Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

S/M KIZUIANI INA UPUNGUFU WA VYUMBA VYA MADARASA 16, NA HAKUNA CHOO CHA WALIMU

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI,BAGAMOYO.

SHULE ya msingi Kizuiani,kata ya Kisutu,Bagamoyo mkoani Pwani inakabiliwa na upungufu wa vyumba vya madarasa 16 hali inayosababisha wanafunzi kusoma kwa awamu ili kuondoa mlundikano madarasani pamoja na shule kukosa hati miliki.

Aidha walimu shuleni hapo hawana vyoo ambapo hulazimika kutumia choo cha nyumba ya mwalimu karibu na shule hiyo.

Akitoa taarifa ya shule ya msingi Kizuiani,kwa mbunge wa jimbo la Bagamoyo dkt.Shukuru Kawambwa ambae alikwenda kuzungumza na walimu katika muendelezo wa ziara yake ya jimbo, kaimu mwalimu mkuu Joseph Ludovick alisema ,kwa sasa kuna jumla ya wanafunzi 1,170 ,vyumba vya madarasa 12 ambavyo havikidhi mahitaji.

"Kuna darasa ambalo linaongezwa kujengwa lakini bado itakuwa haitoshi kutokana na idadi ya wanafunzi na madarasa yaliyopo ,na ndio maana tuliona wasome kwa awamu ili kuondokana na mlundikano wa wanafunzi darasani"alifafanua Ludovick.

Ludovick alieleza, pia walimu wanalazimika kwenda kujisaidia katika choo cha nyumba ya mwalimu shuleni hapo, lakini wanamshukuru mbunge wa jimbo hilo ,dkt Shukuru Kawambwa kwa kuwawezesha kuanza kujenga choo ambacho kipo hatua ya chini.

Alitaja changamoto nyingine kuwa ni, upungufu wa matundu ya vyoo 38, uzio,meza na viti kwa ajili ya ofisi ya walimu na upungufu wa nyumba za walimu 26 kwani iliyopo ni moja.

"Licha ya changamoto hizo lakini tumefanikiwa kumaliza tatizo la madawati na kuinua taaluma "alijieleza.Ofisa elimu kata ya Kisutu, Yusuph Salim alisema, kama kata wamechukua hatua ya kujenga darasa moja ambalo lipo hatua ya gebo hivyo wanaomba wadau na wahisani kujitokeza kusaidia liweze kukamilika.

Nae Kawambwa alisema, ataendelea kushirikiana wadau wa elimu na kamati za shule jimboni humo, kuboresha sekta ya elimu ili kupunguza na kutatua changamoto zilizopo kulingana na uwezo uliopo.

Kawambwa aliutaka, uongozi wa shule hiyo kufuatilia eneo jingine ambalo litasaidia kuanza kujenga shule nyingine -Kizuiani B ambapo wanafunzi wengine waweze kupunguzwa endapo itakuja kukamilika.


RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA KUTOA UZOEFU WAKE KUHUSU NCHI ZA SADC

$
0
0
Na Said Mwishehe,Michuzi TV

RAIS Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa anatarajiwa kuongoza kongamano la majadiliano kuhusu Jumuiya ya Maendeleo ya Wananchi Kusini mwa Afrika(SADC).

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalim Nyerere Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dk.Hassan Abbas amesema kupitia kongamano hilo mzee Mkapa atatoa uzoefu na uzeefu wake kuhusu nchi za SADC.

Dk.Abbas amefafanua pamoja na mambo mengine, kuna ratiba ya shughuli mbalimbali kuhusu SADC , Agosti 15 mwaka huu Mkapa atakuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako ndiko kongamano hilo litafanyika. 

"Kwenye kongamano ambalo litafanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kutakuwa na majadiliano kuhusu nchi za SADC.Mzee Mkapa siku hiyo ataongoza majadiliano hayo kwa kutoa uzoefu na kama tunavyofahamu amekuwa kiongozi wetu kwa muda mrefu,anao uzoefu mkubwa kuhusu SADC ,hivyo tutajifunza mengi kutoka kwake,"amesema Dk.Abbas.

Amesema ni vema wananchi wakajitokeza kwenye kongamano hilo kwani wanaamini litakuwa na somo kubwa kuhusu nchi za jumuiya hiyo ambayo Tanzania imebeba historia kubwa kutokana na mchango wake ,kwanza wa kukomboa nchi za Kusini mwa Bara la Afrika lakini sasa ni katika kushirikiana katika kuleta maendeleo kwa nchi wanachama na Afrika kwa ujumla.

Wakati huo huo Dk.Abass ametoa ufafanuzi kuhusu uwepo wa tetesi kuwa baadhi ya washiriki wachache wameshindwa kushiriki kwasababu mbalimbali ikiwemo ya kukwama mikakati.

Katika hilo Dk.Abass ameeleza madai hayo hapana ukweli na kwa kuwa ni fununu ni vema zikaachwa lakini akatumia nafasi hiyo kueleza nchi zote za jumuiya hiyo nimepata nafasi ya kushiriki na taratibu za kushiriki zinaeleweka. " Hizi ni fununu tu ambazo hazina uthibitisho.Na kwa kuwa fununu tuaache.

"Binafsi nimepita kwenye banda Leo,nimeona namna ambavyo mabanda mengi yalivyokuwa na bidhaa nzuri,tuendelee kuwahamaisha wananchi kuja kutembelea na hakuna kiingilio,"amesema Dk.Abbass na kuongeza mbali ya kuwepo na mabanda kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mwalim Nyerere pia viwanj vya Karimjee nako kuna mabanda ya biashara na kote huko amehamasisha wananchi kwenda kutembelea na kuona bidhaa.  
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dk.Hassan Abass akifafanua jambo na waandishi wa habari leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalim Nyerere jijini Dar es Salaam baada ya kutembelea mabanda katika maonesho ya wiki ya nne ya viwanda kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).

MSEMAJI WA SERIKALI DK.ABASSI ATEMBELEA MAONESHO YA NNE YA WIKI YA VIWANDA SADC

$
0
0

 Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dk.Hassan Abassi akiangalia kiatu kwa ajili ya majeshi akiwa katika banda la Tantrade lililopo kwenye maonesho ya nne ya wiki ya viwanda kwa nchi za SADC.Kulia ni Mkurugenzi wa Tantrade Edwin Rutageruka. Picha na Michuzi Jr
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dk.Hassan Abassi (kushoto) akipata maelezo kwenye banda la Shirika la Ndege Tanzania lililopo kwenye wiki ya nne ya maoenesho ya viwanda kwa nchi za SADC yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

 Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dk.Hassan Abassi akizungumza na waandishi wa habari leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalim Nyerere jijini Dar es Salaam baada ya kutembelea banda katika maonesho ya wiki ya nne ya viwanda kwa nchi za SADC
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dk.Hassan Abassi akiwa kwenye banda la Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) baada ya kutembelea banda la wakala hao kwenye maonesho ya wiki ya nne ya viwanda kwa nchi za SADC.

Na Leandra Gabriel ,Michuzi TV

MKURUGENZI wa Idara ya Habari(MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abassi leo Agosti 7, ametembelea maonesho ya nne ya wiki ya viwanda yanayoendelea katika viwanja vya ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere, viwanja vya Karimjee na Gymkhana jijini Dar es Salaam na kuwashauri watanzania kuzidi kutembelea maonesho hayo ili kuweza kupata huduma, ujuzi na maarifa yanayotolewa na taasisi mbalimbali zilizoshiriki katika maonesho hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea maonesho hayo Dkt. Hassan amesema kuwa maonesho yanaendelea vyema ni nafasi kwa wananchi kutembelea viwanja elekezi bure bila malipo ili kuweza kupata masoko ya uhakika pamoja na kubadilishana ujuzi.

