Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109921 articles
Browse latest View live

MAHAKAMA KUU KUTOA UAMUZI PINGAMIZI LILILOWASILISHWA UPANDE WA SERIKALI DHIDI YA MAOMBI YA ASKOFU MULILEGE KAMEKA

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam Imesema, Agosti 9, 2019 (Ijumaa) itatoa uamuzi juu ya pingamizi lililowasilishwa na upande wa Serikali dhidi ya maombi ya askofu Mulilege Kameka kanisa la Boko Yerusalem, ya kuwataka Mwanasheria wa Mkuu na Kamishna wa Uhamiaji wafike mahakamani hapo kujieleza kwa nini wasifungwe kwa kuipuuuza amri ya mahakama.

Uamuzi huo, unatarajiwa kutolewa na Jaji Atuganile Ngwala, baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili kuhususiana na pingamizi lililowasilishwa na wajibu maombi.

Mwezi Machi Mwaka huu, Mahakama hiyo iliamuru askofu Kameka wa kanisa la wa kanisa la house of prayer shield of faith christian fellowship ( HPSFCFC) lililopo Book Magengeni,

aliyekuwa akishikiliwa na wizara ya mambo ndani ya nchi aachiliwe huru kutoka kizuizini anaposhikiliwa ikisema kwamba uraia wake hauna mashaka.Licha ya kutolewa kwa amri hiyo mpaka leo askofu huyo bado ameshikiliwa na yuko mahabusu gerezani ndio maana ameleta maombi hayo. 

Maombi hayo yamefunguliwa dhidi ya wajibu maombi ambao ni Mwanasheria mkuu wa serikali (AG) na Kamishna wa Uhamiaji na yalipaswa kusikilizwa leo Agosti 6, 2019 lakini upande wa serikali umewasikisha pingamizi ya awali. 

Katika pingamizi hilo, upande wa serikali ukiongozwa na wakili wa serikali Mwandamizi Jackline Nyantori wamedai kuwa, Kifungu cha sheria ambacho wapeleka maombi wamekitumia kupeleka maombi hayo hakiipi mamlaka Mahakama Kuu ya kuweza kusikiliza maombi hayo .

Akijibu hoja hiyo, wakili wa mpeleka maombi, John Mallya amedai kuwa maombi hayo yameletwa kwa mujibu na taratibu, kwani sheria inaruhusu kuleta maombi ya aina hiyo kwa njia ya hati ya maombi na kiapo kama walivyofanya wao katika kupeleka maombi.

Hata hivyo upande wa serikali umesisitiza kwamba kwa kuwa kosa linalodaiwa kutendeka halikufanyika mbele ya mahakama waombaji walipaswa wapeleke malalamiko hayo kwanza polisi walete madai ndipo mahakama iyasikilize na kuyatolea maamuzi.

Akizungumza nje ya mahakama baada ya kesi hiyo kuahirishwa, Wakili Mallya amesema Askofu Kameka alikamatwa na Wizara ya Mambo ya Ndani tangu Desemba,2018, ambapo amekaa kizuizini karibia miezi tisa sasa.

"Msingi wa kukamatwa kwake wanadai sio raia, lakini alikuja hapa Mahakama Kuu Machi,2019,ikaamua kuwa Askofu Kameka ni raia na uraia wake hauna mashaka hivyo Magereza na kitengo cha Uhamiaji kimuachie haraka lakini mpaka leo hukumu hiyo iliyotolewa na Jaji IIvin Mgeta haijatekelezwa ndipo askofu akaleta maombi ya kumshtaki Kamshina Mkuu wa Uhamiaji na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili waje waieleze Mahakama kwa nini wamedharau amri halali iliyotolewa na Mahakama .

" Katika maombi yetu tunataka, mahakama iwakute na hatia ya kuidharau amri hiyo, ambapo adhabu yake ni kifungo cha mwaka mmoja jela au mahakama itakavyoona inafaa, pia ni imani kuwa, Mahakama ni nyumba ya haki na tunatarajia kuona haki inatendeka ndio maana tumekimbilia huku tunaamini haki itatendeka,"amesema Mallya.
Askofu wa kanisa la Boko Yerusalem, Mulilege Kameka, akirudishwa mahabusu kutoka Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Dar ea Salaam, baada ya maombi yake dhidi ya Kamishna wa Uhamiaji na Mwanasheria Mkuu kuahirishwa.
Waumini wa kanisa hilo wakimpungia mkono askafu wao mahakamani hapo baada ya kesi yake kuahirishwa.

WATANZANIA WASHAURIWA KUUNGANISHA NGUVU NA WANAJUMUIYA YA SADC

$
0
0
*Waziri Mkuu asema nchi haina uhaba wa sukari, Kuna viwanda vingi vinavyozalisha sukari Tanzania bara na visiwani Zanzibar

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

WAZIRI Mkuu Kassimu Majaliwa amesema kuwa nchi haina uhaba wa sukari kwa kuwa Kuna viwanda vingi zaidi ya vitano vinavyofahamika ambavyo vinapatikana Tanzania bara na visiwani Zanzibar na huzalisha sukari ya kutosha, hayo ameyaeleza leo mara baada ya kutembelea maonesho ya SADC ya wiki ya viwanda na kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na viwanda vya ndani na nje ya nchi ikiwa ni katika kuelekea katika mkutano mkuu wa 39 wa wakuu wa nchi 16 wa jumuiya ya maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika utakaofanyika Agosti 17 na 18 mwaka huu.

Waziri Mkuu amesema hayo mara baada ya kutembelea maonesho hayo na kusema kuwa maendeleo ni mazuri na washiriki kutoka nchini wamejitokeza kwa wingi na wanaendelea kuonesha bidhaa ambazo nyingi tunazitumia kila siku na huzalishwa katika viwanda vikubwa, vidogo na vya kati pamoja na wafanya kazi za mikono wakiwemo wachoraji na wachongaji na amewataka watanzania kutembelea maonesho hayo na wale wenye hazina ya ardhi na mtaji kuunganisha nguvu na wanajumuiya ya SADC kwa kukaribisha uwekezaji nchini pamoja na kutengeneza masoko ya uhakika na ya kudumu.


Amesema kuwa wananchi waitumie wiki hii katika kwa kuleta mabadiliko nchini kwa kuzingatia kuwa taifa lipo katika mkakati wa kujenga taifa la viwanda;"Wananchi wajitokeze kutangaza bidhaa zao pamoja na kuangalia bidhaa zilizoletwa na makampuni kutoka kwa ndugu zetu wanajumuiya ya SADC na hiyo ni pamoja na kutangaza bidhaa tunazozalisha nchini" Ameeleza Majaliwa 

Aidha amesema kuwa nchi wanachama wameleta bidhaa zao zikiwemo nguo na madawa na wamekuwa wakitembelea katika mabanda ya watanzania na kueleza namna wanavyotumia bidhaa Kama pamba, kahawa na tumbaku katika uzalishaji wao jambo ambalo linatia moyo na kutengeneza fursa ya masoko ya wazi zaidi kwa watanzania.

