Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110029 articles
Browse latest View live

Ushiriki wa Kinababa ni muhimu katika wiki ya Unyonyeshaji-RC Wangabo.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewataka wananchi wa mkoa wa Rukwa hasa kinababa kushiriki katika maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji yanayofanyika kila mwaka kuanzia tarehe 1 hadi 7 ya Mwezi wa Nane ambapo Tanzania huungana na nchi nyingine duniani katika maadhimisho hayo.

Amesema kuwa wiki hiyo ya unyonyeshaji itumike katika mapambano dhidi ya udumavu ambao mkoa wa Rukwa unaongoza kitaifa kwa kuwa na udumavu wa asilimia 56.3 na hivyo kuwataka wananchi kushiriki kwa ukamilifu katika maadhimisho hayo yatakayofanyika katika vijiji 339 vya mkoa huo ili kupata elimu stahiki itakayowawezesha kuwaepusha watoto na udumavu.

‘Msingi Mkubwa kabisa wa kupambana na udumavu uko hapa kwenye unyonyeshaji, ni lazima mama anyonyeshe mtoto wake ipasavyo, kina mama huwa wanapuuza wengine kufanya jukumu hili kwasababu labda ya masuala ya kiuchumi lakini pia hata kijamii na kimazoea, sasa hii elimu ndio inapswa kuitoa ndani ya siku hizi saba,kwasababu inakwenda katika vijiji vyote, kinamama wakisikia huu ujumbe pamoja na jamii kwa ujumla na kinababa wote tutaweza kupambana na udumavu,” Alisisitiza.

Aidha amevitaka vyombo vya habari kushiriki katika kufuatilia utekelezaji wa sheria mbalimbali zinazolinda haki za uzazi na ulishaji wa watoto kwa kufanya tafiti, kuandika au kuripoti matukio mbalimbali kama vile utekelezaji wa haki mbalimbali ikiwemo haki ya kupata likizo ya uzazi.

Mh. Wangabo ameyasema hayo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo tarehe 31.7.2019 katika maandalizi ya maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji ambayo kimkoa itafanyika katika Kijiji cha Kisumbakati, Wilayani Kalambo ambapo maadhimisho hayo yatakwenda sambamba na siku ya Afya ya Kijiji katika vijiji vyote vya mkoa.

Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. Emanuel Mtika alisisittiza kuwa mradi wa Lishe Endelevu ambao unalenga kupunguza udumavu katika Mkoa wa Rukwa umekuja kuongeza kasi ya juhudi za mkoa katika kupambana na udumavu na kuongeza kuwa maadhimisho hayo yanalenga kujenga uelewa wa pamoja katika unyonyeshaji wa mtoto.

“Siku 1000 za makuzi ya mtoto, ukikosea kwenye eneo la unyonyeshaji kuna uwezekano mkubwa sana wa kumuweka mtoto kwenye mazingira magumu, kwahiyo hii inalenga sit u kutoa elimu ya unyonyeshaji lakini pia juu ya maandalizi ya vyakula vya watoto hawa,” Alisema.

Halikadhalika Kaimu Afisa Lishe wa Mkoa Asha Izina alizitaka sekta binafsi kuwapa muda wafanyakazi kina mama wenye watoto ili aweze kuwanyonyesha watoto wao, “Serikali inatia msisitizo kwamba waajiri wahakikishe nao pia wanatoa nafasi au wanatengeneza mazingira ambayo yanakuwa ni Rafiki pale kazini ambapo mama analetewa kazini mtoto wake na kuhakikisha kwamba anamnyonyesha, tukitambua kwamba maziwa ya mama ni ya muhimu kwa afya na maendeleo ya mtoto”.

Kauli mbiu ya mwaka huu 2019 ni: “Mwezeshe mama aweze kunyonyesha.” Ambayo inasisitiza kuwa kwa pamoja tushirikiane kumwezesha mama aweze kunyonyesha ipasavyo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kushoto) akiogea na Waandishi wa habari katika maandalizi ya maadhimisho ya wiki ya Unyonyeshaji Mkoani Rukwa.

Serikali yamrudishia mwananchi Ghorofa alilodhurumiwa kwa nyaraka za kughushi.

$
0
0
Na Chalila Kibuda, MICHUZI TV.

Serikali imerudisha nyumba ya ghorofa Nne kwa mmiliki wa awali ambalo lilikuwa limetapeliwa na mtu mmoja anayedaiwa kuwa Macha.

Ghorofa hilo aliidhinishwa mmiliki Macha kwa nyaraka za kughushi kupitia msajili wa hati ambaye aliondolewa kwa kughushi huko na Waziri Mwenye dhamana ya Ardhi nchini .

Akizungumza na waandishi wa habari wakati akimkabidhi mmiliki halali wa ghorofa hilo Ramadhan Balenga, Waziri Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema kuwa Ramadhan Balenga alighushiwa hati hati na kufukuzwa walinzi waliokuwepo katika ghorofa hilo.

Amesema utapeli huo unakomeshwa kwa wale wote waliofanya hujuma katika sekta ya ardhi ambao kwa kudhutumu haki za watu katika Wilaya za Kinondoni na Ilala.

Waziri Lukuvi amesema kuwa madiwani zamani walikuwa wanahongwa na matajiri kwa kuitisha vikao kupitisha ardhi za watu kwa nyaraka za kutengeneza huku wakisahau kuwa hati za umiliki wa ardhi hazibadiriki.

Mmiliki wa Ghorofa hilo Ramadhan Balenga alisema baada ya kugushiwa nyaraka za Ghorofa hilo alipata ukichaa pamoja na kuachana na mke wake kutokana na anayedaiwa kuwa na Ghorofa hilo Macha kuivuruga ndoa yake.

Amesema kuwa alikuwa anaokota makopo kutokana na ukichaa lakini sasa kapona na kuishukuru serikali kwa kumrudishia haki yake aliohangaikia kwa muda mrefu.Wakati huo Waziri Lukuvi amewataka Kanisa Catholic kufika ofisini kwao kutokana na mgogoro wa eneo la kituo cha mafuta cha Victoria Msimbazi Centre kuondoa utata wa umiliki wa eneo hilo.

Waziri Lukuvi anasema hilo eneo ni mali ya Kanisa kwani hati ndio inasoma hivyo lakini mmiliki wa kituo hicho katatpeliwa na mtu mmoja anayedaikuwa kuwa ni Mwarabu.Mmiliki wa Kituo cha Mafuta cha Victoria Msimbazi Centre Harold Matemba amesema alinunua kwa njia halali kwa mwarabu na nyaraka za manunuzi ya eneo hilo anazo na alipitia hatua zote ikiwemo na Manispaa ya Ilala.
 Waziri wa Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akimweleza mwananchi  Ramadhan Balenga aliyekuwa amenyanganywa haki ya Ghorofa katika eneo la Kigogo jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akimuonesha  mwananchi  Ramadhan Balenga aliyekuwa amenyanganywa haki ya Ghorofa katika eneo la Kigogo jijini Dar es Salaam nyaraka alizopewa za udanganyifu na uhalali wake kwa nyaraka ya waziri huyo.
 Waziri wa Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza na waandishi habari kuhusiana na matapeli wanavyfanya utapeli wa nyuma na viwanja katika jiji la Dar es Salaam.
 Muonekano wa Ghorofa hilo lilojengwa na Ramadhan Balenga na kughushiwa kwa mtu mwingine anayedaiwa kuwa  Macha.
 Mwakilishi wa Kanisa Albart Singombe akitoa maelezo kuhusiana na umiliki wa eneo la kituo cha mafuta kuwa eneo la Kanisa wanashangaa kuwepo kwa kituo  hicho .
Muonekano wa kituo cha mafuta  cha Victoria eneo la Msimabazi.(picha  zote na Chalila Kibuda).

