Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live

MWAKYEMBE APOKEA ZAWADI YA JPM, AWATAKA MASHABIKI KUJAZA UWANJA

$
0
0

Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe amewataka mashabiki wa mpira wa miguu nchini kuacha kuangalia kwenye Televisheni bali wakajaze Uwanja.

Hayo ameyasema wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya wiki ya Mwananchi iliyomalizika kwa mchezo wa kirafiki kati ya Yanga dhidi ya Kariobang Sharks.

Ambapo katika mchezo huo Mwakyembe ameweza kupokea zawadi ya jezi ya Yanga kutoka kwa Mwenyekiti wa Yanga Dkt Mshindo Msolla kwa ajili ya Rais Dkt Magufuli kama kiashiria cha ushiriki wake kwenye michezo nchini.

Mwakyembe amesema kuwa sasa hivi ni muda wa mashabiki kwenda kujaza viwanja vya mpira pale timu zao zinapokuwa zinacheza na kuacha kuangalia kwenye Televisheni.

Amesema, mashabiki wanapojitokeza kwa wingi timu uwanjani inapata hamasa kuwa na hata mapato kwa timu yanakuwa yanapatikana kwa wingi.

Ametoa salamu kwa wana Yanga wote kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ya kuwatakia mchezo mwema pamoja anawapenda wote.
 Mwenyekiti wa Yanga Dkt Mshindo Msolla akimkabidhi jezi Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe zawadi ya jezi ya Rais Dkt John Pombe Magufuli kama kiashiria cha ushiriki wake kwenye michezo wakati wa Kilele cha Wiki ya Mwananchi iliyomalizika kwa mechi ya Kirafiki kati ya Yanga na Kariobang Sharks uliomalizika kwa timu hizo kutoka sare ya 1-1 leo kwenye Uwanja wa Taifa







Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe akizungumza na mashabiki  na wanachama wa Yanga waliojitokeza kushuhudia Kilele cha Wiki ya Mwananchi iliyomalizika kwa mchezo wa kirafiki kati ya Yanga na Kariobang Sharks uliomalizika kwa sare ya 1-1 mchezo uliochezwa kwenye Dimba la Uwanja wa Taifa

TAIFA STARS YAITOA KENYA KWA MIKWAJU YA PENATI

$
0
0
TIMU ya Taifa ya Mpira wa Miguu Taifa Stars wamefanikiwa kuvuka hatua ya mwanzo ya mchujo yq kuwania tiketi ya Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN kuiondoa timu ya Kenya Harambee Stars.

Taifa Stars wamefanikiwa kutinga ya mwisho ya mchujo baada ya ushindi wa penalti 4-1 dhidi ya Kenya jioni ya leo Uwanja wa Moi Kasarani mjini Nairobi, Kenya.

Katika mchezo wa kwanza, uliochezwa Jijini Dar es Salaam Timu hizo zilishindwa kufungana na kutoshana nguvu ya 0-0.

Mchezo wa pili uliweza kumalizika kwa dakika 90 bila kufungana na kwenda kwenye hatua ya matuta na kipa mkongwe, Juma Kaseja aliweza kuwa shujaa owa kuokoa penati ya Michael Kibwage.

Kipa huyo amerejeshwa kikosini baada ya miaka sita na kuendelea kudhihirisha ubora wake.Kwa upande wa Tanzania Waliopata penati ni 
mabeki Erasto Nyoni, Paul Godfrey ‘Boxer’, Gardiel Michael na mshambuliaji Salum Aiyee.

Kenya walipata penalti moja tu, ambayo ilifungwa na Cliffton Miheso Ayisi, huku nyingine wakikosa Michael Kibwage na Joash Achieng Onyango.

Sasa Tanzania itakutana na Sudan katika hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania tiketi ya CHAN ya mwakani nchini Cameroon, mechi ya kwanza ikichezwa Dar es Salaam Septemba 20 na marudiano Oktoba 18 Khartoum.

Kikosi cha Tanzania kilikuwa; Juma Kaseja, Paul Godfrey, Gardiel Michael, Erasto Nyoni, Kelvin Yondan, Jonas Mkude, Frank Domayo/Salim Aiyee, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, John Bocco/Ayoub Lyanga, Iddi Suleiman ‘Nado’ na Hassan Dilunga/Abdulaziz Makame.

Kenya; John Oyemba, Philemon Otieno/Ibrahim Shambi, Cliffton Miheso, Mike Kibwage, Joash Onyango, Dennis Odhiambo, Samuel Onyango, Kenneth Muguna, Sydney Lokale/Enosh Ochieng, Whyvone Isuza na Duke Abuya/ David Owino.

JAJI MSTAAFU WA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA, MHE. JAJI RUGAZIA AFARIKI DUNIA

$
0
0
Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Projestus Aloyce Rugazia (pichani) amefariki dunia. 

Mhe. Jaji Rugazia amefariki dunia alfajiri ya kuamkia Agosti 04, 2019 akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa-Muhimbili jijini Dar es Salaam. 

Msiba upo nyumbani kwake Kinondoni- Dar es Salaam, ratiba ya taratibu za kuaga na mazishi itajulikana mapema Agosti 05, 2019. 

Marehemu Jaji Rugazia alizaliwa Agosti 28, 1954 mkoani Kagera, alianza kazi rasmi Januari 01, 1983 kama Hakimu Mkazi. 

Marehemu aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu Machi 28, 2003. Aidha; Marehemu Jaji Rugazia alistaafu rasmi Agosti 28, 2016 akitokea Mahakama Kuu-Divisheni ya Ardhi. 

Mahakama ya Tanzania imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo chake. 

BWANA AMETOA, BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE 


IMETOLEWA NA : 

KITENGO CHA HABARI, ELIMU NA MAWASILIANO, 

MAHAKAMA YA TANZANIA. 

