Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110078 articles
Browse latest View live

CCM KARATU YAIBUA MAZITO MRADI ULIOSIMAMA MIAKA 12

$
0
0
Kamati ya Siasa ya Wilaya kama inavyoonekana pichani,ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Wilaya ya Karatu Lucian Akonay ,Katibu wa Chama Shaban Mrisho,Katibu Mwenezi pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Karatu Bi.Theresia Mahongo.
Picha ya Zahanati.
Kamati ya Siasa ya Wilaya ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho wakikagua zahanati hiyo.


Na.Vero Ignatus,Arusha.

Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Karatu kimefanya ziara yake na kubaini miradi iliyosimama bila kutekelezwa kwa muda na kusababisha adha kwa wananchi ikiwemo mradi wa zahanati ya kijiji cha ambayo imesimama kwa miaka 12 tangu ilipojengwa bila kukamilika .

Kamati ya Siasa ya Wilaya ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Wilaya ya Karatu Lucian Akonay ,Katibu wa Chama Shaban Mrisho,Katibu Mwenezi pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Karatu Bi.Theresia Mahongo.

Mwenyekiti wa Ccm wilaya ya Karatu Lucian Akonay ameitaka serikali kuharakisha kumalizia zahanati hiyo kwani kukosekana kwa huduma hiyo kunawanyima haki ya matibabu wananchi hivyo amewaonya watendaji wanaolega lega kuchukua hatua kukamilisha mradi huo.

Aidha amewataka Watendaji kukamilisha mradi huo kabla ya mwaka huu kuisha ili wananchi waweze kupata huduma kwa karibu.Mkuu wa Wilaya ya Karatu Theresia Mahongo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Karatu Waziri Morris wamesema kuwa juhudi za kumalizia kituo hicho zinaendelea ili kwa mwaka wa fedha 2019/20 waweze kukamilisha wakishirikiana na nguvu za wananchi.

Hata hivyo Katibu wa Ccm wilaya hiyo Shaban Mrisho amemuomba Raisi Magufuli kuwachukulia hatua waliofanya ufisadi na kukifilisi kiwanda cha maziwa cha Ayalabe kwani kwa kufanya hivyo wanahujuma juhudi za kufukia uchumi wa viwanda na uchumi wa kati.

Rais Magufuli amuomba Rais Ramaphosa kuongeza uwekezaji Tanzania

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemuomba Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Mhe. Matamela Cyril Ramaphosa kuwahamasisha zaidi wafanyabiashara wa Afrika Kusini kuja kuwekeza hapa nchini kwa kuwa Tanzania inayo dhamira ya dhati ya kuongeza ushirikiano wake na nchi hiyo katika nyanja mbalimbali za kiuchumi.

Mhe. Rais Magufuli amesema hayo leo tarehe 15 Agosti, 2019 Ikulu Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wananchi kupitia vyombo vya habari muda mfupi baada ya kufanya mazungumzo na Mhe. Rais Ramaphosa ambaye amewasili hapa nchini jana jioni kwa Ziara ya Kitaifa ya siku 3 na baadaye kuhudhuria Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika Jijini Dar es Salaam.


Katika mazungumzo hayo yaliyotanguliwa na mapokezi rasmi yaliyofanyika katika viwanja vya Ikulu, Mhe. Rais Magufuli amesema katika kutekeleza mipango yake ya maendeleo na dira ya kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 Tanzania inawakaribisha wawekezaji mbalimbali, na kwa kuwa Afrika Kusini imepiga hatua kubwa katika viwanda amewaalika wafanyabiashara wa nchi hiyo kuja kujenga viwanda vya kuzalisha bidhaa mbalimbali zikiwemo dawa na vifaa tiba, kuchakata madini na kwamba Serikali itatoa ushirikiano wowote utakaohitajika.


Mhe. Rais Magufuli pia amemuomba Mhe. Rais Ramaphosa kuongeza ushirikiano na Tanzania katika utalii, hasa ikizingatiwa nchi hiyo inapokea watalii zaidi ya Milioni 10 kwa mwaka ikilinganishwa na Watalii Milioni 1.5 wanaoingia hapa nchini, na katika hilo ametoa wito kwa Afrika Kusini kuongeza safari za treni ya watalii na kwa wawekezaji wake kuja kuwekeza katika hoteli na fukwe za Tanzania.


Kwa upande wa biashara, Mhe. Rais Magufuli amesema Afrika Kusini ni nchi inayoongoza kwa kufanya biashara na Tanzania ikilinganishwa na nchi nyingine za SADC ambapo asilimia 70 ya bidhaa za Tanzania zinazokwenda SADC huenda Afrika Kusini na kwamba biashara kati ya Tanzania na Afrika Kusini imeendelea kukua ambapo katika mwaka 2018 ilikuwa na thamani ya shilingi Trilioni 2 na Bilioni 687 ikilinganishwa na mwaka 2017 ilipokuwa na thamani ya shilingi Trilioni 2 na Bilioni 528.


Amempongeza Mhe. Rais Ramaphosa kwa kuja na wafanyabiashara ambao wanajadiliana na wafanyabiashara wa Tanzania juu ya kushirikiana kibiashara, na amemhakikishia kuwa Tanzania itakuwa tayari kuhakikisha ushirikiano huo unafanikiwa.


“Sisi Tanzania tumeamua kuwa tunanunua bidhaa zetu Afrika Kusini badala ya kununua bidhaa hizo huko mbali, na kwa kuanzia pikipiki za kuongozea misafara ya viongozi tutakazotumia wakati huu wa Mkutano wa 39 wa SADC tumenunua Afrika Kusini” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.


Kwa upande wake Mhe. Rais Ramaphosa amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kumwalika kufanya Ziara ya Kitaifa hapa nchini na amemhakikishia kuwa wananchi Afrika Kusini wanaiona Tanzania ni nyumbani kwao na hivyo Serikali yake ipo tayari kuuendeleza na kuukuza uhusiano mzuri kati yake na Tanzania.


Mhe. Rais Ramaphosa ameelezea kufurahishwa kwake na kuwepo kwa kampuni 228 za Afrika Kusini zilizowekeza nchini Tanzania na kuajiri wa zaidi ya watu 21,000 na ameahidi kwenda kuwahimiza zaidi wafanyabiashara na wawekezaji wa Afrika Kusini kuja kuwekeza nchini Tanzania huku akiwakaribisha wawekezaji wa Tanzania kwenda kuwekeza Afrika Kusini.


Ameipongeza Tanzania kwa kuzalisha mazao mengi ya chakula na ameahidi kuwa Afrika Kusini itaendelea kununua mazao kutoka Tanzania.Aidha, Mhe. Rais Ramaphosa amesema Afrika Kusini ipo tayari kushirikiana na Tanzania katika nyanja nyingine mbalimbali zikiwemo afya, ulinzi na usalama, utalii na amekubaliana na mapendekezo ya Tanzania juu ya mpango wa kufundisha lugha ya Kiswahili nchini Afrika Kusini hasa wakati huu ambapo SADC inatarajia kuifanya kuwa lugha rasmi ya 4.
Katika ziara hii, Mhe. Rais Ramaphosa ameongozana na Mkewe Mhe. Dkt. Tshepo Motsepe ambaye wakati wa mazungumzo rasmi ya Waheshimiwa Marais amekuwa na mazungumzo na Mke wa Rais wa Tanzania Mhe. Mama Janeth Magufuli.

 

 
Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

15 Agosti, 2019

UBORESHAJI DAFTARI LA WAPIGA KURA KUFANYIKA AGOSTI 26 HADI SEPT 1,2019 SHINYANGA

$
0
0
Kamishina wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa nchini Tanzania,Mhe. Balozi Omari Ramadhani Mapuri amefungua mkutano wa wa Tume na Wadau wa Uchaguzi katika mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kupeana taarifa kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura. 

