Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

Waziri Ummy azikaribisha nchi za SADC kutibiwa Muhimbili, MOI

$
0
0

 Daktari Bingwa wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), Dkt. William Mugisha (kulia) akimweleza Waziri Ummy Mwalimu kuhusu huduma ya upasuaji wa mivunjiko ya kikombe cha mfupa wa nyonga alipotembelea banda la MOI leo.
 Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo na Mkuu wa Idara ya Utafiti na Mafunzo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Dkt. Pedro Pallangyo akimweleza Waziri Ummy Mwalimu huduma zinazopatika JKCI zikiwamo huduma za tiba ya umeme wa moyo na  kuzibua mishipa ya damu.
 Daktari wa Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam, Dkt. Andrew Laiser akieleza jinsi walivyojiandaa kuhudumia wajumbe wa mkutano wa SADC na wananchi wengine.
 Waziri Ummy Mwalimu akisoma jarida la Muhimbili linaloeleza huduma mbalimbali za afya zinazopatikana MNH. Kulia ni Dkt. Juma Mfinanga akimweleza jambo Waziri.
  Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, wataalam wa afya pamoja na wataalam wengine wakiwa katika viwanja vya ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) kukagua mabanda na kliniki zitakazotumika kuhudumia wajumbe wa mkutano wa SADC.
Wataalam wa afya wa Muhimbili, MOI, JKCI na Hospitali ya Lugalo wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri Ummy Mwalimu leo katika viwanja vya ukumbi  wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC).

 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari katika banda la Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alipotembelea leo. Kushoto ni Dkt. Juma Mfinanga akiwa na Waziri Ummy Mwalimu baada ya kumweleza jinsi MNH ilivyojiandaa kuwahudumia wajumbe wa mkutano wa SADC pamoja na wananchi wengine.


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu  amezikaribisha nchi wanachama wa SADC kutumia huduma za ubingwa wa juu zinazopatika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).

Ummy ameyasema hayo leo alipotembelea  mabanda ya MNH, MOI na JKCI yanayoshiriki maonesho ya viwanda yanayofanyika katika viwanja vya ukumbi  wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) kuelekea mkutano mkuu wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi zilizopo Kusini mwa Afrika (SADC) ambao utaanza mapema wiki hii.

Waziri Ummy amesema Wizara yake imeweka wataalam wa afya ili kutoa huduma kwa wajumbe wa mkutano wa SADC watakaohitaji huduma za matibabu pamoja na wananchi wengine watakaokuwapo katika viwanja hivyo.

Aidha ameziomba nchi za SADC kupata huduma za ubingwa wa juu zinazopatikana MNH kama upandikizaji figo (kidney transplant), upandikizaji watoto vifaa vya kusaidia kusikia (cochlear implant), tiba kwa njia ya radiolojia (interventional radiology).

Kwa upande wa MOI, Waziri Ummy amezitaka nchi za SADC kuja kupata huduma za upasuaji wa mivunjiko ya kikombe cha mfupa wa nyonga, upasuaji wa kuweka nyonga na magoti bandia na upasuaji wa magoti, ubongo na mgongo kupitia matundu madogo.

Kwa upande wa JKCI amezitaka nchi za SADC kupata huduma za tiba ya umeme wa moyo, kuzibua mishipa ya damu na upasuaji wa kufungua kifua kwa ajili ya kurekebisha valvu au matundu kwenye moyo.

 “Kama Wizara tumeweka wataalam wa afya hapa eneo la mkutano  ili kutoa huduma kwa wajumbe wa nchi za SADC. Wataalam wetu wa Muhimbili, MOI, JKCI na pamoja  Hospitali ya Lugalo wako tayari kuhudumia wageni wetu ambao watapata changamoto yoyote ya kiafya,” amesema Waziri Ummy.

Waziri Ummy ametembelea kliniki maalumu zilizoandaliwa kwa ajili ya kuhudumia wageni na wananchi mbalimbali wanaotembelea maonesho ya viwanda na maandalizi ya mkutano wa 39 wa SADC.

WAZIRI MASAUNI AFANYA ZIARA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA ABEID AMANI KARUME, VISIWANI ZANZIBAR

$
0
0

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa Kaunda suti), akisikiliza maelezo kutoka kwa Mrakibu Muandamizi wa Uhamiaji, Bakari Mohammed Ameir, wakati wa ziara ya kukagua shughuli za Ulinzi na Usalama zinavyoendelea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Visiwani Zanzibar.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akipita kwenye mashine ya ukaguzi wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za Ulinzi na Usalama ,alipotembelea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Visiwani Zanziba
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa ziara ya kukagua shughuli za Ulinzi na Usalama zinavyoendelea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Visiwani Zanzibar.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia), akiangalia mashine itakayotumiwa na Idara ya Uhamiaji ikiwa ni utekelezaji wa mabadiliko ya teknolojia kutoka pasi za zamani za kusafiria kwenda kadi za kusafiria za kielektroniki, alipotembelea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume,Visiwani Zanzibar

WAKULIMA TUMIENI FURSA YA FAHARIKILIMO KUTOKA BENKI YA CRDB – WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, wakati alipowasili kwenye viwanja vya Nyakabindi, Bariadi mkoani Simiyu, katika kilele cha Maonyesho ya 27 ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi (Nane Nane) 2019.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wakulima nchini kuchangamkia fursa zinazotolewa na Benki ya CRDB kupitia akaunti ya “FahariKilimo” ambayo ni maalum kwa ajili ya wakulima. Akizungumza wakati wa kilele cha maonyesho ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi (Nane Nane) 2019 nchini iliyofanyika kitaifa mkoani Simiyu, Waziri Mkuu alisema akaunti hiyo ya “FahariKilimo” ambayo imeambatana na fursa nyingine za uwezeshaji ikiwamo mikopo kwa wakulima itasaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha mnyororo wa thamani wa kilimo nchini.

"Serikali inaridhishwa sana na jitihada kubwa zinazofanywa na Benki hii ya CRDB katika kuboresha sekta ya kilimo nchini. Ubunifu huu wa huduma na bidhaa mnazozitoa kwa wakulima nchini unaambatana na dhamira ya Serikali ya kujenga uchumi wa kati wa viwanda ukizingatia malighafi ya viwanda vyetu inapatikana katika sekta hii mama ya kilimo,” alisema Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mkurugenzi wa Kampuni ya NSAGALI ambaye pia ni Mteja wa Benki ya CRDB Mkoani Simiyu, Emmanuel Silanga alipokuwa akitoa ushuhuda wake wa kuwezeshwa Mkopo uliomuwezesha kununua Pamba kutoka kwa Wakulima, wakati alipotembelea Banda la Benki ya CRDB, katika kilele cha Maonyesho ya 27 ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi (Nane N ane) 2019, kwenye Uwanja wa Nyakabindi, Bariadi mkaoni Simiyu. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela.



Akielezea mkakati wa Serikali katika urasimishaji wa wakulima ilikuwajengea mazingira mazuri ya upatikanaji wa mikopo katika taasisi za fedha, Waziri Mkuu alisema Serikali kupitia Wizara ya Kilimo na Wizara ya Ardhi imeandaa mpango mkakati wa upimaji wa ardhi ya wakulima nchini kote, jambo ambalo pia litasaidia kuongeza thamani ya ardhi ya wakulima hao.

“Nafahamu changamoto kubwa inayopelekea riba za mikopo ya kilimo kuwa kubwa ni pamoja na wakulima kukosa dhamana na mashamba yao kukosa hatimiliki hivyo kuongeza hatari ya mikopo. Jambo hili tunalifanyia kazi lakini pia niyaombe mabenki yote nchini kuweka mkakati madhubuti utakaopelekea kupungua kwa riba kwenye mikopo ya kilimo, riba ikipungua hata wale ambao ni wakopaji wazuri lakini wamekuwa wakihofia gharama za mkopo nao watakuja kukopa,” alisema Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akichukua moja ya vipeperushi wakati alipotembelea Banda la Benki ya CRDB, katika kilele cha Maonyesho ya 27 ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi (Nane N ane) 2019, kwenye Uwanja wa Nyakabindi, Bariadi mkaoni Simiyu. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela.

Abdulmajid Nsekela, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, alisema akaunti ya FahariKilimo ni sehemu ya mkakati mpana wa Benki hiyo kuwahudumia wakulima kwa ukaribu zaidi kwa kuzingatia mahitaji yao. “Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba nikujulishe kuwa akaunti hii ya FahariKilimo hufunguliwa bure kabisa na hakuna gharama zozote za uendeshaji wa akaunti kwa mkulima, tukilenga kumpa mkulima unafuu wa kupokea malipo yake pindi anapopokea malipo baada ya kuuza mazao,” aliongezea Nsekela.

Nsekela alisema mpaka sasa wakulima zaidi ya 30,000 tayari wameshajiunga na akaunti ya FahariKilimo na hivyo kunufaika na fursa mbalimbali zinazotolewa na Benki ya CRDB kwa wakulima. “Mkulima anapofungua akaunti ya FahariKilimo tunamuingiza moja kwa moja kwa mpango wetu maalum wa uwezeshaji ambapo atakuwa akipata mafunzo mbalimbali juu ya kuboresha kilimo chake kupitia huduma na bidhaa za Benki yake ya CRDB,” alisema Nsekela.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Ester Mwambapa, wakati alipowasili kwenye viwanja vya Nyakabindi, Bariadi mkoani Simiyu, katika kilele cha Maonyesho ya 27 ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi (Nane Nane) 2019.

Nsekela aliendelea kusema baadhi ya fursa ambazo Benki hiyo imekuwa ikitoa kwa wakulima ni pamoja na mikopo ya pembejeo, matrekta ya kulimia, mashine za kupandia, mashine za umwagiliaji, mikopo ya vifaa vya ujenzi pamoja mikopo kwa wawekezaji katika viwanda vya kilimo. “Tumekuwa na utaratibu wakushirikiana na wadau mbalimbali wa kilimo nchini katika kuhakikisha wakulima wanapata pembejeo za kisasa zitakazopelekea kuongeza kiwango cha uzalishaji na faida wanayopata. Kama unavyoona leo hii hapa tupo na wenzetu wa ETC Agro ambao kwa pamoja tunatoa mikopo ya matrekta kwa wakulima kwa vigezo na masharti nafuu kabisa,” alisema Nsekela.