Mwisho amewataka watanzania kudumisha ukarimu kama ilivyo desturi katika kipindi chote cha ugeni pamoja na kutumia fursa hiyo kuwakaribisha wageni kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii ikiwemo mlima Kilimanjaro, mbuga za wanyama pamoja na kutembelea vivutio vya utalii.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea Maonyesho ya Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Agosti 6, 2019. Wa pili kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocenti Bashungwa. Wengine kutoka kushoto ni Waziri wa Afya wa Zanzibar, Hamad Rashid, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi, Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU: MAONESHO YA SADC NI FURSA PEKEE KWA WATANZANIA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa George Lous Chuwa kuhusu bidhaa mbalimbali wakati alipotembelea banda la Sekretarieti ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika Maonyesho ya Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa Nchi za SADC kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Agosti 6, 2019. Wapili kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Maofisa Habari wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) , Jamila Mbarouk (kulia) na Ben Mwanantala wakati alipotembelea banda la TRC katika Maonyesho ya Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Agosti 6, 2019. Wapili kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocenti Bashungwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Wickled Msian ambaye ni Meneja wa Kudhibiti Ubora wa Bidhaa wa Kampuni ya Ital shoe (wa pili kulia) wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo katika Maonyesho ya Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Agosti 6, 2019. Wa pili kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocenti Bashungwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Dkt William Mugisha wakati alipotembelea banda la Taasisi ya Mifupa (MOI) katika Maonyesho ya Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dr es salaam, Agosti 6, 2019. Wapili kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocenti Bashungwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama picha yake iliyochorwa kwa kutumia shanga na Bw. Aman Greon (kulia) wakati alipotembelea Maonyesho ya Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Agosti 6, 2019. Wa pili kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea Maonyesho ya Maadhimisho ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Agosti 6, 2019. Wa pili kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocenti Bashungwa. Wengine kutoka kushoto ni Waziri wa Afya wa Zanzibar, Hamad Rashid, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi, Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
………………….
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema wiki ya maonesho ya nne ya viwanda ya nchi za SADC ni fursa pekee ya kutangaza bidhaa zinazozalishwa hapa nchini.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Agosti 6, 2019) wakati akizungumza na waandishi wa habari mara ya kukagua mabanda kwenye maonesho hayo yanayoendelea kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Maonesho hayo ambayo yalifunguliwa jana na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, yanafanyika katika maeneo matatu ambayo ni ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere, viwanja wa Gymkhana na viwanja vya Karimjee.

“Nimekuja kufanya ufuatiliaji wa maandalizi ya mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi za SADC, nimekuta yanaendelea vizuri. Nimekuja kuangalia mwitikio wa wajasiriamali wa pande zote mbili za Muungano pamoja na wajasiriamali kutoka nchi wanachama wa SADC, na pia mwitikio wa wananchi wetu ukoje,” amesema.

Waziri Mkuu amesema fursa hiyo ni muhimu kwa Watanzania kuonesha bidhaa za ndani ili wageni wanaokuja wajue kuna bidhaa zipi zinazozalishwa nchini. “Tumetoa fursa kwa nchi za SADC zote nao pia waoneshe bidhaa zao. Maonesho haya ni ya wazi, Watanzania wanayo nafasi ya kuja kuona na kujifunza,” amesema.

Amesema mbali ya fursa ya masoko, Tanzania inayo pia fursa ya kupata teknolojia mpya na za Kisasa ikiwa ni pamoja na wawekezaji wa viwanda vya usindikaji bidhaa mbalimbali. “Tumeona utaalamu unaotumika kutengeneza bidhaa mbalimbali, hii maana yake ni kwamba tunajifunza na teknolojia zinazotumika,” amesema.

“Tunayo fursa ya kukaribisha viwanda kutoka nje ya nchi, wote hapa wameleta bidhaa zao. Pia tunawakaribisha waje waanzishe viwanda kwa ubia na Watanzania. Sisi tunayo ardhi, tunazalisha mazao mengi tu, kwa hiyo mbia wa nje anaweza kuunganisha mtaji na Mtanzania na wakajenga kiwanda hapa nchini,” amesema.

Mbali ya fursa za kiuchumi kwao binafsi, Waziri Mkuu amewataka washiriki wa maonesho hayo, watangaze vivutio vya utalii vilivyopo nchini ambavyo vitasaidia kuwafanya wageni wanaoshiriki mkutano huo watamani kubaki nchini na kuvitembelea.

“Watanzania tutumie nafasi hii kutangaza vivutio vingine tulivyonavyo. Mbuga za wanyama tunazo nyingi, tunao Mlima Kilimanjaro ambao ni mrefu kuliko yote barani Afrika na huwezi kuupanda kutokea popote. Ili uupande, ni lazima uje Tanzania,” amesema.

“Pia tuna eneo maarufu la Olduvai Gorge ambalo ni chimbuko la binadamu wa kwanza duniani, na hili liko eneo liko Ngorongoro. Tuna fukwe nzuri, zenye mchanga mzuri ambazo ukikaa wala huwezi kuchafuka, zina urefu wa zaidi ya km. 1,400 kutokea Tanga hadi Mtwara,” ameongeza.

Mapema, Waziri Mkuu alifanya kikao na Mawaziri wa Mambo ya Nje, Utumishi na Utawala Bora, Viwanda na Biashara wa SMT, Viwanda, Biashara, Wazee na wa Zanzibar (SMZ), Naibu Mawaziri wa TAMISEMI, Mambo ya Nje na Mifugo na Uvuvina kuwapa maelekezo ya kuboresha maandalizi hayo. Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Makatibu Wakuu wa wizara hizo

WAZIRI SIMBACHAWENE AFIKA OFISI ZA ZANZIBAR

$
0
0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mhe. George Boniface Simbachawene leo Agosti 6, 2019 ametembelea Ofisi ya Makamu wa Rais Tunguu, Zanzibar na kuzungumza na watumishi ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kujitambulisha na kukagua miradi.

SIMA – Tutapunguza Matumizi ya Zebaki Nchini

$
0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima (wa pili kulia) akiangalia namna dhahabu inavyochenjuliwa na Bi. Mary Matiko Makorere kwa kutumia zebaki katika eneo la wachimbaji wadogo katika wa Mtaa wa Kebaga, Kata ya Kenyamanyori Wilayani Tarime. Serikali imeazimia kupunguza matumizi ya zebaki kwa wachimbaji wadogo kutokana na athari kwa binadamu na mazingira.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima akizungumza na wakazi wa Mtaa wa Kebaga, Kata ya Kenyamanyori Wilayani Tarime, Mkoa wa Mara ambao wanajishughulisha na shughuli za uchimbaji madini na kuchenjua dhahabu kwa kutumia zebaki. Naibu Waziri amewaeleza athari za matumizi ya zebaki na kuwataka kujiunga na vikundi rasmi ili waweze kunufaika na mikopo itolewayo na Serikali.
Mjiolojia kutoka Mkoa wa Mara Bw. Solomoni Mwambeje (kushoto) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Mussa Sima mara baada ya kutembelea mtambo maalumu wa kuchenjua dhahabu wa Kakulilo Tarime Mkoani Mara.
……………………….
Na Lulu Mussa,Tarime
Serikali imeandaa Mpango-Kazi wa Taifa wa Kupunguza Matumizi ya Zebaki kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu ambao umeainisha fursa mbalimbali zitakazowezesha sekta ya wachimbaji wadogo kuendelea na shughuli za uzalishaji wa dhahabu bila kuathiri sekta ya Mazingira nchini.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima mara baada ya kufanya ziara ya kikazi ya kukagua shughuli za hifadhi na usimamizi wa mazingira katika Wilaya ya Tarime Mkoani Mara hususan maeneo ya wachimbaji wadogo wa dhahabu.

