Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv
MTOTO wa mfanyabiashara Ester Lymo (47) , anayekabiliwa na tuhuma za kesi ya mauaji ya mjukuu wake Naomi John, Jackline Kessy (25) ameieleza
Mahakama kuwa marehemu Naomi aliyefariki Machi, mwaka 2017 alipigwa na mama yake licha ya kuwa mtoto huyo hakuwa katika haki nzuri ya kiafya kwa siku hiyo.
Jackline ambae ni shahidi wa pili wa utetezi katika tuhumza za kesi hiyo ya mauaji ameeleza hayo leo Julai 29 mwaka 2019 wakati akitoa ushahidi kumtetea mama yake mzazi mshtakiwa Ester mbele
ya Msajili Pamela Mazengo wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.
Wakati akijibu maswali ya Wakili wa Serikali Mwandamizi Cecilia Mkonongo, Jackline amedai, siku ya tukio kabla ya mama yake kumchapa Naomi, hakuwa katika hali yake ya kawaida, kwani alikuwa amelegea.Pia alikuwa hajanywa hata chai lakini mama yake alimchapa na ndipo baada ya kumchapa akalegea kabisa.
Ameidai kuwa wakati mama yake akiendelea kumchapa, Naomi aliishiwa nguvu, ambapo mama yake alikwenda duka la dawa, alishauriwa ampeleke hospitali mtoto kutokana na hali aliyokuwa nayo marehemu.
" Mimi ndio nilimbebe Naomi wakati tunaenda hospitali, tukiwa njiani nilisikia Naomi akiwa ana hema haraka haraka, sikujua kama alikuwa amekufa hadi tulipomfikisha hospitali, ambapo nilimsikia daktari akimwambia mama kuwa mgonjwa wao alikuwa ameishiwa damu", amedai Jackline
Wakili huyo wa Serikali, Mkonongo alimpatia Jackline maelezo yake aliyoyatoa Polisi ili ayasome, kulinganisha na alichokisema mahakamani kama vinalingana au la.
Jackline akisoma maelezo yake aliyoyatoa polisi, alidai kuwa mama yake alikuwa mkali sana ndiyo maana walikuwa hawakai nyumbani, ambapo mwaka 2009, baba yake ndiyo aliwaomba wakae likizo nyumbani.Alidai Naomi alikuwa na vidonda mwilini na mkono wake ulikuwa kama umeteguka, alipomuuliza dada yake (Victoria John) alidai mama ndiyo kamchapa na kumfinya na hata yeye alishawahi kumshuhudia mama yake akifanya hivyo.
"Siku moja Victoria alikuwa anamuogesha Naomi alikuwa anasikia maumivu sehemu za siri, Victoria akampiga akasema anadeka.Mama na Victoria ndiyo walikuwa wanampiga Mimi sikuwahi kumpiga ," Nilimuona mama akitumia maji ya moto kumchoma Naomi. Naomi alipotoka Moshi alikuwa anamapunye kichwani na pia alikuwa hana tabia nzuri, "amedai Jackline mahakamani hapo.
Wakati Mkonongo alipomuuliza kuwa kati ya yeye na mama yake nani anayesema ukweli?, Kessy alidai kuwa ni yeye ambaye anazungumza ukweli, ambapo awali hilo lilitokana na mkanganyiko wa maelezo ya mama yake na yeye.
Katika utetezi wake, mshtakiwa Easter Lyimo ambae ni shahidi wa kwanza katika kesi hiyo amedai wakati anamchapa marehemu alimwambia amechoka lakini yeye alijua ni utani na akaendelea kumchapane Kessy (25).
Akiongozwa na Wakili wa utetezi, mshitakiwa Esther amedai mahakamani hapo kuwa vidonda na makovu katika mwili wa marehemu Naomi vilitokana na shuguli za kuchunga mbuzi kijijini kwao Moshi.
Amedai, Naomi na Andrew ni watoto dada yake na aliwachukua ili aishi nao baada ya kuombwa na Dada yake awasomeshe lakini tangu aishi na Naomi nyumbani kwake Tuangoma hadi siku ya siku anafariki, alikuwa na vidonda na makovu.
"Watoto hawa ni watundu sana, huwa wanakimbizana na kucheza vichakani hivyo ndio maana mwili wake ulikuwa na vidonda na makovu, sijamuua Naomi, nilikuwa nawapenda watoto hao kama watoto wangu wa kuwazaa naomba mahakama iniachie huru,"amedai
Amedai, siku ya tukio, Machi 25, mwaka 2016 wakati anatoka kufanya usafi Saloon kwake, alielezwa na Andrew kuwa Naomi ameamka, amejikojolea yupo barazani."Nilimwambia Naomi akapige mswaki, nikaingia ndàni, lakini aliendelea kukaa barazani, Andrew aliniambia hapigi mswaki anachezea maji, nikaongea kwa sauti kwamba nikitoka ndani nitàmchapa, nilipotoka Naomi akakimbia nikamwambia Andrew amkamate," amedai Esther.
Amedai alipoletwa alichuma fimbo katika mti wa Mparachichi na kumchapa kwa nia ya kumkanya kama mzazi."Wakati namchapa Naomi akasema amechoka, mi nilizani ni utani kwasababu ya kukimbia na ujeuri wake, nilimnyànyua na kumweka barazani, nikaenda kutafuta dawa, nilivyorudi nilikuta amelegea sana hivyo nikachukua gari ya jirani na kumpeleka hospitali Temeke," amedai.
Katika utetezi wake, Esther amedai daktari aliwaambia Naomi alikuwa amepungukiwa damu na baada ya muda akawaeleza kuwa ameshafariki.Amedai wakiwa hospitalini Polisi walikuja kumchukua na kupelekwa Kituo cha Polisi Maturubai na baadae Charambe na Aprili 4, mwaka 2016 akafunguliwa mashitaka ya mauaji.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi itakapopangiwa session nyingine.