Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

BILIONI 4.6 KUJENGA NA KUKARABATI CHUO CHA UFUNDI KARAGWE

$
0
0
Baadhi ya majengo yanayojengwa katika Chuo cha Ufundi cha Halmashauri ya Wilaya yaa Karagwe, ambapo serikali kupitia wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetenga zaidi ya shilingi bilioni nne kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya majengo katika chuo hicho.







Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Wiliam Ole Nasha akizungumza na viongozi na wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya sekta a elimu wilayani humo.


Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Wiliam Ole Nasha akisikiliza maelezo kuhusu utekelezaji wa mradi wa ujenzi na ukarabati wa Chuo cha Ufundi cha Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe


Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Wiliam Ole Nasha akizungumza na wanafunzi wa wanaosoma katika Chuo cha Ufundi cha Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe, ambapo amewasisitiza kusoma kwa bidii na kuwataka kuthamini mafunzo wanayoyapata kwani muhimu katika kujiletea maendeleo na kushiriki katika kukuza uchumi wa nchi.

…………………….

Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetoa zaidi ya shilingi bilioni 4.6 kutekeleza mradi wa ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya majengo ya Chuo cha Ufundi cha Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe.

Hayo yamesemwa Wilayani Karagwe na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Wiliam Ole Nasha katika ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya sekta ya elimu katika wilaya hiyo, ambapo amesema lengo la kutekeleza mradi huo ni kuongeza udahili wa wanafunzi wanaochukua masomo ya ufundi.

Ole Nasha amesema serikali imeweka mkakati wa kukarabati na kujenga vyuo vya ufundi katika kila wilaya, kwani ili kufikia uchumi wa viwanda ni muhimu kama nchi kuwa na vijana wenye maarifa na stadi mbalimbali za ufundi zitakazowawezesha kuajiriwa, kujiajiri na kushiriki katika uchumi wa viwanda.

“Rais ameweka nguvu nyingi katika kuinua uchumi wa nchi yetu, mnaona sasa miradi mikubwa inakuja, hospitali zinajengwa, barabara za lami nyingi zinajengwa, kwa hiyo kuna mambo mengi yanafanyika katika ujenzi na miradi yote hii yote yanahitaji ufundi, hivyo mtambue ufundi ni kitu muhimu sasa” ameongeza Ole Nasha.

Wakati huo huo, Naibu Waziri ametoa miezi mitatu kwa wakala wa majengo Tanzania (TBA) kuhakikisha wanamaliza ujenzi na ukarabati wa chuo hicho, ambapo amesema hajaridhishwa na sababu zilizotolewa na mhandisi msanifu kutoka TBA zilizopelekea kutokamilika kwa mradi kwa wakati.

Ole Nasha anesisitiza kuwa hakuna wakati wowote ambao fedha iliyopaswa kutolewa imeshindwa kutolewa na VETA kwani mpaka sasa TBA imeshalipwa zaidi ya shilingi bilioni moja ambayo ni asilimia 25 ya fedha yote iliyopaswa kulipwa wakati ujenzi umefikia asilimia 44 tu.

Awali Mhandisi Msanifu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Kelvin Joas alimweleza Naibu Waziri kuwa kutokukamilika kwa mradi huo kwa wakati nikutokana na changamoto mbalimbali zilizojitokeza ikiwemo za kimkataba na kuwapelekea kuomba kuongezewa muda wa miezi sita baada ya muda wa mkataba kuisha Julai 26,2019.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya, Godwin Kitonka amesema Halmashauri yake inaishukuru serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kutenga fedha zaidi ya bilioni 4.6 kwa ajili ya kujenga majengo mapya ambayo ni pamoja na jengo la utawala, ukumbi mdogo, vyoo vya nje, bweni la wasichana na kukarabati karakana ya ushonaji na uchomeleaji chuma.

Mwanafunzi Masau Josephat, ameishukuru serikali kwa kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia pamoja na kuongeza majengo ambayo awali hayakuwepo kwani mwanzoni hayakuwa yakiidhisha, huku wakiiomba serikali kuongeza baadhi ya kozi ambazo hazipatikani chuoni hapo ili kupanua wigo wa upatikanaji wa maarifa na stadi kwa vijana wa Karagwe na maeneo ya jirani.

Rais Magufuli atoa salamu za rambirambi kufuatia vifo vya ajali ya lori la mafuta Morogoro

$
0
0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ya vifo vya watu zaidi ya 60 na majeruhi takribani 70 walioungua kwa moto baada ya lori lililokuwa na shehena ya mafuta kupata ajali na kisha kulipuka moto Mjini Morogoro.


Ajali hiyo imetokea leo tarehe 10 Agosti, 2019 majira ya saa 2 asubuhi ambapo lori hilo lililokuwa linatoka Dar es Salaam limepinduka jirani na Kituo Kikuu cha Mabasi cha Msamvu baada ya dereva wa lori kumkwepa mwendesha pikipiki na kisha mafuta yaliyokuwa yakimwagika kushika moto na kuunguza watu waliokuwa wanayachota.


Mhe. Rais Magufuli ametoa pole kwa familia, ndugu, marafiki na wote waliopoteza jamaa zao katika ajali hii na pia amewaombea majeruhi wapone haraka.


“Nimeumia sana kusikia idadi kubwa ya Watanzania wenzetu waliopoteza maisha katika ajali hii, natoa pole kwa wote walioguswa na vifo hivi hasa familia za Marehemu wote, nawaombea Marehemu wapumzike mahali pema peponi na majeruhi wote wapone haraka”amesema Mhe. Rais Magufuli na kumuagiza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Steven Kebwe kufikisha salamu zake za pole kwa familia na wote walioguswa na vifo hivyo.


Mhe. Rais Magufuli ameagiza Wizara zote zinazohusika kushughulikia ajali hii na ametaka Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa kushirikiana na Hospitali ya Taifa Muhimbili kuhakikisha majeruhi wote wanapatiwa matibabu ili kuokoa Maisha yao.


Aidha, Mhe. Rais Magufuli ameelezea kusikitishwa kwake na vitendo vya watu kuvamia magari yanayopata ajali kwa lengo la kujipatia bidhaa mbalimbali zilizobebwa na magari hayo na ametaka vitendo hivyo vikome.


“Baadhi ya magari haya yanabeba mafuta ambayo ni hatari kama ilivyotokea Morogoro, yapo magari yanabeba kemikali za sumu, yapo magari yanabeba milipuko nakadhalika, nawaomba sana tuache tabia hii” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.

 

 
Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

10 Agosti, 2019


WAJUMBE SADC WASIFU JUHUDI ZA SERIKALI KUHAMASISHA UWEKEZAJI WA VIWANDA

$
0
0

*Wengine wasifu teknolojia ya hali ya juu walioyoina kwenye viwanda vya Tanzania

*Wakiri Tanzania inaweza kuliteka solo la Jumuiya ya SADC ,waona fursa lukuki

WAJUMBE wa Mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo kwa Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC) wametapa nafasi ya kutembelea viwanda 21vinavyofanya uzalishaji kwa ajili ya kuangalia ubora wa bidhaa na mazingira ya uzalishaji kwa Tanzania Bara na Zanzibar.

Wakiwa katika viwanda hivyo wajumbe hao wamekiri na kuridhishwa na ambavyo Serikali ya Tanzania namna ilivyodhamiria katika Uwekezaji katika viwanda huku wakieleza wazi Tanzania wanayo nafasi kubwa ya kumiliki soko la Jumuiya hiyo kwani kuna kila.kitu zikiwemo malighafi za uhakika.

Baadhi ya wajumbe wa SADC wameiambia Michuzi TV na Michuzi Blog kuwa Tanzania ipo katika nafasi nzuri ya kulimiliki soko la jumuiya hiyo kwa kuwa kuna nguvu kazi ya kutosha na malighafi za uhakika.

Mjumbe kutoka nchini Afrika Kusini wa Kampuni ya Flexion Renatus Joseph amesema kwamba yeye yupo katika sekta ya viwanda vya chuma jijini Johannesburg, Afrika Kusini na kwamba aliyoyashuhudia katika kiwanda cha Lodha Group of Companies yamenifanya abadili fikra zake kuhusu uwezo wa viwanda kwa nchi ya Tanzania.

Amesema amethibitisha kwa macho yake kuna matumizi makubwa ya teknolojia katika utengenezaji bidhaa za nondo na vifaa vingine vitokanavyo na chuma. "Hakika vikipatikana viwanda vingi vya namna hii SADC tutapiga hatua na tutakuwa na bidhaa zinazoleta ushindani ndani na nje ya Afrika,” amesema.

Wajumbe hao wakiwa kiwandani hapo yameelezwa kiwanda hicho cha chuma kilichopo Mkuranga mkoani Pwani ni miongoni mwa viwanda vilivyoitikia mwito wa Rais Dk. John Magufuli kwa vitendo kuhusu Tanzania ya viwanda.

Akizungumza mbele ya ujumbe wa SADC waliotembelea kiwandani hapo Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Mhandisi Kamara Gombe amesema Tanzania kwa sasa inazalisha tani 200,000 za bidhaa za viwanda huku mahitaji ni tani 300,000.

"Hii maana yake kuna uhaba wa tani laki moja kwenye soko. Hivyo, Kampuni ya Lodhia ni miongoni mwa wadau wa viwanda wanaohakikisha Tanzania inajitegemea katika sekta ya viwanda.Hata hivyo, mbali ya uhitaji huo wa tani laki moja bado kuna tatizo la uhaba wa soko kwa kuwa wanazalisha tani 3000 kwa mwezi

"Lakini uwezo wao ni kuzalisha tani 10,000. Kazi yetu viwanda ni kulinda viwanda vya ndani, tutahakikisha tatizo hili tunalitafutia ufumbuzi ili hizi tani 7,000 zilizobaki ziweze kuzalishwa,” amesema Gombe.