Nsekela alisema ilikupata mkopo huo wa trekta mkulima anatakiwa kuchangia asilimia 35 wakati asilimia 65 itatolewa na Benki ya CRDB ambapo mteja atalipa kwa muda wa miaka 3. “Katika mkopo huu wa trekta mkulima hahitaji kuwa na dhamana, trekta litatumika kama dhamana ya mkopo,” alisema Nsekela.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimuelekeza jambo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakati alipotembelea Banda la Benki ya CRDB, katika kilele cha Maonyesho ya 27 ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi (Nane Nane) 2019, kwenye Uwanja wa Nyakabindi, Bariadi mkaoni Simiyu.

Nsekela alimwambia Waziri Mkuu kuwa asilimia 40 ya mikopo ya kilimo nchini imetolewa na Benki ya CRDB, jambo linaloashiria utayari wa Benki hiyo katika kuboresha sekta ya kilimo nchini. “Kwa mwaka jana pekee Benki ya CRDB kipindi cha mwaka 2018/2019,  tumetoa zaidi ya shilingi bilioni 650 katika kilimo,” alisema Nsekela.

Aliendelea kusema kati ya fedha hizo zaidi ya shilingi bilioni 97.3 zilielekezwa kwenye zao la pamba katika kununua mbegu (bilioni 36) na kulipia pamba (bilioni 61). Nyingine zilielekezwa katika kilimo cha miwa (bilioni 167.3), Kilimo cha kahawa (bilioni 36.6), kilimo cha chai (bilioni 60).

“Leo hii hapa tumeambatana na mteja wetu ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha uchakataji pamba ambacho hivi karibuni tumewapatia mkopo kwa ajili ya ununuzi wa zao la pamba,” aliongezea Nsekela.

Nsekela alimalizia kwa kumhakikishia Waziri Mkuu kuwa Benki ya CRDB imedhamiria kwa dhati kuunga mkono sekta ya kilimo na viwanda ili kutimiza azma ya Serikali ya awamu ya tano yakufikia uchumi wa kati unaoshamirishwa na viwanda. “Ahadi yetu kwa Serikali ni Tupo Tayari,” alihitimisha Nsekela.







Lugalo golf club yakaribisha wachezaji toka nchi za SADC

$
0
0

Mwenyekiti wa klabu ya gofu ya Jeshi la Ulinzi la Tananchi wa Tanzania ya Lugalo amewakaribisha wageni wanaokuja kwa ajili SADC kwenda kucheza mchezo katika uwanja wao.

Akizungumza na waandishi wa Habari Mwenyekiti wa KLabu hiyo Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo amesema klabu hiyo imejiandaa kuwapokea wageni wowote

Akizungumzia Mafanikio ya Klabu hiyo amesema anajivunia Timu ya Wanawake ambayo imekuwa ikifanya vyema katika mashindano mbalimbali ikiwemo ya Coast Open yaliyofanyika Mombasa nchini kenya na wachezaji wa Lugalo kuibuka washindi.

Katika mashindano ya hivi karibuni ya TPC open 2019 mchezaji Zumla Hamisi ameibuka na Ushindi kwa Wanawawake huku katika kundi la wachezaji wa kulipwa Richard Mtweve alishika nafasi ya pili na Nafasi ya Tatu Abdalah Yusuph.

KITABU CHA MDINI YOTE NCHINI CHATIA FORA MAONESHO YA VIWANDA YA SADC

WAJUMBE SADC WATEMBELEA VIWANDA 21, WAKOSHWA NA JUHUDI ZA SERIKALI KUHAMASISHA UWEKEZAJI WA VIWANDA

$
0
0


*Wengine wasifu teknolojia ya hali ya juu walioyoina kwenye viwanda vya Tanzania

 

 
*Wakiri Tanzania inaweza kuliteka solo la Jumuiya ya SADC ,waona fursa lukuki



 Na Ripota, Michuzi TV 


WAJUMBE wa Mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo kwa  Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC) wametapa nafasi ya kutembelea  viwanda 21vinavyofanya uzalishaji kwa ajili ya kuangalia ubora wa bidhaa na mazingira ya uzalishaji kwa Tanzania Bara na Zanzibar.


Wakiwa katika viwanda hivyo wajumbe hao wamekiri na kuridhishwa na ambavyo  Serikali ya Tanzania namna ilivyodhamiria katika Uwekezaji katika viwanda huku wakieleza wazi Tanzania wanayo nafasi kubwa ya kumiliki soko la Jumuiya hiyo kwani kuna kila.kitu zikiwemo malighafi za uhakika.


 

Baadhi ya wajumbe wa SADC wameiambia Michuzi TV na Michuzi Blog kuwa Tanzania ipo katika nafasi nzuri ya kulimiliki soko la jumuiya hiyo kwa kuwa kuna nguvu kazi ya kutosha na malighafi za uhakika.

 

 
Mjumbe kutoka nchini Afrika Kusini wa Kampuni ya Flexion Renatus Joseph amesema kwamba yeye yupo katika sekta ya viwanda vya chuma jijini Johannesburg, Afrika Kusini na kwamba aliyoyashuhudia   katika kiwanda cha Lodha Group of Companies yamenifanya abadili fikra zake kuhusu uwezo wa viwanda kwa nchi ya Tanzania.


Amesema amethibitisha kwa macho yake kuna matumizi makubwa ya teknolojia katika utengenezaji bidhaa za nondo na vifaa vingine vitokanavyo na chuma. "Hakika vikipatikana viwanda vingi vya namna hii SADC tutapiga hatua na tutakuwa na bidhaa zinazoleta ushindani ndani na nje ya Afrika,” amesema.

 

 
Wajumbe hao wakiwa kiwandani hapo yameelezwa kiwanda hicho cha chuma kilichopo Mkuranga mkoani Pwani  ni miongoni mwa viwanda vilivyoitikia  mwito wa Rais Dk. John Magufuli kwa vitendo kuhusu Tanzania ya viwanda.

 

 
Akizungumza mbele ya ujumbe wa SADC waliotembelea kiwandani hapo Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Mhandisi Kamara Gombe amesema Tanzania kwa sasa inazalisha tani 200,000 za bidhaa za viwanda huku mahitaji ni tani 300,000.

 

 
"Hii maana yake kuna uhaba wa tani laki moja kwenye soko. Hivyo, Kampuni ya Lodhia ni miongoni mwa wadau wa viwanda wanaohakikisha Tanzania inajitegemea katika sekta ya viwanda.Hata hivyo, mbali ya uhitaji huo wa tani laki moja bado kuna tatizo la uhaba wa soko kwa kuwa wanazalisha tani 3000 kwa mwezi

 

 
"Lakini  uwezo wao ni kuzalisha tani 10,000. Kazi yetu viwanda ni kulinda viwanda vya ndani, tutahakikisha tatizo hili tunalitafutia ufumbuzi ili hizi tani 7,000 zilizobaki ziweze kuzalishwa,” amesema Gombe.

 

 
Wakati Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Toni Filbert amesema wilaya hiyo pamoja na Mkoa wa Pwani kwa ujumla wanazo fursa nyingi za uwekezaji kutokana na ardhi kubwa yenye rutuba. Vilevile, kuna bidhaa nyingi za kimkakati zinazozalishwa na wazawa.


Akitoa maelezo kuhusu  uwezo wa kiwanda hicho, Mkurugenzi Mkuu wa Lodhia Group of Companies, Harminder Bhachu alisema kampuni hiyo ilianzishwa mwaka 1996 wakiwa wanafanya biashara ya jumla ya kuuza vyuma ambapo mwaka 2004 ndio walianza kuzalisha vyuma katika kiwanda kilichopo mkoani Arusha.

 

 
“Vilevile tuligeukia bidhaa nyingine ikiwemo mabomba ya maji, Gypsum Board, mapipa ya kuhifadhia maji na bidhaa nyingine za ujenzi kwa kuhakikisha Tanzania inajitosheleza katika vifaa vya ujenzi bila kuagiza nje ya nchi,” amesema Bhachu na kufafanua wanamshukuru Rais Magufuli kwa kuwahamasisha kuwekeza kwa nguvu na pia amesaidia kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji kwa kila kampuni bila kupendelea.

 

 
Hata hivyo katika ziara hiyo, wajumbe wa SADC pia walipata fursa kutembelea kiwanda cha kusindika matunda cha Bakhresa Group of Companies kilichopo Mwandege Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.

 

 
Wajumbe walivutiwa na namna ya kipekee waliyoonyesha wafanyakazi wa kiwanda hicho katika usindikaji matunda, mitambo ya kisasa na usafi wa hali ya juu pia ulionyesha ni namna gani kampuni hiyo ilivyo tayari kuliteka soko la SADC.


Akielezea uwekezaji huo mkubwa uliogharimu Dola za Kimarekani Milioni 210, Mkurugenzi wa Mahusiano Bakhresa Group, Hussein Sufian alisema kampuni hiyo ina viwanda mbalimbali vipatavyo vinne ambavyo vinasindika bidhaa za chakula.

 

 
“Soko letu baada ya kujitosheleza ndani tulijipanua katika mataifa mbalimbali ya kiafrika, kwenye muktadha wa SADC tunafikisha bidhaa zetu katika nchi saba ukiondoa Tanzania, ambazo ni DRC, Angola, Comoro, Msumbiji, Malawi, Zimbabwe na Afrika Kuisini.

 

 
“Katika kuhakikisha tunakuza ajira na kuongeza tija katika uzalishaji, kwa asilimia kubwa malighafi zetu zinatoka Tanzania. Tuna ardhi kubwa inayotuwezesha kukusanya matunda kila kona ya nchi, tunayasindika na kuuza nje ya nchi kwa kiwango cha kutosha. Asilimia 15 ya bidhaa zetu tunazisafirisha nje ya Tanzania hasa hizi nchi za SADC,” ameeleza.

