Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

KAWAMBWA AMUANGUKIA RAIS DKT.MAGUFULI KURIDHIA KUWAPATIA WANANCHI ARDHI YA RAZABA

$
0
0




NA MWAMVUA MWINYI,BAGAMOYO

MBUNGE wa Jimbo la Bagamoyo,mkoani Pwani ,dkt Shukuru Kawambwa ameungana na wakazi wa Matumbini ,kata ya Makurunge, kumuangukia Rais.dkt John Magufuli ili kuwapatia hekta 12,000 zilizobaki katika eneo la RAZABA waweze kuishi na kufanya shughuli za kimaendeleo.

Aidha wameshtushwa kuona eneo hilo ambalo bado lipo mkononi mwa serikali huku upande wa ardhi ukiwa umemegwa na kupatiwa kanisa la KKKT ushirika wa Kimanga.

Kawambwa alimuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,asikilize kilio hicho wakati alipokuwa katika ziara yake ya jimbo, Matumbini kata ya Makurunge ambapo wananchi walisema kero kubwa ni ukosefu wa ardhi ya makazi .

Alieleza, awali eneo hilo lilikuwa na hekta 55,000 ambayo serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliipatia ranchi ya Zanzibar (RAZABA) kwa ajili ya ufugaji ng’ombe ambapo baadae ilishindwa kuendelea na shughuli hiyo.

Kawambwa alifafanua, kipindi cha Rais mstaafu Dkt.Jakaya Kikwete alifanikiwa kuzirejesha hekta 22,000 kati ya 55,000 na kupatiwa kampuni ya Eco Energy kwa ajili ya mradi wa miwa.

“Alipostaafu kikaingia kipindi cha awamu ya tano ,ambapo kilibaini Eco Energy nao wanasuasua na uendelezaji wa eneo hilo na kuamua kuhamisha umiliki huo na kupewa BAKHRESA hekta 10,000 kati ya 22,000 kwa ajili ya kiwanda cha sukari na kilimo cha miwa “

“Juhudi zilishafanyika miaka miwili sasa ,kwa kumuomba mkurugenzi aandike barua kwa waziri mwenye dhamana ,na alifanya hivyo kwa kuomba hekta 3,000 ,lakini sisi tunaomba huruma ya Rais, atupatie hekta zote 12,000 sawa na hekari 30,000 ili wananchi hawa waondokane na kero na mgogoro huu,alisisitiza Kawambwa.

Baadhi ya wakazi wa Matumbini akiwemo Mwanaharusi na Sp Kisura walisema ,Rais dkt Magufuli ni mtetezi wa wanyonge basi awaangalie na wao kwani wameteseka kipindi kirefu.

Walielezea, kutokana na kuishi eneo hilo kwa miaka mingi huku wakihamahama wanaendelea kuomba eneo lililobaki baada ya kumegwa kwa Bakhresa ili waishi kwa amani.

Sp Kisura alisema ,hawatambuliki, lakini cha kushangaza kuna kitongoji kiitwacho RAZABA na wakati wa uchaguzi ukifika hutakiwa kufanya uchaguzi ,hivyo ni vyema wakatambulika kwa kupatiwa ardhi hiyo.

Kwa upande wake ,mwenyekiti wa kamati ya mashamba KKKT ushirika wa Kimanga, aliwaambia wananchi kwamba,wao wamefuata taratibu zote hadi kwa waziri wa ardhi na wamepatiwa kihalali eneo hilo.

Ndipo mbunge wa jimbo hilo aliposimama tena,na kuwataka wasiendelee na shughuli zozote,waende ofisini kwake ili apate uhakika kwa waziri waliomtaja kwani eneo hilo lipo chini ya serikali.

RAIS MAGUFULI ATOA UJUMBE MZITO KWA WANAJUMUIYA YA SADC

$
0
0
*Asema waafrika tulichelewa sana, sasa tunatakiwa kukimbia wakati wenzetu wakitembea.

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

RAIS Dkt.John Joseph Magufuli leo Agosti 5 amezindua rasmi wiki ya maonesho ya viwanda ikiwa ni katika kuelekea mkutano mkuu wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo wa nchi za Kusini mwa Afrika unaotarajiwa kufanyika nchini na kuwakutanisha wakuu wa nchi 16 ambao watakaa kwa siku mbili na kujadili masuala mbalimbali ya kiuchumi na kijamii yanayolenga kuimarisha jumuiya iyo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Rais Magufuli amezipongeza nchi wanachama kwa hatua wanazoendelea kuchukua katika kutekeleza mkakati wa Maendeleo wa 2015/2063 na kuwahimiza wanachama kuwa na umoja na kushirikiana na sekta binafsi ambazo kwa kiasi kikubwa zinachangia katika maendeleo.

Ujumbe mkubwa alioutoa Rais Magufuli kwa nchi wanachama ni pamoja na kukuza na kuendelea ubunifu kwa bunifu mbalimbali katika nchi zao na sio kukimbilia wataalamu kutoka nje pekee na hiyo ni  pamoja na kuweka mazingira wezeshi ya kibiashara kwa kuhakikisha kuna umeme wa uhakika na wa bei nafuu huku akitolea mfano Tanzania ambayo kwa sasa inatekeleza mradi mkubwa ya umeme kutoka bonde la mto Rufiji utakaozalisha zaidi ya megawati 2000 pamoja na ujenzi wa reli itakayounganisha Mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Magharibi mwa Tanzania na nchi jirani za  Rwanda na Burundi.

Mbali ya hilo ushauri mwingine alioutoa Rais Magufuli kwa nchi wanachama wa SADC ni kuweka vipaumbele kwa viwanda vya ndani ya jumuiya kwa kuuziana bidhaa na malighafi ili kuweza kuendelea zaidi na kukua kiuchumi kwa nchi zote za SADC.

Vilevile Rais Magufuli amezishauri nchi wanachama wa SADC kutoa vikwazo vinavyokwamisha kufikia maendeleo kwa urahisi zaidi na hiyo ni pamoja na utitiri za kodi, kuwepo kwa taasisi nyingi za usimamizi na sheria kali za udhibiti wa mipaka zinazowakwamisha wafanyabiashara kusafirisha bidhaa zao kutoka nchi moja hadi nyingine.

Magufuli amesema kuwa lazima nchi za jumuiya ya SADC zibadilike kwa kujenga viwanda vyetu wenyewe na kutumia malighafi zinazozalishwa katika  nchi zetu;

" Kuna upotevu mkubwa sana wa fedha za kigeni unaotokana na kuagiza bidhaa kutoka nje, bora tutumie fedha hizo katika kutekeleza miradi ya kimaendeleo. Tanzania tumeweka mkakati wa kujenga viwanda na kutumia malighafi tunazozalisha na kwa miaka mitatu ya uongozi wa serikali ya awamu wa tano zaidi ya viwanda vipya  4000 vimeanzishwa ni vyema nchi wanachama tukajizatiti katika hilo ili tufikie maendeleo" ameeleza Rais Magufuli.