M-pesa yawapa unafuu wasafiri wa anga Wateja wa M-Pesa na Turkish Airline kupata ofa ya asilimia 15

$
0
0
Balozi wa Uturuki  nchini, Ali Davutoglu (katikati) na Mkurugenzi wa shirka la ndege la Uturuki nchini, Ahmet Sahin (Kushoto), wakimkabidhi Mkurugenzi wa Vodacom Business Unit Arjun Dhillon, mfano wa ndege kuashiria uzinduzi rasmi wa huduma ya malipo kwa M-Pesa ambayo wateja wao watapata punguzo la bei kwa asilimia 15 pindi wanaponunua tiketi ya ndege kutoka shirika hilo, kuanzia tarehe 1 Agosti hadi Disemba Mosi mwaka huu. Ofa hiyo ilitangazwa katika hafla fupi iliyofanyika ofisi za Ubalozi wa Uturuki jijini Dar es Salaam jana.
Balozi wa Uturuki nchini, Ali Davutoglu (katikati) na Mkurugenzi wa M-commerce wa Vodacom Tanzania Epimack Mbeteni (wa kwanza kulia) na  Mkurugenzi wa Vodacom Business Unit, Arjun Dhillon (wa pili kulia), wakimsikiliza  Mkurugenzi wa shirka la ndege la Uturuki nchini, Ahmet Sahin, ( wapili kushoto) akielezea  punguzo la bei kwa asilimia 15 kwa wateja pindi wanaponunua tiketi ya kusafiria kutoka shirika la ndege la Uturuki (Turkish airline) kupitia huduma ya M-Pesa kuanzia tarehe 1 Agosti mpaka Disemba Mosi mwaka huu. Ofa hiyo ilitangazwa katika hafla fupi iliyofanyika ofisi za Ubalozi wa Uturuki jijini Dar es Salaam jana.



Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na shirika la ndege la Uturuki (Turkish Airlines), wametangaza ofa ya punguzo la bei kwa asilimia 15 kwa kila mteja atakaye nunua tiketi kutoka shirika hilo kupitia huduma ya M-Pesa, Ofa hii ni kuanzia tarehe 1 mwezi wa nane mpaka tarehe 1 Disemba mwaka huu. Ofa hii ilitangazwa katika hafla fupi iliyofanyika ofisi za Ubalozi wa nchi hiyo jijini Dar es Salaam, na kuhudhuriwa na Mheshimiwa Balozi wa Uturuki nchini, Ali Davutoglu na Mkurugenzi wa M-Pesa Bwana Epimack Mbeteni.


Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Vodacom Business Unit, Arjun Dhillon, M-Pesa Vodacom Tanzania, Epimack Mbeteni , alisema ubia huo umelenga kuchochea malipo ya kifedha kupitia njia za kidijitali kwa kuwawezesha wateja wao kufanya malipo kwa urahisi wanaponunua tiketi za ndege kutoka shirika la ndege la Uturuki (Turkish Airline) na kuelekea sehemu yeyote duniani wakianzia safari zao Tanzania. 

“Tuna wajibu wa kutengeneza bidhaa na huduma za kifedha ambazo zinakidhi mahitaji ya watu binafsi na biashara, kama shirika la ndege la Ututurki. Ulipaji kupitia M-Pesa ni njia rahisi zaidi ya kufanya malipo; wateja wetu watafurahia faida za kulipia tiketi zao mda wowote na wakati wowote kupitia M-Pesa ukizingatia wanazawadiwa pindi wanapofanya malipo”, alisema Arjun 

Akizungumza juu ya ofa hiyo Mkurugenzi wa shirka la ndege la Uturuki nchini, Ahmet Sahin, aliwapongeza Vodacom kwa kutumia teknolojia yao kuchochea huduma za kidijitali nchini. Sahin aliongeza kuwa huduma hii ni yakipekee kwa wafanyabiashara nchini Tanzania kulipia usafiri wa ndege kwenda Uturuki au maeneo 312 ambayo ndege zake zinafika, pamoja na kufaidika kibiashara na kujionea vitu ambavyo nchi zingine zinafanya (exposure). 

“Wateja ambao watanunua tiketi za shirika la ndege la Uturuki kuanzia tarehe moja mwezi wa nane mpaka Disemba mosi watapata, sio tu pungufu ya bei kwa asilimia 15% kwa safari zote zinazoanzia Dar es Salaam, Zanzibar na Kilimanjaro, bali pia watafurahia huduma zinazotolewa kwa masaa 24 kutoka kwa watoa huduma wetu nchini kote. Napenda kuwahimiza wafanyabiashara, watalii na wateja wetu wote kutumia fursa hii,” alisistiza Sahin. 

Shirika la ndege la Uturuki linaruka kwenda maeneo 312 katika nchi 126 duniani na ofa hii inahusu safari zote zinazoanzia nchini Tanzania kuelekea maeneo hayo. 

Vodacom Tanzania Plc inaendeleza nia yake ya kuhakikisha kwamba kila Mtanzania anafaidikia na huduma bunifu zitokanazo na mtandao wa simu, vile vile kufungua fursa za kidijitali kwa Watanzania hasa wakati huu tukielekea kuinua uchumi wa nchi kuwa wa kati ifikapo mwaka 2025.

