Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

IJUE KAMPUNI YA AIRBUS KWA UFUPI

$
0
0


Nilibahatika kutembelea Toulouse, Ufaransa, kujionea kiwanda cha kampuni ya Airbus ya kuundia ndege. Ila nimestuka kusikia kwamba Kampuni ya Airbus imetangaza kwamba itasitisha uundwaji wa ndege zake kubwa za abiria za A380 baada ya mteja wake mkuu Emirates Airline kupunguza oda ya ndege mpya 39.
Baada ya kuwekeza sana kwenye ndege hiyo ya A380, kampuni hiyo kubwa kuliko zote za Ulaya ilitegemea kumshinda mshindani wake mkuu anayetamba kwa ndege yake ya Boeing 747. Lakini wateja wameonekana kutamani ndege ndogo zaidi ambazo gharama ya uendeshaji ni ndogo.
Kampuni hii ndiyo inayounda na kuuza ndege kubwa kuliko zote za abiria za A380, wakati ndege yake ya 10,000, aina ya A350, imenunuliwa mwaka juzi na Singapore Airlines. Kwa jumla ndege za Airbus zimefanya safari milioni 110, ambazo ni kilometa bilioni 215 na kubeba abiria bilioni 12.
Kati ya mwaka 2000 hado 2014 kampuni ya Airbus ilijulikana kama European Aeronautic Defence and Space Company (EADS), ikiwa ni shirika la Ulaya likiwa limesajiliwa Uholanzi na kuwa na hisa za kibiashara na Ufaransa, Ujerumani na Hispania. Shughuli yake kuu ni kuunda na kuuza vifaa vya anga duniani kote, ikiwa na divisheni tatu za kuunda na kuuza ndege za kibiashara, ulinzi na anga na helikopta. 
Shughuli kuu za uundaji wa ndege za biashara zipo mjini Blagnac, Ufaransa, kwenye kitongoji cha mji wa Toulouse, wakati shughuli za uundaji na uzalishaji wake zikiwa Ulaya (Ufaransa, Ujerumani, Spain na Uingereza) na pia nchini China na Marekani.
Sehemu kuu za mwisho za kuunganisha ndege zipo Toulouse, Ufaransa, Hamburg, Ujerumani, Seville, Spain, Tianjin, China na Mobile, Alabama, Marekani.

Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) lina ndege mbili aina ya Airbus A22-300 ambazo pamoja na Beoing 787 Dreamliner zililetw3a kati ya mwezi Mei na Desemba mwaka 2018. 
Kabla ya hapo ndege mbili za Bombadier CASH8 Q400 zililetwa Septemba 2016 na ingine Juni 2017. Hadi Julai mwaka jana shirika hilo lilikuwa linaendesha kazi kwa ndege saba, ikiwemo Bombadier DASG8 Q300 iliyokuwa ikitoa huduma tangia mwaka 2011.

CPB KUZINDUA KINU CHA KUSAGIA NAFAKA KILICHOWAHI KUKODISHWA

$
0
0
SERIKALI kupitia Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) itazindua kinu cha kusagishia nafaka Mkoani Arusha baada ya kuwa chini ya mkodishaji kwa muda mrefu.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Jijini Arusha leo Kaimu Meneja wa Bodi hiyo Kanda ya Kaskazini Kulwa Stephen amesema uzinduzi huo utaanza wiki hii kwa kuiwasha mashine kiwandani hapo kwa majaribio baada ya kufanyika ukarabati mkubwa katika mitambo ya kusagishia nafaka pamoja na maeneo mengine ya kiwanda.

Kaimu Meneja huyo amesema serikali ya awamu ya tano imefanya kazi kubwa katika kurejesha baadhi ya viwanda kutoka maeneo mbalimbali ili kuhakikisha wananchi walio wengi wanapata huduma au bidhaa muhimu ya unga. 

Bodi hii ya Nafaka ambayo awali ilikuwa ikijulikana kama National Milling Cooperation (NMC) na kusitishwa uzalishaji wake na baadae mwaka 2009 serikali ikaunda Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko kwa sheria namba 19.

Kiwanda hiki ni kikubwa kwani kinasagisha unga tani 60 kwa siku na unga huo maarufu uitwao DONA BORA CHAPA NGUVU hivyo kwa mwaka huzalisha zaidi ya tani 18,000 sawa na kinu kingine kilichopo mkoani iringa ambacho pia husagisha tani 60 kwa siku. 

Pia ametoa wito kwa wakazi wa mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga na Dar Es Salaam kukaa mkao wa kula baada ya uzalishaji huu mkubwa kuanza na amesema Bodi itawatumia mawakala mbalimbali katika mauzo mawakala ambao wanaendelea kusajiliwa  na wananchi watarajie kupata bidhaa hii moja kwa moja baada ya kuikosa kwa muda mrefu.

Ameyataka pia mashule na vyuo kuja kupata huduma ya unga huu ambao unawafaa zaidi wanafunzi katika kuwajengea utimamu wa afya.


Aidha amezungumzia ubora wa mashine za kusagishia unga huo kwa kutaja hatua muhimu kuanzia shambani kwa wakulima ambao hupewa mafunzo maalum na serikali katika kulima hasa matumizi ya madawa, kuhifadhi pamoja na kudhibiti unyevunyevu.

Amesema mahindi hayo yanapofika ngazi ya kusagishwa huondolewa takataka zote yakiwemo magunzi, mawe na vitu vingine hatarishi kwa mraji na mwisho, mahindi humenywa na kuacha kiini ambacho hubeba vitamin muhimu kwa walaji wa ugali au uji na kuongeza afya ya mwili kwa mlaji.

Ameongeza kuwa mashine za kumenyea mahindi kiwandani hapo zina ubora wa hali ya juu sana na zimethibitishwa  ubora  na mamlaka zote ikiwemo TBS na mamlaka zingine kwa ajili ya usalama wa kiafya ya mlaji.

Uanzishwaji wa Bodi ya Nafaka kwa mujibu wa sheria ilikuwa na lengo la kununua mazao ya Nafaka, kuongeza thamani na kuuza ndani na nje ya nchi.

Pia kuhusu ajira amesema jamii itapata ajira za aina mbalimbali kutokana na uwepo wa ajira za kudumu pamoja na vibarua wa muda mfupi ambao watakuwa wakijipati huduma za vyakula kwa mama Lishe, vinywaji na mahitaji mengine muhimu.

Kwa sasa ajira za moja kwa moja na vibarua pamoja na madereva lazima na mama Lishe zitanufaisha jamii kubwa katika maeneo yanayozunguka kiwanda hiki.

Kaimu meneja huyo akizungumzia ukubwa wa soko la bidhaa katika maeneo ya karibu pamoja na nchi za jirani  amesema  hivi karibuni serikali kupitia naibu waziri wa Kilimo imepata oda ya mahindi mengi kiasi cha tani millioni 1 kutoka nchini Kenya na kwa kupeleka mahindi nchini Kenya kutaongeza tija kwa kiwanda na kujitanua zaidi katika uzalishaji. 

Vilevile amegusia bidhaa ya Pumba za mahindi kwa ajili ya wafugaji wa mazao ya mifugo mbalimbali na kuwataka wananchi hao wafike kiwandani hapo kwani kuna duka kubwa na Unga pamoja na Pumba kwa bei nafuu.

Amemalizia kwa kuzungumzia huduma ya mzani katika kiwanda na kuwataka wasafirishaji wa mizigo kutumia mzani uliopo ambao hupima tani 1 mpaka  50,000 kwa bei nafuu.