Rais Magufuli amewashauri wanajumuiya iyo kuitumia wiki ya viwanda kwa kubadilishana uzoefu ili kuweza kufikia malengo na kuhimiza majadiliano yatakayofanyika katika wiki hiyo yafanyike wazi bila kuficha na yalete mapinduzi ya kimaendeleo na amewaalika wageni kutembelea vivutio vingi vinavyopatikana nchini zikiwemo mbuga za wanyama, mlima Kilimanjaro na kutalii katika visiwa vya Zanzibar.

Azania Benki yatangaza washindi wa promosheni ya ‘AMSHA NDOTO’

$
0
0
Meneja wa Mauzo ya Reja Reja wa Benki ya Azania, Jackson Lohay (katikati) akiongea kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa promosheni ya ‘Amsha Ndoto’ katika droo iliyofanyika katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam. Jumla ya Sh. 8,000,000/- ilitolewa kwa washindi watatu walioshiriki katika promosheni hiyo.
Benki ya Azania (ABL) leo imewatangaza washindi wa promosheni yake ya ‘Amsha Ndoto’ ambayo ina lengo la kuwahamasisha wateja wake na umma wawatanzania kujenga utamaduni wa kuweka akiba itakayowasaidia kuwa na maisha ya baadaye yaliyo imara kifedha.

Promosheni hii ambayo ni ya mizezi mitatu ilianza rasmi tarehe 27/06/2019 na inatarajia kufikiatamati tarehe 27/09/2019 huku ikihusisha wateja wa Azania Benki wa zamani na wale wapya naimejikita zaidi katika bidhaa mbili kuu za uwekaji akiba, ambazo ni: Ziada Akaunti pamoja naWatoto Akaunti.

Akitangaza washindi kwenye droo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam, Meneja wa Mauzo ya RejaReja wa Benki ya Azania, Jackson Lohay, amesema benki imetimiza ahadi ya kuwapatia zawadiwashindi walioshoriki kwenye promosheni na kwamba zawadi wanazopewa zitawasaidiakutimiza ndoto zao.

Kwa mujibu wa Lohay, washindi wa mwezi Julai wa promosheni hii ambao wamepatikana baadaya droo kufanyika ni;

1. Barakaeli Mmari amejishindia kiasi cha TZS 2,000,000/- (Arusha)
2. Rose Anaeli amejishindia kiasi cha TZS 3,000,000/- (Dar es Salaam)
3. Ketus Isack Malekamo amejishindia kiasi cha TZS 3,000,000/- (Tunduma)

Lohay ameongeza kuwa ili mtu aweze kushiriki kwenye promosheni ya Amsha Ndoto ni lazimakwanza awe mteja wa Azania Benki mwenye akiba ya kiasi kisichopungua TZS 1,000,000 ambayeanapewa tokeni zinazomwezesha kufuzu kwa ajili ya droo ya mwisho inayowapata washindi.

Wanaobahatika kushinda watafurahia riba ya 6% katika kipindi chote cha kampeni na mwakamzima.Akitoa pongezi kwa washindi wa promosheni, Lohay amewahasa wateja wa ABL kushiriki kwawingi na kwamba wana nafasi kubwa ya kujishindia zawadi lukuki katika droo zinazofuata hukuwakijahakikishia kuwa na akiba ya kutosha kwenye akaunti zao kwa ajili ya matumizi yao ya sikuza usoni.

“Tunawahamasisha wazazi wote na walezi kuwafungulia Watoto wao ‘Watoto Akaunti’ ili kuwana uhakika wa maisha yao ya baadaye yaliyo salama. Kwa namna hii hawatahangaika kutafutanamna gani ya kuwaandaa watoto wao kwa maisha ya baadaye kwani akaunti hii inaweka msingiwa kuwaandaa watoto kujifunza namna ya kuweka akiba kuanzia kwenye umri mdogo”,amesema Lohay.

Promosheni hii, yenye kaulimbiu: ‘Weka Akiba Ushinde Tumuwezeshe ada ya shule’,inawasilishwa kupitia mitandao ya kijamii na tovuti za ndani za benki. Benki pia imetengenezatovuti ndogo, maalumu kwa wateja wapya kujiunga na inaweza kupatikana kupitiaamshandoto.com

BANDA LA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI MAONESHO NANENANE SIMIYU 2019, LAVUTIA WANANCHI

$
0
0

Afisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mkaguzi Joseph Mwasabeja
(kulia) akitoa elimu ya kukabiliana na majanga ya moto kwa
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega Bwa. Anderson
Njiginya (wapili kulia) na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Itilima Bi. Elizabeth Gumbo (wapili kushoto), walipotembelea Banda la
Maonesho ya Nanenane simiyu. Picha na Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji
Afisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mkaguzi Joseph Mwasabeja
(kulia) akitoa elimu ya mfumo wa kung,amua moshi kwa Mkurugenzi
Halmashuri ya Wilaya ya Maswa Dkt. Fredrick Sagamiko (kushoto) na
Mkurugenzi wa Halmashuri ya Wilaya ya Bariadi (SACF) Jemes John
(kulia), walipotembelea Banda la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
Maonesho ya Nanenane simiyu. Picha na Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji

Afisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mkaguzi Joseph Mwasabeja
(kulia) akitoa elimu ya kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya moto
kwa Mwenyekiti Halmashauri Kuu CCM Mkoa wa Simiyu Bwa. Ahmed
Abdi, alipotembelea Banda la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Maonesho
ya Nanenane simiyu. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

Afisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mkaguzi Joseph Mwasabeja
(kulia) akitoa elimu ya kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya moto
kwa Wakazi wa Mkoa wa Simiyu Bariadi na Mikoa ya Jirani,
walipotembelea Banda la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Maonesho ya
Nanenane simiyu. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (Simiyu) Konstebo Magreth
Mabago (kusho) akitoa elimu ya kinga natahadhari dhidi ya majanga ya
moto kwa wanafunzi wa Simiyu Sekondari walipotembelea Banda la
Maonesho ya Nanenane simiyu. Picha na Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji

Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Konstebo Robert Mates akitoa
elimu ya kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya moto kwa wanafunzi
wa Shule ya Sekondari Banemhi, walipotembelea Banda la Maonesho
ya Nanenane simiyu. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

WIZARA YA AFYA KUDHIBITI KIFUA KIKUU MAGAREZA 15 NCHINI

$
0
0
Na. Catherine Sungura, WAMJW-DSM.

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto kupitia Mpango wa Taifa wa kudhibiti kifua kikuu na Ukoma kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza nchini wanaanza afua ya ufuatiliaji wa kutathimini hali ya huduma za kutokomeza kifua kikuu katika magereza nchini.

Hayo yamesemwa na Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Jeshi la Magereza (CP) Owesu Ngalama wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa maofisa wa jeshi hilo yanayofanyika kwenye bwalo la magereza ukonga jijini hapa.

CP Ngalama alisema kuwa afua hiyo itasaidia jeshi la magereza kuweza kubaini hali ya TB kwenye magereza kwani wanaoingia kwenye magereza ni wana jamii hivyo itasaidia kubaini ugonjwa huo kwa wafungwa na kwa jamii kwa ujumla.

