Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109592 articles
Browse latest View live

SHUHUDIA UZINDUZI WA PROGRAMU YA KUPINGA VITENDO VYA UKATILI NA UDHALILISHAJI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO


MKUU WA MKOA AWASHANGAA MADIWANI MANISPAA YA SHINYANGA KUVUNJA KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI

0
0
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani wa Manispaa ya Shinyanga leo Na Marco Maduhu - Malunde1 blog Shinyanga. Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack, ameagiza madiwani wa manispaa ya Shinyanga kutengua maamuzi yao ya kumkataa mkurugenzi wa halmashauri hiyo Geofrey Mwangulumbi, kwamba hawakufuata kanuni na taratibu.

Amesema jambo walilolifanya madiwani hao ni ukiukaji wa kanuni na taratibu, ambapo walipaswa kuitisha kikao maalumu pamoja na kumpeleka malalamiko hayo kwake ili ayafanyie kazi, lakini alishaghaa kusikia tu kikao cha baraza la madiwani kimevunjika madiwani wakimkataa mkurugenzi kutokuwa na imani naye. 

Telack amebainisha hayo leo Julai 30, 2019 kwenye kikao cha kawaida cha baraza la madiwani la manispaa ya Shinyanga, ambapo madiwani hao waliamua kuendelea na baraza hilo mara baada ya kutengua maamuzi yao ya jana ya kuvunja kikao cha baraza kwa madai ya kumkataa mkurungezi kutokuwa na imani naye. Mkuu huyo wa mkoa amesema baraza hilo haliwezi kuendelea kuwepo, endapo kama madiwani hawatatengua maamuzi yao ya kumkataa mkurugenzi, ikiwa kanuni na taratibu zilikosewa kufuatwa. Kutokana na hali hiyo, madiwani hao walitengua maamuzi yao na kisha kikao cha baraza kuendelea na kujadili ajenda mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya manispaa hiyo. 

“Taarifa hizi za kumkataa mkurungenzi nilizipata toka juzi nikaona ngoja niwapime upeo wenu madiwani kama mtafuata kanuni na taratibu... lakini nikashangaa tu mmechukua maamuzi, mkavunja kikao cha baraza bila ya kufuata taratibu, hivyo naagiza maamuzi yenu myatengue kwanza ndipo muendelee na kikao, tofauti na hapo baraza lenu ni batiri,”amesema Telack. “Ninachotaka kusema madiwani achaneni na malumbano yasiyo na maana kwa kuvunja tu vikao bila ya kufuata taratibu, pale penye mapungufu tuwasiliane ili tuweze kwenda pamoja, nafahamu mapungufu ya manispaa hii, ni kweli yale ambayo mnalalamikia juu ya maazimio yenu kutotekelezwa mko sahihi kabisa,”ameongeza Mkuu wa mkoa. 

Aidha amesema tatizo ambalo linasababisha migogoro hiyo kuwepo ni kutoelewana kati ya watumishi wa halmashauri na mkurugenzi wao, sababu kila mtu ni mbabe, na hivyo kusababisha miradi mingi kuwa na usimamizi mbovu na kutotekelezeka, na ndio maana maazimio yenu hayafanyiwi kazi. Naye Katibu Tawala la mkoa wa Shinyanga Albert Msovela, amewataka watumishi wa manispaa hiyo, madiwani, pamoja na mkurugenzi, kuzungumza lugha moja ili kuondoa makandokando yaliyopo na kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi. 

Kwa upande wake Naibu Meya wa manispaa hiyo ya Shinyanga John Kisandu, alisema wametengua maamuzi yao ya kumkataa mkurugenzi huyo, na kukiri kwamba hawakufuata kanuni na taratibu, hivyo wataendelea kufanya naye kazi, na kumtaka maazimio yao awe ana yafanyia kazi. Aidha jana kikao cha baraza hilo la madiwani la halmashauri ya manispaa ya Shinyanga kilivunjika baada ya madiwani wa halmashauri hiyo kudai kutokuwa na imani na mkurugenzi wa halmashauri Geofley Mwangulumbi, kwamba amekuwa hatekelezi maazimio ambayo huazimia yakiwamo ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo. 

Baraza hilo limevunjika kwenye kikao cha kawaida cha robo ya nne, ambapo wakati wakusoma na kudhitisha muhtasari, mmoja wa madiwani hao David Nkulila (CCM )kutoka Kata ya Ndembezi, aliibua hoja kuwa kwanini maadhimio yao yamekuwa hayatekelezwi, na kudai kutokuwa na imani na mkurugenzi hoja ambayo iliungwa mkono na madiwani na hatimaye kikao cha baraza kuvunjika. TAZAMA PICHA HAPA CHINI Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack, akizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani la manispaa ya Shinyanga leo Julai 30,2019 na kuwataka watengue maamuzi yao ya kumkataa mkurugenzi wa halmshauri hiyo Geofrey Mwangulumbi, ndipo waendelee na kikao chao tofauti na hapo baraza lao ni batiri, ambapo madiwani hao walitengua maamuzi yao na kukiri hawakufuata taratibu za kumkataa mkurugenzi.Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog. Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Zainab Telack, akikiri pia madai ambayo wanalalamikia madiwani hao ya kutekelezewa mazimio yao ni ya kweli, na kutoa maagizo kwa mkurugenzi akae na watendaji wake na kutekeleza maazimio hayo kwa ajili ya maendeleo ya wananchi. Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye kikao cha baraza hilo la madiwani la manispaa ya Shinyanga, na kuonyesha naye kusikitishwa na tukio lililotokea la kuvunjika kwa kikoa cha baraza hilo la madiwani bila ya kufuata utaratibu. Katibu Tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela, akiwataka Madiwani, watumishi wa manispaa ya Shinyanga pamoja na mkurugenzi kuzungumza lugha moja ili kuondoa makandokando yaliyopo na kuwa kitu kimoja na kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi Naibu Meya wa manispaa ya Shinyanga John Kisandu, akizungumza kwenye baraza hilo na kutengua maamuzi ya baraza ya kumkataa mkurugenzi wa mansipaa hiyo Geofrey Mwangulumbi kuwa hawana imani naye kutokana na kushindwa kutekeleza mazimio yao. Madiwani wa manispaa ya Shinyanga wakiendelea na kikao cha baraza, mara baada ya kutengua maamuzi hayo ya kumkataa mkurugenzi wa manispaa hiyo Geofrey Mwangulumbi, kuwa walikosea sababu hawakufuata utaratibu. Madiwani wakiendelea na kikao cha baraza wakijadili ajenda mbalimbali kwa ajili ya mustakabali wa maendeleo ya manispaa ya Shinyanga. Diwani wa Kata ya Kolandoto Agnes Machiya akichangia ajenda kwenye kikao cha baraza hilo la madiwani la manispaa ya Shinyanga. Diwani wa Kata ya Kitangili Khamis Ngunila akichangia ajenda kwenye kikao cha baraza la madiwani la manispaa ya Shinyanga. Diwani wa viti maalumu manispaa ya Shinyanga Shela Mashandete akichangia ajenda kwenye kikao cha baraza la madiwani la mansipaa ya Shinyanga. Madiwani wakiendelea na kikao cha baraza. Watendaji wa manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha baraza la madiwani. Watendaji wa manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao cha baraza la madiwani. Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog.

KAMPENI YA NSSF NA MARAFIKI YAVUNA WANACHAMA WAPYA

0
0
SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeendelea kuandikisha wanachama wapya kutoka kwenye sekta binafsi na sekta isiyokuwa rasmi kupitia kampeni ya NSSF na Marafiki iliyoanzishwa mwishoni mwa wiki iliyopita.