Amesema kuwa wiki ya viwanda itafungwa rasmi kesho na Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ally Mohamed Shein na majadiliano na mikutano mbalimbali ya wanajumuiya ya SADC itaendelea.

Dkt. Abassi amesema kuwa kuanzia tarehe 9 hadi 12 wiki ijayo maafisa waandamizi (makatibu wakuu) kutoka jumuiya ya SADC watakutana kujadili masuala mbalimbali ya jumuiya hiyo na tarehe 13 na 14 kitafanyika kikao Cha mawaziri wa nchi za SADC ambapo waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki profesa. Palamagamba Kabudi atapokea kijiti cha uenyekiti wa baraza la mawaziri wa nchi za SADC.


Vilevile amesema kuwa kuanzia tarehe 15 wageni mbalimbali wataanza kuingia nchini na tarehe 17 na 18 mkutano mkuu wa 39 wa wakuu na Serikali kwa nchi 16 za jumuiya ya maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika utafanyika ambapo Rais Magufuli atapokea kijiti cha uenyekiti wa jumuiya hiyo kwa muda wa mwaka mmoja kutoka nchini Namibia.

Waziri Ummy, Balozi Misri wakubaliana uwekezaji wa viwanda vya dawa nchini

$
0
0

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akijadiliana jambo na Balozi wa Misri nchini Tanzania, Mhe. Mohamed Gaber Abulwafa (kushoto) wakati walipokutana jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni ofisa kutoka Ubalozi wa Misri nchini Tanzania, Ahmed El- Ghoul na Ofisa kutoka wizara ya Afya.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Misri nchini Tanzania, Mhe. Mohamed Gaber Abulwafa. Kushoto ni ofisa kutoka Wizara ya Afya na na kulia ni ofisa kutoka Ubalozi wa Misri nchini Tanzania, Ahmed El- Ghoul.




Na John Stephen

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu amekutana na Balozi wa Misri nchini Tanzania, Mhe. Mohamed Gaber Abulwafa na kujadiliana kuhusu kushirikiana katika kuboresha huduma za afya nchini.

Katika mazungumzo hayo pande mbili zimependekeza kushirikiana pamoja katika uwekezaji wa viwanda vya dawa na chanjo, kubadilishana wataalam wa afya ili kuwajengea uzoefu wataalam wetu katika nyanja mbalimbali za sekta nchini.

Pia, Waziri Ummy Mwalimu kwa pamoja wamekubaliana kwa pamoja kuendeleza mapambano ya Homa ya Ini aina C (Hepatitis C) ili kuhakikisha wananchi wanapatiwa huduma bora na kwa wakati kuhusu homa ya Ini aina C.

Baada ya majadiliano hayo Waziri Ummy Mwalimu aliagiza kuandaliwa kwa hati ya ushirikiano (MOU) kwa ajili ya kuratibu na kutekeleza maeneo mbalimbali ya kipaumbele katika sekyta ya afya nchini.

MAKAMU WA RAIS SAMIA AWEKA MAWE YA MSINGI UJENZI WA MAABARA SUA, NA KIWANDA CHA KUCHAKATA MIKUNDE MOROGORO

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Maabara kubwa kwa Afrika ya Sayansi katika Chuo Kikuu cha Kilimo SUA Mkoani Morogoro leo Agost 07,2019. Makamu wa Rais yupo Mkoani Morogoro kwa Ziara ya kikazi ya siku Tatu. kulia ni Waziri wa Biashara na Viwanda Innocent Bashungwa. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Maabara kubwa kwa Afrika ya Sayansi katika Chuo Kikuu cha Kilimo SUA Mkoani Morogoro leo Agost 07,2019. Makamu wa Rais yupo Mkoani Morogoro kwa Ziara ya kikazi ya siku Tatu. kulia ni Waziri wa Biashara na Viwanda Innocent Bashungwa. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)



WAZIRI LUGOLA APOKEA TAARIFA YA BODI YA SHIRIKA LA MAGEREZA, AWATAKA WAJUMBE WAHAKIKISHE MAGEREZA INAJITOSHELEZA KWA CHAKULA KUPITIA MIRADI YAO

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati), akipokea taarifa ya Bodi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza, kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Meja Jenerali Mstaafu, Raphael Muhuga, katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo, Jijini Dodoma, leo. Lugola aliizindua Bodi hiyo Mei 30, 2019 na kutoa miezi miwili Wajumbe wa Bodi hiyo kutembelea miradi mbalimbali ya Magereza Tanzania Bara na kumletea taarifa iyakayoambatana na maoni yao. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza, baada ya kupokea taarifa ya Bodi hiyo, katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo, Jijini Dodoma, leo. Lugola aliifurahia taarifa hiyo na kuwataka Wajumbe hao wahakikishe Magereza inajitosheleza kwa chakula kupitia miradi mbalimbali. Kulia meza kuu ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu, na wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Meja Jenerali Mstaafu, Raphael Muhuga. Na wapili kulia ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Phaustine Kasike. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza, Meja Jenerali Mstaafu, Raphael Muhuga, akitoa ufafanuzi baada ya kuwasilisha taarifa ya kipindi cha miezi miwili kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (wapili kushoto). Wapili kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu. Kulia ni Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, ambaye pia ni Katibu wa Bodi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza, Phaustine Kasike, akizungumza katika kikao cha Bodi hiyo cha kuwasilisha taarifa yake kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto meza kuu). Kulia meza kuu ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

***********

Na Felix Mwagara, Dodoma (MOHA)

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amepokea taarifa ya Bodi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Magereza, na kuwataka Wajumbe wa Bodi hiyo kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha Magereza inajitosheleza kwa chakula kupitia miradi mbalimbali inayomilikiwa na Jeshi hilo.

Waziri Lugola aliizindua Bodi hiyo Mei 30, 2019, na kutoa miezi miwili Wajumbe wa Bodi hiyo, kutembelea miradi mbalimbali ya Jeshi hilo na kumletea taarifa ya awali kuhusu miradi hiyo pamoja na maoni yao.

Akizungumza na Wajumbe wa Bodi hiyo baada ya kupokea taarifa yao, katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dodoma, leo, Waziri Lugola alisema taarifa walioiwasilisha ameifurahia licha ya kuwa na mapungufu kadhaa ambayo yanahitaji uboreshaji zaidi.

Alisema Bodi hiyo inawataalamu mbaimbali ambao wanaweza wakaleta mabadiliko makubwa ya uzalishaji mali na kuweza kufanikisha Jeshi hilo linajitosheleza kwa chakula kupitia wafungwa mbalimbali waliopo magerezani.

“Nawapongeza sana kwa kazi nzuri, ila nawataka mfanye kazi zaidi ambayo itatuwezesha kuona mipango mizuri zaidi katika kulisimamia Shirika hili ambalo bodi yake tuliizindua,”alisema Lugola.

Pia Lugola aliwataka Magereza kutumia wataalamu wa Jeshi kupima viwanja vyao ili kufanikisha maendeleo zaidi na siyo kushirikiana na makampuni binafsi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Meja Jenerali Mstaafu, Raphael Muhuga, alisema Bodi yake kwa muda wa miezi miwili ilitembelea mradi wa ng’ombe wa nyama Mbigiri, mradi wa maziwa Kingolwira, mradi wa Uhunzi, mradi wa Kilimo Idete, mradi wa kilimo Kiberege na Mradi wa kilimo Isupilo ambapo Bodi hiyo ilifanya tathmini ya mali zilizopo, mipaka pamoja na historia ya miradi hiyo.

