Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109936 articles
Browse latest View live

MAGAZETI YA LEO JUMATATU JULAI 29,2019


Ohooooo.....ajali.

$
0
0
Mkokoteni ukiwa chini (kulia) kama inavyoonekana pichani eneo laTandika wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, baada ya kugongana na Lori aina ya  Fuso lenye namba za Usajili T618 AKA wakisubiri Askari wa kikosi cha usalama barabarani kuja kupima,kufuatia ajali hiyo iliyosababisa foleni kubwa,hakuna aliyepoteza Maisha.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)


Mbio za nyika kivutio cha watalii kisiwani Pemba

KAMPUNI YA VODACOM TANZANIA YASHIRIKI KONGAMANO LA CORPORATE UNWIND JIJINI DAR

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Plc, Hisham Hendi akizungumza wakati wa kongamano la Corporate Unwind lililoandaliwa na Smart Codes katika makao makuu yake jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Vodacom Tanzania ni kampuni ya mtandao wa simu inayoongoza Tanzania iliyojikita katika kuisaidia Tanzania kufikia uchumi wa kidigitali kwa kuvumbua mifumo suluhishi ya kidigijitali kwa kutumia teknolojia ya simu. Kongamano hilo lilikutanisha wadau mbalimbali kutoka sekta ya biashara na uvumbuzi pamoja na wafanyabiashara, taasisi na makampuni mashuhuri nchini Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Plc, Hisham Hendi akieleza jambo kwa baadhi ya washiriki wa kongamano la Corporate Unwind lililoandaliwa na Smart Codes katika makao makuu yake jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Vodacom Tanzania ni kampuni ya mtandao wa simu inayoongoza Tanzania iliyojikita katika kuisaidia Tanzania kufikia uchumi wa kidigitali kwa kuvumbua mifumo suluhishi ya kidijitali kwa kutumia teknolojia ya simu. Kongamano hilo lilikutanisha wadau mbalimbali kutoka sekta ya biashara na uvumbuzi pamoja na wafanyabiashara, taasisi na makampuni mashuhuri nchini Tanzania.

Taasisi ya Young Scientists Tanzania(YST) kufanya maonesho julai 13 mwaka huu jijini Dar

$
0
0
Taasisi ya Young Scientists Tanzania(YST) inatarajia kufanya maonyesho ya Wanasayansi chipukizi kuanzia Julai 31 mpaka adosti 1 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es Salaam Mwneyekiti w abodi ya YST nchini Profesa Yunus Mgaya amesema kuwa wanafunzi wanaopata fursa ya kushiriki maonyesho aya walipata fursa ya kuboresha ujuzi wao wa kisayansi kupitia mango wa uwezeshaji ulioendeshwa na wanasayansi washauri .


"kwa siku mbili wanasayansi chipukizi wataonyesha kazi zao katika nyanja mbalimbali za sayansi kama kemia, fizikia na hesabu ,biology mazingira na sayansi ya jamii na tekonolojia ,kazi hizi za kisayansi hasa ziwe zimejikitakatika utatuzi wa matatizo katika afya ,Kilimo, usalama wa chakula ,mawasiliano na usafirishaji " Amesema Prof Mgaya.


amesema wanasayansi watakaokuwa na ugunduzi mzuri watazawadiwa pesa taslim na medali wanasayansi wanne watapewa udhamini wa kusoma chuo kikuu na shirika la Karim mjee Jivanjee Foundaton.


Washindi wa jumla wataiwakilisha Tanzania kwenye Maonesho ya kimataifa ya Eskom Expo Young Scientists jijini Johannesburg Afrika Kusuni Oktoba mwaka huu.

Mwenyekiti wa bodi wa Tasisi ya Young Scientists Tanzania(YST), Prof Yunus Mgaya akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juu ya kilele cha Maonesho ya tisa ya wanasayansi chipukizi yatakayofanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere Convention Centre kuanzia Julai 31 mpaka Agosti 1 mwaka 2019.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

Mkurugenzi Mwanzilishi wa YST Nchini Dr.Gosbert Kamugisha (katikati) akieleza namna wanafunzi walioshiriki katika maonyesho hayo katika kipindi cha nyuma fursa walizopata ikiwemo ufadhili wa masomo ya kusoma elimu ya juu nje ya nchi.kushoto Mwenyekiti wa bodi wa Tasisi ya Young Scientists Tanzania(YST), Prof Yunus Mgaya kulia ni Mwanzilishi wa YST,Joseph Clowry.
 waandishi wa habari  wakimsiliza Mwenyekiti wa bodi wa Tasisi ya Young Scientists Tanzania(YST), Prof Yunus Mgaya.

MNYETI ATAMBIA MAENDELEO MANYARA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti akielezea maendeleo mbalimbali yaliyofanyika kwenye mkoa huo katika awamu hii ya tano ya Serikali inayoongozwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli.

………………………………….
MKUU wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti amesema mkoa huo unazidi kupiga hatua kwenye sekta mbalimbali za maendeleo ikiwemo elimu, afya, maji na miundombinu na asiyeona maendeleo hayo atakuwa ana matatizo kichwani mwake.

Mnyeti akizungumza mjini Babati kwenye kongamano la wadau wa biashara alisema Manyara ya sasa ni tofauti na ya zamani katika suala zima la maendeleo.

Alisema miaka iliyopita mkoa huo ulikuwa nyuma kwenye masuala mbalimbali ya maendeleo lakini hivi sasa inashindana na kuishinda mikoa iliyoanzishwa miaka mingi iliyopita.

Alisema mkoa huo ni watatu kwa ukubwa hapa nchini hivyo unahitaji viogozi makini na madhubuti wa kusimamia maendeleo na ndivyo wanavyofanya.

“Kwenye elimu tulikuwa nyuma lakini sasa tupo vizuri kwenye elimu ya msingi tulikuwa nyima lakini mwaka uliopita tumekuwa wanane kitaifa, kidato cha nne tulikiwa wa mwisho mwisho lakini sasa wa 12 na kidato cha sita tumekuwa watano kitaifa tunazidi kusonga mbele, alisema.

Alisema kwenye suala la miundombinu ya barabara za mkoa huo wakala wa barabara nchini (Tanroads) na wakala wa barabarab za mijini na vijijini (Tarura) wamejitahidi ipasavyo kuhakikisha inapitika kwa nyakati zote.

“Ukiacha majiji ya Dar es salaam, Mwanza na Arusha hivi sasa Babati inafuatia kwa barabara nzuri na zilizowekewa taa hadi wamasai na wairaq wanapiga picha usiku kwenye taa za kuongozea barabara tumewashinda Mbeya, Singida na Moshi,” alisema Mnyeti.

Alisema hivi sasa mkoa huo unazidi kupiga hatua kutokana na wananchi wake kuwa na fikra chanya na kumuunga mkono Rais John Magufuli katika kufanya kazi na pia viogozi kuwasimamia ipasavyo.

Mkuu wa wilaya ya Simanjiro, Zephania Chaula alimshukuru Mnyeti kwa kutangaza kuwa yeye ndiye mkuu wa wilaya namba moja ambaye ni mchapakazi na mahiri katika mkoa huo.