Kupitia kampeni hiyo NSSF imeweza kuandikisha wanachama wapya 472 kutoka katika kampuni ya KK Security. Kampuni ya ulinzi ya KK security ilishukuru NSSF kwa kuwapatia elimu ya hifadhi ya jamii kupitia kampeni ya NSSF na Marafiki iliyofanikisha kusajili wafanyakazi 472 na NSSF.

Kampeni ya NSSF na Marafiki itazunguka Tanzania nzima kwa lengo la kuandikisha wanachama wapya kutoka katika sekta binafsi na sekta isiyokuwa rasmi na kuhakikisha waajiri wanawasilisha michango ya wafanyakazi wao kwa wakati.

Kufuatia mabadiliko ya sheria ya hifadhi ya Jamii ya mwaka 2018 NSSF inatoa huduma ya Hifadhi ya Jamii kwa Sekta binafsi na Sekta Isiyokuwa Rasmi. Hivyo, Kampeni hii itasaidia kuongeza wanachama kutoka katika sekta hizo.
Meneja Kiongozi wa Uendeshaji wa NSSF, Cosmas Sasi (kulia) akimuelekeza jinsi ya kujaza fomu mfanyakazi wa Kampuni ya ulinzi ya KK Security wakati wa zoezi la kuandikisha wanachama wapya 472 wa kampuni ya KK Security jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa NSSF mkoa wa Kinondoni Hiza Kiluwasha wakati akijaza taarifa za mwanachama mpya wa NSSF katika mifumo ya kielektroniki ya Shirika.
Meneja Kiongozi Mahusiano na Elimu kwa Umma wa NSSF, Lulu Mengele akisisitiza jambo kwa wafanyakazi wa kampuni ya KK Security wakati wa zoezi la kuwasajili.
Meneja Kiongozi wa Uendeshaji wa NSSF, Cosmas Sasi (kulia) akifuatilia maelekezo anayopewa mwanachama mpya wa NSSF ambaye ni mfanyakazi wa Kampuni ya ulinzi ya KK Security wakati wa zoezi la kuandikisha wanachama wapya kampuni ya KK Security jijini Dar es Salaam.

Mfanyabiashara Arusha mbaroni kwa utoroshaji wa Madini

0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Tv, Manyara .

Mfanyabiashara maarufu wa madini,Mwenye asili ya kiasia ,Samiri Patel anayemiliki kampuni ya Madini ya Gyan gems jewellers ltd jijini Arusha, amekamatwa na Polisi mkoani Manyara kwa tuhuma za kutorosha madini kinyume utaratibu.

Patel ambaye ni mtunza hazina wa chama cha wafanyabiashara wa Madini TAMIDA ,anadaiwa kukamatwa na polisi katika bar ya Songambele ,Mererani wilayani Simanjiro wiki iliyopita akiwa na shehena hiyo ya Madini aina ya Tanzanite akidai kupatiwa na mfanyabiashara mwenzake wakati akijua hana leseni ya biashara hiyo.

Baadhi ya wafanyabiashara wa Madini mkoani humon(Majina yamehifadhiwa)wamedai kuwa Mfanyabiashara huyo amekuwa akitumiwa na wafanyabiashara wenye asili hiyo kutorosha Madini kinyume cha sheria huku akitumia kivuli cha kufahamiana na baadhi ya viongozi wa serikali.

Hata hivyo Polisi Mkoani humo imemwachia kwa dhamana mtuhumiwa huyo kwa Madai kwamba shtaka linalomkabili lina dhamana na wakati huo jalada la shtaka lipo kwa mwanasheria wa serikali likisubiri kurejea ili kuweza kufikishwa mahakamani .

Akiongelea tukio hilo kamanda wa Polisi Mkoani humo,Agustino Senga amethibitisha kushikiliwa kwa mfanyabiashara huyo na kwamba yupo nje kwa dhamana hadi upelelezi utakapokamilika kuweza kumfikisha mahakamani.

" Ni kweli amekamatwa ila tunasubili taarifa ya mwanasheria wa serikali tuweze kumfikisha mahakamani mtuhumiwa "Amesema kamanda Senga.

Hata hivyo taarifa zinadai kwamba mfanyabiashara huyo ni moja ya wanamtandao wa utoroshwaji wa madini ambao kwa sasa mianya yao imedhibitiwa kwa kiwango kikubwa ikiwemo ujenzi wa ukuta wa Mererani.

Katika hatua nyingine Afisa Madini Mkazi Mkoani Manyara ,RMO Daud Ngalula alipotakiwa kuzungumzia madai hayo alishindwa kutoa ufafanuzi badala yake alikata simu ,baada ya kuwepo madai ya kuwabeba baadhi ya wafanyabiashara wa madini wanaoenda kinyume na utaratibu

UTIAJI SAINI MKATABA WA UJENZI WA DARAJA LA KIGONGO-BUSISI LA MWANZA LENYE UREFU WA KM 3.2

ANAYEIDAIWA KUMUUA MKEWE NA KUMCHOMA MOTO APANDISHWA KIZIMBANI

INTRODUCING "MREMBO" BY KENNEDY MY

RAIS DKT. MAGUFULI ATOA POLE KWA FAMILIA YA MAREHEMU MEJA JENERALI MSTAAFU ALBERT MBOWE , SALASALA, JIJINI DAR ES SALAAM.

0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mhe. Freeman Mbowe Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye pia ni kaka wa marehemu Meja Jenerali Mstaafu Albert Lameck Mbowe aliyefariki dunia julai 28,2019 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam, mara baada ya kuwasili nyumbani kwa Marehemu Salasala  kwa ajili ya kutoa pole kwa Familia Julai 30,2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mhe. Freeman Mbowe Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye pia ni kaka wa marehemu Meja Jenerali Mstaafu Albert Lameck Mbowe aliyefariki dunia julai 28,2019 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam, mara baada ya kuwasili nyumbani kwa Marehemu Salasala  kwa ajili ya kutoa pole kwa Familia Julai 30,2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Marehemu Meja Jenerali Mstaafu Albert Lameck Mbowe aliyefariki dunia julai 28,2019 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam, kabla ya kutoa pole kwa Familia na Mhe. Freeman Mbowe Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye pia ni kaka wa Marehemu. Julai 30,2019.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akitoa pole kwa Familia ya Marehemu Meja Jenerali Mstaafu Albert Lameck Mbowe aliyefariki dunia julai 28,2019 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam ikiongozwa na Mhe. Freeman Mbowe Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye pia ni kaka wa Marehemu nyumbani kwao Salasala Dsm. Julai 30,2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akizungumza na Mhe. Freeman Mbowe Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye pia ni kaka wa Marehemumara baada ya kutoa polekwa Familia ya Marehemu Meja Jenerali Mstaafu Albert Lameck Mbowe aliyefariki dunia julai 28,2019 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.

