Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

DK.AKUTANA NA MWAKILISHI WA UNESCO

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Mwakilishi wa Shirika la UNESCO Tanzania Bw.Tirso Dos Santos (katikati) wakati alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo kwa ajili ya kujitambulisha (kushoto) Mathias F.H.Luhanya. [Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akimsikiliza Mwakilishi wa Shirika la UNESCO Tanzania Bw.Tirso Dos Santos (kushoto) wakati wa mazungumzo yao yaliyofanyika leo alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa ajili ya kujitambulisha 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akifuatana na Mwakilishi wa Shirika la UNESCO Tanzania Bw.Tirso Dos Santos (kushoto) baada ya mazungumzo yao alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha.[Picha na Ikulu.]

Wananchi watembelea banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) maonesho ya wiki ya SADC

$
0
0
Daktari bingwa wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Pedro Pallangyo akiwaeleza huduma za matibabu ya moyo wananchi alipotembelea banda la Taasisi hiyo wakati wa maonesho ya viwanda ya SADC yaliyomalizika jana jijini Dar es Salaam huduma .
Daktari wa chumba cha upasuaji wa moyo Tryphone Kagaruki kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) akimwelekeza Bhupendra Vaghele jinsi upasuaji wa moyo unavyofanyika alipotembelea banda la Taasisi hiyo wakati wa maonesho ya viwanda ya SADC yaliyomalizika jana jijini Dar es Salaam.
Daktari bingwa wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Pedro Pallangyo akimtazama Mustafa Abdulkadir akisaini kitabu cha wagonjwa alipotembelea banda la Taasisi hiyo kwa ajili ya kufahamu huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa wakati wa maonesho ya viwanda ya SADC yaliyomalizika jana jijini Dar es Salaam huduma .

WATOA HUDUMA FANYENI KAZI BILA KUSUKUMWA

$
0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Tiba kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Grace Magembe akiongea na watumishi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa iringa (hawapo pichani),kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya hospitali hiyo Bi.Elisifu Mafole na kushoto ni mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Dkt.Alfred Mwakalebela
Mkurugenzi wa Utawala na Rasiliamali watu Bi.Deonatha Makani akifafanua jambo wakati wa kikao cha wakurugenzi wa wizara na watumishi wa hospitali ya rufaa ya mkoa ya iringa




Mkurugenzi Dkt.Grace Magembe wakiongea na Mganga Mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya iringa Dkt.Alfred Mwakalebela
Mwenyekiti wa waganga wafawidhi wa hospitali za mikoa Dkt.Ibenzi Ernest akielezea huduma za kibingwa walizotoa kwa muda wa wiki mbili kwenye hospitali hiyo
Watumishi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa iringa wakimsikiliza mkurugenzi wa tiba(hayupo pichani)ambapo walitakiwa kufanya kazi bila ya kusukumwa na kuonyesha mabadiliko katika utoaji wa huduma za afya
…………………
Na.Catherine Sungura,WAMJW-Iringa.
Watumishi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa iringa wametakiwa kufanya kazi kwa kujituma bila kusukumwa na mtu yeyote.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa idara ya tiba kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Grace Magembe wakati akiongea na watumishi wa hospitali hiyo ikiwa ni ziara ya kujionea huduma za kibingwa zilizofanywa katika hospitali hiyo ambazo zimetolewa na madaktari bingwa kutoka wizarani.

Dkt.Magembe alisema kuwa amepokea majina ya Watumishi ambao wamepewa onyo mara kadhaa na wameshindwa kubadilika hivyo watachukuliwa hatua kulingana na taratibu za kiutumishi.
” Wengine mtapewa muda wa kujirekebisha na kufuatiliwa kuona kama mmebadilika,sitegemei kufukuza mtaalam yeyote kwani wanayo nafasi ya kubadilika”.

“Kama mtumishi wa umma na ulipewa viapo hivyo mnapaswa kufanya kazi bila kusukumwa kwani kwenye utumishi wa umma hakuna kubebana”.Alisisitiza Dkt.MagembeAidha, alisema kuwa wananchi wanawategemea wataalam hao katika kutoa huduma za afya zinazostahili.

“Mgonjwa anapokuja hospitali ya rufaa ya mkoa anatakiwa kuona mabadiliko kuanzia lugha nzuri na huduma kwa mteja izingatiwe,lazima utofauti uwepo wa hospitali ya mkoa na vituo vya huduma vilivyopo chini”.Alisema Dkt.Magembe.

Akitoa ripoti ya huduma za kibingwa zilizofanywa na madkatari hao Mganga Mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa dodoma ambaye ni mwenyekiti wa waganga wafawidhi Tanzania bara Dkt.Ibenzi Ernest alisema tangu huduma hizo kutolewa mwishoni mwa mwezi wa saba mwaka huu wamewaona wagonjwa 656,wagonjwa 41 wamefanyiwa vipimo na wagonjwa 88 wamepata huduma za upasuaji .

Dkt.Ibinza alisema huduma za kibingwa zilizotolewa ni pa
moja na upasuaji,mifupa,magonjwa ya ndani na pua,koo na masikio.
Wizara ya afya imeamua kutoa huduma za kibingwa kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa kwa ajili ya kuboresha na kuwajengea uwezo madaktari bingwa waliopo hospitalini hapo kwa majuma mawili.

OMMY DIMPLES IN THE TRENDY SHOW BY CYNTHIA MASASI MZIRAY AND COMPANY

JIJI LA ARUSHA LAAGIZA KUFANYIKA KWA CHANJO YA HOMA YA INI

$
0
0
Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Arusha Dkt.Maulid Madeni akitoa baadhi ya ufafanuzi na kuongea kwenye kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya jiji la Arusha picha na ahmed mahmoud Arusha
Mstahiki meya wa jiji la Arusha Kalist Lazaro akiwa na mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Arusha Dkt.Maulid Madeni kwenye kikao cha kawaida cha robo ya mwisho katika ukumbi wa shule ya sekondari Arusha picha na ahmed mahmoud Arusha

……………………………………………………….

BARAZA la madiwani wa halashauri ya jiji la Arusha,limemuagiza mganga mkuu wa jiji hilo kuendesha kampeni maalumu ya chanjo ya ugonjwa wa Ini ,ambao ni hatari na hauna dawa pia umekuwa ni tishio kwa maisha ya binadamu .

Agizo hilo limetolewa na Mstahiki wa jiji la Arusha ,Kalisti Lazaro, Augosti 9 kwenye kikao cha baraza hilo kilichofanyika kwenye ukumbi wa shule ya sekondari ya Arusha na kusisitiza kwamba kampeni hiyo ianze mara moja .