 

 
Akizungumza katika kiwanda hiki, Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga amesema watahakikisha wanasimamia haki za msingi za kampuni hiyo kwa sababu imewapa heshima kubwa katika Mkoa wa Pwani kutokana na kupata ajira nyingi za vijana.

 

 
Pamoja  na mambo mengine wajumbe wametembelea pia kiwanda cha kusindika korosho cha Biotan kilichopo wilayani Mkuranga ambapo  Katika kiwanda hiko wajumbe walijionea hatua kwa hatua namna korosho zinavyopokewa kutoka kwa wakulima, zinavyopangwa kwa daraja, zinavyochemshwa kwa kutumia mvuke hadi hatua ya kuzibangua zikiwa tayari kwa kuwekwa kwenye mifuko.

 

 
Akizungumza kiwandani hapo Bahati Mayoma ambaye ni  Mkurugenzi wa Biotan Group Limited amefafanua kampuni yao kwa kiasi kikubwa kinamilikiwa na raia kutoka Australia, ndiyo maana hata bidhaa zao zinazingatia viwango vya hali ya juu kwa kuwa wanazisafirisha katika nchi za Ulaya.

 

 
Ameongeza kuwa wanaliona soko la SADC muhimu kwao kwa kuwa kitu muhimu kinachotakiwa katika kulifikia soko hilo ni kuwa na bidhaa zenye ubora ambazo zinaandaliwa katika mazingira safi na salama kwa kutumia teknolijia za hali ya juu.


“Bidhaa zetu tunazipeleka Denmark, Sweden, Ujerumani, Australia na nchi nyingine nyingi za kiafrika. Lakini kwa sasa soko letu jipya tunaangalia hizi nchi za SADC,” amesema Mayoma.


 

Amesema kwamba kwa mwaka uwezo wao wa kuzalisha ni tani 1500 hadi 2000, lakini wanatarajia baada ya kuliteka soko la SADC ikifika mwaka 2021 uwezo wa uzalishaji utafikia tani 5000 kwa mwaka.

 

 
Kwa kukumbusha tu SADC ni jumuiya ya kimaendeleo ya kiuchumi inayohusisha nchi wanachama 16 ambazo ni Tanzania, Msumbiji, Zambia, Zimbabwe, Malawi, Angola, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Ushelisheli, Comoro, Botswana, Eswatini, Lesotho, Madagascar, Afrika Kusini, Mauritius na Namibia. Kwa mwaka huu mkutano wa wakuu wa nchi wanachama utafanyika Tanzania kuanzia Agosti 17 hadi 18 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Julius Nyerere (JNICC).




Mkurugenzi Mkuu wa Lodhia Group of Companies, Harminder Bhachu akieleza kuhusu namna Nondo zinavyotengenezwa hatua kwa hatua na hatimaye kupelekwa sokoni kwa kuuzwa,mbele ya Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda  waliotembelea kiwanda hicho kwa ajili ya kuangalia ubora wa bidhaa na mazingira ya uzalishaji kwa Tanzania. 

Bhachu alisema kampuni hiyo ilianzishwa mwaka 1996 wakiwa wanafanya biashara ya jumla ya kuuza vyuma ambapo mwaka 2004 ndio walianza kuzalisha vyuma katika kiwanda kilichopo mkoani Arusha.“Vilevile tuligeukia bidhaa nyingine ikiwemo mabomba ya maji, Gypsum Board, mapipa ya kuhifadhia maji na bidhaa nyingine za ujenzi kwa kuhakikisha Tanzania inajitosheleza katika vifaa vya ujenzi bila kuagiza nje ya nchi,” alisema Bhachu na kuongeza.
Mkurugeni wa Kampuni ya Lodhia Group of Companies Sailesh Pandit akiwaongoza Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda  waliotembelea kiwanda hicho leo kwa ajili ya kuangalia ubora wa bidhaa na mazingira ya uzalishaji kwa Tanzania. 
 Mkurugenzi Mkuu wa Lodhia Group of Companies, Harminder Bhachu akiwaonesha Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC nondo zikiwa tayari kusafirishwa maeneo mbalimbali kwa matumizi.
 Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda  wakiangalia namna mabomba ya Platic yanavyotengenezwa  ndani ya kiwanda cha Lodhia Group of Companies, hatua kwa hatua na hatimaye tayari kwa matumizi
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Toni Filbert akizungumza mbele ya Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda (hawapo pichani) mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea kiwanda cha Lodhia Group of Companies,kilichopo wilayani humo mkoani Pwani,Mh.Filbert alisema wilaya hiyo pamoja na Mkoa wa Pwani kwa ujumla wanazo fursa nyingi za uwekezaji kutokana na ardhi kubwa yenye rutuba. Vilevile, kuna bidhaa nyingi za kimkakati zinazozalishwa na wazawa. 

“Tunaihakikishia serikali kuwa kazi tunaiweza, tutatoa fursa za ajira na kuzifanyia kazi rasilimali tulizonazo kwa ajili ya Tanzania mpya ya viwanda. Tunaomba, kampuni kama hizi za kimkakati zipewe fursa katika kushiriki ujenzi wa miradi mikubwa ikiwemo SGR na miradi mingine ikiwemo madaraja na barabara,” alisema Filbert.
Mkurugeni wa Kampuni ya Lodhia Group of Companies, Sailesh Pandit akisoma hotuba yake fupi mbele ya Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda,ambao wametembelea kiwanda hicho leo kwa ajili ya kuangalia ubora wa bidhaa na mazingira ya uzalishaji kwa Tanzania. 
Mkurugeni wa Kampuni ya Lodhia Group of Companies, Sailesh Pandit akizungumza na baadhi ya Waandishi wa habari walioambatana na Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda,ambao wametembelea kiwanda hicho leo kwa ajili ya kuangalia ubora wa bidhaa na mazingira ya uzalishaji kwa Tanzania. 
Mkurugenzi wa Mahusiano Bakharesa Group, Hussein Sufian akitoa ufafanuzi wa jambo mbele ya wajumbe wa SADC waliopata fursa ya kutembelea kiwanda hicho  cha kusindika matunda cha Bakhresa Group of Companies kilichopo Mwandege Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.Katika ziara hiyo Wajumbe walivutiwa na namna ya kipekee waliyoonesha wafanyakazi wa kiwanda hicho katika usindikaji matunda, mitambo ya kisasa na usafi wa hali ya juu,huku ikionesha pia ni namna gani kampuni hiyo ilivyo tayari kuliteka soko la SADC.

Akielezea uwekezaji huo mkubwa uliogharimu Dola za Kimarekani Milioni 210, Mkurugenzi wa Mahusiano Bakharesa Group, Hussein Sufian alisema kampuni hiyo ina viwanda mbalimbali vipatavyo vinne ambavyo vinasindika bidhaa za chakula.“Soko letu baada ya kujitosheleza ndani tulijipanua katika mataifa mbalimbali ya kiafrika, kwenye muktadha wa SADC tunafikisha bidhaa zetu katika nchi saba ukiondoa Tanzania, ambazo ni DRC, Angola, Comoro, Msumbiji, Malawi, Zimbabwe na Afrika Kuisini.
Mkurugenzi wa Mahusiano Bakharesa Group, Hussein Sufian akitoa ufafanuzi wa jambo mbele ya wajumbe wa SADC waliopata fursa ya kutembelea kiwanda hicho  cha kusindika matunda cha Bakharesa Group of Companies kilichopo Mwandege Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.
Mkurugenzi wa Biotan Group Limited,Bahati Mayoma akizungumza mbele ya Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda  na baadaye walitembelea kiwanda hicho cha kusindika Korosho kilichopo Mkuranga mkoani Pwani , Wajumbe hao walijionea hatua kwa hatua namna korosho zinavyopokewa kutoka kwa wakulima, zinavyopangwa kwa daraja, zinavyochemshwa kwa kutumia mvuke hadi hatua ya kuzibangua zikiwa tayari kwa kuwekwa kwenye mifuko.

Akizungumzia kuhusu soko,Mayoma alibainisha kuwa wanaliona soko la SADC muhimu kwao kwa kuwa kitu muhimu kinachotakiwa katika kulifikia soko hilo ni kuwa na bidhaa zenye ubora ambazo zinaandaliwa katika mazingira safi na salama kwa kutumia teknolijia za hali ya juu.Alisema kwa mwaka uwezo wao wa kuzalisha ni tani 1500 hadi 2000, lakini wanatarajia baada ya kuliteka soko la SADC ikifika mwaka 2021 uwezo wa uzalishaji utafikia tani 5000 kwa mwaka. 
Baadhi akina mama wakibangua korosho ndani ya kiwanda cha BIOTAN,kilichopo Mkuranga mkoani Pwani,Wajumbe wa mkutano wa 39 wa SADC walioshiriki wiki ya nne ya viwanda na baadaye walitembelea kiwanda hicho cha kusindika Korosho kilichopo Mkuranga mkoani Pwani , Wajumbe hao walijionea hatua kwa hatua namna korosho zinavyopokewa kutoka kwa wakulima, zinavyopangwa kwa daraja, zinavyochemshwa kwa kutumia mvuke hadi hatua ya kuzibangua zikiwa tayari kwa kuwekwa kwenye mifuko.Picha na Michuzi JR.

PALIPO NA MNADA WA MIFUGO LAZIMA PAWEPO NA MIZANI

$
0
0
Naibu Waziri wa Mifugo Kilimo na Uvuvi Abdallah Ulega akizungumza jambo na wananchi wa Longido Kata ya Ngarnenairu Mkoani Arusha.

Naibu waziri wa Mifugo,Kilimo na Uvuvi akisikiliza kero za wafugaji katika mnada wa Ngarenaiboru uliopo wilaya ya mkoani Arusha
Naibu waziri wa Mifugo,Kilimo na Uvuvi akisisitiza jambo alipokutana na wananchi wa kata ya Ngarenaiboru katika mnada wa Ngarnaiboru leo.



