Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

WAZIRI MHAGAMA AKAGUA MIRADI YA PSSSF NA NSSF MKOANI MWANZA

$
0
0
Msimamizi wa Ujenzi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw. Suleiman Salmin (kushoto) akielezea jambo kuhusu hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa jengo la hoteli ya nyota tano (5) inayojengwa na Mfuko huo, Jijini Mwanza.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akitoa maelezo kwa watendaji wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) alipotembelea kwa lengo la kukagua na kujionea hatua za awali zilizofikiwa katika utekelezaji wa miradi hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akipokea taarifa kutoka kwa Msimamizi wa Ujenzi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw. Suleiman Salmin kuhusu miradi ya ujenzi inayotekelezwa na mfuko huo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akitazama jengo mmoja wapo linalojengwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) wakati ziara yake ya kukagua na kujionea hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa miradi hiyo.PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU

(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)

……………….

Na; Mwandishi Wetu

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ameagiza watendaji wa Mifuko ya hifadhi ya Jamii yaani Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuwa wabunifu katika kuwekeza kwenye vitega uchumi vyenye kuleta tija na inayochochea maendeleo ya Taifa.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa ziara yake Jijini Mwanza alipokuwa akikagua Miradi mbalimbali inayotekelezwa na Mifuko hiyo ya Hifadhi ya Jamii ili kujionea hatua zilizofikiwa katika utekelezaji.

Alieleza kuwa kuwekeza katika miradi yenye tija ni jambo muhimu kwa kuwa miradi hiyo italeta maendeleo endelevu yatakayochangia katika ukuaji wa pato la taifa na ustawi wa mkoa huo.

“Mwanza ni miongoni mwa Mikoa yenye fursa nyingi za kibiashara kutokana na sehemu kubwa ya mkoa huo kuzungukwa na ziwa viktoria, hivyo kurahisisha ukanda huo kufikiwa kwa urahisi na soko la Afrika Mashariki,” alisema Mhagama.

Alifafanua kuwa ubunifu katika kutekeleza shughuli za mifuko ni pamoja na kutafuta masoko ya vitenga uchumi ya miradi hiyo kwa kuangalia fursa zilizopo kwenye kanda ya ziwa.

Aliongeza kuwa fursa ni pamoja na ujenzi wa daraja la Busisi litakalopita ziwa viktoria, Mbuga ya Wanyama ya Burigi pamoja na shughuli za uchimbaji madini zilizopo katika mkoa huo.

Katika Ziara hiyo Waziri Mhagama aliweza kutembelea linapojengwa Soko la Madini katika Jengo la Kibiashara la Rock City Mall. Pia alitembelea jengo la PSSSF Mwanza na alipata fursa ya kukagua shughuli za uwekezaji katika jengo hilo zinazoendeshwa na wawekezaji wazawa katika Hoteli ya Gold Crest.

NAIBU SPIKA AZINDUA BARAZA LA WAFANYAKAZI OFISI YA BUNGE

$
0
0
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akimkabidhi Katibu wa Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai Mkataba kwa ajili ya kuunda Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Bunge mara baada ya kuzindua Baraza hilo. Uzinduzi huo umefanyika katika Ofisi Ndogo za Bunge, Tunguu Zanzibar
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akimkabidhi Katibu Mkuu wa TUGHE Taifa, Ndugu Hery Mkunda Mkataba kwa ajili ya kuunda Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Bunge baada ya uzinduzi. Uzinduzi huo umefanyika katika Ofisi Ndogo za Bunge, Tunguu Zanzibar
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akimkabidhi Katibu Mkuu wa TUGHE Taifa, Ndugu Hery Mkunda Mkataba kwa ajili ya kuunda Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Bunge baada ya uzinduzi. Uzinduzi huo umefanyika katika Ofisi Ndogo za Bunge, Tunguu Zanzibar.





Katibu wa Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai (katikati) akiimba wimbo wa mshikamano wa Wafanyakazi kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Bunge uliofanyika katika Ofisi Ndogo za Bunge, Tunguu Zanzibar pamoja na Ndugu Chacha Nyakega Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Ofisi ya Bunge na Ndugu Triphonia Mng’ong’o Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu.
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Bunge uliofanyika katika Ofisi Ndogo za Bunge, Tunguu Zanzibar

SERIKALI KUJA NA SHERIA YA KUKOMESHA UDUKUZI WA MAWASILIANO NCHINI

$
0
0
Na Said Mwishehe,Michuzi TV 

NAIBU Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashanta Nditiye amesema Serikali inao mkakati wa kupeleka bungeni muswada kwa ajili ya kulinda taarifa binafsi za mtu, lengo likiwa ni kulinda mawasiliano binafsi na kufanya udukuzi.

Mhandisi Nditiye ameyasema hayo leo Agosti 14 , mwaka 2019 wakati anazungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam alipokuwa akielezea mikakati ya wizara hiyo kwa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC).

Hivyo pamoja na kutoa maelezo ya mikakati hiyo ya Wizara, Mhandisi Nditiye aliulizwa iwapo Wizara imeweka mkakati wowote kudhibiti udukuzi wa kuingilia taarifa za mtu binafsi na namna ilivyojipanga kukabiliana na uhalifu wa mtandaoni.

“Matumizi sahihi ya mawasiliano nchini bado yana changamoto na pamoja na juhudi zilizoweka kupambana na wote wanaochafua wenzao kupitia mawasiliano.Tutapeleka muswada wa sheria bungeni mwaka huu.

“Tunapambana na wote wanaochafua wenzao kwa mawasiliano ya simu, Mamlaka yetu ya Mawasiliano (TCRA) kwa kushirikiana na kitengo cha uhalifu wa mtandaoni (Cyber Crime) katika Wizara ya Mambo ya Ndani, tunashirikiana katika hili,” amesisitiza Mhandisi Ndetiye.

Hata hivyo kwa mujibu wa Mhandisi Ndetiye, amesema asilimia 98 ya mawasiliano ya ujanja ujanja wa kuunganisha simu za kimataifa zimedhibitiwa nchini.

Ameongeza sekta ya mawasiliano ni mtambuka na imeendelea kuchangia mapato ya Serikali kutoka asilimia 13.1 mwaka 2017 hadi asilimia 14.7 mwaka 2018 huku akieleza kipaumbele ni kuona inachangia zaidi.

Wakati huo huo Mhandisi Nditiye amesema kwa sasa nchini Tanzania watumiaji wa simu wamefikia milioni 43.6 na wa mtandao wa intaneti wamefikia watumiaji milioni 23.140.Hivyo sekta ya mawasiliano ikitumika vizuri ni muhimili mkubwa wa maendeleo ya uchumi nchini.

Kwa upande wa malengo ya kikanda, amesema nchi ya Tanzania inamkakati wa kuziunganisha nchi zote za jumuiya hiyo kwenye Mkongo wa Taifa kwa lengo la kuhakikisha nchi hizo zinakuwa na uhakika wa mawasiliano kwa ajili ya kuleta maendeleo.

Amefafanua tayari serikali ya Tanzania imeziunganisha nchi mbili za Zambia na Msumbiji na nne za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo ni Uganda , Kenya, Burundi na Rwanda. “Mkakati uliopo kupitia Mkongo wa Taifa tunampango wa kuzifikia nchi zote za SADC”.

NAIBU Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashanta Nditiye akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam alipokuwa akielezea mikakati ya wizara hiyo kwa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC),ambapo pia kulifanyika hafla fupi ya uzinduzi wa machapisho matano yaliyotayarishwa na Kituo cha Utafiti kwa nchi za SADC.Picha na Michuzi JR.

ALIYEOMBA RUSHWA YA NGONO KWA MWANAFUNZI WAKE APANDISHWA KIZIMBANI

$
0
0
Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

MHADHIRI Wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Samsoni Mahimbo (68), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na tuhuma za kuomba rushwa ya ngono kwa mwanafunzi wake.

Akisoma hati ya mashtaka wakili wa serikali kutoka Takukuru Vera Ndeoya amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shahidi amedai, mshtakiwa alitenda kosa hilo Januari 12 , 2017 huko katika nyumba ya kulala wageni ya  Camp David  iliyoko Mlalakuwa Mwenge.

Imedaiwa, Siku ya tukio, mshtakiwa akiwa  muajiriwa wa chuo hicho cha NIT kama mhadhiri kwa muhula wa kwanza wa masomo wa mwaka 2015/2016 wa somo la usimamizi wa barabara na usafirishaji (road transport management), lenye kodi namba 07101 alitumia mamlaka yake kutokana na nafasi yake chuoni hapo na kuomba rushwa ya ngono kutoka kwa mwanafunzi, Victoria Faustine ambae ni mwanafunzi wa chuo hicho  anayosomea mafunzo hayo ya road transport management.

Imeendelea kudaiwa kuwa, mshtakiwa aliomba rushwa hiyo kama sharti kwa mwanafunzi huyo kuwa atamfaulisha katika mtihani wa marudio (Supplement) wa somo hilo  uliokuwa ukifanyika January 5, 2017.

Hata hivyo mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo yuko nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana ambapo Mahakama ilimtaka kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini bondi ya sh. Milioni nne

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo umekamilika. Kesi hiyo imeahirishwa hadi  Septemba 17,2019 mshtakiwa atakaposomewa Maelezo ya awali.

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MKURUGENZI WA UN WOMAN

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amelitaka Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshuhulikia Wanawake Duniani  (UN WOMAN)  kuandaa Tathmini ya kinchi kuhusiana na Kongamano la Beijing.