Ameiagiza ofisi ya mganga mkuu wa Jiji hilo kuhakikisha wananchi wanashirikishwa kikamilifu kupima afya zao na hataki kusikia mtu anapoteza maisha kutokana na kutokuelimishwa ili wapime homa ya Ini

Mbunge viti maalumu, Joyce Mukya,Alisema ugonjwa huo ni hatari kuliko Ukimwi hivyo Idara ya afya isifanye mchezo na ugonjwa huo kwani unaua zaidi kuliko Ukimwi .

Madiwani walisema kuwa wananchi hawana elimu juu ya ugonjwa huo ambao mpaka sasa haujawa na tiba bali tiba yake ni chanjo hivyo wananchi wakipewa elimu watachukua tahadhari na kwenda kupima afya zao kwenye vituo vya afya vya jiji la Arusha.

Akitoa ufafanuzi kaimu mganga mkuu wa Jiji la Arusha Dakta,Baraka Muondhe, alisema kuwa Chanjo iliyokuwepo awali ilikuwa ikitolewa bure kata ya Daraja mbili ,lakini sasa chanjo hiyo imekwisha na inatolewa na Zahanati binafsi .

Alisema kuwa wameshapeleka maombi ya kupatiwa Chanjo hiyo kutoka MSD na itakapopatikana itotolewa ambapo wananchi watachangia shilingi 15,000 na chanjo hiyo itatolewa kwenye vituo vyote vya afya na Zahanati za jiji la Arusha.

Wakati huohuo Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha, Karisti Lazaro, ameitaka halmashauri ya jiji hilo kuwakamata na kuwatia pingu watumishi wote watakaoonekana wanahujumu mapato ya halmashauri hiyo kwa kuwa ni mafisadi wanaokwamisha maendeleo ya jiji hilo.

Ametoa agizo hilo kwenye kikao cha robo ya mwisho yam waka 2018/19 cha baraza la madiwani alipokuwa akimpongeza mkurugenzi wa jiji hilo ,Dakta Maulid Madeni ,kwa kusimamia ukusanyaji wa mapato na hatua anazozichuku za kuwakamata watumishi wote wa halmashauri hiyo wanaojihusisha na uhujumu wa mapato .

Meya Karisti, amesema baraza hilo la madiwani linamuunga mkono kwa hatua hizo anazozichukua za kuwabana watumishi wasio waadilifu ambao ni mafisadi nakuongeza kwamba hata kama kuna madiwani ambao waashirikiana na watumishi wasio waadilifu nao wachukuliwe hatua.

Amesema kuwa mkurugenzi ameziba mianya lakini atambue kuwa hivyo ni vita kubwa lakini baraza hilo linamuunga mkono kwenye vita dhidi ya maafisa wote wanaohujumu halmashauri wapigwe pingu.

Ameipongeza halmashauri hiyo kwa kukusanya mapato kwa asilimia 105%ambapo halmashauri hiyo imekusanya shilingi bilioni 16.4 katika kipindi cha robo ya mwisho ya mwaka na hiyo inatokana na ubunifu wa kuziba mianya ya upotevu wa fedha.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa jiji ,Dakta Maulid Madeni,amesema halmashauri hiyo imechangia shilingi milioni 140 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa bara bara unaofanywa naTarura lengo ni kuzifanya bara bara zote za jiji ziwe za lami.

Amesema kuwa halmashauri haiwezi kujiondoa kwenye maswala ya utengenezaji wa bara bara ndio maana imetoa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kujenga bara bara hizo na kusisitiza kuwa Tarura, licha ya kuondolewa halmashauri lakini bado inawajibika kwa halmashauri hiyo.

Madiwani wakichangia wamesema kuwa Tarura, sasa tangia waondolewe halmashauri wamekuwa huru sana na hawatoi usirikiano kwa madiwani na wana urasimu na hila za ajabu ajabu .

Wamelalamikia Tarura kumrundikia kazi mkandarasi mmoja na hivyo kushindwa kutengeneza na kukamilisha barabara kwa viwango vya changarawe na moramu ziweze kupitika kwa mwaka mzima na kutaka miradi ya bara bara ifike mwisho

WAZIRI MKUU AWAONYA MKURUGENZI NA MWEKAHAZINA SHINYANGA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkurugenzi wa Kiwanda cha Kuchambua Pamba cha Fresho Investment Company,  Fred Shoo wakati alipotembelea kiwanda hicho mjini Shinyanga na kukuta pamba nyingi ya wakulima ikisubiri kununuliwa kiwandani hapo   Agosti 9, 2019. Alikuwa katika ziara ya kukagua mwenendo wa uuzaji wa pamba.  Wa tatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Tellak.

***************

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ametoa onyo kali kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Bw. Geoffrey Mwangulumbi pamoja na Mwekahazina wa Manispaa hiyo, Bw. Pascal Makoye kuwa anawataka wabadilike na waache kugombana na badala yake watekeleze majukumu yao ipasavyo.

Kadhalika, Waziri Mkuu amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Bibi Zainab Telack azisimamishe kazi kampuni zote zilizopewa zabuni ya kukusanya mapato katika Manispaa hiyo kwa kuwa zimeshindwa kufanya kazi vizuri na zina madeni.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo (Ijumaa, Agosti 9, 2019) wakati alipozindua nyumba 10 za Askari Polisi katika Manispaa ya Shinyanga eneo la Kambarage. Mradi huo umetokana na fedha kiasi cha sh. milioni 225 zilizotolewa na Rais Dkt. John Magufuli.

Amesema viongozi hao wameshindwa kutekeleza majukumu yao ikiwemo kusimamia kikamilifu zoezi la ukusanyaji wa mapato na kutoa kazi hiyo kwa kampuni zisizokuwa na uwezo. Amesema mwaka jana walikadiria kukusanya sh. milioni 800 na badala yake walikusanya sh. milioni 500.

Waziri Mkuu amesema Manispaa hiyo haiwezi kusonga mbele kimaendeleo iwapo viongozi wake hawaelewani wanagombana kila siku. “Mkurugenzi na wenzako nawaonya kwa mara ya mwisho badilikeni na hakikisheni mnatekeleza majukumu yenu ipasavyo yakiwemo ya ukusanyaji wa mapato.”