“Ugonjwa huu unaambukizwa kwa hewa hivyo kwa tathimini hii itasaidia kuleta utaalam mkubwa kwa wataalam wetu wa tiba waliopo kwenye jeshi kwani hali ya TB sio kubwa kwenye magereza ila lengo ni kuhakikisha hakuna maambukizi makubwa kwani wafungwa wanaingia na kutoka”.Alisema CP Ngalama 

Aidha,ameishukuru wizara ya afya kwa kuendelea kushirikiana nao kwa muda mrefu hususan kwenye utoaji huduma za afya ikiwemo utoaji wa dawa,vifaa na vifaa tiba pamoja na masuala ya lishe kwenye vituo vya afya vilivyopo kwenye magereza nchini.

Naye Meneja Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma (NTLP) kutoka Wizara ya Afya Dkt. Beatrice Mutayoba alisema ugonjwa wa Kifua Kikuu bado ni jangwa kwani bado kuna takribani watu laki moja na elfu hamsini na nne wanakadiriwa kuugua kifua kikuu kila mwaka na inakadiriwa vifo elfu ishirini na saba kila mwaka nchini.

Dkt. Mutayoba alisema kifua kikuu kinaweza kumpata mtu yeyote kwani maambukizi yake ni ya njia ya hewa hivyo yapo makundi hatarishi zaidi ikiwemo magereza hivyo wanaweka jitihada zaidi kuyafikia makundi hayo ili kutokomeza kifua kikuu ifikapo 2030.

“kama nchi tumepiga hatua kubwa sana kutokomeza ugonjwa huu hivyo tunaongeza juhudi zaidi kwenye makundi hatarishi ikiwemo magereza,migodini,wavuvi ili kuwafikia kwa karibu na kuhakikisha tunapunguza maambukizi ndani ya magereza na maeneo haya”.

Alisisitiza Hata hivyo alisema mkakati wa kudhibiti kifua kikuu upo kwa wananchi wote hivyo kama mpango wanaendelea kutoa elimu kwa watanzania wote mara waonapo dalili waende kwenye vituo vya afya kwani wizara ya afya inatoa dawa,vipimo na huduma za kifua kikuu bila malipo kwenye vituo vya kutolea huduma za afya “Magerezani tunaweza utaratibu kwa wanaoingia kuwe na taratibu za uchunguzi ili anapokutwa na kifua kikuu waanze matibabu kwani unapoanza matibabu ndani ya wiki mbili huwezi kuambukiza wengine”.

Alisema Dkt. Mutayoba Mikoa kumi na tano itakayoanza na utekelezaji huo ni pamoja na Dar es salaam, Dodoma, Iringa, Kagera, Kilimanjaro, lindi, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Pwani, Shinyanga, Singida, Tabora na Tanga.
Kamishna wa Sheria na Uendeshaji Owesu Ngalama(katikati) akiwa na Mganga Mkuu wa Magereza ,SACP Dkt.Hassan Mkwiche na Meneja Mpango wa Taifa wa Kudhibi Kifua Kikuu na Ukoma Dkt.Beatrice Mutayoba kwenye mafunzo ya tathimini na udhibiti wa TB kwenye magereza nchini
Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Jeshi la Magereza Owesu Ngalama akifungua mafunzo ya tathimini ya udhibiti wa TB katika Magereza 15 nchini
Meneja Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma Dkt.Beatrice Mutayoba akiongea na washiriki wa mafunzo hayo(hawapo pichani) kwenye bwalo la Magereza Ukonga
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza mgeni rasmi(hayupo pichani) kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo
Picha ya pamoja ya mgeni rasmi na washiriki wa mafunzo hayo ambayo yana lengo la kuyafikia magereza kumi na tano hapa nchini katika kutathimini hali ya huduma ya TB kwenye magereza nchini

FCF yawataka Wakulima kutumia nyuki kudhibiti tembo na kibiashara

$
0
0
Wananchi wakiwa katika banda la Taasisi ya Friedkin Conservation Fund(FCF), lililopo katika viwanja vya Maonesho ya Nane Nane Nyakabindi, Mkoani Simiyu.
Wananchi wakiwa katika banda la Taasisi ya Friedkin Conservation Fund(FCF), lililopo katika viwanja vya Maonesho ya Nane Nane Nyakabindi, Mkoani Simiyu.


Mwandishi wetu,Babati.

Wambao wanaoishi katika maeneo ambayo yamekuwa yakivamiwa na tembo, wameshauri kutumia nyuki kudhibiti tembo lakini, pia kunufaika na biashara ya asali kutokana na nyuki hao.

Afisa Uhifadhi wa taasisi ya Friedkin Conservation Fund(FCF), Julius Robinson ametoa wito huo, leo wakati akizungumza na wakulima, katika banda la taasisi hiyo, katika maonesho ya Nanenane kitaifa, viwanja vya Vyakabindi wilayani Bariadi mkoa wa Simiyu.

Robinson amesema,Nyuki wanafaida kubwa,kama wakitumiwa vizuri na wafugaji, hasa katika udhibiti wa tembo na kupata asali kwa takriban mwaka mzima.

"kutokana na umuhimu wa nyuki FCF tumekuwa na mradi wa kuwapa mizinga ya kibiashara wananchi wanaoishi wilayani Meatu, ambapo taasisi hii imewekeza katika shughuli za utalii wa picha na uwindaji kupitia kampuni ya Mwiba Holding na nyingine "alisema

Alisemaa hadi sasa mizinga zaidi ya 100 imetolewa kwa vikundi vya ufugaji nyuki, wilayani Meatu mkoa wa Simiyu na sasa vinapata asali lakini mazao yao hayavamiwi na Tembo.

Akizungumza katika banda hilo, Afisa nyuki wa wilaya ya Serengeti, Fares Mwacha alisema mizinga ambayo inatolewa na FCF ni rafiki kwa ufugaji wa nyuki na mfugaji anaweza kuvuna asali mwaka mzima bila nyuki kuhama katika eneo lake.

"hii mizinga ni ya kisasa na unaweza kuvuna asali bila kuuwa nyuki ama nyuki kuhama lakini, pia unaweza kuwatumia nyuki kuzuia wanyama kama Tembo kuvamia shamba lako"alisema.John Masunga mkazi wa Meatu kijiji cha Makao, anasema tangu wameanza kutumia mizinga hiyo, wamekuwa wakivuna asali lakini pia wanadhbiti Tembo, kutokana na kuweka mizinga pembezoni mwa mashamba yao.

Taasisi ya FCF kupitia kampuni zake imewekeza katika eneo la jumuiya ya hifadhi ya jamii ya Makao na pori la akiba la Maswa, wilayani Meatu ambapo kwa mwaka licha ya kutoa misaada katika vikundi vya kijamii, imekuwa ikitoa zaidi ya sh 500 milioni kuchangia miradi ya maendeleo.

WANAJUMUIYA YA SADC WAKUNWA NA UTENDAJI KAZI WA RAIS MAGUFULI WAOMBA ZIADA YA UMEME KUTOKA MTO RUFIJI

$
0
0

*Yashauriwa fursa kutolewa kwa wanawake kutokana na utendaji wao wa kazi.

