Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

WAJASIRIAMALI MIRERANI WAJENGEWA UWEZO

$
0
0
Mmoja kati ya wakurugenzi wa asasi ya Mirerani Tanzanite Mining Tourism ya Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Nuru Mkirery akizungumza kwenye mafunzo ya ujasiriamali.

Mmoja kati ya wakurugenzi wa asasi ya Mirerani Tanzanite Mining Tourism, Charles Mnyalu akizungumza katika semina hiyo.
………………….
WAJASIRIAMALI 50 wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wametakiwa kuwa wabunifu kwa kuandaa vitu vitakavyokuwa endelevu kwa jamii na siyo kupoteza muda kwa kuiga biashara zisizo na tija.

Mtaalamu wa saikolojia wa jijini Arusha, Joseph Mrindoko aliyasema hayo wakati akiwajengea uwezo wajasiriamali hao 50 kwenye ukumbi wa Mazubu Grand Hotel mji mdogo wa Mirerani.

Mrindoko alisema wajasiriamali wanapaswa kutambua kuwa wanatakiwa kufanya kazi kupitia maono ya mioyo yao tangu utotoni kwani ndiyo watapata mafanikio.

Alisema kanuni za maisha zinaeleza kuwa usipofanya chochote hautapata chochote na kadiri unavyofanya ndiyo utakavyopata hivyo wasibweteke kwenye maisha yao.

“Akili ya binadamu ina sehemu tatu tuzitumie zote na ukiwa duniani hakikisha unaacha alama tusilale mchana mfano mimi huu mwaka wangu wa nane nalala kwa muda wa saa nne pekee kwa siku na wala sijaugua ugonjwa wowote,” alisema Mrindoko.

Mmoja kati ya wakurugenzi wa asasi ya Mirerani Tanzanite Mining Tourism, Charles Mnyalu alisema kupitia mafunzo hayo wajasiriamali hao wataongeza uelewa ili wajinufaishe wao wenyewe na jamii kwa ujumla.

Mnyalu alisema wao kama Mirerani Tanzanite Mining Tourism wamedhamini mafunzo hayo kwa lengo la kuwajengea uwezo ili kuwanyanyua kiuchumi wajasiriamali hao pindi wakizingatia elimu waliyoipata.

Mkurugenzi mwenza wa asasi hiyo Nuru Mkirery alisema mafunzo hayo yametolewa bila malipo kwa lengo la kuwajali wajasiriamali hao ili wachangamkie fursa mbalimbali zilizopo.

“Mwalimu Mrindoko amewafundisha wajasiriamali hawa watoke kwenye duara walilopo na kufikiria nje ya hapo kwani binadamu akitumia akili aliyonayo ambayo ni rasilimali aliyonayo anaweza kunufaika maishani mwake,” alisema Mkirery.

Mmoja kati ya wajasiriamali walioshiriki mafunzo hayo Hamis Seif alisema yeye anatengeneza na kuuza mabegi na amefaidika kwa elimu hiyo ikiwemo kuwekeza kwenye muda na kusimamisha jua.

“Katika mafunzo haya nimejifunza pia umuhimu wa kuwa mtanashati kwani mara nyingi watu wanakihukumu kitabu kutokana na muonekano wa jalada lake na siyo kurasa zilizo ndani yake hivyo tunapaswa kubadilika,” alisema.

Mjasiriamali wa mboga Zainabu Mussa alisema amefaidika na mafunzo hayo kwa kutakiwa kuwajali wateja na kuthamini biashara yake ikiwemo kuiboresha kwa kuwafikishia majumbani kuliko kuwasubiri gengeni.

HALMASHAURI YA MERU YAFANIKIWA KUPUNGUZA VIFO VYA MAMA NA MTOTO

$
0
0
Wafanyakazi hospitali ya Wilaya ya Meru, watendaji na wadau wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya Jerru Muro (hayupo pichani), wakati wa uzinduzi wa kampeni ya jiongeze tuwavushe salama katika ukumbi wa Halmashauri ya Meru.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro akisaini hati ya kiapo kati yake Mkuu wa Wilaya ya Maafisa Tarafa wa tarafa za Mbuguni, Poli na King’ori kuhakikisha kampeni ya kuzuia vifo vya Mama na Mtoto vinafanikiwa. Aliyesimama nyuma wa tatu kutoka kushoto ni Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Meru, Dkt Maneno Focus.
Wafanyakazi hospitali ya Wilaya ya Meru, watendaji na wadau wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya Jerru Muro (hayupo pichani), wakati wa uzinduzi wa kampeni ya jiongeze tuwavushe salama katika ukumbi wa Halmashauri ya Meru.
Wafanyakazi hospitali ya Wilaya ya Meru, watendaji na wadau wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya Jerru Muro (hayupo pichani), wakati wa uzinduzi wa kampeni ya jiongeze tuwavushe salama katika ukumbi wa Halmashauri ya Meru.


Na Seif Mangwangi , Michuziblog, Arusha 

SERIKALI wilayani Arumeru imefanikiwa kupunguza vifo vya Mama na Mtoto kufuatia kuboresha huduma za afya wilayani humo ikiwemo dawa na vifaa muhimu vinavyotumika wakati Mama anajifungua. 

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni maalum ya Kitaifa ya kuzuia vifo vya Mama na Mtoto inayojulikana kwa jina la ‘ Jiongeze, tuwavushe Salama’, iliyofanyika katika ofisi za Halmashauri ya Meru, Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo Wilayani Arumeru Dkt. Maneno Focus alisema huduma hizo zimeboreshwa kwa asilimia 98. 

“Katika Wilaya yetu tunataka kutokomeza kabisa vifo vya Mama na Mtoto na tunafanya hivi kwa vitendo, katika kipindi cha Januari hadi Juni 2019 tumepata vifo viwili pekee vya Watoto ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2018 ambapo watoto 5 walikuwa wamefariki,”alisema 

Amesema pamoja na takwimu hizo bado kumekuwa na changamoto ya upatikanaji wa taarifa sahihi na kwa wakati kutoka kwenye jamii hususani kwa wazazi ambao hawafiki kwenye vituo vya afya kwaajili ya kupata huduma. 

Dkt Maneno alisema kampeni hiyo imelenga kuongeza uwajibikaji wa viongozi wa kisiasa, kidini, kijamii na wadau wote kuwajibika na kuhakikisha vifo vya Mama na Mtoto vinadhibitiwa na kufuatiliwa na kila mmoja kushiriki kuvizuia. 

“Halmashauri ya Meru inatarajia kuongeza huduma jumuishi za Kujifungulia (CeMonc), katika kituo cha afya cha USA – RIVER, ambacho majengo ya huduma muhimu yamekamilika, tunaamini hadi kufikia mwakani hakutakuwa na vifo vya Mama wala Mtoto wilayani kwetu,”anasema. 

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro anasema Wilaya ya Arumeru imeazimia kuboresha huduma za Afya na mikakati iliyopo ni kuhakikisha kila kata inakuwa na kituo cha afya na kila kijiji kinakuwa na zahanati. 

Muro aliwaagiza viongozi wa Hospitali ya Meru kutoa matangazo ya katazo la watendaji wa afya hospitalini hapo kutumia simu wakati wa kazi na kuwataka kutumia lugha nyenyekevu kwa wagonjwa na kwamba kwa kufanya hivyo utekelezaji wa kauli mbiu ya kampeni hiyo ya ‘jiongeze tuwavushe salama’ itakuwa imetekelezwa vizuri. 

KYAURI VOICE ILIVYOCHANUA HADI KUPOTEA.

$
0
0

Na Moshy Kiyungi,Tabora.

Bendi ya Kyauri Voice Orchestra ilivunja rekodi ya kudumu kwa kipindi kifupi katika ‘game’ la muziki licha ya kuwa amaarufu kwa upigaji wake.

Bendi hiyo ilikuwa na makao yake makuu katika baa ya Mpakani iliyokuwa Mwenge jijini Dar es Salaam. Kyauri Voice ilikuwa ikipiga muziki kwa mtindo wa ‘Mwendo wa Jongoo’

Waliporomosha vibao ‘matata’ sana vilivyowakuna baadhi ya washabiki na wapenzi wa muziki katika jiji hilo, vikiwemo vya ‘Bangungi ee Nakobelela’, Mwaka wa Watoto na Tondo ulitungwa na Mukumbule Lolembo ‘Parashi’.

Ilikuwa imesheheni wanamuziki wakubwa we

nye vipaji vikubwa katika muziki. Baadhi ya wanamuziki hao ni Monga Stanie aliyekuwa akicharaza gitaa la solo na kuimba, Khatibu Itetei aliyekuwa akipuliza saxophoni, Kabaa Belela aliyekuwa akiliungurumisha gitaa zito la besi na Kawele Mutimanwa kwenye gitaa la solo.

Katika safu ya uimbaji bendi hiyo ilikuwa na mtunzi na mwimbaji Mukumbule Lolembo ‘Parash’

Nguli huyo vilevile alijulikana kama Eugine, ambaye alijiunga katika bendi hiyo akitokea katika bendi ya Orchestra Bana Ngenge, iliyofanya ziara humu nchini mwishoni mwaka 1978, hatimaye ikavunjika.

Alikuwa Khatibu Itetei alipoibua ‘dili’ la kuanzisha bendi hiyo ya Kyauri Voice.Wakati wakiporomosha nyimbo, waalikuwa wa rap “Kata kata kata kata mwendo wa Jongooo pamoja na vumbi nyuma”.