Akizungumzia kuhusu nyumba za Askari Polisi, Waziri Mkuu amesema lengo la ujenzi wa nyumba hizo ni kuhakikisha askari wanaishi katika mazingira mazuri yatakayowawezesha kutekeleza vizuri majukumu yao. “Ili waweze kutekeleza vizuri majukumu yao lazima wawe na makazi mazuri”.
Pia, Waziri Mkuu ametoa wito kwa askari waliopewa funguo kwa ajili ya kuishi katika nyumba hizo wahakikishe wanazitunza vizuri na hata inapotokea wamehamishiwa kwenda katika vituo vingine, wale watakaohamia wakute nyumba hizo zikiwa katika mazingira mazuri.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema ujenzi wa nyumba hizo ni endelevu, ambapo pia amezitaka idara mbalimbali za Serikali ziendelee na mchakato wa ujenzi wa nyumba zake kwani wakiwa na nyumba nyingi itasaidia kupunguza idadi kubwa ya askari wanaoishi uraiani.

Awali, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao alisema awali fedha zilizotolewa zilikuwa zijenge nyumba tisa za vyumba viwili lakini kutokana na ubunifu waliweza kuboresha mradi huo kwa kuongeza nyumba moja sambamba na kuongeza chumba kimoja, hivyo kuufanya mradi huo kuwa na nyumba 10 zenye vyumba vitatu vya kulala.

Pia alimshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa upendo wake mkubwa kwa Jeshi la Polisi Tanzania kwa kulipatia fedha za kuboresha makazi ya askari. Mradi huo umekamilika kwa gharama ya sh. milioni 278, 565, 500 wastani wa gharama za ujenzi kwa nyumba moja ni sh. milioni 27, 856, 550. Alisema kiasi cha nyongeza cha sh. milioni 53, 565,500 zilitolewa na wadau mbalimbali.

BBC DIRA YA DUNIA IJUMAA 09.08.2019

DAWASA WABORESHA HUDUMA ZA MAJI KUELEKEA MKUTANO WA SADC

$
0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Kuelekea kwenye Mkutano Mkuu wa 39 Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) utakaoanza Agosti 17-18 mwaka huu upatikanaji wa maji ndani ya Mkoa Wa Dar es Salaam na viunga vyake umezidi kuimarika. 

Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA) wamejizatiti katika kutoa huduma ya maji safi kwenye maeneo yote Jijini wakati wote wa mkutano huo utakaowahusisha viongozi wakiwemo marais wa Nchi 16 za ukanda wa kusini mwa Afrika. 

Hayo yamewekwa bayana na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja kuelekea kwenye mkutano huo mkuu ambapo kwa Maonesho ya Nne ya wiki ya Viwanda ya Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) yamehitimishwa jana kwa kufungwa Rais wa Zanzibar Dkt Alli Mohamed Shein. 

Luhemeja amesema, maboresho yaliyofanyika ni urekebishwaji wa miundo mbinu yote ili iweze kufanya usambazaji wa maji kwa kiwango cha juu, kuhakikisha mitambo yote ya uzalishaji maji inafanya kazi ili kuhakikisha maji yanapatikana muda wote bila kukosekana. 

DAWASA wamezidi kuimarika katika utoaji wa huduma ya maji safi kwa wananchi wa Mkoa wa Dar Es Salaam na Pwani ikiwemo kuboresha miundo mbinu ya muda mrefu iliyo chakavu, kujenga miradi mipya ya maji na kuwafikia wananchi wote waliokuwa hawapo kwenye mtandao wa maji hususani maeneo ya pembezoni. 

Kwa sasa Mkoa wa Dar es Salaam unapata maji kutoa Mtambo wa Ruvu juu, Mtambo wa Ruvu chini, Mtoni na Visima. 

Katika mkutano huu wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo kwa Nchi za Kusini mwa Afrika SADC,Tanzania inatarajiwa kukabidhiwa kijiti cha uongozi kwa kipindi cha mwaka mmoja ambapo Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli atakuwa Mwenyekiti wa SADC.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja

MATUKIO KATIKA PICHA USAJILI WA NGOs KANDA YA ZIWA JIJINI MWANZA

$
0
0
Mwanasheria kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo yaJamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Idda Kombe (kulia) akitoa huduma kwa mdau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali aliyefika kukamilisha usajili wa shirika lake wakati wa zoezi la usajili wa NGOs zilizokuwa nje ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali linaloendelea katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa jijini Mwanza.
Katibu Mkuu wa Wizaraya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Dkt. John Jingu (kushoto) akizungumza na wadau wa NGOs waliofika kupata huduma za pamoja za usajili wa mashirika yao wakati wa zoezi la usajili wa NGOs zilizokuwa nje ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali linaloendelea katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa jijini Mwanza.
Mwanasheria kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Happy Msimbe akitoa huduma kwa mdau wa NGOs wakati wa zoezi la usajili wa NGOs zilizokuwa nje ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali linaloendelea katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa jijini Mwanza.Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW

WAGENI MBALIMBALI WATEMBELEA BANDA LA BUNGE KWENYE MAONESHO YA NANENANE

$
0
0
Afisa wa Bunge Ndg. Mohamed Salim akitoa Elimu kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Dodoma waliotembelea banda la Bunge kwenye Maonesho ya Wakulima ya Nanenane Jijini Dodoma hii leo. 
Wanafunzi wa Shule ya Awali na Msingi Modern ya Jijini Dodoma wakifurahia Siwa wakati wapotembelea banda la Bunge kwenye Maonesho ya Wakulima ya Nanenane Jijini Dodoma hii leo . (Picha na Ofisi ya Bunge)
Afisa wa Bunge Ndg. Hoseana John akitoa Elimu kwa mgeni aliyetembelea banda la Bunge hii leo kwenye Maonesho ya Wakulima ya Nanenane yanayoendelea Jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Bunge).

NEWZ ALERT: WATU WENGI WAHOFIWA KUPOTEZA MAISHA MSAMVU,MOROGORO BAADA YA TANKI LA MAFUTA KULIPUKA MOTO.

$
0
0
Ínaripotiwa kuwa Idadi kubwa ya watu wanahofiwa kuungua moto na kupoteza maisha baada ya tenka la mafuta kuwaka moto eneo Msamvu Itigi mkoani Morogoro asubuhi hii. 

Inadaiwa kuwa chanzo  ni watu kutaka kuiba betri kutoka kwenye tenka hio iliyokuwa imepinduka huku wengine wakiiba mafuta, ndipo moto ukalipuka. Juhudi za kuopoa miili zinaendelea.