Amesema ni Vyema kuwepo na uwezekano wa kuweza kuandaa Tathmini ya uhakika itakayoweza kuonesha hali halisi ya Idadi ya Wanawake waliopo katika Nafasi mbalimbali za Kiuongozi hususan kwenye Baadhi ya Mashirika na Taasisi Binafsi.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo Agost 14, 2019 Ofisini kwake Ikulu Jijini Dar Es Salaam wakati alipokutana na kuzungumza na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshuhulikia Wanawake Duniani (UN WOMAN) Bibi Hodan Addou.

 Aidha Makamu wa Rais amelishukuru Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshuhulikia Wanawake Duniani  (UN WOMAN) kwa kuendelea kuweza kutoa fursa katika nyanja mbalimbali za Kijamii na kimaendeleo kwa Wanawake Duniani na kulitaka Shirika hilo kuendelea kuzidi kutoa fursa hizo kwa Wanawake Hususan kwenye sekta za Kilimo.

Nae Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshuhulikia Wanawake Duniani Bibi Hodan Addou aliyeambatana na Bw. Denis Maro Biseko Mwakilishi wa Benki ya Dunia hapa Nchini,  amemshukuru Mhe. Makamu wa Rais kwa kuweza kuimarisha Ulizi wa Masoko kwa kuzuwia Utumikishaji wa Wanawake na watoto Masokoni. Ambapo pia amesema Shirika hilo kwa kushirikiana na Benki ya Dunia wameandaa Warsha itakayozungumzia kuhusu Wanawake kuweza kutambua hali zao kwenye suala zima la Biashara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshuhulikia Wanawake Duniani (UN WOMAN) Bibi. Hodan Addou wakati Bibi Addou alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Jijini Dar Es Salaam leo Agost 14,2019 kwa ajili ya kumshukuru Makamu wa Rais kwa kuweza kuimarisha Ulizi wa Masoko kwa kuzuwia Utumikishaji wa Wanawake na watoto Masokoni ambapo pia amesema Shirika hilo kwa kushirikiana na Benki ya Dunia wameandaa Warsha itakayozungumzia kuhusu Wanawake kuweza kutambua hali zao kwenye suala zima la Biashara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimina na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshuhulikia Wanawake Duniani(UN WOMAN) Bibi. Hodan Addou wakati Bibi Addou alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Jijini Dar Es Salaam leo Agost 14,2019 kwa ajili ya kumshukuru Makamu wa Rais kwa kuweza kuimarisha Ulizi wa Masoko kwa kuzuwia Utumikishaji wa Wanawake na watoto Masokoni ambapo pia amesema Shirika hilo kwa kushirikiana na Benki ya Dunia wameandaa Warsha itakayozungumzia kuhusu Wanawake kuweza kutambua hali zao kwenye suala zima la Biashara.

SADC YATAJA YANAYOKWAMISHA KUTEKELEZWA KWA MIKAKATI YA KIMAENDELEO WALIYOJIWEKEA

$
0
0
Na Said Mwishehe, Michuzi TV 

KATIBU Mkuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Dk.Stergomena Tax amezitaka nchi za jumuiya hiyo kuhakikisha mikakati yao ya kimaendeleo kwa kila nchi inauwiana na ile ya mikakati iliyowekwa na jumuiya hiyo.

Amesema changamoto kubwa iliyopo sasa ni kwamba kumekuwa na mikakati mizuri ya maendeleo kwa nchi za SADC lakini inakwama kutekelezeka kwasababu ya kutoendana na mikakati ya maendeleo ya nchi wanachama, hivyo ni vema kukawa na mikakati inayoendana.

Dk.Tax amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati uzinduzi wa Machapisho Matano yalioandaliwa na Kituo cha Utafiti na Machapisho Kusini mwa Afrika (SARDC) .Machapisho yaliozinduliwa la kwanza ni Mkakati wa SADC kuwajumuisha wanawake kwenye ulinzi na usalama ambalo limelenga kuwashirikisha wanawake katika eneo hilo la ulinzi na usalama.

Chapisho la pili linalozungumzia ufuatiliaji wa usawa wa kijinsia kwenye maendeleo alisema nchi nyingi za SADC bado zina hali mbaya wakati chapisho la tatu linazungumzia mkakati na mpango wa kushughulikia ukatili wa kijinsia, ufatiliaji wa maendeleo ya nishati na mpango mfupi wa kutathmini maendeleo ya miundombinu.

Akizungumzia zaidi wakati anaelezea machapisho hayo ,Dk.Tax amesema pamoja na uzuri wa machapisho hayo amesema kwa sasa kuna changamoto mbili kubwa ambazo zinazokwamisha utekelezaji wa mipango yao kwa nchi wanachama.

“SADC imekuwa ikiandaa mipango mingi mizuri kwa nchi wanachama lakini changamoto kubwa ni nchi kushindwa kutekeleza mikakati iliyopo. Changamioto hizo ni nchi wanachama kushindwa kuhuisha mipango ya SADC kwenye mipango ya kitaifa. Iwapo mipango haiwekwi kwenye mipango ya kitaifa ni vigumu utekelezaji kufanyika kwa wakati,”amesema Dk.Tax.

Pia amesema changamoto nyingine ni sekta binafsi kutoshiri kikamilifu kwenye ujenzi wa miundombinu na kuongeza kwa mujibu wa tathmini iliyofanywa na SARDC kati ya mipango 134 ambayo SADC walikubaliana utekelezaji ni asilimia 5 tu hali ambayo inatoa picha mbaya ya kufikia uchumi wa viwanda.

Hivyo ameshauri kwamba ni vema nchi za jumuiya hiyo pamoka na kuweka vipaumbele vyao, ni vema kukawa na mikakati ambayo inausiano na ile ya SADC ili kuhakikisha yote ambayo wanakubaliana yanatekelezwa na nchi wanachama.

Kuhusu machapisho hayo yaliyozinduliwa Mkurungezi Mkuu wa SARDC, Munetsi Madakufamba amesema kuwa machapisho hayo kwa sehemu kubwa yameonesha njia sahihi ya nchi wanachama wa SADC kufikia maendeleo jumuishi.

Amesema chapisho la kwanza la Mkakati wa SADC kuwajumuisha wanawake kwenye ulinzi na usalama na kufafanua kwa muda mrefu wanawake wa jumuiya hiyo wamekuwa wakiachwa nyuma na sasa umefika wakatu wa kuwashirikisha.

Akizungumzia chapisho la pili amesema limejikita katika ufuatiliaji wa usawa wa kijinsia katika maendeleo na kwamba chapisho hilo linaonesha bado nchi nyingi ziko kwenye hali mbaya, hivyo kuna kilasababu ya kuweka mikakati madhubuti. “Moja ya makubaliano ni kuwa na usawa wa kijinsia wa asilia 50 kwa 50 lakini ukweli uliopo bado nchi nyingi za jumuiya hiyo zimeshindwa kufikia lengo hilo.

"Katika eneo hili nchi ambazo zimefanya vizuri ni Afrika Kusini na Shelisheli ambapo uwakilishi upo 50/50 na kwa upande wa Tanzania nayo imejitajidi sana kwani imefikia asilimia huku asilimia 37.Hata hivyo amesema iwapo nchi zote wanachama zitashirikiana kwa pamoja kwa kuweka mikakati yao kwa mipango ya taifa ni dhahiri mafanikio yataonekana.

Wakati huo huo Mjumbe wa Bodi ya SARDC, Madaraka Nyerere amesema kwamba kituo hicho cha utafiti kimejikita katika kufanya tafiti katika ukanda huo kwa lengo la kusaidia sekretarieti ya SADC kufanya kazi zake za kuchochea maendeleo kwa usawa.

Kwa upande wake Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema Tanzania imekuwa ikitekeleza makubaliano ya SADC hatua kwa hatua huku akilezea namna ambavyo Serikali imeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha mwanamke anapata nafasi na kupewa kipaumbele.

‘Serikali imekuwa ikitekeleza makubaliano hayo kwa kutoa mikopo kwa wakina mama ambapo zaidi Sh. bilioni 3 zimetolewa. Pia kuna ongezeko la ushiriki wanawake kwenye vikao vya maamuzi kutoka asilimia 22 mwaka 2010 hadi 37 kwa sasa.Pia uamuzi wa Serikali kutoa elimu bure umesaidia kuongeza idadi ya watoto wa kike kujiunga na elimu ya msingi na sekondari,”amesema.
Katibu Mkuu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Stergomena Tax akiwa pamoja na viongozi wengine wakizindua Machapisho Matano yalioandaliwa na Kituo cha Utafiti na Machapisho Kusini mwa Afrika (SARDC).Pichani kutoka kulia ni Waziri wa Nishati Dkt. Merdad Kalemani, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na kutoka kushoto ni  Mjumbe wa bodi ya Kituo cha Utafiti na Machapisho cha Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC),Madaraka Nyerere  pamoja na  Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Utafiti na Machapisho cha Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC),Munetsi Mdakufamba .
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Dk.Stergomena Tax akizungumza na waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi wa machapisho matano yaliyotayarishwa na Kituo cha Utafiti kwa nchi za SARDC ,leo jijini Dar,ambapo moja ya machapisho hayo yanazungumzia mkakati wa nishati ya meme wa uhakika kwa nchi za jumuiya hiyo katika kuleta maendeleo.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi wa machapisho matano yaliyotayarishwa na Kituo cha Utafiti kwa nchi za SADC ,leo jijini Dar,Waziri Ummy alieleza namna ambavyo Tanzania imekuwa ikitekeleza makubaliano ya SADC hatua kwa hatua,na kufafanua zaidi Serikali ilivyoweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha mwanamke anapata nafasi na kupewa kipaumbele.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Utafiti na Machapisho cha Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SARDC),Munetsi Mdakufamba akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani),Wakati wa hafla ya uzinduzi wa machapisho matano yaliyotayarishwa na Kituo cha Utafiti kwa nchi za SADC,leo jijini Dar.
Mjumbe wa bodi ya Kituo cha Utafiti na Machapisho cha Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SARDC),Madaraka Nyerere (Mtoto wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere), akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani),Wakati wa hafla ya uzinduzi wa machapisho matano yaliyotayarishwa na Kituo cha Utafiti kwa nchi za SADC ,leo jijini Dar.
Pichani ni machapisho hayo yakiwa tayari kuzinduliwa rasmi
Baadhi ya Wageni waalikwa na Waandishi wa habari wakishuhudia tukio la uzinduzi wa machapisho matano yaliyotayarishwa na Kituo cha Utafiti kwa nchi za SADC ,leo jijini Dar

RASILIMALI ZINAZOPATIKANA NDANI YA JUMUIYA YA SADC ZITUMIKE KUNUFAISHA NCHI WANACHAMA

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

NCHI wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) zimeshauriwa kutumia rasilimali zinazopatikana katika jumuiya hiyo kunufaisha wananchi walio ndani ya jumuiya na hiyo ni pamoja na uwekaji wazi wa mikataba ambayo serikali inaingia na makampuni mbalimbali hasa katika sekta za madini, mafuta na gesi asilia.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam mwenyekiti wa taasisi ya kimataifa ya uhamasishaji na uwajibikaji wa mapato yatokanayo na sekta ya uziduaji (mafuta, gesi asilia na madini) Ludovick.