 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akizungumza na Familia ya Marehemu Meja Jenerali Mstaafu Albert Lameck Mbowe aliyefariki dunia julai 28,2019 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam ikiongozwa na Mhe. Freeman Mbowe Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye pia ni kaka wa Marehemu nyumbani kwao Salasala Dsm. Julai 30,2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akiomba dua maalumu na Familia ya Marehemu Meja Jenerali Mstaafu Albert Lameck Mbowe aliyefariki dunia julai 28,2019 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam iliyoongozwa na Mhe. Freeman Mbowe Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye pia ni kaka wa Marehemu nyumbani kwao Salasala jijini Dar es salaam Julai 30,2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akizungumza baada ya kuomba dua maalumu na Familia ya Marehemu Meja Jenerali Mstaafu Albert Lameck Mbowe aliyefariki dunia julai 28,2019 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam iliyoongozwa na Mhe. Freeman Mbowe Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye pia ni kaka wa Marehemu nyumbani kwao Salasala Dsm. Julai 30,2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akizungumza na Mhe. Freeman Mbowe Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye pia ni kaka wa Marehemu mara baada ya kutoa polekwa Familia ya Marehemu Meja Jenerali Mstaafu Albert Lameck Mbowe aliyefariki dunia julai 28,2019 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akiagana na waombolezaji baada ya kutoa pole kwa Familia ya Marehemu Meja Jenerali Mstaafu Albert Lameck Mbowe aliyefariki dunia julai 28,2019 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akisindikizwa na Mhe. Freeman Mbowe Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye pia ni kaka wa Marehemumara baada ya kutoa polekwa Familia ya Marehemu Meja Jenerali Mstaafu Albert Lameck Mbowe aliyefariki dunia julai 28,2019 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli akiagana na Mhe. Freeman Mbowe Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye pia ni kaka wa Marehemumara baada ya kutoa polekwa Familia ya Marehemu Meja Jenerali Mstaafu Albert Lameck Mbowe aliyefariki dunia julai 28,2019 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.
Picha na IKULU

KIKAO CHA MAKATIBU WAKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI NA WIZARA YA HABARI,UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO KUELEKEA MKUTANO WA SADC

0
0
Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt.Faraji Mnyepe akifafanua jambo kwa wasanii wa sanaa mbalimbali nchini kuhusu fursa za mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wanachama wa SADC, katika kikao kilichofanyika Jijini Dar es Salaam Julai 30, 2019.
Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Susan
Mlawi akifafanua jambo kwa wasanii wa sanaa mbalimbali nchini kuhusu fursa zamkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wanachama wa SADC, katika kikaokilichofanyika Jijini Dar es Salaam Julai 30, 2019.
Baadhi ya Wasanii wakifuatilia kikao cha Makatibu Wakuu kutoka Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuhusu Mkutano wa SADC, kilichofanyika Jijini Dar es Salaam Julai 30, 2019.
Rais wa Shirikisho la sanaa za maonesho Tanzania, William Frank Chitanda
akifuatilia kikao cha Makatibu Wakuu kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Wasanii kuhusu mkutano wa SADC, kilichofanyika Jijini Dar es Salaam Julai 30, 2019.
Msanii wa mziki wa kizazi kipya, Peter Msechu, akizungumza katika kikao chaMakatibu Wakuu kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Wasanii kuhusu Mkutano Mkuu wa SADC, kilichofanyika Jijini Dar es Salaam Julai 30, 2019.
Msanii wa Sanaa ya uchoraji, Mosses Luhanga, akizungumza katika kikao chaMakatibu Wakuu kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Wasanii kuhusu Mkutano wa SADC, kilichofanyika Jijini Dar es Salaam.

(Picha na Idara ya Habari-MAELEZO)

MAADHIMISHO NA MAONESHO YA NNE YA WIKI YA VIWANDA YA JUMUIYA YA MAENDELEO YA KUSINI MWA AFRIKA (SADC)

TTCL na TOSCI washirikiana kusaidia wakulima kubaini mbegu 'feki'

0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Waziri Kindamba (wa pili kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya uthibiti ubora wa mbegu Tanzania (TOSCI), Patrick Ngwediagi (wa pili kulia) wakionesha nyaraka za mikataba ya ushirikiano mara baada ya kuingia makubaliano hayo, ambapo TTCL imetengeneza mfumo ujulikanao kama TTCL HAKIKI utakaofanya kazi ya kuhakiki mbegu kwa kutumia simu ya mkulima. Pembeni yao ni wanasheria wa taasisi zote mbili wakishuhudia.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Waziri Kindamba (kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya uthibiti ubora wa mbegu Tanzania (TOSCI), Patrick Ngwediagi (kulia) wakibadilishana nyaraka za makubaliano mara baada ya kusaini makubaliano hayo. 

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Waziri Kindamba (kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya uthibiti ubora wa mbegu Tanzania (TOSCI), Patrick Ngwediagi (kulia) wakisaini makubaliano ambapo TTCL imetengeneza mfumo ujulikanao kama TTCL HAKIKI utakaofanya kazi ya kuhakiki mbegu kwa kutumia simu ya mkulima.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Waziri Kindamba (kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya uthibiti ubora wa mbegu Tanzania (TOSCI), Patrick Ngwediagi (kulia) wakisaini makubaliano ambapo TTCL imetengeneza mfumo ujulikanao kama TTCL HAKIKI utakaofanya kazi ya kuhakiki mbegu kwa kutumia simu ya mkulima. Nyuma yao ni wanasheria wa taasisi hizo wakishuhudia. 


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Waziri Kindamba (kushoto) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) kwenye hafla hiyo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya uthibiti ubora wa mbegu Tanzania (TOSCI), Patrick Ngwediagi.






SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limeingia makubaliano na Taasisi ya Udhibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI), ambapo TTCL imetengeneza mfumo ujulikanao kama 'TTCL HAKIKI' utakaofanya kazi ya kuhakiki mbegu kwa kutumia simu ya mkulima. Mfumo huo utamwezesha mkulima na watumiaji wengine kuthibitisha ubora wa pembejeo za mbegu na vifaa vya kilimo kupitia simu za mkononi na tovuti.

Akizungumza katika hafla hiyo leo, Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba alisema shirika hilo linatambua umuhimu wa sekta ya kilimo nchini katika kuchania maendeleo kiuchumi hivyo imefarijika kushirikiana na TOSCI kuwasaidia wakulima kubaini pembejeo zisizo na ubora.

"...Sote tunatambua kuwa nchini Tanzania, sekta ya kilimo ni muhimili wa maendeleo ya uchumi. Sekta hii inachangia kiasi cha nusu ya pato la Taifa, robo tatu ya bidhaa zinazouzwa nje ya nchi na chaanzo cha chakula pamoja na utoaji fursa za ajira zaidi ya 75% ya Watanzania,"

"Kwa kutambua ukweli huo na kwa kusukumwa na nia ya dhati ya kutaka kuboresha maisha ya Wananchi wetu, TTCL na TOSCI tunaunganisha nguvu ili kuwapatia wakulima mbegu zilizozingatia viwango vya ubora wa mbegu ambazo ni chanzo kikuu cha mavuno mazuri yatakayompatia mkulima faida zinazoendana na juhudi na uwekezaji wake katika shughulihiyo," alisema Bw. Waziri Kindamba.

Huduma hiyo ya kuhakiki pembejeo kwa kutumia 'TTCL HAKIKI' itakuwa ni bure na kwa simu isiokuwa na mtandao wa internet mkulima atatakiwa kutuma ujumbe mfupi wenye code kwenda namba 15035 zilizopo kwenye kifungashio cha mbegu na mteja wa simu janja atatakiwa kupakua app ya TTCL HAKIKI kutoka play store au kuingia www.ttclhakiki.co.tz .

Katika hafla hiyo ya kuingia makubaliano hayo, Taasisi ya Udhibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI), iliwakilishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo, Patrick Ngwediagi ambaye alikiri kuwa mfumo huo utawasaidia wakulima na kupunguza mtawanyiko wa mbegu zisizo na ubora.