RAIS DKT MAGUFULI AFUNGUA WIKI YA VIWANDA KWA NCHI ZA SADC LEO JIJINI DAR

$
0
0
 
 Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mbele ya Wageni waalikwa mbalimbali wakati akifungua maadhimisho ya nne ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za SADC yanayofanyika jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia mkutano wa SADC,ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli mgeni rasmi  katika ufunguzi wa maadhimisho ya nne ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za SADC yanayofanyika jijini Dar es Salaam. Yenye kauli mbiu: Mazingira Wezeshi kwa Maendeleo na Jumuishi ya Viwanda, Kukuza Biashara na Ajira ndani ya Jumuiya. 
Katibu Mtendaji Sekretariati ya SADC Dkt Stergomena Tax akizungumzia katika ufunguzi wa maadhimisho ya nne ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za SADC yanayofanyika jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akibadilishana mawazo na Waziri wa Viwanda na Biashara wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Innocent Bashungwa (kulia) wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya nne ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za SADC yanayofanyika jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu Mtendaji Sekretariati ya SADC Dkt Stergomena Tax wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya nne ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za SADC yanayofanyika jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Balozi kutoka Zanzibar,Mhe.Amina Salum Ali akizungumza katika ufunguzi wa maadhimisho ya nne ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za SADC yanayofanyika jijini Dar es Salaam,ambapo ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli mgeni rasmi katika ufunguzi wa maadhimisho ya nne ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za SADC yanayofanyika jijini Dar es Salaam. Yenye kauli mbiu: Mazingira Wezeshi kwa Maendeleo na Jumuishi ya Viwanda, Kukuza Biashara na Ajira ndani ya Jumuiya. 
Wageni waalikwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli akiangalia burudani ya ngoma wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya nne ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za SADC yanayofanyika jijini Dar es Salaam.

WAZIRI UMMY ARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA YA TANGA, ATAKA IKAMILIKE KWA WAKATI WANANCHI WAANZE KUPATA HUDUMA

$
0
0
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga(CCM) Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa ziara yake wa kukagua na kutembelea Hospitali ya wilaya ya Tanga na Kituo cha Afya cha Mwakidila Jijini Tanga kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya wa Wazazi wilaya ya Tanga Nassoro Makau.
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga(CCM) Ummy Mwalimu kushoto akimsikiliza kwa umakini Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji mara baada ya kutembelea hospitali ya wilaya ya Tanga
Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa ziara hiyo.
MKURUGENZI wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji akizungumza wakati wa ziara ya WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga(CCM) Ummy Mwalimu kulia kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mkoba.
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga(CCM) Ummy Mwalimu katikati akiwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kulia wakati wa ziara ya kutembelea hospitali ya wilaya ya Tanga inayojengwa eneo la Masiwani na kituo cha Afya Mwakidila.
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga(CCM) Ummy Mwalimu katikati akiwa na wakazi wa Masiwani wakati wa ziara yake kutoka kushoto ni Mganga Jiji cha Tanga CMO.
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Ummy Mwalimu katikati akionyeshwa kitu na Mkurugenzi wa Jiji la Tanga daudi Mayeji wakati wa ziara yake.
Sehemu ya wananchi wa Masiwani wakiwemo wazee wakimsikiliza WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga(CCM) Ummy Mwalimu.
KATIBU Mwenezi wa CCM wilaya ya Tanga Lupakisyo Kapange kulia akicheza na wananchi wa Masiwani wakati wa ziara hiyo
Muonekano wa mmoja ya majengo yaliyopo kwenye Hospitali ya wilaya ya Tanga eneo la Masiwani.
Muonekano wa mmoja ya majengo yaliyopo kwenye Hospitali ya wilaya ya Tanga eneo la Masiwani.
Muonekano wa mmoja ya majengo yaliyopo kwenye Hospitali ya wilaya ya Tanga eneo la Masiwani.
Muonekano wa Majengo kwenye Hospitali ya wilaya ya Tanga eneo la Masiwani Jijini Tanga.
Muonekano wa mmoja ya majengo yaliyopo kwenye Hospitali ya wilaya ya Tanga eneo la Masiwani.


WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Tanga inayojengwa eneo la Masiwani Kata ya Masiwani Jijini Tanga huku akitaka umaliziaji wake umalizika kwa wakati ili wananchi waanze kupata huduma za matibabu. 

Kutokana na kazi nzuri iliyofanyika kwenye Hospitali hiyo ya wilaya Waziri huyo alimpongeza Mkurugenzi wa Halamshauri ya Jiji la Tanga Daudi Mayeji na wataalamu wengine akiwemo fundi ambao wanasimamia ujenzi huo kutokana na kujengwa kwa ufanisi mkubwa. 

Aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati alipofanya ziara ya kuitembelea na kukagua ujenzi wake unavyokwenda huku akionyesha kuridhishwa nao huku akimuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji kuhakikisha vitu vidogo vidogo vya umaliziaji vifanyike kwa haraka. 

Licha ya kutembelea hospitali hiyo lakini pia Waziri Ummy alitembelea pia ujenzi wa kituo cha Afya Mwakidila ambapo pia aliridhishwa na kasi yake huku akitaka kikamilika kwa wakati ili wananchi wa maeneo hayo wapata huduma hiyo muhimu. 

Alisema kwani amepita sehemu mbalimbali Tanzania akiwa anakagua hospitali hizo huku baadhi akisema wabomboe kwenye baadhi ya maeneo kutokana na kujengwa chini ya kiwango lakini kwenye wilaya hiyo hajasema hivyo. 

Waziri huyo aliwataka watumie miezi michache kumaliza kazi zilizobakia ili wananchi waanze kupata huduma hawana muda wa kusuburi hosipitali hiyo imesubiriwa kwa muda mrefu sana jiwe la msingi lililwekwa 2013. 

“Maisha mangapi yamepotea kwa kukosa hospitali ya wilaya…wazee wangu na wananchi masiwani niwapongeze kutoka ndani ya moyo wangu kusimama kidete kuhakikisha kwamba hospitali inajengwa na kukamilika,tunawashukuru kwa uvumilivu kwa ushirikianao mkubwa wa kufika eneo hilo"Alisema 

"Lakini pia mwenyezi mungu awazidishie heri mmetizima wajibu wenu kama wana Tanga na Tanzania maendeleo sio kama hayajaletwe yanaanza na sisi wenyewe jambo tunalosisitiza ni ushiriki wananchi katika kuleta maendeleo kwenye maeneo yao yanayowazunguka”Alisema 

Aidha alisema kwamba wamekubaliana na Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Suleimani Jafo ndani ya muda mfupi huduma zianze kutolewa ili kuondosha kero za wananchi wa maeneo hayo. 