“Nawaahidi wananchi wa Simanjiro kuwa nitaendelea kuwatumikia bila kuchoka usiku na mchana na nawashukuru wasaidizi wangu wa karibu katibu tawala wa wilaya Zuwena Omary na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri Yefred Myenzi kwani tunafanya kazi kwa ushirikiano,” alisema Chaula.

VIJANA WAKISHIRIKI IPASAVYO KWENYE KILIMO UCHUMI UTAIMARIKA-MHE HASUNGA

$
0
0

Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo akisisitiza jambo wakati akizungumza na vijana wa Jimbo la Vwawa katika kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi makao makuu ya Chama hicho Wilayani Mbozi, leo tarehe 28 Julai 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)

Vijana wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe wakimsikiliza kwa makini Mbunge wa Jimbo hilo ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga wakati akizungumza katika kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi makao makuu ya chama hicho Wilayani Mbozi, leo tarehe 28 Julai 2019.
Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo akiagana na vijana wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe mara baada ya kikao na vijana hao kilichofanyika katika ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi makao makuu ya Chama hicho Wilayani Mbozi, leo tarehe 28 Julai 2019.
Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo akisisitiza jambo wakati akizungumza na vijana wa Jimbo la Vwawa katika kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi makao makuu ya Chama hicho Wilayani Mbozi, leo tarehe 28 Julai 2019.



Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songwe

Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo anakusudia kuwakutanisha vijana kwa ajili ya kongamano la kujadili fursa zilizopo katika sekta ya Kilimo.

Waziri Hasunga ameyasema hayo tarehe 28 Julai 2019 wakati akizungumza na vijana wa Jimbo la Vwawa katika kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Chama Cha Mapinduzi makao makuu ya Chama hicho Wilayani Mbozi.

Alisema kuwa zaidi ya asilimia 70 ya watanzania wanajihusisha na Kilimo lakini miongoni mwao vijana ni wachache hivyo mkakati huo wa kuwakutanisha vijana ni sehemu ya kueleza kwa viajan fursa zilizopo kwenye sekta ya Kilimo na kuziendeleza.

Alisema kuwa vijana ndio nguvu kazi ya Taifa hivyo kuhusishwa kwenye sekta ya Kilimo ni miongoni mwa mambo msingi yatakayoinua uchumi wa vijana nchini kadhalika kuimarisha uchumi wa Taifa.

Mhe Hasunga amesema kuwa vijana wengi wamekuwa wakijihusisha na mambo yasiyokuwa na tija katika Jamii kama vile kushinda vijiweni badala yake wanatakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kuimarisha kipato chao kitakachopelekea vijana kutojihusisha na uovu wa aina yoyote.

Kuhusu kuimarisha masoko ya mazao mbalimbali ikiwemo zao la kahawa, Mhe Hasunga amesema kuwa tayari wizara ya kilimo imeanzisha mkakati kabambe wa kuongeza minada ya kahawa ambapo kwa upande wa Kanda ya ziwa mnada utafanyika mkoani Kagera, Kanda ya Kaskazini utafanyika Manispaa ya Moshi, Kanda ya kusini utafanyika wilayani Mbinga na Kanda ya nyanda za juu kusini mnada wa kahawa utafanyika Wilayani Mbozi.

Ameongeza kuwa kuongeza minada ya uuzaji wa zao la kahawa utatoa fursa kwa wakulima kunufaika na mazao yao kwa kuuza kwa bei nzuri na kulipwa kwa wakati.Mhe Hasunga amewasihi wakulima mkoani Songwe na Taifa kwa ujumla wake kujishughulisha zaidi na Kilimo kwani ndio sehemu pekee yenye uwezo wa kuwaongezea kipato chao.

Kuhusu kadhia ya mbegu feki kwa wakulima Mhe Hasunga amesema kuwa serikali imejipanga kuimarisha upatikanaji wa viuatilifu kwa wakati na kwa bei nafuu ili wakulima waweze kuvimudu.

"Kumekuwa na mbegu nyingi mtaani ambazo sio sahihi kwa maana hiyo sasa serikali inachukua hatua kali kwa wafanyabiashara wanaojihusisha na biashara hiyo punde watakapobainika" Alikaririwa Mhe Hasunga

Makonda apiga marufu 'watu wachafu ' kuja mjini .

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda, leo Julai 29 amezindua kampeni ya tano ya usafi yenye lengo la kuendeleza kufanya usafi wa jiji Dar es Salaam ikiwa ni hatua za maandalizi ya kupokea ugeni wa viongozi wa Umoja wa Nchi zilizo Kusini Mwa Afrika (SADC).

Akizungumza na waandishi wa Habari Julai 29/2019 katika uzinduzi Kampeni ya Usafi katika Uwanja wa Ndege Terminal I,Makonda amesema lengo kubwa ni kuweka Jiji Safi huku akizitaka Taasisi zote za Serikali kuhakikisha kwamba zinakuwa na watu wao wa usafi katika maeneo yao ya kazi.

Makonda amesema pamoja na kuweka Jiji la Dar es Salaam kuwa safi ni kuonyesha ubora wa wananchi wa jiji hilo na mikoa mingine ifanye hivyo na wakija wajifunze vitu vingine ikiwemo usafi kutokana na kuwepo Marais 16 katika mkutano wa SADC. 

Amesema kuwa Mkoa wa Dar Es Salaam unachangamoto ya usafi hivyo ni vyema wakajenga utamaduni wa kufanya usafi Mara kwa Mara.

"Nataka kuwaambia tu kwamba nimemsikia Mratibu wa kila Taasisi ya Serikali katika mkoa wangu iwe na watu wa usafi" Amesema RC Makonda.Amesema ugeni wa SADC ni heshima kwa Rais Dkt John Magufuli na Mkoa wa Dar Es Salaam kwa ujumla hivyo lazima Jiji liwe safi wakati wa kuwapokea wageni pia usafi huo uwe endelevu.

Katika hotuba yake Makonda amewataka wakazi wa Dar Es Salaam, kuzingatia usafi na kupiga marufuku mtu yoyote kufika mjini kama hajafanya usafi wa mwili wake ikiwemo kuoga, kufua na kupiga pasi nguo zake.

“Tabia ya kuja mjini hujafua, hujaoga usitutie aibu kama umezoea kuja mjini hujaoga wala kufua nguo baki nyumbani walau huu mwezi wa nane uishe, tunataka sio usafi tu wa mazingira, usafi pia wa wananchi wetu, watu wamejaa chawa tu hapa”. Amesema.

“Ule utaratibu wetu wa Lugalo tunauanza rasmi leo haiwezekani wawe na nidhamu kwenye kile kipande cha kukaribia mita 200, 300 kwahiyo ule utaratibu wa mtu kwenye gari kutupa taka hovyo mshusheni akikataa chukueni namba yake ya gari tutamkamata ili aje apige deki” Amesema Makonda.

Pia amesema ifikapo Agosti 5 Jiji la Dar Es salaam liwe safi kwa ajili ya mapokezi ya wageni na amewataka Maafisa Mazingira kuhakikisha miti yote inayopandwa inaota kwani Serikali imekuwa ikitenga bajeti kubwa na pesa hizo hazioneshi matunda na Mazingira chanya kama inavyokusudiwa.

Makonda amewataka Vijana wa usafishaji kuhakikisha kwamba Dereva wa gari akitupa taka taka hovyo apigishwe deki kwa kupewa kipande cha bara bara badala ya kuwapiga faini za pesa na watendaji wa mitaa husika kuhakikisha maeneo yao yanakuwa safi la sivyo watapoteza ajira zao.