“Pia miradi mingine tuliyoitembelea ni mradi wa kilimo Ludewa, mradi wa kilimo na mifugo Kitai, mradi wa kilimo Mkwaya, na pia Bodi itaendelea kutembelea miradi mbalimbali ya Jeshi na kuendelea kutoa taarifa,” alisema Muhuga.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu aliitaka Bodi hiyo, ifanye ukaguzi wa kina wa mali za Shirika hilo kiundani zaidi ili taarifa hizo zije kiuhalisia zaidi na kuleta mikakati imara ya mafanikio.

Baadhi ya maelekezo aliyoyatoa Waziri Lugola kwa Bodi hiyo mara baada ya kuizindua, aliitaka kutekeleza maelekezo ya Rais John Magufuli kuhusu suala la Magereza kujitosheleza kwa chakula na pia bodi ihakikishe maeneo ya magereza yanapimwa na kupata hati miliki kwa kutumia wataalamu wa kupima ardhi wa Jeshi hilo.

Pia aliielekeza Bodi hiyo itembelee Magereza yote yenye miradi ya Shirika, na ifanye mkakati wa kutafuta wawekezaji kama vile wawekezaji kwenye mabwawa ya ufugaji wa samaki, na pia bodi itoe mawazo mapya ili kuondoa kufanya biashara kwa mazoea.

TANZANIA KINARA KUDHIBITI DAWA ZA KULEVYA BARANI AFRIKA NA DUNIANI

$
0
0

*Wanajumuiya ya SADC waombwa kutembelea banda la Life and Hope Rehabilitation na kujifunza mbinu za kudhibiti  dawa hizo na kuokoa vijana

Na Erick Picson, Michuzi TV

WAZIRI Mkuu Kassimu Majaliwa amesema kuwa Tanzania imekuwa ikipewa sifa na nchi mbalimbali duniani kwa jitihada zake za kudhibiti madawa ya kulevya ikiwemo bangi, mirungi na coccaine na kuokoa vijana wengi ambao ndio nguvu kazi ya taifa.

Akizungumza mara baada ya kutembelea banda la taasisi ya Life and Hope Rehabilitation Sober House iliyopo Bagamoyo ambayo inayoshughulika na kuwahudumia waathirika wa dawa za kulevya na kupinga vita matumizi ya dawa hizo Majaliwa amesema kuwa jitihada zinazofanywa na serikali kwa kushirikiana na vyombo mbalimbali zimezaa matunda kwa kiasi kikubwa, elimu inatolewa na hatua zinachukuliwa hali iliyopelekea kupungua kwa kiasi kikubwa kwa tatizo hilo. 

"Tanzania imekuwa ikipokea sifa kutoka nchi nyingi Afrika na duniani kwa kufanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kudhibiti madawa ya kulevya, nilikuwa kwenye mkutano Uingereza waziri mkuu wa Cameron alinipongeza hadharani kutokana na jitihada tunazoonesha na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kupambana na madawa ya kulevya" Ameeleza Majaliwa.

Aidha Majaliwa amezishauri nchi wanachama wa SADC kutembelea banda hilo ili waweze kupata tathimini na mbinu ya kupambana na utokomezaji wa dawa za kulevya ambazo huathiri zaidi vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa taasisi hiyo Emmanuel Mussana Masola ameishukuru serikali kwa kuendelea kupambana na janga hilo linaloathiri jamii hasa vijana na kuiomba kuendelea kupambana na yeyote anayejihusisha na madawa ya kulevya ili kuweza kujenga taifa la vijana wenye nguvu na wachapakazi.

Amesema kuwa wataendelea kutoa elimu zaidi juu ya madhara ya kutumia dawa za kulevya pamoja na kupambana na wasafirishaji wa dawa hizo jambo ambalo hata serikali linaunga mkono, na amewaalika wanajumuiya ya SADC kutembelea banda hilo ili kuweza kujifunza mbinu mbalimbali zitakazowasaidia katika kupambana na dawa za kulevya.

Mmoja wa warahibu kutoka taasisi hiyo ameishukuru serikali kwa kuendelea kusaidia katika kudhibiti tatizo hilo hasa wakati huu ambapo taifa linaelekea kujenga uchumi wa viwanda huku vijana wakiwa nguvu kazi kwa kiasi kikubwa na ameiomba serikali kupambana na njia mbadala zinazotumiwa na vijana Mara baada ya madawa hayo kupigwa marufuku.

Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa (katikati) akizungumza na Mkurugenzi wa taasisi hiyo Emmanuel Mussana (kulia)mara baada ya kutembelea maonesho hayo ambapo amesema kuwa serikali ipo imara katika kupambana na yeyote atakayebainika kujihusisha na madawa ya kulevya, leo jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa akimsikiliza mmoja wa warahibu wa dawa za kulevya ambaye anatoa elimu kwa vijana na wanajamii kuhusiana na madhara ya madawa ya kulevya, na wameishukuru serikali kwa kuonesha jitihada za kupambana vikali na madawa ya kulevya,jana jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa (katikati) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa taasisi ya Life and Hope Rehabilitation Sober House Emmanuel Mussana (kulia) ambapo amesema kuwa elimu zaidi inaendelea kutolewa kwa vijana ili kuweza kujenga taifa la vijana wenye nguvu na wachapakazi, kushoto ni Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki profesa. Palamagamba Kabudi.

WAZIRI MKUU MSTAAFU MIZENGO PINDA AIHIMIZA BENKI YA CRDB KUENDELEA KUWEKEZA KWA WAJASIRIMALI WADOGO

$
0
0
Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda akizungumza wakati akifungua semina ya siku moja kwa wajasiriamali wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wanaoshiriki maonyesho ya Nane Nane iliyodhaminiwa na Benki ya CRDB, yanayofanyika yanayofanyika kitaifa, kwenye eneo la Nyakabindi, Bariadi mkoani Simiyu.

Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda amesema Benki ya CRDB ikiwa benki kinara katika uwezeshaji katika sekta mbalimbali za maendeleo nchini inapaswa kuelekeza nguvu zaidi kwa wajasirimali wadogo kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia juhudi za serikali ya awamu ya tano za kujenga uchumi wa kati.

"Kuna makundi ya wakulima wadogo, bodaboda, machinga  na wajasiriamali wengine wadogo ambao wamekuwa wakisahaulika kutokana na kutokuwa na dhamana na mikopo yao inatolewa kwa riba kubwa. Niwaombe Benki ya CRDB mtengeneze mpango mkakati mzuri wakuyahudumia makundi haya kwa unafuu na tuelekeze nguvu zetu huku kwani hawa ni wengi zaidi," alisema Mizengo Pinda.

Mheshimiwa Pinda amezungumza maneno hayo alipotembelea banda la Benki ya CRDB katika maonyesho ya kilimo, ufugaji na uvivi yanayoendelea mkoani SimiyuBenki ya CRDB imeendelea kuwa mstari wa mbele katika uwezeshaji kwa wajasiriamili kupitia mafunzo mbalimbali ya namna bora ya uendeshaji wa biashara na upatikanaji wa mitaji. 

Meneja Mahusiano wa Benki ya CRDB anayehusika na Mikopo ya Kilimo, Maregesi Shaabaan alimhakikishia Waziri Mkuu mstaafu kuwa Benki hiyo imejipanga vilivyo kuhudumia wajasiriamali wadogo katika sekta zote kupitia huduma na bidhaa mbalimbali zinazotolewa na Benki hiyo.

"Kwa upande wa wakulima tumeanzisha akaunti za FahariKilimo ambayo ni mahsusi kabisa kwa ajili ya wakulima, akaunti hii hufunguliwa bure na hakuna gharama za uendeshaji tukilenga kumpa mkulima unafuu wa kupokea malipo pindi anapouza mazao yake" alisema Maregesi.