Bendi hiyo licha ya kuwa na mtunzi na mwimbaji mahiri aliyepata sifa lukuki Barani Afrika, Moreno Batamba, alisambaratika baada ya kipindi kifupi mno.Moreno Batamba aliaga dunia mwaka 1993 akiwa nyumbani kwake huko Dandora estate, jijini Nairobi nchini Kenya.

Wakati wa uhai wake alitamba na nyimbo nyingi ukiwemo uliompa sifa ndefu wa ‘Pili Muswahili’.Wimbo wake wa mwisho alitunga kabla ya kifo chake ulikuwa wa ‘Vidonge sitaki’ wa mwaka 1983.

Sababu kubwa ya kusambaratika kwa bendi hiyo ilikuwa mmiliki wa bendi ya Kyauri Voice ni kutokuelewana na wanamuziki wake.Wanamuziki wa bendi hiyo ya Kyauri Voice, walikuwa ni raia toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wakati huo Zaire.

Kwa kulikuwepo na bendi mbili Maquis du Zaire na Safari Soud (OSS) zilizokuwa na wanamuziki wengi toka huko DRC, baadhi ya wanamuziki hao walikwenda kujiunga katika benadi hizo.

Mwanamuziki Monga Stinie alikwenda kujiunga katika bendi ya Safari Sound, Batii Osie Senga, Labaa, mwanamuziki aliyejulikana kama Cobra na Biliumbu na wengine kadhaa.

Kawele Mutimanwa akachepukia katika mji wa Bujumbura nchi Burundi baadaye alirejea tena nchini humu akajiunga katika bendi za MK. Group na Tancut Alimasi. Hivi sasa Kawele amefanya makazi yake katika jiji la London nchini Uingereza.

Baada ya bendi ya Kyauri Voice kusambaratika wanamuziki wengine wakaenda kujiunga katika bendi ya Super Matimila, iliyokuwa ikiongozwa na Ramadhani Mtoro ‘Dk. Remmy Ongalla.

Dk.Remmy Ongala naye alizaliwa mwaka 1947 katika mkoa wa Kivu huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mwaka 1947. Mukumbule alichukuliwa katika bendi ya Maquis du Zaire, iliyokuwa ikiporomosha muziki wake katika ukumbi wa White House, Ubungo jijini Dar es Salaam.

Parashi alichukuliwa ka minajiri ya kuziba pengo lililoaca wazi na Kikumbi Mwanza Mpango ‘King Kiki’ aliyekuwa amekwenda kujiunga katika bendi ya OSS.

Hapo Maquis, alijumuika na safu kamambe ya watunzi na waimbaji akina Mbuya Makonga ‘Adios’, Mutombo Lufungula ‘Audax’ na Abubakar Kasongo Mpinda ‘Clyaton’.

Wengine ni pamoja na Kasalo Kyanga na Tshimanga Kalala Assosa wakiongozwa na kiongozi wao Tshinyama Tshiayaza.Baada ya kipindi kifupi wakaenda kurekodi albamu yao katika studio ya RTD, wakati huo.

Katika albam hiyo kulikuwa na nyimbo za Kiongo, Maiga, Zoa Pondamali na nyingine nyingi.Albam hiyo hadi sasa ni miongoni mwa kazi zenye kiwango cha hali ya juu kulichoakuliwa wakati huo.

Maquis du Zaire katika albam hiyo, aliwatumia wanamuziki kujipanga katika uimbaji na jinsi walivyowatuamia wanamuziki wa Tanzania Mafumu Bilal ‘Bombenga’, Abdallah Kimeza walikuwa wakipuliza saxophone.

Mafumu Bilal yupo hai anamiliki bendi yake binfasi, Abdallah Kimeza alikwisha tangulia mbele za haki.Aidha wanamuziki Matei Joseph, Steven Kaigilila Mauffi, Majengo Bakari na mwimbaji Tabia Mwanjelwa nao waliungana na Wakongo hao.

Matei Joseph hivi sasa namiliki bendi yake ya African Minofu, Steven Kaigilila Mauffi, ni mcharazaji wa gitaa la rhythm katika bendi ya Mlimani Park, Majengo Bakari alikuwa katika bendi ya Shikamoo Jazz na Tabia Mwanjelwa aliachana na muziki baada ya kuolewa nchini Ujerumani.

Parashi miaka ya karibuni alikuwa jijini Mwanza akifayakazi ya muziki katika bendi ya Kamanyola, akishirikiana vema na mtuzi na mwimbaji Benno Villa Anthony na Mkuna Roy ‘Mukuna wa Mukuna’ hivi sasa ni marehemu.

Kama ambavyo baadhi ya wanamuziki hususan wa zamani, Parashi naye ametamka kuwa muziki wa dansi haujafa, ila ukosefu wa promosheni katika muziki wa dansi, ikiwemo kwa baadhi ya vituo vya redio kutokuthamini muziki huo pia makampuni yaliyopo hivi sasa imewapa kisogo.

Ni imani yake kuwa muziki huo unaweza kurejea katika nafasi yake iwapo utathaminiwa kama zamani hasa ikizingatiwa kuwa wataalamu wa muziki wa dansi bado wapo ambao wangeweza hata kuwafunza vijana wa sasa kupiga muziki.

SIKU YA UREMBO WA ASILI TANZANIA KURINDIMA KESHO VIWANJA VYA LIFE PARK-MWENGE JIJINI DAR

$
0
0

Tamasha la Urembo wa Asili Tanzania kufanyika kesho Jumamosi na keshokutwa jumapili Viwanja vya life park mwenge ilipo Maisha club ,zamani Sinema mwenge. 

Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mh Naibu waziri wa Habari , Utamaduni, sanaa na michezo Bi Juliana shonza .

Tamasha hili litakua na faida kwa kila atakefika bila gharama yoyote itatolewa huduma ya vipimo vya kansa ya Titi pamoja elimu ya kansa na magonjwa ya ngozi bure kutoka kwa wataalam Ocean Road

Vile vile kutakua na mafunzo ya ujasiriamali utengezaji wa sabuni za maji za kuogea ( shampoo ) bure kutoka kwa mjasiriamali na mwalimu Bi. Ester Mgonja bure siku ya jumapili .

Burudani itaongozwa na Malkia wa Taarabu Khadija Kopa pamoja na Aneth kushaba, mtangazaji na mjasiriamali Dina Marious na Sakina Lyoka watakuwepo , wasanii mwasiti, Grace matata, mchekeshaji jaymond watakuwepo na Rose Ndauka atakuwepo, kutakua Fashion show na burudani ya muziki ya kutosha. 

Sherehe za Urembo wa asili zitaambatana na kutoa zawadi kwa wanawake 300 watakaofika wa kwanza viwanja ni hapo kujipatia zawadi ya pakti moja ya Pedi ya kutoka Belle Bure.

Njoo ukutane na Wajasiriamali wa bidhaa za Urembo wa ngozi na nywele na bidhaa zingine kuanzia asubuhi saa 2 hadi saa 12 jioni. Vyakula na vinywaji vitapatikana pia. 

Urembo wa Asili sio ushamba .
@tanzanianaturalbeautyday
@missmandoza

Naibu Waziri Aweso amsimamisha kazi mkandarasi Geita

$
0
0
Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akikagua ujenzi wa Mradi wa Maji wa Inchwankima-Imalabupina wilayani Chato, mkoa wa Geita.
Mradi wa Maji wa Inchwankima-Imalabupina ambao ujenzi wake umefikia asilimia 80 katika Wilaya Halmashauri ya Wilaya ya Chato, mkoani Geita.
Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akiwa juu ya tenki la maji la Mradi wa Maji wa Inchwankima-Imalabupina wilayani Chato, mkoa wa Geita.
Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akishuka mara baada ya kukagua ujenzi wa Mradi wa Maji wa Inchwankima-Imalabupina wilayani Chato, mkoa wa Geita.
Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akiwa kwenye pampu za kusukumia maji za Mradi wa Maji wa KIkumbaitale wilayani Chato, mkoa wa Geita.
……………….
Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amemsimamisha kazi Mkandarasi; Kampuni ya Ndeenengo Senguo Ltd kwa kushindwa kukamilisha Mradi wa Maji wa Inchwankima-Imalabupina katika Wilaya ya Chato, mkoani Geita kwa wakati, licha ya kuahidi mbele ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa kuwa angekamilisha kazi hiyo mwezi Februari, mwaka huu.

Naibu Waziri Aweso ameelekeza wakati Mkandarasi huyo amesimamishwa, Halmashauri ya Wilaya ya Chato ifanye taratibu za kuvunja mkataba na mkandarasi huyo na timu ya wataalam kutoka Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) na Geita (GEUWASA) pamoja na Wakala ya Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Geita washirikiane kukamilisha kazi zilizobaki na mradi uanze kufanya kazi.

Aweso amesema mkandarasi huyo hana uwezo wa kukamilisha mradi huo ambao umeanza Mei 12, 2017 na ulitarajiwa kukamilika Mei 11, 2018, akashindwa kuukamilisha pamoja na kupewa nyongeza ya muda mara mbili na sasa ameomba kwa mara ya tatu. Akisisitiza jambo hilo halivumiliki na amechukua maamuzi hayo kwa faida ya wananchi 59, 609 waishio katika Halmashauri ya Wilaya ya Chato.