Katika hatua nyingine amewataka Wananchi na Tanzania kwa ujumla wajitokeze kwa wingi katika uzinduzi wa Uwanja mpya wa ndege wa Kisasa wa Mwalimu Nyerere Terminal 3 wenye uwezo wa kubeba Abiria Milioni 6 utakaotarajiwa kuzinduliwa na Rais Dkt John Magufuli Agosti 4/2019 asubuhi.


Takukuru yawanasa waliotaka kumpa rushwa DC Katambi

$
0
0
Na Charles James, MICHUZI TV

TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini (TAKUKURU) mkoa wa Dodoma inatarajia kuwafikisha mahakamani watu saba wanaotuhumiwa kujihusisha na vitendo vya kuomba na kupokea rushwa kinyume na kifungu cha sheria namba 11 ya mwaka 2007.

Moja ya watuhumiwa waliokamatwa ni mfanyabiashara Bahadur Hirji (68) mkazi wa mtaa wa Tembo Kata ya madukani jijini Dodoma na mwanae Nahid Bahadur (33) mhasibu wa Victory Bookshop kwa kosa la kuahidi kumpa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe Patrobas Katambi sh mil 1.2 ili asifuatilie mapungufu katika utekelezaji wa amri ya Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Dodoma kukazia hukumu iliowasilishwa kwake.

Akizungunza na waandishi wa habari Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Dodoma Sosthenes Kibwengo alisema baada ya TAKUKURU kupata taarifa ya watuhumiwa kutoa fedha hiyo ya kishawishi kwa Mkuu wa wilaya walianza kuwafuatilia na kufanikiwa kuwakamata Julai 27 katika hoteli ya Royal village iliopo Area D baada ya mtuhumiwa Nahid kumkabidhi Mkuu wa wilaya rushwa hiyo.

Kibwengo alisema ukiacha watuhumiwa hao pia wamemkamata Omary Mtauka ambae ni msaidizi wa mtendaji wa Kata ya Makutupora iliopo jijini Dodoma baada ya kupokea rushwa ya sh 110,000 kutoka kwa Mzee Paulo Mawope (78) mkazi wa Chilungule Kata ya Makutupora ili wamalize tuhuma dhidi ya kugombana na jirani zake zilizowasilishwa na Mtendaji wa mtaa na badae ofisini kwake.

"Awali tulipokea taarifa kutoka kwa mjukuu wake kwamba amepigiwa simu na mtendaji wa Kata ya Makutupora uchunguzi watu uliweza kuthibitisha juu ya uwepo wa tukio hilo,na mtuhumiwa kujifanya ni mtendaji wa Kata hiyo," alisema Kibwengo.

Aidha alisema TAKUKURU inamshikilia Stanley Motambi(34) ambayo ni mtendaji wa Kijiji cha Matumbulu kilichopo Kata hiyo kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa ya sh 65,000kinyume na taratibu za kiutendaji kutoka kwa Wilfred Mtundu ambaye alikuwa na shauri la mgigoro wa Ardhi mbele ya mtendaji wa kijiji kama kishawishi ili askilize shauri hilo.

Alisema baada ya kupata taarifa hiyo walifanya uchunguzi na kuthibitisha mtuhumiwa hiyo alitenda kosa hilo Junior tatu mwaka huu.

Aliwataka wengine waliokamatwa na vitendo hivyo vya rushwa ni Venance Mayo (34) na Sultan Rusheke (33) ambalo ni walimu wa sekondari ya viwandani iliopo jijini Dodoma ambalo waliomba fedha hiyo ili wampatie cheti cha utambulisho wa kusoma shule hiyo (leaving certificate).

Mtoa taarifa ambaye alikuwa Mwanafunzi wa shule hiyo alihitaji cheti hiko kwa ajili ya kuomba kozi fupi katika taasisi Moja ndipo akaenda shuleni hapo.

Alisema taarifa hiyo ikiwafikia TAKUKURU Julai 26 na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa Mayo akiwa kwenye Bajaji yenye namba MC686BHK ilioegeshwa kwenye uzio wa shule hiyo baada ya kupokea hongo hiyo na kumkabidhi muhusika cheti huku akiwa na muhuri wa Mkuu wa shule na kugonga kwenye cheti,kabla hajaondoka ndio alikamatwa ikiwemo Rusheke pia kwa sababu amehusika kutoa.

Mtuhumiwa Mwingine aliyekamatwa na ni Abdulhakim Kabunga (26) ambaye ni mtumushi wa muda wa mamlaka ya vitambulisho nchini (NIDA) Dodoma ambayo alikamatwa Julai 27 baada ya TAKUKURU kupata taarifa ya kwamba amepokea rushwa ya sh 30,000 kutoka kwa mtu mmoja aliyekuwa akihitaji kitambulisho cha taifa ili amsaidie kuipata haraka.

Alisema baada ya kuhojiwa mtuhumiwa huyo amekiri kuhusika na kitendo hiko huku taasisi hiyo ikiwakumbusha watu wanaofuatilia vitambulisho vya NIDA zoezi hilo utilewa bure na iwapo watatakiwa kutoa rushwa ili wahudumiwe wanatakiwa kutoa taarifa TAKUKURU.

Pia wanaendelea kuwakumbusha watumishi wa umma na wakazi wa Dodoma kwa ujumla kuzingatia maadiki ya utumishi ili kujiepusha na vitendo hivyo kwani vinaminya haki za wananchi.
Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Dodoma Sosthenes Kibwengo.

Tamasha la Cigogo ni heshima nyingine Tanzania

$
0
0
Mkurugenzi Joyce Fisoo akionesha umahiri wake katika ufunguzi wa Tamasha la Muziki wa Cigogo linaloendelea kwenye viwanja vya Ikulu

Na Mwandishi Wetu, Chamwino

SERIKALI imeeleza kwamba Tamasha la muziki wa Cigogo lililofikia tamati jana kwenye viwanja Chamwino Ikulu jijini Dodoma ni muendelezo wa heshima ya Tanzania kwa maendeleo ya sanaa Afrika Mashariki na Kati.

Akizungumza juzi katika ufunguzi wa Tamasha la 11 la muziki wa Cigogo, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa, Joyce Fisoo alisema heshima nyingine iliyopata Tanzania ni kupata nafasi ya kuandaa michuano ya Afrika kwa Vijana wenye umri chini ya miaka 17 (AFCON) sambamba na kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa Nchi za Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaotarajia kufanyika Septemba mwaka huu.

Fisoo alisema heshima nyingine iliyoipata Tanzania ni kuwa mwenyeji wa Tamasha kubwa la Afrika Mashariki la JAMAFEST ambalo ni kichocheo cha ukuzaji sanaa na uchumi wa nchi wanachama.

Alisema tamasha hilo la JAMAFEST linatarajia kuanza Septemba 21-28 jijini Dar es Salaam ambako alitoa wito kwa wadau mbalimbali wa sanaa hapa nchini kuitumia fursa hiyo ya uwenyeji.