Aidha Mashuhuda wa tukio hilo wameviambia vyombo vya habari kuwa lori la mafuta (petroli) lilipinduka, hivyo watu mbalimbali, wengi wao wakiwa madereva wa pikipiki wakaenda eneo la tukio na vibebeo kwa lengo la kupata mafuta. 

Vyombo vya Ulinzi na Usalama vimekwishawasili eneo la tukio kwa ajili ya kutoa msaada kwa kadiri itakavyowezekana,ikiwemo na kubaini idadi ya watu waliopoteza maisha.  

MUNGU AZILAZE ROHO ZA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMEN

TUNAENDELEA KUSUBIRI TAARIFA RASMI KUTOKA KWA MAMLAKA HUSIKA.




RC Mwanri azitaka Taasisi za Fedha Kutoa Elimu Ya biashara kwa Wajasiriamali

$
0
0
Na, Editha Edward-Tabora 

Taasisi za fedha hapa nchini zimeshauriwa kutoa elimu ya biashara kwa Wajasiriamali wadogo ili biashara zao ziwe na tija na kuwainua zaidi

Ushauri huo umetolewa na mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri alipotembelea mabanda ya taasisi mbalimbali ikiwemo za kifedha na wajasiriamali wadogo katika viwanja vya maonesho ya nanenane katika manispaa ya Tabora

Pia amesema kuwa wajasiriamali wadogo wanamchango mkubwa sana katika maendeleo ya nchi yoyote ile hapa duniani hivyo wanapaswa kupewa elimu itakayowasaidia kuimarisha biashara zao ipasavyo

Nae Mkuu wa Wilaya ya Tabora mjini Komanya Erick ametoa wito kwa taasisi zote za kifedha zilizoko mkoani humo kuwajengea uwezo Wakulima na Wafanyabiashara wadogo ili waweze kuinuka kiuchumi

Komanya ameendelea kusisitiza kuwa mabenki yana nafasi kubwa sana ya kuwainua Wakulima na Wafanyabiashara kutoka Kiwango cha chini hadi cha juu ikiwemo kuwawezesha kuanzisha viwanda vidogo vya kati na vikubwa 

Aidha amesema kuwa maendeleo makubwa tunayoyaona hapa nchini yanachochewa na kodi inayolipwa na Wafanyabiashara, hivyo akawataka Wafanyabiashara wakubwa wote mkoani Hapa kuwa na mashine za kielektroniki.
Pichani ni mkuu wa mkoa Aggrey Mwanri Akizungumza na mmoja wa taasisi za Benki kuhusu kutoa elimu kwa wajasiriamali.
 Pichani  ni wafanyakazi wa taasisi za kibenki wakizungumza na Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ( pichani hayupo) .

Naibu Waziri Aweso aitaka Halmashauri ya Tarime kuvunja mkataba na mkandarasi wa mradi wa Maji

$
0
0
Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso ameelekeza Halmashauri ya Wilaya ya Tarime kuvunja mkataba na Mkandarasi wa Kampuni ya Kumba Quality Ltd inayotekeleza kazi ya ujenzi wa Mradi wa Maji wa Gamasara, mkoani Mara.

Naibu Waziri Aweso amechukua maamuzi hayo baada ya kukagua mradi na kutoridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa Mradi wa Maji wa Gamasara ulioanza mwaka 2018 na Serikali imeshamlipa mkandarasi kiasi cha Shilingi milioni 50 lakini mpaka kufikia mwezi Agosti, 2019 utekelezaji wake ni asilimia 20 na mkandarasi akiwa ametoweka site bila taarifa yoyote.

Naibu Waziri Aweso amewataka wataalam wa Wakala ya Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) mkoani Mara na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Musoma (MUWASA) kusimamia ujenzi huo na kukamilisha kazi zilizobaki.

Aidha, Naibu Waziri Aweso amekagua moja ya kisima cha maji katika Kijiji cha Gamasara ambacho kinatumia pampu ya maji ya bei nafuu iliyotengenezwa na mhitimu wa Chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), James Ryoba, Mhandisi wa Maji na Umwagiliaji.

Mhe. Aweso amempongeza James Ryoba kwa kuonyesha ubunifu wa kutengeneza pampu ya maji kwa gharama nafuu kwa ajili ya wananchi wa Wilaya ya Tarime.

Amesema Mhandisi Ryoba ni mfano wa kuigwa kwa vijana wote waliohitimu elimu za vyuo nchini kwa kutumia taaluma zao kuwa wabunifu, baada ya kupoteza muda kwa kusubiri kuajiriwa wakati wakiwa na uwezo wa kujiajiri.

Naibu Waziri Aweso amemuelekeza Mkurugenzi wa MUWASA, Mhandisi Robert Lupoja kumpa ajira ya muda kwenye mamlaka hiyo, wakati unafanyika utaratibu wa kumtafutia ajira ya kudumu.

Waziri Lukuvi aunda timu ya kuchunguza maafisa Ardhi waliosimamishwa

$
0
0
KUFUATIA kusimamishwa kwa maofisa ardhi 183 wa Wizara ya Ardhi,nyumba na Maendeleo ya Makazi,Serikali imetoa Siku 30 ili kufanya uchunguzi kwa watendaji hao waliowafutia wateja madeni ikiwemo kupunguza saizi ya ukubwa wa viwanja kupitia mfumo wa malipo na kuisababishia serikali hasara ya mapato yatokanayo na viwanja.

Baada ya uchunguzi wale watakaobainika kutenda makosa hayo hatua Kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao huku wale ambao hawatakutwa na makosa watarejeshwa Kazini.

Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na Waziri Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema kuwa timu ilioundwa kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa watendaji waliohujumu mfumo wa ulipaji malipo ya viwanja itawajumuisha Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) pamoja na taasisi nyingine ambazo zina wataalamu wanaohusika na mifumo inayotumia mitandao.

Hata hivyo amesema kuwa uchunguzi wa timu hiyo utafanyika kuanzia miaka mitatu yani 2016/hadi 2019 ambapo mfumo huo wa kulipia viwanja ulianza kutumika.Mhe.Lukuvi amesema kuwa watendaji waliosimamishwa kazi wamebainika ndani ya miezi sita ya mwaka wa fedha 2018/19 ambapo mfumo wa malipo Hazina ndio umepeleka wao kubainika kwa sababu unaonyesha moja kwa moja.