Amezitaja fursa hizo kuwa ni pamoja na Upatikanaji wa masoko ya Dhahabu kupitia masoko ya madini ya mikoa yanayojengwa katika mikoa yote nchini; Upatikanaji wa mikopo midogo na ya kati kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu na Kuwezesha vikundi vya kinamama wanaojishughulisha na uchimbaji wa dhahabu kwa kutoa mafunzo kuhusu uchenjuaji salama na rafiki kwa mazingira na mikopo.

Naibu Waziri amesema Ofisi yake inaendelea kutoa elimu kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu kuhusu madhara ya zebaki kwa afya ya binadamu na mazingira na kuwataka wachimbaji wadogo kuchenjua dhahabu kupitia vituo mahiri saba (7) vya mafunzo na uchenjuaji wa dhahabu vinavyojengwa katika mikoa ya Simiyu, Mara, Kagera, Katavi, Mbeya, Ruvuma and Tanga na Geita chini ya Wizara ya Madini.

Amesema, Serikali imeona umuhimu wa kuungana na jumuiya ya kimataifa ili kuweza kukabiliana na madhara yatokanayo na matumizi ya Zebaki katika uchenjuaji wa dhahabu kwa wachimbaji wadogo na kuwaelimisha kutumia katika njia salama na rafiki wa mazingira ikiwemo matumizi ya ”gloves” wakati wa ukamatishaji na matumizi ya vigida wakati wa uchomaji wa dhahabu ili kudhibiti athari za mvuke wenye zebaki unaotokana na uchomaji wa dhahabu.

Akiwa katika Kata ya Kenyamanyori Mtaa wa Kebaga Naibu Waziri Sima amepata fursa ya kujionea shughuli za uchenjuaji wa dhahabu kwa kutumia zebaki ambayo imebainika kuwa na athari kwa afya za binadamu na mazingira kwa ujumla.

Akizungumza na wakazi wa Mtaa wa Kebaga Naibu Waziri Sima amesema zebaki inasababisha magonjwa ya ngozi, Moyo, Figo na kuharibu mfumo wa neva za fahamu endapo watumiaji hawatazingatia miongozo iliopo.
“Sisi kama Serikali lengo letu kubwa ni kuhakikisha tunawaelimisha wananchi wetu kwa kuwaambia madhara ya matumizi ya zebaki na kuwashawishi kutotumia zebaki kwa shughuli za uchenjuaji dhahabu” Sima alisisitiza.

Amesema njia kuu ambazo zinaweza kusababisha binadamu adhurike na Zebaki ni kupitia ngozi hususan wakati wa uchenjuaji wa dhahabu; kuvuta mvuke wa Zebaki; na kunywa maji na kula vyakula vilivyochafuliwa na Zebaki kwa kuwa hudumu katika mazingira kwa muda mrefu.

Zebaki ni metali pekee iliyo katika hali ya kimiminika ambayo hutumika katika sekta ya afya katika vifaa tiba, tiba ya meno na uhifadhi wa chanjo; uzalishaji viwandani kama vile vipodozi, viutatilifu na bidhaa mbalimbali ikiwemo betri, swichi, taa za umeme; na madini katika uchenjuaji wa dhahabu kwa wachimbaji wadogo.

SITA WANUSURIKA KIFO KATIKA AJALI YA NDEGE MAFIA-LYANGA

$
0
0


NA MWAMVUA MWINYI,MAFIA

WATU sita wamenusurika kifo kufuatia ndege ndogo iliyokuwa ikitoka wilayani Mafia ,mkoani Pwani kuelekea Jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa za awali zilizotolewa na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Rufiji ,Onesmo Lyanga zinasema hadi sasa hakuna kifo kilichoripotiwa,zaidi ya watu sita kujeruhiwa.

Lyanga alisema kuwa ndege hiyo ilikuwa ikitoka Mafia kwenda uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere.

“Ndege hiyo ndogo ilianguka ilipokuwa ikitaka kuruka na kurudi chini na kudababisha majeruhi hao ambapo hadi sasa hakuna ripoti ya mtu yoyote aliyefariki dunia,” alifafanua Lyanga.

Alieleza bado jeshi la polisi wako eneo la tukio kukagua na kufuatilia ajali hiyo na taarifa zaidi zitatolewa.

Viongozi watakiwa kuchukua hatua kunusuru wanafunzi wilayani Tarime

$
0
0
 Viongozi hususani wa Serikali kuanzia ngazi ya Kijiji wametakiwa kuchukua hatua ili kupambana na utoro kwa wanafunzi katika Shule mbalimbali za Msingi na Sekondari zilizopo Wilaya Tarime mkoani Mara unaochangia kudhorotesha kiwango cha elimu.

Rai hiyo ilitolewa jana Agosti 05, 2019 kwenye mdahalo wa utoaji elimu ya kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia na kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi hususani wa kike uliofanyika katika Kata ya Muriba wilayani humo.


Mdahalo huo ni sehemu ya utekelezaji kwa vitendo mpango mkakati wa kitaifa wa kupambana na aina zote za ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto (MTAKUWWA) ambapo Wilaya Tarime inatekeleza mpango huo kwa kushirikiana na shirika la kutetea haki za wanawake na wasichana (KIVULINI).Na George Binagi-GB Pazzo, Tarime
 Taswira ilivyokuwa kwenye kampeni ya kutokomeza ukatili wa kijinsia katika Kata ya Muriba wilayani Tarime.
 Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la KIVULINI, Yassin Ally akitoa elimu ya kupambana na ukatili wa kijinsia ikiwemo kuachana na mila ya ukeketaji kwenye mdahalo huo.
 Afisa Elimu Kata ya Muriba wilayani Tarime, Mwl. Kefa Odao akitoa rai kwa wazazi na walezi katika Kata hiyo kuacha kuwapangia majukumu watoto wao siku za masomo hatua inayochochea ongezeko la utoro mashuleni.
 Viongozi na watendaji mbalimbali wilayani Tarime wakifuatilia mdahalo huo.
 Waendesha bodaboda katika Kata ya Muriba wilayani Tarime waliunga mkono juhudi ya kupambana na ukatili wa kijinsia hususani kupambana na mimba na ndoa kwa wanafunzi.
 Wanaharakati wa kujitolea waliopewa mafunzo na shirika la KIVULINI kusaidia utoaji elimu ya kupambana na ukatili wa kijinsia ngazi ya jamii wakiongoza maandamano ya kufikisha ujumbe kwa jamii kuhusu kupinga aina zote za ukatili katika jamii.
 Wanaharakati wa kujitolea wakiwa wamebeba mabango yenye jumbe mbalimbali za kupinga aina zote za vitendo vya ukatili katika jamii.
 Wanafunzi wakitoa elimu ya kupambana na ukatili wa kijinsia kwa njia ya nyimbo.
Tazama Video hapa chini