Wakati Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Toni Filbert amesema wilaya hiyo pamoja na Mkoa wa Pwani kwa ujumla wanazo fursa nyingi za uwekezaji kutokana na ardhi kubwa yenye rutuba. Vilevile, kuna bidhaa nyingi za kimkakati zinazozalishwa na wazawa.

Akitoa maelezo kuhusu uwezo wa kiwanda hicho, Mkurugenzi Mkuu wa Lodhia Group of Companies,Sailesh Pandit alisema kampuni hiyo ilianzishwa mwaka 1996 wakiwa wanafanya biashara ya jumla ya kuuza vyuma ambapo mwaka 2004 ndio walianza kuzalisha vyuma katika kiwanda kilichopo mkoani Arusha.

“Vilevile tuligeukia bidhaa nyingine ikiwemo mabomba ya maji, Gypsum Board, matenki ya ya kuhifadhia maji na bidhaa nyingine za ujenzi kwa kuhakikisha Tanzania ina

jitosheleza katika vifaa vya ujenzi bila kuagiza nje ya nchi,” amesema Pandit na kufafanua wanamshukuru Rais Magufuli kwa kuwahamasisha kuwekeza kwa nguvu na pia amesaidia kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji kwa kila kampuni bila kupendelea.

Mkurugenzi huyo pia aliiomba serikali kuangalia uwezekano wa kuweka “kodi kinzani” kwa asilimia kati ya 30/40 kwa bidhaa za chuma kutoka nje ili kuvilinda viwanda vya ndani ambavyo kwa pamoja vina uwezo wa kuzalisha zaidi ya tani 400,000 kwa mwaka iwapo viwanda hivyo vitafanya kazi kwa asilimia 100.

“kwasasa sisi tunafanya kazi kwa massaa nane tu badala ya masaa 24 na sababu kubwa ni kukosekana kwa soko la ndani la uhakika la bidhaa za chuma kutokana na hatua ya serikali kuruhusu chuma kutoka nje kuingizwa bila ya kulipiwa ushuru hasa kutoka nchi za SADC”alisema Mkurugenzi huyo.

Pandit aliongeza kuwa hatua ya serikali kuweka kodi kinzani italeta manufaa makubwa ya kiuchumi kwa kuongeza ajira kwa watanzania na serikali kuongeza mapato yake.

Mkurugeni Mkuu wa Kampuni ya Lodhia Group of Companies , Sailesh Pandit akisoma hotuba yake fupi mbele ya Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda,ambao wametembelea kiwanda hicho leo kwa ajili ya kuangalia ubora wa bidhaa na mazingira ya uzalishaji kwa Tanzania. 
Mkurugeni Mkuu wa Kampuni ya Lodhia Group of Companies Sailesh Pandit ,akizungumza na baadhi ya Waandishi wa habari walioambatana na Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda,ambao wametembelea kiwanda hicho leo kwa ajili ya kuangalia ubora wa bidhaa na mazingira ya uzalishaji kwa Tanzania. 




Mkurugenzi Mkuu wa Lodhia Group of Companies, Sailesh Pandit  (pili kushoto) akionesha kipande cha nondo huku akieleza namna ambavyo hutengenezwa hatua kwa hatua na hatimaye kupelekwa sokoni kwa kuuzwa,mbele ya Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda  waliotembelea kiwanda hicho kwa ajili ya kuangalia ubora wa bidhaa na mazingira ya uzalishaji kwa Tanzania. 
  Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda  wakiangalia namna nondo zinavyotengenezwa hatua kwa hatua ndani ya kiwanda cha Lodhia Group of Companies kilichopo MKuranga mkoani Pwani.Wajumbe hao wametembelea kiwanda hicho kwa ajili ya kuangalia ubora wa bidhaa na mazingira ya uzalishaji kwa Tanzania. 
Mkurugenzi Mkuu wa Lodhia Group of Companies, Sailesh Pandit (kulia) akiwa na Meneja wa kiwanda hicho Harminder Bhachu wakiwaongoza Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC waliofika kutembelea kiwanda hicho.
Mkurugenzi Mkuu wa Lodhia Group of Companies, Sailesh Pandit  akieleza kuhusu namna Nondo zinavyotengenezwa hatua kwa hatua na hatimaye kupelekwa sokoni kwa kuuzwa,mbele ya Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda  waliotembelea kiwanda hicho kwa ajili ya kuangalia ubora wa bidhaa na mazingira ya uzalishaji kwa Tanzania. 

Pandit  alisema kampuni hiyo ilianzishwa mwaka 1996 wakiwa wanafanya biashara ya jumla ya kuuza vyuma ambapo mwaka 2004 ndio walianza kuzalisha vyuma katika kiwanda kilichopo mkoani Arusha.“Vilevile tuligeukia bidhaa nyingine ikiwemo mabomba ya maji, Gypsum Board, mapipa ya kuhifadhia maji na bidhaa nyingine za ujenzi kwa kuhakikisha Tanzania inajitosheleza katika vifaa vya ujenzi bila kuagiza nje ya nchi,” alisema Bhachu na kuongeza.
 Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC  wakipewa maelezo namna ya uzalishaji wa Nondo unavyofika
Mkurugeni Mkuu wa Kampuni ya Lodhia Group of Companies Sailesh Pandit akiwaongoza Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda  waliotembelea kiwanda hicho leo kwa ajili ya kuangalia ubora wa bidhaa na mazingira ya uzalishaji kwa Tanzania. 
Meneja wa Kampuni ya  Lodhia Group of Companies, Harminder Bhachu akiwaonesha Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC nondo zikiwa tayari kusafirishwa maeneo mbalimbali kwa matumizi.
 Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda  wakiangalia namna mabomba ya Platic yanavyotengenezwa  ndani ya kiwanda cha Lodhia Group of Companies, hatua kwa hatua na hatimaye tayari kwa matumizi
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Toni Filbert akizungumza mbele ya Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda (hawapo pichani) mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea kiwanda cha Lodhia Group of Companies,kilichopo wilayani humo mkoani Pwani,Mh.Filbert alisema wilaya hiyo pamoja na Mkoa wa Pwani kwa ujumla wanazo fursa nyingi za uwekezaji kutokana na ardhi kubwa yenye rutuba. Vilevile, kuna bidhaa nyingi za kimkakati zinazozalishwa na wazawa. 

“Tunaihakikishia serikali kuwa kazi tunaiweza, tutatoa fursa za ajira na kuzifanyia kazi rasilimali tulizonazo kwa ajili ya Tanzania mpya ya viwanda. Tunaomba, kampuni kama hizi za kimkakati zipewe fursa katika kushiriki ujenzi wa miradi mikubwa ikiwemo SGR na miradi mingine ikiwemo madaraja na barabara,” alisema Filbert. 

WATU 62 WAPOTEZA MAISHA BAADA YA ROLI LA MAFUTA KUPINDUKA ENEO LA MSAVU MKOANI MOROGORO

$
0
0

Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi CP Liberatus Sabas (kulia) akipokea taarifa kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Mtafungwa baada ya kuwasili Mkoni Morogoro baada ya kutokea ajali ya lori lililoungua moto na kusababisha vifo vya watu 62 na wengine 72 kujeruhiwa katika eneo la Msamvu Itigi Mkoani humo. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Maafa, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Nasser Mwakamboja.
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi CP Liberatus Sabas akikagua lori la mafuta lililopata ajali na kuungua moto Msamvu Itigi Mkoani Morogoro na kusababisha vifo vya watu 62 na wengine 72 kujeruhiwa. Nyuma yake ni Mkuu wa Kitengo cha Maafa, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Nasser Mwakamboja
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, CGF Thobias Andengenye akizungumza na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi CP Liberatus Sabas (katikati) na Mkuu wa Kitengo cha Maafa cha Jeshi la Polisi ACP Nasser Mwakamboja wakiwa katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro walipowasili kuona majeruhi walioungua moto baada ya kutokea ajali ya lori lililoungua moto na kusababisha vifo vya watu 62 na wengine 72 kujeruhiwa katika eneo la Msamvu Itigi Mkoani humo. Picha na Jeshi la Polisi.

=========  ========  ========

*Wengine 70 wajeruhiwa, ni waliokuwa wanakuwanda kuzoa mafuta kwenye madumu 

*Wengi wao ni vijana wa bodaboda...mashahidi waeleza iliyokuwa eneo la tukio

Na Said MwisheheMichuzi TV

INASIKITISHA SANA! Ndivyo unavyoweza kuelezea kutokana  na kufariki dunia kwa watu 62 na wengine 70 kujeruhiwa na moto huo baada ya kulipukiwa kwa moto baada ya kukimbia  kutoa mafuta ya petroli baada ya gari aina ya roli kupinduka leo eneo la Msavu mkoani Morogoro.
 
Ajali hiyo imetolewa leo Agosti 10,2019 asubuhi katika eneo hilo la Msavu ambapo mashuhuda wa ajali hiyo wameiambia.Michuzi TV kuwa roli ya mafuta ilipinduka baada ya kumkwepa dereva bodaboda,hivyo roli likaacha njia.

Mmoja wa mashuhuda aliyejitambulisha kwa jina la  Bathromeo amesema baada ya ajali hiyo kutokea baadhi ya wananchi waliokuwa eneo hilo walianza kukimbia roli hilo wakiwa na madamu na ndoo wa ajili ya kubeba mafuta.

Hata hivyo baada ya roli kupinduka yaliyoanza kumwagika yalikuwa mafuta ya dizeli na nusu baadae yakaanza kutoka mafuta ya petroli."Ukweli mimi tangu ajali inatokea nilikuwa hapa na nimeona kila kilichokuwa kinaendelea.Wenzetu wenye tamaa waliamua kwenda na  madamu yao kuchukua mafuta,tuliwakataza lakini kwa tamaa zao waliamua kwenda.

"Hapa kuna mama alikuwa anauza chakula lakini baada ajali kutokea akachukua ndoo zake na kwenda kujaza mafuta na kisha kuyaweka hapa kwenye eneo analopikia.Matokeo yake yeye na mtoto wake wamekufa.Inasikitisha sana lakini ajali za aina hii zimekuwa zikitokea ila wananchi hatujifunzi,"amesema shuhuda huyo.