Wakazi wa Kijiji cha Nyamirembe wamemshukuru Naibu Waziri wa Maji kwa hatua aliyochukua kwa kuwa walishapoteza matumaini kutokana na ahadi hewa za mkandarasi huyo, wakisema uamuzi huo umewapa imani kuwa mradi huo utakamilika na kuanza kufurahia huduma ya maji wanayoisubiri kwa muda mrefu.

Utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Inchwankima-Imalabupina umefikia asilimia 80 kwa kazi ya ujenzi wa miundombinu ya maji na asilimia 100 kwa kazi ya ulazaji wa mabomba. Mradi utakapokamilika utagharimu kiasi cha Shilingi bilioni 8.3 na wakazi 59,609 katika vijiji 11 vya Nyamirembe, Kalebezo, Nyambiti, Busalala, Imalabupina, Inchwankima, Kachwamba, Idoselo, Ipandikilo, Mwangaza na Igarula watapata huduma ya majisafi na salama.

BILIONI 600 ZIMETUMIKA KATIKA MPANGO WA MKUE KUBORESHA ELIMU KWENYE MIKOA TISA NCHINI

$
0
0

Waziri wa Nchi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo akiwahutubia wafanyakazi mkoani Tabora wakati wa kikao cha tathmini ya ziara yake katika wilaya za Tabora ,Nzega na Igunga,kukagua shule shikizi. 
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akitoa maneno ya utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo ili azungumze na wafanyakazi mkoani Tabora wakati wa kikao cha tathmini ya ziara yake katika wilaya za Tabora ,Nzega na Igunga,kukagua shule shikizi. 

Baadhi ya Viongozi na watumishi Mkoani Tabora wakimsikiliza hivi karibuni Waziri wa Nchi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo wakati wa kikao cha tathmini ya ziara yake katika wilaya za Manispaa ya Tabora ,Nzega na Igunga,kukagua shule shikizi. 
Mkuu wa Wilaya ya Igunga John Mwaipopo akitoa taarifahivi karibuni kwa Waziri wa Nchi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo (wa pili kutoka kushoto) wakati wa kikao cha tathmini ya ziara yake katika wilaya za Tabora ,Nzega na Igunga,kukagua shule shikizi. 
………………………. 
NA TIGANYA VINCENT 

SERIKALI imeipongeza Uingereza,kwa msaada wake katika sekta ya elimu ambapo imetoa zaidi ya Sh 600 bilioni kwa ajili ya kutekeleza Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania (MKUE). 

Kauli hiyo imetolewa jana na Waziri wa Nchi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo wakati wa kikao cha tathmini ya ziara yake katika wilaya za Nzega na Igunga,kukagua shule shikizi. 

Alisema kuwa Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania (MKUE) ambao uliokuwa unafadhiliwa na Wizara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza,DFID umefanya kazi kubwa ya kuboresha elimu, miundombinu na kuboresha mazingira ya kujifunza kwa wanafunzi. 

Jafo alisema mradi huo umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa kujengwa miundombinu bora na wanafunzi kusoma katika mazingira rafiki na kuwapunguzia adha ya watoato kutembea umbali mfupi tofauti na zamani walipokuwa wakitembea umbali mrefu. 

Aliitaka miradi inayoachwa na mpango huo wa kuboresha elimu iendelezwe na hatua zichukuliwe kwa wale watakaoihujumu. Jafo alisema kuwa kumekuwepo na tabia katika baadhi ya maeneo ambapo wafadhili wanaposaidia miradi ya maendeleo , pindi wanapotoka na miradi inakufa jambo ambalo sio zuri. 

Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri alisema kuwa wameziagiza Halmashauri zote kuhakikisha wanaweka katika bajeti zake vipengeleo vyote vilivyokuwa kuwa katika mpango ili kuhakikisha unakuwa endelevu. 

Alisema Serikali itawachukulia hatua za kisheria wale wote watakaojaribu kuihujumu. Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza,DFID,Beth Arthy alisema kuwa Uingereza imegharamia ujenzi wa madarasa zaidi ya 700 yaliyojengwa katika shule za msingi kwenye mikoa 9 ya Tanzania Bara. 

Alisema madarasa hayo mapya yameongeza nafasi za masomo kwa zaidi zaidi ya wanafunzi 10,000 ambapo ujenzi wa madarasa hayo pia,ulihusisha ujenzi wa vyoo 1,300. Alieleza kwamba ufadhili wa Serikali ya Uingereza ulipitia Mpango ya kuboresha elimu, ambao pamoja na ujenzi wa madarasa na vyoo,umetoa mafunzo kazini kwa zaidi ya walimu 50,000,walimu wakuu 5,000 na waratibu elimu kata 1,300. 

Katika mkoa wa Tabora pekee,mradi huo umejenga madarasa 95,vyoo 176 na ofisi za walimu 32 huku ukitoa mafunzo kwa wakuu wa shule 773 na waratibu elimu kata 206 Beth alisema mpango huo umeleta mafanikio ambapo viwango vya ufaulu katika shule za msingi kwenye Mkoa wa Tabora,vimepanda kutoka asilimia 37 mwaka 2013 kabla ya mradi hadi asilimia 73 mwaka 2018.

PARIMATCH YAWAZAWADIA WASHINDI KUMI WA MCHEZO WA BAHATI NASIBU

$
0
0
 Mshindi wa kwanza katika mashindano hayo Fred Chacha kutoka Geita(katikati) akivaa kofia ngumu ya pikipiki wakati wa kukabidhiwa pikipiki yake aliyoshinda kupitia michezo ya bahati nasibu kwa njia ya tovuti na maduka ya kampuni hiyo yaliyofanyika katika ofisi zao leo jijini Dar es Salaam.
  Mshindi wa kwanza katika mashindano hayo Fred Chacha kutoka Geita akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa pikipiki mpya aliyoshinda kwenye mchezo ya bahati nasibu kwa njia ya tovuti na maduka ya kampuni ya Parimatch leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi muendeshaji wa Paramatch Tumaini Maligana.
Wafanyakazi wa Paramatch wakiwa kwenye picha ya pamoja na washindi 10 kutoka Mikoa mbalimbali nchini walokabidhiwa zawadi zao leo katika ofisi ya Mpuni hiyo leo jijini Dar es Salaam. 

KAMPUNI ya Parimatch ambayo inajihusisha na michezo ya bahati nasibu kwa njia ya tovuti na maduka imepata washindi 10 kutoka Mikoa mbalimbali nchini na kukabidhi zawadi hizo kwa washindi hao.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi muendeshaji wa Paramatch Tumaini Maligana kampuni hiyo ambayo ni mpya na ya kisasa zaidi inaendesha michezo hiyo ya bahati nasibu kwa gharama ndogo zaidi ya shilingi 300 pekee.

Amesema kuwa wana maduka 12 ambayo yanatumia mbinu za kisasa katika uendeshaji wa michezo hiyo na wateja wanaweza kubeti hata mechi moja kwa gharama nafuu.

"Kampuni yetu tunaiendesha kisasa zaidi na hiyo ni kutokana na ukuaji wa teknolojia, tunapatikana kwa njia ya mtandao ya www.parimatch.co.tz na tunatumia kompyuta katika kuendesha michezo hiyo ya bahati nasibu na sio karatasi kama ilivyozoeleka" ameeleza Maligana.

Aidha amesema kuwa michezo ya kubahatisha kwao ni burudani na sio ajira kama inavyotafsiriwa na baadhi ya watu na wanaendesha michezo hiyo kwa ustaarabu wa hali ya juu.

Washindi hao waliopatikana kupitia mbio za Afcon wamejishindia zawadi mbalimbali ambapo mshindi wa kwanza amejishindia pikipiki, mshindi wa pili na watatu wamejishindia Smart TV na mshindi wa nne hadi kumi wamejishindia simu za kisasa za mkononi (smart phone.)

Mshindi wa kwanza katika mashindano hayo Fred Chacha kutoka Geita ambaye amejishindia pikipiki ameeleza kufurahishwa na namna mchezo huo ulivyoendeshwa hadi akaibuka mshindi na kujishindia pikipiki ambayo itampa ajira na amewashauri vijana wengine kutumia michezo hiyo kama burudani na sio ajira kama ilivyozoeleka.

Vodacom wazindua simu janja kuwasaidia wateja kuingia ulimwengu wa kidigitali

$
0
0

Mkuu wa Matukio wa Kampuni ya TECNO, Anuj Khosla, akimkabidhi zawadi ya simu mwandishi wa habari Austin Beyadi, Mwandishi huyo alishinda simu katika hafla fupi ya uzinduzi wa simu aina ya TECNO Yente na Itel Bamba zilizozinduliwa kwa ushirikiano kati ya Vodacom na TECNO kwenye Duka la Vodacom Mlimani City Dar es Salaam jana. Kampuni ya Vodacom imewaletea wateja wao simu hizo kwa lengo la kuwawezesha kuwa na maisha ya kidijitali kupitia simu janja bora zinazouzwa kwa bei nafuu.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano Vodacom Tanzania Plc, Nandi Mwiyombella akionyesha simu mpya aina ya TECNO Yente iliyozinduliwa kwa ushirikiano kati ya Vodacom na TECNO katika hafla fupi iliyofanyika Duka la Vodacom Mlimani City Dar es Salaam, jana. Kampuni ya Vodacom imewaletea wateja wao simu hizo kwa lengo la kuwawezesha kuwa na maisha ya kidijitali kupitia simu janja bora zinazouzwa kwa bei nafuu. Kushoto ni Mkuu wa Matukio wa Kampuni ya TECNO, Anuj Khosla.


