Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

Mahakama ya Afrika kuhamasisha wadau Comoros na Zimbabwe

$
0
0
Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu(AfCHPR) inaendeleza juhudi zake za kuitangaza kwa nchi wanachama wa umoja wa Afrika(AU) pamoja na wadau mbalimbali ili kutimiza kikamilifu dhima ya Mahakama hiyo.

Dhima muhimu ya Mahakama hiyo yenye makao yake makuu jijini Arusha ni kuimarisha jukumu la kulinda Haki za Binadamu na Watu kwa kuongeza usimamizi imara wa mfumo wa Haki za Binadamu barani Afrika.

Katika kufanikisha juhudi hizo,AfCHPR imekua ikifanya ziara katika nchi mbalimbali wanachama wa AU kutoa elimu ya uwepo kwa Mahakama,jukumu lake,dhima yake na pia uendeshaji wa shughuli za Mahakama hiyo.

Hivi sasa ujumbe wa AfCHPR upo visiwa vya Comoro ambapo pia utaitembelea Zimbabwe ili kuitambulisha Mahakama hiyo na kuzihimiza Nchi hizo pamoja na Wananchi wake kuitumia kikamilifu kupeleka mashauri yaliyotimiza vigezo vinavyohitajika shauri kupokelewa katika Mahakama hiyo.

Ukiwa katika Nchi hizo,Ujumbe huo ambao unaongozwa na Rais wa Mahakama hiyo,Mheshimiwa Jaji Sylvain Ore’ utakutana na marais wa Comoro na Zimbabwe pamoja na viongozi wengine waandamizi wakiwemo Maspika wa Mabunge ya Nchi husika,Mawaziri wa mambo ya kigeni na wale wa Sheria,Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) na pia vyama vya wanasheria vya nchi hizo.

“Tunazitembelea nchi mbalimbali za AU ili kuzitolea wito na kuzihimiza zitoe tamko kwa mujibu wa kifungu cha 34(6) kuruhusu watu binafsi na NGOs kupeleka kesi moja kwa moja Mahakamani hapo na hivyo kuimarisha mfumo wa Haki za Binadamu barani Afrika alisema Jaji Ore’.”

Tayari Comoro ilikwisharidhia itifaki ya mkataba wa kuanzishwa kwa AfCHPR tangu mwaka 2013 lakini bado haijatoa tamko la kukubali kuruhusu watu binafsi na NGOs kupeleka kesi moja kwa moja katika Mahakama hiyo ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu.

Kwa upande wake Zimbabwe haijaridhia itifaki ya Mkataba wa kuanzishwa AfCHPR wala kutoa tamko kwa mujibu wa kifungu cha 34(6).

Tangu kukubaliwa kwa itifaki ya kuanzisha Mahakama hiyo mwaka 1998,ni Nchi 30 tu kati ya Nchi 55 za AU ndizo zilizoridhia itifaki na kati ya hizo ni Nchi tisa tu ikiwemo Tanzania ndio zimekwisha toa tamko la kuridhia watu binafsi na NGOs kupeleka mashauri yao yaliyokidhi vigezo katika Mahakama hiyo.

Hadi mwezi July 2019,Mahakama hiyo ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu yenye Majaji 11 kutoka kanda mbalimbali za Afrika imekwisha pokea mashauri 220 kati yake mashauri 62 yamekwisha shughulikiwa.

BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 06.08.2019

TANGA UWASA YAUNGA MKONO JUHUDI ZA WAZIRI UMMY WAMKABIDHI SARUJI NA MADAWATI KWA SHULE ZA MSINGI TATU JIJINI TANGA

$
0
0
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu katika akikata utepe kuashiria kupokea Msaada wa madawati 20 kwa shule ya Msingi Kiruku na madawati 20 kwa shule za msingi Kibafuta na saruji mifuko 40 kwa shule ya Msingi Pande ambavyo vinathamani ya milioni 2.4 uliotolewa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) kushoto ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa Mazingira Jijini (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly kulia ni Afisa Elimu Msingi Jiji la Tanga Ramadhani Shemahonge
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga(CCM) Ummy Mwalimu katikati akikata utepe kuashiria kupokea Msaada wa madawati 20 kwa shule ya Msingi Kiruku na madawati 20 kwa shule za msingi Kibafuta na saruji mifuko 40 kwa shule ya Msingi Pande ambavyo vinathamani ya milioni 2.4 kushoto ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa Mazingira Jijini (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga(CCM) Ummy Mwalimu kulia akimkabidhi madawati madawati 20 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kiruku Mwasi Kerenge kulia ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Mhandisi Geofrey Hilly
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga(CCM) Ummy Mwalimu kulia akimkabidhi madawati hayo pia Katibu wa Siasa na Uenezi wa wilaya ya Tanga Lupakisyo Kapange kushoto mara baada ya kuyapokea kulia ni Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga(CCM) Ummy Mwalimu katikati akiwa na Mkurugenzi wa Tanga Uwasa kushoto Mhandisi Geofrey Hilly kulia ni Afisa Afisa Elimu Msingi Jiji la Tanga Ramadhani Shemahonge
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga(CCM) Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa halfa hiyo kushoto ni Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly kulia ni Afisa Elimu Msingi Jiji la Tanga Ramadhani Shemahonge
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa Mazingira Jijini (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly akizungumza wakati wa halfa hiyo kulia ni WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga(CCM) Ummy Mwalimu kushoto ni Katibu wa Siasa na Uenezi wa wilaya ya Tanga Lupakisyo Kapange
Afisa Elimu Msingi Jiji la Tanga Ramadhani Shemahonge akizungumza wakati wa halfa hiyo
Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Kiruku Mwasi Kerenge akizungumza wakati wa halfa hiyo
Afisa Habari Msaidizi wa Tanga Uwasa Anna Makange akizungumza

Katibu wa Siasa na Uenezi wa wilaya ya Tanga Lupakisyo Kapange akizungumza wakati wa halfa hiyo kulia ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa Mazingira Jijini (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly



Sehemu ya wananchi ambao wamehudhuria kwenye halfa hiyo


WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga(CCM) Ummy Mwalimu akisalimiana na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa Mazingira Jijini (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly mara baada ya kuwasili


Sehemu ya madawati yaliyokabidhiwa


Sehemu ya wanafunzi kwenye shule hiyo










MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) leo wamekabidhi msaada wa samani na vifaa vya ujenzi kwa shule za msingi Kiruku ,Kibafuta na Pande zilizopo kata za Mabokweni na Kiomono kwenye Halmashauri ya Jiji la Tanga. 




Msaada huo ni madawati 20 kwa shule ya Msingi Kiruku na madawati 20 kwa shule za msingi Kibafuta na saruji mifuko 40 kwa shule ya Msingi Pande ambavyo vinathamani ya milioni 2.4 ikiwa ni juhudi za Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tanga (CCM) Ummy Mwalimu. 




Juhudi hizo zinatokana na shule hizo kukabiliwa na upungufu huo hali iliyomlazimu Waziri Ummy kupeleka maombi yake kwenye uongozi wa Tanga Uwasa ambao waliridhia kumsaidia na kuweza kufanikisha vitu hivyo. 




Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo Waziri Ummy aliioshukuru Tanga Uwasa kwa msaada huo ambao utasaidia kuondosha changamoto zilizopo kwenye shule hizo ili kutoa fursa wanafunzi kusoma bila kuwepo kwa vikwazo vya namna yoyote. 




“Niwashukuru sana Tanga Uwasa kwa msaada huu ambao mmetupatia niwaambie kwamba nyie ni taasisi ya serikali inayofanya vizuri zaidi Tanzania kuliko yoyote hivyo tutaendelea kushirikiana “Alisema. 




Aidha pia Waziri huyo alizungumzia afya ya msingi mkubwa wa afya ni lishe huku akieleza kwamba kuna tatizo kubwa la udumavu kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano.





Alisema kwamba tatizo hilo ni kubwa sana nchini ambapo kila watoto 100 watoto 31 wana udumavu maana yake wana utapiamlo uliopitiliza moja ya kupambana nao ni kuhakikisha watoto wanapata lishe bora. 





“labda nihaidi kwamba akupitia Taasisi yangu ya Tawode shamba la ekari tatu lililopo hapa shuleni tutalilima na kupanda viazi lishe wanafunzi waweze kupata chakula wakati wa masomo yao”Alisema 




“Kwa hiyo mwalimu mkuu tukutane atakumtanisha na mtendaji wao wa tawode wapande viazi lishe anaiteba kwa sababu hauwezi kubeba kujenga Tanzania ya viwanda kama watoto milioni 3 kati ya watoto milioni 9 wenye umri chini ya miaka mitano Tanzania wana udumavu “Alisema 




“Kwa sababu ni asilimia 31 ni watoto milioni 3 walimu watafundisha lakini watoto watakuwa wamedumaa na watakuwa hawaelewi hivyo nitakwenda kuhakikisha anakuja mratibu wetu hapa kuweza kushirikiana nanyi. 