Aidha Fisoo ambaye alikuwa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Filamu Tanzania, alisema kutokana na utendaji uliotukuka kwa waandaaji wa tamasha la Cigogo, Kituo cha sanaa Chamwino (CAC) anajipanga kuandaa cheti maalum kwa ajili ya kutambua na kuthamini mchango wa taasisi hiyo.

“Najipanga kuandaa cheti mahsusi kwa ajili ya kutambua mchango wa CAC kwa sababu mbali ya sanaa pia kituo hicho kinatoa elimu kwa mikoa mingine ambayo huhudhuria tamasha hilo kwa ajili ya kujifunza,” alisema Fisoo.

Fisoo alisema kwa sababu ya ukubwa wa tamasha hilo, ataishawishi serikali kuliongezea nguvu zaidi kwa sababu ya maudhui yake.

Mwenyekiti wa tamasha hilo, Dk. Kedmon Mapana alisema tamasha lake lina wigo mpana wa ufanyaji kazi, hivyo jamii ya watanzania inatakiwa kuifanyia kazi sanaa.

Dk. Mapana alitumia fursa hiyo kulitumia tamasha la JAMAFEST kama sehemu ya fursa kwa ajili ya maendeleo.

Kabla ya tamasha hilo kuanza, Fisoo na wadau wengine wa sanaa akiwemo Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mngereza, Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi, Adrian Nyangamale na wadau wengineo walitembelea mabanda ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaa (UDSM), Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa), Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Basata, Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA) na Bodi ya Filamu.

Tamasha hilo lilihudhuriwa na wadau kutoka nchi za Marekani, Uganda, Hispania, Thailand, Zambia, Ujerumani, Bulgaria, Ethiopia na Argentina.

Kabla ya kuanza kwa tamasha hilo, mgeni rasmi alikaribishwa na makundi 30 ya ngoma za asili yaliyoshiriki tamasha hilo.
Kaimu Mkurugenzi wa Sanaa, Joyce Fisoo akiwajibika kwenye tamasha la Cigogo

KAMPENI YA JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA YAZINDULIWA HALMASHAURI YA WILAYA YA MERU.

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Jiongeze tuwavushe Salama.
Kiongozi wa Mila ,Mzee wilson Kaaya,Mshili mkuu ukoo wa Kaaya akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya jiongeze tuwavushe Salama
Mhe.Diwani kata ya Akheri (wa kwanza kulia) Viongozi wa Dini na Mila wakati wa uzinduzi
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Meru Dkt.Maneno Focus akizungumza kwenye kikao hicho.

Kampeni ya jiongeze tuwavushe Salama imezinduliwa katika Halmashauri ya Meru, Wilayani Arumeru ambapo mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro, amesema Wilaya hiyo itasimamia vyema Kampeni hiyo inayolenga kupunguza vifo vya mama wajawazito pamoja na watoto wachanga, hivyo jamii na watoa huduma za afya wanapaswa kutekeleza wajibu wao kwa wakati 

"kuwa mjamzito  na kujifungua si ugonjwa hivyo kinamama na watoto ni lazima wawe salama kwani uhai ni haki yao"amesisitiza Mhe Muro.

Aidha Muro amemwagiza Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo Dkt.Maneno Focus Kuwakumbusha watoa huduma za afya kutekeleza wajibu wao kwa weledi pia kutumia lugha zenye staa na rafiki kwa wagonjwa sambamba na kuacha matumizi ya simu za mkononi yasio muhimu wakati wa saa za kazi "kauli nzuri kwa mgonjwa humpa faraja na kuwa sehemu ya tiba" amefafanu Muro.
Mganga Mkuu Dkt.Maneno Focus amesema Serikali imefanikiwa kwa kiwango kikubwa kuhakikisha dawa na vifaa tiba katika vituo vya kutolea huduma vinakuwepo ambapo kwa Halmashauri hiyo hali ya uwepo wa dawa muhimu wakati wa kujifungua ni zaidi ya asilimia 98.
Aidha  Dkt. Focus  aliainisha kuwa katika kipindi cha mwezi January hadi Juni mwaka 2019 kumekua na vifo  viwili vitokanavyo na uzazi ingawa bado kuna changamoto ya upatikanaji wa taarifa sahihi toka kwenye jamii ambao hawafiki kwenye vituo vya kutolea huduma, hivyo kampeni hiyo inalenga kuongeza uwajibikaji kwa viongozi wa dini, siasa, kijamii na wadau wote kuwajibika na kuhakikisha  vifo vya uzazi vinadhibitiwa.
Naye Mratibu wa Kampeni hiyo ngazi ya Halmashauri Ndg.Sikudhani Mkama amesema Halmashauri imeweka mikakati ya kuhakikisha utekelezaji wa kampeni ya jiongeze tuwavushe salama inafanikiwa na ametoa rai kwa  jamii na familia kutimiza wajibu wao ili kupunguza na kutokomeza vifo vitokanavyo na uzazi.
Akizungumza kwa niaba ya wadau wa Afya Philomena Marijan toka Shirika la kimataifa lisilo laSerikali DSW ambalo huwawezesha vijana kwa kuwajengea mazingira wezeshi pamoja na kuongeza ushiriki wao katika ma swala ya afya ya uzazi,uchumi na uongozi, ameipongeza Halmashauri hiyo  kulipa kipau mbele swala la afya ya vijana na elimu juu ya afya ya uzazi.
Aidha uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa Halmashauri umekamilika kwa maafisa Tarafa  kula kiapo cha usimamizi wa utekeleza wa Kampeni hiyo.

ATE, JUMUIYA YA CHINA WAJADILI CHANGAMOTO ZA KIBIASHARA NCHINI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv

Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) wamefanya mkutano wa hadhi ya juu ili kujadili fursa za uwekezaji nchini kwa wafanyabiashara kutoka China na pia kujadili changamoto za kibiashara wanazokutana nazo katika katika uwekezaji wao. 

Mkutano huo ni ushirikiano baina ATE na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa China nchini Tanzania na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi la Norway (NHO) uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa ATE Dkt. Aggrey Mlimuka alisema kwamba ATE wamekuwa wakiandaa mikutano ya aina hii mara kwa mara ili kujadili na kutoa elimu kuhusiana na sheria za Kazi na Ajira nchini ikiwa ni moja ya juhudi za kuboresha mazingira ya kufanya biashara kwa wawekezaji wa kutoka China ili kuongeza uzalishaji na ushindani wa kibiashara.

“Kama ilivyo kwa wafanyabiashara wengine hapa nchini, Jumuiya wa Wafanyabiashara wa Kutoka China bado wameendelea kukumbana na changamoto nyingi zinazohusiana na Uwekezaji, Masuala ya Kodi, utekelezaji wa sheria za kazi na Ajira, Ajira za wafanyakazi, mikataba, Taratibu za Usitishwaji wa mikataba, Masaa ya kazi, Likizo, Vibali vya Kufanya kazi kwa Wageni," amesema Dkt Mlimuka.

Amesema changamoto nyingine nyingi zinaendana na hivyo ATE kwa kushirikiana na wadau wao wameona ni vyema kuandaa mkutano huo ili kuweza kujadili na kutafuta ufumbuzi wa Changamoto hizo.

Dkt. Mlimuka pia alitumia muda huo kuiomba serikali kuendelea kuboresha mazingira ya kufanya biashara nchini ili kuwavutia wawekezaji wengi zaidi kutoka ndani na nje ya nchi ili kukuza uchumi wa Taifa letu.