Na.Vero Ignatus,Arusha

Naibu waziri wa kilimo mifugo na uvuvi Mhe,Abdallah Ulega ametoa agizo kwa wakurugenzi wote nchini kuhakikisha kuwa kila penye mnada wa mifugo lazima pawe na mizani kama hawatafanya hovyo watanyang'anywa fursa ya kuuza ng'ombe.

Akizungumza katika kata ya Engaranaiboru katika ziara yake ya kikazi wilayani Longido mkoani Arusha,Ulega amesema kuwa uuzwaji wa mifugo Nchini kwa kutumia madalali una lengo la kumnyonya mfugaji na sio kunufaika.

Amesema kuwa 95% ya wakazi wa Longido ni wafugaji hivyo lengo kuu ni kusimamia haki ya mfugi kwani halmashauri nyingi zinachukua mapato katika minada lakini hawafanyi shughuli yenyewe ya kuhuidumia.

Amesema mfugaji anakosa sauti kutokana na mtu wa tatu ambaye ni dalali,ambaye ananufaika wakati aliyefuga ni mtu mwingine.Aidha Ulega amesema Sheria ya kila bidhaa kupimwa ipo wazi na mwogozo wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi upo wazi hivyo Mizani ni lazima ili haki ya mfugaji Ipatikane.

Hata hivyo amesema kuwa ikiwa kila mnada utaanza kutumia Mizani itapelekea wafugaji kubadili uelekeo kwa kufuga mifugo michache,yenye tija badala ya kufuga mifugo mingi.

Naye mbunge msaafu Jimbo la Longido Lekule Ole Laizer ameiomba serikali iwapelekee dawa kwaajili ya majosho kwani yapo ila hayatumiki ,pia ameomba wapatiwe kibali cha kuuza mifugo Kenya kama ilivyo kwa biashara nyingine

Lekule amesema changamoto kubwa waliyonayo ni mifugo yao kushambuliwa na magonjwa kama vile Ormolo,kichaa cha mbwa,brusele( Mfugo kutupa mimba),ndigana baridi na moto, Nemonia, ugonjwa wa mapele na mkojo wa damu.

WAZIRI LUGOLA AITAKA POLISI IRINGA KUCHAPA KAZI, KUANZA ZIARA MKOANI RUKWA KESHO, KUFUATILIA MAAGIZO YAKE

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati), akimsalimia Mkuu wa Nidhamu Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa, (RSM), Flora Lyimo, wakati alipofika Makao Makuu ya Polisi Mkoani humo, leo, akiwa safarini kuelekeza Mkoa wa Rukwa. Kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa huo, ACP Juma Bwire. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akimsikiliza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, ACP Juma Bwire, alipokua anasoma taarifa ya hali ya ulinzi na usalama mkoani humo, leo. Lugola alipita ofisi ya Kamanda huyo, akiwa safarini kuelekeza Mkoa wa Rukwa.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akimsalimia Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, ACP Juma Bwire, wakati alipowasili Mjini Iringa, leo, akiwa safarini kuelekeza Mkoa wa Rukwa. Kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa huo, ACP Juma Bwire. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 


Na Felix Mwagara, MOHA, IRINGA.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewasili mjini Iringa leo, na kulitaka Jeshi la Polisi Mkoani humo kutenda haki katika utendaji wao.

Lugola alifanya ziara ya saa mbili mkoani humo, akiwa safarini kuelekea Mkoa wa Rukwa kwa ziara ya siku tano mkoani humo.

Akizungumza katika kikao cha viongozi wa Polisi wa Mkoa huo, Lugola alisema amefika kuonana na viongozi hao akiwa safarini, kwa lengo la kufuatilia utendaji kazi ikiwa ni utaratibu wake ambao alijiwekea tangu aiongoze Wizara hiyo. 

Lugola alisema lengo la ziara yake mkoani Rukwa ni kufuatilia maagizo yake aliyoyatoa kwa vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo ndani ya Wizara yake, na pia atafanya ziara kama hizo mikoa yote nchini. 

Alisema anatarajia kutembelea Wilaya zote za Mkoa huo kusikiliza kero za wananchi kupitia mikutano mbalimbali ya hadhara itakayofanyika katika wilaya hizo.

“Natarajia kuanza ziara hiyo rasmi kesho Agosti 10, 2019 Mjini Sumbawanga kwa kukutana na Mkuu wa Mkoa pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, kupokea taarifa ya Kamati hiyo, kabla ya kuanza kuzungumza na Wakuu wa vyombo vyake na baadaye kukutana na Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa, na kumaliza kwa kuzungumza na Baraza la Askari na Watumishi wote wa Wizara hiyo waliopo mjini humo,” alisema Lugola.

“Nitafanya mkutano mkubwa wa hadhara katika Mji wa Sumbawanga, utaanza saa 10:00 hadi 12:00 jioni, hivyo nawaomba wananchi wa mji huo wajitokeze kwa wingi kunisikiliza kile ambacho nimepanga kuwaambia, na pia nitawapa nafasi wananchi waulize maswali bila woga, waniambie kero zao nami nitazitatua katika mkutano huo,” alisema Lugola. 

Lugola alisema katika ziara yake aliyoifanya mwaka jana Mkoani Kigoma na mwezi Januari Mwaka huu Mkoa wa Kagera, Arusha Mwezi Februari na Morogoro wiki iliyopita, amegundua wananchi wanakabiliwa na changamoto mbalimbali hivyo hawezi kulala akiwa ofisini, lazima afanye ziara nchi nzima kuwasaidia wananchi kutatua kero zao ambapo wengi wao wakiwalalamikia Polisi wakiwaonea. 

“kupitia kikao hiki hapa Iringa, napenda kuwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi, wanapojitokeza kwa wingi inasaidia kusikiliza matatizo yao yanayowakabili, ndio mana nimepanga kufanya ziara kama hizi nchi nzima, hii inasaidia sana kujua matatizo mbalimbali ya wananchi pamoja na kuangalia utendaji kazi wa Taasisi zangu zilizopo ndani ya Wizara hii, na hakika Serikali ya Rais Dokta John Magufuli inawajali wananchi wake ndio mana inawafuata mahali walipo, ili wazungumze na Serikali yao uso kwa uso,” Alisema Lugola. 

Waziri Lugola baada ya kumaliza ziara yake Mjini Sumabwanga, ataenda Wilaya ya Sumbawanga Vijiji ambapo atatembelea Gereza Mollo kutatua mgogoro wa ardhi na baadaye atazungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara. 

Waziri Lugola, Agosti 12, 2019, atafanya ziara Wilayani Kalambo, na baada atamaliza ziara yake Wilaya ya Nkasi kwa kutembelewa majimbo ya Nkasi Kaskazini na Kusini. 

Katika Wilaya zote atakazozitembelea pia atazungumza na wananchi pamoja na watumishi waliopo ndani ya Wizara yake ambao ni Jeshi la Polisi, Idara ya Uhamiaji, Jeshi la Magereza, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, pamoja na Idara ya Probesheni ambayo jukumu lake kuu ni kupunguza msongamano gerezani na kusimamia wafungwa waliopewa adhabu mbadala na Mahakama au wafungwa waliopata msamaha kupitia sheria ya huduma kwa jamii na kutumikia kifungo chao nje ya Gereza.

Maagizo aliyoyatoa Waziri Lugola mara baada ya kuteuliwa kuiongoza Wizara hiyo, ni dhamana zitolewe saa 24 katika vituo vyote vya polisi nchini, na pia alipiga marufuku tabia ya baadhi ya Polisi kubambikizia kesi wananchi, na pamoja na agizo la pikipiki zote zilizopo vituoni ziondolewe.

Pia aliagiza wakuu wa vyombo kuthibiti rushwa katika taasisi wanazoziongoza, na kutowanyanyasa watumishi katika taasisi zao.

Lugola anatarajia kumaliza ziara yake Agosti 17 mkoani humo na kurejea Dodoma kushiriki vikao vya Kamati ya Kudumu ya Bunge, Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.


MCHUNGUZI MKUU WA TAKUKURU AFIKISHWA KORTINI AKIKABILIWA NA MASHTAKA 7 YAKIWEMO YA KUOMBA RUSHWA ZAIDI YA MILIONI 200

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv

MCHUNGUZI Mkuu Wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Cosmas Batanyita( 44), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashtaka saba yakiwemo ya kuomba na kupokea rushwa ya zaidi ya sh. Milioni 200

Akisoma hati ya mashtaka wakili wa Serikali Mkuu Paul Kadushi amedai mbele ya Hakimu Mwandamizi Mfawidhi, Kelvin Mhina kuwa, Februari 9, 2019 huko Upanga, mshtakiwa Batanyika, alishawishi na kuomba rushwa ya Sh. Milioni 200 kutoka kwa Hussein Gulamal Hasham kwa lengo la kuharibu ushahidi katika kesi ya ukwepaji wa kodi inayomkabili Hasham, wakati akijua kuwa upelelezi wa kesi hiyo ulikuwa unaendelea katika Ofisi ya Takukuru.

Imeendelea kudaiwa kuwa, Februari 10, 2019 katika eneo la Sabasaba, mshtakiwa Batanyita alipokea USD 20,000 kutoka Faizal Hasham ikiwa ni ahadi ya kuharibu ushahidi katika kesi ya ukwepaji kodi inayomkabili Hussein Hasham.

Pia, February 13, 2019, katika ofisi ndogo za Takukuru zilizopo Masaki, mshtakiwa alishawishi rushwa ya USD 50,000 kutoka kwa Thangvelu Vall, ili aweze kuharibu ushahidi katika kesi ya kukwepa kodi inayomkabili Vall.

Katika shtaka la nne, Februari 14, 2019 katika barabara ya Haile Selasie karibu na Merry Brown, mshtakiwa alishawishi rushwa ya USD 20,000 kutoka kwa Thangvelu Vall, kama ahadi ya kuharibu ushahidi katika kesi ya kukwepa kodi inayomkabili Vall, wakati akijua upelelezi wa kesi hiyo unaendelea.