RC Wangabo Atoa Wito kwa Wizara kuhusu Ukarabati wa MV LIEMBA

0
0
Eneo la Gati linaloendelea kujengwa katika Bandari ya Kabwe iliyopo Wilayani Nkasi Mkoani Rukwa.
Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh.Joachim Wangabo (wa tatu toka kulia) alipotembelea ujenzi wa bandari ya Kabwe, Wilayani Nkasi.
……………

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ametoa wito kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuhusu kuharakisha ukarabati wa meli ya MV Liemba ili kurahisisha usafirishaji wa mizigo na wananchi wanaoishi katika mwambao wa Ziwa Tanzganyika.

Mh. Wangabo amesema kuwa wananchi hao wamekuwa wakiweka maisha yao hatarini kwa kutumia vyombo kama mitumbwi na boti ambavyo usalama wake ni mdogo ukilinganisha na meli kubwa ya MV Liemba ambayo usalama wake ni wa uhakika.

“Nitoe wito kwa wizara husika hii meli ya MV Liemba nimeambiwa hapa kwamba ikipita kwenda Zambia inaitwa ‘Our Baby’ mtoto wetu, sasa huyu mtoto wetu anaulizwa yuko wapi, Zambia wanauliza, sasa Wizara husika twende haraka isimamie hili jambo, MV Liemba itengenezwe, watu maisha yao yapo kwenye hatari kubwa ndani ya hili ziwa Tanganyika”

Mh. Wangabo ameyasema hayo alipotembelea mradi wa usanifu na ujenzi wa bandari ya Kabwe iliyopo kata ya Kabwe katika Wilaya ya Nkasi ili kujionea maendeleo ya ujenzi huo ulioanza tarehe 1 Aprili,2018 ambapo hadi sasa mradi huo umetekelezwa kwa asilimia 52 katika miezi 14 na unatarajiwa kukamilika tarehe 1 Aprili 2020 na kugharimu Shilingi Bilioni 7.49 ambazo ni fedha za Mamlaka ya Bandari nchini.

Naye Mbunge wa jimbo la Nkasi Kaskazini Mh Ali Kessy alieleza kuwa meli hiyo ya MV Liemba ilitakiwa kukamilishwa ukarabati wake tangu mwaka wa fedha 2017/2018 lakini fedha za ukarabati hazikutengwa na kudai kuwa Waziri wa Fedha Mh. Filipo Mpango amemuhakikishia kuwa fedha za ukarabati wa meli hiyo zimetengwa katika bajeti yam waka 2018/2019.

Kwa upande wake Meneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika Pasivo Ntetema amesema kuwa mradi huo unahusisha ujenzi wa gati, jengo la kupumzikia abiria, jengo la mgahawa, ofisi, ghala la kuhifadhia mizigo, nyumba za wafanyakazi na uzio na kuongeza kuwa kwa Bandari ya Kabwe peke yake wastani wa usafirishaji kwa mwezi ni tani 1500 hadi 2000 na mwaka wa fedha 2018/2019 zimesafirishwa tani 20,000

“Pamoja na changamoto za miundombinu lakini utaona kuna ‘access’ nzuri ya watu kupita hapa kwahiyo kukishaboreshwa bandari hii ikakamilika lakini pia miundombinu ya barabara ya kuingia hapa ikakamilika ni Imani yetu watu wa bandari ya kwamba kupitia uongozi wako, kupitia mheshimiwa mbunge na mamlaka zote zinazotawala mkoa wa Rukwa pamoja na serikali kuu, tutaangalia sasa uwezekano wa kuboresha barabara hii kwa kiwango cha lami ili shehena kubwa iweze kupita hapa
Mamlaka ya Bandari inatekeleza miradi mitatu katika Mkoa wa Rukwa ambayo ni Mradi wa uboreshwaji wa bandari ya Kasanga iliyopo Wilaya ya Kalambo, Ujenzi wa barabara katika Bandari ya Kipili na Mradi wa Usanifu na Ujenzi wa Gati Bandari ya Kabwe zilizopo katika Wilaya ya Nkasi ambapo miradi yote itagharimu shilingi bilioni 12.7

DKT BASHIRU AONYA WATAKAOPITIA MLANGO WA NYUMA KUWANIA JIMBO LA ILEMELA MWANZA

0
0
Dkt Bashiru Ally akizungumza wana CCM katika mkutano Mkuu wa Jimbo la Ilemela tarehe 30 Julai 2019 kuelezea utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi kama ilivyoahidiwa na Mbunge wa Jimbo hilo wakati wa kampeni za uchaguzi za mwaka 2015.Mbunge wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza katika mkutano Mkuu wa Jimbo la Ilemela tarehe 30 Julai 2019 kuelezea utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi kama alivyoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi za mwaka 2015.Sehemu ya wana CCM wakifuatilia mkutano Mkuu wa Jimbo la Ilemela tarehe 30 Julai 2019 kuelezea utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi kama alivyoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi za mwaka 2015.Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Dkt Bashiru Ally (wa sita kushoto), Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Taifa Kheri James (wan ne kushoto), Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye pia na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (wa pili kushoto) na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Anthony Dialo ( wa nne kulia) wakipiga makofi wakati wa mkutano Mkuu wa Jimbo la Ilemela tarehe 30 Julai 2019 kuelezea utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi kama alivyoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi za mwaka 2015.Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula pamoja na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Taifa Kheri James wakicheza na mmoja wa wana kikundi cha ngoma wakati wa mkutano Mkuu wa Jimbo la Ilemela tarehe 30 Julai 2019 kuelezea utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi kama alivyoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi za mwaka 2015.
Mbunge wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza katika mkutano Mkuu wa Jimbo la Ilemela tarehe 30 Julai 2019 kuelezea utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi kama alivyoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi za mwaka 2015. (PICHA ZOTE NA MUNIR SHEMWETA WIZARA YA ARDHI
……………………..
Na Munir Shemweta, WANMM MWANZA
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Dkt Bashiru Ally amesema hatashangaa kuona mbunge wa jimbo la Ilemela ambaye ni Naibu waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akipita bila kupingwa katika uchaguzi mkuu ujao 2020 kutokana na kazi kubwa aliyoifanya ya kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo lake.

Dkt Bashiru alisema hayo tarehe 30 Julai 2019 katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza katika mkutano Mkuu wa Jimbo la Ilemela kuelezea utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi kama ilivyoahidiwa na Mbunge wa Jimbo hilo wakati wa kampeni za uchaguzi za mwaka 2015.
Katibu Mkuu huyo wa Chama cha Mapinduzi alisema hakuna kumnadi tena Dkt Angeline Mabula kwa kuwa anazo sifa zinazomuwezesha kutetea kiti chake na yeyote anayetaka kuwania nafasi katika jimbo hilo ajue kiti hicho kishakaliwa pamoja na kata zake 19.

‘’Ole wake anayetaka kupita mlango wa nyuma, chama kina utulivu sitashangaa Dkt Mabula akipita bila kupingwa ‘’ alisema Dkt Bashiru.
Alionya Wabunge wa CCM waliozembea kufanya ziara za kutatua kero za wananchi pamoja na kufanya vikao kwenye majimbo yao kuwa hawatakuwa na ulinzi wakati wa kinyanganyiro cha kupendekeza majina ya kuwania nafasi hizo na kusisitiza kuwa kipaumbele kitatolewa kwa wabunge waliokuwa wakichapa kazi.