Mkutano huo umefanyika leo Alhamis Agosti 15,2019 katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga na kuhudhuriwa na mkurugenzi wa uchaguzi,mratibu wa uandikishaji wa mkoa,viongozi wa dini,vyama vya siasa,wawakilishi wa watu wenye ulemavu,vijana,wanawake,asasi za kiraia,watendaji wa tume na waandishi wa habari.

Balozi Mapuri alisema lengo la mkutano huo ni kupeana taarifa kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ulioanza kwa awamu ya kwanza tarehe 18 Julai,2019 katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha.

Alisema uzinduzi rasmi wa zoezi la uboreshaji wa daftari la wapiga kura ulifanyika Mjini Moshi Julai 18 ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa na kwamba katika mkoa wa Shinyanga uboreshaji wa daftari la wapiga kura utafanyika Agosti 26 hadi Septemba 1,2019.

"Lengo la kukutana nanyi leo ni kuwafahamisha kuwa tume imekamilisha maandalizi ya zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura,ikiwemo uhakiki wa vituo vya kujiandikisha,uandikishaji wa majaribio,maandalizi ya vifaa vya uboreshaji wa daftari,maandalizi ya vifaa vya uboreshaji na mkakati wa elimu ya mpiga kura naamini mafanikio ya zoezi hili yanategemea nyinyi wadau",alieleza.

"Tume inatarajia kuanza uboreshaji wa daftari la wapiga kura kwa awamu ya nne katika mikoa ya Mwanza (halmashauri ya wilaya Kwimba),mkoa wa Shinyanga na mkoani Geita (Halmashauri ya Mji wa Geita,Nyang'wale,Bukombe na Mbogwe) kuanzia Agosti 26 hadi Septemba 1,2019",aliongeza.

Alifafanua kuwa uboreshaji wa daftari la wapiga kura unafanyika kwa kutumia teknolojia ya kielektroniki ya Biometriki (BVR) ambayo huchukua taarifa za kibaiolojia za mtu na kuzihifadhi katika Kanzidata(Database) kwa ajili ya utambuzi.

"Uboreshaji wa daftari la wapiga kura wa safari hii hautahusisha wapiga kura walioandikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura mwaka 2015 ambao kadi zao hazihitaji marekebisho yoyote ya taarifa.Uboreshaji huu utawahusu wapiga kura wapya ambao wametimiza umri wa miaka 18 na wale ambao watatimiza umri wa miaka 18 siku ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.",alisema Balozi Mapuri.

Alisema uboreshaji huo pia utahusisha watu ambao wamehama kutoka maeneo yao ya awali na kuhamia maeneo mengine ya uchaguzi na wale ambao kadi zao zimeharibika au kupotea na wale ambao wanatakiwa kufutwa kwenye daftari baada ya kupoteza sifa wakiwemo waliofariki dunia.

Kwa upande wake, Afisa Tehama Mwandamizi kutoka Tume ya Uchaguzi ya Taifa, Frank Mhando aliwataka watu wenye sifa ya kujiandikisha wajitokeze kwa wingi ili waandikishwe na wanaohitaji kuboresha taarifa zao wakati ndiyo huu.

Alisema kila chama cha siasa kina wajibu wa kuweka wakala kwenye kituo cha uandikishaji daftari la wapiga kura huku akikisisitiza kuwa wakala hapaswi kuingilia majukumu ya tume ya uchaguzi na kwamba yeyote atakayeleta masuala ya siasa kwenye vituo atachukulia hatua.

Aliwataka wanasiasa kuepuka kufanya siasa kwenye vituo bali majukumu yao yawe ni kuwatambua wenye sifa ya kujiandikisha wapate sifa ya kupiga kura wakati wa uchaguzi.

"Hakuna uchaguzi bila wapiga kura,hakuna kupiga kura bila kujiandikisha,niwaombe wanasiasa mhamasishe watu wajitokeze kwenda kujiandikisha ili wawe na sifa ya kupiga kura",aliongeza.

ANGALIA PICHA
Kamishina wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa nchini Tanzania,Mhe. Balozi Omari Ramadhani Mapuri akifungua mkutano wa Tume na Wadau wa Uchaguzi katika mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kupeana taarifa kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura leo katika ukumbi wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Kamishina wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa nchini Tanzania,Mhe. Balozi Omari Ramadhani Mapuri akifungua mkutano wa Tume na Wadau wa Uchaguzi katika mkoa wa Shinyanga.
Afisa Tehama Mwandamizi kutoka Tume ya Uchaguzi ya Taifa, Frank Mhando akiwataka watu wenye sifa ya kujiandikisha wajitokeze kwa wingi ili waandikishwe kwenye daftari la wapiga kura.
Katibu Mwenezi wa CHADEMA wilaya ya Shinyanga Mjini,Charles Shigino akiiomba Tume ya uchaguzi kuruhusu mikutano ya hadhara ili wanasiasa waelimishe/wahamasishe wananchi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.
Katibu wa Chama cha ACT-Wazalendo mkoa wa Shinyanga Sebastian Tafuta akichangia hoja wakati wa mkutano huo. 
Wadau wa uchaguzi wakiwa ukumbini.

Kitila Mkumbo atembelea mradi wa maji Nyahiti wilayani Misungwi

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Jiji la Mwanza (MWAUWASA) Mhandisi Anthony Sanga (kushoto) akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Profesa Kitila Mkumbo (katikati) jana alipotembelea mradi wa maji Nyahiti wilayani Misungwi. Kulia ni Mbunge wa Misungwi Charles Kitwanga.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Jiji la Mwanza (MWAUWASA) Mhandisi Anthony Sanga (kushoto) akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Profesa Kitila Mkumbo (katikati) jana alipotembelea mradi wa maji Nyahiti wilayani Misungwi. Kulia ni Mbunge wa Misungwi Charles Kitwanga. 
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Profesa Kitila Mkumbo (katikati) wa pili kutoka kulia kipata ufafanuzi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mwauwasa, Mhandisi Anthony Sanga (wa tatu kutoka kushoto) kuhusu mradi wa chanzo cha maji cha Nyahiti  jana alipotembelea mradi huo Kushoto wa pili ni Mbunge wa Misungwi Charles Kitwanga. 
 Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Profesa Kitila Mkumbo akizungumza na waandishi wa habari jana baada ya kutembelea na kukagua mradi wa maji Nyahiti ambao umekamilika kwa asilimia 97 tayari kutoa huduma ya maji kwa wakazi wa Misungwi wapatao 64000.   
  Katibu Mkuu Wizara ya Maji, profesa Kitila Mkumbo akihutubia wananchi wa Kisesa na Bujora wilayani Magu jana kuhusu kero ya maji kwenye maeneo hayo.
Picha zote na Baltazar Mashaka

TRA YATOA MAFUNZO KWA IDARA YA WALIPAKODI WAKUBWA WA TAASISI NA MASHIRIKA YA UMMA

$
0
0
Kamishina wa walipakodi wakubwa wa Mamlaka ya mapatoTanzania (TRA), Alfred Mregi akizungumza katika semina ya kutoa elimu ya kodi kwa
 wafanyakazi wa taasisi na mashirika ya umma katika ukumbi wa mikutano, benki kuu jijini Dar es Salaam leo. Akimwakilisha Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Dr. Edwin Mhede.
 Naibu Kamishina wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Herbert Kabyemela akizungumza na wawakilishi wa taasisi na mashirika ya umma wakati wa kutoa elimu katika ukumbi wa mikutano, Benki kuu jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wawakilishi  wa taasisi na mashirika ya umma wakimsikiliza Kamishna wa walipakodi wakubwa wa Mamlaka ya mapatoTanzania (TRA), Alfred Mregi katika ukumbi wa mikutano, benki kuu jijini Dar es Salaam leo wakati wakipewa elimu TRA kuhusiana na kujifunza namna kutumia mifumo mipya ya kukusanyaji kodi nchini. 
Kamishna wa walipakodi wakubwa wa Mamlaka ya mapatoTanzania (TRA), Alfred Mregi na Naibu Kamishina wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Herbert Kabyemela wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa taasisi na mashirika ya umma katika ukumbi wa mikutano, Benki kuu jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo, Michuzi Blog

MKUTANO WA WAFANYABIASHARA WA MAZAO YA NAFAKA KUFANYIKA AGOSTI 29,30.