Mkutano huu wa ngazi ya juu umejumuisha wadau mbalimbali kutoka Kituo cha Taifa cha Uwekezaji, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Idara ya Uhamiaji, Ofisi ya Kamshna wa Kazi na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA). 
 Mkurugenzi Mtendaji wa ATE Dkt. Aggrey Mlimuka akizungumza na waandishi wakati wa mkutano wa hadhi ya juu wa kujadili fursa za uwekezaji nchini kwa wafanyabiashara kutoka China na pia kujadili changamoto za kibiashara wanazokutana nazo katika katika uwekezaji wao. 

Washiriki wakiwa wanafuatilia mkutano huo kwa umakini.

KASI YA UTENDAJI WA RAIS DKT MAGUFULI YAMKIMBIZA DIWANI WA CUF PANGANI AJIUNGA CCM

$
0
0
Katibu wa Idara ya Organization ya Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa Pereira Silima kulia akipokea kadi ya Chama cha wananchi (CUF) kutoka kwa aliyekuwa Diwani wa Kata ya Pangani Mashariki (CUF) Akida Boramimi baada ya kujiunga na chama hicho kwenye mkutano wa hadhara wa Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji 
Katibu wa Idara ya Organization ya Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa Pereira Silima kulia akimkabidhi kadi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) aliyekuwa Diwani wa Kata ya Pangani Mashariki (CUF) Akida Boramimi baada ya kujiunga na chama hicho juzi kwenye mkutano wa hadhara wa Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji
Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye eneo la sokoni wilayani Pangani
Katibu wa Idara ya Organization ya Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa Pereira Silima akizungumza wakati akimpokea aliyekuwa Diwani wa CUF Kata ya Pangani Mashariki Akida Boramimi kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Pangani Rajabu Abdallah
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Pangani Rajabu Abdallah akizungumza wakati wa mkutano huo wa Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji 
KATIBU Tawala wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassani Nyange akizungumza wakati wa mkutano huo
Katibu wa Idara ya Organization ya Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa Pereira Silima akivishwa skafu mara baada ya kuwasili wilaya ya Pangani
Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Pangani Mashariki Akida Boramimi(CUF) akizungumza ambapo alisema kasi na utendaji mzuri wa Rais Dkt John Magufuli umemvutia na kuamua kujiunga na CCM
MBUNGE wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji kushoto akimkabidhi vifaa vya kujikingia na jua ikiwemo kofia na vitu vingine kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa ngozi wilayani humo kiongozi wao kulia 
MBUNGE wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji kushoto akiwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Pangani Rajabu Abdallah mara baada ya kukabidhi baiskeli kwa watoto wenye ulemavu 
Sehemu ya wananchi wakimsikiliza MBUNGE wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji 



ALIYEKUWA Diwani wa Kata ya Pangani Mashariki kupitia tiketi ya chama cha Wananchi (CUF) Akida Boramini ametangaza uamuzi wa kuachana na chama hicho na kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM). 

Akida alitangaza uamuzi huo mwishoni mwa wiki mjini hapa wakati wa mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji uliofanyika eneo la Sokoni. 

Baada ya kutangaza uamuzi huo ambao uliibua shangwe na nderemo kwa wana CCM ambao walihudhuria mkutano huo na baadae kulazimika kutembea kwa maandamano mpaka zilizopo ofisi za CCM wilaya hiyo na kwenda kumkabidhi kadi. 

Diwani huyo ambaye ni mahiri kwenye kujenga hoja hususani anapokuwa kwenye vikao mbalimbali vya kimaendeleo kwenye baraza na hata vile vya kawaida alipofika kwenye ofisi hiyo alikabidhiwa kadi na Katibu wa Idara ya Organization ya Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa Pereira Silima 

Alisema kwamba kubwa ambalo limepelekea kuamua kujiunga na chama hicho ni kutokana na kasi ya utendaji ya Rais Dkt John Magufuli ya kuhakikisha wanatanzania wanapata maendeleo na ndio sababu iliyompelekea kuamua kuchukua maamuzi hayo 

“Kwa kweli Rais Dkt John Magufuli amefanya mambo mengi makubwa sana na ndio maana nimeona nimuunge mkono kwani kwenye masuala ya barabara na maji yanayopatikana hakuna haja ya kuendelea kuwa mpinzani…Lakini mimi niseme kwamba nimekuwa kada ya CUF tokea mwaka 1999 na ndio nimekabidhiwa kadi”Alisema 

“Lakini katika kuhamia CCM sijaja pekee yangu nimeambatana na wanachama wengine wa ACT akiwamo aliyekuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi (ACT) Pangani Ally Mbwaro ,Wanachama kutoka Chadema na vijana wa bodadoda Pangani lengo kubwa ni kuhakikisha tunashirikiana kwenye hali ya kuijenga Pangani mpya”Alisema 

Akida Borami ambaye ni mzaliwa wa wilaya ya Pangani alikuwa diwani wa Kata ya Pangani Mashariki (CUF) tokea mwaka 2015akimshinda aliyekuwa mpinzani wake Leopard Abeid kwa kuwa zaidi ya kura 500. 

“Nimekaa nimejitafakari kwa namna mambo ya nchi yanavyokwenda nikaona sina budi kutangaza rasmi kurudi CCM na ni sikuja pekee yangu nimekuja na wenzangu wapatao 50 hivyo ninaomba mtupokee na kututhamini “Alisema. 

Naye kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Pangani Aweso alisema kwamba serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli imefanya mambo mengi makubwa ambayo yamekuwa chachu kubwa ya maendeleo kwa watanzania. 

Alisema kwamba tokea alipochaguliwa kuwa mbunge wa Jimbo hilo ameweza kuhakikisha sekta ya elimu inaimarika wilayani humo ikiwemo kupandisha kiwango cha ufaulu kutoka kuwa wilaya ya mwisho kupanda kwenye nafasi za juu. 

Alisema pia licha ya hivyo lakini pia amesimama imara kwa kuhakikisha wanaanzisha madarasa ya kidato cha Tano na Sita hali ambayo imepelekea wanafunzi wanaofaulu kupata fursa ya kupata elimu. 

“Lakini pia niwaambie tumeweza kushghulikia kwa asilimia kubwa suala la maji ambapo mkataba wa milioni 575 umesainiwa kwa ajili ya ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya maji na utekelezaji wake umefikia asilimia 90”Alisema Mbunge Aweso ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji. 

Watanzania watakiwa kuthamini,kuenzi mila na tamaduni zao.

$
0
0


Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

Watanzania wametakiwa kuendelea kuthamini na kuzienzi mila ,desturi na tamaduni zilizopo katika jamii ili kuendelea kuziridhisha kwa vizazi na vizazi ili zisisahaulike .

Hayo yalisemwa jana na Afisa utamaduni wa mkoa wa Arusha,Irene Ngao wakati akizungumza katika siku ya tamasha la Kanono la wanaumoja wenye asili ya Karagwe na Kyelwa mkoa wa Kagera waishio Arusha.

Ngao alisema kuwa,serikali inatambua uwepo wa mila na desturi mbalimbali zilizopo katika jamii ,hivyo wanategemea ziridhishwe zaidi kwa vizazi vyetu vilivyopo na vinavyokuja ili wao waendeleze na utaratibu huo ili zisahaulike katika jamii.