Hata hivyo aliwaomba wakazi wa masiwani kuendeee kumuombea Rais Dkt John Magufuli heri na baraka kwenye suala zao kutokana na kazi kubwa na mapinduzi makubwa aliyoyafanya kwenye sekta mbalimbali hapa nchini ikiwemo za Afya 

Awali akizungumza katika ziara hiyo Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa alisema kwamba huwezi kuzungunza jambo lolote la kuisifu nchi ukaacha kumtaja Rais Magufuli iwe sekta binafasi au umma kutokana na kufanya kazi kubwa ya kuwapa maendeleo watanzania. 

Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji alisema kwamba ujenzi wa majengo saba kwenye hospitali hiyo yapo kwenye hatua umaliziaji na jengo ambalo limejengwa muda mrefu litajengwa litakuwa la utawala na wameweka utaratubu wa kutenga bajeti kulikarabati ili liweze kufafana na majengo mengine. 

Alisema walipokea bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo na mpaka sasa wamekwisha kutumia zaidi ya bilioni 1.4 lakini kazi zote zinazohusiana na ujenzi huo wamewapa watu wanafanya ukamilishaji, milango, aluminiamu, watu wanaweka umeme, kazi zote na vifaa vyake zimekwisha kununuliwa. 

Hata hivyo alisema kwamba mpaka sasa madaktari sita tayari wametengwa kwa ajili ya kuanzisha hospitali hiyo na wamekwisha kuandaliwa barua za kuhamishiwa kwenye hospitali hiyo. 

ADAIWA KUMUUA MUMEWE KWA KUMCHOMA NA BISIBISI-WANKYO

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI,PWANI

MWAJUMA Omary Malembeka (28)anadaiwa kumuua mume wake Selemani Kondo (43) mkulima na mkazi wa Chamalale,kata ya Vihingo,Mzenga ,wilayani Kisarawe mkoani Pwani, kwa kumchoma na bisibisi kwenye bega .

Akithibitisha kuhusu tukio hilo,kamanda wa polisi mkoani hapo, Wankyo Nyigesa alisema mwanamke huyo alifanya maamuzi hayo kutokana na wivu wa kimapenzi.

Alieleza, kulikuwa na mzozo baina yao ambapo Mwajuma alimtuhumu mume wake kuwa siyo mwaminifu katika ndoa yao."Selemani aliuawa kwa kuchomwa bisibisi katika bega lake la kushoto na sehemu ya juu na mke wake huyo"alifafanua.

Wankyo alisema, kujichukulia sheria mkononi sio jambo la msingi kwani inaweza kuleta madhara kama ya kujeruhi ama kusababisha kifo ,na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo zinazomkabili.

Katika hatua nyingine, huko kijiji cha Lulenga, Ubena ,jimbo la Chalinze polisi walimkamata Kitenye Lumange ,mfugaji wa jamii ya kimasai (24) kwa kosa la wizi wa ng'ombe 13 wenye thamani ya sh.milioni 7.2 mali ya Arisen Hussein mkazi wa kijiji cha Visakazi .

Kamanda huyo alibainisha,wanawasaka watuhumiwa wengine walioshiriki kuiba mifugo hiyo.

NEWS ALERT: KABENDERA AFIKISHWA MAHAKAMA YA KISUTU

$
0
0
 Erick Kabendera pichani kulia akiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akizungumza na Wakiri wake,wakati akisubiri kusomewa mashtaka yanayomkabili


Bashe: Tutaweka Mazingira Rafiki Kwa Ushiriki wa Benki Katika Kilimo

$
0
0
Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, akizungumza na wafanyakazi wa NMB kwenye banda la benki hiyo wakati wa uzinduzi wa maonesho ya nanenane katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe (wa pili kushoto) akitazama Bidhaa za mfanyabiashiara Raphael Buja (Buja Pure Honey) kwenye banda la NMB, wakati wa uzinduzi wa maonesho ya nanenane katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu, kushoto ni Meneja Mwandamizi Biashara na Kilimo wa NMB John Mchunda, Mkuu wa Idara ya biashara kwa Serikali kutoka NMB Vicky Bishubo (aliyevaa skafu).


Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema kuwa wakati serikali ikijiandaa kufanya marekebisho makubwa ya sera ya kilimo, taasisi za kifedha nchini zitajumuishwa katika kutoa maoni jinsi gani zinaweza kushiriki kikamilifu kwenye kilimo. 

Alisema kuwa serikali kupitia wizara ya kilimo imepanga kuweka mazingira rafiki kwa taasisi za kifedha ili ziwekeze kwenye sekta hiyo, ikiwa pamoja na kuangalia mfumo gani sahihi wa utolewaji mikopo kwa wakulima. 

Naibu Waziri huyo ameyasema hayo jana wakati alipotembelea banda la Benki ya NMB kwenye maonyesho ya sikuu ya wakulima kitaifa (Nanenane) yanayoendelea katika viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu. 

Alisema kuwa kumekuwepo na tatizo la pembejeo hasa kwenye kilimo cha pamba, ambapo serikali kupitia bodi ya pamba imekuwa ikitumia fedha nyingi kuziagiza na kupelekwa kwa wakulima lakini matokeo yamekuwa hayaonekani. 

“Nitakutana na taasisi zote za fedha tufanye majadiliano kwenye sera mpya wa kilimo wao wanaweza vipi kushiriki moja kwa moja mpaka kwa wakulima, wanaweza vipi kuweka mfumo mzuri na rahisi wa kutoa mikopo kwa wakulima wa chini,” alisema Bashe. 