Kwa sasa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko  inazo ofisi katika Mikoa mbalimbali kama vile Arusha, Dar Es Salaam, Dodoma, Iringa, Mwanza pia hivi karibuni ofisi zingine zitaendelea kufunguliwa na kufanya kazi na majukumu yote ya iliyokuwa Shirika la Usagishaji la Taifa NMC

SERIKALI YASEMA KIPAUMBELE CHA UMEME VIJIJINI NI KWA TAASISI ZA UMMA

$
0
0
Na Veronica Simba – Kilimanjaro
Serikali imesema kipaumbele cha kupeleka umeme vijijini ni kwa taasisi za umma pamoja na miradi mbalimbali ya maendeleo inayohudumia wananchi.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani aliyasema hayo kwa nyakati tofauti, jana Julai 30 akiwa katika ziara ya kazi wilayani Same na Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kalemawe, wilayani Same, muda mfupi baada ya kuwasha rasmi umeme, Waziri aliwasisitiza viongozi wa taasisi na miradi mbalimbali ya umma kulipia gharama za kuunganishiwa umeme ili huduma hiyo ipelekwe katika taasisi zao badala ya kuendelea kulalamika pasipo kuchukua hatua.

“Niwaambie ukweli ndugu zangu; kuanzia sasa sitaruhusu kiongozi wa taasisi au mradi wa umma kusimama na kulalamika kuwa taasisi yake haina umeme, wakati yeye mwenyewe hajalipia huduma hiyo. Sitampa nafasi. Lipieni ndipo mdai umeme.”

Akifafanua zaidi, Waziri Kalemani alisema kuwa, kutokana na umuhimu wa taasisi za umma kuwa na umeme, Wizara yake imeweka mkakati wa kupeleka huduma hiyo kwenye taasisi yoyote iliyolipia pasipo kujali umbali ilipo. “Hata kama haiko kwenye mpango wa kupelekewa umeme kwa wakati huo; ilimradi imelipiwa, tutaifuata na kuiunganishia.”

Aidha, Waziri Kalemani aliwaambia wanafunzi wa shule ya sekondari Kihurio wilayani Same, wautumie umeme ambao serikali imewapelekea, kuboresha zaidi kiwango cha ufaulu. Kwa upande wa waalimu, aliwataka kuutumia umeme huo kufanya maandalizi ya kufundisha vema zaidi lakini pia kwa maendeleo yao binafsi.

Katika ziara hiyo, Waziri pia aliwasha umeme katika kijiji cha Kigonigoni, wilayani Mwanga ambapo aliwahamasisha wananchi ambao hawajaunganishiwa umeme, kuondokana na kasumba ya kujidharau kuwa hawastahili kuunganishiwa umeme kutokana na aina ya makazi waliyonayo.
“Ndugu zangu, Rais Magufuli ametuagiza tuwaunganishie umeme wananchi wote pasipo kujali aina ya makazi waliyonayo, hivyo nanyi muache kujibagua. Umeme hauchagui nyumba. Tafadhali lipieni shilingi 27,000 ili muunganishiwe,” alisisitiza.

Awali, akiwasilisha kwa Waziri taarifa ya utendaji kazi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoani Kilimanjaro, Meneja husika, Mhandisi Mahawa Mkaka, alisema hali ya usambazaji umeme mkoani humo imeendelea kuimarika kutokana na utekelezaji wa miradi ya kusambaza umeme vijijini na miradi mbalimbali inayotekelezwa na shirika hilo.

Alisema, mpaka sasa vijiji 453 kati ya 519 vimeshapelekewa umeme ambapo ni sawa na asilimia 87.28 na kwamba, matarajio ni kufikia vijiji 493 sawa na asilimia 95 ifikapo Desemba, 2019.

Kwa upande wao, Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Same, Anna Kilango Malecela na Mbunge wa Mwanga (CCM), Jumanne Maghembe, kwa nyakati tofauti waliipongeza serikali kupitia Wizara ya Nishati, kutokana na kazi nzuri inayofanyika, kupeleka umeme katika maeneo ambayo hayakutarajiwa, hususan kwa wananchi walioko vijijini.
Waziri amekamilisha ziara yake mkoani Kilimanjaro na ataendelea na ziara hiyo katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kalemawe, Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro muda mfupi baada ya kuwasha umeme katika Zanahati ya kijiji hicho akiwa katika ziara ya kazi Julai 30, 2019.
 Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, akikata utepe kuashiria uwashaji rasmi umeme katika kijiji cha Kalemawe kilichopo wilayani Same, Mkoa wa Kilimanjaro, Julai 30, 2019. Kulia kwake ni Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Same, Anna Kilango Malecela.
 Sehemu ya umati wa wananchi wa kijiji cha Kalemawe wilayani Same, Mkoa wa Kilimanjaro, wakishuhudia tukio la kuwashwa rasmi umeme katika kijiji hicho. Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) aliwasha umeme katika Zahanati ya Kijiji hicho, Julai 30, 2019.
 Umati wa wanafunzi na walimu wa shule ya sekondari Kihurio iliyopo wilayani Same, Mkoa wa Kilimanjaro wakishuhudia tukio la kuwashwa umeme katika shule hiyo. Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani), aliwasha umeme katika shule hiyo, Julai 30, 2019.
 Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Kijiji cha Kigonigoni, wilayani Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro, alipowasili kwa ajili ya kuwasha rasmi umeme katika kijiji hicho. Kulia, ni Mbunge wa Mwanga (CCM), Jumanne Maghembe.
Taswira ya nyumba ya mmoja wa wakazi wa kijiji cha Kigonigoni, wilayani Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro kama ilivyonaswa muda mfupi kabla ya Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) kuiwashia rasmi umeme, Julai 30, 2019.

DKT. MPANGO: FANYENI KAZI KWA KUZINGATIA MAADILI, KANUNI NA TARATIBU ZA UTUMISHI WA UMMA

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango awataka Waajira wapya  wa Wizara hiyo kufanya kazi kwa kuzingatia maadili, kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma.

Hayo ameyasema alipofanya nao kikao cha kuwakaribisha wizarani hapo Jijini Dodoma, ambacho kilihudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Utawala Dkt. Khatibu Kazungu, Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Sera Bw. Adolf Ndunguru na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara hiyo.

Akizungumza katika kikao hicho Dkt. Mpango alisema kuwa  anatarajia kuona watumishi hao wanafanya kazi kwa kwa bidi na  kujituma,  na kuwa wazalendo kwa nchi yao.

“Umasikini wa watanzania uwasukume kufanya kazi kwa bidii, nchi ina rasilimali nyingi lakini asilimia 26.4 ya wananchi bado hawapati mahitaji ya msingi hivyo tufanye kazi kwa bidii kusaidia watu kuondokana na umasikini.”Alisisitiza Waziri Mpango.

Aliwataka  Watumishi hao kutumia ujuzi wao kufanya kazi kwa weledi mkubwa kwa hadhi ya kimataifa kwa kuzingatia  uadilifu na uaminifu katika kutekeleza majukumu yao.

AIDHA, Dkt. Mpango amewataka Viongozi wa Wizara hiyo, kuwapa ushirikiano Watumishi hao na kuwa tayari kuwasaidia na kuwaelekeza katika majukumu yao watakayo wapangia lakini pia wawe tayari kujifunza kutoka kwao.

‘’Muwe tayari kuwasikiliza na kuwasaidia watakapopata changamoto katika utekelezaji wa majukumu yao”,alisema Dkt. Mpango.

Aliwataka Watumishi hao kuhakikisha wanajiendeleza kielemu wanapopata nafasi na kutoridhika kwa elimu waliyokuwa nayo kutokana na ukuaji wa teknolojia.

Dkt. Mpango alisema Wizara hiyo inamajukumu mengi takribani 20 ikiwemo kubuni na kusimamia sera za bajeti, fedha,ununuzi wa umma pamoja na ubia kati ya sekta za umma na sekta binafsi.

Aliongeza kuwa utekelezaji wa dira ya Taifa, kupanga na kutekeleza mandeleo ya uchumi yaende wapi, pia  ina jukumu la kuandaa muongozo wa bajeti ya Serikali na utekelezaji wake.