Maregesi alisema pia Benki hiyo ipo kwenye mchakato wa kuanzisha mikopo maalum kwa ajili ya wamachinga inayolenga kuwapa uwezo wa kukuza biashara yao kw kuwapa mitaji.

"Mheshimiwa Rais wetu mpendwa Dokta John Pombe Magufuli amefanya jitihada kubwa sana na za kupongezwa katika kurasimisha kundi hili la wajasiriamali, hivyo kuunga juhudi hizi Benki ya CRDB ipo katika mchakato wa kuingiza mikopo maalum kwa ajili ya wamachinga huku vitambulisho vyao vikitumika kama dhamana" alisema Maregesi.

Maregesi aliongezea kuwa Benki ya CRDB pia inatoa mikopo maalum ya kwa madereva na wamiliki wa Uber na mikopo ya pikipiki kwa madereva na wamiliki wa bodaboda.

Mapema kabla ya kutembelea banda la Benki ya CRDB, Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda alifungua semina maalum kwa wajasiriamali iliyoandaliwa na Taasisis ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) katika maonyesho hayo ya Nane nane yanayofanyika kitaifa mkoani Simiyu.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda akimpongeza Meneja Mahusiano wa Benki ya CRDB anayehusika na masuala ya Mikopo ya Kilimo, Maregesi Shaaban kwa maelezo mazuri aliyoyapata juu huduma za Benki ya CRDB kwa wakulima, wakati alipotembelea Banda lao katika maonyesho ya Kilomo, Mifugo na Uvuvi (Nane Nane) yanayofanyika kitaifa, kwenye eneo la Nyakabindi, Bariadi mkoani Simiyu. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima na katikati ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda akifurahia jambo na baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB, wakati alipotembelea Banda lao katika maonyesho ya Kilomo, Mifugo na Uvuvi (Nane Nane) yanayofanyika kitaifa, Nyakabindi, Bariadi mkoani Simiyu.


TUME YA MADINI YAENDELEA KUTOA ELIMU KWENYE MAONESHO YA SADC

$
0
0
Mhandisi Mwandamizi wa Tume ya Madini, Asanterabi Mollel (kulia) akielezea
majukumu ya Tume ya Madini kwa Mchenjuaji wa Madini, Hamis Maliki (kushoto)
kwenye maonesho ya nne ya wiki ya viwanda ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini Mwa
Afrika (SADC) yanayoendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius
Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam tarehe 07 Agosti, 2019. Katikati ni Makamu Mkuu
wa Chuo cha Madini Dodoma (MRI), Kunugula Ignas.

Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Dk. Hassan
Abbas (kulia) akifafanua jambo kwenye banda la Tume ya Madini kwenye maonesho ya
nne ya wiki ya viwanda ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini Mwa Afrika (SADC)
yanayoendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC)
jijini Dar es Salaam tarehe 07 Agosti, 2019.

Mchenjuaji wa Madini, Hamis Maliki (kushoto) akitoa maoni yake kwenye banda la
Tume ya Madini.
Wajumbe kutoka Tume ya Madini na Chuo cha Madini Dodoma (MRI) wakiwa katika
picha ya pamoja kwenye maonesho hayo.
Wajumbe kutoka Tume ya Madini na Chuo cha Madini Dodoma (MRI)wakiwa katika
picha ya pamoja na Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu
kutoka Wizara ya Madini, Nsajigwa Kabiki mara baada ya kutembelea banda la Tume
ya Madini.

WAZIRI MASAUNI AFANYA ZIARA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA ABEID AMANI KARUME, VISIWANI ZANZIBAR

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa Kaunda suti), akisikiliza maelezo kutoka kwa Mrakibu Muandamizi wa Uhamiaji, Bakari Mohammed Ameir, wakati wa ziara ya kukagua shughuli za Ulinzi na Usalama zinavyoendelea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Visiwani Zanzibar.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa ziara ya kukagua shughuli za Ulinzi na Usalama zinavyoendelea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Visiwani Zanzibar.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia), akiangalia mashine itakayotumiwa na Idara ya Uhamiaji ikiwa ni utekelezaji wa mabadiliko ya teknolojia kutoka pasi za zamani za kusafiria kwenda kadi za kusafiria za kielektroniki, alipotembelea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume,Visiwani Zanzibar.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akipita kwenye mashine ya ukaguzi wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za Ulinzi na Usalama ,alipotembelea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Visiwani Zanzibar.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

SERIKALI YAWATAKA WAKANDARASI WALIOTUMIA FEDHA VIBAYA UJENZI TANKI LA MAJI KUKAMILISHA MRADI HARAKA

$
0
0
 SERIKALI imewataka wakandarasi na watu wote walioshiriki katika ujenzi mkubwa wa tenki la maji katika kata ya Makoko Bhalima Mjini Musoma mkoani Mara, na kutumia vibaya fedha za mradi huo kuhakikisha wanakamilisha haraka ujenzi huo.

Naibu Waziri wa Maji Juma Aweso amesema hayo wakati akifungua ziara yake ya kikazi ya siku nne mkoani humo ya kukagua maendeleo ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi hususani wale waishio vijijini na kubaini matumizi halali  ya fedha zinazotolewa na serikali ambazo lengo lake kubwa ni kumtua mama ndoo ya kichwani.

Amesema, mwaka 2017 Serikali ilitoa zaidi ya Sh. milioni 923 ili zitumike katika ujenzi wa tangi hilo ambalo ujenzi huo bado unasua sua,  hivyo Serikali haitatoa fedha nyingine katika kukamilisha ujenzi huo na kuwaasa wakandarasi na wananchi wanaoshiriki kazi hiyo kumalizia ujenzi  huo mara moja.

‘’Sisi kama viongozi wa Wizara hatutatoa fedha nyingine haiwezekani serikali inatoa fedha kwa ajili ya kutatua matatizo ya wananchi wa Musoma lakini zinalipwa ovyo ovyo kwa wajanja wachache ambao utekelezaji wao hauonekani  tutafanya kikao cha wazi kuzungumzia mustakabali wa pesa hizo ili tubaini zilipopelekwa,"ameongeza.

Ameongeza viongozi watakuwa wakali  kuwabini watendaji wa kazi za umma wasiokuwa waaminifu ambao baada ya kutoa kauli alitoa agizo kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mhandisi, Robert Lupoja kuwaalika wakandarasi hao kushiriki mjadala wa ubadhilifu wa fedha hizo kesho.

Aidha Aweso amezindua magari manne yenye gharama ya sh.bilioni 400  yaliyotengenezwa katika mfumo wa majitaka na yatakayozunguka kubeba maji machafu ambayo yatatumiwa na wananchi kwa gharama nafuu katika mtaa wa mradi huo.

 Naye, Muwakilishi wa mradi huo Mponeja John amesema mradi huo umefadhiliwa na kampuni ya Uholand ulianza kutekelezwa Oktoba 25 mwaka 20128 ambapo tayari umekamilika kwa gharama ya Sh.bilioni 27.5 na utakusanya maji taka katika kata za kitaji,Mwigobero na Nyakato mjini hapa.

naibu waziri wa Maji, Juma Aweso akikata utepe kuzindua magari manne yenye thamani ya sh.bilioni 400. Magari hayo  yametengenezwa katika mfumo wa majitaka yatakayozunguka kubeba maji machafu ambayo yatatumiwa na wananchi kwa gharama nafuu katika mradi wa  Baruti kata ya Nyakato mjini hapa.
 Naibu waziri wa Maji, Juma Aweso akijagua Tangi la Nyamiongo lenye ujazo wa lita Milioni Tano  ambapo karibu na tangi hilo  patajengwa Kituo cha Kuongeza Nguvu ya Maji (Booster Station) kwenda kwenye tangi linalotarajiwa kujengwa katika kilele cha Mlima Bharima. 