ATE WAZINDUA MKUTANO MKUU WA PILI WA WANAWAKE KATIKA UONGOZI 2019.

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv

CHAMA cha Waajiri Nchini (ATE) wamezindua mkutano mkuu wa pili wa Wanawake katika uongozi kwa mwaka 2019 utakaoambatana na Mahafali ya Tatu ya Programu ya Mwanamke wa Wakati Ujao.

Mkutano huo unatarajia kufanyika siku ya Alhamisi tarehe 19 Septemba 2019 ambapo wanatarajia Mgeni Rasmi awe ni mmoja wa Viongozi Wakuu wa Kitaifa ambaye atatangazwa baadae baada ya uthibitisho wake.

Akizungumza na waandishi wa Habari, Mkurugenzi Mtendaji wa ATE, Dkt Aggrey Mlimuka amesema Mkutano wa Mwaka huu umebeba kaulimbiu isemayo Mustakabali wa Ajira za Wanawake kwa Wakati Ujao: Je Sera za Mahali pa Kazi zipo tayari? Lengo likiwa ni kuwaleta pamoja viongozi wa makampuni, mashirika binafsi, mashirika ya umma, mashirika ya kimataifa, taasisi mbalimbali pamoja na wadau wote wa uongozi ili kujadili namna ya kuhakikisha uwepo wa sera zinazochochea kuongeza idadi ya wanawake katika Nafasi za Juu za Uongozi na Bodi za Wakurugenzi.

Dkt Mlimuka amesema, Mkutano wa mwaka huu utakuwa ni tofauti na ilivyokuwa mwaka uliopita kwani kwa mara ya kwanza, Mwaka huu tutatumia mkutano huo kuhakikisha na kuyaonesha makampuni na Taasisi mbalimbali njia bora za utekelezaji wa Kanuni za Umoja wa Mataifa za Uwezeshaji wa Wanawake (United Nations Women Empowerment Principles) ambapo tafiti zinaonesha kwamba kwa kufanya hivyo makampuni huongeza ufanisi sehemu za kazi na kupelekea kuongezeka kwa uzalishaji 

Amesema malengo makuu ya Mkutano Mkuu wa Pili wa Wanawake katika Uongozi ni Kujadili Changamoto zinazowakabili viongozi wanawake na fursa zinazohusiana na Mustakabali wa Ajira za Wanawake kwa Wakati Ujao, pili ni Kubadilishana ujuzi na uzoefu kuhusiana na ujumuishwaji wa wanawake katika nafasi za juu za Uongozi wa Makampuni na Taasisi za Kibiashara.

Aidha, lengo la tatu ni Kuzindua rasmi utekelezaji wa Kanuni za Umoja wa Mataifa za Uwezeshaji wa Wanawake ambapo kutatolewa muongozo wa namna nzuri ya Mkampuni kuziweka kanuni hizi katika utekelezaji utakaohusisha pia kuwaleta wafanyakazi wao wa kike kushiriki katika programu ya Mwanamke wa wakati ujao na nne ni Kushuhudia na kusherekea mafanikio mbalimbali yaliyotokana na Programu ya Mwanamke wa wakati ujao tangu kuanzishwa kwake mnamo mwaka 2016.

"Tafiti mbalimbali zimethibitisha kuwa taasisi na makampuni yaliyofanikiwa kuwa na wanawake katika nafasi za juu za uongozi yamepata matokeo chanya kama vile ongezeko la uzalishaji jambo ambalo Chama cha Waajiri wangependa kulifanikisha kwa wanachama wao na wasio wanachama pia katika kuunga mkono jitihada za kitaifa za kujenga Tanzania ya Viwanda ili kufikia Uchumi wa Kati ifikapo Mwaka 2025," amesema Dkt Mlimuka.

Aidha, ameeleza jitihada hizi zinaendana na juhudi ambazo zinafanywa na Chama cha Waajiri Tanzania na Shirikisho la Vyama vya Waajiri Nchini Norway (NHO) kwa kutoa mafunzo ya Mwanamke wa wakati Ujao (Female Future) yaliyozinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Hassan Suluhu mwaka 2016.

Programu hii imefanikiwa sana kuandaa wanawake kwa ajili ya nafasi za juu za uongozi na kuwapa uwezo wa kuingia kwenye bodi mbalimbali na kushiriki katika kutoa maamuzi ambapo wanawake kadhaa waliohitimu tayari wamefanikiwa kupata nafasi za juu za uongozi na pia kuwa wawakilishi kwenye bodi mbalimbali huku mchango wao ukioneka dhahiri na ATE wamekuwa wakishirikiana na Shirikisho la Vyama vya Waajiri Nchini Norway (NHO) pamoja na UN Global Compact Network Tanzania(UNGCN).
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Dkt Aggrey Mlimuka(katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mkutano mkuu wa pili wa Wanawake katika uongozi kwa mwaka 2019 utakaoambatana na Mahafali ya Tatu ya Programu ya Mwanamke wa Wakati Ujao unaotarajiwa kufanyika siku ya Alhamisi tarehe 19 Septemba 2019, Kushoto ni Mratibu wa UN Global Compact Network Emanuel NNko.

DC SABAYA AAGIZA KUKAMATWA NA KUSEKWA NDANI WARATIBU WA 24 TASAF

$
0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Tv, Hai

MKUU wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Lengai Sabaya ameamuru kukamatwa na kuswekwa ndani waratibu wote wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa ngazi ya wilaya hiyo wapato 24.

Pia ameamua kuvunja Kamati zote za TASAF za ngazi ya vijiji mara baada ya kuruhusu kulipwa fedha za mfuko huo wa kaya masikini wakiwemo watu waliofariki dunia ,madiwani na wenyeviti wa Serikali kama kaya masikini .

Mkuu wa Wilaya Sabaya amefikia muamuzi huo baada ya fedha Sh.milioni 44.7 kupotea kwa mwezi kwa kupewa watu wasio na sifa wapatao 1,045 kati ya watu 3,887 kupata fedha za TASAF.

Amesema kiasi cha Sh.milioni 324 zimepotea kwa mwaka kwa kulipwa watu waliofariki dunia na mwengine kuwa na vitambulisho mara mbili jambo ambalo ni kinyume na utaratibu wa TASAF.

Amesema wapo wenyeviti wa vijiji pamoja na madiwani ambao wamekua wakipata fedha za msaada wa TASAF wakati sio masikini na wenye uhitaji wakikosa fedha za mfuko huo.

Awali akisoma ripoti ya TASAF iliyoandaliwa na Kamati Maalum iliyo undwa na Sabaya kufuatilia fedha zilizo tolewa kwa wananchi, Mwanasheria wa Wilaya ya Hai Engelberth Bonifas amesema baada ya kufanya uchunguzi wamebaini fedha kugaiwa kinyume katika kaya masikini.

Amesema kwa kutumia miongozo ya mfuko huo walibaini wapo watumishi wa Serikali waliojinufaisha na fedha za TASAF kinyume na utaratibu wa ugawaji wa fedha mfuko kwa kaya masikini.

Kamati hiyo imegundua zipo familia zinazopokea fedha hizo wakati wahusika walishafariki dunia na kuacha urithi kwa familia zao kuendelea kupokea fedha za mfuko huo kama wahusika.

Mmoja wa wananchi wa wilaya hiyo Farid Juma amemshukuru Mkuu wa Wilaya hiyo kwa uamuzi wake huo kwani wamekua wakifuatilia fedha za Tasaf kwa muda mrefu lakini wanazikosa huku wasio na sifa wakipewa.
Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro Lengai Sabaya akiongea na wananchi.