Aliwaaambia wana Ilemela kuwa, kuna tofauti kubwa sana ya kimaendeleo wakati jimbo la Ilemela lilipokuwa chini ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na sasa linavyoshikiliwa na Chama cha Mapinduzi.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Mabula alisema jimbo lake kwa sasa limepiga hatua kubwa kimaendeleo katika sekta za elimu, Afya, Maji, Mindombinu, Uzalishaji na Mifugo, Viwanda na Biashara pamoja na Utamaduni na Michezo ukilinganisha na miaka iliyopita.

Akielezea maendeleo katika sekta ya Afya ndani ya jimbo hilo, Dkt Mabula alisema jimbo la Ilemela limefanikiwa kujenga zahanati mbili mpya alizozitaja kuwa ni Buganda na Lukobe, hospitali ya Wilaya pamoja na vituo vya afya vya Lumala na Nyamazogo.

Aidha, Mbunge huyo wa Ilemela alisema katika sekta ya elimu walifanikiwa kujenga shule mpya za sekondari za Kayenze, Angeline Mabula na Kisundi huku shule za msingi zikijengwa mbili za Kayenze ndogo pamoja na Ihalalo aliyoielezea kuwa ilijengwa kwa ushirikiano na serikali ya Korea kusini aliyoiita shule ya mfano na kubainisha kuwa wilaya ya Ilemela iliongoza kimkoa katika elimu huku ikishika nafasi ya sita katika kanda ya ziwa.

Akigeukia suala la migogoro ya ardhi katika jimbo lake ambapo yeye ni Naibu Waziri mwenye dhamana, alisema jimbo hilo lilikuwa na migogoro mikubwa ya ardhi kati ya wananchi na jeshi la polisi katika eneo la Kigoto, Jeshi la Wananchi na wakazi wa Nyagugulu na mgogoro uliohusisha wananchi wa Bwiru ambapo alieleza kuwa migogoro hiyo sasa imekwisha baada ya wananchi kupatiwa maeneo na wengine kulipwa fidia.

Katika hatua nyingine Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Dkt Bashiru Ally ameonya dhidi ya wafanyabiashara wanaotumia lumbesa na vipimo visivyokubalika katika kupima mazao ya kilimo kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi yao na kuwataka wakuu wa mikoa, wilaya na vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha wanasimamia suala hilo kwani utekelezaji wake umeonekana kusuasua.

Alisema, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli alishatoa maagizo kwake na Waziri Mkuu juu ya suala hilo na kubainisha kuwa watendaji wa serikali wanapaswa kulisimamia hilo na kusisistiza kuwa iwe Ushirika ama mtu binafsi matumizi ya vipimo visivyozingatia taratibu hayakubaliki na mtu wa kutoa taarifa ya matumizi yasiyofaa ya mizani ni wananchi kupitia CCM.

Wananchi Waipongeza Serikali kwa kujenga Vituo vya afya, Wataka Huduma Ziboreshwe,

0
0
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Seikali za Mikoa anayeshughulikia Afya Dkt. Dorothy Gwajima akikagua mfumo wa uhasibu na utoaji wa taarifa za fedha (FFARS) katika Kituo cha afya cha Mpwayungu, kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Jijini Dodoma, alipokuwa kwenye ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya afya na kuangalia utoaji wa huduma za afya kwa jamii katika Wilaya hiyo.




Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Seikali za Mikoa anayeshughulikia Afya Dkt. Dorothy Gwajima akikagua jengo la wodi ya Mama na Mtoto lililojengwa katika Kituo cha afya cha Mpwayungu, kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Jijini Dodoma, alipokuwa kwenye ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya afya na kuangalia utoaji wa huduma za afya kwa jamii katika Wilaya hiyo.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Seikali za Mikoa anayeshughulikia Afya Dkt. Dorothy Gwajima akiongea na wananchi katika Kituo cha afya cha Mpwayungu, kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Jijini Dodoma, alipokuwa kwenye ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya afya na kuangalia utoaji wa huduma za afya kwa jamii katika Wilaya hiyo
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Seikali za Mikoa anayeshughulikia Afya Dkt. Dorothy Gwajima akiongea na watumishi wa Kituo cha afya cha Mpwayungu, kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Jijini Dodoma, alipokuwa kwenye ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya afya na kuangalia utoaji wa huduma za afya kwa jamii katika Wilaya hiyo.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Seikali za Mikoa anayeshughulikia Afya Dkt. Dorothy Gwajima akiongea na wananchi katika Kituo cha afya cha Mpwayungu, kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Jijini Dodoma, alipokuwa kwenye ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya afya na kuangalia utoaji wa huduma za afya kwa jamii katika Wilaya hiyo
…………………….

Na. Angela Msimbira OR-TAMISEMI

Wananchi wa Kijiji cha Mpwayungu kata ya Mpwayungu, Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwajengea miundombinu ya afya ambayo imesaidia kuboresha huduma za afya katika kijiji hicho.

Wakiongea leo wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua ujenzi wa miundombinu ya afya na hali ya utoaji wa huduma za afya katika kijiji hicho iliyofanywa na Naibu Katibu Mkuu kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya Dkt. Dorothy Gwajima wananchi hao wamesema, kabla ya kujengewa miundombinu ya afya hali ya utoaji wa huduma za afya ilikuwa mbaya kiasi ambacho walikuwa wakifuata huduma hiyo katika Hospitali ya Mvumi

Akiongea kwa niaba ya wananchi wa kijiji hicho Mwenyekiti wa Kamati ya Usimamizi wa Kituo cha Afya cha Mpwayungu Bw. Chibwele Magubika amesema, awali hali ya utoaji wa huduma za afya katika kituo hicho zilikuwa duni kiasi ya kwamba wananchi wengi walikuwa wakikimbilia kupata huduma hizo katika Hospitali ya Misheni Mvumi au Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.

Bw. Magubika ameishukuru Serikali kwa kujenga miundombinu ya afya na kuboresha huduma za afya kwa wananchi ila ameiomba Serikali ihakikishe huduma hizo zinaboreshwa na kwamba, watumishi wanakuwa na lugha nzuri kwa wateja na kufanya kazi kwa weledi ili wananchi wengi waweze kuvutiwa na utoaji wa huduma katika kituo hicho.
“Inasikitisha kuona Serikali imewekeza fedha nyingi katika ujenzi wa miundombinu ya afya yakiwemo majengo mazuri makubwa na yenye kuvutia lakini baadhi ya watumishi bado wanakuwa na lugha chafu ambazo haziwavutii wananchi kuja kupata huduma kwenye vituo kama hivi” Amesema Magubika.

Ameendelea kufafanua kuwa kuna baadhi ya watumishi hapa ni watovu wa nidhamu, wana lugha chafu kabisa, hawana maadili katika utendaji kazi wao, wanalewa pombe, hawatoi huduma kwa wakati jambo ambalo linakatisha tamaa wananchi kufika kupata huduma.

Naye Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Mpwayungu Selemani Kibakaya amesema kuwa, huduma zikiboreshwa, watumishi wakafanya kazi kwa ushirikiano bila kutegeana itasaidia kupunguza changamoto mbalimbali zinazojitokeza ikiwemo ya utoaji wa huduma bora kwa wananchi,Amewataka wafanyakazi kuhakikisha wanatoa huduma kwa wakati, kwa kuwajali wagonjwa ili kuweza kupunguza msongamano pamoja na wananchi kukaa muda mrefu kusubiri huduma za afya jambo ambalo linakatisha tamaa ya kupata huduma za afya.

Wakati huohuo Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya Dkt. Dorothy Gwajima amawaagiza Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha wanafanya ufuatiliaji wa kero wanazopata wananchi wakati wa kufika kwenye vituo vya huduma kwa kuongea na wateja, viongozi wa serikali ya kijiji na Wajumbe wa Kamati ya Usimamizi wa Kituo wanaowawakilisha wananchi kwenye uongozi wa kituo.