Aidha Februari 10, 2019, mshtakiwa Batanyita anadaiwa kutakatisha USD 20,000 kutoka kwa Hasham, wakati akijua fedha hizo ni zao la kosa tangulizi la rushwa.

Pia imedai, Februari 19 2019, katika duka la kubadilishia fedha la Village Super Market huko Oysterbay, mshtakiwa kwa lengo la kuficha chanzo cha fedha USD 7000, alizopewa, alibadilisha fedha hizo na kupata fedha za kitanzania kiasi cha Sh milioni 16 wakati akijua kuwa fedha hizo ni zao La kosa tangulizi la kosa la kuomba rushwa.

Katika shtaka la mwisho imedaiwa, Februari 19, 2019 eneo la Chamazi, mshtakiwa alitumia fedha alizopewa kwa njia ya rushwa, kununulia kiwanja eneo la Chamazi, kwa gharama ya Sh15,8000,000, wakati akijua fedha hizo ni zao tangulizi la kosa la kuomba rushwa.

Hata hivyo, mshtakiwa hakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi.Kwa mujibu Wa upande mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado unaendela na mshtakiwa amerudishwa rumande. Hadi Agosti 23, 2019 kesi hiyo itakapotajwa tena.
 MCHUNGUZI Mkuu Wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Cosmas Batanyita( 44), akifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashtaka saba yakiwemo ya kuomba na kupokea rushwa ya zaidi ya sh. Milioni 200


ASKOFU MULILEGE KAMEKA ADAI KUFUNGUA UPYA KESI DHIDI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI.!

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv

ASKOFU Mulilege Kameka Wa kanisa la Boko Yerusalem, kupitia kwa wakili wake John Mallya anatarajia kufungua upya kesi, Mahakamani dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Kamishna Mkuu wa Uhamiaji kufuatia Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam kufuta maombi yake ya kutaka watu hao waletwe mahakamani hapo na kujieleza kwanini wasifungwe kwa kupuuza amri ya mahakama. 

Akizungumza nje ya mahakama baada ya uamuzi huo kutolewa, Wakili Mallya, amesema, ingawa maombi yao yamefutwa lakini bado hawajakata tamaa, atakwenda kuzungumza na mteja wake pamoja na mawakili wenzake ili kuona njia watakayotumia kufungua upya shauri hilo mahakamani.

Amsema bado wanaamini kwamba Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Kamishna Mkuu wa Uhamiaji wanakosa la kutotekeleza na kutii amri ya Mahakama ya kumuachia huru Askofu hiyo, 

"Jumanne tutakuja mahakamni kufaili kesi kama tulivyoelekezwa na jaji jinsi ya kufanya na kama kuna mtu yeyote anamaswali juu ya uraia wa mtumishi huyu wa Mungu aje mahakamani, " amesema Wakili Mallya. 

Kameka ambaye ni Askofu wa kanisa la House of Prayer Shield of Faith Christian Fellowship Church (HPSFCFC) maarufu kama Boko Yerusalem, anashikiliwa mahabusu kwa zaidi ya miezi tisa sasa kwa tuhuma za kutokuwa raia wa Tanzania, licha ya Mahakama Kuu kuamuru kuwa anapaswa kuachiwa huru kwani uraia wake hauna mashaka. 

Mapema leo Agosti 9,2019 Jaji Dk Atuganile Ngwala alitoa uamuzi wa kufuta maombi hayo kwakuwa yameletwa chini ya vifungu vya sheria ambavyo havihusiki.Akitoa uamuzi huo, Jaji Ngwala alisema, anakubaliana na hoja za mawakili wa serikali kuwa maombi hayo yalipaswa kuletwa chini ya kifungu cha 9 cha sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) badala ya kufungu namba 392 cha CPA na 114 cha sheria ya Kanuni ya adhabu.

Alisema kutokana na hali hiyo anayafuta maombi hayo kwakuwa hayajaletwa kisheria.Katika shauri hilo, Machi 18 Mwaka huu, Mahakama hiyo iliamuru askofu huyo aliyekuwa akishikiliwa na Wizara ya Mambo Ndani aachiliwe huru kutoka kizuizini anaposhikiliwa ikisema kwamba uraia wake hauna mashaka

Amri hiyo ilitolewa na Jaji IIvin Mgeta ambaye alitoa maelekezo kuwa Askofu hiyo atolewe mahali anaposhikili kwani vilelezo vilivyotolewa vimedhibitisha uraia wake kuwa ni mtanzania lakini licha ya amri hiyo kutolewa mpaka leo bado Askofu huyo ameshikiliwa na yuko mahabusu gerezani ndipo kupitia kwa Wakili wake Mallya aliamua kuyaleta maombi hayo.

Maombi hayo yamefunguliwa dhidi ya wajibu maombi ambao ni AG na Kamishna Mkuu Uhamiaji ambayo kabla ya kusikilizwa, upande wa serikali ukiongozwa na wakili wa serikali Jackline Nyantori waliwasilisha pingamizi la awali mahakamani hapo wakidai kuwa, Kifungu cha sheria ambacho wapeleka maombi wamekitumia kupeleka maombi hayo hakiipi mamlaka Mahakama Kuu ya kuweza kusikiliza maombi hayo .

Akijibu hoja hiyo, wakili wa mpeleka maombi, Mallya alidai kuwa maombi hayo yalipelekwa kwa mujibi na taratibu, kwani sheria inaruhusu kuleta maombi ya aina hiyo kwa njia ya hati ya maombi na kiapo kama walivyofanya wao katika kupeleka maombi.

Hata hivyo upande wa serikali ulisisitiza kwamba kwa kuwa kosa linalodaiwa kutendeka halikufanyika mbele ya mahakama waombaji walipaswa wapeleke malalamiko hayo kwanza polisi walete madai ndipo mahakama iyasikilize na kuyatolea maamuzi.

IAskofu Kameka anadaiwa kukamatwa na Wizara ya Mambo ya Ndani tangu Desemba,2018, kwa madai kuwa sio raia waTanzania, lakini alikuja hapa Mahakama Kuu Machi,2019 na mahakama hiyo ikaamua kuwa Askofu Kameka ni raia na uraia wake hauna mashaka hivyo Magereza na kitengo cha Uhamiaji wamuachie haraka amri ambayo mpaka leo haijatekelezwa. 


RC MAKONDA ATOA MWEZI MMOJA KWA MANISPAA YA KINONDONI KUANZA UJENZI WA FUKWE ZA COCO

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo August 09 ametoa Mwezi Mmoja kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kuhakikisha ujenzi wa maboresho ya Fukwe za Coco unaanza mara moja na kama wakishindwa watanyang’anywa fedha hizo na kutafutwa mzabuni.

Mapema leo RC Makonda akiambatana na Katibu Tawala wa mkoa huo wamefika kwenye ufukwe huo kwaajili ya kuangalia maendeleo ya mradi lakini wameshangazwa kuona hakuna chochote kinachoendelea wakati tayari Rais Dkt.John Magufuli alishatoa kiasi cha Shilingi Bilioni 14 za ujenzi huo lakini fedha hizo zimebaki kwenye akaunti bila matumizi huku watendaji wakilumbana kwenye vikao.

RC Makonda amesema kinachomsikitisha zaidi ni kuona mshauri wa mradi amebadili mchoro wa Mwonekano mpya wa fukwe ambao ndio ulioombewa fedha kiasi cha Bilioni 14 na kuja mchoro wake mwingine wa Shilingi bilioni 40 bila kujua fedha hizo zitatoka wapi jambo ambalo RC Makonda amelizungumzia kama mpango wa hujuma kwa serikali.

Aidha RC Makonda amewataka wananchi wajue kuwa kinachochelewesha mradi ni uzembe unaofanywa na watendaji wachache ambao wameishia kushinda kwenye vikao.

Pamoja na hayo RC Makonda amezitaka Halmashauri zote za mkoani humo kuhakikisha fedha zinazotolewa kwaajili ya maendeleo ya wananchi zinatumika na sio kuwekwa kwenye akaunti huku wananchi wakitaabik

WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA USAFIRISHAJI ZANZIBAR, DKT SIRA MAMBOYA ATEMBELEA SHIRIKA LA POSTA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Usafirishaji Zanzibar, Dkt. Sira Ubwa Mamboya, akizungumza na uongozi wa Shirika la Posta, jijini Dar es Salaam leo. 
Postamasta Mkuu wa Shirika la PostaTanzania (TPC),
Hassan Mwang’ombe (kulia), akizungumza wakati akimkaribisha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Usafirishaji Zanzibar, Dkt. Sira Ubwa Mamboya (katikati), alipotembelea shirika hilo, Makao Makuu, jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwa waziri Mamboya ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Mh.Mhandisi Atashasta Nditiye (Mb) na wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya TPC, Kanali mstaafu, Dkt. Haruni Kondo.
Meneja Mkuu wa Shirika la Posta, Menejimenti ya Rasilimali za Shirika, Macrice Mbodo, akitoa maelezo kuhusu shirika hilo, lilikotoka hadi sasa na malengo yake ya baadaye kwa Waziri Dkt. Sira Mamboya, wakati wa ziara hiyo.
Waziri Dkt. Sira Mamboya (wapili kulia), Naibu Waziri wa Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (watatu) na Mwenyekiti wa Bodi ya TPC, Kanali mstaafu, Dkt. Haruni Kondo, wakimsikiliza Meneja Mkuu Menejimenti ya Rasilimali za Shirika, Macrice Mbodo. 
Meneja Mkuu wa Shirika la Posta, Menejimenti ya Rasilimali za Shirika, Macrice Mbodo, akitoa maelezo kuhusu shirika hilo.
Baadhi ya Maofisa wa Shirika la Posta, wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Meneja Mkuu, Menejimenti ya Rasilimali za Shirika, Macrice Mbodo.
Mwenyekiti wa Bodi ya TPC, Kanali mstaafu, Dkt. Haruni Kondo, akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (kushoto), kumkaribisha Waziri Dkt. Sira Mamboya (wapili kushoto) kuzungumza.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (kushoto), akimkaribisha Waziri Dkt. Sira Mamboya kuzungumza na uongozi wa shirika.
Waziri Dkt. Sira Mamboya (katikati), Naibu Waziri wa Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (watatu kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Shirika la Posta. Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya TPC, Kanali mstaafu, Dkt. Haruni Kondo na wa pili kulia ni Postamasta Mkuu, Hassan Mwang’ombe.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Usafirishaji Zanzibar, Dkt. Sira Ubwa Mamboya, akiagana na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye mara baada ya kumaliza kupiga picha ya pamoja katika ziara hiyo.

