Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live

POLISI WATATU AKIWEMO STAFF OFFICER I MKOA WA KIPOLISI RUFIJI WAFARIKI DUNIA

0
0




NA MWAMVUA MWINYI,MKURANGA

ASKARI wawili wa kanda maalum Rufiji,
pamoja na staff officer I mkoa wa kipolisi Rufiji (ACP) ,Issah Bukuku ,wanadaiwa kufariki dunia katika ajali ya gari kupasuka gurudumu la nyuma na kupinduka na kusababisha majeruhi wawili.

Taarifa za awali kuhusu ajali hiyo zinaeleza,imetokea Julai 25 mwaka huu, huko kijiji cha Kilimahewa barabara ya Kilwa wilaya ya Mkuranga na mkoa wa kipolisi Rufiji ambapo gari namba PT. 3822 Toyota land cruiser mali ya jeshi la polisi mkoa wa kipolisi Rufiji likiendeshwa na askari namba F7167 PC Ibrahim likitokea polisi Ikwiriri kuelekea kijiji cha Mwalusembe wilaya ya Mkuranga .

Waliofariki dunia katika ajali hiyo ni staff officer I mkoa wa kipolisi Rufiji (ACP) ,Issah Bukuku ,inspector Esteria wa ofisi ya RCO Rufiji na G 1132 PC Lameck wa FFU Rufiji.

Majeruhi katika ajali ni dereva wa gari hiyo F 7167 PC Ibrahim wa ofisi ya RCO Rufiji ambaye ameumia sehemu mbalimbali za mwili wake na G7651 PC Mgusi wa ofisi ya RPC Rufiji ambaye ameumia sehemu mbalimbali za mwili wake.

Chanzo cha ajali ni kupasuka gurudumu la nyuma kulia na kusababisha gari hilo kupinduka.

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na taarifa kamili za kipolisi kanda maalum Rufiji zinaendelea na uchunguzi na itatoa habari kamili .

MAKAMU WA RAIS KUFUNGUA MAONESHO YA NANENANE KITAIFA 2019 MKOANI SIMIYU

0
0
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba (kulia) akikagua moja ya kitalu nyumba wakati wa ziara ya kukagua maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yatakayofanyika kuanzia Julai 28, 2019 Viwanja vya Nyakabindi Bariadi.
Mtaalam kutoka JKT (kulia) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba (katikati) wakati akikagua moja ya tanki la ufugaji wa samaki wakati wa ziara ya kukagua maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yatakayofanyika kuanzia Julai 28, 2019 Viwanja vya Nyakabindi Bariadi.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba (kulia) akikagua baadhi ya vipando wakati wa ziara ya kukagua maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yatakayofanyika kuanzia Julai 28, 2019 Viwanja vya Nyakabindi Bariadi.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba (kulia) akipokea maelezo kutoka kwa Afisa wa JKT akikagua baadhi ya vipando wakati wa ziara ya kukagua maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yatakayofanyika kuanzia Julai 28, 2019 Viwanja vya Nyakabindi Bariadi.
Baadhi ya vipando vilivyo katika Viwanja vya Maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa Mashariki vilivyopandwa kwa ajili ya maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 .
Mtaalam kutoka JKT (kulia) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba (katikati) wakati akikagua moja ya Bwawa la ufugaji wa samaki wakati wa ziara ya kukagua maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yatakayofanyika kuanzia Julai 28, 2019 Viwanja vya Nyakabindi Bariadi.
Mtaalam kutoka JKT (kulia) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba wakati akikagua moja ya tanki la ufugaji wa samaki wakati wa ziara ya kukagua maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019 yatakayofanyika kuanzia Julai 28, 2019 Viwanja vya Nyakabindi Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adam Kighoma Malima(kulia) akizungumza katika kikao cha Kamati ya maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa 2019 Kanda ya Ziwa Mashariki, kilichofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi, (kushoto) ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.
……………………….
Na Stella Kalinga, Simiyu
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajia kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2019, yatakayofanyika Kanda ya Ziwa Mashariki katika Viwanja vya Nyakabindi Mjini Bariadi kuanzia tarehe 29/07/2019 hadi 08/08/2019.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano maalum wa kutoa taarifa kwa Umma uliofanyika Mjini Bariadi, Julai 24, 2019.

Mtaka amesema Mhe Makamu wa Rais atafungua rasmi maonesho hayo Agosti Mosi, 2019 na waoneshaji mbalimbali zikiwemo Taasisi, Mashirika mbalimbali na wajasiriamali wataanza kuonesha teknolojia, huduma na bidhaa zao Julai 29, 2019 ikiwa ni maandalizi ya ufunguzi rasmi utakaofanywa na Mhe. Makamu wa Rais.

“Shughuli ya ufunguzi itafanywa tarehe 01/08/2019 na Mhe. Makamu wa Rai, haya ni maonesho ambayo yatakaribisha viongozi wa Kitaifa, Agosti 03, 2019 tutakuwa na Mhe. Waziri Mkuu, Agosti 06, 2019 tutakuwa na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda na Kilele tunatarajia kuwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli” alisema.

Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Omary Mgumba amesema ameridhishwa na maandalizi ya Maonesho ya nanenane yanayoendelea mkoani Simiyu na kutoa wito kwa wakulima na wananchi wote kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kushiriki katika maonesho haya ili kuja kujionea teknolojia mbalimbali zitakazojibu changamoto za wakulima, wafugaji na wavuvi.

Aidha, Mhe. Mgumba ametoa wito kwa waoneshaji kuwa wabunifu katika teknolojia, huduma na bidhaa watakazoonesha ili maonesho haya yawe chachu ya kuwasaidia wakulima, wavuvi na wafugaji kuongeza tija katika uzalishaji

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adam Malima amesema matarajio ya mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga inayounda Kanda ya Ziwa Mashariki ni kuwa na maonesho ya tofauti na mwaka jana, lengo likiwa ni kuifanya kanda hiyo kuwa ni mahali pa kudumu pa wakulima, wafugaji na wavuvi kuwa na maonesho ya kilimo biashara.

Maonesho ya Nanenane Kitaifa yanafanyika kwa mara ya pili sasa mkoani Simiyu tangu Kanda ya Ziwa ilipogawanywa katika kanda mbili yaani, Kanda ya Ziwa Mashariki(Simiyu, Mara na Shinyanga) na Kanda ya Ziwa Magharibi(Mwanza, Geita na Kagera) ambapo mwaka huu yanaadhimishwa chini ya kauli Mbiu:-“KILIMO, MIFUGO NA UVUVI KATIKA UKUAJI WA UCHUMI WA NCHI”

CHATO WAITAMANI DHAHABU YA KIJANI ILIYOPO WILAYA YA MUFINDI

0
0
Mkuu wa msafara huo Mkuu wa Wilaya ya Chato Eng. Mtemi Msafiri akipata maelezo kutoka kwa mkurugenzi wa Rasilimali Misitu na Nyuki TFS, Zawadi Mbwambo jinsi gani wanavyoweza kuzalisha miche ya miti ambayo inakuwa kwa muda mfupi sana
Mkuu wa msafara huo Mkuu wa Wilaya ya Chato Eng. Mtemi Msafiri akiwa na baadhi ya viongozi wa kutoka mkoa wa Geita walipokuwa kwenye ziara ya kutembelea shamba la miti ya kupandwa la Sao Hill lililopo mkoani Iringa
Moja kati ya maeneo ambayo yanatumika kuzalia miche ya miti




NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Uchumi wa wilaya ya Mufindi mkoani Iringa umetajwa kutegemea zao la miti katika kukuza uchumi na kuongeza pato la taifa tofauti ya wilaya nyingine kama Chato ambao wamekuwa wakitegemea ufugaji,uchimbaji wa dhahabu,uvuvi na kilimo.

Hiyo imebainika wakati wa ziara ya baadhi ya viongozi wa wilaya ya Chato,Mkoa wa Geita na viongozi wa vijiji vinavyolizunguka Shamba la Miti la Biharamulo lililopo mkoani Geita baada ya kutembelea Shamba la Miti Sao Hill linalosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa lengo la kujifunza shughuli mbalimbali za uendeshaji katika shamba hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari mkuu wa msafara huo Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhe. Eng. Mtemi Msafiri alisema kuwa kwa mara ya kwanza amejifunza faida kubwa inayotokana na zao la miti katika kukuza uchumi wa nchi na kujionea jinsi gani wananchi wa wilaya ya Mufindi wanavyonufaika na dhahabu ya kijani

“Leo ndio nimegundua kuwa zao la miti ni dhahabu ya kijani kwa namna inavyosaidia kukuza uchumi tofauti na walivyodhani hapo awali kwa namna ambavyo wao wamekuwa wakitegemea kuchimba dhahabu ambazo hazionekani tofauti na zao la miti ambavyo limekuwa linaonekana” alisema Eng Msafiri

Eng Msafiri alisema kuwa shamba la Miti Sao Hill ndilo shamba kubwa zaidi kati ya mashamba yote ya Serikali na ni nguzo ya maendeleo, na mkombozi wa mazingira wa Wilaya ya Mufindi na mikoa ya Nyanda za Juu Kusini nasi tumeona ni vema tujifunze kutoka kwa wenzetu.

“Tumejionea jinsi shamba hili lilivyo kuwa dhahabu ya ukuaji wa sekta ya viwanda vidogo na vikubwa vya uchakataji wa mbao, linavyosaidia kuongezeka kwa ari ya upandaji wa miti na utunzaji wa mazingira kwa wananchi wanaozunguka shamba na wananchi wa Wilaya za Mufindi, Kilombero na jamii jirani wamekuwa wakipatiwa gawio la asilimia 5 ya mrahaba kila mwaka”alisema Eng. Msafiri.

Eng. Msafiri anasema ziara hiyo imeweza kuwafumbua macho na kuona jinsi gani shamba hilo lilivyo toa fursa ya ajira zinazotokana na kazi za msimu za mashambani na viwanda tegemezi vya mazao ya misitu, fursa za uwekezaji, na ufugaji wa nyuki unaotokana na na uwepo wa misitu ya asili na ile ya kupandwa pamoja na vyanzo mbalimbali vya maji.

Awali akitoa ufafanuzi wa shamba la Sao Hill mkurugenzi wa Rasilimali Misitu na Nyuki TFS, Zawadi Mbwambo alisema shamba hilo ni miongoni mwa mashamba 23 ya miti ya kupandwa ya serikali ambayo yanasimamiwa na wizara ya maliasili na utalii kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).

“Shamba la Sao Hill lililopo hapa Mufindi lilianzishwa kwa majaribio mnamo mwaka 1939 hadi mwaka 1951 na upandaji kwa kiasi kikubwa ulianza rasmi mwaka 1960 hadi 1980 na shamba hilo linaukubwa wa hekta 135,903 ambazo zimehifadhiwa kwa ajili ya upandaji wa miti na uhifadhi wa mazingira” alisema Mbwambo

Mbwambo alisema shamba hilo limehamasisha kwa kiwango kikubwa upandaji wa miti kwa jamii inayolizunguka ambapo pia hutoa msaada wa mafunzo na miche ya miti kwa ajili ya kupandwa ili kupambana na uharibifu mkubwa wa misitu unaoendelea nchini.

“Takribani hekta 372,000 ya misitu inapotea kila mwaka na ili misitu hii isiweze kupotea tunatakiwa tuendelee kupanda angalau hekta 185,000 kwa mwaka kwa hapa Mufundi na Ukanda wote wa Nyanda za Juuu Kusini hamasa ya kupanda miti imekuwa kubwa kutokana na thamani inayoonekana Sao Hill kiasi kwamba imefikia hatua sasa Serikali inawaelimisha watu waache baadhi ya maeneo kwa ajili ya kilimo cha mazao mengine ya chakula na biashara” Alisema Mbwambo.

