kimewekwa Shule ya Msingi Mahembe kikisimamiwa na kanisa hilo chini ya mradi wa elimu jumuishi.

Askofu Samuel alisema ana uhakika kuwa kila mtanzania mwenye mapenzi mema na uzalendo ni lazima ataziunga mkono jitihada za Rais Dkt.John Magufuli za kutuletea maendeleo nchini.

"Rais Magufuli alipoingia madarakani alianza kwa kusema Tanzania sio nchi maskini lakini baadhi yetu hatukumuelewa lakini baada ya muda mfupi tuliona miradi mikubwa ya maendeleo ikianza kufanyika ikiwa ni pamoja na kununuliwa kwa ndege kubwa za kisasa tena kwa fedha taslimu" alisema Dkt.Samwel.

Alisema pamoja na miradi hiyo kuendelea kujengwa hatujawahi kusikia malalamiko ya wakandarasi kukosa pesa za malipo baada ya kukamilika kwa miradi hiyo na kuwa sasa hivi ile tabia ya nchi kuwa ombaomba imebaki kuwa ni historia.

Mgeni rasmi wa hafla hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Omari Kissuda alilshukuru kanisa hilo kwa msaada huo na kueleza utasaidia ufaulu kwa wanafunzi hao.

Afisa Tawala wa mradi huo, Karistoni Mwenda alisema ukarabati wa kituo hicho kuanzia chumba cha upimaji na vifaa vyake na ujenzi wa ngazi mterezo umegharimu sh.milioni 7.6 ambapo aliiomba Manispaa ya Singida kusaidia kuweka kiyoyozi kwenye chumba cha upimaji.

Mwenda alisema mradi huo umefadhiliwa na Shirika la misaada la Denmark (DANIDA) kupitia shirka la misaada la Danish Mission Council Development (DMCDD) likishirikiana na International Aid Service (IAS).

RC Wangabo apania kufufua kasi vyama vya ushirika kuimarisha uchumi wa wananchi Rukwa

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amevitaka vyama vya ushirika katika Mkoa wa Rukwa kujiunga na chama kikuu cha Ushirika cha Mkoa ili kuwa na umoja na nguvu katika kutafuta masoko ya mazao yao, kuachana na walanguzi, kulima kwa tija na kuzalisha mazao bora kwa kupata pembejeo kwa wakati na hatimae kufanya kazi kwa karibu na wataalamu wa kilimo waliomo ndani ya mkoa.

Amesema kuwa chama kikuu cha Ushirika cha Mkoa Ufipa Cooperative Union Ltd (UCU) ni chama kipya na kinahitahi nguvu ya vyama vya ushirika vya mkoa mzima ili kiwe na uongozi uliokamilika, kiweze kufanya kazi kwa ufanisi na kuweza kumnyanyua mkulima wa mkoa wa Rukwa kutoka alipo sasa na kuwa wakulima wa hadhi ya kimataifa.

“Mkulima ana mahangaiko makubwa sana, sasa huu ushirika ni chombo cha kumkomboa mkulima, ni chombo cha kunyanyua uchumi wa mkulima, ni chombo cha kuikomboa Rukwa, ni chombo cha kuikomboa nchi yetu ya Tanzania, nchi ambayo sasa inaelekea kwenye uchumi wa kati wa viwanda, sasa ushirika ni kitovu cha uzalishaji n ani kitovu cha viwanda, sasa kila tunachokifanya tuchote kwenye ngazi ya mkulima, lazima tujue namba moja kwenye viwanda ni uzalishaji na malighafi za kilimo zinatokana na wakulima, ni lazima azalishe na akizalisha zaidi tutakuwa na viwanda endelevu kutokana na uzalishaji mwingi” Alisisitiza

Ameongeza kuwa hali ya hewa ya mkoa wa Rukwa ni sawa na hali ya hewa za mikoa yote ya nyanda za juu kusini ambayo mikoa hiyo inaongoza kwa kulima matunda na mbogamboga na hivyo kuwa na mazao mengi mbadala kuliko kutegemea mahindi ambapo soko linaposhuka na wananchi wanakosa pa kukimbilia na hivyo kuwataka wajitafakari kutoka katika kilimo cha kutegemea mahindi na hatimae kuanza kulima mbogamboga na matunda ya kutosha kwaajili ya matumizi ya wana-Rukwa ili kupunguza udumavu pamoja na kuuza nje ya mikoa na hatimae nje ya nchi.