Vilevile, Dkt, Gwajima amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha wanachukua hatua stahiki kwa wakati pale wanapopelekewa malalamiko siyo tena nao wanakaa miezi 6 bila kuchukua hatua kama ilivyotokea kituoni hapo.Dkt Gwajima amesema, ukosefu wa hatua stahiki dhidi ya kero zinazoripotiwa na wananchi ndiyo mojawapo ya mambo yanayowakwaza wananchi na kuamua kutotumia vituo husika au kuamua wanavyoona wao inafaa.

“CHMT NA RHMT hakikisheni mnafuatilia na kusimamia utendaji kazi wa watumishi katika vituo vya kutolea huduma, kutoa msaada na ushauri wa kitaalamu pia, kusikiliza kero za wananchi dhidi ya huduma na katika kila jambo, kuchukua hatua stahiki kwa wakati na bila kuonea upande wowote ule. Msisubiri hadi Wizara itembelee ndiyo iibue hizi kero na nyie mpo huku.
Amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino kuhakikisha anafanyia kazi malalamiko ya wananchi na kuchukua hatua stahiki za kiutumishi dhidi ya mtumishi Claude Chilala ambaye anatuhumiwa na wananchi kukiuka maadili ya kiutumishi na kuwa kero sugu kwa wateja.

Dkt. Gwajima amewapongeza watumishi wengine ambao wananchi wamekiri kuwa hawana shida ukilinganisha na huyo anayelalamikiwa na kila mteja.Aidha amewataka watumishi kutoiga tabia ambazo zinakiuka maadili ya utumishi wa umma na kwamba, washirikiane daima vinginevyo, mambo yakiharibika inaweza ikawa vigumu kutowajibika kwa namna moja au ingine.

MAGAZETI YA LEO JUMATANO JULAI 31,2019


WATOA HUDUMA ZA AFYA WATAKIWA KUDHIBITI UGONJWA WA EBOLA USIINGIE NCHINI

0
0
Na WAMJW – Bukoba, KAGERA

Watoa huduma za afya nchini wametakiwa kuweka juhudi madhubuti kuhakikisha Ugonjwa wa Ebola hauingii nchini Tanzania.

Rai hiyo imetolewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Prof. Faustinely Kamuzora alipokuwa akifungua zoezi la utayari jinsi ya kukabiliana na ugonjwa wa ebola kwa wataalam wa afya mkoani humo.

Akifungua zoezi la utayari, Profesa Kamuzora amesema “Tukifanya juhudi zetu za kukabiliana na ugonjwa wa ebola basi maisha yetu hayatokuwa hatarini” na kuendelea “Juhudi hizi zina matunda makubwa kuliko tukaruhusu ugonjwa huo kuingia nchini”

“Mpaka sasa hivi Mwenyezi Mungu ametujaalia hakuna mtu aliyeripotiwa kuwa na ugonjwa wa Ebola nchini, tukifanya yale ambayo tunaelekezwa na wataalam wetu basi maisha yetu hayatokuwa hatarini” amesema Profesa Kamuzora.

Prof Kamuzola amewataka watoa huduma za afya kufuata taratibu zote zilizowekwa ili endapo ikitokea mtu akabainika kuwa na ugonjwa huo, basi aweze kupatiwa huduma na wakati huo huo mtoa huduma akawa salama.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Bashiru Taratibu amesema kuwa zoezi ya utayari lina lengo la kuzuia maafa yasitokee kwa kuwaweka tayari watalaam wa sekta ya afya kukabiliana na tishio la ugonjwa wa ebola kuingia nchini.

“Tuhakikishe tunazuia ugonjwa wa ebola usiingie nchini, na endapo ikitokea umeingia basi tuhakikishe tunapunguza athari zitokanazo na ugonjwa huo” amesema Bw. Taratibu.

Naye Mtaalam wa Afya ya Jamii na Masuala ya Dharura na Maafa kutoka Wizara ya Afya Dkt. Faraja Msemwa amesema kuwa kupitia mazoezi hayo ya utayari wanapata fursa ya kubaini fursa na changamoto zilizopo katika kudhibiti ugonjwa huo wa ebola usiingie nchini.

“Katika zoezi hili tunaangalia hawa watumishi wetu wa afya tuliowandaa wana uwezo wa kiasi cha kuweza kufuata miongozo iliyoandaliwa” amesema Dkt. Msemwa.

Kwa mujibu wa takwimu kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) toka kuripitiwa kuibuka kwa ugonjwa wa ebola nchini Uganda mnamo mwezi Agosti mwaka 2018 jumla ya kesi 2612 za watu kuathiriwa na ugonjwa huo zimeripotiwa huku ukisababisha vifo 1756 (sawa na asilimia 67). Zoezi la utayari limepangwa kufanyika kuanzia leo JULAI 30 mpaka AGOSTI 8 mwaka 2019 ambapo vituo vya kutolea huduma za afya katika Mikoa ya Kagera na Kigoma vitapimwa utayari wao katika kukabiliana na Ugonjwa huo hatari.

Kupitia mazoezi ya utayari, watoa huduma za afya kuanzia ngazi ya jamii wanapata fursa ya kushiriki kwa vitendo namna ya kutambua, kutoa huduma kwa mtu anayehisiwa au kuwa na ugonjwa wa ebola na kuwaondolea woga pindi ikitokea mtu akabainika kuwa na ugonjwa huo.
 Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Prof. Faustin Kamuzora akisema jambo wakati akifungua zoezi la utayari wa kukabiliana na Ugonjwa wa Ebola kwa Watoa huduma za afya katika Mkoa wa Kigoma (hawapo pichani) jana Mjini Bukoba.
.
 Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Bashiru Taratibu akisema jambo wakati wa ufunguzi wa zoezi la utayari wa kukabiliana ana Ugonjwa wa Ebola kwa watoa huduma za afya Mkoani Kagera (hawapo pichani) jana Mjini Bukoba.

 Washiriki wa zoezi la utayari wa kukabiliana na tishio la Ugonjwa wa Ebola kutoka Mkoa wa Kagera wakiwa kwenye majadiliano kuweka mikakati ya ugonjwa huo usiingie nchini.
 Mwakilishi kutoka Shirika la Afya Duniani Dkt. Refeya Ndyamuba (aliyesamama) akisema jambo wakati wa ufunguzi wa zoezi la utayari wa kukabiliana na Ugonjwa wa Ebola nchini kwa watoa huduma za afya katika Mkoa wa Kigoma jana Mjini Bukoba.

 Picha ya Pamoja washiriki wa zoezi la utayari wa kukabiliana na Ugonjwa wa Ebola na Mgeni Rasmi, Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Prof. Faustin Kamuzora (aliyeketi katikati)


WANAFUNZI WENYE ULEMAVU WASHAURIWA KUZINGATIA MASOMO NA KUSOMA KWA BIDII.

0
0
Wanafunzi wenye ulemavu  wameshauriwa  kuzingatia masomo na kusoma kwa bidii ili kujiandalia maisha yao ya baadae kwa kuwa elimu ndio mtaji wa maisha yao.

Ushauri huo umetolewa na Mbunge wa Viti Maalum, Amina Mollel alipotembelea shule ya  Sekondari Longido pamoja na shule ya msingi Longido wilayani Longido katika mkoa wa Arusha, ambazo zote zina vitengo  Maalum kwa ajili ya watoto wenye Ulemavu.