Utouh amesema kuwa tukio la leo ni mwendelezo wa mikutano wa SADC inayoendelea nchini kabla ya kuhitimishwa kwa mkutano wa wakuu wa nchi na serikali utakaofanyika Agosti 17 na 18 na mazungumzo hayo yamezungumzia juunya uwekaji wazi wa mikataba ambayo serikali inaingia na wawekezaji katika rasilimali za madini, mafuta na gesi asilia rasilimali ambazo nyingi hugunduliwa na wananchi lakini hawashirikishwi katika masuala hayo hali inayopelekea hata kuzuka kwa vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Amesema kupitia taasisi kimataifa ya uhamasishaji na uwajibikaji wa mapato yanayotokana na sekta ya uziduaji yenye makao makuu nchini Norway na yeye akiwa mwenyekiti wamedhamiria kuwa hadi kufikia mwaka 2021 nchi zote wanachama wa SADC ziwe na utaratibu wa kuweka mikataba wazi ambapo hadi sasa nchi nane wanachama ikiwemo Tanzania wamekwisha weka mikataba yao wazi ili wananchi waweze kujiridhisha na kile ambacho kinafanywa juu ya rasilimali hizo.

Aidha amesema kuwa nchi nane ambazo ni wanachama ikiwemo Tanzania tayari zimeweka mikataba ya sekta ya uziduaji hadharani na nchi mbili ambazo sio wanachama wa taasisi hiyo ya kimataifa wameweka wazi mikataba yao na nchi sita ambazo ni wanachama wa SADC bado hazijaweka wazi mikataba yao ambayo kwa ujumla ambayo husaidia kupunguza rushwa na kuweka uwazi kwa wananchi, serikali na wawekezaji Kama ikiwekwa wazi.

Pia Utouh ameeleza kuwa nchi za Afrika Zina rasilimali za kutosha ambazo haziwezi kudumu milele hivyo ni vyema mapato yatokanayo na rasilimali hizo yakaelekezwa kwenye maendeleo ya kizazi cha Sasa na baadaye.

Kwa upande wake mratibu wa shirika la Zimbabwe Environment Legal Association Nyaradzo Mutonhori amesema kuwa ni haki ya kila mwananchi kujua uwazi wa mikataba inayoingiwa na wawekezaji;

" Tuna haki ya kujua kwa uwazi kabisa juu ya mikataba hiyo, kwa kuwa tunawaona wawekezaji hivyo tungependa kujua wanachochukua na wananchi wanavyonufaika, pia kuweka wazi mikataba hiyo Kuna faida kwa wananchi kuibariki." ameeleza Nyaradzo.

Nyaradzo amesema kuwa nchi wanachama wa SADC waangalie namna ya kuondoa usiri baina ya serikali na kampuni mbalimbali za uwekezaji pamoja na kubainisha muda mahususi ambao kampuni za uwekezaji umewekeza katika rasilimali husika.

Kwa upande wake mratibu wa mtandao wa haki rasilimali nchini Rachel Chagonja amesema kuwa rasilimali zinazopatikana katika nchi jumuiya za SADC ni vyema zikatumika kunufaisha nchi wanachama wa jumuiya hiyo na sio kufuja rasilimali hizo bila kuangalia kizazi kijacho kitanufaika vipi, hivyo suala la uwazi wa mikataba lazima lizingatiwe ili keki ya taifa igawanywe kwa usawa.

Rachel ameeleza kuwa rasilimali sio za watu wachache na serikali ndio madalali wa wananchi hivyo mrejesho wa namna rasilimali hizo zinavyotumika ni muhimu kuwa wazi pamoja kueleza namna mapato ya rasilimali hizo yanavyochangia katika sekta za maendeleo.
Wawasilishaji wa mada mbalimbali wakiwa katika picha pamoja, leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa taasisi ya kimataifa ya uhamasishaji na uwajibikaji wa mapato yanayotokana na sekta ya uziduaji (mafuta, madini na gesi asilia) Ludovick Utouh akizungumza katika mkutano huo ambapo ameeleza kuwa kuwekwa wazi kwa mikataba kunasaidia katika kupunguza rushwa pamoja na kuweka uwazi kwa wananchi, serikali na wawekezaji leo jijini Dar es Salaam.
Mtoa mada kutoka nchini Botswana Robert Letsatsi akichangia mada katika mkutano huo ambapo ameeleza kuwa nchi jumuiya lazima ziangalia kwa jicho la tatu masuala ya rushwa, uwazi na usawa ili kuweza kufika mbali zaidi leo jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa shirika la Zimbabwe Environment Legal Association (ZELA) Nyaradzo Mitonhori akizungumza katika mkutano huo na kueleza kuwa nchi jumuiya ya SADC ziangalie namna ya kuondoa usiri baina ya serikali na kampuni za uwekezaji leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania, Zimbabwe, Botswana na Msumbiji wakifuatilia mkutano huo, ambapo kwa kiasi kikubwa suala la uwazi wa mikataba baina ya serikali na kampuni za uwekezaji limejadiliwa, leo jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa mtandao wa haki rasilimali nchini Rachel Chagonja akizungumza katika mkutano huo ambapo ameeleza kuwa serikali ndio dalali kwa wananchi wake hivyo lazima waangalie suala la uwazi ili kila mwananchi anufaike na rasilimali hizo leo jijini Dar es Salaam.

POLISI PWANI WAWAKAMATA WATU TISA KUTOKANA NA UTAPELI WA SIMU

$
0
0
JESHI la polisi mkoani Pwani, limekamata watu Tisa wanaodaiwa kujihusisha na matukio ya utapeli kwa kutumia simu za mkononi na laini za simu kutoka makampuni mbalimbali na orodha ya namba za simu za watu .

Watu hao ,walikuwa wakituma ujumbe mfupi sms,kwamba watumiwe pesa na kujifanya waganga wa jadi wanazindika,kusafisha nyota za watu, ndoa na biashara.

Akithibitisha kuhusiana na tukio hilo ,kamanda wa polisi mkoani Pwani, Wankyo Nyigesa alieleza, agost 13 mwaka huu,kata ya Zinga na Yombo wilayani Bagamoyo,walikamatwa watuhumiwa hao wakiwa na simu za mkononi 14,laini za simu za makampuni mbalimbali 22 na orodha ya namba ya simu za watu 16 zilizoorodheshwa kwenye karatasi.

Aliwataja majina yao kuwa ni, Suleimani Athuman (35), Hamis Iddi (30), Dipinde Pango,Adam Nestory,Hamis Kondo,Deus Swai , Julius Joseph(27) na Mohammed Bruno (33) .

Wankyo alibainisha kuwa ,watuhumiwa hao wanahojiwa ni namna gani wanafanya uhalifu wao kwa kutumia mtandao ya simu na kufanya wizi wa pesa kwa kuchepusha salio la pesa ya mtu kwa makusudi ya uhalifu.

"Watafikishwa mahakamani baada ya mahojiano na uchunguzi kukamilika"alifafanua kamanda huyo.

Wankyo aliitaka jamii kufanya shughuli halali za kujiongezea kipato badala ya kufanya uhalifu.

WAZIRI MASAUNI AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI VISIWANI ZANZIBAR

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati wa Kikao cha Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani Visiwani Zanzibar, kulia ni Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Elias Kwandikwa.
Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Elias Kwandikwa ambae pia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani,Elias Kwandikwa akizungumza wakati wa Kikao cha Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani Visiwani Zanzibar.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini,Kamishna Mwandamizi Msaidizi, Fortunatus Musilimu, akizungumza wakati wa Kikao cha Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani Visiwani Zanzibar.
Mjumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani,Hamza Kasongo akizungumza wakati wa Kikao cha Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani Visiwani Zanzibar.
Mjumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani,Henry Bantu akizungumza wakati wa Kikao cha Wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani Visiwani Zanzibar. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

WFT YAKUTANA NA WADAU KUJADILI MBINU ZA KUKOMESHA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO SHINYANGA

$
0
0
Mratibu wa Mradi wa Kusaidia Utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Kuzuia Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto mkoa wa Shinyanga, Glory Mbia akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa haki za wanawake na watoto leo. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Shirika lisilo la kiserikali la Women Fund Tanzania (WFT) linalohusika na utetezi wa haki za wanawake,watoto na ujenzi wa tapo ya wanawake nchini Tanzania limekutana na wadau wa haki za wanawake na watoto halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ili kujadili namna ya kutekeleza Mradi wa Kuwezesha Utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Kuzuia Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Mkutano huo umefanyika leo Jumatano Agosti 14,2019 katika ukumbi wa Karena Hoteli na kukutanisha pamoja maafisa wa serikali ngazi ya halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na mkoa,viongozi wa dini,waandishi wa habari,wawakilishi wa baraza la watoto, na asasi za kiraia zinajishughulisha na utetezi wa haki za wanawake na watoto.