Upandikizaji vifaa vya usikivu Muhimbili wapunguza gharama ya kwenda nje kwa asilimia 60

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv.

 HOSPITALI ya Taifa ya Muhimbili (MNH) katika kipindi cha miaka miwili imesaidia kupunguza gharama kwa asilimia 60 ya wagonjwa waliokuwa wanapelekwa nje ya nchi kufanyiwa upasuaji wa kupandikiza vifaa vya masikio ili waweze kusikia vema.

Imeelezwa, tangu kuanzishwa kwa huduma ya kupandikiza vifaa vya kusikia nchini wagonjwa 30 wamefanyiwa upasuaji wa masikio ambao awali  ulikuwa unafanyika nchini India.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Julai 31, 2019 wakati wakiendelea na upasuaji wa kupandikiza kifaa cha kusikia katika sikio, Daktari bingwa wa magonjwa ya masikio, pua na koo katika Hospitali ya MNH, Edwin Liyombo amesema. Upasuaji huo unaofanyika hapa nchini umeweza kupunguza gharama kubwa kwa serikali na wananchi ambao walikuwa wakilazimika kwenda nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.

"Kuanzia mwaka 2012 hadi 2016 serikali ilipeleka wagonjwa zaidi ya 50 katika hospitali mbalimbali za nchini India kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji hivyo utaona sasa gharama hizo zimepungua," amesema Dk Liyombo.

Amesema zoezi lote la upasuaji linafanywa na madakatari bingwa wa Muhimbuli kwa kushirikiana na mtaalamu kutoka Misri.Ameeleza kuwa asilimia 80 hadi 90 za upasuaji zinazofanyika zinafanywa na wataalamu kutoka hospitalini hapo.

Ameongeza kuwa, huduma hiyo inatolewa kwa yule ambaye amefanyiwa vipimo na kubainika hana uwezo wa kusikia na kumpandikiza kifaa hicho ambacho kinagharamu Sh. Milioni 35.

“Kuna kifaa cha kusaidia kusikia cha kuvaa na kuna kifaa kingine cha kusaidia kusikia kwa njia ya upandikizaji ambacho kinawekwa kwa njia ya upasuaji hicho ndio tunakifanya leo kupandikiza kifaa cha kumuwezesha mtu ambae hana uwezo wa kusikia kabisa, aweze kusikia kama mtu wa kawaida amesema Dk. liyombo.

Amesema tatizo hilo likimpata mtoto mwenye umri mdogo ina maana anashindwa kuongea na ndio maana programu yao imeangalia watoto zaidi waliopo chini ya umri wa miaka sita kuliko watu wazima.

“Lengo letu ni kuwaokoa watoto wadogo ambao wanazaliwa na matatizo ya kusikia kwani hushindwa kujifunza kuongea, hivyo ukimuacha kama alivyyo atakwenda kwenye shule za viziwi endapo ukimuwahi akawekewa mashine ataishi maisha ya kawaida na kusikia,” alisema.

Dk. Liyombo ameema tangu mwaka 2012 serikali ilikuwa inapeleka watoto kwenda kutibiwa nje ya nchi kwa sababu hapakuwa na utaalamu huo nchini.
Alisema utaalamu huo ni wa hali ya juu na matibabu yake ni ya gharama kubwa tangu mwaka 2012 hadi 2016 jumla ya watoto 50 wametibiwa katika hospitali mbalimbali nchini India.

Alisema kumekuwa na changamoto mbalimbali kwani mzazi anapokwenda na mwanae hukaa sio chini ya miezi mitatu kusubiria matibabu na gharama zake zilikuwa ni kubwa kati ya Sh milioni 60 hadi 100 kwa familia moja.

“Vile vile akienda huko nje ya nchi haendi mara moja anatakiwa kurudi kama mara mbili au tatu mpaka mgonjwa awe ameimarika,” alisema Dk. Liyombo.Aidha, alisema serikali ilifanya utafiti na kuona kwa nini wasitoe huduma hiyo wakawezeshwa kuanzisha huduma hiyo ya upasuaji mwaka 2017.

“Hii ni mara ya nne tunafanya na mpaka sasa hivi mgonjwa wa 24 ndio anafanyiwa upasuaji zoezi hili likimalizika wiki hii tutakuwa tumewafanyia jumla ya wagonjwa 30,”Aliongezea kuwa:”Mwaka 2012 hadi 2016 walifanyiwa wagonjwa 50 sisi mwaka 2017  hadi sasa tumewafanyia wagonjwa 30 hivyo ni zaidi ya asilimia 60 ya wagonjwa hao ambao walipelekwa nje ya nchi tumejitahidi kufanikiwa katika hilo,”

Amesema, pia wanatarajia kumfanyia mtu mzima mmoja upasuaji huo mbaye alikuwa anatumia dawa za ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) zilimsababishia madhara na kumfanya ashindwe kusikia chochote na hivyo, watamuwekea kifaa kitakachomsaidia kusikia vizuri.

Alisema kwa upande wa watoto watawawekea kifaa hicho na kuwapa miezi sita kwa ajili ya kuwafundisha kuongea
DAKTARI Bingwa wa Magonjwa ya Pua, Masikio na Koo kutoka Misri, Profesa. Lobna El Fiky (kulia) akisaidiana na Daktari Bingwa wa magonjwa hayo kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk.Aveline Aloyce (kushoto) wakimfanyia upasuaji wa kupandikiza vifaa vya kusaidia kusikia mmoja wa watoto wenye matatizo ya kutokusikia katika hospitali ya MNH Dar es Salaam leo.
Daktari bingwa wa magonjwa ya masikio,pua na Koo Na mkuu wa idara wa magonjwa ya masikio ,pua na Koo wa Hospital ya Taifa Muhimbili, Dk. Edwin liyombo akifafanua kwa waandishi wa habari, namna upasuaji wa kupandikiza kifaa cha kusikia unavyofanyika ambao unafanywa na madaktari wa Muhimbili kwa Kushirikiana na mtaalamu kutoka Misri.

HAYA NDIO MAAJABU YA MCHEZO WA KUOGELEA, SIRI ILIYO JIFICHA KATIKA TIBA...

SERIKALI YANUNUA MAGARI 12 YA HUDUMA YA DHARURA NA UOKOZI

$
0
0
Mkuu wa kitengo cha afya uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl.Julius Nyerere George Ndaki akimuonesha ufanyaji kazi wa mashine za kupima joto(thermo scanner) Naibu Waziri Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile wakati alipotembelea eneo la wasafiri wanaoenda nje ya nchi zilizofungwa kwenye uwanja mpya wa ndege terminal three.
Naibu Waziri Dkt.Faustine Ndugulile akionesha kadi za homa ya manjano”Yelow Fever” ambazo zinatolewa na wizara ambapo wizara imefunga kifaa maalum cha kubaini kadi feki ambazo wasafiri huzinunua bila kuchanjwa chanjo hiyo.
Dkt.Ndugulile akioneshwa utofauti wa kadi halisi na kadi feki za homa ya manjano.Dkt.Ndugulile amewasihi wananchi wanaotarajia kusafiri nje ya nchi kuacha kununua kadi feki bali kuhakikisha wanapata chanjo hiyo kwenye vituo rasmi vilivyoelekezwa na wizara ya Afya.
Naibu Waziri akikagua vifaa vingine vilivyofungwa terminal three kwa ajili ya kubaini wahisiwa wa Ebola.
Katika kuelekea Mkutano wa Kimataifa wa SADC wizara ya afya imejipanga kukabiliana na dharura kwa wageni watakaoshiriki mkutano huo.Pichani.Dkt.Ndugulile akikagua magari ya wagonjwa wa dharura yaliyopo ofisi za Toyota.
Naibu Waziri akikagua moja ya chumba cha dharura kilichoandaliwa kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya washiriki wa mkutano wa SADC.
Mkuu wa Kitengo cha Dharura Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt.Juma Mfinanga (kulia)akimueleza jambo Naibu Waziri wakati alipotembelea kujionea hali ya utayari ya kuwahudumia washiriki wa mkutano wa SADC ambao watapata dharura na hivyo kupatiwa huduma za afya kwenye hospitali hiyo.