========   ========   ===========
Vodacom Tanzania Plc, kampuni nambari moja ya mawasiliano ya simu nchini imeungana na kampuni ya TECNO kuwaletea wateja wao toleo jipya la simu aina mbili za TECNO Yente na Itel Bamba, leo jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huu ni harakati ya Vodacom kuhakikisha jitihada zake za kuwezesha maisha ya kidijitali kwa wateja wao, kwa kupitia simu janja zinafanikiwa.

Akizungumza na waandishi wakati wa uzinduzi wa simu hizo, Mkuu wa matukio wa kampuni ya TECNO, Anuj Khosla alisema, “Tumedhamiria kuhakikisha kila Mtanzania anamiliki simu janja na kwa pamoja tunalifanya taifa la Tanzania kuwa la kidijitali”.

Simu hizi zitapatikana kwa bei ya shilingi 75,000 kwa Itel Bamba - 3G na Shilingi 195,000 kwa TECNO Yente ambayo ni - 4G, simu zote mbili zinakuja na ofa, ambapo kwa simu ya Itel Bamba wateja wetu watapata GB 3 kila mwezi kwa miezi minne na kwa simu ya TECNO Yente watapata GB 2 kila mwezi kwa mwaka mzima.

“Tunafuraha kushirikiana na TECNO kuendelea kuimarisha zaidi azimio letu la kuzidi kuwawezesha wateja wetu kuwa katika ulimwengu wa kidijitali. Uzinduzi huu umekuja katika kipindi muafaka, hasa kwa kuwa Watanzania wengi zaidi wanatumia huduma za simu janja” alisema Nandi Mwiyombella, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania.

Katika zama hizi za kidijitali, kupata taarifa, kununua na kulipia vitu, na kupata burudani za muziki na sinema, vinawezekana kwa kutumia simu janja, na matoleo haya mapya ya TECNO Yente na ITEL Bamba yatawezesha hayo yote na zaidi. “Uzinduzi huu umekuja sambamba na msimu wa sikukuu ya nanenane ili kuhakikisha wateja wetu, ambao ndiyo kipaumbele chetu wanasherehekea sikukuu ya nanenane msimu huu kidijitali zaidi” aliongeza Bi. Mwiyombella.

Simu hizi zitapatikana katika maduka yote ya Vodacom Tanzania Plc na pia katika madawati ya huduma kwa mteja (Service Desks) yanayotoa huduma kwa wateja wa kampuni hiyo maeneo mbalimbali nchini huku pia zikipatikana katika maduka ya TECNO.

TURUDISHE FARAJA KWA DJ STEVE B A.K.A DJ SKILLS

$
0
0
Ndugu yetu Dj STEVE B a.k.a Dj Skills anasumbuLiwa na Maradhi ya FIGO, leo tulienda kumjulia Hali' na tulipoingia katika chumba alicholazwa tukapiga Story sana, katikati ya Maongezi alisema, “Mtu ukiwa mzima ni jambo la kumshukuru Mungu sana”, hii ni kutokana na Situation anayopitia.

Steve anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila, natoa Taarifa kwa Marafiki, Wasanii na Wadau wote wa Muziki, wengi hawana TAARIFA, kama tunavyojua Maradhi ya FIGO ni aghali sana.

Sisi kama MaDj/ndugu/marafiki Wenzake tunaangalia Jinsi ya Kushirikiana na Wadau ku-Raise Fund ili kufanikisha aweze kupata Tiba sahihi nje ya nchi, kwani Familia imefika pahala wanahitaji Msaada wa hali na mali.

Wapo waliochangia Matibabu tutawashukuru sana kwa Majina na Tutapeana Taarifa zaidi jinsi ya Kumsaidia mwenzetu Matibabu yake. 

Kwa Mawasiliano Zaidi wasiliana na Kaka yake 0687536015 #RudishaFarajaKwaDjSteve

SERIKALI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA TAASISI ZA DINI KUJENGA USTAWI WA TAIFA

$
0
0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb) (katikati), akicheza moja ya nyimbo za kwaya, wakati wa Kongamano la Maombi ya Wanawake Waombolezao, tarehe 25 Julai, 2019, jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akifanyiwa maombi maalumu na waratibu wa Kongamano la Maombi ya Wanawake Waombolezao, wakati wa Kongamano hilo, tarehe 25 Julai, 2019, jijini Dar es salaam,.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akimkabidhi sadaka Mratibu wa Kongamano la Maombi ya Wanawake Waombolezao Mchungaji Deborah Malassy, wakati wa Kongamano hilo, tarehe 25 Julai, 2019, jijini Dar es salaam.
Mratibu wa Kongamano la Maombi ya Wanawake Waombolezao Mchungaji Deborah Malassy, akihubiri wakati wa Kongamano hilo, tarehe 25 Julai, 2019, jijini Dar es salaam. Kongamano hilo limebebwa na maudhui ya Mwaka wa Maachilio kwa Wanawake wote.

Baadhi ya washiriki na waalikwa katika Kongamano la Maombi ya Wanawake Waombolezao, wakifuatilia Kongamano hilo tarehe 25 Julai, 2019 jijini Dar es salaam, Kongamano hilo limebebwa na maudhui ya Mwaka wa Maachilio kwa Wanawake wote.
Mratibu wa Kongamano la Maombi ya Wanawake Waombolezao Askofu Dkt. Godfrey Malassy, akihubiri wakati wa Kongamano hilo, tarehe 25 Julai, 2019, jijini Dar es salaam. Kongamano hilo limebebwa na maudhui ya Mwaka wa Maachilio kwa Wanawake wote.
Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Maombi ya Wanawake Waombolezao, wakifuatilia Kongamano hilo tarehe 25 Julai, 2019 jijini Dar es salaam, Kongamano hilo limebebwa na maudhui ya Mwaka wa Maachilio kwa Wanawake wote.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), akieleza umuhimu wa Taasisi za dini katika kujenga ustawi wa Taifa, wakati wa Kongamano la Maombi ya Wanawake Waombolezao, tarehe 25 Julai, 2019, jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), akieleza umuhimu wa Taasisi za dini katika kujenga ustawi wa Taifa, wakati wa Kongamano la Maombi ya Wanawake Waombolezao, tarehe 25 Julai, 2019, jijini Dar es salaam,
Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Maombi ya Wanawake Waombolezao, wakifuatilia Kongamano hilo tarehe 25 Julai, 2019 jijini Dar es salaam, Kongamano hilo limebebwa na maudhui ya Mwaka wa Maachilio kwa Wanawake wote.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
…………………………
Na. OWM, DAR ES SALAAM.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), ameeleza kuwa serikali inatambua juhudi za taasisi za dini hapa nchini ikiwa ni pamoja na kudumisha amani na utulivu, hivyo itaendelea kushirikiana na taasisi hizo katika kuunga juhudi za serkali za kujenga amani, umoja, upendo na mshikamano na hatimaye kuleta ustawi wa Taifa.

“Napenda kuwahakikishia ushirikiano wa serikali katika kutekeleza majukumu yenu ya kiroho na ya huduma za kiuchumi na kijamii kwa maendeleo ya watanzania. Pale mtakapoona mchango wa serikali unahitajika msisite kuwasiliana nasi. Na iwapo mtaona kuna upungufu wowote semeni kwa viongozi wa wilaya, mkoa na wa kitaifa. Sisi ni wasikivu. Tuite tutawaitikia, tutatenda kwa lile ambalo lipo ndani ya uwezo wetu” amesisitiza Mhe. Mhagama.

Akiongea kwa niaba ya Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, katika Kongamano la maombi ya wanawake waombolezao, jijini Dar es salaam, tarehe 25 Julai, 2019, Mhe. Waziri Mhagama amefafanua kuwa waratibu wa Kongamano hilo wanapongezwa na viongozi wote serikalini, akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, kwakuwa linachagiza maendeleo katika Taifa hili na ustawi wa watu wake.
“Viongozi wetu kwa pamoja ni shupavu, wanaoaminiwa na kutumainiwa na wananchi hasa wanyonge. Viongozi wanachukia na kupinga rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma kwa vitendo na Rais anayejipambanua kwa kufanya maamuzi magumu ya kulinda rasilimali za Taifa. Lakini haya yote yamewezekana kwa kuwa wamejikabidhi katika mikono ya Mungu na nyie mmekuwa mkiwaombea” amesema Mhe. Mhagama.

Katika hatua nyingine, Mhe. Mhagama amewataka Wanawawake waombolezao waendelee kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa ambazo anaendelea kuzifanya tangu aliposhika hatamu ya uongozi, kwa kuthubutu kutenda na kuiletea nchi mafanikio makubwa.

“Kwa uchache kazi kubwa ambazo amezitekeleza Mhe. Rais, ni pamoja na kutoa elimu ya msingi bila malipo ambapo ameweza kuwagusa hata walewasiojiweza, kuongeza bajeti ya dawa, vifaa tiba na vitendanishi na kujenga Hospitali na Vituo vya Afya vingi ili watanzania wengi wapate huduma za Afya kwa karibu. Pia umeme kwa sasa umesambazwa vijijini kupitia mradi wa REA na sasa mradi mkubwa wa uzalishaji umeme wa Maji (Rufiji) umeanzishwa” amesisitiza Mhagama.