"Naomba muelewe hawa waliosimamishwa hivi sasa ni wale walioiibia serikali kuanzia sh laki moja na kuendelea,lakini katika uchunguzi utakaofanywa hata kama umeiibia serikali sh moja utachukuliwa hatua za kisheria," amesema Lukuvi.

lengo la kutoa siku hizo chache za uchunguzi ni kutokana na kwamba ushahidi wa mfumo unaonyesha kila kitu kwa hiyo hakuna sababu ya kutumia muda mrefu kufanya uchunguzi."Nimesikia malalamiko yakuwa waliosimaishwa wanasema watu wamewaibia password zao,si kweli hayo ni mawazo yao walijisahau kama mfumo wa malipo wa Hazina unaonyesha Moja kwa Moja ndicho kilichowakamatisha," amesisitiza Lukuvi.

Aidha amewataka waliobaki nao wajiandae na zoezi hilo maana baada ya uchunguzi kuna majina mengine yatabainika kwa sababu wanaanzia kuchunguza tokea mfumo ulipoanza kutumika.

Akitolea mfano wa kiwanja kilichopo mkoani Mbeya ambacho kilikuwa Na square Mita 20,234 lakini katika.mfumo amejaziwa square Mita 502 ambapo amekuwa akilipa sh 63,000 kwa.mwaka badala ya sh mil sita kwa mwaka jambo ambalo ameisababishia Serikali hasara ya sh milioni million 68 tokea kipindi hilo hadi hivi sasa.

" Hivyo nimeuomba nimwambie mwenye kiwanja hicho kama anajua jina hilo ajiandae kulipa fedha hizo pamoja na faini kwa sababu ameibia Serikali pamoja na kuchelewa kulipa ndani ya muda husika," alisema Lukuvi.

Hata hivyo Mhe.Lukuvi amesema kuwa walioshirikiana na watendaji wa Wizara hiyo kufanya mchezo huo wasifikiri wako salama bali watalipa kiasi cha fedha ambacho amefutiwa deni ikiwemo kupunguziwa ukubwa wa kiwanja ambacho amekuwa akilipa fedha pungufu.

Waziri Lukuvi ametolea ufafanuzi huu ya ulipaji wa tozo za kodi ya hati za majengo alisema wananchi wanapaswa kulipa ndani ya miezi sita kuanzia Julai mosi hadi Desemba inamaana ukipitisha muda huo itabidi ulipe na faini.

Hatua hivyo aliwasisitiza wananchi kutokwenda kwa afisa Ardhi kwa ajili ya kufanya malipo ya hati za viwanja Na badala yake wanaweza kulipia benki kupitia simu zao za mkononi na kurejeshewa risiti.

Lukuvi amesisitiza kuwa kuanzia Oktoba mosi mwaka huu huduma zote za upatikanaji wa hati za viwanja zitapatika katika mikoa na kanda kama ilivyokuwa awali ili kuepusha usumbufu kwa wananchi kutoka mikoani kuja Dodoma kufuatilia zoeizi zima la hati.

DC Ndejembi anusa harufu ya ufisadi ujenzi wa Shule ya Sekondari Kongwa

$
0
0
Na Charles James, Michuzi TV

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe Deo Ndejembi ameagiza Mhandisi wa Wilaya hiyo, Christian Mlay pamoja na mhandisi anaejenga mabweni kwenye Shule ya Sekondari Kongwa kuhojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) pamoja na Jeshi la Polisi.

DC Ndejembi amefikia hatua hiyo baada ya kufanya ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa Shule hiyo na kubaini kuwepo kwa ubadhilifu wa fedha za ujenzi katika Shule hiyo kongwe mkoani Dodoma.

DC Ndejembi amesema ameamua kufanya ziara hiyo baada ya kuona ujenzi wa majengo hayo unaenda taratibu tofauti na mkataba walioingia na mkandarasi huku pia akieleza kutoridhishwa na namna majengo hayo yanavyojengwa.

" Lengo lilikua kukagua maendeleo ya ujenzi huu lakini kama mlivyojionea wenyewe hakuna kitu cha maana kilichofanyika, tulitoa maelekezo kwao cha ajabu hawajayafanyia kazi, mkandarasi anajenga kwa kasi ndogo tena kwa kujisikia, ubora wa majengo ni tofauti na makubaliano tuliyoingia nao, mbaya zaidi kuna ufisadi mkubwa kwenye manunuzi ya vifaa vya ujenzi.

" Mhe Rais anafanya kazi kubwa hizi pesa za ujenzi wa Shule hii kongwe imetoka Serikali Kuu, hatuwezi kuruhusu mambo ya hovyo kufanyika, tumepewa nafasi na Mhe Rais lazima tuwatumikie wananchi kwa uadilifu," amesema DC Ndejembi.

Amesema ujenzi huo unahusisha mabweni mawili, madarasa mawili na bwalo la chakula ambapo kiasi cha Shilingi Milioni 290 lakini mpaka sasa kiasi kilichobaki ni Shilingi Laki moja tu huku mkandarasi akiwa hajamaliza kazi.

Mhe Ndejembi amesema sababu zilizosababisha majengo hayo kutokamilika licha kutengewa fedha nyingi ni kutokana na kutofuata maelekezo ya Serikali ya kutumia Force akaunti ambapo walitangaza tenda hali iliyosababisha ununuzi wa vifaa vya ujenzi kununuliwa kwa bei kubwa tofauti na ilivyo kawaida.

Hivyo Mkuu huyo wa wilaya ameagiza TAKUKURU kufuatilia bei ya Manunuzi

ya Bidhaa hizo za Ujenzi ,milioni 74 zilizobaki kwenye akaunti zisitume mpaka uchunguzi ukamilike na wale wote waliohusika katika ubadhilifu huo wanachukuliwa hatua kwa kumdanganya na kumdharau Rais,Waziri wa TAMISEMI pamoja na yeye.
 Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mjs Deo Ndejembi (kulia) akitoa maelekezo kwa mhandisi wa ujenzi wa bwalo shule ya Sekondari ya Kongwa.
DC Ndejembi akiwa kwenye ukaguzi wa ujenzi wa madarasa, mabweni katika Shule ya Sekondari Kongwa.

Timu kutoka Tanzania yaingia fainali Mashindano ya kutafuta ubunifu na suluhisho kimataifa nchini Cambodia

$
0
0
· Yaungana na nyingine 9 kutoka nchi zingine.
· Mshindi kujinyakulia dola za kimarekani $ 50,000

· Bidhaa nyingi zilizochaguliwa ni nzuri na zinawezekana, zinatoa suluhisho kiteknolojia kwa maeneo mengi ya maisha kama mawasiliano ya simu, elimu, IoT, na Biashara kielektroniki. 