Tigo yatoa msaada wa kompyuta 20 katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya

$
0
0


Mkurugenzi wa Tigo, Nyanda za juu Kusini, Henry Kinabo(katikati) akimkabidhi Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST), Profesa Aloys Mvuma, moja ya kompyuta 20 zenye thamani ya 48m/- zilizotolewa na Tigo kwaajili ya kuchangia katika masomo ya TEHAMA katika chuo hicho mkoani Mbeya.Pembeni yao ni Naibu wa makamu mkuu wa chuo Taaluma, Ushauri na Utafiti, Profesa Godliving Mtui.

Mkurugenzi wa Tigo, Nyanda za juu Kusini, Henry Kinabo(katikati), akikaribishwa katika chumba cha kufundishia kompyuta katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) na Rasi Kampasi ya Rukwa, Dkt. Duncan Mwakipesile(Kushoto) baada ya makabidhiano ya komputa 20 zenye thamani ya 48m/- zilizotolewa na Tigo kwaajili ya kuchangia katika masomo ya TEHAMA katika chuo hicho mkoani Mbeya.

Wafanyakazi wa Tigo, kutoka Nyanda za juu Kusini, wakiwa katika ya pamoja na wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST baada ya makabidhiano ya kompyuta 20 katika chuo hicho zenye thamani ya 48m/- zilizotolewa na Tigo kwaajili ya kuchangia katika masomo ya TEHAMA katika chuo hicho mkoani Mbeya.

Katika juhudi za kuchangia malengo ya Serikali ya kuboresha na kuinua viwango vya elimu katika taasisi za elimu ya juu, kampuni inayoongoza katika maisha ya kidigitali nchini Tanzania, Tigo, leo wamekabidhi kompyuta za mezani 20, zitakazo wanufaisha wanafunzi 4,630 katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya(MUST).

Alipokuwa anakabidhi kompyuta hizo katika chuo hicho, Mkurugenzi wa Tigo, Nyanda za juu Kusini, Henry Kinabo alisema: “Tunaamini ya kwamba kompyuta tunazozitoa hapa leo, zitachangia sehemu kubwa katika kubadilisha jinsi wanafunzi wanavyosoma na pia zitaleta nafasi kwao kubuni teknolojia mpya na kuchangia katika ukuaji wa uchumi nchini Tanzania. Tigo ipo mstari wa mbele kwaajili ya kuboresha viwango vya elimu katika vyuo vikuu kwa kuleta nyenzo za kusomea na kuwasaidia wanafunzi na walimu kukuza vipengee muhimu vinavyohitajika katika karne hii ya 21.”

Aliendelea kuelezea zaidi kwamba kupitia mchango huo, Tigo imeunga mkono juhudi za Serikali ya Tanzania katika mtazamo wake wa kubadilisha nchi kuwa ya viwanda na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 ambapo TEHAMA ndio chachu ya maendelea hayo.

Mnamo mwaka 2017, Tigo ilichangia kompyuta 47 katika Chuo kikuu cha Dodoma, zilizo wanufaisha wanafunzi takriban 36,150. Mpaka leo jumla ya wanafunzi 40,780 katika vyuo vikuu nchini wamenufaika na msaada wa kompyuta kutoka Tigo kwa kipindi cha miaka miwili sasa.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia(MUST), Profesa Aloys Mvuma, aliipongeza kwa mchango wao kwa kusema, “Ni kupitia ushirikiano huu ndio tutaweza kutoa stadi za kisasa za TEHAMA za kisasa pamoja na maarifa kwa kizazi kijacho cha wataalam, ili nchi iweze kukidhi mahitaji ya taarifa zinazobadilika mara kwa mara na mitindo ya kidigitali katika jamii na uchumi wa dunia.”

Rasi wa ndaki ya Sayansi na Elimu za Ufundi, Dkt. John.P.John, aliwashukuru Tigo kwa usaidizi wao mkubwa sana na alisema kompyuta hizo zitasaidia kuboresha kiwango cha elimu mkoani Mbeya. “Tunawashukuru Tigo kwa kusaidia juhudi za serikali kwa kutoa mchango wa vifaa vya kufundishia masomo ya TEHAMA katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia(MUST). Tunaamini ya kwamba hizi kompyuta zitaboresha jinsi wanafunzi wanavyosoma na pia itaongeza ueledi katika elimu ya kidigitali hapa Chuoni.”

RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA ATUMA UJUMBE MZITO NCHI ZA SADC, AZITAKA ZIJITEGEMEA BADALA YA KUWA TEGEMEZI

$
0
0

Na Said Mwishehe,Michuzi TV

RAIS Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu nchini Tanzania, Benjamin Mkapa ametuma ujumbe mzito kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), kwa kuzitaka ziweke mfumo mzuri wa kuwasilisha michango kwa wakati kwa ajili ya jumuiya hiyo ili ziweze kutekelezeka majukumu yao kikamilifu huku akisema ni lazima zijitegemee badala ya kuwa tegemezi.

Hayo ameyasema leo Agosti 15,2019 akiwa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo alikuwa anaongoza Mhadhara wa wazi ambao limeandaliwa na Taasisi ya Uongozi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)pamoja na SADC kwa ajili ya kuzungumzia masuala mbalimbali ya Jumuiya.

Hivyo wakati anazungumza kwenye mhadhara huo uliohudhuria na watu wa kada mbalimbali wakiwemo viongozi,wasomi, sekta binafsi, viongozi wastaafu na wanafunzi wa vyuo vikuu Mkapa amesema ili Jumuiya hiyo iweze kutekeleza vema majukumu yake iko haja kwa nchi wanachama kutoa michango waliyojiwekea kwa wakati.

Pia amesema katika nchi za SADC na Afrika kwa ujumla kuna rasilimali za kutosha na za kila aina, hivyo haoni sababu ya nchi hizo kuendelea kutegemea msaada kutoka kwa wahisani katika kutekeleza baadhi ya majukumu yake.

"Malengo na matarajio ya SADC ni kufanya mapinduzi ya kila sekta ili kuchochea uchumi wa nchi na wananchi pamoja na kusimamia amani ya nchi na kanda kwa ujumla.Iwapo kutakuwa na mikakati inayotekelezeka na inayoakisi malengo na matarajio ya SADC nchi wanachama zitaacha kuwa tegemezi.Kwa miaka 14 ambayo nimekuwa nje ya SADC kimaamu bado naona changamoto ni zilezile za siku nyuma hazijapata ufumbuzi,"amesema Mkapa.

Amefafanua kuna changamoto kubwa ya soko la nje, umaskini, ubora hafifu wa bidhaa, teknolojia na miundombinu duni, hivyo ni jukumu la Jumuiya hiyo kuweka mikakati ya kutafuta changamoto hizo huku akibainisha SADC ina historia ndefu kwa nchi za Kusini hasa kisiasa, kiuchumi na kijamii lakini bado haijagusa jamii kwa upana wake na hivyo lazima ni wabadilike.