Kwa upande wake meneja wa Shamba la Miti la Biharamulo Thadeus Shirima alisema kupitia ziara hiyo ya siku mbili anaamini sasa kutakuwa na uelewa wa pamoja wa umuhimu wa shamba hilo katika kuleta maendeleo katika Kanda ya Ziwa na Tanzania kwa ujumla.

Thadeus alitoa shukurani kwa Mkuu wa Wilaya ya Chato, kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya Chato na Mkoa wa Geita, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato na Bukombe kwa msaada na maelekezo yao muhimu yaliyosaidia kuhakikisha uanzishwaji wa Shamba la Miti la Biharamulo unafanikiwa kwa kufanikisha kuwaondoa wananchi waliovamia msitu wa hifadhi Biharamulo ili kuanzishwa shamba hilo la miti.

Ziara hiyo ina wajumbe 45 ambao vingozi wa Wilaya na Mkoa wa Geita, Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Mkurugenzi wa halmashauri,Wenyeviti wa Vijiji, Madiwani, Maafisa tarafa, Jeshi la Zima moto na uokoaji, Mwenyekiti na katibu wa Chama cha Mapinduzi, baadhi ya Wakuu wa Vitengo na Idara za Halmashauri ya Wilaya, baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya , Katibu Tawala wa Wilaya na Wataalamu kutoka Shamba la miti Biharamulo.

WAKAGUZI NA BODI YA UNUNUZI TANGULIZENI UZALENDO DKT.KIJAJI

0
0
NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Ashatu Kijaji amewaagiza Wajumbe wa Bodi za Zabuni, Watendaji wa vitengo vya ununuzi, ukaguzi wa ndani na nje wa Taasisi za Serikali, kutanguliza uzalendo na uadilifu katika manunuzi ya umma, ili kusaidia Tanzania kufikia uchumi wa kati na uanzishwaji wa viwanda.

Akizungumza jana Jijini hapa katika uzinduzi wa kongamano la saba la mwaka la Usimamizi wa umma lililoandaliwa na Mamlaka ya udhibiti wa ununuzi wa umma (PPRA),Dk.Ashatu alisema Serikali kwenye bajeti yake inatumia zaidi ya asilimia 75 katika manunuzi ya umma hivyo kila mtaalamu akizingatia uadilifu Taifa litapiga hatua katika mipango
yake ya maendeleo.

“Eneo hili la manunuzi ni muhimu katika kutekelezwa miradi ya maendeleo, hivyo kila mtaalamu akiliheshimu na kutanguliza uzalendo na uadilifu taifa litafikia mipango yake yote iliyojipangia katika kufikia kiuchumi wa kati na uanzishwaji wa viwanda kabla ya mwaka
2025,”alisema.

Dk.Ashatu alipongeza PPRA kwa kufanya ukaguzi kwenye taasisi za umma na kuokoa fedha zaidi ya Sh.bilioni 46 sawa na asilimia 23 ya taasisi zilizokaguliwa.

“Lakini lazima tujiulize kwanini tunasubiri kukaguliwa hiyo ni kukosa kulitendea haki taifa letu pia tunakosa uzalendo,hivyo kila mmoja ahakikishe anatimiza wajibu wake katika nafasi yake,”alisema.

Aidha aliagiza taasisi zote za umma kuhakikisha zinatumia mfumo wa kimtandao wa manunuzi (E Procurement) na hawatasita kuzifungia taasisi zisizotumia mfumo huo.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Mhandisi Leonard Kapongo alisema kauli mbinu ya kongamano hilo ni:”Manunuzi katika miradi mikubwa kuelekea kiuchumi wa Viwanda.”

Alisema uchumi wa viwanda utafikiwa endapo maafisa hao watazingatia sheria za manunuzi katika miradi mikubwa inayotekelezwa nchini.

Mhandisi Kapongo alisema PPRA ni muhimu katika kuisaidia Serikali kutimiza malengo,kwani katika ukaguzi waliofanya karibuni katika manunuzi kwenye malipo ya Wakandarasi walibaini kufanywa malipo kinyume cha utaratibu na kuokoa zaidi ya Sh.bilioni 46.
Alisema anaamini ukaguzi huo ungefanyika katika taasisi nyingi wangeokoa fedha zaidi ya hizo na kuwezesha Serikali kutimiza malengo yake.

Aliongeza kuwa wameshindwa kukagua taasisi zote za umma,kutokana na changamoto ya ufinyu wa bajeti na baadhi ya taasisi za umma kutoa ushirikiano wakati wa ukaguzi.

Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya PPRA, Prof.Sufian Bukurura alisema Taasisi zao inauhaba wa Wafanyakazi kwani kwa sasa wapo 74 na mahitaji ni 152, hivyo aliomba Serikali kuwaongezea watumishi.

“Kwani tukiongezewa bajeti na wakaguzi itatusaidia kufanya ukaguzi zaidi ya Taasisi 100 tunazofanya sasa kati ya taasisi 540,mfano sasa tumekagua taasisi 100 nabtukaokoa zaidi ya Sh.bilionib46 je tungekagua zote zilizopo tungeokoa zaidi ya hizo,”alisema.

KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA ATAKA MABORESHO YA HAKI JINAI YAJENGE NA SIO KUKOMOA

0
0
Washiriki wa kikao kazi cha Maboresho ya Mfumo wa Haki Jinai wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Afya Ndg. Zainabu Chaula (hayupo pichani), alipotembelea kikosi kazi hicho kinachoendelea na maboresho jijini Dodoma.


Washiriki wa kikao kazi cha Maboresho ya Mfumo wa Haki Jinai wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Afya Ndg. Zainabu Chaula (hayupo pichani), alipotembelea kikosi kazi hicho kinachoendelea na maboresho jijini Dodoma.
*************

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt Zainabu Chaula ataka Haki Jinai itengeneze katika kujenga na sio kukomoana ili kuwa na jamii bora yenye kufuata misingi ya haki.Ameyasema hayo alipotembelea kikao kazi cha Maboresho ya Mfumo wa Haki Jinaikinachoendelea Jijini Dodoma kwa ajili ya kuupitia mfumo wa haki jinai nchini na kuangalia changamoto inazoukabili mfumo huo ili kuona kwa pamoja namna ya kufanya maboresho katika Mfumo wa haki jinai nchini.

“Haki Jinai itengeneze katika kujenga na sio kukomoana” amesema na kuongeza kuwa sehemu kubwa ya jamii haina uelewa wa kutosha kuhusu haki zao na hivyo kusababisha kukosa haki hizo na pale wanapofanikiwa kuzijua hawazipati kwa sababu anayetoa haki ni mbabe.

Hivyo akasisitiza elimu ya haki jinai isambae kwenye jamii kupitia njia mbalimbali ikiwemo vipindi vya redio na Runinga na njia nyingine mbalimbali ambazo zitakuza uelewa kwa jamii ili kuwawezesha kudai haki zao pale zinapokiukwa.

Katibu Mkuu huyo aliongeza kuwa nchi yetu ina mambo mengi mazuri ambayo jamii haiyajui ikiwemo suala zima la Haki Jinai na hivyo kusababisha ukiukwaji wa haki za msingi kwa jamii.

Mfumo wa Haki Jinai unafanyiwa maboresho katika maeneo ya Kisera, kisheria nakiorganizasheni ili kuufanya mfumo huo kuweza kuakisi changamoto za maendeleo zilizopo na zijazo.

Aidha, ameipongeza Wizara ya Katiba na Sheria kwa kukutanisha wadau mbalimbali ili kufanya maboresho ya mfumo wa haki jinai nchini.

TAFRIJA MAALUM KWA WAANDISHI WA HABARI KUADHIMISHA MIAKA 70 YA TAIFA LA CHINA

0
0
Balozi Mdogo wa China alioko Zanzibar Xie Xiaowu (katikati)akiwa na Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Dk,Juma Mohamed Salum wakichukua chakula katika tafrija maalum ya Chakula cha mchana kwa Waandishi wa Habari kuadhimisha kutimia miaka 70 ya Taifa la china hafla iliofanyika Hoteli Verde Maruhubi mjini Zanzibar.Waandishi wa Habari wakichukua chakula katika Tafrija maalum ya Chakula cha mchana kwa Waandishi wa Habari kuadhimisha kutimia miaka 70 ya Taifa la china hafla iliofanyika Hoteli Verde Maruhubi mjini Zanzibar.Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Dk,Juma Mohamed Salum akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kumaliza tafrija maalum ya Chakula cha mchana kwa Waandishi wa Habari kuadhimisha kutimia miaka 70 ya Taifa la china hafla iliofanyika Hoteli Verde Maruhubi mjini Zanzibar.
Baadhi ya Waandishi wa Habari waliohudhuria katika Tafrija maalum ya Chakula cha mchana kwa Waandishi wa Habari kuadhimisha kutimia miaka 70 ya Taifa la china hafla iliofanyika Hoteli Verde Maruhubi mjini Zanzibar.
Balozi Mdogo wa China alioko Zanzibar Xie Xiaowu akitoa hotuba katika Tafrija maalum ya Chakula cha mchana kwa Waandishi wa Habari kuadhimisha kutimia miaka 70 ya Taifa la china hafla iliofanyika Hoteli Verde Maruhubi mjini Zanzibar.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Dk,Juma Mohamed Salum akitoa hotuba katika Tafrija maalum ya Chakula cha mchana kwa Waandishi wa Habari kuadhimisha kutimia miaka 70 ya Taifa la china hafla iliofanyika Hoteli Verde Maruhubi mjini Zanzibar.
Balozi Mdogo wa China alioko Zanzibar Xie Xiaowu (kulia)akimkabidhi zawadi ya Kitabu Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Dk,Juma Mohamed Salum katika tafrija maalum ya Chakula cha mchana kwa Waandishi wa Habari kuadhimisha kutimia miaka 70 ya Taifa la china hafla iliofanyika Hoteli Verde Maruhubi mjini Zanzibar.Balozi Mdogo wa China alioko Zanzibar Xie Xiaowu (katikati)akiwa na Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Dk,Juma Mohamed Salum kushoto yake katika picha ya pamoja na Waandishi wa Habari mbalimbali katika tafrija maalum ya Chakula cha mchana kwa Waandishi wa Habari kuadhimisha kutimia miaka 70 ya Taifa la china hafla iliofanyika Hoteli Verde Maruhubi mjini Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.
…………………
Na Ali Issa,MaelezoSerikali ya Jamhuri ya Watu wa China imekuwa mshirika mkubwa wa kimaendeleo kwa Zanzibar katika sekta mbalimbali zikiwemo za kiuchumi na kijamii.

Hayo yamesemwa huko Hoteli ya Verde na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Dkt. Juma Muhammed Salum katika sherehe za miaka 70 ya kuundwa kwa Jamuhuri ya Watu wa China na miaka 55 ya uhusiano wa Kidiplomasia kati ya China na Tanzania.Amesema China ilikua ni nchi ya kwanza kuiunga mkono Zanzibar mara baada ya Mapinduzi ya mwaka 1964 na ushirikiano huo umekuwa ukiendelea hadi hivi sasa.

Aliongeza kusema kuwa China imekuwa mstari wa mbele kuisaidia Zanzibar na kuiletea maendeleo katika sekta mbalimbali zikiwemo afya, elimu, kilimo, utamaduni na michezo.Alikumbusha juu ya ujenzi wa hospitali ya Abdalla Mzee Pemba, ujenzi wa uwanja wa Michezo wa Amanai na Mao tse Tung na kusaidia kuleta madaktari na vifaa tiba kwa ajili ya Hospitali kuu ya Mnazimmoja na ile ya Mkoani.