Agosti 10, 2019, Kampuni mama ya Viettel na kampuni ya Mawasiliano ya simu ya Halotel wametangaza rasmi orodha ya timu 10 ambazo zilifikia fainali ya mashindano ya Viettel Advanced Solution Track 2019 ambayo yatafanyika katika Phnom Penh nchini Cambodia mnamo Agosti 15, 2019. 

Timu hizo zenye mawazo mazuri sana/ bidhaa nzuri zimechanguliwa kutoka katika makampuni yanayokua ya wajasiriamali zaidi ya 200 kutoka nchi 10 Ulimwenguni. Mawazo hayo yako kwenye miradi iliyo katika fani za Mawasiliano, Elimu, IoT, na Biashara kimtandao.

Mashindano haya yalianza mwezi June 15, 2019 kwa washiriki mbalimbali ulimwenguni kupewa fursa ya kutuma mawazo yao yaliyoambatana na suluhisho ambayo yanaweza kutumika kimataifa katika nyanja mbalimbali hasa katika kuboresha mifumo iliyoko Katika sekta ya Mawasiliano ulimwenguni. 

Kati ya washiriki katika mashindano hayo timu 10 ziliibuka washindi katika mchujo wa kwanza na kuingia katika raundi ya mwisho ambapo washiriki hawa watakutana nchini Cambodia kwaajili ya mashindano ya fainali kupata mshindi wa kwanza.Timu hizo zilizoingia fainali ni pamoja na ya Agrobot kutoka Tanzania. Timu zingine zinatoka Peru, Msumbiji, Kambodia, Indonesia na Vietnam.

Akizungumza wakati wa kutangaza washiriki hao walioingia hatua ya fainali, Mkurugenzi wa Kampuni ya simu Halotel Tanzania, Nguyen Anh Son amesema, “bodi ya washauri ambao ni wataalamu katika fani mbalimbali nchini Cambodia ni wafuatao Bwana Nguyen Manh Dung, Mfuatiliaji wa Shark Tank Vietnam 2019, Mkurugenzi Mtendaji wa mfuko wa uwekezaji wa CyberAgent huko Vietnam na Thailand; Bwana Michael McCarthy, mwanachama wa Kitivo cha Upanuzi; chuo kikuu cha Havard; na Bwana Gene Soo, Mwanzilishi wa StartupsHK Wamezingatia kwa makini kuchaguliwa kwa washiriki hao 10 bora wa raundi hii ya mwisho’.

Aidha, Mkurugenzi huyo, Nguyen Anh Son amesisitiza kuwa kimsingi, bidhaa nyingi zilizochaguliwa zinawezekana, zinatumika na zinatoa suluhisho la kiteknolojia kukidhi mahitaji ya maeneo mengi. 

"Kwa jumla, mawazo/ bidhaa zilizotolewa na washiriki wa Viettel Advanced Solution Track 2019 zimewezekana na kutekelezeka katika maeneo mengi ya maisha. Walakini, mbali na nguvu, mawazo/ bidhaa bado kuna mapungufu ya kushinda. Katika mchakato wa kutathmini, wataalam wanaoongoza watashauriana na watasaidia timu ili kuboresha na kuongeza umuhimu wa utekelezaji wa bidhaa na huduma kuwa tayari kwa matumizi kwa vitendo ”.

Timu zilizochaguliwa zitashindana kwa pamoja katika raundi ya fainali itakayofanyika Agosti 15 2019 huko Phnom Penh (Cambodia) kisha kuchagua "tiketi" 3 za kwenda fainali za VietChallenge –ambalo ni shindano la kifahari la kuanzishwa huko Marekani mnamo Septemba 2019 zenye tuzo ya dola za kimarekani $ 50.000. Alisema Son.

Kuhusu timu ya AGROBOT (Taarifa sahihi kwa Kilimo) kutoka Tanzania, ni huduma inayotumia Ushauri usio asili kusaidia wakulima kutoka kwa kiwango kidogo hadi kikubwa, (wadogo / wakubwa) kupata taarifa sahihi na za kuaminika kuhusu shida za kilimo au ushauri. Kulingana na timu hiyo, nchini Tanzania, wanaamini kuwa ufahamu wa kilimo ndio jambo muhimu kwa mkulima kupata mazao mengi. Kuna wataalam wachache katika vijiji na wadi kwa hivyo ni ngumu kusaidia na kuelimisha kila mkulima kwa wakati anahitaji msaada.

"Tulijiunga na shindano hili sio tu kupata pesa ili kukuza biashara yetu lakini pia kuonesha ulimwengu kuwa tatizo la njaa linaweza kutatuliwa ikiwa wakulima wanayo habari sahihi na ya kitaalam juu ya kilimo cha kisasa. Nchini Tanzania, hakuna bidhaa yoyote iliyopo kama yetu. Katika nchi zingine, zina bidhaa kama zetu lakini zinategemea zaidi mtandao. " Alisisitiza kwa ujasiri Bwana Baridi Mgongowa, kiongozi wa timu, Agrobot.

Inafahamika kuwa majaji na wageni waalikwa wa VietChallenge nchini Merekani unajumuisha Wakurugenzi na Waanzilishi wa nchini Merekani na wengine Ulimwenguni kama vile: Bwana Danny Cowger, Mkurugenzi wa Utawala wa Ortholite - muuzaji na msambazaji anayeongoza ulimwenguni kwa chapa za viatu kama Nike, Adidas, ASICS, Clarks na Mizani Mpya; Bwana Vivek Soni, Mkurugenzi Mtendaji wa TiE Angels Boston; Bwana, Tuan Pham, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Silicon Valley na Wakurugenzi Mtendaji wa Kampuni za Mark Cuban na Washirika wa BDA. Hii inathibitisha kuwa huu ni ushindani uliowekezwa kwa uangalifu, kifahari na ubora. 

Mkurugenzi huyo alibainisha kwamba,pamoja na ujumbe "Kuanza na mtazamo mpya", mashindano ya Viettel Advanced Solution Track 2019 yaliyoandaliwa na Kampuni ya Viettel Group na Halotel kwa kushirikiana na VietChallenge imefungua uwanja sawa wa fani kucheza kwa kuanzia kimataifa kuelezea na tafuta suluhisho zinazochipukia ambazo zinaunganisha nguvu za kimawasiliano na kuunda Bidhaa /Huduma zenye kiwango cha Kimataifa zaidi zinazotumika kwa maisha ya sasa na ya baadaye. Ushindani pia unaonyesha kuungwa mkono na Viettel kwa mara ya kwanza ili kuunganisha ndoto ya kufikia Ulimwengu.