“ Tunahitaji benki zihusike katika kubadilisha mfumo wa kuagiza pembe nje, tuache kutumia mawakala na baadala yake twende moja kwa moja viwandani kwa kutumia fedha zao na zitarejeshwa na wakulima mara baada ya kuvuna,” aliongeza Bashe. 

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Biashara za serikali Vicky Bishubo kutoka NMB alisema kuwa taasisi za kifedha kujumuishwa kwenye marekebisho ya sera hiyo ni suala muhimu. 

Alisema NMB kupitia kilimo biashara (Agri-business) utakuwa wakati sahihi katika kuhakikisha wakulima na wajasliamali nchini wanawezeshwa zaidi kupitia vikundi vyao ili waweze kuongeza tija katika uzalishaji. 

Aliongeza kuwa NMB inatambua kuwa inalo jukumu kubwa la kuhakikisha wakulima na wananchi wote maeneo ya vijini, wanajumuishwa katika mfumo rasmi wa fedha kupitia kupewa elimu na mafunzo. 

Naye Meneja Mwandamizi katika mahusiano ya biashara ya kilimo kutoka NMB, John Mchunda alisema kuwa benki hiyo ilitenga kiasi cha sh. Bilioni 500 kwenye kilimo- biashara kwa muda wa miaka mitano toka mwaka 2015 kwa ajili ya kusaidia mnyororo wa thamani kwenye sekta ya kilimo na wakulima wenyewe. Na baada ya fedha hizo kuisha mwaka jana, NMB imeongeza bilioni 500 nyingine kusaidia kukuza mnyororo wa thamani (Agricultural value Chain) kwa wakulima, Wafugaji na wavuvi na biashara zao. 

MBUNGE MASAUNI AGEUKIA ELIMU JIMBONI KIKWAJUNI

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni,akizungumza katika Kikao cha Wadau wa Elimu lengo ikiwa kujadili jinsi ya kutatua tatizo la kufeli mitihani kwa shule zilizopo katika jimbo hilo,kulia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Riziki Pembe Juma.Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari,Haile Sellasie,Visiwani Zanzibar.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Riziki Pembe Juma, akizungumza wakati wa Kikao cha Wadau wa Elimu kilichoitishwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), kujadili jinsi ya kutatua tatizo la kufeli mitihani kwa shule zilizopo katika Jimbo hilo.Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari,Haile Sellasie,Visiwani Zanzibar.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni, Nassor Saleh Jazeera, akizungumza katika Kikao cha Wadau wa Elimu lengo ikiwa kujadili jinsi ya kutatua tatizo la kufeli mitihani kwa shule zilizopo katika jimbo hilo.Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari,Haile Sellasie,Visiwani Zanzibar.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mwalimu Mstaafu, Ameir Njeketu, akizungumza wakati wa Kikao cha Wadau wa Elimu kilichoitishwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani), kujadili jinsi ya kutatua tatizo la kufeli mitihani kwa shule zilizopo katika Jimbo hilo.Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari,Haile Sellasie,Visiwani Zanzibar.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Haille Selasie Ameir, Almas Mohammed, akizungumza wakati wa Kikao cha Wadau wa Elimu kilichoitishwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani), kujadili jinsi ya kutatua tatizo la kufeli mitihani kwa shule zilizopo katika Jimbo hilo.Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari,Haile Sellasie,Visiwani Zanzibar.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

KABENDERA APANDISHWA KIZIMBANI,ATUHUMIWA KUONGOZA GENGE LA UHALIFU,KUKWEPA KODI NA KUTAKATISHA FEDHA.

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi TV.

Mwandishi Wa Habari za uchunguzi Erick Kabendera amepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mshtaka ya kuongoza genge la Uhalifu, kukwepa kodi na kutakatisha zaidi ya sh. Milioni 173.2.

Hati ya mashtaka dhidi ya mshtakiwa Kabendera imesomwa na mawakili wawili wa wakuu wa serikali, na mmoja Mwandamizi mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustine Rwizile.

Mshtakiwa Kabendera anatetewa na mawakili wa kujitegemea, Gebra Kambore, John Mallya na Benedict inshabakaki.

Akisoma shtaka la kwanza, wakili wa serikali Mkuu, Paul Kadushi amedai, mshtakiwa anadaiwa katika siku tofauti tofauti kati ya Januari 2015 na Julai 2019 katika maeneo tofauti jijini Dar es Salaam, mshtakiwa Kabendera alitoa msaada katika genge la uhalifu kwa nia ya kujipatia faida.

Katika shtaka la pili lililosomwa na wakili Wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi imedaiwa, siku na mahali hapo mshtakiwa  bila kuwa na sababu za msingi kisheria alishindwa kulipa kodi ya sh. 173, 247,047.02 ambayo ilitakiwa ilipwe kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)

Katika shtaka la utakatishaji fedha lililosomwa na wakili Wa serikali Mwandamizi, Wankyo Simon imedaiwa, kati ya Januari 2015 na Julai 2019 ndani ya jiji na mkoa wa Dar es Salaam mshtakiwa alijipatia kiasi hicho cha sh. Milioni 173.2 wakati akizipokea alijua kuwa fedha hizo ni mazao ya makosa tangulizi ya kukwepa Kodi na kujihusisha na genge la uhalifu.

Hata hivyo, mshtakiwa Kabendera hakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo isipokuwa kwa kupata kibali kutoka kwa DPP.

Mawakili wa utetezi wakiongozwa na wakili Kambore, wameomba upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi haraka kwani kesi dhidi ya mteja wao haina dhamana. Hivyo katika terehe itakayokuja wangependa kujua upelelezi umefikia wapi.Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 19 Mwaka huu, mshtakiwa amepelekwa rumande.