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

NCHI za jumuiya ya maendeleo za Kusini mwa Afrika (SADC) wameshauriwa kuitumia wiki ya viwanda katika kutafuta masoko ya uhakika pamoja na kufanya tathimini ya walikotoka na wanapoelekea hasa katika kuiangalia mazingira wezeshi ya biashara, miundombinu na nishati hasa umeme kupitia vikao mbalimbali vitakavyofanyika katika wiki ya viwanda iliyoanza leo kwa kuzinduliwa rasmi na Rais Dkt.John Joseph Magufuli.

Akizungumza katika uzinduzi huo katibu mtendaji  wa jumuiya ya maendeleo wa nchi za Kusini mwa Afrika Dkt. Stergomena Tax amesema kuwa jumuiya hiyo inajukumu la kuongeza kasi ya ukuaji wa viwanda kwa kuweka mazingira wezeshi hasa kwa kuhakikisha kuna uhakika wa nishati hasa umeme pamoja na miundombinu.
"Hatuwezi kushindana katika soko la biashara la kimataifa kama hatuna umeme wa uhakika na wanajumuiya ya SADC tunampongeza Rais Magufuli kwa jitihada zake za dhati za kuhakikisha suala la nishati linakuwa imara zaidi kwa kutafuta vyanzo mbalimbali vya umeme" ameeleza Dkt.Tax.

Aidha Dkt. Tax amemuoamba Rais Magufuli ziada ya umeme utakaobaki katika mradi wa umeme wa bonde la mto Rufiji ukasaidie nchi nyingine za SADC ambazo zina uhaba wa nishati ya umeme na kushauri nchi wanachama kufanya kazi kwa kushirikiana na sekta binafsi ili kuweza kukuza uchumi kwa nchi wanachama pamoja na kuimarisha uwekezaji na uhuru wa kusafiri kwa wafanyabiashara ndani ya nchi wanachama wa SADC.

Vilevile Dkt. Tax amewashauri watanzania kuitumia vyema wiki ya viwanda kwa kushirikiana na wizara ya viwanda na biashara ili waweze kutengeneza masoko ya uhakika pamoja na kubadilishana ujuzi kutoka kwa wafanyabiashara kutoka nchi 16 washirika zenye zaidi ya watu milioni 300.

Kwa upande wake Waziri mwenye dhamana ya Viwanda na biashara Innocent Bashungwa amesema kuwa maonesho ya nne ya wiki ya viwanda yanaendelea vyema na wadau wengi wa sekta za umma na zile binafsi wamejitokeza kwa wingi hali iliyochangiwa na elimu kuhusiana na fursa za ugeni wa SADC.

" Zaidi ya washiriki 3000 wamejitokeza huku idadi kubwa ikiwa ni watanzania na Kati yao waoneshaji wa bidhaa wazawa ni 1401 na 172 ni waoneshaji kutoka nje hii ni ishara njema na mapinduzi ya maendeleo hasa katika umoja wetu na siku ya ijumaa wageni wetu watatembelea viwanda kadhaa ndani ya nchi na visiwani Zanzibar" ameeleza Bashungwa.

Aidha Waziri Bashungwa amewataka jumuiya ya taasisi ya sekta binafsi nchini na shirikisho la wenye viwanda (CTI)  kuchangamkia fursa hiyo kwa kuhakikisha mkutano huo unaacha alama nchini hasa kwa kuwepo kwa masoko pamoja na kubadilishana ujuzi kutoka kwa wafanyabiashara washirika kutoa nchi za SADC.

Awali akitoa salamu kutoka serikali ya Namibia mwenyekiti wa  baraza la biashara la SADC Charity Mwiya amesema kuwa jumuiya hiyo haiwezi kuongelea maendeleo Kama kundi jingine (wanawake) litatengwa na kuwashauri wanawake kutumia fursa kwa kuwa wanaaminika zaidi katika utekelezaji.

Pia Charity ameipongeza serikali ya Tanzania chini ya uongozi wa Dkt. John Joseph Magufuli  kwa kushiriki vyema katika shughuli za kimaendeleo na kuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi 5 zinazokuwa kiuchumi barani Afrika. Na amewashauri wanachama wa umoja huo kushirikiana na sekta binafsi ili kuongeza kasi ya kuyafikia maendeleo.

Ufunguzi huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya nchi huku wafanyabiashara wengi wakijitokeza kuonesha bidhaa zao katika viwanja vya ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere, Karimjee, na Gymkhana jijini humo.

Rais Magufuli atembelea Banda la CRDB katika Mkutano wa SADC

$
0
0
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alipotembelea banda la benki hiyo lililopo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, kunakofanyika mkutano mkuu wa SADC, alipofika kufungua Maonyesho ya  Awamu ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) . Katikati ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki hiyo, Tully Mwambapa. Benki ya CRDB ni mmoja wa wadhamini wakuu wa mkutano wa SADC 2019.


BARAZA LA KILIMO TANZANIA KUHAKIKISHA LINAWASAIDIA WAKULIMA ILI KUPATA TAARIFA SAHIHI ZA PEMBEJEO

$
0
0

Naibu waziri wa Wizara ya Maji Mh Juma Aweso, akizungumza mara baada ya kutembelea Banda la Maonyesho la Baraza la Kilimo Tanzania katika viwanja vya Maonyesho ya wakulima nanenane Kanda ya Mashariki yanayofanyika Mkoani Morogoro.


Baraza la Kilimo Tanzania kuhakikisha linawasaidia wakulima ili wapate taarifa sahihi kuhusu pembejeo hasa mbegu ili waweze kuzalisha kwa tija.
Mh Aweso amesema hayo Agosti 05 mwaka huu mara baada ya kutembelea Banda la Baraza la Kilimo Tanzania katika Maonyesho ya wakulima kanda ya Mashariki yanayofanyika viwanja vya Mwl Nyerere Mkoani Morogoro.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi wa zamani Omary Mahita akifurahia jambo na washiriki wa maonyesho ya wakulima ndani ya Banda la Baraza la Kilimo Tanzania, pia alipata fursa ya kupata maelezo ya kina juu ya bidhaa ya mchele ya Rukwa Super Rice  inayozalishwa na wakulima hao bila kutumia mbolea za kisasa.

 IGP wa zamani Omary Mahita afurahishwa na juhudi za Baraza la Kilimo Tanzania katika kuwawezesha wakulima wanawake, katika picha akiagana na mkulima wa korosho kutoka Mtwara ambaye yuko ndani ya Banda la Baraza la Kilimo.

 Mratibu wa Programu ya Ubia wa KIlimo Tanzania chini ya Baraza la Kilimo Bw. Mark Magila akipata maelezo ya bidhaa zinazoonyeshwa na mshiriki wa maonyesho ya Kilimo mwaka 2019,ndani ya Banda la Baraza la Kilimo.