************

NA.Catherine Sungura,WAMJW-DSM

Serikali kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imenunua magari kumi na mbili kwa ajili ya huduma za dharura nchini.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa wizara hiyo Dkt.Faustine Ndugulile wakati alipofanya ukaguzi kwenye ofisi za Toyota jijini hapa.

Dkt.Ndugulile amesema magari hayo yameletwa muda muafa ikiwa zimesalia siku chache kuanza mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo kwa Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) ambapo magari hayo pamoja na mabasi mawili ya uokozi yatatumika kutoa huduma za kiafya kwenye mkutano huo na baada ya hapo yatagaiwa kwenye maeneo yaliyoanishwa kwa uokoaji wa majeruhi wa ajali.

“Magari na Mabasi hayo yatatumika kwenye mkutano wa SADC na baadae yatasambazwa katika vituo vya dharura nje ya hospitali ambapo yatatumika kusafirishia majeruhi pindi ajali inapokuwa imetoka.

“Tutayatumia katika mkutano wa SADC, pamoja na ambulance hizo 12 kuna mabasi makubwa mawili ambayo yana huduma zote za msingi ndani ambapo watu wapatao 20 wanaweza kubebwa na kupatiwa msaada wa ajali,” alisema.

Alisema serikali imejipanga pia katika njia ya anga kwa kutumia ndege pindi mtu anapohitaji huduma ya dharura kupelekwa haraka katika eneo jingine hususani hospitali ya Taifa Muhimbili.

“Ni utaratibu ambao Serikali inauweka kuhakikisha waathirika wa ajali wanapata huduma za dharura na ajali, mapema iwezekano na tunasema ndani ya masaa yaliyowekwa ya kuwahudumia majeruhi,” alisema Dkt.Ndugulile

Naibu Waziri huyo alisema wameagiza magari ya zimamoto na uokozi kwamba si tu liwe na uwezo wa kuzima moto bali linakuwa na vifaa vya kisasa, kwa mfano ikiwa gari limepata ajali, milango inashindwa kufunguka, iweze kukatwa ili kuokoa majeruhi, iwezekane.

“Haya ni maendeleo makubwa kwa Serikali katika kuhakikisha majeruhi wanapata huduma za dharura za awali mapema inavyowezekana, kwani wengi hufariki dunia kwa sababu hukosa zile huduma za awali za dharura katika lile li-saa limoja la kwanza,” alisema.

Dk. Ndugulile aliongeza “Inawezekana anavuja damu, anashindwa kupumua vizuri, tuna imani magari, mabasi na mafunzo tuliyowapa wataalamu huduma hizi zitaimarika.

“Natoa rai kwa wananchi, kwani nao wamekuwa wakichangia madhara kwa majeruhi, wanawamalizia wale majeruhi, wakiamini wanawasaidia kuokoa maisha.

“Wahakikishe tu wanamtoa majeruhi na kumuweka pahala pengine mbali na tukio la ajali, kama gari litaweza kulipuka moto ule usimfikie, tunapowabeba ‘mzobe mzobe’ tunawasababishia madhara zaidi.

“Muhimu tuhakikishe huduma za msingi zinapatikana pale pale, kikubwa ni kuhakikisha yule Mgonjwa anapumua, havuji Damu kwa wingi na njia yake ya Hewa IPO salama.

“Jambo la msingi si kumkimbiza majeruhi hospitalini kwanza bali ‘kum-stablize’ pale pale eneo la tukio, kama mfupa umevunjika afunge vizuri usining’ingine, abebwe vizuri kama mshipa wa shingo umevunjika usimalizike, kwani wengi kutokana na ule ubebaji huishia kupooza mwili na hata kufa,” alisema.

Sambamba na hilo, mapema asubuhi, Dk. Ndugulile alifanya ziara kwenye kitengo cha afya ndani ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA- terminal III), kujionea hali ya utayari wa kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo Ebola.

Wataalam wa viwango Afrika wakutana Dar

$
0
0
WATAALAM wa suala ya viwango kutoka nchi 31 za Afrika wamekutana jijini Dar es Salaam kujadili na kuainisha viwango vya maji safi na taka, kwa lengo la kupitisha kiwango kimoja kitakachotumika kwa nchi zote za Afrika.

Akizungumza Dar es Salaam jana (JUMANNE) Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt. Yusuf Ngenya, alisema mkutano huo umekutanisha wataalam kutoka nchi wanachama wa Shirika la Viwango la Afrika (ARSO).

Kwa mujibu wa Dkt. Ngenya nchi hizo zipo katika hatua za kutengeneza kiwango kimoja kitakachotumika katika upande wa maji safi na uchakataji wa maji taka.

Alisema kuna njia na hatua nyingi za kutengeneza kiwango kimoja, ikiwemo uainishaji viwango vyote na kupata kiwango kimoja kitakachotumika .

“Kila nchi ina viwango vyake vya ubora, lakini katika mkutano huu wa leo (juzi) umekutanisha wadau wote wanachama wa ARSO ili kuhakikisha tunapata kiwango kimoja kitakachotumika katika maji safi na taka kwa nchi zote za Afrika,”alisema Dkt. Ngenya.

Dkt Ngenya alisema kuna faida kubwa kwa nchi za Afrika kutumia kiwango kimoja, hususan kwa upande wa wafanyabiashara wa hapa nchini wanapopeleka biashara zao kwenye nchi nyingine za Afrika zikiwa na nembo za TBS, kwani hawezi kupata usumbufu wowote.

“Ili kuendana vizuri katika biashara na kuondoa vikwazo mbalimbali kwa wafanyabiashara inabidi viwango hivyo vifanyiwe uainishaji na kuwa na kiwango kimoja kitakachokubalika sehemu zote,”alifafanua Dkt. Ngenya. 

Aidha, alisema kwa upande wa maji taka kutakuwepo na kiwango kimoja ya kuyachakata ili yaweze kutumika tena kufanyiwa shughuli nyingine.Kwa Upande Katibu Mtendaji wa Shirika la Maji Afrika (AMCOW) Dkt.Canisius Kanangire, alisema kuna umuhimu wa kuwepo kwa kiwango kimoja cha ubora kwa maji safi na uchakataji wa maji taka kwa nchi za Afrika.

Alisema kuwepo kwa kiwango kimoja kutasaidia kutambua maji safi na kuhakikisha yanakuwa na ubora mzuri wa kuzuia magonjwa mbalimbali kwa binadamu.

“Kuna umuhimu wa kuwa maji yaliyobora kwani watu wanakufa kwa sababu ya kunywa maji yasiokuwa salama au kuyatumia katika matumizi mbalimbali ikiwemo majumbani na viwandani,”alisema Kanangire.

Naye Meneja wa Habari na Vielelezo wa ARSO, Philip Anyango, alisema maisha ya watu ni muhimu kuliko kitu chochote , hivyo suala la maji na salama haliepukiki. Alisema katika Malengo ya Maendeleo Endelevu suala la maji ni lengo la sita, hivyo uwepo wa maji safi na salama kwa watu ni muhimu kwa afya zao.