Katika hatua nyingine Wakili wa upande utetezi Jebra Kambole ameiomba mahakama kuondoa maombi yao ya awali ya kutaka mshitakiwa afikishwe mahakamani na kupatiwa dhamana  lakini kwa sababu kwa sababu mshtakiwa ameishafikishwa mahakamani na mashtaka yake hayana dhamana hivyo wanaomba kuondoa maombi yao.

Hakimu Rwizile aliyaondoa maombi hayo kama walivyoomba upande wa utetezi utetezi.

INTRODUCING "ISWEKE" BY BARNABA

TIGO YASHIRIKI KWA KISHINDO MAONESHO YA NANE NANE MKOANI ARUSHA

$
0
0
Wananchi wanaotembelea maonyenesho ya Kilimo na Mifugo ya Nane nane, kwenye viwanja vya Taso Njiro jijini Arusha, wakipata huduma za usajili wa kadi za simu za mtandao wa Tigo kwa kutumia alama za vidole na kununua simu janja katika banda lake la maonyesho lililopo kwenye maonyesho hayo.

RAIS DKT MAGUFULI AFUNGUA MAADHIMISHO YA AWAMU YA NNE YA WIKI YA VIWANDA KWA NCHI ZA SADC JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo ya aendeleo ya ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji waShirika la Reli Tanzania TRC) alipotembelea banda la kampuni hiyo akiwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Maonesho ya  Maadhimisho ya Awamu ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumattu Agosti 5, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo ya kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege nchini (ATCL) Mhandisi Ladislaus Matindi lipotembelea banda la kampuni hiyo akiwa mgeni rasmi katika ufunguzi rasmi wa Maonesho ya
Maadhimisho ya Awamu ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumattu Agosti 5, 2019
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo ya maendeleo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Bw. Abdulmajid Nsekela katika banda la benki hiyo kabla ya kuzindua rasmi maonesho ya Maadhimisho ya Awamu ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Agosti 5, 2019. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia kiatu  wakati alipotembelea banda la Kiwanda cha Viatu cha BORA kabla ya kuzindua rasmi maonesho ya Maadhimisho ya Awamu ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Agosti 5, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo ya wakati alipotembelea banda la Shirika la Umoja wa Mataifa la Viwanda (UNIDO)  kabla ya kuzindua rasmi maonesho ya Maadhimisho ya Awamu ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Agosti 5, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Bw. Waziri Kindamba na wafanyakazi wengine wa Shirika wakati alipotembelea banda la TTCL kabla ya kuzindua rasmi maonesho ya Maadhimisho ya Awamu ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo
Agosti 5, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia burudani wakati akitembelea amabanda kabla ya kuzindua rasmi maonesho ya Maadhimisho ya Awamu ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika Ukumbi wa
Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Agosti 5, 2019. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na meza kuu wakimsikiliza  Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa akiongea kabla ya kumkaribisha kuzindua rasmi maonesho ya Maadhimisho ya Awamu ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Agosti 5, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wakati akifungua rasmi Maadhimisho ya Awamu ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Agosti 5, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana Mikono na Mwenyekiti wa baraza la Biasharta wa SADC aliyemaliza Muda wake Bi. Charity Mwiya akkiwa na mrithi wake Bw. Shamte wakati akifungua rasmi Maadhimisho ya Awamu ya Nne ya Wiki ya Viwanda kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Agosti 5, 2019.


GIRLTALKS TUVUNJE UKIMYA: FIKRA POTOFU NA MIIKO JUU YA HEDHI | CHANG'OMBE SECONDARY SCHOOL 19TH JULY 2019

$
0
0
Moja ya mwanzilishi wa mpango wa "Her Africa", Bi. Zena Tenga (kushoto) na mwezeshaji Bi Erica Zilinde (kulia) wakiongea na wanafunzi wa kike wa kidato cha 1 na 2 kutoka Chang'ombe secondary kuhusu fikra potovu na miiko juu ya hedhi kama sehemu ya kampeni ya mpango huo iitwayo "Hedhi yangu, Furaha yangu" inayolenga kuelimisha wasichana juu ya hedhi salama na pia kutoa vifaa vya hedhi kwa wasichana nchini Tanzania. 
Wanafuzi wa kike wa kidato cha kwanza na cha pili kutoka shule ya secondary ya Chang'ombe wakifurahia mifuko yenye vifaa vya hedhi waliyo pewa na mpango wa "Her Africa" kama sehemu ya kampeni yao iitwayo "Hedhi yangu, Furaha yangu" inayolenga kuelimisha wasichana juu ya hedhi salama na pia kutoa vifaa vya hedhi kwa wasichana nchini Tanzania. Jumla ya mifuko 85 ilitolewa kwa wasichana hao.
Daktari Elaina Lengereli na nesi Ziada Kabanda kutoka Sisa Community Center wakiongea na wanafunzi wa kike wa kidato cha 1 na 2 kutoka Chang'ombe secondary kuhusu hedhi salama na afya ya msichana kama sehemu ya kampeni ya mpango wa "Her Africa" iitwayo "Hedhi yangu, Furaha yangu" inayolenga kuelimisha wasichana juu ya hedhi salama na pia kutoa vifaa vya hedhi kwa wasichana nchini Tanzania.

KIGOMA KUANZA ZOEZI LA KUPIMA UTAYARI WA KUKABILIANA NA MLIPUKO WA UGONJWA WA EBOLA.

$
0
0

Na Editha Karlo Michuzi tv,Kigoma

SEREKALI ya Tanzania kupitia uratibu wa wa ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na watoto zitafanya zoezi la kupima utayari wa sekta ya afya,wadau mbalimbali na jamii kwa ujumla katika kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola endapo utatokea.

Bashiru Taratibu mkurugenzi msaidizi wa utafiti na mipango idara ya menejimenti maafa ofisi ya Waziri Mkuu aliyasema hayo leo wakati wa kikao cha wadau mbalimbali watakaoshiriki katika zoezi la kuigiza hali halisi ya utayari wa kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola na mazoezi ya utayari.