Awali akizungumza wakati mara baada ya makabidhiano hayo Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa Mazingira Jijini (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly alisema kwamba mchango huo ni muendelezo wa mpango wa mamlaka hiyo kuchangia sekta ya elimu kwa kuangalia maeneo yenye mahitaji. 





“Tulifahamu Kiruku na shule hizo nyengine walikuwa wana mahitaji hayo ndio maana wameamua kuchangia tunamshukuru Waziri Ummy na mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa alipeleka ombi hilo mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa Tanga Uwasa na wao wakaamua kuunga mkono juhudi hizo mkono juhudi zikiwemo za Serikali inayoongozwa na Rais Dkt John Magufuli ya kutoa elimu bure. 




Aidha alisema kwamba wanategemea vifaa hivyo vitatumika kwa uangalifu mzuri na kwa malengo yaliyokusuiwa na darasa liweze kukamilika huku akishukuru ushirikiano mkubwa ambao wamekuwa wakiupata ikiwemo kuhamasisha wanafunzi wa shule hizo kusoma kwa bidii ili kuwa wataalamu ya maji na mazingira katika maisha yao na huku mbele watapata wataalamu wengi. 




Naye kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Kiruku Mwasi Kerenge alishukuru kwa msaada huo huku akieleza kwamba shule hiyo ilikuwa na changamoto wanahitaji madarasa mawili kutokana na kwamba yaliyopo ni chakavu na yana mashimo na mengine hayana sakafu. 




Alisema pia shule hiyo ina kabiliwa na changamoto ya kutokuwa na maji ya kisima wala bomba wala tenki lolote hivyo wanaomba wasaidiwe japo kuchimbwa kisima huku ekieleza kwamba pia ofisi ya walimu hawana viti ni chakavu na masheflu ya kuhifadhia vifaa vya shule hayapo kwenye ubora unaotakiwa. 




“Mh Waziri mahitaji ya madawati awali tulikuwa tunahitaji madawati 20 yaliyokuwepo madawati 127 pungufu ni 20 baada ya kupokea madawati hayo hatutakuwa na mapungufu tena hivyo kunakushukuru sana kwa msaada huu mkubwa tunakuomba mungu akuzidishie”Alisema 




Hata hivyo kwa wake Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Khalifa Shemahonge ambaye pia ni Afisa elimu Msingi Jiji la Tanga alisema wao wana Tanga wanapomuona mahali popote Tanzania Waziri Ummy wanajisikia farahi kutokana na kwamba kuna vitu ametafsiri kwa vitendo maelekezo ya Rais Dkt John Magufuli kwa kuongeza pale serikali imeishia yeye binafsi kwa nafasi yake 




“Nakumbuka uliniita na kuniambia niandike andiko la shule zenye upungufu nikaombe fedha nikafanya hivyo na andiko hilo lilileta tija kubwa ya uyjenzi wa madarasa nikushukuru sana Waziri Ummy kwani umekuwa msaada mkubwa sana kwetu “Alisema 





Hata hivyo kwa upande wake Katibu Siasa na Uenezi wa wilaya ya Tanga Lupakisyo Kapange alisema kwamba wanasimama kwa kumshuru Mungu lakini kwa juhudi unazofanya kwenye Jiji la Tanga kusaidia sekta ya elimu umekuwa mtu mzuri kwa sababu unakumbuka kwenu,kwa sisi Tanga ww ni mama yetu kwa kila kitu,nakumbuka tulikuwa na tatizo la ongezeko la ufaulu ulisimama kidete na kujengwa vyumba vitano vya madarasa.

WAFANYABIASHARA WEKEZENI KWENYE VIWANDA VYA MAFUTA YA KULA NA SUKARI-MHE HASUNGA

$
0
0
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Kushoto) akiwa na Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya nne Mhe Mizengo Pinda (Katikati) wakati wa ukaguzi wa mabanda ya maonesho ya wakulima (Nanenane) kwenye hafla ya ufunguzi wa kongamano la fursa za Kilimo biashara katika viwanja vya Nyakabindi katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu. Mwingine pichani ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu Ndg Jumanne Sagini. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akizungumza kwenye hafla ya ufunguzi wa kongamano la fursa za Kilimo biashara kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Waziri Mkuu mstaafu wa serikali ya awamu ya nne Mhe Mizengo Pinda katika viwanja vya Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi kwenye maonesho ya wakulima (Nanenane) yanayofanyika kitaifa mkoani Simiyu. 

Sehemu ya wananchi waliojitokeza kwenye hafla ya ufunguzi wa kongamano la fursa za Kilimo biashara wakifatilia kwa makini kongamano hilo kwa makini katika viwanja vya Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi kwenye maonesho ya wakulima (Nanenane) yanayofanyika kitaifa mkoani Simiyu. 




Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Simiyu

Wafanyabiashara nchini Tanzania na nje ya nchi wametakiwa kuwekeza katika viwanda vya uchakataji wa mazao mbalimbali yakiwemo miwa na alizeti.

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo Tarehe 6 Agosti 2019 wakati akizungumza kwenye hafla ya ufunguzi wa kongamano la fursa za Kilimo biashara katika viwanja vya Nyakabindi kwenye maonesho ya Sikukuu ya wakulima (Nanenane) katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.

Mhe Hasunga amesema kuwa endapo wakulima watawekeza katika Kilimo cha alizeti ni wazi kuwa wataimarisha upatikanaji wa mafuta ya kula yanayotokana na zao hilo hivyo kuondokana na dhana ya uagizaji wa mafuta kutoka nje ya nchi.

Alisema kuwa Tanzania inauhitaji wa mafuta ya kula kiasi cha Tani 570,000 lakini pamoja na kuwa na ardhi nzuri na yenye rutuba lakini juhudi za uzalishaji bado ni ndogo kwani kama nchi inazalisha Tani 250,000 pekee.

Alisema kuwa kiasi cha Bilioni 678 zilitumika mwaka 2018 kuagiza mafuta ya kula kutoka nje ya nchi ilihali kuna uwezo wa kuzalisha kwa wingi zao hilo na fedha ambazo zinatumika kuagiza zingeweza kutumika katika kutekeleza miradi mingine.

Kuhusu Sukari, Waziri huyo wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga amesema kuwa Tanzania ina uhitaji wa sukari kiasi cha Tani 675,000 ambapo Tani 175,000 kati ya hizo ni sukari za viwandani ilihali kiasi kilichosalia ni sukari ya kawaida, lakini uwezo wa nchi ni kuzalisha Tani 359,000 pekee.

Alisema kuwa ni jambo la ajabu kuagiza sukari nje ya nchi kwa kutumia gharama kubwa ilihali kuna maeneo mazuri kwa ajili ya kilimo na kuzalisha miwa.Aidha, amewasihi wakulima kuzalisha miwa kwa wingi kwani ni miongoni mwa mazao yanayohitajika zaidi katika biashara sambamba na kufanya mabadiliko katika sekta ya Kilimo kupitia mkazo wa Programu ya kuendeleza sekta ya Kilimo awamu ya pili (ASDP II).

Kongamano hilo la fursa za Kilimo biashara katika viwanja vya Nyakabindi kwenye maonesho ya Sikukuu ya wakulima (Nanenane) katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu limefunguliwa na Waziri Mkuu mstaafu wa serikali ya awamu ya nne ambaye ni mjumbe wa kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa Mhe Mizengo Peter Pinda.

WAFUGAJI WAANGUA KILIO MBELE YA WAZIRI MPINA BAADA YA KUCHOMEWA NYUMBA NA MAZIZI, WAMLILIA RAIS MAGUFULI KUWASAIDIA CHAKULA NA MAHALI PA KUISHI