WAZIRI MKUU AKAGUA MAANDALIZI TERMINAL III

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kizungumza na Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Wilson Kantambula (kulia) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Damas Ndumbaro (kushoto) wakati alipokagua maadalizi ya mapokezi ya wajumbe wa mkutano wa SADC kwenye jengo la pili na la tatu katika kiwanja cha ndege cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Julai 31, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na baadhi ya viongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano pamoja na viongozi wa Mkoa wa Dar es salaam wakati alipokagua maandalizi ya mapokezi kwa wajumbe wa mkutano wa SADC kwenye Jengo la pili na la tatu la abaria katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Julai 31, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua maandalizi ya mapokezi ya wajumbe wa mkutano wa SADC kwenye jengo la pili na la tatu la abaria katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Julai 31, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

***********

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua jengo la tatu la abiria kwenye kiwanja cha ndege cha Mwalimu Nyerere ili kuona maandilizi ya mapokezi kwa wajumbe wa mkutano wa SADC.

Akizungumza na watendaji wa Serikali pamoja na Kamati ya maandalizi uwanjani hapo leo jioni (Jumatano, Julai 31, 2019), Waziri Mkuu amesema maandalizi ni mazuri isipokuwa kwa kasoro chache zilizobakia.

“Nimepita VIP hakuna shida. Pale terminal 2, sehemu ya Uhamiaji iko vizuri, uchunguzi wa afya nayo iko vizuri, lakini vyoo inabidi vibadilishwe haraka sana. Vile vyoo pale nje vimechoka, vibadilishwe mara moja, siyo tu kwa ajili ya ugeni, bali ni kwa faida yetu pia,” amesema huku akimwagiza meneja wa uwanja huo, Bw. Paul Lugasha aharakishe zoezi hilo.

Katika jengo la tatu la abiria kwenye uwanja huo, Waziri Mkuu amekagua eneo ambalo viongozi wakuu wa nchi watashukia, watakagua gwaride la heshima na kuangalia vikundi vya ngoma. Pia amekagua vyumba ambavyo watapumzikia kabla ya kuelekea mjini.

Amesisitiza kuwa usafi wa barabarani bado hauridhishi sababu kuna mawe, udongo na michanga kwenye barabara kuu ya kutoka uwanja wa ndege hadi mjini. “Tulikubaliana kuwa zile bustani ziboreshwe, vyuma vya barabarani vitengenezwe lakini hata leo nimepita kwenye fly-over, bado kuna mawe na michanga, hata sijui vinatokea wapi,” alisema.

Amewataka wahusika waweke banners za kutosha za aina mbalimbali na picha za wanyama kutani, uwanjani hapo ili kuonesha kwamba kuna mkutano mkubwa unafanyika hapa nchini.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amewataka Watanzania watumie fursa ya uwepo wa mkutano huo mkubwa kuendesha biashara zao na ujasiriamali.

“Ziko fursa nyingi za uwepo wa mkutano huu. Kila mmoja atumie nafasi hii kuweza kuongeza na kuboresha kazi yake inayomletea uchumi,” amesema.

MWAKYEMBE ASIKITISHWA NA HALI YA JELLAH MTAGWA

$
0
0

Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe amemtembelea na kumuona mchezaji wa zamani wa timu ya mpira wa miguu ya  Yanga na Taifa Stars Jellah Mtagwa anayeumwa kwa kipindi kirefu.

Dkt Mwakyembe amesikitishwa sana na hali aliyomkuta nayo mchezaji huyo aliyeipa mafanikio timu ya Taifa.

Akizungumza nae, Dkt Mwakyembe amesema wamepata taarifa kupitia vyombo vya habari na kutambua kuwa wao kama serikali na Shirikisho wana wajibu wa kufanya jambo kwa ajili ya mchezaji huyo.

Amesema, hali ya Mtagwa si nzuri kwani anaumwa, ana changamoto anapokaa kwani mazingira ya nyumba sio rafiki kutokana na hali yake ambapo anatakiwa kupelekwa hospitali kwa ajili ya mazoezi ya viungo (physiotherapy).

Dkt Mwakyembe amesema, pia hali ya maisha sio nzuri kwani kwa sasa hafanyi kazi yotote na imefikia hatua mama(mkewe) aache kazi kwa ajili ya kumuuguza.

"Kuna kila sababu Jellah Mtagwa kusaidiwa, nitakaa na Shirika la Posta kumsaidia kwani aliweza kulibeba kwa kuuza stamp zake kwa muda mrefu pamoja na TFF ambao aliweza kuuhudumia mpira kwa ngazi mbalimbali ikiwemo Timu ya Taifa,"amesema Dkt Mwakyembe.

Aidha, Ameeleza kuwa atafikisha pia suala hilo kwa viongozi wengine wa nchi kwa ajili ya msaada na atarejea tena kwa ajili ya kuwaona pamoja na kuwapa mrejesho kwani kwa sasa Mtagwa anahitaji dawa, anahitaji gari kwa ajili ya kumpeleka hospitali na kurudi na mahali anapokaa si pazuri.

Mtagwa akiongea, amemshukuru Waziri Mwakyembe kwa kwenda kumtembelea kwani hakuna kiongozi yoyote aliyewahi kuja kumtembelea toka aanze kuumwa.

Ameongezea kuwa, ana changamoto mbalimbali ila kikubwa ni makazi na usafiri ambavyo angeweza kuvipata angeshukuru sana.
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe akizunguma na mchezaji wa zamani Jellah Mtagwa baada ya kumtembelea na kumjulia hali yake nyumbani kwake akiugua kwa muda mrefu.
Mchezaji wa zamani Jellah Mtagwa akizungumzia kutembelewa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe na kumshukuru na kumuelezea changamoto anazokutana nazo.

WALIMU SHULE ZA SEKONDARI WATOA USHAURI KWA WADHIBITI UBORA WA ELIMU NCHINI

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv.

WALIMU wa Shule za Sekondari nchini wameshauri wadhibiti wa ubora wa elimu kupokea nyaraka zilizoandaliwa kwa njia ya teknolojia badala ya zile zilizomo kwenye vitabu kwani ni rahisi kuchakaa.

Pia walimu hao, wameiomba serikali iwaruhusu wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi kutumia simu na vikokotoo wanapokuwa wanafundishwa na kwenye mitihani ili waweze kutunza kumbukumbu kwa muda mrefu bila ya kuchakaa.

Wakizungumza kwenye warsha iliyoandaliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Watu (HDIF) kupitia Taasisi ya Shule Direct katika maonesho ya Wanasayansi Chipukizi, iliyofanyika leo Julai 31, 2019, walisema sababu inayochangia wanafunzi wengi kutopenda masomo ya sayansi ni sera zilizopo ambazo zinakataza mwanafunzi kutumia kikokotoo awapo shuleni.

Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Azania, Thelesphory Sylvester amesema wanauwezo wa kupata huduma za teknolojia shuleni na pia huandaa nyaraka mbalimbali lakini wadhibiti ubora wa elimu wanapofanya mapitio huko mashuleni hutaka nyaraka zilizo kwenye makaratasi.

"Uwepo wa teknolojia lengo lake ni kurahisisha utendaji wa kazi hivyo wanapaswa kupewa elimu ya kutumia teknolojia ipasavyo na kuachana na matumizi ya makaratasi ambayo huweza kuharibika haraka.

Ameongeza kuwa, ili kuhamasisha wanafunzi kusoma masomo ya sayansi ni lazima kuwepo mazingira mazuri ya masomo iiwemo upatikanaji wa teknolojia na kuruhusu matumizi ya simu na vikokotoo.