SERIKALI KUOKOA FEDHA ZA UMMA KWA KUJINASUA KWA MAWAKALA WA UNUNUZI WA MAGARI YAKE

$
0
0

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu, akiwataka watumishi wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini- GPSA, kufanya kazi kwa weledi, alipofanya ziara ya kikazi katika taasisi hiyo jijini Dar es Salaam, kubaini changamoto za utekelezaji wa bajeti yake ya mwaka 2018/19 na njia za kuzitatua.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu (kulia), akiwa na mwenyeji wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini- GPSA, Dkt. Geraldine Rasheli (kushoto), alipofanya ziara ya kikazi katika taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini- GPSA, Dkt. Geraldine Rasheli, akieleza changamoto za utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2018/19, hususani kwenye miundombinu ya kuhifadhi mafuta, wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu (hayupo pichani), katika ofisi za taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam.
Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Christopher Nkupama (kulia) na Mtaalam wa Sera wa Wizara hiyo Bw. Msabaha Msabaha, wakifuatilia kwa makini maelezo ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini- GPSA, Dkt. Geraldine Rasheli, wakati wa ziara ya kufuatilia changamoto za utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2018/19 kwa taasisi hiyo na njia za kuzitatua.
Baadhi ya maafisa waandamizi wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini- GPSA, wakifuatilia kwa makini Mkutano kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini- GPSA, Dkt. Geraldine(hawapo pichani), katika Ofisi za GPSA, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa masuala ya Biashara wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini- GPSA, Bw. Malik Aram (kulia), akieleza changamoto ya visima vya mafuta, wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Khatibu Kazungu ya kufuatilia changamoto za utekelezaji wa Bajeti ya taasisi hiyo kwa mwaka 2018/19.

(Picha na Peter Haule, WFM, Dar es Salaam)

*************

Serikali inaangalia njia mbadala ya ununuzi wa magari yake kwa kwenda moja kwa moja kiwandani bila kupitia kwa mawakala kutokana na gharama kuwa juu na hazitabiliki.

Hayo yalibainishwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt.Khatibu Kazungu, alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za Wakala wa Huduma yaUnunuzi Serikalini (GPSA), jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kubaini changamoto namafanikio ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2018/19 kwa taasisi hiyo.

Dkt. Kazungu alisema kuwa, ununuzi wa magari ya Serikali unatumia gharama kubwakutokana na kuwatumia Mawakala wa Ununuzi ambao bei zao ni za juu na zinabadilikamara kwa mara, hivyo kuna haja ya kwenda moja kwa moja kiwandani ili kuokoa fedhaza walipakodi zinazopotea.

Aidha Serikali inaangalia namna itakavyo boresha miundombinu ya GPSA hasa kwakuwekeza katika Visima vya mafuta ili kuwa na mafuta ya kutosha hivyo kusaidiakuongeza ufanisi katika kuhudumia magari ya Serikali.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa GPSA, Dkt. Geraldine Rasheli, alimshukuruDkt. Kazungu, kwa kutembelea taasisi yake na kuahidi kuyafanyia kazi maagizoyaliyotolewa ili kupunguza malalamiko katika utoaji huduma na kuongeza tija kwa Taifa.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Kazungu, anaendelea naziara ya kikazi katika taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo, kuangalia changamoto zautekelezaji wa bajeti ya mwaka 2018/19 na njia za kuzitatua kwa bajeti ya mwaka2019/20.

Tumieni bidhaa zinazozalishwa nchini kutekeleza Mradi wa Peri-Urban

$
0
0

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu( mwenye kilemba chekundu)na
Mbunge wa Bagamoyo, Shukuru Kawambwa( kulia) wakiweka jiwe la
msingi kuzindua Utekelezaji wa Mradi wa Kusambaza Umeme katika vijiji
vilivyopo pembezoni mwa Miji( Peri-Urban) katika Wilaya ya Bagamoyo
mkoani Pwani.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu( mwenye kilemba chekundu)na
Mbunge wa Chalinze, Ridhiwan Kikwete ( mwenye kofia) wakikata utepe
kuzindua utekelezaji wa Mradi wa Kusambaza Umeme katika vijiji vilivyopo
pembezoni mwa miji( Peri-Urban) katika Wilaya ya Chalinze mkoani Pwani
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu( kulia) akiwatambulisha kwa
wananchi, Wakandarasi kampuni ya Sinotec kutoka nchini China
wanaotekeleza Mradi wa Kusambaza Umeme katika Vijiji vilivyopo
pembezoni mwa Miji( Peri-Urban) katika Mkoa Pwani
Mbunge wa Bagamoyo, Shukuru Kawambwa( wa pili kushoto), Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijiji ( REA) Wakili Julius
Bundala Kalolo( tatu kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Nishati
vijiji ( REA) Mhandisi Amos Maganga wakicheza ngoma asili ya wenyeji wa
Bagamoyo, wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Kusambaza Umeme katika
Vijiji vilivyopo pembezoni mwa Miji( Peri-Urban) wilayani Bagamoyo mkoaniPwani.
Baaadhi ya wanafunzi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu(
hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Kusambaza Umeme
katika vijiji vilivyopo pembezoni mwa Miji( Peri-Urban) wilayani Bagamoyo
mkoani Pwani.

*************

Na Zuena Msuya, Pwani

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amesema ni marufuku kwa
mkandarasi yeyote kuagiza nje ya nchi vifaaa kwa ajili ya kutekeleza Mradi
wa Usambazaji Umeme katika vijiji vilivyopo pembezoni mwa Miji(Peri-
Urban).

Mgalu alisema hayo kwa nyakati tofauti, Agosti 6, 2019, wakati akiweka
jiwe la msingi kuzindua Mradi wa Usambazaji Umeme katika vijiji vilivyopo
pembezoni mwa Miji(Peri-Urban) katika Kijiji cha Sanzale wilayani
Bagamoyo na katika Kijiji cha Kaloleni wilayani Chalinze Mkoani Pwani.

Katika uzinduzi huo, Mgalu alisema kuwa kwa Sasa Tanzania ina viwanda
Tisa vinavyotengeneza vifaa na miundombinu ya Umeme ikiwemo nguzo,
nyaya, Mashine za LUKU, Transfoma pamoja na vifaa vingine, hivyo
wakandarasi hao watumie vifaa vinavyotengezwa na viwanda vya ndani ili
kukuza uchumi.

Sambamba na hilo, aliwataka wakandarasi hao kufanya kazi usiku na
mchana ili kukamilisha mradi huo kwa wakati na kusitokee visingizio
vyovyote kwa kuwa vifaa vyote vinapatikana nchini.

"Wakandarasi tunatarajia mradi huo utakamilika kwa wakati, na
hakutakuwa na sababu ya kuchelewesha kwa kuwa kila kitu kinapatikana
hapa nchini",alisema Mgalu .

Mradi wa Peri-Urban katika Wilaya za Bagamoyo na Chalinze,
utaunganisha wateja zaidi ya 4000 katika kipindi cha miezi 9 ya utekelezaji,
ambao utangarimu zaidi ya shilingi bilioni 12 hadi kukamilika kwake Katika
wilaya hizo.

Mradi huo utatekelezwa katika mikoa 9 nchini kwa gharama ya zaidi ya
shilingi trilioni moja, na katika Mkoa wa Pwani pekee Mradi huo utagharibu
zaidi ya shilingi bilioni 37.