WAZIRI SINBACHAWENE AFANYA ZIARA ZANZIBAR, AKUTANA NA VIONGOZI WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi (kulia) akizungumza naWaziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. GeorgeBoniface Simbachawene (kulia) alipomtembelea Ofisini kwake Vuga VisiwaniZanzibar kwa ajili ya kujitambulisha.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Waziriwa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. GeorgeBoniface Simbachawene (wa pili kulia) alipomtembelea Ofisini kwake VugaVisiwani Zanzibar kwa ajili ya kujitambulisha.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. GeorgeBoniface Simbachawene (kushoto) akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi yaMakamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohamed Aboud (katikati)alipomtembelea Ofisini kwake Vuga kujitambulisha. Kulia ni Naibu Waziri Ofisi yaMakamu wa Pili wa Rais Mhe. Mihayo Juma Nunga
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. GeorgeBoniface Simbachawene (kushoto) akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi yaMakamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohamed Aboud (katikati)alipomtembelea Ofisini kwake Vuga kujitambulisha.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. MohamedAboud akimuonesha maeneo mbalimbali ya Mji wa Zanzibar Waziri wa Nchi Ofisiya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. George BonifaceSimbachawene baada ya kumtembelea na kufanya nae mazungumzo Ofisinikwake.
Mratibu wa Shughuli za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Khalid Bakari Hamrani(wa pili kulia) akimpa maelezo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa RaisMuungano na Mazingira Mhe. George Boniface Simbachawene kuhusu ujenziunaoendelea wa jengo la Kituo cha Afya Kianga Wilaya ya Magharibi A MkoaniMjini Magharibi unaojengwa kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) nakusimamiwa na wananchi wenyewe. Kulia ni Mkurugenzi wa Muungano Ofisi yaMakamu wa Rais Lupi Mwaikambo.Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. GeorgeBoniface Simbachawene akikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa ujenzi waKituo cha Afya cha Kianga Wilaya ya Magharibi A Mkoani Mjini Magharibiunaojengwa kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) na kusimamiwa nawananchi wenyewe.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. GeorgeBoniface Simbachawene akizungumza alipotembelea eneo la Kilimani mjiniZanzibar kwenye mradi wa miti ya mikoko kando ya Bahari ya Hindi ili kuhifadhimazingira ikiwa ni sehemu ya ziara yake. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara yaMazingira Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Farhat Ali Mbarouk.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. GeorgeBoniface Simbachawene akizungumza na watendaji wa Ofisi ya Makamu wa Piliwa Rais wa Zanzibar alipotembelea Ofisi hiyo kujitambulisha.

MWAKYEMBE AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA UWANJA WA SIMBA

$
0
0
Na Zainab Nyamka,Michuzi TV

WAZIRI wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Uwanja wa klabu ya Simba eneo la Bunju mjini Dar es Salaam.

Uwanja huo utakaokuwa wa nyasi za bandia na nyasi za asili umewekewa jiwe la msingi na kutakuwa na kituo cha michezo, vyumba vya kubadilishia nguo wachezaji na uzio wa eneo lote ambalo tayari zoezi la ujenzi limeanza.

Mwakyembe amesema kuwa Serikali inatambua uwekezaji wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ndani ya Simba, Mohamed Dewji 'Mo' kwani waliweza kuwaruhusu waendelee na mchakato huo.

"Serikali inatambua uwepo wa uwekezaji uliopo ndani ya Simba na amekuwa bega kwa bega na viongozi hivyo nasi tunatambua uekezaji wake na wale ambao wana hofu wasiwe nayo,”amesema Mwakyembe.

Ameeleza kuwa wanaona matokeo ndani ya klabu ya Simba, wameweza kufika mbali kwenye michuano ya Kimataifa na kubwa zaidi ametoa rai kwa wanachama, mashabiki na uongozi wa Simba kuandaa ripoti ambayo itatumika kwa ajili ya kuwapa mafunzo wengine kufanya hivi kwani kila timu inapaswa ifikie hatua kubwa ambayo ni maendeleo kwenye uwekezaji wa mpira wa kisasa.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mo amesema kwamba akiwa mwanachama wa Simba na akiipenda toka utotoni ameamua kutoa fedha zake kwa ajili ya awamu ya kwanza ya ujenzi wa Uwanja huo.

Mo amesema, kwakuwa ujenzi wa uwanja huo bado haujakamilika amekaa na bodi ya wakurugenzi wa Simba na wamekubali kuandaa siku maalumu ‘GALA’ Kwa ajilili ya wanachama na mashabiki 500 kuchangia fedha itakayotumika kwa ujenzi wa awamu ya pili.

Akifafanua kuhusiana na ujenzi huo, Mo amesema fedha alizozitumia kwenye ujenzi wa awamu ya kwanza hazihusiani na zile walizokubaliana kwenye uwekezaji kwenye klabu hiyo.

“Napenda kuelezea dhamira yangu kwa klabu yaSimba ni kuona inashinda kila taji inalowania katika kipindi chote, iwe na miundombinu bora na ya kisasa itakayaoiwezesha kuzalisha na wachezaji vijana watakaotokana na mipango ya muda mrefu na mfupi, kuhakikisha inakuwa na kikosi bora zaidi ya ilichonacho sasa,” amesema Mo.

Akizungumzia mipango mingine ya timu hiyo, Mo ameeleza kuwa baada ya miaka kadhaa ya kutokuwa na uwanja wetu rasmi, leo klabu hii kubwa kabisa nchini hatimaye tunatimiza ndoto zetu.

Amesema iwapo Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) kama watakubali anataka kununua timu ya daraja la kwanza aibadilishe jina iitwe Simba B, itakayoshiriki ligi hiyo, lakini haitacheza Ligi Kuu kwa sababu hawataruhusiwa kuwa na timu mbili za ligi hiyo kubwa nchini.

Simba kesho jioni watahitimisha Simba Day kwa kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Power Dynamos ya Zambia na itazinduia jezi zake za msimu mpya na kutambulisha kikosi kipya kuelekea msimu huo utakaofunguliwa na michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe akisikiliza jambo kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Mohamed Dewji 'Mo' wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Uwanja wa klabu ya Simba eneo la Bunju mjini Dar es Salaam. 
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe akipeana mkono na kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Mohamed Dewji 'Mo' baada ya kuweka wa jiwe la msingi la ujenzi wa Uwanja wa klabu ya Simba eneo la Bunju mjini Dar es Salaam.

YANGA KUWASHTAKI SELCOM KWA SERIKALI, TIKETI ZA SIMBA ZATUMIKA WIKI YA MWANANCHI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, ,Michuzi TV

Uongozi wa Klabu ya Yanga umelalamikia ubadhilifu unaofanywa na Kampuni ya Selcom Tanzania kwa kuuza tiketi mara mbili, wizi na rushwa uliotokea kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi.

Malalamiko hayo yametolewa na Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredirick Mwakalebela baada ya kubaini na kuwakamata wafanyakazi wa Selcom wakiwa wanafanya wizi huo na wanajiandaa kuandika barua kwa serikali ili waweze kuchukuliwa hatua.

Kilele cha Wiki ya Mwananchi kilihitimishwa jana kwa timu ya Yanga kucheza mchezo wao wa kirafiki na Kariobang Shark’s ya Kenya na kumalizika kwa sare ya 1-1 kukiambatana na utambulisho wa kikosi kipya waliosajiliwa kwa msimu wa mwaka 209/20.

Mwakalebela amesema kuwa, wanajiandaa leo Jumatatu kuandika barua kwenda serikalini kuhusiana na utendaji wao (selcom) wa kazi mbaya ambao ulikuwa wa matukio mengi ya wizi na rushwa.

