WAKATI taasisi ya kimataifa ya mapinduzi ya kijani barani Afrika (AGRA) ikitekeleza miradi mbalimbali nchini inayohusiana na maendeleo ya kilimo na masoko, Shirika hilo leo Jumatatu limefikia makubaliano na serikali ya Tanzania ya namna ya kuwezesha mabadiliko katika kilimo hivyo kuwakomboa wakulima kwa kuongeza tija na kuipeleka Tanzania katika uchumi wa viwanda.
Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya mkutano ulioshirikia mawaziri watatu wa Tanzania na ujumbe wa taasisi hiyo ukiongozwa na Rais wake Dk Agnes Kalibata. Ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent bashungwa. Mawaziri wengine ni manaibu wawili wa wizara ya Kilimo Hussein Bashe naOmar Mgumba.
Katika makubaliano hayo, serikali na Agra wameafikiana kuangalia namna ya kusukuma mbele ASDP ll na pia kuwezesha mazao ya kimkakati ya viwanda kama alizeti, mahindi na maharage ya soya am,bayo yanaweza kupelekwa kiwandani katika msim u mmoja yanasaidiwa kupunguza gharama na pia kuongezwa tija ili kutumika katika viwanda vilivyopo nchini.
Rais wa AGRA , Dk Kalibata (wa pili kulia-mbele) akizungumza
Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa akiongoza mkutano
Aidha Agra watatoa ruzuku ya dola 600,000 kwa ajili ya kuimarisha utekelezaji wa ASDPll kwa kusaidia serikali katika masuala ya kiufundi yanayohusu program mbalimbali za kilimo.
Kabla ya kufika Dodoma jana ujumbe wa Rais huyo wa AGRA ulikuwa Iringa kwa siku 2 akifanya mazungumzo na wadau wa sekta ya kilimo waliopo katika mradi unaosimamiwa na AGRA wa Ihemi Ludewa.
Mradi huo ni sehemu ya juhudi za AGRA katika kuinua hali ya wakulima kwa kuwashirikisha wadau wote ikiwemo sekta binafsi na serikali ya mitaa, mkulima akiwa ndio mtu wa kati anayetakiwa kuhudumiwa huku serikali ikihakikisha kwamba hakuna fedha zinazotumika kwa kazi moja kutoka kila idara au ufadhili.
Muuza pembejeo za kilimo Zabibu akizungumza dukani kwake
Kabla ya mkutano wake na wadau wanaosaidia mradi wa Ihemi Ludewa, Rais huyo aliendesha mkutano wa kimataifa wa nchi 11 zinazosaidiwa na AGRA kutekeleza miradi mbalimbali ya kuinua kilimo na kuwezesha masoko.
Nchi hizo ni pamoja na Mali, Burkina fasso, Ghana, Nigeria, Ethiopia, Kenya, msumbiji, Rwanda na Tanzania.Mkutano huo ulikuwa kubadilishana uzoefu wa uendeshaji wa majukwaa huru yanaounganisha wadau muhimu katika sekta ya kilimo kuwezesha kila mmoja kutekeleza wajibu wake.
Katika mkutano huo wadau wa Tanzania walielezea umuhimu wa vyama vya ushirika kuweza kupata elimu ya kilimo,kuunganisha sauti katika soko na pia kujifunza mambo mapya katika teknolojia ya kisasa ya kilimo.
Aidha mataifa mengine yalielezea haja ya kuungana kwa nchi za Afrika katika kuinua sekta ya kilimo kwa serikali kushirikiana na mashirika mbalimbali yanayochangia kilimo ili kuwezesha utekelezaji wa sera za kwenda vizuri.
“ Serikali ndio yenye wataalamu wa kilimo na ndio wasimamizi wa teknolojia ya kisasa, tusiposhirikiana tutafanyakazi ya kuwianua wakulima kuwa ngumu” alisema Rais wa AGRA, Dk Kalibata.
Dk Kalibata wakizungumza na mkulima Victory wakati alipomtembelea shambani kwake
Josephine kutoka taasisi ya uelimishaji Briten akizungumzana mfanyabiashara wa mahindi na mkulima Christina
Aidha katika ziara yake kuwaona wadau wa sekta ya wakulima, Dk Agnes Kalibata ametaka elimu zaidi kutolewa kwa wakulima ili kufanya kilimo cha ushindani kitakachohimili mabadiliko ya soko duniani.
Dk Kalibata alisema kwamba bila kuwaandaa wakulima, kukitokea shida katika bei wakulima watakuwa wanakata tama na kuona kilimo chao hakilipi.
Alitoa hoja hiyo baada ya kutaka kununua soya kutoka kwa mkulima Victory Mhanga wa Magulilwa halmashauri ya Iringa, mkoani Iringa ambaye alitaka kumuuzia bidhaa hiyo kwa bei ya Sh 2000.
Dk Kalibata alisema kwamba bei hiyo ni kubwa kulinganisha na soya inayolimwa Brazil.Hata hivyo wataalamu wa masoko waliokuwapo katika ziara hiyo walisema kwamba bei ya juu ilikuwa sh 800 katika mnada wa Songea uliofanyika hivi karibuni ingawa bei ya rejareja Dar es salaam ni Sh 2,500.