Kwa upande wake shuhuda mwingine amesema vijana waliokuwa eneo hilo yakiwemo wateja na waendesha bodaboda walionekana kubeba madamu na kwenda kuchota mafuta lakini ghafla ukasikika mlipuko mkubwa ambao tulisababisha gari hiyo kuanza kuwaka moto ambao ulikuwa unasambaa kwa kasi kubwa.

Hivyo kutokana na moto huo waliokuwa wakizoa mafuta wakaanza kuungua na wengi wamekuwa kwa kuteketea kwa moto huo ."Wamekufa watu wengi sana kwenye ajali hii ya kulipuka kwa roli la mafuta eneo hili la Msavu.

Amesema kuna baadhi yao walijaribu kukimbia lakini wakati huo tayari moto ulishakuwa umesambaa mwilini na kwamba kuna mmoja alijaribu kupanda juu ya moto lakini mti nao kuanza kuweka.

Hata hivyo tayari viongozi wa ngazi mbalimbali wa Mkoa wa Morogoro wamezungumzia ajali hiyo ambayo imesababisha vifo vya watu hao na kwamba wataendelea kutoa taarifa zaidi ya idadi ya rasmi ya waliopoteza maisha na waliojeruhiwa ingawa tayari watu 62 wameriporiwa kupoteza maisha na wengine zaidi ya 70 wamejeruhiwa kwa moto.

Wakati huo huo Kamanda mstaafu wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaaam Suleiman  Kova ambaye kwa sasa Mkurugenzi wa taasisi binafsi iliyosimamia maafa na majanga amesema ajali hiyo inasikitisha kwani idadi kubwa ya nguvu kazi imepotea.

Kova amesema kwa taarifa zilizopo hadi mchana huu tayari wameporipotiwa watu 62 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 70 wameungua na moto huo na sasa wakimbikizwa Hospitali ya Taifa Muhimbili ili kuokoa maisha yao.

"Ni ajali mbaya sana,watu wengi wamepoteza maisha.Ukweli wengi waliopoteza maisha ni wale waliokuwa wanakwenda kuchukua mafuta baada ya roli kupinduka. Ni mara nyingi elimu imekuwa ikitolewa kuhamasisha wananchi kutokimbilia mafuta baada ya gari kupinduka.

" Ni mara nyingi tumeshuhudia matukio ya aina hii na watu wamekuwa wakipoteza maisha.Ndio maana enzi zetu tuliamua kuanzisha Polisi shirikishi ili wananchi wenyewe kwa wenyewe wazuiane, Hata hivyo moto ni jambo la dharura,hivyo hakuna wa kulaumiwa na hata waliokufa hatuwezi kuwalaumu," amesema Kova.

Ametoa rai kwa wananchi kujiepusha  na  majanga kwa kuhakikisha wanachukua tahadhari na kusisitiza ajali hiyo ni mafunzo huku akitumia nafasi hiyo kutoa pole kwa Rais,Mkuu wa Mkoa wa Morogoro  na Watanzania wote kwani msiba huo ni mkubwa.

Pia viongozi wa dini wamezungumzia ajali hiyo ambapo kwa sehemu kubwa wamesisitiza jamii.kujenga utamaduni wa kuchukua tahadhari na kubwa zaidi ni ajali inatopotokea cha kwanza ni kusaidia waliopata ajali badala ya kufanya tofauti na hivyo.

WANAOKWENDA KINYUME NA BEI ELEKEZI YA SERIKALI WACHUKULIWE HATUA

$
0
0
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akisisitiza jambo wakati wa ziara ya Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mheshimiwa Dk. Sira Ubwa Mamboya (aliyeketi kulia kwake) alipotembelea makao makuu ya Shirika la Posta Tanzania
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mheshimiwa Dk. Sira Ubwa Mamboya (wa pili kushoto) akisikiliza maelezo na kuangalia gari lenye mtambo maalum (halipo pichani) wa kufuatilia matumizi ya masafa kutoka kwa mtaalamu wa TCRA wakati wa ziara yake kwenye taasisi hiyo
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mheshimiwa Dk. Sira Ubwa Mamboya (katikati) akiongea na Bodi na Menejimenti ya Shirika la Posta Tanzania wakati wa ziara yake kwenye taasisi hiyo. Wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye

………………….

Na Prisca Ulomi,Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Serikali imeielekeza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuwachukulia hatua wanaokwenda kinyume na bei elekezi ya Serikali na warudishe fedha au kuwapiga faini. 

Maelekezo hayo yametolewa na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye wakati wa ziara ya Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mheshimiwa Dk. Sira Ubwa Mamboya alipotembelea TCRA ikiwa ni moja ya taasisi ya mawasiliano alizotembelea Tanzania Bara ili kujifunza utendaji kazi wake kwa kuwa mawasiliano ni suala la Muungano ambapo Nditiye ni mwenyeji wa ugeni huo

Nditiye amesema kuwa mwishoni mwa mwaka jana, Serikali ilitoa bei elekezi kwa kampuni za simu za mkononi wakati wa uzinduzi wa Mwongozo wa Watumiaji wa Huduma na Bidhaa za Mawasiliano kuwa ifikapo Januari mosi mwaka huu 2019, gharama ya kupiga simu kutoka mtandao mmoja kwenda mtandao mwingine itakuwa ni shilingi 10.40 kwa dakika moja na sio kwa sekunde kwa kuwa tulikuwa tumetoka shilingi 15.60 kwa dakika moja.

Ameongeza kuwa lakini mpaka sasa hivi huwa nasikia matangazo kutoka kampuni za mawasiliano za simu wanajinadi kuwa kupiga simu mtandao wowote ni shilingi moja kwa sekunde ina maana ukipiga sekunde sitini ni shilingi sitini na inakuwa imezidi mara tano ya gharama ambayo ni mwongozo wa Serikali kwa makampuni ya simu

“Nawataka TCRA sasa waanze kufuatilia makampuni yote ambayo yamekwenda kinyume na bei elekezi ya Serikali, kwanza, wachukue hatua za kinidhamu na wawapige faini lakini wahakikishe hela yetu ambayo hayo makampuni wamekuwa wakichukua isivyo halali inarudi kwa sababu mpango wa Serikali ni kwamba inapofika mwaka 2022 iwe shilingi mbili kwa dakika kupiga mtandao wowote wa simu,” amesisitiza Nditiye.

Nditiye ameipongeza TCRA kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya ya kuhakikisha kuwa Sekta ya Mawasiliano inakuwa juu sana nchini kwetu na tukumbuke kuwa Sekta ya Mawasiliano kupitia wadau kama TCRA tumeweza kwa miaka mitatu mfululizo kuchukua nafasi tatu za mwanzo kuchangia pato kwenye Serikali yetu na tunachangia pato kubwa sana lakini nikawambusha TCRA kuwa bado kuna maeneo ambayo wakiyafanyia kazi vizuri ya kiudhibiti tunaweza tukawa wa kwanza tena bila mashaka yeyote.

Pia, ametoa msisitizo kwa watanzania wajisajii kwa alama za vidole kwa kuwa lengo la Serikali ni zuri na tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuongeza muda hadi mwisho wa mwaka huu watanzania wawe wamejisajili kwa alama za vidole ili kwanza tuwalinde na waweze kufanya miamala mbali mbali wakiwa na uhakika na hatutaki wala hatupendi tuone mtu mmoja ana miliki laini 160 na zaidi za nini

“Ila tunategemea angalau mtanzania amiliki laini chache alizozisajili kwa kila mtandao atakaopenda ili tumjue ni yeye na itakapofika mwisho wa muda ambao umepangwa tutazima laini zote ambazo hazijasajiliwa kwa alama za vidole nia ni kwamba anayepigiwa au anayepiga tumtambue,”amesisitiza Nditiye. 

Pia, ameyataka makampuni ya simu yazingatie na kutoa matangazo ya kitaifa ya kimkakati kama vile homa ya ini na ugonjwa wa UKIMWI kwa kuwa bado upo

Nditiye amesema kuwa Sekta ya Mawasiliano ni ya Muungano hivyo amemshukuru Dkt. Mamboya kwa kuja na amejifunza mambo mengi ikiwemo ukuaji, uendeshaji na udhibiti wa Sekta ya Mawasiliano nchini na amemkaribisha Dkt. Mamboya kuja Tanzania Bara popote pale na akijisikia kwenda kukagua mawasiliano aende iwe Mtwara, Bukoba, Katavi na awe huru kama ambavyo huwa naenda Unguja na Pemba kushughulikia masuala ya mawasiliano 

Katika hatua nyingine, ugeni huo ulitembelea Shirika la Posta Tanzania (TPC) ambapo Dkt. Mamboya ameipongeza TPC kwa kutoa gawio na kwa ujasiri na utayari wa kuendelea kutoa huduma kwa wananchi. Pia, ameipongeza Bodi ya TPC kwa kuwa imara kwa kuwa ukiwa na Bodi legelege hakuna mafanikio ya taasisi na hamuwezi kutoa gawio. Nditiye kwa upande wake ameitaka TPC kutangaza huduma zake mara kwa mara na kuchamkia fursa zilizopo kwa kuhudumia wananchi kwa kuwasogezea huduma na bidhaa karibu nao

DC KASESELA ATATUA MGOGORO WA ARDHI WA FAMILIA YA MZEE MWENDA

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa katika shamba la familia ya marehemu mzee Mwenda kutatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka mingi katika kijiji cha Nduli kata ya Nduli manispaa ya Iringa. 
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa katika shamba la familia ya marehemu mzee Mwenda kutatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka mingi katika kijiji cha Nduli kata ya Nduli manispaa ya Iringa. 
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa katika shamba la familia ya marehemu mzee Mwenda kutatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka mingi katika kijiji cha Nduli kata ya Nduli manispaa ya Iringa na akiwa amezungukwa na wanafamilia pamoja na mashahidi waliohudhuria kutatua mgogoro huo. 


NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amefanikiwa kutatua mgogoro wa familia ya mzee Mwenda iliyopo katika kata ya Nduli uliodumu kwa miaka mingi kutokana na kaka yao Ayubu Mwenda kwenda tofauti na wanafamilia wengine.

Akizungumza kwenye shamba la familia marehemu mzee Mwenda Kasesela alisema kuwa kaka yao Ayubu Mwenda na wanafamilia wote kwa pamoja wamekaa na kufikia makubariano ya kugawana sawa ardhi ambayo ipo katika kijiji cha Nduli kata ya Nduli.

“Kwa leo nimefalijika kuona familia hii imeamua kumaliza mgogoro huu ambao ulikuwa hauna afya katika harakati za kuleta maendeleo kwa wananchi hawa kwa kuwa walikuwa wanapoteza muda mwingi kupigania mgogoro huu” alisema Kasesela

Kasesela alisema kuwa familia hiyo inagombea hekali mia moja na hasini na tisa (159) ambazo waliachiwa na marehemu mzee wao mzee Mwenda na kusema kuwa Ayubu ambaye ndiye kaka yao mkubwa amekuwa kisababishi cha mgogoro huo.

Aidha Kasesela alimtaka afisa mtendaji na afisa tarafa kuhakikisha shamba hilo linagawawiwa kwa wake wote sita wa mzee Mwenda ili kuondo na kumaliza mgogoro huo kwa kugawa kwa usawa na haki ili kila mmoja apate haki yake.

“Mzee Mwenda alikuwa na wake sita hivyo shamba hilo litagawiwa kwa kufuata familia za akina mama wote kwa haki ili kumaliza hili tatizo na hakuna mtu mwingine ataleta mgogoro kwa kuwa nitalipeleka shauri hili mahakamani kuweka zuio la kuanzisha kesi yeyoyte ile katika shamba hilo” alisema Kasesela

Kwa upande wake msimamizi wa mirathi hiyo Sadiki Abdalah Mwenda alimshukuru mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela kwa kuasidia kutatua mgogoro huo ambao umedumu kwa miaka mingi bila kupata ufumbuzi wa mgogoro huo.

Naye askari mstaafu Hawa Mwenda ambaye ni mwanafamilia alimshukuru mkuu wa wilaya na kumuomba awafikishie salaam kwa Rais Dr John Pombe Magufuli kwa kuongoza vizuri na kufanikisha wananchi wanyonge wafikiwe kirahisi na kutatuliwa matatizo yao.

BODI YA MIKOPO TAFAKARINI VIGEZO VYA KUTOA MIKOPO KWA WANAFUNZI-MAJALIWA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia wakati alipofungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu (TAHLISO) katika Ukumbi wa Nkrumah uliopo Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Agosti 10, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisoma hati ya kiwanja ambacho kitajengwa Ofisi ya Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO) kilichopo eneo la Mtumba jijini Dodoma kilichotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi (kushoto) Agosti 10, 2019 wakati Waziri Mkuu alipofungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa TAHLISO katika Ukumbi wa Nkuruma uliopo Chuo Kikuu cha Dar es salaam. Kulia ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako na wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa TAHLISO, Peter Niboye.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu (TAHLISO) wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua Mkutano huo katika Ukumbi wa Nkrumah uliopo Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Agosti 10, 2019.



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako wakati alipowasili katika Ukumbi wa Nkrumah uliopo Chuo Kikuu cha Dar es salaam kufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO), Agosti 10, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa, Joyce Ndalichako (kulia) na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salam, Utawala, Profesa David Mfinanga (kushoto) wakati alipoingia katika Ukumbi wa Nkrumah uliopo Chuo Kikuu cha Dar es salaam kufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO), Agosti 10, 2019. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa TAHLISO, Peter Niboye

………………

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameutaka uongozi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kutafakari namna ya kurekebisha baadhi ya dosari zilizopo likiwemo suala la kuwanyima mikopo wanafunzi kwa kutumia kigezo cha kusoma katika shule binafsi.

Amesema kuna baadhi ya wanafunzi ambao wamefaulu vizuri kidato cha nne na wamekosa nafasi katika shule za Serikali na wanatoka katika familia zisizokuwa na uwezo, hivyo wanatafuta wafadhili ambao wanawasomesha kwenye shule binafsi.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Agosti 10, 2019) wakati akifungua mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO) kwenye ukumbi wa Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Amesema kitendo cha bodi hiyo kuwanyima mikopo baadhi ya wanafunzi kwa kigezo cha kusoma katika shule binafsi bila ya kujiridhisha kama wanatoka kwenye familia zenye uwezo au zisizokuwa na uwezo kinawanyima wanafunzi hao fursa za kuendelea na masomo.

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwaonya wakuu wa vyuo vikuu ambao wanatumia vibaya fedha za mikopo ya wanafunzi kwa kuzipeleka katika miradi mbalimbali baada ya kuzipokea kutoka HESLB na kuwacheleweshea wanafunzi stahiki yao.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amewaagiza viongozi wa vyuo vikuu kuimarisha mafunzo kwa njia ya vitendo kwani tafiti nyingi zinazohusu mambo ya ajira zimebainisha umuhimu wa mafunzo ya vitendo katika kumuwezesha mhitimu kuwa na uelewa na ujuzi mpana wa kile alichokisoma kwa njia ya nadharia.

“Vyuo viongeze umakini na ufuatiliaji wa karibu wa vijana wetu wanapokuwa kwenye elimu kwa vitendo ili kuhakikisha kwamba wanapata maarifa na ujuzi uliokusudiwa katika mitaala yao. Pia natoa wito kwa waajiri wa sekta ya umma na binafsi watoe ushirikiano wa dhati kwa wanafunzi wanaotafuta nafasi za kufanya mafunzo kwa njia ya vitendo kwenye taasisi zao.” 

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TAHLISO, Bw. Peter Niboye amesema miongoni mwa changamoto zinazowakabili wanafunzi wa elimu ya juu ni ucheleweshwaji wa mikopo kwa baadhi ya vyuo licha ya HESLB kuwasilisha fedha hizo mapema, hivyo ameiomba Serikali kuwasaidia katika kutatua tatizo hilo.

Kadhalika, Mwenyekiti huyo wa TAHLISO, ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli kwa ushirikiano mkubwa inaoipatia jumuiya hiyo hivyo kurahisisha utendaji wake.

Awali, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Bw. Patrobas Katambi alimkabidhi Waziri Mkuu hati ya kiwanja kilichoko katika eneo la Mtumba jijini Dodoma kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za TAHLISO, ambapo baada ya kupokea hati hiyo, Waziri Mkuu aliikabidhi kwa Mkwenyekiti wa jumuiya hiyo Bw. Niboye.

Mkutano huo umehudhuriwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Bw. Godfrey Chongolo, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Bw. Kisare Makori pamoja na viongozi kutoka vyuo mbalimbali nchini vinavyounda TAHLISO.

JUMLA YA WAGONJWA 19 WENYE MATATIZO YA MOYO WAFANYIWA UPASUAJI WA KUFUNGUA NA BILA KUFUNGUA KIFUA JKCI

$
0
0
Madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Shirika la Madaktari Afrika la nchini Marekani wakizibua valvu za mgonjwa zilizokuwa zimeziba katika kambi maalum ya matibabu ya moyo ya wiki mbili inayoendelea katika Taasisi hiyo. Jumla ya wagonjwa 19 ambao ni watoto na watu wazima wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo wamefanyiwa upasuaji wa kufungua na bila kifua katika kambi hiyo.Picha na JKCI



Jumla ya wagonjwa 19 wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo wamefanyiwa upasuaji wa kufungua na bila kufungua kifua katika kambi maalum ya matibabu inayofanywa na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Shirika la Madaktari Afrika la nchini Marekani.

Kambi hiyo ya matibabu ya moyo ya wiki mbili inafanywa kwa watoto na watu wazima wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Magonjwa ya Moyo JKCI, Peter Kisenge alisema wagonjwa waliofanyiwa upasuaji hali zao zinaendelea vizuri na wengine wameruhusiwa kwenda nyumbani.

Alisema hadi sasa wagonjwa watu wazima waliofanyiwa upasuaji wa moyo wa bila kufungua kifua ni sita ambapo watatu walizibuliwa valvu ambazo hazikuwa zinafanya kazi vizuri na watatu walizibwa matundu kwenye moyo.

Aliongeza kwamba watu wazima wawili walifanyiwa upasuaji wa kufungua kifua na kubadilishwa valvu zilizokuwa na shida na kuwekewa nyingine za bandia.

Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa Watoto katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Sulende Kubhoja alisema katika kambi hiyo pia wamefanya upasuaji wa kufungua kifua na bila kufungua kifua kwa watoto kumi na moja ambao hali zao zinaendelea vizuri.

Dkt. Kubhoja ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya moyo kwa watoto alisema pamoja na kutoa huduma ya upasuaji katika kambi hiyo pia wanafanya uchunguzi kila siku kwa watoto 20 ambao wanaokutwa na matatizo makubwa wanafanyiwa upasuaji.

Alisema faida ya kambi hiyo ni watoto wanapata huduma katika mazingira rafiki ya nyumbani, madaktari wanapata mafunzo, kubadilishana ujuzi wa kazi na Taasisi kupata vifaa tiba ambavyo ni vya gharama wanavyokuja navyo wageni kwa ajili ya kuvitumia kwa wagonjwa wakati wanafanyiwa upasuaji.

Naye Jenifer Batengi ambaye alifanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua na sasa ameruhusiwa kutoka Hospitali alisema mwezi wa pili mwaka huu akiwa nyumbani kwake Mbagala alikwenda kuchota maji kwenye ndoo ya ujazo wa lita 20 baada ya kubeba ndoo alikosa pumzi na kuanguka chini.