“mawakala wa kampuni hiyo walikuwa tatizo wakiwa wanauza tiketi mara mbili kwa mashabiki waliokuwa wamejitokeza na kiukweli hatukuridhishwa na utendaji kazi wao ambao kama ukiendelea, basi serikali utapoteza mapato mengi,”amesema Mwakalebela.

Ameeleza kuwa “Leo Jumatatu tunatarajia kuandika barua kwenda serikalini kwa ajili ya kuwataarifu wizi na rushwa iliyokuwa inafanyika katika kilele chetu cha Wiki ya Mwananchi, Kikubwa ni kuwafahamisha tatizo lililotokea siku hiyo ya tukio,”

Mwakalebela amesema kuwa, mbaya zaidi wameweza kukamata tiketi za Simba Day zilizopangwa kutumika kesho zimetumika kwenye tamasha letu, hivyo tunashinda kufahamu hizo pesa zinakwenda Simba au kwetu.

KWANDIKWA AWATAKA MTWARA KUONGEZA UZALISHAJI

$
0
0
Kazi ya ujenzi wa barabara ya Mtwara- Mnivata km 50 inayojengwa kwa kiwango cha lami ikiendelea.
Muonekano wa barabara ya Mtwara- Mnivata km 50 ambayo ujenzi wake unaendelea.

Mkuu wa mkoa wa Mtwara Bw, Gelasius Byakanwa akisisitiza jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa alipomtembelea ofisini kwake kabla ya kuanza ziara ya kagua maendeleo ya ujenzi wa barabara na kiwanja cha ndege mkoani humo.
Meneja wa Wakala wa barabara (TANROADS), mkoa wa Mtwara Eng. Dotto John (kulia), akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa alipokagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Mtwara- Mnivata km 50, mkoani Mtwara (kushoto) ni mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bw, Evod Mmanda na Afisa wa Wizara ya Ujenzi Bw, Boniface Myalla .
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa akipata kahawa pamoja na wanakijiji wa Nanguruwe mkoani Mtwara ikiwa ni furaha yao kupata barabara ya lami katika kijiji hicho.
Meneja wa Wakala wa barabara (TANROADS), mkoa wa Mtwara Eng. Dotto John (wa pili kulia), akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa alipokagua maendeleo ya upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Mtwara.
Kazi ya ujenzi wa njia ya kutua na kuruka ndege katika kiwanja cha ndege cha Mtwara ikiendelea, kukamilika kwa ujenzi huo kutawezesha ndege kubwa kutua katika kiwanja hicho.

…………………………………………………..

Wakazi wa mkoa wa Mtwara wametakiwa kuongeza kasi ya uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara ili waweze kutumia vizuri fursa za ujenzi wa miundombinu ya barabara, anga na bandari kujiimarisha kiuchumi.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa amesema Serikali imejipanga kuhakikisha ukanda wa kusini mwa Tanzania unafunguka kimiundombinu katika nyanja za barabara za lami, bandari na usafiri wa anga hivyo kazi inayowakabili wananchi ni kuongeza uzalishaji.

Akizungumza na wanakijiji wa Nanguruwe mkoani humo mhe. Kwandikwa amesisitiza kuwa nia ya Serikali ni kuweka fursa ya miundombinu bora katika kila kanda ili wananchi waitumie kukuza uchumi binafsi na hivyo kuiwezesha Tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo 2025.
“Tumejipanga kuhakikisha nyanja zote za usafiri zinaimarika katika ukanda huu wa kusini hivyo nawaomba zalisheni kwa wingi mazao ya chakula na biashara ili kufikia soko kwa haraka popote lilipo,” amesema mhe. Kwandikwa.

Aidha amemhakikishia mkuu wa mkoa wa Mtwara Bw, Gelasius Byakanwa kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha wilaya zote za mkoa wa Mtwara zinaunganishwa kwa barabara za lami katika kipindi kifupi ili kufikika kwa urahisi wakati wote na hivyo kuimarisha huduma za biashara.

Mhe. Kwandikwa yupo katika ziara ya siku mbili mkoani Mtwara ambapo pamoja na mambo mengine amekagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Mtwara- Mnivata km 50 na uwanja wa ndege wa Mtwara unaorefushwa kutoka mita 2258 hadi mita 2800 hali itakayowezesha ndege nyingi na zinazochukua abiria wengi kutumia uwanja huo.
Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Agosti 5, 2019.

Waziri Mwakyembe Akutana na Kufanya Mazungumzo na Balozi wa Ujerumani Nchini

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni Dk. Harrison Mwakyembe (kulia)akifafanua jambo kwa Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Dk. Detlef Waechter (katikati) wakati Balozi huyo alipomtembelea Waziri katika Ofisi za Dar es Salaam na kujadiliana masuala mbalimbali katika kuimarisha sekta ya Utamaduni, kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Utamaduni kutoka ubalozi huo Bi. Ursula Thraen Lardi.
Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Dk. Detlef Waechter (katikati) akifafanua jambo kwa Waziri wa Habari, Utamaduni Dk. Harrison Mwakyembe (kulia) wakati Balozi huyo alipomtembelea Waziri katika Ofisi za Dar es Salaam na kujadiliana masuala mbalimbali katika kuimarisha sekta ya Utamaduni, kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Utamaduni kutoka ubalozi huo Bi. Ursula Thraen Lardi.
Waziri wa Habari, Utamaduni Dk. Harrison Mwakyembe (kulia) akimuonesha Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Dk. Detlef Waechter (katikati) pikipiki iliyotumiwa na mpigania uhuru wa Msumbiji, Hayati Samora Machel, wakati Balozi huyo alipomtembelea Waziri katika Ofisi za Dar es Salaam na kujadiliana masuala mbalimbali katika kuimarisha sekta ya Utamaduni.
Waziri wa Habari, Utamaduni Dk. Harrison Mwakyembe (katikati)akiagana na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Dk. Detlef Waechter (kulia) wakati Balozi huyo alipomtembelea Waziri katika Ofisi za Dar es Salaam na kujadiliana masuala mbalimbali katika kuimarisha sekta ya Utamaduni, kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Utamaduni kutoka ubalozi huo Bi. Ursula Thraen Lard

Waziri Mwakyembe Aongoza Mapokezi Ya Kilimanjaro Stars

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (kulia) akifurahia jambo na viongozi wa Timu ya Taifa ya Kilimanjaro Stars mara baada ya kuwapokea wakitokea nchini Kenya walikowa katika mchezo wa marudiano na Timu ya Taifa ya Kenya katika mashindaon ya CHAN, Tanzania ilishinda 4 dhidi ya goli moja la Kenya.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (kulia) akisalimiana na viongozi wa Timu ya Taifa ya Kilimanjaro Stars mara baada ya kuwapokea wakitokea nchini Kenya walikowa katika mchezo wa marudiano na Timu ya Taifa ya Kenya katika mashindaon ya CHAN, Tanzania ilishinda 4 dhidi ya goli moja la Kenya.
Baadhi ya Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Kilimanjaro Stars wakiwasili toka nchini Kenya walikowa katika mchezo wa marudiano na Timu ya Taifa ya Kenya katika mashindaon ya CHAN, Tanzania ilishinda 4 dhidi ya goli moja la Kenya.
Nahodha wa Timu ya Taifa ya Kilimanjaro Stars, John Bocco akifanya mahojiano na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili toka nchini Kenya walikowa katika mchezo wa marudiano na Timu ya Taifa ya Kenya katika mashindaon ya CHAN, Tanzania ilishinda 4 dhidi ya goli moja la Kenya.
Viongozi na Wachezaji Timu ya Taifa ya Kilimanjaro Stars wakiwasili toka nchini Kenya walikowa katika mchezo wa marudiano na Timu ya Taifa ya Kenya katika mashindaon ya CHAN, Tanzania ilishinda 4 dhidi ya goli moja la Kenya.Picha na WHUSM – Dar es Salaam.