Naye mmoja wa Waajiriwa wapya ameishukuru Serikali kwa kutoa ajira na kuahidi kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia madili ya Utumishi wa Umma.

Jumla ya Watumishi  wapya 70  wa kada mbalimbali  wakiwemo Wachumi na Wasimamizi wa Fedha wameajiriwa katika Wizara  ya Fedha na Mipango ikiwa ni ajira yao mpya.
 Mkurugenzi wa Utawala na Rasimali Watu  wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw.  Michael John akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara  hiyo  Bw. Adolf Ndunguru  aweze kumkaribisha Waziri  wa Wizara hiyo Dkt. Philip Isdor Mpango ili aweze kuzungumza  na Waajiriwa wapya wa Wizara hiyo (hawapo pichani), Jijini Dodoma.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Adolf Ndunguru akimkaribisha Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Philip Isdor Mpango aweze kuzungumza na Waajiriwa wapya wa Wizarahiyo mkoani Dodoma.
 Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na Waajiriwa wapya, alipofanya nao mkutano Jijini Dodoma na kuwataka waajiriwa hao kufuata maadili ya Utumishi wa Umma.
 Baadhi ya Waajiriwa wapya wa Wizara ya Fedha na Mipango wakimsikiliza Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Philip Isdor Mpango (hayupo pichani), alipokuwa akizungumza wakati wa kikao Jijini Dodoma.
 Baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo vya Wizara ya Fedha na Mipango wakifuatilia kwa karibu kikao cha Waajiriwa wapya  wa Wizara hiyo, kiliongozwa na Waziri wa Wizara hiyo  Dkt. Philip Isdor Mpango (hayupo pichani), Jijini Dodoma.
 Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango akizungumza na Waajiriwa wapya, alipofanya nao mkutano Jijini Dodoma.
 Meza kuu ikiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anayeshughulika Utawala Dkt. Khatibu Kazungu, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anayeshughulikia Sera Bw. Adolf Ndunguru na Mkurugenzi wa Utawala na Rasimali Watu wa Wizara hiyo Bw.  Michael John wakiteta jambo wakati wa kikao na Waajiriwa wapya (hawapo pichani) Jijini Dodoma.
 Mwajiriwa mpya akitoa neno la shukrani kwaniaba ya Waajiriwa wapya kwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango kwa kutenga muda wake na kuzungumza nao Jijini Dodoma, na kuahidi kutekeleza kwa ufanisi  majukumu watakayopangiwa.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anayeshughulika Utawala Dkt. Khatibu Kazungu akimshukuru Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Philip Isdor Mpango (hayupo pichani), kwa kutenga muda wake kuzungumza na Waajiriwa wapya wa Wizara hiyo Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anayeshughulika Utawala Dkt. Khatibu Kazungu, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anayeshughulikia Sera Bw. Adolf Ndunguru na Mkurugenzi wa Utawala na Rasimali Watu wa Wizara hiyo Bw.  Michael John na Katibu wa TUGHE Bi. Jenjelly James wakiwa katika picha ya pamoja na Waajiriwa wapya  baada ya  kumalizika kwa kikao Jijini Dodoma.

WANANCHI WA KATA YA CHITA MELELA WAISHUKURU TARURA

$
0
0

Na Erick Mwanakulya.
Wananchi wa Kata ya Chita Melela iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro, wameshukuru Serikali kupitia Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) baada ya kutatuliwa kwa kero yao ya muda mrefu kwa kujengewa Daraja la Chuma (Mabey Bridge) lililopo Mto Kihansi ambalo linajengwa na TARURA chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Uingereza (DFID).

Hayo yameelezwa na wananchi waliojitokeza kushuhudia ujenzi wa Daraja hilo linalojengwa na Wahandisi wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), wakisaidiana na Mhandisi Mshauri Ebenezer Mollel pamoja na Mtaalamu wa Ufundi  John Hinderer kutoka Kampuni ya Mabey Bridge ya nchini Uingereza.

Wakielezea furaha yao juu ya ujenzi wa daraja hilo, wananchi hao wamesema kuwa wanaishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuwajengea daraja maana walikuwa wanapata shida kubwa hapo awali katika kusafirisha bidhaa zao na kupata huduma mbalimbali za kijamii kwani walikuwa wanatumia mtumbwi kuvuka Mto ambapo ni umbali takribani Km 1.5.

Kwaupande wake, Diwani wa Kata ya Chita Melela Mhe. Chelele John amesema, Serikali ya Awamu ya Tano inastahili kupongezwa kwa maana Daraja hilo ni kiungo muhimu katika uchumi wa Kata yake pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero kwa maana vyanzo vya mapato katika Kata za Mlimba, Chita, Mgeta, Mangula pamoja na Mchombe vitakusanywa kwa urahisi kutokana na uwepo wa daraja hilo.

“Tulikuwa tunatumia mtumbwi kuvuka Mto na wananchi walipata adha kubwa katika Kijiji chetu kwani kufikia huduma za kijamii ilikuwa changamoto kubwa, leo hii naona Wahandisi wa TARURA wapo hapa katika ujenzi wa Daraja hili, hii inadhihirisha kuwa Wakala upo katika kuhudumia wananchi ipasavyo nasi tunawaunga mkono”, alisema Diwani huyo.

Naye, Mratibu wa TARURA Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Godwin Mpinzile amesema Daraja la Chuma (Mabey Bridge) la Mto Kihansi limewekwa baada ya kutengeneza barabara ya Chita Melela yenye urefu wa Km 11.5 na litakuwa mkombozi kwa wananchi wa Chita kutokana na shida wanayoipata wakati wa mvua na kwamba Wakala utaendelea kuikarabati Barabara hiyo hadi kuunganisha Kata ya Mlimba ili kuwarahisishia wananchi kufanya shughuli zao za kila siku.

Pia, amewasihi wakazi wa Chita kutunza miundombinu ya Barabara pamoja na Daraja kwani gharama kubwa zimetumika katika ujenzi wa Daraja hilo.

Daraja la kisasa la Chuma (Mabey Bridge) ambalo limegharimu zaidi ya shilingi milioni 700 ni moja kati ya kazi za Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) katika kuboresha Barabara na kufanya matengenezo pamoja na ujenzi wa Madaraja ili kuwawezesha wananchi kufanya shughuli zao za kiuchumi.

Daraja hilo linalenga kutatua kero ya kudumu kwa wananchi wa Chita Melela kutokana na Madaraja ya hapo awali kusombwa na maji pale mvua zinaponyesha na linatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni.
 Daraja la awali la wananchi wa Kata ya Chita Melela lililopo Mto Kihansi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro, ambalo limekuwa likitumiwa na wakazi maeneo hayo kabla ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kutengeneza Daraja jipya la Chuma (Mabey Bridge) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Uingereza (DFID).
 Msolovea Gasto Kikuji kutoka Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) akiweka usawa na kupima eneo kabla ya kuanza kwa ujenzi wa Daraja la Chuma (Mabey Bridge) lililopo Mto Kihansi katika Halmashauri ya Wilaya kilombero, Mkoani Morogoro.
 Wahandisi kutoka Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) wakiwa katika ujenzi wa Daraja la Chuma (Mabey Bridge) lililopo Mto Kihansi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero, Mkoani Morogoro.
 Wahandisi kutoka Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) wakiwa katika ujenzi wa Daraja la Chuma (Mabey Bridge) lililopo Mto Kihansi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero, Mkoani Morogoro.
 Wahandisi kutoka Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) wakiwa katika ujenzi wa Daraja la Chuma (Mabey Bridge) lililopo Mto Kihansi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero, Mkoani Morogoro.
 Baadhi ya wananchi wa Kata ya Chita Melela wakishuhudia ujenzi wa Daraja la Chuma (Mabey Bridge) lililopo Mto Kihansi (halipo pichani) katika Halmashauri ya Wilaya ya kilombero, Mkoani Morogoro.
 Mtaalamu wa Ufundi John Hinderer kutoka Kampuni ya Mabey Bridge ya nchini Uingereza akiwapa maelekezo Wahandisi kutoka Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) jinsi ya kulifunga Daraja la Chuma (Mabey Bridge) lililopo Mto Kihansi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero, Mkoani Morogoro.
Muonekano wa Daraja la Chuma (Mabey Bridge) lililopo Mto Kihansi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero, Mkoani Morogoro baada ya kukamilika kwa ujenzi wa awali ambapo uzinduzi rasmi wa Daraja hilo utafanyika hivi karibuni. 