"nasisitiza kila kabila liendee kuenzi tamaduni na mila zao na tuhakikishe zinatuunganisha badala ya kutogombanisha kwani serikali nayo kwa upande wake inaendelea kufundisha somo la utamaduni mashuleni ili kuhakikisha watoto wetu wanazitambua mila na desturi zilizopo ."alisema Ngao.

Naye Mwenyekiti wa umoja huo ,Wilibald Ngambeki alisema kuwa,wamekuwa na utamaduni wa kufanya tamasha hilo kila mwaka ambapo hili ni tamasha la 23 kufanyika hapa mkoani Arusha.

Alisema kuwa,lengo la kufanya tamasha hilo ni kuhakikisha watoto wanaozaliwa mjini wanazijua mila na desturi zao na kuhakikisha hazipotei .

Ngambeki alisema kuwa,kila mwaka wamekuwa wakikutana na kuonyesha tamaduni zinazofanywa na jamii hizo na kuwapa fursa watoto wao kujionea maswala mbalimbali na kujifunza ambapo kupitia tamasha hilo wataendelea kuwaridhisha watoto wao mila hizo.

"kwa kweli utamaduni ni kitu muhimu sana kwani zinasaidia sana kupunguza makali ya utandawazi badala yake jamii kuendelea kujikita katika tamaduni zao na kuacha kuiga mambo ya utandawazi ,hivyo nashauri kila kabila liendelee kuenzi ili zisipotee."alisema .

Naye mmoja wa wanachama katika umoja huo,Albert Kakulima alisema kuwa,wamekuwa wakikutana kwa lengo la kutunza mila , desturi na tamaduni zao ili zisipotee kwani asilimia kubwa ya watoto waliozaliwa huku mjini hawazijui na bila kufanya hivyo hawatazitambua na badala yake zitaendelea kupotea.

Aidha aliyataka makabila mengine kuendelea kuenzi tamaduni zao kwa kukutana mara kwa mara kwani bila kufanya hivyo zinaendelea kupotea na itabaki historia.

NI MARUFUKU WANANCHI KULIPIA NGUZO – WAZIRI KALEMANI

$
0
0
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (katikati), akikata utepe kuashiria uwashaji rasmi wau meme katika kijiji cha Loto, Kata ya Dareda, Babati Vijijini, akiwa katika ziara ya kazi Julai 28, 2019.

Na Veronica Simba – Manyara.

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, amesema wananchi hawapaswi kulipia nguzo wanapotaka kuunganishiwa umeme kwani hilo ni jukumu la Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Akizungumza kwa nyakati tofauti, jana Julai 28, 2019 akiwa ziarani katika Wilaya za Babati na Mbulu mkoani Manyara, Waziri alitoa onyo kwa mtumishi yeyote wa TANESCO atakayebainika kutomuunganishia umeme mteja aliyelipia huduma hiyo kwa kisingizio cha kutokuwepo nguzo au kumtaka alipie.

“Wananchi nchi nzima muelewe. Hampaswi kulipia nguzo,” alisisitiza na kuongeza kuwa atakayebainika kwenda kinyume na maagizo hayo ya serikali, atachukuliwa hatua za kinidhamu mara moja.

Katika hatua nyingine Waziri Kalemani alitoa hamasa kwa wananchi vijijini, katika maeneo ambayo tayari miundombinu ya umeme imefika, kulipia shilingi 27,000 tu ili waunganishiwe huduma hiyo.

Alisema Rais John Magufuli ameagiza kila mwananchi aunganishiwe umeme ndiyo kukawekwa punguzo la gharama za umeme kwa walioko vijijini ili wote wanufaike kwa kuutumia umeme katika kujiletea maendeleo.

“Kimsingi, ninyi wananchi wa vijijini mnapata umeme huu bure maana serikali imewalipia gharama zote. Hiyo shilingi 27,000 mnayotakiwa kutoa ni gharama za VAT pekee ambayo ni asilimia 18; hivyo changamkieni fursa hii iliyotolewa na serikali.”

Aidha, Dkt. Kalemani aliwataka viongozi wote wa taasisi za umma na miradi mbalimbali ya maendeleo kama vile vituo vya afya, nyumba za ibada, shule, miradi ya maji, masoko na nyinginezo, kulipia gharama hiyo ya shilingi 27,000 tu ili ziunganishiwe umeme.

Alisema kipaumbele cha Mradi wa Umeme Vijijini (REA) ni kwa taasisi za umma na miradi ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi.

Katika maeneo tofauti, Waziri aligawa vifaa vya Umeme Tayari (UMETA) kwa wananchi, hususan wenye hali duni kwenye jamii alizotembelea, na kutoa maelekezo kuwa waunganishiwe umeme mara moja.

“Ndugu zangu, lengo la serikali ni kuona kila nyumba ya mtanzania inafikiwa na umeme bila kujali aina yake. Nataka hawa watu waunganishiwe umeme ili nao wafurahie matunda ya uchapakazi wa Rais wetu kama ilivyo kwa wengine.”

Waziri alimwagiza Mkandarasi wa REA kuhakikisha anagawa vifaa vya UMETA kwa wananchi katika maeneo yote anayounganisha umeme, kadri ya maelekezo ya serikali pamoja na kuwaelimisha wananchi kuwa vifaa hivyo hutolewa 250 kila eneo na vikiisha wananchi watavinunua kwa gharama ndogo ya shilingi 36,000 tu.

Akielezea matumizi yake, alisema vifaa vya UMETA hutumika kumfungia mteja umeme kwenye jengo dogo lisilozidi vyumba vinne, pasipo kulazimika kutandaza nyaya ambazo ni gharama kubwa.

Wakizungumza katika ziara hiyo ya Waziri, viongozi mbalimbali wa wananchi walipongeza kazi ambayo imekuwa ikifanywa na Wizara ya Nishati, na kusema Waziri Kalemani na watendaji wengine wote wamekuwa wakimwakilisha Rais Magufuli vyema.

Mbunge wa Babati Mjini, Paulina Gekul na Diwani wa Kata ya Dareda, Wilaya ya Babati, Eluthery Burra, ambao awali walikuwa vyama vya siasa tofauti na Chama Cha Mapinduzi (CCM), walikiri hadharani kuwa wamelazimika kurudi CCM kutokana na utendaji kazi wa Rais na watendaji wake.

Katika ziara hiyo, Waziri alitembelea vijiji vya Chemchem, Nangara Kati, Gendi Kuu, Loto, Gabadaw, Gwaami, Hayloto na Ayakule vilivyopo Babati na Mbulu.

Moja ya nyumba zilizowashiwa umeme na Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani alipokuwa kwenye ziara ya kazi, wilayani Babati, Mkoa wa Manyara Julai 28, 2019.
Sehemu ya umati wa wananchi wa kata ya Murray, wilayani Mbulu, Mkoa wa Manyara, wakipunga mikono kumsalimu Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, aliyefika eneo hilo kuzungumza nao akiwa katika ziara ya kazi, Julai 28, 2019.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akielezea manufaa ya kifaa cha Umeme Tayari (UMETA) kwa wananchi wa Kijiji cha Ayakule, Kata ya Ayamohe, wilayani Mbulu; baada ya kuwagawia vifaa hivyo bure ili wavitumie kuunganishiwa umeme katika nyumba zao. Waziri alikuwa katika ziara ya kazi, Julai 28, 2019.
Baadhi ya wataalam kutoka Wizara ya Nishati, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), wakimsikiliza Waziri mwenye dhamana na sekta hiyo, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani), alipokuwa akizungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Babati (hawapo pichani), akiwa katika ziara ya kazi, Julai 28, 2019.