Wakati huo huo amesema pamoja na mipango iliyopo juhudi zinahitajika katika kuwekeza kwa vijana na teknolojia ili kwenda na kasi ya dunia."Teknolojia imewehukua nafasi kubwa kwenye sekta ya viwanda hivyo hakuna sababu ya kubakia katika mifumo ya kizamani,"

Akizungumzia elimu kwa vijana wa Jumuiya hiyo amesema elimu inasaidia kichochea ubunifu na ujuzi na hivyo kuondoa changamoto ya uhaba wa ajira kwa vijana hao.Kwa upande wake Mkuu wa Program Benki ya Dunia (WB), Tanzania, Gilead Teri ameeleza kwenye mhadhara huo kwamba sekta binafsi ipo tayari kushiriana na nchi za SADC ili kuchochea ukuaji wa uchumi.

Hata hivyo amezungumzia umuhimu wa kujikita katika kuendelea kuonesha miundombinu na elimu.Wakati huo huo Katibu Mkuu wa SADC, Dk.Stergomena Tax yeye amesema jumuiya hiyo imejipanga katika kuweka mipango madhubuti kwa lengo la kujitegemea na kuinua uchumi kwa nchi wanachama.

Akizungumza katika mhadhara huo Katibu Mkuu mstaafu wa SADC, Dk. Simba Makoni amesema kunahitajika mikakati ya kuifanya jumuiya hiyo ijulikane kwa wananchi wake na kwamba bado jamii inaamini jumuiya hiyo ni ya viongozi wao jambo ambalo linaweza kusababisha sintofahamu kwa siku zijazo.

Kwa upande wake Mratibu wa Mafunzo ya Ulinzi Shule ya Wits ya Afrika Kusini, Profesa Anthoni van Nieuwkerk amesema SADC imefanikiwa katika eneo la ulinzi, usalama na demokrasi na kwamba ni wakati wa kujikita kwenye maeneo ambayo yatabadilisha wananchi.

Mzee Joseph Butiku wakati anazungumza ametumia nafasi kusisitiza umuhimu wa elimu ambayo itamsaida aliyesoma kujiajiri badala ya kulalamika kutokuwa na ajira na kufafanua kuwa idadi kubwa ya vijana ambao wamesema,hivyo ni wakati wa kutumia elimu yao katika fursa zilizopo ndani ya Jumuiya hiyo.
 Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamini William Mkapa akihutubia katika mhadhara uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) uliokuwa ukizungumzia historia ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), mapema leo Agosti 15, 2019. 

WADAU WAJITOKEZA KUSAIDIA MICHUANO YA FEASSA

$
0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Blog ,Arusha

Wadau mbalimbali jijini Arusha wamejitokeza kusaidia mashindano ya shirikisho la michezo kwa shule za sekondari Afrika Mashariki (FEASSA) kwa kujitolea mahitaji muhimu ikiwemo maji,vyakula na usafiri ili kufanikisha michuano hiyo ya kimataifa.

Mwenyekiti wa Umoja wa Shule zisizomilikiwa na serikali (Tamongsco) mkoa wa Arusha Isabella Mwampamba akizungumza wakati akikabidhi sehemu ya vitu walivyovitoa, amesema kuwa lengo lao ni kuunga mkono serikali katika michuano hiyo ili iweze kufanya kazi vizuri na kuliletea taifa heshima

Afisa Elimu mkoa wa Arusha Halfani Masukira ameushukuru umoja wa shule binafsi kwa kujitoa kufanikisha mashindano hayo muhimu ambayo yanatarajia kuanza Agosti 15 mwaka huu na kuwakutanisha watu zaidi ya 3000

Mjumbe kamati ya michezo hiyo Halifa Kiembe amesema kuwa michezo hiyo ni muhimu katika kukuza na kuibua vipaji muhimu ambavyo vitaiwezesha Tanzania na Afrika Mashariki kung`ara kimataifa

Feassa ya tikisa Arusha Tz ni mashindano ya Esti africa yanayo jumuisha Nchi 7 yatakayo shirikisha shule za sekondari na msingi kuanza mwaka huu mashindano hayo yamenza kutimua vumbi Leo.

MARAIS NCHI ZA SADC WANASHIRIKIANA VEMA KUTATUA CHANGAMOTO-MKAPA

$
0
0
Na Leandra Gabriel Michuzi TV

RAIS wa Awamu tatu Benjamin William Mkapa amesema nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) zina amani ya kutosha huku akitumia nafasi hiyo kuelezea namna ambavyo marais wa nchi za jumuiya hiyo wamekuwa wamoja katika kutatua changamoto mbalimbali kwa lengo la kuleta maendeleo ya wananchi.

Amesema kuwa changamoto zinazoikumba jumuiya hiyo ni pamoja na masoko, umaskini, kiwango kidogo Cha uwekezaji,kiwango duni cha teknolojia na changamoto ya miundombinu rafiki ndani ya jumuiya ni mambo yanayotakiwa kuangaliwa kwa jicho la pekee ili kuweza kuendana na dhima ya jumuiya hiyo ambayo daima imejikita katika kuhakikisha uchumi, uzalishaji, utawala Bora amani na ulinzi vinapewa kipaumbele zaidi.

Akiwa amestaafu katika nafasi hiyo ya uenyekiti wa kwa miaka 14 Sasa Mkapa amesema kuwa Kuna mambo lazima yawekewe mkazo na hayo ni pamoja na kuongeza uzalishaji katika nchi wanajumuiya, viwanda ambavyo vitakakata bidhaa zinazozalishwa, uwekezaji pamoja na teknolojia ili kuweka ushindani katika soko la kimataifa.

Aidha amezishauri nchi wanachama kutengeneza ajira nyingi zaidi hasa kwa kundi la vijana na hiyo ni pamoja na kuweka mifumo rafiki ya elimu ambayo itawapa maarifa ya kutengeneza ajira zao wenyewe na sio kutegemea kuajiriwa pekee na amezitaka taasisi za sekta binafsi na serika kushirikiana katika kutatua changamoto za kiuchumi ili kuweza kujenga uchumi imara ndani ya jumuiya.

Vilevile ameshauri masuala Kama uwekezaji wa vikwazo vya biashara havina budi kuondolewa na kuweka masoko ya uhakika na hiyo ikienda sambamba na kutumia bidhaa ndani ya jumuiya hiyo hali itakayochochea ukuaji wa kasi wa uchumi unaojitegemea kwa nchi wanachama.

Hata hivyo Mkapa amesema kuwa mlengo wa jumuiya ya SADC ni kuleta mapinduzi hasa ya kiviwanda hivyo jumuiya haina shida budi kutoa maarifa na ujuzi kwa vijana ili waweze kuleta mabadiliko hasa ya kiteknolojia yatakayoleta ushindani katika soko la kimataifa na teknolojia hiyo ni kwa kuzingatia uwepo wa uimara katika masuala ya miundombinu, nishati na viwanda.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Benjamini William Mkapa akihutubia katika mhadhara uliofanyika  leo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ,uliohusu historia ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC). 

FEASSSA KUANZA KUUNGURUMA AGOSTI 16 JIJINI ARUSHA

$
0
0
Na Woinde Shizza michuzi blog,Arusha

Mkoa wa Arusha  unatarajiwa kuwa mwenyeji wa mashindano ya michezo kwa shule za Msingi na Sekondari kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki ali maalufu kama FEASSSA.

Akizungumza na waandishi wa habari wa Mkoa wa Arusha,Katibu tawala wa Mkoa huo Richard Kwitega amesema mashindano hayo yatafanyika kuanzia Agosti 16,2017 hadi Agosti 25,2019.

“Mashindano haya ni fursa kubwa sana kwa Mkoa wetu wa Arusha na nchi kwa ujumla kwani inatupa nafasi yakukuza na kudumisha ushirikiano kwa nchi za Afrika Mashariki”.