BALOZI IDDI AZINDUA MRADI WA MAJI KATIKA NYUMBA MPYA ZA ASKARI POLISI MAHONDA

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd(kulia), akifurahia baada ya kumtwisha ndoo ya maji mwananchi wa Mahonda baada ya Uzinduzi wa Mradi wa Maji kwenye Eneo la Nyumba za Polisi, zilizoko katika Jimbo la Mahonda, Mkoa wa Kaskazini Unguja.Wapili kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, akifungua bomba kuashiria Uzinduzi wa Mradi wa Maji kwenye Eneo la Nyumba za Polisi, zilizoko katika Jimbo la Mahonda, Mkoa wa Kaskazini Unguja. Aliyevaa koti ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, akimtwisha ndoo ya maji mwananchi wa Mahonda baada ya Uzinduzi wa Mradi wa Maji kwenye Eneo la Nyumba za Polisi, zilizoko katika Jimbo la Mahonda, Mkoa wa Kaskazini Unguja.Katikati ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

HASUNGA AITAKA NFRA KUTOA ELIMU YA MIFUKO YA PIC'S KWA WAKULIMA

$
0
0
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua Banda la Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) wakati akikagua maandalizi ya Maadhimisho ya 27 ya sikukuu ya wakulima maarufu kama (Nane Nane) yatakayofanyika kuanzia tarehe 1-8 Agosti 2019 Katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa na watumishi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) wakati akikagua maandalizi ya Maadhimisho ya 27 ya sikukuu ya wakulima maarufu kama (Nane Nane) yatakayofanyika kuanzia tarehe 1-8 Agosti 2019 Katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu. 
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akipewa maelezo kuhusu matumizi ya mifuko ya kuhifadhia mahindi ya PIC'S wakati alipotembelea Banda la Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) wakati akikagua maandalizi ya Maadhimisho ya 27 ya sikukuu ya wakulima maarufu kama (Nane Nane) yatakayofanyika kuanzia tarehe 1-8 Agosti 2019 Katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu. 

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Simiyu


Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga jana tarehe 30 Julai 2019 ametembelea na kujionea maandalizi ya Maadhimisho ya 27 ya sikukuu ya wakulima maarufu kama (Nane Nane) yenye lengo la kuwatambua na kuwaenzi Wadau Wakuu wa Sekta ya Kilimo ambao ni Wakulima, Wafugaji, Wavuvi, Wanaushirika, Wasindikaji wa mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi na maliasili kwa mchango wao mkubwa wanaoutoa katika kuendeleza uchumi wa nchi yetu. 

Mhe Hasunga pamoja na mambo mengine akiwa katika Banda la Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ameutaka uongozi wa taasisi huyo kuongeza juhudi za utoaji elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa matumizi ya mifuko maalumu ya kuhifadhia nafaka ya PIC'S.

Mhe Hasunga amesema kuwa NFRA inapaswa kutoa elimu hiyo ili iwafikie wakulima wengi kwani kufanya hivyo itarahisisha huduma za uhifadhi wa mahindi ya wakulima ambao kwa muda mrefu wamekumbwa na kadhia ya kushindwa kuhifadhi mahindi kwa ufasaha.

Pamoja na NFRA kutoa elimu kwa wakulima kupitia vipindi mbalimbali vinavyorushwa na Televisheni lakini pia amesisitiza kuwa NFRA inapaswa kuongeza uwezekano wa kuwafikia wakulima wengi zaidi.

Mwaka huu wa 2019, sherehe za Nanenane zinafanyika Kitaifa mjini Bariadi katika Viwanja vya maonesho ya kilimo Nyakabindi katika Mkoa wa Simiyu hivyo Mhe Hasunga amepongeza Uongozi wa mikoa ya Simiyu, Shinyanga na Mara kwa juhudi zao za kufanikisha kuingiza uwanjani huduma za msingi ambazo ni maji na umeme.

Alisema kuwa jukumu hilo kwa Serikali na Wadau wa Sekta Binafsi ni kuendeleza viwanja hivyo vya Nyakabindi kwa kujenga mabanda ya maonesho ya kudumu na kuboresha huduma muhimu za kijamii ili kuwe na maonesho endelevu yenye sura ya Kitaifa na Kimataifa.

Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula NFRA pamoja na Taasisi zingine za wizara ya Kilimo zimetuama Mkoani Simiyu kwa ajili ya kutoa elimu kwa wakulima kuhusu majukumu wayafanyayo kadhalika namna bora ya kuwa na Kilimo bora na chenye tija.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO.MHE.BASHE ATEMBELEA BANDA LA TAEC,ASHUHUDIA SHUGHULI MBALI MBALI ZINAZOFANYWA NA TAASISI HIYO MAONESHO YA NANE MKOANI SIMIYU

$
0
0
 Naibu wa Waziri wa Kilimo ,Mhe Husein Bashe akipata  maelezo toka kwa ofisa mwandamizi wa Utafiti vifaa vya Mionzi wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Bwana Yesaya  Sungita mara alipotembelea kwenye maonesho ya Nane nane yanayofanyika  kwenye uwanja wa Nyakabindi  Wilayani Bariadi ,mkoani Simiyu ambapo pamoja na mambo mengine , Mh Bashe amehoji ushirikiano wa TAEC na Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) na kupata majibu kuwa ushirikiano kwa Taasisi hizo upo.


DC ARUSHA AMPONGEZA MKURUGENZI WA JIJI KWA USIMAMIZI MZURI WA MIRADI.

$
0
0
Na Jusline Marco,Arusha

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe.Gabriel Daqqaro amempongeza Mkurugenzi wa jiji la Arusha Dkt.Maulidi Suleiman Madeni kwa usimamizi mzuri wa miradi inayoeatibiwa na ofisi ya rais,tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI chini ya Mkandarasi kutoka katika kampuni ya Synohindro Co Ltd ya nchini China na Mhandisi mshauri kutoka kampuni ya UWP Consult(T)Ltd.

Mhe.Daqqaro ametoa pongezi hizo wakati alipotembelea miradi ya ujenzi wa barabara za katikati ya mji,ujenzi wa uwanja wa michezo Ngarenaro pamoja na ujenzi wa bwawa la kuhifadhi taka ngumu lililopo katika eneo la Dampo la Murriet linalosimamiwa na mradi wa maji mkakati Tanzania awamu ya tatu jijini Arusha ikiwa ni moja za ziara zake za kikazi ambapo miradi hiyo imegharimu kiasi cha shilingi bilioni 22.3.

Vilevile miongoni mwa barabara ambazo Mhe.Daqqaro amezitembelea ni barabara ya Oljoro kwenda Murriet yenye urefu wa kilometa 2.85 ambapo ujenzi wa barabara hiyo umekamilika kwa kiwango cha lami huku ujenzi wa mifereji ya maji ya mvua,vivuko na njia za watembea kwa miguu ukiwa unaendelea.

Pamoja na hayo miradi mingine ya barabara ambayo imekamilika kwa kiwango cha lami ni pamoja na barabara ya Sombetini kwenda FFU yenye urefu wa kilometa 2.0,barabara ya Njiro yenye urefu wa kilometa 2.702 huku barabara ya Krokoni yenye urefu wa kilometa 0.575.