Serikali imejenga Miundombinu kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma bora-Askofu Maboya

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV

Serikali imetengeneza miradi mbalimbali katika kuhakikisha jamii inapata huduma bora.

Hayo aliyasema Askofu Mkuu wa Kanisa la Calvary Assemblies of God (C.A.G) Ubungo Dunstan Maboya wakati wa Jubilee ya Miaka 25 ya Kanisa hilo.

Askofu Maboya amesema kuwa serikali inakwenda katika kuandaa mkutano wa Nchi zilizopo Kusini Mwa Afrika (SADC) ambapo Tanzania itanufaika na mkutano huo katika katika adhima ya kwenda uchumi wa Kati wenye Viwanda.

Amesema kuwa nchi imepiga hatua katika Ujenzi wa Barabara, Reli za Kisasa pamoja na ununuzi wa ndege ambapo inafanya watanzania kutembea kifua mbele.

Aidha amesema kuwa wananchi kama watu wa imani wanajifunia huduma zinazotolewa na serikali ikiwa na pamoja na wao kujenga huduma za jamii zikiwemo Hospitali pamoja na Shule.

Askofu amesema wakati wanaanzisha Kanisa hilo watu walijitoa kwa fedha zao kuhakikisha neno la Mungu linasimama .Askofu Maboya amesema kumtumikia Mungu sio lelema ni lazima uwe na imani kwani wengine walipoanzisha Kanisa hilo hawakuendelea lakini Kanisa linasimama na kufikisha miaka 25.

Katika maadhimisho hayo yalikuwa na maandamano ya kumtukuza Mungu pamoja na kuangaza amani ya nchi.Nae Mchungaji wa Kanisa hilo Emelda Maboya amesema kwa hatua walifikia wanamshikuru Mungu katika kusimamisha injili katika Kanisa hilo.

Amesema haikuwa kazi ndogo katika kujitoa kwa waumini katika Ujenzi wa Kanisa pamoja na wachungaji na maaskofu kutangaza neno la Mungu.

Kwa upande wa Askofu Msaidizi wa Jimbo la Dar es Salaam wa Kanisa hilo Jonathan Shemhambu amesema kuwa miaka 25 ya Kanisa ni neema ya Mungu kwani walianza wakati Mugumu katika kufikisha neno la Mungu lakini sasa matokeo yamekuwa mazuri katika kujenga imani kwa waumini.
 Waumini wa Kanisa la Calvary Assemblies of God wakiwa katika maandamano Jubilee ya Miaka 25  ya Kanisa hilo  Ubungo jijini Dar es Salaam.
 Askofu Mkuu wa Kanisa la Calvary Assemblies of God (C.A.G) Ubungo Dunstan Maboya akizungumza katika ibada ya Jubilee ya Miaka 25 ya Kanisa hilo jijini Dar es Salaam.
 Askofu Msaidizi wa Kanisa la Calvary Assemblies of God (C.A.G) Jonathan Shemhambu akizungumza namna walivyotumikia katika kutangaza injili ya Mungu katika Kanisa hilo hadi kufikia Jubilee ya Miaka 25.
Mchungaji wa Kanisa la Calvary Assemblies of God (C.A.G) Emelda Maboya akitoa maelezo kuhusiana na Jubilee ya Miaka 25 ya Kanisa hilo.

MADIWANI WAMKATAA MKURUGENZI WA MANISPAA YA SHINYANGA..WADAI ANAWACHONGANISHA NA WAPIGA KURA

$
0
0

Na Marco Maduhu na Suleiman Abeid - Malunde1 blog

Madiwani katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wakiongozwa na madiwani wa CCM wamemkataa mkurugenzi wa manispaa hiyo, Geofrey Mwangulubi kwa madai ya kushindwa kutekeleza maagizo mbalimbali yanayotolewa kila mara na madiwani hao hivyo.

Madiwani hao wamedai tabia ya mkurugenzi kushindwa kutekeleza maagizo wanayoyatoa katika vikao huenda ikawachonganisha na wapiga kura wao kutokana na kutokuwepo kwa miradi yoyote ya maendeleo inayotekelezwa katika kata zao. 

Hali hiyo imejitokeza leo Jumatatu Julai 29, 2019 katika kikao cha kawaida cha baraza la madiwani wakati madiwani hao wakithibitisha agenda zilizopangwa kujadiliwa ambapo diwani wa kata ya Ndembezi David Nkulila (CCM) alisimama na kuzikataa ajenda hizo na kisha kutoa hoja yake ya kutokuwa na imani na mkurugenzi Mwangulumbi. 

Hoja ya diwani Nkulila iliungwa mkono na baadhi ya madiwani ambapo hata hivyo, Katibu Tawala Msaidizi wa mkoa wa Shinyanga (Serikali za mitaa),Alphonce Kasanyi , na mwanasheria wa manispaa hiyo, Doris Dario walisimama na kuwataka madiwani kusitisha maamuzi yao kwa vile yanapingana na utaratibu. 

Kasanyi alisema madiwani walipaswa waitishe kikao maalumu cha kutokuwa na imani na mkurugenzi pamoja na kumwandikia barua mkuu wa mkoa kuhusu kumkataa mkurugenzi huyo. 

Hata hivyo, ushauri wa Katibu Tawala msaidizi mkoa wa Shinyanga,Alphonce Kasanyi na mwanasheria wa manispaa ya Shinyanga, Doris Dario haukusikilizwa na madiwani na badala yake baadhi yao walisimama na kuchambua kwa kina baadhi ya maagizo yaliyowahi kutolewa na baraza la madiwani na mkurugenzi kushindwa kuyatekeleza kitendo ambacho walidai ni dharau na hawatakuwa tayari kuendelea kufanya naye kazi.

Diwani wa viti maalumu, Shella Mshendate alisema hawako tayari kuendelea kufanya kazi na mkurugenzi anayeitwa Geoffrey Mwangulumbi na kitendo chao hakimaanishi kuvunja baraza bali hawamtaki mtu, na siyo mkurugenzi ambapo alimuomba Naibu Meya atafute mtaalamu mwingine akae kwenye kiti cha mkurugenzi na kikao kiendelee.

Naye diwani wa kata Kambarage ,Hassan Mwendapole (CCM) naye aliunga hoja ya kutokuwa na imani na mkurugenzi huyo kutokana na kushindwa kutekeleza maazimio yao hali inayofanya madiwani kutokuwa na miradi ya maendeleo kwenye kata zao hivyo kuonekana kutoa ahadi kwa wananchi ambao ni wapiga kura wao. 

Diwani wa kata ya Kizumbi Ruben Kitinya (CCM) alisema hawezi kuendelea kufanya kazi na mkurugenzi huyo kwani yale wanayojadili kwenye baraza na kamati mbalimbali hayatekelezwi hivyo hana imani na mkurugenzi huyo. 