$
0
0
 Mfugaji wa Kijiji cha Vilima Vitatu Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara, Dorcas Buyase akilia kwa uchungu mbele ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina (hayuko pichani) aliyefika kijijini hapo kusaka suluhu ya mgogoro huo baada ya wafugaji hao kuchomewa moto nyumba zao na kukosa mahali pa kuishi.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Vilima Vitatu walioondolewa na kuchomewa nyumba, mazizi na makambi ya uvuvi na kukosa mahali pa kuishi. Kulia ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Vilima Vitatu, Mhe. Belela Erasto na Mbunge wa Babati Vijijini, Mhe. Jituson
 Mfugaji wa Kijiji cha Vilima Vitatu Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara, Nanu Mandaga akizungumza kwa majonzi mbele ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina (hayuko pichani) aliyefika kijijini hapo kusaka suluhu ya mgogoro huo baada ya wafugaji hao kuchomewa moto nyumba zao na kukosa mahali pa kuishi
 Wafugaji wa Kijiji cha Vilima Vitatu Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara wakimsilikiza Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina (hayuko pichani) aliyefika kijijini hapo kusaka suluhu ya mgogoro huo baada ya wafugaji hao kuchomewa moto nyumba zao na kukosa mahali pa kuishi
Wafugaji wa Kijiji cha Vilima Vitatu Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara wakiwa juu ya miti wakimsilikiza Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina (hayuko pichani) aliyefika kijijini hapo kusaka suluhu ya mgogoro huo baada ya wafugaji hao kuchomewa moto nyumba zao na kukosa mahali pa kuishi.
Na Mwandishi Wetu, Babati
WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amesitisha operesheni ya kuwaondoa na kuwachomea nyumba, mazizi ya mifugo, makambi ya uvuvi Wananchi wa Kijiji cha Vilima vitatu Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara na kuunda timu ya wataalamu kutoka Wizara 8 kufuatilia utekelezaji wa operesheni hiyo na kuwasilisha ripoti hiyo serikalini kwa maamuzi zaidi.
Operesheni hiyo iliyofanyika mwezi Julai mwaka huu  imesababisha wananchi  wengi kukosa mahali pa kuishi  kutokana na nyumba zao kuchomwa moto ambapo sasa wanaishi chini ya miti hali iliyosababisha adha kubwa kwa wanawake wajawazito, watoto na wagonjwa.
Pia mifugo yao kuvamiwa na wanyama wakali na mingine kupotea baada ya mazizi kuchomwa moto, shughuli za uvuvi kusimama baada ya makambi na zana za uvuvi kuteketezwa kwa moto hali ambayo imeleta taharuki kubwa kwa wananchi na kushindwa kujua la kufanya.
Wakizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika  Kijiji cha Vilimavitatu na kuhudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Babati, Elizabeth Kitundu huku idadi kubwa ya wananchi wakiangua vilio mbele ya Waziri Mpina wakionesha masikitiko yao kuhusiana na unyama waliofanyiwa na Serikali ya wilaya hiyo na kumuomba kuwasaidia ili waweze kurudi katika maisha yao ya awali.
Walisema mbali na madhara hayo pia akiba ya chakula walichokuwa nacho majumbani mwao nacho kimechomwa moto hivyo kukosa kabisa chakula na kumuomba afikishe kilio hicho kwa Rais Dk. John Pombe Magufuli ili wapatiwe msaada wa haraka chakula ili kunusuru wasife kwa njaa katika kipindi hiki kigumu wanachopitia.
Waziri Mpina alihoji iweje operesheni hiyo ifanyike huku kukiwa na katazo la Rais Dk. John Pombe Magufuli la Januari 15 mwaka huu la kusitisha operesheni zote za kuwaondoa wananchi wanaoishi kwenye maeneo yanayodaiwa kuwa ni hifadhi hadi hapo itakapoamuliwa vinginevyo.
Waziri Mpina pia ahoji iweje operesheni hiyo ifanyike kwenye eneo hilo huku kukiwa na Hukumu ya Mahakama iliyoliondoa eneo la Kijiji  cha Vilima Vitatu kwenye Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyapori Burunge (Juhibu) ambapo hukumu hiyo haikukatiwa rufaa wala kutenguliwa na Mahakama.
Pia Waziri Mpina alihoji iweje operesheni hiyo ya kuondoa mifugo  ifanyike bila kushirikisha Wizara ya Mifugo na Uvuvi kama Sheria, Kanuni na miongozo inavyoelekeza hali iliyosababisha mifugo mingi kuteseka kwa kukosa huduma muhimu zikiwemo chanjo, dawa, maji na malisho na kusababisha mifugo kupotea na mingine kufa na kusababisha hasara kubwa kwa wafugaji taifa.
Kwa msingi huo, Waziri Mpina alisema operesheni imefanyika kinyume cha Sheria ya Magonjwa ya Wanyama Namba 17 ya mwaka 2003, Sheria ya Ustawi wa Wanyama Namba 19 ya mwaka 2008, Sheria ya Nyanda za Malisho na Rasilimali za chakula cha Mifugo namba 13 ya mwaka 2010 na Sheria ya Uvuvi Namba 22 ya mwaka 2003.
Hivyo alisema wote waliohusika kufanya operesheni hiyo walipaswa kukamatwa na kushtakiwa kutokana na makosa ya kuvunja sheria hizo za mifugo kwani wanalo jukumu la kuzisimamia ili zisivunjwe kwakuwa  mifugo ni rasilimali muhimu kwa Taifa kama zilivyo rasilimali nyingine nchini.
Waziri Mpina alieleza kasoro nyingine za operesheni hiyo kuwa pamoja na  kutokufanya tathmini ya kina ya idadi ya wananchi, kaya, mifugo na mali zingine kabla ya operesheni kufanyika, kukosekana kwa nyaraka muhimu za kuendesha operesheni na mahusiano dhaifu baina ya wafugaji, JUHIBU na Mwekezaji Kampuni ya Chemchem Lorge ya nchini Ufaransa.
Pia Waziri Mpina alisema kasoro nyingine ni kutokamilika kwa mpango wa matumizi bora ya ardhi kwani kama ungekamilika ungekuwa ndio muarobaini wa migogoro katika Kijiji cha Vilima Vitatu na vijiji vingine 9 vinavyounda Hifadhi ya Wanyamapori Burunge.
Pia Waziri Mpina aliwaonya viongozi wa Chama cha Wafugaji Tanzania kutojihusisha na vitendo kuhamasisha uvunjifu wa sheria za nchi na kama kuna masuala muhimu yanayowahusu wafugaji wafuate njia  sahihi za kukutana na mamlaka husika  kutafuta suluhu, Pia amewataka wafugaji kote nchini kufuata Sheria.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Babati Vijijini, Filbert  Mdachi alisema CCM imesikia malalamiko ya wananchi wa kuwahakikishia kuwa haki itatendeka na kumshukuru Waziri Mpina kwa kufika eneo hilo ili kutafuta suluhu ya mgogoro huo ulisababisha adha kubwa kwa wananchi.
Mkuu wa Wilaya ya Babati, Kitundu alisema alisema operesheni hiyo ilifanyika baada ya kudaiwa kuwepo viashiria vya uvunjifu wa amani katika maeneo hayo na kukiri kupokea maelekezo kutoka mkoani .

UPATIKANAJI WA VIFARANGA VYA SAMAKI NA CHAKULA BORA WAWEKEWA MIKAKATI

$
0
0

Na. Edward Kondela

Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeweka mikakati ya upatikanaji wa vifaranga vingi vya samaki pamoja na chakula bora cha samaki sambamba na kuendelea kutoa elimu ya ufugaji ili wananchi waweze kufuga samaki kwa tija.

Akizungumza kwenye maonesho ya wakulima, wafugaji na wavuvi (Nanenane) kitaifa, katika viwanja vya Nyakabindi vilivyopo Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah amesema serikali imelazimika kuweka mikakati hiyo kutokana na wananchi wengi kuwa na mwamko wa kufuga samaki kibiashara licha ya kuwepo kwa changamoto ya upatikanaji wa vifaranga bora na chakula kwa bei nafuu.

“Kwa mfano mwaka jana uhitaji wa mbegu za samaki ulikuwa unafikia takriban samaki Milioni 40 lakini sisi tumeweza kuzalisha kama Milioni 18 kwa hiyo kuna mikakati ipo kuhakikisha vituo vya serikali pamoja na kuhamasisha vile vya watu binafsi kuzalisha vifaranga bora, changamoto nyingine ni chakula ambapo wapo wanaotengeneza hapa nchini lakini vinakuwa havijafikia ubora unaotakiwa na wengine wanaagiza kutoka nje ya nchi ambapo ni bei ghali, hivyo tunaweka mikakati ya uwepo wa chakula bora na bei nafuu pamoja kutoa elimu ya utengenezaji wa chakula hicho.” Amesema Dkt. Tamatamah

Amefafanua kuwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Maonesho ya Nanenane mwaka huu, sekta ya uvuvi imejikita zaidi katika kutoa elimu ya ufugaji bora wa samaki ili kuwavutia wananchi kuwekeza katika ufugaji samaki kibiashara.

Kuhusu ulaji wa samaki nchini Dkt. Tamatamah amesema kulingana na tafiti kutoka Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) kwa sasa kila mtanzania anakula walau Kilogramu 8.2 za samaki kwa mwaka ilhali FAO inapendekeza mtu mmoja kula samaki kilogramu 20.3 kwa mwaka, hivyo serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imekuwa ikiweka pia mikakati ya uwepo wa ongezeko la uzalishaji wa samaki hapa nchini lakini pia kuhakikisha samaki wachache wanaozalishwa wanamfikia mlaji wakiwa katika hali nzuri.

Katibu mkuu huyo anayeshughulika na sekta ya uvuvi amebainisha pia kupitia Maonesho ya 27 ya Nanenane kwa Mwaka 2019 Wizara ya Mifugo na Uvuvi imejikita zaidi katika utoaji wa elimu kwa wadau katika sekta za mifugo na uvuvi ili kutatua changamoto mbali zinazowakabili na kuweza kufuga kwa tija.