Mkandarasi anaetekeleza mradi huo katika Mkoa wa Pwani ni kampuni ya
ukandarasi ya Sinotec kutoka nchini, China.

Katika hatua nyingine Mgalu alilitaka shirika la umeme nchini Tanesco
kushughulikia kwa wakati malalamiko na changamoto mbalimbali
zinazotolewa ya wateja ili kuendelea kuimarisha mahusiano mazuri baina
ya wateja na shirika hilo.

Alisema hafurahishwi na baadhi ya ujumbe au na malalamiko anayopokea
kutoka kwa wananchi wakilalamikia kutoshughulikiwa changamoto zao na
Tasesco wakati ni haki yao ya msingi kutatuliwa matatizo hayo.
Alitaka shirika hilo kuongeza kasi ama nguvu kazi katika kutatua
changamoto mbalimbali wanazozipata wateja ikiwepo kuunguza vitu
,nyumba, huduma ya umeme kwa wakati husika.

SERIKALI YAWATAKA WAKANDARASI WALIOTUMIA FEDHA VIBAYA UJENZI TANGI LA MAJI KUKAMILISHA MRADI HARAKA

$
0
0
Serikali imewataka wakandarasi na watu wote walioshiriki katika ujenzi mkubwa wa Tangi la Maji katika kata ya Makoko Bhalima, Mjini Musoma mkoani Mara, na kutumia vibaya fedha za mradi huo kuhakikisha wanakamilisha haraka ujenzi huo.

Naibu Waziri wa Maji, Juma Aweso amesema hayo wakati akifungua ziara yake ya kikazi ya siku nne mkoani humo ya kukagua maendeleo ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi hususani wale waishio vijijini na kubaini matumizi halali  ya fedha zinazotolewa na serikali ambazo lengo lake kubwa ni kumtua mama ndoo ya maji kichwani.

Amesema, mwaka 2017 serikali ilitoa zaidi ya Sh milioni 923 ili zitumike katika ujenzi wa tangi hilo ambalo ujenzi wake bado unasua sua,  hivyo serikali haitatoa fedha nyingine katika kukamilisha ujenzi huo na kuwaasa wakandarasi na wananchi wanaoshiriki kazi hiyo kumalizia ujenzi  huo mara moja.

‘’Sisi kama viongozi wa Wizara hatutatoa fedha nyingine, haiwezekani serikali inatoa fedha kwa ajili ya kutatua matatizo ya wananchi wa Musoma lakini zinalipwa ovyo ovyo kwa wajanja wachache ambapo utekelezaji wake hauonekani, tutafanya kikao cha wazi kuzungumzia mustakabali wa pesa hizo ili tubaini zilipopelekwa’’ameongeza Aweso.

Ameongeza kuwa, viongozi watakuwa wakali  kuwabaini watendaji wa kazi za umma wasiokuwa waaminifu.Aidha amemuagiza Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mhandisi, Robert Lupoja kuwaalika wakandarasi hao kushiriki mjadala wa ubadhilifu wa fedha hizo.

Aidha Aweso amezindua magari manne yenye gharama ya sh.bilioni 400  yaliyotengenezwa katika mfumo wa majitaka yatakayozunguka kubeba maji machafu ambayo yatatumiwa na wananchi kwa gharama nafuu katika mitaa ya mradi huo.

 Naye, Muwakilishi wa mradi huo Mponeja John amesema mradi huo umefadhiliwa na kampuni ya Uholand ambapo ulianza kutekelezwa octoba 25 mwaka 2018 na tayari umekamilika kwa gharama ya shilingi bilioni 27.5 na utakusanya maji taka katika kata za kitaji,Mwigobero na Nyakato mjini hapa.

Naibu waziri wa Maji, Juma Aweso akikata utepe kuzindua magari manne yenye thamani ya sh.bilioni 400. Magari hayo  yametengenezwa katika mfumo wa majitaka yatakayozunguka kubeba maji machafu ambayo yatatumiwa na wananchi kwa gharama nafuu katika mradi wa  Baruti kata ya Nyakato mjini hapa.
Naibu waziri wa Maji, Juma Aweso akikata utepe kuzindua magari manne yenye thamani ya sh.bilioni 400. Magari hayo  yametengenezwa katika mfumo wa majitaka yatakayozunguka kubeba maji machafu ambayo yatatumiwa na wananchi kwa gharama nafuu katika mradi wa  Baruti kata ya Nyakato mjini hapa.

 Naibu waziri wa Maji, Juma Aweso akikagua Tangi la Nyamiongo lenye ujazo wa lita Milioni Tano  ambapo karibu na tangi hilo  patajengwa Kituo cha Kuongeza Nguvu ya Maji (Booster Station) kwenda kwenye tangi linalotarajiwa kujengwa katika kilele cha Mlima Bharima. 

ACHANA NA SEMINA WEKEZA VYUONI TUPATE WAHITIMU BORA –DKT CHAULA

$
0
0
NA Mwandishi Wetu Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu ya Afya Dkt. Zainab Chaula amewaagiza viongozi wa Wizara yake kuachana na semina katika sekta ya Afya na badala yake wawekeza fedha zao katika vyuo vya Afya ili kupata Wanafunzi wenye ubora.

Dkt. Chaula amesema hayo wakati alipotembelea Chuo cha Uuguzi Milembe kilichopo Jijini Dodoma ili kuongea na wanafunzi pamoja na uongozi wa chuo kwa lengo la kubadilishana mawazo lakini pia kupata maoni kutoka kwao.

Aidha Dkt. Chaula ameongeza kuwa fedha za semina zinawanufaisha watu wachache lakini zikiwekezwa kwa wanafunzi wa Afya wanapata elimu yenye ubora ambayo matokeo yake hutoa huduma bora za tabibu kwa watu wengine. 

Dkt. Chaula amewapa moyo wanafunzi hao kutokata tamaa na badala yake wafanye kazi na kusoma kwa bidii ili hapo baadae waje kuwa viongozi wa Taifa hili kama ilivyo kwa viongozi wa sasa ambao pia wametokea kwenye fani ya Afya.

Dkt. Chaula amewataka wanafunzi hao kukabiliana na changamoto zilizopo na kuwataka kuiga na kufuta yale mazuri na kuachana na mabaya akiongeza kuwa katika maisha lazima kuwe na changamoto.

Dkt. Chaula aliongeza kuwa zamani shule ziliwaandaa wanafunzi kuwa wazalendo kwa kuwafundisha stadi za maisha akitaja mfano wanafunzi kujifunza shughuli za kilimo wakiwa wa shule kwa kuwapingia kazi za kumwagilia bustani.

Aidha Dkt. Chaula aliwataka wanafunzi pamoja na uongozi wa Chuo kuwa wabunifu ili mambo yaweze kwenda akiongeza kuwa kiongozi mzuri ni yule anayekuja na matokeo na kuacha tabia ya kusubiri serika kufanya kila jambo kwani hakuna serikali ila kuna viongozi wenye dhamana wanaowajibika kwa wananchi.