Mratibu wa Mradi wa Kusaidia Utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Kuzuia Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto mkoa wa Shinyanga, Glory Mbia alisema lengo la mkutano huo ni kuwafahamisha wadau wa utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kuhusu mradi huo. "Tumekutana hapa ili kuwafahamisha hatua tuliyofikia katika utekelezaji wa mradi huu ili tuweze kuunganisha jitihada za kuondoa ukatili kwa wanawake na watoto lakini pia kubaini na kujadili changamoto ambazo wadau wanakutana nazo katika utekelezaji wa MTAKUWWA",alisema Mbia.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa MTAKUWWA katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa kipindi cha Mwezi Aprili hadi Juni mwaka huu,Afisa Ustawi wa Jamii wa halmashauri hiyo,Elizabeth Mweyo alisema tayari wameunda kamati za MTAKUWWA katika kata zote 26 na vijiji vyote 126 kati ya hizo kamati tano za ngazi ya kata zimejengewa uwezo. Alisema kupitia vikundi hivyo wameendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu madhara ya mila na desturi zinazochangia kuwepo kwa ukatili dhidi ya wanawake na watoto pamoja na kuhamasisha wananchi kujikwamua kiuchumi kupitia shughuli za vikundi. 

Nao wadau walioshiriki walizitaja baadhi ya changamoto zinazosababisha kuendelea kuwepo kwa vitendo vya ukatili katika jamii kuwa ni wananchi kutokuwa tayari kutoa ushahidi mahakamani kuhusu matukio ya ukatili huku wakiwanyooshea vidole baadhi ya Madaktari wasio waaminifu ambao wamekuwa hawatoi ushirikiano kwa kutofika mahakamani kutoa ushahidi mahakamani kuhusu matukio ya ukatili wanayopokea. 
Mratibu wa Mradi wa Kusaidia Utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Kuzuia Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto mkoa wa Shinyanga, Glory Mbia akielezea lengo la mkutano wa wadau wa haki za wanawake na watoto uliofanyika leo katika ukumbi wa Karena Hoteli Mjini Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog 
Mratibu wa Mradi wa Kusaidia Utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Kuzuia Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto mkoa wa Shinyanga, Glory Mbia akizungumza kwenye mkutano huo.
Afisa Ustawi wa Jamii wa halmashauri ya Shinyanga ,Elizabeth Mweyo akizungumza katika mkutano wa wadau wa haki za wanawake na watoto.
Mkuu wa Progamu kutoka Women Fund Tanzania, Carol Francis Mango akiwasilisha mada kuhusu Mradi wa Kuwezesha Utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Kuzuia Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Wadau wa haki za wanawake na watoto wakiwa ukumbini. 
Mwakilishi wa BAKWATA Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Hemed Rashid akichangia hoja wakati wa mkutano huo.
Mwenyekiti wa Baraza la watoto kijiji cha Singita kata ya Usanda halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Stevi Peter Kienze akiomba taarifa za matukio ya ukatili zinapotolewa zifanyiwe kasi haraka ili kukomesha vitendo hivyo katika jamii.
Afisa Ustawi wa Jamii mkoa wa Shinyanga ,Lydia Kwesigabo akizungumza wakati wa mkutano huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la AGAPE ACP, John Myola akizungumza katika mkutano huo wa wadau wa haki za wanawake na watoto. 
Mkutano unaendelea. 
Rehema Katabi kutoka shirika la PWWCO akichangia hoja wakati wa mkutano huo.
Mkaguzi Msaidizi wa Polisi kutoka Dawati la Jinsia na Watoto mkoa wa Shinyanga,Victoria Maro akizungumza kwenye mkutano huo.
Afisa kutoka Women Fund Tanzania,Neema Msangi akitoa mada kuhusu mahusiano kati ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto. 
Mdau kutoka shirika la TAI, Jonathan Kifunda akichangia hoja wakati wa mkutano huo. 
Wadau wakiwa ukumbini. 
Mkutano unaendelea.

WAZIRI MKUU AFUNGUA KONGAMANO LA WIKI YA UWEKEZAJI NA MWONGOZO MKOANI KAGERA

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizindua kitabu cha muongozo wa uwekezaji katika Mkoa wa Kagera, baada ya kufungua Kongamano la Wiki ya Uwekezaji Mkoa wa Kagera na Mwongozo wa Uwekezaji mkoani humo. Agosti 14.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi, baada ya kufungua kongamano la uwekezaji mkoani Kagera, Agosti 14.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akioneshwa maeneo ya uwekezaji Mkoa wa Kagera na Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba, Benard Limbe, kabla ya kufungua kongamano la uwekezaji mkoani Kagera, Agosti 14.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wajasiriamali wa kikundi cha Wanawake cha Bezaleli, wakati akikagua mabanda, kabla ya kufungua kongamano la uwekezaji mkoani Kagera, Agosti 14.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwa ameshika madini ya kopa, akifafanuliwa jambo na Mkurugenzi wa Tanzania Plus Minerals Kyerwa, Salim Mhando, wakati akikagua mabanda, kabla ya kufungua kongamano la uwekezaji mkoani Kagera, Agosti 14.2019.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia mvinyo uliyotengenezwa kwa kutumia ndizi, wakati akikagua mabanda, kabla ya kufungua kongamano la uwekezaji mkoani Kagera, Agosti 14.2019. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kagera Women Group, Bertha Kokulengya, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali, Marco Gaguti. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwasili mkoani Kagera, kwa ajili ya kufungua Kongamano la Wiki ya Uwekezaji Mkoa wa Kagera na Mwongozo wa Uwekezaji mkoani humo. Agosti 14.2019.
…………………….

*Azitaka halmashauri nchini kuondoa urasimu, vikwazo kwa wawekezaji

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwaamezindua Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Kagera wenye lengo la kutangaza fursa za Uwekezaji na hivyo, kukuza maendeleo ya mkoa huona ameziagiza halmashashauri zote za wilaya nchini ziondoe urasimu na kupunguza vikwazo kwa wawekezaji.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Agosti 14, 2019) wakati akizindua Kongamano la Wiki ya Kagera na Mwongozo wa Uwekezaji mkoani Kagera, lilifanyika Bukoba mjini.Amewataka Watanzania wahakikishe wanachangamkia fursa za biashara zilizopo.

Amesema Watanzania wanao uwezo wa kutumia fursa za uwekezaji na biashara zilizopo nchini kwa kushirikiana na taasisi za kifedha na kuwekeza katika miradi mbalimbali nchini, badala ya kuachia fursa hizo kuchukuliwa na wageni.

Amesema azma ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli ya kukuza uchumi kupitia sekta ya na kufikia wa kati ifikapo mwaka 2025 itaendelea kutekelezwa, hivyo, ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji wa nje nao waje kuwekeza.

“Serikali itaendelea kusimamia utekelezaji wa Sera ya Maendeleo Endelevu ya Viwanda Awamu ya Tatu (2010/2020) na Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2015/2016 2020/2021) ambao lengo lake ni kuendeleza uchumi wa viwanda”.

Akizungumzia kuhusu maadhimisho ya Wiki ya Uwekezaji Kagera, Waziri Mkuu amesema yamelenga kuwakutanisha wadau wa uwekezaji, ambao ni pamoja na Wafanyabiashara kutoka ndani ya mkoa na nchi jirani zinazozunguka Mkoa wa Kagera.

“Ni ukweli usiofichika kwamba tunahitaji wawekezaji watakaosaidia uchumi wa mkoa huu kukua kwa kasi kupitia fursa zilizopo kwenye nyanja za kilimo, mifugo, uvuvi, viwanda, maliasili na utalii”.

Waziri Mkuu amesema ukuaji mzuri wa uchumi wa mkoa utakuwa na manufaa katika kuongezeka kwa pato la mwananchi wa Kagera, pato la mkoa na hata pato la Taifa nalo litakuwa kwa kasi ndani ya kipindi cha muda mfupi.

Amesema mkoa wa Kagera ndiyo unaoongoza kwa uzalishaji wa kahawa nchini, ambapo zaidi ya nusu ya kahawa yote huzalishwa katika mkoa huo. Wastani wa uzalishaji wa kahawa kwa mwaka ni kati ya tani 50,000 hadi tani 65,000 kutegemea na hali ya hewa ya mwaka husika.

Hivyo, mkoa huo una fursa kubwa ya uwekezaji kwenye viwanda vya kukoboa na kusindika kahawa.Pia mkoa wa Kagera ni miongoni mwa mikoa michache Tanzania yenye fursa nyingi za uwekezaji ambazo kwa namna moja au nyingine hazipatikani katika mikoa mingine ya nchini. Miongoni mwa fursa hizo ni pamoja na soko kwani unapakana nan chi nne za Afrika Mashariki.

“Kagera imepakana na Uganda, Rwanda, Burundi na Kenya. Kupakana na nchi hizo zenye idadi kubwa ya watu katika ukanda huu wanaokadiriwa kufikia takriban milioni 190 ambapo kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2018 ni fursa ya uwepo wa soko kubwa la bidhaa zinazozalishwa au zinazoweza kuzalishwa katika mkoa wa Kagera”.