Aidha alisema wameweza kusaidia ujenzi wa uwanja wa ndege wa Zanzibar na miundo mbinu ya Barabara na huduma za mawasiliano kwa kuweka taa katika barabarani mbali mbali za Zanzibar.Alisema uhusiano uliopo kati ya China na Tanzanzia ni wa kipekee kwani Rais wa kwanza wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere alikuwa kiongozi pekee alieweza kukutana na Baba wa Taifa la China Marehemu Mao mjini Beijing mara nyingi zaidi kuliko kiongozi mwengine yoyote katika uhai wake.
Aidha Mkurugenzi huyo alilieleza kuwa China imekuwa ikitoa elimu kwa vijana wa Zanzibar katika fani tofauti na imekuwa msaada mkubwa katika kuimarisha maendeleo ya kiuchumi Zanzibar.

Nae Balozi mdogo wa China aliepo Zanzibar Xie Xiaowu alisema kuwa Nchi yake imekuwa rafiki wa kweli na Tanzania na imekuwa mstari wa mbele kuongeza misaada yake kwa Taifa hilo na Afrika kwa Ujumla .

Aliongeza kuwa China inaendeleza juhudi za upatikanaji wa huduma za maji safi na salama mijini na vijijini kwa kuchimba visima vipya katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar na kujenga matangi mapya ya kuhifadhia maji Saateni na Kilimani.

SHILATU AIAGIZA TAKUKURU KUCHUNGUZA MRADI UJENZI GHALA

0
0


Na Mwandishi wetu Mihambwe

Afisa Tarafa Mihambwe *Ndugu Emmanuel Shilatu* hajaridhishwa na ujenzi mradi wa ghala uliotumia Tsh. Milioni 40 lakini umeshindwa kukamilika na kuiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kufanya uchunguzi mara moja juu ya ujenzi huo na namna fedha hizo zilivyotumika.

Gavana Shilatu aliyasema hayo alipotembelea ghala hilo lililopo Kijiji cha Kitama Shuleni kata ya Kitama na kusikitishwa namna ambavyo fedha nyingi zikitajwa kutumika huku mradi ukiwa haujafika ukamilifu tarajiwa kiasi kinachopelekea kijiji kukosa mapato jambo ambalo ni kero kwa Wanakijiji waliokuja kulalamika kwa Afisa Tarafa huyo.

*”Serikali imetoa fedha tangu 2012 lakini mpaka sasa mradi haujakamilika na hivyo kunapelekea mapato yanakosekana ambayo yangesaidia kuleta maendeleo kijijini na maeneo mengineyo pia. Hili halikubaliki hata kidogo, naiagiza TAKUKURU kuanza uchunguzi mara moja juu ya ujenzi huu wa ghala.”* Alisisitiza Gavana Shilatu.

Mradi huo wa ujenzi wa ghala lililopo eneo la Kitama Farmers Group kwenye kijiji cha Kitama Shuleni ulianza tangu mwaka 2012 lakini hadi Leo hii haujakamilika na hivyo kukosesha Serikali mapato.

Katika ziara hiyo Gavana Shilatu aliambatana na Mtendaji Kijiji Kitama Shuleni, Halmashauri ya Serikali iliyokuwepo Madarakani na ya sasa pamoja na Wazee maarufu Kijijini hapo ambao wote hawakuridhishwa na matumizi ya fedha ya ujenzi wa mradi huo.

Waziri Kalemani Amshukia Mkandarasi wa Usambazaji wa Umeme wa REA


TRA ITAENDELEA KUWEKA MAZINGIRA YA UWAZI KUDHIBITI MIANYA YA RUSHWA

0
0
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akifungua kikao cha kuwasiliza wafanyabiashara na kupokea maoni yao juu ya sera,sheria, kanuni na taratibu za ukusanyaji kodi kwa mkoa wa Tanga kilicho hudhuriwa na Naibu Kamishna Mkuu wa TRA Msafiri Mbibo kushoto kulia ni Kamishna Msaidizi wa Forodha wa TRA kutoka makao makuu Benard Asubisye 
Naibu Kamishna Mkuu wa TRA Msafiri Mbibo akizungumza wakati wa kikao hicho
KAMISHNA Msaidizi wa Kodi za Ndani kutoka Makao Makuu Abdul Mapembe akizungumza wakati wa kikao hicho kushoto ni Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure
KAMISHNA wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa TRA kutoka Makao Makuu Ben Asubisye akizungumza wakati wa kikao hicho kulia kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa
MMOJA wa wafanyabiashara akichangia kwenye kikao hicho
Sehemu ya wadau wa kikao hicho wakifuatilia matukio mbalimbali
Sehemu ya wadau wakifuatilia kikao hicho
Sehemu ya wadau wa kikao hicho wakifuatilia matumio mbalimbali

Sehemu ya wafanyabiashara na wadau mbalimbali wakifuatilia kikao hicho

Meneja wa Hotel ya Tanga Beach Joseph Ngoyo kushoto akiwa na Meneja wa NMB Tawi la Madaraka Elizaberth Chawinga wakifuatilia matukio mbalimbali

SEHEMU ya wafanyabiashara na wadau wakiwa kwenye kikao hicho

MKURUGENZI wa kampuni ya Katani Limited Juma Shamte akichangia kwenye kikao hicho

NAIBU Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Msafiri Mbibo amesema kwamba mamlaka hiyo itaendelea na utekelezaji wa mikakati ya kuhakikisha wanakuwa na mazingira ya uwazi na uwajibikaji katika utendaji wa watumishi wao itakayojumuisha pamoja na kuzibiti mianya ya rushwa kupitia mifumo ya Tehama. 

Mbibo aliyasema hayo leo wakati wa kikao cha kuwasikiliza wafanyabiashara na kupokea maoni yao juu ya sera,sheria ,kanuni na taratibu za ukusanyaji wa kodi kwa mkoa wa Tanga ikiwemo kuziangalia changamoto zinazowakabili ambapo alisema katika suala hilo wafanyabiashara wanapaswa kutoa ushirikiano ili kuweza kuhakikisha vitendo vya namna hiyo vinakomeshwa.

“Wafanyabiashara tunaomba ushirikiano wenu lakini pia niwaambie kwamba kwenye suala la uadilifu ni muhimu katika utendaji wa shughuli zenu za kila siku na hatutakuwa tayari kuona watumishi wanajihusisha na vitendo vya rushwa na kunyamaza tutaendelea kuchukua hatua kali dhidi yao “Alisema 

Alisema wataendelea na utekelezaji wa mikakati ya kuhakikisha wanakuwa na mazingira ya uwazi na uwajibikaji katika utendaji kazi kwa watumishi wao kwa kuchukua hatua za haraka na nidhamu kwa watumishi wasio waaminifu huku akiwataka wadau mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara kuwafichua watumishi wanaohusika na vitendo vya rushwa miongoni mwa wale wasio waaminifu 

Hata hivyo aliwataka wafanyabiashara na jamii kwa ujumla kuhakikisha wana kuwa mstari wa mbele kuchangia maendeleo ya nchi yao kwa kulipa kodi kwani kodi hiyo inayopatikana kutokana na shughuli za kiuchumia ambazo zinafaywa na raia wa nchi hii. 

“Lakini sisi tutaendelea kuchukua juhuidi za makusudi kuhakikisha mfumo wa ulipaji kodi unakuwa rahisi utakaowezesha wafanyabiashara kuweza kuendesha biashara zake bila wasiwasi na kuweza kuzianisha na kuweza kuzitafutia ufumbuzi”Alisema Naibu Kamishna huyo wa TRA. 

Hata hivyo aliwaeleza wafanyabiashara mambo machache ambayo ni muhimu kuweza kupewa uzito ni utunzaji wa kumbukumbu sahihi za biashara ambalo ni jambo muhimu kwa ukuaji wa biashara muhimu kwa TRA na mfanyabiashara. 

“Lakini pia ni muhimu kwa vyombo vyengine ikiwemo vya fedha kwani zitasaidia uzibiti wa matumizi ya biashara pia kusaidia ukokotoaji sahihi hivyo kuondoa malalamiko yasiyo ya lazima yanayoweza kujitokeza kati ya mlipa kodi na taasisi inayosimamia ulipaji wa kodi”Alisema 

Awali akizungumza Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella alimshukuru Naibu Kamishna huyo wa TRA kwa kufika mkoani humo kukutana na wafanyabiashara ambao ni uamuzi wa hekima,busara na ushirikiano . 

Alisema ushirikiano huo ulipelekea mwaka jana makusanyo kwa mkoa huo yalikuwa sio chini ya asilimia 80 lakini mwaka huu tumefikia si chini ya asilimia 91 hivyo tutaendelea kushirikiana kuziba mianya ya upotevu mapato ikiwemo uletaji bidhaa za magendo. 

“Magendo ni tatizo kubwa sana sio tu kwa wafanyabiashara miongoni mwenu mpo mnafuata sheria lakini baadhi yenu mnapitia nyia za panya kuleta magendo na kuuza bei ya chini na wanaofuata utaratibu wanaumia hivyo mapambano dhidi ya magendo yanaendelea hivyo nashukuru kwa ushirikiano huo tumepunguza shehena ya mzigo ambao ilikuwa inakamtwa kila mara “Alisema

SERIKALI YA CHINA NA TANZANIA KUENDELEZA USHIRIKIANO KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA MALARIA

0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (kushoto) pamoja na Naibu Waziri wa Afya kutoka China Mhe. Lin Bin wakiwa wameshikilia dawa ambazo hutengenezwa nchini China mapema leo wakiwa Ikwiriri-Rufiji Mkoani Pwani kuzindua Mradi wa Ushirikiano baina na China na Tanzania katika Kupambana na Ugonjwa wa Malaria Wilayani Rufiji.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (kushoto) akiangalia kinga za ugonjwa wa malaria pamoja na Naibu Waziri wa Afya kutoka China Mhe. Lin Bin leo Ikwiriri-Rufiji Mkoa wa Pwani kabla ya uzinduzi wa mradi wa ushirikiano wa pamoja kati ya China na Tanzania kupambana na ugonjwa wa malaria Wilayani Rufiji.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akipima ugonjwa wa Malaria leo Ikwiriir Wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani alipoenda kuzindua Mradi wa Ushirikiano wa pamoja baina ya Tanzania na China wa kupambana na ugonjwa wa malaria Wilayani Rufiji.
Picha ya pamoja Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (wa kati kati mstari wa chini) akiwa na Naibu Waziri wa Afya China Mhe. Lin Bin aliyeongozana na wataalam wake kutoka China pamoja na wataalam na wadau wa sekta ya afya nchini.

****************

Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China imeahidi kuendelea kutoa
ushirikiano kwa Serikali ya Tanzania katika mapambano dhidi ya Malaria
ili kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi salama isiyo ya maambukizi ya
Ugonjwa huo.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya kutoka Uchina Mhe. Lin
Bin alipotembelea Ikwiriri, Rufiji Mkoa wa Pwani katika mradi wa
ushirikiano wa pamoja baina ya China na Tanzania katika kudhibiti
ugonjwa wa malaria huku akiongozana na mwenyeji wake Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu.