Hata hivyo ukaguzi wa miradi hiyo ni muendelezo wa ziara ya Mkuu huyo ndani ya Wilaya ya Arusha ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya CCM katika kuleta maendeleo ya wananchi.
 Wakandarasi kutoka katika kampuni ya Synohindro Co.ltd ya nchini China wakitoa maelezo ya ujenzi wa barabara kwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro
 Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro akipata maelekezo ya ujenzi wa bwawa la kuhifadhi taka Ngumu lililopo katika eneo la dampo Murriet Mkoani Arusha
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro akikagua ujenzi wa mifereji wa maji ya mvua

Vijana wa CCM waaswa kuwa wazalendo na kumsaidia kazi Rais Magufuli

$
0
0
Na Charles James, Michuzi TV

Vijana nchini wameaswa kuwa wazalendo Na wabunifu ili waweze kufikia malengo yao na kuacha kuwa tegemezi huku wakisubiri kuajiriwa na badala yake wajikite katika kujiajiri wenyewe.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Sehemu ya Utumishi na Utawala wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Veronica Ndavo wakati wa kuwaaga wanafunzi wa kitivo cha Tiba wa Chuo Kikuu cha Dodoma UDOM.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyoandaliwa na wanafunzi hao ambao ni wanachama wa CCM, Ndugu Veronica amewaasa vijana hao ambao ni wataalamu wa afya, wafamasia, wauguzi na maafisa wa mazingira na matibabu kuhakikisha wanatumia elimu waliyopata katika kukitumikia Chama chao, jamii inayowazunguka pamoja na Serikali.

" Nawapongeza sana kwa kuhitimu niwasihi mnapoelekea mtaani msibague kazi lakini pia hizo kazi zisishushe utu wako, nendeni mtaani mkafanye kazi ili tumsaidie Rais wetu katika kufikia uchumi wa viwanda.

" Niwapongeze pia kwa kukuza kipato cha tawi lenu la Chama kutoka Shilingi Laki Moja hadi kufikia Laki Sita, naahidi kuwapa ushirikiano na nitatoa mifuko ya Saruji yenye thamani ya Shilingi Laki Tatu, pamoja na vitendea kazi vyenu vya Chama zikiwemo Kompyuta ambayo nitaikabidhi hapa leo. Lengo letu ni kuona hamkwami kwenye shughuli zenu za Chama," amesema Veronica.

Aidha Veronica amekabidhi kiasi cha Shilingi Laki mbili kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya CCM ya Kata ya Ng'hong'hona ambayo kwa asilimia kubwa imekua ikitumiwa na wananchi hao ambao ni wanachama wa Chama hicho.

" Niwatake pia mkawe msaada mkubwa wa Chama chetu kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaokuja hivi karibuni, Rais wetu Dk John Magufuli amefanya kazi kubwa za kimaendeleo zawadi pekee tunayoweza kumpa ni ushindi wa kishindo wa CCM kwenye chaguzi hizi. Nyie ni vijana kaonesheni thamani yenu na nguvu yenu ndani ya Chama kwa kukisaidia kushinda uchaguzi huu," amesema Veronica.

Nae Katibu wa CCM Wilaya ya Dodoma Mjini, Diana Madukwa amemshukuru Bi Veronica kwa kujitoa kwake katika kuwachangia vijana hao na kuahidi kuendelea kuwalea wanafunzi wanaobakia katika maadili ya kiuongozi na yenye utumishi ndani ya Chama.

" CCM Wilaya tutaendelea kuwa bega kwa bega na vijana wanaohitimu na wale wanaobaki, tutawalea kichama ili kutimiza ndoto zenu za kuwa viongozi wakubwa kisiasa na kiserikali lakini zaidi kuwa wanachama waaminifu na wazalendo kwa Nchi yao," amesema Diana.
 Mkuu wa Utumishi na Utawala aa Chama cha Mapinduzi, Veronica Ndavo akikabidhi Kompyuta kwa uongozi wa wanafunzi wa kitivo cha afya chuo kikuu cha Dodoma ambao ni wanachama wa CCM
 Mkuu wa Sehemu ya Utumishi, Utawala wa Chama cha Mapinduzi, Veronica Ndavo akizungumza na wanafunzi wa Kitivo cha Afya chuo Kikuu cha UDOM ambao ni wanachama wa CCM wakati wa hafla ya kuwaga wanafunzi wa Jumuiya hiyo wanaohitimu masomo yao
Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Dodoma, Diana Madukwa Akizungumza na wanafunzi wanachama wa CCM kutoka kitivo cha Afya chuo Kikuu cha UDOM wakati wa afya ya kuwaaga wanafunzi wanaohitimu masomo yao

MJALIWA AONGOZA KIKAO CHA UTEKELEZAJI WA HARAKA WA MRADI WA KUFUA UMEME MTO RUFIJI

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongoza kikao cha utekelezaji wa haraka wa maagizo ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu mradi wa kufua Umeme wa mto Rufiji, kilichofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar Es Salaam, Julai 31, 2019 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

WANANCHI WA KATA YA CHITA MELELA WAISHUKURU TARURA

$
0
0
Daraja la awali la wananchi wa Kata ya Chita Melela lililopo Mto Kihansi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro, ambalo limekuwa likitumiwa na wakazi maeneo hayo kabla ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kutengeneza Daraja jipya la Chuma (Mabey Bridge) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Uingereza (DFID).
Wahandisi kutoka Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) wakiwa katika ujenzi wa Daraja la Chuma (Mabey Bridge) lililopo Mto Kihansi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero, Mkoani Morogoro.
Msolovea Gasto Kikuji kutoka Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) akiweka usawa na kupima eneo kabla ya kuanza kwa ujenzi wa Daraja la Chuma (Mabey Bridge) lililopo Mto Kihansi katika Halmashauri ya Wilaya kilombero, Mkoani Morogoro.
Wahandisi kutoka Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) wakiwa katika ujenzi wa Daraja la Chuma (Mabey Bridge) lililopo Mto Kihansi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero, Mkoani Morogoro.
Wahandisi kutoka Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) wakiwa katika ujenzi wa Daraja la Chuma (Mabey Bridge) lililopo Mto Kihansi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero, Mkoani Morogoro.
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Chita Melela wakishuhudia ujenzi wa Daraja la Chuma (Mabey Bridge) lililopo Mto Kihansi (halipo pichani) katika Halmashauri ya Wilaya ya kilombero, Mkoani Morogoro.
Mtaalamu wa Ufundi John Hinderer kutoka Kampuni ya Mabey Bridge ya nchini Uingereza akiwapa maelekezo Wahandisi kutoka Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) jinsi ya kulifunga Daraja la Chuma (Mabey Bridge) lililopo Mto Kihansi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero, Mkoani Morogoro.
Muonekano wa Daraja la Chuma (Mabey Bridge) lililopo Mto Kihansi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero, Mkoani Morogoro baada ya kukamilika kwa ujenzi wa awali ambapo uzinduzi rasmi wa Daraja hilo utafanyika hivi karibuni.

**************

Na. Erick Mwanakulya

Wananchi wa Kata ya Chita Melela iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro, wameshukuru Serikali kupitia Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) baada ya kutatuliwa kwa kero yao ya muda mrefu kwa kujengewa Daraja la Chuma (Mabey Bridge) lililopo Mto Kihansi ambalo linajengwa na TARURA chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Uingereza (DFID).

Hayo yameelezwa na wananchi waliojitokeza kushuhudia ujenzi wa Daraja hilolinalojengwa na Wahandisi wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA),wakisaidiana na Mhandisi Mshauri Ebenezer Mollel pamoja na Mtaalamu wa UfundiJohn Hinderer kutoka Kampuni ya Mabey Bridge ya nchini Uingereza.