Akizungumza na wanafunzi hao,  Amina ametoa ushuhuda kuwa safari yake ya maisha pamoja na kuwa na vikwazo vingi  hadi kufika alipo sasa ni kwa  mapenzi ya Mwenyezi Mungu pamoja na kusoma kwake kwa bidii elimu ambayo imemsaidia  kumpa mwanga katika maisha yake.

Amewataka wanafunzi hao kutokujiona wapweke kwa kuwa Serikali ya awamu ya tano inawapenda na kuwajali na ndio maana Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa mara ya kwanza hapa nchini tangu kupata uhuru amewateua watu wenye ulemavu kumsaidia kwenye serikali yake pasipo kujali ulemavu walionao.

Akiwa katika shule ya Msingi Longido, Amina amewashuhudia watoto wasioona ambao baadhi yao hutelekezwa na wazazi wao wanapowafikisha shuleni hapo.

Mbunge huyo amewaomba wasamaria wema kujitoa katika kuwasaidia watoto wenye uhitaji kwa kuwapatia mahitaji muhimu kama nguo, mafuta, sabuni pamoja na mahitaji mengine muhimu yatakayowasaidia kutimiza malengo yao.

Ameipongeza shule ya Sekondari Longido kwa matokeo mazuri ya kidato cha sita   waliyopata kwa mwaka huu ambapo wanafunzi wengi wamefaulu daraja la kwanza na lile la pili. 

Amina Ametoa zawadi ya Computer  moja, counter book pamoja na sabuni na mafuta kwa shule ya Sekondari Longido.

Katika ziara hii aliongozana na viongozi wa Uwt pamoja na viongozi wa Chama cha Mapinduzi.

 Mbunge wa Viti Maalum, Amina Mollel akizungumza na Wanafunzi wa kidato cha tano na sita wanaosoma katika Sekondari ya Longido
 Mbunge wa Viti Maalum, Amina Mollel akiwa na Wanafunzi 41 wenye ulemavu wanaosoma katika shule ya Sekondari Longido
Mbunge wa Viti Maalum, Amina Mollel akikabidhi moja kati ya zawadi alizojaaliwa kuzipeleka katika shule ya Msingi Longido
Mbunge wa Viti Maalum, Amina Mollel  akiwa na Mwanafunzi Mwenye ulemavu wa ngozi Ummy ambaye aliwakilisha mkoa wa Arusha katika mashindano ya Umiseta Mtwara katika Riadha na hatimaye kuuletea mkoa medali ya dhahabu.

Serikali imeweka usawa wa Dini-Msopa

0
0
Mkurugenzi wa Sharif Condition Sheikh Chief Msopa  amesema kuwa serikali ya awamu ya Tano imeweza kufanya mambo ikiwemo kujenga msikiti mkubwa katika Ofisi za Baraza Kuu la Waislaam Tanzania (Bakwata).

Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam Msopa amesema kuwa Rais Dkt.John Pombe Magufuli hana upendeleo wowote alichofanya ni kuweka usawa wa Dini.Amesema kuwa watu wanataka kuharibu utaratibu kwa kuanza kufikiria uchaguzi sasa wakati bado kuna maendeleo yanafanyika na Rais aliyopo madarakani.

Aidha amesema kuwa hakuna serikali inayoweza kuingiza fedha kwa kila mwananchi kinachotakiwa ni kufanya kazi tu.

Amesema kuwa wananchi wanatakiwa kuangalia katika kipindi kifupi maendeleo yamefanyika kwa kasi kubwa ikiwa kutoa huduma bora kwa wananchi.

Msopa amesema kuwa katika kipindi cha Utawala wa serikali ya awamu ya tano fursa nyingi zimejitokeza kwa ajira kwa vijana yote ni kutokana na ubunifu wa Rais Dkt.John Pombe Magufuli.Aidha ameunngana na Kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam katika Uhamasishaji wa usafi katika jiji la Dar es Salaam.Amesema mkutano wa SADC ni mkubwa hivyo usafi ufanyike na kuwa endelevu.
Mkurugenzi wa Sharif Condition Chief Msopa akizungumza na waandishi habari kuhusiana maendeleo yanayofanyika katika serikali ya awamu ya Tano ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli jijini Dar es Salaam.

NAJUA WAJUA ILA NATAKA KUKUJUZA ZAIDI NA ZAIDI KUHUSU SPORTPESA SIMBA WEEK NA SIMBA DAY

0
0


Na Hashim Mbaga 

Simba Sports club Limited Imefanya Press yake kubwa sana chini ya CEO Mr. Magori na kutangaza Rasmi Msimu mpya kuanza kwa mwaka wa 10 mfululizo kwa Tamasha kubwa la Simba Day.

Mwaka huu Simba Day imepata hamasa sana na imepangiliwa kwaa ufasaha kwa kupata vionjo vipya ikiwemo mdhamini Mkuu wake Sportpesa kushirikiana katika kufanikisha Tamasha hili hivyo ikabidi kufanya Joint ya kibiashara ya Jina na kuwa Rasmi ni Sportpesa Simba Week.

CEO Aliweza kutaja Rasmi Matukio kama Ifuatavyo:

31/07/2019 - JUMATANO

WACHEZAJI KUWASILI DSM
Mabingwa wa nchi, Mabingwa wa kihistoria wa Kagame Cup na Wataalam pekee waliofika Quarter final Champions League Caf kwenye Ukanda huu wa Africa Mashariki na Ndio Wafanikishaji wa kihistoria kuweza Tanzania kuingiza Interclub timu 4 wanaingia Toka kwenye Camp yao iliyowekwa Sports Campus iliyoko Kwenye viunga vya Hotel ya kifahari  The Royal Manang 5star jiji Rustenburg nchini South Africa wakitua na Ndege ya wazalendo Air Tanzania.

KUSAINI MKATABA
Kutakuwa na Press Serena Hotel kuanzia Saa 5 Asubuhi katika hafla ya kusaini mkataba kati ya Simba na Romario Sports 2000 kwa ajili ya Vifaa vya michezo na Jezi kwa ujumla pia Faida ya kimkataba baina yao wataweka wazi.

UZINDUZI WA JEZI MPYA
Ifikapo saa 6 usiku Kwenye mitandao rasmi ya Simba yote pamoja na Sponsor wote wa Simba kutawekwa Jezi mpya za msimu huu zitakazotumika za Rangi 3 tofauti Red, White na Gray.
Watu wote muda huo Usikose Angalia uyape macho ladha yake ndani ya moyo wako.....KUNA ANAETASEKA HAPA?

01/08/2019 - ALHAMISI
UUZAJI WA JEZI
Hii ndio siku rasmi Jezi zote zinaanza kuuzwa nchi nzima na zitapatikana maeneo yote makubwa na mikoa yenye mashabiki wa Simba kirahisi.
Kutatangazwa vituo/sehemu za kupatikana Jezi.

KUUZA TIKETI
Mwanzo wa kuuzwa Tiketi za Aina Mbili ambazo ni Platinum na Platium Plus.
Bei ya Tiketi zote  ni kama ifuatavyo:
Mzunguko  5,000
VIP B        15,000
VIP A        30,000
Platinum 100,000
Platinum Plus 150,000

Kifupi Vingezo au huduma zitakazopatikana kwenye Tiketi za Platinum zitatangazwa baadae ila baadhi yake ni
- Kukaa eneo mahsusi uwanjani
- Kupata usafiri mzuri kwenda
- Kupata jezi Original
- Kupata fursa ya Picha na Wachezaji uwatakao siku maalum wwewena familia yako.
- Kupata vinywaji nk nk.