Mh. Wangabo ameyasema hayo katika Mkutano wa Vyama vya ushirika Mkoani humo aliouitisha ili kuwatafutia wanachama wapya chama kikuu cha Ushirika cha Mkoa pamoja na kusikia mipango yao waliyojiwekea kuanzia wa mawaka mmoja hadi miaka kumi katika kuelekea Tanzania ya uchumi wa kati chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Akitoa taarifa fupi ya hali ya vyama vya ushirika Kaimu Mrajisi vyama vya Ushirika wa mkoa wa mkoa wa Rukwa Anosisye Mbetwa amesema kuwa miongoni mwa mafanikio ya mkoa ni kuanzisha chama cha kikuu cha ushirika (UCU) ambacho kimesajiliwa tarehe 9.1.2019 kikiwa na wanachama 58 na kwa ujumla hadi kufikia tarhe 31.6.2019 mkoa umeweza kutoa mikopo yenye thamani ya Shilingi 17,781,678,000/=.

“Vyama vya Ushirika 81 vimeweza kukaguliwa na shirika la Ukaguzi la vyama vya Ushirika nchini (COASCO) na kuhusu masoko kwa mwaka 2018/2019 soko la Serikali kwa maana ya NFRA liliwezesha upatikanaji wa shilingi 3,010,467,520/= kwaajili ya ununuzi wa mazao ya wakulima kupitia vyama vya Ushirika vya msingi,” Alisema.

Akielezea mpango wa Miaka 10 ya Chama kikuu cha Ushirika Mkoani Rukwa Makamu Mwenyekiti wa UCU Gaspar Chipeta amesema kuwa lengo kuu la chama hicho ni kuwaleta pamoja wakulima wa mkoa wa huo, kuwa na sauti moja, kutambua mahitaji ya pembejeo kwa kila mkulima kupitia vyama vya msingi pamoja na kutafuta soko lenye bei nzuri ili kuweza kuinua uchumi wa wakulima.

“Mkakati mwingi ni kuhakikisha ndani ya hii miaka kumi kuna matokeo ya uboreshwaji wa miundombinu inayotumika katika kilimo, asilimia kubwa ya wakulima katika mkoa wa Rukwa hawatumii miundombinu ya kisasa, kama ulivyosema awali kwamab lazima twende kwenye kilimo cha kisasa, sisi kama chama kikuu tunataka walau kila chama cha ushirika cha msingi, Kila AMCOS iweze kumiliki walau Trekta ambalo litaweza kuwasaidia wakulima wa vyama hivyo,” Alisema.

Kwa upande wake Meneja wa kanda ya Sumbawanga Wakala wa Taifa wa Hiafadhi ya Chakula (NFRA) Abdillah Nyangasa ametahadharisha wakulima wengi wamekuwa wakilima eneo kubwa lakini mazao yanayopelekwa sokoni hayafanani na viwango na hivyo kuwataka kuzingatia ubora wa mazao katika hatua ya mwisho ambayo inapelekwa kwa mlaji, hali ambayo ipo katika mazao mengi yanayolimwa katika Mkoa.

“ Eneo la Ubora baada ya mavuno ni la msingi mno katika kupata soko zuri, wakati mwingine unaweza kuwa umevuna vizuri lakini unaleta mahindi yako sokoni utaambiwa pepeta, utaambiwa pembua mahindi yaliyooza, ondoa punji zilizoharibika na wadudu, ile ni hatua ya ziada mabayo uneifanya mwenyewe kwenye ngazi ya kaya na kwenye hatua ya chama cha msingi, tukazane kuhakikisha mazao yetu tunayaandaa vizuri kwaajili ya soko ili kupunguza gharama zisizo za lazima,” Alifafanua.