"Kwanini tuhamasishe matumizi ya teknolojia ya kompyuta wakati bado nyaraka zinazotakiwa ni za makaratasi..tunaomba muendelee kuwaelimisha wadhibiti kutumia teknolojia pia katika mapitio yao," amesema Mwalimu Sylvester.

Kwa upande wake, mwalimu, aliyejitambulisha kwa jina moja tu la Mathias amesema teknolojia ni nzuri kutumika mashuleni kwani huwasaidia wanafunzi kujikumbushia masomo mbalimbali ikizingatiwa kuwa, kuna changamoto mbali mbali hasa katika masomo ya sayansi ambayo yana maneno magumu ambayo ili mwanafunzi aweze kuelewa anapaswa kueleweshwa kwa lugha rahisi.

"Tumekuwa tukiwakaririsha wanafunzi katika masomo ya sayansi lakini kama teknolojia ikitumika hadi mashuleni inaweza kuleta mapinduzi kwa mwanafunzi kupata picha halisi ya kile anachojifunza", amesema.

Naye, Mtengeneza Tovuti kutoka Shule Direct , Rajabu Mgeni amewaeleza walimu kuwa wanayo fursa ya kuwasaidia wanafunzi wao kwa kuandaa masomo kwa kuyatuma kwenye mtandao ambapo wao kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) wamekuwa wakipitia masomo mbalimbali yanayoandaliwa na walimu nchini kwa ajili ya kutumika na wanafunzi.

Amesema, taasisi yao inatoa mafunzo kidigitali kwa kufuata kanuni za maendeleo ya kidijiti na kwamba mwalimu anahitaji kusaidia idadi kubwa ya wanafunzi hivyo wanapaswa watumie mfumo huo kwani una uwezo wa kufikia walimu na wanafunzi zaidi ya M 1.5

Aidha amezitaja kanuni za maendeleo ya kidijiti kuwa ni kuelewa mfumo wa ekolojia uliopo, kuandaa pamoja na mtumiaji, kushirikiana, ubunifu unaolenga ukuaji, kusukumwa na takwimu, usiri na usalama.
Kamati ya Maandalizi ya Wanasayansi Chipukizi wakijiandaa kufanya maonesho ya bunifu mbalimbali zilizofanywa na wanafunzi katika warsha iliyoandaliwa na Mfuko wa maendeleo ya Watu (HDIF) kupitia Taasisi ya Shule Direct jijini Dar es Salaa
Wanafunzi kutoka mikoa mbalimbali wa shule za sekondari nchini wakiwa kwenye maonesho ya Wanasayansi Chipukizi yaliyofanyika leo Julai 31,2019 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkazi wa Mfuko wa Maendeleo ya Watu (HDIF) Joseph Manirakiza akipiga picha moja ya machapisho yaliyowasilishwa na Wanasayansi Chipukizi leo katika warsha iliyoandaliwa na Mfuko wa maendeleo ya Watu (HDIF) kupitia Taasisi ya Shule Direct jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi walioshiriki maonesho ya Wanasayansi Chipukizi wakitoa maelekezo juu ya bunifu zao kwa mkurugenzi wa HDIF Joseph Manirakiza na pembeni yao ni Mtaalamu wa Mawasiliano wa HDIF Hannah Mwandoloma.

DAWASA KUZIMA MTAMBO WA RUVU JUU NA RUVU CHINI KWA SAA 24 KUPISHA MATENGENEZO YA DHARURA.

TANZANIA NA ZIMBABWE ZATIA SAINI MIKATABA MITANO YA USHIRIKIANO

$
0
0
 Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli (kulia) na Rais wa Zimbabwe Mhe. Komredi Emmerson Mnangagwa 

Tanzania na Zimbabwe zimetiliana saini hati tano za makubaliano ya ushirikiano katika nyanja mbalimbali ikiwa ni kutekeleza maelekezo ya Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na Rais wa Zimbabwe Mhe. Komredi Emmerson Mnangagwa ya kuhakikisha nchi hizo zinashirikiana katika masuala ya kiuchumi ili kuleta maendeleo kwa wananchi wa nchi hizo.

Hati hizo za makubaliano zimesainiwa Harare Nchini Zimbabwe na Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi kwa upande wa Tanzania na Waziri wa Mambo ya Nje na biashara ya kimataifa wa Zimbabwe Luten Jenerali Mstaafu Sibusiso Moyo.

Akizungumza mara baada ya kusaini hati hizo za makubaliano waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. palamagamba Kabudi amesema mkutano huo unafanyika kwa mara ya kwanza baada ya miaka 21 na kuongeza kuwa uhusiano baina ya Tanzania na Zimbabwe ulianza kabla ya ukoloni na kuimarika zaidi wakati wa kupigania ukombozi na sasa ni wakati muafaka kwa nchi hizo kuanza mapambano mapya ya kiuchumi.

Makubaliano hayo yamefikiwa katika nyanja za ushirikiano wa biashara,uchumi na uwekezaji, siasa na diplomasia,utalii,uwezeshaji wa wanawake na masuala ya jinsia pamoja na masuala ya ujasiriamali mdogo na wa kati.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na biashara ya Kimataifa Luten Jenerali Mstaafu Sibusiso Moyo ameshukuru kwa mkutano huo kufanyika baada ya kupita miaka mingi na kusisitiza kuwa jukumu lililosalia ni kuhakikisha utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa yanafnyika kwa kasi kubwa ili kuleta maendeleo kwa wananchi wan chi hizo mbili.

Ametaka ushirikiano baina ya nchi hizo hususani katika nyanja ya uchumi usiachwe ukadorora kwa muda mrefu kama ilivyotokea katika kipindi kilichopita kwani kwa sasa maendeleo ni biashara na ushirikiano baina ya nchi na nchi.

HAFLA YA UPOKEAJI MELI YA MV UMOJA ILIYOBEBA MABEHEWA YA TRENI KUTOKA MWANZA KWENDA UGANDA

$
0
0

Pichani chini ni Matukio ya picha mbalimbali zilizopigwa katika Bandari ya Port Bell (Kampala) nchini Uganda,kwenye Hafla ya upokeaji wa Meli ya mizigo MV Umoja iliyobeba mabehewa ya treni kutoka Mwanza kuja Uganda ikiwa na mizigo ya World Food Programme. (WFP).

Katika Hafla hiyo Serikali ya Uganda iliwasilishwa na Waziri wa Nchi Uchukuzi General Katumba Wamala na kwa Upande wa Tanzania, Balozi wa Tanzania nchini Uganda alimwakilisha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi  Isack Aloyce Kamwelwe.

Njia hii ya usafiri wa reli kutoka Dar Es Salaam hadi Port Bell (Kampala) Uganda, inapunguza gharama kwa asilimia zaidi ya 50 na pia inachukuwa siku 5 tu kwa mzigo kusafiri kutoka bandari ya Dar Es Salaam hadi Kampala.

Kwa mwaka jana WFP walisafirisha tani 40,000 na kwa kutumia njia hii wameokoa zaidi ya USD 2M.Ujumbe uluiosafiri na MV Umoja kuja na mabehewa yanye mizigo ya WFP walikuwepo

Mkurugenzi Mtendaji wa TRC Bwana Masanja Kadogosa, Eng Johnson Kisaka Mkurugenzi wa Uchukuzi kutoka katika Wizara na pia waliambatana na Bwana Michael Dunforf Mkurugenzi wa WFP nchini Tanzania.