MFUMUKO WA BEI KWA MWEZI JULAI 2019 WABAKI ASILIMIA 3.7

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Jamii, Ruth Minja akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari wakati alipokuwa akitoa taarifa ya mfumuko wa bei kwa kipindi cha mwaka ulioishia mwezi Julai 2019. Kulia ni Kaimu Meneja wa Takwimu za Ajira na Bei, Gregory Millinga. Mkutano huo ulifanyika leo Ijumaa Agosti 9, 2019.
Kaimu Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Jamii, Ruth Minja akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari wakati alipokuwa akitoa taarifa ya mfumuko wa bei kwa kipindi cha mwaka ulioishia mwezi Julai 2019.
(PICHA NA MAELEZO).


Ofisi ya Taifa ya Takwimu imetoa taarifa ya mfumuko wa bei nchini ambapo pamoja na mambo mengine mfumuko wa bei ya mwezi Julai 2019, umebakia kuwa asilimia 3.7 kama ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Juni 2019.

Akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari leo Ijumaa (Agosti 9, 2019) Kaimu Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Ruth Minja alisema kiwango hichi kubakia kuwa sawa kwa kiwango hicho kumechangiwa na kuongezeka na kupungua kwa bei za baadhi za vyakula na bidhaa zisizo za chakula kwa kipindi kilichoisha Julai 2019.

Aidha Minja alisema mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Julai 2019 umeongezeka kidogo hadi kufikia asilimia 2.9 kutoka asilimia 2.3 ilivyokuwa kwa mwezi Juni 2019.

“Baadhi ya bidhaa zilizoongezeka bei kwa mwezi Julai zikilinganishwa na Julai 2018 ni pamoja na unga wa mahindi (6.0%), unga wa mhogo (4.0%), mafuta ya kupikia (8.9%), na mbogamboga (4.6%) ambapo kwa uoande wa bidhaa zisizokuwa za vyakula ni pamoja na vifaa vya kieletroniki, majiko ya gesi pamoja na vifaa pamoja na bidhaa za huduma”.

Akizungumzia hali ya mfumuko wa bei kwa baadhi ya Nchi za Afrika Mashariki, taarifa inaonyesha kuwa Nchi ya Kenya ilikuwa na Kiwango cha juu cha mfumuko wa bei kwa mwezi Julai 2019, ambapo kiwango chake kilifikia asilimia 6.27 ikilinganishwa na asilimia 5.70 kwa mwaka ulioishia Juni 2019.

Akifafanaua zaidi Minja alisema taarifa ya mfumuko wa bei katika Nchi ya Uganda katika mwaka ulioishia Julai 2019, taarifa zinaonyesha kuwa Nchi hiyo ilikuwa na kiwango kidogo cha mfumuko wa mdogo bei kilichofikia asilimia 2.6 kutoka asilimia 3.4 kwa mwaka ulioishia Juni, 2019.

MKUU WA WILAYA YA NYASA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI MRADI WA MAJI LIPARAMBA

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Bi Isabela Chilumba hivi karibuni ameweka jiwe la msingi katika Mradi wa Maji unaotekelezwa katika Kijiji cha Liparamba Kata ya Liparamba, Wilayani Nyasa ambao utawanufaisha wakazi 4694. Mpaka kukamilika kwake.

Katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi uliofanyika katika viwanja vya Kituo cha Afya cha Liparamba Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Bi Isabeba Chilumba alimuagiza Mkandalasi anayetekeleza mradi huu kukamilisha kwa wakati na kuhakikisha maji yanatoka kabla ya mwezi wa tisa kama mkataba unavyosema.pia aliwaagiza wananchi waitunze miundombinu inayojengwa na Serikali kwa ajili ya kutatua kero ya maji iliyowasumbua kwa muda mrefu.

Aliongeza lengo la Serikali ni kutatua kero zinazowakabili wananchi wake ili waweze kufanya shughuli za kimaendeleo kama alivyohakikisha kata ya Liparamba inapata maji safi na salama.

“Nakuagiza Mkandarasi wa mradi huu ufanye kazi kwa juhudi usiku na mchana na ifikapo mwezi Septemba uwe umemaliza na maji yatoke ili yatatue kero kwa wananchi wa kata hii ya Liparamba.Pia ninawaagiza wananchi muitunze miundombinu ya maji kwa kuhakikisha jumuiya za watumia maji zinatekeleza majukumu yao”

Awali akisoma taarifa ya maendeleo ya mradi huo,Kaimu Meneja wa wakala wa maji mijini na vijijini Josephat Kayumba alisema mradi umefikia asilimia 85 ya utkelezaji na unatekelezwa na Mkandarasi wa kampuni ya Ovansi Contruction Limited, iliyoshinda Zabuni ya kujenga mradi, kwa gharama ya shilingi (1,020,089,315.00) ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa sekta ya maji awamu ya pili , (WSDP II) Nchini Tanzania ambao ulianza kutekelezwa mwaka wa fedha 2015/2016.

Alizitaja kazi zilizofanyika kuwa, ni kujenga miundombinu ya vyanzo viwili vya maji (intakes) na sehemu moja ya kukusanyia maji, kujenga tanki la kutunzia maji lenye ujazo wa mita sabini na tano (75m3) na Mtandao wa mabomba, ya kusambaza maji kilometa ishirini na tano (25.85) .Pia amejenga vituo vya kuchotea maji ishirini na tisa (29) na matanki madogo ya kupunguza msongo wa maji katika bomba sita (6) chemba thelathini na saba (37) katika maeneo mbalimbali ya mradi, pamoja na alama za bomba.
.
Wananchi wa kijiji cha Liparamba, wamefurahi kutatuliwa kero ya maji kwa kuwa awali walikuwa wakitembea umbali wa kilometa takribani tano kufuata maji huduma ya maji . kituo cha afya kilikuwa hakina maji hali iliyokuwa inawapa shida wagonjwa na wauguzi kutafuta maji wapatapo changamoto ya kuugua au kuuguliwa. Kwa sasa wanaipongeza Serikali kwa kuwatatulia kero ya maji katika kijiji chao.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa kata ya Liparamba Diwani wa Kata hiyo Ditram Nchimbi aliishukuru Serikali kwa kutatua kero ya maji katika kata hiyo na kusema watahakikisha wanaitunza miundombinu ya maji kwa kupanda miti rafiki maji na kuhakikisha vikundi vya watumia maji vinafanya kazi wakati wote.

“Mh Mkuu wa Wilaya tunaishukuru sana Serikali kwa kuhakikisha inatatua changamoto ya maji katika kijiji chetu kwa kuwa Wananchi walikuwa wakiteseka sana kutafuta maji kwa kuwa walikuwa wanatembea umbali wa Kilometa takribani tano kutafuta maji.Tutahakikisha tunaitunza Miundombinu kwa kuhakikisha jumuiya ya watumia maji zinafanya kazi muda wote”Alisema Nchimbi.

Serikali imetoa shilingi bilioni moja na nusu kwa ajili ya kutekeleza mradi mkubwa wa maji katika kata ya Liparamba wilayani hapa ili kutatua changamoto ya maji iliyokuwa inawakabili wakazi hao.
Imeandaliwa na Netho c Sichali,Ofisa Habari Wilaya ya Nyasa,0767417597

MAJALIWA AFUNGUA NYUMBA ZA MAKAZI YA POLISI MJINI SHINYANGA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Agosti 9, 2019 aliwakabidhi funguo za nyumba Askari Polisi 10 baada ya kufungua nyumba za makazi yao mjini Shinyanga. Pichani, Mheshimiwa Majaliwa akimkabidhi, Koplo Tegemea Masatu ufungua wa nyumba aliyopangiwa kuishi. Katikati ni Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Shinyanga, ACP Richard Abwao. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Agosti 9, 2019 aliwakabidhi funguo za nyumba Askari Polisi 10 baada ya kufungua nyumba za makazi yao mjini Shinyanga. Pichani, Mheshimiwa Majaliwa akimkabidhi, Koplo Tegemea Masatu ufungua wa nyumba aliyopangiwa kuishi. Katikati ni Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Shinyanga, ACP Richard Abwao. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kuzindua nyumba 10 za makazi ya Askari Polisi mjini Shinyanga, Agosti 9, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua moja kati ya nyumba 10 za Askari Polisi alizozifungua na kukabidhi funguo kwa Askari waliopangiwa kuishi katika nyumba hizo mjini Shinyanga, Agosti 9, 2019. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Tellak na wa tatu kulia ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, ACP Richard Abwao. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua moja kati ya nyumba 10 za Askari Polisi alizozifungua na kukabidhi funguo kwa Askari waliopangiwa kuishi katika nyumba hizo mjini Shinyanga, Agosti 9, 2019. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Tellak na wa pili kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mbaneko. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipanda mti baada ya kufungua nyumba za makazi ya Askari Polisi mjini Shinyanga, Agosti 9, 2019. Kulia ni Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga na kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zaib Tellak. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU ATEMBELEA KIWANDA CHA PAMBA FRESHO SHINYANGA....ASEMA SERIKALI ITALINDA WANUNUZI WA PAMBA

$
0
0





Na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Kassim Majaliwa ametembelea kiwanda cha Kuchambua pamba cha Fresho kilichopo katika eneo la Ibadakuli Mjini Shinyanga na kujionea hali halisi ya ununuzi wa pamba kutoka kwa wakulima unaofanywa na Kampuni ya Fresho Investment Company Limited. 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametembelea kiwanda cha Fresho kinachomilikiwa na Kampuni ya Fresho Investment Company Limited leo Ijumaa Agosti 9,2019 wakati akiwa kwenye ziara yake ya siku moja mkoani Shinyanga. 