Mkoa wa Rukwa una jumla ya vyama vya Ushirika 172, kati ya hivyo 87 ni vyama vya ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS), 74 ni vyama vya Mazao na Masoko (AMCOS), 4 vyama vya Uvuvi, 3 vyama vya Wafugaji, 1 chama cha Wafuga Nyuki, 3 vyama vya wauza Bidhaa/huduma na Chama Kikuu cha Ushirika kimoja vyenye jumla ya wanachama 19,321.
Baadhi ya Wanachama wa vyama Mbalimbali vya Ushirika Mkoani Rukwa wakisikiliza Nasaha za Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (hayupo Pichani) katika Mkutano Ulioitishwa na Mkuu huyo wa Mkoa kwa lengo la kuwaunganisha wakulima pamoja kupitia chama Kikuu cha Ushirika cha Mkoa. 

RAIS MSTAAFU BENJAMINI MKAPA AONGOZA MHADHARA WA SADC JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamini William Mkapa akihutubia katika mhadhara uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) uliokuwa ukizungumzia historia ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), mapema leo Agosti 15, 2019.  Majaji wastaafu wakiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Bashiru Ali (picha ya juu Kulia) waliohudhuri mhadhara wa uliongoongozwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamini Wiliam Mkapa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) uliokuwa ukizungumzia maendeleo ya nchi za Jumuiya za Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) mapema leo Agosti 15, 2019.
Katibu Mkuu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Dkt. Stagomena Tax akizungumza katika mhadahara uliokuwa ukielezea historia na jinsi SADC ilivyoweza kusonga mbele, mapema leo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
 Mabalozi, Mawaziri na viongozi wa nchi mbali mbali waliohudhuria Mhadhara huo. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe aliyemuwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof Palamagamba Kabudi akitoa machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Rais Mstaafu Mkapa.

 Salamu za hapa na pale...
Wimbo wa Taifa ukiimbwa...
Wageni waalikwa.
Meza kuu.

Vodacom yadhamini mkutano wa 39 wa SADC

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, akisalimiana na Meneja Masoko wa kampuni ya Vodacom Tanzania Noel Mazoya, alipotembelea banda lao katika maonyesho ya nne ya Viwanda ya Jumuiya ya nchi za kusini mwa Afrika (SADC), yaliyofunguliwa rasmi jijini Dar es Salaam. Kampuni ya Vodacom Tanzania ni miongoni mwa wadhamini wa maonyesho hayo, ikiwa ni jitihada ya kuhakisha wageni wote wanapata huduma ya mawasiliano na mtandao wa uhakika. Wakwanza kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano Vodacom Tanzania Jacqueline Materu
Naibu waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Mhandisi Stella M. Manyanya akisoma ripoti ya uwekezaji katika maendeleo ya watu na mpango mpya ya Vodacom Tanzania Foundation, aliyenaye ni Meneja Mahusiano wa kampuni ya Vodacom Tanzania, Alex Bitekeye, katika banda lao kwenye mkutano wa 39 wa SADC , jijini Dar es salaam, hivi karibuni. Katika mkutano huo kampuni ya Vodacom Tanzania imedhamini upande wa mawasiliano ikiwa ni jitihada ya kuhakisha wageni wote wanapata huduma ya mawasiliano na mtandao wa uhakika.
Naibu waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Mhandisi Stella M. Manyanya akisikiliza huduma mbali mbali zitolewazo na kampuni ya Vodacom Tanzania kutoka kwa Meneja Mahusiano wa kampuni hiyo, Alex Bitekeye, katika banda lao kwenye mkutano wa 39 wa SADC , jijini Dar es salaam, hivi karibuni. Katika mkutano huo kampuni ya Vodacom Tanzania imedhamini upande wa mawasiliano ikiwa ni jitihada ya kuhakisha wageni wote wanapata huduma ya mawasiliano na mtandao wa uhakika.
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images