NAIBU WAZIRI KANYASU AMALIZA MGOGORO WA ARDHI KATI YA PORI LA AKIBA LA SELOUS NA KIJIJI ULIODUMU KWA MIAKA 12 MKOANI LINDI

$
0
0
Baadhi ya wananchi wakiwa wanatoka eneo lenye mgogoro ambapo walitaka eneo hilo la mto waweze kilitumia kwa ajili ya kulishia mifugo pamoja na kulima katika mto huo ambapo kutokana na hali hiyo mto huo usingeweza kudumu kwa muda mrefu
Meneja wa Pori la Akiba la Selous, Henock Msocha ( kulia) akizungumza na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu wakati walipotembelea eneo amvalo lilikuwa na mgogoro kati ya Kijiji cha Kikulyungu na Pori la Akiba la Selous
Aniel Heliem mmoia wa wananchi akimuuliza swali Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Cinstantine Kanyasu mata baada ya kuutangaza kuwa eneo la Kihurumila si sehemu ya Pori la Akiba la Selous na wala sio eneo la Kijiji cha Kikulyungu.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu akionesha eneo la Pori Tengefu akiwa kwenye kigingi ambacho ni mpaka kati ya eneo la Kihurumira ambalo lilikuwa ni eneo la mgogoro kati ya wananchi wa kijiji cha Kikulyungu na Pori la Akiba la Selous ambalo limekuja kubainika kuwa eneo hilo sio ardhi ya Kijiji hicho na wala sio sehemu ya Pori la akiba la Selous bali ni ardhi ya Pori Tengefu amabalo lilikuwa imetengwa kwa ajili ya kuzaliana kwa wanyamapori wanaotoka katika Pori la Selous katika wilaya Liwale mkoani Lindi. Wa kwanza kulia ni Mbunge wa Jimbo la Liwale, Zuberi Kuchauka
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu akiwa na Mbunge wa Jimbo la Liwale, Zuberi Kuchauka wakiwa kwenye eneo la kigingi huku Mbunge huyo akiomuonesha Naibu Waziri Kanyasu eneo la Kihurumira ambalo lilikuwa ni eneo la mgogoro kati ya wananchi wa kijiji cha Kikulyungu na Pori la Akiba la Selous ambalo limekuja kubainika kuwa eneo hilo sio ardhi ya Kijiji hicho na wala sio sehemu ya Pori la akiba la Selous bali ni ardhi ya Pori Tengefu amabalo lilikuwa imetengwa kwa ajili ya kuzaliana kwa wanyamapori wanaotoka katika Pori la Selous katika wilaya Liwale mkoani Lindi. Wa kwanza kulia ni Mbunge wa Jimbo la Liwale, Zuberi Kuchauka
Baadhi ya wananchi wakiwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu wakiangalia eneo la Kihurumila sehemu ambayo kuna mto na ambalo lilikuwa na mgogoro kuwa sio mali ya pande zote mbili bali mali ya serikali kuu inayomilikiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii,
Mbunge wa Liwale, Mhe.Zuberi Kuchauka akizungumza na wananchi wake kuhusu kumalizika kwa mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka 12 baada ya Naibu Waziri Kanyasu kuzungumza na wananchi hao
…………………..
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu ametatua mgogoro uliodumu kwa miaka 12 baina ya Pori la Akiba la Selous na Wananchi wa kijiji cha Kikulyungu kilichopo katika wilaya ya Liwale mkoani Lindi
Mgogoro huo wa ardhi ulianza mwaka 2007 ambapo wananchi walianza kudai kuwa eneo la Kihulumira ambalo linapakana na Pori la Akiba la Selous kuwa ni moja ya maeneo yao ya Asili.

Kufuatia hali ilipelekea uhasama mara kwa mara kati ya wananchi na askari wanyamapori hasa pale wananchi walipokuwa wakikamatwa kwa madai kuwa wameingia ndani ya Hifadhi bila kibali.

Akizungumza na wananchi wa wa kijiji cha Kikulyungu mara baada ya kutembelea eneo lililokuwa na mgogoro, Kanyasu alisema eneo hilo lilisajiriwa mwaka 1975 na kijiji kilisajiriwa mwaka 2005 hivyo eneo hilo si sehemu ya kijiji.

Amesema baada ya kuundwa timu hiyo iliyokuwa ikiongozwa na wataalamu wa Ardhi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazo ilibainika kuwa eneo hilo si la wananchi na wala sio sehemu ya Pori la Akiba la Selous bali ni Pori Tengefu ambalo ni mali ya serikali Kuu na linasimamiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii.

Katika hatua nyingine, Kanyasu amewataka wananchi kuacha vitendo vya kukata miti ovyo na kuchoma misitu kutoka na uharibifu mkubwa wa misitu aliuona karibu na eneo lililokuwa na mgogoro baina ya pande hizo mbili.
Kufuatia hali hiyo, Mhe.Kanyasu amewaagiza viongozi wa vijiji hivyo kuweka sheria kali ili kudhibiti hali ya uharibifu wa misitu unaoendelea katika maeneo hayo.

Akizungumza kwa niaba ya wanachi wa wilaya ya Liwale Mbunge Liwale, Zuberi Kuchauka ameishukuru serikali kwa hatua iliyofikia kwani mgogoro huo ni wa muda mrefu na ulikuwa haujapatiwa ufumbuzi
Amesema mgogoro huo uliwafanya wananchi wa maeneo hayo kupunguza kasi ya kujiletea maendeleo badala yake wajanja wachache walikuwa wakitumia nafasi ya mgogoro kuendelea kujinufaisha.

” Sitegemei mgogoro mwingine wa ardhi baada ya kumalizika huu, Nawaomba wananchi sasa tuchape kazi” Alisisitiza Kuchauka.
Kutokana na kumalizika kwa mgogoro huo wananchi wa kijiji hicho wameiomba serikali kulitumia eneo hilo kuanzisha Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ili kuinua kipato katika kijiji hicho

ZOEZI LA UTAYARI KUKABILIANA NA UGONJWA WA EBOLA KATIKA WILAYA YA BUHIGWE MKOANI KIGOMA

$
0
0
Watoa huduma za afya kutoka Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma wakiwa wamembeba mgonjwa anayehisiwa kuwa na ugonjwa wa ebola tayari kumpatia huduma ya kwanza katika zoezi la utayari wa kukabiliana na ugonjwa huo usiingie nchini.
“Mahema ya kuhudumia wagonjwa wa ebola yanatakiwa kuwa na hewa safi muda wote” Dkt. Refaya Ndyamuba kutoka Shirika la Afya Duniani akifungua sehemu ya kuingiza hewa kwenye hema linalotumika kuhudumia wagonjwa wa ebola wakati wa zoezi la utayari wa kukabiliana na ugonjwa huo katika Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma. 

Mtoa huduma za afya katika Wilaya ya Buhigwe akinawa kwa maji safi yaliyochanganywa na kemikali ya “Chlorine” mara baada ya kutoka kumhudumia mgonjwa wa ebola wakati wa zoezi la tayari wa kukabiliana na ugonjwa huo.
Mwezeshaji wa zoezi la upimaji wa utayari wa kukabiliana na ugonjwa wa Ebola kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Christopher Mnzava akifafanua umuhimu wa kuzingatia muda wakati wa maandalizi ya kumhudumia mgonjwa anaehisiwa kuwa na ugonwja wa ebola kwa watoa huduma za afya Katika Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma

Watoa huduma za afya mara baada ya kumhudia mgonjwa wa ebola wakiwa wamebeba mifuko maalum kwa ajili ya utunzaji wa mavazi na vifaa vilivyovyotumika kuhumdumia mgonjwa kabla ya kuyateketeza wakati wa zoezi la kupima utayari wa kukabiliana na ugonjwa wa ebola Mkoani Kigoma.

Dkt. Refaya Ndyamuba kutoka Shirika la Afya Duniani akielekea kukagua kituo kitachokutumika kuhudumia wagonjwa wa ebola katika Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma katika zoezi la utayari wa kukabiliana na ugonjwa wa ebola usiingie nchini linaloendelea Mkoani Kigoma.

……………

Kufuatia nchi ya jirani (DRC) kuendelea kukabiliwa na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola tangu Agosti mwaka 2018. Serikali ya Tanzania imeendelea kuchukua tahadhari za ugonjwa huo kwa kupima utayari wa Watoa huduma za Afya kwa mikoa iliyomo hatarini kuathiriwa na ugonjwa huo.

Serikali kupitia uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Menejimenti ya Maafa kwa kushirikiana na Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, pamoja na wadau wa maendeleo; WHO, FAO, USAID, HRH2030, na USAID Global Health Supply Chain Programu, inaendelea na zoezi la utayari wa kukabiliana na ugonjwa huo katika Wilaya za Mkoa wa Kigoma.

Zoezi hilo linalenga kuwaimarisha watumishi hao katika maeneo maalum ikiwemo ya uratibu, utambuzi na ufuatiliaji wa wagonjwa iwapo atagundulika, matibabu ya wagonjwa, uchukuaji na usafirishaji wa sampuli na kuthibitisha maabukizi pamoja kuimarisha mifumo ya utambuzi wa masuala ya Afya kwa kila abiria wanaopita kwenye mipaka ya mkoa wa Kigoma.

MAGAZETI YA LEO JUMATANO AGOSTI 7,2019

Standard Chartered yatanua wigo wa uwekeaji wa amana kwa wateja wakubwa

$
0
0
BENKI ya Standard Chartered jana imezindua huduma mpya ya fedha kwa wateja wake wakubwa, ambao wataweka fedha hizo katika akaunti zao kwa kutumia mashine maalumu (Cash Deposit Machines services-CDMs) zitakazowekwa kwenye eneo la biashara.
Huduma hiyo ni juhudi za benki hiyo kutekeleza matakwa ya wateja wake ya kuwa karibu nao na kurahisisha uwekaji wa fedha na usalama wake.