Alipouliza zaidi sababu ya bei hiyo kubwa kutozwa na mkulima huyo wakati katika soko la dunia ni dola 0.63 aliambiwa kwamba mkulima huyo anauza kwa nguvu la soko inayomzunguka na kwamba hana tatizo la soko katika eneo lake.
Magulilwa wameanza kulima soya mwaka huu na ingawa wanafahamu faida yake wakulima wachache ndio wamechukua maamuzi ya kulima soya.
Hata hivyo, Rais huyo alisema wakulima lazima waandaliwe kulima na kuzalisha kwa kiwango kikubwa na kupambana na bei ya soko la dunia ambalo huenda likawa chini kuliko wanavyofikiri, lakini wakiwa na mazao ya kutosha bei hiyo ya chini inaweza kabisa isiwaharibie kazi yao na hivyo kuendelea kulima kwa tija kuliko kuwa na bei kubwa na soko finyu.
“ Tusitazame bei tu inayotuzunguka kwa kiasi kidogo. Tukitaka kuwa matajiri katika kilimo ni lazima kutazama kwa upana wake na viongozi wa wakulima lazima wawaeleze wakulima bei ya dunia kitaifa , kimkoa na maeneo yao na kujua manufaa yake,” alisema Rais huyo.
Alisema kwa kuangalia mihimili mitatu inayofanyiwa kazi na AGRA ya uwezeshaji, mfumo na uwekezaji suala la masoko na mauzi ni suala ambalo linatakiwa kuzingatiwa ili mkulima aone faida ya kilimo chake.
Akizungumza kuhusu wauza pembejeo, aliwataka kuwasaidia wananchi kutambua mahitaji halisi na kuyafanyia kazi ili kuweza kuwasaidia kuwa na kilimo cha kisasa hasa matumizi ya pembejeo na mbegu.
Pamoja na kumsifu mkulima huyo na wakulima wengine katika halmashauri ya iringa na Ilolo, Dk kalibata alisifu wakulima kwa kuongeza uzalishaji kufikia hadi magunia zaidi ya 20 kwa ekari na kusema wakiendelea kubadilika watafikisha maguni hata 30.
Rais huyo ambaye pia alipata nafasi ya kutembelea mashamba ya mbegu ya Silverland na kiwanda cha kusaga nafaka cha Seki wanaotengeneza sembe yenye virutubisho, amesema ushiriki wa AGRA katika maeneo ambayo serikali inataka kufanyiwa kazi kumeleta neema kwa wakulima.
Kiwanda cha seki kimekuwa kikinunua mahindi kutoka kwa wakulima na vyama vyao vya msingi na Sliverland ambao pia hununua soya na mahindi kwa ajili ya kutengeneza chakula cha mifuigo pia wana dhamana ya kulima mbegu kwa mujibu wa mkataba wake na kampuni ya mbegu ya Seed Co, wanasaidia kutanuka kwa soko la wakulima, shughuli muhimu inatyofanywa na AGRA kuwezesha taasisi nyingine kusaidia wakulima kupata soko.
Mwaka 2014 AGRA ilianzisha mradi wa miaka mitatu wa kusaidia shughuli mbalimbali za kuinua kilimo kwa wakulima wadogo na kuongeza tija wenye thamani ya dola za Marekani milioni 4.25.
Mradi huo uliotekelezwa na Netherlands Development Organization (SNV), Rural Urban Development Initiative (RUDI), Women in Social Entrepreneurship (WISE) na Dunduliza Network of Savings And Credit Co-operatives (SACCOs) waliwezesha miradi mbalimbali iliyokuwa na lengo la kusaidia kuongeza tija, pato na soko kwa mkulima mdogo kwa maeneo ya ukanda wa SAGCOT.
Mradi huo ambao baadae ulifuatiwa na mradi wa Pata Tija yaani tengeneza utajiri, ulifundisha haja ya matumizi ya mbegu bora na pembejeo katika kuilimo, kufunza wauza pembejeo teknolojia mpya na nakuwuanga wakulima na taasisi za fedha.
Katika mradi huo pia wadau wlaipata nafasi ya kujifunza menejimentiya udongo.Wilaya ambazo zilifadikika na mradi huo ni opamoja na Ifakara, Kilombero, Kilolo, Kyela, Ludewa, Mbarali, Mbeya, Mbozi, Momba, Namtumbo, Songea na Sumbawanga.
AGRA ikiwa imelenga kubadili maisha ya wakulima na vipato vyao katika bara la Afrika jana iliingia katika makubaliano na serikali ya Tanzania kwa kutia saini hati ya maridhiano (MOU) inayoonesha majukumu ya serikali na taasisi hiyo katika lengo la kuinua ushiriki wa kila mdau katika kuinua sekta ya kilimo kuipa tija kwa uzalishaji wa uhakika na soko la uhakika huku mazingira yakilindwa.
Huku bara la Afrika likiwa na asilimia 25 ya eneo la ardhi lenye uwezo wa kuzalisha, sekta ya kilimo barani Afrika inaweza kupanda kama hatua kadha zitachukuliwa kuimarisha tija .
Taarifa ya Shirika la Chakula Duniani ( FAO) ya mwaka 2016 kuhusu usalama wa chakula, inasema kwamba watu milioni 153 ikiwa ni asilimia 26 ya watu waliochi ya miaka 15 Kusini mwa Jangwa la Sahara wamekabiliw ana upungufu mkubwa chakula kwa mwaka 2014/15.