“Nilipewa rufaa ya kuja kutibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete na baada ya kufanyiwa vipimo nilikutwa na tatizo katika valvu zangu mbili. Baada ya vipimo nilianza kutumia dawa lakini moyo ulikuwa unaenda mbio na mwili kuchoka”, alisema Jenifer.

Jenifer alimalizia kwa kuwashukuru wataalamu wa afya wa JKCI na madaktari Afrika kwa huduma ya matibabu aliyoyapata na kusema baada ya kufanyiwa upasuaji na kuzibuliwa valvu mbili ambazo zilikuwa na shida anaendelea vizuri kwani anapata pumzi ya kutosha na kutembea vizuri tofauti na ilivyokuwa mwanzo.

WANUFAIKA WA TASAF WILAYANI KARAGWE WAISHUKURU SERIKALI KWA KUWATHAMINI

$
0
0
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiangalia zizi la mbuzi la mmoja wa Walengwa wa TASAF, Bi. Beatha Katushabe wa kijiji cha Rulalo wilayani Karagwe mkoani Kagera ambaye anamiliki mbuzi 25 aliowapata kutokana na ruzuku ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (katikati) akipokea zawadi ya mkungu wa ndizi kutoka kwa Walengwa wa TASAF katika kijiji cha Rukole, Wilayani Karagwe mkoani Kagera wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF.
Mmoja wa Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika kijiji cha Rukole, Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera, Bi. Rhoda Ernest (wa tatu kushoto kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akionyesha kisima cha kuvuna maji ya mvua alichokijenga kwa kutumia na ruzuku ya TASAF.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akipokea zawadi ya mkeka uliosukwa na mmoja wa wanufaika wa TASAF, Bi.Rhoda Ernest katika kijiji cha Rukole, wilayani Karagwe Mkoani Kagera wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akilakiwa na wananchi wa kijiji cha Rulalo katika Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF na kuhimiza uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akifurahia jambo wakati alipokuwa akizungumza na wananchi na Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika kijiji cha Rulalo juu ya utekelezaji wa miradi ya TASAF.
************



Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wilayani Karagwe
Mkoani Kagera, wameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa
kuwapunguzia kero ya umaskini kupitia Mpango huo unaotekelezwa na
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) katika vijiji vya Rulalo na Rukole,
wanufaika hao wamesema Mpango huo umewawezesha kuboresha
maisha yao kwa kiwango kikubwa sana.

Wamesema mkakati wa Serikali wa kupambana na umaskini kupitia
TASAF umeamsha ari ya kujiletea maendeleo na kuwawezesha kutunza
kaya zao kwa uhakika tofauti na ilivyokuwa kabla ya uwepo wa Mpango
huo.

“Hivi sasa na sisi tunaonekana watu, kwani tunaweza kujikimu na kupanga
namna ya kuendesha maisha yetu kwa uhakika, tunamshukuru sana Rais
Magufuli kwa kutujali’’. Amesema mmoja wa Walengwa katika kijiji cha
Rukole, Bi. Rhoida Ernest.

Dkt. Mwanjelwa amesema kinachofanywa na Serikali kupitia TASAF ni
sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Mwenyezi Mungu ambayo hata katika Vitabu Vitakatifu vinazungumzia suala la kuwajali wasiojiweza ikiwa ni pamoja na yatima, wajane na maskini huku akinukuu Kitabu cha Yakobo: 1:27.

Dkt Mwanjelwa ameshuhudia namna Walengwa wa TASAF walivyoanzisha
miradi mbalimbali ya kujiongezea kipato ikiwemo ufugaji wa mbuzi, kuku,

ujenzi wa visima vya kuvuna maji ya mvua na uboreshaji wa makazi kwa
kujenga nyumba na kuwa na uwezo wa kusomesha watoto ambao
mahudhurio yamekuwa bora ikilinganishwa na hali ilivyokuwa kabla ya
kuingizwa kwenye Mpango.

Amewasisitizia wanufaika hao kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili
kuondokana na umaskini.

Katika hatua nyingine, Dkt. Mwanjelwa amewaagiza watendaji wa Serikali
kuwa karibu na walengwa wa TASAF ili kubaini changamoto zinazowakabili
na kuzitafutia ufumbuzi kwa wakati, lengo likiwa ni kuwawezesha
kujiongezea kipato na kutekeleza shughuli zao za kiuchumi kwa tija zaidi.

Ameongeza kuwa, matokeo chanya yaliyoanza kuonekana kwa Walengwa
wa TASAF yanapaswa kupewa msukumo na wataalamu hususani wa
sekta za kilimo, ufugaji na uanzishwaji wa miradi ya kiuchumi ambayo
itaboresha maisha yao.

Dkt. Mwanjelwa atahitimisha ziara yake ya kikazi mkoani Kagera kwa
kutembelea Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi ambako atakutana na
wananchi na kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF.

PICHA MAZISHI YA KATIBU WA UWT SENGEREMA

$
0
0
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Salum Kalli (kulia) akitoa salamu za rambirambi akiwa pamoja na maktibu wa CCM wa wilaya za Sengerema, Kwimba, Nyamagana, Misungwi, Ilemela, Magu na Ukerewe kabla ya kutoa heshima za mwisho.
Katibu wa wazazi Kwimba Chuki Anthony akitoa heshima za mwisho kwenye jeneza la mwili wa aliyekuwa Katibu wa UWT Wilaya ya Sengerema jana.


Wazazi na watoto wa marehemu Diana Musa, wakiwa kwenye ibada ya maziko iliyofanyika nyumbani kwao na marehemu mtaa wa Ngudu Kwimba jana.
Mwinjilisti wa Kanisa la AICT Reuben Daud akiendesha ibada ya mazishi ya aliyekuwa Katibu wa UWT Wilaya ya Sengerema, marehemu Diana Musa aliyefariki Agosti 6, mwaka huu kwa maradhi ya TB na Kisukari.
Watumishi wa CCM Wilaya ya Sengerema wakiwa pembeni mwa jeneza la aliyekuwa Katibu wa UWT wilayani humo kabla ya kutoa heshima za mwisho.
Baba mzazi wa marehemu Diana Musa, Seleman Bulugu akisaidiwa baada ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa mwanaye jana.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Salum Kalli akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Diana Musa ambaye alikuwa Katibu wa UWT Wilaya ya Sengerema.Kalli alimwakilisha Katibu Mkuu wa CCM. Dk. Bashiru Ally, kwenye maziko ya katibu huyo yaliyofanyika kwenye makaburi ya AICT mjini Ngudu Kwimba.
Vijana wa Green Guard wa CCM wakiwa wamebeba jeneza la mwili wa marehemu Diana Musa tayari kuelekea makaburini jana.

Vijana wa Green Guard wa CCM wakishusha jeneza la mwili wa marehemu Diana Musa kwa ajili ya mazishi.
Mtoto wa kike wa marehemu Diana Musa,akitupia udongo kwenye jeneza na mama yake jana wakati wa mazishi yaliyofanyika mjini Ngudu Kwimba kwenye makaburi ya AICT.
Mzee Selemani Bulugu na mkewe Naomi ngw’ashi Kadoke wakiweka shada la maua kwenye kaburi la mtoto wao, Marehemu Diana Musa, ambaye alizikwa kwenye makaburi ya AICT mjini Ngudu Kwimba jana.
Watoto wa marehemu Diana wakiweka shada la maua kwenye kaburi la mama yao jana baada ya mazishi.

Dkt. Abbasi Aonya Usambazaji Habari za Uongo, Picha Zisizo na Staha Ajali ya Moto Morogoro

$
0
0
Na Betrice Lyimo - MAELEZO 

Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, ametoa onyo kwa wananchi kuacha kusambaza picha za miili ya wananchi walioathirika na moto uliotokana na mlipuko wa mafuta yaliyokuwa kwenye lori lililopinduka asubuhi ya leo mkoani Morogoro. 

Dkt. Abbasi amesema: “Ni kinyume cha sheria na utamaduni wa Mtanzania kusambaza picha za watu wakiwa kwenye hali ya fadhaha”. 

Dkt. Abbasi ametoa kauli hiyo leo mchana Agosti 10, 2019 katika mahojiano maalum kupitia Televisheni ya Taifa (TBC) kuhusiana na ajali hiyo. 

Katika mahojiano hayo, Msemaji Mkuu wa Serikali amewaasa wananchi kuacha kusambaza habari zisizokuwa na uhakika ili kuepusha upotoshaji wa taarifa. 

"Niwaombe wananchi kuacha kusambaza habari za uongo kuhusu idadi ya vifo na majeruhi wa ajali. Ni muhimu sana watumie vyanzo rasmi vya Serikali kupata taarifa hizo ambavyo kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe pamoja na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro (RPC) Wibrod Mtafungwa” ameeleza Dkt. Abbasi. 

Aidha Dkt. Abbasi ameviasa vyombo vya habari kufuata maadili ya uandishi wa habari kwa kuandika habari sahihi na kupiga na kutumia picha zilizo na staha ili kuepusha taharuki katika jamii. 

Ajali hiyo imetokea leo tarehe 10 Agosti, eneo la Msamvu mkoani Morogoro ambapo Lori lililokuwa limebeba shehena ya mafuta lilipinduka na baade kulipuka moto. 

WANJUMBE WA SADC WAVUTIWA NA UWEKEZAJI WA VIWANDA NCHINI

$
0
0
*Rais Magufuli asifiwa kwa utendaji kazi, aungwa mkono, SADC kuleta mabadiliko chanya kwa wenye viwanda

*Kiwanda cha Keda Ceremics Limited kulipa kodi ya zaidi ya dola milioni 12 kwa Serikali

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

WIKI ya nne ya viwanda imehitimishwa kwa washiriki wa maonesho hayo kutoa nchi mbalimbali ndani ya jumuiya ya SADC kutembelea viwanda mbalimbali Tanzania bara na visiwani na kujionea namna viwanda hivyo vinavyofanya kazi pamoja na kutengeneza fursa mbalimbali hasa za masoko kwa wanajumuiya hao.