Wakati huo baadhi ya wanafunzi waliotoa maoni yao kwa kiongozi huyo walitaka kujua vigezo vya kujiunga na mafunzo chuoni hapo ambapo mwanafunzi Jacline James alioji kwanini kiwango cha matokeo ya kuingilia chuni hapo kushuka hadi alama D tofauti na awali ambapo mwanafuzi alidailiwa na kiwango cha ufaulu cha angalau C mbili na D moja lakini aliondolewa wasiwasi kwamba Chuo hicho kidaili wanafunzi kwa vigezo vya NACTE.
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu ya Afya Dkt. Zainab Chaula akiongea na wanachuo wa chuo cha Wauguzi Milembe leo Jijini Dodoma alipotembelea Chuo hicho kwa ajili ya kusikiliza na kubadilishana mawazo na wanachuo hao. 
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu ya Afya Dkt. Zainab Chaula akiongea na wanachuo wa chuo cha Wauguzi Milembe leo Jijini Dodoma alipotembelea Chuo hicho kwa ajili ya kusikiliza na kubadilishana mawazo na wanachuo hao.
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu ya Afya Dkt. Zainab Chaula pamoja na Wakurugenzi walio chini ya Wizara yake  akiongea na wanachuo  wa chuo cha Wauguzi Milembe leo Jijini Dodoma alipotembelea Chuo hicho kwa ajili ya kusikiliza na kubadilishana mawazo na wanachuo hao.
Wanachuo wa Chuo cha uuguzi Milembe Dodoma walimsikiliza  Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu ya Afya Dkt. Zainab Chaula akiongea alipotembelea chuoni hapo kwa ajili ya kusikiliza na kubadilishana mawazo na wanachuo hao.

BENKI YA CRDB YAELEZEA UMUHIMU WA AKAUNTI YA TANZANITE KWA WANADIASPORA KATIKA MKUTANO WA SADC

$
0
0
Meneja Uhusiano wa benki ya CRDB , Godwin Semunyu na Nuru Kilasa Afisa Uhusiano Mwandamizi Benki ya CRDB wakitoa maelezo kwa baadhi ya wateja waliotembelea katika banda la benki hiyo kwenye maonesho ya 4 ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za SADC yanayoendelea kwenye viwanja vya Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Meneja Uhusiano wa benki ya CRDB , Godwin Semunyu , Lucy Kimei Meneja wa Benki ya CRDB Diaspora na Nuru Kilasa Afisa Uhusiano Mwandamizi Benki ya CRDB wakitoa maelezo kwa baadhi ya wateja waliotembelea katika banda la benki hiyo kwenye maonesho ya 4 ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za SADC yanayoendelea kwenye viwanja vya Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
 

NGOs NJE YA SHERIA ZATAKIWA KUKAMILISHA USAJILI NDANI YA MUDA ELEKEZI

$
0
0
Na Mwandishi Wetu Mwanza

Marekebisho ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Namba 3 ya Mwaka 2019 yameweka bayana mipaka ya Mashirika yanayofanya shughuli za kijamii na kiuchumi kutekeleza takwa la kisheria la kujisajili chini ya Sheria Namba 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa mabadiliko ya Sheria ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali Na. 3 ya mwaka 2019, na kwamba muda wa kukamilisha usajili huu ni miezi miwili kuanzia tarehe 1 Julai, 2019.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Mkoani Mwanza Msemaji wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Mendelee ya Jamii) Bw. Erasto Ching’oro ameeleza kuwa NGOs zilizosajiliwa awali chini ya Sheria nyingine zinatakiwa ziwe zimejisajili chini ya Sheria ya NGO mapema kabla ya kukamilika kwa miezi miwili ya takwa la kisheria

Zoezi la Usajili linaendelea katika Kanda ya Ziwa kwa mikoa ya Mara, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Geita na Kagera kwa muda wa siku tatu na utaanza kuanzia tarehe 8 hadi tarehe 10 Agosti, 2019 katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Mwanza. 

Bw. Erasto amesisitiza wadau kujitokeza kwa wingi katika siku zote za zoezi la usajili kwa lengo la kukamilisha zoezi la kuhamisha usajili katika muda elekezi wa miezi miwili kuanzia tarehe 1 Julai, 2019 ili kuepuka usumbufu hivyo kupata uhalali wa kuendelea na shughuli za shirika.

Ameongeza kuwa, walengwa wakuu wa Usajili unaoendelea ni Mashirika na Taasisi zinayofanya kazi za kijamii na kiuchumi kwa manufaa ya jamii, ambao awali walisajiliwa chini ya Sheria nyingine ikiwemo Sheria ya Vyama Sura 337, Sheria ya Udhamini Sura 375, na Sheria ya Makapuni Sura 212/213, kama zilivyofanyiwa mabadiliko na Sheria Namba 3 ya mwaka 2019, na sasa wanatakiwa kusajiliwa chini ya Sheria stahiki ikiwemo Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Namba 24 ya mwaka 2019 ili kuhuisha taarifa za NGOs na kuongeza uwazi na uwajibikaji katika ngazi za utendaji.

“Sheria hii inayataka Mashirika yote yaliojisajili chini ya Sheria nyinginezo kuhakikisha kuwa yamekamilisha uhamisho wao ndani ya kipindi cha miezi miwili kuanzia siku ya tarehe 1 Julai, 2019 ili kuendelea kupata haki na hadhi ya kuendesha shughuli zao katika jamii kwa kuzingatia Sheria, taratibu na kanuni. Alisisitiza Bw.Erasto

Aidha, Bw. Erasto ameongeza kuwa zoezi la kuhuisha usajili wa mashirika yanayofanya kazi za kijamii na kiuchumi katika ngazi ya jamii hapa nchni lina umuhimu ukubwa kwani litawezesha kuwa na matumizi bora ya rasilimali za nchi kwa kuwa na mgawanyiko wenye uwiano wa afua mbalimbali katika kuhudumia jamii, jamii itahamasishwa kuchangia maendeleo yao, itakuza ajira na kuongeza weledi katika utekelezaji wa miradi na kukuza uwazi na uwajibikaji. 

Usajili huu unafanyika ikiwa ni utekelezaji wa takwa la kisheria linaloelekeza Mashirika na Taasisi zote zinazofanya kazi za kijamii na kiuchumi kwa manufaa ya wananchi kuhakikisha kuwa yamekamilisha usajili wake chini ya Sheria Namba 24 ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa mabadiliko chini ya Sheria Namba 3 ya mwaka 2019.

WAZIRI MABULA AAGIZA MASHAURI YA ARDHI KUISHA NDANI YA MIAKA MIWILI

$
0
0
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizindua Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Mbulu jana katika hafla iliyofanyika Dongobesh mkoani Manyara jana, wa pili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Chelestino Mofuga na wa pili kulia ni Mbunge wa jimbo la Mbulu Vijijini Flatei Massey.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akivishwa kitenge kabla ya kuanza kuzungumza na wananchi wa Mbulu wakati uzindua Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Mbulu jana eneo la Dongobesh mkoani Manyara jana. Kulia ni Mbunge wa jimbo la Mbulu Vijijini Flatey Massey.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akitoka katika ofisi ya Halmashauri ya Mji wa Babati mkoani Manyara alipokwenda kukagua masijala ya Ardhi na Mfumo wa ukusanyaji kodi wakati wa ziara yake ya siku moja mkoani humo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Babati Elizaberth Kitundu na kulia ni Mkurugenzi wa Mji wa Babati Fortunatus Fwema.

************



Na Munir Shemweta, WANMM MANYARA

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amewaagiza Wenyeviti wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba nchini kuhakikisha Mashauri ya ardhi yanasikilishwa na kuisha katika kipindi kisichozidi miaka miwili tangu shauri kufunguliwa katika Baraza.

Dkt. Mabula ametoa agizo hilo jana tarehe 6 Agosti 2019 katika eneo la Dongobesh wilayani Mbulu mkoa wa Manyara wakati wa uzinduzi wa Baraza la Ardhi na Nyumba la wilaya ya Mbulu mkoani humo.

Alisema, Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ina jukumu kubwa la kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora inayotolewa kwa weledi na uadilifu hivyo ucheleweshaji wowote wa mashauri unasababisha wananchi kushindwa kupata haki kwa wakati.

Aliwakumbusha watumishi wote wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya kutimiza majukumu yao kwa kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo iliyopo na ile itakayokuwa inatolewa ili kuboresha utoaji huduma ya utatuzi wa migogoro itokanayo na matumizi ya ardhi.