MAAFISA WA BUNGE WATOA ELIMU KWENYE MAONESHO YA NANENANE

$
0
0
Afisa Sheria wa Bunge Ndg. Mossy Lukuvi akitoa Elimu kwa Wagenin waliotembelea banda la Bunge hii leo kwenye Maonesho ya Wakulima ya Nanenane yanayoendelea Jijini Dodoma.
Afisa Utafiti wa Bunge Ndg. Aziza Makwai akitoa Elimu kwa mgeni aliyetembelea banda la Bunge hii leo kwenye Maonesho ya Wakulima ya Nanenane yanayoendelea Jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Bunge)

BENKI CRDB YAENDELEA KUONGOZA KWA FAIDA SOKONI HUKU FAIDA YAKE IKONGEZEKA KWA ASILIMIA 98% KIPINDI CHA MWEZI JANUARI MPAKA JUNI 2019

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza na waandishi wa habari, wakati akitangaza faida ya TZS 86.65 bilioni  kwa kipindi cha mwezi Januari mpaka Juni 2019 ambayo ni ongezeko la asilimia  98%  kutoka  TZS 43.85 iliyoipata katika kipindi kama hicho mwaka uliopita  2018, katika mkutano uliofanyika leo kwenye hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam. Kushoto ni Afisa Biashara Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts na Kulia ni Mkurugenzi wa Fedha wa Benki hiyo, Fredrick Nshakanabo. 

Benki  ya CRDB imetangaza faida ya TZS 86.65 bilioni  kwa kipindi cha mwezi Januari mpaka Juni 2019 ambayo ni ongezeko la asilimia  98%  kutoka  TZS 43.85 iliyoipata katika kipindi kama hicho mwaka uliopita  2018.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema ongezeko la faida hiyo limetokana na kuimarika kwa mazingira ya biashara na jitihada binafsi za benki  na ongezeko pato litokanalo na biashara za fedha za kigeni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza na waandishi wa habari, wakati akitangaza faida ya TZS 86.65 bilioni  kwa kipindi cha mwezi Januari mpaka Juni 2019 ambayo ni ongezeko la asilimia  98%  kutoka  TZS 43.85 iliyoipata katika kipindi kama hicho mwaka uliopita  2018, katika mkutano uliofanyika leo kwenye hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam.

“Mwaka 2019 umekuwa na mafanikio kwa Benki ya CRDB. Mapato na faida yetu vimeongezeka kutokana na kuimarika kwa mapato halisi ya riba na mapato halisi yasiyo ya riba. Tulifanikiwa pia kuongeza kiwango cha mikopo huku tukishusha uwiano wa mikopo chechefu. Mikopo tuliyotoa kwa wateja iliongezeka sambamba na amana za wateja huku tukiwafikia wateja wapya kupitia huduma za kidijitali kama vile SimBanking, SIMAccount, mawakala wetu wa CRDB Wakala.  Pia mapato yetu yameongezeka kufutia kuongezeka kwa pato litokanalo na ubadlishaji wa fedha za kigeni”  amesema Nsekela. 

Akieleza zaidi kuhusu mafanikio hayo, Nsekela alisema: “Tunajivunia ukweli kwamba tupo kwenye uelekeo mzuri kufanikisha malengo yetu tuliyojiwekea. Lengo si kuyafikia tu, bali Tunakusudia kuyavuka. Tutaongeza kasi zaidi ya utendaji hususani  katika ubunifu na utoaji wa huduma za kidijiti zenye ubora wa juu. Tutaendelea  kuimarisha na kupitia mara kwa mara mifumo yetu ya utoaji huduma  kwa wateja ili kuhakikisha kuwa tunakidhi mahitaji ya soko.”
Mkurugenzi wa Masuala ya Kampuni na Mahusiano Benki ya CRDB, Tully Esther Mwampamba, Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa Benki ya CRDB, Prosper Nambaya na Mkurugenzi Rasilimali Watu Benki ya CRDB, Siophoro Kishimbo wakifatikia taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela.

Katika kipindi cha Januari mpaka Juni 2019, mapato halisi ya riba ya Benki ya CRDB yaliongezeka kwa asilimia 30% na kufika TZS 258 bilioni kutoka TZS 198 bilioni ziilizokusanywa katika kipindi kama hiki mwaka 2018. Huku rasilimali zikiongezeka kwa asilimia 8% kufikia shilingi 6.38 trilioni kulinganisha ni shilingi 5.93 zilizopatikana katika robo ya kwanza ya mwaka 2019. Pia amana za wateja wetu ziliongezeka kwa asilimia 15% kufikia TZS 4.95 trilioni kutoka TZS 4.32 trilioni zilizopatikana kwa robo ya kwanza ya mwaka huu” alisema Nsekela.

Bwana Nsekela alifafanua kwamba Benki ya CRDB bado inaendelea kuwa na umiliki wa asilimia 22% ya thamani ya soko la mabenki hapa nchini hii kutokana na kuwa na mtandao mkubwa wenye matawi 238, mashine za kutolea fedha 553 na Mawakala Zaidi ya 10,064 wa CRDB Wakala.

Maeneo muhimu ya ufanisi hadi kufikia Juni  2019
Amana za wateja ziliongezeka kwa asilimia 15%  na kufika TZS 4.95 trilioni kutoka TZS 4.32 trilioni kwa robo ya kwanza ya mwaka
Rasilimali za benki ilikua kwa asilimia 8% na kufika TZS 6.38 trilioni kutoka TZS 5.93 trilioni kwa robo ya kwanza ya mwaka.
Mapato ya riba yaliongezeka kwa asilimia 14% na TZS 315.4 bilioni kutoka TZS 276.8 bilioni za kipindi kama hiki mwaka 2018.
Mapato halisi ya riba yaliongezeka kwa asilimia 30% na kufika TZS 258 bilioni kutoka TZS 198 bilioni za kipindi kama hiki mwaka 2018.
Faida ghafi iliongezeka kwa asilimia 98% na kufikia TZS 86.6 bilioni kutoka  TZS 43.8 bilioni kipindi kama hiki mwaka 2018.
Faida halisi (baada ya kodi) ilikua kwa asilimia 108% na  kufikia TZS61.1 bilioni ikilinganishwa na TZS 29.3 bilioni kipindi kama hiki mwaka 2018.