Awali wakiongea katika Kongamano hilo, waratibu wa Kongamano hilo, Mchungaji Deborah Malassy na Askofu Dkt. Godfrey Malassy wamebainisha kuwa wameamua kuendesha Kongamano hilo kwa kuwa wanatambua kuwa viongozi wa dini kama walivyo wa serikali wanao wajibu maalamu wa kulilea Taifa. Aidha wameongeza kuwa ushirikiano ukiwa imara watafanikiwa kuendeleza amani, umoja na mshikamano uliopo hapa nchini.

“Tutaendelea kutekeleza wajibu pekee wa kujenga uhai wa Taifa letu na watu wake. Tunampongeza Mhe.Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa uongozi wake bora uliokidhi kiu na kilio cha watanzania kwani tumeona jitihada anazofanya pamoja na kutiwa moyo na kazi zake anazozifanya na viongozi wote wa serikali ya awamu ya tano. Kwa hamasa hii tunapata nguvu ya kuendelea na wajibu huu mkubwa tuliopewa na Mungu kwa ajili ya kuendelea kuliombea Taifa letu” amesema, Mchungaji Deborah.

Kongamano hilo la kumi la Kihistoria hapa nchini liliohusisha Wanawake Waombolezao Kitaifa kutoka mikoa yote Tanzania na Zanzibar, pamoja na viongozi wa Taasisi mbalimbali, limebebwa na maudhui ya Mwaka wa Maachilio kwa Wanawake wote. Kongamano hilo ni sehemu ya Maombi ya kila mwisho wa mwaka wa tarehe 31 Disemba ya kuliombea Taifa hili yajulikanayo kama MKESHA MKUBWA KITAIFA DUA MAALUM, ambayo yamekuwa yakifanyika katika viwanja vya wazi katika mikoa mbalimbali ikiwemo Zanzibar.

SERIKALI ITAENDELEA KUSHIRIKIANA NA WADAU WA SEKTA YA UTANGAZAJI-DKT MWAKYEMBE:

$
0
0

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akibadilishana mawazo na Kaimu Mkurugenzi wa Utangazaji wa TCRA, Mhandisi Andrew Kisaka pamoja na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Patrick Kipangula wakati wa mkutano baina ya Waziri na Wadau wa sekta ya habari wakiwemo watayarishaji wa vipindi vya televisheni vyenye maudhui ya ndani uliofanyika jana Alhamisi Julai 25, 2019.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dkt. Ayoub Rioba akizungumza jambo wakati wa kikao baina ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) na wadau wa sekta ya habari wakiwemo watayarishaji wa vipindi vya televisheni vyenye maudhui ya ndani wakati wa mkutano wake uliofanyika jana Alhamisi Julai 25, 2019 .
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (mbele) akizungumza na wadau wa sekta ya habari wakiwemo watayarishaji wa vipindi vya televisheni vyenye maudhui ya ndani wakati wa mkutano wake uliofanyika jana Alhamisi Julai 25, 2019.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (aliyekaa) akiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa sekta ya habari mara baada ya kumalizika kwa mkutano wake baina yake na wadau hao uliofanyika jana Alhamisi Julai 25, 2019. 

(NA MPIGAPICHA WETU) 
………………………. 
Na Mwandishi Wetu,MAELEZO 
DAR ES SALAAM 

WAZIRI wa Habari, Utamadani, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amewahakikishia wadau wa sekta ya utangazaji nchini ikiwemo waandaaji na wazalishaji wa vipindi vya televisheni vya maudhui ya ndani kuwa Serikali itaendelea kushirikiana nao na kuwajengea mazingira wezeshi ili kuwawezesha kutimiza wajibu wao wa msingi katika jamii na Watanzania kwa ujumla. 

Akizungumza katika kikao maalum baina yake watayarishaji wa vipindi vya maudhui ya ndani jana Alhamisi (Julai 25, 2019) Jijini Dar es Salaam, Dkt. Mwakyembe amesema malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha kuwa tasnia ya habari inapiga hatua kubwa za maendeleo na kutoa mchango unaostahiki katika maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla. 

Waziri Mwakyembe alisema Serikali inatambua wajibu na umuhimu wa tasnia ya habari nchini, na hivyo imetunga sheria na kanuni mbalimbali zinazoongoza vyombo vya habari ikiwemo televisheni, ambapo vimewekwa utaratibu wa kurusha na kuandaa vipindi mbalimbali kupitia miongozo inayotolewa mamlaka husika ikiwemo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). 

“Tunatambua kuwa kuna baadhi ya vifungu vya kisheria vinavyoongoza maudhui ya vituo vya utangazaji vimekuwa changamoto, kwa kuwa Sheria hizi sio biblia au msahafu takatifu, tunaweza kuzifanyia marekebisho kila baada ya kipindi cha miaka 3-4 ili kuona ni namna gani inasaidia sekta ya utangazaji sambamba na kutumia fursa mbalimbali zinazojitokeza” alisema Waziri Mwakyembe. 

Aidha Waziri Mwakyembe alisema Wizara yake ipo tayari kupokea aina yoyote ya ushauri, mapendekezo na maoni ya wadau wa wazalishaji na waandaji wa vipindi vya Televisheni hususani masuala yote ambayo yamekuwa yakiwaletea changamoto katika utekelezaji wa majukumu yao ya kuhabarisha umma kupitia vipindi mbalimbali ambavyo vimekuwa daraja la kuwaunganisha Watanzania. 

Akifafanua zaidi Dkt. Mwakyembe alisema Serikali itahakikisha kuwa waandishi wa vyombo vya habari kutoka sekta ya umma na binafsi ikiwemo waandaaji wa vipindi vya maudhui ya ndani wanajengewa uwezo ikiwemo kuwapatia mafunzo ya muda mfupi, ya kati na mrefu, hatua inayolenga kuwaongezea weledi, ujuzi na maarifa na hivyo kutimiza wajibu wao wa msingi katika jamii. 

Dkt. Mwakyembe alisema katika mfumo uliopo sasa wa kutangaza maudhui ya ndani kumekuwepo na changamoto mbalimbali katika kanuni, sheria na taratibu ambazo zimekuwa zikileta malalamiko kutoka kwa wadau, na hivyo Serikali itahakikisha kuwa vipengele hivyo vinafanyiwa kazi kwa kuwa Serikali na vyombo vya habari vyote kwa pamoja vimekusudia kujenga msingi imara wa ushirikiano baina yao. 

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Matukio wa Shirika la Utangazaji Nchini (TBC) Martha Swai amesema TBC imekuwa mstari wa pembe katika kutangaza vipindi vyake vya Televisheni katika maudhuo ya ndani, ambapo asilimia 82 vimegusa masuala ya elimu, biashara na kuburudisha, na asilimia 18 ikijikita katika masuala ya muziki. 

Anaongeza kuwa Shirika hilo limekuwa likiatangaza matangazo yake ya Televisheni katika chaneli kubwa tatu ambazo ni TBC 1, TBC 2 na Tanzania Safari ambazo zote kwa pamoja vimekuwa na mchango mkubwa katika kutangaza habari na matukio ya vipindi mbalimbali vyenye kuakisi maudhui ya ndani. 

Naye Meneja Vipindi wa Kampuni ya Tumaini Media, Paul Mabuga amesema kwa sasa kumekuwepo na changamoto kubwa ya ukosefu wa matangazo ya biashara katika vituo vya Televisheni kwani wafanyabiashara wengi wamekuwa wakitumia zaidi mitandao ya kijamii ili kuweza kufikisha ujumbe wananchi kwa njia ya kisasa na haraka zaidi.

WAZIRI NDALICHAKO AITAKA COSTECH KUBADILIKA.

Tamasha la 11 muziki wa laanza kuonesha cheche zake leo Chamwino

$
0
0
TAMASHA la 11 la muziki wa Cigogo linaanza kurindima leo kwenye viwanja vya Chamwino Ikulu jijini Dodoma ikiwa ni muendelezo wa kukuza na kuendeleza sanaa ya Tanzania.

Tamasha hilo linaanza leo kwa makundi mbalimbali ya ngoma za asili yakitoa elimu kwa jamii kupitia nyimbo zao huku kesho ndio uzinduzi rasmi ambao, mgeni rasmi atakuwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu Anthony Mavunde.

Mavunde katika tamasha hilo ataongozana na watendaji wengine wa ofisi za serikali wanaotumikia Sanaa, lengo likiwa ni kufikisha ujumbe wa jamii kupitia wasanii.

Kwa kuwa tamasha la Cigogo ni mojawapo ya sehemu ambayo inabeba urithi wa utamaduni wa mtanzania kwa sababu ya kukusanya idadi kubwa ya wadau wa sanaa, watanzania wanakaribishwa kwa wingi kujipatia ujumbe ambao ni sehemu ya elimu.

Ingawa hivi sasa Tanzania kuna utitiri wa matamasha lakini umuhimu wa tamasha hilo ni wa kupigiwa mfano kutokana na shughuli zinazofanyika kwenye wiki ya tukio hilo.

Kwani mshindo wa tamasha hilo umefika mbali zaidi ambao umevuka mipaka ya nchi na kutokomea katika mabara ya Ulaya, Amerika na Asia ambayo huchota busara na urithi wa sanaa za Tanzania.