“China kuwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa kimatafa tutaendelea
kushirikiana kwa pamoja katika kusaidia Tanzania inafikia malengo ya
kutokomeza ugonjwa wa malaria” amesema Mhe. Lin Bin na kuendelea
kusema Ugonjwa wa malaria unatibika na kuzuilika
Waziri Lin Bin amesema kuwa ushirikiano baina ya Tanzania na China
umeleta manufaa katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria kwa
kupunguza kiwango cha maambukizi ya ugonjwa huo Wilayani Rufiji
kutoka asilimia 25 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 4.9 mwaka 2019.

“Kwa muda wa miaka 60 tumekuwa tukipambana dhidi ya ugonjwa wa
malaria ambao umeathiri zaidi ya watu milioni 30, na tangia mwaka 2017
hakuna taarifa zilizolipotiwa kuhusu ugonjwa wa malaria nchini China”
amesema Mhe. Lin Bin huku akiipongeza Tanzania kwa mikakati mizuri
yenye lengo la kuhakikisha inatokomeza ugonjwa wa malaria.

Kwa upande wake Waziri wa Afya Tanzania, Mhe. Ummy Mwalimu
ameishuruku Serikali ya China inayoongozwa na Rais Xi Jinping kwa
kuendeleza ushirikiano wa enzi uliopo wa baina ya nchi hizo.

Waziri Ummy amesema kuwa ugonjwa wa malaria bado ni tatizo kubwa
sana nchini Tanzania, huku takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO)
zikionyesha kuwa asilimia 55 ya vifo vitokanavyo na malaria vinatoka
katika nchini saba za Bara la Afrika ikiwemo Tanzania.

“Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe
Magufuli tumechukua hatu ambali mbali kwa kushirikiana na wadau
wakiwemo China kupambana na malaria na yapo mafanikio makubwa
ambayo tumeyapata” Amesema Waziri Ummy Mwalimu na kuendelea
“Tumeweza kupunguza kiwango cha maambukizi ya malaria kutoka
asilimia 14.7 mwaka 2015 hadi 7.3 mwaka 2018”.

Amesema kuwa wagonjwa wapya wa malaria wamepungua kwa asilimia
26 kutoka watu 161 katika kila watu 1000 mwaka 2014 hadi kufikia 119
katika kila watu 1000 mwaka 2018 huku vifo vitokanavyo na malaria
vimepungua kwa asilimia 55, kutoka vifo 20 katika watu 1000 mwaka
2014 hadi kufikia vifo 9 kati ya watu 1000 mwaka 2018.

“Serikali ya Tanzania itaendela kuchukua hatua kwa kushirikiana na
wadau wetu wakiwemo Serikali ya China kuhakikisha tunapunguza
kiwango cha maambukizi ya maralia hadi kufikia asilimia 1 ifikapo mwaka
2020” alisema Waziri Ummy Mwalimu.

HILI NDO JENGO PEKEE LA TAMISEMI LINALOVUTIA MJI WA SERIKALI

0
0

Shikamoo TAMISEMI!!

Heshima hii inakuja baada ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) kukamilisha jengo lake ambalo kwa hakika ni jengo linalovutia katika mji wa Serikali.

Aprili mwaka huu, Viongozi wa wizara hiyo wakiongozwa na Waziri Selemani Jafo walitekeleza agizo la Rais John Magufuli alililolitoa la kuzitaka Wizara zote kuhamia katika mji huo.

Kutokana na agizo hilo, viongozi hao walihamia na kufanya kazi ya kuwahudumia wananchi ndani ya mabanda ya mabati yaliyokuwapo kwenye jengo hilo ambayo yanatumiwa na mkandarasi.

Ikiwa ni miezi minne tangu kufanya kazi zao kwenye mabanda kwasasa wapo ndani ya jengo hilo zuri na la kuvutia.Ama kwa hakika subira yavuta heri na baada ya dhiki ni faraja, kweli TAMISEMI mmeonesha ubora wenu kwenye matumizi ya mfumo wa Force Account.

Akizungumza leo kuhusu jengo hilo, Waziri huyo amesema siri ya mafanikio ya ujenzi wa jengo hilo zuri ni matumizi ya Force Account kwa gharama ya Sh.Bilioni moja na imethibitisha kwamba Serikali ya Dk.John Pombe Magufuli inaweka alama zisizofutika.

"Niwapongeze Viongozi na watendaji wote wa OR-TAMISEMI kwa ubunifu ulio tukuka,"amesema .Ameongezea kuwa Yajayo yanafurahisha kwani siku chache zijazo Jengo lingine Pacha la Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini(TARURA) litaongeza kunogesha Mji wa Serikali.

BBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI JULAI 25, 2019

TAHA WATAKIWA KUFANYA TAFITI ZA KUWAKOMBOA WAKULIMA NCHINI TANZANIA

0
0
 Mgeni rasmi Afisa Kilimo wa mkoa wa Morogoro Isabela Chilumba akipewa maelezo juu ya kilimo cha kisasa cha nyanya kutoka kwa Meneja mradi huo Naimana. 
 Afisa Kilimo wa mkoa wa Morogoro Isabela Chilumba akiongea na wakulima na wageni waalikwa wakati wa sharehe za wakulima wa mazao ya mboga mboga yaliyoandaliwa Taasisi ya Tanzania Horticultural Association SASI (TAHA) iliyofanyika katika mjini Morogoro. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG, Morogoro. Meneja miradi Taasisi ya Tanzania Horticultural Association SASI (TAHA) Bi. Elianchea Shanga akiongea na wakulima na wageni waalikwa wakati wa sharehe za wakulima wa mazao ya mboga mboga yaliyoandaliwa taasisi ya TAHA iliyofanyika katika mjini humo. Wakulima wa Mboga Mboga akinyoosha mikono kujitambulisha.
 Meneja mradi Naimana akizungumza wakati akitambulisha mradi huo huku wakulima na wageni waalikwa wakifuatilia.
 Mmiliki wa shamba la nyanya la kisasa akiongea machache.
Meneja miradi TAHA Bi. Elianchea Shanga akiwatambulisha mabwana shamba wanaosaidia kufundisha wakulima.
 Wafanyakazi wa TAHA wakitoa elimu kwa wakulima.
 Kilima cha kisasa cha nyanya.

 Vingozi wa kijiji wakiwa na Mgeni rasmi.
Wakulima wakiwa na mgeni rasmi. 

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG, Morogoro.

 Watafiti wa mazao ya kilimo nchini wametakiwa kuhakikisha tafiti zao zinawafikia wakulima wadogo wadogo hasa waliopo vijiji ili wakulima hao waweze kulima kilimo chenye tija ikiwa ni katika kubabiliana na changamoto ya ushindani wa masoko kitaifa na kimataifa. 

 Rai hiyo imetolewa na Afisa Kilimo wa mkoa wa Morogoro Isabela Chilumba, wakati wa sharehe za wakulima wa mazao ya mboga mboga yaliyoandaliwa Taasisi ya Tanzania Horticultural Association SASI (TAHA) iliyofanyika katika mjini Morogoro. Bi. Chumba amesema kuwa watafiti hao endapo watafanya zao vyema zinaweza kumkomboa mkulima na akaweza kupata soko bora la mazao yao na itawakwambua kiuchumi. 

"Niwashukuru wataalamu maana nyie mmekuja wakomboa wakulima wadogo ambao mara nyingi huwa ni  ngumu kufikiwa matokeo yake wamekuwa wakilima kilima cha mazoea ambacho hakina manufaa kwao," amesema. Nae Meneja Miradi ya Taasisi ya TAHA, Bi. Elianchea Shanga amesema kuwa kwa sasa wamesambaa mikoa mbali mbali ya Tanzania na lengo lao kubwa ni kumkomboa mkulima kutoka katika kilimo cha mazoea na kulima kilimo cha tija.

 "Sisi lengo kubwa mkulima aone dhamani ya kile anachokilima maana tunasimamia kuanzia kuandaa shamba, madawa na mbolea huku tukimpa ushauri na kumtafutia soko," amesema. Kwa upande wao wakulima Mwajuma Abdala wamefurahishwa na ujio wa Taasisi ya TAHA huku wakielezea kuwa changamoto kubwa ambayo imekuwa mwiba kwao kwa sasa ni mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo yamepelekea ukosefu wa mvua huku wakiiomba serikali kuongezea nguvu katika kusaidia kilimo cha umwagiliaji.

TUMEAMUA KUFANYA MABADILIKO MAKUBWA YA KUWATAMBUA WAKULIMA WOTE NCHINI-MHE HASUNGA

0
0
Sehemu ya Wakazi wa kijiji na kata ya Kilimampimbi wakimlaki mbunge la Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe Mhe Japhet Hasunga ambaye ni Waziri wa Kilimo wakati alipowasili kijijini hapo tarehe 25 Julai 2019 akiwa katika ziara ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo jimboni humo. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Sehemu ya Wakazi wa kijiji na kata ya Kilimampimbi wakimsikiliza mbunge la Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe Mhe Japhet Hasunga ambaye ni Waziri wa Kilimo wakati akihutubia wananchi kijijini hapo tarehe 25 Julai 2019 akiwa katika ziara ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo jimboni humo.
Wakazi wa kijiji cha Ikomela kilichopo kata ya Kilimampimbi wakimsikiliza mbunge la Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe Mhe Japhet Hasunga ambaye ni Waziri wa Kilimo wakati akihutubia wananchi kijijini hapo tarehe 25 Julai 2019 akiwa katika ziara ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo jimboni humo.
Wananchi wa kijiji cha Chizumbi kilichopo kata ya Isandula wakimsikiliza mbunge la Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe Mhe Japhet Hasunga ambaye ni Waziri wa Kilimo wakati akihutubia wananchi kijijini hapo tarehe 25 Julai 2019 akiwa katika ziara ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo jimboni humo.



Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songwe

Wizara ya Kilimo inaendelea na mkakati madhubuti wa kuwatambua wakulima wote nchini ili kuwa na ufahamu wa watu wanaopaswa kuhudumiwa kwa ajili ya pembejeo za kilimo.

Mkakati huo wa wizara wa kuwatambua wakulima nchini unahusisha usajili wa wakulima ili kubaini mahali wanapoishi, ukubwa wa mashamba yao na mazo wanayolima.

Hayo yamebainishwa leo tarehe 25 Julai 2019 na Mbunge la Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe Mhe Japhet Hasunga ambaye ni Waziri wa Kilimo wakati akizungumza kwenye mikutano ya hadhara katika kijiji cha Chizumbi, Ukwile, Chimbuya katika kata ya Isandula pamoja na Kijiji cha Ikomela, Isandula na Kilimampimbi vilivyopo kata ya Kilimampimbi wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo jimboni humo.

Alisema kuwa asilimia kubwa ya waTanzania wanawategemea wakulima katika kukamilisha mahitaji yao lakini wakulima hao hawatambuliki, hivyo mkakati wa utambuzi wa wakulima utaimarisha uwezekano wa kuwahudumia ili kuongeza tija na uzalishaji wa mazao mbalimbali.

Mhe Hasunga pia amewaeleza wananchi hao lengo la serikali kuanzisha mradi mkubwa wa ujenzi wa treni ya kisasa itakayorahisisha huduma za kijamii ikiwemo usafirishaji wa mizigo yakiwemo mazao ya wakulima.

Pia amesema kuwa serikali inaendelea na mchakato wa kuwafikishia wananchi huduma bora ikiwemo upatikanaji wa umeme katika maeneo yote vijijini.Kuhusu sekta ya Kilimo Mhe Hasunga amesema kuwa katika kipindi cha muda mrefu wakulima wamekuwa wakilima lakini matokeo yake wanapata hasara au kipato cha kujikimu hivyo ili kupata faida na tija ni wazi kuwa wakulima lazima wabadilishe mtazamo ili waweze kuwa na Kilimo chenye tija na kibiashara.