KADI MPYA ZA SIMBA
Kutakuwa na Press kubwa sana Serena Hotel katika Tukio la Karne la kutanganza Card Mpya ya Simba.
Kutakuwa na kusainiana mikataba na Washirika wa kibiashara watakaosaidia katika kazi hiyo ili kuweka ufanisi.
Kutaelezwa kila kitu kuhusu upatikanaji wa card na utumiaji wake.
Card zinazokusudiwa kutolewa ni kwa Wanachama waliopo New Members Card, na wapenzi/mashabiki wa Simba New Fans Card ambazo kwa hawa fans ndio ili uwe mwanachama mpya hapo baadae lazima upitie kwenye eneo hili kwanza.
Kadi zinazotolewa sasa zitakuwa na uwezo wa kuhifadhi fedha, kuingilia uwanjani,  kulipia michango nk, kununulia bidhaa mbalimbali kwa Punguzo maalum kifupi zinaitwa E-CARD.

02/08/2019 - IJUMAA

Ni siku maaalum kwa Simba Sports club kutembelea Sponsor wake wote kwenye vituo/ofisi Zao.
Tunaanzia Sportpesa Saa 3 asubuhi halafu Saa 5 kwenda Azam Media na kuendelea.


03/08/2019 - JUMAMOSI

SPORTPESA STREET VISIT
Kampuni ya Sportpesa ikishirikiana na wachezaji wa Simba itafanya au unatembelea Vituo vya Watoto wenye vipaji maalum na mazingira MAGUMU katika kutoa msaada na hamasa kwa jamii.

OCEAN ROAD HOSPITAL
Wachezaji wote wa Simba watatembelea kutoa Pole, faraja na mkono wa heri kwa wagonjwa wote, wasiojiweza na katika kurudisha Shukrani kwa jamii.

WATU WOTE NCHINI
Tunaomba wote kama kawaida sehemu mbalimbali na matawi yote siku hii wakati wachezaji wanaenda Ocean road Hospital nao popote walipo Waende kwenye Hospital au vituo vya Jamii katika kufanya tukio la kijamii.
Pia Wote Tuweze kutoa Damu kama tunavyofanya kila mwaka kwa DSM Tutatangaza Vituo vitakuwa wapi baada ya kushauriana na wenzetu wa Benki ya Damu nchini.

WIMBO WA SIMBA
Kutatambulishwa Wimbo rasmi maalum wa club yetu ya Simba ambao tutakuwa tunauimba mahali popote kuonyesha ufahari wetu.
Utagusa, utaleta hisia na Ushujaa miongoni mwetu na kisababisha ujasiri wa Upambanaji ndani ya Uwanja na Nje ya Uwanja Lengo kuu ni Nguvu Moja.

04/08/2019 - JUMAPILI
KUPIGA PICHA NA WACHEZAJI
Tukio hili limebatizwa jina linaitwa *Photoshoot With Simba Stars*
Ni tukio ambalo itafanyika Serena Hotel kuanzia saa 4 asubuhi kwa watu wote walikataa Tiketi za Platinum na Platinum Plus kuweza kuja na Family zao hasa watoto ili kupiga picha na Wachezaji wanawao wapenda pamoja na kuandika majina wayapendayo kwenye jezi zao.

Baada ya hapo Wachezaji wote wanakwenda kutembelea Vituo vya Watoto Yatima na Mazingira magumu katika kutoka sadaka kwa niaba ya Club ya Simba.



Mwisho siku hii tutamalizia kwa kuwapokea Timu Marafiki wetu wanaokuja kucheza nasi siku ya kilele cha Sportpesa Simba Week timu ya Power Dynamos ya kutoka Zambia.

05/08/2019 - JUMATATU
SIMBA QUEENS
Wachezaji wote wa Simba Queens na warimbwende wa Simba watatembelea Shule ya Makongo Secondary kwa ajili ya kutoa/kuonyesha/Kuwaasa kwa pamoja jinsi ya kuishi, kucheza, elimu na EXPOSURE kwa ujumla walionayo na walioipata toka Germany.

RATIBA YA KIBABE
Saa 8:30 Mchana - Pre match inayofanyika Uwanja wa Taifa.

Saa 9:30 Mchana Press za timu zote mbili zitafanyika.

Saa 10:30 jioni Simba Watafanya mazoezi Uwanja wa Taifa

Saa 11:30 jioni Power Dynamos watafanya mazoezi Uwanja wa Taifa.

06/08/2019 - JUMANNE

Hii ndio siku ambayo nchi nzima inatakiwa kuwa Red yote.
Uwezekano wa Kuwekwa Screen kubwa uwanjani sehemu mbalimbali Dsm na mikoani unafanyiwa kazi ili wote wana Simba waweze kuangalia pamoja tukio hili la Simba popote ulipo.

SAA 4 ASUBUHI
Milango yote inakiwa wazi watu waweze kuanza kuingia uwanjani.

SAA 8 MCHANA
Timu ya Simba Queens inacheza ndio itazindua uwanja kwa mechi.

SAA 9 MCHANA
Timu ya Simba U20 itacheza na FontainGate Academy.

SAA 10:30 JIONI
Utambulisho wa mbwembwe wa wachezaji wote wa Simba.

SAA 11:30 JIONI
Ule mchezo rasmi ndio itacheza
Simba vs Power Dynamos.

07/08/2019 - JUMATANO
Kutakuwa na After Sportpesa Simba week Party ni Dinner maalum kwa wageni maalum katika kuwashukuru kufanikisha Sportpesa Simba week wakiwepo Sponsors, Makundi mbalimbali ya Simba, Wachezaji wa Timu zote ppamojana kuwaagaa timu ya Power Dynamos.

SLOGAN YA MWAKA HUU
Mwaka huu kwenye Sportpesa Simba Week tunakwenda na kauli mbinu maalum na ambayo
Tunaomba kila MwanaSimba akipost kitu amalizie na:
IGA UFE: #This is next level#

Hii ndio Kauli yetu popote pale kwenye Sportpesa Simba week.

PICHA YA MTORI SIO SAWA NA MTORI HALISI

TUNAFANYA FUJO ZISIZOUMIZA💥
IGA UFE:#This is Next level#

TUWE NA UPENDO WA KUJITOLEA NA KUWASAIDIA WALEMAVU-MBUNGE VITI MAALUM AMINA MOLLEL

0
0
Jamii imeshauriwa kuwa na moyo wa upendo na kujitolea katika kuwasaidia watu wenye ulemavu ambao wengi wao wanaishi katika dimbwi kubwa la umasikini.

Hayo yamesemwa na Bi Theresia Kazimoto mkazi wa Kata ya Laroi mwenye  watoto wanne ambao wote wanaulemavu.

Bi Theresia ameyasema hayo alipotembelewa na mbunge wa Viti Maalum Amina Mollel aliyeitembelea familia hiyo nyumbani kwao Laroi na kujionea mateso anayopata mwanamke Huyo  katika kuwalea watoto hao.

Akiwa nyumbani hapo, Mbunge huyo ameisaidia familia hiyo mahitaji mbalimbali na kuahidi kurudi tena ili kufuatilia majibu ya vipimo vilivyopelekwa katika hospitali ya KCMC.
 Mbunge wa Viti Maalum,Amina Mollel akifurahia jambo na Watoto wane wenye ulemavu .

 Mbunge wa Viti Maalum,Amina Mollel akiwa katika picha ya pamoja na watoto wane wenye ulemavu sambamba na Mzazi wao pamoja na wasaidizi wa Mbunge huyo.
Viewing all 109592 articles
Browse latest View live




Latest Images