Huduma hiyo ambayo inawezesha mteja kuwa na mtambo wa kuwekea fedha katika eneo lake la kazi (Cash Deposit Machines services-CDMs) imelenga kwa wafanyabiashara wakubwa kama wenye vituo vya mafuta, maduka makuu, na wauzaji wa vinywaji baridi.
Imeelezwa kuwa CDMs hizo zitafungwa katika maeneo ya biashara hizo na kutoa huduma za kuhifadhi fedha muda wowote ule.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi huo wa huduma za CDMs,  Mkuu wa Kitengo cha huduma za kibenki kwa Mashirika, Biashara na taasisi za kifedha, Bw.  James Meitaron, alisema: “ Benki ya Standard Chartered inazindua Cash Deposit Machines ili kuwezesha wateja wetu wakubwa kuwa na muda zaidi wa kushughulika na kazi na kuacha shaka ya upelekaji wa fedha nyingi kila mara. kwa kuwa na  CDMs wateja wetu sasa wanaweza kuhifadhi fedha katika akaunti zao muda wowote katika mtambo huo. fedha zinazowekwa zitaonesha katika kumbukumbu za kibenki.” 

Aidha alisema kwamba CDMs imeunganishwa na mifumio mingine ya kibenki ya kidigitali ikiwamo Bank’s Corporate Banking Digital platform, S2B, hivyo kumwezesha mteja kuona kinachoendelea katika akaunti yake.

Akizungumzia usalama wa mitambo hiyo, Meitaron alisema kwamba benki inawajibika mara tu fedha hizo zinapowekwa katika mitambo ya CDMs. Pia benki ndiyo itakayosafirisha fedha hizo kutoka katika eneo la mteja hadi benki. 

Mitambo hiyo itawekwa katika maeneo ya mteja yaliyo salama huku hatua zote za kiusalama zikiwa zimetekelezwa.
Pia mitambo hiyo ina uwezo wa kutambua fedha za bandia na kwamba zitakuwa zinaangaliwa na watu ambao watachaguliwa na wateja wenyewe.
“baadhi ya wateja wetu wana huduma hizi na wameomba mitambo zaidi kutokana na haja  kutunza muda na usalama wa fedha. Nashauri wateja wengi  kujaribu huduma hii watafurahi,” alisema Meitaron 

Uzinduzi wa CDMs unafanyika ikiwa ni sehemu ya harakati za benki za kufikia wateja wake pale walipo kwa kutumia njia mbalimbali. Hivi karibuni benki hiyo ilizindua Full Digital Bank on Mobile kwa ajili ya wateja wadogo binafsi na hii ya CDMs ni kwa ajili ya wateja wakubwa.
 Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bi. Juanita Mramba akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki kwa Makampuni makubwa, ya kati na taasisi za kifedha wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bw.  James Meitaron wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa huduma mpya ya fedha kwa wateja wake wakubwa ya kuweka fedha katika akaunti zao kwa kutumia mashine maalumu (Cash Deposit Machines services-CDMs) zitakazowekwa kwenye eneo la kazi uliofanyika Hoteli ya Hyatt-The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Bidhaa za makampuni makubwa na ya kati wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bw. Busara Raymond.
 Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki kwa Makampuni makubwa, ya kati na taasisi za kifedha wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bw.  James Meitaron akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu huduma mpya ya fedha kwa wateja wake wakubwa ya kuweka fedha katika akaunti zao kwa kutumia mashine maalumu (Cash Deposit Machines services-CDMs)  zitakazowekwa kwenye eneo la kazi wakati wa hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyika Hoteli ya Hyatt-The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Bidhaa wa makampuni makubwa na ya kati wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bw. Busara Raymond na kulia ni Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bi. Juanita Mramba.
 Meneja Bidhaa wa makampuni makubwa na ya kati wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bw. Busara Raymond akizungumza jambo na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa huduma mpya ya fedha kwa wateja wake wakubwa ya kuweka fedha katika akaunti zao kwa kutumia mashine maalumu (Cash Deposit Machines services-CDMs) zitakazowekwa kwenye eneo la kazi  uliofanyika Hoteli ya Hyatt-The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki kwa Makampuni makubwa, ya kati na taasisi za kifedha wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bw.  James Meitaron na kulia ni Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa benki hiyo, Bi. Juanita Mramba.
 Baadhi ya mashine maalumu za kuweka fedha (Cash Deposit Machines services-CDMs) zitakazowekwa kwenye  eneo la kazi kabla ya kuzinduliwa rasmi wakati wa hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt-The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.

 Meneja Bidhaa wa makampuni makubwa na ya kati wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bw. Busara Raymond (kulia) akitoa maelezo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) jinsi mashine maalumu ya kuweka fedha (Cash Deposit Machines services-CDMs) kwenye eneo la kazi inavyofanyakazi wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa huduma mpya ya fedha kwa wateja wake wakubwa uliofanyika Hoteli ya Hyatt-The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki kwa Makampuni makubwa, ya kati na taasisi za kifedha wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bw.  James Meitaron.
 Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki kwa Makampuni makubwa, ya kati na taasisi za kifedha wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bw.  James Meitaron akikata utepe ishara ya kuzindua rasmi mashine maalumu ya kuweka fedha (Cash Deposit Machines services-CDMs) kwenye eneo la kazi wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa huduma mpya ya fedha kwa wateja wake wakubwa uliofanyika Hoteli ya Hyatt-The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Meneja Bidhaa wa makampuni makubwa na ya kati wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bw. Busara Raymond pamoja na Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa benki hiyo, Bi. Juanita Mramba.
 Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki kwa Makampuni makubwa, ya kati na taasisi za kifedha wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bw.  James Meitaron (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kuzindua mashine maalumu za kuweka fedha (Cash Deposit Machines services-CDMs) kwenye eneo la kazi wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa huduma mpya ya fedha kwa wateja wake wakubwa uliofanyika Hoteli ya Hyatt-The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa benki hiyo, Bi. Juanita Mramba na kulia ni Meneja Bidhaa wa makampuni makubwa na ya kati wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bw. Busara Raymond.
 Mpiga picha wa gazeti la Mwananchi, Said Nanjundo akiuliza swali kwa uongozi wa Benki ya Standard Chartered wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa huduma mpya ya fedha kwa wateja wake wakubwa ya kuweka fedha katika akaunti zao kwa kutumia mashine maalumu (Cash Deposit Machines services-CDMs) zitakazowekwa kwenye eneo la kazi uliofanyika Hoteli ya Hyatt-The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki kwa Makampuni makubwa, ya kati na taasisi za kifedha wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bw.  James Meitaron katika picha na moja ya mashine maalumu ya kuweka fedha (Cash Deposit Machines services-CDMs) kwenye eneo la kazi wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa huduma mpya ya fedha kwa wateja wake wakubwa uliofanyika Hoteli ya Hyatt-The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.

UVINZA WAPIMWA UTAYARI WA KUKABILI UGONJWA WA EBOLA

$
0
0
 Mkazi wa kijiji cha Ilagala, Wilayani Uvinza, Deborah Yotham, akisoma kipeperushi chenye kueleza kuhusu ugonjwa wa Ebola, wakati wa zoezi la kupima Utayari wa kukabili Ugonjwa huo lililoendelea kufanyika mkoani Kigoma tarehe 6 Agosti, 2019.
 Daktari wa Kituo cha Afya Ilagala Wilayani Uvinza, Reuben Mwakilima, akitoa taarifa kwa njia ya simu kwa Mganga wa Mkoa wa Kigoma, juu ya mgonjwa aliyehisiwa kuwa na ugonjwa wa Ebola kufika kituoni hapo wakati wa kuigiza zoezi la kupima Utayari wa kukabili Ugonjwa huo lililoendelea kufanyika mkoani Kigoma tarehe 6 Agosti, 2019.
 Mmoja wa Watoa huduma ya Afya katika Kituo cha Afya Ilagala Wilayani Uvinza, , akijiandaa kumbemba mgonjwa aliyehisiwa kuwa na ugonjwa wa Ebola kufika kituoni hapo wakati wa kuigiza zoezi la kupima Utayari wa kukabili Ugonjwa huo lililofanyika  katika kituo hicho tarehe 6 Agosti, 2019.
 Mmoja wa Watoa huduma ya Afya katika Kituo cha Afya Ilagala Wilayani Uvinza, , akimuhudumia mgonjwa aliyehisiwa kuwa na ugonjwa wa Ebola kufika kituoni hapo wakati wa kuigiza zoezi la kupima Utayari wa kukabili Ugonjwa huo lililofanyika  katika kituo hicho tarehe 6 Agosti, 2019.
 Mwezeshaji wa zoezi la kupima Utayari wa kukabili Ugonjwa  wa Ebola mkoani Kigoma, kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faraja Msemwa akifafanua umuhimu wa vifaa Kinga, kwa watoa huduma ya Afya katika Kituo cha Afya Ilagala wakati wa kuigiza zoezi la hilo  lililofanyika  katika kituo hicho tarehe 6 Agosti, 2019.
 Mwezeshaji wa zoezi la kupima Utayari wa kukabili Ugonjwa  wa Ebola mkoani Kigoma, kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ambele Eliah akifafanua namna ya uchukuaji wa sampuli, kwa watoa huduma ya Afya katika Kituo cha Afya Ilagala, wilayani Uvinza, wakati wa zoezi hilo  lililofanyika  katika kituo hicho tarehe 6 Agosti, 2019.
Mwezeshaji wa zoezi la kupima Utayari wa kukabili Ugonjwa  wa Ebola mkoani Kigoma, kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Vida Mmbaga akifafanua umuhimu wa zoezi hilo, kwa watoa huduma ya Afya katika Kituo cha Afya Ilagala, wilayani Uvinza, wakati wa zoezi hilo  lililofanyika  katika kituo hicho tarehe 6 Agosti, 2019.