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema Serikali imeendelea kuboresha miundombinu mbalimbali ya usafiri ukiwemo wa anga na wa barabara ili kurahisisha usafiri kutoka Bukoba makao makuu ya mkoa wa Kagera kufika katika nchi hizo.

“Kwa mfano, umbali kutoka Bukoba hadi Kampala ni km. 340, Bujumbura km. 550 na Kigali km. 490. Kadhalika, itakuwa ni rahisi kufikia masoko ya nchi za Sudan Kusini pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Kongo (DRC)”.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti alisema dhamira ya kuandaliwa kwa wiki ya uwekezaji mkoani Kagera ina lengo la kuhakikisha kwamba mkoa huo unafanya vizuri katika sekta ya uwezekezaji na biashara, hivyo kuchangia katika ukuaji wa pato la Taifa.

Alisema mkoa wa Kagera ni miongoni mwa mikoa 10 ambayo inamchango mdogo katika pato la Taifa, hivyo wanataka watoke kwenye kuchangia asilimia 3.9 hadi wafikie asilimia 10.

Kwa upande wao, viongozi mbalimbali wakiwemo Magavana kutoka na wafanyabiashara kutoka nchi za Rwanda na Burundi waliahidi kutumia fursa zilizopo nchini, pamoja na kuwakaribisha wafanyabiashara na wawekezaji wa Tanzania kwenda kuwekeza katika nchi zao.

CHUO KIKUU CHA ST.JOSEPH KIMEKADIRIA KUKUSANYA DAMU LITA 10O KWA AJILI YA MAJERUHI WA AJALI MKOANI MOROGORO

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

CHUO Kikuu cha Afya na Tiba cha St.Joseph jijini Dar es Salaam kwa kushirikiana na wanafunzi wanatarajia kukusanya damu lita 100 kwa ajali ya kusaidia majeruhi wa ajali ya mafuta iliyotokea Agasti 9 mwaka huu mkoani Morogoro.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uchangiaji wa damu Makamu wa Rais wa Serikali ya wanafunzi wa Chuo hicho Joackim Ndali amesema kuwa wameguswa na ajali hiyo na kuona kama wanafunzi wanaweza kutoa msaada wa kuokoa majeruhi waliolazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili ya jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa katika moyo huo watu wengin zikiwmo taasisi zijitokeze katika uchangiaji wa damu na kuwa ni sehemu ya maisha ya kuchangia damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya wenye uhitaji wa damu.

Ndali amesema kuwa kama chuo katika uchamgiaji wa damu wananfunzi wamejitoa kutokana na kuguswa na majeruhi ya ajali ya mafuta mkoani Morogoro.

Nae Mwanafunzi wa Chuo hicho elisafi Elibariki amesema kuwa kuna uhitaji wa damu nyingi licha ya kuwepo kwa majeruhi hao wapo watu wengine wa ajali pamoja na wazazi wakati wa kujifungua.
Makamu wa Rais wa Serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Afya na Tiba cha ST Joseph Joackim Ndali akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uchangiaji damu kwa ajili ya majeruhi wa ajali ya mafuta mkoani Morogoro waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Mwanafunzi wa Chuo hicho elisafi Elibariki akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana umuhimu wa uchangiaji damu wa wahitaji katika kuokoa maisha katika uchangiaji wa damu uliofanyika katika chuo hicho.
Mwanafunzi akichangia damu kwa ajili ya majeruhi wa ajali ya mafuta mkoani Morogoro waliolazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi na wahadhiri wakiwa katika maandalizi ya uchangiaji damu.

MICHUZI UPDATES: MAHAKAMA YA RUFANI YATUPILIA MBALI MAOMBI YA MAREJEO YA HUKUMU YA BAGENI

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii

MAHAKAMA ya Rufaa, Tanzania imetupilia mbali maombi ya marejeo ya hukumu ya aliyekuwa Mkuu wa upelelezi Wilaya ya Kinondoni, Mrakibu wa polisi,  Christopher Bageni aliyekuwa amehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kuwaua wafanyabiashara wanne wa madini kutoka wilaya ya Mahenge Mkoani Morogoro.

Kwa uamuzi huo ambao ndio wa mwisho, sasa Bageni hana namna nyingine ya kufanya kwani hakuna ngazi nyingine ya mahakama nchini wala hatua nyingine ambayo anaweza kuichukua kuupinga uamuzi huo, labda ikitokea neema ya Rais wa awamu ya sasa au awamu zijazo kumsamehe, kumwachia huru au kumbadilishia adhabu kama ataguswa au kuona kuna sababu ya kufanya hivyo.

 Uamuzi huo umesomwa leo Agosti 14, 2019 na Naibu Msajili Mwandamizi wa Mahakama ya Rufaa, Elizabeth Mkwizu baada ya mshtakiwa kushindwa kuishawishi mahakama kuwa ilikosea kumtia hatiani.

 Mapema, mwaka 2016 Mrufani Bageni aliwasilisha maombi ya marejeo mahakamani hapo akiiomba mahakama hiyo ibadilishe uamuzi wake. Akiwasilisha hoja mbili kwamba, wakati mahakama inamtia hatiani ilizingatia ushahidi wa mshtakiwa mwenzie katika kesi ya mauaji ambae alikuwa ni mshtakiwa namba nne, ushahidi ambao hakuungwa mkono na shahidi yeyote mahakamani hapo  ambapo kisheria mtu hawezi kutiwa hatiani kwa kutumia ushahidi wa mshtakiwa mwenzake isipokuwa kama utaungwa mkono na mtu mwingine.

Sababu ya pili alidai kuwa mahakama ilimnyima haki ya kusikilizwa na kuongeza kuwa wakati mahakama ya Rufaa inaamua rufani, kulijitokeza maelezo mapya ambayo hayakuwa kwenye ushahidi.

Akisoma uamuzi huo, Msajili Mkwizu amesema, mahakama imeangalia maombi ya mrufani na  kwamba kuhusu hoja ya kuleta Maelezo mapya, Mahakama imeangalia ushahidi kwa makini na kugundua kuwa hakuna kitu kipya kwani mahakama inawajibu wa kuangalia kilichotokea ili kutenda haki na katika kuangalia ushahidi huo imeona hakuna mambo mapya.

Katika kufanya hivyo, mahakama haikufanya kosa lolote lililopelekea kuathiri haki ya mshtakiwa.

Akizungumzia juu ya hoja ya pili, Naibu Msajili Mkwizu amesema wakati Mahakama ya Rufaa inamtia hatiani mrufani Bageni,  Ilizingatia ushahidi uliotolewa na Koplo Rajabu  Bakari aliyeeleza kuwa Bageni ndiye aliyeamuru marehemu wale wapelekwe msituni na kwamba kule msituni yeye ndiye  alikuwa afisa wa polisi mwenye cheo cha juu kuliko wote ingawa  na ndiye alikuwa na uwezo wa kutoa amri.

Amesema, Koplo Bakari katika ushahidi wake alidai alimsikia Bageni akimuamuru mtu aliyetekeleza mauaji afanye hivyo. Shahidi huyo aliongeza kuwa hakuwepo eneo tukio lakini alisikia milio ya risasi ndipo akashuka kwenye gari na kwenda eneo la tukio ambapo alipofika alikuta marehemu wa NNE anauawa na mshtakiwa akiwa eneo la tukio.

Akichambua hilo naibu msajili amesena, kwa mujibu wa Sheria kuna namna nyingi za kuunga mkono ushahidi wa Koplo Bakari ikiwemo mienendo ya mshtakiwa  alivyokuwa akionyesha baada ya tukio la mauaji

Wameridhika kuwa ushahidi huo uliungwa mkono na namna Bageni alivyo "behave" baada ya tukio kwa namna mbili.
Kwanza alidanganya kwa wakubwa zake kwamba kulikuwaa na majibizano ya risasi kati ya polisi na majambazi kwenye ukuta wa posta sinza wakati mashahidi walioitwa kutoka sinza walisena hakukuwa na majibizano ya risasi.

Mbili. Bageni aliamuru askari wawili kwenda kufyatua risasi 9 baharini na akaja kuonyesha hayo maganda kuwa ndio yaliyopatikana posta sinza kwenye majibishano.

"Mtu yeyote anayedai Mahakama inakosea sehemu katika kufikia maamuzi yake, yeye ndie anayepaswa kuthibitisha madai yake lakini, mshtakiwa ameshindwa kuishawishi Mahakama kwamba ilikosea katika kufikia maamuzi iliyofikia ya kumtia hatiani, hivyo wao hawana namna nyingine zaidi ya kutupilia mbali maombi yake" amesema Mkwizu.

Uamuzi wa kutupilia mbali maombi hayo ya Bageni ulioandaliwa na jopo la majaji watatu wa mahakama hiyo waliosikiliza maombi  hayo.

Jopo la majaji hao waliosikiliza na kutoa uamuzi wa maombi hayo namba 63 ya mwaka 2016 ni Stella Mugasha (kiongozi), Ferdinarnd Wambali na Rehema Kerefu.

Afisa huyo wa zamani wa Polisi alihukumiwa na mahakama hiyo adhabu hiyo Septemba 11, 2016, baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya wafanyabiashara watatu wa madini kutoka Mahenge, Morogoro na dereva teksi wa Manzese Dar es Salaam.

Alitiwa hatiani na mahakama hiyo kufuatia rufaa aliyoikata  Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), akipinga hukumu ya Mahakama Kuu iliyomwachia huru yeye na maafisa wenzake wengine wa polisi katika kesi ya msingi.