Akizungumza kiwandani hapo,Waziri Mkuu aliwahakikishia wakulima wa pamba kuwa pamba yao itanunuliwa kwani lengo la serikali ni kuondoa pamba mikononi mwa wakulima. 

"Nipo kwenye ziara kwenye mikoa inayolima pamba lengo la kufuatilia mwenendo wa masoko ya pamba.Nikiwa hapa Shinyanga nimeshuhudia wingi wa pamba inayoletwa na wananchi kwenye masoko,kwetu sisi kama serikali ni jambo kubwa sana kiuchumi kwani pamba kwa Tanzania ni uchumi mkubwa,pamba imetupa heshima",alisema Majaliwa. 

"Natumia fursa hii kumpongeza Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Fresho bwana Fredy Shoo pamoja mama Fredy na watoto wa Fredy na watumishi wote wa Fresho,mnafanya kazi kubwa sana ya kuunga mkono jitihada za serikali kwa kununua pamba,nikiwa nazunguka kwenye mafurushi ya pamba kule nje,ameniambia mule ndani ni zaidi imeshanunuliwa na wanaendelea kuilipia na bado magari yanaingia kuleta pamba", 
"Kilichonifurahisha zaidi ni ile kauli yake kwamba 'Nitalipa pamba yote' yupo tayari kununua pamba yote. Kampuni ya Fresho mnafanya jambo jema kununua pamba,sisi kama serikali tunakushukuru sana na tutakulinda,hatutakuangusha. Hapa kuna mkuu wa mkoa,ukipata tatizo usisite kumuona",alisema. 

Hata hivyo Majaliwa aliwapongeza wakulima kwa kuzingatia usafi kwenye pamba kwa kuachana na tabia ya kuweka maji,mchanga,mafuta na takataka mbalimbali zinazosababisha pamba ichafuke na kuchangia sasa pamba ya Tanzania inapendwa duniani kote. 

Aidha aliwataka wakulima wa pamba kuiga wakulima wa korosho kwa kufungua akaunti benki badala ya kutembea na mafurushi ya fedha kwa siyo salama. Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kumhamasisha Mkurugenzi wa Kampuni ya Fresho,kuanzisha kiwanda cha kusokota nyuzi za pamba na kiwanda kiwanda cha kutengeneza nguo. 

Akitoa taarifa kwa Waziri Mkuu,Mkurugenzi wa Kampuni ya Fresho Investment Company (1999) Limited, Fredy Shoo alisema mbali na kumiliki kiwanda cha kuchambulia pamba pia wana kiwanda cha vifungashio na kiwanda cha kuchakata mafuta ya pamba. 

Alisema mwaka huu,kampuni yao ipo katika soko la ununuzi wa pamba kwa uwezeshaji wa benki ya NBC na CRDB ambapo mpaka sasa wamenunua pamba kilo milioni 26.5 kati ya hizo kilo milioni 24 zimeshapokelewa kiwandani na wanaendelea kununua pamba kutoka kwa wakulima. 

Alieleza kuwa pesa kutoka benki zimepungua hali inayochangia kupunguza kasi ya ununuzi wa pamba huku akisisitiza kuwa kampuni ya Fresho inategemea kununua pamba nyingi kadri inatakavyowezekana endapo watapata fedha zaidi. 

"Kampuni yetu imebeba dhamana kubwa ya kununua pamba licha ya changamoto kubwa ya soko,hii yote tunafanya ili kumpunguzia adha mkulima lakini pia kuunga mkono jitihada za serikali kutaka pamba ya mkulima inunuliwe",alisema Shoo. 

"Pamoja na changamoto ya soko la dunia kuwa chini, Tumeendelea kununua pamba kwa bei ya shilingi 1,200/= kama serikali ilivyoagiza na baadhi ya wakulima wamekuwa wakileta pamba yao hapa kiwandani nyingine ni ile inayonunuliwa na wamachinga kwa bei ya chini tofauti na iliyoelekezwa na serikali hali inayowapa hasara wakulima",alisema Shoo. 

Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Fresho bwana Fredy Shoo akimwelezea Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Kassim Majaliwa kuhusu hali ya ununuzi wa pamba kutoka kwa wakulima unavyoendelea katika kiwanda cha Kuchambua pamba cha Fresho kilichopo katika eneo la Ibadakuli Mjini Shinyanga alipotembelea Kampuni ya Fresho Investment Company Limited leo Agosti 9,2019. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Kassim Majaliwa akiangalia pamba katika kiwanda cha Fresho. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko,akifuatiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Fresho bwana Fredy Shoo. 
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Fresho bwana Fredy Shoo akimuonesha na kumwelezea Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Kassim Majaliwa pamba iliyoletwa na wakulima katika kiwanda cha Fresho.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Kassim Majaliwa akiangalia pamba iliyoletwa na wakulima katika kiwanda cha Fresho. 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Kassim Majaliwa akiangalia pamba iliyoletwa na wakulima katika kiwanda cha Fresho. 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza wakati akiangalia pamba iliyoletwa na wananchi katika kiwanda cha Fresho. 
Wakulima wakiwa na pamba yao katika kiwanda cha Fresho. 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Kassim Majaliwa akiwasalimia wakulima wa pamba walioleta pamba yao katika kiwanda cha Fresho. 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza jambo na Wanunuzi wa pamba mkoani Shinyanga,Gasper Kileo wa kiwanda cha GAKI (aliyevaa shati la kijani kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Fresho,Fredy Shoo 
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Fresho,Fredy Shoo akimweleza jambo Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa. 
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akielekea katika kiwanda cha kuchambulia pamba cha Fresho. 
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akiingia Ginnery C. 
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akiangalia pamba iliyochambuliwa katika Ginnery C,ambapo kuna Ginnery A,B,C na nyingine ipo wilayani Kahama,zote zikimilikiwa na Kampuni ya Fresho. 
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akiongozwa kiwandani. 
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akizungungumza jambo katika kiwanda cha Fresho. 

Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akitoka Ginnery C. 

Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na wakulima wa pamba na wananchi katika kiwanda cha Fresho. 
Wafanyakazi wa kiwanda cha Fresho wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa. 
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Fresho bwana Fredy Shoo akisoma taarifa fupi kuhusu kiwanda cha Fresho na hali ya ununuzi wa pamba.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Fresho bwana Fredy Shoo akisoma taarifa fupi kuhusu kiwanda cha Fresho na hali ya ununuzi wa pamba. 
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack akiteta jambo na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa. 
Waziri wa Kilimo,Mhe. Japhet Hasunga akizungumza katika kiwanda cha Fresho. 
Kushoto ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga,Mhe. Gulam Hafeez Mukadam,kulia ni Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga,Mhe. Azza Hilal Hamad (CCM). 
Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko akifuatiwa na Mbunge wa Jimbo la Solwa,Mhe. Ahmed Salum na Mkuu wa wilaya ya Kishapu,Mhe. Nyabaganga Talaba. 

Picha ya pamoja viongozi mbalimbali. 
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Fresho bwana Fredy Shoo akiagana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Kassim Majaliwa. 
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Fresho bwana Fredy Shoo akiagana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Kassim Majaliwa. 


Magari yaliyobeba pamba yakiwa katika kiwanda cha Fresho.
Magari yaliyoleta pamba yakiwa nje ya kiwanda cha Fresho. 




Sehemu ya pamba iliyoletwa na wakulima kuuzwa katika kiwanda cha Fresho. 




Sehemu ya pamba iliyoletwa na wakulima kuuzwa katika kiwanda cha Fresho. 




Sehemu ya pamba iliyoletwa na wakulima kuuzwa katika kiwanda cha Fresho. 




Sehemu ya pamba iliyoletwa na wakulima kuuzwa katika kiwanda cha Fresho. 


Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

TAASISI YA TIA KUBORESHWA KUENDANA NA MPANGO WA MIAKA MITANO

$
0
0

Mhadhiri wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Bw. Burkadi Haule, akitoa ufafanuzi wa ramani ya majengo ya taasisi hiyo, katika maeneo mbalimbali nchini, kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu, wakati wa ziara ya kutathimini utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2018/19, jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu, akieleza nia ya Wizara ya Fedha na Mipango ya kutoa fedha kwa ajili ya kuboreshamiundombinu ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania-TIA, ili kwenda sambamba na lengo la Mpango wa Maendeleo wa Miaka mitano.
Mtaalam wa masuala ya Sera kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. MsabahaMsabaha, akihoji kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2018/19 na changamoto zake, wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Khatibu Kazungu (hayupo pichani), katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania- TIA- jijini Dar es Salaam.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya TIA, Bi. Luciana Hembe (kushoto) naMhadhiri wa taasisi hiyo, Bw. Burkadi Haule, wakisikiliza maagizo ya Naibu KatibuMkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu (hayupo pichani), katika Taasisi ya TIA, jijini Dar es Salaam
Baadhi ya watumishi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania- TIA- jijini Dar es Salaamwakisikiliza maelezo ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt.Khatibu Kazungu (hayupo pichani), kuhusu kufanya kazi kwa weledi na maadili kwa ajili ya maendeleo ya Taifa
Moja ya ramani ya majengo ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania- TIA, ambayo yanatakiwa kujengwa ili kuwezesha upatikanaji wa wahasibu wakutosha kulingana na mpango wa maendeleo wa miaka mitano. (Picha na Peter Haule, WFM, Dar es Salaam)

********

Na Peter Haule, WFM, Dar es Salaam

Serikali imeahidi kutoa fedha za kutosha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya
Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) ili kuongeza udahili wa wanafunzi ikiwa ni pamoja na kupatikana kwa wahasibu wa kutosha kama mpango wa Taifa wa miaka mitano ulivyoelekeza.