Alisema wizara yake imejipanga kutoa elimu bora kwa wakulima juu ya Kilimo ili kufuata taratibu za Kilimo bora zinazotolewa na wataalamu mbalimbali wa Kilimo katika vijiji.Kadhalika Mhe Hasunga amesikitishwa na wananchi kutokula vizuri ilihali wao ndio wazalishaji wakubwa wa mazao ya mbogamboga na matunda.

"Ukienda mahospitalini watu wengi wanaoumwa ni wakulima, kwahiyo nawasihi wakulima mkizalisha chakula muwe wa kwanza kula vizuri halafu ziada ndio mkauze" Alisisitiza Mhe Hasunga

WAZEE WILAYA YA ARUMERU WAIOMBA SERIKALI IWASAIDIE VITAMBULISHO VYA HUDUMA YA AFYA BURE KWA WAZEE

0
0
Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha 

Wazee wa halmashauri ya wilaya ya Arumeru wameiomba serikali kuwasaidia kuwapatia Vitambulisho vya wazee ,vitakavyo wawezesha kupatiwa huduma za afya bure popote pale wanapopata matatizo ya kiafya

Aidha pia wameiomba serikali kiwasaidia kupata huduma za kunusuru kaya maskini na zisizo jiweza (Tasaf )kwani katika vijiji vyao hawajapatiwa na kuna wanavijiji wengi ambao ni maskini na wasiojiweza.

Waliyasema hayo  wakati wakizungumza katika mkutano ulioandaliwa na mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mkutano wa halimashauri ya wilaya Arusha mkutano uliowashirikisha wazee wa kimila ,viongozi wa dini, pamja na viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa 

Wazee wamesema kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakikumbana na changamoto mbalimbali zikiwemo za ubovu wa miundombinu ya barabara gharama kubwa ya maisha, ukosefu wa mitaji ,huku wakiwataka mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kuwasogezea huduma ya kupata Vitambulisho hivyo karibu kwani sehemu ambayo wameipanga ni mbali na inawapa changamoto kubwa wazee hao kufika.

"Nida walikuja kutoa elimu wakataka tujiandikishe ,na tumejiandikisha sasa wanatuambia tutembee adi halimashauri tukachukue sisi ni wazee tutaendaje uko tutavukaje barabara kwenda huko hivyo tunaiomba serikali itusaidie kuwaambia Nida watusogezee huduma hii kama walivyokuja kutupa elimu katika ofisi za kata watuletee nahivyo Vitambulisho katika kata zetu" alisema mmoja wa wazee hao aliejitambulisha kwa jina la Maxtone Mollel 

Aisha pia wazee hao walitumia mda huo kuiomba serikali kugawanya wilaya ya Arumeru ili waweze kupata huduma kiurahisi karibu na maeneo hao kwani wazee wengine pamoja na wananchi wanalazimika kufata huduma katika makao makuu ya wilaya kwa umbali mrefu ,ambapo walifafanua kubwa walikuwa wakitumia mda mrefu kufata huduma katika makao makuu ya halmashauri ya wilaya hiyo.

"Tunampongeza sana rais magufuli kwa kazi anayofanya kwani kazi a anayofanya ni nzuri na hawa ndio viongozi tuliokuwa tunawataka maana katika uongozi wake tu ameshatuletea mandege ambayo tulikuwa hatuna sasa ivi tunandege nane ,katuletea elimu bure ambapo enzi zetu tulikuwa tunaziita elimu za upe ,katutengenezea barabara sasa na bado anafanya kazi kwanini tusimuite Nyerere mdogo,pia tunapenda kumpongeza mkuu wetu wa wilaya Jerry Muro kwani amesimamia wilaya yetu vyema kuanzia sekta ya elimu,Afya, maji na zinginezo" walisema wazee hao.

Akiongea na wazee hao mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro aliwashukuru wazee hao kwa kupokea wito wake huku akitaja lengo kuwaita ni kusikia changamoto mbalimbali zinazowakabili wazee hao pamoja kuzungumza ,kuangalia namna ya kuzitatua pamoja na kupata ushauri mbalimbali kutoka kwao kwani wazee ni hazina . 

Aliwataka wazee wasipotoshwe na wanasiasa Bali watumie akili zao kupembua ukweli ni upi ,kwani wakiwasikiliza wanasiasa baadhi ni waongo na hawatekelezi yale ambayo wanahaidi kipindi ambacho wanaomba kura ,huku akiwataka wazee kuendelea kuwaasa Vijana na kuwashauri kuendelea kupenda na kuilinda Tanzania yetu.

Aliwahakikishia wazee hao kutatua kero zao zote ambazo wamezitaja kuanzia kero za Vitambulisho vya huduma za matibabu kwa wazee ambapo alisema kuwa kuanzia sasa wazee wote watakao enda katika vituo vya Afya, wapewe huduma bure kwa haraka na at a kama mzee atakuwa amesahau kitambulisho kinachomtambulisha ,au bima ya afya apatiwe huduma kwanza ndio mengine yafuate,huku akitoa maelekezo kwa wakurugenzi wa halmashauri zote mbili kuhakikisha Ndani ya miezi miwili wazee wawe wamepatiwa Vitambulisho vya huduma za Afya .

"Napenda kuwaambia kuanzia leo mzee yeyote akienda hospitalini apatiwe matibabu bure bila kudaiwa chochote na apatiwe dawa zile zote za msingi zilizopendekezwa na katika halmashauri zetu dawa zetu zote zenye msingi zipo Nana napenda kuwaambia mzee yeyote ambaye atanyimwa huduma anipigie aniambie amekosa huduma ili nimchukulie hatua Kali Mtumishi Huyo maana nyie wazee ni hazina " alisema Muro

Aidha aliwahaidi wazee hao kupitia mabaraza yao kuwapatia kiasi cha shilingili milioni tano kwa ajili ya kutunisha mifuko yao ya wazee hao

Naye Mkurugenzi wa halmashauri ya Arusha Wilson Mahela alisema kuwa serikali ya awamu ya tano inawaheshimu sana na kuwajali wazee na ipo tayari kutatua kero zao zote zinazowakabili.
 Mmoja wa mzee akitoa changamoto yake katika kikao cha wazee wa wilaya ya Arumeru kilichoandaliwa na mkuu  wa wilaya hiyo.
 Mkurugenzi wa halmashauri ya Arusha  Wilson Mahela akiongea na wazee hao.
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro  akiongea na wazee  wa halmashauri ya wilaya ya Arumeru wakati alipokutana nao kujadili changamoto zinazo wakabili wazee hao.

ANNA MWAOLE BADO ‘ANATESA’ KATIKA MUZIKI

0
0
Na Moshy Kiyungi,Tabora.

Baadhi ya Wanawake wanapofikisha umri wa zaidi ya miaka 50, huonekana ‘kuchoka’, hawana uwezo wa kufanya kazi za nguvu nyingi, lakini dhana hiyo ni tofauti kwa Anna Mwaole.

Mama huyu ni mwanamuziki mkongwe, aliyetimiza miaka 54 mwaka huu 2019.

Yawezekana baadhi ya watu hawamfahamu mwanamuziki huyo ambaye amepanda na kushuka milima na mabonde hadi kukubalikana na wapenzi wa muziki wa dansi na taarabu hapa nchini.

Anna Mwaole amefanikiwa kutimiza malengo yake baada ya kyakwepa majaribu lukuki aliyokumbana nayo hususan katika tasnia hiyo ya muziki.

Ni mama aliyejaaliwa vipaji vingi vikiwemo vya uigizaji, uimbaji wa nyimbo za dansi na taarabu.

Mwaole ukimwangalia kwa wasiwasi hauwezi kuamini kama anaweza kulishambulia jukwaa kwa kucheza hasa ukizingatia umbo lake la mwili lilojaa minofu kila maeneo.

Uzoefu na vipaji vyake aliviendeleza baada ya kupitia katika bendi mbalimbali za muziki wa dansi alizopitia na vikundi vya taarab.

Anna Mwaole alizungumza na mwandishi wa makala hii alisema kuwa yeye ameimba nyimbo nyingi za muziki wa dansi na taarabu, katika bendi zaidi ya nane hapa nchini akitafuta maisha na harakati za kujiedeleza kimuziki.

Historia ya maisha ya Mwaole mwenye asili ya mkoa wa Iringa, inaanzia katika mji wa Mpwapwa mkoani Dodoma, ambako mama huyo ndiko alikozaliwa mwaka 1965.

Anna akiwa yu ngali kigori, alikuwa akihusudu sana sauti na uimbaji wa mwanamuziki wa kike toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Marikirala Mboyo ‘M’bilia Bel’.

Alisema kila mara alikuwa akinunua kanda za M’bilia, akanza kujifunza kuimba nyimbo zake.Mwaole alijiunga katika kwaya ya Kanisa mjini Mpwapwa 1989, akiwa na Rahma Shaari.

Anasimulia kuwa yeye na Rahma Shaari walikuwa waimbaji wakutegemewa katika kwaya ya Kanisa hilo.Anna Mwaole alifafanua kwamba kabla ya hapo yeye na Ramha Shaari walikuwa waumini wa dini wa Kikristo.

Alimuelezea Rahma kwamba alikuwa akiitwa Grace, lakini baada ya kuolewa na mwislamu, akalazimika kusilimishwa akapewa jina hilo la Rahma.Halikadharika yeye Anna naye aliolewa na mwanamume mwislamu aliyemtaja kwa jina la Rashidi Nyambya.

Huyo ndiye aliyesababisha kusilimu na kuingia dini ya kiislamu, akachagua jina la Sauda.Sauda Mwaole anamtaja Rahma Shaari kuwa ndiye aliyechangia kwa kiasi kikubwa kwa yeye kuingia katika tasnia ya muziki wa dansi, muda mfupi baada ya kufika jijini Dar es Salaam mwaka 1988.

Alisema wakati huo alimkuta Rahma akiimba katika bendi ya Maquis du Zaire, ambapo alimuombea nafasi ya kuimba katika bendi hiyo mwaka 1989.

Sauda alifafanua kwamba ushawishi wa Rahma kwa uongozi wa Maquis ulifankiwa, akaitwa na kufanyiwa usaili kwa kuimba wimbo wa ‘Nakei Nairobi’ wa M’bilia Bel na ule wa ‘Kama umenichoka mpenzi’ ulioimbwa na Issa Nundu wa bendi hiyo.

Wimbo wa ‘Nakei Nairobi’ kwake ilikuwa kama ‘kumsukuma mlevi’ kwani tayari alikuwa amezifanyia mazoezi nyimbo zote za M’bilia Bell toka wakati akiwa Mpwapwa.

Kwa majigambo Sauda Mwaole alisema aliuimba wimbo huo kwa kujiamini hadi baadhi ya viongozi wa bendi hiyo wakiwemo akina Chibangu Katayi ‘mzee Paul’, Chinyama Chiyaza, Nguza Mbangu ‘Vicking’ na Tshimanga Kalala Assosa, hawakuamini masikio yao, walimkubali papo hapo akapata ajira.

Siku ya kwanza kupanda stejini akiwa na Maquis du Zaire, Mwaole anaeleza kwamba alitetemeka mno mara alipoambiwa kuimba mbele ya wapenzi na mashabiki katika ukumbi wa Wapi wapi’s Bar iliyokuwa Chang’ombe Maduka mawili.

“Nilitamani ardhi ipasuke, nitumbukie humo. Nilihofu hasa baada ya kuona jinsi wapenzi na mashabiki wa Maquis waliokuwa wamefurika ukumbini humo wakiniangalia mimi ” alitamka Mwaole.