Wakielezea furaha yao juu ya ujenzi wa daraja hilo, wananchi hao wamesema kuwa wanaishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuwajengea daraja maana walikuwa wanapata shida kubwa hapo awali katika kusafirisha bidhaa zao na kupata huduma mbalimbali za kijamii kwani walikuwa wanatumia mtumbwi kuvuka Mto ambapo ni umbali takribani Km 1.5.

Kwaupande wake, Diwani wa Kata ya Chita Melela Mhe. Chelele John amesema, Serikali ya Awamu ya Tano inastahili kupongezwa kwa maana Daraja hilo ni kiungo muhimu katika uchumi wa Kata yake pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero kwa maana vyanzo vya mapato katika Kata za Mlimba, Chita, Mgeta, Mangula pamoja na Mchombe vitakusanywa kwa urahisi kutokana na uwepo wa daraja hilo.

“Tulikuwa tunatumia mtumbwi kuvuka Mto na wananchi walipata adha kubwa katika Kijiji chetu kwani kufikia huduma za kijamii ilikuwa changamoto kubwa, leo hii naona Wahandisi wa TARURA wapo hapa katika ujenzi wa Daraja hili, hii inadhihirisha kuwa Wakala upo katika kuhudumia wananchi ipasavyo nasi tunawaunga mkono”, alisema Diwani huyo.

Naye, Mratibu wa TARURA Mkoa wa Morogoro, Mhandisi Godwin Mpinzile amesema Daraja la Chuma (Mabey Bridge) la Mto Kihansi limewekwa baada ya kutengeneza barabara ya Chita Melela yenye urefu wa Km 11.5 na litakuwa mkombozi kwa wananchi wa Chita kutokana na shida wanayoipata wakati wa mvua na kwamba Wakala utaendelea kuikarabati Barabara hiyo hadi kuunganisha Kata ya Mlimba ili kuwarahisishia wananchi kufanya shughuli zao za kila siku.

Pia, amewasihi wakazi wa Chita kutunza miundombinu ya Barabara pamoja na Daraja kwani gharama kubwa zimetumika katika ujenzi wa Daraja hilo.

Daraja la kisasa la Chuma (Mabey Bridge) ambalo limegharimu zaidi ya shilingi milioni 700 ni moja kati ya kazi za Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) katika kuboresha Barabara na kufanya matengenezo pamoja na ujenzi wa Madaraja ili kuwawezesha wananchi kufanya shughuli zao za kiuchumi.

Daraja hilo linalenga kutatua kero ya kudumu kwa wananchi wa Chita Melela kutokana na Madaraja ya hapo awali kusombwa na maji pale mvua zinaponyesha na linatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni.

UHAMIAJI YATOA TAMKO SAKATA LA KUSHIKILIWA KWA MWANDISHI ERICK KABENDERA

$
0
0
*Yasema wanamshikilia ili kuhoji uhalali wa uraia wake
*Ni baada ya kumuita mara kadhaa lakini akakaidi, hivyo wakaamua..

Na Said Mwishehe,Michuzi TV

IDARA ya Uhamiaji imesema inamshikilia Mwandishi Erick Kabendera na kwa sasa wanaendelea kuchukua taarifa zake kuhusu uhalali wa uraia wake.

Kamishina wa Uraia na Pasipoti kutoka Idara ya Uhamiaji Gerald Kihinga amesema wanamshikilia Kabendera ili kujiridhisha na uraia wake na huo ni wajibu wao pale wanapokuwa na mashaka na uraia wa mtu.

"Idara ya Uhamiaji ilipata taarifa kutoka kwa wasamaria wema kuhusiana na utata wa uraia wa Erick Kabendera mwenyewe alikua hajawahi kuhojiwa kuhusiana na uraia wake, kwa kuwa hakufika ofisini pamoja na kumtumia wito mara kadhaa wa kumtaka afike ofisini kwa mahojiano.

"Na ndio maana sasa idara ya uhamiaji kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi imeweza kumtafuta na kumkamata mhusika ili aweze kuhojiwa kwa ajili ya kukamilisha uchunguzi kuhusiana na uraia wake.Uchunguzi utakapokamilika, matokeo ya uchunguzi huo yatatolewa,"amesema Kamishna Kihinga.

Amefafanua ieleweke kuwa uchunguzi wa utata wa uraia umekuwa ukifanyika kwa watu mbalimbali wakiwemo watu mashuhuri katika jamii.Hivyo suala hilo limeibua hisia huenda kwa kuwa mhusika ni mwanahabari.

Amesisitiza Idara ya uhamiaji imekuwa ikishirikiana na vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama katika utekelezaji wa majukumu yake mbalimbali , kwa hiyo hilo sio suala geni.

Hata hivyo idara hiyo imetoa mwito kwa jamii kuendelea kutoa ushirikiano na taarifa mbalimbali ya kiuhamiaji ili kuhakikisha nchi yetu inaendelea kuwa salama.Baada ya taarifa hiyo waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya ndani na nje ya Tanzania vilitaka kufahamu atashikiliwa kwa muda gani na kwa taarifa za awali Kabendera anahusishwa na uraia wa taifa gani.

Kamishina Kihinga amejibu wataendelea kumshikilia hadi pale watakapokamilisha taarifa wanayoihitaji na kuhusu taifa gani anahusishwa nalo hilo kwa sasa bado kwani ndio wanaendelea kukusanya taarifa.

Alipoulizwa Kabendera amekamatwa na nani? Amejibu amekamatwa na Idara ya Uhamiaji kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.Alipoulizwa kwanini waliokwenda kumkamata hawakutaka kutoa vitambulisho na walikuwa wamevaa kiraia, amejibu wana mbinu nyingi za kumkamata mtu ambaye ameitwa na kisha akakaidi.Hivyo waliamua kutumia mbinu ya kutovaa sare za uhamiaji.
Kamishina wa Uraia na Pasipoti kutoka Idara ya Uhamiaji Gerald Kihinga

Mkurugenzi Kunambi awafuta machozi wananchi wake, agawa viwanja 144

$
0
0
Na Charles James, MICHUZI TV

Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi amekabidhi hati ya viwanja kwa wananchi 144 wa Kata ya Tambukareli ambao maeneo yao yalitwaliwa na Serikali.

Kunambi amekabidhi hati hizo kwa wananchi hao ambao wamekuwa wakiangaika kwa miaka minne na kuueleza kuwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma itahakikisha kila Mwananchi anapata haki yake kama ambavyo Rais Dk John Magufuli amekua akisisitiza kuwatumikia wanyonge.

" Leo hii hapa kuna zoezi la kutoa viwanja kwa wananchi ambao ni wahanga wa maeneo yao ambao awali inadaiwa yalitwaliwa na iliyokua mamlaka ya ustawishaji Makao makuu na kuwaacha ndugu zetu hawa wakiwa hawana maeneo.

" Kwa muda mrefu kumekua na malalamiko ya muda mrefu ya wananchi na sisi kama Jiji tulifanya tathimini ya jumla na kuona ndugu zetu hawa wana haki ya kulipwa fidia maeneo yao na hivyo leo tumemaliza kero yao ya muda mrefu kwa kuwagaia viwanja bure na watakacholipia wao ni zile tozo za kawaida za kikatiba," amesema Kunambi.

Kunambi amesema kwa mwaka mmoja wa 2018 wa Fedha tayari wameshatoa hati miliki 5000 na kuwa Jiji la kwanza Nchi nzima.

" Ili tuweze kumaliza matatizo yote Dodoma basi Jiji linapaswa kutoa viwanja kwa mtindo huu wa leo kwa viwanja 5000 ambavyo vitatugharimu Shilingi Bilioni nne. 

" Leo hii hawa wananchi ambao wako 144 tumewapa viwanja bure kwa maana watalipa tu zile gharama za kisheria takribani laki saba kwa kiwanja ambacho angeweza kulipa Shilingi Milioni saba. Hii ni kuonesha jinsi gani Serikali ya Dk Magufuli inatetea haswa wanyonge," amesema Kunambi.