Yaliyomo ndani ya tamasha hilo ni kiota ambacho kimebeba dhamira na taratibu nzima za sanaa kwa sababu anayelisimamia tamasha hilo ni mwanazuoni mbobevu anayefanya kazi hizo na kuzifundisha ikiwa ni eneo la elimu, burudani na taratibu nyingine ambazo ni sehemu ya jamii.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa tamasha hilo Dk Kedmon Mapana vumbi limeanza kufuka leo katika viwanja vya Chamwino lilipo lango la kuingilia Ikulu ambalo litafikia tamati Jumapili.

Anasema tamasha hilo lililoasisiwa mwaka 2005 kijijini hapo na Kituo cha Sanaa cha Chamwino (CAC) kwa lengo la kuenzi na kuuendeleza muziki wa asili ya Kigogo.

Dk Mapana anasema ubora wake umezidi kukua kwa sababu ya matukio ambayo yanaendana na kasi ya maendeleo ya sanaa duniani.

Mapana anasema kadri siku zinavyokwenda mbele ndivyo linavyozidi kupiga hatua kwa matukio ambayo ni sehemu ya maendeleo ya sanaa.

“Kwa kuwa sanaa ni eneo ambalo ninaishi, kila mwaka matukio yanabadilika kuendana na wakati, hivyo ni nafasi ya mashabiki wa sanaa na utamaduni kujitokeza kwa wingi kujionea jinsi makundi ya sanaa yanavyoendeleza utamaduni wa mtanzania,” alisema Dk Mapana.

Dk Mapana ambaye ni Mkuu wa kitengo cha Sanaa za Ubunifu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) anasema kutakuwa na matukio mbalimbali ambayo ni njia ya kufikia malengo yanayokusudiwa.

Anasema katika makundi shiriki huwa wanapewa nafasi ya kuibua vionjo vya asili kama vile aina ya ngoma, uchezaji wake na hata maleba. Makundi shiriki

Anasema tamasha la mwaka huu linatarajia kushirikisha makundi 31 ya hapa nchini ambayo yatabadilishana utamaduni.

Ingawa kutakuwa na wadau zaidi ya 20 kutoka nje ya Tanzania ambao wanakuja kujifunza na kushuhudia utamaduni wa Mtanzania kupitia tamasha hilo.

Anaweka bayana wadau hao kutoka nje ya Tanzania ni Afrika Kusini (4), Bulgaria (4) Amerika (4), Argentina (2) na Thailand (15) na Uganda (1).

Dk. Mapana anasema wafadhili wakubwa wa tamasha la Muziki wa Cigogo ni wasanii wenyewe ambao huwa wanajitoa kwa asilimia kubwa. Tamasha hilo limejijenga kutokuwa tegemezi, yaani hatusubiri wafadhili kuuenzi utamaduni wetu kwani hatusubiri tulipwe pesa.

“Sasa ukionyesha ulichonacho huwezi jua nani atakipenda na atakinunua kwa gharama gani, lakini pia Tamasha hili limejikika katika kufundisha watoto na vijana kuendelea kutambua mila na desturi zao,” alisema.

Kazi kubwa ya Kituo cha Utamaduni Chamwino ni kutafuta fedha ya kuhakikisha wasanii wanakula vizuri.

Anaweka bayana wafadhili wengine wa tamasha hilo ni serikali ya kijiji cha Chamwino ambacho kinatoa maeneo ya kufanyia tamasha hilo bila gharama yoyote pamoja na Shirika lisilo la Kiserikali la Chamwino Connect lililoko Marekani.

Anasema katika makundi shiriki huwa wanapewa nafasi ya kuibua vionjo vya asili kama vile aina ya ngoma, uchezaji wake,na hata maleba.

Kutolewa semina mbalimbali
Mojawapo ya matukio yatakayofanikisha tamasha la 11 ni semina mbalimbali zitakazotolewa na serikali kwa maeneo kama Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Bodi ya Filamu, Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA), Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Dk Mapana anasema semina hizo si mara ya kwanza kufanyika tangu kuasisiwa kwa tamasha hilo ambalo linazidi kukua kadri siku zinavyokwenda mbele.

Msanii Dito ndani ya nyumba
Anasema kama ilivyokuwa mwaka jana, msanii wa muziki wa kizazi kipya, Lameck Dito ni mmoja wa wasanii washereheshaji wa tamasha la 11.

Ditto kwenye tamasha hilo akiiwakilisha taasisi ya Tulia Trust ukiwa ni ushirikiano kati ya CAC na taasisi ya Tulia.

Wanafunzi UDSM kujifunza zaidi
Dk Mapana anasema kama ilivyo ada ya tamasha hilo, wanafunzi wa sanaa wa UDSM hupata nafasi ya kujifunza kwa vitendo uandaaji wa Filamu (Film Documentary), namna ya kuandaa matamasha na matukio mengine ya sanaa.

“Huwa tunalitumia tamasha la Chamwino kama sehemu ya wanafunzi wetu kujifunza kwa vitendo yale ambayo tunayowafundisha darasani,” alisema Dk Mapana.

Kubwa zaidi katika tamasha
Dk Mapana anasema katika tamasha la mwaka huu kutakuwa na mchezo wa kuigiza ulioongozwa na wataalam kutoka Bulgaria ambao utachezwa na wanafunzi wa Shule ya Msingi Chamwino.

Anasema malengo makubwa ya mchezo huo ni kuibua na kuendeleza vipaji kwa watoto ukiwa ni mpango wa CAC.
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Suzan Mlawi akiwasilisha neno kwenye tamasha la kwa jana, kulia kwake ni Dk Mapana
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Suzan Mlawi akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine wa sanaa wa kada mbalimbali.
 Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza na Dk Mapana wakicheza ngoma na kikundi cha watoto cha Ndagwa
 Katibu wa Basata Godfrey Mngereza akipigamarimba kwenye tamasha la Cigogo 2018
 Kundi la Iman Membe likitoa burudani kwenye tamasha la mwaka jana
Wakiserebuka tamashani

WAJANE WAASWA KUCHUKUA TAHADHARI YA UKIMWI

$
0
0
Serikali imewataka wajane kote Nchini kukumbuka kuhusu suala la VVU/UKIMWI na kuwataka kuchukua tahadhari kupunguza maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI kwa kutumia kinga, kuepuka tabia hatarishi, kutokomeza unyanyapaa na ubaguzi kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI.

Akiongea wakati wa kufungua Mafunzo ya kujenga uwezo kwa wajane Mkurugenzi Idara ya Watoto kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii  Mwajuma Magwiza alisema kuwa UKIMWI hadi sasa bado ni janga la Kitaifa hivyo kusisitiza wajane hao kuchukua tahadhari kubwa ili kuepukana maambukizi.

Aidha  Magwiza pamoja na kuzungumzia maambukizi ya UKIMWI lakini pia amesema tayari serikali kwa kushirikiana na wadau inaendelea kuhamasisha jamii kuacha Mila na Desturi potofu za kunyanganya mali za wajane, kuozesha watoto wakike katika umri mdogo ikiwemo kutakasa na kurithi wajane.

Bi. Magwiza ameitaka jamii pia kuachana na mila zenye madhara kwa mwanamke hususan mjane na zinazodhoofisha jitihada zake za kujikwamua kifikra, kiutamaduni, kiuchumi na kijamii akiongeza kuwa kila mmoja anao wajibu wa kutoa fursa sawa kwa makundi yote katika jamii ikiwemo wajane kubadili fikra, mtizamo, kuwa jasiri, kujiamini na kutambua kuwa mabadiliko yanaanza na wao.

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Jinsia kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bi. Mboni Mugaza amewambia wajumbe wa Mafunzo hayo kuwa lengo la Wizara yake ni kuwakutanisha wadau na viongozi wadini ili waweze kujua huduma zinazotolewa na wajane lakini pia kuwajengea uwezo ili waweze kukabiliana na changamoto za kimaisha ukizingatia kuwa wengi wao ni wakuu wa familia.

Bi. Mariamu Aswile ambaye pia ni Mratibu wa Umoja wa Wajane Kanda ya Mashariki akizungumza na vyombo vya habari kuhusiana na mafunzo hayo amesema wosia ni jambo la Msingi kwa kulinda haki za wajane lakini pia akasisitiza suala la mjane kupewa hati ya kifo ili iwe hatua muhimu ya mjane husika kufuatilia mirathi itakayomsaidia kusaidia wazee.

Aidha Bi. Aswile amewata wananchi kufuatilia zaidi madhira na madhara wayapatayo wajane ili na wao wasije yakawakuta matatizo ambayo yanawakabili wajane kwa sasa kwani kila mmoja ni mjane mtarajiwa hivyo ni muhimu kwa wajane watarajiwa na wapya kuhakikisha wanachukua tahadhari kuepukena na madhara na changamoto za wajane walizonazo sasa.

Wakati huohuo Mjane Bi. Stella Maveka kutoka kikundi cha Wajane Tuinuane kilichopo mjini Dodoma ameyataja mafunzo hayo kuwa ya muhimu kwa wajane kwani yatawasaidia wajane kujua taratibu za usajili wa vikundi na wakati huo akilaani baadhi ya vyombo vya dora vinavyokamata biashara za wajane na kuitaka serikali kuchukua hatua ili kuokoa bidhaa hizo ambazo zinazuiliwa na mamlaka za serikali.

Mafunzo haya yanafanyika kufuatia agizo la Naibu Waziri Afya Dkt. Faustine Ndugululile alilolitoa katika Kongamano la Wajane mapema mwezi Juni Mwaka huu kwa Wizara yake kutaka Wajane wapatiwe mafunzo ya ujasiliamali na vifungashio lakini pia namna bora ya kumiliki ardhi na kwa wajane kupatiwa huduma ya Afya.