Lakini anamshukuru mungu alimpa ujasiri akaimba kwa umahiri mkubwa wimbo wa ‘Kama umenichoka mpenzi’ akishirikiana na Issa Nundu.Sauda Mwaole alisema alipoimba wimbo wa ‘Nakei Nairobi’, watu waliinuka kwenye viti vyao wakishangilia na kumtuza pesa, huku wakitamka kwamba wamepata M’bilia Bell wa Tanzania.

Walitamka hayo kwa vile sauti na uimbaji wake haukutofatiana na wa Bell.
Mwaole alisema hatoweza kuisahau siku hiyo katika maisha yake, kwa kuwa ndiyo ilikuwa imemfungulia ukurasa mpya wa maisha yake katika fani ya muziki.

Mwezi Septemba 1989, alichukuliwa katika bendi ya Polisi Jazz, ambako alilazimika kwenda ‘depo’ za kijeshi kwa miezi mitatu, Kilwa road jijini Dar es Salaam.Akiwa katika bendi hiyo alikutana na wanamuziki wengine anawataja kwa majina ya akina Mobari Jumbe, Maimuna Ramadhani, Hamza Mwanamasingi, Ali Moshi na wengine wengi.

Akiwa na Polisi Jazz alitoka na wimbo wa ‘Sitaki sitaki visa vyako’ wimbo uliotungwa na Mobari Jumbe.

Mwaole alipenda kujiendeleza zaidi katika fani hiyo ya muziki, hivyo akaondoka kwenda kujiunga na bendi ya Bantu Group, iliyokuwa ikiongozwa na ‘mzee wa madongo’ Komandoo Hamza Kalala.

Akiwa Bantu Group alikutana na vijana wengine chipukizi akina Muumini Mwinjuma, Musemba wa Minyungu, Rogers na wapiga gitaa Magele Sange na Ali Adinani.

Alisema hakutarajia kwamba ipo siku angelikuja kuingia katika studio kurekodi nyimbo. Lakini kwa mara ya kwanza aliweza kuingia studio kurekodi wimbo wa ‘Emma tupunguze matumizi yasiyo ya lazima’

Safari ya Mwaole haikuishia hapo, kwani mwishoni mwa 1991, alijiunga katika bendi ya Orchestra Makssy iliyokuwa ikiongozwa na Mzee Kitenzogu Makassy.

Baada ya mwaka mmoja kupita ‘alichupa’ na kwenda kujiunga na bendi ya Lego Stars, iliyokuwa na wakali akina Joseph Bartholomew Mulenga ‘King Spoiler’(solo), Anania Ngorika, Kapaya Vivi na Chibanda Sonny (waimbaji)

Bendi ya Legho iliposambaratika, Mwaole akaenda kujiunga na Kikumbi Mwanza Mpango ‘King Kiki’ na bendi yake ya La Capitale.

Nyota yake ikamuangazia zaidi kwani Januari 1993, alijiunga katika bendi ya Washirika ‘Watunjatanjata’ Bendi hiyo ilikuwa na wanamuziki wakubwa ambao waliweza kumsaidia kuinua kipaji chake cha kuimba.

Aliwataja wanamuziki hao kuwa ni pamoja na Madaraka Morris, Adam Bakari ‘Sauti ya zege’, Eddy Sheggy na Christian Sheggy na Mhina Panduka’ Toto tundu’

Hapo napo akaona hapatoshi, akajiengua kati ya mwaka 1993 hadi 1995, akaenda katika bendi ya Tanza Muzika iliyokuwa ikimilikiwa na Elvis Musiba. Elvis Musiba kwa vijana wa zamani watamkumbuka kwa utunzi wake wa kitabu chake cha ‘Simu ya Kifo’

Anna alifafanua kuwa katika bendi hiyo aliwakuta wanamuziki wenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, François Makassy ‘Makassy Junior’, Kasongo Ilunga, na Chibanda Sonny.

François Makassy ni mtoto wa Mzee Kitenzogu Makassy.

Msemo usemao kwamba ‘Wazee dawa’ Sauda Mwaole alioufanyia kazi pale alipoamua kwenda kuchota mawazo, fikra na ujuzi toka kwa wazee wa bendi ya Shikamoo Jazz ya jijini Dar es Salaam.

Wanamuziki wazee aliowakuta katika bendi hiyo anawataja baadhi yao kwamba ni akina Salimu Zahoro, John Simon, Juma Mrisho ‘Ngulimba wa Ngulimba’ na Majengo Selemani.

Akiwa na Shikamoo Jazz, alibahatika kusafiri akiambatana na bendi hiyo iliyofanya ziara na kupiga muziki katika mji wa Kampala nchini Uganda.

Miezi sita ilitosha kuyapata aliyoyadhamiria, hivyo aliondoka kwa wazee wa Shikamoo Jazz na kutimkia bendi ya Matimila ya Dokta Remy Ongalla kwa kipindi kifupi kabla ya kujiunga na bendi ya Super Volcano, iliyokuwa ikiongozwa na Binti ya Mbaraka Mwinshehe Mwaruka, Taji Mbaraka.

Sifa zake za kupitia Jeshi la Polisi zilipelekea yeye apate kazi kiulaini katika bendi ya Magereza Februari 1998.Akiwa Magereza Jazz alitoka na wimbo wake wa ‘Samahani Baba watoto’ akishirikiana kuimba na akina Makoye Kwirukwira, Sharifa Bernard na wengine.

Sauda katika juhudi za kuhangaika kutafuta kujiendeleza zaidi katika tasnia ya muziki, alikwenda kujiunga na bendi ya Vijana Jazz anayomilikiwa na Jumuiya ya Vijana Tanzania. Huko alikutana na waimbaji ambao alisema walimuongezea chachu katika kipaji chake cha kuimba.

Aliwataja wanamuziki hao kuwa ni Suleiman Mbwembwe, Freddy Benjamin, Abdallah Mgonahanzelu, na mwana dada wakati huo Nuru Muhina’ Baby White’ Kwa upande wa ala za muziki, walikuwepo Miraji Shakashia ‘Shakazulu’ Kulwa wa Milonge, Mawazo Hunja na Rashid Pembe. Wote hao anawashukuru kwa kumuongezea ujuzi katika muziki.

Ilikuwa mwaka 2001 ambapo msanii maarufu wa kucheza na Nyoka, Norbert Chenga, alipomchukua mwanamama huyo kwenda kujiunga katika kikudi cha Muungano dancing Troupe.

Alipofika hapo akaambiwa azifanyie mazoezi nyimbo za taarabu za alizokuwa akiziimba Nasma Hamis ambaye alikuwa tayari katimkia kundi lingine.Nyimbo hizo alizitaja kuwa ni za ‘Mtu mzima ovyo’, ‘Hata mkisema’, ‘Sanamu ya mMichelini’ na nyingine nyingi.

Kipaji cha Sauda Mwaole kilijoinnesha mapema hapo Muungano, baada ya kuzitendea haki nyimbo hizo. Aliweza kuziimba huku wapenzi wakisema kumbe pengo laweza kuzibika.

Aliimba nyimbo zote za Nasma pasipo mtu kubaini kuwa anayeimba hakuwa Nasma.Mashabiki papo hapo walimpachika jina la Nasma Junior.Akiwa Muungano dancing troupe, Mwaole licha ya kuimba taarabu pia aliweza kucheza sarakasi na ngoma za asili zalizokuwa zikichezwa na kikundi hicho.

Mwaole alikuwa mtafutaji ikizingatia msemo usemao ‘atafutae hachoki, na akichoka kaisha pata’ Ndivyo ilivyokuwa kwa mama huyo ambaye mwaka 2004 aliachana na Muungano baada ya kutokuelewana katika mpango mzima wa maslahi.

Mwaka 2006 aliomba kurudi kwa King Kiki ‘Bwana Mkubwa’ katika bendi ya La Capitale. Sauda alikubaliwa japo alikaa na bendi hiyo kwa muda mfupi sana, akaamua kwenda kupiga muziki katika hoteli mbalimbali mjini Zanzibar mwaka 2007.

Mkataba ulipomalizika huko Zanzibar, alikwenda katika bendi ya Bana Maquis inayoongozwa na Thsimanga Kalala Assosa ambako aliungana na mwimbaji mkongwe Abubakar Kasongo Mpinda ‘Clayton’

Kama nilivyo kujuza kuwa historia ya Mwaole katika mzuziki haichoshi kuisikia au kuisoma, aliitwa kujiunga na bendi ya Super Kamanyola ya jijini Mwanza ‘Rocky City’.Huko nako alikutana na wakali wengine katika uimbaji akina Mukumbule Lolembo ‘Parash’ na Benno Villa Anthony.

Alipiga muziki na bendi hiyo kwa kipindi cha miaka miwili baadae akarejea katika bendi yake ya Bana Maquis.Sauda Mwaole tayari amekwisha tengeneza album ambayo anasema bado ipo jikoni ikikolezwa viungo kabla ya kupakuliwa hivi karibuni.

Anazitaja nyimbo zilizo katika album hiyo kuwa ni ‘Penye penzi pana mengi’, ‘Penzi la ukweli’, ‘Shoka la bucha’, ‘Siyo kama nina wivu’, ‘Huyu ni chaguo langu’ na ‘Sitaki visa vyako’Mwaole alibahatika kupata watoto watatu, mmoja kati yao alitangulia mbeleza haki. Anawataja watoto walio hai kuwa ni Mariam Rashid na Kassim Farid.

,Kassim alimuelezea kuwa amefuata nyayo zake za kuimba nyimbo za muziki wa dansi, akitumia jina la kisanii la ‘Farid Lokuwa’

Kama mzazi, alitoa wito kwa vijana kufuata maadili mema na kutoiga utamaduni wa nje wa kuvaa nguo nusu uchi hadharani, kuvaa hereni na vipini kwa vijana wa kiume na mengine mengi ya kuudhi.

“Ni kujivunjia heshima mbele ya kadamnasi, aibu kubwa kwa jamii kwa kuwa ni kujidharirisha pasipo sababu” kwa masikitiko anatamka Sauda Mwaole.

Kwa upande wa muziki wa kizazi kipya Mwaole alisema muziki wao ungelikuwa mzuri zaidi kama baadhi yao wasingelikuwa wanatamka maneno ya matusi katika nyimbo zao.

Aliwasihi maproduza wenye studio za kurekodi miziki, kuzichuja nyimbo za wasanii hao pindi wanapobaini kwamba lugha iliyotumika katika nyimbo hizo haziendani na utamaduni wa Mtanzania.

CHIDUMULE MUZIKI WA DANSI HADI INJILI

0
0
Na Moshy Kiyungi,Dar es Salaam.

Kosmas Tobias Chidumule alikuwa mwanamuziki wa muziki wa dansi, akitumia sauti yake nyororo kufikisha ujumbe mwanana kwa wapenzi wa muziki huo.

Baada ya kuutumikia muziki wa kidunia kwa kipindi kirefu, Chidumule aliamua Kuokoka, na hivi sasa ni Mchungaji akihubiri injili .

Licha ya kufanyakazi ya kumtumika Mungu, nguli huyo bado anafanya muziki lakini ni wa injili.Sauti wakati wa kuimba, hadi leo bado haijabadilika licha ya umri kumtupa mkono.

Kosmas popote ukutanapo naye huoneka ni mwenye furaha, afya njema, utanashati wake, ucheshi, utani kwa wingi.Kila bendi aliyopita aliacha simulizi kwa wapenzi na mashabiki wake kufuatia tungo na uimbaji wake usiobadilika Abadan.