Alisema kuwa zoezi hilo litazingatia dhana ya afya moja ambayo hujumuisha sekta ya afya ya mifugo,binadamu,mifugo,wanyamapori na mazingira katika kujiandaa,kufuatilia na kukabili magonjwa ambayo huambukizwa kutoka kwa wanyama kwenda binaadam."Zoezi hili litapima uelewa wa jamii kuhusu namna ambavyo wanapaswa kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa ebola ukitoke hivyo wakati wa zoezi watoa huduma za afya na sekta zingine watakuwa wakifanya zoezi hilo kwa vitendo"alisema

Alisema zoezi hilo litafanyika kuanzia tarehe 5 hadi 9 Agosti katika vituo vya kutolea huduma za afya na maeneo ya mipaka ya Mkoa wa Kigoma.Taratibu alisema kuwa katika zoezi hilo watoa huduma wa afya watakuwa wakifanya zoezi hilo kwa vitendo namna ha kumuhudumia mgonjwa wa ebola atakapogundulika.

Mgeni rasmi katika kikao hicho Daniel Machunda katibu Tawala msaidizi rasilimali watu kwaniaba ya katibu wa Mkoa wa Kigoma Rashid Mchata alisema Mkoa wa Kigoma una njia nyingi zisizo za halali za mipakani(panya road)ambazo zinachangia hatari ya ugonjwa wa Ebola kuingia nchini.

Aliwataka wananchi kuchukua tahadhari hasa wale wanaovuka mipaka kwenda nchi za jirani."Ikumbukwe kuwa zoezi nila kupima utayari utayari kwa Mkoa wa Kigoma na hakuna mgonjwa yeyote wa ebola aliyeripotiwa hadi sasa nchini"alisema Machunda

Mganga mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dkt Paul Chawote alisema kuwa nchi ya jirani ya DRC(Congo)imeendelea kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola tangu Agosti 2018 hadi tarehe 31 Julai 2019 jumla ya watu 2673 waliathiriwa na ugonjwa huo.

Alisema idadi ya vifo vilikuwa 1823 ikiwa ni sawa na asilimia 67 ya idadi watu walioathiriwa na ugonjwa huo huku nchi ya Uganda ambayo inapakana na DRC na Tanzania imekuwa na wagonjwa 3 wa Ebola kwa mujibu wa taarifa maambukizi hayo yametoka DRC.

"Kwenye mipaka yetu ya DRC na Burundi kuna mwingiliano mkubwa wa watu unaochangiwa na shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi hivyo vinachangia hatari zaidi ya ugonjwa wa Ebol kuingia nchini"alisema Dkt Chawote

Remidius Kakulu Afida Afya mwandamizi toka Wizara ya afya,jinsia,wazee na watoto alisema kuwa mpaka sasa mipaka iliyorasmi yote imethibitiwa na serikali imeshafunga vipima joto vya kisasa katika mipaka yote iliyo rasmi.

"Kuna ile mipaka ambayo siyo rasmi ambayo ipo kwenye vijiji na maeneo mengine tunawaomba viongozi wa vijiji pamoja na wananchi kutoa taarifa pale mgeni anapoingia au kumpeleka kituo cha afya ili aweze kupimwa"alisema
 Mgeni rasmi Daniel Machunda katibu msaidizi rasilimali watu akifungua kikao cha washiriki wa zoezi la kuigiza hali halisi ya utayari ya kukabiliana na ugonjwa wa Ebola
 Baadhi ya washiriki wa zoezi la kuigiza hali halisi ya utayari ya kukabiliana na ugonjwa wa ebola wakimsikiliza mtaalam toka Wizara ya afya.
 Viongozi wa meza kuu kutoka Shirika la afya Duniani,Wizara ya afya,jinsia,maendeleo wazee na watoto pamoja na viongozi wa Mkoa wa Kigoma wakifuatilia mada mbalimbali zinazotolewa juu ya zoezi la kuigiza hali halisi ya utayari ya kukabiliana na ugonjwa wa ebola
Washiriki kutoka halmashauri nne za Mkoa wa Kigoma wa zoezi la kuigiza hali halisi ya utayari ya kukabiliana na ugonjwa wa ebola wakiwa katika picha ya pamoja

IGP SIRRO: TUKO TAYARI KUKABILIANA NA UHALIFU NA WAHALIFU.

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro akimsikiliza Mratibu
Mwandamizi wa Programu za Mafunzo ya Kuzuia uhalifu Unaovuka Mipaka
Bwana Willem Els (kulia), kutoka Taasisi ya Mafunzo ya Usalama nchini Afrika ya Kusini wakati alipomtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es salaam leo kwa lengo la kubadilishana uzoefu kwenye masuala ya kiusalama. Picha na Jeshi la Polisi.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro akimsikiliza Mkurugenzi wa
Upelelezi wa Makosa ya Jinai CP Robert Boaz (wa pili kulia) wakati akito neno mbele ya Wajumbe kutoka Kituo cha Ufanisi cha Kuzuia na Kupambana na Ugaidi katika Ukanda wa Afrika Mashariki kilichopo Nairobi nchini Kenya, wakati Ujumbe huo ulipomtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es salaam leo kwa lengo la kubadilishana uzoefu kwenye masuala ya kiusalama. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, Mkurugenzi wa Upelelezi wa
Makosa ya Jinai CP Robert Boaz, wakiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe kutoka Kituo cha Ufanisi cha Kuzuia na Kupambana na Ugaidi katika Ukanda wa Afrika Mashariki kilichopo Nairobi nchini Kenya, wakati walipomtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es salaam leo kwa lengo la kubadilishana uzoefu kwenye masuala ya kiusalama. Picha na Jeshi la Polisi.