KAGERE AANZA MSIMU MPYA SIMBA KWA HAT TRICK

$
0
0

Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv
Klabu ya Simba Imefanikiwa kuanza vyema msimu wake mpya baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Power Dynamos ya Zambia katika mchezo wa kirafiki kwenye tamasha la Simba Day usiku wa leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
 Katika mchezo huo uliokusanya umati wa mashabiki waliosheheni Uwanja wa Taifa, shujaa wa Simba SC alikuwa ni mshambuliaji wake wa kimataifa wa Rwanda, Meddie Kagere aliyefunga mabao yote matatu ya timu yake.

Katika mchezo huo ulioanza majira ya saa 12 jioni ilichukua dakika tatu ya mchezo kwa Mshambuliaji wa Kimataifa Meddie Kagere kuifungia timu yake goli la kuongoza akimalizia pasi ya kiungo Mzambia, Clatous Chama.
 Dakika ya 23, Jimmy Dlingai anaisawazishia Power Dynamos kwa kichwa akimalizia kona iliyopigwa na Larry Bwalya kumtungua kipa Beno Kakolanya.

Mpaka mapumziko timu hizo zimeenda zikiwa zimefungana 1-1. Kipindi cha pili  ilifanikiwa kupata mabao mawili zaidi, yote yakifungwa na Kagere
 Kwenye  dakika ya 58 kwa kichwa akimalizia pasi ya winga mpya, Deo Kanda aliyesajiliwa kutoka TP Mazembe na dakika ya 73 akiandika bao la tatu.

Baada ya mchezo huo, Simba watasafiri kwenda Msumbiji kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, UD do Songo Jumamosi, kabla ya kurejea nyumbani kwa mchezo wa marudiano kati ya Agosti 23 na 25.
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Beno Kakolanya, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Shomary Kapombe/Said Ndemla dk85, Tairon Santos Da Silva/Kennedy Juma dk87, Pascal Wawa, Muzamil Yassin, Deo Kanda/Rashid Juma dk75, Sharaf Eldin Shaibob/Gerson Fraga ‘Viera’ dk49, Meddie Kagere, Clatous Chama na Francis Kahata/Miraj Athumani ‘Madenge’ dk61.
 Power Dynamos; Lawrence Mulenga, Larry Bwalya, Raphael Makubuli, Jimmy Dlingai, John Soico/Clifford Saudi dk75, White Mwamambaba, Benson Sakala, Kondwani Chiboni/Faustin Bakodica dk51, Christian Ntouba/Judo Bolondio dk59, Fredrick Mulamba/Jackob Phiri dk54 na Kassimu Titus/Lameck Kafwaya dk 67.

MAHAKAMA KUU KUTOA UAMUZI WA PINGAMIZI LILILOWASILISHWA NA UPANDE WA SERIKALI KUHUSU ASKOFU KAMEKA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam imesema,  Agosti 9, 2019 (Ijumaa) itatoa uamuzi juu ya pingamizi lililowasilishwa na upande wa Serikali dhidi ya maombi ya askofu Mulilege Kameka kanisa la Boko Yerusalem, ya kuwataka Mwanasheria wa Mkuu na Kamishna wa Uhamiaji wafike mahakamani hapo kujieleza kwa nini wasifungwe kwa kuipuuuza amri ya mahakama.

Uamuzi huo, unatarajiwa kutolewa na Jaji Atuganile Ngwala, baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili kuhususiana na pingamizi lililowasilishwa na wajibu maombi.

Mwezi Machi Mwaka huu,  Mahakama hiyo iliamuru askofu Kameka wa kanisa la  wa kanisa la house of prayer shield of faith christian fellowship (HPSFCFC) lililopo Book Magengeni,
aliyekuwa akishikiliwa na wizara ya mambo ndani ya nchi aachiliwe huru kutoka kizuizini anaposhikiliwa ikisema kwamba uraia wake hauna mashaka.

Licha ya kutolewa kwa amri hiyo mpaka leo askofu huyo bado ameshikiliwa na yuko mahabusu gerezani ndio maana ameleta maombi hayo.

Maombi  hayo yamefunguliwa dhidi ya wajibu maombi ambao ni Mwanasheria mkuu wa serikali (AG) na Kamishna wa Uhamiaji na yalipaswa kusikilizwa leo Agosti 6, 2019 lakini upande wa serikali umewasikisha pingamizi ya awali.

Katika pingamizi hilo, upande wa serikali ukiongozwa na wakili wa serikali Mwandamizi Jackline Nyantori wamedai kuwa, Kifungu cha sheria ambacho wapeleka maombi wamekitumia kupeleka maombi hayo hakiipi mamlaka Mahakama Kuu ya kuweza kusikiliza maombi hayo .

Akijibu hoja hiyo, wakili wa mpeleka maombi, John Mallya amedai kuwa maombi hayo yameletwa kwa mujibu na taratibu, kwani sheria inaruhusu kuleta maombi ya aina hiyo kwa njia ya hati ya maombi na kiapo kama walivyofanya wao katika kupeleka maombi.

Hata hivyo upande wa serikali umesisitiza  kwamba kwa kuwa kosa linalodaiwa kutendeka halikufanyika mbele ya mahakama  waombaji walipaswa wapeleke malalamiko hayo kwanza polisi walete madai ndipo mahakama iyasikilize na kuyatolea maamuzi.

Akizungumza nje ya mahakama baada ya kesi hiyo kuahirishwa, Wakili Mallya amesema Askofu Kameka alikamatwa na Wizara ya Mambo ya Ndani tangu Desemba,2018, ambapo amekaa kizuizini karibia miezi tisa sasa.

"Msingi wa kukamatwa kwake wanadai sio raia, lakini alikuja hapa Mahakama Kuu Machi, 2019, ikaamua kuwa Askofu Kameka ni raia na uraia wake hauna  mashaka hivyo Magereza na kitengo cha Uhamiaji kimuachie haraka lakini mpaka leo hukumu hiyo iliyotolewa na Jaji IIvin Mgeta  haijatekelezwa ndipo askofu  akaleta maombi ya kumshtaki Kamshina Mkuu wa Uhamiaji na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili waje waieleze Mahakama kwa nini wamedharau amri halali iliyotolewa na Mahakama .

" Katika maombi yetu tunataka, mahakama  iwakute na hatia ya kuidharau amri hiyo, ambapo adhabu yake ni kifungo cha mwaka mmoja jela au mahakama itakavyoona inafaa..., pia ni imani kuwa, Mahakama ni nyumba ya haki na tunatarajia kuona haki inatendeka ndio maana tumekimbilia huku tunaamini haki itatendeka,"amesema Mallya.
 Askofu wa kanisa la Boko Yerusalem, Mulilege Kameka, akirudishwa mahabusu kutoka Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Dar ea Salaam, baada ya maombi yake dhidi ya Kamishna wa Uhamiaji na Mwanasheria Mkuu  kuahirishwa.
Waumini wa kanisa hilo wakimpungia mkono askafu wao mahakamani hapo baada ya kesi yake kuahirishwa

MAAFISA WA BUNGE WATOA ELIMU KWENYE MAONESHO YA NANENANE

$
0
0
 Afisa Sheria wa Bunge Ndg. Mossy Lukuvi akitoa Elimu kwa Wagenin waliotembelea banda la Bunge hii leo kwenye Maonesho ya Wakulima ya Nanenane yanayoendelea Jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Bunge)
Afisa Utafiti  wa Bunge Ndg. Aziza Makwai akitoa Elimu kwa mgeni aliyetembelea banda la Bunge hii leo kwenye Maonesho ya Wakulima ya Nanenane yanayoendelea Jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Bunge)

WIMBO MAALUMU WA SADC ULIOIMBWA NA TANZANIA ALL STARS

$
0
0

Singers: Tanzania All-Stars

Song: SADC



Mrisho Mpoto
Christian Bella
Lameck Ditto
Madee
MimiMars
Ziid 
Peter Msechu
Jay Melody
Shilole
Jolie
Merisa
Barnaba
Magic 
Charles Baba
Mataaluma
KalalaJr
Dogo Janja
Alice Kella
Nedy Music
Fobby 
Khadija Kopa



Songwriter - Lameck Ditto
Produced by - Emma The Boy
                          Tudd Thomas
                          Major Key

SOKA LA TANZANIA LINARIDHISHA, ASEMA WAZIRI MKUU

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia mashabiki na wapenzi wa timu ya Soka ya Simba wakati alipoingia kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuwa mgeni rasmi katika Simba Day, Agosti 6, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Simba Day kwenye uwanja  Taifa jijini Dar es salaam, Agosti 6, 2019. Wa tatu kushoto ni  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, Kulia ni Mwekezaji wa Simba, Mohammed Dewji na kushoto ni  Rais wa TFF, Wallece Karia. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali inaridhishwa na maendeleo ya soka la Tanzania.