Utafiti uanaonesha kuwa kati ya 7% hadi 16% ya wanawake wote duniani bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kupoteza haki ya kumiliki mali , umasikini , mila na desturi za kuridhiwa baada yakufiwa uku idadi ya wajane Tanzania ambao ni wa wanachama wa TAWIA(Tanzania Widows Association) ikifikia 800,000.
 Mkurugenzi Idara ya Watoto kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Mwajuma Magwiza akiongea wakati wa kufungua Mafunzo ya kujenga uwezo kwa wajane yaliyofanyika leo Jijini Dodoma.
 Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Jinsia kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Mboni Mgaza akielezea malengo ya mafunzo wakati wa Mafunzo ya kujenga uwezo kwa wajane yaliyofanyika leo Jijini Dodoma.
 Mkurugenzi Idara ya Jinsia kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Julius Mbilinyi akioelezea umuhimu wa kumuwezesha mjane kiuchumi wakati wa Mafunzo ya kujenga uwezo kwa wajane mafunzo yaliyofanyika leo Jijini Dodoma.
 Mratibu wa Chama cha Wajane Tanzania (TAWIA) Kanda ya Mashariki Mariamu Aswile akitoa shukrani kwa niaba ya wajane wakati wa kufungua Mafunzo ya kujenga uwezo kwa wajane yaliyofanyika leo Jijini Dodoma.
Baadhi ya Wajane wakiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi na maafisa kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto mara baada ya ufunguzi wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo leo Jijini Dodoma. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

WALIOFUJA FEDHA MRADI WA MIYOGWEZI UKEREWE KUCHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA

$
0
0
NA BALTAZAR MASHAKA, UKEREWE
SERIKALI imesema waliohusika kwenye ubadhirifu wa fedha za Mradi wa Umwagiliaji wa Miyogwezi wilayani Ukerewe na kusababisha ujengwe chini ya kiwango na kutokamilika licha ya sh. milioni 750 kutolewa watachukuliwa hatua za kisheria.

Naibu Waziri wa Kilimo, Omari Mgumba alisema jana wilayani Ukerewe baada ya kutembelea na kukagua miradi ya umwagiliaji ya Miyogwezi na Bugorola ambao miundombinu yake imechoka na kusababisha ushindwe kufanya kazi.

Akizungumza kwenye eneo la mradi wa Miyogwezi na wakulima wanaotumia bonde la mradi huo kwa kilimo, alisema kuna harufu ya rushwa kwenye mradi huo ambao mkandarasi alilipwa sh. milioni 684 kati ya sh. milioni 750 bila kuukamilisha na kuhoji nani alisababisha fedha zikatumika kinyume cha utaratibu wa serikali.

Alisema serikali iliamua kujenga miradi ya umwagiliaji ili kuleta maendeleo endelevu kwenye sekta ya kilimo baada ya kukusanya na kutenga fedha ili wananchi wafaidi keki ya nchi na kulima kwa tija lakini wajanja wa wizara yake wakaleta kampuni za mifukoni zila fedha, kwamba si haki na hawakuwatendea haki watanzania.

Alisema cha kushangaza Ukerewe ilipewa mradi wa miyogwezi na kampuni ya CODA ya nchini Kenya iliyopewa kazi ya kujenga mradi huo ililipwa bila kustahili malipo ya sh. milioni 684 bila kukamilisha mradi huo kwa asilimia 55 baada ya kujenga mabanio mawili chini ya kiwango, magati, mitaro miwili ya maji lakini haikusakafiwa na haikufika mwisho pamoja na vigawa maji 16.

“Siamini nilichokiona hapa na kilichopo kwenye nyaraka (mkataba), mradi huu una harufu ya rushwa na matumizi mabaya ya fedha za umma.Thamani ya mradi ni sh. milioni zaidi ya 700 bado haujakamilika,umetekelezwa kwa asilimia 45 tu.Mkandarasi amelipwa wakati kazi hailingani na thamani ya fedha na waliofanya hayo bado wapo ofisini na kwa nini bado wapo,” alisema Mgumba.

Alionya fedha hizo hazitakwenda bure na kuiagiza Tume ya Umwagiliaji kuandaa taarifa ya kina ya mradi wa Miyogwezi ikiainisha nani alilipwa wakati kazi haikukamilika,waliohusika kwenye ubadhirifu huo, nani aliyesababisha fedha zitumike kinyume cha mipango ya serikali ili ijue njia wanazotumia kutafuna fedha za umma na makosa yasirudiwe.

Naibu Waziri huyo wa Kilimo alisema miongoni mwa kanda ambazo hazikufanya vizuri kwenye miradi ya umwagiliaji ni Mwanza, kwani miradi hiyo ilijengwa chini ya kiwango na kushangaa kwa nini watendaji waliokuwa wakisimamia miradi hiyo bado wako ofisini na kuwataka wajipime kama wanafaa kukalia nafasi hizo.

Mgumba akijibu ombi la wakulima hao la kutaka waletewe fedha zingine baada ya wajanja wakupiga (walikula) fedha za mradi huo alisema serikali haiwezi kuleta fedha hadi ijue nani aliipiga ili achukuliwe hatua za kisheria na liwe fundisho kwa wengine na kueleza kuwa serikali inafanya kazi kwa bajeti iliyopitishwa na bunge.

Aidha, alieleza kuwa wataalamu wanayo kazi ya kuisaidia serikali ili mradi huo wa Miyogwezi ukamilike na itakuwa tayari kutoa fedha baad ya kujiridhisha kuwa fedha za awali zililiwa ndo maana Tume ya Umwagiliaji imeundwa kusimamia miradi ya umwagiliaji.

Awali Mbunge wa Ukerewe (CCM) Josephat Mkundi alisema mradi huo wa kilimo cha umwagiliaji uliokuwa ukisimamiwa na District Agriculture Investment Project (DASIP) ulijengwa mwaka 2013 kwenye kwa ajili ya kuwanufaisha wakulima 194 lakini haufanyi kazi kutokana na miundombinu yake kutokamilika.

Mbunge huyo wa Ukerewe alisema sh. milioni 200 zilitolewa na Dairy Processing & Infrastructure Development Fund (DIDF) ambapo DASIP ilitoa milioni 550 kwa ajili ya mradi huo lakini hadi sasa haujakamilika ambapo akiwa bungeni Januari mwaka huu alihoji serikali ni lini mradi wa Miyogwezi utaboreshwa na kamilika ili kuweza kuwasaidia wakulima wanaotumia bonde hilo kwa kilimo, kulima kwa tija.
 Naibu Waziri wa Kilimo Omari Mgumba ,wa pili akielekea kukagua miundombinu ya mradi wa umwagiliaji wa Miyogwezi wilayania Ukerewe jana.Wa tatu ni Mbunge wa Ukerewe Josephat Mkundi, nyuma ya Mkundi ni Mhandisi wa Tume ya Umwangiliaji Kanda ya Mwanza, Adelialid Mwesiga na mwisho ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Focus Majumbi.Picha na Baltazar Mashaka
 Naibu Waziri wa Kilimo, Omari Mgumba, wa tatu kutoka kulia akiwa ameanda juu ya banio la maji la mradi wa Miyogwezi jana alipokagua mradi huo uliokwama tangu mwaka 2013.Kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Ukerewe Focua M Majumbi.Wa tatu kutoka kushoto ni Mbunge wa Ukerewe, Josephat Mkundi. Picha na Baltazar Mashaka.

 Kaimu Ofisa Kilimo Wilaya ya Ukerewe Issa Mugenyi (kulia) akitoa maelezo ya mradi wa Miyogwezi kwa Naibu wa Waziri wa Kilimo, Omari Mgumba (wa pili kulia,aliyesimama juu ya banio la maji ) jana alipokwenda kukagua miundombinu ya mradi huo wilayani Ukerewe.Nyuma ya Naibu waziri ni Mbunge wa Ukerewe Josephat Mkundi na kulia wa kwanza ni Katibu Tawala wa Wilaya na Kaimu Mkuu wa wilaya hiyo Focus Majumbi.


 Naibu Waziri wa Kilimo , Omari Mgumba , wa pili akikagua moja ya mitaro ya mradi wa umwagiliaji wa mradi wa Miyogwezi wilayania Ukerewe, numa ni mbunge wa jimbo hilo Josephat Mkundi.

Naibu Waziri wa Kilimo, Omari Mgumba (katikati) akimhoji jambo kaimu Ofisa kilimo Wilaya ya Ukerewe Issa Mugenyi (kulia) baada ya kumpa maelezo yasiyoridhisha ya mradi wa umwagiliaji wa Miyogwezi wilayani Ukerewe jana.