Hayo yamebainishwa jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipang,o Dkt. Khatibu Kazungu, wakati wa ziara yake ya kikazi katika taasisi hiyo iliyochini ya Wizara ya Fedha na Mipango kubaini changamoto za utekelezaji wa Bajeti ya taasisi hiyo kwa mwaka 2018/19.

Dkt. Kazungu alisema kuwa Taasisi ya TIA inakabiliwa na changamoto kubwa ya ufinyu wa bajeti jambo lililosababisha baadhi ya miundombinu yake kutokamilika kwa wakati na hivyo kupunguza kiwango cha udahili wa wanafunzi.

“Lengo la Mpango wa Taifa wa maendeleo wa miaka mitano ni pamoja na taifakuzalisha wahasibu wa kutosha ili kuleta chachu katika maendeleo ya uchumi na nyanja zingine za maendeleo, malengo yanayotegemewa kwa kuimarishwa kwa miundombinu ya taasisi hii”, alieleza Dkt. Kazungu

Alisema kuwa miundombinu inayoangaziwa kwa mwaka huu wa fedha ni pamoja na Mabweni ya wanafunzi, vyumba vya madarasa na ofisi za watumishi, aidha kuangalia uwezekano wa kuongeza wahadhiri kulingana na kozi zinazotolewa jambo litakalokwenda sambamba na ongezeko la wanafunzi.

Kwa upande wake Kaimu Afisa Mtendaji wa Taasisi ya TIA Bi. Luciana Hembe, alieleza kuwa, hatua ya viongozi wa juu kutembelea taasisi wanazoziongoza na kuona uhalisia wa mambo, unaongeza morali ya kiutendaji ya watumishi kwa kuwa hutatua changamoto nyingi hususani za kibajeti.

Alisema kuwa Taasisi ya TIA imejipanga kikamilifu kuhakikisha wahitimu wakewanakuwa na weledi wa kutosha katika kuhimili ushindani wa soko la ajira ndani na nje ya nchi.

WAZIRI LUGOLA APOKEA PIKIPIKI IRINGA

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola aliyekaa kwenye Pikipiki akifurahia jambo na Mbunge wa Kilolo (CCM), Venance Mwamoto mara baada ya Munge huyo kukabidhi msaada wa Pikipiki mbili ili zitumike na Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa. Katikati ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa, ACP Juma Bwire(Picha na Datus Mahendeka, Jeshi la Polisi)



Na Datus Mahendeka, Jeshi la Polisi

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Polisi, Kangi Lugola amepokea msaada wa Pikipiki amanbazo zitatumika kwa ajili ya doria ili kupunguza uhalifu Mkoa wa Iringa.

Aidha, amelitaka Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa kutotumia Pikipiki hizo kwa ajili ya kazi za kihalifu ikiwemo kusingikiza mirungi na badala yake zitumike kwa kazi iliyokusudiwa.

Lugola alitoa kauli hiyo jana, wakati akipokea msaada wa Pikipiki mbili zenye thamani ya Tsh 2.8 zilizotolewa na Mbunge wa Kilolo, Venance Mwamoto kwa ajili ya kituo cha Ikokoto Iringa.

“Tumepokea Pikipiki hizi…wazitunze ili zidumu.. zitumike kwa ajili ya kufanya doria kwenye maeneo korofi hususani maeneo ya mlima Kitonga”alisisitiza.

Hata hivyo alitoa wito kwa wananchi na wadau werevu kuendelea kulisaidia jeshi la polisi kamwe wasichoke kutoa misaada kwa Jeshi la polisi.

TaSUBa YATOA MAFUNZO YA MUZIKI KWA WAUMINI WA KANISA LA WA ADVENTIST WA SABATO

$
0
0
Askofu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato Kanda ya Mashariki Kati mwa Tanzania(E.C.T) Mchungaji Joseph Phidelis Mngwabi akitoa neno kwa wahitimu wa kozi fupi yamuziki kutoka Kanisa la Waadventista wa Sabato iliyofanyika katika Chuo cha Sanaa naUtamaduni Bagamoyo (TaSUBa).
Wahitimu pamoja na wageni mbalimbali wakimsikiliza Askofu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato Kanda ya Mashariki ya Kati mwa Tanzania (E.C.T) Mchungaji Joseph Phidelis Mngwabi (hayupo pichani) wakati wa hafla ya wahitimu wa kozi fupi ya muziki kwa waumini wa Kanisa la Waadventista wa Sabato.
Wahitimu wa mwaka wa tatu walikabidhiwa vyeti viwili, kimoja cha TaSUBa na kingine cha Kanisa lakini mwaka wa kwanza na wa pili walikabidhiwa cheti kimoja cha kitaaluma ambacho ni cha TaSUBa.
Kwaya ya wahitimu wa kozi fupi ya muziki ikitoa burudani kwa wageni mbalimbali
waliohudhuria mahafali hayo.

***********

Kanisa la Sabato limetoa pongezi kwa Umoja wa kanisa hilo kuanzisha mfumo wawaumini wa makanisa kujifunza muziki katika Taasisi ya Sanaa na UtamaduniBagamoyo (TaSUBa) na kutoa wito wa kujitokeza kwa waumini kupata elimu ya muziki kwa ajili ya kumuimbia na kumtukuza Mungu.

Akizungumza katika mahafali hayo na kukabidhi vyeti kwa wahitimu wa kozi fupi ya muziki, Mwenyekiti wa Konferensi ya Kusini mwa Tanzania (SEC), Mchungaji Steven Ngusa, ambae alimwakilisha Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato Jimbo Kuu la Kusini mwa Tanzania (Southern Tanzania Union) Askofu Marwa Marekana, alisema wengi wanaliangalia suala hilo katika kwaya za Makanisa badala ya kwenda mbali zaidi katika muziki kwani nyakati zilizopita waimbaji wa nyimbo za kumtukuza Mungu walikuwa wakiimba bila kutambua taratibu kutoka kwa wataalam.

Mchungaji Ngusa aliwashukuru TaSUBa kwa kukubali kutoa mafunzo kwa waumini wa Kanisa bila kujali wakati wa likizo.

Alisema mafunzo hayo yalishirikisha majimbo karibu yote ya Kanisa la Sabato namadhehebu mengine ya kanisa na kueleza kwamba wahitimu hao wamepata elimu hiyo na wasidhani kama wameshajua bali wameanza kujua na kuwataka kuendeleza zaidi muziki huo kwa kumuimbia Mungu.

“Mafunzo yaliyopatikana yawe chachu na ya matengenezo kwa waumini wengineambao hawana elimu ya muziki, pia napendekeza tuanzishe mfumo kwa kutoa waumini wawili kila sehemu ili tutekeleze matakwa,” alisema Mchungaji Ngusa.

Naye Mkufunzi wa muziki TaSUBa, Heri Kaare alisema Taasisi (TaSUBa) na Jimbo Kuu la Kusini mwa Tanzania wameingia ubia ili kufundisha muziki (taaluma) kwa washiriki wa Kanisa hilo. hiyo imeingia ubia na Jimbo Kuu la Kusini Tanzania katika mahafali ya kwanza kwa wahitimu wa mwaka wa kwanza, wa pili na watatu.

Kaare alisema baada ya mafunzo hayo, wapo ambao walikuwa hawajui na wengine walikuwa na uelewa hafifu lakini baada ya kukamilisha mafunzo hayo sasa wana utaalamu wa muziki wa kuimba na kwa kutumia vifaa.

Mahafali haya ni ya kwanza ambapo jumla ya wahitimu walikua 15 baada ya
kuhudhuria mafunzo kwa miezi mitatu. Wahitimu hawa walipewa vyeti viwili, ambavyo ni cheti cha TaSUBa na cheti cha Kanisa. Aidha wahitimu wengine waliohitimu kwa mara ya pili na ya kwanza walikua 12.

MAKAMU WA RAIS SAMIA AKUTANA NA BALOZI WA RWANDA NCHINI

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Tanzania inajivunia kufanya kazi kwa karibu na Nchi ya Rwanda kutokana na ukarimu mkubwa uliojengeka kwa muda sasa kwa Wananchi wa Nchi mbili hizo.

Makamu wa Rais amesema hayo leo alipokutana na Balozi wa Rwanda Nchini Tanzania Mhe.Eugene Kayihura wakati Balozi Kayihura alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Jijini Dar es salaam leo kwa ajili ya kumuaga Makamu wa Rais Baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa Nchini.

Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amemuhakikishia Balozi Kayihura kwamba Tanzania itaendelea kudumisha Uhusiano wa Nchi mbili hizi uliodumu kwa muda mrefu sasa katika Nyanja mbalimbali za kimaendeleo na kijamii hasa katika kuangalia fursa za kiuchumi pamoja na kuwa na uhusiano mzuri wa huduma ya Fedha kati ya Rwanda na Tanzania.

Mhe. Samia amesema muda umefika sasa kushirikiana pamoja kwa ajili ya kujenga Uchumi wa Mataifa haya, ambapo pia amempongeza Balozi Eugene Kayihura kwa Ushirikiano Mkubwa alioutoa kwa Serikali ya Tanzania katika kipindi chake chote cha kazi hapa Nchini na kumtakia kila la Heri kokote aendako katika kituo chake kipya cha kazi.

Nae Nalozi Eugene Kayihura amemuhakikishia Makamu wa Rais kwamba, Rwanda itaendelea kukuza na kudumisha Ushirikiano na Tanzania katika pande zote za kimaendeleo na kuitakia Serikali ya Tanzania maandalizi mema ya mkutano wa SADC.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Balozi wa Rwanda Nchini Tanzania Mhe. Eugene Kayihura, wakati Balozi huyo alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Jijini Dar Es Salaam leo Agost 09,2019 kwa ajili ya kuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa Nchini. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Balozi wa Rwanda Nchini Tanzania Mhe. Eugene Kayihura, wakati Balozi huyo alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Jijini Dar Es Salaam leo Agost 09,2019 kwa ajili ya kuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi hapa Nchini.

Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images