“Serikali inaridhishwa na maendeleo ya soka la Tanzania. Soka la Tanzania limeanza kukua kwa kiwango kizuri. Timu za Tanzania zinashiriki mashindano ya kimataifa na sasa hivi zinashinda. Tumeona Taifa Stars imeishinda timu ya Kenya, nayo timu ya Taifa ya wanawake imeishinda timu ya Swaziland,” amesema.

Ametoa kauli hiyo leo jioni (Jumanne, Agosti 6, 2019) wakati akizungumza na mashabiki wa timu ya Simba Sports Club mara baada ya kukagua timu hiyo na Power Dynamos ya Zambia kabla ya kuanza kwa mechi ya kirafiki kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Simba Day, amesema mafanikio yanayopatikana hivi sasa kwa ushindi wa timu za Tanzania ni matokeo ya kuwa na vilabu imara vya soka kama vile Yanga, Simba, Azam au Namungo.

“Nyote ni mashahidi kuwa Rais wetu, Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza kuwa anataka kuona Tanzania inashinda makombe ya Afrika, na hii ni fursa kwa timu ya Simba kuonesha hilo kupitia mechi hii ya leo.”

“Leo tunashuhudia mechi kati ya Simba Sports Club na Power Dynamos ya Zambia na uwanja umejaa, umefurika. Ninaiagiza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, isimamie vilabu vyote ili viwe na mifumo mizuri ya mapato,” amesema.

Amewataka Watanzania waendelee kuisapoti timu ya Taifa kila inaposhiriki mashindano ya kimataifa. “Natambua kuwa mwezi ujao, timu yetu itacheza na Burundi na Sudan. Kwa hiyo ninawasihi Watanzania kuishamgilia timu yetu kama tulivyojaa leo,” amesema.

Mapema, kabla ya mchezo huo kuanza, timu ya Simba iliamua kuwatambulisha wachezaji wake ambao imewasajili katika msimu huu pamoja na benchi lake la ufundi.

Wachezaji waliotambulishwa leo ni Rashid Juma, Ally Salim, Yusuph Mlipili, Mzamiru Yassin, Kennedy Juma, Mohammed Hussein, Jonas Mkude, Miraji Othman, Haruna Shamte, Hassan Dilunga, Shomari Kapombe, Aishi Manula na Pascal Wawa.

Wengine ni Henrique Wilker, Tairone Santos da Silva, Gerson Fraga, Beno Kakolanya, Deogracias Kanda, Clatous Chama, Gadiel Michael, Erasto Nyoni, Meddie Kagere, Sharaf Shaibob, Francis Kahata, John Bocco na Ibrahim Ajib.

Waliotambulishwa kwenye benchi la ufundi ni kocha wa timu hiyo Patrick Aussems, kocha msaidizi Dennis Katambi, Adel Zbane, Yassin Gembe, Abbas Ally, Hamisi Mtambo, Patrick Rweyemamu (Meneja) na Muharam Mohammed.

NAIBU WAZIRI KANYASU AMALIZA MGOGORO WA ARDHI KATI YA PORI LA AKIBA LA SELOUS NA KIJIJI ULIODUMU KWA MIAKA 12 MKOANI LINDI

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu ametatua mgogoro uliodumu kwa miaka 12  baina ya Pori la Akiba la Selous na Wananchi  wa kijiji cha Kikulyungu  kilichopo katika  wilaya ya  Liwale mkoani Lindi

Mgogoro  huo wa ardhi ulianza mwaka 2007 ambapo wananchi  walianza kudai kuwa eneo la Kihulumira ambalo linapakana na  Pori la Akiba la Selous kuwa  ni moja ya maeneo yao  ya Asili.

Kufuatia hali ilipelekea uhasama mara kwa mara kati ya wananchi na askari wanyamapori hasa pale wananchi walipokuwa wakikamatwa kwa madai kuwa wameingia ndani ya Hifadhi bila kibali.

Akizungumza na wananchi wa wa kijiji cha Kikulyungu mara baada ya kutembelea eneo lililokuwa na mgogoro,  Kanyasu alisema eneo hilo lilisajiriwa  mwaka 1975 na kijiji kilisajiriwa mwaka 2005 hivyo eneo hilo si sehemu ya kijiji.

Amesema baada ya kuundwa timu hiyo iliyokuwa ikiongozwa na wataalamu wa Ardhi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazo  ilibainika kuwa eneo hilo si la wananchi na  wala  sio sehemu ya   Pori la Akiba la Selous bali  ni Pori  Tengefu ambalo ni mali ya serikali Kuu na linasimamiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii.

Katika hatua nyingine, Kanyasu amewataka wananchi   kuacha  vitendo vya kukata miti ovyo na kuchoma misitu kutoka na uharibifu mkubwa wa misitu aliuona karibu na eneo lililokuwa na mgogoro baina ya pande hizo mbili.

 Kufuatia hali hiyo, Mhe.Kanyasu  amewaagiza viongozi wa vijiji hivyo  kuweka sheria kali ili kudhibiti  hali  ya uharibifu  wa misitu unaoendelea katika maeneo hayo.

Akizungumza  kwa niaba ya wanachi wa wilaya ya Liwale Mbunge Liwale,  Zuberi Kuchauka  ameishukuru serikali kwa hatua iliyofikia kwani mgogoro huo ni wa muda mrefu na ulikuwa haujapatiwa ufumbuzi

Amesema mgogoro huo uliwafanya wananchi wa maeneo hayo kupunguza kasi ya kujiletea maendeleo badala yake wajanja wachache walikuwa wakitumia nafasi ya mgogoro kuendelea kujinufaisha.

" Sitegemei mgogoro mwingine wa ardhi baada ya kumalizika huu, Nawaomba wananchi sasa tuchape kazi" Alisisitiza Kuchauka.

Kutokana na kumalizika kwa mgogoro huo wananchi wa kijiji hicho wameiomba serikali kulitumia eneo hilo kuanzisha Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ili kuinua kipato katika kijiji hicho.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu akionesha eneo la Pori Tengefu akiwa kwenye kigingi ambacho ni mpaka kati ya eneo la Kihurumira ambalo lilikuwa ni eneo la mgogoro kati ya wananchi wa kijiji cha Kikulyungu na Pori la Akiba la Selous ambalo limekuja kubainika kuwa eneo hilo sio ardhi ya Kijiji hicho na wala sio sehemu ya Pori la akiba la Selous bali ni ardhi ya Pori Tengefu amabalo lilikuwa imetengwa kwa  ajili ya kuzaliana kwa wanyamapori wanaotoka katika Pori la Selous katika wilaya Liwale mkoani Lindi. Wa kwanza kulia ni Mbunge wa Jimbo la Liwale, Zuberi Kuchauka
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu akiwa na Mbunge wa Jimbo la Liwale, Zuberi Kuchauka wakiwa kwenye eneo la kigingi huku Mbunge huyo akiomuonesha Naibu Waziri Kanyasu eneo la Kihurumira ambalo lilikuwa ni eneo la mgogoro kati ya wananchi wa kijiji cha Kikulyungu na Pori la Akiba la Selous ambalo limekuja kubainika kuwa eneo hilo sio ardhi ya Kijiji hicho na wala sio sehemu ya Pori la akiba la Selous bali ni ardhi ya Pori Tengefu amabalo lilikuwa imetengwa kwa  ajili ya kuzaliana kwa wanyamapori wanaotoka katika Pori la Selous katika wilaya Liwale mkoani Lindi. Wa kwanza kulia ni Mbunge wa Jimbo la Liwale, Zuberi Kuchauka
 Baadhi ya wananchi wakiwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu wakiangalia  eneo la Kihurumila sehemu ambayo kuna mto na  ambalo lilikuwa na mgogoro kuwa sio mali ya pande zote mbili bali mali ya serikali kuu inayomilikiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii,
 Mbunge wa Liwale, Mhe.Zuberi Kuchauka akizungumza na wananchi wake kuhusu kumalizika kwa mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka 12 baada ya Naibu Waziri Kanyasu kuzungumza na wananchi hao
 Baadhi ya wananchi wakiwa wanatoka eneo lenye mgogoro ambapo walitaka eneo hilo la mto waweze kilitumia kwa ajili ya kulishia mifugo pamoja na kulima  katika mto huo ambapo kutokana na hali hiyo mto huo usingeweza kudumu kwa muda mrefu
 Meneja wa Pori la Akiba la Selous, Henock Msocha ( kulia)  akizungumza na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu wakati walipotembelea eneo amvalo lilikuwa na mgogoro kati ya Kijiji cha Kikulyungu na Pori la Akiba la Selous
Aniel Heliem mmoia wa wananchi akimuuliza swali Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Cinstantine Kanyasu mata baada ya kuutangaza kuwa eneo la Kihurumila si sehemu ya Pori la Akiba la Selous na wala sio eneo la Kijiji cha Kikulyungu.