MAKAMU WA RAIS AZUNGUMZA NA VIONGOZI WA SHIMUTA NA MASHIRIKA YA UMMA

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti wa SHIMMUTA Khamis Mkanachi alipowasili Ukumbi wa Mikutano wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam kwa ajili ya kuzungumza na Viongozi, Wakuu wa Taasisi, Mashirika ya Umma na Makampuni Binafsi juu ya maandalizi ya SHIMMUTA mwaka 2019.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi, Wakuu wa Taasisi, Mashirika ya Umma na Makampuni Binafsi Juu ya maandalizi ya SHIMMUTA mwaka 2019 katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam leo Julai 26,2019. wa pili kulia ni Mwenyekiti wa SHIMMUTA Khamis Mkanachi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi, Wakuu wa Taasisi, Mashirika ya Umma na Makampuni Binafsi baada ya kuzungumza na Viongozi hao kuhusu maandalizi ya SHIMMUTA mwaka 2019 katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam leo.(Pich na Ofisi ya Makamu wa Rais)

WAZIRI WA AFYA HAMAD RASHID AZINDUA CHANJO YA HOMA YA INI KWA WAFANYAKAZI WA AFYA MNAZI MMOJA ZANZIBAR

$
0
0
 Waziri wa Afya Hamad Rashid akitoa Hotuba ya Uzinduzi wa Chanjo ya Homa ya Ini kwa Wafanyakazi wa Hospitali Mnazi mmoja katika Ukumbi wa Hospitali hio mjini Zanzibar.
 Waziri wa Afya Hamad Rashid akimkabidhi Muuguzi Zaina Udi Mwinyi Boksi la sindano za Chanjo ya Homa ya Ini ikiwa ni ishara ya Uzinduzi wa Chanjo hio kwa Wafanyakazi wa Afya Mnazi mmoja Hospita Zanzibar.
Mkurugenzi huduma za uuguzi na Mratibu wa Chanjo ya homa ya Ini Haji Nyonje Pandu akipatiwa Chanjo ya Homa ya Ini na muuguzi Zaina Udi Mwinyi baada ya kuzinduliwa Chanjo hio na Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed kwa Wafanyakazi wa Afya Mnazimmoja Hospitali Zanzibar. PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.
 Baadhi ya Wafanyakazi wa Hospitali ya Mnazi mmoja waliohudhuria katika hafla ya Uzinduzi wa Chanjo ya Homa ya Ini kwa Wafanyakazi wa Hospitali ya Mnazi mmoja iliozinduliwa na Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed Mnazi mmoja Hospitali Zanzibar.
 Kaimu Mkurugenzi mtendaji Hospitali ya Mnazi mmoja Dk,Msafiri Marijan akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Chanjo ya Homa ya Ini kwa Wafanyakazi wa Hospitali ya Mnazi mmoja iliozinduliwa na Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed Mnazi mmoja Hospitali Zanzibar.
 Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dk,Fadhil Mohamed Abdalla akitoa hotuba ya makaribisho kwa Mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa Chanjo ya Homa ya Ini kwa Wafanyakazi wa Hospitali ya Mnazi mmoja iliozinduliwa na Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed Mnazi mmoja Hospitali Zanzibar.

ZAIDI YA KILO 300 ZA MIRUNGI ZAKAMATWA ZIKISAFIRISHWA KWA NJIA YA POSTA

$
0
0
*Wawili washikiliwa, majina bandia ya moringa na mlonge yatumika kusafirisha madawa hayo

* Kampuni  zinazohusika na usafirishaji wa vifurushi zatakiwa kuchukua tahadhari na kutoa taarifa dhidi ya mizigo itakayotiliwa mashaka

Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
MAMLAKA ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya kwa kushirikiana na shirika la Posta, Wizara ya kilimo na mifugo na Wizara ya Maliasili na Utalii imefanikiwa kukamata zaidi ya kilo 300 za dawa za kulevya aina ya  mirungi iliyokuwa ikiingizwa nchini na kusafirishwa kwenda nchi za Ulaya hasa Uingereza kwa njia ya Posta huku wahusika wakitumia majina bandia ya mlonge, moringa tea, dawa, majani ya mboga, tea leaves na moringa leaves.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Kamishina wa Intelijensia kutoka Mamlaka hiyo Fredrick Kibuta amesema kuwa baada ya dawa hizo kukamatwa zilipelekwa kwa mkemia Mkuu wa Serikali uchunguzi umethibitisha kuwa majani hayo yana kemikali aina ya Cathinone ambayo inapatikana kwenye mmea wa mirungi (Cath edulis.)

"Taarifa za awali zilibaini kuwepo kwa usafirishwaji wa kiasi kikubwa cha dawa za kulevya aina ya mirungi kutoka nchini kwenda nchi za Ulaya kwa njia ya Posta huku shehena hizo zikiwa zimepewa majina bandia, na imebainika  kuwa dawa hizo ziliingizwa nchini kutoka nchini Ethiopia kama majani ya mlonge na baadaye kufungwa upya kusafirishwa tena kwenda Uingereza, Canada, Ufaransa na nchi nyingine za Ulaya" ameeleza Kamishina Kibuta.

Amesema kuwa mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya kwa kushirikiana na mamlaka nyingine za kiserikali zinaendelea na uchunguzi na kubaini ukubwa wa tatizo ambapo hadi sasa watu wawili wanashikiliwa kwa uchunguzi zaidi.


Vilevile amesema kuwa suala hilo haliwahusu wafanyabiashara halali wa zao la mlonge na  waendelee kufanya biashara zao na amezitaka kampuni zinazosafirisha vifurushi kama vile DHL, FEDEX, Swiss Port na wengine kuchukua tahadhari na endapo watapata mashaka yoyote kwenye mizigo hiyo taarifa itolewe haraka kwa mamlaka hiyo.

Kwa upande wake Kamishina wa huduma za sheria Edwin Kakolaki amesema kuwa Serikali ipo macho na yeyote atakayebainika anajihusisha na dawa za kulevya kwa namna yoyote ile sheria ipo na itafanya kazi yake na kuongeza kwamba kifungo cha maisha gerezani kitamuhusu yeyote atakayekutwa na dawa la kulevya zaidi ya kilo 50 na kifungo cha miaka 30 kwa watakaokutwa na dawa chini ya kilo tajwa.

WATU 12 KORTINI KWA KUKWEPA KULIPA KODI

$
0
0
Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv.
Watu 12 wakazi wa sehemu tofauti jijini Dar es Salaam, wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la  kukwepa kodi na kusababisha hasara ya zaidi ya sh. Milioni 100.7/-

Akisoma hati ya mashtaka Wakili wa serikali, Janet Magoha amewataja washtakiwa hao kuwa ni, Rose Kerandi, Ally Abdul, Geoffrey Kayanza, Anwar Rubeya,  Khalid Kigoma, Joseph Marcelo, Samir Hussein, Matiku Mgaya Iddi Bogaboga, Edward Maguri, Alex Sanga, Said suleman, Lali Mohamed na Hamidu Abu.
Imedaiwa mbele ya Hakimu Mkazi Salum Ally kuwa, Siku na mahali pasipo julikana, washtakiwa hao walikula njama ya kutenda kosa la kukwepa kodi.

Katika shtaka la pili imedaiwa  February 21, 2019 ndani ya jiji la Dar es Salaam, washtakiwa walishindwa kulipa kodi ya sh. 100,739,873 ya mzigo wa ambao walikuwa wakiuingiza  nchini.
Pia washtakiwa hao wanadaiwa, Siku na mahali hapo waliisababishia TRA hasara ya kiasi hicho cha fedha kwa nia ovu ya kutokulipa kodi ya bidhaa ya kontena la futi 40 lilolokuwa limebeba  mikoba.

Hata hivyo wakato wakisomewa mashtaka hayo, washtakiwa  Anwary Rubeya, Joseph Marcelo, Matiku Mgaya na Idd Bogobogo hawakuwepo mahakamani hapo na mahakama imetoa hati ya wa washtakiwa hao kukamatwa ili waweze kufika mahakamani hapo kujibu mashtaka yao.

Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu Uchumi na imeahirishwa hadi Agosti 6, mwaka huu.

Kwa mujibu wa upande wa utetezi, upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika, washtakiwa wote wamerudishwa rumande.

RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA MRADI WA KUFUA UMEME WA MAJI KATIKA MTO RUFIJI

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Nishati wa Misri Dkt. Mohamed Shaker wakivuta utepe kuashiria uwekaji wa Jiwe la Msingi mradi wa Ujenzi wa Kuzalisha umeme Megawati 2115 katika eneo la mto Rufiji katikati ya Morogoro na Pwani.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Nishati wa Misri Dkt. Mohamed Shaker mara baada ya kuweka Jiwe la Msingi mradi wa Ujenzi wa Kuzalisha umeme Megawati 2115 katika eneo la mto Rufiji katikati ya Morogoro na Pwani.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia pamoja na viongozi wengine mara baada ya tukio hilo la uwekaji wa Jiwe la Msingi.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Nishati wa Misri Dkt. Mohamed Shaker, Waziri wa Nishati Medard Kalemani pamoja na viongozi wengine akisikiliza namna mradi wa Kuzalisha umeme Megawati 2115 katika eneo la mto Rufiji utakavyokuwa ukifanya kazi mara baada ya kukamilika.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia michoro ya ujenzi huo mkubwa wa kufua umeme.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi kabla ya kuweka jiwe la msingi mradi wa Kuzalisha umeme Megawati 2115 katika eneo la mto Rufiji.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri wa Nishati wa Misri Dkt. Mohamed Shaker wakati wakielekea kwenda kuweka jiwe hilo la msingi.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mitambo itakayotumika katika mradi huo mkubwa wa kufua umeme.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia eneo la bonde katika mto Rufiji mara baada ya kuweka jiwe la msingi la mradi huo wa umeme.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi mara baada ya kuwasili katika eneo la Mradi.
Eneo la mto Rufiji ambalo litatumika katika ujenzi huo wa kufua umeme kama linavyoonekana. PICHA NA IKULU
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live


Latest Images