WAJUMBE WA SADC KARIBUNI TANZANIA-SPIKA JOB NDUGAI

$
0
0
  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai akizungumza na  wakati wa hafla ya chakula cha jioni kwa ajili ya wajumbe wa wiki ya maonyesho ya bidhaa za Sadc jana jijini Dar es Salaam. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bw. Albert Jonkergouw akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha jioni kwa ajili ya wajumbe wa wiki ya maonesho ya bidhaa za Sadc.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
 Mwanamuziki Christian Bella akitoaa burudani  wakati wa hafla ya chakula cha jioni kwa ajili ya wajumbe wa wiki ya maonyesho ya bidhaa za Sadc jana jijini Dar es Salaam.  










WANANCHI SIMIYU WAFURAHIA HUDUMA ZA NHIF NANE NANE

$
0
0
Wananchi katika Mikoa ya Simiyu,  Mara na Shinyanga wamepongeza na kufurahia huduma zinazotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) katika maonesho ya Wakulima yanayofanyika Kitaifa mkoani Simiyu.

Huduma hizo ni pamoja na Usajili wa Wanachama,  elimu juu ya huduma za matibabu, upimaji wa afya bure na elimu ya kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti,  Mwenyekiti wa Chama cha Msingi cha Sandai Wilayani Bariadi Bw. Elisha Nkubira alisema kuwa huduma zinazotolewa na Mfuko zimewalenga wananchi wote wakiwemo wa kipato kikubwa na kipato kidogo.
 Ofisa Uhusiano wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),  Grace Michael akimuelekeza jambo mmoja wa wakazi wa Kata ya Nyakabindi, Bariadi mkoani Simiyu, waliojitokeza kupima afya zao katika Banda la NHIF, kwenye maonyesho ya Nane Nane, yanayoendelea Mkoani Simiyu.

"Huu Mfuko unafanya kazi kubwa sana na hizi huduma ambazo wanazitoa kwenye viwanja hivi hakika ni za mfano wa kuigwa na zimelenga kutusaidia Sisi wananchi ili tujue hali za Afya zetu na kuweza kujikinga na maradhi," alisema Bw. Nkubira.

Naye Mkazi wa Bunda Bw. Lameck Mwita ambaye pia ni mwanachama wa Mfuko alitoa wito kwa wananchi wengine kuchukua hatua ya kujiunga na huduma za NHIF ili kuwa na uhakika wa kupata matibabu wakati wote.
 Sehemi ya wakazi wa mkoa wa Simiyu, wakipima afya zao katika Banda la NHIF, kwenye maonyesho ya Nane Nane, yanayoendelea Mkoani Simiyu.

Alisema kuwa kitendo cha familia kuwa na kadi za matibabu za NHIF ni kinga kubwa ya kuepukana na umasikini kutokana na ukweli kwamba maradhi huja bila taarifa na gharama zake ni kubwa.

Naye Ofisa Uhusiano wa Mfuko,  Grace Michael aliwaomba wananchi kutumia fursa hii kutembelea banda la NHIF katika viwanja vya Nyakabindi ili kupata huduma lakini pia kujiunga na Mfuko kupitia makundi mbalimbali yakiwemo ya Toto Afya Kadi, Ushirika Afya, Mwanachama Binafsi na mengine.
"Mbali na hapa NHIF inashiriki pia katika Maonesho ya Nane Nane Kikanda katika mikoa ya Arusha,  Mbeya, Mwanza, Lindi na Morogoro hivyo wananchi wafike na wapate huduma," alisema Grace Michael.



BALOZI SEIF ALI IDDI AENDESHA KIKAO CHA KUTATHMINI HALI YA ELIMU UNGUJA.

$
0
0
Makamu wa Pili wa Raiswa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini “B” Nd. Makame Mwadini na Mkuu wa Wilaya hiyo Nd. Rajab Ali Rajab kabla ya kuanza Kikao cha kutathmini hali ya Elimu Wilayani humo.
Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Walimu Wakuu, Wenyeviti wa Kamati za Skuli, Madiwani Masheha na baadhi ya Maafisa wa Wilaya ya Kaskazini B hapo Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya Kinduni.
Mdau wa Elimu Mwakilishi wa Viti Maalum Mkoa Kaskazini Unguja Mh. Panya Ali Abdulla akitoa mchango katika Kikao hicho kilichosisitiza ushirikiano baina ya washirika wa Elimu Wilayani humo.
Mkurugenzi wa Elimu Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini “B” Maalim Moh’d Juma Makame akitoa ufafanuzi wa mabadiliko ya Mitaala inayowajibikiaWanafunzi kwenda nayo kwa wakati ili kufuzu vyema kwenye Mitihani yao ya Taifa.
Mdau wa Elimu Maalim Muhamed Ali Abduula akihimiza umoja na mshikamano katika mbinu na mikakati ya kuwafinyanga Wanafunzi kufanikiwa katika Mitihani yao.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar {SUZA} Bibi Rehema Abdulrahman akiwakumbusha Walimu kubadilika katika ufundishaji ili kwenda sambamba na mabadiliko ya sayansi na Tekenolojia Duniani.
Mkuu wa Wilaya ya Makaskazini “B” Nd. Rajab Ali Rajab akieleza mfumo utakaotumika katika kuunda Kamati Maalum ya Wilaya itakayosimamia Elimu ndani ya Wilaya hiyo.Picha na – OMPR – ZNZ.

NIDA Yawezesha Wakulima, Wavuvi na Wafugaji Kutambuliwa Kwenye Maonesho ya Nanenane

$
0
0
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), yashiriki maonesho ya 27 ya wakulima, wavuvi na wafugaji yanayoadhimishwa kitaifa katika viwanja vya Nyakabindi, wilayani Bariadi mkoani Simiyu. 

Maonesho hayo yenye kauli mbiu ‘Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa Ukuaji wa Uchumi wa Nchi’ yamelenga kutoa fursa kwa taasisi mbalimbali nchini za serikali na binafsi kutoa elimu hasa ya teknolojia wanazozitumia na namna zinavyoweza kuwasaidia wakulima katika kurahisisha utekelezaji wa majuku yao ya kila siku ya kilimo, ufugaji na uvuvi.
Meneja Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Bi. Julien Mafuru ameeleza kuwa NIDA imeshiriki kwenye maonesho ya Nanenane mwaka huu ili kutoa fursa kwa wakulima, wafugaji na wavuvi Kusajiliwa kwa ambao hawajawahi Kujitokeza Kusajiliwa popote nchini, waombaji kuangalia taarifa za maombi ya Usajili yalikofiki kwa waliokamilisha Usajili, Elimu juu ya namna ya kupata Nakala ya Kitambulisho cha Taifa kupitia tovuti ya NIDA ( www.nida.go.tz ), Matumizi ya Namba ya Utambulisho (NIN) na Kitambulisho cha Taifa, kukusanya maoni ya wateja kwa lengo la kupata mrejesho juu ya huduma zetu, kutangaza njia zetu mbalimbali tunazotumia kuwasiliana na wananchi pamoja na kutangaza ofisi zetu za Usajili zilizopo katika kila wilaya nchini.