Pamoja na vitisho vya kuvunjwa baraza na kufanyika kwa uchaguzi mpya vilivyotolewa na mwakilishi wa katibu tawala msaidizi, kwamba kitendo chao cha kumkataa mkurugenzi kinamaanisha kuvunjwa kwa baraza, bado madiwani walisimama na msimamo wao wa kumkataa mkurugenzi ambapo walivua majoho na kutoka nje ya kikao. 

Kwa upande, mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi amesema hivi sasa hawezi kuzungumza chochote kuhusu maamuzi hayo ya madiwani hao ya kutokuwa na imani naye hivyo anasubiri maamuzi kutoka ngazi za juu.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter,Diwani wa kata ya Ngokolo,Emmanuel Ntobi( CHADEMA) ambaye alishasimamishwa kuhudhuria vikao vya baraza la madiwani kutokana na tabia ya kukosoa utendaji kazi wa mkurugenzi huyo,amewapongeza madiwani wa manispaa hiyo kwa kumkataa mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi.
Awali Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulubi akisoma ajenda za kikao cha baraza la madiwani,kabla baraza la madiwani halijavunjika - Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog
Madiwani wakipitia ajenda za kikao kabla ya kuvunjika kwa kikao cha baraza la madiwani.
Watendaji wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao kabla hakijavunjika 
Diwani wa kata ya Ndembezi (CCM) David Nkulila akizungumza kwenye kikao hicho ambapo alizikataa agendaza kikao na kisha kutoa hoja yake ya kutokuwa na imani na mkurugenzi Mwangulumbi. 
Diwani wa kata ya Ndembezi (CCM) David Nkulila akivua joho kutoka nje kutokana na kutokukubaliana na ajenda za kikao. 
Diwani wa Viti Maalumu,Maria Nyangaka akiwa amevua joho kuunga mkono hoja ya madiwani kutokuwa na imani na mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga,Geofrey Mwangulumbi.
Diwani wa kata Kambarage ,Hassan Mwendapole (CCM) akiunga hoja ya kutokuwa na imani na mkurugenzi huyo kutokana na kushindwa kutekeleza maazimio yao hali inayofanya madiwani kutokuwa na miradi ya maendeleo kwenye kata zao hivyo kuonekana kutoa ahadi kwa wananchi ambao ni wapiga kura wao. 
Diwani wa kata ya Kizumbi Ruben Kitinya (CCM) akiunga hoja. Alisema hawezi kuendelea kufanya kazi na mkurugenzi huyo kwani yale wanayojadili kwenye baraza na kamati mbalimbali hayatekelezwi hivyo hana imani na mkurugenzi huyo. 
Katibu Tawala Msaidizi wa mkoa wa Shinyanga (Serikali za mitaa),Alphonce Kasanyi akizungumza ambapo alisema madiwani walipaswa waitishe kikao maalumu cha kutokuwa na imani na mkurugenzi pamoja na kumwandikia barua mkuu wa mkoa kuhusu kumkataa mkurugenzi huyo. 
Mwanasheria wa manispaa ya Shinyanga Doris Dario akiwataka madiwani kusitisha maamuzi yao kwa vile yanapingana na utaratibu. 
Madiwani wakitoka ukumbini baada ya kikao cha baraza la madiwani kuvunjika. 
Madiwani wakitoka ukumbini. 
Madiwani wakitoka ukumbini 
Madiwani wakitoka ukumbini .Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog

WAZIRI MKUU ASHIRIKI MAZISHI YA BIBI SALMA KALENJE WILAYANI RUANGWA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishirikiana na waombolezaji kubeba jeneza katika mazishi ya Bibi Salima Yusuf Kalanje yaliyofanyika kwenye kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa Julai 29, 2019. Wapili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Ruangwa, Hashim Mgandilwa.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiweka udongo kaburini wakati aliposhirika katika mazishi ya Bibi Salima Yusuf Kalanje kwenye kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa, Julai 29, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wazee wakati aliposhiriki katika mazishi ya Bibi Salima Yusuf Kalanje kwenye kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa, Julai 29, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

CAF YATEUA WAAMUZI WANNE, MAKAMISHNA WAWILI KUTOKA TANZANIA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua Waamuzi Waanne na Makamishna Wawili kutoka Tanzania kusimamia mechi za Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho.

Mwamuzi Hery Sasii atasimama katikati kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa kati ya Aigle Noir ya Burundi na Gor Mahia ya Kenya utakaochezwa Uwanja wa Prince Louis Rwagasore,Burundi Agosti 11,2019.

Sasii atasaidiwa na Mwamuzi msaidizi namba 1 Frank Komba,Mwamuzi msaidizi namba 2 Ferdinand Chacha,Mwamuzi wa Akiba Emmanuel Mwandembwa na Kamishna wa mchezo anatokea Rwanda,Gaspard Kayijuka.

Aidha Mtanzania Ahmed Mgoyi atakua Kamishna wa mchezo wa marudiano Ligi ya Mabingwa Gor Mahia dhidi ya Aigle Noir utakaochezwa kati ya Agosti 23,24 na 25 nchini Kenya.

Naye Mtanzania Khalid Abdallah ameteuliwa kuwa Kamishna wa mchezo wa Kombe la Shirikisho kati ya Proline FC ya Uganda na Master Security Services ya Malawi utakaochezwa Uwanja wa Kampala Startimes nchini Uganda.

TATIZO LA MAJI CHALINZE KUWA HISTORIA,SERIKALI YAPELEKA MRADI WENYE THAMANI YA BILIONI 16.

$
0
0
 Afisa Mtendaji Mkuu DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja ametembelea mradi wa kupeleka Majisafi na salama katika mji wa Chalinze wenye thamani ya Bilioni 16 unaotarajiwa kumalizika mwezi Aprili 2020. Amewahakikishia wakazi wa Chalinze  tatizo la Maji  katika mji wao kubaki kuwa historia.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja  ametembelea mradi wa maji wa Chalinze Mboga utakaomalika mwezi April 2020.


Mradi huo wa kimkakati wa kupeleka majisafi na salama katika mji wa Chalinze hadi kiwanda cha kusindika matunda cha sayona unaojengwa na DAWASA kwa thamani ya Shilingi Bilioni 16.

Luhemeja ameridhishwa na hatua iliyofikiwa na mkandarasi ambapo kwa sasa ulazaji wa mabomba ya kusafirishia maji yameshalazwa.

Aidha, Luhemeja amewakikishia wakazi wa chalinze kwamba mradi huo utamalizika mwezi april mwaka ujao na kufanya tatizo la maji  katika mji wa Chalinze kubaki kuwa historia.Kukamilika kwa mradi huo kutahudumia maeneo ya  Ruvu darajani, Vigwaza,Ranchi ya Taifa Ruvu (NARCO), Chahua -Lukenge, Visenzi, Buyuni na Mdaula -Unebazomozi.

Kwingine ni Chamakweza, Pingi, Pera, Chalinze, Chalinze Mzee, Msoga na Mboga aidha, viwanda vitakavyofaidika ni pamoja na Twyford, kiwanda cha ngozi, kiwanda cha Matunda cha Sayona pamoja na watumiaji wengine wakubwa ikiwemo kampuni Yapi Merkezi wajenzi reli ya kisasa (SGR)
Viewing all 109936 articles
Browse latest View live




Latest Images