Kwitega amesema Mkoa wa Arusha unatarajia kupokea wanamichezo takribani 3500 kutoka katika nchi 6 za Afrika Mashariki na nchi ya Malawi kushiriki kama mwalikwa.Aidha, tofauti na wachezaji hao Mkoa utapokea wageni mbalimbali wakiwemo viongozi mbalimbali, Wazazi, Walimu na Waamuzi wapatao 1500 katika mashindano hayo.

Mashindano hayo yanatarajiwa kuzinduliwa rasmi Agosti 16,2019 katika viwanja vya Sheik Amri Abeid na yataendelea kutimua vumbi katika viwanja vingine kama vya shule ya St. Costantine, Viwanja vya International School of Moshi (ISM),viwanja vya Magereza,Tigiti na ukumbi wa michezo wa Palot.

Amesisitiza kuwa michezo itakayo shindanishwa ni mpira wa miguu, mpira wa pete, mpira wa magongo, mpira wa mikono ,mpira wa kikapu, riadha, mpira wa wavu,mashindano ya kuogolea,mpira wa meza, mpira wa kengele utakaowahusisha watu wenye ulemavu.

Kwitega, amewahamasisha wananchi wote kutumia fursa hiyo katika kukuza uchumi kwa nyanja mbalimbali zikiwemo za Utalii,Hoteli na Usafiri kwa maendeleo ya watu na nchi kwa ujumla.
Picha Katibu tawala wa Mkoa wa Arusha Richard Kwitega akiongea na waandishi Wa habari ofisini kwake

MALINZI AKABIDHI USHAHIDI WA RISITI ZA MALIPO KUTOKA TFF

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imepokea vielelezo viwili ambavyo ni taarifa ya benki ya mwaka 2014 na risiti 13 zilizoonesha TFF ilikuwa ikimlipa Malinzi fedha za mkopo alizokuwa anawadai.

Katika utetezi wake mbele ya Hakimu Mkazi Maira Kasonde, Malinzi ameithibitishia mahakamani hapo kuwa anakumbuka alikuwa anaidai TFF zaidi ya Sh milioni 152.6.

Akiongozwa na wakili Richard Rweyongeza kutoa ushahidi wake Wa utetezi Malinzi amedai kuwa, katika taarifa ya benki ya Januari 2014 hadi Agosti 19, 2014 alikuwa anaidai TFF zaidi ya sh. Milioni 152 huku kiasi cha USD 5000 ambazo anadai kuzitoa nchini Msumbiji hazikuingizwa kwenye mfumo huo badala yake waliingiza kwa mkono.

Ameendelea kudai kuwa, fedha hizo zilipobadilishwa kuwa fesha za kitanzania jumla ilikuwa yake ilifikia Sh milioni 8.3 ambapo kwenye taarifa hiyo ya benki waliandika kuwa ‘’kiasi unachotudai kwa mujibu wa kumbukumbu zetu ni Sh 152,613,004.83.’’

Amedai kuwa alipokuwa analipwa baadhi ya fedha walikuwa wakimpa risiti kwa majina yake na kwamba aliendelea kutoa fedha kwa TFF hadi alipokamatwa mwaka 2017.

Amedai kuwa, miongoni mwa risiti alizonazo zilisainiwa na mhasibu wa TFF Hellen Adam ambaye alikuwa shahidi wa kumi wa upande wa mashitaka na zingine zilisainiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Fedha, Daniel Msangi ambaye alikuwa shahidi wa sita huku risiti nyingine haikuwa na saini lakini kwenye taarifa ya benki ilionesha imeingizwa kama mkopo.

"Risiti zote za TFF zinatunzwa na idara ya uhasibu ya shirikisho hilo na kwamba nilikuwa nikilipwa kwa mafungu mafungu kutokana na hali ya shirikisho hilo kuwa mbaya kiuchumi ambapo idara ya fedha ilikuwa ikikaa na kuangalia namna ya kumlipa kutokana na kile wanachokipata”

Malinzi alidai mwaka 2015 hali ya TFF ilikuwa haijabadilika kwani alikuwa akitoa fedha zake mfukoni na kuwaomba wadau mbalimbali kuendelea kuchangia na mwishoni mwa mwaka 2014 alijenga Ofisi ya Rais na nyaraka alizokuwa anatunza nyumbani alihamishia kuzitunza ofisini.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Kasonde aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 27, mwaka huu kwa ajili ya utetezi.

Mbali na Malinzi, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni aliyekuwa Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa, Mhasibu wa TFF, Nsiande Mwanga na Karani Flora Rauya ambapo wote hao wanakabiliwa na mashitaka 20 yakiwamo ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa fedha wa Dola za Marekani 173,335.

Waziri wa Viwanda na Biashara Zambia akutana na Waziri Issack Kamwelwe

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (kushoto), akijadiliana jambo na Waziri wa Biashara na Viwanda, Chris Yaluma (kulia) kutoka Zambia wakati alipomtembelea katika ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Biashara na Viwanda kutoka Zambia, Chris Yaluma, akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, wakati alipomtembelea katika ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Biashara na Viwanda kutoka Zambia, Chris Yaluma, akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi wa Huduma za Uchukuzi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Aron Kisaka, wakati alipotembelea ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akiagana na Waziri Biashara na Viwanda, Chris Yaluma, kutoka Zambia mara baada ya kukutana na kujadili fursa za uwezekezaji nchini hususan sekta ya usafirishaji katika ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akisisitiza jambo kwa Waziri Biashara na Viwanda, Chris Yaluma, kutoka Zambia kuhusu masuala ya uwekezaji katika miundombinu ya usafirishaji, wakati alipomtembelea katika ofisi ndogo ya Wizara jijini Dar es Salaam.

USAJILI NGOs NYANDA ZA JUU KUSINI WAENDELEA

$
0
0

Mwanasheria wa Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Faki Shaweji (kulia) na Afisa Maendeleo ya Jamii Victor Rugarabamu (kushoto) wakipitia Katiba ya mmoja wa mdau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali aliyefika kuhuisha Usajili wa asasi yake katika zoezi la kusajili mashirika kwa mujibu wa Sheria ya NGOs Na. 3 ya mwaka 2019 katika Kanda ya Nyanda za Juu Kusini katika Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.
Wataalam mbalimbali kutoka Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya kijamii, RITA, BRELA na wasajili wasaidizi kutoka Ofisi ya RAS Mbeya wakiendelea na zoezi la usajili wa wadau wa asasi mbalimbali walioitikia zoezi la kubadili usajili wa mashirika na taasisi zao katika siku ya pili ya usajili huo unaofanyika kwa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini katika Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.
Wanasheria wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya jamii) wakipitia nyaraka za wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali waliofika kukamilisha usajili wa mashirika yao wakati wa zoezi la usajili huo linaloendelea katika Mikoa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini katika Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW

RAIS MAGUFULI: TUTAZIDI KUFUNGUA MILANGO YA BIASHARA NA UWEKEZAJI NA JAMHURI YA AFRIKA KUSINI

$
0
0
RAIS Dkt. John Magufuli amesema Tanzania itazidi kufungua milango ya ushirikiano na Jamhuri ya Afrika Kusini na kuwataka Wafanyabiashara na Wawekezaji wa nchi hizo kutumia fursa za vivutio mbalimbali vilivyopo ili kukuza uchumi kwa manufaa ya wananchi wa Mataifa hayo.

Akizungumza leo Alhamisi (Agosti 15, 2019) Ikulu Jijini Dar es Salaam wakati wa mazungumzo yake na Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, Rais Magufuli alisema Tanzania na Afrika Kusini ni mataifa rafiki yenye historia ya ushirikiano katika nyanja mbalimbali za maendeleo.