Kwa maelezo ya Track ya Advanced Solution Track 2019 tafadhali tembelea: http://vas.viettel.vn./.
 Timu ya Agrobot kutoka Tanzania AGROBOT (Taarifa sahihi kwa Kilimo)
 Timu ya Peru kuhusu  suluhisho la uthibitisho wa simu katika matumizi.
 Timu kutoka Cambodia kuhusu jukwaa la kidijitali ambalo linaruhusu wamiliki wa biahsra za kufua mavazi na wateja wao kujisikia huru kushirikiana na kila mmoja.
 Timu ya Msumbiji kuhusu PortalMuhimu ya Kidijitali.
Timu Vietnam kuhusu suluhisho la kiteknolojia lililojaa ubinadamu kwa watu wenye ulemavu.

SBL yapanda miti 1,000 mkoani Kilimanjaro ili kuchochea utunzaji wa mazingira

$
0
0


Mjumbe kutoka ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania akishiriki zoezi la upandaji miti lililondaliwa na kampuni ya Serengeti Breweries Ltd mkoani Kilimanjaro. 
Ujumbe kutoka ubalozi wa Uingereza ukifurahia jambo ulipofanya ziara katika kiwanda cha SBL mjini Moshi.
Mkurugenzi mtendaji wa SBL, Mark Ocitti (wa pili kushoto) akitoa maelezo juu namna kiwanda kinavyofanya kazi kwa ujumbe kutoka nchini Uingereza uliotembelea kiwanda hicho.
Ujumbe kutoka ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania ukishriki zoezi la upandaji miti liliondaliwa na kampuni ya Serengeti Breweries Ltd mkoani Kilimanjaro.


Kama hatua ya kuchangia katika jitihada za utunzaji wa mazingira pamoja na vyanzo vya maji mkoani Kilimanjaro, kampuni ya bia ya Serengeti, Serengeti Breweries Limited (SBL) kwa kushirikiana na taasisi ya The Kilimanjaro Project imezindua kampeni ya kupanda miti elfu moja mkoani humo.

Miti hiyo imepandwa katika kiwanda cha SBL kilichopo Pasua katika wilaya ya Moshi na mingine imepandwa katika wilaya ya Mwanga.

Akizungumza wakati wa zoezi la upandaji miti, Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Mark Ocitti, amesema SBL imeamua kuongeza jitihada za uhifadhi wa mazingira si tu katika maeneo yaliyo chini ya SBL bali katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania.“Huu ni udhihirisho tosha kwamba SBL imejidhatiti na iko tayari kushirikiana na wadau wengine katika kutekeleza miradi yenye kuleta tija kwa jamii zetu,” amesema Ocitti.

Zoezi la upandaji miti linakuja huku kukiwa na wito kutoka jumuiya ya kimataifa juu kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa kwa kuongeza juhudi za uhifadhi wa misitu ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi na hivyo kuyaweka mazingira katika hali ya usalama kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Mpango huu wa SBL unaenda sambamba na sera ya kampuni katika kurudisha kwa jamii sehemu ya faida, na umejikita zaidi katika utoaji wa huduma bora ya maji safi kupitia mradi uitwao Water of Life (WOL); mpango kwa ajili kuwasaidia wanafunzi kupata ufadhili wa masomo ya elimu ya juu, kuwasaidia wakulima wa ndani hususani wa vijijini pamoja na mpango wa kuhamasisha unywaji pombe kistaarabu.

Zoezi la upandaji miti limehudhuriwa na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Sara Cooke pamoja na Mwakilishi wa Waziri Mkuu wa Uingereza kitengo cha biashara, Andrew Rosindell, ambao walikuwa ziarani kiwandani hapo.

UTUPAJI HOLELA WA TAKA KUDHITIBITIWA – SIMA

$
0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Henry Mbaga kuhusu shughuli za ujenzi wa dampo la kisasa katika Jiji la Mwanza eneo la Buhongwa. Jiji la Mwanza linatelekeleza mradi mkubwa wa Kimkakati wa ujenzi wa dampo ambalo lina ukubwa wa hekta 34 na linatarajia kukamilika 9/12/2019 kwa gharama ya shilingi Bilioni 16.6
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dkt. Philis Nyimbi na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Bw. Kiomoni Kibamba kwa pamoja wakikagua maendeleo ya ujenzi wa dampo la kimkakati. Naibu Waziri Sima ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa dampo hilo la kisasa ambalo limezingatia hifadhi ya mazingira.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dkt. Philis Nyimbi katika kikao na wafanyabiashara wa vyuma chakavu Kanda ya Ziwa (hawapo pichani). Naibu Waziri Sima yuko katika ziara ya kikazi Mikoa ya Kanda ya ziwa yenye lengo la kusikiliza na kutatua changamoto zinazohusu sekta ya Mazingira nchini.

…………………………

Na Lulu Mussa,Mwanza

Serikali imezitaka halmashauri zote nchini, kutenga maeneo maalumu mbali na makazi ya watu yatakayotumika kujenga madampo ya kisasa ili kuzingatia hifadhi ya mazingira.

Rai hiyo imetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima mara baada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa dampo la kisasa linalojengwa eneo la Buhongwa Jijini Mwanza.

Alisema ujenzi wa huo wa dampo la kisasa utasaidia juhudi za Serikali za kutotumia fedha nyingi kwenye ununuzi wa vifaa tiba kwa kuwa taka zitakazolishwa katika Jiji la Mwanza zitapelekwa dampo kwa wakati na kunusuru magonjwa ya mlipuko.

“Huwezi kutenganisha afya na mazingira, mradi huu ni mkubwa sana na kwa namna utakavyotekelezwa hatutaraji kuona taka mjini zinazagaa.Tunatarajia kuona taka zote zinakuja hapa,” alisema Sima.

“Natoa rai kwa halmashuri zingine ambazo zinatekeleza miradi ya kimkakati kutoa kipaumbele kwa ujenzi wa madampo ya kisasa”.

Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Kiomoni Kibamba alisema dampo hilo lina ukubwa wa hekta 34 na linatarajia kukamilika desemba mwaka huu na kwa sasa ujenzi upo asilimia 78 ukigharimu Sh bilioni 16.6, ukienda sambamba na ujenzi wa barabara.