Bi. Mafuru ameeleza kuwa mwitiko wa wananchi ni mkubwa hasa kundi la watu ambao waliokamilisha Usajili siku za nyuma, wengi wamefika katika banda la NIDA Na. 7 kwenye viwanja vya Nyakabindi na kupatiwa namba zao za Utambulisho wa Utaifa (NIN) kwa ambao zimeshatoka. Namba hizo zimewasaidia kutambulika na kuweza kufika pia katika mabanda ya wadau wetu walioko katika maonesho haya ili kupata huduma nyingine za kijamii na kiuchumi kama vile kusajili laini, kukata TIN, kufungua akaunti ya benki, kupata mkopo kwenye SACCOSS n.k.
Kwa Upande wake Bi Fatuma Odoyo, mwananchi mkazi wa Bariadi ameishukuru serikali ya awamu ya 5 kupitia NIDA kwa kusogeza huduma karibu na wananchi kupitia kutoa huduma za Usajili kwenye maonesho ya Nanenane kwani alikuwa bado hajafika kwenye ofisi za Usajili za NIDA kupata huduma hiyo. 

’Ndani ya maonesho haya niliposikia matangazo kwenye redio kuwa NIDA wapo nikafika kwenye banda lao na kuanza Kujisajili kwani nahofia laini yangu ya simu kufungwa muda wa ukomo ukifika wa kutakiwa kusajili laini ya simu kwa kutumia alama za kibaiolojia ambapo wanatuhitaji tuwe na namba ya NIDA’ Bi Fatuma amesema.
 Mmoja wa wananchi wa Mkoa wa Simiyu aliyejitokeza kujiandikisha ili kupata Kitambulisho cha Taifa akijaza fomu ya usajili.

Bi Careen Kuwite Afisa Msajili Mkoa wa Simiyu ameeleza kuwa wananchi hususan kundi la wakulima, wavuvi na wafugaji wanapotambuliwa katika mfumo wa Utambuzi unaosimamiwa na NIDA na kupatiwa Namba ya Utambulisho, kunawawezesha kupata huduma za kijamii kirahisi kama vile kupata ruzuku za pembejeo za kilimo, kusajili laini ya simu, kujisajili kwenye vyama vya ushirika (kwa wakulima, wavuvi na wafugaji), kufungua akauti ya benki, kupata msaada wa TASAF unaotolewa kwa kaya masikini, hati miliki ya kiwanja na nyumba, hati ya kusafiria ya kielekroniki, kusajili biashara na kampuni brela, kukata leseni ya udereva, kukopesheka kirahisi kwenye taasisi za fedha, kupata mkopo wa elimu ya juu kwa wanafunzi, kuomba ajira, malipo ya pensheni pamoja na huduma nyingine nyingi.
Baadhi ya Wananchi wa Mkoa wa Simiyu wakiendelea kupatiwa huduma ya kujisajili ili wapate vitambulisho vya taifa, walipotembelea banda ya NIDA katika maonyesho ya Nane Nane yanayoendelea katika uwanja wa Nyakabindi, Bariadi mkoani Simiyu leo.

Akihitimisha Bi. Julien amewasihi wakulima, wavuvi, wafugaji na wananchi wote kiujumla kujitokeza Kusajiliwa kwa wingi ili kupata Namba ya Kitambulisho cha Taifa kwa wakati. 

Aidha ameeleza kuwa wananchi watakaoshindwa kutumia fursa ya Kusajiliwa kwenye maonesho haya ya 27 ya Nanenane wafike kupata huduma katika ofisi za Usajili za NIDA zilizoko katika kila wilaya nchi nzima wakiwa wamekamilisha kujaza fomu za Usajili zinazopatikana serikali za mitaa, kwenye tovti ya NIDA na kwenye ofisi za Usajili za NIDA.

ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM DKT BASHIRU MISUNGWI

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ally akiangalia shughuli za uzalishaji wa mikanda ya Gypsum unavyofanyika katika kiwanda cha Idetemya wilayani Misungwi jana.Picha na Baltazar Mashaka.
Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally, akiwa nje ya jengo la ofisi ya CCM Tawi la Ng'ombe, baada ya kuweka jiwe la msingi, ujenzi ambao umegharimu sh. 8,835,000 ambapo Diwani wa Kata ya Igokelo lilipo tawi hilo Bernad Poly akichangis sh. milioni 2.3, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela na wasaidizi wake sh. milioni 2. Charles Kitwanga (Mbunge) akichangia mabati 80 yanayotakiwa kumalizia jengo hilo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Dk. Anthony Diallo (mwenye kofia) akimuongoza Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally (kushoto), baada ya kumaliza kukagua ujenzi wa ofisi ya CCM Tawi la Igokelo wilayania Misungwi. 
Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ally (kulia) akizungumza na Mbunge wa Misungwi, Charles Kitwanga 'Mawe Matatu' kushoto, kabla ya kuendesha harambee ndogo ya kuchangia ujenzi wa ofisi ya tawi la CCM Ng'ombe,Dk. Bashiru aliahidi kuchangia sh. milioni 2, huku Kitwanga alitoa mabati 80.
Mbunge wa Misungwi Charles Kitwanga 'Mawe Matatu' (kulia) wakiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM MKoa wa Mwanza, Dk. Anthony Diallo (kushoto)wakati wa mkutano wa Katibu Mkuu Dk. Bashiru Ally, wilayani Misungwi jana, katikati ni Mjumbe wa NEC mkoani humu, Jamal Abdul Babu. Picha na Baltazar Mashaka

Mlezi wa Mkoa wa Mwanza ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally, akizungumza na wanachama wa CCM na watendaji wa serikali wilayani Misungwi jana.Picha zote na Baltazar Mashaka .
Vijana wa Chipukizi wilayani Misungwi wakimvisha shada la maua, Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally baada ya kuwasili wilayani Misungwi mapokezi yaliyofanyika katika Kijiji cha Usagala jana.Picha na Baltazar Mashaka

WAFANYAKAZI WENGI HA WAZIJUI HAKI ZAO ZA UNYONYESHAJI NCHINI

$
0
0
Na Andrew Chale

IMEELEZWA kuwa wafanyakazi wengi  hapa Nchini hawazijujui haki zao za unyonyeshaji kutokana na dhana ya kutoelewa haki na wajibu wa sheria zilizopo.

Hayo yameelezwa leo Jijini Dar es Salaam wakati wa semina ya Waandishi wa Habari  katika wiki ya unyonyeshaji maziwa ya Mama iliyoandaliwa na Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC).

Akitoa mada juu ya kanuni ya kazi na unyonyeshaji  maziwa ya mama, kanuni ya mwaka 2017, amebainisha kuwa, Mwanamke na Mwanaume wote kwa pamoja wanazo haki za uzazi kwa kila mmoja kulingana na haki hizo hata hivyo baadhi yao hawazijui haki zao.

“Mwanamke mwajiriwa anazo haki za kutimiza majukumu yake ya uzazi na kufanya kazi au kuzalisha bila kubaguliwa, kubugudhiwa au kupoteza ajira.

Likizo ya uzazi ikiwa ni moja ya haki za uzazi, humpa mama muda wa kumuwezesha kutoa matunzo muhimu kwa mtoto miezi ya mwanzo ya maisha yake hii ikiwa ni pamoja na kumnyonyesha.