Msomaji wa makala hii, nikukumbushe wimbo mmoja wa Neema, ambao mpaka leo unaporindima watu hawakosi kutikisa vichwa vyao, ni kati ya tungo nzuri za Kosmas.

Chidumule ni mwanamuziki mwenye vipaji vya kutunga na kuimba kwa umahiri mkubwa nyimbo za muziki wa dansi na sasa za injili.Gwiji huyu kabla ya kuokoka alipitia bendi nyingi za muziki wa dansi hapa nchini.

Alisimulia kwamba alianza kupenyeza katika tasnia ya muziki wa dnsi miaka ya 1970, akiwa katika bendi ya Butiama Jazz.Butiama Jazz ilikuwa na makao yake jijini Dar es Salaam, kukienzi kijiji alichozaliwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Kosmas akielezea safari yake katika muziki wa dansi, alibainisha kuwa alipiga muziki katika bendi hiyo kabla ya kuhamia bendi ya Urafiki Jazz, iliyokuwa ikiongozwa na Juma Mrisho ‘Ngulimba wa Ngulimba.

Hata hivyo huko nako hakudumu kwa kipindi kirefu, aliondoka akaenda kujiunga na wanamuziki wengine miaka hiyohiyo ya 1970, wakaanzisha bendi ya Dar International, ambako aliungana na mtunzi na mwimbaji Marijani Rajabu. 

Katika harakati zake za muziki Chidumule alichomoka akaenda kungana na wanamuziki wengine wakaanzisha bendi ya Orchestra Mlimani Park, iliyompatia umaarufu mkubwa.

Akizungumzia kilichopelekea kuhama kwake mara kwa mara toka bendi moja hadi nyingine Chidumule alisema kwamba hizo zilikuwa ni harakati zake binafsi za kutaka kujiinua kimuziki na kimaslahi zaidi.

Katika harakati hizo za kusaka maslahi, aliwahi kupiga muziki katika bendi za Vijana Jazz wakati huo ilikuwa ikiongozwa na Hemed Maneti na Orchestra Mlimani Park, inayotumia mtindo wa ‘Sikinde Ngoma ya Ukae’

Baadhi ya wanamuziki aliokuwa nao wakati huo ni Abel Balthazar, ambaye ndiye aliyekuwa kinara wa waanzilishi wa bendi ya Orchestra Mlimani Park.Wengine ni pamoja na yule aliyekuwa mtaalamu wa kupiga ala zote Michael Enoch ‘Teacher’, Joseph Bernard, Joseph Mulenga ‘King Spoiler’ Abdalah Gama, Machaku Salum na Habib Jeff.

Bendi hiyo ilikuwa imeweka maskani yao katika Klabu ya Mlimani, maeneo ya Mwenge jijini Dar es Salaam.Mlimani Park ‘iliwanyakua’ watunzi na waimbaji mahiri akina Muhidin Maalim Gurumo na Hassan Rehani Bitchuka.Kwa pamoja walishirikiana vyema kutunga na kuimba vibao motomoto wakitumia mtindo wa ‘Sikinde ngoma ya Ukae’.

Chidumule aliweza kutunga na kuimba nyimbo nyingi zilizompatia umaarufu mkubwa kufuatia ujumbe uliokuwamo kwenye nyimbo zake zikiwa na mafundisho mazuri kwa jamii.Baadhi ya nyimbo hizo ni 'Barua kutoka kwa mama', 'Neema', 'Telegramu', pia alitunga na kuimba nyimbo za Ubaya, Nalala kwa taabu, Usitumia pesa, Ugomvi wa Baba na Mama, Epuka na maeneo.

Mwishoni mwa miaka ya 1980 Chidumule alijiunga katik bendi ya Orchestra Super Matimila, iliyokuwa ikiongozwa na Ramadhan Mtoro Ongala ‘Dk. Remy’.Akiwa na bendi hiyo alitunga nyimbo nyingi ukiwemo wa “Dodoma makao Makuu”, uliompa sifa lukuki kila pembe humu nchini.

Katika wimbo huo alijizolea sifa lukuki kwa kuongeza maneno machache ya lugha ya Kiingereza.Chidumule alibainisha kwamba kujiunga kwake na bendi ya Orchestra Super Matimila, ilikuwa ni mapenzi yake makubwa kwa Ramadhan Mtoro Ongala ‘Dk. Remy’, zaidi ya bendi yenyewe."Nilimpenda Dk. Remy tangu alipokuja katika bendi ya Ochestra Makassy na yeye pia akinikubali sana nilipokuwa Urafiki…" alisema.
Alifafanua kuwa mara baada ya kujiunga na bendi hiyo kuna wakati Dk. Remy alimwachia bendi kwa miezi sita, alipokwenda Ulaya.

Orchestra Super Matimila ilipata mwaliko wa kushiriki katika maonesho barani Ulaya mwaka 1988, baada ya shirika linalopandisha chati wanamuziki na wasanii mbalimbali kutoka katika nchi za dunia ya tatu, World of Music, Arts and Dance (WOMAD) kuvutiwa na nyimbo zao.

Chidumule akaunda kundi la Serengeti. Dk. Remy aliporudi akaendelea kutumia kundi la Serengeti maana wale aliokwenda nao Ulaya wengi ‘walizamia’ huko.Kosmas baada ya kuokoka alianza kutamba katika medani ya muziki wa injili mwaka 1999.

Akithibitisha hilo alisema, alitoka kwenye bendi ndogo sana na kuweza kupiga muziki kwenye bendi kubwa zenye wanamuziki wenye majina makubwa.Akizungumzia uamuzi wake wa kuachana na muziki wa dansi Chidumule alisema "Niliacha bendi ya Orchestra Matimila nipoamua kuokoka baada ya kupata maono tulipokuwa safarini kwenda Dodoma kupiga muziki. Sauti iliniijia ndotoni na iliniuliza nini hatma ya maisha yangu ya kimuziki…"

"Sauti hiyo ilinisimbua sana hata baada ya kufika Dodoma. Tulipofika ukumbini sikuwa na hamu ya kuimba.Kiongzi wangu Dk. Remmy alibaini jinsi nilivyokuwa nimenyong'onyea, akanipa glasi ya Konyagi ili nitoe ‘Nishai’, ikanidondoka na kuvunjika nikakimbia stejini maana kwenye glasi ile niliona umetoka upanga au mkuki.

Siku iliyofuatia nikarudi Dar es Salaam asubuhi nikatangaza redioni, Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) na kwa uongozi na wanamuziki wa bendi yangu kwamba mimi nimeamua kumfuata Mungu, nimeokoka…" alisema Kosmas Chidumule.

Kosmas Chidumule alipiga na bendi Super Matimila hadi ilipotimu mwaka 1993, alipoamua kuokoka na kuamua kumtumikia Bwana.Hivi sasa ni mchungaji, mhubiri, mtunzi na mwimbaji wa nyimbo za ijili.

Alifanikiwa kutoa albamu yake ya kwanza ya injili iitwayo 'Yesu ni Bwana'. Baadaye alitoka na Hosanana, Nani Alaumiwe na Furaha yangu. 'Yesu ni Bwana', 'Kimbilia kwa Yesu' na 'Sioni pa Kwenda.

Kama mwanamuziki mzoefu, Chidumule hakusita kutoa ujumbe akisema “Ujumbe wangu kwa wapenzi wa muziki wa dansi wanakazi kubwa ya kuwahurumia wanamuziki kwa sababu wengi wao wanaishi maisha halisi ambayo ni tofauti kabisa na kile wanachokiimba.

Mazingira ya muziki wa dansi ni hatarishi sana, japo wanamuziki wanaimba vyema. Tunapiga kwenye vilabu, wengi wa wapenzi wa muziki ni walevi, hata kama hunywi unalazimika kuishi kama mlevi ili ukubalike kwa wapenzi wa kazi yako…"

"Nyimbo zangu za dansi zilikuwa na mafundisho kabla ya kuokoka kwani Mungu alishanichagua tayari, tatizo mimi mwenyewe nilikuwa sijajitambua. Nilikuwa nawakanya watu lakini mimi mwenyewe nikifanya kinyume na yale niliyoimba." alisema Chidumule.

Chidumule alienda mbali zaidi akasema

“Wokovu ni maisha ya Yesu ndani ya mwanadamu sio dini, ndo maana mimi sishughuliki na dini bali miili na nafsi za watu…”

Akizungumzia utunzi wa nyimbo zake, Chidumule alikuwa na haya ya kusema, "Utunzi wangu huongozwa na maono, nikisukumwa sana na wazo fulani ndipo ninapotengeneza nyimbo zangu. Naandika sana na kuhifadhi kwenye maktaba. Ziko nyimbo niliandika kama "Naifariji Nafsi Yangu", iliyo kwenye albamu yangu ya mwisho, mwaka 1996, iko kwenye albamu yangu ya tatu."

"Pamoja na kuhubiri kwa muziki naheshimu pia vyombo vya binadamu kama COSOTA. Vyombo hivi vinahitaji kushirikiana na Jeshi la Polisi au Mahakama ili kuweza kudhibiti vyema kazi za watunzi wa kazi za muziki..” alitamka Kosmas Chidumule.

Aidha aliiomba COSOTA ifike hadi ngazi ya chini kabisa kama Kanda, na ifanye kazi kwa mtazamo wa Kiafrika Mashariki.Chidumule alijinasibu kwa kuusifia muziki wake kwamba umempa umaarufu lakini bado hajafaidika kama muuzaji wa muziki wake anavyofaidika.

Alitolea mfano ukiuzalisha kwa gharama ya shilingi milioni 3, ukisharudisha fedha hiyo huingia mkataba mwingine mpya wa namna ya kugawana mapato hayo lakini hiyo ni tofauti.Chidumule alilalama akisema unaweza kumkuta mtu anauza kazi yake hata baada ya miaka mitano na bado hupati chochote, wakati yeye ananunua magari na kujenga majumba.

MBUNGE WA GEITA MJINI, MHE.KANYASU AWAWASHIA MOTO VIONGOZI NA WAZAZI WASIODHIBITI MIMBA SHULENI

0
0
Mbunge wa Geita mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Nyaseke kuhusiana na umuhimu wa viongozi pamoja na wazazi katika kushirikiana kwenye vita dhidi ya wanaume wanawapa mimba watoto wa kike wakiwa bado shule.
Mbunge wa Geita mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ( wa pili kulia)( akiwa na baadhi ya viongozi wa CCM wa wilaya ya Geita pamoja na madiwani wa Kata ya Bulela na Shiloleli mara baada ya kuanza mkutano wa hadhara ambapo pamoja na mambo mengine alitumia fursa hiyo kuwaeleza wananchi wake ahadi mbalimbali alizozitekeleza yakiwemo masuala ya afya, miundombinu pamoja mikopo tangu walimpomchagua kuwa Mbunge wao
Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Geita, Barnabas Mapande akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara akiwaeleza ahadi mbalimbali alizozitekeleza na anazoendelea kutekeleza Mbunge wa Geita mjini, Mhe, Constantine Kanyasu


Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Mbunge wa Geita mjini, Mhe.Kanyasu wakati wa mkutano wa hadhara katika eneo la Bulela

Diwani wa viti maalum wa Bulela, Mhe, Salome Kitula akizungumza na wananchi wa kata ya Bulela kabla ya kumkaribisha Mbunge wa Geita mjini Mhe, Kanyasu kuzungumza na wananchi.wa kata hiyo


Diwani wa viti maalum wa Kasamwa, Mhe. Jesca Kalalio akizungumza na wananchi wa kata ya Kasemwa kabla ya kumkaribisha Mbunge wa Geita mjini Mhe, Kanyasu kuzungumza na wananchi.wa kata ya Bulela
………………….
Mbunge wa Geita mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amesema atawashughulikia Watendaji Kata wote watakaobainika kushindwa kuchukua hatua kwa Wanaume wanaowapa mimba wanafunzi wa kike wakiwa bado shule.