Kwa upande wa Uganda timu ya WFP Uganda walikuwepo katika mapokezi ya meli na shehena ya mizigo wakiongozwa na Naibu Mkurugenzi Bi Julie Anne MacDonald.Hii ni njia nafuu na yenye tija katika kukuza biashara na matumizi ya bandari ya Dar Es Salaam na reli ya kati ambayo ni muhimu wafanyabiashara kati ya Tanzania na Uganda wanatakiwa kuichangamkia.

 Dkt Aziz P. Mlima, Balozi wa Tanzania nchini Uganda akisoma Hotuba kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isack Aloyce Kamwelwe.
 Kutoka Kushoto kwenda Kulia Bwana Michael Dunford ( WFP- Tanzania)  Dr. Aziz P. Mlima ( Balozi wa Tanzania Uganda) na Bi Julie Anne MacDonald.
Mhandisi  Johnson Kisaka akisalimiana na Gen Karumba Wamala.

TRA YAKUSANYA TRILIONI 15.9 KWA MWAKA WA FEDHA 2018/19

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imekusanya Sh. trilioni 15.9 kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ,kuanzia Julai Mosi mwaka 2018 hadi Juni 30,2019  kati ya lengo la Sh. trilioni 18.

Hayo yamesemwa leo Julai 31,2019  jijini Dar es Salaam na  Kaimu Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo wakati akitoa taarifa ya makusanyo ya kodi kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2018/2019.

Amesema katika robo ya nne ya mwaka huo wa fedha (Machi hadi Juni 2019), TRA ilikusanya Sh trilioni 1.1, Sh trilioni 1.2 na Sh trilioni 1.5 kwa mwezi Aprili, Mei na June.

Kayomb amesema katika mwaka huo wa fedha, Serikali ilianzisha mfumo wa stempu za Kodi za Kieletroniki (ETS) ambapo utekelezaji wake umefanyika kwa awamu mbili.

"Awamu ya kwanza, ilihusisha bidhaa za sigara, mvinyo, pombe kali, bia na Ain's zote za vileo, ambayo ilianza kutekelezwa Januari 15,2019 imeendelea vizuri na maandaalizi ya awamu ya pili ya utekelezaji wa ETS inayojumuisha bidhaa za vinywaji baridi, maji, juisi na bidhaa za filamu kama CD/DVDs," amesema Kayombo

Kayombo amesema mfumo huo wa ETS kwa awamu  ya pili unatarajiwa kuanza kufanya  kazi Agosti Mosi, 2019, kwa lengo la kukusanya kodi stahiki.

"Lengo Kuu la kubandika stempu hizi za kieletroniki ni kuongeza usimamizi na ufanisi wa ukusanyaji wa ushuru wa bidhaa ikiwa  ni pamoja na kupata taarifa sahihi za uzalishaji viwandani ili kukusanya kodi stahiki,

" Ni matumaini ya TRA, wazalishaji, waingizaji, wasambazaji, wauzaji wote wa bidhaa zinazotozwa ushuru wa bidhaa pamoja na umma wataendela kutoa ushirikiano wa TRA ili kufanikisha utekelezaji wa mfumo huu kila mmoja kutimiza majibu wake kwa majibu wa sheria, kanuni na taratibu zilizopo,"amesema 

Barabara ya Njombe-Makete km 107,4 kukamilika mwakani.

$
0
0
Muonekano wa barabara ya Moronga - Makete km 53.5 ambayo ni sehemu ya barabara ya Njombe - Ndulamo-Makete km 107.4 inayojengwa kwa kiwango cha lami mkoani Njombe.
Mkandarasi China Railway Seventh Group Co. Ltd (CRSG), akiendelea na kazi ya kuweka lami katika barabara ya Moronga - Makete km 53.5 ambayo ni sehemu ya barabara ya Njombe - Ndulamo-Makete km 107.4 
Mkandarasi China Railway Seventh Group Co. Ltd (CRSG), akiendelea na kazi ya kuweka lami katika barabara ya Moronga - Makete km 53.5 ambayo ni sehemu ya barabara ya Njombe - Ndulamo-Makete km 107.4 
Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Mkoa wa Njombe Mhandisi Yusufu Mazana akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa alipokagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Moronga- Makete km 53.5 inayojengwa kwa kiwango cha lami.


Muonekano wa box calvat linalojengwa katika barabara ya Moronga - Makete km 53.5 ambayo ni sehemu ya barabara ya Njombe - Ndulamo-Makete km 107.4 inayojengwa kwa kiwango cha lami mkoani Njombe.
Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe Bw, Ali Kassinge akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa alipokagua ujenzi wa barabara ya Moronga - Makete km 53.5 inayojengwa kwa kiwango cha lami.
Muonekano wa nyumba ya Mwalimu wa Chuo cha Ufundi Stadi VETA Wilayani Makete zinazojengwa na Wakala wa Majengo nchini (TBA), mkoani Njombe
Muonekano wa bweni la wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi VETA Wilayani Makete linalojengwa na Wakala wa Majengo nchini (TBA), mkoani Njombe. 

Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Julai 31,2019. 

MADEREVA WATAKAOWABEBA VIONGOZI WA SADC WAPIGWA MSASA

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV 

MADEREVA watakaobeba viongozi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Umoja wa nchi zilizo Kusini Mwa Afrika (SADC) wameaswa kuwa na weledi wakati kuwaendesha viongozi hao.

Hayo ameyasema Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Amani wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Ushirikiano wa Kimataifa na Kikanda Stephen Mbundi wakati akifunga mafunzo kwa madereva watakaosafirisha viongozi wa SADC yaliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) jijini Dar es Salaam.

Mbundi amesema mkutano huo ni wa kimataifa Dunia nzima inaangalia hivyo kama nchi haitaki aibu yeyote katika ujio wa viongozi hao ikiwa ni pamoja na kuwa na lugha nzuri katika mawasiliano.

Amesema nchi imewapa heshima madereva katika mkutano huo na kuandika historia kwa nchi katika utoaji wa huduma ya kuwasafirisha na kuongeza kuwa masilahi yao yatalindwa.

Mratibu wa Mafunzo hayo ni Mkaguzi Msaidizi Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Ibrahim Samwix .

Nae Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT)Profesa Zakaria Mganilwa amesema kuwa mafunzo hayo ni faida kwa madereva katika mkutano wa SADC.

Amesema kuwa madereva waliopata mafunzo wa uzoefu kilichofanyika ni kuwaongezea maarifa namna kuwa na weledi katika kuwaendesha viongozi wa SADC.
Sehemu ya Madereva waliopata mafunzo kwa ajili kuwabeba viongozi wa SADC.
 Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Amani wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Ushirikiano wa Kimataifa na  Kikanda Stephen Mbundi akimkabdhi cheti mafunzo mmoja  wa Madereva watakaobeba viongozi wa Mkutano wa SADC  George Mkwakwa yaliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT)jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Profesa  Zakaria Mganilwa akitoa maelezo wakati wa kufunga mafunzo ya Madereva watakaobeba viongozi wa Mkutano wa SADC   yaliyoendeshwa katika Chuo hicho jijini Dar es Salaam.
 Mwakilishi wa Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani Deus Sokoni akitoa maelezo kuhusiana na usalama wakati kuendesha viongozi wa Mkutano wa SADC wakati wa mafunzo ya madereva yaliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT)jijini Dar es Salaam.
 .Mratibu wa Mafunzo hayo ni Mkaguzi Msaidizi Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Ibrahim Samwix  akiwasikiliza maelezo ya viongozi katika kamati ya usafiri kw viongozi wa SADC.
 Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na madereva na baadhi ya watendaji mara baada ya kufunga mafunzo kwa madereva.
 Picha ya pamoja ya Mgeni rasmi na  watendaji.