Kwa upande wake Diwani wa Kata hiyo, Juma Mazengo amemshukuru Mkurugenzi wa Jiji kwa namna alivyolivalia njuga suala lao na kuweza kumaliza kero ya wananchi wake ambao wameteseka kwa miaka minne.

" Nimshukuru Mhe Rais kweli tumeona jinsi gani anatetea wanyonge. Hii inaonesha jinsi gani anaziishi ahadi zake alizowaahidi wananchi wakati wa kampeni, tunayo furaha sana na hakika tumeona heshima tuliyopewa na Serikali yetu,"amesema Mh Mazengo.
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi (kushoto) akimkabidhi hati ya kiwanja mmoja wa wananchi wa kata ya Tambukareli ambao walitwaliwa maeneo yao.


 Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Mhe Godwin Kunambi akizungumza na Wananchi 144 wa Kata ya Tambukareli wakati wa kuwakabidhi hati za viwanja vyao ikiwa ni fidia baada ya Serikali kutwaa maeneo yao

MWENGE WA UHURU WAGOMEA KUZINDUA MRADI WA MAJI BOKOMNEMELA HUKO KIBAHA VIJIJINI

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA VIJIJINI

MWENGE wa uhuru ,umekataa kuzindua mradi wa maji Bokomnemela,Kibaha Vijijini,mkoani Pwani baada ya kubaini taratibu za ujenzi kukiukwa katika zege la juu lililotengewa kiasi cha sh.milioni 1.5.#

Aidha kamanda wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU), wilayani Kibaha Vijijini amepewa wiki mbili kuufuatilia na kuchunguza kwa kina juu ya mapungufu yaliyoyabainika kisha baada ya uchunguzi taarifa zipelekwe Makao Makuu ya TAKUKURU na afikishiwe taarifa.

Akizungumza baada ya kufanya ukaguzi wa mradi huo,kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa 2019 ,Mzee Mkongea Ali alisema ,pia mfuniko upo taabani,hali mbaya kiusalama na ngazi za ndani ndani nazo ni tatizo .

"Tumefanya ukaguzi, tumebaini mfuniko haupo kiusalama,akitokea mtu asiyependa maendeleo anaweza kuweka vitu vibaya,tunaomba jitihada za makusudi zichukuliwe ili kurekebisha mapungufu hayo"

"Fedha ya zege la juu imetengwa milioni 1.5 na katika taarifa inaonyesha imelipwa yote,vipimo vipo vitatu kwanini hiki kimoja kisifanyike ,kipimo cha zege la juu hakuna ,kutokana na hili mwenge wa uhuru hauwezi kuzindua mradi huu'"alisisitiza Mkongea.

Mkongea alieleza kuwa, huwa wakipitia miradi ,wanaomba taarifa na kujiridhisha kwakuwa fedha zinazotumika kwenye miradi ni za serikali na kodi za wananchi hivyo inapaswa zisimamiwe vizuri.

"Tunamshukuru Rais dkt .John Magufuli kwa kazi anayoifanya ,":Kwenye miradi ya maji sisi sote mashahidi tunajionea miradi ya milioni 400,kuna mradi wa jiji la Arusha,mradi wa miji ,Chalinze,Same,Mwanga na Korogwe"alisema Mkongea.Aliwataka wananchi waendelee kutumia maji kupitia mradi huo kwakuwa vipimo vinaonyesha ni safi na salama.

Kwa upande wake, mhandisi wa maji Kibaha injinia Rebman Ganshonga alifafanua mradi huo unagharama ya sh.milioni 459.458.0 ambao uliibuliwa ili kuhudumia vijiji vitatu ikiwemo Mkarambati,Mnemela Kibaoni na Bokomnemela na watu 6,000.

Ganshonga alibainisha,DAWASA imefanya maboresho makubwa kwenye chanzo cha maji cha Ruvu ambayo yamewezesha kuongezeka kwa msukumo wa maji kutoka 1.5 bar hadi kufikia 3.5 bar hivyo kufanya maji kuwa na uwezo wa kufikia maeneo yote yenye vituo vya kuchotea maji bila kupitia tanki la kuhifadhia maji.

Awali akipokea mwenge wa uhuru ukitokea Bagamoyo,mkuu wa wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama alisema, miradi iliyotembelewa ni Tisa yenye thamani ya sh.bilioni 4.121.

Naibu Waziri wa kilimo Hussein Bashe awahakikishia Masoko Wakulima wa Pamba Tabora

$
0
0
Na, Editha Edward-Tabora 

Naibu waziri wa kilimo Hussein Bashe amekagua soko la pamba katika wilaya za Nzega na Igunga Mkoani Tabora soko ambalo limekuwa likisua sua kutoka na wanunuzi kukosa fedha za kununua zao hilo huku akiwahakikishia Wakulima wa zao hilo kupata fedha zao 

Ineelezwa kuwa hadi sasa wilaya za Nzega na Igunga kuwa zina zaidi ya kilo milioni 30 za pamba huku Ikiwa Bado kilo milioni 27 haijanunuliwa ambapo naibu waziri Bashe amelazimika kutoa msimamo wa Serikali kwa Wakulima wote wa zao hilo hapa nchini ambao  pamba yao Bado haijanunuliwa 

Akiwa Katika ukaguzi huo wa soko la pamba ambao umekwenda sambamba na kukuta na Wakulima wa zao hilo kama alivyoagizwa na Rais Dkt. John Magufuli wakati akiapishwa ikulu jijini Dar- es - Salaam, Naibu  waziri huyo amekutana na Wakulima wa zao hilo ili kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano

Hata hivyo katika Ziara hiyo Naibu waziri Bashe amebaini Mapungufu kadhaa ikiwemo mchezo mchafu kwenye Mikopo ya pembejeo inayotolewa na vyama vya Ushirika kwa Wakulima wa zao la pamba wamekuwa wakiibiwa.
 Pichani ni Naibu waziri wa kilimo Hussein Bashe akiongea na Wakulima wa pamba wilaya za Nzega na Igunga.
 Pichani ni Naibu Waziri wa kilimo Hussein Bashe akikagua soko la pamba wilayani Igunga.
Pichani ni zao la pamba ambalo tayari limeshavunwa.

Article 5

MBUNGE VITI MAALUM AKABIDHI KOMPYUTA NNE KWA UWT

$
0
0
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.

MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Magharibi kupitia Baraza la Wawakilishi Mhe.Amina Idd Mabrouk,amewasihi Viongozi na Wanachama wa CCM kufanya Kazi za Chama Cha Mapinduzi kwa bidii ili kuandaa Mazingira rafiki ya Ushindi wa Mwaka 2020. 

Rai hiyo aliitoa wakati akikabidhi Komputa Nne zenye Thamani ya Shilingi Milioni Nane kwa Ofisi za UWT Zanzibar ambazo ni Afisi Kuu ya UWT Zanzibar, UWT Mkoa wa Magharib,UWT Wilaya ya Dimani na UWT Wilaya ya Mfenesini ambapo kila Ofisi imekabidhiwa komputa Moja,Hafla hiyo imefanyika katika Ofisi za CCM huko Kiembembe Samaki Unguja.

Mhe.Amina alisema ili Chama kishinde katika Uchaguzi Mkuu ujao kila mwanachama anatakiwa kuweka mbele maslahi ya CCM badala ya maslahi binafsi.

Katika maelezo yake Mhe.Amina, alisema Vifaa hivyo ni mwendelezo wa Utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020,ikiwa ni sehemu ya kutekeleza kwa vitendo ahadi alizozitoa kwa Wananchi.

Pamoja na hayo aliwaahidi Akina Mama wa Mkoa wa Magharibi kuwa ataanzisha Vikundi vya Ujasiriamali ili kuwakwamua kiuchumi Wanawake hao.