“Dampo hilo litakuwa na chemba sita za kuhifadhi taka na mabwawa ya kuhifadhi maji taka, barabara za kisasa zenye urefu wa kilomita 1.9, taa za nishati ya jua na maabara maalumu ya kupima maji taka” Kibamba alisema 

Kukamilika kwa dampo hilo la kisasa litakuwa na uwezo wa kuteketeza taka mara baada ya kufikishwa kwenye eneo hilo na,litaongeza mapato katika jiji hilo.Kwa mujibu wa Kibamba, tani 33 hadi 36 zinatarajia kupelekwa katika dampo hilo mara baada ya ujenzi kukamilika na linatarajia kudumu kwa zaidi ya miaka 15

MWAUWASA wazungumzia mabadiliko ya bei mpya za maji

$
0
0
 Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira jijini Mwanza (MWAUWASA) imetoa ufafanuzi kuhusu mabadiliko mapya ya ankra za maji huku ikitumia fursa hiyo kuwaelekeza wafanyabiashara wa maji kwamba bei elekezi kwa ndoo moja ya maji yenye ujazo wa lita 20 ni shilingi 50 tu.

Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Antony Sanga alitoa ufafanuzi huo Agosti 09, 2019 kwenye ziara ya waandishi wa habari mkoani Mwanza kutembelea miradi mbalimbali ya maji inayosimamiwa na mamlaka hiyo ili kujifunza utendaji kazi wake.
Na George Binagi-GB Pazzo, Mwanza
 Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Antony Sanga akitoa ufafanuzi kwa wanahabari (hawako pichani)  kuhusu miradi ya maji inayosimamiwa na mamlaka hiyo pamoja na ongezeko la bei mpya ya maji.
 Wanahabari walitembelea eneo hili la mradi wa maji Capripoint jijini Mwanza kujifunza maji yanavyosafishwa na kutibiwa kabla ya kumfikia mtumiaji.
 Mradi wa maji MWAUWASA Capripoint jijini Mwanza.
Wanahabari pia walitembelea mradi mpya wa maji Nyahiti wilayani Misungwi na kushuhudia kwa mara ya kwanza mashine za kusukuma maji zikiwashwa kwenye mradi huo.
 Tenki kubwa la kusambazia maji katika mji wa Misingwi kutoka chanzo cha maji Nyahiti.
 Ziara hii iliratibiwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa Mwanza (MPC) ikilenga pia kuimarisha mahusiano na MWAUWASA.
Tazama Video hapa chini

SERIKALI HAITAKUWA TAYARI KUONA MIFUGO YETU INANUFAISHA NCHI NYINGINE-ULEGA

$
0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

Serikali imesema kuwa haitakuwa tayari kuona rasilimali za nchi yetu zinatoka hapa nchini badala ya kunufaisha wananchi wa Tanzania zina kwenda kuzinufaisha serikali za nchi zingine .

Naibu Waziri Wa Wizara ya Mifugo na uvuvi Abdalla Ulega  ameyasema hayo Leo wakati akiongea na wafugaji na wafanyabiashara Wa wilayani Longido  wakati alipofanya ziara ya kukagua na kujionea  miradi mbalimbali ya Mifugo pamoja na kusikiliza kero mbalimbali za wafugaji na wafanyabiashara Wa Mifugo

Alisema kuwa serikali haitamfumbia macho mfugaji yeyote ambaye atatorosha Mifugo na kupeleka nje ya nchi kwani atakuwa anapoteza mapato makubwa ya nchi ,kwani atakuwa amekwepa kulipa tozo mbalimbali ikiwemo kodi ya serikali

Alisema kuwa katika kuthibiti hili serikali imepiga hatua kubwa katika kuzibiti utoroshwaji Wa Mifugo kwenda nje ya nchi kwani hadi sasa wameweza kuweka ulinzi mkali wa askari polisi katika mipaka yetu ambapo amebainisha kuwa  kwa sasa utoroshwaji Wa Mifugo umepungua kwa asilimia 90% hali iliosababisha makusanyo kupanda kutoka milioni sita kwa Siku kwa kipindi  hakuna walinzi na kufikia makusanyo ya shilingi milioni tisa kwa Siku  kwa kipindi ambacho askari Polisi wapo

"Askari polisi hawa wanaolinda mipaka yetu wamesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza utoroshwaji Wa mifugo  Nana penda kusema tutaongeza bajeti kwaajili ya kuwalipa askari hawa kwani wanafanya kazi vizuri"

Aidha Naibu Waziri alitoa agizo kwa halmashauri zote hapa nchini kuweka mizani za kupimia uzito ng'ombe katika minadani yote ili kuweza kupima mifugo yao na sio kuuza kwa kukadiria kilo hii itasaidia kumnufaisha mfugaji na sio mfanyabiashara tu.

"Hichi kitendo cha kukisia uzito Wa ng'ombe serikali hauutaki kwani unamuumiza sana mfugaji,kwani anakuwa anauza mfugo wake kwa hasara na anakuwa anamnufaisha mfanyabiashara na mfugaji anadidimia kitu ambacho serikali atukubali kumuona mfugaji ananyanyaswa ,kwa kuzulumiwa serikali yetu inataka kumuinua mfugaji na sio kumdidimiza ,na serikali yetu mnajua inatetea wanyonge" alisema Ulega

Aidha alisema kuwa serikali itawapa Elimu ya kutosha kuhusiana na tozo na hasara za utoroshwaji Wa Mifugo  ili wafugaji hao wasiendelee kutorosha Mifugo hiyo,kwani imebainika kuwa wafugaji wengi hawana Elimu ya kutosha ya sheria za utoroshwaji Wa mifigo,uku akibainisha kuwa iwapo mfugaji  atakamatwa anatorosha Mifugo sheria Kali itafuatwa ikiwemo kupelekwa mahakamani pamoja na kulipa faini .

 Kwa upande  wananchi  hao walitumia muda huo kuomba serikali kuwapa kipaumbele cha kuuza Mifugo yao katika soko la kimataifa linalotarajiwa kufunguliwa katika Kijiji cha  Olendeki kilichojengwa karibu na Mpaka Wa Namanga uliopo wilayani Longido mkoani hapa.

Nae mbunge Wa jimbo la Longido Steven Kiluswa aliomba serikali kuwapunguzia tozo wanazolipia Mifugo kwani iwapo watapunguziwa ,wataacha kabisa kutorosha Mifugo  nafedha zitaingia serikalini na mapato ya nchi yataongezeka ,aidha pia aliomba serikali kuanda semina za kuwaelimisha wafugaji juu ya Elimu ya kodi pamoja na tozo wanazolipa.
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images