ASASI ZA KIRAIA ZAKUTANA DAR KUPATA MREJESHO WA JUKWAA LA KISIASA LA HALI YA JUU LA MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU

$
0
0
Na Said Mwishehe,Michuzi TV

WADAU wa maendeleo kutoka asasi za kiraia zipatazo 28 nchini Tanzania wamekutana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupata mrejesho wa wenzao wapatao 20 waliokwenda nchini Marekani kushiriki mkutano wa Jukwaa la Kisiasa la hali ya juu la malengo ya maendeleo endelevu.

Kupitia jukwaa hilo asasi hizo zimepata nafasi ya kuwasilisha ripoti yao kuhusu malengo ya maendeleo endelevu huku wakieleza kufurahishwa na hatua ya Serikali ya Tanzania kuahidi kusimamia na kutekeleza malengo yote 17 yaliyoko kwenye mkakati wa maendeleo endelevu.

Akizungumza na Michuzi TV pamoja na Michuzi Blog leo Julai 31 jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Forumcc Angela Damas amesema jumla ya ujumbe wa watu 20 walikwenda nchini Marekani katika jukwaa hilo kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo endelevu.

"Leo hii tumekutana hapa kwa ajili ya kupata mrejesho kutoka kwa wenzetu waliotuwakilisha Marekani katika Jukwaa la Kisiasa la Hali ya Juu la Maendeleo Endelevu ambalo limefanyika kwa wiki mbili.

"Katika mkutano huo nchi yetu nayo imepata nafasi ya kuwasilisha ripoti yake ya namna ambavyo inatekeleza malengo ya maendeleo endelevu.Kwetu ni faraja kuona nchi inawasilisha ripoti lakini wakati huo huo asasi za kijamii nazo zimepata nafasi hiyo na kwa pamoja tunaamini tutasonga mbele,"amesema Damas.

Pia amesema watatumia nafasi hiyo kuangali ni kwa namna gani asasi za kiraia zinaweza kushiriki kikamilifu kuhakikisha malengo ya maendeleo endelevu yanafanikiwa.

Ameongeza wao ni mara kwa kwanza kushiriki na ripoti iliyowasilishwa ilihusu malengo sita tu kati ya malengo 17 yaliyowekwa na kufafanua kila baada ya miaka mitatu kunakuwa na kikao cha kuwasilisha ripoti.
Alipoulizwa iwapo malengo hayo yamefanikiwa , amejibu ni ngumu kupima kwa haraka na kueleza kama kuna mafanikio au laa lakini kikubwa kuna hatua nzuri ambazo zinaonekana, hivyo ni kuunganisha nguvu ya pamoja.

"Hivyo hakuna jibu la moja kwa moja, binafsi naweza kueleza hata ripoti hii iliyowasilishwa inatoa tu muelekeo wa awali jinsi gani tunaendelea kuweka nguvu katika kufikia malengo yaliyowekwa,"amesema Damas.

Hata hivyo amesema kwenye mkutano wa jukwaa hilo, kuna baadhi ya changamoto ambazo zimeonekana na kutoa mfano nchi za Afrika Kusini na Namibia zinajihusisha zaidi na uchimbaji madini na shughuli za viwanda.

"Nchi hizo licha ya uchumi kukua bado hali halisi ya maendeleo haiendani na huduma za kijamii kama elimu na afya. Hivyo kuna kila sababu ya kuweka mikakati ya kuleta maendeleo ya pamoja katika maeneo yote na sisi asasi za kijamii tunalo jukumu la kushirikiana na Serikali zetu kuleta maendeleo,"amesema Damas.

Wakati huo huo amesema pamoja na ripoti yao ambayo wameiandaa kwa kipindi cha mwaka mmoja, wapo kweny mchakato wa kufanya uchambuzi na kisha kuwasilisha serikalini.

Kwa upande wake Katibu Mkuu -UN Tanzania Reynald Maeda ambaye pia anatoka kwenye Waratibu wa Jukwaa la Maendeleo Endelevu nchini amesema katika jukwaa hilo nchi yetu ya Tanzania nayo ilikuwa inatoa ripoti yake kuhusu utekelezwaji wa malengo ya maendeleo endelevu kuanzia tulipoanza na tulipo sasa.

"Maoni yetu asasi za kiraia nayo yalijumuishwa kwenye ripoti ya nchi na kuna asasi nyingi ambazo zimeshiriki.Malengo sita ndio yaliwakilishwa kwa mwaka huu.

"Na jambo kubwa zaidi ni ushirikishwaji na kutoacha mtu nyuma, kwani malengo ni kutoacha mtu nyuma kwenye maendeleo endelevu,"amesema Maeda.
 Baadhi ya viongozi wa za kiraia nchini Tanzania wakiwa wameshika ripoti yao ambayo  pamoja na mambo mengine anaelezea kuhusu makongo ya maendeleo endelevu.Ripoti hiyo wameizundua rasmi leo jijini Dar es Salaam wakati wa kikao cha kupata mrejesho kwa wenzao waliorejea nchini wakitoa nchini Marekani kwenye Jukwaa la Kisiasa la hali ya juu la malengo ya maendeleo endelevu
 Wadau wa maendeleo kutoka asasi za kiraia wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati walipokutana kupata mrejesho wa wenzao waliowawakilisha nchini Marekani  katika Jukwaa la Maendeleo la hali ya juu la malengo ya maendeleo endelevu
 Baadhi ya wajumbe wa asas za kiraia waliofika kupata mrejesho  wakiwa katika picha ya pamoja
 Sehemu ya wajumbe wa asasi za kiraia wakifuatilia mrejesho unaotolewa na wenzao waliofika nchini Marekani katika mkutano wa jukwaa la kisiasa la hali ya juu la malengo ya maendeleo endelevu
Mkurugenzi wa Programu kutoka FORUMCC   Angela Damas akifafanua jambo wakati wa mkutano huo

MAGAZETI YA LEO AGOSTI 1/2019

NEWZ ALERT:MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MKURUGENZI WA MOROGORO VIJIJINI

$
0
0
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli leo Agosti  1/2019 amemtengua Bw. Kayombe Masoud Lyoba aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro kwa usimamizi usioridhisha wa miradi ya Maendeleo hususani ujenzi wa hospitali ya Wilaya .

Akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI , Suleimani Jafo(MB) amesema Mkurugenzi huyo alifanya ununuzi wa dawa ya mchwa kwa gharama kubwa ya milioni 66 kinyume cha gharama halisi.

“kutozingatia taratibu za manunuzi na miongozo ya matumizi y fedha za ujenzi wa hospitali za halmashauri ,kufanya ununuzi wa kokoto kwa gharama ya shilingi Milioni 45 na kuzisafirisha kwa gharama ya milioni 42” Amesema Jafo

Kufuatia utenguzi huo nafasi hiyo ya ukurugenzi kwa sasa itakaimiwa na Mhandisi Godfrey George Mlowe amabye ni Meneja wa TARURA Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro hivyo namlekeza Mhandisi Godfrey Mlowe kusimamia Halmashauri hiyo pamoja na miradi yote ya maendeleo katika wilaya hiyo ikiwemo, ukamilishaji wa majengo ya Hospitali ya Wilaya, Ujenzi wa Vituo vya afya vya Mikese na Kinoko vilivyopokea fedha hivi karibuni .

Waziri jafo amesema kuwa ansisitiza ujenzi wa vituo vya afaya vijengwe kwa utaratibu wa force Account kwa usimamizi wa kamati zilizoundwa katika ujenzi wa vituo hivyo

Waziri Jafo ameiagiza TAKUKURU iendelee na uchunguzi wa kina wa michakato yote ya ujenzi wa Hospitali hiyo ya Wilya.
Viewing all 110029 articles
Browse latest View live




Latest Images