Lakini siku chache baadaye, alifungua maombi hayo akiiomba mahakama hiyo ifanye marejeo ya hukumu yake hiyo kisha imuondolee hatia na kumfutia adhabu hiyo na iamuru aachiwe huru, akidai kuwa hiyo iliyomtia hatiani ina kasoro za dhahiri.

Siku ya usikilizwaji wa maombi hayo, wakili wake Gaudiosus Ishengoma alidai kuwa mahakama hiyo ilimtia hatiani bila kumpa fursa ya kumsikiliza kwani ilimtia hatiani kwa ushahidi ambao haupo kwenye kumbukumbu za mahakama na wala haukujadiliwa kwenye rufaa ya DPP.
Hata hivyo mahakama hiyo katika uamuzi wake wa leo, imetupilia mbali sababu hizo ikisema kwamba hazina msingi kwa kuwa hoja zake hazina msingi kwa kuwa hakuna jambo jipya ambalo mahakama ililiibua na kwamba hakunyimwa haki ya kusikilizwa kwa kuwa alikuwa na wakili wakati wa rufaa hiyo.

Mkwizu alisema kuwa mahakama hiyo ilitekeleza majukumu yake na kwamba katika kumtia hatiani ilifanya tu uchambuzi wa ushahidi uliowasilishwa mahakamani ukiwemo wa aliyekuwa mshtakiwa mwenza, aliyeeleza ukweli wa tukio na Bageni hakuupinga.
“Mwombaji ameshindwa kuonesha makosa kwenye hukumu hii (iliyomtia hatiani, kama alivyodai kwenye sababu zake za maombi.Kwa hiyo hatuna namna nyingine zaidi ya kuyatupilia mbali maombi haya, kwani.”, alisema Mkwizu. 

Katika kesi ya msingi, Bageni na wenzake 13, walikuwa wakikabiliwa na kesi ya mauaji ya wafanyabiashara hao Sabinus Chigumbi ( Jongo) na ndugu yake Ephrahim Chigumbi na mwenzao Mathias Lunkombe pamoja na Juma Ndugu, dereva teksi aliyekuwa akiwaendesha,
Walikuwa wakidaiwa kuwaua kwa kupigwa risasi katika mstu wa Pande wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, Januari 14, 2008.

Kabla ya kuuawa, walitiwa mbaroni na askari hao eneo la Sinza Palestina nyumbani kwa mchimbaji mwenzao, ambao waliwafunga pingu wakiwatuhumu kuhusika katika uporaji wa pesa za kampuni ya Bidco na baadaye polisi walidai kuwa walifariki wakati wakirushiana nao risasi.

Mahakama Kuu katika hukumu yake iliyotolewa Agosti 17, 209 na aliyekuwa Jaji Kiongozi Salum Massati, aliyeisikiliza, ingawa alikiri kuwa kwa mujibu ushahidi uliowasilishwa mahakamani, Bageni alikuwepo ndiye aliyeongoza msafara wa washtakiwa kwenda eneo la mauaji, lakini iliwaachia huru wote.

Jaji Massati alisema kuwa kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa mahakamani hapo, mauaji hayo yalitekelezwa na Koplo Saad Alawi, ambaye hakuwa miongoni mwa washtakiwa (hadi sasa hajulikani aliko) na kwamba hakuna ushahidi kwamba Bageni aliamuru au alisaidia au aliwezesha mauaji hayo.

Lakini baada ya DPP kukata rufaa, Mahakama ya Rufani katika hukumu iliyotolewa na jopo la majaji watatu Bernard Luanda (kiongozi wa jopo), Sauda Mjasiri na Semistocles Kaijage ilimtia hatiani Bageni, na kumhukumu adhabu hiyo.

HATMA YA LUGHA YA KISWAHILI SASA MIKONONI MWA WAKUU WA NCHI ZA SADC

$
0
0
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

BARAZA la Kamati ya  Mawaziri la Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC)  leo Agosti14  wamekubaliana na kuifanya lugha ya Kiswahili kuwa lugha rasmi ya nne ya jumuiya hiyo huku wakieleza kuwa kwa sasa wanasubiri baraka za wakuu wa nchi hizo ili ianze kutumika.

Akizungumza mara baada ya kikao cha mawaziri wa SADC , Mwenyekiti wa kamati ya baraza hilo la mawaziri wa SADC ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na uUhirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi amesema baada ya baraza la mawaziri kukaa kwa siku mbili wametoka na mapendekezo 107 ambayo yatapelekwa kwa wakuu wa nchi kwa ajili ya majadiliano yatakayofanyika Agosti 17 na 18 mwaka huu.

"Mkutano wa mawaziri hautoi maamuzi bali uamuzi utatolewa na wakuu wa nchi baada ya kukaa katika kikao cha siku mbili, moja ya pendekezo kubwa na lenye kuleta heshima kwa watanzania ni kuichagua lugha ya Kiswahili kuwa lugha rasmi ya nne ambayo itatumika katika ngazi mbalimbali ikiwemo katika vikao vya baraza la mawaziri, vikao vya wakuu wa nchi, hotuba mbalimbali na baadaye kutafsiriwa katika nyaraka mbalimbali" ameeleza Kabudi.

Pia amesema katika mapendekezo hayo ambayo yamejikita katika kauli mbiu ya mazingira wezeshi ya biashara na ukuaji wa viwanda ndani ya jumuiya wanachama kwa muda wa mwaka mmoja uenyekiti utakaoongozwa na Rais. Dkt. JohnJoseph Magufuli utahakikisha biashara inakua katika ukanda wa SADC.

"Tupo chini sana katika masuala ya umiliki wa biashara tunamiliki asilimia20 pekee huku asilimia 80 tukizitumia kununua bidhaa kutoka nje hali inayokosesha ajira kwa vijana wetu" ameeleza.

Aidha amesema kuwa kwa muda wa mwaka mmoja wa uenyekiti Tanzania itahakikisha  asilimia 60 ya vijana ambalo ndilo kundi kubwa linapata ajira aidha kwa kujiajiri au kuajiriwa na hiyo ni kwa kuhakikisha biashara zinafanywa kwa kuhusisha nchi zote wanachama na pia watahakikisha wanashirikiana katika kuhakikisha Zimbabwe inaindolewa vikwazo walivyowekewa na baadhi ya nchi na hiyo ni baada ya nchi hiyo kufanya uchaguzi na kubadilisha mifumo mbalimbali hivyo hakuna sababu ya kuwekewa vikwazo ambavyo huwaumiza wananchi.

Mapendekezo hayo 107 yatajadiliwa na kufanyiwa maamuzi katika kikao Cha wakuu wa nchi na Serikali kitakachofanyika Agosti 17 na 18 mwaka huu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) Profesa Palamagamba Kabudi (kulia) akigonga meza kuashiria kufungwa kwa kikao cha kamati ya baraza hilo kilichokutana kwa siku mbili katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Katibu Mkuu wa SADC Dkt Stergomena Tax .
Washiriki wa kikao cha Kamati ya Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika(SADC)wakiwa wamesimama wakati wimbo wa jumuiya hiyo na wimbo wa Taifa wa Tanzania ukipigwa ukumbini hapo leo Agosti 14, 2019 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa kikao cha Kamati ya Baraza la Mawaziri wa nchi za SADC wakiwa wamesimaam wakati wimbo wa jumuiya hiyo ukiendelea kabla ya kufungwa kwa kikao cha kamati hiyo kilichoketi leo Agosti 14,2019 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam 
Wajumbe wa Kamati ya Baraza la Mawaziri wa nchi za SADC wakifuatilia kikao katika Ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo 
Mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika(SADC) Profesa Palamagamba Kabudi akizunguza leo Agosti 14,2019 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam wakati wa akifunga kikao cha baraza la mawaziri hao ambacho kimekutana kujadili masuala mbalimbali ya jumuiya hiyo 
Mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika(SADC) Profesa Palamagamba Kabudi akizunguza leo Agosti 14,2019 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam wakati wa akifunga kikao cha baraza la mawaziri hao ambacho kimekutana kujadili masuala mbalimbali ya jumuiya hiyo.

WAKAZI DAR ES SALAAM WAUNGANA NA BENKI YA EXIM KUCHANGIA DAMU KWA AJILI YA MAJERUHI WA AJALI YA MOTO MKOANI MOROGORO.

$
0
0

Mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam hii leo Jumatano Agosti 14, wamejitokeza kwa wingi ili kuungana na Benki ya Exim Tanzania ambayo kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS) waliendesha zoezi la uchangiaji damu kwa ajili kuwasaidia majeruhi wa ajali ya moto iliyosababishwa na lori la mafuta lililopinduka na kulipuka eneo la Msamvu Mkoani Morogoro ambapo watu zaidi ya 70 walifariki dunia na wengine kujeruhiwa.

Zoezi hilo litakalodumu kwa siku tatu mfululizo limefanyika kwenye viunga vya Stendi ya mabasi ya Mbagala jijini Dar es Salaam ambapo imeshuhudiwa idadi kubwa ya wakazi wa jiji hilo wakijitokeza kwa wingi ili kujitolea damu huku wadai kuwa muitikio huo umetokana na kuguswa kwao na tukio hilo la kusikitisha lililotokea mkoani Morogoro.

Meneja Masoko na Mahusiano ya jamii wa Benki ya Exim, Bw Abdulrahman Nkondo (alievaa kofia nyeupe) akiwagawia vinywaji baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kwa wingi kwenye viunga vya Stendi ya mabasi ya Mbagala jijini Dar es Salaam ili kuchangia damu kwa ajili ya majeruhi wa ajali ya moto iliyosababishwa na lori la mafuta lililopinduka na kulipuka eneo la Msamvu Mkoani Morogoro ambapo watu zaidi ya 70 walifariki dunia na wengine kujeruhiwa. Zoezi hilo la siku tatu limeratibiwa na benki hiyo kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS)na linatarajiwa kukamilika Agosti 16.



Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kwenye viunga vya Stendi ya mabasi ya Mbagala jijini Dar es Salaam wakifuata taratibu ili kuchangia damu kwa ajili ya majeruhi wa ajali ya moto iliyosababishwa na lori la mafuta lililopinduka na kulipuka eneo la Msamvu Mkoani Morogoro ambapo watu zaidi ya 70 walifariki dunia na wengine kujeruhiwa. Zoezi hilo la siku tatu limeratibiwa na benki ya Exim Tanzania kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS)na linatarajiwa kukamilika Agosti 16.
 


Jafo atoa agizo kali kwa Halmashauri zilizokusanya mapato chini ya asilimia 50

$
0
0
Charles James, Michuzi TV

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo ametoa wiki mbili kwa halmashauri  zote zilizokusanya mapato chini ya asilimia 50 ya malengo yao kuandika barua ya kujieleza kwa Katibu Mkuu TAMISEMI  ya kwanini wasichukuliwe hatua kwa kutofikia malengo.

 Pia amesema Wakurugenzi walioshindwa kukusanya mapato watapewa vinyago vya uzembe na kutofikia lengo kisha kutakiwa kuviweka mbele ya ofisi zao na za wakuu wa mikoa hiyo.

 Amebainisha kuwa agizo hilo pia limewahusu wakurugenzi kutoka halmashauri zaidi ya 40 walioshindwa kutoa fedha za mikopo kwa kwa makundi ya vijana, walemavu na wanawake chini ya asilimia 50 zilizotakiwa kutengwa.

Hayo ameyabainisha Jijini Dodoma wakati akizungumza na wanahabari, Waziri Jafo amezitaja halmashauri ambazo wakurugenzi wake watapewa vinyago kwa kushindwa kukusanya mapato.

 “Vinyago nitakavyovitoa  vitakuwa na sura mbaya sana na Wakurugenzi wa halmashauri hizo wanatakiwa kuviweka kwenye ofisi zao na ofisi za wakuu wa mikoa husika,” amesema.

 “Halmashauri ambazo zitahusika zilizoshika mkia kwa kigezo cha wingi wa mapato yaliyokusanywa (pato ghafi) ni  Halmashauri za Wilaya za Kakonko (Sh. milioni 408.2), Buhigwe (Sh. milioni 403.8), Kigoma (Sh. milioni 397.1), Gairo (Sh.milioni 396.2) na  Halmashauri ya Mji wa Nanyamba (Sh. Milioni 257.6)” amesema.

Amezitaja halmashauri za mwisho kwa kigezo cha asilimia ya mapato ya ndani yaliyokusanywa ukilinganisha na makisio ya halmashauri ya mwaka ni Halmashauri za Wilaya za Newala (27%), Masasi (26%), Msalala (19%), Tandahimba (19%) na Halmashauri ya Mji wa Nanyamba (11%).  

Pia amebainisha kuwa kuna uwepo wa Halmashauri zaidi ya 40 ambazo zimeshindwa kuchangia katika Vikundi vya Wanawake, Vijana, na Watu wenye Ulemavu.

“Nataka na hawa nao wajieleze sababu za kushindwa kusimamia Kanuni za Usimamizi wa Fedha za michango ya Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu,”  amesema.

Waziri Jafo amezitaja halmashauri tano zilizoongoza kwa kigezo cha wingi wa mapato yaliyokusanywa (pato ghafi), Jiji la Dodoma limeongoza kwa kukusanya sh. bilioni 71.7, Halmashauri za Manispaa za Ilala sh. bilioni 58.2, Kinondoni (Sh.Bilioni 34.0), Temeke (Sh. Bilioni 33.3) na Ubungo (Sh. Bilioni 18.6).

“Mikoa iliyoongoza ni Dar es Salaam (Sh. Bilioni 163.6), Dodoma (Sh. Bilioni 82.7), Mwanza (Sh. Bilioni 32.7), Arusha (Sh. Bilioni 31.9) na Mbeya (Sh. Bilioni 31.4)” amesema Jafo.

Ameitaja mikoa mitano ya mwisho kwa kigezo cha wingi wa mapato yaliyokusanywa (pato ghafi) ni Njombe (Sh. Bilioni 11.5), Simiyu (Sh. Bilioni 8.8), Rukwa (Sh. Bilioni 8.2), Kigoma (Sh. Bilioni 7.8) na Katavi (Sh. Bilioni 7.4).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe Suleiman Jafo kizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) Ofisi kwake Ihumwa jijini Dodoma leo.

Waziri Mkuu kuwa mgeni rasmi wa maadhimisho ya siku ya vijana kimataifa

$
0
0

Charles James, Michuzi TV

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 20 ya siku ya kimataifa ya vijana kwa mwaka 2019 ambayo yatafanyika Jijini Dodoma.

Akitoa taarifa kwa wanahabari Meneja program ya vijana na maendeleo kutoka UNFPA- Tanzania Dkt Majaliwa Marwa, amesema katika maadhimisho hayo yanayowezeshwa na UNFPA, UNESCO, ILO na UNIC yana lengo la kuhakikisha vijana wanajengewa uwezo na kuwa na ubunifu mbalimbali.

Amesema maadhimisho hayo yatashirikisha vijana zaidi ya mia tano kutoka Tanzania bara na visiwani na kwa mwaka huu wamejikita zaidi katika kutilia mkazo kuhusu elimu kwa vijana.

“Mwaka huu ni maadhimisho ya 20 ya siku ya vijana kimataifa na mwaka huu tumejikita katika elimu ili kuwajengea vijana uwezo na kuwa wabunifu kuweza kujitegemea, dhamira Tanzania iliyopendekezwa kuelekea 2030 ni Tanzania ya viwanda boresha elimu kwa ajili ya maendeleo ya vijana.

“Tarehe 15 tutakuwa na kongamano litakuwa na mada mabalimbali ikihusisha ubunifu na afya ya uzazi kwa vijana, na siku ya pili kutakuwa na tamasha litakuwa katika eneo la Chang’ombe eneo lenye mkusanyiko wa vijana wengi na kutakuwa na burudani nyingi” amesema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Shirika la RESLESS DEVELOPMENT, chini ya mradi wa Kijana wajibika kwa mkoa wa Dodoma, Ridhiwani Juma amesema wao kama wenyeji wameweza kuratibu na kuhakikisha hata vijana wenye mahitaji maalumu nao wanakuwa sehemu ya mmaadhimisho hayo.

Muwakilishi wa vijana ambaye ni katibu Afriyan Tanzania, Seif Ibrahimu amesema kundi la vijana linakabiliwa na tatizo la ukosefu wa ajira kwa kiasi kikubwa.
Meneja Program Maalum ya vijana kutoka Umoja wa Mataifa, Dk Majaliwa Marwa akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dodoma leo kuhusiana na kongamano la vijana litakalofanyika kesho ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu, Mhe Kassim Majaliwa

INFOY YAWAWEZESHA WADAU WA LISHE KUTOMEZA UDUMAVU

$
0
0
Msindikaji wa Bidhaa za Lishe Dorice Assenga akifafanua juu ya virutubisho na viini lishe vinavyopatikana katika unga wa lishe kwa Mratibu wa Shirika lisilokua la kiserikali la INFOY ,Laurent Sabuni katika maonyesho ya bidhaa za lishe jijini Arusha.


Na Vero Ignatus ,Arusha.

Shirika lisilokua la kiserikali la Infoy limeendeleza juhudi zake katika kuwawezesha vijana wanaojishughulisha na uzalishaji na usindikaji wa bidhaa za lishe ili waweze kutokomeza tatizo la udumavu nchini pamoja na kupunguza utegemezi.

Mratibu wa Shirika lisilokua la kiserikali la Infoy Laurent ,Sabuni alisema hayo katika maonyesho ya bidhaa za lishe yaliyoandaliwa na shirika hilo kwa kushirikiana na shirika la kuhudumia viwanda vidogo la Sido mkoa wa Arusha ,ambapo alisisitiza kuwa wazalishaji na wasindikaji wa bidhaa za lishe wanapaswa kushiriki kutatua matatizo ya lishe duni katika jamii na kuhakikisha kuwa wanazifikisha bidhaa hizo vijijini.

Sabuni alisema kuwa wamekua wakitoa mafunzo kwa wasindikaji wa bidhaa za lishe juu ya namna bora ya kusindika na kuzifungasha ili ziweze kuwafikia wateja na kusaidia kupunguza tatizo la udumavu linalowakabili watoto wengi licha ya uzalishaji wa nafaka ulioko.

Meneja wa Sido mkoa wa Arusha Nina Nchimbi aliwataka wasindikaji watengeneza unga wenye virutubisho na viini lishe ili kukidhi afya ya mlaji na kuhakikisha suala la viwango vya ubora katika bidhaa za lishe wanazozalisha unazingatiwa.

Nina alisema kuwa Sido imefanya juhudi za kuwaunganisha wajasiriamali hao na taasisi za ubora ikiwemo TBS,TFDA ili bidhaa zao ziweze kuthibitishwa ubora na kupata masoko ya kitaifa na kimataifa.

Kwa upande wao Wasindikaji na Wajasiriamali wa bidhaa za lishe Dorice Assenga na Walter David wameeleza kuwa wamekua wakitoa elimu juu ya umuhimu wa matumizi ya unga wa lishe kwa watoto wadogo na kuzipeleka bidhaa za maeneo ya pembezeni na vijijini ambako kuna hitaji kubwa la lishe ili kuwasaidia kinamama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano.