RAIS MAGUFULI AZITAKA SEKTA BINAFSI KUPAMBANA NA CHANGAMOTO ILI KUWEZA KUFIKIA MALENGO

$
0
0

*Salumu Shamte apokea kijiti cha uenyekiti wa baraza la biashara (SADC) kutoka Namibia ahidi ushirikiano

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

TAASISI za sekta binafsi zimetakiwa kupambana na changamoto wanazokumbana nazo katika kujenga na kuimarisha uchumi badala ya kulalamika kwa kuwa hakuna njia rahisi katika kuyafikia mafanikio.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Rais Dkt. John Joseph Magufuli wakati akizindua rasmi wiki ya maonesho ya nne ya viwanda ikiwa ni katika kuelekea mkutano mkuu wa 39 wa wakuu wa nchi 16 kutoka ukanda wa SADC, Magufuli amesema kuwa mchango wa taasisi za sekta binafsi unaonekana na wamekuwa karibu sana serikali katika kuhakikisha azma ya kujenga uchumi imara inafanikiwa hivyo hawana budi kulalamika pindi wanapokutana na changamoto mbalimbali kwani hakuna njia rahisi ya kuyafikia maendeleo.

Rais Magufuli amezipongeza taasisi za sekta binafsi kwa kushiriki katika mkakati wa kujenga viwanda vipya ambapo kwa miaka mitatu pekee ya uongozi wa serikali ya awamu ya tano jumla ya viwanda vipya 4000 vimeanzishwa.

"Mchango wenu ni mkubwa na unaonekana, tudumishe umoja na mshikamano kupitia jumuiya yetu katika kuhakikisha nchi wanachama zinanufaika kupitia umoja huulu ili tufike mbali zaidi mbali na kuwa na uchumi wetu wenyewe ulio imara zaidi" Ameeleza Rais Magufuli.

Kwa upande wake mwenyekiti wa taasisi za sekta binafsi nchini Salum Shamte ambaye pia leo amekabidhiwa kiti Cha uenyekiti wa baraza la biashara (SADC) kutoka kwa Bi. Charity Mwiya (Namibia) amesema kuwa kazi kubwa wanayoifanya ni pamoja na kushirikiana na serikali katika kujenga uchumi na kutengeneza ajira na wamekuwa wakishirikisha na nchi wanachama wa SADC katika masuala ya biashara  kwa kuhusisha nchi wanachama.

Shamte amesema kuwa mchango wa jumuiya hiyo ni mkubwa na katika maonesho ya nne ya wiki ya viwanda watanzania wajitokeza na kutumia fursa katika kujipatia masoko, kubadilishana ujuzi na uzoefu pamoja na kutangaza bidhaa zao kwa wageni.

"Mkutano huu kufanyika hapa nchini lazima ulete mabadiliko kwa sisi wenyeji, tujitokeze kwa wingi na kunadi bidhaa zetu ambazo bila shaka zitapata soko la uhakika na hatimaye kuweza kufikia malengo ambayo serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais Dkt. Magufuli umedhamiria kuyafikia" Ameeleza Shamte.

Ni wazi kwamba mchango wa taasisi za sekta binafsi unachangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa uchumi wa nchi mbalimbali hasa za ukanda wa SADC na nafasi ya uenyekiti iliyokabidhiwa leo kwa Salum Shamte ni daraja wezeshi zaidi katika kufikia malengo ya kujenga uchumi wa kati na kujenga taifa la viwanda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli akishuhudia makabidhiano ya Baraza la Biasha la SADC,ambapo Mh. Salum Shamte ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la SADC kutoka kwa Charit Mwiya Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la SADC aliyemaliza muda wake,katika ufunguzi wa maonesho ya nne ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za SADC yanayofanyika jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Agosti 5, 2019 kulia ni 

KMC WATAJA KIKOSI CHAO CHA MSIMU WA 2019/20

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Michuzi TV

WAWAKILISHI wa Michuano ya Kombe la Shirikisho CAF, Timu ya KMC imeweka wazi kikosi chake kitakachotumika kwa msimu wa mwaka 2019/20 kwenye Ligi kuu Tanzania Bara na Michuano ya kimataifa.

Kikosi hicho kitakachokuwa kinaongozwa na Kocha wa zamani wa klabu ya Simba Jackson Mayanja kina jumla ya wachezaji 28 kukiwa na usajili wa wachezaji wapya wa kimataifa.

Katika dirisha la usajili, Uongozi wa KMC uliweza kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji kwa kusajili mchezaji wa kitanzania aliyeongoza kwa magoli msimu uliopita Sali Aiyee, Vitalis Mayanga na kwa upande wa maeneo mengine waliweza kumsajili mchezaji wa zamani wa Simba Besala Bukungu na Jean Baptise Mugiraneza aliyecheza Azam.

Timu ya KMC itaanza kutupa karata yake ya kwanza kwenye michuano ya Kimataifa dhidi ya As Kigali Agosti 10 mwaka huu mechi itakayopigwa kwenye dimba la Kigali Stadium nchini Rwanda.

Wachezaji wengine ni Ismail Gambo, Serge Nogues, Cliff Buyoya, Denis Richard, Abdull Hilary, Charles Inlafia, na Ally Ramadhani, Amos Kadikilo, Ally Msengi,Juma Kaseja, Kelvin Kijili, Boniphace Maganga, Rayman Mgungila, Jonathan Nahimana, na James Msuva.

Wengine ni Sadala Lipangile, Kenny Ally, Yusuph Ndikumana, Abdallah Mfuko, Ramadhan Kapera, Hassan Kabunda, Mohamed Samata, George Sangija na Melly Sivirwa.

TCRA katika Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Kusini Mkoani Lindi

$
0
0
Wananchi wakipata huduma za usajili laini za simu kwa alama za vidole pamoja na usajili wa kupata kitambulisho cha Taifa cha Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)
Afisa akiwahudumia wananchi katika Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Kusini
Wananchi wa Lindi na viunga vyake wakipata huduma za usajili laini za simu kwa alama za vidole katika banda la TCRA ambapo NIDA na watoa huduma walikuwepo.

*************

 *Usajili laini za  simu kwa alama za vidole waendelea u

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) imesema kuwa wananchi wa Kanda ya Kusini watumie maonesho ya Nane Nane kupata elimu ya Mawasiliano pamoja na usajili wa laini za simu kwa alama za vidole.