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, Serikali kwa kuzingatia umuhimu wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya katika kushughulikia mogogoro inayotokana na matumzi ya ardhi inalo jukumu la kuyapatia Mabaraza Watumishi ili yaweze kutekeleza majukumu yake vizuri.

‘’ Mabaraza ya Ardhi yalikuwa yanakabiliwa na uhaba mkubwa wa wenyeviti ambapo katika kukabiliana na changamoto hiyo katika mwaka wa fedha 2018/2019 Serikali imeajiri wenyeviti wapya ishirini kwa ajili ya kuongeza nguvu kazi kwenye maeneo yenye migogoro mingi ya ardhi ikiwemo wilaya ya Mbulu’’ alisema Dkt Mabula.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi pia alizitaka halmashauri zote nchini kuhuisha Mabaraza ya Ardhi ya Kata na Vijiji kwa yale yaliyomaliza muda wake na kutoa elimu au semina kwa wajumbe wa Mabaraza hayo kuwafahamisha majukumu yao.

Aidha, alisema idadi ya migogoro inayotokana na matumizi ya ardhi imeendelea kuongezeka siku hadi siku na kuwaasa wananchi wa Mbulu kutumia huduma za Baraza lililozinduliwa na kufuata taratibu za utatuzi wa migogoro inayotokana na matumzi ya ardhi ili kupata ufumbuzi wa migogoro kwa mujibu wa sheria.

Kwa upande wake Msajili wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba nchini Stela Tulo alisema uanzishwaji wa Baraza la ardhi na nyumba la wilaya ya Mbulu umejibu kiu ya wananchi wa wilaya hiyo kwa kuwa Baraza hilo litasaidia kupunguza mlundikano wa mashauri uliopo katika Baraza la Babati lakini pia litawarahisishia wananchi wa Mbulu kupata huduma iliyo karibu zaidi.

Mbunge wa jimbo la Mbulu Vijijini mkoani Manyara Flatei Massey na Yule wa Mji Zakaria Isaay wameishukuru Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kuanzisha Baraza la Ardhi na Nyumba katika wilaya hiyo na kueleza kuwa Baraza hilo litawasaidia wananchi wa Mbulu mkoani Manyara waliokuwa wakitembea umbali mrefu wa kilomita 120 kufuata huduma ya Baraza katika wilaya ya Babati.

Hata hivyo, Wabunge hao walisema matatizo ya Ardhi katika wilaya ya Mbulu hayawezi kuisha iwapo jitihada za kupima ardhi ya wilaya hiyo haitafanyika na eneo kubwa la wilaya hiyo halijapimwa.

Baraza la Ardhi na Nyumba la wilaya ya Mbulu lililozinduliwa linakuwa Baraza la nne katika mkoa wa Manyara wenye wilaya tano. Mabaraza mengine ni Simanjro, Babati na Kiteto.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi amevitaka vijiji vyenye fedha katika wilaya ya Mbulu kuchangia fedha kwa ajili ya kufanyiwa mpango wa matumizi bora ya ardhi ili kuepusha migogoro ya ardhi.

Dkt Mabula alisema vijiji vyote katika wilaya hiyo ambavyo havina mpango wa matumizi bora ya ardhi vichukue hatua hiyo ili kuepusha migogoro ya wafugaji na wakulima na kubainisha kuwa iwapo zoezi hilo litafanyika maeneo katika vijiji hivyo yatajulikana kulingana na matumizi yake na kusisitiza kuwa hapo migogoro haitatokea tena.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alitoa kauli hiyo kutokana na kutoridhishwa na kasi ya Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi katika vijiji vya wilaya ya Mbulu ambapo kati ya vijiji 449 ni vijiji 145 pekee ndivyo vyenye Mpango huo jambo linalosababisha migogoro ya ardhi kuendelea.

Airtel yajipanga kutoa huduma kwa wateja wakubwa katika mkutano wa SADC.

$
0
0
Waziri Mkuu kasim Majaliwa akizungumza na baadhi ya watoa huduma wa Kampuni ya Airtel Tanzania inayomilikiwa na Serikali kwa asilimia 49 wakati alipotembelea banda la Airtel lililopo JNICC katika mkutano wa SADC unaondelea jijini DSM #SADC2019 #TZTUNATEKELEZA
Baadhi ya wateja wa Airtel tanzania wakihudumiwa kusajili laini zao kwa alama za vidole katika banda la Airtel lililoko JNICC wakat wakati wa mkutano wa SADC unaondelea jijini DSM #SADC2019 #TZTUNATEKELEZA

*Airtel yapeleka huduma za usajili kwa alama za vidole SADC.

Kampuni ya simu za mkononi Airtel Tanzania Plc kupitia Meneja Mawasiliano wake bw, Jackson Mmbando imesema kuwa wateja wote wanaoingia katika naonesho na mkutano wa SADC unaoenselea wanatoa huduma zote za kampuni katika bada lao ikiwemo kukamilisha usajili wa SIM Card kwa wateja wao wote kwa njia ya alama za vidole yaani Beometric Registration.

"sisi Kama watoa huduma tayari tumeweka kambia hapa tunatoa huduma za usajili kwa alama za visole hapa kwa kuwa tunafaham watu wengi wanatembelea hapa hivyo ni jukumu letu kuwasaidia kuokoa muda wao" alisema Mmbando

Airtel ina mabanda mawili katika viwanja vya JULIUS NYERERE INTERNATINAL CONFERENCE CENTRE (JINCC) ,ambapo maonesho na mkutano wa SADC unaendelea katika ukumbi huo jijini DSM.

RC Makonda amtembelea kijana mwenye uvimbe usoni

$
0
0
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, leo amemtembelea kijana aitwaye Hamza Ashiraf ambaye hivi karibuni alimsaidia kwa kumsafirisha kutoka nyumbani kwao Bukoba na kumleta jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi juu ya uvimbe wake kwenye paji la uso.

SIKU chache zilizopita kijana Ashiraf akiwa kwao Bukoba, alijitokeza hadharani kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii akiomba msaada wa matibabu ya tatizo lake la uvimbe uliojitokeza kwenye eneo la uso wake.

Lakini kwa kudra za Mwenyenzi Mungu,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh.Makonda alijitoa kumsaidia na mara moja akamfanyia utaratibu wa ndege ya kumfikisha jijini Dar es Salama na mara moja akaelekeza apelekwe katika hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi zaidi jambo ambalo tayari limeshafanyika na kwamba siku chache zijazo atafanyiwa upasuaji mkubwa ambao utapelekea sehemu kubwa ya uso wake kutoka.

Taarifa kutoka kwa Dkt Bingwa wa upasuaji wa Macho na masikio Edwin Lyombo, amesema, wakati Ashiraf anatolewa Bukoba tayari alikuwa ameshaanza kufanyiwa matibabu lakini Haya kuwa mazuri.

“Nitoe shukurani nyingi kwa Mh Makonda kwa moyo wake wa kujitolea kama huu, kwani endapo watu wengi Zaidi watapatikana kujitolea hapa nchini kusaidia watu wenye matatizo makubwa kama haya basi uwezokano wa kupunguza Malachi makubwa kama haya utaleta tija,” alisema Lyombo.

Ashiraf yeye ameendelea kutoa shukurani zake kwa Makonda kwa kumwezesha kumfikisha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

“Niendelee kutoa shukurani zangu kwa Mh Makonda kwa kuendelea kutoa mahitaji yote hadi muda huu, na kwamba niwaambie tu watanzania kuwa was iwe na hofu na mimi kwani nipo kwenye mikono salama kabisa,” alisema Ashiraf.
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images