TAARIFA KUHUSU UWEPO WA MTU ANAYESADIKIWA KUWA NI MCHAWI WODINI

SIMBA CREAM TANGA WATOA MSAADA KITUO CHA KULEA WATOTO YATIMA RASKAZONE CHA CASAFAMILIA ROSSETE

$
0
0
KATIBU Msaidizi wa Tawi la Simba Cream la Jijini Tanga Edgar Mdime ambaye pia ni Mweka Hazina kulia akimkabidhi biskuti mtoto Huchirachi Ally leo anayelelewa kwenye kituo cha Kulea watoto yatima cha Casafamilia Rosetta Centre kilichopo Raskazone Jijini Tanga wakati wapenzi na wanachama wa Simba Jijini Tanga walipokwenda kutoa misaada kwenye kituo hicho ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya simba
KATIBU Msaidizi wa Tawi la Simba Cream la Jijini Tanga Edgar Mdime ambaye pia ni Mweka Hazina kulia akimkabidhi biskuti mtoto Huchirachi Ally leo anayelelewa kwenye kituo cha Kulea watoto yatima cha Casafamilia Rosetta Centre kilichopo Raskazone Jijini Tanga wakati wapenzi na wanachama wa Simba Jijini Tanga walipokwenda kutoa misaada kwenye kituo hicho ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya simba
KATIBU Msaidizi wa Tawi la Simba Cream la Jijini Tanga Edgar Mdime ambaye pia ni Mweka Hazina kulia akimkabidhi msaada wa vitu mbalimbali Mkurugenzi wa MKURUGENZI wa Kituo hicho Irine Kaoneka
Sehemu ya wana Simba
Sehemu ya wana Simba wakiwa wamebabe vitu mbalimbali baada ya kufika kwenye kituo hicho
KATIBU Msaidizi wa Tawi la Simba Cream la Jijini Tanga Edgar Mdime kushoto akiwa na Mwanachama mwenzie Bertha Mwambela wakiingia kwenye kituo hicho wakiwa na vitu mbalimbali
Sehemu ya vitu ambavyo vimekabidhiwa leo vikiwa vimetolewa
TAWI la Simba Cream la Jijini Tanga leo wamekabidhi misaada ya viti mbalimbali kwenye kituo cha Kulea watoto yatima cha Casafamilia Rosseta ikiwa ni kuelekea kilele cha siku ya Simba maarufu kama Simba Day. 

Hafla ya makabidhiano ya msaada wa vitu ulifanywa na katibu Msaidizi wa tawi la Simba Cream Edgar Mdime kwa Mkurugenzi wa Kituo hicho Irine Kaoneka .

Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo MKURUGENZI wa Kituo hicho Irine Kaoneka amesema kwamba wamekuwa wakiiombea kila mara klabu ya Simba iweze kufanya makubwa kwenye soka hapa nchini na nje ya mipaka ya Tanzania. 

Alisema kwamba wamefurahishwa na ugeni huo kutoka Simba Tanga kwani wamefanya jambo jema bibilia inasema ibada njema ni iliyosafi kusaidia jamii inayokuwa ikihitaji mahitaji mbalimbali 

“Hivyo kwa hili Simba Cream hapa mmefanya ibada njema na sisi tutaendelea kuiombea Simba kila wakati ili iweze kupata mafanikio makubwa pamoja na kuendelea kuiwakilisha nchi kwenye mashindano makubwa “Alisema 

Awali akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Katibu Msaidizi wa Tawi la Simba Cream la Jijini Tanga alisema kwamba wameamua kukabidhi msaada huo ili kurejesha shukrani kwa jamii 

“Leo hii tumekabidhi msaada huu tunaamini kwamba utakuwa chachu kwenye kituo hiki lakini pia niwatumie salamu watani wetu wa Jadi Yanga wajipange kwani msimu ujao hawatasalimika na kipigo kutoka kwa Mnyama “Alisema 

Mdime ambaye pia ni Mweka Hazina alisema pia utaratibu huu wa Simba Day umekuwa ukifanyika kwa kipindi cha miaka 10 sasa kwa kutoa misaada mbalimbali kwa watoto yatima na kuwafariji wagonjwa . 

Alisema wameandaa Coaster na wanachama 33 wataondoka kuelekea dar kwa ajili ya kushuhudia Simba day wamejipanga wapo vizuri na hawana presha. Hata hivyo alisema kutokana na uwepo kwa kikosi kipana ndani ya timu hiyo hakuna mtu ambaye wanaweza kumuogopa wala kushindana nao isipokuwa TP Mazembe. 

SPIKA NDUGAI AFUNGUA MKUTANO WA WABUNGE KUTOKA BARA LA ASIA NA AFRIKA UNAOHUSU MASUALA YA IDADI YA WATU NA MAENDELEO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akisalimiana na Balozi wa Japan nchini, Shinichi Goto wakati wa Mkutano wa Wabunge kutoka Bara la Afrika na Asia unaohusu masuala ya Idadi ya watu na Maendeleo katika Hoteli ya Serena, Jijini Dar es Salaam.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akifungua Mkutano wa Wabunge kutoka Bara la Afrika na Asia unaohusu masuala ya Idadi ya watu na Maendeleo katika Hoteli ya Serena, Jijini Dar es Salaam.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akifungua Mkutano wa Wabunge kutoka Bara la Afrika na Asia unaohusu masuala ya Idadi ya watu na Maendeleo katika Hoteli ya Serena, Jijini Dar es Salaam.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akisalimiana na Wabunge kutoka Bunge la India mara baada ya kufungua wa Mkutano wa Wabunge kutoka Bara la Afrika na Asia unaohusu masuala ya Idadi ya watu na Maendeleo katika Hoteli ya Serena, Jijini Dar es Salaam.
PICHA NA BUNGE
Viewing all 109996 articles
Browse latest View live




Latest Images