MCHUNGAJI MKOANI SINGIDA APIGWA BUTWAA NA KAZI ZA RAIS DKT.JOHN MAGUFULI

$
0
0
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la FPCT Utaho (B) Yungi, Francis Pius akiongoza ibada iliyofanyika Jumapili katika kanisa hilo lililopo Puma wilayani Ikungi mkoani Singida.
Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu, akivikwa skafu baada ya kuwasili katika kanisa hilo kushiriki ibada hiyo.
Watoto wa kanisa hilo wakiwa ibadani.
Waumini wa kanisa hilo wakiwa ibadani.
Waumini wa kanisa hilo wakiwa ibadani.
Wake wa viongozi wa kanisa hilo wakiwa kwenye ibada hiyo.
Mbunge Kingu akizungumza kwenye ibada hiyo.
Mchungaji Pius na viongozi wengine wa kanisa hilo wakiwaombea Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi,Elibariki Kingu na Katibu wake Njou Muna katika ibada hiyo.


Kaimu Mtendaji wa Kijiji cha Utaho B, ambaye ni muumini wa kanisa hilo, Paul Singi akizungumza.
Viongozi wa kanisa hilo wakiwa ibadani. Kutoka kushoto ni Mchungaji Mathayo Trotimi, Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo, Francis Pius na Mchungaji Elisha Ngoi.
Mbunge Kingu (wa pili kushoto), akiwa katika ibada hiyo. Kutoka kushoto ni Katibu wa Mbunge Njou Muna, Mzee wa Kanisa hilo, Ayubu Kisuda na Dereva wa Mbunge, Yusuf Daffi.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Utaho ambaye pia ni Muumini wa Kanisa hilo, Saimon Andalu akizungumza. 
Kwaya ya Vijana ya kanisa hilo, ikitoa burudani.
Mbunge Kingu, akitoa msaada wa sh.50,000 kwa bibi huyo kwa ajili ya kununulia sare za shule za mjukuu wake.



Na Dotto Mwaibale, Singida

MCHUNGAJI Kiongozi wa Kanisa la FPCT la Utaho (B) Yungi, lililopo Puma wilayani Ikungi mkoani Singida, Francis Pius amesema anapigwa butwaa kwa kasi ya kazi za maendeleo zinazofanywa na Rais Dkt.Johnn Magufuli hapa nchini.

Mchungaji Pius aliyasema hayo katika ibada ya Jumapili iliyofanyika katika kanisa hilo na kuhudhuriwa na Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu.

"Kwa kweli Rais wetu Dkt. John Magufuli ananifanya nipigwe na butwaa kwa kazi kubwa anazozifanya za kutuletea maendeleo kwani katika miaka minne ya uongozi wake tumeona kazi nyingi zikifanyika hakika ni Rais wa wanyonge" alisema Mchungaji Pius.

Akizungumza katika ibada hiyo, Kingu aliwashukuru viongozi wa dini kwa umoja wao wa kumuombea Rais Dkt. John Magufuli na viongozi wengine na Taifa kwa ujumla na kuifanya nchi kuwa na amani na utulivu.

" Ninyi viongozi wa dini mnafanya kazi kubwa ya kuifanya nchi yetu kuwa na amani kutokana na maombi yenu ya kumuombea Rais wetu pamoja na Taifa mungu awabariki sana" alisema Kingu 

Akizungumzia shughuli za maendeleo zinazofanyika hapa nchini tangu Rais Magufuli achaguliwe kuongoza nchi alisema inatokana na Rais Magufuli kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za Serikali na kuzielekeza kufanya miradi ya maendeleo ya nchi.

" Kwa kweli Rais wetu amebana matumizi yasio ya lazima ya fedha za Serikali na hata sisi wabunge tangu achaguliwa hatujawahi kuongezwa mshahara na wala hatujawahi kusafiri kutoka nje ya nchi bila ruhusa yake" alisema Kingu.

Alisema katika kipindi cha miaka minne Rais Magufuli ameweza kununua ndege ambazo wanapanda watalii na kupata fedha za kigeni, ujenzi wa mradi wa umeme Rufiji, Ujenzi wa Reli ya treni ya mwendo kasi kutoka Dar es Salaam hadi Makutopora Dodoma, miradi ya maji, ujenzi wa zahanati na vituo vya afya, barabara, shule na miradi mingine mingi.

Alisema kazi hizo zote zinafanyika kutokana na uzalendo mkubwa alionao Rais Magufuli kwa kuwatumikia wananchi wa Tanzania.

Katika ujenzi unaoendelea wa kanisa hilo, Mbunge Kingu aliweza kuchangia sh.milioni mbili na laki moja kwa ajili ya kutengeneza madirisha.

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA, PHAUSTINE KASIKE AWAVISHA VYEO MAAFISA MAGEREZA WA MKOA WA DAR ES SALAAM NA PWANI WALIOPANDISHWA VYEO HIVI KARIBUNI

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(kulia) akimvalisha cheo Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Lipina Lyimo kuwa Kamishina Msaidizi wa Magereza katika hafla fupi iliyofanyika kwenye viwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam, jana Agosti 6, 2019.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(kulia) akimvalisha cheo Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Merkiory Komba kuwa Mrakibu wa Magereza katika hafla fupi iliyofanyika kwenye viwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam, jana Agosti 6, 2019. Mrakibu wa Magereza, Merkiory Komba ni Msaidizi wa Mkuu wa Jeshi hilo.
Baadhi ya Maafisa waliopandishwa vyeo katika ngazi mbalimbali wakiwa timamu kabla ya Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike kuwasili kwa zoezi la uvishaji vyeo , jana Agosti 6, 2019 kwenye viwanja wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(kulia) akikagua Gwaride maalum kabla ya zoezi la uvishaji vyeo kwa Maafisa wa Mkoa wa Dr es Salaam na Mkoa wa Pwani waliopandishwa vyeo hivyo hivi karibuni.
Gwaride maalum likipita kwa mwendo wa pole mbele ya Kamishna Jenerali wa Magereza nchini(hayupo pichani) kwenye hafla ya uvishaji vyeo kwa maafisa wa Mkoa wa Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani jana Agosti 6, 2019.
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakitoa heshima wakati Gwaride maalum likipita mbele ya Kamishna Jenerali wa Magereza nchini(hayupo pichani) kwenye hafla ya uvishaji vyeo kwa maafisa wa Mkoa wa Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani jana Agosti 6, 2019.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, Phaustine Kasike(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa wa ngazi mbalimbali wa Jeshi la Magereza waliopandishwa vyeo (waliosimama)baada ya hafla uvishaji vyeo iliyofanyika katika viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji, Ukonga jijini Dar es salaam, jana Agosti 6, 2018(Picha zote na Jeshi la Magereza).

Benki ya Stanbic yazindua I Go Tanzania kukuza sekta ya utalii

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Stanbic Tanzania (kushoto) akimkabidhi zawadi Mh. Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke wakati wa uzinduzi wa kampeni ya 'I Go Tanzania' ambayo inatoa punguzo la bei na ofa mbali mbali kwa wamiliki wa kadi za benki ya ICBC watakaotembelea Tanzania. Kampeni hii inalenga kukuza sekta ya utalii na kuongeza idadi ya watalii kutoka China nchini Tanzania.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Dr Hamisi Kigwangalla (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Stanbic Tanzania, Ken Cockerill wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya 'I Go Tanzania' ambayo inatoa punguzo la bei na ofa mbali mbali kwa wamiliki wa kadi za benki ya ICBC watakaotembelea Tanzania. Kampeni hii inalenga kukuza sekta ya utalii na kuongeza idadi ya watalii kutoka China nchini Tanzania.    
 Mkurugenzi Msaidizi wa Benki ya Viwanda na Biashara ya China (ICBC), Ofisi ya uwakilishi ya nchini Afrika Kusini, Gang Sun (kushoto), Mh. Balozi wa China nchini Tanzania (wa pili kushoto), Wang Ke, Waziri wa Maliasili na Utalii. Mh. Dr Hamisi Kigwangalla (katikati),Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Stanbic Tanzania, Ken Cockerill (wa pili kulia) na Mkuu wa kitengo cha kadi na malipo kutoka Standard Bank Group, Lincoln Mali (kulia) wakati wa uzinduzi wa  kampeni ya 'I Go Tanzania' ambayo inatoa punguzo la bei na ofa mbali mbali kwa wamiliki wa kadi za benki ya ICBC watakaotembelea Tanzania. Kampeni hii inalenga kukuza sekta ya utalii na kuongeza idadi ya watalii kutoka China nchini Tanzania.     
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images