Aidha alisema kwa kushirikiana na Viongozi mbali mbali wa Mkoa huo hasa Wabunge na Wawakilishi watakuwa mstari wa mbele kutatua changamoto za Wananchi bila ubaguzi wa kisiasa,kidini na kikabila.

Aliwasihi Viongozi na Wanachama wa UWT kuthamini juhudi za kimaendeleo zinazofanywa na Viongozi hao ili wazidi kupata nguvu na Uthubutu wa kutatua changamoto zinazowakabili Wananchi.

"Tukiwa Viongozi wa Mkoa huu kwa pamoja tutaendelea kushirikiana kwa kuhakikisha tunatekeleza Ilani ya CCM kwa kasi kubwa na kutatua changamoto mbali mbali za Wananchi" ,alisisitiza Mhe.

Akizungumza katika Hafla hiyo Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Ndugu Tunu Juma Kondo,alimpongeza Mbunge huyo na Viongozi mbali mbali wa Mkoa huo, ambao wamekuwa karibu na Wananchi kwa kutekeleza kwa Vitendo Ilani ya CCM.

Ndugu Tunu,aliwataka Viongozi na Watendaji waliokabidhiwa Komputa hizo kuzitunza vizuri ili zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa katika kuhakikisha shughuli za kiutendaji za UWT zinatekelezwa kwa ufanisi zaidi.

Alisema Viongozi wa Chama na Serikali wanatakiwa kufuata nyayo za Viongozi Wakuu ambao ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kwa katika kuwatumikia Wananchi kwa uadilifu.

Awali Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Magharibi Ndugu Zainab Ali Maulid,alisema Umoja na Mshikamano ndio siri ya mafanikio ya kuimarika kwa Umoja huo.
NAIBU Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Ndugu Tunu Juma Kondo(kulia),akimkabidhi Komputa Moja Katibu wa UWT Wilaya ya Dimani Ndugu Sunna Said Mzee(wa kwanza kushoto),Komputa hiyo imetolewa na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Magharib kupitia Baraza la Wawakilishi Mhe.Amina Idd Mabrouk(wa pili kushoto).
VIONGOZI na Wanachama wa UWT wa Mkoa wa Magharibi wakiwa katika hafla ya kukabidhi komputa nne ya Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Magharib kupitia Baraza la Wawakilishi Mhe.Amina Idd Mabrouk, iliyofanyika katika Ofisi za CCM Kiembe Samaki Unguja.

WAKAZI WA BAGAMOYO KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI

$
0
0
MWENGE wa Uhuru,umezindua mradi wa tanki kubwa la maji linalojengwa Bagamoyo ,mkoani Pwani ambalo litakuwa na uwezo wa kuhifadhi lita milioni sita linatarajiwa kuondoa tatizo la ukosefu wa maji kwa wakazi wa wilaya hiyo na maeneo jirani.

Baadhi ya wakazi wilayani hapo ,akiwemo Asia Rajabu na Ashura Selemani ,walielezea kero ya maji imepungua kama sio kubakia historia.

"Mradi huu ni mkombozi kwa sisi wananchi kipindi cha nyuma tulikuwa hatupati huduma ya maji safi na salama kwa uhakika,maana tulikuwa tunatumia visima vya kupampu na wakati mwingine vilikuwa vibovu,"

"Ilikuwa ni shida na kero maana tulikuwa tukikosa maji siku 5-7 ,lakini sasa tunashukuru mamlaka ya maji safi na maji taka (DAWASA )na serikali kututua ndoo kichwani hasa sisi wanawake"walieleza.

Awali akimuelezea kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa, juu ya mradi huo, meneja wa DAWASA Bagamoyo Alex Ngw'andu alisema katika hatua ya kwanza DAWASA wanatarajia kupata wateja 3,000 katika kata ya Ukuni,Sanzale,Nianjema na Kisutu ambapo hadi sasa wameshawaunganishia watu 250.

Alielezea kuwa, kata hizo zina watu 26,000 ambapo kila kaya itafikiwa hivyo waombe huduma waweze kusogezewa."Nia na madhumuni kupata mtandao wa kusambaza maji maeneo yote ya Bagamoyo na maeneo jirani"alisema Ngw'andu.

Akitoa maelekezo kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa ,Mzee Mkongea Ali aliwataka wamalizie maeneo ambayo hayajakamilika ili kufikia kila eneo asilimia 100 walizoziweka kwenye taarifa.

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo,Zainab Kawawa alisema mwenge wilayani hapo umepitia miradi 15 yenye thamani ya bilioni 4.370.

MWENGE WA UHURU WAGOMEA KUZINDUA MRADI WA MAJI BOKOMNEMELA HUKO KIBAHA VIJIJINI

$
0
0
NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA VIJIJINI

MWENGE wa uhuru ,umekataa kuzindua mradi wa maji Bokomnemela,Kibaha Vijijini,mkoani Pwani baada ya kubaini taratibu za ujenzi kukiukwa katika zege la juu lililotengewa kiasi cha sh.milioni 1.5.#

Aidha kamanda wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU), wilayani Kibaha Vijijini amepewa wiki mbili kuufuatilia na kuchunguza kwa kina juu ya mapungufu yaliyoyabainika kisha baada ya uchunguzi taarifa zipelekwe Makao Makuu ya TAKUKURU na afikishiwe taarifa.

Akizungumza baada ya kufanya ukaguzi wa mradi huo,kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa 2019 ,Mzee Mkongea Ali  alisema ,pia mfuniko upo taabani,hali mbaya kiusalama na ngazi za ndani ndani nazo ni tatizo .

"Tumefanya ukaguzi, tumebaini mfuniko haupo kiusalama,akitokea mtu asiyependa maendeleo anaweza kuweka vitu vibaya,tunaomba jitihada za makusudi zichukuliwe ili kurekebisha mapungufu hayo"

"Fedha ya zege la juu imetengwa milioni 1.5 na katika taarifa inaonyesha imelipwa yote,vipimo vipo vitatu kwanini hiki kimoja kisifanyike ,kipimo cha zege la juu hakuna ,kutokana na hili mwenge wa uhuru hauwezi kuzindua mradi huu'"alisisitiza Mkongea.

Mkongea alieleza kuwa, huwa wakipitia miradi ,wanaomba taarifa na kujiridhisha kwakuwa fedha zinazotumika kwenye miradi ni za serikali na kodi za wananchi hivyo inapaswa zisimamiwe vizuri.

"Tunamshukuru Rais dkt .John Magufuli kwa kazi anayoifanya  ,":Kwenye miradi ya maji sisi sote mashahidi tunajionea miradi ya milioni 400,kuna mradi wa jiji la Arusha,mradi wa miji ,Chalinze,Same,Mwanga na Korogwe"alisema Mkongea.

Aliwataka wananchi waendelee kutumia maji kupitia mradi huo kwakuwa vipimo vinaonyesha ni safi na salama.

Kwa upande wake, mhandisi wa maji Kibaha injinia Rebman Ganshonga alifafanua mradi huo unagharama ya sh.milioni 459.458.0 ambao uliibuliwa ili kuhudumia vijiji vitatu ikiwemo Mkarambati,Mnemela Kibaoni na Bokomnemela na watu 6,000.

Ganshonga alibainisha,DAWASA imefanya maboresho makubwa kwenye chanzo cha maji cha Ruvu ambayo yamewezesha kuongezeka kwa msukumo wa maji kutoka 1.5 bar  hadi kufikia 3.5 bar hivyo kufanya maji kuwa na uwezo wa kufikia maeneo yote yenye vituo vya kuchotea maji bila kupitia tanki la kuhifadhia maji.

Awali akipokea mwenge wa uhuru ukitokea Bagamoyo,mkuu wa wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama alisema, miradi iliyotembelewa ni Tisa yenye thamani ya sh.bilioni 4.121.

Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images