Mtaalamu wa Lishe Prisca Mwakalasi alisema kuwa mchango wa wadau wa lishe ni mkubwa kwani madhara ya udumavu huonekana hasa mtoto anapokua na kuwa mtu mzima inakua vigumu kufanya maamuzi sahihi kwani anakua amedumaa hadi akili hivyo masuala ya lishe kwa watoto na watu wazima yanapaswa yapewe kipaumbele kwani lishe ni kiini cha maendelea.

JAMII YATAKIWA KUWATAMBUA, KUWATUMIA WASAIDIZI WA KISHERIA KUPATA MSAADA WA KISHERIA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (katikati) akizungumza na wadau wa Huduma za Msaada wa Kisheria Mkoani Simiyu, wakati wa kikao cha Uundaji wa Kamati ya Uratibu wa Huduma za Msaada wa kisheria Mkoani humo kilichofanyika Mjini Bariadi.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (kushoto) akizungumza na wadau wa Huduma za Msaada wa Kisheria Mkoani Simiyu, wakati wa kikao cha Uundaji wa Kamati ya Uratibu wa Huduma za Msaada wa kisheria Mkoani humo kilichofanyika Mjini Bariadi.

Msajili wa Watoa Huduma ya Msaada wa Kisheria Tanzania, Bi. Felistas Joseph(kulia) kutoka Wizara ya Katiba na Sheria akiwasilisha mada katika katika kikao cha Uundaji wa Kamati ya Uratibu ya Huduma za Msaada wa kisheria Mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi, kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka
Mwakilishi wa Taasisi za watoa huduma za msaada wa kisheria mkoani Simiyu akichangia hoja katika kikao cha Uundaji wa Kamati ya Uratibu wa Huduma za Msaada wa kisheria Mkoani humo kilichofanyika Mjini Bariadi.
Wakili wa Serikali Lilian Kilembe kutoka Wizara ya katiba na Sheria akiwasilisha mada katika katika kikao cha Uundaji wa Kamati ya Uratibu wa Huduma za Msaada wa kisheria Mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi.
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha Uundaji wa Kamati ya Uratibu wa Huduma za Msaada wa kisheria Mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati akifungua kikao hicho.

Baadhi ya wajumbe wa kikao cha Uundaji wa Kamati ya Uratibu wa Huduma za Msaada wa kisheria Mkoani Simiyu kilichofanyika Agosti 13, 2019 Mjini Bariadi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati akifungua kikao hicho.


Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu na Mwenyekiti wa Kamati ya Uratibu wa Huduma za Msaada wa kisheria Mkoa, Bw. Jumanne Sagini (katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa kikao cha Uundaji wa Kamati hiyo kilichofanyika Mjini Bariadi.

……………..


Na Stella Kalinga, Simiyu RS

Msajili wa Watoa Huduma ya Msaada wa Kisheria Tanzania, Bi. Felistas Joseph kutoka Wizara ya Katiba na Sheria ametoa wito kwa jamii kuwatambua na kuwatumia wasaidizi wa kisheria pindi wanapohitaji msaada katika masuala ya kawaida ya kisheria, ikiwemo migogoro ya ardhi, migogoro ya ndoa, utelekezaji wa familia na masuala mengine wanayokutana nayo siku kwa siku, ambao amesema wanatoa huduma hizo bila malipo yoyote.



Bi Felistas ameyasema hayo jana katika kikao cha Uundaji wa Kamati ya Uratibu wa Huduma za Msaada wa kisheria Mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi.

Amesema kada hii inatambuliwa kwa mujibu wa sheria ya msaada wa kisheria na wamefundishwa mafunzo ya awali ya sheria katika masuala ambayo wananchi wanakutana nayo siku kwa siku hivyo ni vema jamii na wadau wengine wakawatambua na kuwapokea kwa kuwa ni watu waliojitoa kuisaidia jamii bila malipo yoyote.

“Nia yetu ni kwamba jamii iweze kuwafahamu na kuwapokea wasaidizi wa kisheria, hawa ni watu wanaojitolea kwa dhati kufanya hii kazi bila kudai malipo, wanachohitaji ni ushirikiano na wadau wengine wa Serikali pamoja na wananchi; kada hii inatambuliwa rasmi chini ya sheria ya msaada wa kisheria na wameshapewa vigezo na mipaka ya kufanyia kazi” alisema.

Ameongeza kuwa Serikali imeandaa mtaala wa kufundisha wasaidizi wa huduma za kisheria na hadi sasa takribani wasaidizi wa kisheria 4500 wamefundishwa katika kipindi cha miaka mitatu nyuma ambao wamejiunga katika vikundi na kujisajili kama mashirika ambapo hadi sasa kuna jumla ya mashirika 200.



Awali akifungua kikao cha Uundaji wa Kamati ya Uratibu ya Huduma za Msaada wa kisheria Mkoani Simiyu, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema endapo wasaidizi wa kisheria watutumiwa vizuri kero nyingi za wananchi zitatatuliwa na kufikia mwisho, huku kutoa wito kwa Wakuu wa wilaya, wabunge, madiwani na viongozi wengine kuwashirikisha wasaidizi wa kisheria katika mikutano ya hadhara ambapo wananchi huwasilisha kero zao.

Aidha, Mtaka amesema ili kuongeza uewelewa wa masuala ya msaada wa kisheria mkoani Simiyu ni vema Wizara ya Katiba na Sheria ikaona haja ya kuendela kutoa elimu kwa jamii, ambapo amewaalika kutoa elimu hiyo katika kambi za kitaaluma mkoani hapa ambazo zinatarajia kuanza mwezi Septemba, 2019 kwa kidato cha nne..

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Jumanne Sagini amesema viongozi wa Mkoa watahakikisha kamati za uratibu wa huduma za kisheria ngazi ya wilaya zinaundwa na wasaidizi wa kisheria wanatumiwa ipasavyo.

Naye Sheikh wa Mkoa wa Simiyu, Mahamoud Kalokola amesema viongozi wa madhehebu ya dini wataendelea kutoa elimu kupitia makusanyiko ya ibada kwa waumini wao ili wananchi hususani wale ambao hawana na uwezo wa kifedha wa kuwalipa mawakili wajue kuwa wasaidizi wa kisheria wapo katika jamii na wanaweza kuwasaida kutatua changamoto zao.

Kamati ya Uratibu wa Shughuli za Huduma za Msaada wa Kisheria mkoa wa Simiyu imeundwa na kuzinduliwa chini ya Katibu Tawala wa Mkoa ambaye ni Mwenyekiti, Msajili msaidizi(Afisa Maendeleo ya jamii Mkoa), mtaalamu wa ardhi, jeshi la polisi (dawati la jinsia) Magereza, TAKUKURU, Mahakama, Mwanasheria, Afisa wa dawati la malalamiko, viongozi wa dini na Afisa ustawi wa jamii na Afisa habari ngazi.

Wajumbe wengine ni mwakilishi wa vyombo vya habari, wawakilishi wa wadau wa maendeleo, wawakilishi wa taasisi za watoa huduma za msaada wa kisheria,Mwenyekiti wa baraza la ardhi na mwakilishi kutoka Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), ambapo kwa muundo huu huu kamati za wilaya zitaundwa ziweze kutekeleza jukumu la uratibu wa shughuli za huduma za kisheria wilayani

MKURUGENZI MKUU MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA AKABIDHIWA UENYEKITI KAMATI YA SEKTA NDOGO YA HALI YA HEWA NCHI ZA SADC

$
0
0

 Na Ripota Wetu,Michuzi TV

WAKATI Rais Dkt  John  Magufuli akielekea kupokea Uenyekiti wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Tanzania kupitia Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dk.Agnes Kijazi amekabidhiwa Uenyekiti wa Kamati ndogo ya Sekta ya hali ya hewa ya nchi wanachama wa jumuiya hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Aidha Dk.Kijazi amechaguliwa bila kupingwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Taasisi za Hali ya Hewa za nchi za SADC “SADC Meteorological Association of Southern Africa (SADC-MASA)” kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia mwaka huu wa 2019.  

Taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari nchini imeeleza kuwa Wilbert Timiza Muruke  ambaye amemwakilisha Dkt. Kijazi amekabidhiwa nafasi hizo katika mikutano ya SADC-SCOM na SADC-MASA iliyofanyika kwa kufuatana jijini Windhoek, Namibia kuanzia Agosti 5 hadi 9 Agosti, 2019. 
 
Imefafanua kuwa  Kama ilivyo kawaida baada ya Rais Dkt. John Magufuli kukabidhiwa Uenyekiti wa SADC, Sekta zingine zote zinakuwa chini ya uenyekiti wa Tanzania, hivyo kwa upande wa Sekta ya hali ya hewa, tayari TMA imekwishakabidhiwa Uenyekiti wa kamati hiyo ya SADC Sekta ya hali ya hewa (SADC SCOM) kutoka kwa Taasisi ya Hali ya Hewa ya Namibia.

 Aidha, Uenyekiti wa Tanzania kuongoza umoja wa Taasisi za Hali ya Hewa za SADC (SADC MASA) utadumu kwa miaka miwili, ambapo Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya hali ya hewa ya Lesotho amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa SADC MASA. 

Kabla ya kupokea nafasi hiyo ya kuwa Mwenyekiti wa MASA, Dkt. Kijazi alikuwa Makamu Mwenyekiti na  Franz Uirab kutoka Namibia alikuwa Mwenyekiti.

Akipokea dhamana hizo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Meneja wa Uhusiano wa Hali ya Hewa Kimataifa, Wilbert Timiza Muruke ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu katika mikutano hiyo, alishukuru kwa nafasi hizo na kumpongeza aliyekuwa Mwenyekiti.

Viewing all 110000 articles
Browse latest View live


Latest Images