Aliongeza kuwa Jamhuri ya Afrika Kusini ni miongoni mwa Mataifa yaliyopiga hatua kubwa za maendeleo ya kiuchumi katika Bara la Afrika, hivyo Tanzania itatumia fursa hiyo na mshirika wa karibu kwa ajili ya kupanua wigo wa sekta za kibiashara ikiwemo ununuzi na uuzaji wa bidhaa na mazao mbalimbali.

“Katika Nchi za SADC, mwaka 2018 Tanzania imeongoza katika ukanda wa SADC kwa thamani ya mauzo ya bidhaa zake Nchi ya Afrika Kusini iliyofikia thamani Dola Milioni 742.02, na biashara baina ya Mataifa haya ilifikia thamani ya Dola Bilioni 1.18 kutoka Dola Bilioni 1.11 mwaka 2017” alisema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli alitoa wito kwa Wafanyabiashara na wawekezaji wa Afrika Kusni kuja kwa wingi nchini kwa ajili ya kuwekeza na kufanya biashara kwa kuwa Serikali imeendelea kuimarisha na kuweka mazingira wezeshi ikiwemo ujenzi wa miundombionu ya uhakika, pamoja na uimarishaji wa mifumo ya kitaasisi katika usimamizi wa kodi na biashara.

Akifafanua zaidi Rais Magufuli alisema Tanzania imejipanga kikamilifu katika kuimarisha mfumo imara wa uchumi wake ikiwemo kupitia ujenzi wa viwanda, ambayo ndiyo Dira na dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tanzania katika kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025, hivyo aliwataka wawekezaji wa Afrika Kusini kuja nchini na kujenga viwand.

“Katika Bajeti ya Serikali kwa mwaka tunatenga kiasi cha Tsh Bilioni 270 kwa ajili ya ununuzi wa madawa nje ya nchi, tunawaomba wawekezaji wa Afrika Kusini waje Tanzania wajenge viwanda vya madawa kwani kwa kufanya hivyo tutakuwa tumepunguza gharama kubwa za uagizaji wa madawa kutoka nchi ya nchi” alisema Rais Magufuli.

Akifafanua zaidi Rais Magufuli alisema Serikali imekusudia miundombinu ya usafiri wa reli Tazara ili kuweza kutumika na Wafanyabiashara wa Afrika Kusini kwa ajili ya usafirishaji wa bidhaa mbalimbali pamoja na kutangaza fursa za vivutio vya utalii na fukwe za bahari zenye urefu wa takribani Kilometa 1400 zilizopo nchini.

Kwa mujibu wa Rais Magufuli alisema Tanzania ipo tayari kufanya biashara na Jamhuri ya Afrika Kusini ikiwemo ununuzi wa vifaa mbalimbali ikiwemo magari, ambayo Tanzania imekuwa ikiyanunua katika nchi za mbali, huku akitolea mfano wa pikipiki zinazotumika katika Mkutano wa 39 wa SADC zimenunuliwa kutoka nchini Afrika Kusini.

Kwa upande wake Rais Cyril Ramaphosa alisema ziara yake nchini Tanzania ni kielelezo cha kuendelea kuimarika kwa ushirikiano baina ya Mataifa hayo na kusema Serikali yake itaweka mazingira wezeshi kwa Wafanyabiashara na wawekezaji wa Tanzania kwenda nchini Afrika Kusini kufanya biashara na kutafuta fursa ya maeneo ya uwekezaji na biashara.

Aliongeza kuwa Serikali yake inatambua umuhimu wa sekta ya biashara na uwekezaji katika kukuza uchumi katika Nchi za SADC kupitia ajenda ya Maendeleo Endelevu ya jumuiya hiyo ya mwaka 2030 ambayo imedhamiria katika kujenga mazingira bora ya biashara katika Jumuiya hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Cyril Ramaphosa kabla ya kuanza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipongezana na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Cyril Ramaphosa mara baada ya kubadilishana zawadi Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Cyril Ramaphosa mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania MheshimiwaDkt. John Pombe Magufuli akiongoza ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo ya pamoja na Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Cyril Ramaphosa pamoja naujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya AfrikaKusini Cyril Ramaphosa wakati wakizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Cyril Ramaphosa mara baada ya kumaliza kikao chao na Waandishi wa Habari Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU



TRA yatoa mafunzo kwa wahasibu wa taasisi za Umma

$
0
0
Kamishina wa walipakodi wakubwa wa Mamlaka ya mapatoTanzania (TRA), Alfred Mregi akizungumza katika semina ya kutoa elimu ya kodi kwa
 wafanyakazi wa taasisi na mashirika ya umma katika ukumbi wa mikutano, benki kuu jijini Dar es Salaam leo. Akimwakilisha Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Dr. Edwin Mhede.
 Naibu Kamishina wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Herbert Kabyemela akizungumza na wawakilishi wa taasisi na mashirika ya umma wakati wa kutoa elimu katika ukumbi wa mikutano, Benki kuu jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wawakilishi  wa taasisi na mashirika ya umma wakimsikiliza Kamishna wa walipakodi wakubwa wa Mamlaka ya mapatoTanzania (TRA), Alfred Mregi katika ukumbi wa mikutano, benki kuu jijini Dar es Salaam leo wakati wakipewa elimu TRA kuhusiana na kujifunza namna kutumia mifumo mipya ya kukusanyaji kodi nchini. 
Kamishna wa walipakodi wakubwa wa Mamlaka ya mapatoTanzania (TRA), Alfred Mregi na Naibu Kamishina wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Herbert Kabyemela wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa taasisi na mashirika ya umma katika ukumbi wa mikutano, Benki kuu jijini Dar es Salaam leo.Picha na Avila Kakingo, Michuzi Blog

Na Karama Kenyunko, blog ya jamii.

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), amezitaja changamoto ambayo  taasisi na mashirika ya umma zimekuwa zikikabiliana nazo ikiwemo kushindwa kuwasilisha ritani na kushindwa kuwasilisha mapema.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina  iliyohusisha Wahasibu wa Taasisi mbalimbali za umma , Kamishna wa Idara ya Walipakodi wakubwa, Alfred Mregi kwa niaba ya Kamishna Mkuu wa TRA, amesema,  kuwa taasisi hizo zimekuwa zikifanya manunuzi au matumizi yasiyokuwa na stakabadhi au Ankara za kodi za kielektroniki.

Pia ameongeza kuwa, taasisi hizo zimekuwa na madeni makubwa ya kodi ya muda mrefu na wamekuwa wakikosea katika kufanya malipo ya kodi mbalimbali mara kwa mara kwenye mfumo wa malipo wa kodi na maduhuli.

‘’Bado kuna changamoto au mapungufu katika tafsiri na ukokotoaji wa kodi kwenye mishahara, posho na stahiki mbali mbali za watumishi, vibarua na makandarasi hususani kwenye miradi mbali mbali,’’ amesema Dk Mregi..

Ameongeza kuwa yapo mapungufu katika tafsiri na utozaji wa kodi ya zuio hususani katika kandarasi, miradi na zabuni mbali mbali na kutokuzingatia matumizi sahihi ya mabadiliko mbali mbali yatokanayo na sheria za fedha za miaka husika, hivyo kusababisha taasisi na mashirika husika kukadiriwa ongezeko la kodi, adhabu na riba. 

Mregi amesema lengo la kuwataka wananchi kulipa kodi litatimia endapo watashirikiana kutimiza wajibu ikiwemo kulipa kodi stahiki kwa wakati, kuboresha ushirikiano baina ya serikali na wafanyabiashara, kutofumbia macho vitendo vya rushwa, uhalifu na uhujumu uchumi na vitendo vingine ambavyo vinasababisha nchi kupoteza mapato.