Pia, Ametangaza vita kwa Waendesha pikipiki (Bodaboda ) kuwa yeyote atakayebainika kumpatia mimba mtoto wa kike akiwa bado shule hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Ameyasema hayo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Nyaseke Kata ya Bulela mkoani Geita.

Amesema mtoto wa kike anayepata mimba akiwa shule na hivyo kulazimika kukatisha masomo yake haiwezi kuwa Mama bora kwa sababu atashindwa tu kumlea watoto wake ipasavyo.

“Ninyi wanafunzi someni hata ukipata daraja la mwisho baada ya kufika kidato cha nne ni lazima utakuwa Mama bora” alisisitiza Kanyasu

Amesema maisha ya sasa yamebadilika sana tofauti na zamani ambapo kwa sasa bila kusoma maisha ni magumu sana

Mhe.Kanyasu amesema haiwezekani Serikali itoe pesa nyingi kila mwezi katika shule zote nchini ili watoto wa kike waweze kusoma huku idadi ya watoto wakike wanaoacha shule kwa sababu za kupata mimba ikizidi kuongezeka.

” Nawambieni Watendaji wa Kata mkishindwa kuwachukulia hatua waharibifu wa ndoto za watoto wa kike nitaanza na ninyi” alisema Mhe.Kanyasu.

Katika hatua nyingine, Mhe.Kanyasu amewaonya wazazi wanaowalinda Wanaume wanaowapa mimba watoto wa kike kwa kukubaliana nao kuwa ni jambo lisilokubalika.

” Mimi Mbunge wenu nimekuwa nikihakikisha napigania ujenzi wa shule bora pamoja na walimu bora lakini baadhi ya wazazi mmekuwa mkiwalinda wanaofanya uharibifu, si jambo zuri”

Amewataka wazazi waache tabia ya kuelewana katika ngazi ya kifamilia kwa wanaume wanaokatiza ndoto za watoto wa kike wakiwa bado shule.

” Nawasihi wazazi mzungumze na Watoto wa kike kuhusu umuhimu wa kusubili huku mkiwasisitiza kuhusu umuhimu wa elimu katika dunia ya sasa” amesititiza Mhe.Kanyasu.

Naye, Diwani wa viti maalum wa Kata ya Bulela, Mhe, Salome Kitula amesema tatizo la mimba kwa watoto wa shule ni kubwa linahitaji ushirikiano kwa wapenda maendeleo wote.

Amesema jitihada nyingi zimekuwa zikifanyika ikiwa pamoja na kufanya semina na wazazi kuhusu umuhimu wa kuwafuatilia watoto wakike wakiwa eansonesha mienendo isiyofaa pamoja na kufanya ziara katika shule kwa ajili ya kuzungumza na wanafunzi kuhusu athari za kupata mimba wakiwa bado shule.

Ameongeza kuwa kwa mwaka 2018 takribani wanafunzi zaidi ya kumi walibainika kupata mimba na tayari kesi zinaendelea mahakamani

MAGAZETI YA LEO IJUMAA JULAI 26,2019

Msimu wa kombe la Standard Chartered wafunguliwa

0
0
Timu ya wafanyakazi wa Benki ya Standard Chartered wametandikwa goli moja kwa bila na timu ya Wanahabari katika mechi ya uzinduzi wa kombe la Standard Chartered.

Mchezo huo wa dakika 10 mpaka wanaenda mapumzikoni walikuwa suluhu ya kutofungana. Lakini dakika ya pili ya kipindi cha pili Mwandishi wa Habari za Michezo wa ITV Sebastian Kolowa alitungua goli la benki ya Standard Chartered na kufanya mpira huo kumalizika kwa goli 1-0.

Ufunguzi huo wa michuano ya Kombe la Standard Chartered Bank wakishirikiana na timu ya Liverpool ya Uingereza umefungua msimu wa nne mfululizo kufanyika nchini Tanzania.

Akizungumza katika ufunguzi huo Kaimu Mkurugenzi wa Standard Chartered Bank Tanzania, Rayson Foya amesema kwamba michuano hiyo itakuwa na timu 32 za kampuni mbalimbali zenye wachezaji saba. Alisema kwa sasa dirisha lipo wazi la usajili mpaka Agosti 16 kabla ya michuano hiyo kuanza kuunguruma rasmi Agosti 24, mwaka huu.

Michuano hiyo itafanyika katika Uwanja wa JMK Park, Dar es Salaam na mfumo utakaotumika wa mechi hizo ni kila timu kuingia uwanjani na wachezaji watano wakiwa na wachezaji wa akiba wawili. Kila mechi itachezwa kwa dakika 10.

Timu itakayoibuka bingwa itapata nafasi ya kwenda katika Uwanja wa Anfield, England unaotumiwa na Liverpool na kupata nafasi ya kukutana na wakongwe wa timu hiyo na kupata nafasi ya kushuhudia moja ya mechi za Liverpool kwenye michuano ya Ligi Kuu England.

Alisema kwamba michuano hiyo itafanyika kwa Knock outs.
Benki ya Standard itagharamia safari za wachezaji saba wa timu itakayoshinda yaani tiketi za ndege na malazi yao kwa siku tatu.
Aidha alisema mwaka huu hawatawaleta magwiji wa nje na badala yake watatumia magwiji wa hapa nyumbani kuhakikisha soka linaendelezwa.

 “Pamoja na yote hayo lakini safari hii Standard Chartered tumeamua kushirikiana na TFF (Shirikisho la Soka Tanzania) na wakongwe wa soka nchini kwa ajili ya kupanua wigo wa vipaji na kukuza soka nchini kote. Kwa hiyo kwa kuanza tutakuwa na Ali Mayay na wengine ambao tutakuwa nao wakati wa michuano hii,” alisema Foya.

Kipindi kilichopita Benki hiyo iliwaleta magwiji wa soka wa Liverpool akiwemo Sami Hyppia huku mwaka juzi walimleta John Barnes kwa lengo la kukuza vipaji.
Kuwapo kwa kombe hilo ni matokeo ya udhamini wa benki ya The Standard Chartered Group kuanzia mwaka 2010. Na mwaka jana ilitia saini ya kuendelea na udhamini hadi msimu wa mwaka 2022/23.

Kombe hilo ni sehemu ya makubaliano kati ya beniki hiyo na klabu ya Liverpool ya kuendeleza mahusiano yake na nchi ambazo inafanya nazo biashara  Asia, Africa na mashariki ya Kati, kwa lengo la kuinua soka. Mashindano hayo kwa sasa yapo katika mwaka wa nane na yanazidi kuwa na nguvu yakianzia Singapore mwaka 2012.
 Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bi. Juanita Mramba (kushoto) akitambulisha meza kuu kwa waandishi wa habari Kutoka kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Standard Chartered Bank Tanzania, Bw. Rayson Foya, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Bw. Wilfred Kidau, Mchambuzi mkongwe wa soka nchini ambaye ni shabiki wa timu ya Liverpool, Dk. Leaky Abdallah pamoja na Mkongwe wa soka nchini, Bw. Ali Mayay wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa kombe la Standard Chartered Bank uliofanyika katika viwanja vya JMK Park jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi wa Standard Chartered Bank Tanzania, Bw. Rayson Foya (wa pili kushoto) akizungumza kuhusu mashindano ya kombe la Standard Chartered Bank ambapo dirisha la usaji wa timu limefunguliwa rasmi wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa kombe hilo uliofanyika katika viwanja vya JMK Park jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bi. Juanita Mramba na wa tatu kushoto ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Bw. Wilfred Kidau pamoja na Mchambuzi mkongwe wa soka nchini ambaye ni shabiki wa timu ya Liverpool, Dk. Leaky Abdallah
 Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Bw. Wilfred Kidau (katikati) akizungumzia mipango ya TFF kwa kushirikiana na Benki ya Standard Chartered katika kuinua soka la Tanzania kupitia michuano ya kombe la Standard Chartered Bank wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mashindano ya kombe hilo uliofanyika kwenye viwanja vya JMK Park jijini Dar.
 Mchambuzi mkongwe wa soka nchini ambaye ni shabiki wa timu ya Liverpool, Dk. Leaky Abdallah (wa pili kulia) akitoa tathmini ya timu ya Liverpool kuelekea michuano ya Ligi Kuu England wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa kombe la Standard Chartered Bank uliofanyika katika viwanja vya JMK Park jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkongwe wa soka nchini, Bw. Ali Mayay na kutoka kushoto ni Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bi. Juanita Mramba, Kaimu Mkurugenzi wa Standard Chartered Bank Tanzania, Bw. Rayson Foya pamoja na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Bw. Wilfred Kidau.
 Mkongwe wa soka nchini, Bw. Ali Mayay  (kulia) akielezea furaha yake kushiriki kwenye mashindano ya kombe la Standard Chartered Bank yatakayoanza kutimua vumbi mwezi ujao wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa kombe hilo iliyofanyika katika viwanja vya JMK Park jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bi. Juanita Mramba akisalimiana na kikosi cha wanahabari wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa kombe la Standard Chartered Bank uliofanyika katika viwanja vya JMK Park jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Bw. Wilfred Kidau na Kaimu Mkurugenzi wa Standard Chartered Bank Tanzania, Bw. Rayson Foya wakisalimiana na timu ya wanahabari  iliyochuana na wafanyakazi wa benki ya Standard Chartered wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa kombe la Standard Chartered Bank uliofanyika katika viwanja vya JMK Park jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi wa Standard Chartered Bank Tanzania, Bw. Rayson Foya, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Bw. Wilfred Kidau, Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Bi. Juanita Mramba, Mchambuzi mkongwe wa soka nchini ambaye ni shabiki wa timu ya Liverpool, Dk. Leaky Abdallah pamoja na Mkongwe wa soka nchini, Bw. Ali Mayay  wakiwa kwenye picha ya pamoja na timu ya wafanyakazi wa benki ya Standard Chartered pamoja na timu ya wanahabari walioshiriki hafla ya uzinduzi wa kombe la Standard Chartered Bank uliofanyika katika viwanja vya JMK Park jijini Dar es Salaam.



 Timu ya wafanyakazi wa Benki ya Standard Chartered (jezi nyekundu) na timu ya wanahabari (jezi nyeusi) wakimenyana kuashiria uzinduzi wa kombe la Standard Chartered Bank 2019 katika hafla fupi iliyofanyika kwenye viwanja vya JMK Park jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi wa Standard Chartered Bank Tanzania, Bw. Rayson Foya, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Bw. Wilfred Kidau pamoja na Mkongwe wa soka nchini, Bw. Ali Mayay wakiwa kwenye picha ya pamoja na timu ya wanahabari iliyoibuka kidedea kwa goli 1-0 dhidi ya timu ya wafanyakazi wa benki ya Standard Chartered wakati wa hafla ya uzinduzi wa kombe la Standard Chartered Bank uliofanyika katika viwanja vya JMK Park jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Bw. Wilfred Kidau akitoa zawadi kwa timu ya wanahabari iliyoibuka kidedea kwa goli 1-0 dhidi ya timu ya wafanyakazi wa benki ya Standard Chartered wakati wa hafla ya uzinduzi wa kombe la Standard Chartered Bank uliofanyika katika viwanja vya JMK Park jijini Dar es Salaam.
Viewing all 109607 articles
Browse latest View live




Latest Images