Vilevile likizo ya uzazi humpa mwanamke mmwajiriwa muda wa kupumzika na hivyo kusaidia mwili wake kurudi hali ya kawaida baada ya kujifungua.  Kwa mantiki hiyo, ni muhimu mwajiri na mwajiriwa kufahamu vizuri haki na wajibu wao katika utekelezaji wa sheria hiyo” Alieleza Nchimbi.

Nchimbi aliongeza kuwa, katika sheria mpya  Mwanamke mwajiriwa anapaswa kumfahamisha mwajiri wake nia ya kuchukua likizo ya uzazi angalau miezi mitatu kabla ya tarehe ya makisio ya kujifungua akiwa ameambatanisha vielelezo vya madaktari.

“Mama ana haki ya kupewa likizo ya uzazi sio chini ya  siku 84 yenye malipo. Kwa mama aliyejifungua mtoto zaidi ya mmoja (mapacha au zaidi) anapaswa kupewa likizo ya uzazi  ya siku  100 yenye malipo.
Mama  ana haki ya kuchukua likizo yake ya mwaka  (siku 28) katika mwaka huo huo aliyopata likizo ya uzazi. Aidha anaweza kujadilina na mwajiri kuunganisha likizo ya uzazi na ya mwaka” alieleza Nchimbi.

Aidha, sheria hiyo imefafanua kuwa, endapo mtoto huyo atafariki, Mwanamke ana haki ya kupewa tena likizo ya uzazi ya siku 84 yenye malipo endapo mtoto wake atafariki kipindi cha mwaka mmoja tangu kuzaliwa.

Katika sheria hiyo mpya pia imebainisha kuwa, mwajiri aharuhusiwi kumpa mwanamke mwenye mimba au anayenyonyesha  kazi zinazohatarisha afya yake au mtoto.

“Mwajiri anapaswa kumpa mwanamke mjamziti ama mwenye mtoto kazi mbadala bila ya kwenda tofauti ya mkataba au makubaliano ya ajira yake.

Kisheria mwajiri anawajibika kumpa mwanmke mwajiriwa likizo nne tu za uzazi katika kipindi chote cha ajira. Pia mwajiri haruhusiwi kumuachisha kazi mwanamke kutokana na sababu zinazohusiana na ujauzito au kujifungua” alieleza Nchimbi.

Hata hivyo Nchimbi alimalizia kuwa, Mama anayenyonyesha ana haki ya kupewa  muda wa saa mbili  kwa siku wakati wa kazi kwenda kulimsha ama kumnyonyesha mtoto wake.

“Hii kuongeza namna ya kumsaidia mama, mwajiri na mwajiliwa wanaweza kukubaliana kutenga muda katika saa mbili za wakati wa kazi, wao watakavyoona lakini pia kwa sasa kuna utararibu umeanzishwa baadhi ya ofisi kuwa na sehemu ya mama kunyonyesha mtoto kwa muda huo, akiwa kazini” alimalizia Nchimbi.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi idara ya Elimu ya lishe na mafunzo, Bi. Sikitu Simon amevipongeza vyombo vya habari nchini kwa kutoa ushirikiano namna ya kuripoti masuala ya lishe  kwani kupitia vyombo vyao ujumbe umekuwa ukifika kwa wakati.

“Navipongeza vyombo vya habari kwa namna vinavyofikisha habari muhimu juu ya lishe. Hivyo kupitia mafunzo haya yatakuwa chachu  kwenu kuendelea kuelewa vizuri na kwa kina ili mkawe mabalozi wazuri.
Milango ipo wazi watalaam wetu wapo hapa na mnakaribishwa muda wowote”alieleza Bi. Sikitu Simon.

Katika semina hiyo wanahabari kutoka vyombo mbalimbali waliweza kupata mafunzo yaliyowasilishwa kwa njia ya mada na watalaam wa taasisi hiyo huku pia wakipata wasaha wa kuuliza maswali na kujibiwa.

Afisa Utumishi wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, Maurice Nchimbi akiwasilisha mada juu ya likizo za uzazi kwa mwanamke wakati wa semina ya waandishi wa habari iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
  Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa  kwenyenye   semina hiyo.
Picha ya pamoja (Pichana na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

Bodi ya Utalii yaahidi 'kuibeba' Rock City Marathon

$
0
0


Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bw Geofrey Tengeneza (wa pili kushoto) akionyesha fulana maalumu ya mbio za Rock City Marathon msimu mwa mwaka 2019 kwa wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa mbio hizo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio, Bw Clement Mshana (wa pili kulia) Mratibu wa mbio hizo kutoka kampuni ya Capital Plus International (CPI), Bw Kasara Naftali (wa kwanza kulia) Pamoja na muwakilishi kutoka Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Bi Ombeni Zavara.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio, Bw Clement Mshana (Kulia) akizungumza kuhusiana na maandalizi ya mbio hizo. Wengine ni pamoja na Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bw Geofrey Tengeneza (Kulia kwake), muwakilishi kutoka Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Bi Ombeni Zavara (wa pili kushoto) pamoja Mshauri wa masuala ya Ufundi wa mbio hizo Bw John Bayo (Kushoto)

Waratibu wa mbio hizo kutoka kampuni ya Capital Plus International (CPI), Bw Kasara Naftali (kushoto) na Bi. Irine Lyimo wakionyesha muonekano wa T-shirts na medali maalumu kwa ajili ya msimu wa mwaka 2019 wa mbio za Rock City marathon.
Mshauri wa masuala ya Ufundi wa mbio hizo Bw John Bayo (kushoto) sambamba na mmoja wa raratibu wa mbio hizo kutoka kampuni ya Capital Plus International (CPI), Bi Irine Lyimo wakionyesha muonekano wa T-shirts maalumu kwa ajili ya msimu wa mwaka 2019 wa mbio za Rock City marathon.
Mojawapo ya medali zitakazotelewa kwa washiriki wa mbio za Rock City Marathon msimu wa mwaka 2019
Baadhi ya wakiambiaji (joggers) kutoka klabu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam wakifurahia muonekano wa Tshirts pamoja na medali maalumu kwa ajili ya mbio za Rock City Marathon msimu wa mwaka 2019 wakati wa hafla ya uzinduzi wa mbio hizo.



Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imeahidi kushirikiana na waandaaji wa mbio za Rock City Marathon ili kuhakikisha kuwa mbio hizo zinatumika vema kuutangaza utalii wa ndani hapa nchini.

Akizungumza hii leo jijini Dar es Salaam wakati wa unzinduzi wa msimu wa kumi (10) wa mbio hizo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Bi Devota Mdachi, Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa TTB,Bw Geofrey Tengeneza alisema adhma hiyo inasukumwa na malengo ya mbio hizo ambayo ni kutumia mchezo wa riadha katika kutangaza utalii hususani katika Ukanda wa Ziwa.

Hafla hiyo iliyofanyika kwenye viunga vya ofisi za TTB jijini Dar es Salaam ilihudhuriwa na wadau mbalimbali wa mchezo huo wakiwemo viongozi wa serikali pamoja na wadhamini mbalimbali wa mbio hizo.