Hayo ameyasema Afisa wa TCRA Abdulrahaman Millas katika Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Kusini mkoani Lindi , amesema maonesho ya Nane Nane yatumike kwa wananchi kusajili laini za simu alama za vidole kwa huduma zote za kufanya usajili zipo ndani za maonesho hayo.

Millas amesema muda uliokuwepo wananchi kusajili laini za simu kwa alma za vidole kwani mwisho wa usajili huo ni Desemba 31 mwaka huu.

Amesema kuwa muda uliopangwa lazima utumike kikamilifu kupunguza kujazana kwa watoa huduma katika tarehe za mwisho za Desemba.

“Muda umewekea ni mkubwa kwa wananchi kupata kitambulisho cha Taifa na kusajili laini zao za simu na walio na vitambulisho vya Taifa kusajili laini zao za simu kuondokana na usumbufu wa kufungiwa mawasiliano simu hizo.

Aidha amesema kuwa TCRA iko bega kwa bega katika kutoa elimu kwa wananchi kwa huduma mbalimbali za mawasiliano ili wasitumie mawasiliano kinyume cha sheria.

VETA WAENDELEZA UBUNIFU, MAMIA WAFURIKA KUONA VIBAO VYA KUFULIA NGUO NA MASHINE YA KUCHAKATA NYASI

$
0
0
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Simiyu
MAMLAKA ya Elimu na Ufundi Stadfi VETA, imeendelea kuja na ubunifu katika kutengeneza mashine na vifaa mbalimbakli ili kurahisisha utendaji kazi katika maisha ya kila siku katIka jamii.
VETA ambao wako kwenye maonesho ya Nanenane kitaifa kwenye viwanja vya Nyakabindi nje kidogo ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu, banda lao limekuwa kivutio kikubwa kwa wananchi wanaotembeela maonesho hayo ambapo, miongoni mwa vifaa vilivyobuniwa ni kibao cha kufulia nguo, ambapo wanafunzi wa VETA mjini Songea kwa kushirikiana na Ruta Kamoto kutoka Shirika la JICA. Wamebuni njian rahisi ya kufua nguo kwa kutumia kibao.
Ruta Kamoto ambaye pia ni Afisa Maendeleo Songea vijijini alisema, kibao hicho kilibuniwa na wanafunzi wa VETA Songea ili kumrahisishia mfuaji w anguo badala ya kutumia nguvu nyingi katika kufikicha nguo, kibao hicho hakihitaji mayumiazi makubwa ya nguvuy katika kufua kwani ni rahisi na hutumia mufa mfupi kufua nguo.
“Kibao hiki kina migongo midogo, unaweza kutumia sabuni ya kipande na kupaka katika nguo kama kawaida, au kuweka nguo katika machanganyiko wa maji na sabuni ya unga baada ya kukolea, unachukua nguo na kuilaza kwenye kibao na kusugua taratibubu na baada ya muda mfupi nguo itakuwa imetakata.” Alisema Ruta Kamoto.
Aidha wananchi wanaotembelea banda hilo la VETA pia wamepata fursa ya kujionea mashine ya kusaga nyasi kwa ajili ya malisho ya mifugo, kama vile Mbuzi na Ng’ombe ambapo mashine hiyo inaweza kutumia umeme au jenereta.
Mbunifu Fredrick Uliki ambaye ni Mwalimu wa ufundi mitambo VETA Morogoro, yeye alisema wao wamebuni mashine ya kukatakata malisho ya mifugo ili yaweze kuliwa kwa urahisi, “majani yakiwa makubwa makubwa huliwa kwa asilimia kama 30 lakini ukikata nyasi kuwa ndogondogo mnyama anaweza kula hadi asilimia 90 ya chakula ulichompa, pia mashine inaweza kuchakata mahindi, dagaa na mashudu ya alizeti ili kuwezesha mifugo kama ndege na kuku kula kwa urahisi” Alifafanua Bw. Uliki.
Maonesho ya Nanenane Nyakabindi yalizinduliwa rasmi Agosti 1, 2019 na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na yanatarajiwa kufikia kilele Agosti 8, 2019 huku yakiwa yamebeba kaulimbiu isemayo “Kilimoi, Mifugo na Uvuvi kwa ukuaji wa Uc humi w aNchi.”.
 Ruta Kamoto kutoka Shirika la JICA akielezea jinsi kibao kinavyoweza kurahisisha kazi ya ufuaji nguo kwa wananachi waliotembela banda la VETA kwenye maonesho ya Nanenane ,kitaifa viwanja vya Nyakabindi nje kidogo ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.

 Mwananchi akijaribu yeye mwenyewe kufua kwa kutum ia kibao hicho ambapo alikiri kuwa ni rahisi mno.
 Wananchi wakipata elimu kutoka maafisa wa VETA.
 Mwanafunzi wa VETA, akielezea jinsi mashine waliyobuni inavyoweza kunyoosha matairi ya gari (Wheel balance).


Vijana Zaidi ya 2000 Washiriki Sherehe za Kimila

$
0
0

Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Manyara

Vijana wa jamii ya Wamasai zaidi ya 2000 katika kijiji cha Irkujit kata ya Edonyongijape wilaya ya Simanjiiro mkoani Manyara, wameingia kwenye rika jipya linalojulikana kama Irkimayan ikiwa ni miaka 10 baada ya kumaliza jando .

Kiongozi wa Mila wa rika hilo maarufu kama Laigwanan Lembris Moringe alisema hao kwa sasa wanafurahi kuingia kwenye rika jipya ambapo wataendeleza ushiriki wao katika masuala ya kijamii na kuchangia maendeleo.

Lembris amesema kuwa vijana wengi hawamiliki ardhi hivyo ameiomba serikali za vijiji kuweka utaratibu wa kutoa maeneo kwa ajili ya vijana ili waweze kushiriki katika shughuli za kijamii na kiuchumi kwa kutumia ardhi kama nyenzo muhimu.

Lembris aliwataka vijana kujitokeza katika masuala ya kijamii na kuwa mstari wa mbele katika kutatua changamoto zilizoko kwenye jamii pamoja na kuchangia katika shughuli za maendeleo.

Diwani wa kata ya Endonyongijape Lucas Moringe ameuagiza uongozi wa vijiji vyote katika kata hiyo kuweka vikao na kutenga maeneo kwa ajili ya vijana ili waweze kujiletea maendeleo yao kwa kutumia ardhi kwa ajili ya kilimo,ufugaji na biashara.

Moringe alisema kuwa serikali itaendelea kuwa bega kwa bega na vijana na kuwawezesha kupitia mikopo ya asilimia 10% kwa wanawake na vijana ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Mbunge wa Simanjiro James Ole Millya alisema kuwa vijana ndio msingi wa maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla hivyo wanapaswa kupewa kipaumbele na kushirikishwa katika shughuli za kimaendeleo.

“katika kata hii kuna kero ila tunashuru serikali tayari imetenga kiasi cha shilingi bilioni 41.3 za kuvuta maji kutoka mto Ruvu jitengeni mradi ambao utamaliza kero ya maji katika kijiji hicho na wilaya ya Simanjiro kwa ujumla” Alisema Mbunge huyo.

Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images