‘’Mamlaka ya mapato inaendelea kushirikiana na wadau wake ili kuongeza uelewa wa sheria na taratibu mbalimbali na kuongeza uhiari katika ulipaji kodi,’’ amesisitiza.

 Aidha, amesema kuwa mafunzo hayo yanalenga kuongeza, ujuzi, elimu na weledi wa matumizi bora ya mifumo ya kodi kwani TRA ina wajibu wa kusimamia sheria mbalimbali za kodi pamoja na maduhuli kwa niaba ya serikali na ina mkataba wa huduma kwa mlipa kodi na kwamba dhamira yake ni kutoa huduma bora kwa walipakodi na wadau wengine katika utekelezaji wa majukumu yake kisheria.

Naye Naibu Kamishna wa Idara ya walipakodi wakubwa Herbert Kabyemela amesema kuwa katika mwaka wa fedha wa 2019/20 mamlaka ya mapato inajukumu la kukusanya Sh trilioni 19.1 ikiwa ni asilimia 57.6 ya Bajeti ya serikali ya Sh trilioni 33.11.

Amesema lengo hilo ni sawa na ongezeko la Sh trilioni 1.1 ukilinganisha na lengo la mwaka wa fedha wa 2018/19 

Kwa upande wake Dinna Zacharia ambaye ni muhasibu kutoka Shirika la 
 Mawasiliano Tanzania (TTCL) alisema kuwa semina hiyo itawasaidia 
walipakodi kujua mifumo ya kodi iliyopo lakini pia aina za kodi 
wanazotakiwa kulipa.

Amesema pia itawawezesha kujua mabadiliko ya shera za kodi yaliyojitokeza  na kuweza kuyafanyia kazi na hatimae kuiwezesha serikali kutimiza lengo.

RAIS DKT. MAGUFULI NA RAIS RAMAPHOSA WASHIRIKI MKUTANO BAINA YA WAFANYABIASHARA WA TANZANIA NA AFRIKA KUSINI

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihotubia mbele ya mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Cyril Ramaphosa katika mkutano baina ya Wafanyabiashara wa Tanzania na Ujumbe wa Wafanyabiashara toka Afrika kusini uliofanyika katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akihotubia mbele ya mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano baina ya Wafanyabiashara wa Tanzania na Ujumbe wa Wafanyabiashara toka Afrika kusini uliofanyika katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Cyril Ramaphosa na Mawaziri wa Serikali ya Tanzania na Afrika kusini mara baada ya kumalizika kwa mkutano baina ya Wafanyabiashara wa Tanzania na Ujumbe wa Wafanyabiashara toka Afrika kusini uliofanyika katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Cyril Ramaphosa wakisalimiana mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere Mzee Joseph Butiku mara baada ya kumalizika kwa mkutano baina ya Wafanyabiashara wa Tanzania na Ujumbe wa Wafanyabiashara toka Afrika kusini uliofanyika katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam. . PICHA NA IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpongeza Rais wa Afrika kusini, Cyril Ramaphosa mara baada kukamilisha kusoma hotuba yake katika kongamano la biashara la Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati wa kikao cha wafanyabiashara na wawekezaji wa Tanzania na Afrika Kusini leo Agosti 15, 2019 jijini Dar es Salaam. Ambapo Mkutano huo umeudhuriwa na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ambaye yupo nchini kwa ziara ya Siku mbili huku akisubiri kuhudhuria mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) unaotarajia kufanyika Agosti 17 na 18, 2019.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa (wa tatu kutoka kushoto) akipiga makofi. 
Wageni waliofika katika mkutano wa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Tanzania na Afrika Kusini.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akihutubia katika wakati wa kikao cha wafanyabiashara na wawekezaji wa Tanzania na Afrika Kusini leo Agosti 15, 2019 jijini Dar es Salaam. Ambapo Mkutano huo umeudhuriwa na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ambaye yupo nchini kwa ziara ya Siku mbili huku akisubiri kuhudhuria mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) unaotarajia kufanyika Agosti 17 na 18, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mkono na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi mara baada ya kumaliza kuhutubia kikao cha wafanyabiashara na wawekezaji wa Tanzania na Afrika Kusini leo Agosti 15, 2019 jijini Dar es Salaam.
Wageni waliofika katika mkutano wa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Tanzania na Afrika Kusini.

MAHAKAMA KUU KANDA YA DAR ES SALAAM KUSIKILIZA MAOMBI YA LISSU AGOSTI 23 KUHUSU UBUNGE JIMBO LA SINGIDA MASHARIKI

$
0
0
Karama Kenyunko

MAHAKAMA Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, imepanga Agosti 23 mwaka huu kusikiliza maombi ya chini ya hati ya dharura ya kutoa amri ya kusitisha mchakato wa kuapishwa kwa mbunge mteule wa Singida Mashariki, Miraji Mtaturu (CCM) yaliyofunguliwa na aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Tundu Lissu.

Maombi ya Lissu namba 18 ya mwaka 2019 yametajwa jana mahakamani hapo mbele ya Jaji Sirilius Matupa ambapo Lissu anawakilishwa na jopo la Mawakili wanne akiwemo Peter Kibatala, huku upande wa Serikali ambao ni wajibu maombi ukiwakilishwa na mawakili wanne akiwemo Wakili wa Serikali Mkuu, Vincent Tango.

Hatua hiyo imefikwa leo Agosti 15, 2019 baada ya Wakili Kibatala kuwasilisha ombi la kuitaka mahakama itoe amri ya kusitisha kuapishwa kwa mbunge mteule Mataturu, Wakili wa Lissu ambaye ni Kibatala aliomba mwongozo wa mahakama ili waweze kuzungumzia suala hilo la kusimamishwa kuapishwa kwa mbunge mteule wa jimbo hilo, lakini ombi hilo likapingwa na mawakili wa Serikali wakidai kuwa kwa sasa sio muda sahihi wa kuanza kulisikiliza jambo hilo. 

Pia upande wa wajibu maombi waliomba muda wa siku nane ili waweze kuwasilisha hati ya kiapo kinzani pamoja na hati ya maelezo kinzani kabla ya maombi hayo kupangiwa siku ya kuanza kusikilizwa.

Wakili wa Serikali Mkuu, Tango alidai wanaomba siku hizo kwa kuwa shauri hilo linahusisha mhimili mwingine, yaani Bunge hivyo wanahitaji kupata muda wa kushauriana na Bunge (Spika) ili kuweza kuandaa kiapo kinzani.

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote, Jaji Sirilius Matyupa alisema atatoa uamuzi wa kusitisha mchakato wa kuapishwa kwa mbunge huyo mteule Mtaturu baada ya kusikiliza maombi yote ya Lissu, Agosti 23, mwaka huu.

Katika maombi yake, Lissu anaiomba Mahakama kumwamuru Spika wa Bunge Job Ndugai awasilishe mahakamani taarifa ya kumvua Ubunge aliyoitoa bungeni ili iweze kupitia na kisha iamuru kuutengua na kuutupilia mbali. 