Ziara iliyofanywa katika kiwanda cha usindikaji wa matunda cha Elven agri kilichopo Mapinga Bagamoyo Mkoani Pwani walishiriki walijionea namna matunda yanavyochakatwa na kukaushwa na baadaye kusafirishwa katika nchi mbalimbali ndani ya jumuiya ikiwemo Botswana na Zambia pamoja na nchi za nje ikiwemo Marekani, kiwanda hicho chenye takribani ya heka 900 kinatoa ajira kwa wanawake na vijana pamoja na kushiriki shughuli za kiuchumi na kijamii ikiwemo kujenga shule pamoja na miundombinu ya maji.

Msimamizi wa kiwanda hicho Martin Matembo amesema kuwa bidhaa za matunda yakiwemo maembe, nanasi, papai, na ndizi zinazosindikwa kiwandani hapo zinauzwa nchini pamoja na kupelekwa nje ya nchi na kupitia SADC wamepata fursa kubwa kupitia wiki ya viwanda kwani wamejenga mahusiano bora na makubaliano ya kibiashara na washiriki wa mkutano huo kutoka nchi za Afrika Kusini, Zambia na Botswana.

Amesema kuwa mkutano mkuu wa 39 wa wakuu wa nchi na serikali utaleta mabadiliko chanya nchini hasa kwa wenye viwanda katika jumuiya hiyo, na amesisitiza ushirikiano ndani ya jumuiya hiyo ili kuleta ushindani katika soko la dunia.

Kiwanda cha pili kilichotembelewa ni cha Motisun Group kilichopo Chalinze Mkoani Pwani ambacho kina viwanda vinavyozalisha bidhaa za plastiki, vinywaji, mabati pamoja na rangi za nyumba (kiboko paints).

Kiwanda hicho kinachozaliwa sharubati (juisi) ni matokeo ya jitihada za Rais Dkt. John Magufuli katika kujenga nchi ya viwanda na kupitia kiwanda hicho wakulima wamekuwa wanafaidika kwa kuwa kiwanda hununua matunda kutoka kwa mkulima yeyote huku uhitaji wa matunda kwa kiwanda hicho ukifika tani 300 kwa siku.

Abubakar Mlawa mkuu wa kitengo Cha Mawasiliano wa kiwanda hicho ameeleza kuwa kupitia maonesho hayo ya viwanda lazima wananchi wajifunze kupenda na kuthamini bidhaa za ndani;

"Mahitaji ya juisi ni makubwa sana hasa katika nchi za Zambia, Kongo na Malawi ila tuna changamoto ya maji, tunahitaji maji zaidi ya lita milioni mbili kwa siku kwa ajili ya uendeshaji lakini tunapata maji litatano hivyo tunaomba Serikali itusaidie tuweze kupata maji kutoka mto Ruvu" ameeleza Mlawa.

Kiwanda hicho ambacho hulipa kodi kwa serikali takribani zaidi ya shilingi milioni 700 kimetoa ajira kwa wazawa kwa asilimia 95, huku bidhaa zikiuzwa ndani kwa asilimia 70 na ziuzwazo nje ni asilimia 30 pekee.

Aidha kiwanda hicho kinashiriki kwa kutoa bure huduma za kijamii zikiwemo afya, gari la wagonjwa na huduma ya zima moto bure.

Kiwanda cha tatu kilichotembelewa ni cha Keda Ceremics Limited kilichopo Chalinze Mikoani Pwani ambacho kinazalisha Tiles ambazo huuza na kusafirishwa katika nchi za Kenya, Ghana na Senegal.

Akitoa taarifa ya kiwanda hicho Kaimu Mkurugenzi wa kiwanda hicho Bruce Ni amesema kuwa kiwanda hicho chenye uwekezaji wa dola milioni 56 ni matokeo ya jitihada zilioneshwa na Rais Magufuli na asilimia 30 za malighafi zinazotumika katika uzalishaji hupatikana Tanzania.

Ni amesema kuwa mkutano huu umetengeneza fursa kwao na kujenga mahusiano bora na nchi za Kenya, Rwanda, na Burundi na mipango yao hadi kufikia mwaka 2026 watakuwa wamelipa kodi kwa serikali zaidi ya dola milioni 12.
Meneja Masoko na Mauzo Tanzania wa kiwanda cha kusindika matunda cha Elven Agri company,Brit Bahyare akisoma hotuba yake fupi mbele ya Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda,ambao wametembelea kiwanda hicho jana kwa ajili ya kuangalia ubora wa bidhaa na mazingira ya uzalishaji kwa Tanzania. 
Afisa Msimamizi wa kiwanda cha matunda cha Elven Agri ,Martin Leonard Matemba (kulia) akitoa ufafanuzi mbele ya wajumbe wa SADC waliopata fursa ya kutembelea kiwanda hicho cha kusindika matunda Elven Agri company kilichpo wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani.
Msemaji wa Makampuni ya Motisun Group wamiliki wa Sayona,Aboubakary Mlawa akiwaonesha wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC box la Juice ikiwa tayari kusafirishwa maeneo mbalimbali katika kiwanda cha kusindika matunda cha Sayona kilichopo Mboga - Msoga Chalinze mkoa wa Pwani.
Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda wakiangalia namna Juice inavyo sindikwa katiak kiwanda cha Sayona kilichopo Mboga - Msoga Chalinze mkoa wa Pwani.
Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda wakikagua kiwanda cha Keda kinachotengeneza marumaru aina ya Twyford kilichopo Chalinze mkoani Pwani
Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda wakiendelea kukagua kiwanda cha Keda kinachotengeneza marumaru aina ya Twyford kilichopo Chalinze mkoani Pwani.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
(Picha zote na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

SERIKALI YAITAKA NIC KUCHANGIA PATO LA TAIFA KWA ZAIDI YA ASILIMIA TANO

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Shirika la Bima la Taifa- NIC, Dkt. Elirehema Doniye (kulia), akikabidhiwa rasmi ofisi hiyo na aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika hilo, Bw. Sam Kamanga, jijini Dar es Salaam.
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Bima la Taifa- NIC, Bw. Sam Kamanga (kushoto), akitoa maelezo wakati wa kukabidhi rasmi ofisi kwa Mkurugenzi mpya wa Shirika hilo, Dkt. Dkt. Elirehema Doniye (wa pili kushoto).
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu (kushoto) na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Bima la Taifa- NIC, Bw. Laston Msongole, wakishuhudia makabidhiano ya ofisi kati ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la NIC. Bw. Sam Kamanga na Mkurugenzi Mtendaji mpya waShirika hilo, Dkt. Elirehema Doniye.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu (kushoto), akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Shirika la Bima Tanzania- NIC, Dkt. Elirehema Doniye, baada ya kukabidhiwa ofisi rasmi, jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Bima la Taifa- NIC, Bw. Laston Msongole (kulia) akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Shirika hilo, Dkt. Elirehema Doniye, kabla ya kukabidhiwa rasmi Ofisi, jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu (kushoto), akipeana mkono na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Bima la Taifa- NIC, Bw. Laston Msongole (kulia), baada ya kushuhudia makabidhiano ya ofisi kati ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika hilo, Bw. Sam Kamanga (hayupo pichani) na Mkurugenzi mpya , Dkt. Elirehema Doniye (katikati), jijini Dar es Salaam.(Picha na Peter Haule, WFM, Dar es salaam)

…………………

Na. Peter Haule, WFM, Dar es Salaam

Serikali imelitaka Shirika la Bima la Taifa- NIC kuhakikisha mchango wake unafikia zaidi ya asilimia tano katika pato taifa badala ya chini ya asilimia moja ya sasa ili kuweza kuchochea kasi ya ukuaji wa Sekta ya Fedha nchini. 

Hayo yamebainishwa Jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu, wakati akishuhudia kukabidhiwa rasmi Ofisi Mkurugenzi mpya wa Shirika la Bima la Taifa- NIC, Dkt. Elirehema Doniye.

Dkt. Kazungu amesema kuwa Shirika la NIC, linatakiwa kujipanga kimkakati kuwa chanzo kizuri cha mapato na kuhakikisha linawafikia wananchi wengi zaidi hususani katika Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

Aidha amelitaka Shirika la NIC kuhakikisha linajipanga kiushindani kutoa bima ya miradi yote mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya NIC, Bw. Laston Msongole, amesema kuwa Shirika hilo linawagusa watanzania wote kwa kuwa linatoa huduma zake Tanzania Bara na Zanzibar.

Alisema kuwa Shirika la NIC, limeanza kufanya vizuri katika soko hivyo ni jukumu la Mkurugenzi mpya kuendeleza juhudi hizo kwa kuwa hapo awali lilikuwa miongoni mwa mashirika yaliyotakiwa kubinafsishwa, kwa kuona umuhimu wake Shirika hilo limebaki kuwa la wananchi na sasa linatakiwa kujiendesha kibiashara.

Naye Mkurugenzi mpya wa Shirika hilo Dkt. Elirehema Doniye, amesema kuwa anafanya jitihada kuhakikisha Shirika hilo linaongeza ufanisi zaidi ili liweze kuchangia katika pato la Taifa kikamilifu kama alivyoelekeza, Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Kazungu.

Alisema kuwa Shirika hilo linajiendesha kibiashara hivyo ni lazima watendaji kufanya kazi kwa nidhamu ya juu, kuwafikia wateja wadogo na wakubwa na kwenda na kasi ya Serikali ya awamu ya tano.

Aidha aliyekuwa Mkurugenzi wa NIC, Bw. Sam Kamanga, amesema kuwa amemkabidhi Mkurugenzi mpya Shirika ambalo limeanza kufanya vizuri, kwa kuwa tayari kuna bima ya Kilimo ambayo itawafikia wananchi wengi, lakini pia NIC imepata tuzo mbalimbali hivyo ni jukumu la uongozi mpya kuendeleza mafanikio hayo.