"Kwa kuzingatia uzito wa malengo ya mbio hizi nitamke bayana kuwa TTB tupo tayari kushirikiana na waandaaji wa mbio hizi kuhakikisha kwamba mwaka huu mbio hizi zinafana na zinavutia washiriki wengi zaidi hususani wa kimataifa,'' alisema Bw Tengeneza.

Zaidi, Bw. Tengeneza pia alithibitisha ushiriki wake Pamoja na viongozi waandamizi wa bodi hiyo kwenye mbio hizo zinazoratarajiwa kufanyika Octoba 20, mwaka huu kwenye viunga vya jingo la kibishara la Rock City Mall, jijini Mwanza ambapo washiriki wa mbio hizo watapita katika barabara mbalimbali za jiji hilo kabla hazijamalizikia katika viunga hivyo.

Mbali na ushiriki huo, Bw Tengeneza pia alitoa pongezo kwa mashirika mbalimbali yenye dhamana ya utalii hapa nchini ikiwemo la Hifadhi za Taifa(TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)kwa kuwa sehemu ya wadau wakubwa wa mbio hizo hizo.

"Ukanda wa Ziwa una vivutio vingi ambavyo sisi kama kama chombo chenye dhamana ya utalii lazima tuendelee kuvitangaza kwa nguvu na kwa njia tofauti ikiwemo michezo,'' alisema Bw Tengeneza huku akivitaja baadhi ya vivutio hivyo kuwa ni pamoja na Kisiwa cha Saanane, Makumbusho ya kabila la Wasukuma pamoja na tamaduni za makabila ya wakazi wa Kanda ya Ziwa.

Mbio za Rock City Marathon zilizoanzishwa miaka kumi iliyopita zinazozidi kujiongezea umaarufu kila mwaka na tayari zimefanikiwa kuwavutia baadhi ya wadhamini ikiwa ni pamoja na kampuni za TIPER, Pepsi, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA).

Wadhamini wengine ni pamoja na kampuni ya uwakili ya Lis Law Chambers & Consultants, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), CF Hospital, Mwanza Water, Isamilo Lodge, Pigeon Hotel, Real PR Solutions Limited na Afrimax Strategic Partnerships Limited.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio hizo kutoka kampuni ya Capital Plus International waandaaji wa mbio hizo, Bw Clement Mshana alitoa wito kwa washiriki wa ndani hususani wa mikoa ya Kanda ya Ziwa pamoja na wadhamini kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mbio hizo ambazo kwa mwaka jana zilifanikiwa kuhusisha washiriki zaidi ya 3000.

Alisema mbio za mwaka huu zinatarajiwa kuhusisha washiriki wengi zaidi kutoka kila kona ya dunia ikiwemo Afrika, Ulaya, China, Mashariki ya Kati hususani Israel na Marekani huku akitoa wito kwa washiriki wa ndani kujisajili kwa wingi ili kuthibitisha ushiriki wao kwenye mbio hizo.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Mshauri wa masuala ya Ufundi wa mbio hizo Bw John Bayo alisema maandalizo ya mbio hizo kwasasa yamekamilika kwa asilimia 60 huku akitumia uzinduzi huo kuonyesha Tshirts na medali za zitakazotimika katika msimu wa mbio hizo kwa mwaka huu.

MAONESHO YA VIWANDA NA TAASISI MBALIMBALI KATIKA MKUTANO WA SADC NDANI YA VIWANJA VYA KARIMJEE JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Baadhi ya wananchi wakitembelea maonesho ya viwanda na taasisi mbalimbali katika Mkutano wa SADC m katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
















wananchi wakiendelea  kutembelea  mabanda mbalimbali katika Mkutano wa SADC  katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv) 

GST YAENDELEA KUTOA ELIMU KWA UMMA NA WADAU WA SEKTA YA MADINI KATIKA WIKI YA MAONESHO YA VIWANDA SADC.

$
0
0
Pichani wadau mbalimbali wakipata maendelezo kutoka kwa wataalam wa GST ndani ya Banda la Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) katika maonesho ya Jumuhiya ya nchi za maendeleo kusini mwa Afrika(SADC) yaliombatana na maonesho ya wiki ya viwanda. 
Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) , yaendelea kutoa elimu kwa wadau wa sekta ya madini nchini katika maonesho ya wiki ya viwanda yanayoendelea katika mkutano mkuu wa 39 wa Nchi za Jumuhiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). 

Moja ya elimu inayotolewa na GST ni juu ya kazi za utafiti wa jiosayansi kwa maana ya jiolojia , jiokemia , jiofikia , miamba na madini nchini ikiwemo madini ya viwandani , madini nakshi (Dimension Stone), elimu nyingine ni juu ya uwepo wa madini ya ujenzi nchini. 

Sambamba na elimu hiyo GST ipo na machapisho mbalimbali ya vitabu vya utafiti wa jiosayansi kama vile kitabu cha Madini yapatikanayo Tanzania toleo la nne kitabu hiki kinaelezea uwepo wa madini kuazia ngazi kijiji mpaka taifa. 

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA MGENI RASMI SIMBA DAY

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia mashabiki na wapenzi wa timu ya Soka ya Simba wakati alipoingia kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuwa mgeni rasmi katika Simba Day, Agosti 6, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Simba Day kwenye uwanja Taifa jijini Dar es salaam, Agosti 6, 2019. Wa tatu kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, Kulia ni Mwekezaji wa Simba, Mohammed Dewji na kushoto ni Rais wa TFF, Wallece Karia. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

TCRA yawataka Wananchi waliopata changamoto ya mawasiliano kwenda Maonesho kupata ufumbuzi.

$
0
0
Wananchi wa mkoa wa Arusha na maeneo ya jirani wamehimizwa kutumia fursa ya maonyesho ya 88 yanayoendelea kusajili upya namba zao za simu na kuthibitisha kwa njia ya kibiometria kwani huduma hiyo inapatikana katika maonyesho pamoja na waliopata changamoto ya mawasiliano kwenda katika kupata ufumbuzi.

Akizungumza katika Banda la maonyesho la Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) kanda ya Kaskazini Mkuu wa kanda Hiyo Mhandisi Imelda Salum amesema TCRA ikishirikiana na makampuni ya simu wamehakikisha kuwa huduma hiyo inakuwepo kurahisisha na kusogeza huduma kwa wananchi.

Amesema sambamba na huduma hiyo TCRA pia inatoa elimu ya matumizi bora na salama ya huduma za mawasiliano na kuwataka wananchi wenye matatizo wafike bandani hapo kwa ajili ya ushauri.
 Wanafunzi wakipata elimu ya mawasiliano katika banda la TCRA katika Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kaskazini mkoani Arusha
 Wananchi wakipata huduma katika Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kaskazini mkoani Arusha.
 Wanafunzi  na Wananchi wakipata wakipata maelezo katika banda la TCRA katika Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kaskazini mkoani Arusha.
Afisa wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Noah Lalataika akimpa maelezo huduma mwananchi aliyetembelea Banda la TCRA katika Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kaskazini Mkoani Arusha.
Viewing all 109921 articles
Browse latest View live




Latest Images