Pia anaomba Mahakama imwamuru Spika ampatie yeye Lissu nakala ya taarifa ya kumvua ubunge

RAS SIMIYU ASITISHA UAMUZI WA DC KUWATAKA WATUMISHI KUCHANGIA FEDHA ZA KUNUNUA MASHINE YA ULTRASOUND ILIYOIBIWA BARIADI

$
0
0
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akizungumza na watumishi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Bariadi, leo Agosti 15, 2019 mjini Bariadi, kwa lengo la kutoa ufafanuzi juu ya kusitisha uamuzi wa watumishi hao kuchangia mashine ya ULTRASOUND iliyoibiwa Agosti 05, 2019 ambao ulitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga hapo jana . 
Watumishi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Bariadi, wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini leo Agosti 15, 2019 mjini Bariadi, kwa lengo la kutoa ufafanuzi juu ya kusitisha uamuzi wa watumishi hao kuchangia mashine ya ULTRASOUND iliyoibiwa Agosti 05, 2019 ambao ulitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga hapo jana . 
Baadhi ya Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Mkoani Simiyu wakiwa katika kikao na Watumishi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Bariadi, leo Agosti 15, 2019 mjini Bariadi, kwa lengo la kutoa ufafanuzi juu ya kusitisha uamuzi wa watumishi hao kuchangia mashine ya ULTRASOUND iliyoibiwa Agosti 05, 2019, ambao ulitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga hapo jana. 
Watumishi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Bariadi, wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini leo Agosti 15, 2019 mjini Bariadi, kwa lengo la kutoa ufafanuzi juu ya kusitisha uamuzi wa watumishi hao kuchangia mashine ya ULTRASOUND iliyoibiwa Agosti 05, 2019. 
Watumishi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Bariadi, wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini leo Agosti 15, 2019 mjini Bariadi, kwa lengo la kutoa ufafanuzi juu ya kusitisha uamuzi wa watumishi hao kuchangia mashine ya ULTRASOUND iliyoibiwa Agosti 05, 2019 ambao ulitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga hapo jana .
Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Mkoa wa Simiyu, Bi. Catherine Nyingi akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani mara baada ya kikao cha uongozi wa Mkoa wa Simiyu na Watumishi wa Watumishi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Bariadi, leo Agosti 15, 2019 mjini Bariadi.
Mtumishi Frola Katoyo akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani mara baada ya kikao cha uongozi wa Mkoa wa Simiyu na Watumishi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Bariadi, leo Agosti 15, 2019 mjini Bariadi.

………………….

Na Stella Kalinga, Simiyu RS 

Uongozi wa Mkoa wa Simiyu kupitia kwa Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Jumanne Sagini umesitisha uamuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga, uliotolewa jana Agosti 14, 2019 ambapo watumishi wote 137 wa Hospitali ya Mji wa Bariadi walitakiwa kukatwa mishahara yao kwa ajili ya kuchangia fedha ya kununua mashine ya ULTRASOUND, iliyoibiwa katika wodi ya wazazi hospitalini hapo badala yake ameagiza vyombo vya dola vifanye uchunguzi kubaini aliyeiba mashine hiyo na hatua stahiki zichukuliwe.

Sagini ameyasema hayo leo Agosti 15, 2019 wakati akizungumza na watumishi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Bariadi katika Ukumbi wa Hospitali hiyo Mjini Bariadi.

Amesema uongozi wa Mkoa umetafakari na kuona kuwa si watumishi wote wa hospitali hiyo wamehusika katika upotevu wa mashine hiyo kwa kuwa wanafanya kazi katika idara tofauti na baadhi yao siku ya tukio hawakuwepo, hivyo ni vema vyombo vya dola vikafanya uchunguzi kubaini waliohusika.

” Uongozi wa Mkoa tunarekebisha baadhi ya hatua zilichukuliwa na Mhe. DC jana, hili jambo haliwezi kuwa la watumishi wote 137, kama Serikali tunavyo vyombo vya dola ambavyo kuna watu wanalipwa mishahara kwa kazi hizo za kiuchunguzi, tunataka kifaa hicho kirejeshwe, vyombo hivi vifanye uchunguzi, vichukue hatua kwa watakaobainika ikiwemo kupelekwa mahakamani” amesema.

Katika hatua nyingine Sagini amewataka watumishi wa Hospitali ya Mji wa Bariadi kuimarisha mfumo wa makabidhiano ya kazi na vifaa vya kazi ili kuwepo na taarifa sahihi za wagonjwa na vifaa tiba kama utaratibu unavyotaka.

Kwa upande wao watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi wamewashukuru viongozi wa Mkoa wa Simiyu kwa kusitisha uamuzi wa awali ambao ungewaathiri kiuchumi na kupunguza ari ya kufanya kazi hususani wale ambao hawajahusika na upotevu wa mashine hiyo.

” Tunamshukuru sana kiongozi wetu kwa msamaha aliotutolea kwa sababu tangu jana tumelala kwa presha baada ya kuambiwa kuwa kila mtu alip, mimi uwezo wangu mdogo na mshahara wangu ni mdogo nilikuwa sioni pesa ya kulipa hicho kifaa;namshukuru Mungu kwa uamuzi wa viongozi wa mkoa yaani naongea kwa uchungu mpaka nasikia kulia kwa furaha niliyonayo” amesema Frola Katoyo Mtumishi katika idara ya dawa.

“Nimepokea vizuri uamuzi uliofanywa na viongozi wetu wa mkoa kwa sababu maanuzi yaliyotolewa jana kiuhalisia si kila mtumishi alipaswa kuhusishwa kwenye hili, maana wengine walikuwa likizo, wengine hawakuwepo kazini, hivyo ni sahihi kabisa kuviachia vyombo vya dola; nina uhakikia kuanzia leo watu watafanya kazi maana jana utendaji kazi ulipungua baada ya kupata tu taarifa kuwa wanapaswa kuchangia” alisema Simon Chisomeko Afisa Afya.

Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Mkoa wa Simiyu, Bi. Catherine Nyingi amesema Chama hicho kinaushukuru uongozi wa mkoa kwa kutambua sheria, kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma na wameiomba Serikali iendelee kuwa macho katika kusimamia sheria, kanuni na taratibu.

Mashine ya kupima magonjwa ya ndani ya mwili wa Binadamu (ULTRASOUND MACHINE) iliripotiwa kuibiwa katika Wodi ya wazazi katika Hospitali ya Mji wa Bariadi Agosti 05, 2019 na jana Agosti 14, 2019 Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akaagiza watumishi wote 137 wa Hospitali hiyo wakatwe fedha kwenye mishahara yao ili mashine hiyo iliyoibiwa inunuliwe.

BENKI KUU YAZITAKA TAASISI ZA KIFEDHA KUZINGATIA UADILIFU

$
0
0
Naibu Gavana wa benki kuu Tanzania (BoT) Dr.Bernard Kibesse amezitaka taasisi za kifedha kuzingatia uwadilifu katika utoaji wa huduma za kifedha hasa katika zama hizi za kidigitali ili kuwahahikishia wateja wao usalama wa fedha zao.

Akizungumza katika kongamano la Taasisi za kifedha za Afrika Mashariki linaloendelea jijini Arusha ,Naibu Gavana amesema kuwa licha ya changamoto za wizi kwa njia za mitandao bado taasisi hizo zina jukumu la kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu Mkubwa kwani ndio nguzo kuu ya huduma hizo.

Aidha amesema kuwa serikali haitasita kuwachukulia hatua taasisi za kifedha zinazokiuka sheria ,maadali na tararibu za utoaji wa huduma ikiwemo kuzinyang'anya leseni .

Nae Mkurugenzi mtendaji wa Tanzania institute of bankers,
Patrick  Mwisusa amesema kuwa kongamano hilo linalenga kuangalia maswala ya nafasi ya maadili katika utoaji wa huduma za kifedha na kuhimiza suala la uadilifu katika kulinda tasnia ya fedha Katika nchi za Afrika Mashariki 

Mshiriki wa kongamano ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi za Kifedha nchini Kenya, Gilbert Allela amesema kuwa taasisi za fedha zina nafasi kubwa ya kulinda na kutunza uaminifu wa wateja wao kwa kujifunza mbinu za kisasa za kukabiliana na wizi wa kimtandao.
Viewing all 110078 articles
Browse latest View live




Latest Images