Majeruhi wa ajali ya moto wapokelewa Muhimbili usiku huu

$
0
0
Wataalam wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wakiwapokea majeruhi wa ajali ya moto iliyotokea mkoani Morogoro baada ya lori lililokuwa limebeba mafuta kuanguka.
Magari yaliyobeba majeruhi kutoka mkoani Morogoro yakiingia MNH.
Wataalam wa MNH wakimweka mgonjwa kwenye kitanda kwa ajili ya kumpatia matibabu.
Madaktari na wataalam wengine MNH wakimuhudumia mgonjwa wa ajali ya moto iliyotokea mkoani Morogoro.
Mmoja wa majeruhi akipelekwa katika chumba cha matibabu
006: Wataalam wa MNH wakiendelea kuwahudumia majeruhi wa ajali ya moto.
Maandalizi ya kupokea wagonjwa yakiendelea Muhimbli.
Wataalam wakipokea wagonjwa ili kupatiwa matibabu zaidi. 


Na John Stephen


Majeruhi wa ajali ya moto iliyotokea mkoani Morogoro baada ya lori la mafuta kuanguka, usiku huu wamepokelewa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi na wataalam wa MNH.

Majeruhi wameanza kupokelewa MNH saa 4:30 usiku wakitokea Hospitali ya Mkoa wa Morogoro ambako watu kadhaa wamejeruhiwa kwenye ajali na kupelekwa MNH kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Gari la kwanza la wagonjwa lililobeba majeruhi kutoka Hospitali ya Mkoa wa Morogoro lilingia Muhimbili saa 4:30 usiku na kufuatiwa na magari manne yaliyoingia saa 5:10 usiku na ilipofika saa 6:30 tayari wagonjwa 25 walikuwa wamepokelewa na kuanza kupatiwa matibabu na wataalam mbalimbali wa MNH.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa MNH, Bw. Aminiel Aligaesha amesema kuwa baada ya kutokea kwa ajali mkoani Morogoro, MNH ilituma wataalam mbalimbali kwa ajili ya kuongeza nguvu wakiwamo madaktari bingwa wa magonjwa ya dharura, Dkt. Juma Mfinanga.

Bw. Aligaesha amesema Muhimbili imetuma wataalam wa upasuaji kwa wagonjwa walioungua moto, madaktari bingwa wa upasuaji na madaktari bingwa wa usingizi ili kushirikiana na wataalam wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kutoa huduma kwa majeruhi pamoja na kufanya uchunguzi kwa wagonjwa wanaopaswa kuhamishiwa MNH.

“Kwa upande wetu, tumeandaa madaktari 28, wauguzi 64 na wahudumu wa kawaida 10. Pia, tumeandaa vitanda 89 na kati ya hivyo vitanda 21 ni vya wagonjwa watakaohitaji uangalizi maalumu,” amesema Bw. Aligaesha.

Mbali na maandalizi haya, vile vile MNH imeandaa dawa za kutosha vikiwamo vitendanishi vyote vinavyohitajika kuhudumia majeruhi ambao wameanza kupatiwa huduma mbalimbali za matibabu.

Mbunge Ditopile atimiza ahadi aliyoitoa mbele ya Rais Magufuli

$
0
0
Charles James, Michuzi TV

Mbunge wa Viti Maalum Taifa anayewakilisha kundi la vijana, Mhe Mariam Ditopile ametimiza ahadi aliyoitoa mbele ya Rais Dk John Magufuli alipofanya ziara wilayani Kongwa mkoani Dodoma.

Mhe Ditopile aliahidi kuchangia mabati 200 yenye thamani ya Sh Milioni Tano kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Msingi Sagara ambayo iliezuliwa na upepo mkali na hivyo kusababisha changamoto kwa wanafunzi wa shule hiyo.

Amesema yeye kama Mbunge anayewakilisha vijana ni lazima aoneshe kwa mfano utumishi wake kwa vijana ambao aliomba ridhaa ya kuwatumikia bila kujali itikadi zao.

" Nwapongeze waalimu kwa uzalendo wenu wakuendelea kuwafundisha watoto hawa katika mazingira haya magumu naamini Mwenyezi Mungu atawalipa hapa hapa Duniani na kesho kwa namna mnavyojitoa kwa kizazi hiki ambacho ndio Taifa la kesho.

" Niwafikishie salamu za Rais Magufuli anawasalimu sana wana Sagara na naamini atakuja mwenyewe kuja kujionea ukarabati huu, pia anasema anawapenda sana," amesema Mhe Ditopile.

Aidha Mhe Ditopile ametoa salamu za Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai na kuwaeleza kuwa Mbunge wao ameshindwa kufika katika tukio hilo kutokana na kubanwa na majukumu mengine.

" Niwaase ndugu zangu sasa tutumie hichi kidogo tulichonacho mkononi mpaka kiishe ili tujue tumekwama wapi, isipokuwa ili hiki kidogo kiweze kufanya kazi kubwa niwaombe wana Sagara kama mlivyoanza muendelee hivyo hivyo kwa kujitolea nguvu kazi pamoja na mchanga na kokoto.

Pia niwakumbushe hii shule ni moja ya shule kongwe katika Mkoa wetu wa Dodoma na imetoa viongozi wengi wa serikali na nje ya serikali basi tusisite kuwashirikisha katika ukarabati huu," amesema Mbunge huyo.

Nae Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Santus Haule amemshukuru Rais Magufuli kwa kuguswa kwake na shida za Watanzania na kumpongeza kwa utendaji kazi wake na kuahidi kumpa kura za ndio kwa niaba ya wananchi wa Sagara ifikapo Uchaguzi Mkuu wa 2020.

" Tunampongeza Rais Magufuli kwa namna anavyofanya kazi, ziara yake hapa kwetu ilizaa matunda makubwa sana na sasa tunakamilisha ujenzi wetu. Tunamuahidi ushindi wa kishindo 2020," amesema Mwalimu Haule.
 Mbunge wa Viti Maalum Mariam Ditopile (kulia) akikabidhi ahadi ya mabati aliyoahidi kuyatoa kwa Shule ya Msingi Sagara wilayani Kongwa
Mbunge wa Viti Maalum, Mhe Mariam Ditopile akihutubia wananchi wa Kata ya Sagara wilayani Kongwa alivyoenda kukabidhi ahadi yake ya Mabati 200 aliyoitoa

WAJUMBE WA SADC WAVUTIWA NA UWEKEZAJI WA VIWANDA NCHINI

$
0
0
*Rais Magufuli asifiwa kwa utendaji kazi, aungwa mkono, SADC kuleta mabadiliko chanya kwa wenye viwanda

*Kiwanda cha Keda Ceremics Limited kulipa kodi ya zaidi ya dola milioni 12 kwa Serikali

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

WIKI ya nne ya viwanda imehitimishwa kwa washiriki wa maonesho hayo kutoa nchi mbalimbali ndani ya jumuiya ya SADC kutembelea viwanda mbalimbali Tanzania bara na visiwani na kujionea namna viwanda hivyo vinavyofanya kazi pamoja na kutengeneza fursa mbalimbali hasa za masoko kwa wanajumuiya hao.

Ziara iliyofanywa katika kiwanda cha usindikaji wa matunda cha Elven agri kilichopo Mapinga Bagamoyo Mkoani Pwani walishiriki walijionea namna matunda yanavyochakatwa na kukaushwa na baadaye kusafirishwa katika nchi mbalimbali ndani ya jumuiya ikiwemo Botswana na Zambia pamoja na nchi za nje ikiwemo Marekani, kiwanda hicho chenye takribani ya heka 900 kinatoa ajira kwa wanawake na vijana pamoja na kushiriki shughuli za kiuchumi na kijamii ikiwemo kujenga shule pamoja na miundombinu ya maji.

Msimamizi wa kiwanda hicho Martin Matembo amesema kuwa bidhaa za matunda yakiwemo maembe, nanasi, papai, na ndizi zinazosindikwa kiwandani hapo zinauzwa nchini pamoja na kupelekwa nje ya nchi na kupitia SADC wamepata fursa kubwa kupitia wiki ya viwanda kwani wamejenga mahusiano bora na makubaliano ya kibiashara na washiriki wa mkutano huo kutoka nchi za Afrika Kusini, Zambia na Botswana.

Amesema kuwa mkutano mkuu wa 39 wa wakuu wa nchi na serikali utaleta mabadiliko chanya nchini hasa kwa wenye viwanda katika jumuiya hiyo, na amesisitiza ushirikiano ndani ya jumuiya hiyo ili kuleta ushindani katika soko la dunia.

Kiwanda cha pili kilichotembelewa ni cha Motisun Group kilichopo Chalinze Mkoani Pwani ambacho kina viwanda vinavyozalisha bidhaa za plastiki, vinywaji, mabati pamoja na rangi za nyumba (kiboko paints).

Kiwanda hicho kinachozaliwa sharubati (juisi) ni matokeo ya jitihada za Rais Dkt. John Magufuli katika kujenga nchi ya viwanda na kupitia kiwanda hicho wakulima wamekuwa wanafaidika kwa kuwa kiwanda hununua matunda kutoka kwa mkulima yeyote huku uhitaji wa matunda kwa kiwanda hicho ukifika tani 300 kwa siku.

Abubakar Mlawa mkuu wa kitengo Cha Mawasiliano wa kiwanda hicho ameeleza kuwa kupitia maonesho hayo ya viwanda lazima wananchi wajifunze kupenda na kuthamini bidhaa za ndani;

"Mahitaji ya juisi ni makubwa sana hasa katika nchi za Zambia, Kongo na Malawi ila tuna changamoto ya maji, tunahitaji maji zaidi ya lita milioni mbili kwa siku kwa ajili ya uendeshaji lakini tunapata maji litatano hivyo tunaomba Serikali itusaidie tuweze kupata maji kutoka mto Ruvu" ameeleza Mlawa.

Kiwanda hicho ambacho hulipa kodi kwa serikali takribani zaidi ya shilingi milioni 700 kimetoa ajira kwa wazawa kwa asilimia 95, huku bidhaa zikiuzwa ndani kwa asilimia 70 na ziuzwazo nje ni asilimia 30 pekee.

Aidha kiwanda hicho kinashiriki kwa kutoa bure huduma za kijamii zikiwemo afya, gari la wagonjwa na huduma ya zima moto bure.

Kiwanda cha tatu kilichotembelewa ni cha Keda Ceremics Limited kilichopo Chalinze Mikoani Pwani ambacho kinazalisha Tiles ambazo huuza na kusafirishwa katika nchi za Kenya, Ghana na Senegal.

Akitoa taarifa ya kiwanda hicho Kaimu Mkurugenzi wa kiwanda hicho Bruce Ni amesema kuwa kiwanda hicho chenye uwekezaji wa dola milioni 56 ni matokeo ya jitihada zilioneshwa na Rais Magufuli na asilimia 30 za malighafi zinazotumika katika uzalishaji hupatikana Tanzania.

Ni amesema kuwa mkutano huu umetengeneza fursa kwao na kujenga mahusiano bora na nchi za Kenya, Rwanda, na Burundi na mipango yao hadi kufikia mwaka 2026 watakuwa wamelipa kodi kwa serikali zaidi ya dola milioni 12.
Meneja Masoko na Mauzo Tanzania wa kiwanda cha kusindika matunda cha Elven Agri company,Brit Bahyare akisoma hotuba yake fupi mbele ya Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda,ambao wametembelea kiwanda hicho jana kwa ajili ya kuangalia ubora wa bidhaa na mazingira ya uzalishaji kwa Tanzania. 
Afisa Msimamizi wa kiwanda cha matunda cha Elven Agri ,Martin Leonard Matemba (kulia) akitoa ufafanuzi mbele ya wajumbe wa SADC waliopata fursa ya kutembelea kiwanda hicho cha kusindika matunda Elven Agri company kilichpo wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani.
Msemaji wa Makampuni ya Motisun Group wamiliki wa Sayona,Aboubakary Mlawa akiwaonesha wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC box la Juice ikiwa tayari kusafirishwa maeneo mbalimbali katika kiwanda cha kusindika matunda cha Sayona kilichopo Mboga - Msoga Chalinze mkoa wa Pwani.
Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda wakiangalia namna Juice inavyo sindikwa katiak kiwanda cha Sayona kilichopo Mboga - Msoga Chalinze mkoa wa Pwani.
Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda wakikagua kiwanda cha Keda kinachotengeneza marumaru aina ya Twyford kilichopo Chalinze mkoani Pwani
Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda wakiendelea kukagua kiwanda cha Keda kinachotengeneza marumaru aina ya Twyford kilichopo Chalinze mkoani Pwani.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
(Picha zote na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

Rais Magufuli atangaza siku 3 za Maombolezo ya Kitaifa kuanzia tarehe 10 Agosti, 2019

RAIS DK.SHEIN ATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI AJALI YA LORI MOROGORO

$
0
0
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk. Kebwe Stephan Kebwe kufuatia ajali ya kuripuka kwa lori la mafuta na kusababisha vifo pamoja na majeruhi kadhaa.

Katika salamu za rambirambi ambazo Rais Dk. Shein amemtumia Mkuu wa Mkoa, alieleleza kuwa amemepokea kwa huzuni na masikitiko makubwa taarifa ya vifo vilivyotokana na ajali ya kuripuka kwa lori la mafuta iliyotokea asubuhi ya leo, tarehe 10 Agosti, 2019 katika maeneo ya Itigi Msavu Mkoani Morogoro na kusababisha vifo vya Watanzania waliopungua 60 na majeruhi kadhaa.

Rais Dk. Shein katika salamu hizo alieleza kuwa yeye binafsi pamoja na wananchi wote wa Zanzibar anatuma salamu za rambi rambi kwa wanafamilia wa marehemu, marafiki, wananchi wa Mkoa wa Morogoro na Jamahuri ya Muungano wa Tanzania kwa jumla.

“Kwa hakika msiba huu umetugusa wananchi sote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuondokewa ghafla na ndugu zetu ambao ni nguvu kazi ya Taifa” ilieleza sehemu ya taarifa ya Rais Dk. Shein.

Aidha, salamu hizo zilimuomba Mwenyezi Mungu ampe Mkuu huyo wa Mkoa, wanafamilia pamoja na Watanzania wote moyo wa subira katika kipindi hichi kigumu cha msiba.

Vile vile katika salamuhizo za rambirambi, Rais Dk. Shein alimuomba MwenyeziMungu awalaze mahala pema wote na awape nafuu ya haraka majeruhi wa ajali hiyo ili waweze kupata shifaa na waendelee na majukumu yao mbalimbali ya ujenzi wa Taifa.

Mapema leo asubuhi lori lililokuwa limebeba shehena ya mafuta aina ya petroli likitokea Dar-es-Salamu lilipinduka na kuwaka moto katika eneo la Itigi Msamvu wakati wananchi wakijaribu kuchota mafuta yaliyomwagika baada ya gari hilo kupata ajali na kuanguka

WACHUKUZI WAISHUKURU SERIKALI

$
0
0


Na Mwandishi wetu Mihambwe

Wachukuzi wameishukuru Serikali iliyopo madarakani inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kusimama pamoja nao na kuhakikisha wanalipwa fedha zao ambazo walikosa matarajio lini watazipata.

Hayo yamebainishwa na Wachukuzi wa Chama cha msingi (Amcos) cha Kitama shuleni kilichopo kata ya Kitama ambao fedha zao zilienda kulipa madeni ya Amcos badala ya kulipwa haki zao na ndipo Serikali ikaingilia kati na kuhakikisha wanalipwa fedha zao.

“Tunaishukuru Serikali ya Rais Magufuli, tunamshukuru sana Afisa Tarafa wetu kwa kusimama pamoja nasi kuhakikisha tunalipwa fedha zetu. Tunamshukuru sana Gavana Shilatu.” Alisema mmoja wa Wachukuzi.

Akizungumza na Mwandishi wetu, Afisa Tarafa Mihambwe *Ndugu Emmanuel Shilatu* alisema Serikali ya awamu ya 5 inasimama na Watu wanyonge ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakipoteza haki zao pasipo Mtetezi.

“Niliposikia fedha za Wachukuzi zimeenda kulipa madeni ya chama cha Kitama shuleni nilikasirika sana, nikawaita viongozi pamoja na Wachukuzi mezani na hatimaye mwafaka ukapatikana na Amcos wamekubali kulipa fedha zao mapema iwezekanavyo. Nitasimamia hili mpaka ukamilifu wake.” Alisisitiza Gavana Shilatu.

Wachukuzi wa Kitama shuleni wanaidai Amcos hiyo fedha za msimu 2018/2019 ambazo sasa wamepata mwangaza wa malipo ya fedha zao.

Kikao hicho kilihudhuliwa na Afisa Tarafa Mihambwe Gavana Shilatu, Mwenyekiti wa Serikali Kijiji cha Kitama Shuleni, Mtendaji Kijijini cha Kitama Shuleni, Uongozi na Bodi nzima ya Kitama Shuleni Amcos pamoja na Wachukuzi wenye madai na Amcos hiyo.

MKOA WA PWANI WADHAMIRIA KUWA UKANDA WA VIWANDA,”WAFIKIA VIWANDA 836-NDIKILO

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI,PWANI

MKOA wa Pwani unaendelea kujipanga na kuonyesha adhma yake ya kudhamiria kuwa ukanda wa viwanda ambapo kwa sasa una jumla ya viwanda 836 .

Kati ya viwanda hivyo vikubwa vipo 56,vya kati vipo 80 na viwanda vidogo 338 huku viwanda vidogo sana vimefikia 362.

Mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ,aliweka bayana hayo wakati alipokuwa akielezea kuhusiana na namna wavyoshirikiana na sekta binafsi katika shughuli za kiuchumi na maendeleo kwa wawekezaji na wafanyabiashara mbalimbali.

Hata hivyo alieleza, pia halmashauri zimetenga maeneo kwa ajili ya viwanda hekta 22,937 ,hivyo amewataka wawekezaji kukimbilia fursa hiyo.

“Ila zipo changamoto za fidia na upimaji wa maeneo husika,licha ya jitihada kufanywa na halmashauri kuuza maeneo kwa bei kubwa na kutenga fedha za ndani ili kufidia gharama za upimaji na fidia,”

Ndikilo alisema ,serikali inaendelea kufuta hati za watu wasioendeleza maeneo yao na kuyaacha pori na kuyapangia matumizi mbalimbali ikiwemo shughuli za viwanda na uwekezaji,”:Halmashauri endapo zitabaini mashamba na maeneo yasiyoendelezwa wanapendekeza yanatwaliwa na serikali kwa ajili ya uzalishaji,uwekezaji na kilimo.

Aliwaomba wafanyabiashara na wawekezaji kukimbilia mkoani Pwani kwenda kujenga viwanda kwani maeneo yapo ya kujenga viwanda vikubwa,vya kati na hata vidogo.

Katika hatua nyingine, mkoa huo unashirikiana na sekta binafsi kuboresha mazingira ya kibiashara na uwekezaji,kuwaweka katika umoja wafanyabiashara kwa kuanzisha wiki ya viwanda na maonyesho na kupata fursa ya kujitangaza na kupanua wigo wa kimasoko.

Ndikilo”Mwaka 2018 tulifanikiwa kuandaa wiki ya viwanda na maonyesho hivyo tunatarajia kufanya zaidi ya mwaka uliopita ,tunaandaa kongamano kubwa la uwekezaji ili kuwaweka karibu wadau wa uwekezaji na wafanyabiashara,taasisi za fedha,taasisi za uwezeshaji ,mabalozi na wanahabari wa ndani na nje ya nchi.
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live




Latest Images